Hotuba Ya Waziri Wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt

Hotuba Ya Waziri Wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt

HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI, MHESHIMIWA DKT. JOHN POMBE MAGUFULI (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO WA MAENDELEO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA 2013/2014 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika , baada ya Bunge lako Tukufu kupokea taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Miundombinu, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako tukufu likubali kupokea na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka 2012/13. Aidha, naomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango na bajeti ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2013/2014. 2. Mheshimiwa Spika , awali ya yote napenda kuchukua nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunilinda na kunipa nguvu ya kutekeleza majukumu yangu na kuniwezesha kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu kuwasilisha bajeti hii. 3. Mheshimiwa Spika , kwa heshima na taadhima nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa 1 kuendelea kuiongoza nchi yetu vyema na kwa utekelezaji mahiri wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 pamoja na mipango na programu mbalimbali za kuiletea nchi yetu maendeleo. Mheshimiwa Rais amekuwa mstari wa mbele katika kutafuta fedha za kutekeleza miradi iliyopo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010 ambayo pia inajumuisha barabara. Aidha, nawapongeza Mheshimiwa Dkt. Mohamed Gharib Bilal, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Waziri Mkuu kwa jinsi ambavyo wamemsaidia Mheshimiwa Rais kusimamia na kuongoza shughuli zote za Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 4. Mheshimiwa Spika, naomba nikupongeze wewe binafsi, Naibu Spika na Wenyeviti wa Bunge kwa hekima, umahiri na busara mnazotumia katika kuliongoza Bunge hili Tukufu. Namwomba Mwenyenzi Mungu azidi kuwajalia busara na hekima katika kazi hiyo. 5. Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua nafasi hii kutoa pole kwa kifo cha ghafla cha Mhe. Mbunge mwenzetu Hayati Salim Hemed Khamis, Mbunge wa Chambani kwa tiketi ya CUF. Naungana na Waheshimiwa Wabunge wenzangu kutoa pole kwa familia, wewe Mhe. Spika, Bunge lako tukufu, ndugu, 2 jamaa na marafiki wa marehemu na wananchi wote wa Jimbo la Chambani. Mwenyezi Mungu aiweke roho ya marehemu mahali pema peponi, Amina. 6. Mheshimiwa Spika, napenda nichukue fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Peter Joseph Serukamba, Mbunge wa Jimbo la Kigoma Mjini na Mheshimiwa Athumani Juma Kapuya, Mbunge wa Jimbo la Urambo Magharibi kwa kuteuliwa kuiongoza Kamati ya Bunge ya Miundombinu. Vile vile nawapongeza wajumbe wote wapya walioteuliwa kuunda Kamati ya Bunge ya Miundombinu. Ushauri wa Kamati na Wabunge wote kwa ujumla utaendelea kuzingatiwa katika utekelezaji wa majukumu ya kila siku ya Wizara ya Ujenzi ili kuiletea nchi yetu maendeleo. 7. Mheshimiwa Spika, napenda kuungana na Waheshimiwa Wabunge wenzangu, katika kumpongeza na kumshukuru Waziri Mkuu, Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, Mbunge wa Jimbo la Katavi kwa hotuba yake ambayo imetoa mwelekeo wa jumla katika masuala ya Mipango na Uchumi kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2013/2014. Naomba pia kuwashukuru Waheshimiwa Wabunge waliochangia hotuba hiyo. Ni matumaini yangu kuwa maoni yao yatasaidia kuboresha mipango ya Serikali katika sekta mbalimbali ikiwemo Sekta ya Ujenzi. 3 DIRA NA DHIMA YA WIZARA 8. Mheshimiwa Spika, Dira ya Wizara ni kuwa na Barabara, Madaraja, Vivuko, Nyumba za Serikali na Huduma za Ujenzi zenye ubora wa kiwango cha juu, zenye gharama nafuu na zinazozingatia usalama na utunzaji wa mazingira. Aidha, dhima ya Wizara ni kuwa na Barabara, Vivuko, Nyumba za Serikali na Huduma za Ujenzi zilizo na uwiano na ambazo zinakidhi mahitaji kwa viwango bora na kwa bei nafuu zinazoendana na mikakati ya Serikali ya maendeleo ya kiuchumi na kijamii na wakati huo huo zikiwa endelevu kiuchumi na kimazingira. MAJUKUMU YA WIZARA 9. Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi ina majukumu ya kusimamia Sera za ujenzi na usalama barabarani; ujenzi na matengenezo ya barabara, madaraja na vivuko; ujenzi na ukarabati wa majengo ya Serikali; pamoja na masuala ya ufundi na umeme. Aidha, Wizara inasimamia shughuli za usajili wa makandarasi, wahandisi, wabunifu majengo na wakadiriaji majenzi; masuala ya usalama barabarani na mazingira katika sekta; uboreshaji utendaji na uendelezaji wa watumishi wa Wizara; pamoja na kusimamia utekelezaji wa majukumu ya Taasisi zilizo chini ya Wizara. 4 MALENGO YA WIZARA 10. Mheshimiwa Spika, katika kufanikisha utekelezaji wa majukumu yake, Wizara imelenga kujenga barabara ili kufungua fursa za maendeleo na kuhakikisha miji yote mikuu ya mikoa inaunganishwa kwa barabara za lami ifikapo mwaka 2017/18; kufanya matengenezo ya barabara kuu na za mikoa; kujenga barabara za kupunguza msongamano wa magari mijini hususan katika Jiji la Dar es Salaam; kuhakikisha kuwa usafiri wa vivuko unaimarishwa katika maeneo yote yanayohitaji huduma hiyo; na kusimamia ujenzi wa nyumba za Serikali na watumishi. Aidha, Wizara itaendelea kusajili na kusimamia Makandarasi, Wahandisi, Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi kwa kutumia bodi husika pamoja na kuweka mazingira mazuri ya kuvutia sekta binafsi kuwekeza katika sekta ya Ujenzi. Wizara pia itaendelea kusimamia masuala ya usalama na mazingira katika barabara na vivuko pamoja na kufanya matengenezo na ukarabati wa Magari ya Serikali na Mitambo. Vile vile Wizara itaendelea kushirikiana na taasisi husika katika kushughulikia masuala mtambuka kama vile kampeni za kupunguza maambukizi ya ugonjwa hatari wa UKIMWI, uhifadhi wa mazingira, masuala ya jinsia pamoja na uendelezaji wa matumizi ya Teknolojia ya Habari na 5 Mawasiliano (TEHAMA) katika utekelezaji wa shughuli mbalimbali za Serikali. MIKAKATI YA WIZARA KATIKA KUFIKIA MALENGO 11. Mheshimiwa Spika, ili kuweza kutekeleza malengo yake, Wizara itaendelea kuzingatia kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2010, Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano wa mwaka 2011/12 – 2015/16, Ahadi za Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Ahadi za Viongozi Wakuu wa Serikali na Mkakati wa Kukuza Uchumi na Kupunguza Umaskini Tanzania (MKUKUTA). Aidha, Wizara ya Ujenzi inazingatia utekelezaji wa Programu ya Uwekezaji katika Sekta ya Miundombinu ya Usafirishaji (Transport Sector Investment Program – TSIP ) ambayo ni programu ya miaka kumi (2006/07-2016/17) inayolenga kuimarisha na kuboresha miundombinu ya usafirishaji. Wizara inatekeleza Sera ya Taifa ya Ujenzi (2003), Sera ya Usalama Barabarani (2009) na Sera ya Ushirikiano kati ya Serikali na Sekta Binafsi (PPP). Wizara pia itaendelea kusimamia utoaji elimu kwa wananchi kuhusu matumizi ya barabara kwa mujibu wa Sheria ya Barabara Na. 13 ya mwaka 2007 pamoja na sheria nyingine ili miundombinu ya barabara iweze kutunzwa na kudumu kwa muda uliokusudiwa. Wizara vile vile itaboresha mfumo wa upimaji 6 magari ya mizigo kwa kuweka mizani itakayopima uzito wa magari yakiwa kwenye mwendo (weigh-in-motion) kwa lengo la kuzuia uharibifu wa barabara kutokana na magari yanayozidisha mizigo. 12. Mheshimiwa Spika, mikakati mingine ni pamoja na kusimamia fedha za Mfuko wa Barabara zinazopelekwa Mikoani ili kazi za matengenezo ya barabara zinazotekelezwa zilingane na thamani ya fedha (value for money). Wizara pia itaendelea kutafuta vyanzo vipya ili kupanua wigo wa Mfuko wa Barabara. Aidha, Wizara itaendelea kuzifanyia marekebisho sheria za kisekta ili ziweze kuendana na mazingira ya sasa na kufikia viwango vinavyokubalika kimataifa na kikanda kama vile Jumuiya ya Afrika Mashariki na Jumuiya ya Uchumi ya Nchi za Kusini mwa Afrika. Wizara itahakikisha kuwa Makandarasi, Wahandisi Washauri na Wabunifu Majengo na Wakadiriaji Majenzi wa kizalendo wanahusishwa kikamilifu katika ujenzi wa miradi mikubwa hususan miradi ya barabara, madaraja, nyumba na vivuko inayogharamiwa na Serikali badala ya kutegemea kampuni za nje. Lengo ni kuwajengea wananchi uzoefu stahili katika Sekta ya Ujenzi na kupunguza kasi na wingi wa fedha zinazotokana na vyanzo vyetu kuhamishiwa nje ya nchi kwa kulipia kazi za kampuni za nje. 7 B: TAARIFA YA UTEKELEZAJI WA MPANGO NA BAJETI YA MWAKA 2012/13 Ukusanyaji wa Mapato 13. Mheshimiwa Spika , katika mwaka 2012/13, Wizara ilipanga kukusanya jumla ya Shilingi 15,628,580.00 kupitia Idara zenye vyanzo vya mapato. Idara hizo ni Utawala, Huduma za Ufundi na Menejimenti ya Ununuzi. Hadi kufikia Aprili, 2013, jumla ya Shilingi 36,388,193.24 zilikuwa zimekusanywa. Sababu za kukusanya fedha zaidi ikilinganishwa na bajeti iliyopangwa ni kuongezeka kwa makusanyo ya ada za usajili wa vyombo vya Serikali kufuatia zoezi la kufuta matumizi ya namba za kiraia kwenye magari, pikipiki, bajaj na mitambo ya Serikali na kusajiliwa kwa namba za Serikali. Zoezi hili lilianza tarehe 19 Novemba, 2012 na hadi kufikia Aprili, 2013 jumla ya magari, pikipiki, bajaji na mitambo ya Serikali iliyosajiliwa kwa namba za Serikali ni 2,268. Bajeti ya Matumizi ya Kawaida 14. Mheshimiwa Spika , katika mwaka 2012/13, Wizara ilitengewa kiasi cha Shilingi 329,085,354,000.00 kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Hadi kufikia Aprili, 2013, Shilingi 8 257,177,456,588.75 zilikuwa zimetolewa na Wizara ya Fedha kwa ajili ya Matumizi ya Kawaida. Kiasi hicho ni asilimia 78.15 ya bajeti ya matumizi ya kawaida ya Wizara kwa mwaka 2012/13. Kati ya fedha zilizotolewa, Shilingi 15,490,538,152.00 zilikuwa za Mishahara ya Watumishi wa Wizara na Taasisi zake, Shilingi 237,811,447,236.75 ni za Mfuko wa Barabara na Shilingi 3,875,471,200.00 ni kwa ajili ya Matumizi Mengineyo ya Wizara, Taasisi na Wakala. UTEKELEZAJI WA MIRADI YA MAENDELEO KWA MWAKA 2012/13 15. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2012/13, Wizara iliidhinishiwa Shilingi 693, 948, 272,000.00 kwa ajili ya utekelezaji wa miradi ya maendeleo. Kati ya fedha hizo, Shilingi 296,896,892,000.00 zilikuwa fedha za ndani na Shilingi 397,051,380,000.00 zilikuwa fedha za nje. Hadi kufikia Aprili, 2013, Wizara ilishapokea fedha zote za ndani kiasi cha Shilingi 296,896, 892,000.00 na Shilingi 236,782,437,956.41 za nje. Utekelezaji wa Miradi ya Barabara na Madaraja 16. Mheshimiwa Spika, nchi ya Tanzania ina mtandao wa barabara wenye jumla ya kilometa 87,581. Kati ya hizo, kilometa 35,000 9 ni Barabara Kuu na za Mikoa zinazosimamiwa na Wizara ya Ujenzi kupitia Wakala wa Barabara (TANROADS).

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    252 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us