Dodoma Aprili, 2019
JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO MHESHIMIWA MHANDISI ISACK ALOYCE KAMWELWE (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020 DODOMA APRILI, 2019 HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO MHESHIMIWA MHANDISI ISACK ALOYCE KAMWELWE (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2019/2020 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, baada ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuweka mezani Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara, naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2018/2019. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango na Bajeti ya Wizara kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 2. Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uhai na kutuwezesha kukutana tena leo kujadili maendeleo ya shughuli zinazosimamiwa na sekta za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. 3. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa 1 hii kuwapongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Alli Mohammed Shein, Rais wa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb.), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wao thabiti ambao umewezesha kutekelezwa kwa mafanikio makubwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015, ahadi za Viongozi pamoja na kutatua kero mbalimbali za wananchi.
[Show full text]