Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA __________________ MAJADILIANO YA BUNGE __________________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Ishirini na Tatu - Tarehe 14 Julai, 2003 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Naibu Spika (Mhe. Juma J. Akukweti) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Taarifa ya Mwaka ya Utekelezaji na Hesabu zilizokaguliwa za Bodi ya Usajili wa Wahandisi kwa Mwaka wa Fedha 2001/2002 (The Annual Performance Report and Audited Accounts of the Engineers Registration Board for the Financial year 2001/2002). NAIBU WAZIRI WA AFYA: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya kwa Mwaka wa Fedha 2003/2004. MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII: Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Afya katika mwaka uliopita, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2003/2004. MASWALI NA MAJIBU Na. 220 Mashamba ya Mifugo MHE. MARIA D. WATONDOHA (k.n.y. MHE. PAUL P. KIMITI) aliuliza:- Kwa kuwa Mkoa wa Rukwa unayo mashamba makubwa ya mifugo kama vile Kalambo, Malonje na Shamba la Uzalishaji wa Mitamba (Nkundi):- (a) Je, Serikali inatoa tamko gani kwa kila shamba ili wananchi wajue hatma ya mashamba hayo? (b) Kwa kuwa uamuzi na jinsi ya kuyatumia mashamba hayo unazidi kuchelewa; je, Serikali haioni kuwa upo uwezekano wa mashamba hayo kuvamiwa na wananchi wenye shida ya ardhi? WAZIRI WA MAJI NA MAENDELEO YA MIFUGO alijibu:- 1 Mheshimiwa Naibu Spika, swali hili linafanana sana na swali Na. 75 lililoulizwa na Mheshimiwa Ponsiano D. Nyami, tulilolijibu tarehe 20 Juni, 2003. Mheshimiwa Naibu Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Paul P. Kimiti, Mbunge wa Sumbawanga Mjini, naomba kutoa maelezo yafuatayo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kutokana na kasi ndogo ya utekelezaji wa mkakati wa ubinafsishaji wa mashamba ya Serikali wa mwaka 1996, Serikali ilirejea upya mkakati huo kwa kuzingatia uwekaji wa mazingira mazuri ya uwekezaji kwa wananchi ili kutoa nafasi kwa wananchi wengi zaidi kushiriki katika kumiliki na kuendesha ranchi na mashamba na kuzingatia matatizo ya ardhi katika baadhi ya maeneo yanayozunguka mashamba na ranchi hizo. Mashamba ya Kalambo, Malonje na Nkundi ni kati ya mashamba yaliyoguswa na mkakati huo. Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya maelezo hayo, sasa naomba kujibu swali la Mheshimiwa Paul P. Kimiti, Mbunge wa Sumbawanga Mjini, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Serikali imekwishatoa tamko kuhusu mashamba haya. Ranchi ya Kalambo yenye ukubwa wa hekta 64,650 itatenga hekta 20,000 zitakazotumika kama ranchi ya mfano chini ya Kampuni ya NARCO na eneo litakalobaki litagawanywa katika maeneo ya hekta 4,000 yatakayomilikishwa kwa wafugaji wadogo wadogo watakaofuga kibiashara. Shamba la Malonje lenye ukubwa wa hekta 15,000 litagawanywa katika vipande vya hekta 50 tayari kwa ajili ya kuwagawia wafugaji wadogo wadogo wenye nia ya kuendeleza ufugaji wa ng’ombe wa maziwa. Utaratibu wa kuyagawa maeneo ya mashamba haya ya Kalambo na Malonje unaandaliwa na wananchi watajulishwa na kushirikishwa. Shamba la kuzalisha mifugo la Nkundi limekwishagawiwa kwa mwekezaji mwananchi, anayejulikana kwa jina la Sumbawanga Agricultural and Animal Food Company wa huko huko Sumbawanga. (b) Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba, jinsi tunavyochelewa kuyagawa mashamba haya, ndivyo uwezekano wa mashamba hayo kuvamiwa na wananchi unavyoongezeka. Kwa bahati nzuri, utekelezaji wa tamko la Serikali kuhusu mashamba haya umekwishaanza. Aidha, taratibu za kupima na kuligawa Shamba la Malonje na Ranchi ya Kalambo, zinaendelea na mara kazi hii itakapokamilika, wananchi wenye shida ya ardhi na wenye nia ya kufuga watajulishwa na watakaribishwa na hatimaye waweze kuyamiliki maeneo hayo. MHE. MARIA D. WATONDOHA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza maswali mawili madogo ya nyongeza. Kwa kuwa ni dhahiri kwamba wananchi wana njaa na kiu ya kupata mashamba haya; na kwa kuwa Mkoa wa Rukwa ni Mkoa mmojawapo uliovamiwa na wafugaji wengi ambao wanafuata malisho; je, Serikali itakuwa tayari kutupa deadline badala ya kusema kwamba wanatarajia tu kuandaa utaratibu? Pili, je, Serikali itaweka bayana kwa uwazi kabisa ili wananchi wasipate mizengwe katika ugawaji wa mashamba hayo? WAZIRI WA MAJI NA MAENDELEO YA MIFUGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ninakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwa suala la kuweka kipindi. Kwa taarifa yako, tutamaliza kuyagawa mashamba haya kabla ya Bajeti ya mwaka kesho. Tunakwenda taratibu kwa sababu inabidi uyapime ili unapokwenda kumwonyesha hekta 4,000 zinakuwa zimekwishapimwa na unampa hati yako ili aweze kwenda kupata fedha Benki. Mheshimiwa Naibu Spika, pili, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba, ni kweli kuna matatizo ya ardhi kule Sumbawanga na wakati tunagawa mashamba haya, tutazingatia maombi na rai za viongozi kuhusu wananchi wao ambao hawana maeneo. MHE. LUDOVICK J. MWANANZILA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru sana kwa kunipatia nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa Mheshimiwa Waziri ameeleza kwa kina 2 jinsi shamba la Serikali lilivyoweza kubinafsishwa na akapewa mwekezaji Mtanzania. Lakini kwa sababu Shamba la Kalambo lipo katika Jimbo la Kalambo na linapakana na Nkasi na hili shamba la Serikali lililobinafsishwa kwa mwekezaji binafsi, suala la kuwajali wananchi na kuweza kuwapatia nafasi halikufanyika na wasiwasi huo umeongezeka sana kwa wananchi wale ambao wamekuwa na kiu ya kusubiri ili waweze kupewa maeneo katika hilo Shamba la Kalambo; je, Serikali inawathibitishia vipi kwamba lile lililotokea katika Shamba la Nkundi halitatokea katika Shamba la Kalambo kwa wananchi wa Jimbo la Kalambo pamoja na Wilaya ya Nkasi? WAZIRI WA MAJI NA MAENDELEO YA MIFUGO: Mheshimiwa Naibu Spika, nimerudia kueleza hapa kwamba, Serikali itawashirikisha viongozi wa Wilaya na Mkoa na mimi mwenyewe nitakuja Rukwa kuhakikisha kwamba kazi hiyo inatekelezwa katika utaratibu unaotakiwa. (Makofi) Na. 221 Matatizo ya Mifugo MHE. EMMANUEL E. KIPOLE aliuliza:- Kwa kuwa afya ya mifugo ni muhimu sana katika kupata mifugo bora yenye ushindani wa biashara hasa katika kipindi hiki tunapoelekea kufungua mipaka ya biashara katika nchi za Jumuiya ya Afrika Mashariki; na kwa kuwa afya mbaya ya mifugo yetu husababishwa zaidi na maji machafu wanayonyweshwa na kupe wanaowashambulia; na kwa kuwa imeelezwa bayana kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2000 kwamba matatizo niliyoainisha hapo juu yangeshughulikiwa kwenye awamu hii ya uongozi:- (a) Je, ni mabwawa na majosho mangapi yamefufuliwa na mapya mangapi yanajengwa kwenye Jimbo la Msalala katika kipindi cha 2000 - 2002? (b) Kwa aina ya ufugaji hapa nchini hasa kwenye maeneo ya wafugaji kama yale ya Shinyanga; je, ni wastani wa ng’ombe wangapi wanaotumia bwawa moja la maji kwa mwaka? WAZIRI WA MAJI NA MAENDELEO YA MIFUGO alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Emmanuel E. Kipole, Mbunge wa Msalala, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli afya bora ya mifugo itawezesha kutoa ushindani mzuri wa biashara ya mifugo na hasa tunapolenga masoko ya Jumuiya ya Afrika ya Mashariki na mengineyo. Mheshimiwa Naibu Spika, afya mbaya ya mifugo husababishwa na sababu mbalimbali. Hii ni pamoja na magonjwa, ukosefu wa lishe na maji hasa vipindi vya ukame. Lakini pia si sahihi kuwanywesha mifugo maji machafu maana kwa kufanya hivyo kutasababisha madhara ya afya zao. Napenda nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge kwamba, Wizara inatekeleza kikamilifu, maagizo yote yaliyoelekezwa na Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2000. Mheshimiwa Naibu Spika, katika Jimbo la Msalala, kwa kipindi cha mwaka 2000/2002, hakuna bwawa lililofufuliwa. Lakini katika kipindi cha mwaka 2002/2003, mabwawa ya Mwashigini, Ngaya na Banhi yamepewa jumla ya shilingi milioni tisa, sawa na shilingi milioni tatu kwa kila bwawa. Huo ni mchango wa Serikali. Katika taratibu za uchimbaji wa mabwawa, mambo yanayopaswa kuzingatiwa ni kwamba, Serikali inatoa asilimia 50, Halmashauri asilimia 30 na wananchi wenyewe asilimia 20. Serikali imekwishatoa mchango wake ila bado Halmashauri na wananchi ambao nao wakitimiza mchango wao kazi hiyo ya ujenzi wa mabwawa itakamilika mapema iwezekanavyo. Kwa upande wa majosho taarifa tulizonazo ni kwamba, Josho la Bulige, Ntobo A, Ntobo B na Mondo, yamefufuliwa na yanafanya kazi. Juhudi zinafanywa za kuunda vikundi ili viweze kuyaendesha kwa ufanisi. 3 (b) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa aina ya ufugaji hapa nchini hasa kwenye maeneo yenye mifugo mingi kama Shinyanga, inatakiwa iwe na mabwawa ya kutosha kwa kila Kijiji. Wastani wa mahitaji ya ng’ombe mmoja ni lita 40 za maji kwa siku. Kwa hiyo, bwawa lenye ujazo wa lita milioni kumi na tano litakidhi mahitaji ya ng’ombe elfu moja kwa mwaka mmoja. Pamoja na kukidhi mahitaji ya maji, vile vile tahadhari inatakiwa kuchukuliwa ili idadi ya mifugo iwiane na uwezo wa ardhi. Mathalani kwa Mkoa wa Shinyanga, uwezo wa ardhi yake (Carrying Capacity) ni ng’ombe mmoja kwa hekta nne kwa mwaka. MHE. EMMANUEL E. KIPOLE: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi ili niweze kuuliza swali la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri sana ya Mheshimiwa Waziri, ambayo kwa kweli ni sahihi kama alivyotaja; hizi pesa shilingi milioni tisa alizozitaja ni kweli zimefika Wilayani lakini kumekuwa na tatizo kubwa sana la vitendea kazi; wananchi pia wako tayari kutoa mchango alioutaja wa asilimia aliyoitaja lakini tatizo kama nilivyosema ni vitendea kazi; je, Wizara itakuwa na mpango wowote wa kufanya utaratibu wa kupeleka