4 DESEMBA, 2013 MREMA 1.Pmd

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

4 DESEMBA, 2013 MREMA 1.Pmd Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA KUMI NA NNE Kikao cha Pili – Tarehe 4 Desemba, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 16 Uhalali wa Baadhi ya vyama vya Siasa Nchini MHE. MARIAM R. KASEMBE (K.n.y. MHE. PROF. DAVID H. MWAKYUSA) aliuliza:- Matamanio ya kila Chama cha Siasa ni kupata uungwaji mkono kwa idadi kubwa ya wananchi ili siku moja kishike dola na kuongoza nchi, kati ya vyama kumi na nane (18) vya siasa vyenye usajili wa kudumu nchini baadhi yake havijaweza kushinda hata uongozi wa kitongoji katika chaguzi mbalimbali zilizopita:- Je, vyama hivyo vinapata uhalali kutoka kipengele gani cha sheria kinachoviwezesha kubakia katika daftari la usajili wa vyama vya siasa? 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) WAZIRI WA NCHI,OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Profesa David Homeli Mwakyusa, lililoulizwa hapa na Mheshimiwa Kasembe, Mbunge wa Masasi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, hadi sasa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ni ishirini na moja (21) na siyo (18) kama ilivyoulizwa na Mheshimiwa Mbunge. Aidha, ni kweli kwamba baadhi ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu havijawahi kushinda uongozi katika chaguzi wa Serikali za Mitaa au Uchaguzi Mkuu. Mheshimiwa Spika, Sheria ya Vyama vya Siasa Namba 5 ya mwaka 1992 haitoi mamlaka kwa msajili kuvifutia usajili vyama vya siasa ambavyo havijashiriki au kushindwa katika uchaguzi mbalimbali za kisiasa. Kwa mujibu wa kifungu cha 19 cha Sheria hiyo, chama cha siasa kinaweza kufutwa iwapo kimekiuka masharti ya usajili. MHE. MARIAM R. KASEMBE: Ahsante sana Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa kuwa katika majibu ya Mheshimiwa Waziri amesema kwamba Sheria tuliyonayo kwa hivi sasa hairuhusu kufutiwa usajili wa vyama kwa sababu ya kukosa nafasi katika uchaguzi. Je, Serikali iko tayari kuleta Sheria hiyo ili tuweze kuifanyia marekebisho? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, Ofisi yangu sasa hivi inafanya mapitio ya Sheria hii na sasa tuko kwenye zoezi la kushirikisha wadau. Kwa kadiri mchakato utakavyoendelea kwa vyovyote vile tutakuwa tayari kuleta marekebisho muhimu ya Sheria hii hapa Bungeni. SPIKA: Naomba tuendelee na swali linalofuata Mheshimiwa Salum Khalfan Barwany, kwa niaba yake Mheshimiwa Rajab ndiyo. 2 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) Na. 17 Mikopo Benki ya Dunia MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED (K.n.y. MHE. SALUM K. BARWANY) aliuliza:- Benki ya Dunia inatoa mikopo kwa Halmashauri kadhaa hapa nchini kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara:- (a) Je, kwa nini miundombinu hiyo inaharibika bila matengenezo? (b) Je, taa za barabarani za mtaa wa Buguruni Malapa zimekwenda wapi? (c) Je, uharibifu kama huu unaotokea Dar es Salaam utakuwa vipi kwa Manispaa ya Lindi inayopewa mgao wa kata 13 badala ya 18 zilizopo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Salum Khalfan Barwany, Mbunge wa Lindi Mjini, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, miundombinu hii imeharibika ndani ya kipindi kifupi baada ya kumalizika kwa ujenzi kutokana na kukithiri kwa matumizi ya barabara yasiyozingatia usalama, wizi wa vifaa vya barabarani na uwingi wa magari yanayotumia barabara hizi. (b)Mheshimiwa Spika, mradi wa Community Infrastructure Upgrading Programme (CIUP) katika mitaa ya Madenge na Malapa ilihusisha uwekaji wa taa barabarani 91, kujenga barabara ya Lami ya Mnyamani na mifereji ya mvua yenye urefu wa kilometa 3.23 na kampuni ya M/S Estim Contruction Ltd. kwa gharama ya shilingi bilioni 1.6 ambazo 3 WAZIRIHii ni WANakala NCHI, OFISI ya YAMtandao WAZIRI MKUU, (Online TAWALA ZADocument) MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) zilikuwa ni mkopo kutoka Benki ya Dunia. Baadhi ya taa na nguzo za barabarani katika mtaa wa Buguruni Malapa zimeibiwa na wananchi wasio waaminifu na zingine kugongwa na magari na kuanguka na kesi moja ipo Mahakamani. (c)Mheshimiwa Spika, suala la mgao wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa ULGSP unazingatia idadi ya watu walio kwenye Manispaa na Miji. Miradi hiyo haipangwi kwa kuzingatia maeneo ya Kata. Hivyo, Manispaa ya Lindi ni kati ya Halmashauri 18 nchini zinazonufaika na mradi wa huo utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2013/2014 na imepangiwa dola za kimarekani milioni 5.6 sawa na shilingi bilioni 9 kwa kipindi chote cha mradi. MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED: Ahsante nakushukuru Mheshimiwa Spika. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri nilikuwa na maswali mawili madogo ya nyongeza. Kwanza ni kwamba Mheshimiwa Waziri wakati anajibu swali hili la msingi anasema kwamba kuharibika kwa barabara hizi zimetokana na uwingi wa magari yanayotumia barabara hizi. Nataka kumwuliza Mheshimiwa Waziri hivyo ni kusema kwamba kabla ya huu mradi hakukufanyika feasibility study, ili kukajulikana magari ambayo yatakuwa yanatumia barabara hizi? Lakini la pili, ni kwamba hivi karibuni tu wafadhili wetu ambao wanafadhili Local Government Reform Programme ambayo sasa hivi anataka kuingia katika program namba mbili walitishia kusitisha fedha zao kwa sababu ya ubadhirifu, wizi na ufisadi uliofanywa na TAMISEMI. Je, Mheshimiwa Waziri Wizara yako imejipangaje katika huu mradi mkubwa wa ULGSP? (Makofi) 4 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, feasibility study imefanyika. Lakini mara nyingi barabara ikiwa mbovu magari mengi yana kawaida ya kutoipenda hiyo barabara kuipita na mara inapotengezwa idadi ya magari yanaongezeka na pia katika barabara zetu nyingi za mitaani hatuna mizani ya kuweza kuzuia magari ambayo yanazidisha uzito. Kuhusu suala la pili la wafadhili kutishia katika mradi wa Local Government Reform ni kweli kwamba wakati wafadhili walivyofanya uhakiki au walivyofanya audit ukaguzi wa mradi huu wa Reform kwa mwaka 2009/2010, na 2010/ 2011 waligundua kuwepo kwa ubadhirifu na mimi kama Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu niliingia kati. Wale ambao walikuwa wanasimamia huo mradi tulisimamisha mkataba wao kwa sababu walikuwa wameajiriwa kwa mkataba. Tukateua watu wengine na pia gratuity yao ambayo walipaswa kupata tuliizuia na pia tumewapeleka katika vyombo ya Sheria ili waweze kuchukliwa hatua. MHE. MUSSA Z. AZZAN: Nakushukuru Mheshimiwa Spika. Mradi huu wa ULGSP uko katika Mkoa wa Dar es Salaam katika Wilaya ya Ilala na Wilaya ya Ilala iko jumla kilomita 26 za lami. Lakini cha kushangaza Mheshimiwa Spika, TAMISEMI ilileta maagizo, wanavyosema Watendaji wetu. Inawezekana si kweli. Katika kilomita 26 hizi Jimbo la Ilala imepewa kilometa 2 tu na ndiyo Centre ya uchumi wa nchi yetu na Jimbo la Ukonga walipata kilomita zingine waligawana kilomita 24. Je, Serikali iko tayari sasa ku-revisit mpango huu na kuzigawia kilomita nane nane kila Jimbo katika Wilaya ya Ilala? 5 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, kwa kweli Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI haikuhusika katika kupanga kilometa ngapi ziende katika Jimbo gani. Sisi kama TAMISEMI tulichofanya tuliwapelekea manual ambao wao wenyewe walikuwa na uwezo wa kuchagua wanataka kutekeleza miradi ya aina gani kwa sababu inahusu utengenezaji wa barabara za lami za changarawe, uwekezaji wa taa za barabarani. Ujengaji wa mifereji ya maji ya mvua. Kwa hiyo, Halmashauri yenyewe husika ndiyo inayohusika kuchagua wanatekeleza miradi gani na maeneo gani. Lakini kwa vile yapo malalamiko, nitawaagiza wataalam wangu wafuatilie kuona kama kweli hayo mambo yamefanyika kwa kisingizio kwamba sisi tumewaagiza. Lakini napenda nikuhakikishie Mheshemiwa Mbunge, ni Wilaya yenyewe ya Ilala ambayo imechagua maeneo gani iende. Lakini nakuahidi kwamba tutafuatilia na kama itabidi basi tutaingilia kati. (Makofi) SPIKA: Naomba tuendelee na swali linalofuata. Mheshimiwa Felix Mkosamali. Na. 18 Mapato Yatokanayo na Minara ya Simu MHE. FELIX F. MKOSAMALI aliuliza:- Ipo minara ya simu kwenye maeneo mbalimbali ya Kibondo Mjini:- (a) Je, ni utaratibu gani unaotumika kuilipa fedha Serikali ya Kijiji cha Kibondo Mjini kutokana na minara hiyo? 6 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [MHE. FELIX F. MKOSAMALI] (b) Je, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo imekusanya fedha kiasi gani mwaka 2003 hadi 2013 na kiasi gani Kijiji cha Kibondo kimepata kati ya hizo? (c)Je, utaratibu gani wa mapato unatumika kwa mtu aliyetoa kiwanja, Serikali ya Kijiji na Halmashauri kwa ajili ya minara? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Felix Francis Mkosamali, Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, lenye kipengele (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, hakuna utaratibu wowote wa kulipa fedha Serikali ya Kijiji cha Kibondo Mjini. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Kijiji ya Kibondo Mjini haina eneo la ardhi inayomiliki kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 176 la tarehe 9 Agosti, 1996, ambalo lilitangaza kuwa maeneo ya Kibondo Mjini na Kifura yaliyopo katika Wilaya ya sasa ya Kibondo kuwa ni maeneo ya Mipango Miji. Kwa mujibu wa Tangazo hilo la Serikali na Sheria za Ardhi katika maeneo ya Kibondo Mjini
Recommended publications
  • Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 BUNGE LA TANZANIA
    Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ________________________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Kumi na Tisa – Tarehe 27 Mei, 2014 (Mkutano Ulianza Saa tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha kwa Mwaka 2012/2013 (The Annual Report and Accounts of Arusha International Conference Centre for the Year 2012/2013). Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. BETTY E. MACHANGU (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na Maoni ya Kamati 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. ABDULKARIM E.H. SHAH (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014 na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015.
    [Show full text]
  • 1458125471-Hs-6-8-20
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA __________________ MAJADILIANO YA BUNGE __________________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Ishirini na Tatu - Tarehe 14 Julai, 2003 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Naibu Spika (Mhe. Juma J. Akukweti) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Taarifa ya Mwaka ya Utekelezaji na Hesabu zilizokaguliwa za Bodi ya Usajili wa Wahandisi kwa Mwaka wa Fedha 2001/2002 (The Annual Performance Report and Audited Accounts of the Engineers Registration Board for the Financial year 2001/2002). NAIBU WAZIRI WA AFYA: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Afya kwa Mwaka wa Fedha 2003/2004. MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII: Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Afya katika mwaka uliopita, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2003/2004. MASWALI NA MAJIBU Na. 220 Mashamba ya Mifugo MHE. MARIA D. WATONDOHA (k.n.y. MHE. PAUL P. KIMITI) aliuliza:- Kwa kuwa Mkoa wa Rukwa unayo mashamba makubwa ya mifugo kama vile Kalambo, Malonje na Shamba la Uzalishaji wa Mitamba (Nkundi):- (a) Je, Serikali inatoa tamko gani kwa kila shamba ili wananchi wajue hatma ya mashamba hayo? (b) Kwa kuwa uamuzi na jinsi ya kuyatumia mashamba hayo unazidi kuchelewa; je, Serikali haioni kuwa upo uwezekano wa mashamba hayo kuvamiwa na wananchi wenye shida ya ardhi? WAZIRI WA MAJI NA MAENDELEO YA MIFUGO alijibu:- 1 Mheshimiwa Naibu Spika, swali hili linafanana sana na swali Na. 75 lililoulizwa na Mheshimiwa Ponsiano D. Nyami, tulilolijibu tarehe 20 Juni, 2003.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Ishirini na Tano - Tarehe 16 Julai, 2003 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Pius Msekwa) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA SAYANSI, TEKNOLOJIA NA ELIMU YA JUU: Hotuba ya Waziri wa Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu kwa Mwaka wa Fedha 2003/2004. MHE. MARGARETH A. MKANGA (k.n.y. MHE. OMAR S. KWAANGW’ - MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA ZA JAMII): Taarifa ya Kamati ya Huduma za Jamii kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Sayansi, Teknolojia na Elimu ya Juu katika mwaka uliopita, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka 2003/2004. MASWALI NA MAJIBU Na. 239 Majimbo ya Uchaguzi MHE. JAMES P. MUSALIKA (k.n.y. MHE. DR. WILLIAM F. SHIJA) aliuliza:- Kwa kuwa baadhi ya Majimbo ya Uchaguzi ni makubwa sana kijiografia na kwa wingi wa watu; je, Serikali itashauriana na Tume ya Uchaguzi ili kuongeza Majimbo ya Uchaguzi katika baadhi ya maeneo nchini katika Uchaguzi wa mwaka 2005? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (MHE. MUHAMMED SEIF KHATIB) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Dr. William Shija, Mbunge wa Sengerema, naomba kutoa maelezo yafuatayo:- Mheshimiwa Spika, lilipokuwa linajibiwa swali la Mheshimiwa Ireneus Ngwatura, Mbunge wa Jimbo la Mbinga Magharibi na pia swali la Mheshimiwa Sophia Simba, Mbunge wa Viti Maalum, CCM 1 katika Mikutano ya Saba na Kumi na Moja sawia ya Bungeni, nilieleza kwamba, kwa mujibu wa Ibara ya 75(1) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungao wa Tanzania 1977, Jamhuri ya Muungano inaweza kugawanywa katika Majimbo ya Uchaguzi kwa idadi na namna itakavyoamuliwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi baada ya kupata kibali cha Mheshimiwa Rais.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge
    [Show full text]
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? With Partial Support from a TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? ACKNOWLEDGEMENTS This review was compiled and edited by Tanzania Development Research Group (TADREG) under the supervision of the Steering Group of Policy Forum members, and has been financially supported in part by Water Aid in Tanzania and Policy Forum core funders. The cartoons were drawn by Adam Lutta Published 2013 For more information and to order copies of the review please contact: Policy Forum P.O Box 38486 Dar es Salaam Tel: +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] ISBN: 978-9987 -708-09-3 © Policy Forum The conclusions drawn and views expressed on the basis of the data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. Every effort has been made to verify the accuracy of the information contained in this review, including allegations. Nevertheless, Policy Forum cannot guarantee the accuracy and completeness of the contents. Whereas any part of this review may be reproduced providing it is properly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. Designed by: Jamana Printers b TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TABLE OF CONTENTS POLICY FORUM’s OBJECTIVES .............................................................................................................
    [Show full text]
  • MKUTANO WA 18 TAREHE 5 FEBRUARI, 2015 MREMA 1.Pmd
    5 FEBRUARI, 2015 BUNGE LA TANZANIA _________________ MAJADILIANO YA BUNGE __________________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Tisa – Tarehe 5 Februari, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, Kiongozi wa Kambi ya Upinzani Bungeni, leo sijamwona. Kwa hiyo tunaendelea na Maswali kwa Waziri Mkuu na atakayeanza ni Mheshimiwa Murtaza A. Mangungu. MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa vipindi tofauti vya Bunge Mheshimiwa Peter Msigwa, Mheshimiwa Mussa Zungu na hata Mheshimiwa Murtaza A. Mangungu wamekuwa wakiuliza swali kuhusiana na manyanyaso wanayoyapata wafanyabiashara Wadogo Wadogo pamoja na Mamalishe. Kwa kipindi hicho chote umekuwa ukitoa maagizo na maelekezo, inavyoonekana mamlaka zinazosimamia hili jambo haziko tayari kutii amri yako. 1 5 FEBRUARI, 2015 Je, unawaambia nini Watanzania na Bunge hili kwa ujumla? WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Murtaza Mangungu swali lake kama ifuatavyo:- Suala hili la vijana wetu ambao tunawajua kama Wamachinga, kwanza nataka nikiri kwamba ni suala kubwa na ni tatizo kubwa na si la Jiji la Dar es Salaam tu, bali lipo karibu katika miji mingi. Kwa hiyo, ni jambo ambalo lazima twende nalo kwa kiwango ambacho tutakuwa na uhakika kwamba tunalipatia ufumbuzi wa kudumu. Kwa hiyo, ni kweli kwamba mara kadhaa kuna maelekezo yametolewa yakatekelezwa sehemu na sehemu nyingine hayakutekelezwa kikamilifu kulingana na mazingira ya jambo lenyewe lilivyo. Lakini dhamira ya kutaka kumaliza tatizo hili la Wamachinga bado ipo palepale na kwa bahati nzuri umeuliza wakati mzuri kwa sababu jana tu nimepata taarifa ambayo nimeandikiwa na Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI ambayo wanaleta mapendekezo kwangu juu ya utaratibu ambao wanafikiri unaweza ukatatua tatizo hili ambalo lipo sehemu nyingi.
    [Show full text]
  • Consequences for Women's Leadership
    The Politics Behind Gender Quotas: Consequences for Women’s Leadership Equity in African Legislatures by Christie Marie Arendt B.A. in Interdisciplinary Studies in Social Science, May 2004, Michigan State University M.A. in International Affairs, May 2006, The George Washington University A Dissertation submitted to The Faculty of The Columbian College of Arts and Sciences of The George Washington University in partial fulfillment of the requirements for the degree of Doctor of Philosophy January 31, 2017 Dissertation directed by Kimberly J. Morgan Professor of Political Science and International Affairs The Columbian College of Arts and Sciences of The George Washington University certifies that Christie Marie Arendt has passed the Final Examination for the degree of Doctor of Philosophy as of December 16, 2016. This is the final and approved form of the dissertation. The Politics Behind Gender Quotas: Consequences for Women’s Leadership Equity in African Legislatures Christie Marie Arendt Dissertation Research Committee: Kimberly J. Morgan, Professor of Political Science and International Affairs, Dissertation Director Jennifer Brinkerhoff, Professor of International Affairs, International Business, and Public Policy & Public Administration Eric Kramon, Assistant Professor of Political Science and International Affairs, Committee Member ii © Copyright 2017 by Christie Marie Arendt All rights reserved iii Dedication To my parents, Anne and Steve Arendt, none of this was possible without your enduring love and support. iv Acknowledgments This dissertation benefitted from the encouragement and guidance of a number of people. As an alumna of The George Washington University’s Elliott School of International Affairs, I knew that GW would provide a perfect environment to pursue my doctoral studies.
    [Show full text]
  • Secretariat Distr.: Limited
    UNITED NATIONS ST /SG/SER.C/L.615 _____________________________________________________________________________________________ Secretariat Distr.: Limited 6 October 2006 PROTOCOL AND LIAISON LIST OF DELEGATIONS TO THE SIXTY-FIRST SESSION OF THE GENERAL ASSEMBLY I. MEMBER STATES Page Page Afghanistan.........................................................................5 Cyprus.............................................................................. 32 Albania ...............................................................................5 Czech Republic ................................................................ 33 Algeria ...............................................................................6 Democratic People’s Republic of Korea .......................... 34 Andorra...............................................................................7 Denmark........................................................................... 35 Angola ................................................................................7 Djibouti ............................................................................ 36 Antigua and Barbuda ..........................................................8 Dominica.......................................................................... 36 Argentina............................................................................8 Dominican Republic......................................................... 37 Armenia..............................................................................9
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA NANE Kikao Cha
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Kumi na Tatu – Tarehe 29 Juni, 2007 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii kwa Kuwasilisha Hati. Naomba niwashukuru nyote jinsi tulivyoshirikiana kwa pamoja kuweza kumsindikiza mwenzetu Marehemu Amina Chifupa Mpakanjia, katika safari yake ya mwisho. Waheshimiwa Wabunge, napenda niwashukuru Kamati ya Uongozi na Tume ya Huduma za Bunge, lakini pia TWPG kwa kushirikiana vizuri sana kuweza kumsindikiza mwenzetu kwa heshima; na kipekee naomba Mheshimiwa Waziri Mkuu atutolee salamu za shukrani kwa Mheshimiwa Rais kwa jinsi ambavyo Mheshimiwa Rais alivyokuwa karibu nasi kila dakika kwa mawasiliano hadi hapo jana kule Njombe. Waheshimiwa Wabunge, narejea tena Mungu ailaze roho ya Marehemu Mheshimiwa Amina Chifupa Mpakanjia, mahali pema peponi. Amin. Hati ifuatayo iliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MALIASILI NA UTALII: Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Shirika la Hifadhi ya Taifa (TANAPA) kwa mwaka 2005/2006 (The Annual Report and Accounts of the Tanzania National Parks for the Year 2005/2006). MASWALI NA MAJIBU Na. 106 Ubovu wa Barabara za Jiji la Dar es Salaam MHE. MUSSA A. ZUNGU aliuliza:- 1 Kwa kuwa sura ya nchi yetu iko katika Jimbo la Ilala; na kwa kuwa barabara nyingi za Jiji la Dar es Salaam ni mbovu sana hali inayosababisha msongamano wa magari na
    [Show full text]
  • Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 MAJADILIANO YA BUNGE
    Nakala ya Mtandao (Online Document) MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA ISHIRINI __________ Kikao cha Ishirini na Moja - Tarehe 5 Juni, 2015 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, napenda kuchukua nafasi hii kuwapa pole wote kwa msiba uliotupata, msiba ulitokea wakati nikiwa Geneva ambapo tulikuwa na kikao cha Kamati Ndogo ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Maspika wote duniani utakaofanyika mwezi wa Nane, sasa kuna Maspika kumi ndiyo tupo kwenye maandalizi ya mkutano huo na kilikuwa ni kikao chetu cha mwisho kabla ya mkutano huo. Kwa hiyo, wakati msiba unatokea nilikuwa huko, nilipewa taarifa na nilisikitika sana. Kwa hiyo, tutatangaza baadaye mchana, ni akina nani watakaokwenda kuzika kesho. Katibu! HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. CHARLES M. KITWANGA): Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa Fedha, 2015/2016. MHE. DAVID H. MWAKYUSA (k.n.y. MHE. PROF. PETER M. MSOLLA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2015/2016. MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED (k.n.y. MHE. MAGDALENA H. SAKAYA - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA MAJI): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016.
    [Show full text]
  • Tarehe 3 Agosti, 2012
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Arobaini – Tarehe 3 Agosti, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Naibu Spika, (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha, 2012/2013. NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha, 2012/2013. MHE. MUSSA HASSAN MUSSA (K.n.y. MHE. EDWARD N. LOWASSA - MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka 2011/2012 pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha, 2012/2013. MHE. RAYA IBRAHIM KHAMIS (K.n.y. MHE. EZEKIA D. WENJE - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA USHIRIKIANO WA AFRIKA YA MASHARIKI): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha, 2012/2013. MASWALI NA MAJIBU Na. 315 Malipo ya Malimbikizo ya Wafanyakazi – Geita MHE. DONALD K. MAX aliuliza:- Wafanyakazi wa Wilayani wananyanyaswa sana na hawalipwi malimbikizo yao na wakati mwingine fedha zao zinapoletwa wanalipwa kidogo kidogo:- Je, ni lini wafanyakazi Wilayani Geita watalipwa mafao yao? Kwani malimbikizo hadi sasa yanafikia Sh.
    [Show full text]