Tarehe 1 Juni, 2021

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Tarehe 1 Juni, 2021 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Arobaini na Moja – Tarehe 1 Juni, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge leo ni Kikao cha Arobaini na Moja katika Mkutano wetu wa Tatu ambao unaendelea. Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2021/ 2022. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. VITA R. KAWAWA K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu utekelezaji wa majukumu na bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Vita Kawawa. Kwenye Kamati hii ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mheshimiwa Vita Kawawa ni moja ya Wabunge wakongwe kabisa kwenye Kamati ile, alikuwa Mjumbe wakati huo Mwenyekiti wa Kamati akiwa ni Mama Anna Abdallah, kwa hiyo, mpaka leo ni mzoefu kwenye Kamati ya Mambo ya Nje. Ahsante sana Mheshimiwa Vita Kawawa, tunafurahi kuwa nawe. (Makofi/Kicheko) Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 341 Maprofesa wa Kigeni Kufanya Kazi Nchini MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaboresha Sheria ya Ajira na kuweka mazingira mazuri ili maprofesa wa kigeni waweze kufanya kazi nchini? SPIKA: Ahsante sana, majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, aah Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Jenista Mhagama, tafadhali. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Thea Medard Ntara, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali katika kuboresha utoaji ajira kwa wageni ilitunga Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni, Namba 1 ya mwaka 2015 pamoja na Kanuni za Kuratibu Ajira za Wageni za mwaka 2016 ili kuratibu ajira za raia wa kigeni wanaokuja kufanya kazi nchini ikiwa ni pamoja na kulinda ajira za wazawa na kuruhusu ujuzi adimu kutoka nje kuingia na kurithishwa nchini. Serikali kwa sasa inaendelea na mapitio ya sheria ili kuifanyia maboresho kwa kuzingatia mazingira ya sasa. Mheshimiwa Spika, ili kuweka mazingira mazuri ya kuruhusu uwepo wa wafanyakazi wa kigeni nchini, Serikali imeanzisha mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia maombi ya vibali vya kazi na ukaazi kwa raia wa kigeni wanaokuja kufanya kazi nchini na mfumo husika umeanza kutumika kwa majaribio (piloting) kuanzia tarehe 23 Aprili, 2021. Mfumo huu utaongeza Ufanisi katika kushughulikia maombi husika. Mheshimiwa Spika, mfumo huu pia utaondoa changamoto ya upatikanaji wa taarifa unganishi za kisekta za kurahisisha upatikanaji wa vibali vya wageni wakiwemo Maprofesa kwa wakati kwa kuzingatia uhitaji. Mheshimiwa Spika, kulingana kwa taarifa zilizopo mpaka sasa jumla ya vibali vya kazi 74 vimetolewa kwa Maprofesa na Wahadhiri wa Vyuo Vikuu nchini vikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (St. Augustine University) na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Tanzania na vinginevyo. SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Thea nimekuona, swali la nyongeza. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibuyake, lakini niseme tu kwamba mpaka sasa vyuo vikuu vina shida sana ya wahadhili na mfumo huo unachukua muda mrefu mno, yaani mtu anaomba kibali inachukua miezi sita na zaidi. Ni lini watarekebisha na kuona kwamba huo mfumo unakuwa mwepesi ili tupate wahadhili wa kutosha katika vyuo vikuu? Ahsante. (Makofi) SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Jenista Mhagama, tafadhali. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa naomba nimpongeze sana Dkt. Thea Ntara ni mwakilishi wa vyuo vikuu hapa ndani ya Bunge na kwa kweli anaitendea haki sana nafasi yake. (Makofi) Mheshimiwa Spika, tulitambua kwamba mifumo ambayo tulikuwa nayo nyuma ndiyo iliyokuwa ikileta matatizo na kusababisha ucheleweshaji mkubwa sana wa upataji wa vibali vya wageni. Mfumo ambao ninauzungumza ambao upo kwenye piloting kwa sasa ni mfumo mpya na tulipoanza kufanya majaribio kibali kina uwezo wa kutoka ndani ya siku moja ama siku mbili. Naomba tu Mheshimiwa Mbunge awe na amani, tutausimamia vizuri mfumo hu una kuondoa tatizo la upatikanaji wa vibali kwa maprofesa, wahadhili, lakini na wageni wote wanaotaka kupata vibali hapa nchini. (Makofi) SPIKA: Ahsante tunaendelea, nimekuona Mheshimiwa uliza swali la nyongeza. (Kicheko) MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia kuona wasomi, wahadhiri, maprofesa wakiondoka katika taasisi za kufundisha na kuingia katika utumishi mwingine tofauti. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, upi umekuwa mkakati wa Serikali kama succession plan kwamba ikimuondoa profesa fulani mwenye uzoefu fulani katika chuo anaweza kuwa replaced ili kuondoa lile pengo ambalo linakuwa linajitokeza? SPIKA: Waliondoka wachache sana. Mheshimiwa Waziri wa Nchi majibu ya swali hilo tafadhali. Wakina AG wanapoondoka huko. (Kicheko) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana. Mheshimiwa Spika, ndani ya Serikali na hasa kupitia Sheria za Utumishi wa Umma ipo mipango ya succession plan kuhakikisha kwamba ikama za utumishi wa umma zinazingatia mahitaji tuliyonayo nchini. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge asiwe na wasiwasi, tutaendelea kusimamia mifumo tuliyoiweka ya kuzingatia na kulinda ikama ya utumishi wa umma nchini ili kuhakikisha kwamba mapungufu hayapatikani pale ambapo wataalam wanahamia katika masuala mengine ya kiutendaji. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana. Tunaenda TAMISEMI Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile. Na. 342 Gari la Wagonjwa Katika Kituo Cha Afya Mgololo MHE. DAVID M. KIHENZILE aliuliza:- Je, ni lini Serikali italeta gari la wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Mgololo? SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri - TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt. Festo John Dugange, tafadhali. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, ahsante sana na kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile, Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Mgololo kilipatiwa gari la kubeba wagonjwa mwaka 2018 ambalo linalotumika kwa sasa kuhudumia wagonjwa wa dharura kwenye kituo hicho. Hata hivyo, kutokana na udogo wa gari hilo na ugumu wa jiografia ya eneo husika, gari la kubebea wagonjwa lililopo Kituo cha Afya Kasanga hutumika kuhudumia wagonjwa wa dharura inapohitajika. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto ya uhaba wa magari ya kubebea wagonjwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi na kwa kulizingatia hilo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri imenunua gari ya wagonjwa kwa kutumia mapato yake ya ndani lenye thamani ya shilingi milioni 174. Aidha, Halmashauri imefanya matengenezo ya magari mawili ya wagonjwa ambayo yalikuwa mabovu kwa muda mrefu na kufanya Halmashauri kuwa na jumla ya magari matano ya kubebea wagonjwa. Magari haya yanatumika kubeba wagonjwa mara tu dharura zinapotokea katika vituo vya afya vilivyopo Wilayani Mufindi. Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa magari ya wagonjwa ili kuboresha huduma za rufaa Wilayani Mufindi na nchini kwa ujumla, ahsante. SPIKA: Mheshimiwa Kihenzile swali la nyongeza tafadhali. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Spika, nilikuwa naomba Mheshimiwa Naibu Waziri anisaidie kujibu, hicho kituo cha afya kipo mbali sana, kimejitenga ndio kila siku napigia kelele habari za barabara. Atuambie ni lini sasa Serikali itapatia kituo cha afya pale gari ya kubebea wagonjwa kwa sababu ipo mbali sana, ni tofauti na maeneo mengine anayosema? SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri, TAMISEMI tafadhali. NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kihenzile, Mbunge wa Mufindi Kusini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kituo cha afya ambacho gari hilo linatoa huduma kipo mbali na kituo hiki ambacho kinahitaji gari lingine la nyongeza kwa ajili ya kusaidia gari dogo lililopo. Kwa kutambua hilo, Serikali imeona ni busara gari lile liwe standby wakati wowote kusaidia ikitokea kuna dharura pamoja na umbali wakati tunaendelea kutafuta fedha, Serikali kwa kushirikiana na wadau ili tuweze kupata gari kwa ajili ya kuhakikisha linapelekwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie
Recommended publications
  • Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 BUNGE LA TANZANIA
    Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ________________________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Kumi na Tisa – Tarehe 27 Mei, 2014 (Mkutano Ulianza Saa tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha kwa Mwaka 2012/2013 (The Annual Report and Accounts of Arusha International Conference Centre for the Year 2012/2013). Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. BETTY E. MACHANGU (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na Maoni ya Kamati 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. ABDULKARIM E.H. SHAH (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015.
    [Show full text]
  • Hotuba Ya Mgeni Rasmi Mhe. Kassim Majaliwa Majaliwa (Mb) Waziri Mkuu Wa Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Katika Ufunguzi Wa Mkuta
    HOTUBA YA MGENI RASMI MHE. KASSIM MAJALIWA MAJALIWA (MB) WAZIRI MKUU WA JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA KATIKA UFUNGUZI WA MKUTANO WA MWAKA WA WADAU WA LISHE, SEPTEMBA 10, 2019 Mheshimiwa Jenista Mhagama (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na wenye Ulemavu, Mheshimiwa Ummy Mwalimu (Mb), Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Suleiman Jafo (Mb), Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Mheshimiwa Prof. Joyce Ndalichako (Mb), Waziri wa Elimu, Sayansi, Teknolojia na Mafunzo ya Ufundi, Mheshimiwa Dkt. Philip Mpango (Mb), Waziri wa Fedha na Mipango. Mheshimiwa Japhet Hasunga (Mb), Waziri wa Kilimo, Mheshimiwa Luhaga Mpina (Mb), Waziri wa Mifugo na Uvuvi, Mheshimiwa Innocent Bashungwa (Mb), Waziri wa Viwanda, Biashara na Uwezeshaji, Mheshimiwa Prof. Makame Mbarawa (Mb), Waziri wa Maji na Umwagiliaji. Mheshimiwa Doto Biteko (Mb), Waziri wa Madini, Waheshimiwa Manaibu Waziri na Makatibu Wakuu, Mheshimiwa Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Dkt. Bilinith Mahenge; pamoja na viongozi wengine wa ngazi za Mkoa na Halmashauri mliopo, Waheshimiwa Wabunge na viongozi wa Vyama vya Siasa, Waheshimiwa Mabalozi wanaoziwakilisha nchi mbalimbali, Ndugu Viongozi waandamizi wa Idara, Taasisi, Wakala za Serikali, Wakuu wa Vyuo vya Elimu ya Juu, Wawakilishi wa Mashirika ya Kimataifa, Wadau wa Maendeleo na Asasi za Kiraia, 1 Ndugu Mkurugenzi Mtendaji wa Taasisi ya Chakula na Lishe Tanzania, Ndugu Wageni Waalikwa, Waandishi wa habari na wadau wote wa Lishe, Mabibi na Mabwana. Habari za asubuhi Kwa mara nyingine tena nina furaha kubwa sana kujumuika na wadau wa lishe siku hii ya leo. Hii ni mara yangu ya tatu kuhudhuria mkutano wa mwaka wa wadau wa lishe nchini na hivyo nahisi kuwa mwanafamilia wa wadau waliohamasika katika masuala ya lishe.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    NAKALA YA MTANDAO (ON LINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ BUNGE LA KUMI NA MOJA ___________ MKUTANO WA KWANZA Kikao cha Kwanza - Tarehe 17 Novemba, 2015 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) DKT. THOMAS D. KASHILILAH - KATIBU WA BUNGE: Naomba tukae. TANGAZO LA RAIS LA KUITISHA MKUTANO WA BUNGE DKT. THOMAS D. KASHILILAH - KATIBU WA BUNGE: Waheshimiwa Wabunge, kwa mujibu wa masharti ya Katiba, Mkutano huu wa Kwanza unaanza kwa Rais kuuitisha. Naomba kuchukua nafasi hii kusoma Tangazo la Rais kama ambavyo tumelipokea. Tangazo la Serikali Na. 513 la tarehe 6 Novemba, 2015. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Sura ya Pili, hati iliyotolewa kwa mujibu wa Ibara ya 90(1). Hati ya Kuitisha Mkutano wa Bunge Jipya. KWA KUWA, Uchaguzi Mkuu ulifanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; NA KWA KUWA, masharti ya Ibara ndogo ya kwanza ya Ibara ya 90 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, yanamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuitisha Mkutano wa Bunge Jipya kabla ya kupita siku saba tangu Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu; NA KWA KUWA, matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 yalitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tarehe 29 Oktoba, 2015; HIVYO BASI, mimi John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mamlaka niliyonayo chini ya Ibara ya 90(1) ya 1 NAKALA YA MTANDAO (ON LINE DOCUMENT) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, naitisha Mkutano wa Bunge Jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ufanyike katika ukumbi wa Bunge uliopo Mjini Dodoma tarehe 17 Novemba, 2015 kuanzia saa tatu asubuhi.
    [Show full text]
  • Ruaha Journal of Business, Economics and Management Sciences, Vol.1, Issue 1, 2018  Ms Hadija Matimbwa , Faculty of Business and Management Science, RUCU Iii
    RUAHA JOURNAL of Business, Economics and Management Sciences Faculty of Business and Management Sciences Vol 1, Issue 1, 2018 A. Editorial Board i. Executive Secretarial Members Chairman: Dr. Alex Juma Ochumbo, Dean Faculty of Business and Management Sciences, RUCU Chief Editor: Prof. Robert Mabele, Faculty of Business and Management Sciences, RUCU Managing Editor: Dr.Venance Ndalichako, Faculty of Business and Management Sciences, RUCU Business Manager: Dr. Alberto Gabriel Ndekwa, Faculty of Business and Management Science, RUCU Secretary to the Board: Ms. Hawa Jumanne,Faculty of Business and Management Science, RUCU ii. Members of the Editorial Board Dr. Dominicus Kasilo, Faculty of Business and Management Science, RUCU Bishop Dr. Edward Johnson Mwaikali,Bishop of Mbeya, Formerly with RUCU Dr. Theobard Kipilimba, Faculty of Business and Management Science, RUCU Dr. Esther Ikasu, Faculty of Business and Management Science, RUCU ii Ruaha Journal of Business, Economics and Management Sciences, Vol.1, Issue 1, 2018 Ms Hadija Matimbwa , Faculty of Business and Management Science, RUCU iii. Associate Editors Prof. Enock Wicketye Iringa University,Tanzania. Dr. Enery Challu University of Dar es Dr. Ernest Abayo Makerere University, Uganda. Dr. Vicent Leyaro University of Dar es Salaam Dr. Hawa Tundui Mzumbe University, Tanzania. B. Editorial Note Ruaha Journal of Business, Economics and Management Sciences would like to wish all our esteemed readers on this first appearance A HAPPY NEW YEAR. We shall be appearing twice a year January and July. We hope you will be able to help us fulfill this pledge by feeding us with journal articles, book reviews and other such journal writings and stand ready to read from cover to cover all our issues.
    [Show full text]
  • 2019 Tanzania in Figures
    2019 Tanzania in Figures The United Republic of Tanzania 2019 TANZANIA IN FIGURES National Bureau of Statistics Dodoma June 2020 H. E. Dr. John Pombe Joseph Magufuli President of the United Republic of Tanzania “Statistics are very vital in the development of any country particularly when they are of good quality since they enable government to understand the needs of its people, set goals and formulate development programmes and monitor their implementation” H.E. Dr. John Pombe Joseph Magufuli the President of the United Republic of Tanzania at the foundation stone-laying ceremony for the new NBS offices in Dodoma December, 2017. What is the importance of statistics in your daily life? “Statistical information is very important as it helps a person to do things in an organizational way with greater precision unlike when one does not have. In my business, for example, statistics help me know where I can get raw materials, get to know the number of my customers and help me prepare products accordingly. Indeed, the numbers show the trend of my business which allows me to predict the future. My customers are both locals and foreigners who yearly visit the region. In June every year, I gather information from various institutions which receive foreign visitors here in Dodoma. With estimated number of visitors in hand, it gives me ample time to prepare products for my clients’ satisfaction. In terms of my daily life, Statistics help me in understanding my daily household needs hence make proper expenditures.” Mr. Kulwa James Zimba, Artist, Sixth street Dodoma.”. What is the importance of statistics in your daily life? “Statistical Data is useful for development at family as well as national level because without statistics one cannot plan and implement development plans properly.
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 114 May - Aug 2016
    Tanzanian Affairs Issued by the Britain-Tanzania Society No 114 May - Aug 2016 Magufuli’s “Cleansing” Operation Zanzibar Election Re-run Nyerere Bridge Opens David Brewin: MAGUFULI’S “CLEANSING” OPERATION President Magufuli helps clean the street outside State House in Dec 2015 (photo State House) The seemingly tireless new President Magufuli of Tanzania has started his term of office with a number of spectacular measures most of which are not only proving extremely popular in Tanzania but also attracting interest in other East African countries and beyond. It could be described as a huge ‘cleansing’ operation in which the main features include: a drive to eliminate corruption (in response to widespread demands from the electorate during the November 2015 elections); a cutting out of elements of low priority in the expenditure of government funds; and a better work ethic amongst government employees. The President has changed so many policies and practices since tak- ing office in November 2015 that it is difficult for a small journal like ‘Tanzanian Affairs’ to cover them adequately. He is, of course, operat- ing through, and with the help of ministers, regional commissioners and cover photo: The new Nyerere Bridge in Dar es Salaam (see Transport) Magufuli’s “Cleansing” Operation 3 others, who have been either kept on or brought in as replacements for those removed in various purges of existing personnel. Changes under the new President The following is a list of some of the President’s changes. Some were not carried out by him directly but by subordinates. It is clear however where the inspiration for them came from.
    [Show full text]
  • Bunge Newsletter
    BungeNe ewsletter Issue No 008 June 2013 New Budget Cycle Shows Relavance For the first time in recent Tanzania history the engage the government and influence it make sev- Parliament has managed to pass the next financial eral tangible changes in its initial budget proposals. year budget before the onset of that particular year. This has been made possible by the Budget Commit- This has been made possi- tee, another new innovation by Speaker Makinda. ble by adoption of new budget cycle. Under the old cycle, it was not possible to influence According to the new budget cycle, the Parliament the government to make changes in budgetary allo- starts discussing the budget in April as opposed to cations. That was because the main budget was read, old cycle where debate on the new budget started on debated and passed before the sectoral plans. After June and ends in the first or second week of August. the main budget was passed, it was impossible for the MPs and government to make changes in the When the decision was taken to implement the new sectoral budgets since they were supposed to reflect budget cycle and Speaker Anne Makinda announced the main budget which had already been passed. the new modalities many people, including Mem- bers of Parliament, were skeptical. Many stakehold- These and many other changes have been made possi- ers were not so sure that the new cycle would work. ble through the five components implemented under the Parliament five years development plan. “Govern- But Ms Makinda has managed to prove the doubt- ment and Budget Oversight and Accountability is one ers wrong.
    [Show full text]
  • By Martin Sturmer First Published by Ndanda Mission Press 1998 ISBN 9976 63 592 3 Revised Edition 2008 Document Provided by Afrika.Info
    THE MEDIA HISTORY OF TANZANIA by Martin Sturmer first published by Ndanda Mission Press 1998 ISBN 9976 63 592 3 revised edition 2008 document provided by afrika.info I Preface The media industry in Tanzania has gone through four major phases. There were the German colonial media established to serve communication interests (and needs) of the German administration. By the same time, missionaries tried to fulfil their tasks by editing a number of papers. There were the media of the British administration established as propaganda tool to support the colonial regime, and later the nationalists’ media established to agitate for self-governance and respect for human rights. There was the post colonial phase where the then socialist regime of independent Tanzania sought to „Tanzanianize“ the media - the aim being to curb opposition and foster development of socialistic principles. There was the transition phase where both economic and political changes world-wide had necessitated change in the operation of the media industry. This is the phase when a private and independent press was established in Tanzania. Martin Sturmer goes through all these phases and comprehensively brings together what we have not had in Tanzania before: A researched work of the whole media history in Tanzania. Understanding media history in any society is - in itself - understanding a society’s political, economic and social history. It is due to this fact then, that we in Tanzania - particularly in the media industry - find it plausible to have such a work at this material time. This publication will be very helpful especially to students of journalism, media organs, university scholars, various researchers and even the general public.
    [Show full text]
  • Madini News Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Toleo Na.2 Wa Tanzania Machi, 2020 HALIUZWI
    Toleo Na.2 // Machi 2020 Yaliyomo // Biteko - Nitasimama na Mzee Tume ya Leseni ya TanzaniteOne Imefutwa na Kisangani mpaka “asimame” Kurudishwa Serikalini - Biteko... Uk.04 ... Uk.08 Madini Bilioni 66.5 zapatikana tangu Wanawake Tume ya Madini kuanzishwa kwa masoko Wawakumbuka ya madini ... Uk.10 Yatima ... Uk.18 www.tumemadini.go.tz Tume ya Madini 2020 www.tumemadini.go.tz /TAHARIRI Salamu Kutoka kwa Waziri wa Madini Maoni ya Mhariri SEKTA YA MADINI INAIMARIKA, MAFANIKIO MASOKO TUENDELEZE USHIRIKIANO YA MADINI TUMEWEZA! Katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Wizara ya Madini ilipanga kutekeleza majukumu yake kupitia miradi Katika kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mbalimbali ikilenga katika kuimarisha Sekta ya Madini, hivyo kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa Taifa, Serikali kupitia uchumi wa nchi. Tume ya Madini kuanzia Machi, 2019 ilifungua masoko ya madini Katika Toleo lililopita nilielezea kwa kifupi kuhusu yale ambayo yamesimamiwa na kutekelezwa na Wizara na vituo vya ununuzi wa madini lengo likiwa ni kudhibiti utorosh- kwa kipindi cha takribani miaka miwili tangu kuanzishwa kwake. waji wa madini kwa kuwapatia wachimbaji wa madini nchini Katika Toleo hili nitaelezea kwa kifupi mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kipindi cha sehemu ya kuuzia madini yao huku wakilipa kodi mbalimbali kuanzia Julai, 2019 hadi Februari, 2020. Kama ambavyo nilieleza Bungeni katika Hotuba yangu wakati Serikalini. nikiwasilisha Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2019/2020, nilieleza kuwa, Wizara imepangiwa kukusanya Shilingi 470,897,011,000.00 katika Mwaka wa Fedha 2019/2020. Uanzishwaji wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa Napenda kuwataarifu wasomaji wa Jarida hili kuwa, hadi kufikia Februari, 2020 jumla ya Shilingi madini ni sehemu ya maelekezo yaliyotolewa kwenye mkutano wa 319,025,339,704.73 zimekusanywa ambazo ni sawa na asilimia 102 ya lengo la makusanyo ya nusu mwaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania, Dkt.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Ishirini na Tano - Tarehe 16 Julai, 2003 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Pius Msekwa) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA ELIMU YA JUU: Hotuba ya Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu kwa Mwaka wa Fedha 2003/2004. MHE. MARGARETH A. MKANGA (k.n.y. MHE. OMAR S. KWAANGW’ - MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII): Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu katika mwaka uliopita, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2003/2004. MASWALI NA MAJIBU Na. 239 Majimbo ya Uchaguzi MHE. JAMES P. MUSALIKA (k.n.y. MHE. DR. WILLIAM F. SHIJA) aliuliza:- Kwa kuwa baadhi ya Majimbo ya Uchaguzi ni makubwa sana kijiografia na kwa wingi wa watu; je, Serikali itashauriana na Tume ya Uchaguzi ili kuongeza Majimbo ya Uchaguzi katika baadhi ya maeneo nchini katika Uchaguzi wa mwaka 2005? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (MHE. MUHAMMED SEIF KHATIB) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Dr. William Shija, Mbunge wa Sengerema, naomba kutoa maelezo yafuatayo:- Mheshimiwa Spika, lilipokuwa linajibiwa swali la Mheshimiwa Ireneus Ngwatura, Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi na pia swali la Mheshimiwa Sophia Simba, Mbunge wa Viti Maalum, CCM 1 katika Mikutano ya Saba na Kumi na Moja sawia ya Bungeni, nilieleza kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 75(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungao wa Tanzania 1977, Jamhuri ya Muungano inaweza kugawanywa katika Majimbo ya Uchaguzi kwa idadi na namna itakavyoamuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kupata kibali cha Mheshimiwa Rais.
    [Show full text]
  • Republic of Burundi United Republic of Tanzania Joint
    1 REPUBLIC OF BURUNDI UNITED REPUBLIC OF TANZANIA JOINT COMMUNIQUE ON THE OCCASION OF THE STATE VISIT TO THE REPUBLIC OF BURUNDI BY HER EXCELLENCY SAMIA SULUHU HASSAN, PRESIDENT OF THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA FROM 16th TO 17th JULY 2021 ---------------------------------------------------------------------------------------------------------- 1. At the invitation of His Excellency Evariste Ndayishimiye, President of the Republic of Burundi, Her Excellency Samia Suluhu Hassan, President of the United Republic of Tanzania, undertook a State Visit to the Republic of Burundi from 16th to 17th July 2021. 2. Her Excellency Samia Suluhu Hassan led a high-level delegation including Ministers and other senior governmental officials of the United Republic of Tanzania. 3. The President of the United Republic of Tanzania expressed her gratitude to His Excellency Evariste NDAYISHIMIYE, President of the Republic of Burundi, the Government and the people of Burundi for the warm welcome extended to her and her delegation during her first and historic State visit to Burundi. 4. The two Heads of State noted with satisfaction and commended the existing excellent bilateral ties between the two countries that have a historic, solid foundation. 5. The two Leaders reaffirmed their shared commitment to strengthen the spirit of solidarity and cooperation in various sectors of common interest between the two Governments and peoples. 2 6. During her State visit, Her Excellency Samia Suluhu Hassan visited FOMI, an organic fertilizer industry in Burundi and the CRDB Bank on 16th July 2021. 7. At the beginning of the bilateral talks, the two Heads of State paid tribute to the Late Excellency Pierre Nkurunziza, former President of the Republic of Burundi, the Late Excellency Benjamin William Mkapa, the third President of the United Republic of Tanzania and the Late Excellency John Pombe Joseph Magufuli, the fifth President of the United Republic of Tanzania.
    [Show full text]
  • Tarehe 30 Juni, 2017
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Hamsini na Saba – Tarehe 30 Juni, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Tunaendelea na Mkutano wetu wa Saba, leo ni Kikao cha Hamsini na Saba. Katibu! NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na Ofisi ya Mheshimiwa Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Swali la kwanza linaulizwa na Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo, Mbunge wa Maswa Mashariki. Mheshimiwa Nyongo. Na. 468 Mikopo kwa Walimu Kwa Ajili ya Ujenzi wa Nyumba MHE. STANSLAUS H. NYONGO aliuliza:- Walimu Wilayani Maswa wana uhaba wa nyumba za kuishi; pamoja na juhudi za wananchi kujenga nyumba za walimu wa shule za msingi na sekondari lakini walimu hao bado wanahitaji kujenga nyumba zao wenyewe za kudumu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, ni lini Serikali itaweka utaratibu maalum wa kutoa mikopo kwa walimu hao ili wajenge nyumba zao binafsi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Stanslaus Haroon Nyongo, Mbunge wa Maswa Mashariki kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ina uhitaji wa nyumba za walimu 1,358. Nyumba zilizopo ni 479 na hivyo upungufu ni nyumba 879. Mheshimiwa Spika, kutokana na upungufu huu Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Maswa ina mpango wa kujenga nyumba 16 katika mwaka wa fedha 2017/2018. Aidha, kati ya nyumba hizo, nyumba nane zitajengwa kwa bajeti ya 2017/2018 (CDG) na nyumba nyingine nane zitajengwa kwa kutumia mapato ya ndani y (own source) ya Halmashauri.
    [Show full text]