Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI (Kikao cha Thelathini na Sita - Tarehe 31 Julai, 2003) (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Pius Msekwa) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. ABDISALAAM ISSA KHATIBU): Taarifa ya Mkuu wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha kuhusu shughuli zao Chuo kwa Mwaka 2001/2002 (Report on the Activities of the Institute of Finance Management for the Year 2001/2002). NAIBU WAZIRI WA USHIRIKA NA MASOKO: Hotuba ya Wizara ya Ushirika na Masoko kwa Mwaka 2003/2004. MHE. MOHAMED A. ABDULAZIZ (k.n.y. MHE. WILLIAM A. SHELLUKINDO - MWENYEKITI WA KAMATI YA UWEKEZAJI NA BIASHARA): Taarifa ya Kamati ya Uwekezaji na Biashara kuhusu utekelezaji wa Wizara ya Ushirika na Masoko katika mwaka uliopita, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka 2003/2004. MASWALI NA MAJIBU Na. 349 Usafiri kwa Madiwani MHE ISMAIL J. R. IWVATTA (k.n.y. MHE. MOHAMED H. MISSANGA) aliuliza:- Kwa kuwa tatizo la usafiri kwa Waheshimiwa Madiwani ni la kweli na ni la msingi; na kwa kuwa imeshindikana kuwakopesha Waheshimiwa Madiwani pikipiki kutokana na uhaba wa fedha Serikalini; je, Serikali haioni kuwa ni muhimu kuwatatulia Madiwani tatizo la usafiri kwa kuwakopesha baiskeli ambazo bei yake ni kiasi cha Sh. 70,000/= na kisha kuwakata walau Sh. 3,000/= kwa mwezi kwa kipindi cha miaka miwili kutoka katika posho yao wanayolipwa kila mwezi isiyopungua Sh. 30,000/=? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed H. Missanga, Mbunge wa Singida Kusini, kama ifuatavyo: - 1 Mheshimiwa Spika, kwanza, naomba kuliarifu Bunge lako Tukufu kwamba, hii ni mara ya nne mfululizo kwa Bunge lako kuulizia suala la mikopo kwa Waheshimiwa Madiwani na masuala mengine yanayohusiana na mafao yao. Hii inadhihirisha jinsi Waheshimiwa Wabunge, wanavyoguswa na tatizo hili. Naomba kulihakikishia Bunge lako Tufuku kuwa, Serikali pia inaguswa na inatambua sasa juu ya kuwepo kwa tatizo hili la Waheshimiwa Madiwani. Mheshimiwa Spika, mpaka sasa Serikali haijaweka utaratibu wa kuwawezesha madiwani kupata mikopo, iwe ya baiskeli, magari, pikipiki na kadhalika kutatua shida ya usafiri. Kwa mujibu wa taraibu zilivyo sasa, Diwani anaweza tu kukopo chombo chochote cha usafiri ikiwemo baiskeli kwa maelewano binafsi na mkopeshaji. Lakini Halmashauri haikatazwi hata kidogo kutoa dhamana kwa maana ya kumhakikishia mkopeshaji kwamba, makato ya posho ya Diwani yatakatwa na Halmashauri na kuwasilishwa kwake na siyo kwa kutumia moja kwa moja fedha za Halmashauri. Mheshimiwa Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba, Madiwani ni Wasimamizi Wakuu wa mapato ya Halmashauri na maendeleo yake, lakini vile vile hawana budi kuzingatia sheria zilizotungwa na Bunge lako Tukufu. Mheshimiwa Spika, kwa kupitia Bunge lako Tukufu, naendelea kuwaagiza tena Wakurugenzi wa Halmashauri, kufuata sheria na miongozo mbalimbali na kuelekeza mapato ya Halmashauri katika kuimarisha huduma za jamii na kutekeleza miradi ya maendeleo ili iwe chachu ya kuendeleza Halmashauri zetu. (Makofi) MHE. DR. MILTON M. MAHANGA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ningependa niulize swali kama ifuatavyo:- Kwa kuwa hawa Madiwani kuna wengine wana uwezo wa kujinunulia vyombo hivi vya usafiri, sasa Serikali itakubali angalau kuwasamehe kodi za VAT kama inavyofanya kwa walimu na watumishi wengine wa Serikali? (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, ushauri alioutoa Mheshimiwa Mbunge, ni mzuri na tayari katika ofisi yetu tulikwishaanza kulifanyia kazi, kwa maana ya kuona kama hilo Serikali inaweza ikalikubali. (Makofi) Lakini la pili ambalo Mheshimiwa Waziri, analifanyia kazi vile vile ni kujaribu kuona uwezekano wa kuona kama posho zilivyo sasa zinaweza zikapandishwa angalau kidogo. (Makofi) Na. 350 Usafiri kwa Makatibu Tarafa MHE. IRENEUS N. NGWATURA (k.n.y. MHE. PROF. SIMON M. MBILINYI) aliuliza:- Kwa kuwa Serikali imewapa Makatibu Tarafa usafiri wa pikipiki; na kwa kuwa Makatibu Tarafa wa Jimbo la Peramiho wameeleza kuwa hawapati mafuta ya kuendeshea pikipiki hizo; je, Serikali ina mpango wa kuwapa mafuta/petrol? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Prof. Simon Mbilinyi, Mbunge wa Peramiho, kama ifuatavyo:- 2 Mheshimiwa Spika, kama nilivyokwisha wahi kueleza hapa Bungeni, naomba kurudia tena kuwa, pikipiki zilizotolewa kwa Makatibu Tarafa bado ni mali ya Serikali. Hivyo, bado Serikali kwa kupitia Makatibu Tawala wa Mikoa itaendelea kuzipatia mafuta. Mheshimiwa Spika, kwa kipindi cha mwaka 2003/2004, Serikali imeziagiza Ofisi ya Wakuu wa Mikoa nchini kutenga katika Bajeti zao kiasi cha fedha kwa ajili ya kuhudumia pikipiki za Makatibu Tarafa. Mkoa wa Ruvuma ni mmojawapo wa Mikoa iliyofanya hivyo na jumla ya Sh. 4,842,400/= zimetengwa kwa madhumni hayo. Mheshimiwa Spika, Serikali inakamilisha taratibu za kuwakopesha Makatibu Tarafa pikipiki hizo na mara tu pikipiki hizo zitakapokopeshwa kwa Makatibu Tarafa, Serikali itatoa maelezo mengine kuhusu namna tutakavyopata huduma nyingine. (Makofi) MHE. IRENEUS N. NGWATURA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri. Kwa kuwa Tarafa nyingi zinatofautiana kwa ukubwa wa maeneo; je, Mheshimiwa Naibu Waziri atakubaliana na mimi kwamba kuna haja ya kuhakikisha kwamba mafuta au gharama za kutengeneza pikipiki hizo ziwe zinatolewa kulingana na ukubwa wa Tarafa hizo? (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza nimesema wazi kabisa kwamba, ndiyo maana tuliagiza Mikoa itenge katika Bajeti zao viwango ambavyo wanaona vifaa kwa ajili ya kutoa mafuta na vile vile kuhudumia pikipiki hizo. Naamini watakuwa wamezingatia ukubwa wa Tarafa pengine na matatizo mengine yaliyomo katika Tarafa husika. (Makofi) MHE ISMAIL J. R. IWVATTA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana kwa kuniona na kunipatia nafasi niulize swali la nyongeza. Kwa kuwa swali la msingi linasema Makatibu Tarafa hawapati hela za mafuta; na kwa kuwa tatizo kama hilo walikuwa wanalipata Wakuu wa Wilaya na Serikali hii hii badala ya kupitisha fedha hizo kupitia Ofisi ya Katibu Tawala wa Mkoa imeamua kuzipeleka moja kwa moja; je, utaratibu kama huo hauwezi ukafanywa kwa Makatibu Tarafa ili wawe wanazipata moja kwa moja kupitia mishahara yao? (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, nia ya Serikali muda wote ni kutafuta njia nyepesi na rahisi kuwezesha shughuli kuweza kuendeshwa vizuri. Kwa hiyo, uamuzi wa kupeleka fedha moja kwa moja kwa Ma-DC ulitokana na msingi huo. RAC anatajwa kwa kuwa ndiyo Accounting Officer na ndiye anayetakiwa kupanga mipango ya Bajeti. Lakini hilo ninalosema kama halijazingatiwa, basi tutalifanyia kazi. (Makofi) Na. 351 Vituo vya Watoto Yatima na Wasiojiweza MHE. GWASSA A. SEBABILI aliuliza:- Kwa kuwa tangu kabla ya Uhuru kulikuwa na vituo vya kulelea watoto nchini japokuwa vilikuwa vichache ambavyo viliongezeka baada ya Uhuru; na kwa kuwa wakati wote huo mpaka miaka ya 1990 vituo vya yatima vilikuwa vikipata ruzuku toka Wizara ya Afya pamoja na zilizokuwa Hospitali za Mashirika ya Dini, misaada ambayo ilisitishwa kwa vituo hivyo; na kwa kuwa tangu miaka ya 1980 lilipojitokeza janga la Ukimwi vituo vya yatima vimeongezeka mno na watoto yatima wanazidi kuongezeka kila wakati kiasi kwamba hali hiyo huko vijijini sasa ni balaa:- (a) Je, Serikali ina mpango gani mahsusi wa kukabiliana na tatizo hilo zito linaloongezeka kwa kasi nchini na fedha kiasi gani zilizotengwa kwa vituo hivyo nchini kila mwaka tangu 1998 na ni vituo vingapi vilivyopata fedha kuviendesha na kiasi gani kwa kituo tangu mwaka 1998? 3 (b) Je, Vituo vya Shirika la Mtakatifu Bernadeta na Masista wa Thereza wa Calcuta katika Jimbo la Katoliki Rulenge Wilayani Ngara vinavyopokea watoto tangu wa siku moja, vinawatunza vilema wasio na jamaa, wakongwe wasiojiweza, shule ya awali, wanasomesha yatima shule ya Msingi Rulenge na wengine katika sekondari, vilisaidiwaje katika kipindi hicho? (c) Je, kwa jumla vituo vingapi vya aina hiyo nchini kwa mgawanyo vinavyoendeshwa na Serikali, Mashirika yasiyo ya Serikali na watu binafsi? WAZIRI WA KAZI, MAENDELEO YA VIJANA NA MICHEZO alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Gwassa Angus Sebabili, Mbunge wa Ngara, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, Serikali chini ya Wizara yangu ilikuwa na utaratibu wa kutoa ruzuku kwa wakala za hiari, Mashirika ya Dini na watu binafsi ambao hupokea na kutunza watoto yatima na wenye shida kwenye makao. Mpango huu ulisimama mwaka 1994 kutokana na ufinyu wa Bajeti ya Serikali. Mwaka wa fedha 2000/2001, Wizara yangu ilianza tena kutoa ruzuku kwa makao hayo kama ifuatavyo: Mwaka 2000/2001 tulitoa Sh. 1,500,000/= kwa vituo 15, mwaka 2001/2002 tulitoa Sh. 1,000,000/= kwa vituo 10. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2002/2003, tumetoa ruzuku kwa vituo mbalimbali kama ifuatavyo: Oktoba hadi Desemba Sh. 7,00,000/= kwa vituo 5, Januari hadi Machi Sh. 1,925,000/= kwa vituo 15, Aprili hadi Juni Sh. 2,000,000/= kwa vituo 20. Kwa hiyo, kuanzia mwaka 2000/2001 hadi mwaka 2002/2003, Wizara yangu imetoa kiasi