MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao Cha Tisa – Tarehe 13 Aprili, 2
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Tisa – Tarehe 13 Aprili, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae, Katibu. NDG. PAMELA PALLANGYO – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 68 Huduma ya Upasuaji – Kituo cha Afya Kala MHE. DESDERIUS J. MIPATA aliuliza:- Serikali kupitia Mradi wa Mfuko wa Benjamin Mkapa ilidhamiria kujenga na kukamilisha huduma ya upasuaji kwenye Kituo cha Afya cha Kata ya Kala na baada ya mfuko huo kuacha shughuli zake hakuna juhudi inayoendelea. (a) Je, kuna mpango wowote kuendeleza nia hiyo njema? (b) Kwa kuwa kituo hicho kina upungufu mkubwa wa wataalam; je, Serikali ina mpango gani wa kuongeza watumishi wakiwepo wauguzi? 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa za Serikali za Mitaa, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Desderius John Mipata, Mbunge wa Nkasi Kusini lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Wilaya ya Nkasi ina vituo vya afya saba, kati ya hivyo vituo vinne vinamilikiwa na taasisi za kidini na vitu vitatu vinamilikiwa na Serikali. Vituo vya afya viwili vinavyomilikiwa na Serikali vinatoa huduma za upasuaji. Kituo cha Afya Kala kinamilikiwa na Kanisa Katoliki Jimbo la Sumbawanga. Taasisi ya Benjamin Mkapa ilijenga chumba cha upasuaji (theatre) pamoja na kutoa baadhi ya vifaa kwa ajili ya huduma za upasuaji katika Kituo cha Afya Kala mnamo mwaka 2016/2017. Hata hivyo, huduma hizo zimekuwa hazitolewi kutokana na changamoto mbalimbali kubwa zikiwa ni upatikanaji wa wataalam kwa ajili ya kufanya huduma za upasuaji na kukosekana kwa huduma ya umeme na mfumo wa maji kwa ajili ya kuendeshea shughuli za upasuaji. Ili kukabiliana na hali hiyo Halmashauri imetenga kiasi cha shilingi milioni 17.3 katika mwaka wa fedha 2017/2018, kwa ajili ya miundombinu ya maji na umeme ambapo fedha hiyo bado haijapokelewa. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana na upungufu wa watumishi katika Kituo cha Afya Kala, Halmashauri ilipeleka tabibu mmoja na wauguzi wawili ili kutoa huduma katika kituo hicho mwaka 2015. Aidha, Halmashauri ilipeleka gari moja la wagonjwa lenye namba za usajili SM 4467 mwaka 2017 kutoa huduma katika kituo hicho. Serikali itaendelea kupeleka wataalam wa afya katika kituo hicho kwa kadri watakavyopatikana. Serikali inaendelea kufanya mazungumzo na wamiliki wa Kituo cha Afya Kala ili kushirikiana katika kutatua changamoto ya 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) watumishi katika kituo hicho kwa kuwa watumishi watatu waliopo sasa katika kituo hicho wote wameajiriwa na Serikali. MWENYEKITI: Mheshimiwa Mipata. MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana kunipa nafasi pamoja na majibu ya Serikali, naomba nieleze kwamba gari lililopo Kituo cha Afya Kala ni bovu sana na halifanyi kazi na Kala ipo umbali wa kilometa 150; hakuna mawasiliano yoyote ya simu wala barabara haifai. Nina maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, kutokana na changamoto mbalimbali zinazojitokeza kwenye huduma za afya zinazotolewa kwenye vituo vyenye udau wa Serikali na wadau wengine, wananchi wa Kala wameamua kujenga kituo cha afya kwenye Kijiji cha King’ombe wao wenyewe, lakini vilevile wako wananchi wengine wameamua kujenga kutoka kwenye kata zao, Kata ya Ninde, Kata Kate na Kata ya Nkandasi. Je, Serikali iko tayari kuunga mkono juhudi hizi za wananchi? Swali la pili Waziri wa Afya alipotembelea kwetu alituahidi kutupata shilingi milioni 400 kwenye Kituo cha Afya cha Wampembe na mpaka sasa sijaona fedha hiyo zimeonekana katika vitabu mbalimbali, lakini pia hatujazipokea; je, Serikali bado ina mpango huo wa kutupatia pesa katika Kituo hicho cha Wampembe? (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nichukue fursa hii kuwapongeza wananchi kwa dhati kwa moyo wao wa kujitoa kuhakikisha kwamba vinajengwa vituo vya afya baada ya kuona kwamba changamoto ya kuwa katika hivi vya ubia inawakabili. Katika Serikali kuunga jitihada za wananchi naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge katika pesa 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ambayo inatarajiwa kupatikana muda si mrefu Kituo cha Afya Kasu nacho ni miongozi mwa vituo vya afya ambavyo vinaenda kupatiwa fedha ili viweze kujengwa na kuweza kutoa huduma ambazo wananchi wanatarajia. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika swali lake la pili ameniambia kwamba Mheshimiwa Waziri wa Afya alivyoenda baada ya kuona changamoto kwa wananchi wa Wampembe aliahidi kituo hicho kingeweza kupatiwa jumla ya shilingi milioni 400 ili kiweze kupanuliwa. Naomba nimhakikishie kwamba ahadi hiyo bado ni thabiti ni suala la tu la muda, pesa ikipatikana hatutasahau. Mheshimiwa Mwenyekiti, pia kwa ujumla wake naomba uniruhusu, unajua unapokuwa na Waheshimiwa Wabunge ambao wako kwenye Halmashauri moja na majimbo yako mawili ni sawa na ambavyo unapokuwa na watoto mapacha. Ni wajibu wako kuhakikisha kwamba unakuwa na balancing ambalo kama Serikali tunaenda kulifanya. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Paresso. MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niweze kuuliza swali dogo la nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imetoa waraka wa kusitisha taratibu wa upandishwaji wa baadhi ya zahanati kwenda vituo vituo vya afya ikitaka vituo vya afya vijengwe kwenye kila kata, lakini kwamba Halmashauri zetu hazina fedha za uhakika za kujenga lakini hata wananchi wenyewe hali ya uchumi ni ngumu kuweza kujenga vituo hivyo vya afya. Je, Serikali kwa nini msifikirie kwa upya kubatilisha uamuzi huo na kuangalia zile zahanati ambazo kwa kweli zinakidhi haja ziweze kupandishwa kuwa vituo vya afya? MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri kwa kifupi. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, juu ya suala zima la kupandisha zahanati kuwa vituo vya afya, kwanza naomba tukubaliane, zahanati zina ramani zake na vituo vya afya vina ramani zake. Hoja ya msingi ni kwamba tungependa wananchi wapate huduma ya afya jirani sana, naomba kwa sababu mpaka sasa hivi tulikuwa tunaongelea tuna asilimia 12 tu ya vituo vya afya na bado na uhitaji wa zahanati bado uhitaji ni mkubwa. Naomba azma hiyo ya Serikali yakuhakikisha kwamba kila kijiji kinakuwa na zahanati na kila Kata kunakuwa na kituo cha afya bado ndio msimamo wa Serikali na wananchi waendelee kushiriki ili tuhakikishe kwamba huduma hii ina inawasogelea wananchi kwa karibu. MWENYEKITI: Ahsante. Tunaendelea Wizara ya Afya na Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mheshimiwa Aida Joseph Khenani. Na. 69 Uhaba wa Vitanda katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa MHE. AIDA J. KHENANI aliuliza:- Katika Hospitali ya Rufaa ya Rukwa kumekuwepo na tatizo la wanawake wajawazito na waliojifungua kulazwa katika kitanda kimoja. Je, Serikali ina mkakati gani wa kumaliza tatizo hilo katika hospitali hiyo? NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee, Watoto, naomba kujibu 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) swali la Mheshimiwa Aida Joseph Khenani, Mbunge, Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kumekuwa na changamoto ya akina mama wajawazito na waliojifungua kulala katika kitanda kimoja inayochangiwa na ufinyu wa nafasi katika jengo la wazazi lililopo kutokana na ongezeko la idadi ya watumiaji wa huduma hizi hasa kwa kuwa hospitali hii ilianza kama kituo cha afya mwaka 1974. Vilevile tatizo hili linachangiwa na ukosefu wa Hospitali za Wilaya katika Halmashauri za Kalambo na Sumbawanga hali inayosababisha Hospitali ya Rufaa ya Mkoa kuhudumia wateja wote wanaotoka kwenye halmashauri zote mbili. Mheshimiwa, Mwenyekiti, Wizara imeweka mikakati ya ufumbuzi wa changamoto hii kama ifuatavyo:- (i) Kupitia Mpango Kabambe wa Hospitali wa mwaka 2017/2018 yaani Comprehensive Hospital Operation Plan, Wizara imekamilisha ukarabati wa wodi mbili na hivyo kuongeza nafasi ya vitanda kwa ziada 20 ambavyo tayari vinatumika na hivyo, kupunguza msongamano uliokuwepo. (ii) Serikali inafanya ujenzi na upanuzi wa miundombinu katika vituo vya afya sita ambavyo ni Mazwi, Nkomolo, Kirando, Mwimbi, Legezamwendo na Milepa ndani ya Mikoa hii. Kupanua wigo wa kujifungua kwa njia ya upasuaji. Hatua hii itapunguza tatizo la akina mama wajawazito wengi kupewa rufaa kujifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa. (iii) Serikali kupitia Ofisi ya Rais – TAMISEMI imetenga jumla ya shilingi bilioni 100.5 katika mwaka 2018/2019 kwa ajili ya upanuzi wa Hospitali za Halmashauri 67 ambapo kila moja imetengewa jumla ya shilingi bilioni 1.5. Halmashauri za Mkoa wa Rukwa zinatarajiwa kunufaika na fedha hizi. Mheshimiwa Mwenyekiti, ni matarajio yangu kwamba Serikali kupitia mikakati hii itatoa tatizo la msongamano wa 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) akina mama wajawazito waliojifungua katika Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Rukwa. MWENYEKITI: Mheshimiwa Aida. MHE. AIDA J. KHENANI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru, niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Naibu Waziri umekiri kwamba katika Mkoa wa Rukwa hakuna Hospitali ya Wilaya hata moja na nia ya sisi wawakilishi na Serikali kwa ujumla ni kuhakikisha sio kuepusha au kupunguza vifo vya wanawake na watoto ila