Tarehe 1 Juni, 2021

Tarehe 1 Juni, 2021

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Arobaini na Moja – Tarehe 1 Juni, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge leo ni Kikao cha Arobaini na Moja katika Mkutano wetu wa Tatu ambao unaendelea. Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2021/ 2022. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. VITA R. KAWAWA K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu utekelezaji wa majukumu na bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Vita Kawawa. Kwenye Kamati hii ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Mheshimiwa Vita Kawawa ni moja ya Wabunge wakongwe kabisa kwenye Kamati ile, alikuwa Mjumbe wakati huo Mwenyekiti wa Kamati akiwa ni Mama Anna Abdallah, kwa hiyo, mpaka leo ni mzoefu kwenye Kamati ya Mambo ya Nje. Ahsante sana Mheshimiwa Vita Kawawa, tunafurahi kuwa nawe. (Makofi/Kicheko) Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 341 Maprofesa wa Kigeni Kufanya Kazi Nchini MHE. DKT. THEA M. NTARA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itaboresha Sheria ya Ajira na kuweka mazingira mazuri ili maprofesa wa kigeni waweze kufanya kazi nchini? SPIKA: Ahsante sana, majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, aah Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Jenista Mhagama, tafadhali. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Thea Medard Ntara, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali katika kuboresha utoaji ajira kwa wageni ilitunga Sheria ya Kuratibu Ajira za Wageni, Namba 1 ya mwaka 2015 pamoja na Kanuni za Kuratibu Ajira za Wageni za mwaka 2016 ili kuratibu ajira za raia wa kigeni wanaokuja kufanya kazi nchini ikiwa ni pamoja na kulinda ajira za wazawa na kuruhusu ujuzi adimu kutoka nje kuingia na kurithishwa nchini. Serikali kwa sasa inaendelea na mapitio ya sheria ili kuifanyia maboresho kwa kuzingatia mazingira ya sasa. Mheshimiwa Spika, ili kuweka mazingira mazuri ya kuruhusu uwepo wa wafanyakazi wa kigeni nchini, Serikali imeanzisha mfumo wa kielektroniki wa kushughulikia maombi ya vibali vya kazi na ukaazi kwa raia wa kigeni wanaokuja kufanya kazi nchini na mfumo husika umeanza kutumika kwa majaribio (piloting) kuanzia tarehe 23 Aprili, 2021. Mfumo huu utaongeza Ufanisi katika kushughulikia maombi husika. Mheshimiwa Spika, mfumo huu pia utaondoa changamoto ya upatikanaji wa taarifa unganishi za kisekta za kurahisisha upatikanaji wa vibali vya wageni wakiwemo Maprofesa kwa wakati kwa kuzingatia uhitaji. Mheshimiwa Spika, kulingana kwa taarifa zilizopo mpaka sasa jumla ya vibali vya kazi 74 vimetolewa kwa Maprofesa na Wahadhiri wa Vyuo Vikuu nchini vikiwemo Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Chuo Kikuu cha Dodoma, Chuo Kikuu cha Mtakatifu Agustino (St. Augustine University) na Chuo Kikuu cha Mtakatifu Joseph Tanzania na vinginevyo. SPIKA: Mheshimiwa Dkt. Thea nimekuona, swali la nyongeza. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. DKT. THEA M. NTARA: Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibuyake, lakini niseme tu kwamba mpaka sasa vyuo vikuu vina shida sana ya wahadhili na mfumo huo unachukua muda mrefu mno, yaani mtu anaomba kibali inachukua miezi sita na zaidi. Ni lini watarekebisha na kuona kwamba huo mfumo unakuwa mwepesi ili tupate wahadhili wa kutosha katika vyuo vikuu? Ahsante. (Makofi) SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Jenista Mhagama, tafadhali. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa naomba nimpongeze sana Dkt. Thea Ntara ni mwakilishi wa vyuo vikuu hapa ndani ya Bunge na kwa kweli anaitendea haki sana nafasi yake. (Makofi) Mheshimiwa Spika, tulitambua kwamba mifumo ambayo tulikuwa nayo nyuma ndiyo iliyokuwa ikileta matatizo na kusababisha ucheleweshaji mkubwa sana wa upataji wa vibali vya wageni. Mfumo ambao ninauzungumza ambao upo kwenye piloting kwa sasa ni mfumo mpya na tulipoanza kufanya majaribio kibali kina uwezo wa kutoka ndani ya siku moja ama siku mbili. Naomba tu Mheshimiwa Mbunge awe na amani, tutausimamia vizuri mfumo hu una kuondoa tatizo la upatikanaji wa vibali kwa maprofesa, wahadhili, lakini na wageni wote wanaotaka kupata vibali hapa nchini. (Makofi) SPIKA: Ahsante tunaendelea, nimekuona Mheshimiwa uliza swali la nyongeza. (Kicheko) MHE. ANATROPIA L. THEONEST: Mheshimiwa Spika, nakushukuru, katika siku za hivi karibuni tumeshuhudia kuona wasomi, wahadhiri, maprofesa wakiondoka katika taasisi za kufundisha na kuingia katika utumishi mwingine tofauti. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, upi umekuwa mkakati wa Serikali kama succession plan kwamba ikimuondoa profesa fulani mwenye uzoefu fulani katika chuo anaweza kuwa replaced ili kuondoa lile pengo ambalo linakuwa linajitokeza? SPIKA: Waliondoka wachache sana. Mheshimiwa Waziri wa Nchi majibu ya swali hilo tafadhali. Wakina AG wanapoondoka huko. (Kicheko) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Mheshimiwa Spika, ninakushukuru sana. Mheshimiwa Spika, ndani ya Serikali na hasa kupitia Sheria za Utumishi wa Umma ipo mipango ya succession plan kuhakikisha kwamba ikama za utumishi wa umma zinazingatia mahitaji tuliyonayo nchini. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge asiwe na wasiwasi, tutaendelea kusimamia mifumo tuliyoiweka ya kuzingatia na kulinda ikama ya utumishi wa umma nchini ili kuhakikisha kwamba mapungufu hayapatikani pale ambapo wataalam wanahamia katika masuala mengine ya kiutendaji. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana. Tunaenda TAMISEMI Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile. Na. 342 Gari la Wagonjwa Katika Kituo Cha Afya Mgololo MHE. DAVID M. KIHENZILE aliuliza:- Je, ni lini Serikali italeta gari la wagonjwa katika Kituo cha Afya cha Mgololo? SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri - TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt. Festo John Dugange, tafadhali. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, ahsante sana na kwa niaba ya Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais - TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa David Mwakiposa Kihenzile, Mbunge wa Jimbo la Mufindi Kusini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Kituo cha Afya Mgololo kilipatiwa gari la kubeba wagonjwa mwaka 2018 ambalo linalotumika kwa sasa kuhudumia wagonjwa wa dharura kwenye kituo hicho. Hata hivyo, kutokana na udogo wa gari hilo na ugumu wa jiografia ya eneo husika, gari la kubebea wagonjwa lililopo Kituo cha Afya Kasanga hutumika kuhudumia wagonjwa wa dharura inapohitajika. Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua changamoto ya uhaba wa magari ya kubebea wagonjwa kwenye vituo vya kutolea huduma za afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi na kwa kulizingatia hilo kwa mwaka wa fedha 2020/2021 Halmashauri imenunua gari ya wagonjwa kwa kutumia mapato yake ya ndani lenye thamani ya shilingi milioni 174. Aidha, Halmashauri imefanya matengenezo ya magari mawili ya wagonjwa ambayo yalikuwa mabovu kwa muda mrefu na kufanya Halmashauri kuwa na jumla ya magari matano ya kubebea wagonjwa. Magari haya yanatumika kubeba wagonjwa mara tu dharura zinapotokea katika vituo vya afya vilivyopo Wilayani Mufindi. Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na wadau mbalimbali wa maendeleo itaendelea kutenga fedha kwa ajili ya ununuzi wa magari ya wagonjwa ili kuboresha huduma za rufaa Wilayani Mufindi na nchini kwa ujumla, ahsante. SPIKA: Mheshimiwa Kihenzile swali la nyongeza tafadhali. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. DAVID M. KIHENZILE: Mheshimiwa Spika, nilikuwa naomba Mheshimiwa Naibu Waziri anisaidie kujibu, hicho kituo cha afya kipo mbali sana, kimejitenga ndio kila siku napigia kelele habari za barabara. Atuambie ni lini sasa Serikali itapatia kituo cha afya pale gari ya kubebea wagonjwa kwa sababu ipo mbali sana, ni tofauti na maeneo mengine anayosema? SPIKA: Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Naibu Waziri, TAMISEMI tafadhali. NAIBU WAZIRI OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Kihenzile, Mbunge wa Mufindi Kusini kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kituo cha afya ambacho gari hilo linatoa huduma kipo mbali na kituo hiki ambacho kinahitaji gari lingine la nyongeza kwa ajili ya kusaidia gari dogo lililopo. Kwa kutambua hilo, Serikali imeona ni busara gari lile liwe standby wakati wowote kusaidia ikitokea kuna dharura pamoja na umbali wakati tunaendelea kutafuta fedha, Serikali kwa kushirikiana na wadau ili tuweze kupata gari kwa ajili ya kuhakikisha linapelekwa kwenye Halmashauri ya Wilaya ya Mufindi. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nimhakikishie

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    274 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us