MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao Cha Nane

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao Cha Nane Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Nane - Tarehe 18 Juni, 2004 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Pius Msekwa) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA KILIMO NA CHAKULA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Bodi Ya Tumbaku kwa Mwaka unaoishia Tarehe 31 Machi, 2003 (The Annual Report and Accounts of the Tanzania Tobacco Board for the Year ended 31st March, 2003). Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Bodi ya Pamba na Mbegu kwa Mwaka Ulioishia tarehe 30 Juni, 2003 (The Annual Report and Audited Accounts of the Tanzania Cotton Lint and Seed Board for the Year ended 30th June, 2003). MASWALI NA MAJIBU Na. 69 Mabaraza ya Ardhi Vijijini MHE. LEKULE M. LAIZER aliuliza:- Kwa kuwa katika utaratibu wa ardhi ya Vijiji, kila Kijiji kinatakiwa kuunda Mabaraza ya Ardhi kwa ajili ya kusuluhisha migogoro ya ardhi Vijijini na kwa kuwa migogoro ya ardhi ilikuwepo kila mara hata kabla ya kutungwa kwa Sheria ya Ardhi Vijijini:- (a) Je, Serikali haioni kwamba imechelewa kuanzisha Mabaraza hayo? 1 (b) Je, Serikali itakuwa tayari kuwaelimisha wananchi juu ya jambo hilo ili utekelezaji wake uanze kuliko kuyaacha mambo hayo kwenye maandishi tu? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lekule Michael Laizer, Mbunge wa Longido, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, uamuzi wa kuanzisha Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji ulitokana na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 1999. Sheria hii inazielekeza Serikali za Vijiji kuunda Mabaraza ya Vijiji kwa madhumuni ya kutatua migogoro ya ardhi katika ngazi hiyo badala ya Mahakama za Mwanzo. Aidha, Sheria Na. 2 ya Mwaka 2002 ya Mahakama za Ardhi (The Land Disputes Court Act, 2002) inatoa ufafanuzi wa kina juu ya utaratibu, Mamlaka ya uundaji wa Mabaraza hayo na majukumu ya vyombo vinavyohusika na utatuzi wa migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji. Kufuatia Tangazo la Serikali Na. 223 la tarehe 8 Agosti, 2003 lililotolewa na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Sheria Na. 2 ya 2002 imeanza kutekelezwa rasmi tarehe 1 Oktoba, 2003. Pamoja na maandalizi hayo, Wizara yangu pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, pamoja na Waziri wa Ardhi, tumeshirikiana kufanya tafsiri ya Sheria pamoja na kanuni zote zinazohusiana na masuala haya ya ardhi na sasa Halmashauri zimeshaanza kutekeleza sheria hiyo na tukitoa mifano hasa ya Rungwe, Bariadi na Monduli. Katika Halmashauri ya Monduli, Vijiji 36 kati ya 72 vimekwishaunda Mabaraza hayo. Mheshimiwa Spika, kutokana na taratibu nilizozielezea, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kuwa, Serikali imechelewa kuanzisha Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji tangu Sheria Na. 5 ya mwaka 1999 ilipopitishwa. Hata hivyo, ilikuwa ni muhimu kwa Serikali kuelekeza juhudi kwanza katika kufafanua na kutafsiri sheria ili iwe rahisi kueleweka kwa jamii wakati Mabaraza hayo yanapoundwa na Mabaraza yenyewe kuelewa vema majukumu yake, hivyo kufanya kazi kwa ufanisi na tija. Aidha, Serikali ilikwishaanzisha utaratibu wa Mabaraza ya Kata, ambayo pamoja na mambo mengine, yanayo majukumu vile vile ya kusikiliza rufaa za migogoro ya ardhi ngazi ya Vijiji. (b) Mheshimiwa Spika, Serikali inalo jukumu la kwanza la kuwaelimisha wananchi juu ya uundaji na uendeshaji wa Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji kwa ufanisi. Ofisi yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, pamoja na Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba, inaandaa mwongozo wa kuwaelimisha wananchi kuhusu Sheria ya Mahakama za Ardhi. Aidha, waraka unaandaliwa na Ofisi yangu kuzielekeza zaidi Halmashauri juu ya Mabaraza haya. Kutokana na sheria hii inatarajiwa kwamba, mazingira katika Vijiji yataboreka zaidi kama wananchi wataelewa vyema sheria hiyo. MHE. LEKULE M. LAIZER: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niulize swali la nyongeza. Kwa kuwa tangu sheria hii ipitishwe mpaka sasa bado hayo Mabaraza hayajapata semina jinsi ya kuongoza, ni lini basi Serikali itachukua muda huo kwenda kuelimisha hayo Mabaraza ili watekeleze wajibu wao? 2 NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, maandalizi yanakamilishwa kwa maana ya kuandaa miongozo mbalimbali, lakini la msingi zaidi lilikuwa ni kuweka kwanza sheria zenyewe katika lugha ya Kiswahili ambayo inaeleweka vizuri zaidi. Nina hakika baada ya muda si mrefu, juhudi hizo za kuanza kutoa elimu zitaanza. MHE. PHILIP S. MARMO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, Waziri atalieleza Bunge hili nani anawajibika kugharamia uendeshaji wa Mabaraza haya? (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, Sheria zote ambazo zilipitishwa na Bunge hili zimeweka utaratibu mahsusi kabisa wa namna ya kusimamia Mabaraza haya katika ngazi za Vijiji na hizo ndio zitakazotumika. SPIKA: Maswali mafupi mafupi kama haya ndiyo yanayotakiwa na kanuni zetu. Kwa hiyo, kuna nafasi nyingine. Mheshimiwa Dr. Wilbrod Slaa nilikuona, maswali mafupi mafupi. (Makofi) MHE. DR. WILBROD P. SLAA: Mheshimiwa Spika, swali langu lilihusiana na hilo lakini sehemu ya pili yake bado halijajibiwa, kwa hiyo naomba niulize swali moja la nyongeza. Kwa kuwa Mabaraza haya hayajaanza kazi na Baraza la Ardhi la Wilaya lililokuwepo bado linaendelea. Je, Waziri sasa ataeleza nini kwamba mwisho wa Mabaraza yale ya zamani utakuwa lini na haya mapya yanategemewa kuanza lini? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taratibu zilivyo, Mabaraza haya yalipewa transition period ya miaka miwili ili kuweza ku-handover majukumu haya mengine kwenye Mabaraza ya Vijiji kwa ubora zaidi. Na. 70 Utekelezaji Sahihi wa Mpango na Maagizo ya Kitaifa MHE. MBARUK K. MWANDORO aliuliza:- Kwa kuwa mara nyingi panakuwepo na pengo baina ya malengo, mipango na mikakati ya Kitaifa ya maendeleo na hali halisi ya kimipango na kiutekelezaji katika ngazi za Wilaya na Vijiji na mfano hai ni matarajio ya kuwepo kwa mazao maalum ya kiuchumi na ya chakula kwa kila Wilaya, hali halisi ya ukosefu wa mipango hiyo na hatua thabiti za utekelezaji wa mipango inayotarajiwa:- (a) Je, Serikali inatambua kwamba mara nyingine viongozi katika Halmashauri za Wilaya na Serikali za Vijiji hawazingatii ipasavyo au wanapuuza tu maagizo muhimu kutoka ngazi za juu? 3 (b) Je, Serikali ina utaratibu gani wa kuhakikisha kuwa mtiririko na utekelezaji sahihi na ulio thabiti wa mipango na maagizo ya Kitaifa ya kuendeleza sekta mbalimbali za kiuchumi na huduma za jamii hadi kufikia ngazi za Wilaya au Vijiji unasimamiwa ipasavyo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbaruku Kassim Mwandoro, Mbunge wa Mkinga, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa Namba 7 inayohusiana na Mamlaka za Wilaya na Namba 8 ya Mamlaka za Miji za mwaka 1982, Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na mengineyo zinao wajibu wa kusimamia na kutekelzea sera, mikakati, sheria, taratibu na miongozo mbalimbali ya kisekta. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia majukumu ya kisheria ya Serikali za Mitaa, Serikali inatambua kuwepo kwa baadhi ya viongozi ikiwa ni pamoja na watendaji wake, kutozingatia kikamilifu maagizo na maelekezo yanayotolewa na Serikali Kuu na hata maamuzi halali ya Mabaraza ya Madiwani ya Halmashauri na Mikutano Mikuu ya Vijiji. Pale ambapo imebainika kukiukwa au kupuzwa kwa maelekezo au maagizo yanayotolewa na Mamlaka halali, hatua zinazostahili kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo huchukuliwa. Kwa mfano, Juni, 1996 Serikali ililazimika kuvunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na mara kwa mara kusimamisha, kukemea na kufukuza watendaji wa ngazi mbalimbali katika Utumishi wa Serikali za Mitaa. Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 43(5) cha Sheria Na. 9 ya mwaka 1992 ya Fedha za Serikali za Mitaa, Baraza la Madiwani la Halmashauri linalo jukumu la kuhakikisha shughuli za Halmashauri zinatekelezwa na kumwajibisha mtendaji mkuu au mtumishi mwingine pale anaposhindwa kutekeleza wajibu wake. (b) Mheshimiwa Spika, Serikali inazo taratibu zilizokubalika kisheria katika kuwezesha mitiririko wa mawasiliano na utekelezaji wa mipango na maagizo ya Kitaifa hadi ngazi ya Vijiji. Taratibu hizo ni pamoja na kuwepo kwa miundo ya Wizara, Mikoa, Wilaya na Serikali za Vijiji ,ambazo zina uhusiano wa kirasimu toka juu hadi chini unaoleta uwajibikaji. Utaratibu huu unahakikisha maelekezo ya Serikali yanawafikia wahusika, yanatekelezwa, yanafuatiliwa na yanatolewa taarifa. Aidha, upo pia utaratibu wa kupitisha maamuzi na maagizo kuanzia Baraza la Mawaziri kwenda Wizara husika, Mikoa hadi Wilaya, kwa maana ya Serikali na Halmashauri. Mfumo huu pia unasisitiza ufuatiliaji wa maagizo na utoaji wa taarifa. Vile vile, sheria mbalimbali zinazotungwa na Wizara na Halmashauri, zinalenga kusimamia utekelezaji wa sera, maagizo na mipango inayoandaliwa. Kupitia sheria zilizotungwa, miongozo na nyaraka mbalimbali za Serikali, wananchi wanazo haki zote kufuatilia na kuuliza au kwa upande wa Mabaraza ya Madiwani kumchukulia hatua mtumishi mzembe. 4 Mwisho ni mfumo uliopo kuanzia ngazi ya Taifa, Wilaya na hadi Vijijini. Mfumo huu unawawezesha viongozi hawa kutoa maelekezo na ufafanuzi wa miongozo mbalimbali na maagizo ya Serikali. MHE. MBARUK K. MWANDORO: Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa
Recommended publications
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 114 May - Aug 2016
    Tanzanian Affairs Issued by the Britain-Tanzania Society No 114 May - Aug 2016 Magufuli’s “Cleansing” Operation Zanzibar Election Re-run Nyerere Bridge Opens David Brewin: MAGUFULI’S “CLEANSING” OPERATION President Magufuli helps clean the street outside State House in Dec 2015 (photo State House) The seemingly tireless new President Magufuli of Tanzania has started his term of office with a number of spectacular measures most of which are not only proving extremely popular in Tanzania but also attracting interest in other East African countries and beyond. It could be described as a huge ‘cleansing’ operation in which the main features include: a drive to eliminate corruption (in response to widespread demands from the electorate during the November 2015 elections); a cutting out of elements of low priority in the expenditure of government funds; and a better work ethic amongst government employees. The President has changed so many policies and practices since tak- ing office in November 2015 that it is difficult for a small journal like ‘Tanzanian Affairs’ to cover them adequately. He is, of course, operat- ing through, and with the help of ministers, regional commissioners and cover photo: The new Nyerere Bridge in Dar es Salaam (see Transport) Magufuli’s “Cleansing” Operation 3 others, who have been either kept on or brought in as replacements for those removed in various purges of existing personnel. Changes under the new President The following is a list of some of the President’s changes. Some were not carried out by him directly but by subordinates. It is clear however where the inspiration for them came from.
    [Show full text]
  • 1458125471-Hs-6-8-20
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA __________________ MAJADILIANO YA BUNGE __________________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Ishirini na Tatu - Tarehe 14 Julai, 2003 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Naibu Spika (Mhe. Juma J. Akukweti) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Taarifa ya Mwaka ya Utekelezaji na Hesabu zilizokaguliwa za Bodi ya Usajili wa Wahandisi kwa Mwaka wa Fedha 2001/2002 (The Annual Performance Report and Audited Accounts of the Engineers Registration Board for the Financial year 2001/2002). NAIBU WAZIRI WA AFYA: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya kwa Mwaka wa Fedha 2003/2004. MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII: Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Afya katika mwaka uliopita, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2003/2004. MASWALI NA MAJIBU Na. 220 Mashamba ya Mifugo MHE. MARIA D. WATONDOHA (k.n.y. MHE. PAUL P. KIMITI) aliuliza:- Kwa kuwa Mkoa wa Rukwa unayo mashamba makubwa ya mifugo kama vile Kalambo, Malonje na Shamba la Uzalishaji wa Mitamba (Nkundi):- (a) Je, Serikali inatoa tamko gani kwa kila shamba ili wananchi wajue hatma ya mashamba hayo? (b) Kwa kuwa uamuzi na jinsi ya kuyatumia mashamba hayo unazidi kuchelewa; je, Serikali haioni kuwa upo uwezekano wa mashamba hayo kuvamiwa na wananchi wenye shida ya ardhi? WAZIRI WA MAJI NA MAENDELEO YA MIFUGO alijibu:- 1 Mheshimiwa Naibu Spika, swali hili linafanana sana na swali Na. 75 lililoulizwa na Mheshimiwa Ponsiano D. Nyami, tulilolijibu tarehe 20 Juni, 2003.
    [Show full text]
  • By Martin Sturmer First Published by Ndanda Mission Press 1998 ISBN 9976 63 592 3 Revised Edition 2008 Document Provided by Afrika.Info
    THE MEDIA HISTORY OF TANZANIA by Martin Sturmer first published by Ndanda Mission Press 1998 ISBN 9976 63 592 3 revised edition 2008 document provided by afrika.info I Preface The media industry in Tanzania has gone through four major phases. There were the German colonial media established to serve communication interests (and needs) of the German administration. By the same time, missionaries tried to fulfil their tasks by editing a number of papers. There were the media of the British administration established as propaganda tool to support the colonial regime, and later the nationalists’ media established to agitate for self-governance and respect for human rights. There was the post colonial phase where the then socialist regime of independent Tanzania sought to „Tanzanianize“ the media - the aim being to curb opposition and foster development of socialistic principles. There was the transition phase where both economic and political changes world-wide had necessitated change in the operation of the media industry. This is the phase when a private and independent press was established in Tanzania. Martin Sturmer goes through all these phases and comprehensively brings together what we have not had in Tanzania before: A researched work of the whole media history in Tanzania. Understanding media history in any society is - in itself - understanding a society’s political, economic and social history. It is due to this fact then, that we in Tanzania - particularly in the media industry - find it plausible to have such a work at this material time. This publication will be very helpful especially to students of journalism, media organs, university scholars, various researchers and even the general public.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE ________________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Ishirini na Tano – Tarehe 17 Julai, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA HABARI, VIJANA, UTAMADUNI NA MICHEZO:- Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo kwa mwaka wa Fedha 2012/2013. NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:- Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa Fedha 2012/2013. MHE. EUGEN E. MWAIPOSA (K.n.y. MHE. EDWARD LOWASSA - MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA):- Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka 2011/2012 Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MHE. VINCENT J. NYERERE – MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaanza maswali kwa Ofisi ya Waziri Mkuu, atakayeuliza swali letu la kwanza ni Mheshimiwa Beatrice Matumbo Shellukindo kwa niaba yake Mheshimiwa Herbert Mntangi.
    [Show full text]
  • Globalization, National Economy and the Politics of Plunder in Tanzania's
    'Conducive environment' for development?: Globalization, national economy and the politics of plunder in Tanzania's mining industry Author: Tundu Lissu Date Written: 1 January 2004 Primary Category: Resource Extraction Document Origin: Lawyers Environmental Action Team Secondary Category: Eastern Region Source URL: http://www.leat.or.tz INTRODUCTION We live in a world transformed in ways that even the most brilliant of the 19th and early 20th century philosophers and political thinkers would find hard to recognize. The power and mobility of finance capital has created the conditions under which rapid scientific and technological change has taken place. This has in turn augmented this power and made it extremely difficult for the state to direct economic and social policy. Capital and foreign exchange controls have everywhere been scrapped; regulations which protected jobs, consumers and the environment; subsidies which benefited the lowest strata of both the urban and rural masses have all gone, as have trade restrictions meant to protect local industries and increase government revenue. These processes have now attained the sanctity of international law through the instrumentality of such institutions as the World Bank Group and WTO and its trade negotiation rounds that have produced GATS, TRIPs, etc. The frontiers of the state have indeed been rolled back. These processes have produced a massive growth in international trade, foreign direct investment flows and unprecedented wealth. Yet they have not led to general prosperity across the world, particularly in poor countries such as Tanzania. On the contrary, general impoverishment comes as an integral part of a global economic order in which an ever-shrinking arrogant officer class , to use the phrase of an eminent British author, lives in affluency.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Sita
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Tano – Tarehe 15 Juni, 2009 (Mkutano ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- MWENYEKITI WA KAMATI YA FEDHA NA UCHUMI: Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha Mezani Taarifa ya Kamati ya Fedha na Uchumi Kuhusu Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2008/2009 na Mwelekeo wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2009/2010. MHE. MWADINI ABBAS JECHA K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA FEDHA NA UCHUMI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Wizara ya Fedha na Uchumi, naomba kuwasilisha Mezani Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Fedha na Uchumi juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2009/2010. MASWALI NA MAJIBU Na. 33 Athari za Milipuko ya Mabomu - Mbagala MHE. KHADIJA SALUM ALI AL-QASSMY K.n.y. MHE. ANIA S. CHAUREMBO aliuliza:- Kwa kuwa, tukio la tarehe 29 Aprili, 2009 la milipuko ya mabomu kwenye Kambi ya Jeshi la Wananchi – JWTZ, Mbagala Kizuiani, limesababisha hasara kubwa kama vile, watu kupoteza maisha, watu wengi kujeruhiwa, uharibifu mkubwa wa mali na 1 nyumba za wananchi, kuharibika kwa miundombinu na kadhalika. Na kwa kuwa, kuna Kamati maalum inayoshughulikia majanga yanapotokea ambayo iko chini ya Ofisi ya waziri Mkuu:- Je, ni sababu zipi zilizofanya Kamati hiyo isifike kwa haraka kwenye eneo la tukio na kutoa msaada wa haraka uliotakiwa? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU – SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Spika, kabla sijajibu swali hili naomba kutoa mkono wa pole sana kwa Mheshimiwa Ania Chaurembo, kwa msiba wa Mama yake Mzazi.
    [Show full text]
  • 4 MEI, 2013 MREMA 1.Pmd
    4 MEI, 2013 BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kumi na Nane - Tarehe 4 Mei, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. Waheshimiwa Wabunge Mkutano wa 11 unaendelea, kikao hiki ni cha 18. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI:- Randama za Makadirio ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. 1 4 MEI, 2013 MHE. OMAR R. NUNDU (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA ULINZI NA USALAMA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ulinzi na Usalama Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA (K.n.y. MHE. MCH. ISRAEL Y. NATSE - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA:- Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. HOJA ZA SERIKALI Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2013/2014 Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Mheshimiwa Naibu Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ulinzi na Usalama, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu likubali kujadili na kupitisha Mpango na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa mwaka wa fedha 2013/2014.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA PILI Kikao Cha Tisa
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA PILI Kikao cha Tisa - Tarehe 17 Februari, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Taarifa ya mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa fedha unaoishia tarehe 30 Juni, 2004. Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. MASWALI NA MAJIBU Na. 94 Uwekaji wa Lami Barabara ya Kigogo - Mabibo - Mandela - Tabata MHE. HALIMA J. MDEE aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuweka lami kwenye barabara ya Kigogo- Mabibo hadi barabara ya Mandela kuelekea Tabata ili kupunguza msongamano wa magari katika barabara ya Morogoro? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Halima Mdee, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- 1 Mheshimiwa Spika, barabara ya Kigogo - Mabibo- Mandela kuelekea Tabata ni barabara ya mjini yaani urban road na inahudumiwa na Halmashauri ya Manispaa ya Kinondoni. Barabara hii ni muungano wa barabara tatu ambazo ni Kigogo - Mabibo, Mabibo - Mandela na Mandela - Tabata. Barabara hii imekuwa ikifanyiwa matengenezo ya mara kwa mara na Manispaa ya Kinondoni. Kwa mwaka 2005/2006 jumla ya shilingi 9,836,000 zilitumika kuweka kifusi kwenye sehemu korofi na kuichonga kwa greda. Mheshimiwa Spika, barabara hii inapitika isipokuwa katika mpaka wa Manispaa za Kinondoni na Ilala eneo la Tabata ambapo pana mkondo wa maji na hakuna daraja.
    [Show full text]
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? With Partial Support from a TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? ACKNOWLEDGEMENTS This review was compiled and edited by Tanzania Development Research Group (TADREG) under the supervision of the Steering Group of Policy Forum members, and has been financially supported in part by Water Aid in Tanzania and Policy Forum core funders. The cartoons were drawn by Adam Lutta Published 2013 For more information and to order copies of the review please contact: Policy Forum P.O Box 38486 Dar es Salaam Tel: +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] ISBN: 978-9987 -708-09-3 © Policy Forum The conclusions drawn and views expressed on the basis of the data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. Every effort has been made to verify the accuracy of the information contained in this review, including allegations. Nevertheless, Policy Forum cannot guarantee the accuracy and completeness of the contents. Whereas any part of this review may be reproduced providing it is properly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. Designed by: Jamana Printers b TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TABLE OF CONTENTS POLICY FORUM’s OBJECTIVES .............................................................................................................
    [Show full text]
  • Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1
    Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Pili – Tarehe 13 Mei, 2015 (Mkutano Ulianza Saa 3.00 Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu! MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa, maswali tunaanza na ofisi ya Waziri Mkuu, anayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Josephine J. Genzabuke, kwa niaba yake Mheshimiwa Likokola! Na. 11 Fedha za Mfuko wa JK kwa Wajasiriamali Wadogo MHE. DEVOTHA M. LIKOKOLA (K.n.y. MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE) aliuliza:- Mfuko wa Wajasiriamali wadogowadogo maarufu kama mabilioni ya JK uliwavuta wengi sana lakini masharti ya kupata fedha hizo yamekuwa magumu:- (a) Je, Serikali ina mkakati gani wa kufanya mpango huo uwe endelevu kwa lengo la kuwanufaisha wanyonge? (b) Je, ni wananchi wangapi wa Mkoa wa Kigoma wamenufaika na mpango huo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephine Johnson Genzabuke, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2006/2007, Serikali ilianzisha mpango wa uwezeshaji wananchi kiuchumi na kuongeza ajira kwa kutoa mikopo yenye masharti nafuu. Lengo la mpango huu ni kuwawezesha wananchi mijini na vijijini kupata mikopo ya kuanzisha au kuendeleza shughuli za kiuchumi ili kuongeza ajira na kipato. Masharti ya kupata mikopo hii si magumu sana ikilingalishwa na ile inayotolewa na mabenki, kwa sababu riba inayotozwa kwa mikopo hii ni asilimia 10, ikilinganishwa na riba inayotozwa na mabenki mengine, ambayo ni zaidi ya asilimia 20.
    [Show full text]
  • Bspeech 2008-09
    HOTUBA YA WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA, MHESHIMIWA STEPHEN MASATO WASIRA (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA KWA MWAKA 2008/2009 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu baada ya kuzingatia taarifa iliyowasilishwa hapa Bungeni leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji inayohusu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, sasa lijadili na kukubali kupitisha makadirio ya Matumizi ya Kawaida na ya Maendeleo ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa mwaka wa Fedha wa 2008/2009. 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote nitumie fursa hii kuungana na Watanzania wenzangu kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika. Kuchaguliwa kwake, na mchango wake alioutoa tangu kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Umoja huo umelijengea Taifa letu heshima kubwa katika medani ya kimataifa. Aidha, uongozi wake na juhudi zake za kupambana na maovu katika jamii yetu, licha ya kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa ajili ya Uchaguzi wa Mwaka 2005 ni kielelezo dhahiri kuwa ni kiongozi anayejali haki na maendeleo ya nchi yetu. Juhudi zake hizo zimedhihirisha uwezo wake mkubwa wa kuongoza na utumishi wake uliotukuka aliouonyesha katika nyadhifa mbali mbali alizowahi kushika katika Serikali na Chama cha Mapinduzi. Wananchi wanaendelea kuwa na imani na matumaini makubwa kwa uwezo wake katika kuliongoza Taifa letu. 1 3. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kumpongeza Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda (MB) kwa kuteuliwa kwake kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
    [Show full text]