Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA KUMI NA NNE Kikao cha Pili – Tarehe 4 Desemba, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 16 Uhalali wa Baadhi ya vyama vya Siasa Nchini MHE. MARIAM R. KASEMBE (K.n.y. MHE. PROF. DAVID H. MWAKYUSA) aliuliza:- Matamanio ya kila Chama cha Siasa ni kupata uungwaji mkono kwa idadi kubwa ya wananchi ili siku moja kishike dola na kuongoza nchi, kati ya vyama kumi na nane (18) vya siasa vyenye usajili wa kudumu nchini baadhi yake havijaweza kushinda hata uongozi wa kitongoji katika chaguzi mbalimbali zilizopita:- Je, vyama hivyo vinapata uhalali kutoka kipengele gani cha sheria kinachoviwezesha kubakia katika daftari la usajili wa vyama vya siasa? 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) WAZIRI WA NCHI,OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Profesa David Homeli Mwakyusa, lililoulizwa hapa na Mheshimiwa Kasembe, Mbunge wa Masasi, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, hadi sasa vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu ni ishirini na moja (21) na siyo (18) kama ilivyoulizwa na Mheshimiwa Mbunge. Aidha, ni kweli kwamba baadhi ya vyama vya siasa vyenye usajili wa kudumu havijawahi kushinda uongozi katika chaguzi wa Serikali za Mitaa au Uchaguzi Mkuu. Mheshimiwa Spika, Sheria ya Vyama vya Siasa Namba 5 ya mwaka 1992 haitoi mamlaka kwa msajili kuvifutia usajili vyama vya siasa ambavyo havijashiriki au kushindwa katika uchaguzi mbalimbali za kisiasa. Kwa mujibu wa kifungu cha 19 cha Sheria hiyo, chama cha siasa kinaweza kufutwa iwapo kimekiuka masharti ya usajili. MHE. MARIAM R. KASEMBE: Ahsante sana Mheshimiwa Spika kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa kuwa katika majibu ya Mheshimiwa Waziri amesema kwamba Sheria tuliyonayo kwa hivi sasa hairuhusu kufutiwa usajili wa vyama kwa sababu ya kukosa nafasi katika uchaguzi. Je, Serikali iko tayari kuleta Sheria hiyo ili tuweze kuifanyia marekebisho? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, Ofisi yangu sasa hivi inafanya mapitio ya Sheria hii na sasa tuko kwenye zoezi la kushirikisha wadau. Kwa kadiri mchakato utakavyoendelea kwa vyovyote vile tutakuwa tayari kuleta marekebisho muhimu ya Sheria hii hapa Bungeni. SPIKA: Naomba tuendelee na swali linalofuata Mheshimiwa Salum Khalfan Barwany, kwa niaba yake Mheshimiwa Rajab ndiyo. 2 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) Na. 17 Mikopo Benki ya Dunia MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED (K.n.y. MHE. SALUM K. BARWANY) aliuliza:- Benki ya Dunia inatoa mikopo kwa Halmashauri kadhaa hapa nchini kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya barabara:- (a) Je, kwa nini miundombinu hiyo inaharibika bila matengenezo? (b) Je, taa za barabarani za mtaa wa Buguruni Malapa zimekwenda wapi? (c) Je, uharibifu kama huu unaotokea Dar es Salaam utakuwa vipi kwa Manispaa ya Lindi inayopewa mgao wa kata 13 badala ya 18 zilizopo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Salum Khalfan Barwany, Mbunge wa Lindi Mjini, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, miundombinu hii imeharibika ndani ya kipindi kifupi baada ya kumalizika kwa ujenzi kutokana na kukithiri kwa matumizi ya barabara yasiyozingatia usalama, wizi wa vifaa vya barabarani na uwingi wa magari yanayotumia barabara hizi. (b)Mheshimiwa Spika, mradi wa Community Infrastructure Upgrading Programme (CIUP) katika mitaa ya Madenge na Malapa ilihusisha uwekaji wa taa barabarani 91, kujenga barabara ya Lami ya Mnyamani na mifereji ya mvua yenye urefu wa kilometa 3.23 na kampuni ya M/S Estim Contruction Ltd. kwa gharama ya shilingi bilioni 1.6 ambazo 3 WAZIRIHii ni WANakala NCHI, OFISI ya YAMtandao WAZIRI MKUU, (Online TAWALA ZADocument) MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) zilikuwa ni mkopo kutoka Benki ya Dunia. Baadhi ya taa na nguzo za barabarani katika mtaa wa Buguruni Malapa zimeibiwa na wananchi wasio waaminifu na zingine kugongwa na magari na kuanguka na kesi moja ipo Mahakamani. (c)Mheshimiwa Spika, suala la mgao wa fedha kwa ajili ya utekelezaji wa mpango wa ULGSP unazingatia idadi ya watu walio kwenye Manispaa na Miji. Miradi hiyo haipangwi kwa kuzingatia maeneo ya Kata. Hivyo, Manispaa ya Lindi ni kati ya Halmashauri 18 nchini zinazonufaika na mradi wa huo utakaotekelezwa kwa kipindi cha miaka mitano kuanzia mwaka 2013/2014 na imepangiwa dola za kimarekani milioni 5.6 sawa na shilingi bilioni 9 kwa kipindi chote cha mradi. MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED: Ahsante nakushukuru Mheshimiwa Spika. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri nilikuwa na maswali mawili madogo ya nyongeza. Kwanza ni kwamba Mheshimiwa Waziri wakati anajibu swali hili la msingi anasema kwamba kuharibika kwa barabara hizi zimetokana na uwingi wa magari yanayotumia barabara hizi. Nataka kumwuliza Mheshimiwa Waziri hivyo ni kusema kwamba kabla ya huu mradi hakukufanyika feasibility study, ili kukajulikana magari ambayo yatakuwa yanatumia barabara hizi? Lakini la pili, ni kwamba hivi karibuni tu wafadhili wetu ambao wanafadhili Local Government Reform Programme ambayo sasa hivi anataka kuingia katika program namba mbili walitishia kusitisha fedha zao kwa sababu ya ubadhirifu, wizi na ufisadi uliofanywa na TAMISEMI. Je, Mheshimiwa Waziri Wizara yako imejipangaje katika huu mradi mkubwa wa ULGSP? (Makofi) 4 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, feasibility study imefanyika. Lakini mara nyingi barabara ikiwa mbovu magari mengi yana kawaida ya kutoipenda hiyo barabara kuipita na mara inapotengezwa idadi ya magari yanaongezeka na pia katika barabara zetu nyingi za mitaani hatuna mizani ya kuweza kuzuia magari ambayo yanazidisha uzito. Kuhusu suala la pili la wafadhili kutishia katika mradi wa Local Government Reform ni kweli kwamba wakati wafadhili walivyofanya uhakiki au walivyofanya audit ukaguzi wa mradi huu wa Reform kwa mwaka 2009/2010, na 2010/ 2011 waligundua kuwepo kwa ubadhirifu na mimi kama Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu niliingia kati. Wale ambao walikuwa wanasimamia huo mradi tulisimamisha mkataba wao kwa sababu walikuwa wameajiriwa kwa mkataba. Tukateua watu wengine na pia gratuity yao ambayo walipaswa kupata tuliizuia na pia tumewapeleka katika vyombo ya Sheria ili waweze kuchukliwa hatua. MHE. MUSSA Z. AZZAN: Nakushukuru Mheshimiwa Spika. Mradi huu wa ULGSP uko katika Mkoa wa Dar es Salaam katika Wilaya ya Ilala na Wilaya ya Ilala iko jumla kilomita 26 za lami. Lakini cha kushangaza Mheshimiwa Spika, TAMISEMI ilileta maagizo, wanavyosema Watendaji wetu. Inawezekana si kweli. Katika kilomita 26 hizi Jimbo la Ilala imepewa kilometa 2 tu na ndiyo Centre ya uchumi wa nchi yetu na Jimbo la Ukonga walipata kilomita zingine waligawana kilomita 24. Je, Serikali iko tayari sasa ku-revisit mpango huu na kuzigawia kilomita nane nane kila Jimbo katika Wilaya ya Ilala? 5 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, kwa kweli Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI haikuhusika katika kupanga kilometa ngapi ziende katika Jimbo gani. Sisi kama TAMISEMI tulichofanya tuliwapelekea manual ambao wao wenyewe walikuwa na uwezo wa kuchagua wanataka kutekeleza miradi ya aina gani kwa sababu inahusu utengenezaji wa barabara za lami za changarawe, uwekezaji wa taa za barabarani. Ujengaji wa mifereji ya maji ya mvua. Kwa hiyo, Halmashauri yenyewe husika ndiyo inayohusika kuchagua wanatekeleza miradi gani na maeneo gani. Lakini kwa vile yapo malalamiko, nitawaagiza wataalam wangu wafuatilie kuona kama kweli hayo mambo yamefanyika kwa kisingizio kwamba sisi tumewaagiza. Lakini napenda nikuhakikishie Mheshemiwa Mbunge, ni Wilaya yenyewe ya Ilala ambayo imechagua maeneo gani iende. Lakini nakuahidi kwamba tutafuatilia na kama itabidi basi tutaingilia kati. (Makofi) SPIKA: Naomba tuendelee na swali linalofuata. Mheshimiwa Felix Mkosamali. Na. 18 Mapato Yatokanayo na Minara ya Simu MHE. FELIX F. MKOSAMALI aliuliza:- Ipo minara ya simu kwenye maeneo mbalimbali ya Kibondo Mjini:- (a) Je, ni utaratibu gani unaotumika kuilipa fedha Serikali ya Kijiji cha Kibondo Mjini kutokana na minara hiyo? 6 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [MHE. FELIX F. MKOSAMALI] (b) Je, Halmashauri ya Wilaya ya Kibondo imekusanya fedha kiasi gani mwaka 2003 hadi 2013 na kiasi gani Kijiji cha Kibondo kimepata kati ya hizo? (c)Je, utaratibu gani wa mapato unatumika kwa mtu aliyetoa kiwanja, Serikali ya Kijiji na Halmashauri kwa ajili ya minara? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Felix Francis Mkosamali, Mbunge wa Jimbo la Muhambwe, lenye kipengele (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, hakuna utaratibu wowote wa kulipa fedha Serikali ya Kijiji cha Kibondo Mjini. Mheshimiwa Spika, Serikali ya Kijiji ya Kibondo Mjini haina eneo la ardhi inayomiliki kwa mujibu wa Tangazo la Serikali Na. 176 la tarehe 9 Agosti, 1996, ambalo lilitangaza kuwa maeneo ya Kibondo Mjini na Kifura yaliyopo katika Wilaya ya sasa ya Kibondo kuwa ni maeneo ya Mipango Miji. Kwa mujibu wa Tangazo hilo la Serikali na Sheria za Ardhi katika maeneo ya Kibondo Mjini
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages279 Page
-
File Size-