JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, MHESHIMIWA ENG. ISACK ALOYCE KAMWELWE (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/21 DODOMA MEI, 2020 HOTUBA YA WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO, MHESHIMIWA ENG. ISACK ALOYCE KAMWELWE (MB), AKIWASILISHA BUNGENI MPANGO NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA FEDHA KWA MWAKA WA FEDHA 2020/21 A. UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa humu Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, ninaomba kutoa hoja kwamba Bunge lako sasa lipokee na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Mpango na Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2019/20. Aidha, kwa mara nyingine ninaomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2020/21. 2. Mheshimiwa Spika, sisi sote kwa ujumla wetu, hatuna budi kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kutujalia uhai na afya njema na hivyo kutuwezesha kukutana leo kwa ajili ya kushiriki katika Mkutano huu wa 19 na wa mwisho wa Bunge la 11, ili kujadili utekelezaji wa majukumu ya Sekta za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2019/20 pamoja na kujadili Mipango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Sekta hizo kwa mwaka wa fedha 2020/21. Aidha, ninamuomba Mwenyezi Mungu aendelee kutupatia ulinzi wake dhidi ya janga linaloisumbua dunia kwa sasa la mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID -19). 3. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2019/20, Bunge lako Tukufu lilipatwa na simanzi kubwa kufuatia vifo vya wapendwa wetu ambao ni Mhe. Rashid Ajali Ahkbar aliyekuwa Mbunge wa jimbo la Newala Vijijini, Richard Mganga Ndassa aliyekuwa Mbunge wa Jimbo la Sumve na Mhe. Mchungaji Dkt. Getrude Pangalile Rwakatare, Mbunge wa Viti Maalum. Ninachukua fursa hii kutoa pole kwako wewe binafsi, Mheshimiwa Naibu Spika, Familia za Marehemu hao, Bunge lako Tukufu, Wananchi wa Jimbo la Newala Vijijini na Watanzania kwa ujumla kwa kuondokewa na wanasiasa hao wakongwe na mahiri. Mwenyezi Mungu aziweke roho za marehemu hao mahali pema peponi. Amina. 4. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii kuwapa pole ndugu wa marehemu na wafanyakazi wa Shirika la Reli Tanzania (TRC) kwa 2 msiba mkubwa wa wafanyakazi watano (5) waliopoteza maisha na mmoja kujeruhiwa katika ajali iliyotokea eneo la Mwakinyumbi na Gendagenda ambapo treni iligongana na kiberenge, wananchi 104 waliopoteza maisha kutokana na moto uliosababishwa na lori la mafuta mjini Morogoro, ajali ya lori kugongana na basi la abiria eneo la Mkuranga - Pwani ambapo abiria 20 walipoteza maisha na 15 kujeruhiwa. Aidha, ninawapa pole wote waliofikwa na majanga ya kupoteza ndugu zao kufuatia mvua zilizonyesha kupita kiwango katika maeneo mbalimbali nchini. Mwenyezi Mungu awape nafuu ya haraka majeruhi wote na aziweke roho za marehemu hao mahali pema peponi. Amina. 5. Mheshimiwa Spika, kwa heshima na taadhima ninaomba uniruhusu kutumia fursa hii kumpongeza Mhe. Dkt. John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 kwa umakini mkubwa na hivyo kuendelea kuiongoza nchi yetu kwa amani na utulivu. Aidha, ninampongeza Mhe. Rais kwa kuchaguliwa kuwa Mwenyekiti wa Jumuiya ya Maendeleo Kusini mwa Afrika (SADC) pamoja na kuiongoza vyema Jumuiya hiyo hususan katika kipindi hiki cha mlipuko wa ugonjwa wa homa kali ya mapafu inayosababishwa na virusi vya Corona (COVID -19). Vilevile, ninawapongeza Mhe. Samia Suluhu Hassan, Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wao thabiti. 6. Mheshimiwa Spika, ninaomba nikupongeze wewe binafsi, Naibu Spika, Wenyeviti wa Bunge, Katibu wa Bunge, Watendaji wa Ofisi ya Bunge pamoja na Bunge lako Tukufu kwa ushirikiano ninaoendelea kuupata wakati wote ninapotekeleza majukumu yangu ikiwa ni pamoja na kuwasilisha taarifa mbalimbali kuhusu sekta ninazozisimamia. Ninapenda kuwahakikishia kuwa, Wizara yangu itaendelea kutoa ushirikiano unaohitajika ili kufikia malengo ya Kisekta na Kitaifa kwa ujumla. Vilevile, kwa namna ya pekee ninaomba kuishukuru familia yangu na wapiga kura wa Jimbo langu la Uchaguzi la Katavi kwa kuendelea kunipa ushirikiano katika kutekeleza majukumu yangu kwa Watanzania. 7. Mheshimiwa Spika, nitumie pia fursa hii kuwapongeza Mhe. Mussa Azzan Zungu (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais 3 (Muungano na Mazingira) na Mhe. George Boniface Taguluvala Simbachawene (Mb), Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi kwa kuteuliwa kuwa Mawaziri. Aidha, ninapenda kutoa pongezi kwa Mhe. Miraji Jumanne Mtaturu, Mbunge wa Jimbo la Singida Mashariki na Mhe. John Danielson Pallangyo, Mbunge wa Jimbo la Arumeru Mashariki kwa kuchaguliwa kuwa Wabunge katika chaguzi ndogo zilizofanyika nchini katika mwaka wa fedha 2019/20. Ushindi wao wa kishindo ni kielelezo tosha cha kuonyesha namna Chama cha Mapinduzi kinavyoendelea kuaminika na kupendwa na Watanzania. Vilevile, ninampongeza Dkt. Zainab Abdi Seraphin Chaula kwa kuteuliwa kuwa Katibu Mkuu wa Sekta ya Mawasiliano. 8. Mheshimiwa Spika, mwisho lakini siyo kwa umuhimu, ninapenda kuchukua fursa hii kuishukuru Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu inayoongozwa na Mhe. Seleman Moshi Kakoso (Mb), Mbunge wa Mpanda Vijijini na Makamu Mwenyekiti wa Kamati Mhe. Hawa Mchafu Chakoma (Mb). Nakiri kuwa Wizara imenufaika sana na umahiri, umakini na ushirikiano wa Kamati hiyo katika kuchambua, kushauri na kufuatilia maendeleo ya Sekta za Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Ninapenda kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba maoni, ushauri na mapendekezo yaliyotolewa na Kamati yamezingatiwa katika Bajeti hii. 9. Mheshimiwa Spika, kabla ya kuwasilisha Hotuba hii, ninapenda kuwashukuru Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb), Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango kwa hotuba zao zilizotangulia. Hotuba hizo zimeeleza kwa ujumla maendeleo ya sekta za Kijamii na Kiuchumi kwa mwaka 2019/20 na mwelekeo kwa mwaka 2020/21. Ninawashukuru na kuwapongeza pia Mawaziri wote waliowasilisha hotuba zao. 10. Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo ya utangulizi, ninaomba sasa kuwasilisha hotuba yangu ambayo imejikita katika Utekelezaji wa Mipango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2019/20 pamoja na Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara yangu kwa mwaka wa fedha 2020/21. Aidha, kabla ya kuelezea utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kipindi cha mwaka wa fedha 2019/20, ninapenda nitoe kwa muhtasari taarifa ya utekelezaji wa Ilani 4 ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2015` kwa kipindi cha miaka minne ya Serikali ya Awamu ya Tano. B. UTEKELEZAJI WA MALENGO YALIYOAINISHWA KATIKA ILANI YA UCHAGUZI YA CCM YA MWAKA 2015 KWA KIPINDI CHA MWAKA 2016/17 – 2019/20 B-1 SEKTA YA UJENZI 11. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha kuanzia mwaka 2015 hadi 2020, Serikali kupitia Wizara yangu imepata mafanikio makubwa katika kuboresha miundombinu ya barabara na madaraja kwa kuzingatia vipaumbele ambavyo ni; Kujenga barabara zetu zinazounganisha nchi yetu na nchi jirani, kujenga barabara zinazounganisha mikoa kwa kiwango cha lami na kujenga barabara zinazokwenda kwenye maeneo yenye fursa za kiuchumi. Katika kipindi hicho, barabara zenye urefu wa jumla ya kilometa 2,624.27 zimejengwa na kukamilika kwa kiwango cha lami. Aidha, jumla ya kilometa 82.6 za barabara za kupunguza msongamano wa magari katika miji zimejengwa kwa kiwango cha lami na barabara kuu zenye urefu wa kilometa 1,298.44 zinaendelea kujengwa kwa kiwango cha lami. Vilevile, ukarabati wa barabara kuu zenye urefu wa kilometa 300.9 umekamilika. 12. Mheshimiwa Spika, katika kipindi hicho, jumla ya madaraja makubwa 13 yalikuwa katika hatua mbali mbali za utekelezaji. Kati ya hayo, madaraja makubwa nane (8) yamekamilika, ambayo ni Daraja la Magufuli, Magara, Mlalakuwa, Momba, Lukuledi II, Mara, Sibiti na Daraja la Nyerere (Kigamboni). Aidha, madaraja makubwa matano (5) yapo katika hatua mbalimbali za ujenzi, ambayo ni Daraja Jipya la Selander, Msingi, Wami, Kitengule na Ruhuhu. Madaraja makubwa nane (8) ya Kigongo – Busisi, Sukuma, Simiyu, Mkenda, Mtera, Godegode, Malagarasi Chini na Ugalla yako kwenye hatua mbalimbali za maandalizi ya kazi za ujenzi. 13. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu imekamilisha upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa kilometa 4,856 kwa ajili ya kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami wa barabara kuu na za mikoa pamoja na madaraja mapya 12. Aidha, upembuzi yakinifu wa kilometa 452.3 kwa ajili ya ukarabati wa barabara kuu na za mikoa kwa kiwango cha lami ulikamilika. Vilevile kazi za upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa 5 jumla ya kilometa 3,653.13 upo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. 14. Mheshimiwa Spika, Wizara yangu iliendelea kujenga na kuboresha miundombinu ya viwanja vya ndege nchini. Viwanja vya ndege vilivyokamilika ni: Ujenzi wa Jengo la Tatu la Abiria (Terminal III) katika Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Julius Nyerere (JNIA) pamoja na ukarabati na uboreshaji wa Kiwanja cha Ndege cha Mwanza. Ujenzi wa Kiwanja cha Ndege cha Kimataifa cha Msalato upo katika hatua ya maandalizi ya kuanza utekelezaji. Aidha, Viwanja vya Ndege vya Songea, Kigoma, Shinyanga, Sumbawanga, Tabora, Iringa na Musoma vipo katika hatua mbalimbali za utekelezaji. Vilevile, kati ya viwanja kumi na
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages260 Page
-
File Size-