Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Nane - Tarehe 18 Juni, 2004 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Pius Msekwa) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA KILIMO NA CHAKULA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Bodi Ya Tumbaku kwa Mwaka unaoishia Tarehe 31 Machi, 2003 (The Annual Report and Accounts of the Tanzania Tobacco Board for the Year ended 31st March, 2003). Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Bodi ya Pamba na Mbegu kwa Mwaka Ulioishia tarehe 30 Juni, 2003 (The Annual Report and Audited Accounts of the Tanzania Cotton Lint and Seed Board for the Year ended 30th June, 2003). MASWALI NA MAJIBU Na. 69 Mabaraza ya Ardhi Vijijini MHE. LEKULE M. LAIZER aliuliza:- Kwa kuwa katika utaratibu wa ardhi ya Vijiji, kila Kijiji kinatakiwa kuunda Mabaraza ya Ardhi kwa ajili ya kusuluhisha migogoro ya ardhi Vijijini na kwa kuwa migogoro ya ardhi ilikuwepo kila mara hata kabla ya kutungwa kwa Sheria ya Ardhi Vijijini:- (a) Je, Serikali haioni kwamba imechelewa kuanzisha Mabaraza hayo? 1 (b) Je, Serikali itakuwa tayari kuwaelimisha wananchi juu ya jambo hilo ili utekelezaji wake uanze kuliko kuyaacha mambo hayo kwenye maandishi tu? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lekule Michael Laizer, Mbunge wa Longido, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, uamuzi wa kuanzisha Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji ulitokana na Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 1999. Sheria hii inazielekeza Serikali za Vijiji kuunda Mabaraza ya Vijiji kwa madhumuni ya kutatua migogoro ya ardhi katika ngazi hiyo badala ya Mahakama za Mwanzo. Aidha, Sheria Na. 2 ya Mwaka 2002 ya Mahakama za Ardhi (The Land Disputes Court Act, 2002) inatoa ufafanuzi wa kina juu ya utaratibu, Mamlaka ya uundaji wa Mabaraza hayo na majukumu ya vyombo vinavyohusika na utatuzi wa migogoro ya ardhi ikiwa ni pamoja na Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji. Kufuatia Tangazo la Serikali Na. 223 la tarehe 8 Agosti, 2003 lililotolewa na Waziri wa Ardhi na Maendeleo ya Makazi, Sheria Na. 2 ya 2002 imeanza kutekelezwa rasmi tarehe 1 Oktoba, 2003. Pamoja na maandalizi hayo, Wizara yangu pamoja na Ofisi ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali, pamoja na Waziri wa Ardhi, tumeshirikiana kufanya tafsiri ya Sheria pamoja na kanuni zote zinazohusiana na masuala haya ya ardhi na sasa Halmashauri zimeshaanza kutekeleza sheria hiyo na tukitoa mifano hasa ya Rungwe, Bariadi na Monduli. Katika Halmashauri ya Monduli, Vijiji 36 kati ya 72 vimekwishaunda Mabaraza hayo. Mheshimiwa Spika, kutokana na taratibu nilizozielezea, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kuwa, Serikali imechelewa kuanzisha Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji tangu Sheria Na. 5 ya mwaka 1999 ilipopitishwa. Hata hivyo, ilikuwa ni muhimu kwa Serikali kuelekeza juhudi kwanza katika kufafanua na kutafsiri sheria ili iwe rahisi kueleweka kwa jamii wakati Mabaraza hayo yanapoundwa na Mabaraza yenyewe kuelewa vema majukumu yake, hivyo kufanya kazi kwa ufanisi na tija. Aidha, Serikali ilikwishaanzisha utaratibu wa Mabaraza ya Kata, ambayo pamoja na mambo mengine, yanayo majukumu vile vile ya kusikiliza rufaa za migogoro ya ardhi ngazi ya Vijiji. (b) Mheshimiwa Spika, Serikali inalo jukumu la kwanza la kuwaelimisha wananchi juu ya uundaji na uendeshaji wa Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji kwa ufanisi. Ofisi yangu kwa kushirikiana na Wizara ya Ardhi na Maendeleo ya Makazi, pamoja na Wizara ya Sheria na Mambo ya Katiba, inaandaa mwongozo wa kuwaelimisha wananchi kuhusu Sheria ya Mahakama za Ardhi. Aidha, waraka unaandaliwa na Ofisi yangu kuzielekeza zaidi Halmashauri juu ya Mabaraza haya. Kutokana na sheria hii inatarajiwa kwamba, mazingira katika Vijiji yataboreka zaidi kama wananchi wataelewa vyema sheria hiyo. MHE. LEKULE M. LAIZER: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niulize swali la nyongeza. Kwa kuwa tangu sheria hii ipitishwe mpaka sasa bado hayo Mabaraza hayajapata semina jinsi ya kuongoza, ni lini basi Serikali itachukua muda huo kwenda kuelimisha hayo Mabaraza ili watekeleze wajibu wao? 2 NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kama nilivyosema, maandalizi yanakamilishwa kwa maana ya kuandaa miongozo mbalimbali, lakini la msingi zaidi lilikuwa ni kuweka kwanza sheria zenyewe katika lugha ya Kiswahili ambayo inaeleweka vizuri zaidi. Nina hakika baada ya muda si mrefu, juhudi hizo za kuanza kutoa elimu zitaanza. MHE. PHILIP S. MARMO: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Je, Waziri atalieleza Bunge hili nani anawajibika kugharamia uendeshaji wa Mabaraza haya? (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, Sheria zote ambazo zilipitishwa na Bunge hili zimeweka utaratibu mahsusi kabisa wa namna ya kusimamia Mabaraza haya katika ngazi za Vijiji na hizo ndio zitakazotumika. SPIKA: Maswali mafupi mafupi kama haya ndiyo yanayotakiwa na kanuni zetu. Kwa hiyo, kuna nafasi nyingine. Mheshimiwa Dr. Wilbrod Slaa nilikuona, maswali mafupi mafupi. (Makofi) MHE. DR. WILBROD P. SLAA: Mheshimiwa Spika, swali langu lilihusiana na hilo lakini sehemu ya pili yake bado halijajibiwa, kwa hiyo naomba niulize swali moja la nyongeza. Kwa kuwa Mabaraza haya hayajaanza kazi na Baraza la Ardhi la Wilaya lililokuwepo bado linaendelea. Je, Waziri sasa ataeleza nini kwamba mwisho wa Mabaraza yale ya zamani utakuwa lini na haya mapya yanategemewa kuanza lini? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa taratibu zilivyo, Mabaraza haya yalipewa transition period ya miaka miwili ili kuweza ku-handover majukumu haya mengine kwenye Mabaraza ya Vijiji kwa ubora zaidi. Na. 70 Utekelezaji Sahihi wa Mpango na Maagizo ya Kitaifa MHE. MBARUK K. MWANDORO aliuliza:- Kwa kuwa mara nyingi panakuwepo na pengo baina ya malengo, mipango na mikakati ya Kitaifa ya maendeleo na hali halisi ya kimipango na kiutekelezaji katika ngazi za Wilaya na Vijiji na mfano hai ni matarajio ya kuwepo kwa mazao maalum ya kiuchumi na ya chakula kwa kila Wilaya, hali halisi ya ukosefu wa mipango hiyo na hatua thabiti za utekelezaji wa mipango inayotarajiwa:- (a) Je, Serikali inatambua kwamba mara nyingine viongozi katika Halmashauri za Wilaya na Serikali za Vijiji hawazingatii ipasavyo au wanapuuza tu maagizo muhimu kutoka ngazi za juu? 3 (b) Je, Serikali ina utaratibu gani wa kuhakikisha kuwa mtiririko na utekelezaji sahihi na ulio thabiti wa mipango na maagizo ya Kitaifa ya kuendeleza sekta mbalimbali za kiuchumi na huduma za jamii hadi kufikia ngazi za Wilaya au Vijiji unasimamiwa ipasavyo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mbaruku Kassim Mwandoro, Mbunge wa Mkinga, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, kwa mujibu wa Sheria za Serikali za Mitaa Namba 7 inayohusiana na Mamlaka za Wilaya na Namba 8 ya Mamlaka za Miji za mwaka 1982, Mamlaka za Serikali za Mitaa pamoja na mengineyo zinao wajibu wa kusimamia na kutekelzea sera, mikakati, sheria, taratibu na miongozo mbalimbali ya kisekta. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia majukumu ya kisheria ya Serikali za Mitaa, Serikali inatambua kuwepo kwa baadhi ya viongozi ikiwa ni pamoja na watendaji wake, kutozingatia kikamilifu maagizo na maelekezo yanayotolewa na Serikali Kuu na hata maamuzi halali ya Mabaraza ya Madiwani ya Halmashauri na Mikutano Mikuu ya Vijiji. Pale ambapo imebainika kukiukwa au kupuzwa kwa maelekezo au maagizo yanayotolewa na Mamlaka halali, hatua zinazostahili kwa mujibu wa sheria, kanuni na taratibu zilizopo huchukuliwa. Kwa mfano, Juni, 1996 Serikali ililazimika kuvunja Halmashauri ya Jiji la Dar es Salaam na mara kwa mara kusimamisha, kukemea na kufukuza watendaji wa ngazi mbalimbali katika Utumishi wa Serikali za Mitaa. Aidha, kwa mujibu wa kifungu cha 43(5) cha Sheria Na. 9 ya mwaka 1992 ya Fedha za Serikali za Mitaa, Baraza la Madiwani la Halmashauri linalo jukumu la kuhakikisha shughuli za Halmashauri zinatekelezwa na kumwajibisha mtendaji mkuu au mtumishi mwingine pale anaposhindwa kutekeleza wajibu wake. (b) Mheshimiwa Spika, Serikali inazo taratibu zilizokubalika kisheria katika kuwezesha mitiririko wa mawasiliano na utekelezaji wa mipango na maagizo ya Kitaifa hadi ngazi ya Vijiji. Taratibu hizo ni pamoja na kuwepo kwa miundo ya Wizara, Mikoa, Wilaya na Serikali za Vijiji ,ambazo zina uhusiano wa kirasimu toka juu hadi chini unaoleta uwajibikaji. Utaratibu huu unahakikisha maelekezo ya Serikali yanawafikia wahusika, yanatekelezwa, yanafuatiliwa na yanatolewa taarifa. Aidha, upo pia utaratibu wa kupitisha maamuzi na maagizo kuanzia Baraza la Mawaziri kwenda Wizara husika, Mikoa hadi Wilaya, kwa maana ya Serikali na Halmashauri. Mfumo huu pia unasisitiza ufuatiliaji wa maagizo na utoaji wa taarifa. Vile vile, sheria mbalimbali zinazotungwa na Wizara na Halmashauri, zinalenga kusimamia utekelezaji wa sera, maagizo na mipango inayoandaliwa. Kupitia sheria zilizotungwa, miongozo na nyaraka mbalimbali za Serikali, wananchi wanazo haki zote kufuatilia na kuuliza au kwa upande wa Mabaraza ya Madiwani kumchukulia hatua mtumishi mzembe. 4 Mwisho ni mfumo uliopo kuanzia ngazi ya Taifa, Wilaya na hadi Vijijini. Mfumo huu unawawezesha viongozi hawa kutoa maelekezo na ufafanuzi wa miongozo mbalimbali na maagizo ya Serikali. MHE. MBARUK K. MWANDORO: Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages122 Page
-
File Size-