MKUTANO WA KUMI NA SABA Kikao Cha Tano
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _______ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA KUMI NA SABA Kikao cha Tano - Tarehe 11 Novemba, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Saba na leo ni kikao cha tano. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, swali linaulizwa na Mheshimiwa Mary Pius Chatanda Mbunge wa Korongwe Mjini. Na. 56 Ukarabati wa Shule Korogwe MHE. MARY P. CHATANDA aliuliza:- Serikali imefanya kazikubwa sana ya ukarabati wa Shule ya Sekondari Korogwe lakini haikuunganisha nyumba za Walimu zilizopo Shuleni hapo. Je, Serikali ina mpango gani wa kuzikarabati nyumba hizo? 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Majibu ya swali hilo, Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Jafo tafadhali. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mheshimiwa Mary Pius Chatanda, Mbunge wa Korogwe Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Shule ya Sekondari Korogwe ni miongoni mwa shule 45 zilizokarabatiwa katika awamu ya kwanza ya ukarabati wa shule kongwe nchini. Ukarabati wa shule kongwe awamu ya kwanza ulihusisha vyumba vya madarasa, matundu ya vyoo, mabweni, maabara, ofisi za walimu, majengo ya utawala, mabwalo ya chakula na majiko, mifumo ya maji safi na taka na mifumo ya umeme. Mheshimiwa Spika, ukarabati wa shule kongwe awamu ya kwanza haukuhusisha nyumba za walimu kutokana na sababu za kibajeti. Awamu ya pili ya ukarabati unaoendelea inahusisha shule shule kongwe 19 ikiusisha halikadhalika nyumba za walimu kwenye shule zinazokarabatiwa. Serikali inatafuta fedha ili kukarabati nyumba za walimu ambazo hazikujumuishwa kwenye mpango wa ukarabati wa shule kongwe awamu ya kwanza. SPIKA: Mheshimiwa Mary Chatanda, swali la nyongeza. MHE. MARY P. CHATANDA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kunipa nafasi niulize maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa napenda kuishukuru Serikali kwa namna ambavyo imekuwa ikitukimbilia pale shule yetu imekuwa na majanga ya moto zaidi ya mara mbili. Tunaishukuru sana Serikali. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, lakini la pili nishukuru kwa majibu mazuri niliyopewa na Waziri. Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, katika huu mpango wa pili ambapo watakuwa wametafuta fedha, je, Shule ya Korongwe Girls itapewa kipaumbele cha kwanza hasa ikizingatiwa kwamba pia ina watoto wenye ulemavu ili walimu wale wawe na moyo wa kuendelea kufanya kazi? Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa tunazo shule za kata katika Halmashauri zetu kwa nchi nzima ambapo tulikuwa tumeweka mipango kwa ajili ya ujenzi wa maabara lakini kwa bahati mbaya sana Halmashauri nyingine zimeshindwa kukamilisha mahabara hizo. Je, mtakuwa tayari sasa kuweka mpango wa kukamilisha zile maabara zilizoko kwenye Halmshauri zetu ili watoto waweze kupata elimu iliyo bora kuliko bora elimu? SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, tafadhali. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la mama yangu Mheshimiwa Mary Chatanda, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nimshukuru sana Mheshimiwa Mary Chatanda maana kwa vipindi tofauti tumefanya ziara jimboni kwake Korogwe na awamu ya mwisho tulienda naye katika shule yetu ya Sekondari Korongwe na kuongea na wanafunzi na kubainisha changamoto mbalimbali. Nafahamu kwamba juzijuzi hapa shule ilipata madhara ya bweni kuungua na ndiyo maana nimetuma wataalamu ili bweni lile tulikarabati haraka iwezekanavyo. Mheshimiwa Spika, katika programu hii ya kukarabati, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Chatanda tutakapoanza awamu hii shule ya Korongwe tutaiweka katika awamu ya kwanza bila kigugumizi chochote. (Makofi) 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, hali kadhalika mpango wa kuhakikisha tunamalizia maabara, kama mnavyokumbuka kwamba hapa katikati tulitoa zaidi ya shilingi bilioni 32.5 kwa lengo la kuhakikisha kwamba tunamalizia maboma mbalimbali. Tunajua fika fedha hii haitoshi kwani kuna mabweni mengine hayajakamilika. Mheshimiwa Spika, ni azma ya Serikali hata katika mpango wa bajeti ya mwaka 2019/2020 tutahakikisha katika maeneo mbalimbali tunakamilisha ujenzi wa maabara na vifaa. Juzijuzi tumetumia zaidi ya shilingi bilioni 17 ili tupate vifaa vya maabara vijana waweze kufanya practically katika maeneo ya shule. SPIKA: Tunaendelea na swali linalofuata, litaulizwa na Mbunge wa Mbullu Mjini Mheshimiwa Zacharia Paulo Issaay. Na. 57 Hitaji la Vituo vya Afya Tarafa ya Nambis – Mbulu MHE. ZACHARIA P. ISSAAY aliuliza:- Sera ya Afya ni kuwa na Kituo cha Afya kwa kila Kata na Zahanati kwa kila Kijiji; Tarafa ya Nambis katika Jimbo la Mbulu Mjini haina Kituo cha Afya. Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga Vituo vya Afya kwenye Kata za Kainem, Murray, Nambis na Nahasey? SPIKA: Majibu ya swali hilo, bado tupo TAMISEMI, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Mheshimiwa Jafo, tafadhali. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Zacharia Paul Issaay,Mbunge wa Mbulu Mjini, kama ifuatavyo:- 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa Tarafa ya Nambis haina Kituo cha Afya na wananchi wa Tarafa hiyo wanapata huduma kwenye Zahanati 4 za Serikali zilizoko katika Tarafa ya Nambis pamoja na Hospitali ya Wilaya ya Mbulu ambayo iko jirani na Kata ya Nambis. Mheshimiwa Spika, ili kuboresha huduma za afya katika Mji wa Mbulu, Serikali imetoa kiasi cha shilingi bilioni 3 kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa Vituo vya Afya Daudi na Tlawi sambamba na vifaa tiba ambapo hadi Oktoba, 2019 Kituo cha Afya Daudi kimepokea vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi milioni 203.8 na Kituo cha Afya Tlawi kimepokea vifaa tiba vyenye thamani ya shilingi 203.8. Vilevile Mkoa wa Manyara umepatiwa kiasi cha shilingi billioni 3 kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali za Halmashauri za Wilaya za Mbulu na Simanjiro. Ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Mbulu utapunguza msongamano katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu iliyoko Mbulu Mjini. Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kujenga na kukarabati Vituo vya Afya nchini kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha uliopo. SPIKA: Mheshimiwa Issaay nimekuona, swali la nyongeza. MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali kupitia Waziri, nina maswali madogo mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Spika, swali la kwanza, kwa kuwa hospitali ya Mji wa Mbulu inategemewa na kata zinazopakana kutoka Wilaya ya Babati, Karatu na hata upande wa Jimbo la Mbulu Vijijini; na kwa kuwa hospitali hii inakabiliwa na upungufu mkubwa wa fedha za uendeshaji hali inayopelekea wagonjwa kujigharamikia wakati wa rufaa na ukosefu mkubwa sana wa dawa. Mheshimiwa Waziri ameshafika mara kadhaa na sasa hivi tuko kwenye mpango wa bajeti wa 2020/2021. Je, Serikali ina mkakati 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) gani wa kusaidia hospitali ya Mji wa Mbulu kwa kuiongezea fedha za uendeshaji? Mheshimiwa Spika, swali la pili, kwa kuwa Vituo vya Afya ya Daudi na Tlawi tayari vimeanza kutoa huduma, tunaishukuru sana Serikali. Pia nia ya Serikali ni njema kujenga Kituo cha Afya katika Tarafa ya Nambis ambapo vijiji vyake baadhi vina umbali wa kilomita 30 mpaka 40 kwenda hospitali wa Mji wa Mbulu. Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka maombi niliyowasilisha ya gari la ambulance kutafutwa haraka ili wananchi wa kata hizo za Nambis na maeneo mengine ya pembezoni wapate huduma ya usafiri haraka kwenda kupata matibabu? (Makofi) SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, tafadhali. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la kaka yangu Mheshimiwa Zacharia Paul Issay, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, nimshukuru sana Mheshimiwa Mbunge na pacha wake Mheshimiwa Flatei Massay hapa karibuni tulienda kufanya ziara katika Halmashauri hizi mbili na niwapongeze Wabunge hawa wamefanya kazi kubwa sana ya kusimamia miundombinu kwa fedha ambazo tumepeleka kule. Mheshimiwa Spika, ni kweli hospitali ya Mheshimiwa Mbunge siyo suala la mgao wa fedha peke yake hata hali ya majengo haipendezi. Ndiyo maana kwa ombi la Mheshimiwa Mbunge nilipendekeza na nilielekeza kwamba zile shilingi milioni 500 sasa zianze kuibadilisha Hospitali ya Mbulu kwa sababu tunajua itakapokuwa na mazingira mazuri hata suala zima la ukusanyaji wa mapato litaongezeka. Hata hivyo, ni azma ya Serikali Mheshimiwa Mbunge wala usihofu tutaangalia nini kifanyike kuhakikisha mgao wa dawa katika eneo lile ambapo tunajua fedha nyingi sana zinaenda vijijini kuwasaidia Halmashauri ya 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mbulu Mjini kuweza kuongeza ule mfuko wao wa dawa ili waweze kupata huduma vizuri. Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini ajenda ya upatikanaji wa ambulance, naomba nimhakikishie tutashirikiana na dada yangu Mheshimiwa Ummy Mwalimu, Waziri wa Afya pale tutakapopata gari aina yoyote tutawapelekea. Kwa kweli nimefika kule na nimeona changamoto kubwa katika eneo hilo lazima tupate usafiri. SPIKA: Nimekuona Mheshimiwa Shangazi, swali la nyongeza, tafadhali. MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa nafasi. Mheshimiwa Spika, tarafa ya Mtae katika Halmashauri ya Lushoto ambayo ina kata tano ndiyo pekee mpaka sasa hivi haijapata kituo cha afya. Je, ni