Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Mbili

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Mbili Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Kumi na Sita – Tarehe 2 Julai, 2008 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA MIUNDOMBINU: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Miundombinu kwa Mwaka wa Fedha 2008/2009. MHE. MOHAMMED H. MISSANGA - MWENYEKITI WA KAMATI YA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Kamati ya Miundombinu kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Miundombinu kwa mwaka Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2008/2009. MHE. SAVELINA S. MWIJAGE (K.n.y. MHE. KABWE Z. ZITTO - MSEMAJI WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA MIUNDOMBINU): Taarifa ya Msemaji wa Kambi ya Upinzani kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Miundombinu kwa Mwaka wa Fedha uliopita, pamoja na maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2008/2009. MASWALI NA MAJIBU Na. 142 1 Utaratibu wa Makabidhiano kwa Waheshimiwa Wabunge MHE. VITA R. KAWAWA (K.n.y. MHE. ENG. STELLA M. MANYANYA) aliuliza:- Kwa kuwa Wabunge wanawakilisha kwa muda wa miaka mitano na kwa kuwa katika kipindi hicho huwa wamepata nyaraka pamoja na mwendelezo wa shughuli mbalimbali katika maeneo yao:- (a)Je, Wabunge wanapoacha uwakilishi hufanya makabidhiano na Mbunge mpya? (b)Kama utaratibu huo haupo, je, Serikali haioni kuwa wananchi wananyimwa mwendelezo wa mambo yanayokuwa yanafuatiliwa? (c)Je, Serikali ina mpango gani wa kuboresha utaratibu uliopo katika kuachiana madaraka kama ilivyo kwenye mihimili mingine ya dola? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Engineer Stella Martin Manyanya, Mbunge wa Viti Maalum lenye sehemu (a), (b) na (c) kwa pamoja kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba Wabunge ni wawakilishi halali wa wananchi kwa mujibu wa Katiba na kwamba uwakilishi wao ni kwa kipindi cha miaka mitano ambapo baada ya kipindi hicho kwisha, uchaguzi Mkuu hutakiwa kufanyika kuchagua wawakilishi wapya wa wananchi kwa njia ya kupigiwa kura. Aidha, kwa mujibu wa mfumo uliopo sasa hakuna utaratibu wa makabidhiano baina ya Mbunge aliyemaliza muda wake na yule anayeingia kuanza muhula mpya wa miaka mitano. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa Waheshimiwa Wabunge ni wawakilishi wa wananchi kwenye Majimbo wanayotoka na kwa kuwa masuala yote yanayohusu utekelezaji wa mipango ya maendeleo kwenye Majimbo hufanyika kupitia vikao halali vya Madiwani kwenye ngazi ya Halmashauri ambapo Waheshimiwa Wabunge ni Wajumbe, Serikali haioni kuwa wananchi wananyimwa fursa ya mwendelezo wa mambo yanayokuwa yanafuatiliwa na Mbunge husika Jimboni kwake, ukiacha utekelezaji wa ahadi binafsi ambazo Mheshimiwa Mbunge alikuwa amewaahidi wananchi wa Jimbo husika wakati wa kampeni za uchaguzi. 2 Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu nyaraka muhimu zinazohusu mambo yaliyojadiliwa katika kipindi kilichopita, taasisi ya Bunge inayo maktaba na Website yenye kumbukumbu za kutosha kuweza kukidhi haja pale inapohitajika. Aidha, nyaraka kuhusu mipango ya maendeleo kwenye Halmashauri ambapo Mbunge anawakilisha Jimbo nazo huweza kupatikana kupitia Ofisi ya Mkurugenzi wa Maendeleo kwenye Halmashauri husika kwani mtendaji huyo hushiriki au kuwakilishwa kwenye vikao vyote vya Baraza la Madiwani na huwajibika pia kutunza taarifa zote muhimu zinazohusu maazimio na maamuzi mbalimbali yanayofanyika kupitia vikao hivyo vya Halamashauri. Kwa sasa Serikali haina mpango wa kubadili utaratibu uliopo isipokuwa msisitizo utaendelea kuwekwa katika kuhakikisha kwamba angalau katika kila Jimbo inajengwa Ofisi ya Mbunge kama ilivyokwishaahidiwa na Serikali. MHE. VITA R. KAWAWA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii ili niulize swali moja la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri lakini naomba niseme kwa kuwa nature ya Wabunge kazi zetu huwa zingine tunazifanya kwa kufuatilia wenyewe tunavyoona zinafaa lakini Mbunge anapomaliza kazi yake huwa haweki kumbukumbu ana kazi gani, amefuatilia wapi na imeishia wapi. Sasa je, Serikali haioni kwamba ni vema kuweka utaratibu wa Mbunge kuacha kumbukumbu katika ofisi yake anapomaliza Ubunge wake kazi alizozifanya na alizoachia kuzifuatilia? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwa mfumo wetu kwa sasa hakuna utaratibu wa makabidhiano lakini hii haina maana kwamba pale inapowezekana inakatazwa na sheria. Kwa hiyo, pale ambapo inawezekana makabidhiano yanaweza kufanyika. Hata hivyo, bado tunasisitiza kwamba nyaraka zote muhimu za maendeleo ya Jimbo zitapatikana kwenye Ofisi ya Mkurugenzi wa Halmashauri husika. Yale masuala ya binafsi ya Mbunge kama ahadi ambazo zinatekelezwa au nyaraka zake huhifadhiwa na msaidizi wa Mbunge husika, basi utaratibu wa kawaida wa mawasiliano kati ya mtu na mtu yanaweza kutumika kupata nyaraka au kumbukumbu zinazohitajika. MHE. DR. WILBROD P. SLAA: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwa kuwa katika utekelezaji wa kazi zao Wabunge wanapofanya kazi na Halmashauri wanakuwa wajumbe lakini wala hakuna utaratibu wa kuwataka wakabidhi nyaraka au mchakato wa kazi zao kwa Mkurugenzi na kwa kuwa uchaguzi unapomalizika Ofisi za Wabunge zipo tofauti na Ofisi za Wakurugenzi ni kwa nini Serikali isiandae utaratibu kamili wa kisheria kwamba yaliyoko katika ofisi ya Mbunge 3 ambayo ni tofauti na Ofisi ya Mkurugenzi yakabidhiwe kwa utaratibu maalum unaokuwa endelevu kwa Mbunge anayefuata? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, lakini nashangaa mmeburuzana kwenye uchaguzi unamkabidhi nini!! (Kicheko) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Naibu Spika, sote tunafahamu hali halisi inavyokuwa mara baada ya uchaguzi na wewe ni shahidi. Sasa utaratibu uliopo sasa pale ambapo kuna ofisi nyaraka kama vile Hansard za Bunge kama Wabunge wanaweza kuzihamisha kutoka Dodoma kwenda Wilayani huwa zinakuwa kwenye Ofisi za Mbunge, lakini zile ahadi ambazo ni za Mbunge binafsi bado ni majukumu ya Mbunge na msaidizi wake kuyatekeleza. Lakini ifahamike pia, la msingi ni kwamba, yale masuala muhimu ya maendeleo ya Jimbo, masuala ya msingi huwa nyaraka zake zinahifadhiwa kwenye Halmashauri husika. Na. 143 Sheria Zinazotawala Uanzishaji CDA MHE. EPHRAIM N. MADEJE aliuliza:- Kwa kuwa CDA ilianzishwa mwaka 1973 kwa Sheria Ndogo (G.N. No. 230 of 1973) kwa lengo la kuharakisha ujenzi wa uhamiaji wa Makao Makuu Dodoma na kwa kuwa Manispaa ya Dodoma imeundwa Kikatiba na Sheria Mama za Serikali za Mitaa zinazoipa mamlaka mbalimbali pamoja na yale yanayohusu usimamiaji wa ardhi na maendeleo yake:- (a)Je, kati ya Sheria Mama na Sheria Ndogo ni ipi yenye uzito na kauli ya mwisho Kikatiba na Kisheria? (b)Je, Serikali haioni kwamba kwa kuinyang’anya Halmashauri haki ya kusimamia ardhi yake kwa kutumia Sheria Ndogo ni kuwanyima wananchi uhuru wa kusimamia mambo yao? (c)Je, ni lini Serikali itatekeleza ahadi yake ya Ibara ya 125 ya Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 kwamba itatunga sheria ya Uhamishaji Makao Makuu ya Serikali kuja Dodoma ili kuondoa mkanganyiko wa madaraka uliopo kati ya CDA na Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma? 4 WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ephraim Nehemia Madeje, Mbunge wa Dodoma Mjini ambaye pia ni Mjumbe wa Bodi ya Wakurugenzi ya CDA lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a)Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuzingatia uzito wa sheria tunaweza kuzipanga sheria zetu za Jamhuri ya Muungano wa Tanzania katika sehemu nne muhimu:- (i)Katiba ambayo ndiyo Sheria Mama. (ii)Sheria za kawaida zinazojadiliwa na kupitishwa na Bunge lako Tukufu. (iii)Sheria ndogo ndogo (By laws or Regulations, Orders na kadhalika ambazo sio lazima kupitishwa na Bunge. (iv)Tangazo la Serikali (Government Notice) ambalo hutolewa na Rais au Waziri kwa mamlaka aliyopewa na sheria fulani. (b)Kiutendaji mamlaka ya Ustawishaji Makao Makuu pamoja na Halmashauri ya Manispaa ya Dodoma katika nafasi zao tofauti huwa ni vyombo vilivyowekwa maalum ili kuwasilisha maslahi tofauti. CDA ni chombo kilichowekwa maalum kuwakilisha Serikali katika kutekeleza Program ya Ustawishaji Makao Makuu wakati Halmashauri ya Manispaa ni chombo cha utawala cha Dodoma Mjini. Serikali haijainyang’anya utawala wa Dodoma bali ni vile tu tunatumia sheria ndogo za CDA. Sheria ndogo hizo ni halali na kwa mujibu wa sheria hizo ndogo hasa ile ya mwaka 1987 ardhi yote ya Dodoma ilitolewa kwa CDA kwa hati miliki ya muda mrefu ya miaka 99 ambayo Namba yake ni 4585 iliyo katika Land Registry ya Dodoma. Hata hivyo, kazi ya kusimamia ardhi inayofanywa na CDA huwa kwa kawaida inaishirikisha Manispaa kama ambavyo mifano mingi inaonyesha, mifano michache ni kama ifuatavyo:- (i) Special Planning Committee inashirikisha wajumbe wanne kutoka Manispaa. (ii) Kamati ya Udhibiti wa Uendelezaji na kutoa vibali vya ujenzi. (Building Control Committee) ina wajumbe watatu kutoka Manispaa. (iii) Kamati ya Ugawaji Viwanja /Ardhi (Plot Allocation Committee) ina wajumbe watano kutoka Manispaa akiwemo Mstahiki Meya na Madiwani wawili. (iv) Kamati ya Kutoa Majina ya Mitaa (Street Naming Committee) ya maeneo ya Dodoma yenye Sekretarieti yake Manispaa ina wajumbe wanne kutoka CDA. 5 (v) Mkurugenzi Mkuu wa CDA ni mjumbe mwalikwa wa Full Council ya Halmashauri ya
Recommended publications
  • Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI NA SABA YATOKANAYO NA KIKAO CHA NNE (DAILY SUMMARY RECORD OF PROCEEDINGS) 7 NOVEMBA, 2014 MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI NA SABA KIKAO CHA NNE – 7 NOVEMBA, 2014 Kikao kilianza saa 3:00 Asubuhi kikiongozwa na Mhe. Job Y. Ndigai, Mb Naibu Spika ambaye alisoma Dua. MAKATIBU MEZANI 1. Ndg. Charles Mloka 2. Ndg. Lina Kitosi 3. Ndg. Hellen Mbeba I. MASWALI YA KAWAIDA Maswali yafuatayo yaliulizwa na wabunge na kupitia majibu Bungeni:- 1. Ofisi ya Waziri Mkuu – swali na. 38 la Mhe. Anne Kilango 2. Ofisi ya Waziri Mkuu – swali na. 39 la Mhe. Salum Khalfan Barwary 3. Ofisi ya Waziri Mkuu – swali na. 40 la Mhe. Moses Joseph Machali 4. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – swali na. 41. La Mhe. Omar Rashid Nundu 5. Wizara ya Maendeleo ya Mifungo na Uvuvi – swali na. 42. La Mhe. Hilda Ngoye 6. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi – swali na. 43. La Mhe. Zitto Kabwe Zuberi 7. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Tecknolojia – swali na. 44 –la Mhe. Murtaza Mangungu 8. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia - swali na. 45-la Mhe. Godfrey Mgimwa 9. Wizara ya Katiba na Sheria - swali na. 46 – la Mhe. Neema Mgaya Hamid 2 10. Wizara ya Katiba na Sheria- swali na. 47 – la Mhe. Assumpter Mshana 11. Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo – swali na. 48 la Mhe. Khatib Said Hji. 12. Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo - swali na. 49 la Mhe.
    [Show full text]
  • 1458125471-Hs-6-8-20
    [Show full text]
  • Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA PILI Kikao cha Nane – Tarehe 4 Februari, 2016 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae. Tunaendelea na Kikao chetu cha Nane katika Mkutano huu wa Pili wa Bunge la Kumi na Moja. Orodha ya Shughuli zetu za leo mnayo. Katibu! HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha (Mapitio ya Nusu Mwaka 2015/2016 [Monetary Policy Statement (The Mid-Year Review 2015/2016)] 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) MASWALI NA MAJIBU Na. 92 Watumishi Wasio na Sifa Katika Vituo vya Afya na Zahanati Nchini MHE. RIZIKI S. MNGWALI aliuliza:- Kumekuwa na tatizo sugu nchini kwa baadhi ya vituo vya afya na zahanati kuwa na watumishi wasio na sifa za utabibu:- Je, Serikali inatumia vigezo gani kuwapeleka watumishi wasio na sifa katika zahanati na vituo vya afya? MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Naibu Waziri (TAMISEMI). Subiri kidogo Mheshimiwa Waziri. Waheshimiwa Wabunge, jana tulipewa taarifa kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu leo hatakuwepo Bungeni kwa sababu yupo nje ya Dodoma. Kwa mujibu wa Kanuni zetu yeye ni Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni na Serikali imo humu. Mheshimiwa Waziri Mkuu anapokuwa hayupo Dodoma, anaweza kuwa ofisini lakini yupo, anapokuwa nje ya Dodoma, Kanuni zinataka awepo Kaimu Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni. Kwa leo Mheshimiwa William Lukuvi ndiye Kaimu Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni. Tunaendelea, Naibu Waziri TAMISEMI, Mheshimiwa Jafo. (Makofi) NAIBU WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAMISEMI, UTUMISHI NA UTAWALA BORA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (TAMISEMI), napenda kujibu swali la Mheshimiwa Riziki Shahari Mngwali, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, utaratibu ambao unatumika kuajiri watumishi wa kada za afya ni kuwapanga moja kwa moja kwenye vituo vya kazi kadiri wanavyohitimu na ufaulu wa masomo yao.
    [Show full text]
  • Process in Tanzania the Political, Civil and Economic Society
    Tanzania has been independent in 2011 for 50 years. While most neighbouring states have Jonas gone through violent conflicts, Tanzania has managed to implement extensive reforms with- out armed political conflicts. Hence, Tanzania is an interesting case for Peace and Develop- ment research. E Challenges for the This dissertation analyses the political development in Tanzania since the introduction of wald the multiparty system in 1992, with a focus on the challenges for the democratisation process democratisation in connection with the 2000 and 2005 elections. The question of to what extent Tanzania has moved towards a consolidation of democracy, is analysed through an analysis of nine different institutions of importance for democratisation, grouped in four spheres, the state, Challenges for the process in Tanzania the political, civil and economic society. Focus is on the development of the political society, and the role of the opposition in particular. The analysis is based on secondary and primary Moving towards consolidation 50 years material collected in the period September 2000 to April 2010. after indepencence? The main conclusion is that even if the institutions of liberal democracy have gradually developed, in practice single-party rule has continued, manifested in the 2005 election when the CCM won 92% of the seats in the parliament. Despite an impressive economic growth, poverty remains deep and has not been substantially reduced. On a theoretical level this brings the old debate between liberal and substantive democracy back to the fore. Neither the economic nor the political reforms have apparently brought about a transformation of the political and economic system resulting in the poor majority gaining substantially more political influence and improved economic conditions.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Mbili
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Kumi na Tano – Tarehe 1 Julai, 2008 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 132 Kuimarisha Ulinzi na Usalama Jiji Dar es Salaam MHE. CHARLES N. KEENJA : Kwa kuwa, Serikali ya Awamu ya Nne imechukua hatua madhubuti za kuimarisha Ulinzi na Usalama kwenye Jiji la Dar es Salaam kwa kuligawa Jiji kwenye Mikoa na Wilaya za Ki-ulinzi ; na kwa kuwa, hatua hiyo haikwenda sanjari na ile ya kuigawa Mikoa ya Kiutawala:- (a) Je, ni lini Serikali itachukua hatua za kuligawa eneo la Jiji la Dar es Salaam kwenye Mkoa/Wilaya zinazokwenda sanjari na zile za Ulinzi na Usalama ? (b) Je, Serikali haioni kwamba Viongozi kwenye eneo lenye hadhi zinazotofautiana kunaleta matatizo ya ushirikiano na mawasiliano hatimaye kukwamisha utendaji kazi ? (c) Kwa kuwa, zaidi ya 10% ya wananchi wa Tanzania wanaishi Dar es Salaam. Je, Serikali haioni kwamba sasa ni wakati muafaka wa kuweka utaratibu mzuri zaidi wa Uongozi kwenye Jiji hilo ? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- 1 Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Charles Keenja, Mbunge wa Ubungo, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, ni kweli kuwa katika hatua za kuimarisha Ulinzi na Usalama kwenye Jiji la Dar es Salaam Serikali iliamua kuligawa eneo katika ngazi ya Mikoa ambapo Wilaya zote tatu za Kinondoni, Temeke na Ilala ni Mikoa ya Kiulinzi na ngazi ya Mkoa kupewa hadhi ya Kanda Maalum ya Ulinzi na Usalama.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA KUMI NA NNE Kikao cha Kwanza – Tarehe 27 Januari, 2009 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) WIMBO WA TAIFA Hapa Wabunge Waliimba Wimbo wa Taifa D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua TAARIFA YA SPIKA Waheshimiwa Wabunge katika mkutano wa Kumi na Tatu wa Bunge tulipitisha Miswada saba ya Sheria ya Serikali ifuatayo: The Contractors Registration Amendment Bill , 2008, The Unity Titles Bill 2008, The Mortgage Finance Special Provisions Bill 2008, The Height Skins Bill, 2008, The Animal Welfare Bill 2008, The workers Compensation Bill 2008 na The Mental Health Bill 2008. Baada ya kupitishwa na Bunge Miswada hiyo iliwasilishwa kwa Mheshimiwa Rais ili kama inavyohitaji Katiba yetu ipate kibali chake. Kwa taarifa hii nawaarifu Waheshimiwa Wabunge kwamba tayari Mheshimiwa Rais amekwishatoa kibali chake na sasa Miswada hiyo ni sheria za nchi na sasa inaitwa The Contractors Registration Amendment Act, 2008 Na. 15 ya mwaka 2008, The Unit Titles Act, 2008 Na. 16 ya 2008, The Mortgage Finance Special Provisions Act, 2008 Na. 17 ya mwaka 2008 The Height Skins and Leather Trade Act, 2008. Kwa hiyo, ni sheria Na. 18 ya Mwaka 2008. The Animal Welfare Act 2008 Sheria Na. 19 ya mwaka 2008 na The Mental Health Act 2008 Sheria Na. 21 ya mwaka 2008 huu ndiyo mwisho wa taarifa. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA):- Taarifa ya Matoleo yote ya Gazeti la Serikali pamoja na nyongeza zake zilizochapishwa tangu Kikao cha mwisho cha Mkutano wa Bunge uliopita.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao Cha Arobaini Na Moja – Tareh
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Arobaini na Moja – Tarehe 9 Juni, 2020 (Bunge lilianza Saa Nane Kamili Mchana) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Naomba tukae. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI - KATIBU WA BUNGE: AZIMIO LA BUNGE Azimio la Bunge la kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Pombe Magufuli, kwa namna alivyoongoza Taifa katika mapambano dhidi ya Janga la Ugonjwa wa Corona (Covid – 19). MASWALI NA MAJIBU (Maswali yafuatayo yameulizwa na kujibiwa kwa njia ya mtandao) Na. 386 Upungufu wa Vituo wa Afya Tabora MHE. EMANUEL A. MWAKASAKA aliuliza:- Jimbo la Tabora mjini lina Kata 29 lakini - lina kituo cha kimoja tu cha afya. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, Serikali ina mkakati gani wa kuongeza Vituo vya Afya katika Manispaa ya Tabora? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Emmanuel Adamson Mwakasaka, Mbunge wa Tabora Mjini, kama ifuatavyo; Mheshimiwa Spika, halmashauri ina jumla ya vituo vya kutolea huduma za afya vya Serikali, vikijumuisha Hospitali mbili, Kituo cha Afya kimoja na Zahanati 22. Katika mwaka wa fedha 2020/21 Serikali imetenga shilingi milioni 100 kwa ajili ya kukamilisha maboma ya Zahanati ya Ituru na Igombe. Vilevile Serikali imetenga shilingi bilioni 1 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa Hospitali ya Manispaa ya Tabora. Serikali itaendelea kujenga, kuratabati na kupanua vituo vya kutolea huduma za afya Manispaa ya Tabora kwa kadri ya upatikanaji wa fedha. Na.
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA NANE Kikao Cha Kumi Na Tano
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Kumi na Tano – Tarehe 3 Julai, 2007 (Kikao Kilianza Saa 3.00 Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI:- Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, mkiangalia Order Paper yetu ya leo, hati za kuwasilisha Mezani iko, Ofisi ya Makamu wa Rais, yuko Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili na Mazingira, tumemruka Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria na Utawala, halafu atakuja Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MAZINGIRA): Hotuba ya Bajeti ya Wizari wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha wa 2007/2008. MWENYEKITI WA KAMATI YA MALIASILI NA MAZINGIRA: Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mazingira kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha uliopita pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2007/2008. MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA (MHE. RAMADHAN A. MANENO): Tarifa ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano kwa mwaka wa Fedha 2006/2007 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2007/2008. MHE. RIZIKI OMARI JUMA (k.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI): 1 Maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha uliopita pamoja Maoni ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2007/2008.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA KUMI NA MBILI ___Kikao Cha Sita
    Hii ni nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI __________ Kikao cha Sita - Tarehe 18 Juni, 2003 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Juma J. Akukweti) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 50 Upungufu wa Watumishi - Hospitali ya Wilaya ya Mbulu MHE. PHILIP S. MARMO aliuliza:- Kwa kuwa siku zilizopita Wizara imekiri upungufu mkubwa wa watumishi katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu katika fani zote kama Madaktari, Wauguzi, Wataalam wa X-ray na Famasia na mfano mmoja ukiwa ni kwamba mashine mpya za chumba cha X- ray hazitumiki kwa sababu ya ukosefu wa wataalam. Je, ni lini Serikali itawaajiri wataalam niliowataja ili kutatua tatizo hilo sugu? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Philip Marmo, Mbunge wa Mbulu, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba tarehe 18 Julai, 2002 wakati nikijibu swali Na. 873 la Mheshimiwa Mbunge, nilikiri upungufu wa wataalam wa afya katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu. Naomba kumpongeza kwanza Mheshimiwa Philip Marmo, Mbunge wa Mbulu, kwa juhudi zake kubwa sana anazozichukua katika kutatua matatizo yaliyoko katika Hospitali ya Wilaya ya Mbulu ikiwa ni pamoja na upungufu wa watumishi. Halmashauri 1 za Wilaya nyingi hapa nchini bado zina upungufu wa wataalam katika fani mbalimbali. Ofisi ya Rais, pamoja na Idara Kuu ya Utumishi inajitahidi sana kutoa vibali vya ajira, lakini waombaji wa kazi hizo mara nyingi wamekuwa ni wachache. Mheshimiwa Naibu Spika, Hospitali ya Wilaya ya Mbulu ni moja ya Hospitali za Wilaya ambazo zina upungufu wa Madaktari, Wauguzi na wataalam wengine.
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 105 May - Aug 2013
    Tanzanian Affairs Text 1 Issued by the Britain-Tanzania Society No 105 May - Aug 2013 Even More Gas Discovered Exam Results Bombshell Rising Religious Tensions The Maasai & the Foreign Hunters Volunteering Changed my Life EVEN MORE GAS DISCOVERED Roger Nellist, the latest volunteer to join our panel of contributors reports as follows on an announcement by Statoil of their third big gas discovery offshore Tanzania: On 18 March 2013 Statoil and its co-venturer ExxonMobil gave details of their third high-impact gas discovery in licence Block 2 in a year. The new discovery (known as Tangawizi-1) is located 10 kilometres from their first two discoveries (Lavani and Zafarani) made in 2012, and is located in water depth of 2,300 metres. The consortium will drill further wells later this year. The Tangawizi-1 discovery brings the estimated total volume of natural gas in-place in Block 2 to between 15 and 17 trillion cubic feet (Tcf). Depending on reservoir characteristics and field development plans, this could result in recoverable gas volumes in the range of 10-13 Tcf from just this one Block. These are large reserves by international stand- ards. By comparison, Tanzania’s first gas field at Songo Songo island has volumes of about 1 Tcf. Statoil has been in Tanzania since 2007 and has an office in Dar es Salaam. It operates the licence on Block 2 on behalf of the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) and has a 65% working interest, with ExxonMobil Exploration and Production Tanzania Limited holding the remaining 35%. It is understood that under the Production Sharing Agreement that governs the operations, TPDC has the right to a 10% working participation interest in case of a development phase.
    [Show full text]
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? With Partial Support from a TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? ACKNOWLEDGEMENTS This review was compiled and edited by Tanzania Development Research Group (TADREG) under the supervision of the Steering Group of Policy Forum members, and has been financially supported in part by Water Aid in Tanzania and Policy Forum core funders. The cartoons were drawn by Adam Lutta Published 2013 For more information and to order copies of the review please contact: Policy Forum P.O Box 38486 Dar es Salaam Tel: +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] ISBN: 978-9987 -708-09-3 © Policy Forum The conclusions drawn and views expressed on the basis of the data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. Every effort has been made to verify the accuracy of the information contained in this review, including allegations. Nevertheless, Policy Forum cannot guarantee the accuracy and completeness of the contents. Whereas any part of this review may be reproduced providing it is properly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. Designed by: Jamana Printers b TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TABLE OF CONTENTS POLICY FORUM’s OBJECTIVES .............................................................................................................
    [Show full text]
  • 1458125147-Hs-6-4-20
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA SITA Kikao cha Nne – Tarehe 3 Februari, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO: Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Tume ya Ushindani kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010 [The Annual Report and Audited Accounts of Fair Competition Commission for the Financial year 2009/2010]. NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge juu ya Uendeshaji wa Sekta Ndogo ya Gesi Nchini. MASWALI NA MAJIBU Na. 39 Uwekezaji wa Kibiashara wa Nchi ya Libya Tanzania MHE. JOSEPH O. MBILINYI aliuliza:- Aliyekuwa Kiongozi wa Libya Marehemu Kanali Muamar Gaddafi, alijulikana sana kwa kuwekeza mabilioni ya dolla kwenye nchi mbalimbali za Kiafrika, kibiashara na kijamii kama hoteli, barabara na misikiti: (a) Je, Tanzania ilifaidikaje na uwekezaji wa Gaddafi kibiashara hapa nchini? (b) Kwa kuwa, Serikali ya Tanzania haitambui Serikali ya mpito ya Libya. Je, ni nani anayesimamia uwekezaji wa biashara wa Marehemu Kanali Gaddafi hapa nchini? NAIBU SPIKA: Ahsante sana, mabadiliko hayo hayabadilishi maudhui ya swali. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Osmund Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo katika Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Marehemu Kanali Muammar Gaddafi hakuwahi binafsi kuwekeza kibiashara hapa nchini.
    [Show full text]