Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document)

BUNGE LA ______

MAJADILIANO YA BUNGE ______

MKUTANO WA NANE

Kikao cha Kumi na Nane – Tarehe 6 Julai, 2012

(Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi)

D U A

Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua

HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI

Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani:-

WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA UTARATIBU):

Mheshimiwa Spika, Kabla sijawasilisha Hati Mezani ninapenda kutumia dakika yako moja kutoa shukrani za dhati kabisa kwako. Kwanza kwa kuwa wa kwanza kutangaza msiba wa Mama yangu na vilevile kuwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wote ambao wameniletea rambirambi kwa namna moja au nyingine kwa njia ya sms na kwa simu na hii imefanyika kwa wananchi wengi nchini kote.

1 Mheshimiwa Spika, ninawashukuru sana wote sina kitu cha kufanya isipokuwa kuwaambia kuwa asanteni sana, nimepata faraja na Mama yetu tumemwweka mahali pema katika nyumba yake ya milele. Kwa hiyo, baada ya maelezo hayo mafupi na kwa kuwapongeza na kuwashukuru wote naomba sasa kuwakilisha Hati Mezani.

Taaarifa ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, 2011/2012 - 2015/2016.

NAIBU WAZIRI WA MAJI:

Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha, 2012/2013.

MASWALI NA MAJIBU

Na.143

Serikali Kujenga Nyumba za Walimu

MHE. SULEIMAN M. N. SULEIMAN (K.n.y. MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA) aliuliza:-

Shule nyingi za msingi zina upungufu mkubwa wa nyumba za walimu hivyo kusababisha walimu kuishi katika mazingira magumu na kutoripoti katika shule kama Nyamsebhi, Mnekezi, Shibela, Kageye, Ntono na Nyasalala katika Jimbo la Busanda.

2 Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga nyumba za walimu katika shule hizo na nyingine ili kuboresha mazingira ya walimu kufanya kazi?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa , Mbunge wa Busanda kwa kutoa maelezo yafuatayo.

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Geita ina jumla ya shule za msingi za Serikali 271 na binafsi 6. Aidha, idadi ya walimu waliopo ni 3,531 na nyumba za walimu ni 770 ambazo hata hivyo hazitoshi. Serikali inatambua umuhimu wa kuwa na nyumba za kutosha za walimu ili kuboresha mazingira ya kuishi na kuwawezesha kufanya kazi zao ipasavyo.

Kwa kuzingatia azma hiyo Serikali imekuwa ikitenga fedha na kuhamasisha wadau mbalimbali kuchangia katika ujenzi wa miundombinu ya shule ikiwemo ujenzi wa nyumba za walimu.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2006/2007 hadi 2009/2010 Serikali ilitoa jumla ya shilingi 22,800,000.00 kuchangia jitihada za wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kujenga nyumba za walimu zipatazo 25. Shule zilizonufaika na fedha hizi ni shule ya msingi Nyamisebhi, Shilabhela, Buyagu,Kageye, Mnekezi na shule ya msingi Nyalwanzaja.

3 Mheshimiwa Spika, Serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/2011 ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu katika shule za msingi. Kati ya kiasi hicho shilingi milioni 49 kilitengwa na kutumwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu.

Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua fursa hii kuzihimiza Halmashauri kuweka kipaumbele katika ujenzi wa nyumba za walimu katika mipango yao ya bajeti na kusimamia vizuri matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kazi hiyo ili kuboresha mazingira ya kazi za walimu.

MHE. SULEIMAN M. N. SULEIMAN: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tatizo la nyumba za walimu katika Jimbo la Geita liko sambamba kabisa na tatizo la nyumba za walimu katika Jimbo la Kishapu. Kwa sababu mfano wa nyumba za walimu katika Jimbo la Kishapu ni kama picha niliyokuonyesha. Je, Serikali inaridhika na walimu wa Jimbo Kishapu kuwa na nyumba ambazo zina mazingira magumu na hatimaye wakawa wanakimbia katika Jimbo letu kwa sababu wengi wao hawawezi kuishi katika nyumba za aina hii? (Makofi)

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mheshimiwa Nchambi kutoka Kishapu.

4 Serikali bado inao mpango mzuri wa kujenga nyumba za walimu kwenye maeneo yao. Mwaka huu wa fedha 2012/1213 tumetenga jumla ya shilingi bilioni 296 kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote nchini. Miongoni mwa fedha hizi sasa katika Halmashauri zile waweke kipaumbele kwenye maeneo yenye changamoto nyingi ikiwemo nyumba za walimu.

Mheshimiwa Spika, ili kuwawezesha walimu ambao tunawapangia kazi katika maeneo hayo waweze kuishi kwenye nyumba. Hata hivyo kila Halmashauri kupitia bajeti zake za mapato ya ndani mbali ya hizi ambazo ni za Serikali nao tunatoa wito kuweka kipaumbele kwenye maeneo haya yale yote yenye changamoto katika sekta ya elimu kuwezesha sekta hii kufanya kazi yake vizuri.

MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kilio cha nyumba za walimu ni kubwa sana na tumeona kwamba TBA imekuwa ikitengewa fedha chache sana na Serikali kama tulivyoeleza katika bajeti kivuli jana cha Wizara ya Ujenzi. Ni kwanini Serikali isiiongezee TBA fedha za kutosha ili ijenge hizi nyumba za walimu?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, mpango wa ujenzi wa nyumba za walimu pamoja na ule ambao umewekwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu lakini pia suala la TBA liko kwenye Wizara ambayo sasa hivi inawasilisha bajeti yake. Ninaomba sana Waheshimiwa Wabunge tuipitishe bajeti ya

5 Wizara ya Ujenzi ambayo pia ina kitengo cha TBA ili pia pia nayo iweze kuweka mipango endelevu ya ujenzi wa nyumba kwa ajili ya kutoa huduma kwa walimu kwenye maeneo yale ambayo wanaweza kuyafikia.

MHE. FAIDA M. BAKAR: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, walimu wengi wana matatizo ya makazi na kwa kuwa, wengi wanaishi katika nyumba za kupanga. Je, Serikali itakubaliana na mimi kwamba sasa ni wakati muafaka wa kuwaongezea posho za makazi walimu hawa?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU,TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, Ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Faida Bakar. Ni kweli kwamba tumekuwa tukisikia kilio cha walimu wenyewe lakini hata Waheshimiwa Wabunge mmesema sana juu ya kuongeza maslahi ya walimu ili waweze kufanya kazi zao katika mazingira rahisi zaidi.

Lakini ninapenda kusema kwamba mpango wa Serikali wa kuboresha maslahi ya walimu ili waweze kumudu kuishi na kufanya kazi yao vizuri tunao lakini yataweza kubodreka kadri fedha za Serikali zinavyoweza kupatikana ili kuweza kuboresha maslahi ya walimu kama ambavyo tumeweza kusema. (Makofi)

Pia hata wakati tunachangia hoja ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwamba Serikali inayo azma njema ya kuweza kuboresha maslahi. Kwa hiyo, katika mipango hiyo ambayo inaendelea kadiri ya fedha zinavyoweza

6 kupatikana hilo ni eneo mojawapo ambalilo tutataka kuliboresha ili walimu waweze kufanya kazi zao vizuri.

Na. 144

Ukamilishaji wa Ujenzi wa Shule za Sekondari Rombo

MHE. MUSTAPHA B. AKUNAAY (K.n.y. MHE. JOSEPH R. SELASINI) aliuliza:-

Kutokana na uhaba wa ardhi katika Kata ya Keni, Mrao Keryo, katika Jimbo la Rombo, wananchi wameamua kujenga shule za sekondari kwa mtindo wa ghorofa na shule hizo ni pamoja na sekondari za Keni, Bustani na Shimbi.

Je, Serikali itakuwa tayari kuchukua shule hizo na kukamilisha ujenzi wake ili kuunga mkono juhudi za wananchi wa Rombo na kuwapa nafasi kuchangia miradi mingine?

NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Roman Selasini, Mbunge wa Rombo lakini pia kabla sijaanza kujibu swali lake ninatambua kabisa kuwa Mheshimiwa Mbunge mwenzetu alipata ajali mbaya sana iliyoweza kusababisha vifo vya watu wane akiwemo Mama yake Mzazi.

7 Kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu tunampa pole sana na tunajua kuwa yeye bado yupo hospitalini tunamtakia uponaji mwema yeye na Mke wake, na sasa naomba nijibu swali lake nikijua kabisa anayo hamu ya kulisikia hili kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mchango mmojawapo wa wananchi katika kufanikisha ujenzi wa sekondari za Kata ni kuwezesha upatikanaji wa ardhi kupitia Serikali za vijiji. Kutokana na ufinyu wa ardhi wananchi wa Rombo waliamua kujenga shule za Sekondari za Kata kwa mtindo wa ghorofa.

Shule za sekondari za Kata zinazojengwa kwa mtindo wa ghorofa ni shule ya Sekondari Keni, inayojengwa katika Kata ya Keni, shule ya Sekondari Shimbi inayojengwa katika Kata ya Shimbi na shule ya Sekondari Bustani inayojengwa katika Kata ya Mrao Keryo.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2010/2011 Serikali katika kuunga mkono jitihada za wananchi wa Rombo kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ilitoa jumla ya shilingi 625,000,000/= kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya ya elimu katika Kata zote 41 za Serikali. Kwa kuzingatia gharama za ujenzi wa ghorofa shule hizo tatu zilipata mgao ufuatao:-

(i) Shule ya Sekondari Bustani ilipewa 57,645,850/=;

(ii) Shule ya Sekondari Keni ilipewa shilingi 53,995,850/=; na

8 (iii) Shule ya Sekondari Shimbi shilingi 53,995,850/=.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa shule za sekondari za Kata ni ubia kati ya wananchi, Halmashauri na Serikali Kuu. Shule za Sekondari za Kata zinazojengwa ni mali ya Halmashauri husika.

Katika mwaka wa fedha 2012/2013 Serikali imejenga jumla ya shilingi bilioni 296 kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote nchini, Halmashauri ya Wilaya ya Rombo imetengewa jumla ya shilingi bilioni 2.2.

Mheshimiwa Spika, natoa wito kwa Hamashauri kusimamia matumizi ya fedha hizi na kuhakikisha maelekezo sahihi ya kukamilisha miradi ya zamani yanazingatiwa kabla ya kuanza miradi mipya. Ukiwemo ukamilishaji wa ujenzi wa shule za sekondari Keni, Bustani na Shimbi.

MHE. MUSTAPHA B. AKUNAAY: Kwa kuwa tatizo la nyumba za walimu limekuwa ni tatizo kubwa katika Halmashauri zote nchini:-

(a) Je, Serikali ina mpango gani wa kati na wa muda mrefu kuondoa tatizo hili kabisa katika nchi nzima ili tatizo lisiwe linajirudiarudia?

(b) Je, Bilioni 296 Serikali ina hakika kuwa itapatikana au itakuwa ni pesa kidogokidogo ambazo hazitasaidia?

9 WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Mheshimiwa Spika, ningependa kujibu maswali mawili ya Mheshimiwa Akunaay, kama ifuatavyo:-

(a) Mheshimiwa Spika, katika mpango wa maendeleo ya walimu wa Sekondari awamu ya pili ambayo imeanza mwaka 2010 kwa kipindi cha miaka mitano mpaka 2015. Msisitizo tuliouweka ni kuhakikisha kwamba sasa tunakuza ubora wa elimu na mkakati mmojawapo ni kukamilisha miundombinu ile itayowezesha utoaji bora wa elimu ikiwemo ujenzi wa nyumba.

Kwa hiyo, nyumba za walimu ni mpango maalum wa Serikali na kila mwaka kwa miaka mitano hii tutakuwa tunatenga fedha kwa ajili ya kujenga nyumba za walimu mpaka pale ambapo tutakuwa tumefikia hali ambayo kero hii ya nyumba ikiwa imemalizika. Kwa hiyo, siyo jambo la muda tu mwaka huu lakini tutaendelea chini ya SEDEP mbili.

SPIKA: Swali la pili anasema hizo fedha zitakuwa kidogokidogo au ndiyo basi?

WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Mheshimiwa Spika, oh! Hizi fedha hazitakuwa kidogokidogo mwaka huu tumetenga fedha kama alivyozungumza Naibu Waziri shilingi bilioni 296 na kwasababu ziko katika mpango maalum hizi pesa zitakuwa moja kwa moja HAZINA na kwenda kwenye Halmashauri kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu hiyo kwasababu zitakuwa zinatoka kwa awamu ndani ya mwaka na hataweza kupitia mahali pengine isipokuwa

10 zitakwenda moja kwa moja kwa ajili ya miundombinu hiyo. (Makofi)

SPIKA: Hili swali linafanana na lile lililotangualia kwa hiyo tusubiri Wizara itakapokuja tutaendelea. Sasa tunaelekea Wizara ya Maji. (Makofi)

Na. 145

Tatizo la Maji Manispaa ya Tabora

MHE. SAIDI M. MTANDA (K.n.y. MHE. MUNDE A. TAMBWE) aliuliza:-

Manispaa ya Tabora inakabiliwa na tatizo la maji kwa muda mrefu na mtaalam mshauri ili alipofanya upembuzi yakinifu alishauri Serikali itenge kiasi cha shilingi bilioni 45 lakini Serikali imetenga shilingi bilioni 4.2 tu kwa ajili ya kutatua tatizo hilo.

(a) Je, kiasi hicho kidogo kitakidhi haja na ushauri uliotolewa na wataalam?

(b) Je, kwa nini Serikali isitenge kiasi ambacho kilipendekezwa na Mtaalam Mshauri ili kukamilisha na kuo ndokana na kero hiyo ya maji?

NAIBU WAZIRI WIZARA YA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Munde Tambwe Abdallah, Mbunge viti maalum, lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:-

11

Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia programu ya maendeleo ya Sekta ya Maji (WSDP) na ufadhili wa Serikali ya Uswisi kupitia Shirika lake la SECO ilifanya upembuzi yakinifu, usanifu na kuandaa makabrasha ya zabuni kwa ajili ya mradi wa kuboresha huduma ya maji katika mji wa Tabora. Hii ni pamoja na kuongeza uzalishaji wa maji kutoka mita za ujazo 15,000 kwa siku za sasa hadi 30,000 kwa siku na kujenga mtandao wa majitaka. Makadirio ya gharama za kutengeneza mradi huo yalitolewa na mtaalamu Mshauri ni Dola za Kimarekani milioni 26.5 sawa na shilingi za Kitanzania bilioni 45 mwaka 2010.

Mheshimiwa Spika, kutokana na ufinyu wa Bajeti ya Serikali, mradi huo utatekelezwa kwa awamu ambapo awamu ya kwanza ina maeneo makubwa mawili. Eneo la kwanza ni kuboresha mtandao wa maji mjini Tabora ambao unatekelezwa kwa fedha za SECO, Dola za Kimarekani milioni 5.4 au shilingi bilioni 9.2.

Kazi zinazotekelezwa kwa fedha hizo ni ukarabati wa mtandao wa maji kilomita 27 maeneo mjini, ulazaji wa bomba kuu la maji lenye kipenyo cha milimita 500 na urefu wa kilomita 2.7 kutoka Igombe, Ununuzi wa pampu mbili za kusukuma maji pamoja na transfoma mbili, ujenzi wa matanki yenye jumla ya meta za ujazo 5,000, ununuzi wa wa dira za maji 5,000, uboreshaji wa chanzo cha pamoja na kujenga vituo vya post chlorination.

12 Hadi sasa utekelezaji wa kazi hizo umefikia asilimia 30. Aidha, eneo la pili ni ukarabati wa upanuzi wa chujio la maji katika eneo la Bwawa la Igombe unaotekelezwa kwa kutumia fedha za Serikali kupitia WSDP. Kiasi cha shilingi bilioni 4.2 zimetengwa kwa kazi hiyo ambayo kwa sasa iko kwenye hatua za kumpata Mkandarasi na ujenzi utaanza mwezi Septemba 2012. Hivyo, kwa hatua hii jumla ya shilingi bilioni 13.4 zitatumika kukamilisha kazi zote zilizopangwa.

Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutekeleza kazi zingine zilizobaki kwa awamu kulingana na fedha zitakavyopatikana. Kazi hizo ni ulazaji wa bomba kuu kutoka Igombe, ujenzi wa matanki mawili, kupanua mtandao wa mabomba ya kusambaza maji kufikia kilomita 95 na ujenzi wa mtandao wa majitaka. (Makofi)

MHE. SAIDI M. MTANDA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, ninaomba kumwuliza maswali madogo mawili ya nyongeza:-

(a) Kwa kuwa, Serikali inasema hadi kufikia Septemba 2012, itakuwa imetumia kiasi cha shilingi bilioni 13 kwa ajili ya kusambaza maji katika Manispaa ya Tabora. Wakati mkandarasi mshauri anahitaji matumizi ya shilingi bilioni 45 haioni kuwa fedha hizi ni kidogo sana, kwa hiyo Wananchi wa Tabora ikiwa ni mji unaokuwa kwa kasi na ongezeko kubwa la watu watakosa huduma hii muhimu ya maji?

13 (b) Kwa kuwa, maeneo ya Namkongo, Mang’ole ni miongoni mwa maeneo ambayo yana upungufu mkubwa wa maji na visima vya World Bank vimechimbwa kwa muda wa miaka mitano sasa hakuna maji.

Je, Wizara hii imejipangaje kupitia Bajeti hii kuhakikisha tatizo la maji linamalizwa katika vijiji vya Namkongo na Mang’ole katika Jimbo la Mchinga?

SPIKA: Haya, swali la pili sijui, lakini Waziri jibu, umekuwa honesty kiasi kizuri tu. Naibu Waziri Majibu.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ni kweli fedha hazitoshi kama nilivyoeleza kwenye jibu la msingi na kwamba Serikali itaendelea kutenga fedha kulingana na fedha zilizopatikana. Lakini jambo la msingi la kuelewa hapa ni kwamba hata kama fedha zingewepo hizo bilioni 45 tusingeweza zote kuzipeleka Tabora kwa mara moja.

Kwa hiyo fedha zinakwenda kwa awamu za utekelezaji. Mnapokuwa mmemaliza awamu fulani ndipo zinaongezeka fedha zingine na hii inatusaidia kwenye shughuli nzima ya usimamiaji. Hizo bilioni 13.4 ni fedha nyingi, itakapokuwa inakamilika utekelezaji wa ile mipango iliyowekwa Serikali itakuwa imefikia hatua ya kupata fedha zingine za kuendeleza huo mradi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu swali la pili kuhusu visima ambavyo vipo katika Jimbo lake la Mchinga na kwamba tuna mkakati gani wa kutekeleza suala hili zima. Suala la msingi ni kwamba kwanza tulikuwa na

14 mchakato mzima ambao ulikuwa unapitia hatua mbalimbali ambao umechukua muda mrefu. Tumeainisha kwenye jedwali letu ambalo tumesambaza jana Halmashauri ambazo zimeshatekeleza zile awamu zote zinazotakiwa zinazofikia 61 kwa maana ya kwamba hizo zipo kwenye hatua ya utekelezaji.

Hii programu ya maji iko katika awamu ya miaka mitano kuanzia 2006 mpaka 2025. Kwa hiyo, kama tutafanikiwa kutekeleza awamu ya kwanza kwa Halmashauri hizo zikapata zote vibali inatupa nafasi ya kwenda awamu ya pili na kwa maana hiyo Vijiji alivyojitaja Mbunge havikuwepo awamu ya kwanza vitaingizwa kwa awamu ya pili.

Mheshimiwa Spika, suala la msingi nataka niliseme hapa, tatizo kubwa siyo uhaba wa fedha, uhaba wa fedha ni kigezo kimojawapo, lakini tatizo kubwa ni usimamizi wa miradi hii. Wabunge wote tushirikiane kusimamia ili fedha zinazopelekwa kwenye Majimbo zifanye kazi inayotakiwa na matokeo yake tuhamie baada ya kukamilisha miradi tuende kwenye miradi mingine, hiyo itakuwa ndiyo ukombozi wa miradi mingi ya maji. Ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Kule kwenye pigeon holes zenu kuna karatasi ya programu ya maji ya vijiji kumi, jana nilisahau kuwatangazia, mkaangalie huko mtaona kila mahali.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi, nami nilitaka nimwulize

15 Waziri pamoja na majibu mazuri. Kama ilivyo tatizo la Mkoa wa Tabora Manispaa ya Kigoma Ujiji pamoja na kwamba Lake Tanganyika iko usoni mwa Manispaa hiyo, lakini sasa tumekuwa na mradi wa EU Water Facility imesemwa huu ni mwaka wa kumi sasa, naomba niulize mradi huu utatekelezwa lini?

SPIKA: Swali jipya, lakini utapata jibu la jumla, Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ni kweli ni muda mrefu mradi huu umechukua lakini nataka kumhakikishia kwamba kwenye Bajeti ambayo tunaleta safari hii huu mradi wa Kigoma upo.

SPIKA: Ahsante sana na wengine mtazungumza huko mtapata muda wa kutosha Jumatatu.

Na. 146

Maji ya Ziwa Victoria Kufika Miji ya Ngudu, Sumve na Malya

MHE. EZEKIEL M. MAIGE (K.n.y. MHE. RICHARD M. NDASSA) aliuliza:-

Kama Maji ya Ziwa Victoria yameshafika katika kijiji cha Mhalo, Kwimba km. 70 kutoka Mji wa Ngudu:-

Je, ni lini maji haya yatafika katika Miji ya Ndugu, Sumve na Malya.

16 NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri wa Maji, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Richard Mganga Ndassa, Mbunge wa Sumve kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spiika, tanki la Mhalo Wilayani Kwimba liko umbali wa kilomita 23 kutoka bomba kuu linalotoa maji Ziwa Victoria kupeleka katika miji ya Kahama, Shinyanga. Tanki hilo lilijengwa katika miaka ya sabini, lakini halikutumika kutokana na ukosefu wa chanzo cha maji.

Hata hivyo, ujenzi wa mradi wa maji wa Kahama- Shinyanga ulipokamilika, Serikali ilifunga bomba kuepeleka maji katika tanki la Mhalo na kwa sasa tanki hilo lina Maji. Vijiji 22 katika Tarafa ya Mwamashimba vyenye jumla ya wakazi 67,744 vitafaidika na huduma ya maji kutoka kwenye tanki hilo. Kwa sasa vijiji vitano ambavyo ni Bupamwa, Mhalo, Chasalawi, Kawekamo na Sanga tayari vimeanza kupata maji. Lengo la Serikali ni kujenga matanki madogo katika vijiji 17 vilivyobaki na kuunganisha vijiji hivyo na maji ya tanki la Mhalo kwa njia ya mtiririko. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kutokana na hatua hiyo, maji ya tanki la Mhalo hayatatosha kuipatia maji Miji Midogo ya Ngudu, Sumve na Malya. Hivyo, Serikali ina mpango wa kujenga mradi wa maji kutoka Ziwa Victoria kwenda mji wa Magu hadi Ngudu. Mradi huo utahudumia pia vijiji na miji ya njiani litakapopita bomba kuu ukiwemo Mji mdogo wa Sumve. Serikali

17 tayari imekamilisha usanifu na kukokotoa mahitaji ya maji katika miji ya Magu na Ngudu mwezi Machi 2012. Kazi ya upembuzi yakinifu, usanifu na uandaaji wa makabrasha ya zabuni ya bomba la maji la mradi utakaoleta maji na kuunganisha miji hiyo itatekelezwa katika mwaka wa fedha 2012/2013. Ujenzi utaanza baada ya usanifu kukamilika na fedha kutengwa. Taarifa ya usanifu huo pia itatoa mapendekezo ya njia itakayotumika kuupatia maji Mji mdogo wa Malya.

MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Spika, naomba nimshukuru sana Naibu Waziri kwa majibu yake mazuri, naomba kuuliza swali moja dogo la nyongeza.

Mheshimiwa Spika mpango wa kuongeza vijiji au miji inayonufaika na maji ya ziwa Viktoria umekuwepo kwa muda mrefu na kwa miji midogo inayozunguka Mji wa Kahama, miji inayoguswa na mpango huo ni pamoja na Mji mdogo wa Kagongwa na Isaka na mpango huu umekuwepo tangu mwaka 2008 na mipango imekuwa ikiendelea. Nilitaka kufahamu. Je, Serikali imefikia hatua gani sasa katika mpango wa kuwapatia maji wananchi wa Isaka na Kagongwa Wilayani Kahama ambao wapo kwenye mpango wa maji ya Ziwa Victoria?

NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, ni kweli kumekuwa na mpango wa kupeleka maji kwenye vijiji vilivyokuwa kandokando ya bomba linalotoa maji kutoka ziwa Victoria kwenda Kahama na Shinyanga na mpango huu umekuwa ukitekelezwa kwa awamu. Awamu ya kwanza ilikuwa ni kupeleka kwenye vijiji

18 vilivyo kilomita tano kutoka umbali wa bomba ambavyo vilipatikana vijiji 54 na 39 vikaanza kupata maji.

Awamu ya pili ikaongezwa vifikie vijiji 96 na uongezeke umbali wa kilomita 12 kutoka katikati ya bomba kila upande. Sasa hivi kinachofanywa ni kwamba tayari Serikali imeshatenga fedha katika awamu hii tunayokwenda kwenye Bajeti bilioni moja kwa ajili ya kufanya usanifu kwenye vile vijiji ambavyo vipo umbali wa kilomita 12, lakini vile vile kama utazingatia juzi tarehe 4 Julai, 2012 Wizara imeshatoa tangazo kwenye magazeti kuhusu zabuni ya kuepeleka maji Magu na Miji ya Ngudu na vile vile kutoka Victoria kwenda miji ya Meatu. Kwa hiyo, mipango inaendelea na tutaendelea kukamilisha awamu kwa awamu. (Makofi)

MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Spika ahsante sana kwa kunipatia nafasi nami niulize swali la nyongeza.

Mheshimiwa Spika, bahati mbaya hadithi za Serikali kuhusu tatizo la maji ya Kwimba limekuwa linajirudia, yaani hizi hadithi zimekuwa za miaka nenda rudi. Ukifuatilia majibu yanayotolewa na Mawaziri ni yale ambayo yametolewa tangu miaka mitano iliyopita. Naomba sasa Serikali mbele ya Bunge lako Tukufu itoe ahadi ya mwisho jinsi gani watatatua tatizo la maji Kwimba ambalo linaathiri vijiji vingi, ikiwemo Mwamashimba, ikiwemo Hungumarwa, ikiwemo Ngudu Mjini na kwingineko? (Makofi)

19 SPIKA: Ahsante anaweza kwa hili lakini siyo swali lako la msingi. Kwa hiyo hakujiandaa kwa hili lakini jibu tu, Waziri kwa kifupi kwa sababu bado ni Wizara yako.

WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Spika, katika jibu letu la msingi tumeeleza kwamba hivi sasa maji yako kwenye tanki la Mhalo na vijiji vyote 22 vilivyopo kwenye Tarafa ya Mwamashimba inagawiwa maji. Kwa hiyo, Serikali haiko kwenye biashara ya kutoa hadithi.

Mheshimiwa Spika, kwa ajili ya Ngudu, ningemwomba Mbunge aangalie gazeti la Guardian ataona tangazo la Serikali la kutafuta consultant kwa ajili ya kutengeneza mradi kutoka Ziwa Victoria kwenda mpaka Mji wa Ngudu. Nakushukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Sasa unaona hilo swali inawezekana hukujibiwa kwa sababu halikuwa kwenye origin, I am sure Ngudu is not the same Mji uliokuwa unaosema. Ndiyo hasara ya kuuliza swali ambalo siyo lenyewe utajibiwa kama ulivyojibiwa.

Na. 147

Kupeleka Umeme Makao Makuu ya Wilaya ya Kakonko Kutoka Kibondo.

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE aliuliza:-

Serikali bado haijaweza kuunganisha Mkoa wa Kigoma kwenye umeme wa grid ya Taifa zaidi ya

20 kununua majenereta ya kuwezesha Miji ya Kibondo na Kasulu kupata umeme:-

Je, Serikali iko tayari kuvuta umeme kutoka Mjini Kibondo kwenda Makao Makuu ya Wilaya mpya ya Kakonko?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephine Johnson Genzabuke, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Kigoma katika Miji ya Kigoma, Kasulu na Kibondo inapata umeme kwa kutumia jenereta mpya ambazo zimetokana na dhamira ya Serikali ya kutekeleza mkakati wa kupeleka umeme katika Makao Makuu ya Wilaya zote nchini. Hata hivyo, Mji wa Kigoma una jenereta 5, kibondo jenerata 2 na Kasulu jenereta 2, zenye uwezo wa kuzalisha MW 1.25 kila moja. Aidha, umeme unaozalishwa na majenereta hayo ni mwingi kuliko mahitaji yaliyopo katika Miji hiyo kwa sasa. Kufuatia kukamilika kwa mradi wa kufikisha umeme Makao Makuu ya Wilaya ya Kibondo, Serikali kwa kushirikiana na TANESCO imewasilisha maombi ya fedha kwa Wakala wa Nishati Vijijini (REA) kwa ajili utekelezaji wa mradi huo.

Aidha, mradi huu utatekelezwa katika mwaka wa fedha 2012/2013 na kukamilika katika kipindi cha miezi

21 24. Vijiji vifuatavyo vitafaidika na mradi huu, Kilemba, Kambi ya JKT Kanembwa, Kasanda na Kabingo.

MHE. JOSEPHIN J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika nakushukur kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili ya nyongeza.

Kwa kuwa, ni sera ya Serikali ya ya kuwa kila Makao Makuu ya Wilaya yatapatiwa umeme, nilitaka kujua, Wilaya ya Kakonko, Uvinza na Bihigwe ni lini zitapatiwa umeme?

Swali la Pili, kwa kuwa baada ya umeme kufika katika Wilaya ya Kasulu wananchi wengi walihamasika kwa wingi kulipia gharama za umeme ili waweze kuwekewa umeme kwenye nyumba zao, lakini kwa zaidi ya miezi kumi sasa hawajaweza kupatiwa huduma hiyo ya umeme kwa visingizio kwamba hakuna nguzo wala nyaya za kusambazia umeme.

Je, ni lini wananchi hao watapatiwa umeme ikiwa ni pamoja na vijiji vya Heru Juu, Msambala, Nyakitondo, Kitye ambako kuna mradi mkubwa wa umwagiliaji? (Makofi)

SPIKA: Ahsante Naibu Waziri majibu, naona Wakigoma wote wanapiga makofi siwapi nafasi ya swali lingine. (Kicheko)

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, kwanza kama nilivyosema katika jibu langu la msingi kwamba mradi huu wa kupeleka umeme katika Wilaya

22 mpya ya Kakonko upo mbioni katika utekelezaji wa miradi ya awamu ya pili ya REA na nimesema hapa katika miezi 24 tu mradi huu utakuwa umekamilika.

Lakini la Pili, wateja walioomba umeme katika Wilaya ya Kasulu na vijiji alivyovitaja, ninayo programu ambayo tumeiandaa kwa awamu ya pili ya REA lakini kwa kushirikiana na TANESCO ambayo tutaifanya katika kipindi cha mwaka 2012/2013 naomba Mbunge baada ya hapa tuwasiliane ili niweze kumwonesha kazi ambayo itafanyika Wilaya ya Kasulu kwa waombaji wale walioomba.

MHE. MOSES J. MACHALI: Nakushukuru kwa kuniona, Kwa kuwa mradi wa umeme uliopo katika Wilaya za Kasulu pamoja na Kibondo hautoshelezi mahitaji, na vile vile kwa kuwa katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2008/209 Serikali ilikuwa imetenga kiasi cha shilingi bilioni kumi kwa ajili ya kuunganisha Mkoa wa Kigoma na gridi ya Taifa, lakini fedha zile zilihamishwa Serikali ikisema kwamba zimekwenda kutatua matatizo yaliyoikumba nchi yetu ya njaa kwa maana ya kusaidia watu wetu na hivyo kuweza kuahirisha utekelezaji wa mradi ule.

Je, Serikali inatoa kauli gani kwa kuwa hivi sasa nafikiri ni wakati muafaka wa kuweza kuunganisha Mkoa wa Kigoma na gridi ya Taifa kwa kuweza kutenga kiasi kingine cha fedha?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, sijui tafsiri ya gridi maana yake nini, lakini maana yake ni

23 kuunganisha kwenye mkongo ule ambao unaiunganisha nchi nzima, lakini hata huo mkongo wa Taifa unapata umeme wa kutoka kwenye majenereta, tunazalisha pale Dar es Salaam tunaingiza kwenye gridi.

Lakini hapa nizungumzie tu kwamba Serikali Ilichofanya sasa ni kwamba Wilaya ya Kasulu na Wilaya ya Kibondo zina majenereta haya tayari na uwezo wa uzalishaji wa umeme kwa mfano kwa Kibondo tunazalisha pale megawati 2.5 na uwezo wenu mnatumia karibu Kilowati 315. Uwezo wa Kasulu inazalisha 2.5 megawati uwezo matumizi ni kilowati 374. Utaona kwamba bado tuna umeme unaobakia ambao bado hautumiki kwa sababu ya uwezo mdogo wa matumizi. Kwa hivyo mimi nitoe wito hapa kwamba tutajitahidi kuhakikisha kwamba kama ni suala la kuunganisha kwenye gridi bado hata hizo jenereta zitazalisha kupeleka kwenye gridi lakini na ninyi tuendelee kujenga uwezo wa watu wetu kujiunga katika umeme huo ambao upo ambao haufanyi kazi.

Mheshimiwa Spika nakushukuru sana. (Makofi)

SPIKA: Ahsante, tumetumia karibu dakika nane kujibu swali hilo, tunamwita sasa Mheshimiwa Kangi Lugola aulize swali linalofuata, kwa niaba yake Mheshimiwa Bulaya, sijui hawa jamaa wamekwenda wapi, mpirani au wapi? (Kicheko)

Na. 148

Utafiti wa Madini ya Dhahabu Jimbo la Mwibara.

24

MHE. ESTER A. BULAYA (K.n.y. MHE. ALPHAXARD K. LUGOLA) aliuliza:-

Kwa muda mrefu inasadikiwa kuwa sehemu kubwa ya Jimbo la Mwibara ina utajiri mkubwa wa Madini ya dhahabu na wapo wachimbaji wadogo wadogo ambao wanachimba kwa kubahatisha sehemu zenye madini:-

(a) Je, Serikali iko tayari kusaidia utafiti wa Madini haya ili wachimbaji wasibahatishe?

(b) Kama Serikali iko tayari. Je, ni lini itanza utafiti huo?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nishati na Madini naomba kujibu swali la Mheshimiwa Alphaxard Kange Lugola, lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, taarifa za utafiti uliofanywa miaka ya sitini zinaonesha kuwa Jimbo la Mwibara Wilayani Bunda liko katika ukanda wa miamba ya green stone belt ambayo huambatana na dhahabu. Miamba hiyo inapatikana katika vijiji vya Bunyere, Nayasimo, Mwitende, Mukukoko, Susi, Mwigundu, Bulendabufwe, Nyamuhura, Bulmba na Karukekere.

25 Wachimbaji wadogo wanachimba dhahabu pia katika maeneo ya Nyamuhura na Bulamba.

Mheshimiwa Spika, hadi sasa hakuna utafiti wa kina uliofanywa kuthibitisha kiasi cha dhahabu kilichopo katika maeneo hayo japo kuna leseni za utafutaji mkubwa, leseni za uchimbaji mdogo pamoja na maombi ya leseni.

Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo wamekuwa wakichimba kwa kubahatisha katika maeneo mbalimbali ya nchi yetu kutokana na kutokujua mashapo katika maeneo wanayochimba. Hivyo Serikali imeamua kuandaa mikakati madhubuti inayolenga kuendeleza uchimbaji mdogo nchini.

Tarehe 23 Juni, 2012 Waziri wa Nishati na Madini alikutana Mjini Dodoma na wawakilishi wawili wa wachimbaji wadogo kutoka kila Mkoa kuzungumzia matatizo yanayowakabili pamoja na mikakati ya kuyatatua, moja kati ya matatizo yaliyoelezwa ni kutokuwa na taarifa za utafiti katika maeneo ya wachimbaji wadogo. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wizara itayafanyia utafiti maeneo yanayoonekana kufaa kwa ajili ya wachimbaji wadogo na kutenga maeneo kwa ajili yao. Aidha, ili kujua taarifa za kijiolojia katika maeneo hayo, Serikali itawasaidia wachimbaji wadogo wakiwemo wa Jimbo la Mwibara kufanya utafiti kwa kuwatumia STAMICO na wakala wa jiolojia Tanzania (GST).

26 MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Spika, ahsante naomba niulize maswali mawili ya nyongeza. Kwa kuwa uzoefu unaonyesha wachimbaji wadogo wadogo wa maeneo husika wanapogundua eneo husika kwamba lina madini fursa inatolewa kwa makampuni makampuni makubwa.

(a) Sasa je, eneo la Mwibara likijulikana lina madini Serikali itakuwa tayari kuwasaidia wachimbaji wale wadogo kuwawezesha kupata vifaa vya kisasa na wao waweze kuchimba madini katika eneo hilo badala ya kuwapa fursa makampuni makubwa?

(b)Kwa kuwa nchi kama Ne w Papuan Guinea eneo husika litakapogundulika lina madini wananchi wa eneo hilo hupata asilimia fulani. Sasa je, Wananchi wa Mwibara na Bunda kwa ujumla watanufakaje kwa ardhi yao endapo itagundulika ina madini?

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Ester Bulaya, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, wachimbaji wadogo wanapogundua maeneo yenye madini na kwamba wakishagundua basi wachimbaji wakubwa huwavamia na baadaye kuchukua yale maeneo. Sisi tumejipanga Wizarani na katika Bajeti hii ya mwaka 2012/2013 tumetenga kiasi cha shilingi karibu bilioni 9 kwa ajili ya wachimbaji wadogo. Bilioni 9 hizo ni kwa ajili ya kutoa elimu kwa maana elimu katika uchimbaji wa madini.

27

Lakini pia kwa ajili ya kusaidia kuwafanya wapate na wenyewe vifaa au zana zitakazowawezesha waweze kufanya kazi yao kwa urahisi zaidi. Kwa hiyo, tumejipanga kubwa hapa Mheshimiwa Bulaya tusaidie tu Bajeti yetu itakapokuja iweze kupita basi wachimbaji wadogo wataweza kupata msaada huu wa vifaa kwa namna yoyote ya kukopeshwa au vinginevyo ili waweze kurahisisha shughuli yao. (Makofi)

Lakini la pili umeuliza juu ya kama kutagundulika je, wananchi wanaoishi maeneo yale watanufaika vipi? Ni kweli kwamba iko sheria na sheria inataka lazima katika mikataba na mikataba yetu iko hivyo kwamba lazima kuwe kuna wajibu wa makampuni hayo kwa jamii inayozunguka yaani Corporate Social Responsibility.

Sasa hii ni lazima na nichukue nafasi hii kuwaomba makampuni yote ya madini yaliyofanya uwekezaji hapa nchini kwamba kipengele hiki cha kutoa au kusaidia jamii inayozunguka katika maeneo ya migodi ni muhimu sana wakatekeleza kwa sababu ndio itakayosababisha mahusiano yao na wananchi kuwa mazuri. Hapa nitoe wito tu kwamba kwa kuwa madini haya hayajagundulika bado basi Mheshimiwa Bulaya avumilie mpaka hapo yatakapogundulika ndipo tutakapozungumzia juu ya kipengele hiki vizuri zaidi na tutawalazimisha waweze kulipa na kusaidia jamii katika maeneo hayo. (Makofi)

28 MHE. DESDERIUS JOHN MIPATA: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kuniona. Naomba kuuliza kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, kuna mwekezaji mzalendo ana leseni ya kuchimba mkaa wa mawe pale kijiji cha Nkomolotuu na Namwele.

SPIKA: Lakini kanuni hairuhusu usome.

MHE. DESDERIUS JOHN MIPATA: Mheshimiwa Spika, na kwamba mwekezaji huyu ana uwezo mdogo wa kuweza kusisimua akiba kubwa sana inayosemekana iko pale. Je, Serikali kupitia PPP iko tayari kushirikiana naye ili kumwezesha aweze kupata uwezo wa kutafiti zaidi na kupata uwezo wa kuchimba?

SPIKA: Huko kijijini kwako ni sawa sawa na huko Mwibara unampa matatizo sana Waziri mimi sijui kama anasemaje Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. GEORGE B. SIMBACHAWENE): Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mhesimiwa Mipata kama ifuatavyo:-

Sisi Serikali taasisi yetu ya STAMICO Shirika la Madini la Taifa liko kwa ajili ya kufanya mambo kama haya. Kwa hiyo, jambo hili kama kweli katika kijiji hicho Namwele kuna Mchimbaji Mdogo anayeendesha uchimbaji wa makaa ya mawe na uwezo wake ni mdogo basi tutajaribu kuwasiliana na STAMICO tuone namna gani wanaweza wakaona namna ya

29 kumsaidia kwa namna yoyote ili kuweza kuwa na uchimbaji wenye tija na kutoa ajira kwa watu wengi zaidi. Nakushukuru sana. (Makofi)

Na. 149

Barabara Kuunganisha Mpanda – Mlele – Sikonge – Tabora

MHE. SAID AMOUR ARFI aliuliza:-

Miundombinu ni muhimu sana katika kuunganisha nchi na kuharakisha maendeleo:-

Je, ni lini Serikali itajenga barabara ya lami ya kuunganisha Wilaya ya Mpanda, Mlele, Sikonge na Tabora?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Said Amour Arfi, Mbunge wa Mpanda Mjini, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Serikali imeanza maandalizi kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami barabara ya Mpanda – Mlele – Sikonge – Tabora, yenye urefu wa kilomita 359. Kazi ya upembuzi yakinifu, usanifu wa kina na tathimini ya athari kwa mazingira kwa barabara hii ilianza mwezi Juni, 2009 na kukamilika Aprili, 2012.

30 Mheshimiwa Spika, baada ya usanifu kukamilika, Serikali inatafuta fedha ili ujenzi kwa kiwango cha lami uweze kuanza.

MHE. SAID AMOUR ARFI: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri yenye matarajio makubwa kutoka kwa Mheshimiwa Naibu Waziri nina maswali mawili ya nyongeza.

(a)Kwa kuwa Barabara hii ina umuhimu wa kipekee kwa ajili ya kusafirisha nafaka kutoka Mpanda kupeleka katika maeneo yenye shida ya chakula na hali ya barabara ni mbaya hata Makamu wa Rais alipofanya ziara katika Mkoa wa Katavi alishindwa kufika Mlele mpaka akapelekwa kwa helicopter. Je, Wizara sasa itaongeza fedha ya kuhakikisha barabara hii inaimarika wakati ikisubiri kujengwa kwa kiwango cha lami?

(b) Kwa kuwa barabara ya kutoka Mpanda mpaka Kanyani ni muhimu na ni kiungo kikubwa kwa ajili ya kuunganisha nchi ya Zambia, Rwanda, Burundi na Uganda ili kuziunganisha nchi za Afrika. Serikali ina mpango gani sasa wa kuijenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Said Arfi, Mbunge wa Mpanda Mjini, kama ifuatavyo:-

Kwanza, kabisa naomba nikuhakikishie kwamba baada ya kwamba tumeshaanza usanifu wa barabara

31 hiyo, tutaendelea kuimarisha matengenezo ya kawaida na Bajeti ambayo tunayo ambayo nakuomba uipitishe tumeweka fedha za kutosha kwa ajili ya matengenezo hayo.

Swali lako la pili ni lini tutajenga barabara ya Mpanda – Kanyani. Kwanza kabisa sera yetu ya taifa ni kwamba tumeanza kujenga barabara zinazounganisha Mikoa kwa Mikoa, barabara kuu, kujenga kwa kiwango cha lami. Tutapomaliza tutaanza kushughulikia barabara za Mikoa ambazo zinaunganisha Wilaya na maeneo muhimu ya uzalishaji. Kwa hiyo, barabara hii tutaiangalia katika kipindi kijacho cha Bajeti.

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kuniona. Tatizo hili lililokuwepo katika barabara za Mpanda linawiana kabisa na tatizo lililokuwepo katika barabara ya Kilwa Road. Tatizo lililosababisha kusimama kwa ujenzi wa Barabara kutoka Ndundu hadi Somanga ni lipi ambapo mkandarasi yuko pale na vifaa vyote vipo lakini ujenzi umesimama hivi sasa?

SPIKA: Kusema linafanana halifanani isipokuwa kwa sababu barabara hii ni maarufu basi jibu Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mangungu kama ifuatavyo:-

32 Ujenzi wa barabara ya Ndundu – Somanga haujasimama ulikuwa umepunguzwa kasi kutokana na upatikanaji wa fedha. Lakini tatizo hilo tumeshalitatua na sasa hivi mkandarasi anaendelea na kazi. Tumeahidi hapa Bungeni kwamba kazi hiyo itaisha katika mwaka huu wa fedha. (Makofi)

Na. 150

Ujenzi wa Daraja la Ruhuhu

MHE. DEO HAULE FILIKUNJOMBE aliuliza:-

Daraja la Ruhuhu ni muhimu kwa wananchi wa Ludewa, Manda, Masasi na Lwilo:-

Je, Ujenzi wa Daraja hilo utaanza na kukamilika lini?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Deo Haule Filikunjombe, Mbunge wa Ludewa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi ilianza maandalizi kwa ajili ya usanifu wa Daraja la Mto Ruhuhu mwaka 2009/2010. Aidha, katika mwaka wa fedha 2011/2012 jumla ya shilingi milioni 90.60 zilitengwa kwa ajili ya kazi hiyo. Kufuatia kuanza kwa zoezi hili Wizara ya Maji na umwagiliaji ilitoa pendekezo la kuunganisha nguvu la kujenga structure moja

33 itakayotumika kama daraja na wakati huo huo kama Bwawa na Banio litakalotumika kwa umwagiliaji.

Mheshimiwa Spika, baada ya mapendekezo hayo mnamo mwezi Agosti 2010 kikosi kazi cha watalaam toka Wizara za Ujenzi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Maji na Umwagiliaji, Kilimo na Chakula kiliundwa ili kushughulikia suala hili. Ili kusimamia mradi huu Kamati ya kuongoza mradi (Steering Committee) imeundwa inayowajumuisha Makatibu wa kutoka Wizara za Ujenzi, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Maji na Umwagiliaji na Kilimo na Chakula.

Mheshimiwa Spika, juhudi zinazoendelea sasa ni za kumtafuta Mhandisi Mshauri wa kufanya upembezi yakinifu na usanifu wa kina. Taratibu za kumpata Mhandisi Mshauri ziko katika hatua za mwisho na anategemewa kuwa amepatikana ifikapo Agosti, 2012.

Mheshimiwa Spika, kazi za ujenzi wa daraja na bwawa la umwagiliaji zitaanza baada ya kukamilika kwa usanifu. (Makofi)

MHE. DEO HAULE FILIKUNJOMBE: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri naomba kuuliza maswali mawili kama ifuatavyo:-

(a) Kwanza kabisa ningependa kujua mwaka huu wa fedha Serikali imetenga fedha kiasi gani kwa ajili ya kukamilisha zoezi hili la ufanisi wa kina kwenye hili daraja?

34 (b)Ninaomba kauli thabiti ya Mheshimiwa Waziri wa ujenzi wenyewe wa daraja Ruhuhu kwa ajili ya wananchi wa Ludewa pamoja na Mbinga utaanza lini?

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Deo Filikunjombe, Mbunge wa Ludewa, kama ifuatavyo:-

Kwanza naomba nimpongeze kwa namna anavyofuatilia maendeleo ya wananchi wa Ludewa ikiwa ni pamoja na miundombinu na hayo madaraja. Anaulizia ni kiasi gani kimetengwa? Kwenye jibu la msingi nimesema kwamba tuko katika hatua ya mwisho kumpata Mhandisi Mshauri sina kiasi gani lakini kwenye Bajeti hii ambayo tumewasilisha tumeweka kitu ambacho tutahakikisha kwamba kazi hiyo ambayo imepangwa inafanyika. Ujenzi utaanza baada ya kukamilisha ule usanifu wa kina.

MHE. MOZA ABEDI SAIDY: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza swali moja la nyongeza.

Kwa kuwa katika Wilaya ya Kondoa kuna daraja ambalo ni la kivutio lililokuwepo toka enzi na kuingizia mapato taifa na Wilaya pia, ni daraja la mnesoneso likiwa ni matumizi kwa wananchi. Je, Serikali inasema nini kuhusu kulijenga daraja lile na kulirejesha upya na wananchi waweze kulitumia?

35 SPIKA: Utauliza wakati wa mshahara wa Waziri. Maana hilo lingine kabisa halifanani na hili hapa. Wakati wa mshahara wa Waziri utasimama uulize.

Na. 151

Ulinzi wa Urejeshaji wa Maeneo ya Mji

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMED aliuliza:-

Mbinu na mikakati endelevu inahitajika kuendeleza miji pamoja na kuhifadhi na kulinda maeneo ya wazi, pia kurejesha maeneo yaliyovamiwa katika hali yake.

(a) Je, Serikali kupitia kikosi kazi chake cha Askari wa Makazi (Land Rangers) imefanikisha kurejesha maeneo mangapi yaliyovamiwa katika majiji yetu nchini?

(b) Je, Serikali ina mikakati gani endelevu ya kuamsha ari ya ulinzi shirikishi wa maeneo ya uhifadhi na yaliyowazi?

NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI alijibu:-

Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Rajab Mbarouk Mohamed, Mbunge wa Ole, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:-

36 (a) Mheshimiwa Spika, mwaka 2011/2012 Wizara yangu iliajiri Askari Ardhi kumi na tano na kuwapangia kazi kwenye Manispaa za Jiji la Dar es Salaam.

Lengo lilikuwa ni kupata uzoefu kabla ya zoezi hilo kuendelea katika Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya nyingine nchini. Kutokana na kuajiriwa kwa Askari Ardhi, Serikali imepata mafanikio ambayo ni pamoja na haya yafuatayo:-

(i) Askari Ardhi waliopangiwa Manispaa ya Temeke walibaini maeneo manne ya wazi yaliyovamiwa ambayo ni Miburani, Chang’ombe, Temeke na Sudani. Hivyo wavamizi waliondolewa na maeneo hayo yalirudishwa kwenye matumizi ya awali.

(ii) Askari Ardhi waliopangiwa Manispaa ya Kinondoni walibaini uvamizi katika maeneo ya wazi kumi eneo la Sinza. Hatua za kuyarejesha maeneo hayo zinaendelea. Aidha, Wizara imeanza kusimika mabango kwenye maeneo ya wazi yanayotahadharisha wavamizi waondoke katika maeneo hayo wakati hatua za kisheria zinachukuliwa.

(b) Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua umuhimu wa kuwepo kwa ulinzi shirikishi katika kulinda maeneo ya wazi na uhifadhi wa mazingira. Wizara yangu imeanzisha programu ya kutoa elimu kwa umma juu ya sera na sheria zinazosimamia sekta ya ardhi.

Programu hii itatekelezwa kwa kushirikiana na wadau mbalimbali vikiwemo vyombo vya habari. Hata

37 hivyo ninaendelea kuwahamasisha wananchi kuwa wa kwanza kutambua uvamizi unaofanywa kwenye mitaa yao hususan maeneo ya wazi na ya huduma. (Makofi)

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMED: Mheshimiwa Spika, ahsante kwanza nataka niipongeze Wizara kwa kuanzisha kikosi kazi hiki kwa majaribio.

Mheshimiwa Spika, uvamizi wa ardhi, ujenzi, umiliki wa vibali vya kujengea, umiliki vya vibali vya maeneo unajumuisha taasisi nyingi, taasisi ambazo Maafisa Ardhi wengine wanakuweko chini ya Halmashauri, Halmashauri wana sheria zao.

(a) Je, Mheshimiwa Waziri huoni kwamba watendaji hawa ambao umewaweka kwa ajili ya kuangalia haya maeneo watakuwa hawana nguvu katika Halmashauri hizo?

(b) Serikali kupitia ndani ya Jeshi la Polisi imeweka vitengo kwa ajili ya kulinda baadhi ya maeneo hasa yale ya kiuchumi, reli, posta na maeneo mengine. Huhisi kwamba sasa hivi ukakaa kitako ukashauriana na wenzako mkaanzisha kitengo katika Jeshi la Polisi ambacho kitaitwa Polisi Ardhi?

WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Mheshimiwa Spika, naomba nifafanue kwamba alivyozungumza Mheshimiwa aliyeuliza swali anagusia mambo muhimu na ni ushauri ambao tayari tunaufanyia kazi.

38 Kama vile anavyofahamu tumeshakutana na Mheshimiwa Waziri wa Ulinzi, Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, kukubaliana kwamba sasa imefika wakati wa vitendo. Maana yake matatizo mengi yanayoeleweka kama matatizo ya ardhi kimsingi ni matatizo ya kiutawala ni sheria ya TOT siyo sheria ya ardhi sheria inayosimamia trace passes yaani mtu kuingilia mali ambayo siyo ya kwako.

Kwa hiyo, nichukue nafasi hii katika kujibu swali hilo kusema kwamba tunakubaliana kabisa na ushauri Land Rangers tumeanza Dar es Salaam na tunahimiza Halmashauri zote kuwa na kitengo hiki. Hii kada ya watumishi ambayo ilikuwepo lakini sasa mambo yaliyopita watu wakafikiria siyo muhimu athari zake zimejitokeza. Hilo ni la kwanza. (Makofi)

Sasa la pili kwamba Maafisa, Maafisa wengi wa Serikali siyo tu wa ardhi hata walimu, hata madaktari hata wauguzi wote wako chini ya himaya ya Halmashauri za Wilaya.

Sasa inapokuja kwenye sekta ya ardhi kwa sababu sekta hii ni lazima iendeshwe kisheria na kitalaam ni kweli kwamba zimetokea nyakati maafisa wenyewe wa ardhi wakati mwingine wameogopa wakaanza kutekeleza mambo kinyume na maadili na matakwa ya kazi yao. Mimi nimekuwa nikiwahimiza kwamba atakayeogopa hata akisema Madiwani wameniagiza hili au lile yeye mwenyewe ndio atawajibishwa.

39 Kwa hiyo, inabidi wawe na ujasiri wafanye kazi yao bila kutishwa na mtu yeyote. Kiongozi yeyote awe Kiongozi wa Serikali au sisi wenyewe viongozi kama Wabunge.

Kiongozi wa namna yeyote ile, kwa kweli hatufanyiwi haki wanapowatishia Maafisa Ardhi. Wenyewe imeonekana kwamba wamechukua nafasi hii sasa kufanya vitendo vingine ambavyo wanajua hatimaye watasema mimi niliambia na Halmashauri ninfanye hivyo, mimi niliambaiwa na Madiwani nifanye hivyo.

Nasema visingizio hivi tunavikomesha na kikosi cha askari ardhi sasa hivi, kitawezeshwa kuwa na askari ndani ya Jeshi la polisi ambao sasa itakuja kuangalia trace passes, trace pass nitoe tu mfano kama ifuatavyo; watu wengi wanakwenda kwa maafisa ardhi kulalamika kwamba viwanja vyao vimevamiwa, kwani mtu ukienda dukani ukanunua kitanda, ukakuta sasa mtu ameshakalia kitanda chako, unarudi dukani kupiga kelele? Si unaita polisi? (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo naomba tuelewe sheria inavyokwenda kwamba uvamizi ni suala la polisi kama wewe una hati halali, unakuta mwenzako hana karatazi yeyote anaanza kujenga, unakwenda kutafuta polisi, usimtafute Afisa Ardhi na Maafisa Ardhi wengine wamejifanya na wenyewe Mahakimu, hatuna madaraka sisi ya kuamua vitu ambavyo sio vya kwetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru.

40

SPIKA: Haya semina ya bure tunaendelea na swali linalofuata. Nasikitika hiyo semina inawatosheni sana. Wizara ya Fedha, Mheshimiwa Conchesta Rwamlaza kwa niaba yake namwona Dkt. Anthony Mbassa.

Na. 152

Mwenendo wa Mashirika ya Mikopo Nchini

MHE. DKT. ANTHONY G. MBASSA (K.n.y. MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA) aliuliza:-

Je, Serikali inahusika vipi katika kuratibu mwenendo wa utendaji wa Mashirika yanayotoa mikopo nchini kama vile PRIDE, BLAC, FINCA na kadhalika?

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. JANET Z. MBENE) alijibu:-

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Fedha, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Conchesta Rwamlaza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, moja ya kazi za Serikali ni kuweka na kuboresha mazingira ya uwekezaji na kufanya biashara kwa mashirika na taasisi binafasi kama PRIDE, BRAC, FINCA na kadhalika. Ili kutekeleza jukumu hili muhimu, Serikali inawajibika pamoja na mambo mengine kutunga Sera na Sheria inayotoa mwongozo na kusimamia mashirika na taasisi ndogo

41 ndogo zinazotoa huduma za fedha hususan mikopo kwa manufaa ya pande zote, yaani mashirika/taasisi na walaji.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2000, Serikali ilitunga Sera ya Taifa ya huduma ndogo ndogo za kifedha (micro finance policy) ambayo pamoja na mambo mengine; iliweka mfumo unaoelekeza jinsi taasisi zote zinazotoa huduma ndogo ndogo za kifedha zitakavyotakiwa kufanya kazi, ilitengeneza Kanuni zinazoongoza shughuli za utoaji huduma ndogo ndogo za kifedha, iliainisha majukumu ya wadau mbalimbali wa huduma ndogo ndogo za kifedha na kutoa mwongozo wa jinsi huduma ndogo ndogo za kifedha zinavyotakiwa kuratibiwa.

Mheshimiwa Spika, mwaka 2005, Serikali ilifanya marekebisho ya Sheria ya Fedha na kutoa Kanuni kwa lengo la kutoa mwanya kwa mashirika kama haya yanayotaka kuendesha shughuli zake kwa kutumia akiba za wanachama kama mtaji, ili yaweze kuomba na kupewa leseni na Benki Kuu.

Jukumu la Benki Kuu kwa Mashirika yaliyo chini yake ni kusimamia utendaji wake kwa nia ya kuhakikisha kwamba, kuna ushindani ulio salama, usalama wa mfumo wa fedha pamoja na usalama wa fedha za wananchi.

Mheshimiwa Spika, Serikali inaandaa chombo maalum ambacho kitatoa usimamizi kwa mashirika ambayo yanataka kuendelea kutoa huduma za kifedha kwa kutumia mitaji binafsi. Jukumu la chombo

42 hiki litakuwa ni kusimamia utendaji wa mashirika hayo ili kuhakikisha kuwa, kuna ushindani na usalama wa mfumo wa fedha.

Mheshimiwa Spika, katika kudhibiti mienendo hasi ya kiutendaji kwa mashirika haya, Serikali inaandaa mifumo ifauatayo:- Mfumo wa elimu ya huduma za kifedha kwa wananchi ili kuwawezesha wananchi kuzielewa huduma hizo na namna ambayo wanaweza kuzitumia kwa manufaa yao. Mfumo wa kumlinda mtumiaji wa huduma za kifedha na athari za mienendo hasi ya kushindani na mfumo wa kumbukumbu za madeni (credit reference system) kwa faida ya wadau wote. Ahsante sana.

MHE. DKT. ANTHONY G. MBASSA: Mheshimiwa Spika, ninashukuru kwa majibu niliyopata kutoka kwa Naibu Waziri lakini nilikuwa na maswali mawili ya nyongeza.

(a) Kwa kuwa mashirika haya, ukopesha na kutoza riba na kujiendesha zaidi kibiashara kuliko kutoa huduma. Je, kama Sera ipo, Sheria iansemaje kuhusu riba za juu zinazotozwa na mashirika haya?

(b) Wakopaji wengi ni akina mama na wanapokopa wakashindwa kurudisha, hunyanyaswa na aidha kuchukuliwa vifaa vya nyumbani na kufedheheshwa.

Je, kama mashirika haya yana Bima, kwa nini Bima isisaidie katika kutatua tatizo hili? Ahsante sana.

43 SPIKA: Ahsante sana, maswali yako umeuliza vizuri. Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. JANET Z. MBENE): Mheshimiwa Spika, nisamehe sijapata jina la Mheshimiwa Mbunge.

SPIKA: Anaitwa Dkt. Anthony Mbassa.

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. JANET Z. MBENE): Mheshimiwa Spika, Dokta?

SPIKA: Dkt. Anthony Mbassa, ni Dakitari wa hospitali huyu, sijui kwa nini hakwenda huko Muhimbili kusaidia. (Kicheko)

NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. JANET Z. MBENE): Mheshimiwa Spika, anawakilisha hapa hapa ndani. Naomba nijibu maswali mawili ya nyoneza ya Mheshimiwa Dkt. Anthony Mbassa, kama ifauatavyo:-

(a) Swali lake la kwanza linahusiana na riba kubwa inayotozwa na mashirika haya na kuwa mashirika haya yanafanya zaidi kazi kibiashara kuliko kihuduma.

Napenda tu kumfahamisha kuwa haya mashirika yanatoa huduma vile vile pamoja na kufanya biashara na kwa kiasi kikubwa pesa ambayo inatumika ni mitaji ambayo inatokana na mashirika haya, lakini vile vile mitaji ambayo ni akiba zinazowekwa na washiriki wa

44 taasisi hizi. Na katika kuhakikisha kuwa mitaji hiyo inalindwa, yaani mitaji ya wawekezaji pamoja na mitaji ya wananchi ambao wao wenyewe wanawekeza pesa zao, inabidi hizi riba ziwekwe ili kuhakikisha kuwa ile pesa haiharibiki.

Lakini vile vile kama nilivyozungumza katika jibu langu la msingi, taasisi hizi zinaongozwa na zinalindwa na taratibu za kisheria ambazo zinahakikisha kuwa hakuna matokeo yeyote hasi ambayo yatatokea kwa ajili ya kulinda mitaji hii na kuwalinda wakopaji.

(b) Kuhusiana na unyanyaswaji wa wakopaji pale pindi wanaposhindwa kulipa. Ni kweli kuwa kuna taratibu ambazo zinawekwa za kuhakikisha kuwa watu wanaokopa wanalipa kwa sababu hiyo ndiyo njia pekee yake ya kuhakikisha kuwa shughuli za huduma zinaendelea kwa wengine na ikumbukwe kuwa wanakopeshwa mitaji ambayo ni ya wenzao na vile vile ni ya taasisi hizi. (Makofi)

Kwa kiasi kibuwa nafikiri tutakachoweza kufanya ni kujadili tu nao kuwa wahakikishe kuwa wanapofuatilia madeni yao hawatumii njia ambazo sio za kibinaadamu na njia ambazo ni za kistaarabu, pengine hata kujaribu kuangalia kama wanaweza kuwaongezea muda wakopaji katika kurejesha mikopo yao. Lakini vile vile nitoe tu ari kwa wanaokopa kuwa wajitahidi kwa kadri iwezekanavyo kutumia mikopo hii kwa madhumuni waliokopea ili waweze kuzalisha na kulipa. (Makofi)

45 SPIKA: Wheshimiwa muda umekwisha na maswali yamekwisha, kwa hiyo, naomba tunapojadiliana na nyie muwe mnaangalia saa maana itaonekana Kiti kinawanyanyasa sivyo. Kwa hiyo, nawashukuru sana maswali yameisha.

Sasa nitangaze kuhusu wageni. Wageni waliopo hapa ukumbini kwetu ambao nimepewa majina yao hapa, kwanza kabisa ni wageni wa Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Dkt. , ambao ni Dkt. Edward Ngwale, huyu Dokta yeye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Ushauri ya Wakala wa Majengo, ahsante sana.

Halafu kun awageni wa Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Engineer , hawa ni Madiwani 23 kutoka Mkoa wa njombe wakiongozwa na Ndugu Anthony Maweta, naomba Waheshimiwa Madiwani popote walipo wasimame, ahsante sana, nashukuruni sana, nadhani kule Wanyalukolo hawajambo. (Makofi)

Halafu nina wageni wanane (8) wa Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI Ofisi ya Waziri Mkuu ambao wako Mkoani Dodoma kwa ajili ya kuliombea Taifa, wanaongozwa na Mama Grace Mwanri, sasa hapa Mama Grace Mwanri yuko wapi? Wageni wako wapi wasimame walipo, ahsante sana, tunashukuru sana.

Sasa Mama Grace Mwanri sasa hapa hatujui maana Waswahili wanatumia vibaya, ni Mrs. Mwanri au nani? Hapa tena maana yake ukisema Mama Mwanri siyo huyu, huyu ni Mke wa Mheshimiwa Mwanri.

46 Kwa hiyo tunashukuru ahsante sana. Tuna wageni wengine waliopo Bungeni kwa mafunzo. Hawa ni wanafunzi 120 kutoka shule ya msingi ya DMI ya Kimara Dar es Salaam, naomba wasimame walipo, hawa watoto wetu, ahsante sana, nashukuru mlikotoka safari ndefu, kwa hiyo, naamini mtajifunza vizuri hapa, ahsante sana.

Halafu tuna wanachama wa CCM 26 kutoka Tawi la Makangira Mkoa wa Dare es Salaam na Vikokotoni Zanzibar. Naomba msimame mliko, ahsante sana, karibuni sana. Tuna Viongozi wnne (4) wa Bendi ya muziki wa dansi ya Mashujaa kutoka Dar es Salaam na hawa wapo wapi? Wasimame hawa Viongozi okay ahsante sana. Bahati mbaya hamkuunganisha siku ambayo sisi tutafanya tafrija mje, lakini hamkuunganisha basi bahati yenu mbaya. (Makofi)

Tunao wanafunzi 15 wa shule ya sekondari ya Wilaya ya Kondoa na Chemba walioshinda mashindano ya essay writing wakiongozwa na mwalimu Mohamed Omar Mohamed. Hawa watoto walioshinda essay wako wapi? Ahsante sana, hongereni sana na tunakushukuru Mwalimu kwa kufanya vizuri. Mwendelee mkishinda mara ya kwanza, mnatakiwa mshinde mara nyingine isiwe tena wenzenu wanawapiku, ahsante sana.

Tuna Waheshimiwa Madiwani 11 kutoka Serengeti wakiongozwa na Mheshimiwa Zakaria Kisiroti, Waheshimiwa Madiwani hawa wa Serengeti wako wapi? Wako kule nyuma, ahsante Waheshimiwa Madiwani karibuni sana. Halafu tuna walimu saba (7)

47 wa shule ya msingi ya kutoka Hanang, hawa walimu wetu wa kutoka hananga wako wapi? Wasimame na wenyewe wako sehemu hii huku, karibuni sana. Ukumbi wetu unazoeleka sasa unakuwa kama hautoshi.

Tuna wanafunzi 70 na walimu watatu (3) kutoka kituo cha Mbulika Happy Watoto cha Arusha, wenyewe wako basement nadhani baadaye mchana watapata nafasi huku juu. Halafu tuna wanafunzi wengine 50 wa Chuo cha Afya kilichopo Mpwapwa na wao pia wako basement. Nadhani mchana watakuja huku juu. Halafu pia kuna wanafunzi 40 wanaotoka Chuo cha Hombolo Dodoma, wapo wapi hawa wanaotoka Hombolo? Nadhani pia nafasi huku itakuwa imekosekana wataingia mchana.

Waheshimiwa Wabunge, sasa shughuli za kazi. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii, Mheshimiwa Margaret Sitta, anaomba niwatangazie Wajumbe wa Kamati yake kwamba leo saa nane mchana kutakuwa na kikao cha Kamati kitakachofanyika ukumbi namba 219. Halafu napenda pia kuwatangazia kwamba kesho tutakuwa na semina katika ukumbi wa Msekwa Wabunge wote na semina hiyo itahusu maendeleo ya Shirika la Nyumba la Taifa na utekelezaji wa miradi mbalimbali.

Kwa hiyo, nategemea Waheshimiwa Wabunge mtapata nafasi ya kuweza kuhudhuria. Halafu taarifa nyingine nataka kuwaambieni Waheshimiwa Mbunge yeyote anaesafiri lazima aombe ruhusa kwa Spika, sio

48 mnasafiri tu halafu inatokea jambo mahali hatujui ukikuwa wapi.

Kwa hiyo, naomba kabisa, maana naambiwa kuna Wabunge wengine wanatakiwa kwenda sijui wapi. Kwa hiyo, kila Mbunge anaeondoka na nikisema Mbunge ni pamoja na Mawaziri, Mawaziri wenyewe wataomba ruhusa mara mbili, wataniomba mimi na Waziri Mkuu. Kwa hiyo, asiondoke mtu hapa bila kuomba ruhusa na wale ambao wanakusudia kwenda sijui habari za michezo naomba leo msiondoke, muondoke kesho asubuhi.(Kicheko/Makofi)

Msiondoke leo kwa sababu ninayo sababu. Kwa sababu mkiondoka leo, tutashindwa kupitisha Wizara ya Ujenzi, hata kama huwa mnatokatoka katikati, lakini wakati wa maamuzi lazima nusu ya Wabunge wawepo hapa ndani. Kwa hiyo, msipokuwepo hapa tunawarudia huku nyuma mpaka tutajua nani hayupo. Kwa hiyo, mnakwenda kesho sio leo, kwa sababu idadi yenu inaonekana ni kubwa.

Wale Madiwani wa kutoka Jimbo la Njombe Magharibi kwa Mheshimiwa Naibu Waziri wa Ujenzi, wanaongonzwa na Mheshimiwa Nyagawa ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Halmashauri ya Wilaya ya Njome. Jimbo la Magharibi sasa ni Wilaya kamili ya Wangin’gombe, Mheshimiwa yuko wapi? Oka, ahsante sana. (Makofi)

Halafu nina Mheshimiwa Buyogera yeye ni Kamishna, leo amemkaribisha Mr. Buyogera na watoto, wako wapi? Ahsante sana. Hawa wageni wa

49 Kamishna wanakaa sehemu ile pale, wanakaa kwenye sehemu ya Spika ndiyo utaratibu. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na kazi. Katibu tuendelee.

MBUNGE FULANI: Mwongozo wa Spika.

HOJA ZA SERIKALI

Makadirio ya Matumizi ya Serikali Kwa Mwaka 2012/2013 - Wizara ya Ujenzi

(Majadiliano yanaendelea)

SPIKA: Ahsante. Waheshimiwa jana nimewatangazia wale ambao ningependa leo wazungumze. Naomba mpunguze sauti za kuongea ndani ya ukumbi wa Bunge. Tuliwataja ambao watabidi waongee leo na ni kusudio letu kwamba Naibu Waziri aweze pia kuzungumza kipindi hiki cha asubuhi, halafu mchana tukija, Waziri anaehusika aweze kuanza kujibu hoja na ikiwezekana sana tutoe muda mwingi kwenye Kamati ya Matumizi kwa sababu inakuwa kila mara, najua tu wote mtasimama kuchukua mshahara wa Waziri. Lakini ndiyo hivyo tujitahidi kidogo. Kwa hiyo, nilimwita jana Mheshimiwa Modestus Dickson Kilufu, Mheshimiwa Peter Joseph Serukamba halafu Mheshimiwa Freeman Mbowe, halafu atafuata na Mheshimiwa Mchungaji Msigwa na Mheshimiwa Mhonga Saidi Ruhanywa ataongea. Kwa hiyo, Mheshimiwa Kilufi.

MHE. MODESTUS D. KILUFI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

50

SPIKA: Mheshimiwa Suleiman nini? Naomba kidogo Mheshimiwa Kilufi u tulie.

MWONGOZO WA SPIKA

MHE. SULEIMAN M. N. SULEIMAN: Mheshimiwa Spika, kwa kutumia Kanuni ya 47(3): “Hoja itatolewa na Mbunge kwa kusimama mahali pake na kuomba idhini ya Spika kutoa hoja ya kuahirisha shughuli za Bunge kwa madhumuni ya kujadili jambo halisi la dharula na muhimu kwa Umma.”

Kuna Watanzania milioni 16 waliojiajiri kwa zao la pamba na Watanzania hawa, milioni 16 hivi sasa hawajui wafanye nini juu ya soko lao la zao la pamba. Bei iliyotolewa ni 660 na kwa ruhusa yako naomba nitoe mchaganuo mdogo sana wa kuonyesha.

SPIKA: Hata, dakika tano. Eleza tu hoja yako, mchanganuo haujafika.

MHE. SULEIMAN M. N. SULEIMAN: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa bei hiyo ya 660 kwa kilo moja ya pamba haitaweza kuwalipa jasho lao wakulima, naomba sasa Bunge lako Tukufu lijadili suala hili ili wakulima wa pamba milioni 16 waweze kunufaika na jasho la mavuno ya pamba. Waheshimiwa Wabunge naomba kutoa hoja.

SPIKA: Ungeisoma vizuri ile Kanuni, ingekuambia vizuri. Sasa wewe umesoma nusu ile Kanuni. Kanuni anayosema ya 47 ni Kuhairisha shughuli za Bunge ili

51 kujadili jambo la dharura, sasa neno jambo la dharura sio tunahairisha ili kusudi kujadili, hapana. Halafu jambo lenyewe unapewa dakika tano kueleza halafu Spika ataamua. Swali la bei za pamba haliwezekani kuwa la dharura toka tunaingia kikao hiki mnaongelea habari hiyo hiyo. Kwa hiyo hairuhusiwi tutumie muda wetu vibaya. Kwa hiyo, tunaendelea Mheshimiwa Kilufi endelea.

MHE. MODESTUS D. KILUFI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya wananchi wa Mbarali, naomba na mimi nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, kwa kazi nzuri anazozifanya hasa katika kusimamia miundombinu ya barabara. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, itakuwa si busara sana kupongeza kwa usimamizi mzuri ambao Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi anaufanya. Nishukuru vilevile barabara ya Rujewa Madibira Mafinga yenye urefu wa kilomita 152 na yenyewe imeangaliwa, lakini vilevile nikumbuke nimpongeze kwa kuiweka barabara ya Ilongo Usangu na yenyewe iko kwenye mpango pamoja na Igawa – Rujewa – Ubaruku na yenyewe imekumbukwa.

Lakini vilevile nishukuru kwa barabara za Igurusi, Utengule na Majombe – Madibira na zenyewe zimeangaliwa. Suala la barabara ni muhimu sana kwa maendeleo. Wilaya ya Mbarali ni miongoni mwa wilaya ambayo inazalisha sana zao la Mpunga. Lakini kwa bahati mbaya sana barabara zake siyo nzuri, namshukuru Mwenyezi Mungu tumepitiwa na barabara kuu ya kutoka Dar es Salaam kwenda Zambia. Vinginevyo sisi lami tungekuwa tunaisikia.

52

Pamoja na mazuri mengi ambayo Mheshimiwa Waziri amekuwa akiyafanya, lakini nilikuwa namwomba kwa dhati kabisa kwa niaba ya wananchi wa Mbarali hebu ajaribu kuiangalia na Mbarali. Mimi ile Barabara Kuu siihesabii sana naangalia Mbarali mtandao wake wa barabara siyo mzuri.

Kwa mfano barabara ndogo inayotoka Igawa kwenda Ubaruku, barabara ambayo ni mashuhuri sana kwa kusafirisha mchele ambao unakobolewa kwenye vinu vya mpunga pale Mbarali. Barabara hii imeleta matatizo makubwa sana mwaka uliopita kwa sababu ya magari makubwa yanayobeba mchele kupeleka Dar es Salaam na maeneo mengine kutokukubalika kupita kwa kiwango kwamba ile barabara haina kiwango cha kupitisha magari mazito kama yale. Ikaleta mgogoro mkubwa sana. (Makofi)

Sasa, hivi kwa fedha hizi alizotenga sina uhakika kama zitaweza kukamilisha barabara ile kwa sababu zimebakia kilomita kama kumi kufika kule Mbarali. Lakini fedha zilizotengwa kwa kiwango cha lami nyepesi ni milioni 150 kwa gharama za ujenzi wa barabara sina uhakika kama hizi fedha zinaweza zikatosheleza.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Rujewa Madibira, imekuwa ikizungumzwa toka mwaka 2000, lakini mwaka jana Bajeti iliyopita niliambiwa kwamba wataanza na madaraja, madaraja hayakuanzwa kujengwa. Sasa hivi imetengewa, mimi nimeona hata Kiswahili kilichotumika hapa kama sina imani nacho

53 sana shilingi bilioni sifuri mia nane sabini na tisa sasa hata kutamka bilioni mimi naona hakukuwa na sababu. Kwa sababu barabara yenye urefu wa kilomita 152 inamaana hata mwaka huu bado hakuna uwezekano wa kuanza kujenga kiwango cha lami inawezekana hata sasa hivi ikawa bado ni suala la madaraja ambalo mwaka jana yalitengewa Bajeti lakini kazi hiyo haikufanyika. Sasa nataka nipate majibu ya kuridhisha ni lini itajengwa kwa kiwango cha lami hii barabara, itajengwa kwa sababu ni muda mrefu imekuwa ikiahidiwa kwamba itajengwa, itajengwa inazidi kwenda toka mwaka 2000. Kama sitapata majibu kwa kweli sitaunga mkono hoja hii, Bajeti ya Mheshimiwa Waziri kwa sababu nitakuwa nawafanyia mzaha wananchi wa Mbarali ambao wanapata ahadi kila mwaka, kila mwaka, lakini utekelezaji hakuna.

Mheshimiwa Spika, Mbarali ina maeneo mengi yanayohitaji barabara lakini yaliyoainishwa ni haya machache niliyotaja kwa mfano barabara ya Igurusi – Utengule. Hii barabara imekuwa ikisumbua sana hasa wakati wa mvua nilikuwa naomba barabara hii iangaliwe vizuri zaidi kwa sababu ni nyembamba sana kwa magari kupishana na kule kuna uzalishaji mkubwa wa mazao mengi. Lakini barabara ile kupishana magari mawili inakuwa ni tabu sana na maeneo yale ambayo kuna maji pamekuwa na usumbufu mkubwa sana hasa ukiangalia wembamba wa hizi barabara.

Mheshimiwa Spika, tuna barabara nyingi ambazo zinahitaji kutengenezwa kwa ajili ya kusaidia wakulima kuweza kutoa mazao mashambani. Najua barabara hizi nyingine ziko chini ya Halmashauri. Kwa mfano

54 barabara ya kutoka Maniyenga Kangaga, barabara ya kutoka Manienga Ipwani Iuwango, barabara ya kwenda Kata ya Ruiwa na yenyewe bado si nzuri sana inahitaji kuimarishwa. Barabara ya kwenda Mwatengwa na barabara kuu kwenda Ukwavila kupitia Uturo na yenyewe bado si nzuri sana japo kwenye Bajeti hii sijaiona kama imeingizwa.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nilikuwa naomba barabara ni mkombozi kwa maendeleo ya Tanzania naomba kwa dhati kabisa barabara ambayo nategemea walau kwa kiwango cha lami nyepesi kuingia wilayani Mbarali ni hii ya kutoka Rujewa Igawa, hii barabara ya Rujewa Madibira na yenyewe naomba nipate majibu ni lini itaanza kujengwa kwa kiwango cha lam, i kwa sababu fedha zilizotengwa siamini kama zinaweza kutosha kujenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, nikipata majibu hayo mimi nitakuwa tayari kuunga mkono Bajeti ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi. Lakini nizungumze kitu kingine, ukipita nchi nzima utakuta nyumba zimewekwa X, X, X na kwangu Mbarali ni hivyo hivyo.

Sasa matokeo yake Mheshimiwa Waziri anatamka anasema waliowekewa alama za X maana yake wako eneo la barabara na kwamba waondoke wenyewe na kama hawaondoki hawatalipwa na Serikali itakapoanza kubomoa na ameagiza zibomolewe hizo nyumba. Lakini nataka nijue hivi Mheshimiwa Waziri nyumba hizo zilipokuwa zinajengwa wataalam wa barabara hawakuwepo? Kwa sababu kama

55 walikuwepo walichukua hatua gani, walingoja mpaka Watanzania hawa wapate tabu wabomolewe nyumba zao. Kwa hilo mimi siungi mkono kabisa kubomoa nyumba za watu hawa bila kuwalipa fidia, itakuwa ni kuwaonea kabisa na mwingine ukimbomolea nyumba ile au akibomoa hana uwezo wa kujenga nyumba nyingine ataishi wapi?

Kwa hiyo, nilikuwa nashauri kwa busara kabisa zitumike. Mheshimiwa anafanya kazi nzuri sana lakini katika hili kwa kweli atakuwa hajawatendea haki Watanzania. Tunakubaliana kwamba kweli barabara zitengenezwe na watu wapishe, lakini siyo wapishe kwa kuondoka bila kulipwa chochote.

Kwa kweli jambo hili naomba liangaliwe kwa umakini ni kweli Mheshimiwa ana nguvu sana ya kutoa amri kwamba watu watoke, lakini tutakuwa hatujawatendea haki Watanzania. Kwa sababu si kwamba walikuwa wanajenga hii Wizara, ilikuwepo na walikuwa wanaona watu wanajenga na inawezekana sheria hii ya kuongeza eneo la barabara imekuja wakati wao wameshajenga tayari. Sasa unawaadhibu kwa kosa gani?

Mimi naomba jambo hili liangaliwe kwa umakini hatupingi, kuongeza kupanua barabara na wananchi hawakatai lakini kumwambia mtu aondoke hivi hivi kwa kutumia sheria itakuwa pengine ni matumizi mabaya ya hiyo sheria. Kwa hiyo, hilo naomba watu wote waliowekewa X waangaliwe wasitolewe hivi hivi tutakuwa tunatengeneza dhambi ambayo baadaye itatuhukumu wenyewe.

56

Mheshimiwa Spika, tunazo barabara zinazokwenda kwenye maeneo ya uzalishaji kama nilivyosema mwanzoni, kama barabara ya kutoka Ubaruku kwenda Mahongole, Mwanawala kwenda Mnazi Mashambani. Hizi barabara inawezekana ziko chini ya Halmashauri lakini Halmashauri kama Halmashauri haina uwezo wa kugharamia barabara hizi. Kwa hiyo, naomba vilevile kwa siku zinazokuja ni kuona tunawatia moyo Watanzania wanaojituma kuzalisha chakula; basi hata barabara zao zikumbukwe. (Makofi)

SPIKA: Haya ahsante umemaliza vizuri.

MHE. MODESTUS D. KILUFI: Nashukuru sana Mheshimiwa Spika kwa kunipa muda huu.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, na mimi nikushukuru kwa kunipa nafasi niweze kuchangia Bajeti ya Wizara ya Ujenzi. Kwanza nianze kwa kuishukuru Serikali kwamba kuna watu wamesema Kigoma hamna kilichofanyika hapana, Kigoma kazi iliyofanyika ni kubwa sana. (Makofi)

Kwa sababu toka awamu ya nne imeanza ni kilomita nyingi za lami zimejengwa mkoani Kigoma na kwa hili naomba nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi na tumwombe aendelee kutusaidia ili tuweze kufanya kazi mkoani Kigoma. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Kigoma tumejenga barabara kilomita 60 Mwandiga Manyovu, tumejenga kilomita

57 30, kutoka Kigoma mpaka Kidahwe na sasa hivi kuna mkandarasi anajenga kilomita 76 kutoka Kidahwe kuja Malagarasi. Kwa hiyo kwa namna yoyote ile lazima tuishukuru Serikali kwa kazi kubwa inayofanyika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pili iko habari ya barabara ya kutoka Nakanyazi kwenda Kidahwe mimi najua Serikali inalifanyia kazi jambo hili ni kweli mwaka jana pesa zilitengwa hazikupatikana zote kwa sababu ambazo wote tunazijua.

SPIKA: Mheshimiwa utangaze nafasi yako wewe ni Mwenyekiti, maana una-pre-v knowledge.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mimi ni Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, kwa hiyo yanayofanyika mengi nayajua.

SPIKA: Haya basi endelea.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Kwa hiyo, nilitaka kusema na watu wa Kigoma wasije wakadhani kwamba mambo hayaendi, mambo yanafanyika na naamini barabara hizi zitajengwa. Nachokiomba tu Mheshimiwa Waziri tunalo tatizo pale, tumejengewa barabara ya Kigoma kuja Kidahwe barabara ile ina taa za barabarani, ningeomba zile taa za barabarani sasa kwa sababu zimeshajengwa hazitumiki zingehamishiwa TANROADS ili zile taa ziweze kuwaka.

Pili, tungeomba pale round about ya Mwandiga na pale Kigoma Mwanga, pawe na round about

58 tukipata round about kwa sababu ajali ni nyingi sana kwenye maeneo hayo.

SPIKA: Mheshimiwa Chambiri naomba urudi ulikotoka, rudi ulikotoka huku. Haya endelea Mheshimiwa Serukamba I m sorry.

MHE. PETER J. SERUKAMBA: Mheshimiwa Spika, nilikuwa naomba tupatiwe hizo round about hayo mawili pale Mwanga pamoja na Mwandiga ajali ni nyingi sana na kwa sababu barabara ni nzuri watu wanakimbiza sana magari, hivyo wanakutana ghafla, tunapoteza watu wengi sana. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mimi leo nilitaka nichangie jambo moja na kwa kweli hili siyo wala la Wizara ya Ujenzi ni suala la Serikali, ukisoma kitabu cha Wizara ya Ujenzi , unaona nia njema ya kufanya nchi hii iwe na barabara maeneo yote. Ni kilomita nyingi sana ambazo zitajengwa mwaka huu.

Lakini ukiangalia kwenye Bajeti unaona pesa iliyotengwa kwa kweli hizi barabara zitajengwa siyo kama ambavyo tumepanga tatizo la kujenga halipo Wizara inafanya kazi nzuri sana lakini tatizo ni fedha. Kwa hiyo nilitaka niombe Wabunge na niombe Serikali tufanye maamuzi tutafute pesa tukope kwenye mabenki ili tuweze kutengeneza barabara hizi.

Mheshimiwa Spika, kwa sababu tusipokopa pesa nyingi na wenzetu wamefanya Kenya walianzisha special fund kwa ajili ya kujenga mabarabara waka-

59 issue bonds infrastructure bond kwa ajili ya kujenga barabara. Juzi wenzetu wa Angola wamechukua dola bilioni tatu kwa ajili ya kujenga barabara na reli ni maamuzi yalifanyika makubwa lakini tukienda kibajeti tutakuwa tunalamika kila mwaka.

Mimi ningeomba sasa wenzetu wa Wizara ya Fedha waliangalie jambo hili kwa sababu kwenye mpango wetu tumesema infrastructure ndiyo jambo la kwanza katika maendeleo. Kwa hiyo ni lazima tufanye maamuzi tukienda kibajeti muda huu tuliojipangia miaka mitano hatuwezi kuwa tumemaliza barabara hizi. Ukisoma kwenye kitabu chetu utaona kuna kilomita karibia 3000 ambazo zinatakiwa zijengwe angalau kwa miaka hii mitatu.

Ni kweli Waziri ameweka fedha lakini fedha hizi haziwezi kutosha kwa hiyo lazima tufanye maamuzi sisi hapa tuiombe Serikali watafute fedha tukope ili tuweze kujenga barabara hizi. Lakini tusipokopa tukaenda namna hii ya kibajeti tatizo letu bado litakuwa ni pale. Maana leo tunaingia kwenye Bajeti, tunapitisha Bajeti hii inaonekana kubwa lakini si kubwa ukiangalie zile fedha kwanza tuna deni karibia bilioni 150 ambayo maana yake Waziri anapoanza kazi anaanza kulipa deni, tukilipa deni analipa deni kutoka kwenye fedha hizi tulizozipitisha hatuwezi kwenda.

Kwa hiyo ningeomba sana Serikali jambo hili mkae mlitafakari twende kwenye mabenki tuchukue pesa tumalize hizi bank loan lakini pia tuweze kujenga barabara zetu na ndiyo ambavyo tutaweza kufanikiwa kama nchi. Otherwise tutaenda kidogo kidogo yes

60 tutafika lakini baada ya muda mrefu. Ningeomba niwaombe kabisa kabisa watu wa Serikali waamue tutafute pesa za ziada tuweze kujenga kama wenzetu walivyofanya naamini na sisi tunaweza.

Mheshimiwa Spika, la mwisho ni suala la mizani. Tumelisema sana kwenye Kamati yetu, ningeomba wenzetu watusaidie, ukiangalia jamani barabara zetu zimeharika sana. Sasa tujiulize tatizo liko kwenye mizani ama tatizo ni kwa sababu reli haifanyi kazi. Kwa hiyo mizigo mingi inabidi ipite kwa sababu tunajua tumejenga barabara nyingi sana lakini na rate ya kuharibika kutokana na mizigo mikubwa ni kubwa sana. (Makofi)

Angalia barabara hii ya kutoka Dodoma kuja Morogoro imemalizika juzi miaka minne iliyopita leo ukipita barabara ile kwa kweli unaanza kuiona imeanza kupata shida, tatizo ni reli haifanyi kazi, kama reli haifanyi kazi tunafanyaje, lazima tuamue sasa kutafuta pesa ili reli isaidie kubeba mizigo mingi.

Otherwise tukiendelea na kupitisha malori kwenye barabara hizi tutakuwa tunazijenga baada ya miaka miwili tunatarajia kuzifanyia rehabilitation matokeo yake zile barabara zingine zitachelewa kujengwa. Lazima tuamue kama Serikali ili tuweze kufanya kazi hii.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo naomba niunge mkono hoja ya Waziri wa Ujenzi. (Makofi)

61 MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kunipa nafasi na mimi kuchangia katika hoja ya ujenzi. Niungane na Mheshimiwa Serukamba, kwamba pamoja na nia njema sana ya Serikali ya kujenga mitandao ya barabara nchi nzima, sasa tufanye maamuzi kama Taifa tutafute fedha ili tujenge barabara.

Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna miradi mingi ya barabara inayoendelea lakini kwa bahati mbaya sana kwa kufuata mafungu yanayoweza kutengwa na Bunge lako Tukufu kwenye Bajeti, miradi hii inachukua muda mrefu kuliko ambavyo ingestahili kuchukua.

Matokeo yake ni kwamba faida ambayo ingepatikana kwa ujenzi wa barabara hizi zinatolewa na kwa maana hiyo ni vyema sasa tupange tutafute kama Taifa fedha kwa ajili ya kujenga barabara tuwa- engage ma-contractors wakati tuna uhakika tuna fedha ya kuwalipa ma-contractors ili ujenzi uweze kuwa wa haraka na wa kasi na wa viwango vinavyostahili. Kuchelewesha kuwalipa ma-contractors kwanza tunawafilisi ma-contractors kwanza tunawafilisi ma-contractor local na hata wale ambao ni international tunawakwaza. Vilevile hali kadhalika tunachelewa kupata benefit ya barabara ya kujenga mwaka mmoja inajengwa miaka minne na vilevile juu ya yote hayo tunapanua kwa kiwango kikubwa sana gharama za ujenzi wa barabara ambazo zingeweza kuthibitiwa na kuwa ndogo kama zingejengwa kwa wakati.

62 Mheshimiwa Spika, niondoke katika hilo nizungumzie barabara mbili za jimboni kwangu Hai. Namshukuru sana Mheshimiwa Waziri kwamba amefanya kazi nzuri na mtu akifanya kazi nzuri lazima tumpongeze. (Makofi)

Lakini niombe kuzungumzia barabara mbili kwanza nianze na barabara ya Kwa Sadala, Masama katika jimbo la Hai. Barabara ambayo ilikusudiwa kujengwa kwa kipindi cha mwaka mmoja kuanzia mwaka 2010 na kukamilika mwaka 2011.

Barabara hii imeanza tunaishukuru Serikali kwa kazi hiyo lakini sasa ni mwaka wa pili na siku za karibuni niliuliza swali kwa Naibu Waziri wa Ujenzi naye alinihakikishia kwamba barabara hii itakamilika Desemba, 2012 taarifa ambazo kwa kweli ni habari nzuri lakini nilivyoangalia makabrasha yangu ya bajeti sijaona fungu kubwa lililowekwa nimeona bajeti imewekwa shilingi milioni 150 katika ujenzi ambao ulikuwa hauna salio la shilingi kama bilioni nne. Nitaomba Mheshimiwa Waziri utusaidie hili wakati wa kujumisha hoja zako ili wale wananchi waweze kunufaika na barabara hii kama ambavyo Serikali ilikusudia.

Lakini nikumbushe tu kwamba barabara hii kwa bahati mbaya kutokana na msongamano mkubwa wa watu katika maeneo ya Masama barabara hii inabidi ijengwe wakati huo huo inaendelea kutumika na wananchi kwa sababu sehemu zake zote mbili za pembeni zimejaa makazi ya watu.

63 Kwa hiyo, kuchelewesha barabara hii kwa miaka mingi kwa kweli kunasababisha usumbufu mkubwa sana kwa wananchi. Kwa hiyo, ningeomba sana Mheshimiwa Waziri kwa sababu ni kweli ni barabara fupi ya kilomita kumi na mbili tu, uweze kuitolea tamko na mkakati maalum ili tuweze kuimaliza na kuondoa tatizo hili once and for law. Aidha, niombe tena kukumbusha Waheshimiwa Mawaziri ahadi yenu ambayo mlitoa hapa Bungeni siku za karibuni kwamba tungetembelea barabara kuweza kuangalia matatizo yaliyopo ikiwemo fidia kwa baadhi ya wananchi ambao wanadai kwamba fidia haikufuata viwango ambavyo havistahili ili tupate ufumbuzi wa moja kwa moja wa kudumu.

Barabara ya pili ambayo iko chini ya TANROADS katika jimbo langu la Hai, ni barabara inayotoka Kilimanjaro Machine Tools kwenda mpaka Machame Gate ambayo ndiyo inayoongoza kwa kuingiza watalii katika mbuga ya Mlima Kilimanjaro. Wote tunajua kwamba mbuga hii ya Kilimanjaro National Park inachangia zaidi ya bilioni 80 kwa mwaka na hii ni njia muhimu sana ya kuwafikisha watalii katika mlima ule. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, barabara hii ilijenga Katika mid sixteen ni 1965 yaani barabara ambayo ina umri zaidi ya miaka 40. Lakini tangu ilivyojengwa kipindi kile barabara hii imekuwa inafanyiwa matengenezo madogo madogo ya mara kwa mara na ni kweli kutokana na kuongeza kwa idadi kubwa ya watu, matumizi makubwa ya kiuchumi katika barabara hii matumizi makubwa ya magari ni lazima sasa barabara

64 hii iweze kupanuliwa kuweza kukidhi mahitaji ya sasa hivi ya matumizi yake.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naomba sana Wizara ifikirie uwezekano wa kuipanua barabara hiyo kujenga sehemu za watumiaji kwa miguu katika barabara hii, vile vile kutenga maegesho ya magari kwa sababu barabara hii inahudumia wananchi ambao ni wengi sana na vile vile kuweza kurekebisha maeneo kadha wa kadha yenye kona kali ambayo kutokana na milima na miteremko inaweza ikasababisha ajali za mara kwa mara.

Mheshimiwa Spika, nina hakika Mheshimiwa Waziri ataweza kutupa taarifa nzuri kwa sababu naona katika mwaka huu wa fedha ametutengea milioni 300 kwa ajili ya maintenance ya kilomita mbili za barabara hii, lakini nina hakika anaweza akafanya la ziada, hata kama siyo katika mwaka wa fedha huu basi katika mwaka wa fedha ujao iwe katika mpango ambao unaweza kuirekebisha barabara hii ambayo ni ya muhimu sana kwa uchumi wa Mkoa wa Kilimanjaro.

Mheshimiwa Spika, nizungumzie msongamano wa magari Dar es Salaam, naishukuru Serikali ina mipango mingi kwa kweli ya muda wa kati ya kuzuia tatizo la msongamano wa Dar es Salaam. Lakini naomba nishauri mambo saba ambayo yakifanyika tunaweza tuka-improve flow ya magari katika Jiji la Dar es Salaam kwa kiwango kikubwa kwa kutumia fedha kidogo wakati mipango mikubwa ya Serikali inatekelezwa. Ni dhahiri kwamba tatizo kubwa la traffic katika Jiji la Dar

65 es Salaam ni CBD (Central Business District) ya Dar es Salaam yenyewe.

Mheshimiwa Spika, kama hatukutengeneza miundombinu ya CBD ya Dar es Salaam flow ya magari ndani ya Jiji na kutoka nje ya mji ikawa smooth hakika bado msongamano wa magari utakuwa mkubwa. Kwa hiyo, lazima tuanzishe kitu kinachoitwa CBD Management ambapo tunakuwa na udhibiti wa magari yanayoingia na kutoka katika CBD ya Dar es Salaam. Wenzetu wa London walifanya jambo hili, baada ya Jiji la London kuwa limezidiwa na flow ya magari kuingia central London, walianzisha utaratibu huu ambapo magari yote yaliyokuwa yanaingia Central London yalikuwa yanalipiwa fees maalum wakaweza kukusanya fedha nyingi sana zikaboresha miundombinu ya Jiji la London.

Mheshimiwa Spika, naiomba Wizara na Serikali iangalie uwezekano huu wa kuanzisha utaratibu huu ambapo magari yote yanayoingia katika muda wa kazi katika maeneo ya Jiji la Dar es Salaam katikati ya jiji CBD (Central Business District) yaweze kulipa fee maalum ambayo itasaidia kukarabati na kupanua miundombinu ya Jiji la Dar es Salaam.

Pili, barabara ya Jiji la Dar es Salaam katika CBD imejaa mashimo na port holes hizi zinasababisha magari kutembea kwa muda mdogo sana yaani kwa mwendo mdogo na kwa mwendo huu mdogo zinafanya magari yanazidi kujazana na kusongamana. Niiombe Serikali iangalie uwezo wa kuli-surface yaani ya kuweka lami katika barabara zote za CBD Dar es

66 Saalam, maana yake nyingi zimeachwa kwa muda mrefu kwa miaka mitano barabara za CBD Dar es Salaam zina mashimo na hazijawahi kufanyiwa maintenance. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kingine nilichokuwa nataka nikizungumzie kuhusu CBD, nishauri turekebishe utaratibu wa parking za Dar es Salaam, parking za Dar es Salaam magari yanapaki kwenye pedestrian walk ways, magari yanapaki sehemu za waendao kwa miguu, waendao kwa miguu wanapita katikati ya barabara wanachelewesha magari. Sasa tuweke utaratibu ambapo magari yatakuwa yanapakiwa kwa utaratibu unaoeleweka, walk way za wananchi ziachwe ziwe huru na zijengwe wananchi wapite kwenye maeneo yao magari yapaki vizuri, barabara ziwe resurface, nina hakika flow ya traffic itakuwa nzuri itaondoa kwa kiwango kikubwa sana msongamano wa magari. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tuheshimu sana sehemu za watembea kwa miguu katika barabara ya Jiji za Dar es Salaam. Hili ni tatizo kubwa na linasababisha ajali nyingi ambazo hazina sababu. Tupanue barabara za Jiji la Dar es Salaam katika junction, katika junction barabara nyingi unakuta kuna barabara moja ama mbili, tunaweza tukapanua pale kwenye junction kwa muda mfupi tu tukawa na line sita kwa utaratibu huo tutafanya flow ya magari iwe rahisi sana. Tuanzishe overhead bridges katika maeneo mengine ya kuvuka. Katika barabara ya Morogoro Road kuna bridge moja ambayo iko manzese. Tunaweza tukaanzisha bridge za kuvuka ng’ambo ya pili ya barabara katika maeneo

67 mengine ya Dar es Salaam watu wakaacha kukatisha katikati na magari yaka-flow kwa kasi. (Makofi) Au tunaweza tukaanzisha kitu kinaitwa underpass kwamba kunakuwa na daraja la chini ya barabara watu wanatokea upande wa pili, utaratibu wa kuweka matuta panapokuwa pana raia na magari utaratibu umepitwa na muda. Ningeomba Serikali iangalie namna ya kulifanya hili. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, la mwisho, katika kuwawezesha Wakandarasi ambao ni Watanzania, hatuwezi kujenga uchumi wetu kwa kutegemea Wakandarasi kutoka nchi za nje, ni lazima tuwezeshe wazawa na lazima tuwe na mipango ya makusudi ya kuwawezesha wazawa. Kama tunatoa kandarasi kwa Wakandarasi wa nje, hatuoni sababu ya kutokuweka sheria ambayo ni ya lazima kwamba mikataba yote mikubwa hata kama wazawa hawawezi basi angalau wapewe kati ya asilimia 20 na thelathini ya miradi hii ili tuweze kupata ulinzi katika nchi yetu. Asilimia 95 ya miradi mikubwa ya ujenzi wa barabara sasa unafanywa na makampuni ya nje na hawa wote wana externalize mapato yote wanayopata. Tuwasaidie Watanzania kuwajengea nafasi za kisheria kwa sababu hii ni nchi yao na hawa ndiyo watakaojenga nchi yao, hatuwezi kutegemea wenzetu wa China ambao wameshaendelea watusaidie kurekebisha uchumi wetu bila sisi wenyewe kujitegemea. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nakushukuru. Bahati mbaya muda ni mdogo sana. Nakutakia kazi njema. (Makofi)

68 SPIKA: Ahsante sana kwa mchango mzuri. Sasa nitamwita Mchungaji Peter Msigwa, atafuatiwa na Mheshimiwa Mhonga Ruhwanya ambaye pia atafuatiwa na Mheshimiwa .

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Spika, nikushukuru kwa kunipa nafasi hii ili niweze kuchangia kidogo katika Wizara hii ya ujenzi. Kwanza kabisa nimshukuru Mheshimiwa Magufuli kwa kazi nzuri japokuwa yupo upande siyo sahihi sana kwa jinsi anavyofanya kazi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumwomba kwamba, barabara ya kutoka Manispaa ya Iringa kwenda uwanja wa National Park Ruaha, nashukuru kwamba kuna upembuzi yakinifu unafanyika kwa sababu barabara ilikuwa inajengwa kilomita moja kwa mwaka ambayo karibu sisi wote tungekuwa tumekufa ndiyo hizo kilomita 80 zingekwisha, lakini sasa wamesimamisha wanafanya upembuzi yakinifu. Kwa hiyo, naomba baada ya upembuzi huu, ile kasi isiwe tena ya kujenga kilomita moja moja kila mwaka. Naomba ijengwe kwa kasi sana kwa sababu ile barabara ikijengwa italeta kipato kikubwa katika Manispaa ya Iringa, ikizingatiwa Mheshimiwa Magufuli umesoma Mkwawa, itakuwa ni fadhila zako kwa Mkwawa pale.

Mheshimiwa Spika, vilevile nimuombe Mheshimiwa Waziri wakati wa majumuhisho yake katika Jimbo langu kuna wakazi wa Kihesa, Kilolo, TANROADS kuna watu wengine waliwalipa fidia wengine hawakuwalipa. Kwa hiyo, imekuwa ni kero sana, sasa nataka nijue ni vigezo

69 gani vilitumika kuwalipa watu wa sehemu moja wengine hawajalipwa? Kwa hiyo, mimi kama Mbunge nimekuwa nikisumbuliwa na wananchi na wanataka nirudi na majibu hayo. Naomba Mheshimiwa hili tatizo lifahamike ni namna gani mlifanya upembuzi huo.

Mheshimiwa Spika, lakini vile vile ningeomba Wakandarasi wanaojenga barabara hii ya kutoka Iringa na Dodoma, kwa sababu barabara hii ikifunguka ni ya muhimu aliyeanzia Iringa anakwenda kwa kasi sana, lakini anayetokea huku Dodoma naona kasi ile haiendi sana, sielewi kuna tatizo gani naomba nipate ufafanuzi.

Mheshimiwa Spika, lakini jambo lingine ambalo ningependa nizungumze ni kuhusu msongamano wa magari ambao wachangiaji wawili waliopita pamoja na Kiongozi wa Kambi ya Upinzani wamezungumza na wametoa suluhisho labda la muda mfupi, lakini nataka nijikite kwenye suluhisho la muda mrefu. Mwezi wa pili au mwaka jana wakati nachangia kwenye bajeti ya Uchukuzi niliwahi kutoa baadhi ya vifungu au nilitoa quotation za hotuba ya Peak Bother ya mwaka 1985, watu wengine hawakunielewa walianza kunishambulia.

Mheshimiwa Spika, lakini naomba nirudie baadhi ya mistari nijenge hoja ili mpate kunielewa. Yule bwana katika moja ya misemo yake alisema kwamba Pretoria unayoiona imejengwa kwa akili ya Kizungu na anasema South Africa unayoiona leo imejengwa kwa gharama za akili, it was build at the expense of intelligent. Alisema hivyo kwa kutudharau watu weusi

70 na maneno haya yatabaki kuwa kweli unless we prove kwamba we are intelligent katika mambo yetu tunayoyafanya.

Mheshimiwa Spika, nasema hivyo kwa sababu tunapoiona Dar es Salaam, tunapoona msongamano wa magari, tunapoona system za maji zinapokuwa tabu, nyumba zimejengwa hovyo, ni kiwango cha akili kilichotumika kujenga ule mji. Sasa ili tutoke kwenye matatizo yale ni lazima kiwango cha akili cha juu zaidi kifanye upembuzi wa kutosha ili tutoke na si kwa masuluhisho ya zima moto. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Magufuli ni mmoja wa Mawaziri ambao nawaheshimu sana na nitaendelea kumheshimu kwa sababu anachapa kazi, ana uwezo wake binafsi. Lakini mipango mitatu mliyoweka ya kujenga daraja, ile mitatu naiona ni temporary solution, hatuwezi kutokana na matatizo ya Jiji la Dar es Salaam. Jiji la Dar es Salaam ni kitovu kikubwa cha uchumi wa Tanzania, ni lazima akili kubwa itumike kutatua matatizo yaliyopo Dar es Salaam. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, mfano mzuri tuangalie Beijing, China wakati wa michezo ya Olympic, sitaki niende sana huku uangalie jinsi Wachina walivyofanya. Tatizo la Dar es Salaam ni lazima tutoe majibu yanayolingana na matatizo yale. Tuna hiyari kama Chama cha Mapinduzi aidha, tuiache Dar es Salaam kama ilivyo, ilivyokaa shaghalabaghala vile au tuamue kujenga mji mwingine mbali wa kisasa au vinginevyo ushauri wangu ninaoipa Serikali tuamue kutafuta makazi mbali

71 kabisa, Serikali iwe na mpango wa muda mrefu wa kujenga nyuma na kuwahamisha wakazi Dar es Salaam ili tujenge barabara za kutosha kama miji mingine duniani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nasema hivyo kwa sababu Mawaziri wa Tanzania mnasafiri sana, mmeona Majiji kama Johansburg. Mnakwenda sana Marekani, mnakwenda Ulaya, huwa hatujifunzi tukaona miji mingine? Huwezi kusema Dar es Salaam utatatua msongamano kwa kujenga Daraja la Kigamboni, haiwezekani. Ili tujenge hizo flyovers nyingi ni lazima watu wengi wahame na kuwahamisha watu wengi lazima tuwe na mpango wa muda mrefu kwamba tutajenga nyumba kama walivyofanya Beijing.

Mheshimiwa Spika, wao walitafuta eneo wakawajengea watu nyumba wakawahamisha, ni maamuzi magumu ambayo yanaathari lakini ni tiba ya muda mrefu. Lakini tupo kwenye dilemma kama Serikali saa zingine tunafanya maamuzi kwa sababu tunalenga kura, tunataka Serikali ibaki madarakani, lakini matatizo ni makubwa ambayo tunapata kama Taifa. Jiji la Dar es Salaam tunapoteza pesa nyingi sana kwa sababu ya msongamano. Tukirudi hapa tunakaa tunasifia Majiji ya watu wengine, kwamba wamejenga, lakini uwezo huo tunao. Nikuombe Mheshimiwa Waziri mpango wa muda mrefu ni lazima tutoe tiba, hatuwezi kunywa panado wakati tuna matatizo ya malaria. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kutibu malaria lazima upate dozi inayohusika. Matatizo ya Dar es Salaam usije na

72 temporary solution. Hii aliyokuja nayo Mheshimiwa Waziri ni temporary solution, angalia kwa mfano barabara ya Mwenge, tayari saa hizi imeshajaa. Hii njia mnayosema iendayo kasi baada ya wiki mbili itajaa, hakuna cha kasi hapa, msongamano utaendelea kwa sababu ita-encourage watu kununua magari hatuna solution ya kutosha. Kwa hiyo niwaombe kama Serikali tuwe na mpango wa muda mrefu ambao utasaidia kupunguza msongamano wa magari.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo ningependa nizungumzie ni kuhusu alama za barabarani, ambalo nimezungumza sana, lakini naona bado halifanyiwi kazi. Kwanza nikushukuru kwa barabara ya kutoka Morogoro kuingia Iringa Mjini, ni barabara nzuri inapendeza, lakini vibao vya barabarani Tanzania hatuna maximum speed limit, alama za barabarani za speed mfano, unazikuta tu kwenye kijiji unachofika, ndiyo unakuta speed 50. imagine kama ulikuwa unakwenda speed ya gari mia ghafla unakuta imeandikwa 50 na traffic walivyo wajanja anakaa hapo hapo mita chache.

Mheshimiwa Spika, haiwezekani ulikuwa 100 unaikuta 50, ukasimama hapo hapo utasababisha ajali. Barabara zote za kisasa mmetembea sehemu nyingi mmekwenda huko Afrika Kusini na Ulaya. Kama kwa mfano, South Africa, maximum speed limit ni 120, unapo-approach kupunguza unakuwa 120, inakuja 100, inakuja 80 mpaka unapita mahali ambapo unatakiwa upunguze hiyo speed. Hii haihitaji elimu ya Chuo Kikuu kuweka alama barabarani. Naomba

73 Mheshimiwa Magufuli hilo lizingatiwe ili tuwe na maximum speed limit kupunguza matatizo ya ajali barabarani.

Mheshimiwa Spika, lingine ambalo Kiongozi wa Kambi ya Upinzani amelizungumza ambalo nalo kweli litapunguza matatizo ni hizi njia za kupita. Ukienda miji mingi kupita juu ya barabara na kupita chini ni kawaida kabisa, zinapunguza misongamano na siyo Dar es Salaam hata maeneo mengine kama Mwanza tuwe na plan za namna hiyo ili kuondoa misongamano ambayo haina sababu. Narudia kusema ile speech ya Bother ambayo alisema; A black man can not plan his life beyond a year. Kama hatuwezi kujipanga vizuri itasimama kwamba ni kweli unless we prove otherwise kwamba tuna uwezo wa kupanga, tuna uwezo wa ku- plan long term plan ili tuonekane kwamba yule mzungu alikuwa anatudanganya. Lakini kama tunaendelea kuwa na mipango ya muda mfupi, hatujipangi vizuri, ile speech inaendelea kuwa ni ukweli. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, niwaombe mliopewa dhamana tusimame tuoneshe kwamba sisi siyo inferior kupita wazungu. Juzi nilikuwa St. Peters, ule mji umejengwa karne ya kumi na saba, ukiangalia mji ulivyojengwa wale watu wanaonekana walikuwa na akili kuliko sisi. Naomba Mheshimiwa Waziri uyazingatie haya.

SPIKA: Ahsante sana, Mchungaji unataka kusema Mungu aliumba wengine wana akili, wengine hawana. Naomba ukae chini kwanza utaitwa. Mheshimiwa

74 Muhonga Said Ruhwanya atafuatiwa na Mheshimiwa Jenista Mhagama.

MHE. MHONGA S. RUHWANYA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ili niweze kuchangia machache katika Wizara hii ya Ujenzi. Kwanza namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunipa afya mpaka nimeweza kusimama leo kuchangia.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza na mambo ambayo naona kama ni udhaifu katika Wizara hii ambayo yanahitaji kufanyiwa marekebisho. La kwanza kabisa, tunafahamu kwamba barabara zetu tunazijenga kwa pesa nyingi lakini vile vile tumejikuta kwamba zabuni inapofungwa siyo kiwango halisi ambacho kinalipwa mwishoni. Mimi ni Mjumbe wa Kamati ya PAC tumetembelea barabara nyingi tumegundua hilo. Barabara inaweza ikapangiwa may be bilioni 50, lakini mwisho wa siku inaweza ikalipwa hata bilioni 100 ambapo kunakuwa na kulimbikiza matokeo yake kunakuwa na fidia inatakiwa pia ilipwe. Kwa hiyo mimi nashauri kwamba TANROADS wawe wanaweka utaratibu mzuri, kwa hiyo mimi nashauri kwamba TANROADS wawe wanaweka utaratibu mzuri wa kupitia na kurekebisha usanifu na waangalie pia makadirio ya miradi mara baada tu ya kuandaliwa ili kuepuka tatizo hili kabla ya ujenzi kuanza.

Mheshimiwa Spika, lakini vile vile baadhi ya barabara zinakabidhiwa zikiwa katika hali ya chini sana na matokeo yake zimekuwa zinatakiwa kurudiwa mara kwa mara. Kwa mfano, barabara ya Mandela Dar es Salaam, ni barabara ambayo ilishatengenezwa, lakini

75 sasa wanarudia tena. Ukipita pia katika barabara ya Morogoro kuja Dodoma, kuna maeneo ambayo yana utelezi sana na kuna maeneo mengine ambayo unakuta barabara inabanduliwa, inatengenezwa tena. Sasa nafikiri tunapoteza muda, tungeweza tuka- concentrate katika maeneo mengine, ni bora TANROADS wawe na uwezo wa kusimamia vizuri barabara zao ili zinapokabidhiwa ziwe katika kiwango na hata ukiangalia pale eneo la Chalinze, ni sehemu ambayo ni mbaya sana, kwa kweli wakati watu tukipita tutaona kabisa kwamba iko chini ya kiwango. Kwa hiyo, inabidi TANROADS wahakikishe kwamba wanaboresha usimamizi na udhibiti wa wakandarasi ili barabara tunazopokea ziwe juu ya viwango.

Mheshimiwa Spika, Wizara hii pia ina udhaifu mkubwa wa kuchelewesha kulipa Wakandarasi matokeo yake tunapelekea kulipa fidia. Kwa mfano, tu kwa Mkoa wa Shinyanga, ukiangalia bajeti iliyopita kwa mkoa mmoja tu inadaiwa kiasi cha shilingi bilioni 80 na milioni kama 95, lakini kuna fidia pale ya bilioni nane na milioni kama 929. Hiki ni kiwango kikubwa sana ambapo hiyo fidia ingeweza kujenga hata barabara nyingine angalau hata kilomita tano za lami. Tunaomba Serikali iangalie uwezekano wa kwamba iwe inahakikisha kwamba, ina pesa za kutosha katika kukamilisha barabara zetu.

Mheshimiwa Spika, pia naomba Waziri atueleze kwa mwaka huu tunapitisha kiasi gani ambazo zitalipa madeni peke yake na zile ambazo zitakwenda kujenga barabara mpya na zile ambazo zitatumika kulipa madeni tena. Ukiangalia bajeti iliyopita kuna bilioni 420

76 zililipwa, kwa hiyo, maana yake ni kwamba, kuna miradi mingine ambayo itafanyika chini ya mikopo na madeni makubwa, tutaendelea kulipa madeni na fidia ambapo hizo pesa zingeweza kujenga barabara zingine kwa kiwango kizuri tu.

Mheshimiwa Spika, sasa nakwenda kwenye mtandao wa barabara zetu za Kigoma, nilikuwepo katika Bunge lililopita, barabara ya Kigoma-Nyakanazi, naomba niseme ni muhimu sana kwa maisha ya watu wa Kigoma, kwa sababu ni barabara ambayo inatuunganisha na Mikoa ya Kagera kwenda mikoa mingine kama Kahama, Shinyanga, lakini vilevile ni barabara ambayo inatuunganisha Wilaya ya Kibondo, Kasulu kwa pamoja na kwa kweli sisi tunaiona kama ni barabara kuu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini nasikitika kidogo kwamba, sielewi hapa naona barabara hii imeunganishwa Mpanda, Nyakanazi road, halafu vile vile barabara hii tena inaitwa barabara ya Nyakanazi yaani kupita Kasulu, Kibondo, Nyakanazi, sasa kidogo nachanganyikiwa ni barabara hii hii moja au ni ipi, au ni katika tu kutuchanganya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu nikiangalia kipindi kilichopita, Wabunge wa Kigoma tulikuwa tukisimama tukiongelea sana hii barabara, lakini mwisho wa siku tunaambiwa tu tuko kwenye upembuzi yakinifu, usanifu wa kina na mambo mengi mengi tu. Tunaambiwa, yaani mimi nasema kulaghaiwa, halafu inakuja mwisho wa siku fedha zinatengwa, hazionekani na kipindi hiki tena tutaangalia toka mwaka 2010, zilitengwa bilioni

77 sita lakini hazikutolewa. Ikatengewa tena mwaka 2011/2012 bilioni mbili nukta tatu, lakini haikutolewa na nina wasiwasi kama hata hii bilioni tatu na nukta tano itatolewa kwa sababu imekuwa ni mtindo wa kawaida. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kilomita 310 kwa pesa hii ni ndogo mno. Naomba Mheshimiwa Waziri atuambie mkakati maalum wa ujenzi wa barabara hii kwa sababu ni muhimu sana. Nakumbuka kuna siku tulikuwa na dinner na Mheshimiwa Rais akatuelezea mipango mbalimbali ya Mkoa wa Kigoma Bunge lililopita. Alituelezea mipango mbalimbali na akasema kwamba aligundua barabara hii ni muhimu mno. Siku moja alikuwa katika mkutano wa hadhara Kasulu akaelezea barabara hii ya Tabora–Kigoma watu hawakushangilia lakini alipoitaja hii barabara watu walishangilia mno.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, nafikiri kama Serikali ina uwezo wa kukopa pesa maeneo mengine kwa ajili ya kujenga barabara za mikoa mingine, nimeona kuna pesa za JICA, MCC na nyingine nyingi, kwa nini inashindikana kukopa pesa kwa ajili ya ujenzi wa barabara hii ya Kigoma–Nyakanazi. Kwa sababu tumekuwa tukipewa maneno mazuri katika Bunge hili kwa muda mrefu na ndiyo maana natoa masikitiko yangu kwa sababu imekuwa haitekelezeki. Matokeo yake sasa leo tunaona inaitwa Kigoma-Kasulu– Kibondo–Nyakanazi na humo humo tunaiona tena inatakiwa itokee Sumbawanga sasa tunakuwa hatuelewi.

78 Mheshimiwa Spika, hii barabara ya kutoka Sumbawanga mpaka kufika huko Nyakanazi ni karibu kilomita 575.7. Sasa hatujui itajengwa upande huu na huu ili tukutane katikati au tutaanzia Sumbawanga? Mpaka ije ifike kwetu kwa kweli ni muda mrefu sana na kwa taarifa tu ni kwamba, mvua inaponyesha katika hii barabara magari yanateleza mno, magari mengi yanakwama, wananchi wanakaa muda mrefu katika ile barabara. Tumesikia katika maeneo mengi hasa msitu wa Malagarasi kuna majambazi wengi wamekuwa wakiteka magari pale. Barabara hii maana yake ingekuwa nzuri at least speed ingekuwa inaongezeka hata wale majambazi wasingekuwa wakifanikiwa.

Mheshimiwa Spika, naendelea kuisemea barabara hii na naomba ikiwezekana ikopewe pesa iweze kutengenezwa kama nyingine kwa sababu kama kuna uwezekano wa kulipa madeni ya barabara nyingine maana yake na hii pia inawezekana. Tusiendelee kuachwa nyuma kwani tumeshabaki nyuma mno.

Mheshimiwa Spika, barabara hii kwetu sisi kuna watu wanataka kufanya kama ni siasa lakini siyo siasa, ni muhimu kwa sababu inatusaidia kuinua uchumi wa mkoa wetu ukizingatia kwa sasa hivi reli yenyewe ndiyo imeanza kufufuliwa na ndiyo usafiri ambao kidogo tulisema ni wa hali ya chini, ungeweza kuwasaidia wananchi wengi lakini bado nao una matatizo. Hii barabara ikifunguka itasaidia wananchi wengi, lakini bado nao una matatizo. Kwa hiyo, tunaamini na hii barabara ikifunguka tutarahisisha usafiri ule wa kwenda

79 mikoa ya karibu kama Mwanza, Shinyanga na maeneo mengine. Naamini niliyoyasema yamesikika

Mheshimiwa Spika, naomba tena barabara ya Kobondo–Mabamba ipatiwe pesa ili iweze kutengenezwa, lakini vile vile tuunganishe barabara ya Kasulu-Manyovu ili iweze kutokea katika ile barabara ya Manyovu ambayo inakwenda mpakani mwa Burundi na kuwasaidia wananchi wa maeneo haya waweze kusafirisha bidhaa zao kufika nchi ya jirani kwa ajili ya kuinua uchumi wao.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba niongee jambo lingine dogo kuhusu mizani. Naamini iliwekwa kwa sababu ya kutunza barabara zetu na vile vile ili ku-control magari makubwa yasiweze kuzidisha uzito na kufanya barabara ambazo zimejengwa kwa gharama kubwa sana ziweze kutengenezwa mara kwa mara halafu tutakuwa tukipata hasara.

Mheshimiwa Spika, lakini naomba nisikitike kidogo kwani katika hotuba yako ukurasa wa 14 imeoneshwa kwamba bado mizigo inazidishwa uzito katika magari. Magari 482,638 yameonekana yamezidisha uzito kiasi kwamba imetokea kwamba wametakiwa walipe faini ya shilingi 3,260,000,000/=. Hatuwezi kufurahia kupokea pesa za faini kwa sababu ile mizani siyo kitega uchumi. Tunachotakiwa ni ku-discourage hawa ambao wanazidisha mizigo wasiweze kuzidisha ili barabara zetu ziweze kudumu.

80 Mheshimiwa Spika, nashauri kama sheria inaonekana ni nyepesi ibadilishwe au siyo tuongeze kipengele kingine cha kanuni na hiyo inawezekana, iko chini yake Mheshimiwa Waziri anaweza kufanya hivyo. Ikiwa mtu anazidisha uzito adhabu yake ni kukaa wiki nzima bila kusafiri yaani gari inawekwa pembeni atakaa wiki nzima. Kwa kuwa mtu ni mfanyabiashara basi next time hawezi kurudia tena kosa hilo.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba pia mizani iboreshwe ili magari yawe yanapimwa haraka haraka ili kuondoa usumbufu wa foleni ambao unasababishwa katika mizani.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, nasema siungi mkono hoja mpaka nipatiwe majibu ambayo nimeyaomba. Ahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana. Hotuba yako nzuri isipokuwa maneno ya ulaghai hayakuwa mazuri. Tunaendelea na Mheshimiwa Jenista Mhagama na Mheshimiwa Haroub Mohamed Shamis ajiandae.

MHE. JENISTA J. MHAGAMA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi. Kwanza kabisa kabla sijasahau naomba niseme naunga mkono hoja asilimia mia moja.

Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri, Katibu Mkuu, Naibu Katibu Mkuu lakini na Wataalam wote wa Wizarani. Nimpongeze pia Mwenyekiti wa Bodi ya Mfuko wa Barabara, kaka yetu Wanyancha. Lakini kwa

81 kweli niseme kwa niaba ya wananchi wa Mkoa wa Ruvuma naomba niishukuru sana sana Serikali ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Spika, kwa mara ya kwanza toka nchi yetu imepata uhuru unaona kabisa dhamira ya dhati ya Serikali ya kutekeleza mpango wa maendeleo kufungua miundombinu ya barabara, nguvu kubwa imeelekezwa mikoa ya Kusini. Hakika kama sitaipongeza Serikali katika hilo nitakuwa sijatenda haki kabisa. Kwa hiyo, nasema ahsante sana, tuna karibu shilingi bilioni 592 kuanzia Mkoa wa Lindi, Mtwara na Ruvuma. Pia na unapata picha vile vile barabara zilizopewa kipaumbele katika Mkoa wa Njombe, Iringa lakini Mkoa wa Rukwa na Mkoa wa Katavi. Mikoa hii kwa miaka mingi sana barabara zilikuwa hazipitiki. Ukitoka Mtwara unakuja mpaka Tunduru, Songea mpaka Mbinga barabara ile yote ilikuwa ni vumbi tupu wakati wa masika tulikuwa hatuwezi kuwasiliana. Kwa hiyo, naishukuru sana Serikali yangu.

Mheshimiwa Spika, Serikali imetenga shilingi bilioni 79.8 kwa barabara ya Peramiho–Mbinga na barabara hii inapita Kijiji cha Matomondo, Lipokela na Kijiji cha Liganga. Hawa wananchi wanafurahi sana na barabara imeshaanza kuwekwa lami katika kipande kikubwa sana. Huko kwenye Kijiji cha Lipokela, Liganga na Matomondo, sasa hivi tuna mwekezaji mkubwa ameanzisha kilimo cha kahawa. Sasa hayo yote unaona kabisa ni ufunguzi mkubwa wa uchumi wa wananchi wa Jimbo la Peramiho katika eneo hilo ambalo limepata fedha nyingi za barabara, lakini pia tunaanza hata kujifungua hata katika mpango wa

82 kilimo bora cha mazao ya biashara. Kwa nini nisimpongeze Mheshimiwa Magufuli? Kwa nini nisiipongeze Serikali yangu ya Chama cha Mapinduzi?

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana naomba wananchi wa Matomondo, Lipokela na Liganga, leo nasimama hapa kwa niaba yenu naishukuru Serikali na tuliwaambia wakati wa kampeni mwaka 2010 kwamba barabara hii itawekwa lami. Haijawa uongo na ninyi ni mashahidi tunasonga mbele Chama cha Mapinduzi na wala hatuna matatizo, tutatekeleza na mengine yanayotusubiri. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana wakati wa kampeni mwaka 2010, Serikali iliahidi kujenga barabara ya Makambako-Songea ambayo tayari ina lami ila kwa kuwa tayari imeshachakaa sana. Serikali iliahidi kwamba sasa itaweka tabaka lingine jipya la lami. Kwenye bajeti hii zimetengwa shilingi milioni 979, barabara hiyo ina urefu wa kilomita karibu 295, hapo ndiyo nina wasiwasi kidogo kama fedha hii inaweza kutosha kwa barabara yote. Lakini niiombe Serikali na Mheshimiwa Waziri wangu Magufuli naomba anisikilize sana, barabara hii inapita Kata ya Wino ambayo ina vijiji visivyopungua sita, inapita Kata ya Mahanje eneo la Madaba na Kibaoni, inapita Kata ya Mkongotema kuna Lutukila na vijiji vingine, inapita Kata ya Gumbilo na Mtengimboli.

Mheshimiwa Spika, naomba nimwombe Mheshimiwa Waziri Magufuli kwamba katika matengenezo ya barabara hii, barabara hii ni mbaya ukitoka Songea kuelekea Njombe kwenda

83 Makambako. Kutoka Makambako kuja Songea ina unafuu mkubwa sana, lakini kutoka Songea kupita hivyo Vijiji na Kata nilizozisema kwenda Njombe na kuendelea mbele.

Mheshimiwa Spika, wewe ni jirani yangu, Majimbo yetu yanapakana na barabara hii umeiona na nadhani unakubaliana na mimi. Matengenezo haya sasa yasianze Makambako kwenda Songea bali matengenezo haya sasa yaanze Songea kwenda Njombe na ndivyo yaende Makambako. Mheshimiwa Waziri nakuomba sana eneo hilo ni eneo baya ukilinganisha na kutoka Njombe kwenda Makambako. Sasa kama fedha hii shilingi milioni 979 ikianza Makambako kwenda Songea hakutakuwa na maana kwa sababu kule itakuwa ni kuondoa tabaka la lami ambalo ni bora ukilinganisha na tabaka la lami kutoka Songea kwenda Njombe kwenda Makambako. Kwa hiyo, naomba hii milioni 979 ianze Songea, Katibu Mkuu unanisikia na wataalam wote, tusipokubaliana katika hili kwa kweli tutaanzisha ugomvi mkubwa sana. Ni lazima tuangalie kule kuliko kubovu ndiko kushughulikiwe kwanza.

Mheshimiwa Spika, pia tuna machimbo ya kokoto Lilondo ambayo ni mazuri tu, kwa hiyo, hatuna matatizo. Naomba sana barabara hii sasa ianze kutoka Songea ikipita maeneo niliyoyataja ya vijiji yangu hivyo na nashukuru sana Serikali katika kuendeleza hiyo hiyo miundombinu, miundombinu ni barabara lakini unaona hata umeme nao unapita katika maeneo hayo hayo. Sasa ni faida kubwa sana kwa wananchi wangu watajifungua kibarabara, lakini

84 pia watajifungua pia katika masuala yote ya uzalishaji mali na naishukuru sana Serikali yangu.

Mheshimiwa Spika, lakini niishukuru sana Wizara kwa kutupatia shilingi milioni 500 ambazo tunazitumia kutengeneza barabara ya kutoka Mpitimbi kwenda Ndongosi, lakini kwenda Nambendo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji. Fedha hiyo siyo nyingi sana lakini imetuwezesha kuanza kutoka Ndongosi kwenda Nambendo, lakini inatusaidia pia kuanza matengenezo kutoka Matimila kwenda Mkongo tukipakana na Wilaya ya Namtumbo. Hata hivyo, naomba kama wanaweza watuongeze fedha ili barabara hizo tuweze kuzimaliza.

Mheshimiwa Spika, ila niombe sana barabara ya Peramiho kwenda Kilagano, ni barabara ya Mkoa. Fedha za Mkoa za matengenezo ya barabara ya Mkoa wa Ruvuma zimekuwa chache. Tunaomba mtuongezee, kule tunazalisha mahindi na ndiko tunakotoa chakula cha kuwalisha Watanzania, tuongezeeni fedha ili tuweze kutengeneza barabara hiyo.

Mheshimiwa Spika, lakini tuna barabara ya Wino kwenda Ifinga. Ulipokuwa Mkuu wa Mkoa wa Ruvuma unajua Wino kwenda Ifinga ilivyo shida kubwa. Naomba kwanza barabara hi ipandishwe hadhi kuwa barabara ya mkoa, lakini pia ipewe fedha za matengenezo kila mwaka, hakika maisha ya wananchi kule ni ya shida. Kwa hiyo, naomba sana kupitia Kiti chako basi Wizara ichukue barabara hii kuwa ya Mkoa, lakini baada ya kuichukua kuwa barabara ya Mkoa

85 ihakikishe kila mwaka inatuchangia fedha angalau kwa ajili ya matengenzo.

Mheshimiwa Spika, lakini ipo barabara nyingine inaunganisha Mkoa wa Ruvuma na Mkoa wa Njombe, unaifahamu kwani barabara hiyo inatoka kwenye Kijiji changu cha Maweso, inakuja kwako Mheshimiwa Spika. Kwa nini na hii isichukuliwe tu kuwa kule kwako ichukuliwe na Mkoa wa Njombe na huku kwangu Taifa watukubalie ichukuliwe kuwa barabara ya Mkoa na ipewe fedha, itafungua mawasiliano mazuri sana ya wananchi katika maeneo hayo niliyoyasema.

Mheshimiwa Spika, lakini nimalize kwa kusema kwamba haja ya kufungua miundombinu ni azma ya Serikali, shida kubwa ninayoiona hapa tuna Wakala wa Barabara ambaye anasimamia barabara za Mkoa, barabara za Wilaya zinaendelea kusimamiwa na Halmashauri zetu na kila mwaka fedha nyingi zinakwenda kwenye barabara, Halmashauri na huko kwenye Mkoa. Lakini bado tuna matatizo makubwa sana ya kutengeneza barabara zetu huko vijijini, uwezo wa kuzijenga kwa lami kwa mara moja hatuna, hivi hatuwezi tukafikiria huko mbele tukatengeneza agency moja itakayokuwa inafanya kazi chini ya Wizara ya Ujenzi lakini ikashughulikia barabara zote katika nchi nzima ya Tanzania.

Mheshimiwa Spika, lakini tunaweza tukaamua kwamba ofisi sasa ya agency hiyo ikawe na branch mpaka kwenye Wilaya zetu ili kusimamia barabara ambazo zipo ndani ya Wilaya. Vinginevyo kila siku tutaendelea kulia kwamba barabara hii ipandishwe

86 hadhi, iwe ya mkoa na kadhalika, mwishoni barabara zote za nchi nzima zitakuwa ni barabara za Mkoa. Sasa zikishakuwa zote ni barabara za Mkoa, utaona kabisa kwamba hapa kuna kitu fulani kinatakiwa kifanyike.

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya wananchi wangu wa Jimbo la Peramiho, naunga mkono hoja na naomba pesa hizi zikishafika basi tutaendelea kusonga mbele. (Makofi)

SPIKA: Ahsante, lakini hiyo barabara ya Maweso kuingia Njombe ni ile barabara ya zamani na wale wanajeshi walikufa pale kutokana na barabara hii kuvunjika, lakini eneo lile ndiyo lenye uzalishaji mkubwa kuzidi maeneo yote. Imeanza kujengwa na madaraja yameshajengwa isipokuwa bado kumalizia daraja la Mundu ambalo linabomoka hovyo, garbage’s, ndiyo hicho anachokisema, lakini mengine sipingani nayo maana yake ni jirani.

Sasa namwita Mheshimiwa Haroub Mohamed Shamis atafuatiwa na Mheshimiwa Anna Marystella John Mallack.

MHE. HAROUB MOHAMED SHAMIS: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili niweze kutoa mchango wangu katika Wizara hii ya Ujenzi. Kabla ya hapo naomba kwanza nikupe pole kwa msiba uliokupata na pia naomba nipeleke pole kwa wapiga kura wangu wa Jimbo la Chonga hasa wa Kijiji cha Kidongo kwa kuvamiwa na majambazi na kujeruhiwa Mwalimu Mkuu wa Skuli ya Matale Bi.

87 Rahma Mohamed Said. Kwa hiyo nawapa pole na wajue kwamba niko nao pamoja.

SPIKA: Hiyo microphone naomba uishike vizuri tunakusikia kidogo.

MHE. HAROUB MOHAMED SHAMIS: Mheshimiwa Spika, namshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijaalia afya Ijumaa hii ya leo na naomba nianzie katika msongamano wa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, kama tunavyojua Dar es Salaam ndiyo kioo cha nchi yetu, kila mtu Dar es Salaam inamgusa, Dar es Salaam ndiyo uso wa nchi yetu na uso ni kiungo muhimu katika mwili wa binadamu. Mtu anaweza akaugua mkono akaweza kufanya shughuli zake lakini kama uso una matatizo basi akili yote inakuwa haifanyi kazi. Lakini kama tunavyojua Dar es Salaam inakusanya mapato takribani 84% ya uchumi wa nchi yetu, kwa hiyo, kuna umuhimu wa pekee wa kupewa miundombinu ya Dar es Salaam kuwa yenye hali ya juu.

Mheshimiwa Spika, napenda nitoe ushauri kama kawaida yangu kwa kushauri kwamba Dar es Salaam inahitajika kuundwa mamlaka moja ya kusimamia Jiji kwa sababu sasa hivi kunaonekana kama kuna conflict of interest, wengine wanasema tutengeneze barabara, lakini wengine wanasema tuziache hivyohivyo kwa sababu kukiwa na uchafu wao ndiyo wanapata kukusanya fedha. Kwa hiyo, nashauri iundwe mamlaka moja itakayoweza kusimamia Jiji la Dar es Salaam. Ikifanyika hivyo itasaidia kuondoa haya

88 matatizo kwani mvutano utapungua, lakini pia nashauri kwamba barabara ndogo ndogo zote za Jiji la Dar es Salaam zile streets ziwekwe lami ili ziweze kupitika kwa masaa yote na kwa siku zote za mwaka.

Mheshimiwa Spika, sasa hivi ikinyesha mvua kidogo pale Dar es Salaam basi kama unatoka mjini kuelekea mitaa mingine huwezi, ni lazima upite barabara ya uhuru au barabara ya Ally Hassan Mwinyi kwa sababu barabara nyingine zote hazipitiki kwa mashimo, matope na zinakuwa flooded kutokana na drainage mbovu. Kwa hiyo, hili litawezekana kufanywa kwa kasi ikiwa kutakuwa na mamlaka moja inayosimamia, lakini sasa hivi kila sehemu kila mamlaka inasimamia sehemu ndogo tu kwa hiyo inakuwa vigumu kutokana na mvutano wa kimaslahi.

Mheshimiwa Spika, pia kuna nia njema ya Serikali kujenga flyover TAZARA kwa ajili ya kupunguza msongamano, ni jambo zuri tunalipongeza. Lakini flyover moja haiwezi kuondoa msongamano kwa sababu magari makubwa yanayotoka Bandarini yakielekea Ubungo yakifika Ubungo yana stuck, kwa hiyo, pale Ubungo Mataa inahitajika flyover nyingine ili iweze kufungua ile congestion ya barabarani.

Mheshimiwa Spika, mambo haya lazima yaende sambamba na naungana na Mwenyekiti wangu Mheshimiwa Serukamba na mimi pia ni Mjumbe wa Kamati ya Miundombinu kwamba Serikali kwa sababu inaaminika, basi itafute fedha kwa lump sum, fedha nyingi za kufanya hili jambo la miundombinu ya barabara na Reli kwa pamoja, tukiwa tunafanya

89 mipango mizuri halafu tunatekeleza kidogo kidogo hatuwezi kufika.

Mheshimiwa Spika, mfano mdogo, kama unapika chakula chako cha kula mchana yaani lunch, lakini ikawa unakula kidogo unakiacha tena unakula kidogo unakiacha huwezi kushiba. Kwa hiyo, ni lazima tutafute fedha kwa sababu Serikali hii chini ya Rais Jakaya Kikwete inaaminika, tutafute fedha za kujenga miundombinu kwa pamoja na kwa haraka ili tuweze kulikomboa Taifa hili.

Mheshimiwa Spika, nchi hii ina uchumi mkubwa, Serikali hii ikienda kukopa kiasi cha dola bilioni tano tukajenga hizi barabara pamoja na reli kwa kipindi kifupi zitaweza kurejeshwa kwa sababu uchumi uliopo katika nchi hii ni mkubwa sana. Naamini kama tukijenga miumbonu hii katika kipindi kifupi basi mapato ya nchi hii yanaweza yakapanda hata mara tatu, kama sasa hivi tunapata trilioni nane au tisa tutapata trilioni 24 kwa kufungua miundombinu hii.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kidogo niingie kwenye barabara hii ya Namtumbo–Tunduru. Barabara hii inayojengwa huko Kusini ina urefu wa kilomita 193 na imegawanywa katika vipande vitatu. Barabara hii inayounganisha barabara ndefu ambayo ina urefu wa kilomita 649 inayokwenda Masasi-Songea mpaka Mbamba Bay, ina umuhimu mkubwa kwa uchumi wa nchi yetu. Lakini jambo la kushangaza ni kwamba pamoja na kugawanywa katika vipande vitatu barabara hii amepewa Mkandarasi mmoja. Hili ni jambo la kushangaza!

90

Mheshimiwa Spika, nadhani labda kwa sababu wameigawa, basi watapewa Wakandarasi watatu ili kazi ifanyike mara moja na kufungua uchumi wa maeneo yale. Lakini amepewa Mkandarasi mmoja ambaye inaonekana uwezo wake ni duni sana kwa sababu katika sehemu ya mwanzo ambayo inatoka Namtumbo mpaka Kilimasera ni kilomita 60.7 Mkandarasi aliyepewa kwa muda wa miezi 14 sasa ambayo muda wa kukamilisha kazi hii ni miezi 27 ameshatumia karibu asilimia 50 ya muda lakini kazi aliyoifanya ni asilimia tisa (9%) tu.

Mheshimiwa Spika, hili jambo kwa kweli linatia mashaka sana. Katika phase ya pili kutoka Kilimasera mpaka Matemanga kilomita 68.2, Mkandarasi ametumia muda kama huo wa miezi 14 lakini amefanya kazi kwa asilimia 2.5 tu. Hii inaleta wasiwasi, Mkandarasi huyu inakuwaje! Phase ya tatu kutoka Matemanga–Tunduru kilomita 58.7, hapa ndiyo unaweza ukalia. Mkandarasi amefanya kazi kwa asilimia moja (1%) kwa miezi 14 na muda uliobakia ni miezi 13. Kweli ataweza kumaliza kwa speed hii ya konokono (snail speed)? Hawezi kufika! Atamaliza maisha yake hajafika anakokwenda. Mkandarasi huyu anaitwa Progressive Higleig J.V. kutoka India.

Mheshimiwa Spika, napenda kuishauri Serikali hii kwamba, fedha zilizotumika kujenga barabara hii zaidi ya shilingi bilioni 180, ni nyingi sana. Tulitegemea fedha hizi zitolewe na barabara ijengwe, uchumi ufunguke, maisha ya wananchi yaboreke, lakini kwa hali hii nahisi sijui kuna tatizo gani.

91

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, leo namwomba Mheshimiwa Waziri hapa atueleze inakuwaje ujenzi wa barabara hii unakwenda kwa kusua sua namna hii? Mkandarasi huyu anasimamiwa na ma- consultants watatu tofauti, lakini ma- consultants hawa hawaoni kama huyu Mkandarasi hawezi! Kwa nini hawaishauri Serikali? Ma-consultants hawa wanafanya kazi gani? Je, ni kwamba hawaiambii Serikali au Serikali haisikii? Ikiwa Serikali inashauriwa kwa nini haichukui hatua? Hawa ma-consultants watatu wanaosimamia barabara moja wanalipwa zaidi ya shilingi bilioni tisa (9,000,000,000/=), lakini hawaishauri Serikali au Serikali haisikii kwamba inashauriwa! Uozo kama huu hakuna kinachofanyika!

Mheshimiwa Spika, naomba niingie kidogo katika jambo la pili hapa ambalo ni la Wakala wa Majengo ya Serikali (TBA). Hii ni taasisi ambayo inatakiwa ijenge majengo kwa ajili ya Viongozi wa Serikali na sisi Wabunge ni part au sehemu ya Serikali. Lakini hakuna uendelezaji wa majengo haya kwa ajili ya kuwatatulia matatizo viongozi wa Serikali, badala yake imejiingiza katika majengo ya kibiashara ya kukodisha wafanyabiashara wakubwa na kufanya shareholdings badala ya kufanya shughuli ile iliyokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, pia hapa Dodoma na maeneo mengine, lakini nitoe mfano wa hapa Dodoma kuna nyumba hizi ambazo zinamilikiwa na Wakala huyu wa Serikali, lakini Wabunge wanaishi mle, mie sijapata nyumba hiyo. Sisemi kwa interests zangu, lakini hao wanaokaa humo wanalalamika kwamba, nyumba hizi

92 ni mbovu na hazishughulikiwi na zinasababisha gharama ya matengenezo kuwa kubwa kutokana na kwamba wanaacha kutengeneza sehemu ndogo iliyoharibika na hivyo tatizo linaongezeka. Mfano, drainage systems zikiwa mbovu nyumba inaweza ku- cost hata kujenga tena ukuta au kubadilisha floor nzima.

Mheshimiwa Spika, tusipoziba ufa tutajenga ukuta. Ushauri wangu ni kwamba, pale panapoharibika hata kama gharama yake ni 50,000/=, 100,000/= au 200,000/= pashughulikiwe ili kuepuka fedha za wananchi kutumika kwa ajili ya kufanya ukarabati mkubwa zaidi.

Mheshimiwa Spika, napenda nikushukuru. Ahsante sana. (Makofi)

MHE. ANNA MARYSTELLA J. MALLACK: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi hii ili na mimi niweze kuchangia katika Wizara hii ya ujenzi.

Mheshimiwa Spika, kwanza nimtangulize Mwenyezi Mungu aliyenipa uhai na afya njema ya kuweza kusimama mbele ya Bunge lako Tukufu. Pia napenda nitoe pole kwako kwa msiba uliokupata, nasema pole sana.

Mheshimiwa Spika, kama ilivyo kawaida nianze kwa kuitetea kwanza mikoa yangu ya Rukwa na Katavi. Kwa kipindi kirefu sana mikoa ya Rukwa na Katavi tumesahaulika pamoja na kwamba, Rukwa ni mkoa wa zamani na una vigezo vyote vya

93 kuipendezesha na kuinufaisha Tanzania. Tuna Mbuga ya Katavi yenye wanyama wazuri wakubwa wa kupendeza kuangalia. Tuna maziwa mawili Rukwa na Tanganyika. Tuna misitu minene, mizuri inayopendeza. Tuna kilimo, mifugo na kila kitu, mpaka tunashindwa kusifia kwa kweli na sisi wenyeji wa kule ni wakarimu, lakini tumeshindwa kukumbukwa katika suala la barabara, tunatembea katika barabara za vumbi. Mheshimiwa Waziri, kama ingekuwa matope na vumbi ni lishe kwa ajili ya afya bora tungekuwa tumenenepa kweli. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, lakini wananchi wa Katavi na Rukwa wanashukuru kidogo kwa sababu asiyeshukuru ni kafiri. Tunashukuru sana kuona mmetukumbuka kwamba na sisi ni binadamu. Mmeanza kututengenezea barabara zetu; barabara ya kutoka Tunduma–Sumbawanga na Sumbawanga-Mpanda kupitia Kibaoni kwa kiwango cha lami. Tunasema ahsante sana, lakini siwezi kushukuru mia kwa mia mpaka tutembee juu ya lami, ndiyo tutashukuru vizuri.

Mheshimiwa Spika, kitu kingine napenda kuisisitiza Serikali sasa kupitia Wizara itoe fedha kwa wakati kuwalipa Wakandarasi ili kazi isisimame kwa sababu hapa katikati miezi iliyopita kazi ilikuwa imesimama. Tulitembea kwa kuhangaika sana. Kufika nyumbani wakati ukitokea safari kwa kweli ni shughuli, ndugu zako wanapokuona kwa kweli wanafurahi na kumshukuru Mungu kwamba umefika salama. Kwa kweli ni balaa kupitia njia hii ya Tabora-Inyonga-Mpanda kutokea Mbeya–Tunduma–Sumbawanga–Mpanda, zote ni

94 shida tupu kiasi kwamba, hata mzunguko wa biashara zetu unakuwa ni shida sana.

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, naiomba Serikali sasa kupitia Wizara hii ikaze buti, isisimamishe hii kazi. Ihakikishe inawalipa Wakandarasi kwa wakati ili kazi isisimame kusubiri kipindi cha masika tena ambapo mvua zikija zinaharibu ile barabara, kazi inarudi nyuma na hivyo kupoteza fedha za Serikali. Kwa hiyo, naomba mlipe kipaumbele suala hili la barabara jamani na sisi tunatamani tutembee juu ya barabara za sementi kama wenzetu wa mikoa iliyoendelea.

MBUNGE FULANI: Barabara za simenti!

MHE. ANNA MARYSTELLA J. MALLACK: Nina maana ya lami, kwa sababu wazee wanasema nimetoka Pwani, kule Pwani wenzetu wanatembea kwenye barabara za simenti, wakimaanisha lami. Kwa hiyo, naomba na sisi Wanarukwa mtukumbuke, tumechoka kula vumbi na matope. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, lingine ni barabara za vijijini. Serikali ya CCM inaangalia mjini zaidi, lakini vijijini imewasahau. Wale wananchi wa vijijini ndiyo wazalishaji wakubwa. Sisi wananchi wa mijini tunapendeza, tunang’aa kupitia wananchi wa vijijini wanaolima wanatuletea mazao tunanunua, tunakula tunashiba, tunanenepa na tunapendeza. Kwa hiyo, naomba Serikali ya CCM iangalie sana barabara za vijijini.

95 Mheshimiwa Spika, kule kwetu barabara vijijini ni ndoto. Kuna wengine wakiona gari limewafikia kijijini kwao wanakimbia. Nimewahi kutembelea vijiji vingine kwa lengo la kuangalia maisha ya Watanzania wenzetu, wanakimbia gari. Wanasema machinja chinja hao sijui wamevamiwa. Eeh, wanaona ni ndoto! Barabara hazipitiki na kule ndiyo kuna wakulima lakini wanashindwa kukusanya mazao yao kupeleka kwenye barabara zile kubwa za mikoa ili kutafuta soko.

Mheshimiwa Spika, mpaka ninavyoongea hivi kuna wananchi ambao wana mpunga wa tangu mwaka jana wameshindwa kuusafirisha. Wananchi wanatembea kwa shida kutafuta huduma za kimsingi kama vile afya na elimu. Mwanafunzi anakwenda shuleni anapita kwenye vichaka vyenye visiki porini kitu ambacho ni hatari na kwa kurahisisha anaona ni heri ajitwike viatu kichwani kwa sababu akivaa anaona ni mzigo. Kwa hiyo, kule vijijini kuna maeneo ambayo ni mabaya sana, naomba myafuatilie. Kwa mfano; Vikonge–Bugwe, Vikonge–Ifisi, Ikola-Kafisha, Kapanga- Bujombe, Kalilankurukuru-Kamsanga na kuendelea, vijiji ni vingi siwezi kuvitaja vyote, lakini naomba wakumbukwe. Kama Halmashauri zimeshindwa basi naomba mkae meza moja muone ni jinsi gani labda muwatupie mzigo TANROADS ili hizi barabara za vijijini ziweze kutengenezwa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, vile vile asiyeshukuru ni kafiri. Niliwahi kumlalamikia Waziri kuhusu daraja la Nzaga ambalo linatoka Inyonga kwenda kuikuta Msaginya. Lile daraja nililalamika kuwa limetitia na lilikuwa limepasuka lakini mabasi yalikuwa yanapitisha

96 wananchi pale, kitu ambacho kingekuwa ni hatari. Lakini Waswahili wanasema ziba ufa kabla hujajenga ukuta kwa sababu Tanzania tumekuwa tunajifunza vitu, tunasubiri mpaka litokee janga ndiyo sasa tunaanza michakato ya kuimarisha, kitu ambacho sivyo. Kwa hiyo, napenda nimshukuru Mheshimiwa Waziri lile daraja la Nzaga sasa limejengwa. Nasema ahsante sana na udumu. Magufuli Oyee!

WABUNGE FULANI: Oyeeee.

MHE. ANNA M. J. MALLACK: Mheshimiwa Spika, nimemaliza ahsante sana. (Makofi/Kicheko)

SPIKA: Umetia na chumvi kwa kweli, maana ulipokwenda na gari watu wote wakakukimbia, sasa sijui ulionana na nani! Ahsante dada Anna Marystela. (Kicheko)

MHE. FAITH M. MITAMBO: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwanza nianze kukupa pole wewe mwenyewe kwa kufiwa. Tunajua kwamba ulimpenda mama huyu aliyefariki, lakini Mungu alimpenda zaidi.

Mheshimiwa Spika, naomba niungane na wasemaji wenzangu waliopita kumpa pongezi Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Daktari Magufuli, kwa kazi nzuri ambazo anazifanya katika ujenzi wa mitandao hii ya barabara Tanzania nzima. Kwa kweli nakubali mimi niko kwenye Kamati ya Miundombinu, tunampongeza Mheshimiwa Magufuli kwa kazi anayoifanya, anafanya kazi nzuri sana na kwa kasi hii

97 anayokwenda nayo na mwenendo huu basi ananipa matumaini kwamba, na mimi siku moja barabara yetu ile ya kutoka Nangurukuru–Liwale kabla hajastaafu anaweza akawa ametupatia lami. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo nirudi wilayani kwangu nilikotoka Liwale. Wilaya ya Liwale ina barabara kuu mbili; barabara moja ni ile ya Liwale– Nachingwea yenye urefu wa kilomita 135 na ya pili ni ile ya Liwale–Nangurukuru ambayo ina urefu wa kilomita 231. Barabara hizi zinaangaliwa na ndugu zangu wa TANROADS. Napenda nichukue nafasi hii kumtaarifu Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, katika barabara ya Liwale– Nachingwea napenda nimtaarifu Mheshimiwa Waziri kwamba, nimeridhika kabisa na matengenezo ya kilomita 30 za barabara kutoka Liwale Mjini mpaka eneo moja linaloitwa Mtawatawa. Lakini sijaridhika na matengenezo au uchongaji uliofanywa katika barabara hii ya Liwale-Nachingwea katika eneo la kutoka Mtawatawa–Nangano. Sijafurahishwa kabisa. Barabara ile imechongwa below standards, na hailingani na value for money. Kama inawezekana Mheshimiwa Waziri anisaidie Wakandarasi wale waliotengeneza kipande kile cha kutoka Mtawatawa hadi Nangano warudie kuchonga upya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna utaratibu wa kuchonga barabara hasa katika Wilaya yangu wakati Mwenge unakaribia kufika. Mafungu yaliishatolewa muda mrefu. Kama barabara hii ya Liwale-Nachingwea bajeti yake ya 2011/2012 iliishatolewa Julai, lakini barabara hii

98 haikuchongwa mpaka mwezi uliopita ikiwa imebakia wiki moja au siku kama tatu, nne hivi Mwenge unaingia wilaya ile ndiyo Magreda yanachonga. Ni kwanini wakati bajeti iliishapitishwa na karibu sasa ni mwaka mzima na mafungu yake yaliishakwenda? Tunategemea nini barabara zinapochongwa tunaposikia Mwenge unakuja? Kwa vyovyote haziwezi kuchongwa katika standard inayotakiwa.

Mheshimiwa Spika, mimi namuomba Mheshimiwa Waziri awape maelekezo watu wa TANROADS waliangalie hili. Kama mafungu yametoka ni vyema kazi ile ifanywe mapema. Hayo nimeyashuhudia mwenyewe mwezi uliopita, Mwenge unapita kesho na barabara inachongwa mpaka leo usiku saa mbili. Hii siyo sahihi.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Liwale– Nangurukuru. Barabara hii ilitengewa fedha mwaka 2011/2012. Ni kweli barabara ile imechongwa kutoka Nangurukuru mpaka mpakani mwa Wilaya ya Kilwa na Liwale. Mpaka naondoka huko kutoka mpakani mwa Kilwa na Liwale mpaka kufika Liwale Mjini barabara ile haijachongwa hata mara moja na mafungu yake ya 2011/2012 yalishapangwa. Barabara ina mashimo makubwa yanayofanana na mahandaki. Hata wewe ukifika utaona huruma. Mheshimiwa Waziri wa Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto, atakuwa shahidi kwani alipita katika barabara hii mwezi mmoja uliopita na alinikuta kule na ameshuhudia hali mbaya ya ubovu wa barabara ile. Namwomba Mheshimiwa Magufuli awape maelekezo watu wa TANROADS

99 wafike mahali pale na washuhudie ubovu wa barabara zile.

Mheshimiwa Spika, sasa niongelee barabara ya Liwale–Kingupira. Mwaka 2010 Mheshimiwa Rais alipotembelea Jimbo hili alitoa ahadi kwamba, wananchi wale watajengewa barabara kutoka Liwale mpaka Kingupira. Sasa hivi ni miaka miwili tangu ahadi ile imetoka, ni kwa nini utekelezaji haujaanza wakati Mheshimiwa Rais yeye alishasema? Nafikiri kwamba kinachofuatia sasa ni utekelezaji, lakini bado tuko kwenye losgistics, barabara hii bado inazungumziwa simply kwa sababu imepitia kwenye hifadhi ya Selous haiwezi kujengwa mpaka wadau wote wa Hifadhi ya Selous waafikiane.

Mheshimiwa Spika, juzi UNESCO imekubali kuimega Selous Game Reserves upande wa Kusini kwa ajili ya machimbo. Kuna tatizo gani sasa na sisi kupatiwa kibali sasa barabara hii ikaanza kujengwa? Napata mashaka huu ni mwaka wa pili, utafika mwaka wa tatu na utakapofika mwaka wa nne barabara ile haijajengwa nitarudi kuwaambia nini wananchi wale kuhusu barabara hii? Nitasema nini au Serikali itasema nini kuhusu ile barabara ya Liwale–Kingupira? Namwomba Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi atakapofanya majumuisho yake...

(Hapa kengele ililia kuashiria kwisha kwa muda wa mzungumzaji)

MHE. FAITH M. MITAMBO: Mheshimiwa Spika, asante, naunga mkono hoja. (Makofi)

100

SPIKA: Ahsante. Sasa nimwite Mheshimiwa Stephen H. Ngonyani, Mheshimiwa James Mbatia ajiandae na pia Mheshimiwa Rajab Mbarouk Hemed ajiandae. Siyo saa hizi!

MHE. STEPHEN NGONYANI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru sana. Kwanza nakupa pole kwa msiba uliokukuta Mungu akuzidishie na Mungu amrehemu kwa sababu amefiwa na nyanya, kwa hiyo Mungu amzidishie.

Mheshimiwa Spika, kwanza nimshukuru sana Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi kwa kazi nzuri ambayo anaifanya, mimi binafsi nampongeza sana. Pili, vile vile niwashukuru wananchi wangu kwa uvumilivu mkubwa walioupata kule Jimboni kwa wakati huu mgumu nikiwa hapa Bungeni kwa ajili ya kutetea maslahi ya wananchi wangu. Nisiache kumshukuru Meneja wa TANROAD wa Mkoa wa Tanga, mara nyingi sana inapotokea matatizo ya barabara, ukimpigia simu anatokea haraka na kumpigia contractor na kuanza kuzitengeneza zile sehemu ambazo zinakuwa na usumbufu wa hali ya juu sana.

Mheshimiwa Spika, sasa nirudi kwenye mada yangu. Katika Mkoa wa Tanga tunashukuru wametufanyia kazi nzuri sana. Tulikuwa tuna malalamiko ya kutoka Tanga kupitia Segera kuja Chalinze. Nashukuru ile barabara sasa hivi inatengenezwa na inatengenezwa vizuri na contractor pale ni mzuri hata wananchi wenyewe wamefurahia. Vile vile nimshukuru Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi kwa

101 kutengeneza barabara ya kutoka Korogwe kwenda Same. Barabara hii ilikuwa kilio kikubwa sana cha wananchi wa Mikoa miwili Tanga na Kilimanjaro. Sasa ujenzi umeanza, kwa hiyo, naamini kabisa kwamba barabara hii itajengwa vizuri kama zinavyojengwa sehemu nyingine.

Mheshimiwa Spika, ila kuna barabara zilizozunguka katika Jimbo langu la Korogwe Vijijini. Kuna barabara ya changarawe ya kutoka Old Korogwe kupitia Mnyuzi na kwenda Maguzoni ambayo inaunganisha na Wilaya ya Muheza. Hii barabara kwa kweli ni barabara ya mkoa, lakini kuna daraja lililopo pale Lwengela wakati wowote linaweza kukatika na likaacha kuunganisha Wilaya hizi zote mbili kwa sababu lile daraja limekuwa katika hali mbaya. Vile vile kuna kipengele, kuna sehemu ya kutoka Kwagunda kwenda Gereza. Mkandarasi aliyotengeneza lile eneo ni eneo baya sana, ikinyesha mvua hakuna usafiri wa aina yoyote. Kuna eneo la kutoka Mnyuzi kwenda Maguzoni hapo katikati napo kuna sehemu ambayo Mkandarasi hajafanya kazi nzuri, ikinyesha mvua wananchi wangu wanapata shida kubwa sana.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa eneo langu ni sehemu kubwa kuna barabara ambayo inatoka Old Korogwe kwa kupitia Magoma na kutokea Malamba na kwenda kutokea Mombasa na kuunganisha Mji wa Tanga. Barabara hii imejengwa kwa kiwango cha changarawe, namshukuru sana Meneja wa TANROAD ameisimamia sana barabara hii, lakini kuna sehemu ambazo ni nyeti ambazo ikinyesha mvua leo, hata

102 mimi mwenyewe niliwahi kutaka kubebwa na maji katika barabara hiyo.

Mheshimiwa Spika, tatizo ni dogo sana, kuna sehemu ambayo wamelima mkonge, mwenye mkonge ametaka alipwe fidia kidogo watengeneze mfereji mkubwa wa kuvusha maji sehemu ya Magoma, Makorora na sehemu hiyo mpaka leo hii imekuwa ni tishio kubwa. Barabara inaweza kuwa nzuri kwa mwaka, ikinyesha mvua tu, barabara hiyo inakuwa imeharibika. Kuna sehemu ya kutoka Magoma kwenda Kulasi, hii sehemu mara kwa mara inakuwa na mafuriko. Kwa hiyo, namwomba Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi kama kuna uwezekano Serikali itenge fedha kwa ajili ya kupandisha kifusi ili yale maji yanayotoka milimani kwa jirani yangu Mheshimiwa yasiwe yanabeba barabara na kuiharibu. Hili ndilo eneo kubwa linalosafirisha mkonge na wakulima wengi wanaolima mahindi na mazao mengine ya chakula na biashara ndio wanaotumia barabara hii.

Mheshimiwa Spika, nisisahau kulia kilio changu cha barabara zile zinazounganisha wakulima wa chai. Barabara za kutoka Korogwe kupitia Dindila kwenda Bungu na kupitia Vugili kwenda Bungu na kutokea Dindila. Hii barabara naomba ipanuliwe, matengenezo yake kwa kweli hayaridhishi. Ni barabara ndogo kiasi ambacho hata mtu wa mguu akitembea akiona gari hapo kwa hapo inaweza kumletea madhara makubwa na wakati wa mvua barabara hiyo haipitiki. Huko kuna viwanda vikubwa viwili vya chai; kuna Kiwanda cha Ambangulu na

103 Kiwanda cha Kunga ambavyo vinatengeneza chai nzuri na bora. Nafikiri hata wewe mwenyewe Mheshimiwa Spika, ni mkulima wa chai, unajua.

Mheshimiwa Spika, kuna barabara ya kutoka Mombo kwenda Mzeri kupitia Handeni. Barabara hii kwenye eneo la Liverpool kutokea Uwanja wa Ndege sehemu hii kwa kweli hairidhishi. Ma-contractor wanaotengeneza barabara ikifika wakati wa mvua Mto wa Mkomazi ukimwaga maji hakuna usafiri na ni sehemu ambayo kuna mifugo, kuna wakulima wengi ikifika wakati wa mvua za masika basi barabara hizi hazipitiki. Sasa inakuwa watu wanakaa mpaka maji yapite au watu wanakwenda pale kwa kutumia mitumbwi. Naomba barabara hii ya kutoka Liverpool kutokea Uwanja wa Ndege ikitokea Mzeri Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi aiangalie sana kwa sababu vile vile ni eneo la biashara kwa wale wakulima wadogo wadogo.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri ana ma- contractor wazuri sana ambao wanatengeneza barabara zetu, lakini naomba vile vile awaangalie wajasiriamali. Kuna vijana ambao wanahitaji kupata kazi katika maeneo yale, inakuwa ni ngumu sana kwa baadhi ya Ma-contractor wakishapata kazi wanawatumia watu kutoka sehemu nyingine wale wenyewe walengwa wanaachwa pale. Hata kuchanganya kokoto pia ukamlete mtu kutoka eneo lingine! Naomba pia hili liangaliwe.

Mheshimiwa Spika, kuna ma-contractor wameshabomoa maji kwa mfano, pale Hale sasa hivi

104 wana mwaka mzima na nusu hawajapata maji. Lakini walitengeneza wakaahidi kwamba maji yale watayatengeneza, wananchi wa Hale wanalia mpaka kudai kwamba Mbunge huyu hatufai. Sisi tuliahidiwa kwamba mabomba ya maji yaliyotengenezwa yatatengenezwa lakini mpaka leo hii hakuna yaliyotengenezwa. Naomba Mheshimiwa Waziri awafuatilie hawa Ma-contractor zile sehemu ambazo zimebomolewa basi waturudishie ili wananchi wapate maji safi. Watu wanapata kipindupindu kwa hali ya juu sana.

Mheshimiwa Spika, kuna barabara ambazo zimesahauliwa kabisa kutoka Malamba kwenda kwa wachimba madini kule Kararani mpaka Kigwasi. Hii barabara haikumbukwi na Halmashauri wala na Serikali na ndiko sehemu ambazo wakulima wengi na wachimba madini wako hapo. Naiomba Serikali iangalie barabara hii. Naomba fidia kwa hao ambao wanapitiwa na hizi barabara ambao barabara zinawafuata wenye nyumba. Kwa mfano Handeni, Korogwe, Mombo, Mazinde, Makuyuni na Korogwe Mjini. Naomba hawa watu kama kuna fidia yao inayohitajika kulipwa naomba Mheshimiwa Waziri yeye ni mstaarabu sana wala hana haja ya kusumbuliwa sana, naomba walipwe. Wananchi kule wanasikitika, kuna wengine wamelipwa na wengine hawajalipwa na ukizingatia eneo ni hilo hilo moja sasa wanajiuliza mbona mwenzangu amepata na mimi sijapata, naomba Mheshimiwa Waziri aliangalie.

Mheshimiwa Spika, kuna barabara ya kutoka kwa Shemshi kwenda Bumbuli kutokea Soni, barabara ya

105 kiwango cha lami. Naomba Serikali iniambie hii lami itawekwa lini kwa sababu ndani ya Ilani ya Uchaguzi ipo lakini safari hii kwenye makabrasha sijaiona kabisa. Naomba hii barabara ni muhimu sana kwa wakulima wa hiliki.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja asilimia mia kwa mia. Ahsante sana. (Makofi)

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipatia nafasi hii. Nami niungane na wengine nikupe pole kwa msiba uliokufika kwa Waziri Wassira na yule Mbunge rafiki yetu wa Zanzibar, yote ni mapenzi ya Mwenyezi Mungu.

Mheshimiwa Spika, kwenye hoja hii ya Waziri wa Ujenzi, kwanza, nianze kwa kusema kwamba fedha zilizotengwa kwa ajili ya Wizara hii shilingi trilioni 1.023 kwa makusudio yaliyowekwa ni fedha kidogo sana. Kupanga ni Kuchagua. Watanzania wanachohitaji kuona ni barabara zipitike, barabara zenye kiwango kizuri, barabara zinazounganisha mikoa yote kwa lami. Bajeti ya Waziri inaonesha kwamba, Mikoa ya Tanzania itaunganishwa yote na Miji Mikuu ifikapo mwaka 2017/2018, miaka mitano kuanzia sasa. Nashauri ingekuwa ni bora basi akasema mwaka huu wa fedha mikoa hii itaunganishwa, mwaka huu mikoa hii itaunganishwa ili ieleweke ionekane kabisa kwamba ifikapo mwaka 2017 Tanzania yote itakuwa imeunganishwa na ndipo tutapata maendeleo endelevu.

106 Mheshimiwa Spika, mfano Mkoa kama wa Kigoma barabara hii inayozungumzwa sana ya Kidahwe-Kasulu kupita Kibondo-Kakonko mpaka Nyakanazi. Ni kweli barabara hiyo yenye kilomita 310 kuitengea shilingi bilioni tatu ni kama unapoteza tu hizi fedha, niwe mkweli kwa sababu kwenye mtindo wa ujenzi huwa haikubaliki au barabara ya kutoka Kibondo kwenda Mabamba kilomita 35. Ukiangalia ya Kasulu, unakwenda mpaka Buhigwe unakwenda mpaka Manyovu huioni ambayo inaunganisha na Burundi ambayo ingeleta maendeleo ya haraka katika Mkoa wa Kigoma, ni tatizo.

Mheshimiwa Spika, barabara ya kutoka Kidahwe kwenda Uvinza kilomita 76.6, lakini ukiangalia ile ya Mto Malagarasi unaunganishaje na mkoa wa Tabora ufike Kaliua mpaka Urambo kwa Mheshimiwa mpaka ufike Tabora Mjini. Utakuta kwamba barabara hizi tusipozipa kipaumbele na hasa mikoa ile ambayo inazalisha kwa dhati hatutafanya kitu. Kwa mfano Mkoa wa Katavi, wanapozungumza kutoka Namanyere kwenda Kirando au kutoka Namanyere kwenda mpaka Wampembe kwenda mpaka Kala kuunganisha na nchi ya Burundi kuna matatizo makubwa. Sasa uzalishaji unaweza ukafanyika namna gani? Wanaunganisha Katavi Bonde la Ufa alipozungumzia Mbunge wa Kwela huku Kilyamatundu, Mto Wisa, Muze mpaka ukafika Kibaoni utakuta kwamba barabara hizi zikiunganishwa maendeleo yatapatikana kwa haraka na kuunganishwa na Mkoa wa Rukwa.

107 Mheshimiwa Spika, matatizo haya tutaweza tukiamua kama Taifa na kwa kuwa wote wanaona umuhimu wa kuipongeza Wizara hii na kazi nzuri inayofanyika ni bora kama Taifa tukakubali hata kama ni kukopa kwa muda fulani na tukajua kwamba ni deni la Taifa lakini linaleta maendeleo endelevu kwa Taifa letu la Tanzania. Ziko nidhamu katika fani ya ujenzi kuangalia ukubwa wa project yenyewe, lakini kuna pembe tatu ya time, cost and quality. Sasa tukizingatia suala la time, cost and quality na inazunguka yenyewe, unapokosa fedha time inazidi kwenda na time inazidi kwenda na value of money kwa wakati huo inakuwa ni tatizo. Kwa hiyo, unakuta kwa mfano, bajeti ya mwaka huu zile fedha zaidi ya shilingi bilioni 150 ni za kulipa madeni. Kwa hiyo, utakuta tutazungumza na bajeti hii imeandikwa kwa kirefu, Wabunge watafurahi, lakini hatutaona chochote cha maana mwisho wa mwaka kitakachotokea katika Taifa letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna dhana inayojitokeza kwamba na niongee kabisa kwa kitaalam kuna classification theory. Kuna dhana inayojitokeza kwamba kuna Mikoa ya Kaskazini imepata upendeleo sana, napingana kabisa na dhana hii. Napingana na dhana hii kwa makusudi kabisa kwa sababu kwa fact ukiangalia mikoa hii barabara nyingine kwa mfano ile The Great North Road kutoka Cairo Misri mpaka Cape Town ambayo inapitia Mombasa huko ije itokee mkoa wa Kilimanjaro iende Babati ije ifike Dodoma iende mpaka Iringa iende Kusini.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia leo hii kuanzia Mkoa wa Manyara na Dodoma haujaunganishwa na hii

108 barabara, iliyokuweko ilikuwa ni ya asili. Sasa mikoa hii hasa mkoa kama wa Kilimanjaro barabara hizi zilikuweko nyingine kabla hata wakati wa ukoloni. Sasa kitu kinachotakiwa kufanyika hapa ni kufanya routine maintenance ili barabara hizi ziendelee kupitika wakati una upgrade barabara nyingine kutoka Class B kwenda Class A. Ni dhana kama alivyoongea Mbunge wa Peramiho.

Mheshimiwa Spika, kwenye kufanya routine maintenance unatakiwa uanzie Songea kwenda Njombe kwa sababu hii ya Njombe ni vizuri zaidi iko kwenye Class A, inabidi iendelee kuwa maintained kwenye Class A wakati ile nyingine inakuwa upgrade kwenda kwenye Class B na nyingine iendelee mpaka Class A. Sasa tukikubaliana kwamba kwenye classification theory ya barabara zetu hasa kwenye routine maintenance itatusaidia sana katika kuhakikisha barabara zote ambazo ziko kwenye hali nzuri zinaendelea kuwa kwenye hali nzuri na zile barabara nyingine tunaendelea ku-upgrade mwaka kwa mwaka na zionekane.

Mheshimiwa Spika, nimesoma kwenye bajeti imeandikwa vizuri tu, lakini vile vile hata lugha huku nyuma kwenye majedwali ukiangalia legend barabara hizi kuna Kiingereza, Kiswahili sijui ni watu wangapi wenye taaluma ambao wanaweza wakaisoma na wakaielewa vizuri kwenye michoro hii ya huku mwisho. Imeandikwa kwenye engineering zaidi perspective labda kwenye knowledge ambayo ni ya juu zaidi kuliko watu ambao wako kwenye fani hiyo. Ni nzuri sana,

109 lakini nishauri basi wakati ujao tuhakikishe kwamba tunaifanya iliyo bora zaidi.

Mheshimiwa Spika, ili barabara hizi zijengwe vizuri hatuwezi tukasahau usafiri wa maji na usafiri wa reli. Kwa mfano, ukanda wa bahari ya Hindi wa Tanzania una kilomita 1,424. Jiji la Dar es Salaam linaweza likafanya usafiri wa maji ambao ndio ulio rahisi kuliko wote kuanzia Bagamoyo kuja katikati ya mji. Tunaweza tukafanya usafiri wa reli vile vile katika Jiji la Dar es Salaam na pia usafiri wa barabara. Linalotokea Dar es Salaam leo hii ni janga na kwa kuwa janga wakati wote tunafanya kazi kama team work hakuna wa kumlaumu mwenzake.

Mheshimiwa Spika, nimesikia hapa Bungeni Wabunge wote kwa vyama vyote wanazungumzia Jiji la Dar es Salaam, sasa kwa kuwa hili ni janga basi litafutiwe immediate solution na immediate solution itapatikana kwa Waziri wa Ujenzi, Mawasiliano, Ulinzi, Mambo ya Ndani na Utawala Bora. Wakae as a team chini ya Waziri Mkuu kuondoa tatizo la Jiji la Dar es Salaam na solutions zipo nyingi tu. Tusikilizane ili tatizo la Jiji la Dar es Salaam liweze kuondoka. Hili ni tatizo kubwa sana kwa sababu kwa mwaka mmoja Jiji la Dar es Salaam tunapoteza zaidi ya shilingi trilioni 1.46 kwa ajili ya muda unaopotea barabarani na kwa ajili ya msongo wa mawazo watu wanaoupata, mafuta tunayochoma na uchafuzi wa mazingira, hili ni janga na janga halisubiri kesho, inabidi tulifanyie kazi leo na sio kesho.

110 Mheshimiwa Spika, haya yote yakiweza kufanyika, nitatoa mfano, kwa mfano, wakati wa mafuriko mwezi Desemba mwaka jana. Ilionekana kwamba tatizo la mafuriko ni la Polisi la hasha sio Mapolisi. Mtu kama afande Kova mpaka saa 7.00 za usiku halali au ile tarehe 11 ilivyotokea tishio la tetemeko kule Indonesia kwamba Dar es Salaam yote ingeondoka liliachiwa Askari Polisi peke yao na hasa yanapotokea matatizo ya namna hii.

Mheshimiwa Spika kwa sababu ya muda nashukuru kwa kunipa fursa ya kuzungumza. ahsante sana. (Makofi)

SPIKA: Hii hadithi ilikuwa tamu, lakini ndio muda umekwisha.

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMED: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nami nimshukuru Mwenyezi Mungu ambaye amenijalia leo hii kuweza kusimama na kueleza mchango wangu katika Wizara hii. Kwanza nataka ku-declare interest kwamba mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Miundombinu, nafikiri Mheshimiwa Magufuli ananifahamu.

Mheshimiwa Spika, nataka nianzie katika Bodi ya Mfuko wa Barabara. Nimpongeze sana Mwenyekiti wa Mfuko wa Barabara, baba yangu, mzee wangu Mheshimiwa Wanyancha. Lengo la kumpongeza Mzee wangu Wanyancha ni namna anavyofanya kazi ili kuhakikisha huu Mfuko unaboreka. Lakini zaidi ya hilo nimpongeze kwa namna ambavyo waliweza kukabiliana na mafuriko ambayo yalikuja kuikumba

111 nchi na wao kama Mfuko huu waliweza kutoa zaidi ya shilingi bilioni 19 katika kudhibiti janga lile, kwa kweli kwa hili nataka nimpe pongezi kubwa.

Lakini vilevile kwa makusanyo, makusanyo yake yanaonekana yanakwenda vizuri na yanaelekea pazuri ila nataka niseme kwamba makusanyo haya bado hayajakidhi haja. Makusanyo ambayo anayakusanya hayawezi kuzidi kutengeneza barabara zetu kwa zaidi ya asilimia 50. Kwa hiyo bado tuna upungufu wa asilimia 50 ambazo zinatakiwa zijazwe kwa ajili ya matengenezo ya barabara zetu. Sasa kuna maombi, maelezo na changamoto ambazo wao kama Bodi naamini kwamba wameshazipeleka hata Serikalini na nina uhakika kwamba pengine na Waziri naye anazifahamu.

Mheshimiwa Spika, tumeamua kama nchi kuweka tozo au kuondoa ushuru katika mafuta ya taa kwa sababu mbili moja kuweza kudhibiti uchakachuaji wa mafuta, lakini la pili kusaidia katika ule Mfuko wa Barabara. Sasa hapa tumesahau sehemu ya tatu ya kwamba tunawaumiza wananchi maskini.

Mheshimiwa Spika, kwa kweli binafsi yangu nahisi Serikali sasa hivi, muda wa kufikiri upya katika suala la mafuta ya taa umefika. Tumeshatumia mwaka mzima tumejua namna gani athari iliyotokea kutokana na kupandisha kodi katika mafuta ya taa hususan kwa kuwaondolea ile kodi wale wananchi. Wananchi wengi hasa vijijini wanaumia sana kwa suala la mafuta ya taa. Wananchi hawa wanafikia hadi kutumia simu zao

112 za mkononi kutokana na kushindwa kupata mafuta kwa ajili ya kuweka katika vikoroboi vyao.

Mheshimiwa Spika, nina mfano mdogo kule kijijini kwangu, wapo wanangu.

SPIKA: Mheshimiwa Mbarouk ujielekeze kwenye barabara.

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMED: Nakwenda huko, utaifahamu point yangu.

SPIKA: Ngoja kwanza kidogo. Kwa sababu dakika zako ni kumi inaonekana unazungumzia mambo ya energy itakuja wakati wake. Wewe sema barabara, sasa hayo mafuta yanahusianaje.

MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMED: Mheshimiwa Spika, ahsante. Lakini naamini point yangu wataifahamu. Hivi sasa hivi kuna Makampuni zaidi ya matano ya uchimbaji wa madini yanatuharibia barabara. Hawa hawalipi katika Mfuko wa Barabara, kampuni zote tano hizi zinalipa only one billion katika Mfuko wa Barabara na nitazitaja hapa. Hawa kwa mujibu wa hesabu au utafiti uliofanywa na wenyewe watu wa Road Fund, hawa wanatumia lita 133 milioni kwa mwaka, vipi leo tukawatoze wananchi kodi, tukawaumize wananchi katika mafuta ya taa wakati fedha hizi zipo?

113 Mheshimiwa Spika, nilikuwa najenga hoja yangu. Kwa hiyo, hili ni suala la kulifikiria upya. Haya makampuni lazima yalipe. Haya ndiyo ambayo yanaharibu barabara. Kwa mujibu wa utafiti walitakiwa wailipe Serikali 26.6 billion per year. Leo wanalipa only one billion, 25.6 billion tunawachia, tunakwenda kuwakamua wananchi kwenye mafuta ya taa. Kwa kweli lazima tukae tufikiri upya.

Mheshimiwa Spika, haya mapendekezo walishayatoa kwamba, haya makampuni jamani msiyaachie, tuna Bulyang’hulu, Geita, Talawaka, North Mara, Williamson, wanatumia barabara, wanapitisha magari, wanachukua michanga, wanapeleka Tanga wanatuharibia barabara. Kwa nini walipe fedha kidogo na sisi tuendelee kuwakamua wananchi? Kuna watoto wangu kule katika Kijiji cha Lusi katika Kata ya Ludoyasambu, Arusha kule. Mimi nina watoto kule kwa sababu unajua hawa ni wanangu wote, Ole Medeye, Ole Telele unaanzia na Ole, mimi ndiyo baba yao, kwa hiyo kule mimi nina watoto kule. (Kicheko)

Mheshimiwa Spika, sasa nijielekeze katika Vyuo vya Ufundi. Tuna Vyuo viwili ambavyo vinasimamiwa na Wizara hii. Tuna Chuo cha Appropriate Technology Institute kilichopo Mbeya na kile ambacho kiko Morogoro. Nimwombe Mheshimiwa Waziri, Mzee wangu Mzee Muhegi anajitahidi sana katika ile Bodi yake ya Usajili wa Makandarasi na hapa tunazungumza suala la Makandarasi wazawa. Hebu Serikali ijaribu kuelekeza macho yake pale. Hivi vyuo mbali ya kusaidia baadhi ya watu kupata ajira, lakini

114 vile vile vina uwezo wa kutoa wataalam ambao watasaidia kuboresha barabara za vijijini.

Mheshimiwa Spika, tunaweza tukawachukua hawa vijana tukawapeleka katika Halmashauri wakaweza kusaidia matengenezo madogo madogo ya barabara. Tena Serikali itakapokuja kupata uwezo mzuri tutakuja kuendeleza. Nafikiri kuna haja ya kuviangalia vizuri na kuwaongezea bajeti yao hawa na hivi vyuo kuvitafutia mitaala ambayo inakwenda na wakati wa sasa ili tuweze kupata at least wataalam ambao wataweza kusaidia katika vijiji vyetu.

Mheshimiwa Spika, nizungumzie Wakala wa Majengo (TBA). TBA wanalalamika kwamba mtaji wao ni mdogo wanahitaji mikopo, lakini tatizo ambalo nawaambia TBA hawajataka kuwa wazi. Mheshimiwa Waziri tunaomba TBA wawe wazi. Sisemi hivi kwa ajili ya mgogoro wangu mimi na wewe, hapana ,leo hapa haupo, lakini naomba TBA uiangalie upya. TBA imefanya kazi nzuri na tumeona pale Dar es Salaam na wanaendelea kufanya kazi nzuri katika baadhi ya Mikoa, wanafanya kazi sawa na makampuni mengine ya binafsi, it means faida wanapata. Hebu hii faida sasa waelekeze kunakohusika hasa katika kujiendeleza.

Mheshimiwa Spika, naomba nimalizie kwa TANROAD. Kuna mchangiaji mmoja hapa aliwahi kuzungumza hapa TANROAD inafanya vizuri sana hususan katika udhibiti na nidhamu ya matumizi na kwa fedha zao wamefikia wanaiweka Benki kiasi ya kwamba wanapata faida kubwa. Naomba Mheshimiwa Waziri utakapokuja hapa utueleze

115 TANROAD fedha hizi ambazo mara nyingi wanaweka CRDB na zinazaa yaani wanapata riba, je, riba ile wanaitumiaje? Je, riba ile inasaidiaje katika barabara zetu au riba ile inapata Mamlaka kutoka kwa nani iweze kutumiwa?

Mheshimiwa Spika, ahsante. (Makofi)

SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa.

MICHANGO KWA MAANDISHI

MHE. ALLY K. MOHAMED: Mheshimiwa Spika, tangu mwaka 2011 nilizungumzia kipande cha barabara cha kilometa saba toka Kipili mpaka bandarini. Hakuna barabara ya kufika bandari ya Kitili kwenye maelezo ya Waziri. Katika bajeti ya mwaka 2011/2012 Waziri alieleza kuwa watashughulikia katika bajeti ya mwaka 2012/2013, lakini hakuna kilichoonekana katika hiyo bajeti, na Serikalii imetoa Shilingi milioni 800 kujenga hiyo bandari ya Kipili ambayo haifikiki na magari.

Mheshimiwa Spika, vijiji vifuatavyo havina barabara, gari kwao ni ajabu. Vijiji hivyo ni kama ifuatavyo: Izinga, Lusembwa, Mwinza, L’yapinda, Msamba, Kisamba, Katete, Chongo, Isaba, Kazovu, Mpenge, Kachui, Mkombe na Kalila.

Mheshimiwa Spika, Kijiji cha Kalila, ipo barabara ya Kabwe – Korogwe; Katika Kijiji cha Izinga, ipo barabara ya Kirando – Kipili, barabara ya Wampembe ambayo ni mbaya sana, Barabara ya Kala ambayo pia ni mbaya sana na Kijiji cha Kasanga pia ipo barabara.

116

Mheshimiwa Spika, sehemu nyingine zote zilizobaki, nilizotia alama katika mchoro wangu katika mchango wangu wa maandishi, havina kabisa barabara na Halmashauri haina uwezo kabisa.

Mheshimiwa Spika, wananchi huwa wanatumia mitumbwi kufika sehemu za barabara, lakini Ziwa Tanganyika kila mara huwa linachafuliwa kwa upepo na inakuwa taabu sana mpaka hata kusababisha akina mama wajawazito kufa njiani na maharamia kuvamia vijiji hivyo watakavyo.

Mheshimiwa Spika, pia Serikali kwa ujumla haina habari kama kando ya Ziwa Tanganyika kuanzia Kigoma mpaka Kasanga hakuna Vijiji mwambao mwa Ziwa Tanganyika. Kuachia Halmashauri kujenga hizo barabara ni sawa na kumwachia mlala hoi ajenge nyumba ya ghorofa kumi wakati hata pesa za kununulia bati moja hana.

Mheshimiwa Spika, vijiji vilivyopo mwambao mwa Ziwa Tanganyika havina barabara kabisa, navyo ni Kazovu, Isaba, Chongo, Katete, Kisambala, Ninde, Izinga, Mkombe, Mwinza, Lusembwa na Kalila – Mpenge. Hivyo, ni katika Wilaya ya Nkasi, tu na Halmashauri haiwezi kabisa kuzijenga hizo barabara; pia ni sehemu nyeti kwa ulinzi wa nchi hii maana kila mara Vijiji hivi vinavamiwa na maharamia toka DRC Congo.

MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuunga mkono bajeti hii ya Wizara

117 ya Ujenzi kwa asilimia mia moja. Napenda kumpongeza Waziri wa Ujenzi kwamba kwenye Mkoa wa Tanga kuna barabara nyingi ambazo zimetengenezwa na sasa zinapitika wakati wote wa mvua na kiangazi.

Mheshimiwa Spika, namshukuru Mheshimiwa Waziri kwa kutengeneza barabara kutoka Segera kupitia Mombo Mkomazi, amesikia kilio cha wananchi wa Korogwe vijijini. Kuna barabara kutoka Korogwe kwa Semangube kupitia Vugiri na kutokea Bungu. Hii barabara huwa inasahaulika sana. Kuna barabara ya kutokea Bungu kutokea Lutindi kupitia Msambiazi, hii barabara wakati wa masika inakuwa na shida kubwa sana ya kupitika. Naomba barabara hii iangaliwe kwa macho yote.

Mheshimiwa Spika, kuna barabara kutoka kwa Shemshi kupitia Dindira kwenda Bungu. Barabara hizi hupitika kwa muda mfupi. Ikinyesha mvua huwa hazipitiki. Vile vile barabara ya kutoka Korogwe – Magoma –Mashewa - Maramba kutokea Tanga, kuna sehemu chache ikitokea mvua magari hayawezi kupita.

Mheshimiwa Spika, mwisho, barabara ya kutoka Old Korogwe Road kupitia Bumbuli na kutokea Soni, ilikuwa ijengwe kwa kiwango cha lami. Je, barabara hii itaanza kutengenezwa lini? Naomba kutoa shukrani zangu za dhati kwa manager wa TANROAD (M) Tanga kwa kufuatilia ujenzi wa barabara zote za Mkoa wa Tanga.

118 Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. VINCENT J. NYERERE: Mheshimiwa Spika, napenda kushukuru sana kwa kupata nafasi ya kuchangia japo kwa maandishi. Nisingependa kuongelea mambo mengi sana ambayo Wabunge wenzangu wameyaongelea, isipokuwa napenda tu kujikita katika maeneo machache ambayo nadhani ni vizuri wakati Mheshimiwa Waziri anahitimisha, basi ayatolee ufafanuzi.

Mheshimiwa Spika, TEMESA bila kuijengea uwezo kivifaa, mabadiliko ya teknolojia na mafundi, bado, hata tukiwapa fedha nyingi, impact haitaonekana. Tukumbuke malalamiko makubwa ya wananchi wetu ni kuhusu matumizi makubwa ya gharama au fedha za umma katika ununuzi wa magari na matengenezo yake.

Mheshimiwa Spika, Magari ya Serikali karibu yote, yamekuwa yakipelekwa kufanyiwa matengenezo katika karakana (Garage) binafsi ambapo mbali na kukiuka Sheria ya Manunuzi ambayo imetungwa na Bunge lako Tukufu, pia bei ya vipuri na matengenezo imekuwa kubwa sana na wajanja wachache wenye uchu wamekuwa wakijipatia fedha nyingi sana kutoka eneo hili na kuisababishia Serikali kupata hasara kubwa katika utengenezaji wa magari na mitambo ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, kama kitengo hiki cha TEMESA kikipatiwa uwezo wa kifedha, vifaa na mafunzo ya mara kwa mara kwa wataalam wake, kwa kuwa na teknolojia ya magari na mitambo hubadilika haraka

119 sana, basi tutaokoa fedha nyingi sana ambazo tumekuwa tukizitoza kwa kupeleka magari na mitambo ya Serikali kwenye karakana binafsi.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kuishukuru Serikali kwa kujenga maegesho ya kivuko na kununua kivuko cha Mv. Musoma ambacho ni hivi karibuni tu kimeanza kufanya kazi, japo zipo changamoto ndogo ndogo ambazo ni eneo la kusubiria wasafiri wakati wa mvua kubwa au jua au choo na maegesho ya pikipiki na magari kwa wale ambao wanatumia kivuko hicho cha Mv. Musoma kinachohudumia katika Wilaya ya Rorya (Kinezi) na Musoma Mjini (Mwigobero).

Mheshimiwa Spika, pia napenda tena kutoa shukrani kwa Serikali kwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara (Kwangwa) ambayo sasa inaitwa Mwalimu Nyerere Medical Centre.

Mheshimiwa Spika, barabara inayopita hospitali hii inaunganisha Wilaya ya Musoma Mjini na Musoma Vijijini, tungependa sasa katika kipindi hiki ambacho hospitali hii ingejengwa, basi na barabara inayopita katika hospitali hii ikawa chini ya TANROAD na ikawekewa lami kwa ajili ya kurahisisha huduma ya kupeleka wagonjwa ikawa ya haraka zaidi pale itakapokuwa imejengwa kwa kiwango cha lami hata kama ni lami nyepesi (water seal).

Mheshimiwa Spika, vile vile ningependa Mheshimiwa Waziri awasiliane na Mkandarasi anayejenga barabara ya Nyanguge Musoma, basi

120 maeneo ya utekelezaji katika eneo la Musoma Mjini lifanyiwe kazi haraka, kwani sasa imeanza kuwa kero ukizingatia kwamba Mkandarasi amechukuwa muda mrefu sana na barabara iingiayo na kutoka Musoma Mjini ni moja peke yake.

Pia ni vizuri sana kama Mkandarasi huyu anaweza japo kutuongezea kilomita mbili tu za lami katika Mitaa ya Mji wa Musoma tutakuwa tumepunguza mzigo mkubwa sana kwa Serikali kwa kuhudumia barabara za changarawe, ambazo zimekuwa zikitumia fedha nyingi sana kwenye ukarabati wa kila siku baada ya kipindi cha mvua. Napenda kuwaeleza pia na kutoa rai kwa Watanzania wenzangu wanaotumia barabara na vivuko, basi wawe watumiaji wazuri na wanaofuata sheria.

Mheshimiwa Spika, naomba kuhitimisha mchango wangu na kusubiri Mheshimiwa Waziri atakapotoa ufafanuzi.

MHE. THUWAYBA IDRISA MUHAMED: Mheshimiwa Spika, kwanza, natoa pongezi nyingi kwa Wizara hii kutokana na mipango na utendaji wake wa kazi hasa katika ujenzi wa barabara. Ingawa kuna vikwazo vingi vya vifaa na ukosefu wa fedha, lakini bado inaonyesha juhudi ya kutekeleza malengo waliyojipangia. Keep it up!

Mheshimiwa Spika, katika ziara tuliyofanya Kamati ya Hesabu za Serikali kwa kuangalia barabara ya Singida - Babati - Minjingu - Arusha ya kilometa 321 kwa Shilingi milioni 29,717.56 ni barabara iliyojengwa kwa

121 kiwango na hata value for money unaiona. Kinachofurahisha, barabara hizi Singida - Kateshi, Kateshi - Dareda, Dareda - Babati, Babati - Minjingu, utafikri haikujengwa na ma-contractor tofauti kwa vile kiwango kinachojionesha kuwa ni kimoja, ingawa moja ya barabara hizi lami yake ni ya mtelezo na ya pili ni ngumu. Hata hivyo, kuna baadhi ya sehemu bado mitaro, mifereji haijawekwa. Ni vyema ikawekwa ili kuweka usawa na unadhifu wa barabara hizo.

Mheshimiwa Spika, pia kuna baadhi ya sehemu road reservation alama zimewekwa, lakini kwingine bado. Wizara au TANROADS waziweke, hizi zitawasaidia wale ambao wanaotaka kujenga katika eneo la barabara kutojenga na wale walioambiwa wahame. kuondoka.

Mheshimiwa Spika, wananchi wanahitaji elimu ya kutosha. Kwa wale wanaotaka kuvunjiwa, inaonesha elimu hii hawana ya kutosha, ndiyo maana inawawia vigumu kuhama hata wakilipwa. Hii ndiyo kesi iliyojitokeza kwa mwananchi aliyelipwa fidia kisha hakuhama na fedha yake kumtafuta Wakili ikawa vyote viwili kuvikosa; siyo fedha wala siyo nyumba.

Pili, Wizara inakawia sana kuzivunja nyumba, ndiyo inapelekea mwenye nyumba kwa fedha na kukataa kuhama, mara nyingine fedha mnayoitoa ni ndogo kulingana na maisha yalivyo sasa. Ni vizuri kutoa fedha kutokana na uchumi ulivyopanda ili wahusika waweze kupata nafasi ya kujenga nyumba nzuri yenye kiwango.

122 Mheshimiwa Spika, kunajengwa barabara za Majiji: Je, kuhusu packing za gari zinafikiriwaje? Hivi sasa Jiji la Dar es Salaam gari zimeshakuwa nyingi, packing hakuna na barabara zinaongezwa. Hili lifikiriwe. Naomba Waziri atapokuja kujumuisha atueleze kuhusu hili.

Mheshimiwa Spika, alama za barabarani hazikidhi kuwa za kimataifa. Maximum speed ni ngapi? Kimataifa ni 120,80,60, sasa speed limit ya Tanzania ni ipi au zipi?

Mheshimiwa Spika, vile vile nashauri alama kwa walemavu ziandaliwe ili nao waweze kuwa na haki ya kutumia barabara kwa uangalifu na uhakika wa maisha yao. Ulemavu hauna chapa, inaweza wewe au mimi wakati wote wote ule tukawa walemavu. Wizara ifanye kila njia ya kutatua tatizo hili kwa walemavu. Namwomba Mheshimiwa Waziri atapojumuisha, atueleze kuhusu kadhia hii ya walemavu na alama zao na matumizi ya barabara.

Mheshimiwa Spika, majumba yanajengwa, tena mazuri, lakini kuna hila moja, contractor, sub- contractor, engineer ndio huyo huyo. Tumeziona nyumba hizo na zimeshaanza kuwa na ufa. Hili nalo liangaliwe.

MHE. DKT. FESTUS B. LIMBU: Mheshimiwa Spika, naipongeza Wizara ya Ujenzi, Waziri wake, Naibu Waziri, Katibu Mkuu, na kadhalika, kwa kazi nzuri mnayoifanya kitaifa na katika Jimbo langu la Magu. Katika Jimbo

123 langu TANROADS wamejitahidi sana kujenga na kukarabati barabara na madaraja. Hongera.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Lumeji - Nyashana katika Jimbo langu la Magu imekarabatiwa kipande cha Nyashana na Kadashi peke yake. TANROAD Mwanza wamekuwa wakiniambia tayari Mkandarasi ameshateuliwa kujenga kukarabati kipande cha Lumeji na Nyashana.

Mheshimiwa Spika, nimepita barabara hii jana, sijaona dalili zozote za Mkandarasi kuwepo site. Je, nini kinaendelea iwapo fedha zote zimeishia Nyashana kadashi? Itakuwaje kuhusiana na sehemu korofi sana zilizoko katika kipande cha Lumeji na Nyashana iwapo hazitatengenezwa kabla ya msimu ujao wa mvua? Barabara haitapitika. Naomba majibu.

Mheshimiwa Spika, ni sera ya Taifa ya kuunganisha Makao Makuu ya Mikoa barabara ya lami. Je, barabara ya lami itakayounganisha Makao Makuu ya Mkoa wa Simiyu (Bariadi) na Makao Makuu ya Mkoa wa Mwanza itapita wapi?

Mheshimiwa Spika, Makandarasi wanaotengeneza barabara za lami za kitaifa kwa kiwango cha chini wasipewe kandarasi tena, ila wanaoathirika kufanya vizuri sana ndiyo waendelee (watafutwe ikiwezekana) kupewa kandarasi zaidi. Mfano, Mkandarasi aliyejenga barabara ya kutoka Nyasamba (Ilula) kupitia Shinyanga – Tinde – Isaka amejenga barabara hii kwa kiwango kizuri cha juu sana na hadi amalize kuijenga haina dalili ya kutoboka

124 toboka. Kiwango ni cha juu kiasi kwamba hata uchakavu wa matairi ya magari huwa nimdogo. Mkandarasi aliyejenga barabara ya Nzega na Shelui na Misigiri hafai na asipewe kazi nyingine.

Mheshimiwa Spika, Kisiwa cha Ijinga katika Jimbo la Magu TEMESA, watembelee waone namna ya kujenga angalau gati pande zote mbili wakati Serikali inaangalia uwezekanao wa kuweka feri, hii ni kero ya muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja mia kwa mia.

MHE. MUSTAPHA B. AKUNAAY: Mheshimiwa Spika, huu ni mchango wa nyongeza kwenye mchango wangu wa mdomo.

Mheshimiwa Spika, kuweka lami barabara kutoka Bariadi – Meatu – Haydom – Mbulu – Karatu kwa sababu ya matumizi ya barabara hii kwa ajili ya Hospital ya Haydom na kusafirisha zao la pamba na mifugo barabarani, hii inatakiwa iwe ya lami hata kwa mipango ya muda mrefu kama hakuna fedha kwa sasa.

Mheshimiwa Spika, barabara nyingi zinakabiliwa na ng’ombe kwa kukosekana kwa cattle routes. Nashauri Halmashauri za Wilaya zikishirikiana na TANROADS kuhakikisha kila barabara inakuwana mapitio ya ng’ombe.

125 Mheshimiwa Spika, naomba Mfuko wa Barabara uhakikishe fedha zote zinatumika kwa ajili ya barabara tu.

Mheshimiwa Spika, Kituo cha One Border Post - Namanga, ni muhimu sana kwa ajili ya kazi iliyopangwa. Kwa hiyo, inaharakishwe ili kuondoa bughudha wanayopata wasafiri wanaopitia eneo hilo.

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Mbulu wanaishukuru Serikali kwa matengenezo ya barabrara katika Wilaya yao hasa barabara zifuatazo: Mbulu – Mbuyu wa Mjerumani; Mbulu – Kuta – Babati; Kilimapunda – Haydom* (Ndiyo inayopendekezwa kuwa ya lami hadi Karatu), Kilomita saba za lami Mjini Mbulu (wanaomba slabs za access to property).

Mheshimiwa Spika, ndiyo inayopendekezwa kuwa ya lami hadi Karatu.

MHE. SELEMANI J. ZEDI: Mheshimiwa Spika, mchango wangu ni kuhusu barabara maarufu kama Mwanza Road inayotokea Tabora kupitia Mambali na kupitia Chona na kufika Kahama Mjini na hatimaye kufika Mwanza.

Mheshimiwa Spika, barabara hii iko vizuri kutoka Tabora hadi Mambali, lakini kutokea Mambali kupitia Semembelea hadi Chona na Chambo barabara hii imekufa kabisa. Haijafanyiwa matengenezo kwa miaka mingi sana na iko katika hali mbaya sana na haipitiki kabisa.

126 Mheshimiwa Spika, barabara hii ni muhimu sana kwa kuwa ndiyo barabara pekee inayotegemewa na wananchi wengi wanaopitiwa na barabara hii hasa kwa kusafirisha mazao kama mbolea na pembejeo, na pia kuwezesha magari yanayopeleka huduma muhimu za afya.

Mheshimiwa Spika, Mhandisi wa barabara wa Wilaya ya Nzega ameshaanza kuchukua hatua za kuhakikisha barabara hii muhimu inafufuliwa na kurudi kwenye hali yake ya miaka ya nyuma ambapo barabara hii ya Mwanza Road, kutoka Tabora – Mambali – Semembele – Chona na Chambo – Kahama – Mwanza inarudi kwenye hadhi yake.

Mheshimiwa Spika, naomba Wizara isaidie kwa maana ya kuwezesha kupatikana fedha za kuihudumia barabara hii.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. MCH. ISRAEL Y. NATSE: Mheshimiwa Spika, wakati wa Kampeni ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Mheshimiwa Rais aliahidi ahadi nyingi kwa nchi nzima katika kuleta maendeleo akipewa nafasi ya kuongoza nchi hii. Waswahili husema, ahadi ni deni na ili hilo litekelezwe ni lazima Serikali itekeleze ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais ya kutengeneza barabara ya lami ya urefu wa kilometa mbili katika viunga vya Mji wa Karatu.

Je, Waziri anawaambiaje wananchi wa Karatu katika kutekeleza ahadi hiyo ya Mheshimiwa Rais? Pili,

127 naomba Serikali itupe kitabu cha orodha ya ahadi zote za Rais kwa nchi nzima ili ituwezeshe sisi Wabunge Wawakilishi wa wananchi kuhakiki utekelezaji wa Serikali kwa ahadi za Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, kuhusu utengenezaji wa barabara chini ya kiwango, naomba kusisitiza umakini wa usimamizi wa Makandarasi wajenzi wa barabara. TANROADS iwe na meno makali kuwawajibisha wale wote watakaojenga barabara chini ya viwango. Kwa mfano, barabara ya Karatu – Kilima pande ambayo inatengenezwa kwa kiwango cha Moram, Moram inayowekwa ni udongo na hivyo kazi haijakamilika. Tayari imeshaharibika kule ilikoanziwa, hakuna usimamizi makini.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi katika awamu yake ya kwanza ndio alifanikisha barabara ya Makuyuni – Ngorongoro Gate, na sasa amerudi katika Wizara hii, tafadhali naomba aangalie barabara hiyo, imekuwa na viraka vingi kupindukia. Hii ni kutokana na kutengenezwa kwa barabara chini ya kiwango. Umakini na uzalendo unahitajika sana kwa wote waliopewa dhamana ya kusimamia utekelezaji wa miradi yetu ya maendeleo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu bomoa bomoa kwenye hifadhi ya barabara, ni kweli zimewekwa alama za ‘X’ maeneo mengi ambamo watu wamejenga katika hifadhi ya barabara. Kwanza niseme kwamba elimu sahihi itolewe kwa wananchi kuhusu hifadhi za barabara.

128 Mheshimiwa Spika, pili, ni vyema kwa Serikali kulipa fidia kwa wale ambao barabara imewafuata na fidia hiyo ifanane na hali halisi ya sasa ili kuwaondolea wananchi hasara na kuweza kujenga makazi yao. Ni wale ambao wamekuwepo kabla ya Sheria ya Hifadhi ya Ardhi ya mwaka 2007 haijatungwa.

MHE. EUSTACE O. KATAGIRA: Mheshimiwa Spika, nawapongeza Mheshimiwa Waziri na timu yake, na ninaunga mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, ninaongezea kwenye yale niliyochangia kwa kuongea kwamba barabara ya Bugere, Nkwenda – Murongo, naomba ipandishwe hadhi toka ya regional road na iwe trunk road. Inaunganisha Tanzania na Uganda. Ina traffic density kubwa sana, inaunganisha Miji ya Wilaya ya Karagwe na Wilaya mpya ya Kyerwa.

Mheshimiwa Spika, Kilimo cha Rwabunuka (escarpment) tunaomba sana matengenezo yafanyike. Metre 70 za matengenezo kweli ni kichekesho.

Mheshimiwa Spika, tunaomba haya maelekezo ya Mheshimiwa Rais ambayo aliyatoa baada ya kupitia pale yeye mwenyewe yatekelezwe with deserving seriousness. Kwa kweli metre 70 ni kama utani.

Mheshimiwa Spika, tunaomba pia malengo yatimizwe na siyo kupakaa surface kwa lami tu. Kona hatarishi zirekebishwe, gradient kwenye maeneo kadhaa ipunguzwe.

129

MHE. DEO H. FIKIKUNJOMBE: Mheshimiwa Spika, tunaomba barabara ya Itoni – Ludewa – Nanda ipewe mtazamo wa pekee na ijengwe kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, barabara hii ya Njombe – Ludewa ni barabara muhimu katika uanzishwaji wa miradi ya Liganga na Mchuchuma, miradi ambayo italifanya Taifa lizalishe chuma na makaa ya mawe.

Mheshimiwa Spika, barabara hii ya Itoni - Ludewa – Manda ni barabara muhimu, kwani inaunganisha Tanzania (Ludewa) na Malawi.

Mheshimiwa Spika, pongezi tele kwa utendaji mzuri wa Mheshimiwa John P. Magufuli – Waziri wa Ujenzi, wananchi wa Ludewa tuna imani kubwa naye na Naibu Waziri wake.

MHE. ALIKO N. KIBONA: Mheshimiwa Spika, Chuo cha Matumizi stahiki ya nguvu kazi (ATTI) kilichoko Rungwe Mbeya kinatoa elimu ya mafunzo ya kutengeneza barabara kwa njia rahisi kwa wananchi wengi. Mwaka 2011 pekee kilitoa mafunzo kwa watu 665. Kwa bahati mbaya, watu hawa wakihitimu na kurudi kwenye Halmashauri zao, kila wanapoomba kazi Halmashauri hizi hazitambui kazi au ujuzi wao licha ya maagizo ya Serikali kuwa wapewe kazi.

Mheshimiwa Spika, Swali: Je! Serikali inaweza kutoa kauli kwa ajili ya mkanganyiko huu wakati huu

130 ambapo watu wanasikiliza na kufuatilia matangazo ya Bunge?

MHE. JOHN P. LWANJI: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Kwa kuwa tayari kuna ujenzi unaoendelea wa barabara itokayo Mbeya kuja Makongolosi, naiomba Wizara ipange ujenzi wa barabara ya Mkiwa – Itigi – Rungwa – Makongolosi ianzie Mkiwa kwa sababu katika barabara hii ‘concentration’ ya watu inaanzia Itigi Mgandu( kuanzia Itigi – Doroto – Luganga – Itagata – Kayui – Mtakuja – Makale – Mitundu – Kalangali – Kiyombo - Kirumbi – Mwamagembe – Kintanula- Rungwa – Kambikatoto na kadhalika). Kwa hiyo, kama unavyoona, watu wengi walio eneo hili kuliko upande wa Makongolosi ambako maeneo mapana ni mapori zaidi, naiomba Wizara ilione hili ili Mkandarasi aanze kazi kutokea upande wa Mkiwa.

Mheshimiwa Spika, pale Sinza Dar es Salaam barabara inayokwenda nyumbani kwa Mheshimiwa Spika na maeneo hayo ya Sinza barabara ni mbaya sana, mashimo kila mahali barabarani kiasi kwamba wakati wa mvua ni madimbwi makubwa. Wananchi wanashindwa kuelewa ni kwa nini barabara hiyo ambayo kuna kiongozi wa mhimili mmoja wa dola kama Bunge haiangaliwi ipasavyo ili eneo hilo kwa ujumla liwe mfano kwa wananchi?

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali na Wizara iitupie macho barabara hii ambayo inatia aibu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Naomba majibu.

131

MHE. ANGELLAH J.KAIRUKI: Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hii kumpongeza Waziri wa Ujenzi - Mheshimiwa Magufuli na Naibu Waziri, Mheshimiwa Eng. Lwenge, Katibu Mkuu, pamoja na Watendaji wote wa Wizara hii kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mheshimiwa Spika, napenda kuishauri TBA kujenga angalau nyumba tano au zaidi katika Makao Makuu ya Kata kwa ajili ya kuzipangisha kwa watumishi mbalimbali wa Serikali waishio katika maeneo hayo. Hii itasaidia kupunguza upungufu wa nyumba kwa watumishi wa Serikali. Aidha, kwa kuwa tuna miradi mingi ya ujenzi ya barabara tunayoikusudia, lakini imekuwa ikishindikana kwa ukosefu wa fedha. Naona imefika wakati sasa tuchukue sovereign bonds kwa ajili ya kumaliza ujenzi wa barabara zote nchini kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, Bodi ya Mfuko wa Barabara ni chombo chenye manufaa kwa maendeleo ya barabara. Hata hivyo, kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambao una Wabunge zaidi ya wawili wa Viti Maalum ni vyema Wabunge wote wa Viti Maalum wakaingia katika vikao hivyo hata kama ni bila malipo na endapo itaonekana ni lazima waingie wawili tu, basi Wabunge wenyewe wachaguane ili kupata wawakilishi wa Viti Maalum na kuingia katika Road Boards.

Mheshimiwa Spika, kwa maelezo hayo machache, naunga mkono hoja hii kwa asilimia mia moja.

132 MHE. DKT. ANTONY G. MBASSA: Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kunijalia afya njema na kuchapa kazi ya kuwatumikia wananchi. Napenda nianze kwanza kwa kuipongeza Wizara ya Ujenzi chini ya Waziri mahiri na mzalendo Dkt. John Pombe Magufuli. Hakika ni mchapa kazi na mtendaji hodari, hakika anamudu kazi yake vizuri.

Mheshimiwa Spika, sasa niongelee suala la uharibifu wa mazingira unaofanywa na wakandarasi pindi wanapokuwa eneo la kazi; hakika hawana urafiki wa mazingira yetu kwa kiasi kikubwa sana. Wakandarasi hawa pindi wanapoanza kuchimba changarawe wanaacha mashimo makubwa sana bila hata ya kuyafukia. Hali hii haijalishi ni porini au maeneo ya makazi ya watu. Hii ni hatari, hususan kipindi cha mvua, mashimo haya hujaa maji na kuwa hatari kwa wanyama wafugwao na hata wanyamapori na hata kwa maisha ya wananchi. Nitoe rai kwa Serikali na Wizara kwa ujumla kabla ya kujaza Mikataba ya kazi, hili suala la mazingira liwe mojawapo ya vigezo katika kupata kazi. Mkandarasi pale anapokabidhiwa kazi, basi na mashimo haya yafukiwe kwanza ndipo malipo yao ya mwisho yafanyike.

Mheshimiwa Spika, kupitia Mfuko wa Road Fund zinaosimamia barabara ya Wilaya na Mikoa, nashauri kazi hizi ziwe zinatolewa kwa Makandarasi wenye uwezo na mitambo ya kutosha. Kumekuwepo na uharibifu wa mara kwa mara wa barabara ambazo kimsingi zimekuwa zikitengenezwa na Makandarasi hawa bila ya kujali thamani ya pesa kwa kazi husika

133 (value for money). Aidha, barabara inaweza kuchongwa au kifusi kuwekwa na hakuna ushindiliaji, hivyo, baada ya muda, hali ya barabara huwa mbaya sana. Hivyo, natoa rai kwamba kuwepo na upembuzi yakinifu wa kupata wakandarasi wa ndani wenye uwezo na Wazalendo wa kufanya kazi hii kwa moyo na siyo kujali pesa tu.

Mheshimiwa Spika, niongelee sasa suala la mizani katika barabara zetu. Leo hii kumekuwa na idadi kubwa sana ya vituo vya mizani kiasi muda mwingine kunakuwa na foleni kubwa sana. Idadi hii ya vituo ipungue na hii itasaidia kupunguza foleni za magari. Mpaka sasa hakuna taarifa rasmi ya kuwa mizani yetu imeingizia Serikali kiasi gani cha pesa tofauti na kuwaneemesha wafanyakazi wa mizani hii. Mizani hii na ukiritimba uliopo, imepelekea hata baadhi ya wafanyabiashara kuamua kupitisha mizigo yao bandari nyingine ili kuepukana na adha hii. Aidha, naishauri Serikali na Wizara kupunguza idadi ya vituo vya mizani hii ili kuboresha huduma hii ya usafirishaji. Kwani hata magari yanapozidisha uzito, suluhisho siyo kutozwa faini na kuruhusiwa kuendelea na safari, bali ni kupunguza mzigo. Ikiwezekana vituo toka Dar es Salaam hadi Rusumo kuwepo na vituo vitatu tu.

Mheshimiwa Spika, suala la alama za barabarani ni tatizo kubwa sana. Leo hii sehemu nyingi, alama hizi hazipo kabisa, kitu ambacho ni hatari kubwa sana kwa usalama wa barabara na watumiaji wa barabara. Suala hilo haliishii hapa tu, bado hata kwa makandarasi wanapokuwa sehemu ya kazi, hawaweki alama yoyote ile na hii imefanya watumiaji wa

134 barabara ya dharura kupata shida kubwa sana na hata muda mwingine kutumbukia kwenye mashimo ambayo hayajafukiwa.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali kupitia Wizara ya Ujenzi, kuangalia suala la alama za barabarani au kingo zinazokuwa kwenye maeneo ya barabara zifanyiwe marekebisho. Kama kuweka alama kwenye nguzo za vyuma kunaleta hasara ya kuibiwa, basi nashauri alama hizo zingekuwa kwenye nguzo za zege, na ninaamini hawataweza kuiba au kung’oa.

MHE. PHILEMON K. NDESAMBURO: Mheshimiwa Spika, wakati wa kampeni za mwaka 2010, moja ya ahadi za Rais alipokuwa Moshi Vijijini ilikuwa ujenzi wa barabara ya Moshi Mjini mpaka Kidia, Old Moshi. Hii ni barabara muhimu, kwani inaunganisha barabara ya Rombo - Marangu Mtoni – Kilema – Kivuna, ni barabara muhimu kwa utalii.

Mheshimiwa Spika, wananchi wa Old Moshi wamekuwa wakiuliza, hii barabara mara kwa mara. Katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri hakuitaja hii hasa. Naomba kama ameisahau, aiweke, ili isije ikasahaulika, kwani hii ni ahadi ya Mheshimiwa Rais kwa wakazi wa Old Moshi.

MHE. NYAMBARI C. M. NYANGWINE: Mheshimiwa Spika, pamoja na salamu nyingi kutoka kwa (Mb), tafadhali sana naomba hii karatasi ya mchango wangu wa maandishi ipitiwe. Nakuomba uingilie Wilaya ya Tarime kwa jicho la huruma hasa hiyo barabara ya security road.

135

Mheshimiwa Spika, napenda kuungana na Wabunge wenzangu waliochangia hoja hii kwa kuzungumza au kwa maandishi na kumpongeza Waziri wa Wizara hii kwa kufanya kazi kwa juhudi na maarifa. Shukurani pia zimfikie Naibu Waziri wa Wizara bila kumsahau Katibu Mkuu wa Wizara, pamoja na Watendaji wengine wa Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, kwa masikitiko makubwa, naomba kukumbushia suala la mgawanyo wa rasilimali za Taifa hapa nchini kwa kuangalia Mikoa ambayo bado iko nyuma kwa suala la maendeleo hasa miundombinu. Suala hili nililizungumzia kwa mapana sana katika bajeti ya mwaka 2011/2012. Sina haja ya kulirudia hapa, kwani Wizara ilijibu kuwa ushauri umezingatiwa na kwa kuwa Waziri bado ni yule yule, sijui kama kweli amefuata ushauri huo. Hata hivyo, kama Wizara ingekuwa imefuata ushauri huo, ni matumaini yangu kuwa mtandao wa barabara katika Wilaya ya Tarime ungetengewa fedha za kutosha. Hivyo, naamini ushauri wangu ulipuuzwa. Hali hii inasikitisha na inakera sana.

Mheshimiwa Spika, ifahamike wazi kuwa suala la miundombinu ya barabara Wilayani Tarime siyo ya kuridhisha, kwani wakati wa mvua, hasa masika, barabara takribani zote hazipitiki hata kidogo. Hivyo suala la mawasiliano linakuwa gumu sana na hivyo shughuli za maendeleo husimama. Wakati wa kiangazi, kuna vumbi kubwa sana kutokana na hali ya udongo ulioko katika eneo husika.

136 Mheshimiwa Spika, maswali ya kujiuliza ni: Je, Mheshimiwa Waziri anaifahamu vizuri Jiografia ya Wilaya ya Tarime? Je, Waziri anafahamu juu ya adha wanayoipata wakazi wa Tarime juu ya suala la barabara? Je, ushauri nilioutoa na Serikali ikaahidi kuufanyia kazi ulikuwa ni porojo za kisiasa? Kwa nini Wilaya ya Tarime ambayo ni ya zamani sana katika nchi hii, haina hata barabara moja ya lami?

Mheshimiwa Spika, barabara ya Nyamwaga Road ni ya Mkoa. Barabara hii ni kiungo kikuu cha uchumi katika Mkoa wa Mara. Barabara hii huanzia Tarime Mjini – Mogabiri - Nyamwigura – Rozana – Kemahorere – Nyarero – Nyamwaga – Nyamwago - Mrito hadi Mto Mara kuelekea Wilaya ya Serengeti. Barabara hii ina urefu wa kilometa 53. Serikali kupitia Naibu Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Dkt. Harisson Mwakyembe iliahidi kuwa itaanza kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami nyepesi, lakini hadi sasa hakuna kinachoendelea na wala hakuna hata upembuzi yakinifu kama Serikali ilivyoahidi wala cha nini? Hii ni aibu sana, tena aibu sana! Swali: Kwa nini Serikali haikutenga fedha kwa ajili ya barabara hii? Je, ujenzi wa barabara hii utaanza lini? Au Serikali ilidanganya umma wa Watanzania? Au kilikuwa ni kiini macho kwa wana Tarime? Basi kama barabara hiyo haijengwi kwa kiwango cha lami, naiomba Serikali kupitia Waziri wa Ujenzi afute kauli ya Serikali kuhusu ujenzi wa barabara hii.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Security Road ni barabara ya Mkoa, iko mpakani mwa nchi ya Kenya, inatoka Wilayani Rorya kupitia Susuni – Kubiterere – Remagwe – Gwitivyo – Nyabisaga – Borega –

137 Ganyange – Kimusi – Nyantira – Muriba – Kobori – Itivyo – Nyamombara – Mangucha hadi Kegonga. Kitu cha kushangaza ni kwamba, kwenye bajeti hii hakuna sehemu yoyote iliyooneshwa kwamba barabara hii imetengewa kiasi gani cha fedha. Swali: Je, Serikali haiko makini? Je, Serikali haina taarifa yoyote kuhusu hii barabara?Je, Serikali haiko serious kuhusu hii barabara? Je, nani aihudumie hii barabara?

Mheshimiwa Spika, tutafakari kwa makini. Naishauri Serikali iweke mkazo kwenye barabara hii hata ikiwezekana iwekewe lami nyepesi, kwani ni kero kwa wakazi wa Tarime.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Nyamwaga – Muriba ni barabara ya Mkoa. Naishauri Serikali iweke lami nyepesi kwenye barabara hii yenye urefu upatao kilometa nane, kwani ni kero sana kwa wakazi wa eneo hili. Hata kama ikitengenezwa ndani ya siku chache, huharibika. Hivyo, ili kuepukana na tatizo hili, naishauri Serikali iweke lami nyepesi au changarawe katika barabara hii, wala siyo udongo.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Mangucha – Masanga – Gibaso – Mrito, Mheshimiwa Waziri Mkuu aliahidi wakazi wa maeneo yanayopita barabarani hii kuwa ataipandisha hadhi ili iwe ya Mkoa. Vikao vyote halali vilishakaa na kupitisha uamuzi wa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Sasa sijui tatizo liko wapi? Swali: Kwa nini hii barabara haijatengewa fedha katika bajeti hii? Ombi au uamuzi wa vikao halali umefikia wapi? Ni lini Mkoa utaanza kuhudumia barabara hii?

138 Mheshimiwa Spika, barabara ya Komaswa – Manga – Nyarwana – Nyamongo ina tarkribani kilometa 40. Pamoja na kwamba ombi langu la mwaka 2011 la kuipandisha hadhi barabara hii bado halikukubaliwa, lakini bado jitihada zinafanyika ili ichukuliwe na kuhudumiwa na TANROADS. Mheshimiwa Spika, madaraja ya Kyoruba na Mto Mori, kwa kuwa yako mpakani mwa barabarani zinazohudumiwa na Mkoa, naishauri na kuiomba Wizara kuangalia uwezekano wa kuyajenga madaraja haya, kwani ni kero kubwa sana kwa wakazi wa Tarime. Chonde chonde Waziri nakuomba ufikirie suala hili kwa makini.

Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2011 nilipendekeza ujenzi wa nyumba za watumishi Wilayani Tarime, na Wizara ilijibu kuwa ina mpango huo wa kujenga nyumba hizo katika nchi nzima, hasa Wilaya zilizo pembezoni mwa nchi na Tarime ikiwemo. Je, mpango huo umefikia wapi?

Mheshimiwa Spika, nasisitiza barabara za Mkoa zilizopo Wilayani Tarime zitengewe fedha za kutosha. Kama itashindikana kujengwa kwa lami nyepesi, basi nashauri zijengwe kwa changarawe, wala siyo udongo. Madaraja ya Kyoruba na Mto Mori yajengwe na TANROADS. Barabara ya Mangucha – Gibao hadi Mrito ipandishwe hadhi. Vilevile suala la ujenzi wa nyumba za watumishi Wilayani Tarime lizingatiwe.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

139 MHE. JENISTA J. MHAGAMA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, tunaishukuru sana Serikali yetu kwa kutujali sana Mikoa ya Kusini kwa kutenga jumla ya Shilingi bilioni 592.058. Miradi hiyo ni pamoja na mradi wa barabara ya Peramiho – Mbinga kilometa 78.00 yenye jumla ya Shilingi bilioni 79.81 shilingi. Nawashukuru sana.

Mheshimiwa Spika, Pamoja na shukrani za barabara ya Peramiho – Mbinga, tunashukuru kupokea Shilingi milioni 979 kwa barabara ya Makambako Songea. Hata hivyo, tunaomba sana matengenezo ya barabara hiyo awamu hii tuanzie Songea kwenda Njombe mpaka Makambako. Tunaomba hivi kwa sababu ya namna ya uharibifu uliopo. Eneo la Songea – Njombe, limeharibika zaidi, lakini hasa eneo la Songea - Rukumburu. Tunaishukuru Serikali sana kwa fedha za mradi huo. Barabara hii ni muhimu sana, kwani inapita vijiji vya Igawisenga, Lilondo, Madaba, Mgongo team, Rutukila, Ngadinda, Gumbiro, Mtwangimbole, Luhimba na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, tunaishukuru sana Serikali, kwani kupitia mfuko wa barabara, tumepata Shilingi milioni 500 na kidogo kwa mradi wa Matimila kwenda Mkongo na Mpilimbi kwenda Nambendo. Hata hivyo, tunaomba tufikiriwe kuongezewa fedha zilizobaki ili kumalizia kipande cha Mpilimbi kwenda Ndongosi.

Mheshimiwa Spika, tunaomba pia sasa barabara ya Likuyufusi kwenda Mkenda mpakani mwa Tanzania

140 na Msumbiji iwekwe katika bajeti ijayo ili iwekwe lami. Barabara hiyo ni ya mpakani, hivyo ni barabara muhimu inayofungua uchumi wa nchi yetu na hasa Mkoa wa Ruvuma. Kwa kuwa upembuzi yakinifu umekamilika, ni lini sasa tutaanza kuweka lami barabara hiyo?

Mheshimiwa Spika, ninaomba barabara zifuatazo sasa ziwe za Mkoa; Wino kwenda Iringa – Morogoro, Matimila kwenda Mkongo, Mpitimbi kwenda Mambendo mpakani mwa Tanzania na Msumbiji.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema haya, naomba kuunga mkono hoja.

MHE. REBECCA M. MNGODO: Mheshimiwa Spika, napenda kutoa maoni yangu kuhusu hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi juu ya makadirio ya mapato na matumizi ya fedha kwa mwaka 2012/2013.

Mheshimiwa Spika, fedha zilizoombwa Sh. 296,896,892,00/= kwa ajili ya miradi ya maendeleo. Kwa maoni yangu ni kidogo sana, Serikali iangalie jinsi ya kuongeza kiwango hicho.

Mheshimiwa Spika, Mfuko wa Barabara kutengewa Sh. 300,764,800,000/= kuna barabara nyingi nchini zinahitaji matengenezo. Vivuko vilivyo katika hali mbaya vinavyohitaji kununuliwa vipya kama vile Ifungi Kyela, hata hivyo, barabara za Vijijini zina hali mbaya zaidi. Wananchi wengi waishio Vijijini wanashindwa kusafirisha mizigo yao hadi sokoni kutokana na ukosefu wa barabara nzuri.

141

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa walimu wengi na pia watumishi wengi wa Serikali wanaishi katika nyumba zilizo chini ya viwango, kiasi kilichotengwa kwa TBA, kingeongezwa ili watumishi wa Serikali wajengewe nyumba za kutosha.

Mheshimiwa Spika, katika ukurasa 143, zimetengwa Sh. 5,978,772,000/= kwa ajili ya ujenzi na ukarabati wa nyumba na majengo ya Serikali. Sioni uhalisia wowote wa kiwango hicho kidogo cha fedha kwa tatizo kubwa kama la ujenzi wa nyumba za Serikali. Ni vigumu kuelewa ni nyumba ngapi zitajengwa na ngapi zitakarabatiwa kwa kiwango hicho cha fedha.

Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi ukurasa wa 155, Wizara kupitia kitengo cha ushirikishwaji wanawake katika kazi za barabara itatembea Mikoa 12 kuona ushiriki wa wanawake katika kazi za barabara na pia kuhamasisha wanawake wengi zaidi washiriki kama makandarasi. Je, ni jambo gani limepelekea Wizara hii kupenda kuhamasisha wanawake wengi zaidi?

Mheshimiwa Spika, kwa mantiki hiyo, naishauri Wizara iweke vivutio maalum kama vile malipo mazuri zaidi kwa wakandarasi wanawake ili wengi zaidi wavutiwe na sekta hiyo.

Mheshimiwa Spika, nashauri mkakati wa kupambana na UKIMWI kwa Wizara hii, uboreshwe zaidi kwa kuongeza elimu kwa njia ya redio ili watumiaji

142 wa barabara na hasa madereva wanaosafiri kwa muda mrefu waweze kufaidika na elimu ya kupambana dhidi ya VVU/UKIMWI.

Mheshimiwa Spika, kwa haya machache, naomba kuwasilisha.

MHE. DKT. LUCY S. NKYA: Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na Watendaji wao kwa kutayarisha hotuba nzuri sana ya bajeti ya Wizara ya ujenzi. Aidha, naipongeza sana Serikali ya Chama cha Mapinduzi kwa kujenga mtandao mzuri wa barabara za lami ambazo sasa zinaunganisha Miji Mikuu ya Mikoa yote ya Tanzania Bara.

Mheshimiwa Spika, baada ya pongezi, naomba sasa nitoe kero za miundombinu ya barabara na madaraja katika Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, barabara ya Bigwa - Kisaki, imetengewa Shilingi milioni 50 tu ambazo hazitoshi hata kutengeneza eneo korofi la mlima Pangawe. Ikumbukwe kwamba barabara hii inaunganisha Makao Makuu ya Mkoa na Makao Makuu ya Wilaya. Naomba Serikali iangalie uwezekano wa kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami, kwani katika kampeni ya mwaka 2005 na 2010 Mheshimiwa Rais alituahidi hivyo.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Madamu - Kinohe, ni ya TANROAD, lakini bado utunzaji wake ni tete. Hii barabara ni nyembamba (narrow)

143 ukilinganisha na watumiaji wa hii barabara. Maeneo mengine ni korofi na hatari sana nyakati za mvua. Naomba sehemu korofi za vilima zijengwe kwa zege, kwani ni imara na haibomoki mara kwa mara.

Mheshimiwa Spika, Kipande cha barabara ya Tandai – kinole mpaka Tegetero ni muhimu sana kwa ajili ya soko la matunda na viungo katika Kata za Kimole, Tegetero na Kibogwa. Halmashauri ya Morogoro Vijijini haina uwezo wa kifedha na kuteknologia wa kujenga hizi barabara za milimani. Sisi wakazi wa milimani ni Watanzania, tunaomba huduma hii muhimu ya barabara ili tuweze kuendelea kiuchumi, kwani uwezo na fursa tunazo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu daraja la Gizigizi ambalo linaunganisha Vijiji vya Hung’ala, Ludewa na Mkuyuni naomba lijengwe kwani, wananchi wanashindwa kupata huduma za tiba, Shule, Soko na kusafiri kwenda Makao Makuu ya Wilaya na Mkoa. Zimekuwa zinatokea ajali nyingi sana hata walimu wamepoteza maisha yao katika mto huu ambao ndiyo chanzo cha mto Ruvu. Daraja katika eneo la Tonunguo kuvuka mto Ruvu, wananchi wanavuka kutoka upande wa Mbarangwe kwenda Kisanga stesheni kupata huduma za hospital, shule, soko na kilimo.

Mheshimiwa Spika, wananchi wengi, hususan wajawazito, watoto na raia wengine wamepoteza maisha yao kutokana na ajali za mitumbwi na wanashambuliwa na mamba. Halmashauri yetu haina uwezo wa kujenga hili daraja, kwani ni mradi mkubwa kuliko uwezo wake kifedha na teknolojia.

144

Mheshimiwa Spika, naomba sana Serikali iliangalie Jimbo hili lililosahaulika kabisa kwa jicho la huruma na upendo.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. SALOME D. MWAMBU: Mheshimiwa Spika, kwanza naunga mkono hoja na kutoa shukrani zangu kwa Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi na jopo lake kwa kazi nzuri wanayowatumikia Watanzania. Nashukuru kwa bajeti aliyoniwekea kuhusu ujenzi wa daraja la Sibiti. Nina imani ujenzi utaanza wakati wowote baada ya kutiliana sahihi na Mzabuni.

Pili, natoa shukrani kwa Wizara kwa ajili ya barabara zote zilizotengenezwa katika Jimbo langu, kwani zimebakia zinasuasua zile za Halmashauri.

Mheshimiwa Spika, narudi tena kumwomba Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, ikiwezekana kwa sababu daraja la Sibiti limekuwa la muda mrefu, wanapotiliana sahihi na mkandarasi itangazwe kwenye vyombo vya habari.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

MHE. MARYAM S. MSABAHA: Mheshimiwa Spika, nami nachukue nafasi hii kuchangia hotuba ya Waziri wa Ujenzi.

145 Mheshimiwa Spika, zile barabara zinazosimamiwa na Halmashauri zingekarabatiwa katika kiwango cha lami au (moram), zingesaidia kupunguza foleni katika kiwango kikubwa, kwa mfano barabara ambazo zimezoeleka kutumika Bagamoyo, Morogoro, Kawawa Road. Ni barabara ambazo zimezoeleka kutumika na zinaongoza kwa msongamano wa magari na hata hizi barabara nilizozitaja, baadhi zimejegwa chini ya kiwango cha lami, zina mashimo ambayo yanasababisha msongamano wa magari hasa kipindi cha mvua, barabara inamomonyoka kama hii barabara ya Kilwa Road ni barabara ambayo imejengwa kwa muda mfupi na imeharibika kwa muda mfupi.

Barabara nyingine kama hiyo ya Samnujoma ina matatizo, kama barabara ya Kilwa Road (ina mashimo) na hawa watu ambao wanaitwa Makandarasi wanaisababishia Serikali hasara kubwa. Kwanini Serikali isiwachukulie hatua inapotokea barabara kuwa mbovu kiasi hicho?

Mheshimiwa Spika, kingine katika Mji wa Dar es Salaam ni Sheria za Barabarani zinavyokiukwa. Kwa mfano, barabara nyingi za Dar es Salaam zina zebra (alama inayowaruhusu watembea kwa miguu), lakini alama hizi zimekuwa hazitumiii ipasavyo. Pale watembea kwa miguu wanapotaka kuvuka barabara, madereva wamekuwa hawasimami na kusababisha ajali na usumbufu. Kwa ninavyofahamu mimi, matumizi ya zebra ni lazima dereva asimame anapoona watu wanataka kuvuka barabara, lakini kwa Dar es Salaam imekuwa too much! Naiomba Serikali, wanaobainika

146 na makosa haya ya kuvunja Sheria za Barabarani wachukuliwe hatua za kisheria.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la matuta barabarani, matuta haya yamekuwa ni kero kwa madereva na kusababisha ajali kwa sababu matuta hayo hayapo katika ubora, kwani yamekuwa ni makubwa kama matuta ya viazi, na hata hivyo, hamna alama ya kumwonyesha dereva kama mbele kuna tuta. Kwa mfano, mabasi yanayotoka Mikoani, abiria ambao wanakaa siti za nyuma, wengi wao wamekuwa wakiteguka viuno na wanawake wajawazito kujifungua kabla ya siku zao. Hata sisi Waheshimiwa wakati tunatoka Dodoma au kusafiri nyakati za usiku, tumekuwa hatuyaoni matuta na magari yetu kukatika spring na kusababisha ajali. Naomba kumwuliza Waziri hii, imekuwa ni kero ya siku nyingi, ahakikishe hawa makandarisi wanaojenga barabara waweke matuta na alama za matuta na hayo matuta yawekwe katika viwango vinavyotakiwa ili kuepusha ajali na uharibifu wa magari ya wananchi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu suala la mizani, malori yanayosafirisha mizigo yamekuwa yakipimwa kwenye mizani, lakini cha kushangaza, bado barabara zinaharibiwa na kujenga migongo (miinuko) japokuwa tumekuwa na vituo viingi vya mizani. Utendaji wake wa kazi umekuwa ni mdogo sana. Kwa hiyo, naiomba Serikali ifanye uchunguzi. Inaonekana kuna rushwa inayofanyika kati ya wafanyakazi wa mizani na madereva. Hivyo wanaendelea kuisababishia Serikali hasara ya kukarabati barabara wakati kuna mambo Serikali inatakiwa kuyafanya.

147

MHE. DEOGRATIAS A. NTUKAMAZINA: Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri pamoja na timu yake yote, Wizarani na Mikoani kwa kazi nzuri ya kuweka mtandao wa barabara za lami nchi nzima ambazo zikikamilika zitaikwamua nchi hii kutoka kwenye dimbwi la umasikini.

Mheshimiwa Spika, ombi langu la kwanza kwa Wizara ni kuimarisha usimamizi wa ujenzi wa barabarani unaoendelea. Tatizo ninaloliona ni ubora wa barabara zinazojengwa. Makandarasi wengi siyo waaminifu, kwa hiyo, barabara nyingi ziko chini ya kiwango.

Mheshimiwa Spika, ombi la pili kwa Waziri linahusu mgawanyo wa fedha za ujenzi wa barabara. Ninavyoona mimi, kuna upendeleo wa aina fulani kwa baadhi ya maeneo ya nchi hii na kutojali scheme nyingine. Fedha hizi ni zetu sote, kwa hiyo, ni muhimu kuzigawa kwa uaminifu mkubwa ili tuwe na mtandao (network) wa barabara nchi nzima.

Mheshimiwa Spika, ombi langu la tatu ni kwamba miundombinu ya barabara ni moja ya vipaumbele katika mpango wetu wa maendeleo wa miaka mitano na ule wa muda mrefu (The Tanzania Long Term Perspective Plan(LTPP) 2011/2012 – 2025/2026) kuelekea ile nchi ya ahadi (the promised land) nchi yenye uchumi wa kati (a medium income economy), na kwa kuwa kuna barabara zinategemewa kwa asilimia 80 passenger traffic na asilimia 70 freight traffic, ni muhimu sana kwa Wizara kuwa very serious katika kusimamia ujenzi na ukarabati (maintenance) wa mara kwa mara

148 ili kuhakikisha kwamba usafiri wa watu na mizigo haukwami.

Mheshimiwa Spika, mwisho, nirudi kwenye barabara ya Mnzani (Nyakuhuru) Keza – Rulenge hadi Murugarama - Wilaya ya Ngara. Barabara hii ni ahadi ya Mheshimiwa Rais ya kuijenga kwa kiwango cha lami. Mara mbili nimedanganywa na Wizara Bungeni kwamba fedha za ujenzi wa barabara hii zingewekwa kwenye bajeti ya mwaka 2011/2012 na baadaye nikaambiwa zingewekwa kwenye bajeti ya mwaka 2012/2013.

Mheshimiwa Spika, jambo hilo limeshindikana, sasa hivi fedha kidogo zimewekwa kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu yakinifu. Barabara hiyo itajengwa lini? Jambo linalonisumbua kichwa ni kuona fedha zikimwagwa katika Majimbo mengine lakini siyo Ngara.

Mheshimiwa Spika, barabara hii inangojewa kwa hamu na Serikali ya Burundi ili kupitisha malori yao ya mizigo. Barabara ya sasa ina milima mirefu sana, kiasi cha kuyafanya malori yao yakwame.

Mheshimiwa Spika, Barabara hii pia ni muhimu sana kwa mgodi wa Kabanga na Nickel ambao ni mgodi wa pili duniani kwa utajiri wa madini ya Nickel. Mradi huu uko Wilayani Ngara. Mgodi huu unajengwa sasa na utakamilika katika miaka miwili ijayo. Malori ya mizigo ya mgodi huu yatatumia barabara hii. Naiomba Wizara ya Ujenzi ione umuhimu wa barabara hii na hasa kwa sababu itarahisisha usafirishaji wa mizigo ya nchi jirani ya Burundi.

149

Mheshimiwa Spika, vile vile naiomba Wizara iiombe Benki ya Maendeleo ya Afrika (African Development Bank) isaidie katika ujenzi wa barabara hii. Ninaamini ADB ikiombwa kusaidia ujenzi wa barabara hii itakubali. ADB iko tayari kutoa msaada (grant) na siyo mkopo.

MHE. SALUM K. BARWANY: Mheshimiwa Spika, barabara ya Kibiti – Mingoyo – Lindi, kipande cha km 60 za barabara hiyo cha Nyamwage na Somanga kimedumu zaidi ya miaka mitano sasa na kilomita 20 tu zimejengwa kwa kiwango cha lami. Kwa hali hiyo, itachukuwa miaka mingapi kumaliza hiyo kilometa 40 zilizobakia? Kipande hicho ni kero kwa wananchi hasa wakati wa masika. Ni vyema Serikali ikatoa taarifa rasmi, kwa nini kipande hicho kimechukua muda mrefu kiasi hicho?

Mheshimiwa Spika, makampuni makubwa yanayoingiza mafuta katika migodi wamepewa misamaha ya levy na ni pesa nyingi, zinapata misamaha hiyo, wanaoingiza mafuta hayo nchini. Huduma wanazotumia kwa kuingiza mafuta hayo zinahitaji matengenezo makubwa kama barabara na kdhalika. Ni muhimu kwa sasa Serikali kuangalia upya utaratibu wa kutoa misamaha hiyo.

Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu sasa Serikali imekuwa na utaratibu wa kujenga barabara nyingi ambazo zinachukuwa muda mrefu kumaliza miradi hiyo. Kwa wingi wa miradi na uwezo mdogo wa Serikali kulipa wakandarasi, ni vyema sasa Serikali ikaainisha

150 kwa utaratibu maalum, kuwe na barabara muhimu zitakazojengwa kwa ubora na ufanisi mkubwa kuliko ilivyo sasa, Wizara inashindwa kuzisimamia kwa karibu kama vile Nangurukuru - Mbwera na kulazimika kurudia.

MHE. DKT. CHRISTINE G. ISHENGOMA: Mheshimwa Spika, kwanza kabisa nakushukuru kwa kunipatia nafasi hii kuchangia katika Bunge lako Tukufu. Natoa pongezi kwa Waziri wa Wizara ya Ujenzi - Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli kwa kazi nzuri sana anayoifanya. Pongezi pia kwa Naibu Waziri, Katibu Mkuu, Wakurugenzi, wafanyakazi na watendaji wote kwa kazi nzuri wanazozifanya katika kuendeleza Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana kwa kazi nzuri itakayofanyika na inayofanywa katika barabara za Mkoa wa Morogoro. Mkoa wa Morogoro na hasa Morogoro Vijijini, namwomba Mheshimiwa Waziri aone huruma ya kuitazama barabara ya Morogoro – Pangawe – Matombo – Bwakila mpaka Kisaki kujengwa kwa lami. Sababu kubwa ni kuwa sehemu hizi nilizozitaja, wananchi wanalima sana na kuvuna mazao kwa wingi. Kwa hiyo, barabara hii wakati wa masika ni matatizo sana kupitika, ikijengwa kwa lami mazao yatasafirishwa bila matatizo.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Iringa – Kilolo kwa ukweli wenyewe, siyo nzuri. Namwomba Mheshimiwa Waziri aione kwa jicho la huruma, kwani barabara hii ikitengenezwa kwa lami itawanufaisha wananchi kwa kusafirisha mazao yao mpaka Iringa Mjini na Mikoa mingine jirani.

151

Mheshimiwa Spika, barabara ya Kyaka – Bugene – Kasulo, nashukuru Waziri na Wizara kwa kuiona. Usanifu na upembuzi yakinifu kufuatana na bajeti, itafanyika mwka 2012/2013. Naishukuru Wizara. Ni matumaini yangu baada ya hapo, lami itaendelea kujengwa.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Iringa Mjini mpaka Tumaini Chuo kikuu Iringa, ni mbaya. Naomba itengenezwe kwa kiwango cha lami. Vyuo vyote hapa nchini kwa wastani vinafikika kwa urahisi, sehemu hii ni sehemu fupi na mchepuko wa kutoka barabara ya Iringa – Dodoma. Kwa hiyo, naomba Mheshimiwa Waziri, Chuo hiki akiangalie kwa huruma, watengewe fedha wazi wazi ili barabara hii ya kuunganisha na Chuo Kikuu cha Tumaini ijengwe kwa lami.

Mheshimiwa Spika, nitashukuru sana wananchuo hawa wakitengenezewa barabara hii kwa lami.

Mheshimiwa Spika, nashukuru, bajeti hii ni nzuri, na kweli Wizara imefanya kazi nzuri.

Mheshimiwa Spika, baada ya hayo yote, naunga mkono hoja.

MHE. JOSEPHINE J. GENZABUKE: Mheshimiwa Spika, naomba kwa dhati kabisa barabara ya Kigoma – Kidawe – Kasulu – Nyakanazi iweze kupatiwa pesa ya kutosha ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami.

152 Mheshimiwa Spika, barabara hiyo ni kiungo kikubwa kwa Wilaya za Mkoa wa Kigoma. Hivyo, tunaomba Serikali itusaidie wananchi wa Mkoa wa Kigoma, kwa sababu barabara hiyo inatuunganisha hata na Mikoa mingine na ndiyo inayotumika kusambaza pembejeo.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, naunga mkono hoja.

MHE. HALIMA J. MDEE: Mheshimiwa Spika, kwa ufupi sana, naomba nipate ufafanuzi katika masuala yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, nyumba zilizokuwa za kiwanda cha saruji (Shirika la Umma) ambazo zilibaki Serikalini na baadaye kukabidhiwa TBA kufuatia ubinafsishwaji wa kiwanda cha saruji kwa mwekezaji Twiga Cement, nyaraka zilizopo na ambazo pia nilishaziwasilisha bila kupatiwa majibu yoyote kutoka katika Ofisi ya Waziri wa Ujenzi zinaonesha kwamba wapangaji ambao wengi ni watumishi wa Serikali, wamekuwa wakisumbuliwa na kiwanda kwa madai kwamba wameuziwa nyumba na TBA. Naomba Waziri anipe majibu. Nyaraka zote za ushahidi kuonyesha kwamba nyumba zilibaki Serikalini zipo, na nyaraka zote nilikabidhi kwa aliyekuwa Naibu Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa Mwakyembe.

Mheshimiwa Spika, Serikali haioni kuna haja ya kuwa na mbinu za dharura kuweza kuokoa janga la foleni linalolikabili Jiji la Dar es Salaam ambalo ndiyo roho ya mapato ya Serikali? Mikakati ya kutumia njia za

153 maji na reli zitaanza rasmi lini? Fedha zinazotengwa kwa ajili ya uboreshwaji, matengenezo ya barabara za pembezoni za mzunguko kwa Mkoa wa Dar es Salaam ambazo zina mchango mkubwa sana wa kupunguza foleni zimekuwa kidogo sana, hazilingani kabisa na mchango wa Mkoa katika tozo za barabara, mchango wa Mkoa katika pato la Taifa.

Mheshimiwa Spika, ufinyu huo unasababisha barabara kutengenezwa kwa kiwango vya udongo, changarawe au lami nyepesi, matokeo yake hazidumu na hivyo kulazimika kila mwaka fedha kutengwa kufanya kazi zile zile. Serikali haidhani kwamba ni muhimu kwa kuzingatia umuhimu wa Mkoa wa Dar es Salaam kuwa na mipango ya kuzijenga hizi barabara kwa lami nzito ili kupata suluhisho la kudumu?

Mheshimiwa Spika, kufuatilia upanuzi wa barabara ya Mwenge-Tegeta, kuna wananchi ambao waliathirika kwa maeneo yao kuchukuliwa kwa maelezo kwamba watalipwa fidia. Wengine bado hawajalipwa mpaka leo. Wizara inatoa tamko gani? Mchakato wa fidia bado unaendelea au umekwisha?

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Mwenge - Tegeta unaoendelea hivi sasa hauonyeshi kama mkandarasi ana nia au dhamira ya kujenga mitaro mikubwa yenye uwezo wa kupokea maji mengi sana yanayotokea maeneo yenye mwinuko ya Kata za Mbezi juu na Wazo, ambazo nazo zinavuna maji toka Jimbo la Ubungo, halikadhalika, mitaro ya kutoa maji kuelekea baharini.

154 Mheshimiwa Spika, nalizungumza hili kwa kuwa kama Mbunge, nimewasiliana na watu wa TANROAD ambao walinithibitishia kwamba, Mkandarasi anajenga barabara na mitaro ya kawaida. Naiomba Wizara, ili kulinda kazi nzuri inayofanyika, ije na mpango muafaka wa kuokoa hii barabara. Kuna tathmini ilishafanywa na Wizara kipindi hicho, ikiwa barabara moja hakuna kilichofanyika mpaka sasa?

Mheshimiwa Spika, nilikuwa nashauri kwamba, Waziri awe anaeleza na anatoa taarifa za miradi mipya, na ile ambayo imeshajadiliwa na kupitishwa na Bunge hili Tukufu isijumuishwe, na kama ikijumuishwa, iwe basi ni ya kazi zinazoendelea na kuonyeshwa kiasi ambacho kimetengwa mwaka huu mpya wa fedha kwa kuonyesha kiasi kipya. Siyo kuendelea kurudia miradi na kwa fedha ambazo zilishapitishwa, na miradi inaendelea na kuzungumzia miradi ambayo imeshakwisha. Ukurasa wa 90 na 91 una upotoshwaji mkubwa sana. Tunaweza kuokoa fedha na makaratasi kwa kuandika vitu ambavyo ni muhimu na mahususi kwa mwaka huu wa fedha.

MHE. JOYCE J. MUKYA: Mheshimiwa Spika, napenda kuzungumzia mambo matatu kwa njia ya maandishi, msongamano wa Magari Arusha, ajali za barabarani nchi nzima, ujenzi wa barabara na road licence.

Mheshimiwa Spika, tatizo la msongamano wa magari limekuwa likikua siku baada ya siku na hii ni kutokana na tatizo la miundombinu yetu na ongezeko kubwa la watu, kwani wakati barabara hizi

155 zinatengenezwa enzi hizo za ukoloni, fikra hazikwenda mbali, kuwa baada ya kipindi fulani eneo husika halitatosha na kukidhi matakwa ya eneo fulani au watu fulani na kwa wakati fulani. Mfano mzuri ni barabara ya Mkoa wa Arusha na naongelea Arusha Mjini ambapo ndiyo Makao Makuu ya Mkoa.

Mheshimiwa Spika, Arusha Mjini kuna barabara moja tu ambayo inaingia na kutoka katika eneo la Mjini, na kwa kuwa Arusha ni kitovu cha mapato ya fedha za kigeni kupitia utalii, basi lazima hatua za haraka au dhamira ya makusudi ichukuliwe ili kudhibiti tatizo hili ambalo limeshakuwa sugu katika Mkoa wa Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, pili, napenda kuzungumzia ajali za barabarani, mfano ajali za pikipiki. Kwa kipindi cha muda mfupi kumekuwa na tatizo kubwa la ajali za pikipiki ambazo zimesababisha madhara mbalimbali kama ulemavu wa kudumu, vifo na kupotelewa na vifaa vya usafiri na kulazimika kununua nyingine kwa wale wenye uwezo, au kuishia kuwa masikini kwa kukosa uwezo wa kununua kifaa kingine.

Mheshimiwa Spika, napendekeza kwamba, waendesha pikipiki wote kabla ya kupewa leseni, lazima wawe na kofia mbili za kuzuia au kupunguza kutokuumia kichwa chake na kwa dereva wake mara wapatapo ajali. Hili limekuwa likipuuzwa sana na waendesha pikipiki na hata askari na barabarani. Mfano, hadi kufikia mwaka 2011/2012; mwaka 2011, January – February ajali 4,080 vifo 530 na majeruhi

156 3,227; kwa mwaka 2012, January – February ajali 36,888, vifo 603 na majeruhi 3,026.

Mheshimiwa Spika, kati ya miaka hiyo miwili ajali zimepungua, lakini vifo vimeongezeka kwa asilimia 19. Kwa hiyo, rai yangu, naomba utoaji leseni uende sambamba na kofia mbili za abiria na isiruhusiwe kupandisha abiria zaidi ya mmoja katika pikipiki.

Mheshimiwa Spika, kumekua na tatizo kubwa kwa baadhi ya wamiliki wa magari kutokulipia licence kwa wakati na kukosesha Serikali mapato mengi kwa wakati, na wengi wanaofanya hivi ni viongozi, kwa kuwa wanafahamu magari yao hayakaguliwi au hata kama yanakaguliwa wamekuwa wakijitetea kuwa wao ni viongozi, na magari yao kutokuchukuliwa hatua. Kwa hiyo, huendelea kuendesha magari hayo wakati hayana road licence au zimekwisha muda wake.

Mheshimiwa Spika, naomba kufahamishwa, fedha hizo zinakwenda wapi na zinafanya kazi gani za maendeleo especially kwa upande wa ujenzi wa barabara?

Mheshimiwa Spika, nazungumzia sana ujenzi wa barabara (Musoma Serengeti – Arusha). Barabara hii imekua kikwazo kikubwa kwa wananchi wanaoishi maeneo ya Wilaya zifutazo: Arusha, Monduli, Longido, Ngorongoro, Serengeti, Tarime, Bunda mpaka Musoma iliyopita upande wa Mashariki wa Hifadhi ya Serengeti.

Mheshimiwa Spika, Mataifa ya nje na ujenzi wa barabara hiyo kupitia Mahakamani ya EAC wakati eti

157 kwa kuwa barabara hiyo inapita ndani ya Mbuga ya Serengeti, hiyo itaathiri ikolojoa ya wanyama wanaohama kutoka hifadhi ya Serengeti nchini Tanzania kwenda hifadhi ya Masai Mara nchini Kenya kila mwaka.

Mheshimwa Spika, wananchi wa maeneo hayo, wana haki ya kupata huduma za kijamii mfano, afya, elimu, usafiri na kdhalika. Mfano, tatizo la barabara hiyo kutokujengwa kwa kiwango cha lami, imefanya tatizo la usafiri kuwa kubwa sana kwa wakazi wa eneo hilo. Mabasi ya abiria huanza safari saa 12.00 asubuhi na kufika Arusha Mjini saa 1.00 usiku, huku nauli ikiwa Sh. 12,000/=. Endapo barabara hiyo itatengenezwa, itapunguza gharama hizo pamoja na muda wa kusafiri muda mrefu barabarani. Hata bei za bidhaa mbalimbali zimepanda na ubovu wa barabara hiyo. Mfano, soda ni Sh. 500/=, lakini Loliondo ni Sh. 1,500/= na sukari ni Sh. 3,000/=.

Mheshimiwa Spika, mbona Masai Mara kuna barabara ya lami? Je, hao Wakenya hawalioni hilo na hata kutaka Mbuga ya Serengeti barabara isijengwe?

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia katika hoja hii kuhusu barabara za mara na bajeti hii tuliyotengewa ambayo kiuhalisia haionyeshi utimilifu wa barabara zile kwa kiwango kilichoonyeshwa.

158 Mheshimiwa Spika, barabara ya Musoma – Mwanza – Mara imechukua muda mrefu sana kumalizika, na kwa jinsi ilivyo, hata mwaka huu wa fedha hautaweza kumalizika. Barabara hii inasababisha ajali nyingi sana, na usumbufu huu ni wa muda mrefu sana. Naomba Mheshimiwa Waziri hii sehemu imalizike mapema ili kuondoa usumbufu wa kusafiri kwa muda mrefu sana kuliko kawaida na kupunguza au kuondoa ajali kabisa.

Mheshimiwa Spika, pili, naomba kwa masikitiko makubwa sana licha ya kufinywa bajeti kwenye Mkoa wetu wa Mara, ikilinganishwa na Mikoa mingine, na ikizingatiwa kwamba mbuga yetu ya Serengeti inachangia fedha nyingi Serikalini kuliko urejesho wa maendeleo kwenye Mkoa wetu, pia tumezungukwa na maziwa migodi, lakini Serikali haitengi fedha nyingi kwa ajili ya maendeleo ya Mkoa wetu.

Mheshimiwa Spika, nasikitika kwa Serikali kutokutoa kipaumbele kwenye barabara hizi zifuatazo: baraba ya usalama, yaani security road ya kuanzia Shirati Wilayani Rorya, unapita Susuni – Mwema - Sirari hadi Mangucha. Hii barabara ikijengwa kwa kiwango cha lami itasaidia kukuza uchumi wa maendeleo ya jamii husika, kwani watu wale hulima mazao ya aina mbalimbali kama mahindi, ulanzi, mihogo, kahawa, chai, alizeti, mtama na mazao mengine mengi, kama miti ya mbao. Barabara hii ipo kandokando na nchi jirani ya Kenya na inaunganisha bandari ya Kirani nchini Kenya, hivyo kuwa na umuhimu mkubwa mno.

159 Mheshimiwa Spika, vile vile kuna barabara tena ambayo ipo kwenye ahadi ya Mheshimiwa Rais wakati wa kampeni zake za mwaka 2010, barabara ya Shirati – Utegi hadi Mika, tunaomba sasa Serikali izipe kipaumbele barabara hizi.

Mheshimiwa Spika, barabara nyingine ni ile ya Nyerere kwa maana, inayoanza Makutano - Lapita - Nata Mto wa Mbu; kwa masikitiko imetengewa Shilingi bilioni tatu tu. Are we serious for sure? Yaani tunachangia fedha nyingi, lakini mapato finyu sana kama mrejesho wa maendeleo.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha, ila naomba kuwepo na uwiano pamoja na uhalisia wa resource allocation.

Mheshimiwa Spika, siungi mkono hoja.

MHE. ELIZABETH N. BATENGA: Mheshimiwa Spika, napenda nimpongeze Mheshimiwa Waziri, Naibu wake, pamoja na Watendaji wote wa Wizara hiyo ikiwa ni pamoja na Watendaji wa TANROADS kwa kazi nzuri inayofanywa kuhakikisha kuwa mtandao wa barabara unazidi kupanuka. Kipekee, nampongeza Mheshimiwa Magufuli kwa hotuba nzuri yenye vielelezo na namna alivyoiwasilisha. Tunaipongeza Serikali kwa ajili ya kuzifanyia matengenezo ya mara kwa mara barabara za Mkoani Kagera. Tunashukuru sana barabara ya Kagoma – Lusahunga, ikikamilika, itarahisisha usafiri na usafirishwaji kutoka kona hadi kona nyingine za nchi yetu.

160 Mheshimiwa Spika, tunaomba fedha iliyotengwa kwa ajili ya kukamilisha barabara ya Kyaka - Bugene zitolewe mapema ili kazi iishe. Aidha, tunaomba upembuzi yakinifu na usanifu katika barabara ya Bugene - Kasulo ifanyike kama hotuba inavyosema katika ukurasa wa 107 ibara ya 157.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kazi nzuri inayofanyika, naomba Mheshimiwa Waziri atakapokuwa anahitimisha, aeleze ili tujue ni kwa nini kipande cha barabara cha Bwanga - Kalebe hakijengwi kwa kiwango cha lami. Kipande hiki kinawafanya watu wajiulize maswali mengi. Aidha, kipande cha barabara cha Ruuzewe - Bwanga nacho kinastahili kujengwa kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, nawatakia Mheshimiwa Waziri utekelezaji mwema wa bajeti hii.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. PROF. KULIKOYELA K. KAHIGI: Mheshimiwa Spika, nianze kwa kumpongeza Waziri, Naibu Waziri na wataalamu wa Wizara ya Ujenzi kwa hotuba iliyoandaliwa na kuwasilishwa kwa umahiri mkubwa. Naipongeza pia Kamati ya Miundombinu na Kambi Rasmi ya Upinzani kwa hotuba zao ambazo zina mapendekezo mengi ambayo ni mazuri na ingefaa Wizara iyazingatie.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo napenda kulitanguliza ni kwamba Wizara hii ni muhimu kwa kuwa inasimamia sehemu ya muhimili wa uchumi,

161 miundombinu (barabara, vivuko na kadhalika). Kwa sababu hiyo, usimamizi thabiti unahitajika, na kwa jumla Waziri wa Ujenzi – Mheshimiwa Dkt. Magufuli na wasaidizi wake wanajitahidi kusimamia sekta hii muhimu kulingana na upatikanaji wa fedha. Kwa hili, wanastahili pongezi kwa kazi nzuri wanayoifanya. Pamoja na mafanikio ambayo Wizara hii imepata, bado inakabiliwa na changamoto mbili kubwa katika ujenzi wa barabara. Kwanza ni tatizo sugu la madeni katika miradi mingi inayogharamiwa kwa fedha za ndani na pili, ni tatizo la kiwango cha chini cha ubora katika utekelezaji wa baadhi ya miradi.

Mheshimiwa Spika, tatizo la kwanza, linaihusu miradi yote inayoendelea kutekelezwa iliyokaguliwa na Kamati ya Miundombinu tarehe 10/05 – 27/05/2012 Mikoa mbalimbali nchini. Madeni yanazidi kuongezeka pamoja na riba. Swali: Kwanini Serikali isitafute fedha za kutosha ili kumaliza kabisa tatizo hili?

Kuhusu tatizo la pili, hatua ambazo zimechukuliwa hadi sasa zimesaidia, hata hivyo ipo haja ya kuimarisha vigezo vya kuwateua Makandarasi na Wahandisi Washauri na pia kuimarisha usimamizi unaofanywa na TANROAD.

Mheshimiwa Spika, baada ya kuyasema hayo, napenda sasa kujielekeza kwenye Jimbo langu la Bukombe, nitaanza na barabara ya Uyovu – Bwanga. Katika mipango ya Wizara, barabara hii ni sehemu ya Mradi wa Uyovu - Biharamulo iliyo na kilometa 112. Katika mpango wa mwaka 2012/2013, mradi huu umetengewa Shilingi bilioni 2.4 ili uanze kutekelezwa.

162 Fedha hii ni kidogo sana kwa kilometa 112, lakini nafahamu kuwa huu ni mwanzo tu na mwaka 2013/2014 Wizara itatenga fedha zaidi. Je, barabara hii itaanza kujengwa lini na itaanzia wapi? Wananchi wanaulizia kuhusu fidia: Je, wale wanaostahili kufidiwa kisheria watafidiwa lini?

Mheshimiwa Spika, barabara nyingine ni ya Ushirombo – Geita. Hii barabara imeshapimwa na nyumba zilizo kwenye hifadhi ya barabara ziliwekewa alama ‘X’ toka mwaka 2010. Waathirika wa zoezi hili wakiungwa mkono na Madiwani, wamependekeza barabara hii ihamishwe na ianze eneo la Nipha badala ya kufuata njia iliyopimwa. Maswali: Wizara inaonaje ingehamisha barabara hii ili kuokoa fedha ambaye ingelipwa kwa waathirika wa upimaji kwenye njia iliyopo? Barabara hii ya Ushimbo – Geita itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami lini?

Mheshimiwa Spika, sasa nitazungumzia tatizo la maeneo katika Jimbo la Bukombe ambalo halifikiki kwa magari wakati wote wa mwaka. Maeneo hayo hayafikiwi kwa sababu ya mito inayoyatenga na maeneo mengine. Wananchi katika baadhi ya maeneo hayo wamejitahidi kujenga madaraja ya magogo. Nakayenze na Muhama/Ilyamchele wamefanya hivyo. Lakini madaraja ya magogo hayasaidii sana katika kubeba mazao ya kilimo kwa sababu magari hayawezi kupita kwenye madaraja hayo. Wagonjwa na akina mama wajawazito wanataabika sana kuja kupata huduma za afya kwenye Kituo cha Afya Uyovu.

163 Nilimtembeza Injinia wa Wilaya kwenye maeneo hayo, akanihakikishia kuwa Halmashauri haina uwezo, kwani panahitajika makalvati makubwa makubwa yenye gharama kubwa. Wananchi wa maeneno hayo wamenituma nilete ombi maalum kwa Waziri, wanaomba madaraja ya makalvati katika maeneo yafuatayo: Namonge – Muhama/Ilyamchele; Busonzo – Nakayenze; na Busonzo - Nalusunguti. Wananchi wako tayari “kusesa” barabara kwa njia ya kujitolea. Wananchi wanaomba Wizara iwasaidie.

Mheshimiwa Spika, jambo la mwisho ni malalamiko kuhusu kampuni ya ujenzi ya Strabarg ambayo ina mgodi wa kokoto Kata ya Busonzo, Kijiji cha Busonzo. Malalamiko yanahusu uharibifu wa vyumba vya madarasa ya Shule ya Msingi Busonzo. Injinia wa Wilaya ameshakagua uharibifu huo, lakini hadi sasa hakuna lililokwishafanyika. Vumbi la mgodi wa kokoto limesababisha uchafuzi wa vyanzo vya maji. Wanachoomba, ni visima virefu kama viwili na vile vilivyopo vifunikwe.

Mheshimiwa Spika, jambo hili pia linafahamika kwenye Halmashauri, lakini hadi sasa hakuna lililofanyika, wananchi wanaomba Wizara iingilie kati.

Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, naunga mkono hoja.

MHE. ASHA MOHAMED OMARI: Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi hii kumpongeza Mheshimiwa Waziri wa ujenzi kwa namna alivyopangilia hotuba yake kwa umakini mzuri.

164

Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi hizo nilitaka kuishuruku Serikali kuwa na utaratibu wa kuwa na miradi midogo ambayo ina uhakika wa kuimaliza kwa wakati kuliko kuwa na miradi mingi inayopewa fedha kidogo kidogo na hatimae inashindwa kukamilika kwa wakati, jambo ambalo lina hasara kutokana na Wakandarasi waliopewa barabara hizo kuidai Serikali fedha kwa kuchelewesha kutoa fedha.

Mheshimiwa Spika, Serikali inapopanga miradi ya barabara, ijaribu kuangalia Mikoa ambayo ipo haja ya kufungua, kama vile Mikoa ya Rukwa, Katavi na Kigoma; na Mikoa inayozalisha mazao ya chakula kwa wingi kwa sababu chakula ndiyo uti wa mgongo. Serikali iiangalie kwa jicho la huruma Mikoa hii.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. ALPHAXARD K. N. LUGOLA: Mheshimiwa Spika, naomba nichangie yafuatayo:-

Kwanza, nampongeza Waziri kwa juhudi zake kubwa katika ujenzi wa barabara hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, naomba maeneo yote ambayo ujenzi wa barabara unatakiwa kufanyika majengo yaliyomo ndani ya akiba ya barabara yaendelee kubomolewa bila kujali ni mali ya nani, vinginevyo, hatutajenga barabara. Lazima Sheria za Barabara zifuatwe na hususan Miji mikubwa.

165 Mheshimiwa Spika, kumekuwepo mkanganyiko juu ya matumizi ya alama ‘X’ kwenye majengo hasa ambayo yamo ndani ya akiba ya barabara. Kwa mujibu wa sheria mpya, mita 30, inakuwaje jengo ambalo sheria imelikuta lichafuliwe kwa alama ya ‘X’ na kumjenga hofu mmiliki akidhani hatafidiwa mali yake? Naomba nyumba kama hizo zisichafuliwe kwa vile kuwepo kwake siyo kwa kuvunja sheria mpya, japo sheria mpya imezikuta nyumba hizo, zibainike tu na baadaye zikifidiwa ndipo zibomolewe.

Mheshimiwa Spika, naishukuru Serikali kwamba sasa imeanza kutenga fedha za ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya Bunda – Kisonya – Nansio. Ningependa nijue, hizi fedha Shilingi bilioni 1.9 kama zinahusu na ulipaji wa madeni katika shughuli za upembuzi yakinifu. Aidha, kwa vile barabara hii inahusu Majimbo matatu, Bunda, Mwibara na Ukerewe, napendekeza ipewe Wakandarasi wawili, kwamba mmoja aanzie Kisorya kuelekea Bunda na mmoja atokee Nyamswa kuelekea Bunda ili ku-balance matarajio ya wananchi wa Wilaya ya Bunda.

Mheshimiwa Spika, napendekeza pia ujenzi uanzie Kisorya kuelekea Bunda kwa vile barabara hiyo inatuunganisha na Mkoa wa Mwanza kwa Wilaya ya Ukerewe ina viwanda vinne vya kuchambua pamba ambapo magari makubwa hubeba pamba kutoka Vijijini kwenda viwandani na kubeba marobota toka viwandani kupeleka Mwanza. Aidha, upande huo wa barabara, kuna maari yanayobeba samaki kupeleka viwandani Mwanza na Musoma na pia magari yanayobeba matunda kama maembe, mananasi na

166 machungwa, na mbao kutoka msitu wa Rubya Wilayani Ukerewe.

Mheshimiwa Spika, naomba Waziri anipe maelezo ya kutosha juu ya hoja zangu nilizozitoa ikihusu pia kivuko cha MV. Ukora nilichoomba kwa ajili yaKkisiwa cha Nafuba.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Spika, Wizara ya ujenzi ni chombo muhimu katika ujenzi wa Taifa. Miundombimu ya barabara na madaraja ni nyenzo muhimu ya kuinua uchumi wa nchi na kuboresha maisha ya wananchi katika kuchangia juu ya mapitio ya utekelezaji wa bajeti ya mwaka 2011/2012 na makadirio ya matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2012/2013. Naomba kujikita kwenye uchambuzi wa miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, kwenye mapitio ya utekelezaji wa miradi ya kupunguza msogamano katika Jiji la Dar es Salaam aya ya 82 (ukurasa wa 55) naomba Wizara ieleze pia usanifu wa flyover eneo la makutano ya Mandela na Morogoro eneo la Ubungo umefikia wapi? Aya ya 83 (ukurasa wa 56) naomba kupewa ripoti ya mpango wa awali ulioandaliwa kuhusu ujenzi wa barabara ya Dar es Salaam – Chalinze mpaka Morogoro kwa uratibu wa PPP, ni lini hasa Serikali imepanga ujenzi wa barabara hiyo kuanza?

167 Aidha Wizara imeelezwa kuwa barabara za Dar es Salaam, zimekasimiwa kuhudumumiwa na TANROADs, ufafanuzi utolewe juu ya kukasimiwa huko dhidi kwa barabara za Dar es Salaam aya ya 84 (ukurasa wa 57) barabara ya Ubungo Bus Terminal – Mabibio – Kigogo round about (6.4 km) utekelezaji umefika asilimia 82. Naomba nguvu iongezwe kurahishisha, kwa kuwa ni barabara ambayo ujenzi wake awali ulipangwa kuwa umekamilika mwaka wa fedha 2010/2011.

Vile vile, kwa barabara ya Tabata – Dampo – Kigogo Ubungo Maziwa External (2.25) maelezo ya kuwa usanifu umekamilika yamerudiwa tena kwa mara nyingine tena. Nilitarajia kuwa ujenzi ungeanza mwaka 2011/2012 na kukamilika mwaka 2012/2013. Hivyo badala ya maelezo kuwa fedha za ujenzi zinatafutwa, naomba Wizara ipitie kiasi kilichotengwa na TANROADs mwaka 2011/2012 na iongezee kiasi kingine cha fedha 2012/2013 ili ujenzi uanze na kukamilika kwa kuwa barabara hii ni fupi, lakini ina mchango mkubwa katika kupunguza foleni (aya ya 86 – ukurasa wa 57 na 58).

Mheshimiwa Spika, naomba kufahamu iwapo usanifu wa barabara tajwa uliofanyika umejumlisha pia tathmini ya fidia na kwamba kiasi gani cha fedha kinahitajika kwa ajili ya fidia na ujenzi wa barabara husika? Aidha, Wizara imeeleza kuwa hatua itakayofuata ni kutafuta fedha. Ninaomba kupata ufafanuzi, ni kwanini bado Serikali iko katika hatua ya kutafuta fedha wakati ambapo kwa mujibu wa Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano, barabara hizo zilipaswa ziwe zinatengewa fedha kama ifuatavyo:-

168

Mheshimiwa Spika, mwaka 2011/2012 Shilingi bilioni 68.6 na mwaka 2012/2013 Shiling bilion 31.5 (rejea ukurasa wa 147 na 152 aya ya 87); kuhusu ujenzi wa miundombinu ya mradi wa mabasi yaendayo haraka (DART BRT) (ukurasa wa 58 na 59), inaonyesha kwamba mradi utakamilika katika awamu ya kwanza mwka 2015/2016. Hivyo ni muhimu kuweka mkazo kwenye barabara za pete (ring roads) katika kipindi hiki cha mpito. Aidha, Wizara ya Ujenzi iombe msukumo kutoka Ofisi ya Rais na Waziri Mkuu kuhusu fidia kwenye Kituo cha Mabasi cha Ubungo (UBT) ili Mkandarasi asiendelee kuchelewa kuanzia kazi.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyochangia awali, kwamba nitajielekeza katika miradi ya kupunguza msongamano wa magari katika Jiji la Dar es Salaam, baada ya kufanya mapitio ya utekelezaji wa bajeti kwa mwaka wa fedha 2011/2012, naomba sasa nijielekeze kwenye makadirio ya matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa mwaka wa fedha 2012/2013.

Mheshimiwa Spika, ukilinganisha maelezo yaliyoko kwenye aya ya 167 (ukurasa wa 112 na 113 na 114) ambapo imeelezwa kuwa Wizara inaendelea kutekeleza miradi yenye thamani ya Shilingi bilioni 899 na ya aya ya 127 (ukurasa wa 90, 921 na 92) kwamba miradi inavyoendelea kwa Mikoa ya Dar es Salaam na Pwani ya Shilingi bilioni 961, inaonekana kwamba orodha ya mgawo wa fedha kwa miaka ya fedha 2010/2011, 2011/2012 na 2012/2013 inarudiarudia.

169 Pamoja na kushukuru kwa maelezo yaliyotolewa na kutambua pia kazi inayofanywa na Wizara ya Ujenzi ikiwemo katika Jimbo la Ubungo, kuna haja ya kuainisha miradi na mgawanyo wa fedha kwa kuzingatia Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano na vipaumbele vilivyopitishwa na Baraza la Mawaziri kuhusu miradi ya kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, naomba Waziri wa Ujenzi Dkt John Magufuli, Wizara ya ujenzi pamoja na vyombo vyake ikiwemo TANROADS, Mfuko wa Barabara Dar es Salaam na Taasisi zote kuzingatia yafuatayo, kuhusu makadirio ya matumizi ya Wizara kuhusu miradi ya kupunguza msongamano katika Jiji la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, Mosi, aya ya 167, (ukurasa wa 113 na 114) ujenzi wa flyover TAZARA uende sambamba katika mwaka 2012/2013 ili ujenzi wake uanze mwaka 2013/2014. Ukamilishaji wa barabara za pete (ring roads) za Ubungo Bus Terminal - Mabibo uende sambamba na ujenzi wa barabara ya chini ya kilometa 2.25 ya Ubungo Maziwa mpaka external ambayo tayari usanifu ulishafanyika. Barabara ya Mbezi Malamba – Kinyerezi – Banana (kilometa 14) kiasi kilichotengwa cha 1.75 mpaka Shilingi bilioni mbili ni kidogo sana. Barabara hii ina uwezo mkubwa wa kupunguza foleni. Hivyo, kiasi cha fedha kiongezwe. Pia kutenga Shilingi bilioni 4.3 tu kwenye barabara ambazo Wizara imezikasimu na TANROADS ni dalili kwamba matengenezo kwa sehemu kubwa itakuwa ni kwa kiwango cha changarawe. Ni vizuri pamoja na kupandisha hadhi barabara husika, Wizara ifanye

170 maamuzi ya kisera na kuharakisha ujenzi kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, pili, aya ya 168 (ukurasa wa 114, 115 na 116) barabara za pete (ring roads) kilometa 98.15 zimetengewa Shilingi bilioni 10.5 tu wakati ambapo kwa mujibu wa Mpango wa Miaka Mitano, kwa mwaka wa fedha 2011/2012 na 2012/2013, zilipaswa kutengwa jumla ya Shilingi bilioni 100.1.

Kwa kuwa foleni Dar es Salaam ni janga lenye hasara kubwa kwa uchumi wa nchi na maisha ya wananchi; na kwa kuwa miradi ya upanuzi wa barabara kuu ikiwemo ya Morogoro za mudawa kati; kwa hatua za muda wa dharura, Waziri wa ujenzi amshauri Mheshimiwa Rais ili nyongeza ya fedha iwekwe kwenye barabara na madaraja ya mzunguko ya pembezoni ili kupunguza foleni kama ilivyo katika mpango wa Taifa.

MHE. CAPT. JOHN Z. CHILIGATI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, naunga mkono hoja hii.

Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Watendaji wote wa Wizara na TANROADS kwa kazi kubwa na nzuri wanazozifanya za kutengeneza barabara takribani katika kila pembe ya nchi hii. Tunashukuru ujenzi wa barabara ya Dodoma - Manyoni – Singida na vile vile mradi wa barabara ya Manyoni – Itigi - Choya – Tabora. Ahsante sana.

171 Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi hizi, napenda kutoa maombi maalum kwa niaba ya wananchi wa Jimbo la Manyoni Mashariki kama ifuatayo:-

Mheshimiwa Spika, Bodi ya Barabara ya Lami ya Dodoma - Manyoni kupitia nje ya Mji wa Manyoni, Mheshimiwa Waziri Mkuu alitoa ahadi kwamba barabara iliyokuwa inapita katikati ya Mji (ukurasa wa 4) itajengwa kwa kiwango cha lami. Aidha, Wizara inalifahamu jambo hili na naomba utekelezaji ufanywe mwaka huu na fedha, kwani wananchi wanahisi Serikali imewadanganya.

Mheshimiwa Spika, ombi la kuipandisha daraja barabara ya Chikuji – Mijiri – Ikosi (kilometa 60), limewasilishwa Wizarani tangu mwaka 2010 kupitia kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa. Barabara hii inaunganisha truck road (Dodoma - Manyoni) na barabara ya TANROAD ya Manyoni – Sanza – Ikasi. Pia inaunganisha Mkoa wa Singida na Dodoma. Aidha, barabara hii inapita Kata za Chikiyu, Sesilo, Mjiri na Sanza, zenye kilimo cha mpunga ufuta karanga na mtama Pia ni eneo la ufugaji na viwanda vidogo vya kutengeneza chumvi. Kwa hiyo, naomba Wizara ikubali barabara hii iwe chini ya TANROADS, kwani Halmashauri haiwezi kutengeneza kwa kuwa uwezo wake ni mdogo.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa kilimo cha ukaguzi wa magari ya mizigo iendayo nje ya nchi, chini ya utaratibu wa East Africa Trade Facilitation, barabara ya korido ya kati vinajegwa vituo vitatu vya Ukaguzi wa

172 Magari ya Mizigo iendayo nje ya nchi (Transit Goods Inspection Centres). Vituo hivi vinatazamiwa kujengwa Vigwaza, Manyoni na Nyahuwa ili kupunguza kero ya magari hayo kusimamishwa kila mahali na kuchelewesha mizigo.

Mheshimwa Spika, napenda kuuliza: Je, ni lini vituo hivyo vitaanza kujengwa na ni lini viongozi wa maeneo hayo wataelezwa utaratibu mzima ili nao wahimize wajibu wao wa kuhakikisha maeneo ya ujenzi (site) zinawekwa katika miliki ya Serikali, na kama kuna umuhimu mzima, wafanyiwe utaratibu wa kuondoka kupisha mradi huo.

Mheshimiwa Spika, mwisho, naunga mkono hoja hii.

MHE. MARGARET S. SITTA: Mheshimiwa Spika, nawapongeza Mawaziri na Naibu Waziri kwa kazi nzuri wanayoifanya.

Mheshimiwa Spika, barabara za Mkoa wa Tabora zinazoendelea kujengwa, zinasuasua. Hali inayotupa wasiwasi sisi wakazi wa Mkoa huo. Je, Serikali inasemaje kuhusu kusuasua huko wakati Mkoa huo hauna hata barabara moja ya lami inayounganisha Mkoa huo na Mikoa mingine?

MHE. DKT. MILTON M. MAHANGA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Hata hivyo, nina mchango ufuatao:-

173 Mheshimiwa Spika, Mradi wa DART wa barabara mbili au tatu na flyover moja ya TAZARA haziwezi peke yake kuondoa msongamano katika Jiji la Dar es Salaam. Ili tatizo hili liondolewe, ni lazima barabara zote za ring roads na outer ring roads zijengwe, na hizi barabara haziwezi kujengwa haraka kwa utaratibu wa bajeti ya mwaka huu.

Mheshimiwa Spika, Serikali lazima iamue kwa makusudi kuweka programu mahsusi kwa ajili ya kujenga barabar za Dar es Salaam. Kwa mfano, tungeweza kuweka mpango wa miaka mitatu (2013/2014, 2014/2015 na 2015/2016) wa kutafuta na kukopa kwa kutumia Shilingi bilioni 300 (bilioni 100 kila mwaka) kujenga barabara zote za ring roads na za ndani za Jiji la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali sasa hivi itoe tamko la kuweka mpango huo kuanzia mwaka ujao wa fedha.

Mheshimiwa Spika, naunga tena mkono hoja hii.

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia hoja ya Waziri wa Ujenzi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nashauri kwamba mwaka huu wa Fedha, Serikali isianzishe miradi mipya ya barabara hadi hapo tutakapomaliza miradi ambayo imeshaanzishwa kwanza. Hata kama tukikopa, basi tukope kukamilisha kwanza iliyoanza na kisha baada

174 ya hapo ndiyo tuanze awamu nyingine ya barabara mpya.

Mheshimiwa Spika, kuna ubadhirifu mkubwa katika ujenzi wa barabara na madaraja nchini. Hali hii husababishwa pamoja na mambo mengine yafuatayo: uwezo mdogo wa Makandarasi kulingana na uwezo wao. Suluhisho la jambo hili, nashauri kwamba vitengo vya Ugavi katika Taasisi za Umma zisitoe mikataba kwa Makandarasi pasipo kupata clearance toka kwa Bodi ya Makandarasi (CRB – Contactors Registration Boards) ambao ndiyo wanajua hali halisi na uwezo wa Makandarasi katika nchi nzima.

Mheshimiwa Spika, ni vyema pia Mkandarasi anapoharibu Mkoa au eneo moja asikimbilie Mkoa au eneo lingine na akapewa kazi au mradi mwingine wa ujenzi.

Mheshimiwa Spika, CRB ishirikishwe kwenye Public Procuring Units za Taasisi za Umma as a compulsory case katika kufanya due diligence case. Itasaidia sana kudhibiti Wakandarasi wasio na sifa, kupata miradi ambayo hatimaye haikamiliki kwa kiwango na muda stahiki.

Mheshimiwa Spika, ujenzi endelevu wa nchi yetu hauwezi kutegemea wageni milele. Ni kweli kuwa Makandarasi Watanzania walio wengi hawana uwezo mkubwa wa kuhimili miradi mikubwa itakayohitaji mitaji mikubwa, utaalamu na teknologia ya kisasa sambamba na mitambo mikubwa na ya kisasa. Ni vyema basi, sasa tuwajenge Makandarasi wetu kwa

175 kutunga sheria itakayowalazimisha Makandarasi wa nje ku-subcontract local contactors katika miradi yote wanayopata angalau kwa 20 – 30 %.

Mheshimiwa Spika, Bajeti ya mwaka huu imeninyonga. Barabara yangu ya Kwa-Sadala – Masama, imetengewa jumla ya shilingi milioni 150 katika Mradi wa zaidi ya shilingi bilioni tano. Imagine yule contractor aliyeko site kwa miaka miwili sasa atafanyaje; ilikuwa contract ya one year?

Mheshimiwa Spika, babaraba yangu ni hiyo moja tu, Serikali ingefunga macho ikatujengea.

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Spika, nampongeza Waziri wa Ujenzi Dkt. John P. Magufuli kwa hotuba nzuri, kadhalika na watendaji wa Wizara yake. Napenda kuchangia mambo machache kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, napenda kushauri kwamba, TBA ifanye kazi kibiashara. Kuna majengo mengi ya Halmashauri, majengo ya Mashirika ya Umma na kadhalika, Uongozi wa TBA wasijifungie Ofisini, watafute tenda zinazotangazwa na kufanya kazi kibiashara zaidi.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kwa uamuzi wa kupanua barabara za Jiji la Dar es Salaam kwa njia ya mabasi yaendayo kasi. Naiomba Serikali mwaka ujao wa fedha, barabara hizo ziwe zimekamilika ili Watanzania waepukane na usumbufu kupoteza muda mwingi njiani bila kazi, bila sababu.

176 Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais aliwaahidi wananchi wa Kongwa na Mpwapwa kwamba barabra ya Mbande – Kongwa – Mpwapwa itajengwa kwa kiwango cha lami. Hadi sasa hakuna kinachoendelea. Wananchi hao wanaomba kujua kilichokwamisha ujenzi wa barabara hiyo japo upembuzi yakinifu ulishafanyika.

Mheshimiwa Spika, Daraja la Kigamboni limezungumzwa sana tangu mwaka 2007, nashauri ifike wakati sasa daraja hilo lianze kujengwa. NSSF walikuwa tayari kuanza ujenzi wa daraja hilo miaka mitano iliyopita. Pia wananchi wajulishwe tatizo ni nini kati ya Serikali na NSSF.

Mheshimiwa Spika, naomba kujua hatua iliyochukuliwa kwa Mkandarasi aliyejenga barabara ya Singida - Shelui na Msimamizi wa ujenzi wa barabara hiyo, kwani barabara hiyo iliharibika na kuwa na mashimo makubwa baada ya mwaka mmoja tu. Hatuwezi kuendelea kwa kuwaendekeza wabadhirifu wa mali ya umma.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. DKT. PUDENCIANA W. KIKWEMBE: Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia katika maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, naishukuru Serikali kwa kuweza sasa kuikumbuka Mikoa ya Kusini hasa Katavi na Rukwa, kwa kuifungia Mikoa hiyo ili wananchi waweze kujiwezesha kiuchumi, kwani Mikoa hiyo ni sehemu muhimu katika uzalishaji mali hasa mazao ya chakula.

177

Mheshimiwa Spika, napenda kuiomba Serikali ifikirie namna ya kuunganisha Wilaya ya Kaliuwa na Mpanda kwa upande wa barabara kwa kupitia Ugala. Serikali haijatenga fedha katika eneo hilo, yaani barabara hiyo. Hivyo basi, ni vyema Serikali itafute pesa kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo ili iweze kuunganisha Wilaya ya Kaliua na Mpanda, kwani kwa kutegemea reli pekee yake ambayo kwanza ni kama mara mbili tu kwa wiki. Hivyo ni vyema barabara hiyo ikatengewa pesa kutokana na umuhimu wake kiuchumi na pia ni rahisi kupita kwa barabara hiyo, kwani itaondoa usumbufu wa kuzunguka Tabora ndipo ufike Kaliua. Hivyo naomba Serikali ione umuhimu wake; ni vyema kutumia barabara hiyo kwani ni kama kilometa 200 toka Kaliua – Mpanda kuliko kuzunguka Tabora, ambapo ni kama kilometa 500. Barabara hii itawasaidia zaidi wananchi wa Ugala ambao wengi ni wakulima kupitisha mazao yao kupitia Kaliua Tabora.

Mheshimiwa Spika, barabara toka Ilunde mpaka Tabora kutoka Kata ya Ilunde kwenda Tabora ni karibu sana kuliko wananchi kuzunguka Inyonga – Tabora. Hivyo basi, naiomba Serikali iangalie na iipatie kipaumbele barabara hiyo ili wananchi waweze kupunguza makali ya nauli na gharama nyinginezo ili kujiinua kiuchumi, kwani eneo la Ihunde limekuwa kama kisiwa na wananchi hawana mawasiliano ya aina yoyote.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

178 MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Spika, napenda kuwasilisha kwako mchango wangu katika hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi kuhusu makadirio ya matumizi ya fedha ya Ofisi yake kwa mwaka 2012/2013 kama ilivyowasilishwa Bungeni.

Mheshimiwa Spika, kwanza, naanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli – Waziri wa Ujenzi kwa uwasilishaji wake mzuri na wenye weledi uliotukuka. Pili, nampongeza kwa utendaji makini wa majukumu yake. Nampongeza pia Naibu Waziri wa Ujenzi -Mheshimiwa Gerson Lwenge, utendaji mzuri umeonyesha ni jinsi gani yupo makini.

Mheshimiwa Spika, tatizo la bomoa bomoa limekuwa ni kero ya kwanza, na ni la kipaumbele kabisa kwa nchi nzima, maana malalamiko ni makubwa. Naiomba Serikali isikie kilio hiki kwa kuzingatia haki. Katika eneo la Jimbo la Kilwa Kaskazini, mathalan, wananchi wemejenga wakati kabla hata ya sheria iliyotajwa kutungwa na kuridhiwa na Bunge ama kuidhinishwa na mamlaka husika. Hili limethibitshwa na historia ya nchi yetu kwamba Wakoloni wamekuwepo kuanzia karne ya 18 na kabla ya hapo walikuwapo Waarabu na Washirazi katika maeneo ya Kilwa.

Mheshimiwa Spika, hivyo, sikubaliani kabisa kuwa uwepo wa wananchi hawa katika maeneo hayo ni kuvunja sheria, kwa tafsiri kwamba wamekuwapo kabla. Lakini haitoshi, itakua pia Katiba inakiukwa kama ibara ya 13(1) ambayo inatamka kwamba watu wote ni sawa mbele ya sheria na wanayo haki bila ya

179 ubaguzi wowote, kulindwa na kupata haki sawa mbele ya sheria.

Mheshimiwa Spika, Bunge la February, 2011, tumejadili na kuridhia hotuba ya Mheshimiwa Rais ambayo aliisoma wakati wa uzinduzi wa Bunge la Kumi. Katika vipaumbele 13, ameainisha kuwa Serikali itafanya kila iwezalo kuwawezesha wananchi. Je, wananchi wanawezeshwaje kwa kuwavunjia nyumba zao na kupoteza mali zao bila ya fidia? Naiomba Serikali katika hili utumie busara zake na usikivu wake na kuwasaidia wananchi na kuokoa mali zao ambazo wamezipata kwa jitihada kubwa na za muda mrefu ili tusiwakatishe tamaa na kuwaweka katika hali tata. Ifikiriwe namna hata kwa kuwapa kifuta machozi, kwani upande wa Serikali pia umechangia wao kuingia katika tatizo, kwa maana uongozi na Watendaji wa chini hawasimamii ipasavyo sheria husika na kuruhusu wananchi kujenga holela.

Mheshimiwa Spika, tatizo la ujenzi wa barabara, gharama zinaongezeka kila siku. Ifike wakati sasa tuwe na mpango mkakati kuhakikisha tunamaliza ujenzi wake haraka na kuepuka gharama ambazo zinaongezeka kwa kasi sana. Lakini sasa tuhakikishe makampuni ya kitanzania yanapewa (yanajengewa) uwezo ili yaweze kushiriki kikamilifu katika miradi kwa maana ya kuwa tunaposhirikisha kampuni za nje, tunatoa pesa zetu nyingi na tunaimarisha uchumi wa nchi nyingine.

Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia taarifa ambazo zimekuwa zikitolewa na vyombo vya habari, wananchi,

180 lakini hata ushuhuda wake Mheshimiwa Waziri katika hotuba kwa barabara za Kilwa, Dar es Salaam, Nangurukuru, Mingoyo na kwingineko, mara kadha Wakandarasi wengi wanakiuka vigezo vilivyowekwa na kufanya kazi bila kufikia vigezo. Barabara zinapojengwa kabla ya kumaliza hata miezi miwili, inakuwa na mawimbi, lakini pia inakua ishaharibika. Namwomba Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri kuongeza jitihada na kuongeza adhabu kwa Wakandarasi wa aina hii, kwani wanaipa gharama kubwa Serikali kuyumbisha mipango ya Serikali.

Mheshimiwa Spika, Ofisi za mikoa za wakala wa barabara (TANROADS) zipewe uwezo na kufuatilia kwa ukaribu kandarasi ambazo wanatoa. Izingatiwe kuwa mara kadha sasa wakandarasi wake kuwa wababaishaji, hawatekelezi kwa wakati na viwango. Hii ni jambo linalokera sana na kuwafanya wananchi wasiwe na imani na Serikali yao.

Mheshimiwa Spika, lipo tatizo katika matumizi ya madaraja, hasa daraja la Mkapa ambapo sasa wafugaji wamekuwa wanapitisha mifugo juu yake. Licha ya kuhatarisha usalama kwa watumiaji wengine, pia ni matumizi mabaya. Kwanini wasitumie magari?

Mheshimiwa Spika, wakati wa ziara ya kampeni, Mheshimiwa Rais alitoa ahadi kwa wananchi wa Kilwa Kaskazini kuwa barabara ya Kipatimu - Nyamwage itajengwa. Naiomba Serikali itekeleze ahadi hii haraka ili kuwaondolea kero wananchi.

181 Mheshimiwa Spika, pamoja na ufuatiliaji mzuri wa viongozi wa Wizara hizi, naishauri Serikali ihimize na kuhakikisha barabara ya Ndundu – Somanga inakamilika kwa wakati, ili iwe na pumziko kwa wananchi wa Kilwa na Mikoa ya Kusini kwa ujumla ambao kwa kipindi kirefu wameteseka na kutopata kutumia vyema fursa za kiuchumi zilizopo. Hotuba ya Mheshimiwa Waziri kwenye aya 45 imeonyesha hatua mbalimbali ambazo barabara hii imefikia pamoja na kutenga fungu la Shilingi bilioni 4.0071 kwa ajili ya ukamilishaji wa barabara hii Oktoba, 2012.

Mheshimiwa Spika, jitihada zimefanywa kwa barabara ya Nangurukuru – Njinjo - Liwale na ile ya Njia nne, Kipatimu. Tunaishukuru sana Serikali kwa jitihada zake, ila sehemu korofi bado zinahitaji jitihada zaidi kurekebishwa na kuimarishwa ili barabara ipitike wakati wote.

Mheshimiwa Spika, tatizo la Kivuko cha Kigamboni, naishauri Wizara ifanye utafiti wa haraka na kuwaondolea kero wananchi, malalamiko mengi sana, kutokana na uendeshaji wake.

Mheshimiwa Spika, nimekuwa nafuatilia kwa makini jitihada za Serikali katika kuondoa kero za msongamano wa magari hasa katika Jiji la Dar es Salaam, ila kwa sasa sikubaliani na wazo la kujenga fly overs. Mpango ni mzuri, ila haufai kwa sasa. Ni vyema tukaimarisha barabara ya Kilwa na kujenga barabara ambayo itaanzia Mbagala hadi Kisarawe na kutokea Mlandizi au Chalinze. Hii itapunguza sana traffik volume na kuongeza wepesi zaidi kwa watumiaji wa

182 pembezoni mwa Mji kama Mbagala, Chamazi, Kisarawe, Ukonga, Pugu, Segerea kutolazimika kufika maeneo ya Mjini ili kuweza kupata Morogoro Road. Lakini pia itasaidia kuboresha maeneo ya pembezoni mwa Mji na kupunguza magereji ya Mtaani kwa maana huko pembezoni zinaweza kujengwa. Halmashauri za Wilaya husika zinaweza kunufaika kwa kujenga maeneo ya maegesho (trunk ports) ambazo zitaondoa kabisa tatizo la maegesho Mijini au katika maeneo yasiyostahili.

Mheshimiwa Spika, kwa haraka, tatizo la msongamano linaweza likapungua kwa kuweka muda maalum (saa 2.00 usiku) wa malori kutoka bandarini au nje ya Mji kwa maana yenyewe ndiyo husababisha sana msongamano.

Pamoja na yote haya, naishauri Wizara ishirikiane na Wizara ya Mambo ya Ndani (Askari Polisi) kuhakikisha madereva hasa wa daladala kuwa wazingatie sheria zilizowekwa na wanaokiuka wapewe adhabu ili iwe funzo na mfano kwa wengine.

Mheshimiwa Spika, tatizo la msongamano pia linasabishwa na mizani katika baadhi ya maeneo kutokana na ufinyu wa eneo ama uwezo wa mizani kupima kwa wakati malori na mabasi. Hii inasababisha kero kubwa kwa abiria, lakini pia inachangia msongamano usio wa lazima. Napendekeza mabasi ya abiria na malori ya mafuta yasipimwe kwa maana hayawezi kuongeza mzigo njiani baada ya kupakia.

183 Mheshimiwa Spika, kumekuwa na tatizo la ung’olewaji na uharibifu mkubwa sana wa alama za barabara ambazo huwa zinagharimu sana, ila wachache wanatumia kwa kuuza chuma chakavu bila kujali thamani halisi au madhara yanayotokea. Sheria kali itungwe au zilizopo zisimamiwe kukomesha hali hii.

Mheshimiwa Spika, Wakala wa Nyumba za Serikali kwa kipindi kirefu wamekuwa wanashiriki katika miradi kadhaa ambayo ina faida sana. Tatizo kubwa ni mtaji wa kutosha. Naishari Serikali itenge mtaji wa kutosha na ikiwezekana hata kwa kuruhusu washirikiane na Taasisi nyingine za umma kama NHC, NSSF, PPF na mifuko mingineyo ya jamii.

Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kupokelewa maoni yangu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. RIZIKI SAID LULIDA: Mheshimiwa Spika, natoa pongezi za dhati kwa Waziri wa Ujenzi - Mheshimiwa John Pombe Magufuli.

Mheshimiwa Spika, barabara zifuatazo Mkoa wa Lindi ni kero sana kupita barabara zote nchini.

Mheshimiwa Spika, Lindi inahitaji huruma ya kipekee. Mkoa wa Lindi leo hii mwananchi wa Liwale anapata taabu ya kusafiri kutoka Dar es Salaam - Lindi - Masasi - Liwale. Wananchi wa Liwale hawana mtetezi hivyo, naomba Mheshimiwa Waziri awakomboe kwa

184 kuwajengea barabara ili wapunguze adhabu ya nauli na wenye magari walete magari yao.

Mheshimiwa Spika, Mkoa wa Lindi hauna lami katika barabara zake za Mkoa, hivyo kuwa na kero ambazo hazina mwisho.

Mheshimiwa Spika, namwomba Mheshimiwa Waziri mwenye dhamana asaidie barabara zifuatazo: Mchinga – Kijiweni, Mkwajuni – Matapwa, Chikonji – Nangaro, Nangurukuru – Liwale, Nanganga – Nachingwea – Liwale.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, fidia kwa wananchi wa Kijiji cha Chala katika Mradi wa ujenzi wa barabara wa Sumbawanga-Kanazi hawajafidiwa lakini pia maeneo ya mashamba yanayochimbwa changarawe hawajalipwa, ni kero kubwa sana.

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya iliomba barabara zake mbili zipandishe hadhi kwa kuwa haina uwezo kuzihudumia, Mkoa ulizipitisha, Kamati ya Kitaifa ilikuja ikasema zina sifa, nimezisemea sana sana hapa Bungeni, nimeshauriwa kuomba ombi maalum, lakini hazijasaidiwa hata kidogo.

185 Mheshimiwa Spika, nakuomba zisaidie uokoe vifo vya watoto na akinamama, ni vingi. Barabara hizi ni ahadi ya Mheshimiwa Rais Jakaya Kikwete.

Mheshimiwa Spika, tuanze kuona umuhimu wa kujenga Reli toka Mpanda na Sumbawanga kwenye Maghala ya nafaka, ili kupunguza gharama za Serikali za kusambaza chakula nchini.

Mheshimiwa Spika, nimeona miradi inayosimamiwa na Wizara, utaona fedha zimepelekwa katika baadhi ya Mikoa huku Mikoa mingine ikipata kiduchu tu, na hii unaoina hata mwaka uliopita kana kwamba sehemu nyingine hazina changamoto.

Mheshimiwa Spika, vile vile fedha inayopelekwa kwenye Mikoa mingine mwaka hadi mwaka mwingine huku Mikoa kama Rukwa ikipata kiduchu, angalia mfano hapo chini; Kilimanjaro mwaka 2011/2012 Shilingi milioni 1.2; mwaka 2012/2013 Shilingi milioni 106; Manyara Shilingi milioni 584.98; mwaka 2012/2013 Shilingi milioni 2,480; Rukwa Shilingi milioni 320, mwaka 2012/2013 Shilingi milioni 450; Simiyu Shilingi milioni 400; mwaka 2012/2013 Shilingi milioni 1,010. Tofauti hii sababu yake ni nini hasa?

Mheshimiwa Spika, Rukwa ndiyo kimbilio wakati wa njaa, Rukwa imekithiri kwa viwango visivyoridhisha vya ufaulu ukilinganisha na Mikoa iliyopiga hatua. Rukwa kunahitaji upendeleo ili kuikuta Mikoa ya Kaskazini Mashariki mwa Tanzania ambao licha ya barabara zao kuwa nzuri, wanapewa fungu kubwa

186 hata kuzidi Wanarukwa ambao vifo vya akina mama na watoto ni vingi.

Mheshimiwa Spika, naomba maelezo.

MHE. IDDI M. AZZAN: Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi kwa Waziri, Naibu Waziri na Watendaji wote wa Wizara hii kwa juhudi kubwa wanazofanya kuhakikisha nchi inapitika kwa barabara nzuri, lakini bado naiomba Serikali na Wizara kuhakikisha msongamano wa magari Dar es Salaam unakwisha.

Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara ya Kigogo – Tabata Dampo, tumekuwa tukiomba kwa muda mrefu ili barabara hiyo ijengwe kwa kiwango cha lami ili kuondoa usumbufu na msongamano usiokuwa wa lazima.

Mheshimiwa Spika, ni mategemeo yangu kuwa pesa kidogo zilizotengwa kwa barabara hii zitatumika angalau kwa kujenga kilomita chache za lami.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni kituo cha mabasi kilichojengwa kwenye viwanja vya michezo Jangwani, kwa kuwa mmechukua eneo hilo na kufanya vijana washindwe kucheza kwa kukosa viwanja, hivyo basi, naiomba Wizara isaidie kuboresha eneo lililobaki pale jangwani kwa kulijaza vifusi na kusawazisha pamoja na kupanua mifereji ya maji ili eneo hilo litumike kama viwanja vya kuchezea vijana wetu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

187

MHE. JOSEPH O. MBILINYI: Mheshimiwa Spika, nakubaliana na mpango wa Serikali kujenga barabara ya Mbeya – Makongorosi (Chunya). Wanambeya tunatambua umuhimu wa barabara hii kwa maendeleo ya uchumi wetu kama Mkoa. Lakini naishauri Serikali ishughulikie kwa busara na umakini na pia kwa kujali utu suala la wahanga wa bomoa bomoa inayotokana na mradi huo ambao ni wakazi wa Mbeya Mjini na Kata za Isanga na Iganzo. Kuna utata mkubwa katika zoezi zima la bomoa bomoa kitu ambacho kimezaa manung’uniko ya muda mrefu sasa kwa wakazi wa maeneo ya Kata nilizozitaja.

Mheshimiwa Spika, wahanga wale hawakubaliani, na wanataka kujua Serikali ilitumia vigezo gani kulipa fidia kwa baadhi ya wananchi na wengine wengi kukosa fidia hiyo, wakati ukweli ni kwamba wote nyumba zao ziko umbali sawa wa mita 15 kutoka barabarani. Mheshimiwa Spika, mkanyanyiko huu wa malipo kwa wahanga ni mkubwa na ndiyo maana nikashauri busara na umakini hasa ukizingatia Isanga na Igauzo ni Miji mikongwe iliyojengwa miaka mingi kabla hata mipango ya barabara hiyo. Zaidi, wananchi walichanganywa kwa Serikali kupima mara mita 15 mara mita 25 na sasa tena wanaambiwa watabomolewa mita 30.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Spika, naomba kumpongeza Waziri, Naibu Waziri na Watendaji wote katika Wizara hii kwa kazi nzuri ya utumishi wa kutumikia Taifa letu.

188

Mheshimiwa Spika, naomba kumshauri Waziri kuhusu uimarishaji wa kitengo cha kuzuia na kupambana na majanga. Risk Management Department ni kitengo muhimu sana ili kutoa ushauri na kusimamia miradi yote ya ujenzi katika Wizara hii (uhakiki).

Mheshimiwa Spika, naamini Wizara inaweza kuandaa utaratibu mzuri kwa kila Jimbo la mbunge ili iweze kuwa rahisi kwa kutumia jedwali lililo na takwimu zinazowezesha Waheshimiwa Wabunge kuwa na uelewa wa kueleza wapiga kura wao.

Mheshimiwa Spika, nashauri vigezo katika nidhamu ya usimamizi wa ujenzi vizingatiwe, scope, time, cost, quality, integration, human resources, communication, risk, procurement and contract.

Mheshimiwa Spika, Watanzania wanataka waone matokeo na matarajio kutoka kwenye miradi yote ya ujenzi, in other words make the project happen.

MHE. MOZA ABEDI SAIDY: Mheshimiwa Spika, bajeti ya Wizara ya Ujenzi ni nzuri iwapo itatekelezeka. Serikali inajitahidi kutenga bajeti yake ipasavyo kutokana na mahitaji, ni mengi, lakini Wakandarasi wanaoajiriwa hawana viwango vya ujenzi wa barabara, hata madaraja kutokana na kuwa kuna maeneo barabara ina upana mita 20 kwingine 10, kitu ambacho hata gari hazipishani. Hilo liangaliwe.

189 Mheshimiwa Spika, pesa nyingi zinazotengwa kwenye maeneo ya Wilaya hazifiki kwa wakati na barabara nyingi hazitengemai kutokana na kujengwa wakati wa mvua.

Mheshimiwa Spika, kwanini Serikali isijenge barabara moja ikakamilika kwa kiwango cha lami na pesa nyingi hupotea? Naomba Waziri afuatilie, hata barabara za Wilayani hasa huko Kondoa, ni nyingi, korofi, na zinapoteza pesa za Serikali.

Mheshimiwa Spika, miundombinu katika nchi yetu bado ni ya mfumo wa toka awali ya matumizi mabaya ya ardhi na kusababisha migogoro ya wananchi na Serikali kupisha ujenzi wa sasa na mipaka ya barabara.

MHE. DKT. TEREZYA P. L. HUVISA: Mheshimiwa Spika, nawapongeza sana Waheshimiwa Mawaziri na Watendaji wote wa Wizara kwa kazi nzuri za ujenzi wa barabara nchi nzima.

Mheshimiwa Spika, naomba sana barabara ya kutoka Namtumbo mpaka Tunduru ipewe kipaumbele. Mkandarasi aliyepewa barabara hii, hafanyi kazi, barabara imesimama. Hiki ni kilio cha wananchi wa Songea, Namtumbo na Tunduru.

Mheshimiwa Spika, tafadhali sana tunaomba wakandarasi waliopewa barabara hiyo, kama hawawezi, waondolewe na wapewe Makandarasi watakaofanya kazi vizuri.

190 Mheshimiwa Spika, nawapongeza sana na hongera kwa kuisimamia Wizara vizuri.

MHE. SABREENA H. SUNGURA: Mheshimiwa Spika, nami napenda kuchangia hotuba hii kama ifuatavyo:-

Kwa kuwa barabara ni muhimu hasa katika Nyanja za kikuchumi, hivyo basi, ni lini barabara ya Kigoma - Nyakahazi itakamilika? Lakini pia barabara ya Tabora - Kigoma ni lini itamalizika?

Mheshimiwa Spika, kumekuwa na tatizo kubwa la mashimo katika barabara zetu hususan maeneo ya Sekenke. Majambazi wanachimba mashimo makusudi ili gari zikwame wafanye uharamia. Je, Waziri hili halijui? Kama analijua, anachukua hatua gani?

Mheshimiwa Spika, kata ya Kagera katika Manispaa ya Kigoma Ujiji inatenganishwa na maeneo ya Kabogo Mgumile na Mto Lwiche na wananchi wengi wamepoteza maisha wakiwa wanavuka hususan wanawake na watoto. Je, ni lini Serikali itajenga daraja kwenye mto huo wa Lwiche? Mheshimiwa Spika, mwaka 2011 zilitengwa fedha kwa ajili ya miradi maalum ya ujenzi wa barabara takriban Sh. 348,075,000,000/=, na fedha hizi Serikali ilisema ni kwa ajili ya utekelezaji wa miradi tunayotakiwa tuchangie fedha (counter part fund) ili tupewe mkopo. Je, mwaka huu hatupewi mikopo? Mbona hakuna fedha yoyote iliyotengwa?

MHE. EZEKIEL M. MAIGE: Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri

191 wa Ujenzi, Daktari John Magufuli na Naibu wake Engineer Gerson Lwenge pamoja na viongozi wengine wa Wizara hiyo kwa kazi kubwa na nzuri wanayofanya ya kuboresha mawasiliano ya barabara na vivuko hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, nimeisoma hotuba ya Bajeti ya Waziri na kwa kiasi kikubwa sana imezingatia mpango wa Maendeleo wa Taifa pamoja na Ilani ya CCM ya mwaka 2010. Kwa kutambua kwamba Ilani ya miaka mitano, nina imani kwamba machache ambayo hayajatengewa fedha mwaka huu yatazingatiwa katika bajeti tatu zijazo kabla ya muda wa mwisho wa Ilani, yaani 2015. Hivyo, naunga mkono hotuba hii.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kutambua ukweli kwamba, ahadi zetu za uchaguzi nyingi bado tuna muda wa kuzitekeleza, naomba niikumbushe Wizara juu ya ahadi zifuatazo na hivyo kuitaka izingatie katika mipango yake na kwa kweli ni lazima maandalizi na utekelezaji walau uanze mwaka huu wa bajeti.

Mheshimiwa Spika, barabara zilizoahidiwa kujengwa kwa kiwango cha lami katika Jimbo langu la Kahama–Buyange–Bukoli-Geita na barabara ya Kagongwa–Itoba–Bukene–Mombali–Tabora. Barabara hizi hazijatengewa fedha za feasibility study na Detailed Design kwa mwaka huu. Mbaya zaidi, kwa upande wa Mkoa wa Geita fedha zimetengwa kwa ajili ya kuanza feasibility study na detailed design ya barabara ya Geita, Kahama upande wa Geita, lakini upande wa Shinyanga hakuna fedha zilizotengwa! Je, lami itakapoanza kujengwa itaishia upande wa Geita

192 pekee? Naomba Wizara, itenge fedha na za barabara hiyo upande wa Shinyanga (Buyange – Kahama) ili kazi iende kwa pamoja.

Mheshimiwa Spika, barabara hizi, ambazo ni kiunganishi cha Mkoa wa Shinyanga na Tabora na Shinyanga na Geita ni barabara muhimu sana kiuchumi. Barabara ya Kahama–Geita ambayo inahudumia migodi mikubwa ya dhahabu ya Bulyanhulu na Geita imekuwa ikipigiwa kelele sana na wananchi kutokana na vumbi linalotimuliwa na malori makubwa ya bidhaa na malighafi za migodi hii. Aidha, kutokana na kuwa bize sana, uharibifu ni mkubwa sana.

Mheshimiwa Spika, kama nilivyoshauri wakati nachangia bajeti ya Waziri Mkuu, tarehe 27 Juni, 2012, ni vyema Serikali ikashirikisha wawekezaji wa mgodi wa Bulyanhulu (ABG) kwa kuingia mkataba wa kugharamia ujenzi wa barabara hii kwa lami na kuweka makubaliano ya kukatana kwenye mrahaba na kodi zingine kwa muda ambao mgodi utakuwepo. Hivyo ndivyo PPP na ndiyo njia sahihi ya kuondoa kilio cha wananchi kutonufaika na dhahabu na madini yao mwingine kwenye maeneo yao.

Mheshimiwa Spika, tayari mgodi wa Geita, kwa kuzungumza na uongozi wa Mkoa wa Mwanza au Geita, umeonesha njia ya kushiriki katika ujenzi wa kipande cha barabara ya Geita–Bukoli-Buyange- Kahama kwa upande wa Geita. Naiomba Wizara ishiriki katika mazungumzo haya na wawekezaji na iwashawishi wawekezaji wote (wa Geita na Bulyanhulu)

193 washiriki katika ujenzi wa barabara hii kabla ya 2014. Naomba Serikali itoe ahadi kuhusu utekelezaji wa ujenzi wa barabara hii sasa.

Mheshimiwa Spika, katika hali ya sasa barabara ya Kahama–Bulyanhulu inakarabatiwa na TANROADS Shinyanga kwa kiwango cha changarawe. Hata hivyo, kumekuwepo ukiukwaji wa makubaliano kati ya Bulyanhulu Gold Mine na TANROADS kuhusu ugharamiaji wa ukarabati huo. Mwaka 1996 Wizara ya Ujenzi iliruhusu mgodi wa Bulyanhulu kutumia barabara hiyo kupitishia mizigo yao kwa makubaliano kwamba watawajibika kuitengeneza, lakini toka mwaka 2008 mgodi haufanyi matengenezo ya barabara hiyo!

Mheshimiwa Spika, naomba Wizara ichukue hatua kuhusu mgodi huo na kuwajibika kukarabati barabara hiyo kama walivyokubaliana mwaka 1996. Hii itaipa nafasi TANROADS Shinyanga kuhudumia barabara zingine za Shinyanga. Kwa upande wa barabara za Kagongwa–Itobo–Bukene–Mambali-Tabora na Kahama–Kaliua–Mpanda ni vyema na muhimu Wizara kuanza upembuzi yakinifu mwaka huu kwani muda wa ilani unayoyoma.

Mheshimiwa Spika, naomba Waziri atoe kauli kuhusu barabara ya Kahama–Geita katika majumuisho yake kesho.

Mheshimiwa Spika, nashukuru sana.

MHE. NIMROD E. MKONO: Mheshimiwa Spika, kwa miaka 12 mfululizo nimekuwa napiga kelele kuhusu

194 ujenzi wa barabara tatu (3) ambazo ni muhimu sana katika uchumi wa Wilaya ya Musoma. Kilio cha wananchi wa Musoma Vijijini mwaka hadi mwaka hakijasikika. Barabara ambazo zimekuwa nikizipigia kelele ni:-

- Barabara toka Makutano–Butiama- Nyamuswa–Nata–Mugumu/Loliondo hadi Mto wa Mbu, maarufu kama Barabara ya Nyerere.

- Barabara toka Musoma mjini kwenda Busekela ikipitia Mugango, Suguti, Murangi, Bukima, Makojo, hadi Busekila, maafuru kama Majita Road.

- Barabara toka Kirumi iendayo Serengeti kupitia Kiagata, Sirari Simba hadi Mugumu, maarufu kama barabara ya Kiagata.

Mheshimiwa Spika, barabara ya makutano Nata, Mugumu/Loliondo, Mto wa Mbu imekuwa ndani ya Ilani ya CCM tangu enzi za Mwalimu Nyerere takribani miaka 40 sasa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na lugha kwamba tunamuezi baba wa Taifa nashangaa kuona kwamba barabara ya Makutano-Nata–Mto wa Mbu ambayo wakati wa uhai wake wote Mwalimu Nyerere aliipigania ijengwe na Serikali hadi sasa imewekwa pembeni.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kupanga ni kuchagua, nataka sasa nipate kusikia kauli ya Serikali

195 kuhusu mradi huu ambao Serikali imeshindwa kuutekeleza.

Mheshimiwa Spika, itakuwaje miradi ambayo haikuwemo kwenye Ilani ya CCM ijengwe, kwa mfano, barabara zilizojengwa Chato, Dumila-Kilosa na nyingine nyingi zipewe kipaumbele, lakini ile barabara ya Baba wa Taifa kusahaulika.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Musoma kwenda Majita iliahidiwa na Rais akiwa Busekela kwamba itajengwa kwa kiwango cha lami. Hii ni ahadi ya Rais. Mheshimiwa Magufuli pia aliwahakikishia wananchi wa Mugango alipotembelea Jimbo langu kwamba atahakikisha atalifuatilia kwa karibu sana ili lijengwe, lakini sioni chochote kinachoendelea.

Mheshimiwa Spika, siungi hoja hii mpaka hapo Serikali itakapotoa kauli kuhusu barabara ya Mwalimu Nyerere.

MHE. ABDULKARIM E.H. SHAH: Mheshimiwa Spika, pamoja na salaam za ujenzi wa Taifa, naomba kuipongeza Serikali yangu kwa kujali wananchi wake.

Mheshimiwa Spika, pia naomba sana sana kumpongeza Mheshimiwa Daktari John Pombe Magufuli, Waziri wa Ujenzi; Naibu wake Mheshimiwa Engineer Gerson Lwenge; Katibu Mkuu; Balozi Mrango; Naibu Katibu Mkuu, Engineer Daktari Ndunguru; CEO wa TANROADS Bwana Mfugale; Meneja Mkuu wa Mfuko wa Barabara, Ndugu Haule; Wakuu wa Idara

196 zote na wataalam wote na kwa ujumla wafanyakazi wote wa Wizara hii. Mungu awabariki.

Mheshimiwa Spika, namwombea Mheshimiwa Magufuli Mungu ampe afya njema na uhai mrefu yeye na mama yake (yetu) na famila yake yote.

Mheshimiwa Spika, kwa ufupi nimepitia hotuba hii na kuisoma vizuri, hivyo ukurasa wa 33 kifungu 58, ukurasa 188 (jedwali kifungu 4165) ukurasa 220 (Mkoa wa Pwani) na ukurasa 269 (Coast Region–Kilindoni– Utende na tuta la barabara kati ya Vijiji vya Jimbo la Banja.

Mheshimiwa Spika, hakika, asiyeshukuru kwa haya na hasa ukiwasikia wengine wakilalamika. Itakuwa sitendi haki na ukosefu wa fadhila.

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya wananchi wa Mafia naomba kuishukuru tena Serikali kwa ujumla mimi binafsi na kwa niaba ya wananchi hao wa Mafia.

Mheshimiwa Spika, ahsante sana na naunga mkono hoja hii na hotuba hii nzuri kwa asilimia mia moja.

MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA: Mheshimiwa Spika, kwanza napenda kuunga mkono hoja ya bajeti ya Wizara hii ya ujenzi. Nampongeza Mheshimiwa Waziri Daktari Magufuli, Naibu Waziri na timu yao nzima ya wataalam katika Wizara hii kwani chini ya uongozi wake Mheshimiwa Waziri nimeona utendaji mzuri unaoonekana kwa vitendo, mipango mikakati yenye

197 tija. Hata hivyo, ninachojiuliza ni kuwa je, pamoja na mikakati na mipangilio mizuri na iliyobainishwa kulingana na makadiro pia, lini utekelezaji wake utakamilka kwa vitendo? Hii pia katika kutekeleza ilani ya CCM.

Mheshimiwa Spika, hii ni hususan barabara ya lami Mbeya–Luwanjilo–Chunya kupitia Kawetere na nyingine Mbeya–Mbalizi–Mkwajuni–Makongolosi. Naipongeza Serikali kwa kutenga bajeti kwa ajili hiyo, hata hivyo, kama nilivyosema, zitakamilika lini hasa? Bila kusahau barabara ya Tunduma–Sumbawanga kwa kiwango cha lami pia; Mpemba–Ileje (Isongole); Ipinda–Matema, Dodoma-Iringa, Tangibovu pale Goba–Mbezi mwisho. Nipatiwe majibu barabara hizi nilizotajwa zitakamilika lini?

Mheshimiwa Spika, Wakandarasi wanaopewa tenda; ni kwa nini huwa wanasuasua hata kama wamelipwa? Uzembe unatoka wapi? Wote wanaosababisha haya wachukuliwe hatua ya haraka kama fundisho maana huku ni kurudisha nyuma gurudumu la maendeleo.

Mheshimiwa Spika, Fly overs hazipo, nawapongeza sana kwa hili endapo litafanyika kweli pia itakuwa ni legacy kwa Mheshimiwa Spika, kwa Mheshimiwa Waziri na kubadilisha sura nzima ya majiji kimaendeleo; hali ambayo pia itapunguza foleni ambayo imekithiri hususan Jijini Dar es Salaam imezidi kero na haielezeki. Kuna pia ile barabara ya pale Uyole itawekwa lini junction ya kupitia pembeni ili itokee Mbalizi? Pale ni T-junction inayoelekea au

198 kutokea Iringa-Dar kwenda Malawi, Zambia na kadhalika. Malori, mabasi na nakala hukutania hapo; ni hatari kwa ajili na kusababisha msongamano usio na tija pia.

Mheshimiwa Spika, bomoa bomoa imezidi sana na inaathiri wahanga wamiliki halali wa ardhi/nyumba bora kuepuka shari kuliko kukumbana na fidia na ambayo pia gharama zake ni kubwa hence hasara. La msingi haya yazingatie sera na kanuni za ardhi pia na maslahi ya wamiliki ardhi pia. Utaratibu mzuri ufanyike ikiwezekana kukwepa adha hii.

Mheshimiwa Spika, Daraja la Kigamboni litakamilika? Hii imekuwa ni hadithi ya muda mrefu. Barabarani, kila baada ya kilomita kadhaa kuwe na vibao vinavyoashiria ramani na kilometa za unakokwenda. Maandishi yawe makubwa na visible.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja, lakini maswali yangu yafanyiwe kazi tafadhali.

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Spika, kuhusu Serikali kutotumia classification theory katika ujenzi wa barabara. Sikubaliani na mfumo unaotumiwa katika ujenzi wa barabara hapa nchini. Mfumo wa kujenga barabara nchi nzima, bila kuzingatia uwezo wa Serikali ni kujitakia lawama. Ni wazi kuwa kamwe Serikali haitaweza kujenga barabara zote kwa mfumo huu.

Mheshimiwa Spika, nini kifanyike? Serikali itumie classification theory katika ujenzi wa barabara yaani

199 ianze kujenga barabara za lami kikanda badala ya utaratibu wa sasa wa kujenga nchi nzima wakati fedha zenyewe ni kidogo. Mfano wa sasa umekaa kisiasa zaidi, tena “siasa za kilaghai.” Kwa mfano, mwaka huu 2012/2013, Serikali ingeamua kujenga barabara za ukanda wa Kusini mwa Tanzania Mtwara, Ruvuma, Lindi, Iringa na Mbeya) kwa kiwango cha lami ambapo nadhani barabara kuu zote za ukanda huo zingekamilika na hivyo kuleta tija katika uchumi wa ukanda huo.

Mheshimiwa Spika, kwa muda huu 2012/2013 tungeachana na ujenzi wa barabara za kanda nyingine kwa kiwango cha lami isipokuwa tungehakikisha zinakarabatiwa ili zipitike yaani periodic maintenance, kanda hizo ni kanda za Magharibi, Mashariki, Kaskazini, Kanda ya Ziwa na Kanda ya Kati. Maana yangu ni kwamba, baada ya kufanya kazi nzuri ya ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami katika Mikoa ya Ukanda wa Kusini mwa Tanzania, ndipo sasa tungehamia kanda nyingine mwaka 2013/2014 na kuanza kujenga barabara kwa kiwango cha lami kama vile kuanza kujenga barabara za Kanda ya Magharibi (Rukwa, Tabora, Kigoma na Shinyanga) hali inakuwa hiyo hiyo katika kila mwaka,

Mheshimiwa Spika, namhakikishia Mheshimiwa Waziri kuwa Serikali ikifanya hivyo, tutaweza kuona impact chanya ya fedha zote zinazowekezwa katika sekta ya barabara. Utaratibu wa sasa hauna tija sana kwa kuwa pesa ni kidogo, lakini pia hazipatikani zote.

200 Mheshimiwa Spika, hivi jiulize mwenyewe swali lifuatalo: ni haki au sahihi kutenga Sh. 3.5 bilioni kwa ajili ya ujenzi wa barabara yenye urefu wa kilomita 310 (Kidahwe–Kasulu–Kibondo–Nyakanazi)?

Mheshimiwa Spika, fedha hizi zitafanya nini? Sana zinaweza kujenga kilomita tatu au nne za lami. Lakini pia mwaka 2010/2011 Serikali ilitenga Sh. 6 bilioni kwa aujili ya Kidahwe–Kasulu (kilomita 56) mwaka jana 2011/2012, Wizara yako ilitenga Shilingi bilioni 2.2 kwa ajili ya barabara ya Nyakanazi–Kibondo–Kasulu– Kidahwe hazikutolewa. Mwaka huu 2012/2013, zimetengwa Shilingi bilioni 3.5, zitajenga nini au lami gani kwenye barabara yenye kilomita 310?

Mheshimiwa Spika, inaniwia vigumu nimwone Waziri na washirika wake wote kuwa si matapeli. Hii ni kwa sababu ahadi za ujenzi wa barabara hiyo ya Kigoma–Kasulu–Kibondo–Nyakanazi ni za muda mrefu. Miaka mitatu mfululizo zimekuwa zikitengwa fedha tena kidogo sana, lakini hazikutolewa, nini tafsiri yake? Ni utapeli wa Serikali.

Mheshimiwa Spika, suluhisho na ushauri, Serikali kupitia Wizara ya ujenzi ibadili mfumo wa ujenzi wa barabara, itimie classification theory kama nilivyoeleza hapo mwanzo. Yaani ujenzi wa barabara za lami unaotumia fedha nyingi ufanyike Kikanda mwaka hadi mwaka kwa barabara kuu za mikoa zilizo chini ya TANROADS. Aidha, ujenzi wa barabara kwa kusaidiwa na washirika wa maendeleo kama vile JICA, ABUDHAB, EU, DANIDA, MCCOPEC, Benki ya Dunia (WB) na wengine usiwe wa kibaguzi kwa kuwa ushahidi

201 unaonesha wazi kwamba miradi yote imejengwa kwa fedha za washirika hao wa maendeleo zimekuwa zikikamilika kwa wakati, ni tofauti na zile zinazojengwa kwa fedha za ndani yaani Government of Tanzania, ndiyo maana barabara ya Kidahwe-Kasulu, Kibondo– Nyakanazi inasua sua kuanza kwa ujenzi wake. Inatengewa fedha za ndani ambazo ni mgogoro lakini pia commitment ya kuzitoa fedha za ndani haipo.

Mheshimiwa Spika, sioni na sidhani kama Mheshimiwa Waziri ana jipya kuhusu sababu za kutoitengea fedha barabara ya Kigoma hadi Nyakanazi kwa mfumo huo wanaokwenda nao. Naomba watumie classfication theory.

Mheshimiwa Spika, nasubiri majibu kutoka kwa Mheshimiwa Waziri.

MHE. AMINA M. MWIDAU: Mheshimiwa Spika, awali ya yote nichukue nafasi hii kumpongeza kwa dhati Mheshimiwa Waziri, kwa hotuba yake nzuri, iliyojaa mipango mizuri yenye matumaini kwa Watanzania.

Mheshimiwa Spika, vile vile nimpongeze Waziri kwa uchapaji kazi wake mzuri sana ni matumaini yetu kuwa mipango hii mizuri iliyomo humu itatekelezeka

Mheshimiwa Spika, pili nichukue nafasi hii kuipongeza Serikali kwa ujenzi wa barabara ya Tanga– orohoro (kilomita 65), kazi iliyoanza tarehe 22/12/2009 na ujenzi umekamilika Mei 2012, sasa hivi unaweza ukaenda Mombasa asubuhi na kurudi jioni, kwa kweli barabara hii imetuletea hadhi kubwa Watanzania,

202 tumeshawishi mpaka Kenya sasa nao wanataka kukarabati barabara yao wanaiona chafu.

Mheshimiwa Spika, katika barabara hii ya Tanga- Horohoro wakati wa ujenzi kulikuwa na malalamiko ya malipo ya fidia kwa wananchi. Lakini kilichonifurahisha katika hotuba hii kwa mwaka wa fedha huu 2012/2013, kiasi cha shilingi milioni 12 zimetengwa kwa ajili ya kukamilisha malipo ya fidia, hii ni faraja kubwa kwangu, kwani kilikuwa ni kilio chao kikubwa wananchi, ila hiyo milioni 12 imepangwa kuwalipa watu wangapi? Naona pesa iliyotengwa ni kidogo sana ukilinganisha na madai ya wananchi.

Mheshimiwa Spika, tafadhali naomba Mheshimiwa Waziri akija kufanya majumuisho aniambie hiyo milioni 12 ya fidia ni ya akina nani na imelenga watu wangapi?

Mheshimiwa Spika, katika ukarabati wa vivuko pesa zilizotengwa sijaona Pangani ikitajwa, je, Pangani haihitaji ukarabati wa kivuko chake? Huwa ni kibovu na kinaharibika mara kwa mara.

Mheshimiwa Spika, katika kiambatisho Na. 1 cha mgawanyo wa fedha za bajeti ya maendeleo kwa mwaka 2012/2013. Kasma 4109 kuna miradi miwili Wazo Hill–Bagamoyo–Msata ambao umetengewa pesa Sh. 7,108,257 milioni na huu wa Bagamoyo– Makurunge–Sadani–Tanga and lower Wami Bridge (DD) imetengewa pesa ya Sh. 288.550 million. Naomba niipongeze Serikali kwa hatua hii ya awali. Kama kweli pesa hizi zitapatikana na miradi hii kwisha, basi

203 itafungua maendeleo makubwa kutoka Tanga mpaka Dar kupitia Bagamoyo–yaani Ukanda wa Pwani.

MHE. MKIWA A. KIMWANGA: Mheshimiwa Spika, napenda kukupa pole kwa kufiwa na mpendwa wako, Mwenyezi Mungu akupe moyo wa subira.

Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza Mheshimiwa Magufuli kwa kazi zake nzuri za usimamiaji wa barabara kwa uwezo wake wote pamoja na Serikali kutotoa pesa kwa wakati na miradi mingi kukwama kwa ukosefu wa pesa. Ni vyema sasa Serikali ikatoa pesa kwa wakati ili kuendana na ujenzi ambao utakidhi haja, bila kutoa riba kwa ucheleweshaji ulipwaji wa Certificates. Hazina ni bora kupeleka pesa hizo kwa wakati, kama pesa zingekwenda kwa wakati, bila shaka tungekuwa mbali sana kwa ujenzi wetu.

Mheshimiwa Spika, ni wajibu wangu tena kwa moyo mweupe kwa kuamua sasa kuichukua barabara ya Mwanza Airport by pass kwa kuitengeneza kwa kiwango cha lami, Mungu akulinde sana, kwani umesikia kilio cha wananchi wa eneo hili kupitia kwa mimi mwakilishi wao, nasema ahsante.

Mheshimiwa Spika, katika kuwasamehe wawekezaji, wachimba madini kulipia kodi, naomba wawekezaji hawa waweze kulipa Road fund board, kwani wao ndiyo hasa hubeba mizigo mizito ambayo huchangia uharibifu wa barabara, kwani mizigo huwa mizito sana (mitambo yao), hivyo huchangia uharibifu wa barabara.

204 Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali katika bajeti hii iweze kutoa pesa kwa wakati ili Mheshimiwa Waziri afanye kazi yake.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

MHE. HAMAD ALI HAMAD: Mheshimiwa Spika, ni hali halisi kwamba barabara za reli ndizo ambazo zinaunganisha mikoa yetu na mawilaya. Lakini pia ndizo ambazo zinategemewa sana na wananchi wetu pamoja na wageni wale ambao wanasafirisha mizigo yao ambayo ni mizito sana na ambayo ni ngumu sana kuisafirisha kwa njia ya barabara na hasa tukizingatia kwamba barabara nyingi zimeharibika kwa sababu ya kutumika kusafirishia mizigo ambayo ingestahili kusafiri kwa treni.

Mheshimiwa Spika, kwa hivi sasa ambapo Serikali bado haijaweza kutatua tatizo hili la kukamilisha ujasiri wa reli hizo ni vyema basi, Serikali kupitia Wizara hii ikawa na mpango mahususi wa kuhakikisha kwamba wanakuwa na udhibiti katika kusafirisha na au usafirishaji wa bidhaa ambao ni nzito sana. Pia ihakikishe kwamba, tunakuwa na udhibiti katika kuona kwamba malori hayapakii uzito zaidi ya unaoruhusiwa, kwani jambo hili, linaiongezea gharama kubwa Serikali kila mwaka ya kukarabati barabara hizi ambazo zinaharibika kutokana na kutumika kusafirisha mizigo mizito sana kwa muda wote wa masaa 24 kwa siku zote.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali itengainshe mizani ya kupima uzito kati ya malori ya mizigo na yale

205 mabasi ya abiria kwani utaratibu huu wa kuchanganya magari yote katika mizani mmoja yanaleta usumbufu mkubwa kwa abiria ambao wanakaa sana katika mizani wakisubiri msongamano huo wa malori na mabasi ya abiria upungue. Hii ni kutokana na kwamba, abiria wanaosafiri katika mabasi hayo, wanakuwa na hali zisizofanana, kwani wengine ni watoto, wazee, wagonjwa na hata wajawazito. Lakini pia unaposafiri kwa gari maana yake ni kwamba, unahitaji ufike safari yako mapema na kwa wakati, hivyo basi, kuchelewa kwenye mizani kunachelewesha pia kufika safari mapema na kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri amesema katika kipindi hiki cha fedha anategemea kujenga maegesho ya vivuko huko kati ya Dar es Salaam na Bagamoyo katika ile kujibu hoja ya kupunguza tatizo la msongamano wa wasafiri pale katika eneo la Jiji la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, hili ni wazo jema sana katika kupunguza msongamano wa wasafiri wanaotumia magari, katika eneo la Jiji la Dar es Salaam lakini, je, maegesho hayo yatakapokamilika, Serikali pia itakuwa na vyombo vyake vitakavyotumika kusafirisha abiria kama vile feri pale Kigamboni (pantoni) au kwa kuwa masafa yatakuwa ni marefu tofauti na yale ya Kigamboni, wananchi kwa kuzingatia usalama wao Serikalini inakusudia kuruhusu vyombo binafsi kama vile Dar es Salaam–Zanzibar au kuna mpango gani na hasa ukizingatia usalama wa watu wetu na usafiri wa baharini.

206 Mheshimiwa Spika, waishauri Serikali, itafute pia boti za kisasa kwa ajili ya kuhudumia wananchi wetu ili kutimiza dhamira hiyo njema ya Serikali kuwapunguzia usumbufu wananchi wake, lakini pia tutapunguza kwa kiwango kikubwa wananchi hawa kusafiri kwa kutumia mitumbwi, ambayo si salama sana kwa kusafiria na pia tutaweza kupunguza ajali za mara kwa mara kwa wasafiri wa njia hii.

Mheshimiwa Spika, ahsante na naomba kuwasilisha.

MHE. DKT. DAVID M. MALLOLE: Mheshimiwa Spika, kutokana na Mji wa Dodoma kuwa na Mamlaka nyingi, jambo hili limeleta utata, kuwa nani awajibike kwa kazi ya barabara za Mji. Endapo barabara za Mji wa Dodoma hazitajengwa vizuri, je, ni CDA, Manispaa, TANROAD, Wizara ya Ujenzi, au nani?

Mheshimiwa Spika, natoa rai kwa Wizara iwe na sauti kuhusu ujenzi wa barabara za Mji wa Dodoma, kwa kuwa ndiyo Mji Mkuu wa nchi, ili barabara ziweze kujengwa vizuri na kwa viwango sahihi vinavyotakiwa Kitaifa na Kimataifa. Hivi sasa Makampuni mengi yamepewa barabara nyingi za mji na mvua zimekaribia. Mifereji haijaanza kujengwa kwa ajili ya maji ya mvua. Pia lami bado haijaanza kuwekwa. Aidha, barabara mbovu zinafumuliwa robo au nusu, sehemu nyingine ya barabara ikiwa imebaki na kipande cha zamani cha lami mbovu. Je, nani awajibike katika mapungufu haya?

207 Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Waziri wa ujenzi, Daktari John Magufuli afanye yafuatayo:-

(i) Atoe kauli ya wazi kuwa nani awajibike kama barabara za Dodoma hazitajengwa kwa viwango vinavyotakiwa?

(ii) Naamini kuwa barabara zote zipo chini ya Wizara, wengine wote ni Mawakala, naomba atoe kauli na kuwaagiza mawakala wote waliokasimiwa kujenga barabara za mji mkuu:-

- Wajenge barabara za Mji wote wa Dodoma kwa viwango vya Kitaifa na Kimataifa.

- Wakandarasi wote wafanye kazi kwa bidii usiku na mchana, kampuni ya Saberg Interplan ilivyoweza kujenga mifereji mikuu ya maji ya Dodoma, usiku na mchana na kwa viwango bora. Waanze mapema kuweka mifereji ya barabara kuweka lami, kabla ya mvua za Dodoma hazijaanza.

(iii) Afanye ziara ya makusudi ya kutembelea barabara zote za Mji wa Dodoma, ili kuweka msukumo mkubwa katika ujenzi wa barabara za mji.

Mheshimiwa Spika, majuzi nilitoa hoja ya kuomba barabara zinazoingia vyuo vikuu ziwekewe lami. Mheshimiwa alitoa jibu zuri sana, alisema mamlaka zilizopo Mkoani wajitahidi kufanya hivyo. Mara nyingi watu hawaoni umuhimu. Mimi ndiyo Mbunge wa Dodoma, nilileta swali hili baada ya malalamiko ya muda mrefu ya Vyuo, kutoka mwaka 2009. Nashukuru

208 lami itafika Chuo kikuu cha Dodoma. Namwomba Mheshimiwa Daktari Magufuli aziagize Mamlaka za Dodoma, wafikishe lami Chuo Kikuu cha Saint John’s, Chuo cha Mipango, Chuo cha Madini, Chuo cha Ufundi Don Bosco na Chuo cha Ualimu Capital.

Mheshimiwa Spika, kama lami haitafika kwenye vyuo hivyo, wakati bararabara ya Iringa–Dodoma– Babati inapita jirani na wakati lami inapelekwa Chuo Kikuu cha Dodoma, jambo hili litajenga matabaka na linaweza kuleta athari katika uchaguzi Mkuu wa mwaka 2015. TANROAD na CDA, wafikishe lami kwenye vyuo hivyo, ni vipande vidogo tu vya barabara wala siyo barabara ndefu. Nashauri kwa moyo mweupe, si kwa kutafuta kura, bali kusaidia kuleta ushindi kwa wagombea wote wa Chama Tawala, Rais, Mbunge, na Diwani mwaka 2015. Ahsante.

MHE. SAID A. ARFI: Mheshimiwa Spika, ili kukuza uchumi wa Taifa ni lazima tuwe na miradi ya kipaumbele kama inavyoainishwa katika mpango wa maendeleo wa miaka mitano na tuondokane na kutawanya rasilimali chache kwa kutaka kufungua nchi hii kwa wakati mmoja, haja ya kufungua nchi kwa barabara za lami ni muhimu na je, uwezo wetu wa kuhimili tunao? Hivyo basi, nashauri tu kuwa na barabara za kipaumbele ikiwa barabara ya kutoka Mpanda-Mlele-Koga-Sikonge-Tabora kwa sababu zifuatazo:-

Moja, kuunganisha Mkoa wa Tabora, Katavi na Rukwa. Kuunganisha Wilaya ya Mpanda na Mlele, na Wilaya ya Sikonge na Wilaya ya Tabora. Pili, njia pekee

209 ya usafiri toka Mpanda ni reli ambayo ina matatizo lukuki, hivyo shehena ya mahindi na tumbaku pia sasa madini (mawe ya shaba), tunahitaji kuwa na njia mbadala ya reli na barabara hii Mpanda/Tabora.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Mpanda-Kanyani- Nyakanazi ni muhimu sana kwa kukuza uchumi katika Kanda ya Magharibi na pia ni kiungo kati ya Zambia, Burundi, Rwanda na Uganda. Barabara hii imechelewa sana na ni muhimu katika kukuza uchumi na kuunganisha Afrika.

Mheshimiwa Spika, barabara hizo mbili ni za kipaumbele, lakini pia ni vyema sasa pia Wizara ikaangalia namna gani sasa tunaweza kuunganisha Mkoa wa Katavi, Tabora na Shinyanga kwa kufungua barabara ya Mpanda-Kaliua hadi Kahama. Barabara hii itapunguza sana gharama za usafiri kwa wananchi wa Mikoa hii ya Katavi, Tabora na Shinyanga.

Mheshimiwa Spika, kuhusu fidia katika miradi ya barabara, kwa wananchi waliokutwa na maendeleo haya ya ujenzi wa barabara walipwe fidia. Vinginevyo Watanzania hawa angalau walikuwa wamejikomboa, mnawarudisha katika umaskini na wala hawataweza kujenga tena nyumba za kuzihifadhi na familia zao.

Mheshimiwa Spika, nitafurahi kama wakati wa hitimisho itatolewa kauli juu ya utata huu na kwa makusudi Serikali iwe tayari hata kutoa kifuta jasho kwa waathirika. Nitapenda kusikia kauli itakayowapa faraja Watanzania hususan wakazi wa Mtaa wa Ilembo na

210 Misunkumilo katika Mji wa Mpanda na kwingineko hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, nashukuru.

MHE. YUSSUF HAJI KHAMIS: Mheshimiwa Spika, nachukua fursa hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa amani na utulivu aliotujalia sote. Naanza kwa pongezi zangu za dhati kwa Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Daktari John Pombe Magufuli kwa hotuba yake nzuri na uwasilishaji mzuri.

Mheshimiwa Spika, naanza na barabara ya Dar es Salaam–Dodoma, barabara hii ni muhimu sana kwa uchumi wa Taifa letu. Kwa hiyo, inapaswa kutunza vizuri sana. Ukiangalia barabara hii utakuta sehemu nyingi zimeharibika kutokana na kutumiwa na magari makubwa ya mizigo yenye uzito mkubwa. Kwa hiyo, pamoja na kuwa kuna lami, lakini utakuta ina milima na mabonde sehemu nyingi ya barabara. Jambo lingine rasta ni nyingi mno ambazo zinatoa usumbufu hasa kwa magari madogo madogo na kusabisha magari kuvunjika.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni matuta yaliyomo katika barabara hii, sehemu nyingine hamna alama na kutoa usumbufu kuonekana kwa madereva. Kwa hiyo, inaweza kusababisha ajali.

Mheshimiwa Spika, mtindo mwingine mbaya ambao umejitokeza kwa watu wachache wenye tamaa na kuharibu miundombinu hasa katika Mji wa Dar es Salaam, wanachukua mifuniko ya makaro

211 (mifuniko ya vyuma) na kuiuza skrepa hali ambayo ni hatari kwa maisha ya watu. Vile vile makaro yanabaki wazi mvua zikinyesha zinasomba takataka kuingiza katika mashimo ya karo na kuharibu miundombinu ya barabara. Hili linahitaji mipango, nashauri kudhibitiwa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu uvamizi wa maeneo ya barabara, watu wengine huvamia maeneo ya barabara kwa kujenga nyumba za makazi ambapo wanasababisha mvutano na Serikali na kusababisha usumbufu sheria inapochukua mkondo wake kwa kubomolewa.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali iwe makini kuangalia maeneo haya na kutotoa fursa ya ujenzi wa aina yoyote. Serikali isisubiri mpaka mtu amalize ujenzi ndiyo ichukue hatua ya kubomoa, hatua ichukuliwe mapema tena mara moja hata kabla hajaanza msingi.

MHE. JOHN P. LWANJI: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Daktari John Pombe Magufuli kwa kuteuliwa tena na Mheshimiwa Rais kuendelea kuiongoza Wizara hii nyeti, aidha, nimpongeze pia Mheshimiwa Engineer Gerson Lwenge kuwa Naibu Waziri wa Wizara hii.

Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa hatua ya kutengea Sh. 109 bilioni barabara ya Manyoni–Itigi– Chanya kutokana na fedha za Serikali (GOT) lakini uzoefu umeonesha kuwa mara kadhaa fedha zinazopatikana na GOT huchelewa sana na mara kwa mara kutolewa kwa Wakandarasi, matokeo yake ni ucheleweshaji wa ujenzi wa barabara hii, ni muhimu.

212 Ukilinganisha kati ya barabara zinazojengwa chini ya GOT na zile zinazojengwa chini ya ufadhili wa nchi za nje au World Bank kama vile barabara kuliko za GOT. Nashauri fedha za Serikali zitolewe mapema ili kazi ya ujenzi wa barabara hii muhimu ya Manyoni–Itigi Chanya (kilomita 89) iweze kukamilika katika muda uliopangwa. Vinginevyo nayo itafutiwe mfadhili kama ile ya Malagalasi. Haleluya!

Mheshimiwa Spika, aidha, naishukuru sana Serikali kwa kutenga Sh. 200 bilioni kwa ajili ya barabara ya Makongolosi–Rungwa–Itigi–Mkiwa, nazo chini ya GOT zije haraka tu kazi ianze. Mungu awabariki sana kwa hili.

Mheshimiwa Spika, aidha bado naiomba Wizara itoe kibali kwa Wilaya ya Manyoni, ichukue majengo ya Mhandisi Mkazi pale ieleweke. Tayari madhumuni ya majengo hayo imeainishwa yawe Chuo cha Ufundi na mamlaka ya Mkoa imeitaarifu Wizara juu ya suala hili.

Tafadhali naomba ufafanuzi juu ya hili maana majengo haya hayatumiki na yanaendela kuharibika.

Mheshimiwa Spika, lingine muhimu, je barabara hii ya Itigi-Makongorosi inaanza wapi kujengwa? Inaanzia Mkiwa–Itigi-Rungwa au vice versa?

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. KAIKA S. TELELE: Mheshimiwa Spika, nazungumzia barabara ya Makutano–Natta– Mugumu/Loliondo–Mto wa Mbu (kilomita 328)

213 Mheshimiwa Waziri Magufuli fedha aliyoitengea barabara hii ni kidogo mno hasa ukizingatia yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, haya ni maono ya baba wa Taifa hili tangu miaka ya 1980; ni vyema tukaenzi mawazo yake kwa kujenga barabara hii kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais Kikwete alipigania ujenzi wa barabara hii licha ya upinzani mkali toka kwa Mashirika ya Kitaifa ya Wanyamapori na Mazingira pamoja na nchi jirani. Wote hawa hawajui jiografia ya nchi yetu, wanatuonea wivu rasilimali zetu nyingi na hawatutakii mema. Tuwapuuze!

Mheshimiwa Spika, barabara hii itaunganisha Mkoa wa Arusha na mikoa ya Kanda ya Ziwa na kufungua uchumi na mawasiliano. Pia barabara hii itaboresha utalii katika eneo la Lake Natron/Mlima Lengai na Serengeti.

Mheshimiwa Spika, Mradi huu wa barabara utakuwa ukombozi kwa Wilaya za pembezoni za Monduli, Longido na Ngorongoro. Barabara hii iko katika Ilani ya CCM ya 2010 - 2015

Mheshimiwa Spika, naomba fedha zaidi kwa barabara hii hususan sehemu ya Mto wa Mbu–Loliondo (Wasso) kilomita 213 kwa kuwa ni ndefu ukilinganisha na sehemu ya Makutano–Natta–Mugumu–Loliondo yenye kilomita 115. Jumla ya Sh. 3,827.96 zilizotengwa

214 kwa barabara hii yenye jumla ya kilomita 328, ni fedha ndogo sana.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, kupitia kwa Mheshimiwa Waziri naipongeza sana Serikali na Wizara ya Ujenzi anayoingoza kwa kazi nzuri ya ujenzi wa barabara nchi nzima. Mbunge mmoja kutoka Lindi alisema: “Nchi nzima imetanda vumbi kutokana na ujenzi wa barabara kila kona ya nchi.” Hongera sana Mheshimiwa Waziri na timu yako yote, lakini naomba uzingatie ombi langu la nyongeza ya fedha kwa barabara hii na caterpillar zianze kutimua vumbi katika barabara hii.

MHE. ABDUL J. MAROMBWA: Mheshimiwa Spika, nianze kwa kuunga mkono hoja hii kwa kuwa maelezo yake yameelezwa kwa kina na yamezingatia mahitaji halisi ya sasa ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kuunga mkono hoja hii bado kuna mambo machache ambayo nadhani yakiboreshwa yanaweza kuondoa kero kubwa ya usafiri katika nchi hii. Miongoni mwa kero hizi ni kutokamilika kwa barabara ya Ndundu-Somanga. Ujenzi wa barabara hii ulitakiwa kukamilika zaidi ya mwaka mmoja sasa, lakini hadi sasa zaidi ya kilomita 40 bado hazijakamilika ikiwa ni pamoja na madaraja hasa lile la Malendego. Naiomba Serikali kuweka mkazo kwa Mkandarasi ili aweze kukamilisha ndani ya miezi mitatu inayokuja.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ni barabara ya Kibiti–Utete–Nyamwage, barabara hii ni ya muhimu

215 sana, inatakiwa kuimarishwa kwa kuwa ni barabara mbadala (Alternative Trunk Road) ya barabara Kibiti– Ndundu–Nyamwage. Ni vizuri kwa barabara hii ikawekwa lami kwani kama patatokea matatizo yoyote kwenye Daraja la Mkapa basi hii ndiyo njia mbadala ya kuweza kupita kwa magari yote yanayokwenda Mikoa ya Kusini mwa Tanzania.

Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu kuna kilio kikubwa kwa wananchi wanaokaa katika Tarafa ya Mbwera eneo la Delta. Wananchi hawa kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji, kila mwaka wamekuwa wakiomba Serikali kujenga madaraja ya Kipoka, Mbirambi na Usimbe ili maeneo haya ya Delta yaweze kufikika maeneo haya ya Delta, ndiyo yanayozalisha kamba (Prawns) kwa wingi pamoja na chakula. Tumekuwa tukiyaweka katika bajeti kila mwaka, lakini hayapati fedha.

Mheshimiwa Spika, naishauri na naiomba Serikali iwasaidie wananchi hawa zaidi ya 20,000 ambao tangu uhuru hawajaona gari. Gharama za madaraja haya ni zaidi ya Sh. 1,200,000,0000/= (bilioni moja na milioni mbili).

Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kuzungumzia suala la kuhifadhi barabara zetu kuu na zile za Mkoa zisiweze kuingiliwa na wavamizi. Barabara nyingi kuu za nchi yetu, haziwekwi beacons (vigingi) vya kuonesha mwisho wa Road Reserve, baadhi ya barabara kama vile ya Dodoma-Singida, vigingi vimewekwa vizuri na si rahisi kuweza kuvamiwa na wananchi.

216

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali kuwa popote pale ujenzi wa barabara unapofanyika, basi Mkandarasi awe anaweka vigingi vya kuonesha hifadhi ya barabara ili eneo hili lisiweze kuvamiwa.

Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, naunga mkono hoja hii.

MHE. ALI KHAMIS SEIF: Mheshimiwa Spika, pamoja na juhudi zinazofanywa na Wizara za kuondoa msongamano Dar es Salaam nashauri kasi ya kuondoa tatizo hilo iongezeke kwani hali iliyoko Dar es Salaam ikiwa ni kituo kikuu cha uchumi wa nchi yetu ni mbaya sana kwa msongamano.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeweka mezani sehemu mbalimbali katika barabara hii ili kuhakikisha gari zinazopita kwenye barabara hiyo haizidi uzito unaotakiwa. Juu ya juhudi hizo nataka kuiarifu Wizara kuna ujanja wa mabasi ya abiria baadhi yao yanapofika masafa machache kabla ya kituo abiria hupunguzwa kwenye mabasi hayo na mara magari hayo yanapokuwa yameshapita kwenye mizani kwa masafa ya mbele abiria hurudi tena kwenye mabasi. Ipo haja mwenendo huo utafutiwe dawa ili kulinda barabara zetu.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia ukurasa 165 wa hotuba ya Waziri, kifungu 239 kinachoishia ukurasa 166, Wizara ina nia ya kujenga nyumba za Viongozi Dar es Salaam. Kwa vile nia ya Serikali hii ni kuhamia Dodoma,

217 kwa hiyo, kwa nini kama nia yao bado ya Makao Makuu Dodoma nyumba hizi zisijengwe Dodoma.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia kifungu 110, kwenye ukurasa wa 76, yapo maelezo yanayohusiana na usajili wa Wakandarasi. Inavyooneka mwaka uliopita Wakandarasi 35.7 wamefutiwa usajili na kufanya Wakandarasi waliofutiwa usajili kufikia 2,576. Hao Wakandarasi waliofutiwa usajili ni wengi. Je, chombo kilichowasajili wahusika hakikuwa makini na kutoa usajili kiholela na matokeo yake wakasajili Wakandarasi wasio na sifa na ikawa rahisi kufutiwa usajili wao?

Mheshimiwa Spika, vifungu mbalimbali vikiwemo kifungu 238, ukurasa wa 164, kimeelezea juu ya Baraza la Ujenzi wa nyumba ya ghorofa 18 kwa ushirikiano wa Shirika la Taifa la Nyumba (NHC). Ninachotaka kujua kwa mazingira yapi Baraza la Ujenzi litashirikiana katika ujenzi ukitilia maanani kila Taasisi ina uwezo wa kujenga jengo hilo la ghorofa 18. Baraza la Ujenzi na Shirika la Taifa la Nyumba kila moja lina uzoefu katika ujenzi. Naomba niambiwe kwa mazingira yapi ikabidi taasisi hizo kushirikiana?

Mheshimiwa Spika, ahsante.

MHE. MTEMI ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Spika, napenda kupitia mchango wangu huu wa maandishi kumpongeza Mheshimiwa Daktari John Pombe Magufuli, Waziri wa Ujenzi; Naibu Waziri wake Mheshimiwa Engineer Gerson Lwenge; Katibu Mkuu pamoja na watendaji wengine wa Wizara hii bila kuwasahau watumishi wote wa Wakala wa Barabara

218 wakiongozwa na Afisa Mtendaji wake Engineer Mfugale kwa kazi nzuri wanayoifanya, ni kazi inayoonekana. Hongereni sana.

Mheshimiwa Spika, hotuba ya Waziri wa Ujenzi imesheheni mambo mengi mazuri iwapo yatatengewa fedha kama yalivyoombewa.

Mheshimiwa Spika, mwaka jana wakati wa bajeti nilibahatika kuchangia katika hotuba ya Waziri wa Ujenzi. Miongoni mwa mambo yaliyochangia ni barabara ya Lamadi–Bariadi–Maswa–Mwigumbi yenye urefu wa Kilomita 171.8, sehemu ya Lamadi–Bariadi ilianza tangu mwaka wa fedha 2011/2012 kujengwa kwa kiwango cha lami. Hata hivyo, ujenzi wa barabara hiyo umesimama kwa kipindi kirefu kutokana na Serikali TANROADS kushindwa kumlipa Mkandarasi kwa kazi aliyokamilisha. Katika mwaka huu wa fedha barabara hiyo imetengwa Shilingi milioni 5,500,000.

Mheshimiwa Spika, hiki ni kiwango kidogo, zana ikilinganishwa na hali halisi ya mahitaji. Kwa mtaji huu, iwapo kwa mfano, gharama kwa kutengeneza kilomita moja ya barabara hiyo ni Sh. 800,000 milioni (kiwango cha chini sana) kwa fedha iliyotengwa itatosheleza kilomita 6.87 tu na kwa maana hiyo itachukua miaka 10 kukamilisha kipande cha kilomita 71.8. Hii haikubaliki. Aidha, napenda Waziri anihakikishie kuwa kipande cha Bariadi–Maswa na kile cha Maswa–Mwigumbi chenye urefu wa kilomita 50 kila moja, itatangazwa ili ujenzi kwa kiwango cha lami uanze katika mwaka huu wa fedha 2012/2013 pamoja na kwamba fedha iliyotengwa ni kidogo (Shilingi milioni 1,500,000)

219 nitashukuru kama nitapata ahadi hiyo na lini zabuni zitaitishwa?

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara ya Bariadi– Lamadi katika baadhi ya maeneo barabara imefuata makazi ya wananchi ambao makazi yao yapo nje ya hifadhi ya barabara na hivyo kustahili kulipwa fidia. Hadi sasa ulipaji wa fidia kwa wananchi umekuwa kitendawili. Namshauri Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi ategue kitendawili hiki kwa Serikali kulipa fidia stahiki.

Mheshimiwa Spika, katika mji wa Bariadi ujenzi wa barabara hii ya Bariadi–Lamadi umeibua mvutano kati ya baadhi ya wananchi na Wakala wa barabara. Inaonekana survey ya barabara iliyofanywa ilikosewa kwa kuacha eneo la barabara lililopo na kuelekezwa kwenye makazi ya watu. Meneja wa TANROADS Simiyu analifahamu tatizo hili. Hata hivyo, hadi sasa ameshindwa kulipatia suluhu. Kwa kuwa kiini cha tatizo hili ni survey iliyokosewa (na ushahidi upo), nashauri TANROADS – Serikali igharamie upimaji mpya wa eneo hilo ili kukata mzizi wa fitina.

Mheshimiwa Spika, Simiyu ni miongoni mwa mikoa mipya minne iliyoanzishwa na Serikali. Nashauri TANROADS (Meneja wa Mkoa na timu yake) iangalie jinsi Mkoa ulivyokaa kwa madhumuni ya kuwasilisha mapendekezo ya kuwa na road network itakayofungua Mkoa huu pamoja na kuunganisha Mikoa jirani, hasa Mikoa ya Mwanza, Shinyanga, Singida na Arusha.

220 Mheshimiwa Spika, mwisho kabisa, napenda kushauri Serikali ifanye kila lililo ndani ya uwezo wake ili kupata fedha za kulipia deni la takriban shilingi milioni 152.00 ambalo TANROADS inaanza nalo katika mwaka huu wa fedha. Hilo lisipofanyika litaathiri utekelezaji wa miradi ya barabara iliyopangwa kutekelezwa katika mwaka huu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. HERBERT J. MNTANGI: Mheshimiwa Spika, napenda kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi pia Naibu Waziri, Watendaji wa Wizara na viongozi wa Taasisi zake. TANROADS na Bodi ya Uandikishaji wa Makandarasi kwa jitihada kubwa wanazofanya kuwezesha Tanzania kushika nafasi ya juu katika ujenzi wa Miundombinu, hasa ya barabara kwa kiwango cha lami kwa mfumo wa kuizunguka nchi nzima, kwa mfumo wa mzunguko mkuu wa pembezoni na mfumo wa mzunguko wa kati ya nchi unaolenga kuunganisha Mikoa yote na mwelekeo wa kuunganisha pia Wilaya zote.

Mheshimiwa Spika, nashauri Wizara ya Ujenzi itoe taarifa hii muhimu ya mchanganuo wa Ujenzi wa barabara Kimkoa kama zinavyoainishwa katika Kitabu cha Hotuba ya Wizara, ukurasa 82, hadi ukurasa 94, katika vyombo vya habari na viongozi wa Serikali Mkoa, Wilaya na Kata hata ikibidi vikabrasha vitengenezwe Kimkoa ili wananchi wajue ukweli na kazi zinazokusudiwa kukamilishwa na kuanzishwa 2012/2013.

221 Mheshimiwa Spika, pamoja na maelezo hayo napenda kueleza yafuatayo:-

Barabara ya Mkoa ya Pangani (Boza)–Mkunazi – Kilulu–Muheza. Barabara hii ni ya Mkoa ndani ya Wilaya ya Muheza. Narudia tena kusema sijaona mpango wake wa matengenezo katika viambatanisho vyote 1–4 na 5 (A)–(G). Hii ni sehemu ya barabara iliyoathirika sana katika mradi wa PMMR chini ya Mkandarasi Y.N. Investment.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Mkoa ya Bombani–Mashewa–Kimbo kama katika (1) hapo juu Barabara hii pia sijaona mpango wake hata katika Mifuko ya Barabara.

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Muheza-Amani. Napenda kupongeza kuwepo kwa barabara hii katika Mradi wa Maendeleo ya Barabara (kasma 4132) 2012/2013 hasa baada ya kuathirika sana katika mradi wa PMMR Tanga East. Nitapenda kufahamu mchanganuo wa kazi zinazokusudiwa kufanyika kwa hatua za dharura ili kuwezesha chai au miwa na maziwa kufika sokoni na hasa chai katika Soko la Kitaifa kuwezesha nchi kupata fedha za kigeni na kuboresha wakulima na wafugaji. Mkakati mkubwa wa dharura ni kuweka zege maeneo ya kona korofi tano zilizobaki na hatua ya kuweka lami eneo linalobaki chini ya kilomita 30 ili kukamilisha ahadi ya Mheshimiwa Rais ndani ya kipindi chake cha Urais 2005/2015 hasa baada ya kupita kwa awamu ya 2000–2005 ahadi ambayo haikutekelezwa.

222 Mheshimiwa Spika, makazi wa ujenzi wa Daraja Muheza mjini (barabara ya Muheza Amani) na usimamizi wa matumizi ya barabara. Katika mwaka wa fedha 2010/2011 TANROADS walipanga kujenga Daraja eneo la Muheza Mjini katika barabara ya Muheza–Amani. Baada ya makubaliano ya kumaliza mgogoro uliokuwepo wa kuhamisha bomba la maji lililowekwa kwa makosa ya Halmashauri ya Wilaya ya Muheza, ningependa kufahamu ni lini kazi ya ujenzi huo utaanza.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa barabara ya Muheza–Amani inasimamiwa na TANROADS, nashauri TANROADS isimamie sheria za barabara ili kuondoa athari za uharibifu mkubwa unaofanyika katika maeneo yafuatayo:-

- Mchepuo wa kuingia na kutoka stendi ya Mabasi, Muheza, maeneo hayo yanaharibika sana kutokana na uzito na idadi kubwa ya mabasi yanayoingia na kutoka stendi.

- Eneo la Muheza Mjini hadi Mikwamba, katika eneo la Mikwamba kuna uchimbaji wa kifusi na magari makubwa sana yanapita na kuharibu barabara hiyo, eneo lenye lami Muheza–Mbaramo na eneo la changarawe–Mbaramo–Mikwamba.

Eneo la Muheza Mjini–Bombani-Lunguza eneo hili linaharibiwa na malori makubwa yanayobeba magogo kutoka shamba la Msitu wa Lunguza, Muheza na pia magari toka nje ya Muheza yanayoleta magogo katika viwanda vya mbao vitano kati ya

223 Muheza–Bombani. Halmashauri ya Wilaya ya Muheza haina uwezo wa usimamizi na udhibiti wa barabara hizo za Mkoa.

Mheshimiwa Spika, mwisho, naomba Wizara ya ujenzi itoe majibu kwa fursa za elimu zilizotolewa kwa Watanzania kupitia Mtanzania aliyepo Marekani Mr. Mwakalinga juu ya utengenezaji wa barabara kwa kutumia teknolojia ya lami nyepesi.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kwamba teknolojia hiyo imejaribiwa katika barabara ya Muheza-Amani (kilomita mbili) na kutoridhishwa na matokeo yake bado fursa ya Watanzania kuijua vizuri teknolojia hiyo kunawezesha uwezo wa ubunifu mpya kuboresha teknolojia hiyo kwa manufaa ya Watanzania hapo baadaye. Fursa hiyo imekuwa wazi tangu 2011 hadi Juni, 2012. Mkurugenzi wa TANROADS aliwahi kufanya mawasiliano na huyo Mtanzania Mr. Mwakalinga 2010/2011.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. AGRIPINA Z. BUYOGERA: Mheshimiwa Spika, pamoja na ahadi ya Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuufungua Mkoa wa Kigoma kwa kujengea barabara za kutuunganisha na mikoa mingine inapigwa na watendaji wa Serikali maana ni ukweli kwamba kila mwaka zinawekwa fedha za kutupumbaza wananchi wa Kigoma ambazo haziwezi kujenga barabara ya lami, ndiyo maana kila baada ya bajeti kupita pesa zilizopangwa kujenga barabara ya

224 Kidahwe hadi Nyakanazi huwa zinaondolewa. Inauma sana sana.

Mheshimiwa Spika, kwa miaka yote tangu nimekuwa Mbunge wa Jimbo la Kasulu Vijijini nimekuwa nikiwakilisha kilio cha barabara mbovu sana ya kutoka Kijiji cha Makerere hadi Kitanga, ni vyema sasa Mheshimiwa Waziri unisaidie kujenga barabara hiyo kupitia Mfuko wa Barabara.

Mheshimiwa Spika, ukisikia Kigoma hatujawahi kuletewa chakula cha msaada kwa kuwa tunajitosheleza. Kasulu ndiyo Wilaya inayoongoza kwa kilimo cha mazao ya chakula, barabara hiyo ndiyo ambayo inakwenda kwenye miradi mikubwa ya kilimo.

Mheshimiwa Spika, ni vyema nami nimwambie Mheshimiwa Waziri kwamba Watanzania wengi wana imani kubwa sana na utendaji wake ikiwemo wananchi wa Jimbo la Kasulu Vijijini.

Mheshimiwa Spika, hebu naomba tusitengwe. Maandiko Matakatifu yanasema; mpende jirani yako kama nafsi yako. Hatuna sababu ya kulia kila siku.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. SALIM HEMED KHAMIS: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Watendaji wote wa Wizara hii kwa kazi nzuri wanayoifanya katika ujenzi wa barabara zetu.

225 Mheshimiwa Spika, kwa muda mrefu barabara zetu zimekuwa hazipitiki wakati wa mvua hasa zile za vijijini ingawa juhudi ya Serikali sasa za kujenga barabara ni kubwa zaidi kwa kuongeza bajeti ya Wizara.

Mheshimiwa Spika, ubora wa barabara hii ni tatizo kubwa. Barabara zinazojengwa kwa gharama kubwa zinaharibika baada ya muda mfupi na kulitia Taifa hasara kubwa. Mfano hai ni barabara iliyopo mbele ya Bunge letu hapa Dodoma, haina viwango hata kidogo. Suala la value for money liangaliwe kwa uzito mkubwa ili kuepuka Wakandarasi waharibifu na wasio waaminifu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu matumizi ya Mkandarasi. Ni vizuri kutumia Wakandarsi wa Kitanzania ikiwa wanakidhi viwango. Hata hivyo, matumizi ya Wakandarasi wa Kitanzania isiwe sababu ya kuwa na barabara zisizo na viwango kwa sababu wao ni wenzetu.

Mheshimiwa Spika, kuhusu malipo ya Wakandarasi; kuna tatizo lililojitokeza la kutowalipa pesa zao Wakandarasi wetu. Aidha, wapo wakandarasi wamelipwa fedha nyingi kinyume na kazi waliyofanya. Je, ni kwa nini hilo linatokea? Kutokuwalipa Wakandarasi waliokwishafanya kazi na kuwalipa kiwango kikubwa cha fedha wakati kazi waliyofanya ni ndogo? Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara za Dar es Salaam, ili kupunguza msongamano Jijini ni lazima Serikali ibuni mradi wa muda mfupi wa kutengeneza

226 feeder roads kuokoa hali mbaya ya usafiri Jijini. Mradi wa muda mrefu haufai kwa sababu kadri tunavyochelewa ndivyo ongezeko la watu na vyombo vya usafiri linavyozidi.

Mheshimiwa Spika, kuhusu bomoabomoa ya nyumba pembezoni mwa barabara za Dar es Salaam; kwa mujibu wa sheria, wananchi wanatakiwa kujenga mbali na barabara (kilomita 30), inasikitisha kuwa wananchi wengi hawafahamu ni masafa gani (mita ngapi) nyumba inatakiwa ijengwe kutoka barabara kuu. Matokeo yake nyumba nyingi huvunjwa ili kupisha ujenzi wa barabara.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali iandae siyo fidia bali kifuta machozi kwa wale watakaovunjiwa. Hili la kutoa kifuta machozi kwa walengwa liwe kwa wale tu waliojenga kabla ya Uhuru.

Mheshimiwa Spika, nawatakia watendaji wote wa Wizara hii kazi njema na naunga mkono hoja.

MHE. SYLVESTER M. MABUMBA: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napenda kumpongeza sana Mheshimiwa Waziri, Naibu wake na watendaji wote wa Wizara ya Ujenzi kwa kazi nzuri anayoifanya kwa Taifa letu.

Mheshimiwa Spika, kama alivyoelezea Waziri mwenyewe katika hotuba yake ni kwamba, nchi yetu ina ukubwa wa kilomita za mraba 949,000. Hivyo ujenzi wa barabara zetu lazima uongozwe na mpango mkakati wa ujenzi wa barabara ambazo kipaumbele

227 cha kwanza kiwe ni kusaidia kuinua uchumi wa nchi yetu. Nashauri kwamba maeneo yote yenye uzalishaji mkubwa wa mazao ya chakula na biashara yapatiwe barabara za uhakika ili vyakula vinavyozalishwa viweze kusafirishwa hadi kwa wananchi wanaokabiliwa na njaa. Pia barabara hizi zitakazojengwa zitaweza kusafirisha vyakula na mazao mengine kufika kwenye masoko.

Mheshimiwa Spika, kutokana na umuhimu wa barabara kwa maendeleo ya nchi yetu, napenda kutoa rai kwamba, ifanye uamuzi wa makusudi wa kujenga barabara chache kwa awamu ambazo kukamilika kwake kutachochea kwa kasi kubwa ukuaji wa uchumi hasa kwenye maeneo yenye uzalishaji mkubwa. Hii itasaidia kuokoa hela nyingi kwani utaratibu wa sasa wa kujenga barabara nyingi kwa wakati mmoja na matokeo yake Wakandarasi wengi hushindwa kuendelea na ujenzi kutokana na ukosefu wa fedha kutoka Hazina. Hali hii huilazimu Serikali kulipa faini kwa makampuni ya ujenzi kutokana na kupotezewa muda wao.

Mheshimiwa Spika, eneo lingine ninalotaka kuliongelea ni uwepo wa udhibiti wa kweli kwa Wakala wa Barabara TANROADS kwani kuna upotevu wa mapato mengi kwenye vipimo. Mapato yanayotokana na TANROADS ndiyo kichocheo cha kujenga barabara zetu hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, napenda pia kuzungumzia eneo muhimu sana la usalama barabarani. Naomba sana Serikali yetu iweke msimamo kwamba, inawekeza

228 katika kuweka alama zote za usalama na kuzilinda ili zisiibiwe na wananchi wakorofi ili zitumike kutoa tahadhari kwa watumiaji wote wa barabara na hivyo kuepusha ajali zisizokuwa za lazima na kuweza kuokoa maisha ya Watanzania.

Mheshimiwa Spika, kutokana na ajali nyingi ambazo Taifa letu limeshuhudia, nashauri kwamba elimu ya usalama barabarani iendelee kutolewa bila kuchoka. Matumizi ya kamera maalum yaanzishwe ili madereva wanaovunja sheria za usalama barabarani waweze kukamatwa na adhabu kali zitolewe dhidi ya hao wanapopatikana na hati.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. HAROUB MUHAMMED SHAMIS: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, namshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kunijalia afya na ufahamu wa kuweza kuandika machache kuchangia bajeti hii kwa faida ya nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, tatizo la msongamano wa Dar es Salaam linakwaza sana uchumi si wa wakazi wa Dar es Salaam tu bali wa Taifa zima kwa ujumla wake Dar es Salaam inachangia asilimia 84 ya uchumi wa Taifa, hivyo, tatizo la msongamano halina budi kutatuliwa kwa haraka na kwa ufanisi ili kuokoa mdororo wa uchumi wa Dar es Salaam na wa nchi nzima.

Mheshimiwa Spika, Ujenzi wa flyover eneo la TAZARA ni jambo jema sana, lakini kwa hali ya msongamano ulivyo ni lazima kuwe na ujenzi

229 sambamba wa flyover eneo la Ubungo Mataa pamoja na eneo la Keko.

Mheshimiwa Spika, ulazima wa kujenga flyover maeneo haya matatu kwa pamoja ndiyo kutasaidia kwa kiasi kikubwa kupunguza msongamano. Kujenga flyover eneo la TAZARA pekee kutajaza msongamano zaidi eneo la Keko na pia Ubungo Mataa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara ya Namtumbo–unduru yenye kilomita 193; ujenzi wa barabara hii iliyogawanywa katika vipande vitatu kama ifuatavyo: Namtumbo–Kilimasera kilomita 60.7 Kilimasera–Matemanga kilomita 68.2 Matemanga– Tunduru kilomita 58.7.

Mheshimiwa Spika, pamoja na barabara hii kugawanywa katika vipande vitatu kama nilivyoonesha ili kuleta ufanisi na uharaka katika ujenzi wake, inashangaza sana vipande vyote vitatu hivyo kupewa Mkandarasi mmoja tu. La ajabu zaidi ni Wizara kutoa ripoti ya Mkandarasi huyu kushindwa kukidhi vigezo na bado hakuna hatua zozote dhidi yake zilizochukuliwa.

Mheshimiwa Spika, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Miundombinu na tulifanya ziara na Kamati kukagua barabara nyingi ikiwemo hii. Barabara ya Namtumbo– Tunduru katika vipande vyote vitatu, amepewa Mkandarasi aitwae Progressive-Higleig JV of India.’

Mheshimiwa Spika, Ufanisi wa Mkandarasi huyu ni very poor kwa muda wa miezi 14 ya ujenzi kati ya miezi

230 27 ya muda wote wa ujenzi, Mkandarasi huyu amefanya kazi kwa asilimia tisa tu, kwa kipande cha Namtumbo–Kilimasera!

Mheshimiwa Spika, kwa kipande cha kuanzia Kilimasera–Matemanga kwa muda wa miezi 14 kazi aliyofanya ni asilimia 2.5 tu. Pia kwa kipande cha kuanzia Matemanga–Tunduru kwa muda huo wa miezi 14 kazi aliyofanya ni asilimia moja tu.

Mheshimiwa Spika, huu ni ushahidi na uthibitisho tosha kuwa Mkandarasi huyu hana uwezo wa kujenga barabara, lakini kama haitoshi, Wizara imekiri udhaifu wa Mkandarasi huyo, kwa kuieleza Kamati kuwa, Mkandarasi amekumbwa na tatizo la kuleta vifaa vya ujenzi, wataalam na hata kushindwa kuleta dhamana zinazomwezesha kupata malipo ya awali.

Mheshimiwa Spika, la kustaajabisha, baada ya ithibati yote hiyo kupatikana, hakuna hatua zilizochukuliwa za kumuadhibu Mkandarasi huyu, kwa nini? Ana kinga gani? Kapataje tender hiyo?

Mheshimiwa Spika, ahsante sana.

MHE. MARIAM R. KASEMBE: Mheshimiwa Spika, naomba nichukue nafasi hii kuchangia kwa maandishi hotuba ya Wizara ya Ujenzi kama ifuatavyo:

Mheshimiwa Spika, hotuba ya Wizara hii imefungua matumaini mapya kwa wananchi wa Mkoa wa Mtwara kwa jinsi ambavyo imetoa mchanganuo wa bajeti ya ujenzi wa barabara mbalimbali za Mkoa

231 wetu na upembuzi yakinifu kwa barabara ya Mtwara– Tandahimba–Newala–Masasi.

Mheshimiwa Spika, sitatenda haki kama sitaizungumzia barabara ya Kibiti-Lindi hasa kwa kilomita sitini ambazo hazijakamilika hadi sasa. Mikoa ya Kusini inaongoza kwa kupanda kwa bei za bidhaa mbalimbali kutokana na gharama za usafirishaji kuwa kubwa kwa ajili ya hali mbaya ya barabara kutoka Ndundu-Somanga. Serikali ilichukua uamuzi mzuri sana wa kujenga barabara hii, lakini wananchi wanataka kujua ni kwa nini kilomita 60, hizi zinachukua miaka mingi kukamilika? Kwani kila bajeti Serikali huwa inatoa tarehe ya kukamilisha ujenzi lakini imekuwa kinyume na ujenzi unakwenda taratibu sana. Naiomba Serikali isimamie kikamilifu eneo hili likamilike kwa wakati kama bajeti hii inavyojieleza, tafadhali sana.

Mheshimiwa Spika, sambamba na hilo Serikali inafanya vizuri sana katika ujenzi wa barabara, lakini niiombe Serikali iwe karibu katika kusimamia na kuhakikisha barabara zinajengwa kwa viwango vinavyostahili ili kuepusha ukarabati wa mara kwa mara ambao unaisababishia Serikali kutumia fedha nyingi ambazo zingeweza kutumika katika ujenzi wa barabara nyingine.

Mheshimiwa Spika, naishukuru Serikali kwa kutenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja la Nangoo, wananchi wa Masasi wamefarijika, lakini bado ujenzi huu unakwenda taratibu sana. Naomba wasimamizi wanaohusika kusimamia ujenzi huu wawe karibu na kuangalia ujenzi huu, unajengwa kwa viwango na kasi

232 ili adha ambayo tumeipata kwa miaka mingi tuondokane nayo.

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Masasi kwa upande wa Mashariki tunapakana na Wilaya ya Newala kwa Vijiji vya Ndanda na Miyuyu ambako tunategemeana katika huduma za jamii, lakini miundombinu ya barabara si nzuri, tuna barabara ambayo ni ya kiwango cha changarawe. Ningeiomba Serikali ianze kufikiria ili iweze kujengwa kwa kiwango cha lami, kwani masika wananchi wanashindwa kuja kupata huduma ya afya katika Hospitali ya Rufaa ya Ndanda. Tafadhali naomba Serikali iangalie eneo hili kwani ni muhimu sana.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naomba yale yote niliyoishauri Serikali yapewe umuhimu na yanayohitaji majibu, Serikali itoe majibu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

MHE. MARTHA M. MLATA: Mheshimiwa Spika, kwanza nashukuru sana kwa nafasi hii nami nitoe mchango wangu kwa njia ya maandishi. Naomba nichukue nafasi hii kumpongeza Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Watendaji wote bila kumsahau Mtendaji Mkuu wa TANROAD. Siwapongezi kwa hotuba nzuri tu bali ni kwa kazi nzuri ambayo wamekuwa wakiifanya tangu bajeti tuliyoipitisha ya mwaka jana. Pamoja na hali ngumu ya uchumi uliopo na uliolikumba Taifa letu na Duniani, bado wameendelea kutekeleza yote yaliyopangwa na kupitishwa na Bunge, pia

233 yaliyotajwa kwenye Ilani ya uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi. Nawaombea afya na heri toka kwa Muumba Mungu wetu, Waswahili wanasema mnyonge mnyongeni, lakini haki yake mpeni.

Mheshimiwa Spika, natoa pongezi hizi kwa sababu, Mkoa wangu wa Singida kwa sasa barabara nyingi za vijijini zinapitika, watu wana uwezo sasa hata wa kuita au kukodi taxi toka Mjini Singida, Kiomboi au Manyoni hadi Kijijini kabisa hata wagonjwa na wanawake wajawazito wanapopatwa na uchungu wa uzazi kweli hali ni nafuu sana ya kupata usafiri. Tunashukuru sana. Mwaka 2005 wakati naingia Ubunge, mahali pengine sikuweza kufika kutokana na kutokuwa na barabara kabisa, lakini sasa nafanya ziara popote, kwa sasa hata pikipiki ziko vijijini kwani barabara ni nzuri. Ninachoona ni hatua kubwa sana ya maendeleo imefikiwa.

Mheshimiwa Spika, ombi langu, tafadhali kwa pale ambapo bado panahitaji kutengenezwa, msisite. Mfano, barabara ya Misigiri-Shelui, inatutia doa katika kazi nzuri iliyofanyika. Mkandarasi aliyejenga pale atafutwe arudie haraka, ni hatari sana. Barabara ya Sekenke-Shelui, naomba ifike hadi kwenye Ziwa dogo la Kiteka kwani ndiko uchumi ulipo.

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Sepuka-Ndago- Urughu-Mtekente hadi Shelui, tunaomba sana patiliwe mkazo kwani kule kuna uchumi mkubwa sana. Biashara ya wakulima wa mahindi, alizeti na kadhalika. Pia kama Mheshimiwa Waziri ataona vyema basi, hata akiweka kalami kadogo tu kila mwaka, nitashukuru

234 maana na Mbunge Martha Mlata anaishi pale Ndago Kibaya. Vingineyo endeleeni na kasi hiyo hiyo bila kusikiliza kelele za mlango maana hazimnyimi usingizi mwenye nyumba.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ni kuhusu TBA, napongeza kwa ujenzi wa nyumba za watumishi wa Serikali na Umma. Pia kwa mpango mlionao wa kwenda mikoa miwili nchini naamini Singida imo.

Mheshimiwa Spika, jambo ambalo TBA wamenifanya niwe na mashaka na kutendewa haki au usawa kwa wapangaji wa nyumba ni kwa shabby, mimi ni muathirika wa kutotendewa haki na TBA, maana niliingia mkataba na TBA Dodoma 2006 kisha nikaenda kusoma UK na waliendelea kuchukua fedha toka ofisi ya Bunge kwenye mshahara wangu, lakini cha kushangaza walimpangisha mtu mwingine bila kunipa taarifa na kuvunja mkataba. Kweli hali hiyo iliniuma sana.

Mheshimiwa Spika, pamoja na hayo, baada ya kurudi wakasema watanipa nyumba nyingine, lakini walishindwa na hivyo ikanilazimu niombe wanirudishie fedha ambayo ilishaingia kwenye account yangu tangu siku hiyo hadi leo sijapata nyumba. Pamoja na ahadi yao ya kunipa nyumba nyingine, lakini bado hawajanipa na naona wengine wanapata. Hivyo, ninahisi kuwa, kuna ubaguzi ama kuna element ya rushwa. Naomba hili litazamwe sana na naomba pia kujua.

235 Mheshimiwa Spika, je, niendelee kuwa na tumaini la kupata nyumba maana nimesubiri sana bila mafanikio.

Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, naunga mkono hoja asilimia mia moja.

MHE. PHILIPO A. MULUGO: Mheshimiwa Spika, natoa masikitiko yangu kwa Mheshimiwa Waziri na Wizara ya Ujenzi hasa kwa Meneja wa TANROAD, Mkoa wa Mbeya kutoingiza kwenye bajeti ya mwaka huu, barabara za Kata ya Kapalala mpaka Gua na Kapalala mpaka Ngwala na Kapalala na Udiude kuingiza kwenye orodha ya barabara zinazotakiwa kuhudumiwa na TANROAD, badala ya Halmashauri ya Chunya ambayo imeshindwa kabisa kuhudumia barabara hizi kwa kiwango cha changarawe. Mimi kama Mbunge wa Jimbo hili la Songwe, Wilayani Chunya ambako katika kitabu cha leo ulichowasilisha Bungeni, nimepitia na kubaini yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, imeandikwa na kuwekewa bajeti hivi kutoka Mbalizi na Igalula–Namkukwe hapo sina tatizo. Ila kutoka Mkwajuni–Saza-Kapalala, nimeona fedha zimewekwa kwenye bajeti.

Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Waziri anisaidia kuiweka barabara ya Kapalala mpaka Udinde kilomita nane, Kapalala mpaka Gua kilomita 35, Kapalala mpaka Ngwala kilomita 45.

Mheshimiwa Spika, barabara hizo ni muhimu sana sana kwa maendeleo ya Kata zangu nne. Za

236 Kapalala, Gua, Ngwala na Udinde, ambapo kuna Milima kufika Kijiji cha Udinde ambako ndipo Ziwa Rukwa linaanza na mizigo ya samaki, inatoka hapo Udinde. Kutoka Kapalala mpaka Udinde ni kilomita nane tu. Naomba Mheshimiwa Waziri anisaidie aiweke kwenye mpango wa TANROAD kuliko kuhudumiwa na Halmashauri, fedha huwa hazitoshi maana kuna mteremko au mlima mkali na ni vumbi tupu.

MHE. : Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja mia kwa mia.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa flyover ya TAZARA ni wazo jema la Serikali la kujenga ujenzi huo, lakini tumekuwa tunasema sana utekelezaji unakuwa unachukua muda mrefu. Hivyo, nashauri Wizara kupitia Serikali iharakishe ujenzi huo kwani ajali zinakuwa nyingi.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa majengo ya ghorofa hasa kwa upande wa Dar es Salaam majengo mengi huwa yanapata kibali cha ujenzi kutoka Wakala wa Majengo (TBA) na moja ya masharti katika vibali hivyo ni kuweka sehemu ya parking ya gari sehemu ya chini ya majengo hayo, lengo na madhumuni ni kupunguza msongamano wa magari, Dar es Salaam. La kusikitisha majengo hayo hujengwa na awali huacha eneo la chini wazi kama kugeresha, lakini baadaye eneo hilo hujengwa maduka na Wakala wa Majengo wanaiona hali hiyo. Hivyo, nashauri suala hili lisimamiwe ipasavyo kwa mujibu wa sheria.

237 Mheshimiwa Spika, suala la uwekaji (parking) ovyo kwa magari eneo la Jiji la Dar es Salaam, imekuwa ni mtindo kwa kila mwananchi kupaki gari lake nje ya duka lake na kufunga mnyororo jambo ambalo linachukua nafasi na kuzinga nafasi ya barabara na kusababisha msongamano wa magari. Hivyo, naishauri Wizara kutoa tangazo kwa wenye mtindo huo kuacha mara moja na kwa wale wanaopinga suala hilo, wachukuliwe hatua na Wizara na kwa umakini wa Waziri Magufuli suala hili si gumu kwake.

Mheshimiwa Spika, kuhusu majengo ya Serikali au nyumba za kuishi; ni kwa muda mrefu Waheshimiwa Wabunge wanapata tabu ya nyumba za kuishi hasa Dodoma wakati wa Bunge. Kwa utafiti kuna nyumba nyingi za Serikali wanaishi watu binafsi tena bila ya mikataba na malipo. Hivyo, naishauri Wizara kuandaa utaratibu mzuri wa kuwapatia nyumba Waheshimiwa Wabunge, nyumba hizo ili kuwaondoshea aibu ya kutanga tanga ovyo na kuishi katika magesti na mahoteli. Tunaelewa nyumba hizo zipo ila muhali umezidi.

Mheshimiwa Spika, fidia za wananchi katika ziara ya Kamati ya Miundombinu, tumekuta malalamiko mengi ya wananchi hawajalipwa fidia zao kwa nyumba au mazao na viongozi wao wakifuatilia wanambiwa wamo katika Road Reserve na sheria imewabana. Hata hivyo, sote sisi ni binadamu tena wananchi wa Tanzania, hivyo usipomsaidia mtu huyo aende akadai au akaomba msaada katika Serikali ya nani. Naishauri Wizara ising’ang’anie msimamo wa

238 sheria na ubinadamu uwekwe mbele na Mungu atatulipa kwa mema.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Wakandarasi waliokuwa si waaminifu; naishauri Serikali kutowapa kazi Wakandarasi wote ambao si waaminifu na hawafuati muda wa ujenzi kwa barabara zetu.

MHE. FAITH M. MITAMBO: Mheshimiwa Spika, nianze kwa kuunga mkono hoja. Pia naipongeza sana Wizara ya Ujenzi kwa kazi nzuri ambayo imefanya tangu huko nyuma hadi mwaka wa fedha 2011/2012. Wizara ya Ujenzi nakiri kabisa imefanya kazi nzuri isipokuwa kuna baadhi ya maeneo hasa kwenye Wilaya, matengenezo ya barabara ambazo zinaangaliwa na TANROAD. Aidha, matengenezo yake bado hayakufanyika kwa mwaka huo wa 2011/2012 au yamefanyika kwa kiwango kisichoridhisha ukilinganisha na value for money, barabara hizi hazikidhi viwango.

Mheshimiwa Spika, wakati mwingine barabara hizo hazitengenezwi kwa wakati na wakati mwingine barabara hizi zinaanza kutengenezwa mara baada ya kusikia ama Mwenge unakuja mahali pale au kiongozi fulani muhimu anatembelea sehemu husika na hivyo kuzifanya barabara hizo kutengenezwa kwa kulipuliwa. Suala la utengenezaji wa barabara hizi kwa staili hii ni vyema uangaliwe na ufuatiliwe, hauwezi kuwa sawasawa.

Mheshimiwa Spika, mwezi uliopita Mwenge ulitutembelea Wilaya ya Liwale, nimeshuhudia Mwenge unapitishwa na barabara inachongwa hapo

239 hapo, barabara ya kutoka Nachingwea kwenda Liwale.

Mheshimiwa Spika, Siku zote wakandarasi hawa walikuwa wapi, kwa hali hii tutegemee uchongaji wa barabara hii utakuwa mzuri na utalingana na pesa zilizotengwa kweli?

Mheshimiwa Spika, napenda nichukulie nafasi hii kumtaarifu Waziri wa Ujenzi kwamba sijaridhika kabisa na matengenezo yaliyofanywa na ndugu zangu wa TANROAD katika barabara ya Nachingwea, Liwale na hasa kutoka eneo la Mtawatawa hadi mpakani mwa Liwale na hasa kutoka eneo la Mtawata hadi mpakani mwa Liwale na Nachingwea eneo la Nangano.

Mheshimiwa Spika, ikiwezekana Wakandarasi waliopewa eneo hili warudie kufanya kazi hiyo upya. Nimeridhika kabisa na kazi ya Mkandarasi wa kutoka Mtawatawa hadi Liwale Mjini, amefanya kazi nzuri sana.

Mheshimiwa Spika, aidha, natoa masikitiko yangu kwa Waziri wa Ujenzi barabara ya Nangurukuru- Liwale hasa kutoka mpakani mwa Wilaya ya Kilwa hadi Liwale haijafanyiwa kazi kabisa, barabara ni mbovu kupita kiasi ina mashimo makubwa ya kutisha, lakini katika bajeti ya mwaka 2011/2012 barabara hii ilitengewa fedha, nashangaa ni kwa nini barabra ile ni mbovu kiasi kile.

Mheshimiwa Spika, nimwombe Waziri wa Ujenzi amuombe Meneja wa TANROAD Makao Makuu aende

240 kutembelea barabara hizi tu, barabara ya Liwale- Nachingwea eneo la Mtawatawa hadi Nangano na barabara ya Liwale-Nangurukuru, kutoka mpakani mwa Wilaya ya Kilwa na Liwale hadi Liwale Mjini ajionee yeye mwenyewe haya ninayoyasema hapa.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Liwale–Kingupira, mwaka 2010, Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete alitoa ahadi kwa wananchi wa Jimbo la Liwale, kwamba barabara ya kutoka Liwale hadi Kingupira itajengwa.

Mheshimiwa Spika, sijakata tamaa bado nategemea ahadi hii ya Mheshimiwa Rais itatekelezwa. Nimekuwa nikiuliza maendeleo ya ujenzi wa barabara hii mara kwa mara na mara ya mwisho niliambiwa kwamba wadau wa hifadhi ya Selous bado wako kwenye majadiliano ya jinsi gani barabara hii itajengwa bila kuathiri hifadhi hii ya Selous.

Mheshimiwa Spika, katika majumuisho yake Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, nitaomba anipatie majibu mchakato wa ujenzi wa barabara hii ya Liwale- Kingupira umefikia wapi na ujenzi wake utaanza lini?

Mheshimiwa Spika, UNESCO imeridhia Hifadhi ya Selous kumegwa kwa upande wa Kusini kwa ajili ya uchimbaji wa madini ya Uranium, sasa sisi wananchi wa Liwale tunahitaji ki-strip kidogo tu cha kupitisha barabara ndani ya hifadhi hii. Kwa nini maamuzi ya ujenzi wa barabara hii yanachukua muda mrefu?

241 Mheshimiwa Spika, nategemea kupata jibu na wananchi wenzangu kule Liwale wapate mategemeo.

MHE. PROF. ANNA K. TIBAIJUKA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kunipa nafasi, nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Daktari John Pombe Magufuli, Waziri wa Ujenzi na Katibu Mkuu wake na timu zao hapa Wizarani na TANROADS kwa kazi nzuri inayoonekana katika nchi yetu Tanzania. Mheshimiwa Waziri Magufuli ni best practice mfano wa kuigawa.

Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya wananchi wa Muleba Kusini, nimshukuru na kumpongeza Waziri kwa hatua kubwa aliyofikia katika barabara ya Kigoma- Lusahunga. Ni matumaini yangu kwamba, mwaka huu kazi hii itakamilika. Wananchi wa Muleba wana kiu kuona barabara hii inakamilika ukizingatia kuwa tayari ilichelewa sana hapo nyuma.

Mheshimiwa Spika, nimshukuru Waziri pia kutenga fedha za ukarabati wa barabara ya Muhutwe- Kamachumu-Muleba, lakini wasiwasi wangu ni kwamba barabara hii inatakiwa kuwa na lami. Hii ni ukizingatia Hospitali Teule ya Wilaya ya Muleba, Rubya Hospital ipo kwenye barabara hii. Sasa hivi wagonjwa wanakwama sana kwenye Mlima wa Kanyambogo, mvua inaponyesha changarawe yote huporomoka, kwa kifupi bila lami Mlima wa Kanyambogo hauna tiba nyingine. Aidha, Mheshimiwa Waziri aiagize TANROADS kufanya upembuzi yakinifu wa barabara hii ya Muleba Rubya-Kamachumu-Muhutwe kwa kiwango cha lami ili tuangalie uwezekano kwa Halmashauri kuchangia barabara hii ya Mkoa. Aidha, uchumi wa Wilaya ya

242 Muleba unatokana na barabara hii maana iwe ndizi kahawa au maharage vinasombwa kupitia barabara hii kuingia barabara kuu ya Muleba Bukoba.

Mheshimiwa Spika, nichukue pia nafasi hii kumwomba Mheshimiwa Waziri kuangalia ukarabati wa barabara ya Kyamyorwa-Chato ambayo lami yake imeharibika na kuchakaa kutokana na kuchelewa kwa barabara ya Kigoma-Rusahunga, malori ya mizigo mikubwa yalitumia njia ya Chato na hivyo kuharibu barabara. Wahenga walisema usipoziba ufa utajenga ukuta. Naomba tulinde barabara za lami katika Mikoa ya pembezoni kama Kagera ambayo ilikuwa imesahaulika kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, nimesikitika kidogo kuhusu kutoona katika bajeti hii fedha kwa ukarabati wa barabara ya Kasindoga-Karumbi-Ngote-Kasharunga ambayo ni ya Mkoa. Barabara hii pia ni uti wa mgongo wa Wilaya ya Muleba ikatumikia kusomba kahawa na maharage na karanga.

Mheshimiwa Spika, hapo hapo sina budi kuomba barabara ya Kasharungu-Burigi ipandishwe hadhi kuwa ya Mkoa na kuwekwa chini ya himaya ya TANROADS. Ziwa Burigi ni hazina kubwa sana na hivi sasa uchumi wake katika kilimo cha mpunga na ufugaji vinakua haraka sana. Pia Halmashauri ya Muleba iko katika mkakati wa kuwahamisha vijana ambao hawana ardhi kutoka sehemu za Kata za Nshambo, Kashasha, Ijumbi, Kishando, Buganguzi, Bureza na Muleba kupewa maeneo ya Burigi na Kyebitembe walime mpunga, vijana hao watahitaji huduma muhimu ikiwemo

243 barabara yenye uhakika. Aidha, eneo hili la Burigi pia linatumika kwa kuwapokea wawekezaji. Hakika bila barabara ya uhakika mpango huu wa Halmashauri kuwavuta wawekezaji unaweza kushindwa.

Mheshimiwa Spika, Jimbo la Muleba Kusini, lina eneo kubwa la Hifadhi ya Pori la Taifa la Rwiga. Sasa hivi pori hili limevamiwa na wahamiaji haramu kutoka nchi jirani, wakichunga na kuchoma mkaa, wananchi jirani wanahangaika kutafuta maeneo ya kuchunga wakati wageni wanatamba katika msitu huu wa hifadhi, ukosefu wa barabara ya kufikia pori hili kupitia Ziwa Burigi, umechangia sana uvamizi wa pori hili na wimbi la majambazi wanaojificha humo.

Mheshimiwa Spika, nikigeukia upande wa shughuli nyingine za Wizara ya Ujenzi sina budi kumpongeza Waziri kwa hatua kubwa alizopiga katika ujenzi wa majengo ya Serikali kupitia TBA. Nichukue fursa hii kutoa mapendekezo kwa nini TBA isiishie tu kujenga nyumba Dar es salaam bali ijenge pia katika Wilaya ya Muleba ambayo ina uhaba mkubwa wa nyumba. Inapokuja kujenga nyumba Dar es Salaam, nimpongeze Mheshimiwa Waziri Magufuli kuiweka barabara ya Mlimani City-Ardhi-Makongo-Goba katika bajeti hii kwa kuwa, Wizara ya Ardhi ina mpango wa kuendeleza eneo la Makongo juu kwa kiwango cha barabara za lami. Naomba Mheshimiwa Waziri kuagiza TANROADS kuupa mradi huu kipaumbele. Aidha, nimwombe Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi aharakishe zoezi la barabara hii kabla kandarasi anayejenga barabara ya Mwenge-Tegeta haja-demobilize ili tupate unafuu wa gharama.

244

Mheshimiwa Spika, nimalizie kwa kumwomba Mheshimiwa Waziri kulieleza Bunge lako Tukufu hatua atakazowachukulia Wahandisi wa Halmashauri wasio waaminifu na hivyo kujihusisha kutoa vibali vya ujenzi bila kuzingatia sheria za mipango miji. Aidha, Wahandisi hawa wamekuwa wakitoa building permit kwenye maeneo bila kuzingatia building height restrictions. Pamoja na kuipongeza TBA, kuingia ubia na sekta binafsi imekuwa ikifanya hivyo kwa kujenga maghorofa marefu kinyume cha sheria. Mfano, ni jengo zuri sana ambalo Mheshimiwa Waziri ameonesha kwenye cover ya kitabu cha bajeti yake. Jengo hili la TBA, hapa ocean road, limevuka viwango, Mheshimiwa Waziri mwenye utendaji usio na mfano naamini ataonesha ushirikiano kulisimamia jambo hili, kufuata sheria za mipango miji ili pia tuwe na viwango na miji yenye mandhari.

Mheshimiwa Spika, nampongeza sana Mheshimiwa Waziri.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Spika, kuhusu barabara zinazosimamiwa na Wilaya; barabara hizi hupata fedha za matengenezo madogo madogo na kusimamiwa na Wahandisi wa Wilaya. Hata hivyo, barabara hizi bado hazionekani kama zinatengenezwa na kuwa stahimilivu kwani fedha zinazopelekwa ni kidogo zisizolingana na mahitaji na mara nyingi fedha huchelewa sana. Uzoefu umeonesha fedha hizi hufika wakati tunaelekea mwisho wa mwaka wa fedha.

245

Mheshimiwa Spika, nashauri kwamba, fedha ziwe zinafika kwa wakati ili kuleta ufanisi wa ujenzi wa Barabara Wilayani kama ilivyopangwa na Halmashauri husika. Fedha zinazopelekwa Local Government ziongezwe kadri ya mahitaji ya Halmashauri husika.

Mheshimiwa Spika, mahusiano ya TANROADS na Wahandisi wa Wilaya yapo mbali na hayaridhishi, hatuoni kama TANROADS wanawapa ushirikiano wa kutosha Wahandisi wa Wilaya. Hata hivyo, hatuoni umuhimu wa uwepo wa TANROADS kwani ni kuongeza mamlaka au urasimu wa kiuongozi usiokuwa na tija ya moja kwa moja. Wahandisi wa Wilaya ndiyo wapo katika Halmashauri za Wilaya zenye wananchi, hata hivyo, takwimu zinaonesha TANROADS hupata 75% ya fedha za barabara na Halmashauri za Wilaya kupitia TAMISEMI wenye uhitaji mkubwa wa barabara itakuwa ni Halmashauri za Wilaya.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu ni kwamba, kuanzishwe District Road Agency, zitakazowajibika moja kwa moja Wizarani kwa kuipa mamlaka kamili ya kisheria. Kufanya hivi kutapunguza urasimu usio wa lazima na huduma kufika moja kwa moja kwa wananchi na kwa ufanisi mkubwa.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Wahandisi na Wakandarasi wasio na sifa. Katika Halmashauri za Wilaya Wakandarasi wengi wanaopewa kazi za matengenezo ya barabara hawana sifa stahili na hupewa kazi kindugu au urafiki na Wakurugenzi, Wenyeviti wa Halmashauri au Wahandisi husika wa

246 Wilaya hii hupelekea barabara nyingi kutengenezwa chini ya kiwango bila kuwepo value for money.

Mheshimiwa Spika, nashauri kuwa, pawepo au kuandaliwe mkakati au mechanism itakayowabana Wahandisi wanaopewa kazi za matengenezo ya barabara katika Wilaya na wawe na sifa zinazokidhi kulingana na taaluma zao. Mikataba inayofikiwa kati ya Wakandarasi na Halmashauri ipitiwe na kuridhiwa na Baraza la Madiwani ili Madiwani nao wahusike katika kuwatambua Wakandarasi wanaopewa kazi za barabara na si kupata tu taarifa za utekelezaji (hii haimaanishi kuwa Madiwani watachukuliwa kuwa ni watendaji).

Mheshimiwa Spika, uvamizi wa hifadhi za barabara, Serikali inalazimika kuendelea kutoa elimu kwa wananchi kutoendelea kuwavamia hifadhi za barabara na hili lifanyike katika maeneo yote nchini, hii ni kuweza kuona barabara zetu zinadumu kwa muda mrefu. Hata hivyo, katika maeneo ambayo tayari kuna uvamizi wa maeneo ya hifadhi ya barabara, wananchi wapewe muda wa kuondoka katika maeneo hayo na si kuvamia kwa kuwaondoa kwa nguvu na kuharibu mali za wananchi huku wananchi wenyewe wakiwa katika hali ngumu ya maisha.

Mheshimiwa Spika, Tanzania Building Agency (TBA), majukumu ya Shirika hili yanaonekana kutekelezwa katika maeneo ya Serikali Kuu tu na haihusiki katika Serikali ya Mitaa. Hivyo ni vyema TBA ikashirikiana kwa karibu zaidi na mamlaka ya Serikali za Mitaa pale ambapo nyumba za Serikali zinajengwa

247 kwa fedha za walipa kodi wa Tanzania, hivyo TBA ihusike kusimamia miradi husika. Hata hivyo ni vyema Wakala wa TBA wawepo katika Serikali za mitaa.

Mheshimiwa Spika, maswali ya ufafanuzi, kwa nini barabara ya Karatu Junction-Mangola-Mataka kilomita 150 kwa mwaka wa fedha 2012/2013, imetengewa fedha kidogo kulinganishwa na mwaka 2011/2012?

MHE. ENG. RAMO M. MAKANI: Mheshimiwa Spika, miradi ya barabara inayojengwa na Wakandarasi wa nje itumike kama shule kwa Wahandisi wazalendo. Hali ya sasa katika miradi mingi inasikitisha, ajira kwa Wahandisi wazalendo iwe ni sehemu ya mikataba ya ujenzi kwa Wakandarasi. Wanafunzi wa vyuo vikuu na vyuo vya kati wapatiwe nafasi ya kufanya mafunzo (field practical training) iwe sehemu ya mkataba.

Mheshimiwa Spika, ushiriki wa wataalam wazalendo ni kujenga uwezo (capacity building), Technology transfer, uwezo wa kufanya matengenezo (maintenance) wakati wa uhai wa barabara hizo ambazo ni kilomita nyingi zitakazoanza kuwa na mahitaji ya maintenance kwa wakati mmoja.

Mheshimiwa Spika, hatuwezi kujenga barabara zote kwa kiwango cha lami, barabara za udongo na zile za changarawe bado zinahitajika katika baadhi ya maeneo ambako hatuna uwezo wa kujenga barabara za lami. Suluhisho ni kujenga barabara hizo kwa viwango stahiki na (design period) inayotakiwa ifikiwe.

248 Mheshimiwa Spika, ili hilo liwezekane tunahitaji kuwa na wataalam wa kutosha na wenye ujuzi stahiki. Halmashauri za Wilaya LGAs nyingi hazina Wahandisi na Mafundi Sanifu (Technicians) wa kutosha hivyo kutekeleza miradi hiyo chini ya kiwango na kwa gharama zaidi.

Mheshimiwa Spika, Wizara ishirikishe na kuiagiza Bodi ya Usajili wa Wahandisi ikishirikiana pia na TCU na NACTE, pamoja na Vyuo Vikuu waratibu utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo wa miaka mitano 2011/2012 na 2015/2016 kwa kuhakikisha lengo la kuzalisha Wahandisi Wasanifu majengo na Mafundi Sanifu husika wanafikia 88,000 mwaka 2015. Hivi sasa kuna Wahandisi wasiofikia 12,000 na wasanifu majengo wasiofikia 600, (12,000+600=18000).

Mheshimiwa Spika. Kuhusu Kaguzi za barabara (miradi) ikiwa ni pamoja na zile za CAG, zishirikishe wadau wote, CAG, ERB, AQRB. Kufanyike pre-audits badala ya hali ya sasa ya post audits, ili kubaini potential challenges mapema. Kwa mfano, kwa nini tupeleke fedha nyingi katika Halmashauri wakati huko hakuna wataalam.

Mheshimiwa Spika, Resource Sharing, fedha za Mfuko wa Barabara zisitawanywe katika kila Halmashauri. Halmashauri kadhaa zinaweza ku-share Wahandisi na Mafundi Sanifu kisha kupatiwa fedha ili kujenga barabara za vipaumbele na kuhamia nyingine hatua kwa hatua na hasa kwa kuunganisha kazi ili kuvutia Wakandarasi kibiashara.

249 Mheshimiwa Spika, Wakala wa Barabara Vijijini, TANROADS haiwezi kumudu work load ya mtandao wote wa barabara nchini yaani Truck roads, Regional Roads na District Roads, (za lami, changarawe na udongo) hata sheria zilizopo haziruhusu kiundwe chombo hiki haraka?

MHE. DKT. DALALY P. KAFUMU: Mheshimiwa Spika, naishukuru Serikali kwa kuanza ujenzi wa daraja la Mbutu ambalo lilikuwa ni kero kubwa kwa wananchi na lilisumbua kwa kuwa baadhi ya wananchi wa Wilaya ya Igunga walisombwa na maji ya Mto Mbutu wakati wa masika.

Mheshimiwa Spika, barabara itokayo Igunga kupitia daraja la Mbutu kupitia Vijiji vya Mbutu, Mwamashimba, Imalanguzu, Mwamakona, Igurubi hadi Mkoa wa Shinyanga, sasa inahitaji kujengwa kwa kiwango cha changarawe ili kuunganisha wananchi wa mikoa hii. Barabara hii pia ni muhimu sana kwa usafirishaji wa zao la pamba. Kwenye bajeti hii barabara hii haijapewa fedha yoyote, pamoja na kujenga daraja la Mbutu bila kuijenga barabara hii, ujenzi wa daraja hili unaweza usiwe na value for money.

Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Igunga sasa iko kwenye mchakato wa kuomba barabara kutoka Igunga, kupitia Vijiji vya Mwanzugi, Lugubu, Itumba, Mihama, Susujanda, Miswaki (Mpyagule) Loya hadi Iyumbu (Mkoani Singida) iwe barabara ya Mkoa na ihudumiwe na TANROADS. Kujengwa kwa barabara hii kutaweza kuunganisha

250 Mkoa wa Tabora na Mkoa wa Singida kwani barabara itokayo Singida hadi Iyumbu, hii ni barabara ya TANROADS. Tutakapoleta ombi letu tunaomba barabara hiyo ipandishwe hadhi na kupewa fedha za kujengwa.

Mheshimiwa Spika, Wilaya ya Igunga haina barabara ya lami isipokuwa ile barabara ya Kitaifa inayopita Wilayani ikitokea Dar es Salaam kwenda Mwanza. Naiomba Serikali ianze kutafakari ujenzi wa barabara ya lami kukatisha Wilaya ya Igunga kutoka Shinyanga kupitia Uenyege, Igumbi, Mwamashimbi, Igunga, Itumbi, Miswaki, Loya, Iyumbo hadi Singida. Pia barabara kutoka Ziba, Nkinga, Simbo, Ndala, hadi Puge ijengwe kwa kiwango cha lami ili kuifungua Wilaya hii ambayo haina barabara ya lami hata moja isingekuwa na uwepo wa barabara ya Dar es Salaam na Mwanza kutatisha.

Mheshimiwa Spika, nimalizie tena kwa kuishukuru Serikali kwa kazi nzuri ya kujenga miundombinu ya barabara katika nchi yetu. Naiomba Wizara ya Ujenzi iendelee na tempo hiyo hiyo ya kazi nzuri. Nashukuru kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja.

MHE. NASSIB SULEIMAN OMAR: Mheshimiwa Spika, kwanza niunge mkono hoja mia kwa mia. Katika miradi mingi ya ujenzi wa barabara na madaraja, nyumba na mali nyingine zimevunjwa au kuondolewa kuruhusu kujengwa miradi hii. Tatizo lilojitokeza ni kuwa watu hawa hawajafidiwa kwa muda mrefu ingawa Serikali

251 imekubali kulipa fidia hiyo, tulipotembelea miradi hii katika mwezi wa Juni, 2012, Kamati ya Miundombinu tulishuhudia kwa macho yetu wananchi wanalalamika kwa muda mrefu hawajafidiwa.

Mheshimiwa Spika, namwomba Waziri ahakikishe watu wote wanaodai fidia wanalipwa haraka kama inavyowezekana.

Mheshimiwa Spika, kuhusu wizi katika miradi ya njia na madaraja. Nitoe masikitiko yangu kwa matokeo mengi ya wizi wa vifaa vya ujenzi na alama za barabarani. Lazima Serikali iweke mikakati maalum ya kudhibiti vitengo hivi vibaya. Pendekezo ni kuwataka Wakuu wa Wilaya waweke Kamati Ndogo za ulinzi na usalama kushugulikia suala hili. Vilevile wananchi washirikishwe kulinda miradi iliyomo katika maeneo yao.

Mheshimiwa Spika, matumizi mabaya na magari na matengenezo ya magari, ripoti ya CAG ya tarehe 31/03/2012 umeonesha matumizi mabaya ya magari na matengenezo yake. Hii imesababisha Serikali kupoteza fedha nyingi. Namtaka Mheshimiwa Waziri atekeleze ushauri uliotolewa na CAG ili kuokoa fedha nyingi za Serikali.

MHE. IGNAS A. MALOCHA: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Rais kwa kutukumbuka wananchi wa Mikoa ya Rukwa na Katavi na mikoa mingine ya pembezoni kwa kazi inayofanyika kwa kuwatengenezea kwa kiwango cha lami.

252 Mheshimiwa Spika, pamoja na jitihada za Serikali kuendelea kujenga barabara za lami, ili barabara hizo ziweze kuwanufaisha wananchi lazima Serikali ihakikishe inajengwa na barabara kwenda kwenye uzalishaji kwa maana ya vijijini. Bila kufanya hivyo itakuwa haileti tija sana, kwa wananchi ambao ndiyo wazalishaji wa malighafi itakayotumiwa na barabara hiyo.

Mheshimiwa Spika, naomba sasa nizungumzie barabara iliyopo ukanda wa Ziwa Rukwa, barabara inayoanzia Kibaoni-Muze-Mto Wisa-Kilyamatundu hadi Mloo.

Mheshimiwa Spika, huu ni Ukanda wa Bonde la Ufa ambalo ni maarufu sana katika kilimo lenye rutuba nyingi na linalokubali karibu mazao yote. Barabara hii inatakiwa ifikiriwe kutengenezwa kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, Daraja la Mto Momba, linalounganisha Wilaya ya Sumbawanga na Wilaya ya Mbozi Magharibi, naiomba Serikali ifikirie kujenga daraja hilo. Kuna tatizo kubwa la kukosa Daraja la Mto Momba, kiungo cha Kilyamatundu na Kamsamba. Mheshimiwa Waziri ana uwezo mkubwa sana, ajaribu kuwaonea huruma wananchi wa sehemu hiyo wanateseka mno. Naomba nipatiwe majibu.

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Ntendo-Muze, Mkataba wa PMMR uendelee.

253 Mheshimiwa Spika, naomba kuendelea kukumbusha ahadi za Mheshimiwa Rais wakati wa uchaguzi 2010, kujenga barabara zifuatazo kwa kiwango cha lami ambazo ni Kalambanzite-Ilemba na Miangalua-Chombe.

Mheshimiwa Spika, mwisho, nampongeza sana Mheshimiwa Magufuli kwa umakini wake wa kusimamia Wizara hiyo vizuri na Mwenyezi Mungu akuzidishie afya njema ili uendelee kulitumika Taifa hili.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, nakupongeza kwa hatua yako ya kutuwezesha Wilaya Mbogwe kupata barabara ya Mkoa, hongera sana.

Mheshimiwa Spika, nakuomba sasa baada ya kazi nzuri ufikirie kutuunganisha na barabara kuu itokayo Kahama-Geita kupitia barabara ambayo tayari ipo ya TANROADS ya Malito hadi Muga inapakana na Kata za Ng’homolwa Bukandwe na Lingunga ili iungane na barabara yetu hii mpya ya Butengo, Lumasa, Iparamasa na Masumbwe.

Mheshimiwa Spika, nitashukuru sana kwa ushirikiano wako.

MHE. ABDALLA HAJI ALI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napenda kumshukuru Mwenyezi Mungu mwingi wa rehema na mwingi wa ukarimu.

254 Mheshimiwa Spika, naanza mchango wangu kwa kusema kwamba barabara ni suala muhimu sana kwa maendeleo ya kiuchumi katika kila nchi duniani kote.

Mheshimiwa Spika, wazalishaji wote wawe wa kilimo, viwanda, madini, uvuvi na hata wafugaji, ufanisi wa yote hayo ni mtandao mzuri wa barabara. Bila barabara yote hayo yatakuwa magumu sana.

Mheshimiwa Spika, ili kuwasaidia wananchi wetu naiomba Serikali, suala la barabara pamoja na jitihada ya Serikali juu ya jambo hili iongeze juhudi zaidi na zaidi. Mheshimiwa Spika, msongamano wa magari Dar es Salaam unasababishwa na mtandao wa barabara kuzidiwa na magari. Naishauri Serikali iliangalie hili hasa ikingatia kwamba, msongamano huu unasababisha wafanyakazi kuchelewa kazini. Mtu huganda barabarani kwa masaa na hawezi kutimiza wajibu wake kutokana na kuchelewa kufika kazini kutokana na foleni ya barabarani.

Mheshimiwa Spika, hili linaweza kusababisha hasara kubwa kwa Taifa, naishauri Serikali itimize azma yake ya upanuzi wa barabara na ujenzi wa barabara za juu (flyover) nadhani hili litapunguza adha ya kuganda barabarani.

Mheshimiwa Spika, pia naishauri Serikali kuipatia Wizara ya ujenzi pesa walizoziomba kwa ukamilifu na kwa wakati sahihi. Hii itasaidia Wizara kutekeleza ahadi zake nchi nzima na kuondoa malalamiko juu ya Serikali yao.

255 Mheshimiwa Spika, ujenzi wa reli una umuhimu wa kipekee katika suala zima la uzima na uimara wa barabara zetu katika matumizi ya reli yataondoa mzigo mzito inaoielemea barabara zetu. Barabara nyingi zinaharibika mapema baada ya kujengwa kwa kupitiwa na mizigo mizito ambayo kama reli ikifanya kazi vizuri hakutakuwa na ulazima wa kusafirisha mzigo na shehena nzito kwa kutumia barabara. Sote ni mashahidi kwa barabara zetu jinsi zinavyogharibika kwa kipindi kifupi.

Mheshimiwa Spika, hata vituo vya mizani vya kupimia uzito wa magari na vyenyewe vinapaswa kuangaliwa sana. Je, wafanyakazi wanafanya kazi ile kwa uadilifu au wakati mwingine magari yanarusiwa tu?

Mheshimiwa Spika, mwisho nampongeza Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi kwa juhudi zake.

MHE. JASSON S. RWEIKIZA: Mheshimiwa Spika, hii ni nyongeza ya mchango wangu wa maneno. Nasisitiza kuwa Bukoba lazima tufikiriwe sana katika ujenzi wa barabara hadi leo Bukoba vijijini tuna barabara za lami zisizozidi kilomita 18. Bukoba nzima (kuongeza na mjini) hatuzidi kilomita 30 au 25.

Mheshimiwa Spika, hii ni hatari, ule mradi niliosema wa Kabengo Bay, wenye barabara yenye kilomita 42 upewe kipaumbele cha pekee. Hii itakuwa mkombozi wetu kwa watu wa Bukoba. Mheshimiwa Spika, pia kuna suala la road reserve katika barabara ya Naruku, kule Bukoba. Barabara hii

256 imetengwa kufanyiwa extension kule vijijini. Wananchi hawajaambiwa ukweli kuhusu extension hii, kwamba barabara itapanuliwa kiasi gani? Je, watapata fidia au la na kadhalika. Hili nalo ni muhimu kwani hata hawawezi kujua hatima yao na hawawezi kujenga, hata kulima.

MHE. JAMES D. LEMBELI: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa napenda kukiri kwamba, naunga mkono hoja kwa sababu moja kubwa kwamba, kazi zinazofanywa na Wizara hii zinaonekana. Pamoja na ufinyu wa bajeti yake, kidogo wanachopata wanakifanyia kazi na kwa ustadi mkubwa.

Mheshimiwa Spika, lakini pia naipongeza Wizara na hususani Waziri wake kwa kudhibiti ufisadi mkubwa uliokuwa umesheheni katika kukadiria gharama za ujenzi wa barabara, hivyo kupunguza gharama za ujenzi wa barabara, zaidi ya shilingi bilioni moja hadi shilingi 700,000/=. Huu ni ushahidi tosha kwamba Wizara hii inaongozwa na viongozi wenye uzalendo wa hali ya juu.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kazi nzuri hii katika Jimbo langu, lipo tatizo moja la utengenezaji wa barabara ya Mkoa ya kutoka Nyandeka kwenda Nghwade kupitia Uyogo. Barabara hii ilipandishwa daraja kutoka ya Halmashauri kwenda Mkoa katika mwaka wa fedha wa 2009/2010. Lakini cha ajabu mwaka wa fedha wa 2010/2011 barabara hii haikupewa fedha na mwaka huu wa fedha 2012/2013 imetengewa fedha kidogo sh. 200,000,000/=. Ambazo

257 zitatengeneza kilomita 11 tu kati ya kilomita zisizopungua 120.

Mheshimiwa Spika, barabara hii ni muhimu sana kwa uchumi wa Wilaya, Mkoa na Taifa, ni eneo muhimu kwa uzalishaji wa mazao ya tumbaku, pamba na mazao ya misitu. Naomba sana Wizara iipe kipaumbele zaidi barabara hii ambayo ni muhimu.

MHE. ALBERT O. NTABALIBA: Mheshimiwa Spika, naomba kupongeza juhudi kubwa zinazofanywa na Serikali yetu chini ya Jemedari hodari Daktari Mheshimiwa Magufuli wa Wizara ya Ujenzi. Katika awamu hii ya uongozi wa Magufuli ndipo barabara za nchi hii zinasonga mbele. Kwa upande wa Mkoa wa Kigoma, napenda kuona na kupongeza juhudi zinazoendelea kwa barabara za Kidahwe-Uvinza na mipango iliyopo ya Kidahwe-Nyakanazi.

Mheshimiwa Spika, mimi ambaye ni Mbunge wa Manyovu naendelea kuomba Serikali yetu na Waziri Magufuli kuona na kuamua kujenga barabara ya Manyovu na Kasulu (42 kilomita), ijengwe kiwango cha lami kwa sababu zifuatazo:-

Mheshimiwa Spika, inaunganisha toka Burundi mpaka mikoa mingine, Manyovu kuna Masoko ya Kimataifa matatu yanayojengwa ili watu wa Burundi waweze kuja kununua mazao mbalimbali. Kupunguza urefu uliopo wa kuzunguka mpaka Kigoma. Kunusuru utelezi uliopo kwenye milima ya heri juu na kuokoa ajali zinazotokea.

258 Mheshimiwa Spika, muhimu sana, barabara kwa Mkoa wa Kigoma imekuwa ni siasa. Wananchi wanaona ukichagua Mpinzani ndipo barabara ya lami inapatikana, barabara zinazojengwa zote ziko kwa Wapinzani. Naomba muokoe CCM, Kigoma jengeni hii barabara na muokoe Ubunge wangu.

Mheshimiwa Spika, napenda niipongeze TANROADS Kigoma, wanafanya kazi nzuri sana nami kama Mbunge naomba niwapongeze.

Mheshimiwa Spika, kuhusu fidia kwa wananchi wa Vijiji vya Kinanzi na Janda katika Jimbo la Manyovu, barabara ya Kisili-Buhigwe ni ya Mkoa. Wao wamewekewa X na hawajaambiwa lolote huku kisheria watu wale wanatakiwa kulipwa kwa sababu barabara imewafuata.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali itoe kauli juu ya madai ya maduka 120 ambapo kesi iliyofunguliwa na wakazi wa Mnanila kutolewa au kufutwa toka Mahakamani ili suluhu ipatikane nje ya Mahakama, watu wale bado wanadai fidia.

Mheshimiwa Spika, mwisho, nikupongeze Mheshimiwa Magufuli kwa uchapaji kazi wako.

MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Spika, nianze mchango wangu kwanza kwa kuwapongeza wafuatao: Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Daktari John Magufuli; Naibu Waziri, Mheshimiwa Engineer Gerson Lwenge; Katibu Mkuu, Balozi Mlango; Naibu Katibu

259 Mkuu, Daktari Ndunguru na watendaji wote wa Wizara hii kwa uwasilishaji wa bajeti yao hapa Bungeni.

Mheshimiwa Spika, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu, bahati nzuri nilipata nafasi ya kutembelea na kukagua baadhi ya miradi na madaraja ya Kanda ya Ziwa, niipongeze Serikali kwa kazi nzuri na kubwa iliyofanywa katika miradi hiyo.

Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi hizo yapo mapungufu yaliyojitokeza katika miradi hiyo. Tulishuhudia wenyewe na kupokea taarifa za Mameneja wa TANROAD Mikoa wakilalamika kutokana na baadhi ya miradi kusimama na hata kusababisha Wakandarasi kuondoa vifaa katika maeneo ya kazi, mbaya zaidi tuliambiwa kuna tozo zinazotozwa kila siku kutokana na ucheleweshaji wa malipo hayo.

Mheshimiwa Spika, pengine ingekuwa vizuri sana Serikali iwe na vipaumbele vya miradi michache ambayo haitasababisha kuwa na tozo hizo ambazo zinaongeza ukubwa wa bajeti na kutomaliza miradi kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, jambo lingine ambalo ningependa kulichangia ni pamoja na Kitengo cha (TEMESA). Naamini Serikali ilipoanzisha Kitengo hiki ilianzisha kwa nia nzuri kabisa, yaani ni pamoja na kutengeneza magari yote ya Serikali. Lakini kama Serikali ina nia thabiti ya kutumia kitengo hiki ni vyema sasa kitengo hiki kipewe umuhimu wa kutenga fedha za kutosha ili kiwe na vifaa vya kisasa vya kazi na

260 wataalam ili Serikali iweze kuokoa fedha nyingi sana za Serikali zinazotumika katika magereji ya watu binafsi. Utaona kila Kitengo cha Wizara zote za Serikali na Mashirika ya Umma wanatenga fedha kwa ajili ya matengenezo makubwa na madogo ya magari. Ni imani yangu pesa yote hiyo ingekwenda katika Kitengo hicho, Wizara ingekuwa na chanzo kizuri sana cha mapato kuliko hivi sasa na wapo wafanyakazi wanaolipwa pesa bila kufanya kazi iliyokusudiwa.

Mheshimiwa Spika, pia nijielekeze kwa Wakala wa Majengo (TBA), niwapongeze sana wafanyakazi wa kitengo hiki kwa ajili ya huduma hiyo ya ujenzi wa nyumba za wafanyakazi wa Serikali na ofisi, lakini pamoja na uzuri wa majengo hayo ni vyema pia fungu la matengenezo lingeongezwa, sababu miundombinu mingi ya majengo hayo ni mibovu sana ambayo itasababisha kutodumu kwa nyumba hizo.

Mheshimiwa Spika, vile vile niungane na Kamati ya Miundombinu kwa kuishari Serikali kwamba ni vizuri sasa Wakala huu ujiendeshe kibiashara ili iweze kusaidia wafanyakazi wengi zaidi.

Mheshimiwa Spika, niendelee kuipongeza Serikali kwa kutoa kipaumbele kwa barabara za Jiji la Dar es Salaam kwa kuimarisha miundombinu ya barabara na kuendeleza mpango wake wa kujenga flyover ili kupunguza msongamano wa magari.

Mheshimiwa Spika, ni ukweli usiopingika kuwa uchumi wa nchi hii kwa sehemu kubwa unategemea shughuli za kiuchumi zinazofanyika katika Jiji la Dar es

261 Salaam. Ningeomba pia uwepo utaratibu wa TANROAD kuainisha barabara za Halmashauri ambazo ni za kiuchumi. Kuna barabara ambazo wakati wa masika hazipitiki na kusababisha wakulima kushindwa kusafirisha mazao yao. Kama barabara hizi zingechukuliwa na wakala wa barabara zingesaidia pia kukuza uchumi wa nchi yetu kwa sababu Halmashauri zetu nyingi hazina uwezo wa kuzitunza barabara hizi na hazina wataalam wa kutosha.

Mheshimiwa Spika, mwisho ningeomba Mheshimiwa Waziri utusaidie ujenzi wa daraja letu la Igumbilo lililopo katika Kata ya Ruaha, Jimbo la Iringa mjini. Upembuzi yakinifu unaonesha kama shilingi 1.09 bilioni na uwezo wa Halmashauri ni mdogo sana, wapo wananchi takribani 4,002 wakiwemo wanafunzi wa shule ya Igumbilo 955 na wanachuo 220. Daraja hili lishaleta maafa, kila mwaka wanafunzi wanapoteza maisha.

Mheshimiwa Spika, baada ya mchango wangu huu, naunga mkono hoja.

MHE. JUMA OTHMAN ALI: Mheshimiwa Spika, napendekeza rasta zinazowekwa barabarani ziwe na viwango bila ya kusumbua magari.

Mheshimiwa Spika, Wizara iweke mkakati maalum wa kutengeneza magari ya Serikali kwani magari ya Serikali bado yanapelekwa gereji za nje.

Mheshimiwa Spika, naishauri Wizara kuwa na utaratibu au ratiba maalum ya kutembelea miradi ya

262 barabara ili kupata taarifa za uhakika kwani inavyoonekana Wizara inakosa taarifa sahihi.

MHE. CYNTHIA H. NGOYE: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa napenda kumpongeza Waziri wa ujenzi Mheshimiwa Daktari John Magufuli kwa kazi nzuri ya kuendeleza ujenzi wa barabara hapa nchini.

Mheshimiwa Spika, katika kuchangia hotuba hii naomba kueleweshwa juu ya barabara ya Katumba– Lwangwa–Mbambo–Tukuyu Wilayani Rungwe. Barabara hii ilitolewa ahadi na Mheshimwa Rais mwaka 2005 na mwaka 2010 kwamba ingejengwa kwa kiwango cha lami. Wananchi wa Wilaya ya Rungwe wanaishukuru Serikali kwa hatua yake ya kuifanyia feasibility study na detailed engineering design, hatua ambayo imejenga matumaini ya kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha 2011/2012, barabara hii ilitengewa fedha kiasi cha shilingi milioni 600 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa madaraja mawili ya Mito Mwalisi na Mbaka. Kwa masikitiko makubwa pamoja na kufanyika utaratibu wa kumpata Mkandarasi wa kutekeleza kazi hiyo, fedha hazikutolewa na kwa hiyo kazi haikufanyika. Baada ya kupitia mgao wa fedha za maendeleo kwa mwaka 20012/2013, hakuna fedha zozote zilizotengwa kwa ujenzi wa barabara hii.

Mheshimiwa Spika, ningependa kufahamu hatua ya mradi huu ambao tayari wananchi walianza kupata matumaini ni nini sasa? Nimepitia pia miradi

263 itakayotekelezwa kupitia Road Fund, mradi wa ujenzi wa barabara hii haumo, isipokuwa chini ya utengenezaji wa barabara za changarawe ambapo zimetolewa fedha kiasi cha shilingi milioni 170.9 tu, ambazo ni kidogo sana.

Mheshimiwa Spika, naomba ieleweke kwamba eneo hili la mradi lina mvua nyingi sana, kwa mwaka hupata si chini ya milimita 2,500-2800, jambo ambalo husababisha kuharibika sana kwa barabara na kutopitika. Ufafanuzi unahitajika sana kutoka kwa Waziri wakati atakapojibu hoja za Wabunge.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ambalo ningependa kulizungumzia ni juu ya utunzaji wa barabara zinazojengwa hapa nchini. Naomba kumshauri Mheshimiwa Waziri ashirikiane na Waziri wa mambo ya Ndani kupitia askari wa usalama barabarani, kuhakikisha madereva wote hapa nchini wanafuata alama rasmi za barabarani, badala ya kutumia matawi ya miti, magogo na kadhalika wanayoyatumia kama alama wanapoharibikiwa na magari, hasa katika barabara kuu za lami. Matawi hayo yanaachwa barabarani yaoze hapo, yachafue barabara na kuzifanya barabara ziwe na udhaifu mkubwa.

Mheshimiwa Spika, umefika wakati sasa, tuache tabia ya kujenga matuta katika barabara za lami na nyingine za Kimataifa ili kuzuia ajali badala ya alama rasmi zinazotambuliwa kisheria. Matuta kwa sehemu kubwa huleta ajali na hasa matuta hayo yanapokosa alama zinazoonesha kuna matuta. Tufuate alama

264 zinazotumika Kimataifa badala ya matuta na magogo ambayo hayakubaliki.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hotuba ya Waziri wa Ujenzi na namtakia utekelezaji mzuri wa hayo niliyoyazungumzia.

MHE. GOSBERT B. BLANDES: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Naipongeza Hotuba hii ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi. Pamoja na pongezi, ninayo machache ya kuboresha.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Barabara ya Kyaka - Bugene (km 59.1), unakwenda kwa spidi ndogo sana. Tatizo tunaambiwa ni uecheleweshwaji wa fedha za Mkandarasi. Je, Serikali imetenga fedha za kutosha kuhakikisha Barabara hii inaisha kwa wakati uliopangwa? Vile vile kuna upembuzi yakinifu (detail design) kwa ajili ya kipande cha barabara hii iliyobaki cha Bugene – Kasulo (Benaco). Ni matumaini ya Wananchi wa Jimbo la Karagwe na Ngara kuwa upembuzi yakinifu utakamilika mapema kabla ya Desemba 2012 ili zabuni ya barabara hii itangazwe na barabara ianze kujengwa na kisha ikamilike katika Mwaka wa Fedha wa 2013/2014.

Mheshimiwa Spika, Serikali imeahidi katika swali langu la msingi hapa Bungeni kuwa itaanza upembuzi yakinifu wa Barabara ya Gakoronga – Murongo katika Mwaka wa Fedha wa 2012/2013 na baada ya upembuzi yakinifu tunategemea kuona ujenzi wa barabara hii unaanza katika Mwaka wa Fedha wa 2012/13 na kumalizika 2013/14.

265

Mheshimiwa Spika, barabara hizi ni muhimu sana kwa Maendeleo ya Uchumi wa Taifa letu kama zilivyo barabara nyinginezo nchini, hivyo ni muhimu zikamilike mapema. Wasiwasi wangu ni ufinyu wa bajeti ya ujenzi inayoombwa, bajeti ni ndogo na wakati huo huo wakandarasi wengi hawajalipwa madeni ya nyuma. Naomba Serikali itafute fedha za kutosha kulipa madeni ya nyuma ili wakandarasi waendelee na kazi zao kwani wengine walishaondoka. Pia kwa kulipa madeni, Serikali itapona kulipa riba kubwa sana zinazotokana na madeni ya wakandarasi. Vilevile Serikali itafute fedha za kutosha kwa ajili ya kikamilisha miradi inayoendelea.

Mheshimiwa Spika, Bajeti ya Wizara ya Ujenzi inayoombwa not realistic haitekelezeki ni ndogo sana, nashauri Serikali iiangalie upya ije na fedha za kutosha.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja

MHE. FELIX F. MKOSAMALI: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Waziri, kwa uwasilishaji mwema wa Hotuba ya Wizara ya Ujenzi.

Je, Mheshimiwa Waziri anaikumbuka Barabara ya Nyakanazi – Kibondo – Kidahwe?

Namwomba Mheshimiwa Waziri, aikumbuke ahadi ya Rais ya Kibondo Mjini kwenye Road Fund.

MHE. MWIGULU L. N. MADELU: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, nampongeza Mheshimiwa John

266 Magufuli, Waziri wa Ujenzi, kwa jinsi anayoonesha ushupavu wa kuyamudu majukumu ya Wizara. Ni dhahiri na kila Mtanzania ni shahidi kuwa, ameyamudu majukumu na kuleta ufanisi mzuri wa Wizara kwa maisha ya Wananchi wa Tanzania.

Pili, nawapongeza kama Raia wa Tanzania kuwa kwa kuimarisha barabara wamesaidia kusawazisha bei za bidhaa zikiwemo za mazao ya kilimo. Pia naipongeza Serikali ya Awamu ya Nne kwa dhamira na utekelezaji mzuri wa Ilani kwa kujenga kilomita nyingi za lami kwa wakati kuliko kipindi chochote katika awamu zote tangu nchi ipate Uhuru.

Mheshimiwa Spika niende Barabara za Iramba; nianze kwa kukumbusha ahadi yake Mheshimiwa Waziri kuhusu kusaidia matengenezo ya barabara ya kutokea Shelui – Mtoa – Mtekente – Urughu. Wakati anajibu swali langu la nyongeza katika moja ya kikao hapa Bungeni, katika majibu yake aliahidi kuwa barabara hii itatengewa fedha katika Mwaka huu wa Fedha wa 2012/13. Kufuatia ahadi hii na kwa kuzingatia umuhimu wa barabara hii kiuchumi na mahitaji ya barabara, naomba Wizara yake itoe kipaumbele kwenye barabara hii. Mheshimiwa Spika, mwisho, naendelea kuiomba Wizara iangalie uwezekano wa uanzishwaji wa Mamlaka ya Kujenga na Ku-maintain Barabara Wilayani ili tuwe na barabara bora Wilayani kama zile za Mkoa zinazosimamiwa na Wakala wa Barabara (TANROADS).

267 Mheshimiwa Spika, nimtakie Mheshimiwa Waziri afya njema ili aendelee kuitumikia Tanzania. Ahsante sana na na kazi njema.

MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA: Mheshimiwa Spika, Bbarabara ya Mbeya – Chunya – Makongorosi, upembuzi yakinifu ulifanyika katika kipindi cha mwaka 2000 – 2005. Ilani ya Uchaguzi wa CCM ya Mwaka 2005 ilionesha kuwa, Babaraba hii ingejengwa kwa kiwango cha lami katika kipindi cha mwaka 2005 – 2010. Mkandarasi alipatikana na ujenzi ulianza rasmi mwaka 2007.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano alifungua ujenzi huo mwaka 2008, lakini mpaka mwaka 2010, hakukuwa hata na mita moja ya lami iliyokuwa imejengwa! Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya Mwaka 2010 nayo imeonesha kuwa Barabara hiyo itajengwa kwa kiwango cha lami katika kipindi cha mwaka 2010 – 2015; mpaka sasa hakuna hata mita moja ya lami ambayo imejengwa.

Mheshimiwa Spika, kuna barabara zingine ambazo ujenzi wake umeanza baada ya barabara hii nazo zinapewa fedha na ujenzi unaendelea. Wananchi wa Chunya wanaona kuwa labda wao ni raia daraja la pili wa nchi hii.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali iseme kama itaijenga barabara hii au haitajenga.

Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya vizuri sana kuanzisha consulting firm ya Serikali, yaani Wakala wa

268 Ujenzi wa Serikali (TBA). Pia Serikali imeijengea uwezo firm hii katika taaluma zifuatazo: Wasanifu/wabunifu majengo; wahandisi wa ujenzi; wahandisi wa umeme; wahandisi wa mitambo; wahandisi wa mazingira na maji; na wakadiriaji wa gharama za ujenzi.

Mheshimiwa Spika, baada ya Wakala huu kuwa na uwezo mkubwa katika nyanja hizi, naiomba Serikali itoe ufafanuzi katika yafuatayo:-

- Uwiano wa Miradi ya Ushauri ya Serikali waliyopewa Makampuni Binafsi na ile iliyopewa Wakala wa Ujenzi

- Ukubwa wa Miradi ya Ushauri wanayopewa Makampuni Binafsi na ile wanayopewa Wakala wa Ujenzi.

Mheshimiwa Spika, siungi mkono hoja.

MHE. MCH. LUCKSON N. MWANJALE: Mheshimiwa Spika, naomba nianze kutoa mchango wangu katika hoja hii, kwa kukushukuru wewe kwa kunipatia nafasi ili niweze kuchangia hoja ya Waziri wa Ujenzi. Sambamba na shukrani hizo, nampongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli - Waziri wa Ujenzi, Mheshimiwa Gerson H. Lwenge - Naibu Waziri wa Ujenzi, Katibu Mkuu wa Wizara na Wasaidizi wote wa Wizara, kwa kazi nzuri wanayoifanya.

269 Mheshimiwa Spika, baada ya pongezi hizo, mchango wangu utakuwa katika mambo au hoja kadhaa zifuatazo:-

Mheshimiwa Spika, nasikitika kuona Barabara ya Mbeya - Lwanjilo hadi Chunya imetelekezwa, mkandarasi hayuko kwenye site. Je, Mkataba wa kujenga barabara hii ya Mbeya – Chunya ulikuwaje? Nahitaji jibu kwa nini Barabara hii haijengwi.

Barabara ya Mbalizi – Mkwajuni Chunya ambayo imejengwa kwa lami kilometa nane tu; je, Serikali ina mpango gani wa kuikamilisha kwa kiwango cha lami hadi Mkwajuni?

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Isyonje – Makete inatengewa fedha kila mwaka kwa ajili ya kuikarabati lakini fedha hizo hazitoshi kutokana na kwamba, barabara hizo zipo kwenye ukanda ambao mvua inanyesha kwa muda mrefu kuliko maeneo mengine nchini. Hata hivyo, kwa vile barabara hii ndiyo inayounganisha Mkoa wa Njombe na Wilaya ya Makete, naiomba Serikali iijenge Barabara hiyo kwa lami ili kuepuka matengenezo ya mara kwa mara.

Mheshimiwa Spika, barabara ambayo mazingira yake ni sawa na hiyo iliyotajwa hapo juu ni Barabara ya Mbalizi hadi Iwiji na hatimaye Ileje. Kanda hii inakopita hii barabara kuna mvua nyingi. Mvua hunyesha kwa miezi mingi kuliko sehemu zingine za Mkoa na nchi kwa ujumla. Kwa hiyo, inahitajika kutenga bajeti kubwa zaidi. Barabara hata ikitengenezwa lakini huharibika haraka kwa sababu ya

270 mvua nyingi maana ni eneo lililo kanda ya juu kabisa kama ilivyokuwa Barabara ya Isyonje – Makete.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali itenge fedha nyingi kwa ajili ya Barabara za Vijijini.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru tena na naunga mkono hoja.

MHE. FAIDA MOHAMMED BAKARI: Mheshimiwa Spika, pamoja na kumpongeza Mheshimiwa Waziri kwa Hotuba yake inayoleta matumaini, napenda kumpongeza pia Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa ushirikiano wao na ufuatiliaji wa kazi vizuri. Naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia hoja kwa upande wa barabara.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali yangu inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi, kwa kutekeleza vyema Ilani yake ya Mwaka 2010 – 2015 kwa asilimia kubwa.

Mheshimiwa Spika, barabara ni nyenzo kubwa katika kuleta maendeleo ya nchi na ndiyo maana Serikali yetu inachukua uamuzi mzuri wa kutawanya barabara maeneo mengi ya nchi hii ili kuwarahisishia wananchi kusafirisha mazao mbalimbali pamoja na wananchi wake kwa madhumuni ya kuwakwamua kiuchumi.

271 Mheshimiwa Spika, napenda kuishauri Serikali wakati Wakandarasi wanajenga Miundombinu hiyo, wajenge kwa kiwango kinachoridhisha, kinyume chake watachukua fedha na kuwaacha wananchi wanapata shida.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali itoe elimu ya matumizi mazuri yahusuyo barabara kwa madhumuni ya kuzifanya barabara hizi ziendelee kuwa imara kwa muda mrefu.

Mheshimiwa Spika, nashauri barabara zinazojengwa zifanyiwe ukarabati wa mara kwa mara pale zinapoharibika.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

MHE. RICHARD M. NDASSA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii. Nampongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Watendaji wote walio chini ya Wizara, kwa utendaji uliotukuka. Nampongeza kwa dhati Mhandisi wa TANROAD Mkoa wa Mwanza, Ndugu Kadashi, kwa ufuatiliaji makini wa ujenzi wa barabara zilizo chini yake hasa pale ambapo wakandarasi hulipua kazi. Mfano, Barabara ya Bukwimba – Kadashi – Nyashana hadi Maligisu, ilitengenezwa chini ya kiwango, lakini kwa umakini wake alimwamuru Mkandarasi kurudia kazi naye akafanya hivyo.

Mheshimiwa Spika, naipongeza sana Serikali kwa kutenga pesa kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa

272 Daraja la Mto Simiyu (Maligisu). Daraja hili Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi analijua vizuri, tangu enzi akiwa Naibu Waziri wa Ujenzi na wakati huo Mhandisi Lwenge akiwa Meneja wa TANROAD Mkoa wa Mwanza, ambaye ndiye aliyeandika kwako gharama za ujenzi wa Daraja hilo. Nafurahi leo Naibu Waziri ni Mheshimiwa Lwenge, Waziri ni yeye mwenyewe Mheshimiwa Magufuli, naomba Daraja hili likamilike mwaka huu. Namwomba Mheshimiwa Waziri tukiwa hapa Bungeni, afanye ziara ya kwenda kuliona ili aone fedha zilizotolewa na Wizara yake na zinazoendelea kutolewa kama zinafanana na kazi inayofanyika.

Mheshimiwa Spika, lakini pia nimwombe mara kazi ya ujenzi wa daraja hili itakapomilika, amwombe Mheshimiwa Rais aje kulifungua rasmi; ni daraja kubwa na refu Kanda ya Ziwa (mita 105).

Mheshimiwa Spika, nawatakia kila la kheri, nawaomba Wahandisi wote nchini waende kusimamia vizuri Miradi yote iliyo chini ya maeneo yao.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. DKT. MARY M. NAGU: Mheshimiwa Spika, naomba nikupe pole nyingi kwa kufiwa na ndugu yako wa karibu, aliyemtunza marehemu mama yetu.

Mheshimiwa Spika, naomba nimwombe Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, apokee pongezi zetu za dhati kwa kazi nzuri hasa ya ujenzi wa barabara za lami.

273 Mheshimiwa Spika, naomba nimwombe apeleke wataalamu wake ili waweze kuona Barabara zinazofaa kupandishwa hadhi kuwa za Mkoa. Fedha zinazopita Halmshauri ni ndogo sana. Hata hivyo, Mkoa wetu ni mpya ukiacha mikoa iliyoundwa hivi karibuni, hivyo tunahitaji kuunganisha Wilaya zetu, Mkoa wetu na Mikoa mingine ya jirani kwa mfano Hanang na Iramba (Kiomboi – Mbulu – Meatu) ili kuunganisha Mkoa wa Manyara na Mkoa wa Shinyanga, Mkoa wa Mara na Manyara, Manyara na Tanga kupitia Handeni na kadhalika. Vile vile uwezo wa Halmashauri kubeba ujenzi wa barabara zinazohitajika ni mdogo.

Mheshimiwa Spika, tunaomba TANROADS wasaidie kujenga madaraja makubwa ya barabara za Wilaya kwani Halmashauri hazina uwezo wa kitaalam na kifedha.

Mheshimiwa Spika, TBA isaidie kujenga nyumba za Halmashauri kwa makubaliano maalum ili kuokoa fedha zilizotumiwa vibaya na Mkandarasi katika Sekta Binafsi.

Mheshimiwa Spika, nawashukuru na kumpongeza Meneja wetu wa TANROADS Mkoa Manyara.

MHE. DKT. KEBWE S. KEBWE: Mheshimiwa Spika, Barabara ya Makutano – Natta – Mto wa Mbu imetengewa fedha kidogo mno (shilingi bilioni 3.0); hii ni ya kazi gani? Tunaambiwa upembuzi yakinifu umefanywa mbona hatuoni wataalamu huko site ama upembuzi huo unafanyikia mezani au chumbani? Kasi

274 ni ndogo na fedha iliyotengwa ni kidogo mno kwa barabara ya kilomita 452.

Mheshimiwa Spika, fidia kwa walioguswa watalipwa lini na Shilingi ngapi? Kwa nini barabara ambazo tarehe 8 Machi 2011 mbazo Kikao cha RCC kiliidhinisha baada ya kupitiwa katika Kikao cha Bodi ya Barabara ya Mkoa tarehe 7 Machi 2011 kiliidhinisha? Je, Serikali ina mpango gani ili barabara hizo ikiwemo ya Majimoto – Nyansumra (Mto Mara) kilomita 36 na Manchimwena – Ring’wani kilomita nane hadi leo hii hatujui nini kinaendelea? Pia barabara hizo zinaishia katikakati (from somewhere to no where); ni vyema barabara hizo zifike maeneo yanayofika centre kubwa (mwisho wa barabara husika kuliko kuishia njiani).

Mheshimiwa Spika, je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara ya lami kutoka Musoma kwenda Mugumu kupitia Masurura - Kiagata – Sirori Simba ili kuinua uchumi na kuongeza utalii Wilayani Musoma Vijijini na Serengeti. Pia hii itarahisisha usafiri wa kutokea Kenya.

MHE. SAID J. NKUMBA: Mheshimiwa Spika, naomba nianze kwa kuunga mkono hoja. Aidha, naishukuru Serikali kwa kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara ya lami Sikonge – Tabora.

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Sikonge – Mibono – Kipiri ilikwisha pandishwa hadhi na kuwa Barabara ya Mkoa. Fedha zinazotengwa kutokana na eneo kubwa kuwa halijafunguliwa ni ndogo sana; hivyo, naiomba Serikali iangalie uwezekano wa kuifungua Barabara hii

275 ili iweze kurahisisha mawasiliano kwenye Wilaya ya Sikonge.

MHE. MCH. DKT. GERTRUDE P. RWAKATARE: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Wizara kwa bajeti nzuri inayokidhi. Hongera kwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Wasaidizi wote, kwa maandalizi mazuri ya Bajeti ya 2012/13.

Mheshimiwa Spika, natoa pongezi kwa Mheshimiwa Waziri, kwa umakini wake. Hongereni kwa maendeleo mengi hasa barabara na madaraja na hasa Daraja la Mto Kilombero.

Mheshimiwa Spika, kero ya wananchi wa Wilaya ya Kilombero ni Barabara ya Kidatu – Uchindile na Kidatu - Mahenge (Masagati) kwa kiwango cha lami. Ahadi za Rais zimetolewa awamu zote mbili 2005/2010 lakini mpaka leo hii barabara hizi bado za vumbi. Hii inakwamisha maendeleo na hata kuzuia wawekezaji kuja Kilombero. Barabara ni kila kitu katika maendeleo.

Mheshimiwa Spika, namwomba Mheshimiwa Waziri, kwenye mahitimisho awaambie Wananchi wa Kilombero Daraja la Kilombero litajengwa lini? Tuambiwe tarehe itakayoanza.

Je, ni lini Barabara ya Songea – Malinyi itafunguliwa? Madenaja - Fulua na Mwatisi imekwishakamilika.

276

MHE. AMINA ABDULLA AMOUR: Mheshimiwa Spika, Bajeti iliyopita ilishindwa kutekeleza zile barabara kutokana na pesa zilizopatikana kuwa kidogo mno. Barabara ambazo zilikuwa zinafadhiliwa na wafadhili angalau zimeweza kujengwa lakini zile za pesa za ndani zilishindwa kujengwa.

Mheshimiwa Spika, nimefurahishwa sana kuona Barabara ya Kilwa ambayo ilijengwa na Serikali ilikataa kuipokea kwa sababu ipo chini ya kiwango. Hivi sasa imeshaanza kujengwa tena, lakini naishauri Serikali hizi barabara zikianza tu kujengwa, Wakandarasi wa Serikali wazifuatilie kuliko huu mfumo wa sasa wa kungojea ikamilke halafu ndiyo igundulike kuwa ipo chini ya kiwango.

Mheshimiwa Spika, msongamano wa magari umekuwa mkubwa sana hasa katika Jiji la Dar es Salaam. Naishauri Serikali ijenge maeneo maalum ya kuegesha magari ambayo wananchi wataweka magari yao ili watakapoingia mjini wawe wanatembea bila magari, hii itapunguza msongamano wa magari.

Mheshimiwa Spika, tunashuhudia kila siku Serikali kuwa na migogoro na wananchi ambao wamejenga maeneo ya barabara. Hili nasema ni makosa ya Wizara ya Ujenzi; kwa nini hawawazuii wananchi hawa wanapoona wanaanza hayo majengo? Wizara inawaona na inawaachia wajenge na kukaa muda mrefu tu ndiyo wanataka wahame ili wajenge hiyo barabara. Naiomba Serikali ilione hili ilipatie ufumbuzi

277 Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali itekeleze ahadi zake na hii inaweza kutekelezwa pindi mkijipanga vizuri; ni bora mjielekeze kwenye barabara chache kuliko nyingi na baadaye mkashindwa kuzijenga. Nashauri Serikali ijielekeze sehemu ambazo zina mazao mengi.

Mheshimiwa Spika, majengo mengi tu makubwa yanaendelea kujengwa Dar es Salaam lakini mitaro ipo ile ile ya zamani; naiomba Serikali ilione hili na ijenge mitaro mipya. Mheshimiwa Waziri alisema wanatayarisha bandari ndogo tano kwa ajili ya usafiri wa bandari kutoka Dar es Salaam hadi Bagamoyo; je, hizo barabara tayari zilishatengenezwa; na je, haya maboti yatakuwa ya Serikali au ya binafsi?

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali imalize barabara zilizoanza kujengwa halafu ijielekeze kujenga barabara nyingine.

MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA: Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia kutoka maeneo yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, kumekuwepo na udhaifu mkubwa wa Wakandarasi wanaopewa tender za kujenga barabara au majengo makubwa. Wakandarasi hawa wamekuwa aidha hawakamilishi kazi zao kwa wakati kama walivyosaini kwenye mikataba au wanapokamilisha kazi yao inakuwa ni ya kiwango cha chini sana na baada ya muda mfupi barabara huharibika au jengo huanguka. Kwa nini Serikali inaingia mkataba na Wakandarasi hawa

278 ambao hulingizia Taifa hasara kubwa sana na kupoteza fedha za walipa kodi wa nchi hii? Mfano mzuri ni barabara ya kutoka Singida – Shelui katika maeneo ya Sekenke na kurudi nyuma, imeshaharibika vibaya na ni hivi juzi tu imekamilika. Serikali ilifanya jambo jema sana kutujengea barabara hii hasa kutoka Mwanza – Dar es Salaam lakini dosari hizi zinaondoa nia njema ya Serikali ya kurahisishia wananchi wake usafiri. Naomba Serikali iwachukulie hatua kali wakandarasi hawa wanaorudisha maendeleo nyuma.

Mheshimiwa Spika, mfano mwingine ni rehabilitation ya Barabara ya Sindiga – Mwankonko – Ighombwe – Mgungira – Iyumbu – Msusa (Mkoa wa Sindia), ujenzi wake unasikitisha maana upo chini ya kiwango sana. Hivyo, naiomba Wizara ifanye juhudi za makusudi kufanya ziara ili kuitembelea barabara hii. Naomba Makao Makuu ya TANROADS watume mtu wao na si kumwamini Meneja wa TANROADS wa Mkoa wa Singida maana anaonekana hatimizi majukumu yake sawasawa.

Mheshimiwa Spika, pamoja na nia njema ya Serikali kuona umuhimu wa kuwajengea watumishi nyumba za kuishi kwa bei nafuu, nyumba hizi zimekuwa zikitumika kinyume na makusudi yake. Mfano mzuri ni nyumba zilizoko Dodoma, ambazo kwa kiwango kikubwa zimewasaidia sana Waheshimiwa Wabunge kuishi kwa amani hapa Dodoma wanapokuwa katika shughuli za Bunge. Masikitiko makubwa, nyumba hizi zimefanywa ni za urithi au zimegeuzwa za biashara pindi mtumishi anapohama au Mbunge anapokuwa Mbunge, nyumba hizi badala ya kurudishwa TBA ili

279 ziwanufaishe watumishi wengine wahusika, wapangaji waliohama wanazitumia kama kitega uchumi kwa kupangisha watu wengine au kuwarithisha ndugu zao! Kwa nini TBA haifanyi uhakiki kuzikagua nyumba hizi na kuwasaidia watu wengine wenye shida hususan Wabunge ambao wamekuwa wakipata shida sana ya vyumba wawapo Dodoma kwenye shughuli za Bunge? Hii inapelekea Wabunge kupanga nyumba mitaani kwa watu binafsi kuanzia Sh. 400,000 hadi 600,000 kwa mwezi, kitu ambacho ni ghali sana.

Mheshimiwa Spika, tumekuwa tukizungumzia nyumba za Serikali zilizouzwa kila mara na naendelea kusisitiza kwamba, Serikali irudishe nyumba zilizouzwa hasa kwa Watendaji Wakuu, mfano; Majaji, Mawaziri, Makatibu Wakuu na kadhalika, ambao hupata tabu kubwa ya kukaa hotelini pindi wanapopewa nyadhifa hizi. Matokeo yake, Serikali inaingia gharama kubwa sana ya kulipia hoteli wakati ilikuwa na nyumba zake kwa ajili ya Wakuu hawa. Serikali ifanye maamuzi magumu ya kuzirudisha nyumba hizi na hata zile ambazo ziliuzwa kihalali, walionunua walazimishwe kumalizia madeni yao, kwa wale ambao bado hawajamaliza; la sivyo, sheria ichukue mkondo wake au wanyang’anywe na wauziwe watu wengine wenye nia ya kuzinunua na kuzilipia kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia kwenye eneo la ushirikishwaji wa wanawake katika kazi za barabara.

280 Mheshimiwa Spika, katika Hotuba ya Mheshimiwa Waziri amesema, Wizara iliendelea kuhamasisha wanawake kushiriki katika kazi za ujenzi na matengenezo ya barabara. Hofu yangu kwa hili, inawezekana wanawake wengi katika ujenzi wa barabara huenda wameongezeka kwenye ubebaji wa zege badala ya kuongezeka kwenye kazi za usimamizi.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa Hotuba ya Mheshimiwa Waziri imeainisha kuwa idadi ya kampuni za makandarasi wa barabara zinazomilikiwa na wanawake imeongezeka kwa asilimia tu ni dhahiri kwamba, Serikali inahitaji kuongeza nguvu zaidi katika kuwajengea uwezo wanawake kuliko ilivyo sasa kwa kuainisha utaratibu madhubuti utakaosaidia kuongeza idadi ya kampuni za makandarasi zinazomilikiwa na wanawake.

Mheshimiwa Spika, kuna sheria nyingi zilizopitishwa nchini ili kulinda haki za wanawake, lakini kwa bahati mbaya hazifanyiwi kazi ipasavyo na matokeo yake wanawake wanaendelea kukosa haki zao nyingi ikiwemo haki ya kushika nyadhifa za juu kwenye Idara mbalimbali ikiwemo Ujenzi.

Mheshimiwa Spika, kitendo cha kuwa na sheria za kumpa haki zake mwanamke bila utekelezaji ni sawa na kumwandikia mtu cheki ukijua kabisa akaunti yako haina pesa.

Mheshimiwa Spika, naishauri Wizara ya Ujenzi itilie mkazo uwiano kati ya wanaume na wanawake ili wale

281 wanawake wanaostahili nafasi za ngazi za juu wapatiwe haki yao kulingana na uwezo wao.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

MHE. DUNSTAN D. MKAPA: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, ninaunga mkono hoja hii ya Hotuba ya Makadirio ya mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka 2012/2013. Ningependa kuchukua fursa hii, kuipongeza Serikali kwa kuanza ujenzi wa Daraja la Mto Nangoo Wilayani Masasi.

Mheshimiwa Spika, aidha, napenda kuipongeza Serikali kwa juhudi zake za kutaka kujenga barabara ya kutoka Mtambaswala – Mangaka hadi Tunduru. Ujenzi ambao unatarajiwa kuanza hivi karibuni.

Mheshimiwa Spika, pamoja na pongezi hizi, ninapenda kuchangia kama ifuatavyo:-

Wakati wa Kampeni kuelekea Uchaguzi Mkuu wa Mwaka 2010, Mheshimiwa Rais aliahidi ujenzi wa barabara ya kutoka Nangomba hadi Nanyumbu. Hivyo, ninaomba Wizara inipe majibu ni lini barabara hii itaanza kujengwa kwa kiwango cha lami ili kutimiza ahadi hii ya Mheshimiwa Rais. Aidha, ninaomba wakati wa majumuisho Waziri awaarifu wananchi waliowekewa alama za X kwenye nyumba zao ni lini watalipwa fidia ili waweze kuhamia maeneo mengine kupisha ujenzi wa barabara hizo.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa daraja juu ya Mto Lukwamba pale Mpombe katika Kata ya Napacho

282 umekuwa ni kizungumkuti. Daraja hili limekuwa likiahidiwa kujengwa kila mwaka kwa fedha. Pamoja na kwamba, daraja hili limekuwa likitengewa fedha, lakini fedha imekuwa haipelekwi. Mwaka wa Fedha wa 2010/11 zilitengwa Sh. 120 milioni na mwaka 2011/12 Wizara ilitenga Sh. 80 milioni lakini nazo hazikupelekwa. Wananchi wanateseka sana wakati wa masika na kuwakata kabisa na mengine Wilayani Nanyumbu. Ninaiomba Wizara na hasa Waziri anipe majibu ni lini daraja hili litaanza kujengwa ili kutatua kero inayowakabili Wananchi wa Mpombe na wa maeneo mengine Wilayani Nanyumbu.

Mheshimiwa Spika, ninaunga mkono hoja hii.

MHE. HEZEKIA N. CHIBULUNJE: Mheshimiwa Spika, kwanza, napenda niipongeze kazi nzuri sana zinazofanywa na Wizara. Nawapongeza sana Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na Watendaji Wakuu wote wa Wizara, kwa kufanya kazi kwa ushirikiano mkubwa.

Mheshimiwa Spika, Wananchi wa Mkoa wa Dodoma, tunatoa shukrani nyingi kwa Serikali, hatimaye kutatua tatizo la ujenzi wa barabara kuu ya kutoka Iringa – Dodoma – Babati. Tumefarijika sana kuona kwenye bajeti ya mwaka huu wa fedha, kipande cha barabara ya kutoka Mayamaya – Bonga nacho sasa kimepatiwa fedha kutoka ADB/JICA.

Mheshimiwa Spika, ombi letu ni kuihimiza Serikali isimamie ujenzi huo uende haraka. Tunaomba tujue ujenzi wa kipande hicho cha barabara kutoka

283 Mayamaya hadi Bonga utaanza lini? Wananchi wa eneo hili wangependa kusikia tamko la Serikali ni lini ujenzi wa barabara hiyo utaanza?

Mheshimiwa Spika, katika kupitia majukumu ya msingi ya Kitengo cha TBA, imedhihirika wazi kuwa kazi za Kitengo hiki ni muhimu sana katika kukabiliana na matatizo ya nyumba za kuishi Watumishi wa Serikali na Majengo ya Ofisi za Serikali.

Mheshimiwa Spika, wakati wa kupitia Taarifa za Ukaguzi wa CAG, Kamati ya Hesabu za Serikali (PAC) ilibaini kwamba, majengo mengi ya Serikali hayana Title Deeds inayoonesha mmiliki rasmi wa majengo hayo na viwanja mbalimbali vinavyomilikiwa na Serikali.

Mheshimiwa Spika, kwa vile TBA ndiyo Kitengo cha Serikali kinachosimamia majengo hayo, Serikali iangalie uwezekano wa kukipa Kitengo hiki mamlaka ya kumiliki Majengo ya Serikali na hivyo kiwe na wajibu wa kufuatilia upatikanaji wa Title Deeds za majengo ya Serikali.

Jambo hili ni vyema likaangaliwa kwa uzito wake na hasa ukizingatia ya kwamba, hivi sasa majengo yote yanayojengwa kwa fedha za Serikali yakiwemo na yale yaliyoko nje ya nchi kwenye Balozi zetu mbalimbali; Kamati ya PAC ilione kuwa Wizara ya Serikali inayoweza kulisimamia suala hili ni Wizara ya Ujenzi kupitia TBA.

Mheshimiwa Spika, nawapongeza sana kwa kazi nzuri.

284

MHE. CHARLES M. KITWANGA: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, nawapongeza Wizara ya Ujenzi, kwa kazi nzuri wanayoifanya. Hiki ni kielelezo kizuri katika utekelezaji wa Mpango wa Maendeleo kuelekea 2025. Vile vile naishukuru Wizara kwa kuitengea pesa za matengenezo barabara iendayo Ihelele kwenye Mradi wa Maji (Lake Victoria – Kahama – Shinyanga – Nzega – Igunga na Tabora). Naomba Wizara vile vile iangalie barabara hii iweze kupandishwa Daraja kwani magari yapitayo katika barabara hii hupita uzito wa tani 40 badala ya tani 12 zilizoainishwa. Vile vile ifahamike kwamba, barabara hii inaunganisha Mkoa wa Shinyanga na Geita. Hii inaonesha ni kwa kiasi gani barabara hii inastahili kupandishwa.

Mheshimiwa Spika, namwomba Waziri tutembelee kwa pamoja ili kujionea hali halisi.

Mheshimiwa Spika, natambua utendaji mzuri wa Wizara hii na inaamini suala hili litashughulikiwa kwa haraka na umuhimu unaostahili.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja na moja.

MHE. RASHIDI ALI ABDALLAH: Mheshimiwa Spika, kwanza, sina budi kumshukuru Mwenyezi Mungu, kwa kuniwezesha kuchangia kwa maandishi leo hii. Pia sina budi kumshukuru Mheshimiwa Waziri, kwa kuwasilisha vizuri Hotuba yake.

285 Mheshimiwa Spika, kazi iliyofanywa na Wizara ya Ujenzi ni nzuri kwa kiasi Fulani, lakini msisitizo wangu mkubwa kwa Mheshimiwa Waziri ni kusimamia viwango vya barabara. Mheshimiwa Waziri kama hatakuwa makini katika usimamizi wa kuangalia viwango katika barabara zetu, basi maendeleo ya Tanzania kiuchumi yatakwama huko mbele.

Mheshimiwa Spika, katika kutilia mkazo hoja yangu, nimeangalia barabara inayotoka Dar es Salaam – Morogoro, barabara hii tayari imeanza kuweka mashimo au matuta, yaani barabara imedidimia chini na kwa maana hiyo kunahitajika fedha nyingine nyingi kuifanyia matengenezo.

Mheshimiwa Spika, Serikali haina uwezo kujenga barabara zote, lakini pale Serikali inapopata fedha za kujenga barabara, madaraja na fly over, lazima kuwe na umakini juu ya kusimamia viwango vya ujenzi huo.

Mheshimiwa Spika, naamini kazi hii inaganywa. Nasisitiza zaidi, kwani likifanyika kosa la kutoangalia viwango, juhudi zote za Serikali zitakuwa zimegonga mwamba; kwa maana hiyo basi lazima Mheshimiwa Waziri avalie njuga swala hili bila kuchoka.

Mheshimiwa Spika, nakutakia kila la kheri. Naomba kuwasilisha.

MHE. HENRY D. SHEKIFU: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja na kuipongeza Wizara kwa kufanya kazi yake vizuri, pamoja na changamoto

286 kubwa ya uhaba wa fedha za utekelezaji Miradi kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, Serikali ijitahidi kuheshimu kauli zake kwa kupeleka fedha kwenye Miradi iliyokusudiwa na kama ilivyoainishwa na Bunge.

Mheshimiwa Spika, Miradi yote inayoendelea ikamilishwe kabla ya kutenga fedha za Miradi mipya isipokuwa Miradi ya Usanifu iendelee ili inayotekelezwa ikikamilika, basi iwepo mipya ya kuanzishwa bila kusubiri usanifu.

Mheshimiwa Spika, kwa vipindi mbalimbali nimeomba Wizara ikubali kupandisha daraja barabara katika Wilaya ya Lushoto ambayo huhudumia Majimbo yote matatu ya Mlalo, Lushoto na Bumbuli. Barabara hiyo inatoka Mlalo – Ngwelo – Mlola – Makanya – Milingano hadi Mashewa, Wilaya ya Korogogwe. Barabara hii imetimiza vigezo vyote vya kupandishwa daraja. Naomba Wizara isikie vilio vya Wabunge wote watatu wa Wilaya ya Lushoto. Barabara hiyo imekwisha pendekezwa na Mkoa kwenda Wizarani ili iwe ya Mkoa.

Mheshimiwa Spika, barabara kujengwa kwa kiwango cha lami Lushoto – Kwenda – Magamba – Coast, kilomita kumi imechukua miaka kumi na imekamilika kilomita kiasi cha tatu hadi nne tu. Kwa nini Serikali haitengi fedha za kutosha kukamilisha barabara hiyo hizo kilomota saba zilizobakia? Ni gharama sana kujenga barabara kilomita kumi kwa

287 miaka 15. Busara hazitumiki; hivyo, naomba Wizara izingatie ombi hili.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Wizara kwa utendaji wa kutia moyo sana; mmethubutu, mmeweza, songeni mbele.

MHE. LUHAGA J. MPINA: Mheshimiwa Spika, kwanza, nampongeza Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, kwa jinsi anavyotekeleza majukumu yake, ufuatiliaji na usimamizi wake umemjengea heshima kubwa kwa Watanzania; Mungu ambariki.

Je, ni lini Serikali itapandisha hadhi Barabara ya Simiyu Darajani – Mwandoya – Nghoboko JC?

Je, ni lini Serikali itafanya upembuzi yakinifu na kuanza ujenzi wa Barabara ya Bariadi – Kisesa (Mwandoya) – Mwanhuzi – Karatu – Arusha kwa kiwango cha lami? Barabara hii ni muhimu sana kwa ukuaji wa Uchumi wa Taifa.

Mheshimiwa Spika, kutokana na upembuzi yakinifu uliofanywa na katika Daraja la Mto Sibiti, kiasi cha shilingi bilioni 2.5 zilizotengwa zitawezesha ujenzi kumalizika katika Mwaka huu wa Fedha wa 2012/2013.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa ni zaidi ya miaka mitano iliyopita fedha zimekuwa zikitengwa kujenga Barabara ya Mmigumbi – Maswa – Bariadi kwa kiwango cha lami lakini hakuna kinachoendela hadi sasa. Je, kuna uhakika gani kuwa ujenzi utaanza mwaka huu wa fedha?

288

Je, kiasi kilichotengwa cha shilingi bilioni 1.5 kitatumia kugharamia shughuli zipi mwaka huu wa fedha?

Mheshimiwa Spika, pia naishukuru Serikali kwa kukubali kuanza ujenzi wa Daraja la Mto Lubiga, kazi za usanifu na kuanza ujenzi. Ahsante sana.

MHE. PROF. JUMANNE A. MAGHEMBE: Mheshimiwa Spika, napenda nimpongeze sana Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Waziri wa Ujenzi, kwa hotuba nzuri na uwasilishaji mzuri sana. Napenda pia nimpongeze Mheshimiwa Eng. Gerson Lwenge na Balozi Herbert Mrango, kwa kazi nzuri na utekelezaji uliotukuka.

Mheshimiwa Spika, kazi ya ujenzi wa barabara nchini imefanikiwa sana na barabara lukuki zinajengwa katika kila Wilaya na Mkoa wa nchi hii. Tunamshukuru sana Mheshimiwa Rais wetu Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, kwa uamuzi huu wa kihistoria.

Mheshimiwa Spika, tumefurahishwa sana na uamuzi wa Mheshimiwa Dkt. John Magufuli, kwa kukubali kuangalia Sheria ya Barabara ili Hifadhi ya Barabara (Road Reserve) katika maeneo ya Milimani kama Milima ya Upare Kaskazini, Wilaya ya Mwanga, iwe fupi. Sisi tunapendekeza mita 7.5 kutoka katikati ya Barabara mpaka kila upande wa barabara, yaani span ya meta 15 (7.5 metres from the middle of the road to the end of each side of the road reserve).

289 Mheshimiwa Spika, barabara zetu za Wilaya ya Mwanga zilizo barabara za Mkoa ni chache lakini barabara hizi ni za milimani; hivyo matengenezo yake ya kila mwaka ni ya ghali na Halimashauri yetu haiwezi kuzihudumia vizuri. Tunaomba Wizara katika mwaka 2012/13 ichukue hatua zifuatazo:-

(i) Iongeze fedha katika utengenezaji wa Barabara ya Mwanga – Kikweni kufikia Otta Seal Standard ili barabara hii ikamilike.

(ii) Barabara ya Kifaru – Kigonigoni – Kwakoa – Kichwa cha Ng’ombe (70km) ifanyiwe matengenezo makubwa. Kwa miaka 12 sasa imefanyiwa spot maintenance pekee.

(iii) Barabara ya Mwanga Mjini – Kagongo katika Nyumba ya Mungu ipandishwe daraja kama Mheshimiwa Waziri alivyoahidi Wananchi wa Nyumba ya Mungu alipowatembelea alipokuwa anaongoza Sekta ya Mifugo na Uvuvi.

(iv) Barabara ya Lembeni – Kilomeni – Ndorwe – Lomwe ipandishwe daraja kuwa Barabara ya Mkoa. Nia ni kufungua eneo la Kilomeni, Sofe, Mlevo na Ndorwe na kuwapatia wakulima masoko ya mazao yao.

Mheshimiwa Spika, naomba kuunga mkono hoja.

MHE. HENRY D. SHEKIFU: Mheshimiwa Spika, kule Lushoto tunayo barabara aliyoibuni yeye Waziri mwaka 2004; Lushoto – Magamba. Mimi naiita barabara ile

290 Mkapa Road maana inaelekea kwenye Makazi ya Rais Mstaafu. Kwa nini Serikali haimalizii hizo kilomita tano zilizobaki?

Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Waziri aliangalie suala hili kwa uzito wa kuwaenzi Viongozi Wastaafu. Ahsante.

MHE. DESDERIUS JOHN MIPATA: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Waziri, kwa kazi zake nzuri sana; hakika ana-deserve heshima ya Serikali yetu ya CCM. Mungu amtangulie.

Mheshimiwa Spika, naomba niokolewe au nisaidiwe; zipo barabara mbili za Halmashauri za Nkana – Kala (km 67), Kitosi – Wampembe (km 68), ziliombewa na Mkoa zipandishwe hadhi. Kamati ilikuja na kuona umuhimu huo na tukabaki na matarajio lakini hazina kitu. Mwaka jana nilimwona Mheshimiwa Waziri akaniahidi kuziombea ombi maalum tulifanya hata hatukufanikiwa. Mkuu wa Mkoa wa Rukwa na mimi Mbunge tulimwandikia aone namna ya kutusaidia barabara hizi zilizokwisha shindikana kwa Halmashari ya Wilaya mpaka sasa hazijafanikiwa chochote japo ni ahadi pia ya Rais, lakini changamoto zinazowakumba wananchi ni kubwa. Hali ni baya sana!

Mheshimiwa Spika, nilipotembelea Machi 2012 nililala siku mbili na nilikuwa na Mbunge mwenzangu wa Viti Maalum, Mheshimiwa Abia Nyakabari.

Mheshimiwa Spika, naomba Serikali inisaidie.

291 MHE. BENEDICT N. OLE-NANGORO: Mheshimiwa Spika, naanza kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri, Katibu Mkuu na Wataalamu, kwa kuandaa Hotuba nzuri sana.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa barabara una tofauti kubwa sana katika usanifu, ujenzi na maintenance. Barabara za hadhi sawa hazipo sawa katika upana, mwinuko, mitaro ya kutoa maji na ushindiliaji wa moram na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, barabara zote zifuate standards na specifications husika. Regulations zikazaniwe na zisimamiwe na kufuatwa.

Mheshimiwa Spika, Serikali ifanye maandalizi ya ujenzi wa Barabara ya Narco Kongwa, Kibaya Orkesumet hadi Oljoro Mbauda kwa kiwango cha lami. Barabara hii ni muhimu sana kwa uchumi wa mifugo na mahindi yatokayo Kiteto, Simanjiro na Arusha.

Mheshimiwa Spika, Mipango ya over fly za kujengwa Dar es Salaam ianze mara moja ili kuondoa tatizo la msongamano wa magari jijini.

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Iringa - Dodoma hadi Babati iwekwe kwenye mikakati ya barabara za kukamilishwa kwa kipindi kifupi ili iunge Kusini na Kaskazini mwa nchi na kuchangamsha uzalishaji.

MHE. PROF. PETER M. MSOLLA: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napenda kumpongeza Mheshimiwa

292 Waziri, Naibu Waziri na Katibu Mkuu, kwa kuwasilisha Bajeti yao vizuri.

Mheshimiwa Spika, aidha, napenda kushauri kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, nyumba ambazo zimewekewa alama na Hifadhi ya barabara imezifuata, Serikali ifanye kila linalowezekana ili wahusika walipwe fidia wakatafute maeneo mengine ya ujenzi kuliko kuendelea kuaacha wananchi husika wanaishi kwa wasiwasi.

Mheshimiwa Spika, Barabara ya TANZAM (Tanzania – Zambia) ni muhimu sana kwa Uchumi wa Tanzania na Nchi za Afrika ya Kusini na hususan wakati huu ambapo Reli ya TAZARA haifanyi kazi vizuri. Eneo moja ambalo ni muhimu sana katika barabara hii ni Mlima wa Kitonga, ambayo kama barabara katika eneo hili itakatika, mizigo itokayo Dar es Salaam kwenda Nchi za Kusini au kinyume chake, itakwama na kuathiri uchumi wake. Hivyo, kwa eneo hili ambalo ni sehemu ya Kilolo ni vyema Serikali iangalie njia mbadala ya kufika Dar es Salaam na Nchi za Kusini ambayo ni rahisi.

Mheshimiwa Spika, hali ya usafiri Dar es Salaam siyo ya kuridhisha hata kidogo na kufanya uendeshaji wa Serikali kuwa wa gharama sana. Serikali iangalie kwa makini namna ya kutatua tatizo hili.

Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha.

293 MHE. SELEMANI S. JAFO: Mheshimiwa Spika, naipongeza Serikali kwa kuleta Bajeti yenye matumaini makubwa kwa Watanzania.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali iangalie uwezekano wa kuanza ujenzi kwa kiwango cha lami kwa Barabara ya Kisarawe - Maneromango (km 54), ambayo imeainishwa katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Wizara kwa kazi kubwa inayofanya ambapo mtandao wa Barabara Tanzania ni wa kupigiwa mfano. Naomba juhudi na kasi hii iendelee zaidi.

Mheshimiwa Spika, nimepitia Kitabu chote cha Hotuba sikuweza kuona kiwango hata cha kilomita moja cha ujenzi wa barabara ya lami kwa Barabara ya Kisarawe – Maneromango (54). Nimekuwa mnyonge sana kwani sijui nitawaeleza nini wale wananchi kwa mwaka huu. Ningepata hata kilomita mbili za kuanzia ningekuwa na nafasi ya kupumua.

Mheshimiwa Spika, kipindi cha mwezi wa kumi mwaka 2011, alikuja Jimboni kwangu Mheshimiwa Dkt. Slaa, akatukana sana kwamba Majimbo ya CCM hayana maendeleo ila Majimbo ya Wapinzani ndiyo maendeleo yanapatikana. Akasema ahadi waliyopewa Wananchi wa Kisarawe ya ujenzi wa barabara ya lami ya kilomita 54 kutoka Kisarawe hadi Maneromango ni kiini macho cha CCM. Alisema wakitaka kujua hilo, waende Kilimanjaro waone jinsi Majimbo ya Wapinzani yanavyotengewa fedha nyingi kwa barabara za lami.

294

Mheshimiwa Spika, bahati mbaya zaidi, mwaka huu akina Mheshimiwa Mbowe tumewaongezea kiburi cha kututukana tena Wazaramo kwani wametengewa fedha za kutosha katika ujenzi wa barabara za lami.

Mheshimiwa Spika, namwomba sana Mheshimiwa Waziri, mtani wangu, aniokoe na aibu hii japo ile Barabara ya Kisarawe – Maneromango nipate angalau kilomita mbili za kuanzia mwaka huu ili isije ikaonekana kwamba waliyoyasema CHADEMA walipokuja Kisarawe ni mambo ya kweli.

Mheshimiwa Spika, namwomba sana mkubwa wangu anisitiri kwa aibu hii. Ahsante.

Mheshimimwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. RUKIA KASSIM AHMED: Mheshimiwa Spika, kwanza, napenda niipongeze Wizara hii kwa kazi nzuri wanayoifanya. Nchi yetu kwa kiasi kikubwa barabara nyingi zimetengenezwa kwa kiwango cha lami na baadhi yake kwa kiwango cha changarawe.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kuna baadhi ya watu huiba na kuharibu alama hizi za barabarani na kusababisha uharibifu mkubwa na wakati mwingine kusababisha ajali; naishauri Serikali alama hizi ziwekwe kwa kutumia saruji na nondo ili waharibifu hawa wanaotoa yale mabati na kwenda kutengeneza mikungu, maseredani na matumizi mengine, basi washindwe kuzichukua. Pia itungwe Sheria ya kuwadhibiti waharibifu hawa na pia tuzinusuru

295 barabara zetu ambazo zimegharimu fedha nyingi na kwa usalama wa watumiaji wa barabara zetu.

Mheshimiwa Spika, mara nyingi wananchi wengi wanaathirika sana wakati wa bomoabomoa inayofanywa kupisha ujenzi wa barabara. Hivyo basi, naishauri Serikali kabla ya kufanya bomoabomoa, wananchi walioathirika na ujenzi huu walipwe. Pia wapewe ardhi maeneo mengine na iwe imepimwa ili kuepusha bomoabomoa nyingine. Hali ya kutokuwalipa mapema wananchi hawa wanaopisha ujenzi wa barabara inawafanya wananchi hawa washindwe kujenga kutokana na gharama za maisha kupanda. Matokeo yake ni kuwafanya wananchi hawa waishi maisha ya kutangatanga ndani ya nchi yao.

MHE. ABIA M. NYABAKARI: Mheshimiwa Spika, naomba Serikali ielewe kuwa kuna Watanzania wengi wanaoishi shimoni au kuzimuni, ambao wananchi hao ni Kana – Kala na Kitosi – Wampembe, wamekata tamaa na Serikali yao. Barabara hizo mbili zina urefu wa km 135, ambazo Halmashauri siyo rahisi kuzitengeneza na wananchi kuendelea kukosa huduma za kijamii hasa wakati wa masika.

Mheshimiwa Spika, tumekuwa tukipiga kelele hapa Bungeni juu ya barabara hizo bila mafanikio na Wapambe wa CHADEMA siku tuliyofika Kata ya Kala walituzomea kama Viongozi tusioleta maendeleo na kidogo tushughulikiwe kwani tulizuiliwa kwa zaidi ya saa tatu na mawe makubwa ili tusipite. Katika njia ya Kana – Kala tulikuta magari matano yakiwa yamekwama na

296 sisi wenyewe tulikwama kwa muda wa siku mbili, tulikuwa na gari mpya la Mheshimiwa Mipata, lilizama mpaka usawa wa milango hata kutoka ndani ya gari ilikuwa shida.

Mheshimiwa Spika, baada ya kukwamuliwa, kwani tulitoa fedha ili likwamuliwe, baada ya zoezi hilo gari jipya la Mheshimiwa Mipata, bodi lilionekana kuchoka sana kwani ilichanika na kubonyea ovyo. Si hivyo tu, tulipotoka pale tulikuta gari kubwa limezama, wao hawakujali Uongozi wetu, walichimba barabara kwa jembe na kushusha mahindi na kuyatandaza barabarani na mapipa ya mafuta ili tusipite, tulipata matusi ya Chama cha Mapinduzi na kutulazimisha kuwa wapole mpaka tulipopita porini hapo tukawa tumeokoka.

Mheshimiwa Spika, Serikali hii tunaiomba barabara hizi izipokee na Wakala TANROADS ili wenzetu nao waweze kuishi kama Watanzania katika nchi yao.

Mheshimiwa Spika, tunaiomba Serikali itengeneze Barabara ya Kasesya kwani itakuwa ukombozi kwa Wanarukwa, pia itawaweka huru hata wafanyakazi wenzetu walioko porini ambao ni Uhamiaji, TRA, Polisi, Forodha, Mifugo na Afya.

Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tuna Waziri mchapakazi, Mheshimiwa John Pombe Magufuli, Watu wa Rukwa tuna imani naye kwamba ataishauri Serikali ipokee barabara hizo za Kitosi – Wampembe na Kana – Kala, pamoja na ujenzi wa Matai – Kasesya kabla hajamaliza muda wake wa Uwaziri. Wanarukwa

297 tunaiombea Wizara hii ya Ujenzi kuwa na moyo wa kuikwamua Rukwa kimaendeleo kwani katika Mikoa yote ya Tanzania tuko namba mbili toka chini. Mheshimiwa Spika, naomba Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi katika hitimisho lake atupatie majibu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. ALIKO N. KIBONA: Mheshimiwa Spika, natoa pongezi nyingi kwa Waziri, Naibu Waziri na Watendaji wote, kwa kazi nzuri hasa kwa kusimamia ujenzi wa barabara za lami katika nchi yetu.

Mheshimiwa Spika, maoni yangu ni kuwa, Miradi iliyo kwenye mpango wa ujenzi wa kiwango cha lami kama kupandishwa hadhi kutoka barabara ya kawaida kuwa Otta Seal au Bituman Standard ielezwe na Waziri nini kitafanyika ili wananchi wapate nafasi ya kujua ni kitu gani kitafanyika katika mwaka huu wa fedha.

Mheshimiwa Barabara za Jiji la Dar es Salaam zikiwa nzuri zitawavutia watu wengi watapenda kuendelea kuwekeza katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, athari zake kutakuwa na mrundikano mkubwa wa watu na magari katikati ya Jiji la Dar es Salaam.

Ninashauri badala ya kujenga barabara za kuvutia watu kuwekeza Dar es Salaam, Serikali ijenge barabara na miundombinu itakayowavutia wawekezaji kwenda

298 nje ya Dar es Salaam. Kwa sababu Dar es Salaam hapatakuwa na parkings kwa magari.

Mheshimiwa Spika, barabara za pembezoni ni pamoja na zile za Wilaya ya Ileje. Barabara ya kutoka Mpemba hadi Kasumulo Kyela, ilijengwa miaka ya 70 wakati wa msuguano kati ya Tanzania na Malawi, technology ya wakati ule ilikuwa ya chini kwa kuwa ni miaka takriban 40 barabara hii hasa kutoka Isongole hadi Kaomulu Kyela. Barabara ni nyembamba, kona kali na ambazo hazilingani na ukubwa wa magari ya hivi sasa kama Fuso na mengine, ambayo miaka ya 70 hayakuwepo. Je, Wizara inaweza kuweka katika mpango wa kupitia upya ramani ya barabara hizi ili ipitike kirahisi badala ya ilivyo sasa ambapo mabasi yanashindwa kukata baadhi ya kona?

Mheshimiwa Spika, uharibifu wa barabara unafanywa na magari makubwa ya ndani na ya kutoka au kwenda nje ya nchi. Magari yanabeba mafuta, shaba, nondo, mabati na vitu vingine vizito. Yapo malalamiko kuwa magari hayo ni ya vigogo ambao Serikali inawaogopa na kuacha waendelee kuliletea Taifa hasara.

Mheshimiwa Spika, ushauri wangu ni kuwa, kauli itolewe kama ilivyokuwa kwa udhibiti wa vitendo vingine viovu. Suala hili linaleta sifa mbaya kwa Taifa.

Mheshimiwa Spika, barabara ya kutoka Kasumulo Kyela hadi Ndambo Ileje ipo katika hali mbaya, mwaka huu Mwenge ulishindwa kufuata ratiba yake kupitia

299 barabara hii kwa sababu ipo katika hali mbaya na haipitiki kabisa.

Mheshimiwa Spika, ninaomba barabara hii ipatiwe fedha ili iweze kuwahudumia Wananchi wa Tanzania walioko Kyela na Ileje. Barabara hii ni muhimu sana kwa sababu ndiyo njia pkeee ya kuwafikisha watu katika Hospitali ya Isoko DDH.

MHE. ABDULSALAAM S. AMER: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

Mheshimiwa Spika, nakupongeza kwa jitihada za ujenzi wa barabara nchini kama Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

Mheshimiwa Spika, katika Bajeti ya mwaka huu, zimetolewa pesa za ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami toka Dumbe hadi Rudewa (Kilosa). Je, tokea Kilosa hadi Mikumi hazikutoletwa? Ili barabara ikamilike kwa haraka, ningeomba Mkandarasi mwingine angeanzia Mikumi hadi Kilosa. Wasiwasi unakuja toka Mradi huu uanze barabara yangu tokea Mikumi hadi Kilosa haijaweza kuguswa kabisa. Labda aliyekuwa Waziri wa Fedha ambaye ndiye Mbunge wa Jimbo la Kilosa, alikuwa akishinikiza au kuongeza pesa kwa Mradi huu.

Mheshimiwa Spika, nashangaa na sina matumaini kama barabara hii itaweza kukamilika kwa kuondolewa kwa Waziri wa Fedha. Naomba Mheshimiwa Waziri ajitahidi sana na naamini kwa

300 uzoefu wake ataongeza pesa za kukamilisha Barabara hii.

Mheshimiwa Spika, kwa Barabara ya kuunganisha Mkoa wa Morogoro na Dodoma, yaani Wilaya ya Kilosa na Mpwapwa, tuliomba kupitia RCC na Bodi ya Barabara ila nashangaa katika Bajeti hii sijaona pesa au fungu lililotengwa.

Mheshimiwa Spika, tuliomba pia ujenzi wa Daraja la Mto Ruhende. Daraja hilo ni kiunganishi cha barabara ya lami Mikumi – Kilosa hadi Kijiji cha Ruhembe; ni daraja ambalo kila mwaka lazima watu wafe kutokana na mvua za masika. Wakazi wa Ruhembe ni wakulima wakubwa wa miwa na ni tegemeo kwa Kiwanda cha Sukari cha Ilovo.

Mheshimiwa Spika, nakushukuru.

MHE. OMARI R. NUNDU: Mheshimiwa Spika, naomba kuchangia hoja ya Wizara ya Uchukuzi, nikijikita kwenye Barabara za Wilaya ya Tanga, zenye kilomita 809, ambazo kati yao kilomita 94.9 zipo chini ya TANROADS na hizo za TANROADS km 39.7 ni za lami wakati 55 ni za udongo. Kwa miaka zaidi ya 60 barabara ya lami ya Wilaya ya Tanga kwenda nje ya Tanga ilibakia moja tu ambayo ni Barabara ya Korogwe, ambayo kipande cha Tanga ni km 24.3. Kwa umuhimu wa kuiunganisha Tanzania na Kenya kupitia Tanga na pia kuunganisha Mji Mkuu wa Wilaya ya Pangani na kwingineko kupitia Tanga, Barabara za Tanga – Pangani na Tanga – Horohoro zingepaswa kufikiriwa lami siku nyingi zilizopita kwa kuwa hata urefu

301 wa barabara hizo si mkubwa na hali zao zimekuwa mbaya.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Barabara ya Tanga - Horohoro ulianza mwaka 2010. Kwa kuunga mkono ujenzi huo, wakazi wa sehemu ilipopita barabara hizo, walipoombwa kuvunja nyumba zao na kuondoa mashamba yao walipisha ujenzi wa barabara hiyo, ujenzi ulipoanza wale ambao hawakuwa wamejitolea kubomoa nyumba zao kwa hiari wamelipwa wakati malipo ya wale waliojitolea hayajafanyika na hadi leo hakuna kauli thabiti kuhusu hilo. Ninaiomba Serikali wawalipe raia wema hawa mapema na ni mategemeo yangu kuwa Serikali itatoa kauli kuhusu hili.

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Tanga – Pangani ni kigano kisichoeleweka. Mwaka jana tulielezwa kuwa upembuzi yakinifu ulikuwa unafanywa na leo katika Hotuba ya Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi ametamka tena usanifu utakaogharimu shilingi bilioni 2.55, utafanywa kwa barabara nzima ya Tanga – Pangani – Bagamoyo. Ikumbukwe kuwa, ilikuwa ni ahadi ya Mheshimiwa Rais katika Kampeni za Uchaguzi mwaka 2005 kuwa Barabara ya Tanga – Pangani ingejengwa kwa kiwango cha lami kati ya mwaka 2005 – 2010. Katika Ilani ya CCM ya 2010 – 2015, Barabara hii imeahidiwa tena kujengwa kwa kiwango cha lami. Hivyo ni ombi langu kuwa Serikali ijitahidi ili barabara hiyo yenye urefu wa kilomita 50.5 tu ambazo zinaunganisha Wilaya tatu, yaani Tanga, Muheza na Pangani ikamilike. Mheshimiwa Spika, kwa ujumla Barabara za Tanga ambazo zina urefu wa kilomita 809 zinaunganisha vijiji

302 ambavyo viko mbali na Jiji la Tanga. Halmashauri inajitahidi kuhudumia barabara zilizo chini ya himaya yake, zenye urefu wa km 714. Barabara hizi ambazo ni za lami, kati ya hizo ni km 84 tu, asilimia 50 yake zipo kwenye hali mbaya. Serikali ingefikiria kuzihamisha baadhi yake kama ile ya Tanga – Pande na Tanga – Mapojoni ziwe chini ya TANROADS. Papo hapo TANROADS isimamie vyema km 94.9 za barabara wanazohudumia sasa.

Mheshimiwa Spika, namaliza kwa kusisitiza mambo mawili; malipo ya waliopisha Barabara ya Tanga - Horohoro kwa hiyari yao na ujenzi wa Barabara ya Tanga – Pangani na Kivuko cha Mto Pangani.

MHE. ANNA MARYSTELLA J. MALLACK: Mheshimiwa Spika, nachukua nafasi hii kuchangia kwa maandishi Wizara hii ya Ujenzi na kama ilivyo kawaida, nachukua nafasi hii kumshukuru Jalali wetu kwa kutupa uzima wa kuwatetea Watanzania.

Mheshimiwa Spika, bila kusahau, naomba nikupe pole wewe kwa kufiwa na dada yako; nasema pole sana.

Mheshimiwa Spika, niende moja kwa moja kwenye mchango wangu nikianzia na barabara.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa barabara hasa Mkoa wangu wa Rukwa na Katavi, napenda kusema asiyeshukuru ni kafiri kwani kama Mpinzani siwezi kupinga au kukosoa kila jambo. Nashukuru kuona Serikali imetupa matumaini ya kutengenezewa

303 Barabara ya kutoka Tunduma – Sumbawanga na Sumbawanga – Mpanda, kwa kiwango cha lami. Mchakato tunaouona unavyoendelea. Vile vile Sumbawanga – Kasanga, pia Ipole – Inyonga na Inyonga – Mpanda na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, Wakazi wa Sumbawanga, Mpanda tutashukuru sana tutakapoona barabara hizi zimekamilika kwani miaka 50 sasa ya Uhuru, Mkoa huu wa Rukwa na sasa kuna Katavi, tulikuwa tumesahaulika sana kimaendeleo na ndiyo maana maendeleo yetu yanakwenda taratibu sana, pamoja na kwamba Rukwa na Katavi ni wazalishaji sana wa chakula kupitia kilimo.

Mheshimiwa Spika, pia Mkoa wetu tuna madini, tuna maziwa mawili; Tanganyika na Rukwa, tuna Hifadhi ya Taifa Katavi, yenye wanyama wakubwa na wanaovutia kuangalia na kadhalika. Je, sisi ni wa kukaa miaka yote hii tunakula vumbi kila kukicha?

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali sasa izingatie kukamilisha ahadi inazotoa. Naiomba Serikali iwalipe wakandarasi fedha wanazodai ili wafanye kazi kwa haraka bila kukwama na kuokoa muda ili masika isiharibu barabara na kurudisha kazi nyuma.

Mheshimiwa Spika, vile vile barabara za vijijini ni tatizo kubwa kwani nyingi hazipitiki na hivyo kuwapa wananchi wakati mgumu wa kutembea kuzifikia huduma muhimu kama zahanati, shule na ugumu wa kusafirisha mazao yao kutoka shambani na kupeleka Barabara Kuu kwa ajili ya kupeleka mazao yao sokoni.

304 Hivyo, naiomba Serikali ione suala la barabara vijijini ni muhimu sana kwani mpaka hivi sasa kuna wananchi ambao hawajatoa mazao yao majumbani kupeleka kwenye masoko kutokana na vijiji vyao kukosa barabara za kupita kuikuta Barabara Kuu; mfano, barabara kutoka au kwa kuvitaja vijiji vya Kalila Nkurukuru kwenda Kamsanga, Mkokwa kwenda Mnyagala, Kapanga kwenda Bajombe, Kasokola – Ngomalusambo. Hivyo ni mfano tu, lakini vijiji vingi sana havina sehemu ya kupitisha mazao yao na pia visima havijajengwa, Wananchi wanahangaika.

Mheshimiiwa Spika, wakandarasi wapimwe uwezo ili tender za kazi kwa wakandarasi zisitolewe kama njugu. Wakandarasi wachukuliwe wenye fani ya uhandisi au ufundi sanifu, lakini wengi ambao hawana fani wamekuwa wakipewa kazi na hao ndiyo wamekuwa wakifanya kazi bila kuzingatia viwango na kujenga madaraja au nyumba za Serikali, ambao akikabidhi kazi Mkandarasi huyo ni muda mfupi tu daraja au nyumba zinapasuka na kuharibika hovyo. Naomba suala hili lizingatiwe ili kuokoa fedha za Serikali kutumiwa vibaya.

Mheshimiwa Spika, nawasilisha.

MHE. STEPHEN M. WASIRA: Mheshimiwa Spika, nampongeza Mheshimiwa Waziri, kwa juhudi anazofanya katika ujenzi wa barabara. Hata hivyo, ninayo hoja mahususi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, mapema mwaka huu nilimwandikia Mheshimiwa Waziri kuhusu kuangalia

305 uwezekano wa kujenga Barabara za Mkutano – Natta – Mugumu hadi Loliondo – Mto wa Mbu na Barabara ya Namswa – Bunda – Kisorya. Pamoja na kumwandikia mapema barabara zipo katika hotuba zikiwa na token budget kwa mfano Barabara ya Makutano – Natta – Mugumu kilomita kumi, shilingi bilioni 3.0, Barabara ya Nyamswa – Bunda – Kisorya kilomita 118, shilingi bilioni 1.9.

Mheshimiwa Spika, hizi barabara zilikwishafanyiwa feasibility study na engineering design; sasa shilingi bilioni tatu au bilioni 1.9 zitafanya kazi gani? Ningeomba kupata maelezo ya kinagaubaga kuhusu hatima ya barabara. Bila kutengeneza barabara hizi, zinauacha Mkoa wa Mara kuwa wa mwisho kwa mtandao wa lami.

Mheshimiwa Spika, tunasikitika kwamba, wakati Barabara za Mkoa wa Mara zinanyimwa fedha, Barabara za Vijiji katika baadhi ya Mikoa zinapewa fedha nyingi!

Mheshimiwa Spika, mwisho, nakumbusha ahadi ya Rais ya kutengeneza kilomita mbili za lami katika Mji wa Bunda.

MHE. WARIDE BAKARI JABU: Mheshimiwa Spika, naishukuru Serikali kwa juhudi kubwa inayofanya katika kuimarisha ujenzi wa miundombinu nchini.

Mheshimiwa Spika, naishauri Serikali iimarishe ujenzi wa reli ili mizigo mizito ipite kwa kutumia reli na hivyo kulinda barabara zetu.

306

Mheshimiwa Spika, mpaka bado kuna changamoto kubwa katika mizani kwani foleni ni kubwa sana katika vituo vya kupimia magari. Naiomba Serikali iweke utaratibu mzuri ili kupunguza kero za foleni katika mizani iliyopo barabarani.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. MHONGA S. RUHWANYA: Mheshimiwa Spika, lengo la kuweka mizani katika barabara zetu ni kwa ajili ya ulinzi wa barabara zetu ili siziharibiwe na magari ya mizigo na vile vile kuzuia magari yasizidishe uzito ili barabara zetu zidumu.

Mheshimiwa Spika, nasikitika kwamba, magari mengi bado yanazidisha uzito, rejea ukurasa wa 14 wa Hotuba ya Wizara hii, utaona magari 482,638 yalizidisha uzito wa mizigo hivyo kutakiwa kulipa faini ya shilingi milioni 3,260.53. Nimesikitika kwani lengo la mizani si kupata pesa ni kulinda barabara, hapo maana yake kwa mizigo hiyo kuzidi na kulipa faini hiyo maana yake barabara zimeelemewa hivyo ni rahisi kuharibika wakati ujenzi wa barabara ni wa gharama kubwa mno. Hivyo basi ni vyema sheria izingatiwe na ikibidi faini iongezeke mpaka wenye kuzidisha mizigo washindwe kulipa ili wawe na discipline ya kutozidisha uzito wa mizigo.

Mheshimiwa Spika, vile vile wapo watumishi katika mizani ambao wanaweza kurubuniwa kupokea rushwa ili mwenye mzigo mzito apitishe mzigo wake. Hivyo, mizani iboreshwe ili iweze kupima magari kwa haraka ili

307 kupunguza msongamano wa magari hasa eneo la Kibaha.

Mheshimiwa Spika, lakini pia reli ikiboreshwa, barabara zitadumu kwani mizigo mingi itatumia reli.

Mheshimiwa Spika, nashauri Serikali iangalie uwezekano wa kujenga barabara ya njia nne kutokea Mbezi hadi Kibaha, kwani mara nyingi folini ni kubwa mno kutokana na mizani, lakini pia inapotokea ajali eneo la katikati ya Kibaha na Mbezi, hali huwa mbaya mno kwani msongamano wa magari huwa mkubwa sana na hakuna njia mbadala. Vile vile Serikali iangalie uwezekano wa kuboresha barabara ya kutokea Bagamonyo Baobab School mpaka Wilayani Kibaha katika Barabara Kuu ya Dar es Salaam – Morogoro. Hii itasaidia wananchi wanaotokea Mbezi Beach, Bagamoyo na maeneo ya Bunju na Kawe wasirudi nyuma kupitia Ubungo wapitie njia ya Baobab – Kibaha kama wanaelekea Morogoro na Mikoa mingine. Hii itasaidia kupunguza foleni isiyo ya lazima.

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Kigoma – Nyakanazi, imetengewa Sh. 3,500,000,000. Barabara hii ni muhimu sana kwani inaunganisha Wilaya za Mkoa wa Kigoma, Kasulu, Kibondo na inatuunganisha na Mkoa wa Kagera lakini pia Mkoa wa Shinyanga.

Barabara hii inatumika mno, ni njia kuu na muhimu lakini vile vile tumekuwa tukiizungumza sana toka Bunge la Tisa lakini bado haijatengewa fedha za kutosha kujenga kwa kiwango cha lami. Kwa kuwa njia ni mbaya, magari hayaendi kwa speed inayotakiwa na

308 wakati wa mvua barabara hii huteleza sana, hivyo wananchi wanateseka sana. Vile vile njia hii ina misitu mikubwa ambayo majasusi hujificha humo na kuteka magari, ikitengenezwa kwa kiwango cha lami magari yatapita kwa speed na hivyo hata watekaji hawatafanya kazi yao kirahisi kuliko ilivyo sasa ingawa ulinzi pia unahitajika sana.

Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali itueleze barabara hiyo itakamilika kwa kiwango cha lami lini? Je, kiasi cha shilingi 3,500,000,000 kimepangwa kwa ajili ya kazi gani kwani ni kidogo mno?

Mheshimiwa Spika, naomba kufahamu kwanini Serikali iliziunganisha barabara za Sumbawanga – Mpanda – Nyakanazi road imetengewa Sh. 16,800,000,000, barabara hii ni ndefu mno! Nashauri ujenzi ufanyike kuanzia Nyakanazi na kwa upande wa Sumbawanga, ili zikutane katikatai tukisubiri kuanzia Sumbawanga- Nyakanazi – Kigoma itachelewa sna kufika. Hivyo hivyo kwa barabara za Kigoma, Kidahwe, Uvinza - Kaliua, Tabora ujenzi uanze kila upande wakutane katikati.

Mheshimiwa Spika, napongeza ujenzi wa Barabara ya Mwandiga – Manyovu kwani imerahisisha usafiri na imepandisha hadhi bidhaa za wakulima na maisha yao na imerahisisha usafiri wa Kagoma, Tanzania na Burudi. Naomba pesa ziendelee kutengwa kwa ajili ya maintenance ili idumu.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi ina udhaifu wa kuchelewa kulipa madeni, hali inayopelekea kulipa

309 faini kwa wakandarasi. Hivyo, nashauri Wizara hii iboreshe mchakato wa shughuli ya mwanzo katika utekelezaji wa Miradi ya Ujenzi kama vile kutimiza masharti ya mikopo na taratibu za manunuzi.

Mheshimiwa Spika, vile vile barabara hujengwa kwa pesa nyingi tofauti na iliyopitishwa wakati wa kufanya zabuni; hivyo basi, TANROADS wanapaswa kuweka utaratibu mzuri wa kupitia na kurekebisha usanifu na makaridio ya miradi mara baada ya kuandaliwa na washauri na kabla ya ujenzi kuanza. Usimamizi wa miradi unapaswa kuboreshwa na udhibiti uongezeke ili tuepuke kuongezeka kwa gharama na kulazimika Serikali kufanya matengenezo ya barabara iliyotengenezwa kwa muda mfupi pindi usimazi usipokuwa mzuri. Mfano wa kuthibitisha udhaifu huo, rejea Taarifa ya Mkaguzi Mkuu ya 2009/10 ya TANROADS, madeni yaliyokuwepo kwa ajili ya wakandarasi na washauri waelekezi yalikuwa Sh. 43,183 milioni au USD 31.8 (Juni 2010).

Mheshimiwa Spika, lakini pia robo ya mwaka 2010, 31 Desemba, ilieleza wakandarasi walikuwa wanadai shilingi 321,581 (USD 224.9m) na malimbikizo ya madeni kwa ajili ya fidia ilikuwa jumla ya Sh. 49.605 milioni na mpaka Machi 2011 Serikali ilikuwa imelipa 242.8 kutoka Mfuko wa Barabara. Je, Serikali itaendelea na style hii mpaka lini tuepuke hali hii ili ujenzi wa barabara uwe wa ufanisi na wa faida na si wa hasara? Katika Bajeti ya 2011/2012 Serikali imelipa bilioni 420; hivyo, Miradi itaendelea kutekelezwa kwa mkopo.

310 MHE. LUCY P. OWENYA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kupata nafasi ya kuchangia.

Mheshimiwa Spika, mabango yaliyopo nchi nzima yaliyowekewa X ni zaidi ya miaka miwili vibao hivyo bado vipo barabarani na vinaonekana kama uchafu. Je, ni sababu zipi zilipelekea kuweka X wakati Serikali haipo tayari kuyatoa wala kuwachukulia hatua hao waliowekewa X? Kwa nini hawayatoi?

Mheshimiwa Spika, hali ya barabara kutoka Kibaha mpaka Chalinze hasa sehemu za Mlandizi mpaka Ruvu ni mbaya sana, barabara ile inanepa na kusababisha ajali kwa magari kupinduka na barabara zinazojengwa hazina nafasi za ku-park pembeni, hata kama gari limeharibika hakuna njia za waenda kwa miguu na kadhalika.

Je, Serikali ina mikakati gani katika barabara zilizopo kwenye Wilaya kuhakikisha zinakuwa rafiki kwa watu wenye ulemavu?

Je, Nyumba za Serikali na Ofisi zake ni lini zitakarabatiwa ikiwa ni pamoja na vyoo ili ziwe rafiki kwa watu wenye ulemavu?

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Old Bagamoyo katika maeneo ya TMJ kuna daraja lipo pale na ni hatari kwa wananchi kwa kuwa mvua zikinyesha mto ule unajaa maji na daraja linafunikwa na maji. Tatizo hili ni la muda mrefu; hivi mpaka ajali itokee na watu wafe pale kwa gari kuzama ndiyo TANROADS watakuja kuweka daraja la uhakika katika sehemu ile?

311

MHE. MAJALIWA K. MAJALIWA: Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, naunga mkono hoja kwa asilimia mia moja, kutokana na kazi nzuri inayofanywa na Wizara.

Tatizo langu kubwa ni Barabara ya Nanganga – Ruangwa, ya urefu wa kilomita 52, inayosafirisha mazao mbalimbali, shughuli za madini kutoka Ruangwa; haijatengewa fedha mwaka huu wa 2012, ikiwa mfululizo wa miaka kadhaa. Sasa ni wakati wa kutenga fedha za ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami ili Wananchi wa Wilaya hii waweze kupata mabasi, kusafirisha mizigo, kukaribisha na kuvutia wawekezaji kuja kuwekeza kwenye Sekta ya Madini.

Mheshimiwa Spika, Barabara hiyo ina tatizo la madaraja ambayo siyo imara tena ya miti.

Mheshimiwa Spika, Wizara ione umuhimu wa ujenzi wake ili kufanya usafiri wa eneo hili kuwa muhimu.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. ASSUMPTER N. MSHAMA: Mheshimiwa Spika, barabara nyingi hapa nchini zinataka kujengwa na zote ni muhimu sana, lakini kama kweli Serikali inataka kuona impact vyema kila mwaka, ziwepo barabara kadhaa za kuanzia, tuwe na awamu. Ikiwezekana zigawiwe kwa mikoa kila mwaka mikoa mitano hata sita au kikanda au zile zinazounganisha nchi nzima zikiisha tutengeneze zinazotuunganisha nchi na nchi na baada ya hapo mikoa inayozalisha mazao muhimu ya chakula na biashara na mwisho barabara zingine.

312

Mheshimiwa Spika, napenda kushauri tuanze kujenga Daraja la Kigamboni hata kwa mkopo bila woga huku kila Mtanzania akilipia licha ya wale wanaopita, tunaweza kuweka tozo kidogo kupitia simu, petroli, maji na vinywaji vyote hata ikiwa ni Sh. 50, nina uhakika tunaweza kulipa deni hilo bila shida. Pia daraja hili likiwa tayari eneo la Kigamboni litavutia wawekezaji na litatangazwa kama eneo la kitalii na hivyo kujenga majengo ya hali ya juu kama vile hoteli, majengo ya sinema na sehemu ya michezo ya watoto ya hali ya juu. Hata sehemu za kurekodia sinema mbalimbali za kimataifa kama ilivyo Hollywood inawezekana kwa nature ya hali ya Kigamboni.

Barabara za Dar es Salaam ni vyema zijengwe kwa haraka sana, kwa mpango wa Build Own Operate And Transfer (BOOT). Hii njia itarudisha deni maana inaweza kuongezwa kupitia magari yote Tanzania kupitia kwenye Registration na Insurance na kadhalika. Hii ni njia bora zaidi na tutarudisha deni.

Mheshimiwa Spika, suala la bomoabomoa nyumba za wananchi bila kuwalipa ni kosa kubwa sana na hili linafanya wananchi wengi kuichukia Serikali yao na hata kuona haijali watu wake. Mheshimiwa Spika, nadhani Serikali imekuwa na uzembe mkubwa juu ya suala la barabara, mfano, pale Misenyi, Kata ya Kyaka, Jimbo la Nkenge, wananchi wako pale tangu mwaka 1942 mpaka leo, lakini bila kujali Serikali inataka kubomoa nyumba zao bila fidia. Wananchi hawatakubali na hii italeta vurugu sana.

313

Je, wananchi wanapojenga ndani ya Hifadhi ya Barabara Serikali au Wizara mnakuwa wapi?

Je, Serikali inajua kuwa haitoi elimu ya kutosha kwa wananchi kuhusu maeneo ya kujenga na ya kutojenga? Kwa nini wapewe adhabu na siyo Serikali kubeba mzigo?

MHE. AGGREY D.J. MWANRI: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Wananchi wa Wilaya au Jimbo langu la Siha, naomba kuchukua fursa hiii kumpongeza sana Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli (Mb), Waziri wetu wa Ujenzi, kwa Hotuba yake nzuri na makini ambayo ameitoa asubuhi hii. Kazi anayoifanya Mheshimiwa Waziri ni ya hali ya juu na inaonesha kwa dhati namna Ilani ya Uchaguzi inavyotekelezwa nchini. Aidha, nampongeza Mheshimiwa Eng. Gerson H. Lwenge (Mb), Naibu Waziri wa Ujenzi na jirani yangu ambaye amekuwa na mchango mkubwa kwa Wizara.

Mheshimiwa Spika, kipekee, naomba nimshukuru Mheshimiwa Waziri, kwamba safari hii (mwaka 2012/2013) Barabara ya Sanya Juu – Kamwanga imetengewa shilingi milioni 2,926.00 Kwa ajili ya kuanza ujenzi. Nimefurahi kwa sababu barabara hii imekuwa ikitengewa fedha kidogo kidogo katika kipindi cha miaka 12 ya uwakilishi wangu na hakuna kazi iliyofanyika ukiacha upembuzi yakinifu, preliminary design na detailed designs. Aidha, mwaka jana tulitengewa shilingi bilioni 1.8 na hatukuona jambo lolote lililofanywa katika barabara hii muhimu kwa Taifa letu kiuchumi.

314

Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Waziri kwa Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010/2015, imetambua barabara hii na kuahidi kujenga na leo tunaanza kushuhudia utekelezaji wake katika Hotuba hii. Viongozi wetu wa Kitaifa akiwemo Rais wa Jamhuri ya Tanzania, Mheshimiwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete na Mheshimiwa Waziri Mkuu, wamezungumzia barabara hii kwa uzito mkubwa na kuahidi kuijenga.

Mheshimiwa Spika, namkaribisha Mheshimiwa Waziri Wilayani Siha ili apate fursa ya kutoa hizi taarifa (breking news), kwa wananchi wangu ambao kwa muda mrefu wamekuwa wakisubiri ujenzi wa Barabara ya Sanya Juu hadi Kamwanga.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja hii.

MHE. FATUMA A. MIKIDADI: Mheshimiwa Spika, kwanza, ninaunga mkono hoja kwa asilimia mia moja na nina haya ya kusema:-

Mheshimiwa Spika, tunaiomba Wizara itusaidie kujenga Kivuko cha Lindi Mjini kwenda Kitunda, kule kuna watu wengi sana lakini hakuna usafiri wa kuaminika.

Mheshimiwa Spika, ili kupunguza msongamano wa magari Dar es Salaam, tutumie usafiri wa treni angalau asubuhi na jioni kwenda katika maeneo kwani kuna miundombinu ya reli na mabehewa, tayari kuna uwezekano wa kuwabeba abiria wa Ubungo, Tabata,

315 Mabibo, Buguruni, Vituka Yomba na Tabata Reli wakati tunasubiri mpango wa fly over.

Mheshimiwa Spika, Barabara za Liwale hazina pacha kwenda vijijini, ukitaka kwenda kijiji chochote lazima uanze safari kuanzia pale pale Mjini Liwale kwenda Kata zote 21 kama Liwale kwenda Mikunya, Liwale – Mahata, Liwale – Mihumo, Liwale – Mpiga na kadhalika.

Tunaiomba Wizara iweke barabara za ndani kwenda vijijini badala ya kuanzia kituo kimoja. Barabara ziwekwe pacha.

Mheshimiwa Spika, tunaiomba Serikali ianze sasa kujenga madaraja kwa kutumia cement badala ya kutumia mbao kwani mbao huoza haraka.

Mheshimiwa Spika, mwisho, tunaomba Barabara ya Kibiti - Lindi iishe mapema kwaka huu.

MHE. GODFREY W. ZAMBI: Mheshimiwa Spika, napenda kuchangia kwa kifupi kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Mlowo – Kamsamba, kilomita 130, ni muhimu sana kwa Uchumi wa Wilaya za Mbozi na Momba. Hii ni Barabara ya Mkoa, nafahamu kwamba Serikali kupitia TANROADS imekuwa inafanya jitihada za kutosha kuitengeneza Barabara hiyo muhimu. Hata hivyo, pesa zinazotengwa kwa ajili ya Barabara hiyo huwa ni kidogo sana. Kubwa zaidi, uwingi wa mvua zinazonyesha katika Wilaya ya Mbozi, hufanya

316 barabara hiyo iharibike sana kila mwaka na hivyo kuhitaji matengenezo makubwa sana na hivyo inatumia pesa nyingi sana.

Mheshimiwa Spika, napenda nishauri Serikali kupitia Wizara hii iweke kwenye mipango yake kuijenga barabara hii kwa kiwango cha lami, bitumen au ota seal. Shughuli kubwa za kiuchumi zinazobebwa na barabara hii ni kilimo cha Kahawa, mazao mengine mchanganyiko, shughuli za ufugaji na uvuvi. Kubwa zaidi, barabara hii inaungaisha Mkoa wa Mbeya na Rukwa, hivyo kuna kila sababu ya kuijenga kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Hasamba – Hezya – Ileje kimsingi huanzia Mji wa Vwawa – Hasamba – Nyimbili – Hezya kuingia Wilaya ya Ileje. Vwawa - Hasamba kuna Barabara ya TANROADS lakini pia kuna Barabara ya Ruanda – Idiwili – Hezya ya TANROADS na pesa kwa ajili ya barabara hizo zimetengwa. Hata hivyo, Barabara ya Hasamba – Hezya ni mbaya sana na kimsingi ilishapandishwa hadhi kuwa ya Mkoa. Bahati mbaya Barabara hii haijatengewa fedha hata senti tano; nataka kujua kulikoni?

Je, Wizara ipo tayari kurekebisha kasoro hiyo; yaani kuitengea Barabara hiyo pesa ili iweze kutengenezwa na hivyo kuwawezesha wananchi wa maeneo hayo waweze kushiriki shughuli za kiuchumi, kijamii na kadhalika bila matatizo makubwa kama ilivyo sasa?

317 Mheshimiwa Spika, kwanza, naipongeza Serikali kupitia Wizara hii (TBA), kuamua kujenga nyumba kwa Watumishi wa Serikali. Tumeambiwa zinajengwa nyumba kwa Viongozi ambao wanastahili kupewa nyumba. Nashauri nyumba hizo zikijengwa zisiuzwe tena na hivyo kuiingiza Serikali kwenye matumizi makubwa sana ya pesa kwa kuwaweka Viongozi wanaoteuliwa hotelini. Hata hivyo, nyumba nyingine zote zinazojengwa ziuzwe kwa Watumishi wa Serikali. Kujenga nyumba nyingi na kuzipangisha itakuwa ni kuibebesha Serikali mzigo mwingine kwani sote tunajua kwamba ni mzigo mkubwa wa kuzifanyia matengenezo ya mara kwa mara.

Mheshimiwa Spika, natambua jitihada za Wizara katika kudhibiti uzito wa magari barabarani yanayoharibu barabara. Hata hivyo, bado zipo changamoto za kutosha. Bado magari yanayobeba mizigo kupita uzito unaoruhusiwa yanaendelea kupita katika barabara zetu! Kinachoshangaza ni kwamba, gari linapita Kibaha (mizani) linapita Mikese (mizani), likifika Mikumi au Makambako, linakamatwa kwa kubeba mizigo kupita kiasi kinachoruhusiwa! Hili tatizo huwa ni nini? Baadhi ya mizani ni mbovu au rushwa?

Mheshimiwa Spika, nashauri Wizara iendelee kudhibiti uzito wa magari yanayotumia barabara zetu ili kulinda barabara zetu. Pia makondarasi wanaojenga barabara zetu, wajenge kwa viwango vinavyokubalika. Wizara pia isimamie eneo hili kwa karibu sana.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

318

MHE. AUGUSTINO M. MASELE: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja kwa asilimia mia kwa mia.

Mheshimiwa Spika, baada ya pongezi hizo, ninaiomba Wizara sasa itekeleze kwa uhakika yale yote yaliyopangwa ndani ya Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya Mwaka 2010 – 2015.

Mheshimiwa Spika, naipongeza Wizara kwa kupandisha hadhi Barabara ya Masumbwe hadi Butengolumasa kuwa ya TANROAD; hongera sana Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi kwa kazi nzuri.

Mheshimiwa Spika, ninayo imani kubwa kwamba, sasa Wilaya yetu ya Mbogwe tunakwenda vizuri; nina uhakika tutaanza kupata samaki wabichi toka Chato, kwa ajili ya wananchi wetu na kudumisha udugu baina ya Wilaya zetu mbili.

Mheshimiwa Spika, kwa upande wa utalii katika Kisiwa cha Rubondo wananchi wetu watafaidika vile vile.

Mheshimiwa Spika, namwomba Mungu siku moja barabara yetu ya Masumbwe – Paramasa – Butengalumasa iwe ya lami.

Mheshimiwa Spika, Mungu aibariki Wizara ya Ujenzi na Waziri wake.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

319 MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana, nimeona Barabara ya Nyololo – Igowole – Kibao – Mtwango – Mgololo, ipo katika Mpango wa FS RDD kwa ajili ya kiwango cha lami.

MHE. LIVINGSTONE J. LUSINDE: Mheshimiwa Spika, kwanza, nampongeza Mheshimiwa Waziri wetu, kwa kazi nzuri sana za kusimamia Wizara vizuri na kwa kweli ni mchapa kazi mzuri, pamoja na Watendaji wote wa Wizara hiyo, kwa kuchapa kazi bila kuchoka tena kwa uaminifu mkubwa.

Mheshimiwa Spika, jambo la pili ni kuhusu Mheshimiwa Waziri wetu kupunguza gharama za ujenzi wa barabara kwa kiwango cha lami kwani ilikuwa kilometa moja ya lami shilingi bilioni moja. Kwa sasa Mheshimiwa Waziri ameishusha mpaka milioni mia saba hivi. Hoja yangu; sababu zilizofanya gharama zipande ni zipi? Je, kulikuwa na uchakachuaji? Kama ndivyo waliochakachua wamechukuliwa hatua gani?

Pili, pongezi kwa ujenzi wa barabara ya lami kutoka Dodoma kwenda Iringa, unaendelea kwa kiwango kizuri ila kuna nyumba za Wananchi wa Mlodaa zilizovunjwa hawajafidiwa.

Mheshimiwa Spika, naomba Kauli ya Waziri watalipwa lini?

MHE. GREGORY G. TEU: Mheshimiwa Spika, katika mwaka 2011/2012 na kwa wajibu wa kutekeleza Ilani ya CCM (2010), Wizara ya Ujenzi ilipanga kufanya kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa Barabara

320 ya Mbande – Kongwa – Mpwapwa (km 53), kwa nia na lengo la kuijenga kwa kiwango cha lami. Je, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina umeshaanza?

Katika mwaka 2012/13 ni hatua zipi zitaendelezwa ili kukamilisha ujenzi wa barabara hii ambayo ni kiungo kikubwa kwa kupitisha mazao ya kilimo pamoja na madini.

MHE. KAPT. MST. GEORGE H. MKUCHIKA: Mheshimiwa Spika, natanguliza shukrani za Wananchi wa Jimbo la Newala, kwa kazi nzuri inayofanywa na Wizara hii kuhakikisha kuwa, Mkoa wa Mtwara unaunganishwa na Mikoa mingine kwa kiwango cha lami hasa Mtwara – Lindi – Dar es Salaam na Mtwara – Songea – Mbambabay. Aidha, naishukuru Serikali kwa kupitia Wizara ya Ujenzi, kwa kuanza ujenzi wa barabara za lami Newala Mjini. Maombi yangu ni yafuatayo:-

Mheshimiwa Spika, Wizara iendelee kutoa fedha mwaka huu wa 2012/13 ili kuongeza urefu wa Barabara za Newala Mjini kwa kiwango cha lami na kukarabati lami iliyokwishajengwa. Maombi yetu ni kujenga kiwango cha lami Barabara ya Boma Road – Hospitali, Boma Road – Halmashauri ya Wilaya na Halmashauri ya Wilaya kwenda Hospitali ya Wilaya. Aidha, tunaomba barabara ya lami Newala Mjini kwenda Masasi iongezwe hadi Viwanda vya Korosho ambako wakati wa msimu wa ununuzi wa Korosho barabara inaharibika sana kwa sababu ya wingi wa magari.

321 Mheshimiwa Spika, katika Ilani ya Uchaguzi ya CCM 2010 – 2015, kuna ahadi ya kufanya upembuzi yakinifu ujenzi wa barabara ya lami kati ya Mtwara – Tandahimba – Newala – Masasi. Mheshimiwa Rais, wakati wa Kampeni za Uchaguzi alipohutubia Newala Mjini aliahidi kuwa kabla hajamaliza kipindi chake cha Uongozi, atahakikisha anaweka Jiwe la Msingi ujenzi wa barabara hii. Fedha zilizotengwa mwaka jana na shilingi 67 bilioni za mwaka huu ni kidogo sana na kazi hii itachelewa kuanza. Hii ndiyo Barabara ya Uchumi inayounganisha Wilaya zote tano za Mkoa wa Mtwara. Naomba Wizara itilie mkazo Mradi huu ili uanze kabla ya mwaka 2015 kama alivyoahidi Mheshimiwa Rais.

Mheshimiwa Spika, Wakala wa Majengo umejenga jengo zuri sana la ghorofa moja Ofisi ya Mkuu wa Wilaya Newala, lililofunguliwa na Mheshimiwa Rais Kikwete, tarehe 27 Julai 2011. Tatizo kubwa la jengo hili ni ukosefu wa uzio. Tunaomba kila mwaka kwa miaka mitatu mfululizo lakini bado hatujatengewa fedha. Jengo liko mbali na makazi ya watu (zamani Uzunguni). Naomba Wizara iangalie namna ya kutusaidia kama special request.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. GOODLUCK J. OLE-MEDEYE: Mheshimiwa Spika, kwanza, nampongeza sana Mheshimiwa John Pombe Magufuli (Mb) - Waziri wa Ujenzi na Mheshimiwa Gerson H. Lwenge (Mb) - Naibu Waziri wa Ujenzi, kwa namna wanavyojituma kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria za Sekta ya Ujenzi nchini. Hongereni sana kwa uchapaji wenu wa kazi.

322

Mheshimiwa Spika, pili, nampongeza sana Katibu Mkuu, Balozi Herbert Mrango, Dkt. John Stanslaus Ndunguru, Naibu Katibu Mkuu, Wenyeviti na Watendaji Wakuu wote wa Bodi, Wakala na Taasisi zilizo chini ya Wizara ya Ujenzi, kwa kazi nzuri wanayofanya ya kusimamia utekelezaji wa Sera na Sheria mbalimbali.

Mheshimiwa Spika, tatu, kwa niaba ya Wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, natoa shukrani za dhati kwa Uongozi wa Wizara ya Ujenzi na Mfuko wa Bodi ya Barabara, kwa kutusaidia kiasi kidogo cha fedha zilizosaidia kuboresha walau barabara mbili na kuwezesha kupitika kipindi chote cha mwaka. Vile vile naipongeza Wizara na Uongozi wa Wakala wa Barabara, kwa kazi kubwa na nzuri wanayoifanya kuboresha barabara zote nchini. Nimefurahishwa sana na ujenzi wa Barabara ya Dodoma – Babati kwa kiwango cha lami. Tunayo matumaini kuwa, itakapokamilika itasaidia sana kupunguza umbali toka Makao Makuu ya Afrika Mashariki, Arusha hadi Makao Makuu ya nchi yetu Dodoma na kuunganisha Mikoa ya Kaskazini na Mikoa ya Nyanda za Juu Kusini na nchi jirani.

Mheshimiwa Spika, hali mbaya ya Barabara za Halmashauri ya Wilaya ya Arusha: Mwaka jana wakati nachangia mjadala wa Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Ujenzi, nilielezea masikitiko ya Wananchi wa Jimbo langu kuwa tokea nchi hii ipate Uhuru, hatujawahi kuwa na barabara bali wanapita njia zilizofanana na zile za ng’ombe. Hali hiyo imetuacha tukiteseka mabondeni na milimani tukipambana na vumbi wakati

323 wa kiangazi na matope wakati wa masika, huku tukiwa tumebeba mizigo vichwani, kwa sababu magari hayawezi kufika tunakoishi ambako ndiko pia viwanja vyetu vya kuzalisha kahawa na ndizi, mboga mboga na mazao mengineyo, pamoja na mifugo, yanayotumiwa kulisha wakazi na wageni wa Jiji la Arusha. Niliomba tupewe upendeleo maalum kwa kutuwezesha kutengeneza njia hizo zifikie kiwango cha barabara zinazopitika mwaka wote. Naomba nirudie tena kuwasilisha ombi hilo kwa niaba ya wapiga kura wangu. Naomba nisaidiwe barabara zifuatazo: -

(a) TPRI – Likamba – Nengung’u;

(b) Kisonga – Oloitushula – Olchorovus;

(c) Kilimamoto – Imbibia – Engalaoni;

(d) Ngaramtoni – Sambasha- Ilboru;

(e) Oljoro-Laroi (machimbo ya morrum);

(f) Mbuyuni – Mirongoine (machimbo ya mchanga);

(g) Mashono – Bwawani – Temi ya Simba – Oljoro;

(h) Oldonyosambu – Oldonyowas;

(i) Losinoni – Engutukoiti – Kaanani;

(j) Kimandolu – Sokon II – Ng’iresi;

324 (k) Kisongo – Lemugur – Laroi;

(l) Loruvani – Oldonyosapuk – Olgilai;

(m) Sekei – Loruvani; na

(n) Ngulelo – Bangata – Ng’iresi.

Mheshimiwa Spika, Inshallah, Mwenyezi Mungu, awaongoze wanaofanya maamuzi ili walipokee ombi hili na kulipa umuhimu unaostahili.

Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Barabara ya Arusha (Mbauda JCT) – Orkesumet – Kibaya – Kongwa (Dar es Salaam – Dodoma Road JCT): Barabara hii ipo kwenye Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano (2011/12 – 2015 -/16). Umuhimu wa Barabara hii kwa Uchumi wa Taifa hauhitaji kupigiwa ngoma. Mahindi yanayouzwa kwenye Soko la Kibaigwa yanatoka Kiteto na Simanjiro na husafirishwa kupitia Barabara hii. Mchanga unaotumika kujenga nyumba zote Jijini Arusha, Arumeru na Monduli kutoka Oljoro husafirishwa kwa Barabara hii. Vile vile madini yanayochimbwa Komolo, Losinyai na Simanjiro husafirishwa kwa Barabara hii. Kiulinzi, Barabara hii hutumiwa na Vikosi vya Jeshi Oljoro na Kikosi cha Misinga (Themi Holding Grounds). Aidha, hii ndiyo barabara itumiwayo na Wakulima wa Mahindi Lolkisalie na mashamba mengine makubwa yaliyo Morongoine na maeneo jirani.

Mheshimiwa Spika, nashauri Barabara hii ipandishwe hadhi kuwa ya Kitaifa na itengewe fedha za upembuzi na usanifu ili ujenzi wake uanze.

325

Mheshimiwa Spika, kuna kero kubwa katika Halmashauri ya Arusha inayohusu usimamizi wa Sheria ya Barabara Na. 13 ya 2007. Watendaji wamegeuka wanasiasa kiasi kwamba badala ya kusimamia Sheria ipasavyo, wanasikiliza watakayo watu waliojenga kwenye eneo lililotengwa kwa ajili ya barabara, hivyo kukwaza matengenezo na utunzaji wa barabara pale fedha kidogo zinapopatikana. Namwomba Mheshimiwa Waziri, aingilie kati suala hili na kutolea maelekezo ya Kisera na Kisheria kwa kuwa wenye mamlaka wilayani wameshindwa kutimiza wajibu wao.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja.

MHE. ROSWEETER F. KASIKILA: Mheshimiwa Spika, naiomba Serikali iharakishe au iongeze speed katika kumalizia Barabara za Tunduma – Sumbawanga, Sumbawanga – Kasanga na Kasesya, lakini Sumbawanga – Mpanda, Kibaoni.

Mheshimiwa Spika, Barabara ya Tunduma - Sumbawanga fedha zake ni za MCA (T), zipo, hatuoni kwa nini ujenzi wa barabara hii haumaliziki katika muda uliopangwa. Ninatoa rai kuwa wakandarasi wasichelewe kupewa fedha (mafungu yao).

Mheshimiwa Spika, Mtandao wa Barabara za Mkoa wa Rukwa siyo mzuri ukiacha hizo nilizozitaja hapo juu. Barabara za Ilemba – Kalambazite, Laela – Mambwe Kenya – Mwazye, Barabara za Nkundi, Kate, Kala – Wampembe, Kabwe Korongwe, ndiyo zinazotumika na wananchi walio wengi Mkoa wa

326 Rukwa. Akina mama wajawazito walio wengi ndiyo wanaozitumia kwenda Zahanati, Vituo vya Afya na Hospitali wanapopata rufaa au kwenda kujifungua.

Mheshimiwa Spika, naomba ziangaliwe na zifanyiwe kazi.

MHE. CLARA D. MWATUKA: Mheshimiwa Spika, kwanza, namshukru Mungu, kwa kunijalia afya njema na kuniwezesha kuiona siku hii. Pia napenda kutoa pongezi kwa Mheshimiwa Waziri na jopo lake, kwa kazi nzuri ambayo imeonesha matumaini. Kwa nafasi ya pekee ni kwake Waziri kwa kubakizwa kwake katika Wizara hii ya Ujenzi. Hii inadhiririsha ni kwa jinsi ya utendaji wake bora na makini alionao. Ni kiasi cha kumwomba Mola azidi kumpa afya njema ili azidi kuifanya kazi yake kwa moyo zaidi.

Mheshimiwa Spika, napenda kuchukua nafasi ya shukrani kwa Wizara juu ya Barabara ya Kibiti – Lindi, ambayo kwa hivi sasa inatia moyo na kuna matumaini ya kumalizika mwaka huu. Vile vile naishukuru kwa ujenzi ambao umeanza wa Daraja la Mto Mbwinji – Nangoo, ambayo roho za watu wengi zimepotea pale. Zoezi hili naomba pia lifanyike kwa barabara kutoka Masasi – Tunduru – Songea.

Mheshimiwa Spika, napenda kuiomba Serikali isaidie Barabara ya Mkoa Mtwara ambayo ni kiunganishi cha Wilaya ya Masasi na Newala. Njia hii inaanzia Kijiji cha Nanganga, Wilaya ya Masasi kupitia Mihima – Mkongi katika Wilaya ya Newala ikipitia aidha Mnyambe, Nakahaku, Nambunga hadi Newala au

327 kutoka Mkongi kupitia Mikumbi, Chihangu, Kitangali hadi Newala. Njia ni fupi Masasi ukilinganisha na ya Newala – Masasi. Njia hii Kilima chake ni kidogo na kifungu, ukilinganisha na Mlima Namaleche. Isitoshe njia hii kuna vijiji vingi, ikitengenezwa njia hii itakuwa ni mkombozi kwa vile watu wengi wa vijiji hivyo hadi Newala, tegemeo lao kwa Hospitali ya uhakika ni Ndanda Misheni. Vile vile njia hii kwa wale waendao Hospitali hiyo ya Ndanda wa Wilaya hiyo ya Newala, wanapitia njia ya Rukohe, Miyuyu kutoka Kidanda na kwenda kukutanisha Kijiji cha Mikumbi au Namdimba hadi Mnyambe. Njia hii ina kilima kikali na kirefu (kimetambaa) sana. Hivyo, naiomba Serikali kwa manufaa ya umma wa maeneo hayo niliyoyataja, ilione hilo.

MHE. SUSAN L.A. KIWANGA: Mheshimiwa Spika, ningependa kupata majibu kwa niaba ya Wananchi wa Kilombero, kuhusu kilio chetu cha miaka mingi, miundombinu ya barabara na Daraja la Kilombero na Ulanga.

Mheshimiwa Spika, Mwaka wa Fedha wa 2011/2012 Waziri alisema katika hotuba na alipojibu swali langu la msingi la tarehe 11 Julai, 2011 likihusu Barabara toka Kidatu – Ifakara, kilomita 80, ijengwe kiwango cha lami na Ifakara – Mlimba hadi Madeke kilomita 235 mpakani mwa Njombe pia ijengwe kwa kiwango cha lami kutokana na umuhimu wa barabara hiyo kwani ni Wilaya iliyoteuliwa kwa kilimo na uzalishaji mkubwa wa mpunga.

328 Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi katika majibu yake alisisitiza kuwa, Serikali itajenga barabara hiyo kwa kiwango cha lami Kidatu hadi Ifakara kilomita 80 na Ifakara hadi Mlimba Madeke mpakani Njombe kwa kiwango cha Changarawe. Hadi leo ninapochangia, barabara hizo zimebaki kama zilivyo kabla ya Mwaka wa Fedha wa 2011/2012, ambapo ilikuwa na kilomita 17 tu za kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, pamoja na uwekezaji mkubwa uliofanywa wa KPL Mngeta, lakini barabara ni mbovu sana na haipitiki kipindi cha mvua. Serikali haijaweka au haijajenga hata kiwango cha changarawe ilichoahidi. Naomba nipate majibu ya Serikali kuhusu uboreshaji wa barabara hiyo.

Mheshimiwa Spika, kuhusu Daraja la Mto Kilombero, katika Bajeti ya 2011/2012 Serikali iliahidi kuanza ujenzi wa Daraja hilo, lakini mpaka leo hakuna dalili zozote, hata vifaa vya mkandarasi havijapelekwa site ingawa Viongozi mbalimbali wa Serikali kwa nyakati tofauti walisema kuwa Mkandarasi ameshapatikana na fungu lilitengwa kwenye mwaka wa fedha ulioisha; hatuoni matokeo yake. Sasa nahitaji majibu na taarifa za kuanza kwa ujenzi wa daraja hilo.

Mheshimiwa Spika, ahsante.

MHE. KOMBO KHAMIS KOMBO: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, nachukua nafasi hii kutoa mawazo yangu kwa Wizara ya Ujenzi, nikijiua kwamba Wizara hii

329 ni miongoni mwa Wizara Mama inayotegemewa kukuza na kuboresha Pato la Taifa.

Mheshimiwa Spika, Wizara ya Ujenzi ukiacha Wizara ya Mambo ya Nje ambayo inaitangaza Tanzania nchi za nje, lakini ndiyo yenye nafasi pekee ya kuionesha nchi ya Tanzania kwa Jumuiya za Kimataifa endapo miundombinu ya ujenzi wa barabara, reli, bandari, bandari kavu, vivuko pamoja na mipango miji itaimarika.

Mheshimiwa Spika, umaskini wa Tanzania ni wa kujitakia kwa kuwa bado Viongozi hawajawa na nia ya dhati ya kuijenga Tanzania na Watanzania. Hii ni kwa sababu Tanzania imebarikiwa ardhi kubwa, yenye rutuba na vyanzo vya maji, ambapo kama Viongozi wangalikuwa na nia ya dhati, leo Tanzania ingalikuwa inategemewa na Mataifa mengine badala ya kutegemea.

Mheshimiwa Spika, vile vile Tanzania imebarikiwa kuwa na mito, maziwa, jambo ambalo hata nchi nyingi jirani hawana baraka hizo. La kusikitisha, sisi tuliojaaliwa na Mungu tukamilikishwa kuwa navyo, hatuvienzi na kuvitumia ipasavyo. Leo Tanzania tuko nyuma ya watu tuliowasaidia kupigania Uhuru kimaendeleo, mfano wa nchi hizo ni Zimbambwe, Afrika Kusini, Rwanda, Burundi na kadhalika.

Mheshimiwa Spika, tuna wajibu wa kujiuliza kuna kosa gani ambalo tumemkosea Mungu ili turudi tupite kwenye mstari unaokubalika na kama ni ubadhirifu unaofanywa na watumishi, makampuni au viongozi

330 kwa maslahi yao binafsi, wachunguzwe na wawajibishwe kama wengine walivyowajibishwa na kama ni mikataba mibovu basi ifutwe, wale waliohusika na mikataba hiyo wachukuliwe hatua za kisheria.

Mheshimiwa Spika, awali nilisema kwamba, endapo miundombinu ya ujenzi wa barabara, reli, bandari, bandari kavu, vivuko, pamoja na mipango miji itaimarishwa, itachangia Pato la Taifa kutokana na sababu zifuatazo:-

(a) Kwa kuwa karibu nchi sita zimetuzunguka, bandari zetu zitakapoboreshwa nchi nyingi zitapitishia mizigo yao kupitia bandari zetu.

(b) Njia za Reli zitakapojengwa mizigo hiyo hiyo itachangia Pato la Taifa kupitia reli zetu.

(c) Barabara zitakapojengwa vile vile zitachochea maendeleo ya ya nchi.

Mheshimiwa Spika, hata hivyo, Serikali ina wajibu wa kuangalia kwa makini na ukaribu juu ya Wakandarasi wa Ujenzi wa Barabara. Serikali iache kutiliana mikataba na wakandarasi au makampuni ambayo ujenzi wao haukubaliki Kimataifa.

Mheshimiwa Spika, hivi sasa kuna njia au barabara ambazo zimeshachafuka na ambazo zimejengwa miaka ya karibuni. Vile vile njia za reli zitakapojengwa zitaimarisha wakulima vijijini kwa sababu watakuwa na uhakika wa kusafirisha mazao yao ya biashara. Hivyo,

331 reli itakuwa mkombozi wa wanyonge lakini hata wafanyabiashara wa nchi jirani.

Mheshimiwa Spika, pamoja na kutaka Mji wa Kisasa Kigamboni, lakini Serikali ina wajibu wa kuzingatia maisha ya raia wake ambao wamekaa eneo hilo kama sehemu ya maisha yao. Kwanza, wafidiwe na siyo kufidiwa tu, wapatiwe maeneo wajenge kwa kuwekewa muda maalum ambao wataweza kumaliza ujenzi katika makazi yao mapya.

Mheshimiwa Spika, Mji wa Dar es Salaam unahitaji kufanyiwa marekebisho ili uendane na Miji mingine Duniani. Mji wa Dar es Salaam umekuwa kama kero kutokana na kukosekana kwa miundombinu ya barabara na ujenzi holela. Ili kupunguza msongamano wa magari barabarani ambao unakosesha ufanisi wa wafanyakazi kufika kazini kwa wakati na hata kuwakosesha wananchi kufika katika harakati zao za maendeleo, lakini pia ukosefu wa miundombinu niliyoitaja, huchangia pia uharibifu wa mazingira katika nchi yetu.

MHE. AMOS G. MAKALLA: Mheshimiwa Spika, naomba nichangie Wizara ya Ujenzi nikijieleleza katika mambo makubwa matatu.

Mheshimiwa Spika, mwaka jana niliomba kupandishwa hadhi kwa barabara katika Wilaya ya Mvomero, Serikali ilijibu kuwa nifuate taratibu kwa barabara hizo kupitishwa kwenye Kikao cha Bodi ya Barabara.

332 Mheshimiwa Spika, mapema mwaka huu Bodi ya Barabara ilipokea maombi na kuziombea barabara za Mhonda – Ibiri – Pemba, Dakawa – Dihombo na Langali – Nyandira. Naomba Waziri atoe ufafanuzi wakati wa kuhitimisha Hotuba yake.

Mheshimiwa Spika, kwanza, naishukuru Serikali kwa kutenga shilingi bilioni nne kukamilisha ujenzi wa Barabara ya Dumila – Turiani – Mziha – Korogwe. Naomba kasi ya ujenzi iongezwe na ukamilike kwa wakati.

Mheshimiwa Spika, mwaka jana nilichangia kuomba Serikali iwalipe fidia wananchi wote waliopisha ujenzi wa Barabara ya Dumila – Turiani – Mziha na waliopisha ujenzi wa Barabara ya Mvomero – Makuyu – Ndole – Kibati na Barabara ya Sangasanga – Langali.

Mheshimiwa Spika, naomba sana Serikali iharakishe malipo yaweze kuhakikiwa ili kuondoa matatizo ya madai haya ambayo yamechukua muda mrefu sasa.

Mheshimiwa Spika, naunga mkono mkono hoja.

MHE. DKT. AUGUSTINE L. MREMA: Mheshimiwa Spika, naunga mkono hoja. Naishukuru na kuipongeza Wizara na Waziri wake, Mheshimiwa Magufuli, kwa uhodari na uadilifu wake wa kusimamia ujenzi wa barabara. Nashukuru na kuipongeza Serikali kwa ujenzi wa barabara ya lami kuanzia Kawawa, Nduoni, Kinea Vunjo Magharibi, Kilema Kaskazini hadi Marangu Mtoni.

333 Mheshimiwa Spika, kuna barabara muhimu sana itokanayo Kilema Pofo kwenda Kilema Hospitali. Barabara hii yenye mrefu wa kilomita kumi inasumbua sana ikizingatiwa eneo hilo lina taasisi muhimu zifuatazo: Mandaka TTC; ST. James Seminary; Olaleni Secondary School; Lombeta Secondary School; Kilema Hospital (ya Wilaya); Maua Seminary; Chuo cha Ufundi Mandaka; na Msarikie Secondary School.

Nyumba ya Hayati Calist Lekule na wenzake walioko Himo, imeagizwa ivunjwe kufuatia kupanuliwa kwa akiba ya barabara kwa mujibu wa Sheria Na. 13 ya 2007, sehemu ya nyumba imeingizwa kwenye akiba ya barabara. Nashauri wapewe fidia ya ardhi na maendelezo.

Mheshimiwa Spika, mizani ya Njia Panda Himo imekuwa kero; kwanza, imejengwa barabarani na hivyo kusababisha foleni kubwa ya magari kwenye barabara ya kwenda Himo, barabara ya kwenda Tanga na barabara ya kwenda Moshi.

Pili, magari yanayotoka Dar es Salaam ingawa yatakuwa yamepitia katika mizani za njiani bila matatizo, yakifika kwenye mizani ya Njia Panda yanapopima yanaambiwa yamezidisha uzito. Kuna haja ya kuangalia mizani hiyo huenda ni mbovu.

Mheshimiwa Spika, tatu, magari hata yasiyokuwa na mzigo yanalazimishwa kupima. Naona kama huu ni usumbufu.

334 Mheshimiwa Spika, nne, naomba Njia Panba pawe na mizani mbili ili kuondoa msongamano wa magari eneo hilo.

MHE. SAID M. MTANDA: Mheshimiwa Spika, shukrani kwa Serikali. Hatua iliyopigwa katika kuboresha miundombinu nchini si haba.

Umuhimu wa Barabara ya Mchinga – Kilolambwani – Kijiweni kuwa Barabara ya Mkoa. Barabara hii ni muhimu kiusalama na kiuchumi kwa kuwa eneo hilo ni muhimu kwa kilimo cha korosho, ufuta, lakini ni eneo la Bahari Kuu ya Hindi. Vikao vyote vya Halmashauri na RCC vimeridhia jambo hili, Wananchi wa Mchinga wanataka kujua kauli ya Wizara juu ya jambo hili na hatima yake.

Ujenzi wa Daraja la Mchinga I ni ahadi ya Rais, lakini tathmini imefanyika na Sh. 280,355,000 zinahitajika kuwaunganisha wananchi hawa ambao mvua na bamvua linapojitokeza, mawasiliano yanakatika kabisa. Hivyo, kutekeleza ahadi ya Rais ya shilingi milioni 280 nalo ni jambo kubwa?

Mheshimiwa Spika, toka mwaka 2010, 2011 na 2012 tumekuwa tunapewa ahadi ya kutoa Sh. 200 milioni kwa ajili ya Barabara ya Ngongo – Rutamba – Milola – Kwawa hadi Mandawa; jamani Wataalam wa Wizara waende kuona hali ya Mlima wa Kiwawa, hata Mbunge na DC wanatembea kwa miguu kwenda Kiwawa, miguu yangu nahisi itazama Mheshimiwa Magufuli, TANROAD – Lindi waliambie Taifa kupitia Wizara kwa nini suala hili haliishi.

335

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, wale wote waliokuwa wameomba kuchangia Wizara hii wamechangia na orodha yangu imekwisha, lakini kutokana na aina ya Wizara hii ambayo inawagusa watu wengi, tumeona kwamba Naibu Waziri aanze kujibu sasa na tutampa dakika 30. Tukirudi jioni Mheshimiwa Waziri ataanza kujibu hoja na najua kabisa mtakuwa na maswali mengi wakati huo, hivyo naomba mfike wote wakati huo. Mheshimiwa Naibu Waziri!

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote naomba nimshukuru sana Mwenyezi Mungu kwa mambo mengi ambayo ameendelea kunitendea pamoja na kunipa afya njema ya kuweza kutekeleza majukumu yangu. Naomba pia nimshukuru Rais wangu Mheshimiwa Daktari Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuniteua kuwa Naibu Waziri wa Wizara hii nyeti na naomba niahidi kwamba nitaifanya kwa uaminifu kumsaidia Mheshimiwa Magufuli ili tuweze kutekeleza mambo yote ambayo Waheshimiwa Wabunge mmeyazungumza hapa. Naomba nimwahidi kwamba nitafanya kwa uaminifu nikishirikiana pia na Madiwani wangu 23 kutoka Jimbo la Njombe Magharibi. Tumepata Wilaya Mpya na Mkoa Mpya wa Njombe. Kwa hiyo, wananchi wa Njombe waamini kabisa Mbunge wao nafanya kazi ambayo inawaletea heshima.

Mheshimiwa Spika, namshukuru sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kunipa maelekezo ambayo naendelea kuyafanya kwa kufanya kazi yangu ya

336 uadilifu. Nishukuru sana wapiga kura wangu wa Wilaya mpya hii ya Wanging’ombe. Tumepata Wilaya Mpya na Makao Makuu mapya Igwachanya. Sasa wapo wengine wanawachanganya. Wilaya mpya hiyo hakuna mtu anaweza kubadilisha panaitwa Igwachanya sio mahali pengine na naomba Mkuu wa Wilaya ahamie Igwachanya.

Mheshimiwa Spika, nikushukuru sana wewe mwenyewe pamoja na Wabunge wote kwa ushirikiano wenu ambao mmekuwa mnanipa toka nilivyokuwa Wizara ya Maji na sasa nipo Wizara ya Ujenzi. Ushauri wenu nitauchukua na nitaufanyia kazi.

Mheshimiwa Spika, kabla sijasema maneno mengi kwanza niunge mkono hoja hii. Kama mnavyofahamu kwa kweli mtu anayeweza kusema Wizara ya Ujenzi haijafanya kitu, nafikiri anahitaji kupata miwani ambayo labda ni zaidi ya miwani ya kawaida. Ukizunguka nchi nzima barabara zinajengwa na wakati Waziri anatoa Hotuba yake alionesha na picha, sasa usipounga mkono maana hayo madaraja tuyaache bila kuyamaliza. Kwa hiyo, naomba sana hata kama una ombi maalum la barabara yako tutaiangalia kulingana na uwezo wa Serikali. Kwa hiyo, naomba sana Waheshimiwa Wabunge wote wa upande wa Chama Tawala na Upinzani, tuunge mkono Bajeti hii ili tuweze kufanya haya ambayo tumeyapanga.

Mheshimiwa Spika, sasa nitajibu baadhi ya hoja na najua Waheshimiwa Wabunge wengi mmetushauri, mengi ni mazuri, lakini kwa sababu ya muda

337 hatutaweza kuyasema yote na tutajitahidi yote, tutawapa kwa maandishi.

Mheshimiwa Spika, nianze na Mheshimiwa anazungumzia barabara ya Kyaka-Bugene- Kasulo inatekelezwa kwa kasi ndogo sana kutokana na Mkandarasi kutolipwa. Jibu ni kwamba, Mkandarasi ameshalipwa shilingi 4.5 na kazi inaendelea kwa kasi inayostahili. Aidha, Mhandisi Mshauri pia ameshalipwa tutafuatilia utekelezaji wa Mkandarasi huyu na kama kuna Mkandarasi yeyote ambaye analeta visingizio visivyokuwa vya muhimu tutamtoa na kumweka mwingine.

Mheshimiwa Felix Mkosamali, amezungumzia barabara ya Nyakanazi-Kibondo-Kidahwe imetengewa fedha katika mwaka 2012/2013, anauliza barabara ya Kibondo Mjini zitengewe fedha na Road Fund. Majibu ni kwamba, katika mwaka wa fedha 2012/2013, Serikali imetenga shilingi bilioni 3.5 kwa ajili ya kuanza ujenzi wa barabara hiyo. Usije ukafiria kwamba ni kidogo. Bilioni 3.3 zinatosha kabisa kwanza kumpata Mkandarasi na kumpa advance. Unaweza ukatenga fedha nyingi na Mkandarasi akashindwa kuzitumia. Sasa nataka fedha hizi tuzitawanye katika miradi yote ambayo tumepanga. Kwa hiyo, angalau tunakuhakikishia kwamba barabara hiyo imeanza kujengwa na Mkandarasi atalipwa advance ili aweze kujenga barabara hiyo.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mwigulu Lameck Nchemba, amezungumzia barabara ya Shelui– toa- Mtekente hadi Ulugu ifanyiwe matengenezo. Barabara

338 hii ni ya Wilaya. Hata hivyo, Serikali kupitia TANROAD katika mwaka wa fedha 2012/2013, Serikali imetenga milioni 150/= kwa ajili ya kufanya matengenezo kwa kiwango cha changarawe kwa kilometa nane. Pia aanzishwe Mamlaka ya kuhudumia barabara za Wilaya kama ilivyo TANROAD. Ushauri huu tunaupokea na nafikiri mchakato wa kuanzisha kitu kama TANROAD, TAMISEMI wameanza kushughulikia na itakapokuwa kamili tutawajulisheni.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mwambalaswa amesema kwamba, Serikali ioneshe nia ya kweli ya kujenga barabara ya Mbeya–Lwanjilo–Chunya hadi Makongorosi. Anataka kujua fedha ngapi zimetengwa? Kwa mwaka huu wa fedha tumetenga shilingi bilioni 9.3, fedha hizi zinatosha kabisa na wale Wakandarasi wa vipande hivi vya Mbeya-Lwanjilo, Lwanjilo-Chunya walikuwa wamesimama kwa sababu hawajalipwa malipo yao. Tumeshawalipa hawana sababu ya kujitetea na tutafuatilia kuona kwamba kazi zilizopangwa zinatekelezwa.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mwanjale anaulizia barabara ya Lwanjilo nimeshalijibu. Anauliza barabara ya Isonje-Makete imetengewa fedha ambayo haitoshi. Majibu ni kwamba, barabara ya Isonje–Makete itaendelea kutengenezwa kwa kiwango cha changarawe. Mwaka huu wa fedha barabara hii imetengewa shilingi milioni 686 kwa ajili ya matengenezo. Mheshimiwa Faida Mohamed Bakari anashauri Wakandarasi wajenge barabara kwa viwango vinavyoridhisha. Ushauri wake tunaupokea na tutaufuatilia.

339

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa anasema shukrani kwa Serikali kwa kutenga fedha za kukamilisha ujenzi wa daraja la Mto Simiyu, shukrani hizo tunazipokea.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Daktari amezungumza kwamba, barabara ziunganishe Mkoa wa Manyara na Mkoa wa Shinyanga kupitia Meatu-Iramba-Singida. Barabara zinazohudumiwa na Halmashauri za Wilaya zitapandishwa hadhi kwa kufuata vigezo vilivyomo kwenye Sheria namba 13 ya mwaka 2007 na Kanuni zake. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge wengi wameleta mapendekezo ya barabara zao ziweze kupandishwa.

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa mapendekezo yenu lazima yajadiliwe kwenye Bodi za Mikoa, lakini pia muisome ile Sheria, vigezo vimeelezwa, barabara inapandishwa hadhi kwa vigezo vipi. Kama ni barabara ya Wilaya ili iweze kuwa barabara ya Mkoa vigezo vimeainishwa kwenye Sheria. Kwa hiyo tunaomba sana kuizingatia Sheria ile otherwise barabara zote zitakuwa za TANROAD kama Mheshimiwa mmoja alivyosema, sasa Wilaya itabaki haina barabara ya kutengeneza.

Mheshimiwa Spika, nafikiri hili sio lengo. Unaposema hiyo TANROAD maana unataka itengenezwe kwa kiwango kinachotakiwa. Tutatengeneza mtandao ambapo hata Wilayani kule lazima watengeneze barabara kwa kiwango kinachotakiwa. Sasa asilimia 70 ya fedha za Mfuko wa

340 Barabara zinakwenda TANROAD, lakini asilimia 30 zinakwenda kwenye Halmashauri zetu na hizo asilimia 30 lazima tuzisimamie.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Daktari Kebwe anasema, fedha zilizotengwa kwa ajili ya barabara ya Makutano-Nata-Mugumu, shilingi bilioni tatu ni kidogo sana na upembuzi yakinifu utafanyika lini? Majibu ni kwamba, barabara ya Makutano-Nata-Mugumu utekelezaji wake utafanywa kwa awamu. Awamu ya kwanza Kilomita 80, imetengewa bilioni tatu, ni kwa ajili ya maandilizi ya kuanza ujenzi. Kwa hiyo, Mkandarasi akishapatikana tutamlipa mobilization ili aweze kuendelea na kwa kadiri kazi inavyoendelea kulingana na jinsi anafanya kazi.

Mheshimiwa Spika, upembuzi yakinifu na usanifu wa kina tayari umekamilika mwaka 2009. Wananchi wanaostahili fidia watalipwa lini na ni shilingi ngapi? Wananchi wanaostahili fidia watalipwa kabla ya Mkandarasi kuanza kazi na kiasi kitajulikana baada ya tathmini kukamilika. Kwanza, lazima tathmini ifanyike baada ya ile michoro ya kuonesha barabara inapita wapi, ni nyumba zipi zitaathiriwa, ukishakamilika ndiyo tutaanza kulipa na kazi ya Ujenzi itaanza. Kwa hiyo, kazi ya ujenzi haiwezi kuanza kabla ya tathmini na wanaohusika kupewa fidia.

Mheshimiwa yeye ametoa shukrani kwa kuanza maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Sikonge-Tabora, shukrani tunazipokea. Serikali itenge fedha za kutosha kwa ajili ya Sikonge-Mibono–Kipiri.

341 Serikali imetenga shilingi milioni 255 mwaka 2012/2013 kwa ajili ya ukarabati wa barabara hii kuanzia Mibono kwenda Kipiri na kazi hii itaendelea kulingana na fedha zitakavyokuwa zinapatikana.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Getrude Rwakatale anasema hongera kwa kazi nzuri, tunaipokea hongera hiyo. Pili, anaulizia barabara ya Kidatu-Uchindile na Kidatu-Mahenge kwa kiwango cha lami na ni ahadi ya Rais, itajengwa sasa. Serikali imeanza mchakato wa ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami katika mwaka 2012/2013, tutamtafuta Mhandisi Mshauri kwa ajili ya upembuzi yakinifu kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Amina Abdul Amour, anasema Bajeti iliyopita ilishindwa kutekeleza ujenzi wa barabara kwani fedha zilizopatikana zilikuwa kidogo sana ukilinganisha na barabara na zenye wafadhili pia. Majibu ni kwamba, fedha zote za ndani zilizotengwa kwa bajeti ya barabara zote zilitolewa kama ilivyokuwa imepangwa.

Mheshimiwa Spika, pia ametoa shukrani kwa Serikali kukataa barabara ya Kilwa kwa kujengwa chini ya kiwango. Shukrani hizi tunazipokea na barabara zote ambazo zitajengwa chini ya kiwango hatutazipokea. Miradi yote ya Kitaifa tumewaagiza Mameneja wa TANROAD wawe karibu sana na utendaji kila hatua ili tukiona tu kwamba, Mkandarasi anaanza kufanya vitu ambavyo havikubaliki tunatoa taarifa pale mara moja na kuweza kusimamisha ujenzi pale itakapokuwa inawezekana.

342

Mheshimiwa Spika, Serikali iwazuie watu kujenga kwenye eneo la barabara kuliko kusubiri wajenge ndiyo wavunje. Kusema kweli Sheria ya Hifadhi ya Barabara tumeilezea vizuri, tatizo wananchi wetu sehemu zingine wanakuwa ni wabishi bila sababu. Unaambiwa hapa umejenga ndani ya hifadhi, tumekupa alama lakini unakuta mtu mwingine alama ile anaifuta. Sasa unapofuta unakuwa umefanya nini.

Mheshimiwa Spika, tunaomba sana wananchi washirikiane na sisi ili tujenge barabara ambazo ni nzuri. Kwa mfano, Dar es Salaam tunapata tatizo. Wengi mnasema kuna msongamano, tumepata mradi wa mabasi yanayokwenda kwa kasi, lakini kikwazo tunachokipata ni wananchi hawataki kupokea mradi, hawataki kupisha tuendelee maana wameshapata na fidia lakini kubomoa imekuwa ni matatizo, wanakwenda Mahakamani, yaani kuzuia tu kazi ile isifanyike.

Mheshimiwa Spika, naomba sana Watanzania tushirikiane, tunapotaka maendeleo lazima tukubali kwamba baadhi ya majengo lazima tutayabomoa kwa sababu labda planning yetu ya awali haikuwa nzuri. Lakini jinsi tunavyoendelea tunaboresha. Kwa hiyo, wananchi naomba tukubaliane, wale ambao wako ndani ya hifadhi tafadhalini sana mkubali kupisha, lakini barabara ikikufuata tutawalipa fidia kulingana na Sheria.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Christowaja Mtinda huyu alizungumzia barabara ya Singida Shelui

343 hasa eneo la Sekenke kwamba imejengwa chini ya kiwango. Serikali imechukua hatua gani kwa Mkandarasi aliyejenga barabara hii. Majibu ni kwamba, Serikali iliunda Kamati ikijumuisha, Mkandarasi na Mhandisi Mshauri kuchunguza sehemu iliyoharibika ili kujua chanzo cha tatizo. Baada ya uchunguzi, Mkandarasi pamoja na Mhandisi Mshauri wameamriwa kurudia ujenzi, kipande hicho kwa gharama zao na sisi tutafuatilia kuhakikisha kazi ile inatengenezwa kwa gharama zao.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Leticia Nyerere alisema, Wizara ihamasishe wanawake katika ujenzi wa barabara hususan katika kazi na usimamizi na isiwe kubeba zege. Serikali pia iongeze nguvu zaidi katika kuwajengea uwezo Makandarasi wanawake na kuongeza idadi yao.

Mheshimiwa Spika, Wizara yangu inacho kitengo maalum kinachoshughulikia kuwahamasisha wanawake katika kujiunga na kazi za ujenzi wa barabara na Ofisi zote za TANROADS kila Mkoa, na yupo mratibu anayeshughulikia kuwahamasisha akina mama.

Mheshimiwa Spika, tunayo makampuni mengi sasa hivi ambayo yamesajili na ambayo Wakurugenzi wake ni akina mama. Kwa hiyo, Serikali kupitia Bodi ya Makandarasi imesajili Makandarasi wanawake 161. Kkatika hao, 120 wako katika fani ya ujenzi wa barabara. Haya ni maendeleo mazuri kama Mheshimiwa Leticia Nyerere alivyopendekeza.

344 Mheshimiwa Dunstan Mkapa alitoa pongezi kwa Serikali kwa kuanza ujenzi wa daraja la Nangoo. Pongezi tunazipokea. Pia aliomba barabara ya Nangombo - Nanyumbu ijengwe kwa kiwango cha lami kwani ilikuwa ni ahadi ya Rais.

Mheshimiwa Spika, majibu ni kwamba usanifu wa kina wa barabara hii kwa ajili ya ujenzi kwa kiwango cha lami umekamilika. Kwa sasa Serikali itafuta fedha kwa ajili ya kuanza ujenzi. Kuhusu ni lini wananchi waliowekewa ‘X’ kwenye nyumba zao wataanza kulipwa fidia, Serikali itawalipa fidia wananchi wote ambao wanastahili kwa mujibu wa Sheria.

Mheshimiwa Ezekiel Chibulunje alitoa pongezi kwa kazi inayofanywa na Wizara hii. Pongezi tunazipokea. Alipongeza ujenzi wa Barabara kuu inayotoka Dodoma kwenda Iringa na Dodoma Babati, akaomba ujenzi uanze haraka na Serikali itoe tamko ujenzi ya Mayamaya - Bonga utaanza lini.

Mheshimiwa Spika, majibu ni kwamba kipande hiki baada ya kuwa tumepata fedha kutoka ADB na JICA, tayari tumeshapeleka nyaraka kwa mfadhili ili tupate no objection ili tuweze kutangaza tenda ya kuanza kujenga barabara hii. Kwa hiyo, ninaamini kabisa kazi hiyo itaanza mara moja katika mwaka huu wa fedha. TBA kupitia majukumu ya msingi ya kitengo hiki imedhihirika wazi kuwa kitengo hiki ni muhimu katika kukabiliana na matatizo ya nyumba za kuishi alichokizungumza hapa. Ni kuwa, anashauri kwamba wapate title debts ya viwanja. Kwa hiyo, title debts kwa majengo ya Serikali na viwanja vyake inashughulikiwa,

345 TBA imeshapata hati miliki zaidi ya 400 na mchakato wa kutafuta hati miliki kwa majengo yaliyobaki unaendelea.

Mheshimiwa Kitwanga - Mbunge wa Misungwi anatoa pongezi, tunazipokea. Vile vile anashukuru kwa Wizara kutenga fedha za matengenezo ya barabara iendayo Ihelele kwenye mradi wa maji. Anaomba barabara hiyo ipandishwe daraja. Nimeshazungumza kwamba barabara zitapandishwa daraja kulingana na Sheria na hii lazima ianzie kwenye Bodi ya Barabara ya Mkoa.

Mheshimiwa John Mipata anaulizia Sumbawanga - Kanazi na Kibaoni iongezewe fedha kwa sababu Shilingi bilioni 6.4 hazitoshi. Serikali itaendelea kutafuta fedha zaidi kwa ajili ya kumalizia ujenzi wa barabara hii ya barabara ya Sumbawanga - Matai - Kasanga itengenezwe mpaka mwisho. Barabara hii itatengenezwa kulingana na mkataba ambao tayari umeshatengenezwa.

Mheshimiwa Rashid Ali Abdallah, alisema Wizara isimamie viwango vya ujenzi wa barabara, mfano barabara ya Dar es Salaam - Morogoro imeanza kudidimia. Ushauri umepokelewa. Wizara kupitia Wakala wa Barabara itasimamia kwa karibu utekelezaji wa miradi hii ili zijengwe kwa kiwango.

Mheshimiwa Henry Shekifu anatoa pongezi kwa Wizara; tunapokea pongezi hizo. Pia anazungumzia habari ya barabara ya kutoka Mlolo - Ngwelo - Mlolo - Makanya - Mlingano - Mshewa. Tunaomba sana

346 Mheshimiwa Mbunge kwa sababu barabara hii iko chini ya Wilaya, maombi yake yaanzie kule ili kusudi yaweze kupendekezwa katika kupandisha hadhi ya barabara hii.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Luhaga J. Mpina, Mbunge wa Kisesa, alishauri Serikali ifanye upembuzi yakinifu kwa barabara za Bariadi - Kisesa - Mahunzi - Karatu Arusha kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami. Barabara ya Bariadi - Kisesa Junction imefanyiwa upembuzi yakinifu kutegemeana na upatikanaji wa fedha. Mwaka wa fedha 2012/2013 Shilingi milioni 630 zimetengwa na Serikali kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu na usanifu kwa ujenzi wa kiwango cha lami barabara ya Kolandoto - Lalago - Mwanh’uzi - Bukundi - Sibiti - Matale - Mang’ole mpaka Njia Panda.

Pia aliuliza kwamba Shilingi bilioni 2.5 zilizotengwa mwaka wa fedha 2012/2013 kwa ajili ya mto Sibiti, zitatosha? Majibu ni kwamba fedha hizo zimetengwa kwa ajili ya kuanza kazi. Ninaamini kabisa Mkandarasi akishapata mobilisation, ataendelea kuifanya kazi hiyo. Fedha za certificate, tutaendelea kuzitafuta.

Mheshimiwa aliomba Serikali iangalie uwezekano wa kupunguza hifadhi ya barabara kwa maeneo ya milimani kuwa mita saba na nusu kila upande, badala ya mita 30 ushauri wake tumeupokea na tutaufanyia kazi.

Mheshimiwa Aloyce Malocha aliomba Serikali isaidie kujenga daraja la Mto Momba linalounganisha Kilyamatundu na Kamsamba, kwani wananchi

347 wanateseka sana. Majibu ni kwamba, Serikali inatambua umuhimu wa daraja la Momba na hatua kadhaa zimeshachukuliwa katika kutatua tatizo hili. Upembuzi yakinifu na usanifu wa awali kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo umekamilika. Kwa sasa Serikali inaendelea kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa daraja hilo.

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Freeman Mbowe, barabara ya kwa Sadala - Masoma imetengewa fedha kidogo Shilingi milioni 150 katika mradi wa shilingi bilioni tano. Serikali itenge fedha za kutosha. Majibu ni kwamba kwanza kabisa kazi imeshakuwa na mkandarasi, fedha hizi ambazo tumezitenga ni kumwezesha mkandarasi aendelee kujenga, lakini kila atakapokuwa anatoa certificate, Serikali itatafuta fedha za kulipa ili kazi ile ambayo tayari tumeshamwekea mkataba iweze kukamilika.

Mheshimiwa Henry Shekifu alishauri Serikali ikamilishe ujenzi wa barabara ya Lushoto - Magamba inayoelekea kwenye makazi ya Mheshimiwa Rais Mstaafu. Nadhani ujenzi wa barabara ya kutoka Lushoto - Magamba kwa kiwango cha lami unatekelezwa kwa kadri ya upatikanaji wa fedha na tayari kilomita 4 .2 zimekamilika.

Mheshimiwa Desderius Mipata, yeye anasema barabara mbili za Halmashauri ya Nkaa, Kala na Kitosi wa Pembe ziliombewa kupandishwa hadhi. Naomba sana Mheshimiwa Mipata kama nilivyosema, barabara hizi zitapandishwa hadhi kulingana na Sheria ambayo tuliipitisha hapa Bungeni. Mheshimiwa Benedict Ole –

348 Nangoro, pongezi kwa Wizara na sisi tunazipokea. Anasema, ujenzi wa barabara una tofauti kubwa. Barabara za hadhi sawa ziwe sawa katika upana, mwinuko, mitaro na ushindiliaji. Barabara zote zifuate standard na specification. Ushauri wake unazingatiwa na ndivyo tunavyofanya. Barabara zitajengwa kufuatana na specifications ambazo zimewekwa na jinsi msanifu alivyoweka ule usanifu. Kwa hiyo, mkandarasi lazima afuate standards ambazo zimewekwa kwenye michoro.

Pia kuna ushauri kwamba Serikali ianze maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Narco - Kongwa - Kibaya - Okesmeti mpaka Oljoro Mbauda kwa kiwango cha lami. Maandalizi ya ujenzi wa barabara ya Narco - Kongwa - Kibaya - Okesmeti hadi Oljoro - Mbauda kwa kiwango cha lami, yatafanyika pindi Serikali itakapotaka fedha. Kwa sasa hivi maandalizi yanafanyika kujenga barabara ya Handeni - Kibaya - Kondoa - Singida kwa kiwango cha Lami.

Kulikuwa na ushauri kwamba mipango ya flyovers ianze mara moja. Tumelizungumza kwenye Hotuba ya Waziri kwamba tutaanza na flyover ya Tazara, lakini baada ya hapo, tutaendelea na flyover nyingine kwa jinsi hali ya fedha itakavyokuwa inaruhusu.

Mheshimiwa Spika, kulikuwa na hoja kwamba barabara ya Iringa - Dodoma - Babati iwekwe katika mkakati wa kukamilishwa. Nimeshailezea hiyo. Mheshimiwa Prof. Msolla alisema nyumba zilizowekewa ‘X’ ambazo barabara imezifuata zilipwe fidia mapema. Tumepokea ushauri wake, alama za ‘X’ zimewekwa

349 kwa maendelezo yaliyoko nje ya mita 22.5 mpaka 30 kama tahadhari kuzuia maendelezo mengine ndani ya hifadhi ya barabara kulingana na Sheria ya barabara namba 13 ya mwaka 2003 ya mwaka 2007 na kanuni zake mwaka 2009.

Mheshimiwa Spika, tulishauriwa kwamba Serikali itatue tatizo la msongamano wa magari Dar es Salaam. Ushauri huu tumeupokea, na kuna barabara nyingi ambazo tumeziorodhesha kwenye hotuba yetu na zote hizo zinalenga katika kupunguza msongamano wa magari Mjini Dar es Salaam.

Katika Mpango wa Dar es Salaam, unaweza ukajenga barabara nyingi, lakini pia tunaangalia, watu wanakwenda katikati ya Mji kufanya nini? Kama tunaweza kuweka huduma nje ya Mji, watu hawana sababu ya kwenda kutafuta mchicha Kariakoo kama wanaweza wakaupata Kawe. Kwa hiyo, ni mipango ambayo nafikiri Jiji linabidi liangalie sasa kuwa yale mambo muhimu ambayo siyo lazima yawe katikati ya Jiji, tutayashughulikia kuwa wasiende mjini bila sababu. (Hapa kengele ililia kuashiria muda wa Mzungumzaji kwisha)

SPIKA: Nimekuongezea dakika kumi tena.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rukia Kassim Ahmed anasema, Serikali itumie alama za barabarani zinazotengenezwa kwa nondo na saruji. Ushauri wake tunaupokea na sasa hivi tumeshaanza kwasababu ya wizi wa alama za

350 barabarani. Kwa kweli tunaomba sana Watanzania, alama za barabarani ni usalama wetu. Naomba sana watu wasing’oe alama za barabarani. Ajali nyingi zinatokea, kwa sababu hakuna alama. Sasa Watanzania watuunge mkono katika kujenga barabara zetu, tunaweka alama pia kuonyesha mtu apunguze mwendo. Naomba sana Watanzania tuangalie kama tunasema hapa nenda kwa kilomita 50 kwa saa, lazima twende kilomita 50 kwa saa. Tunakuwa na sababu, inakuwa ni eneo la makazi au pengine kuna wanafunzi wanavuka barabara. Sasa naomba sana tufuate alama za barabarani na tusing’oe.

Mheshimiwa Abia Nyabakari, yeye anaomba Amatai - Ekisesa - Nkasi iongezeke ili barabara hiyo iweze kukamilika kwa wakati. Ushauri wake tunaupokea.

Mheshimiwa alisema barabara ya Kisarawe hadi Manerumango ya kilomita 54 ijengwe kwa kiwango cha lami kama ilivyoainishwa katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi. Ahadi ya Serikali ya kujenga barabara ya Kisarawe - Manerumango kwa kiwango cha lami inatekelezwa kama ilivyoainishwa kwenye Ilani ya Uchaguzi. Mchakato wa kumpata mhandisi mshauri unategemewa kukamilika mwisho wa mwezi Julai, 2012 na kazi ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kukamilika ifikapo mwaka 2012/2013.

Mheshimiwa Aliko N. Kibona anasema, Serikali ijenge barabara na miundombinu mingine inayovutia wawekezaji kuwekeza nje ya Jiji la Dar es Salaam.

351 Suala hili ushauri wake tunaupokea na nimeshalielezea. Mheshimiwa Abdulsalaam Selemani Amer, Mbunge wa Mikumi anasema barabara inayounganisha Mkoa wa Morogoro na Dodoma, yaani Wilaya ya Kilosa na Mpwapwa iliombewa kupandishwa hadhi, mbona haijatengewa fedha?

Mheshimiwa Spika, jibu ni kwamba jumla ya Shilingi milioni 274.34 zimetengwa kwa ajili ya barabara hii kwa mwaka huu wa fedha.

Mheshimiwa Omari Rashid Nundu -Mbunge wa Tanga, yeye anasema Serikali iwalipe fidia wananchi wa Mkoa wa Tanga waliobomoa nyumba zao kwa hiari yao kupisha ujenzi wa barabara ya Tanga - Horohoro. Majibu ni kwamba, kulingana na Sheria ya Barabara ya mwaka 2007, watu wanaostahili kulipwa fidia ni wale tu waliopo nje ya eneo la hifadhi ya barabara ya mita 22.5 kila upande na ambao barabara imewafuata.

Mheshimiwa Spika, wananchi ambao wamebomoa nyumba zao kwa hiari yao baada ya kupewa notisi ya kubomoa mwaka 2003 kwa barabara ya Tanga - Horohoro walikuwa ndani ya hifadhi ya barabara. Hivyo wananchi hawa hawastahili kulipwa fidia yoyote.

Kuhusu swali kwamba barabara ya Tanga - Pangani na daraja la mto pangani vitajengwa lini? Barabara na daraja imo kwenye mpango wa ujenzi chini ya Jumuia ya Afrika ya Mashariki, kwa sasa inafanyiwa upembuzi yakinifu na usanifu wa kina

352 pamoja na kuandaa vitabu vya zabuni za kuanza ujenzi inaendelea. Serikali ifikirie kuhamisha barabara za lami za Tanga - Pande na Tanga - Mapurini kutoka chini ya Halmashauri kwenda TANROADS. Nadhani hili tumeshalisema kwamba ukitaka kuhamisha ni lazima upandishe hadhi ya daraja ndiyo TANROADS wataweza kuzihudumia.

Mheshimiwa Spika, namshauri Mheshimiwa Mbunge ayapitishe maombi haya kupitia Bodi za Barabara za Mkoa wa Tanga ili tuweze kuona kama inawezekana zikapandishwa hadhi au vipi. Mheshimiwa AnnaMaryStella John Mallac – Mbunge wa Viti Maalum anasema shukurani kwa Serikali kwa ujenzi wa barabara za lami Mkoani Rukwa na Katavi, shukurani tunazipokea. Kuhusu suala kwamba Serikali ilipe kwa wakati madai yote ya makandarasi kwa barabara, tunapokea ushauri wake na sasa hivi tumeshaanza kulipa na tutafuatilia kwa kuhakikisha kuwa makandarasi hawa hawasimami kwasababu wanaidai Serikali. Kulikuwa na ushauri kwamba Wakandarasi wasajiliwe kwa kuzingatia uwezo katika fani zao, ushauri huu tunaupokea.

Mheshimiwa alisema fedha zilizotengwa kwa ajili ya barabara ya Mkutano - Nata ni kidogo sana. Kwanza kitu kikubwa ni kwamba barabara hii ikishakuwa imepata mkandarasi na tukamlipa advance, tayari ni commitment, itakuwa ni juu ya Serikali kutafuta fedha kuhakikisha kuwa mkandarasi huyu hasimami. Kwa hiyo, barabara hiyo itajengwa na hizo fedha zinatosha kwa kuanzia. Pia anasema fedha zilizotengwa kwa barabara ya

353 Nyamuswa Shilingi bilioni 1.9 ni kidogo. Majibu ni kwamba Nyamuswa - Bunda - Busorya Shilingi bilioni 1.9 zinatosha kwa ajili ya maandalizi ya kuanza ujenzi. Majibu yake yote yanafanana. Yote itakuwa ni kumpata mkandarasi na kumpa malipo ya awali.

Kuhusu utekelezaji wa ahadi ya Mheshimiwa Rais, ya kujenga barabara za Mjini Bunda umefikia wapi? Majibu ni kwamba barabara za Mjini Bunda ziko chini ya uangalizi wa Halmashauri ya Wilaya. Kwa hiyo, ahadi hii ya Mheshimiwa Rais itapaswa kutekelezwa kupitia Halmashauri husika.

Mheshimiwa Waride Bakari Jabu alisema kuna msongamano wa magari kwenye Vituo vya Mizani. Majibu ni kwamba katika kuzuia msongamano kwenye Vituo vya Mizani, Wizara imeweka utaratibu wa kujenga mizani nje ya barabara kujenga mizani za kutosha katika pande zote mbili za barabara katika sehemu zenye magari mengi. Maswali haya ya msongamano kwenye mizani yamerudiwa, na sasa hivi tunafanya mapitio ya mizani yetu, tunataka kwanza mizani hii iwe ya kisasa zaidi. Kwa hiyo, maeneo ambayo tunaona kuna msongamano, tutajenga kwasababu sehemu nyingine mizani zipo upande mmoja tu, tutahakikisha tunajenga na upande wa pili.

Mheshimiwa Spika, vile vile kulikuwa na ushauri kwamba Serikali iangalie uwezekano wa kujenga njia nne katika ya barabara ya Mbezi hadi Kibaha. Serikali imeanza mchakato wa kujenga barabara ya njia sita kutoka Dar es Salaam hadi Chalinze kwa kiwango cha expressway. Kwa hiyo, itakuwa na njia sita. Njia tatu

354 upande mmoja na njia tatu upande wa pili. Mheshimiwa Lucy Owenya anasema kwa nini mabango nchi nzima yamewekwa ‘X’, kwa takribani miaka miwili lakini hayaondolewi? Majibu ni kwamba lengo la uwekaji wa alama za ‘X’ ni kuwatahadharisha wananchi kwamba wamevamia hifadhi na huwa tunaomba sana wananchi wayatoe wao wenyewe, maana Serikali ikija kuyatoa yale mabango itabidi ulipe gharama za kuyatoa. Kwa hiyo, huwa tunawashauri sana wananchi tukiweka alama ‘X’ maana yake ni kwamba lile bango ulitoe mwenyewe kwa fedha zako kuliko kupata usumbufu baadaye.

Suala lingina ni kuhusu barabara ya Kibaha hadi Chalinze kwamba ni mbaya, sehemu ya Mlandizi hadi Ruvu, hivyo husababisha ajali. Barabara hii imejengwa muda mrefu na inapitisha magari mengi kuliko uwezo wake. Sasa hivi Serikali inatafuta fedha kwa ajili ya kuikarabati barabara hiyo kwa kuipanua hadi njia sita.

Kuhusu nyumba na Ofisi za Serikali kwamba ni lini zitakarabatiwa na ziwe rafiki kwa wenye ulemavu; suala hili tunalipokea na tutalishughulikia. Lingine ni kwamba maji hupita juu ya daraja karibu na TMS Old Bagamoyo Road, hivyo daraja kubwa lijengwe; jibu ni kwamba Wizara kupitia TANROADS na kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara, imekamilisha usanifu wa barabara ya Old Bagamoyo eneo jirani na bonde la mpunga kwa lengo la kujenga mifereji ya kuondoa maji yatakayotumia eneo hilo ikiwa ni pamoja na kujenga upya daraja la eneo hilo.

355 Mheshimiwa Majaliwa alisema barabara ya Nanganga - Lwangwa itengewe fedha kwa ajili ya ujenzi wa kiwango cha lami ili kuinua shughuli za kiuchumi na kijamii. Kipande cha barabara ya Nanganga - Lwangwa Mjini kilomita 1.5 hivi sasa kinajengwa kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa Assumpter Mshama anasema, Serikali iandae mpango wa kujenga barabara kwa vipaumbele na kwa awamu tuanze na zinazounganisha nchi, halafu Mikoa na baadaye Wilaya na hasa maeneo yanayozalisha mazao ambayo yanainua uchumi wa nchi. Ushauri wake tunaupokea na ndiyo maana ninasema tumeshaanza barabara zile ambazo zinaunganisha Mikoa na Mikoa na zile barabara ambazo zinainua uchumi na baadaye ndiyo tutaingia kwenye barabara ambazo ziko ndani ya Wilaya na Vijiji.

Vile vile tulipokea mchango kwamba barabara za Dar es Salaam ziwe ni kwa mpango wa BOT ili kuondoa tatizo la msongamano wa magari. Serikali imeshaanza utekelezaji wa ujenzi wa daraja la Kigamboni kwa mpango wa BOT. Kwa hiyo, ushauri wake ni mzuri na tutaendelea nao.

Mheshimiwa kwanza anatoa pongezi kwa Serikali kutoa fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara ya Sanya Juu hadi Kamwanga kwa kiwango cha lami. Anachoomba ni kwamba anamkaribisha Mheshimiwa Waziri na Naibu Waziri kutembelea eneo hilo ili kuwapa taarifa wananchi kuhusu mradi wa Sanya Juu mpaka Kamwanga. Ushauri wake

356 tunaupokea na ombi hilo linapokelewa, Mheshimiwa Fatuma Mikidadi anasema, ili kukabiliana na tatizo la msongamano, nafikiri tumeshalijibu. Kuhusu ujenzi wa barabara Kibiti - Lindi kwamba ukamilike mapema, ushauri unazingatiwa na tutasimamia kuhakikisha barabara hiyo inakamilika kwa muda uliopangwa na kulingana na mkataba.

Ombi la Serikali kujenga Kivuko Lindi Mjini kwenda Kitunda ili sehemu hii ipate usafiri wa kuaminika; Wizara kupitia Wakala wa Ufundi na Umeme TAMESA imetuma wataalamu na kuona kuwa eneo linafaa. Aidha, Wizara inatafuta fedha kwa utekelezaji wa mradi huo.

Mheshimiwa Godfrey Weston Zambi anasema kuwa barabara ya Mloo - Kamsamba yenye urefu wa kilomita 130, ijengwe kwa kiwango cha lami. Majibu, tunasema ni kweli kuwa barabara hiyo inaunganisha maeneo yenye uchumi mkubwa, mifugo na uvuvi, pia inaunganisha Mkoa wa Mbeya na Rukwa. Serikali itendelea kuifanyia matengenezo kwa kiwango cha changarawe hadi hapo itakapopata uwezo wa kifedha kujenga kwa kiwango cha lami.

Mheshimiwa - Mbunge wa Mbogwe anasema Wizara itekeleze yale yote yaliyopangwa kwenye bajeti ya mwaka 2012/2013. Wizara imejipanga kutekeleza yote ambayo yamewekwa kwenye bajeti hii. Pongezi kwa Wizara kwa kupandisha hadhi barabara ya Masumbwe hadi Butengomrasa kuwa ya TANROADS. Pongezi tunazipokea.

357 Mheshimiwa Kigola anashukuru kwa barabara ya Nyololo - Igowole - Kibaomtango kwa kuwa katika mpango wa upembuzi yakinifu. Shukurani tunazipokea na kusimamia kuhakikisha kwamba kazi hiyo inafanyika. Mheshimiwa Livingstone Lusinde, pongezi kwa Wizara tunazipokea; alisema kuna wananchi wanadai fidia kwa kubomoa nyumba ili kupisha ujenzi wa barabara ya Iringa - Dodoma ambayo bado hawajalipwa. Suala hilo tunamwahidi kwamba tutalifuatilia na kuona kama wanastahili, wananchi hao watalipwa.

Mheshimiwa aliuliza, upembuzi yakinifu wa barabara ya Mbande- Kongwa - Mpwapwa uliokuwa umepangwa umefikia wapi? Majibu ni kwamba zabuni zilishatangazwa na kufunguliwa. Kwa sasa zinafanyiwa tathmini kwa ajili ya kumpata Mhandisi Mshauri kwa ajili ya kufanya upembuzi yakinifu, na kazi hiyo itakapokuwa imekamilika, kazi ya ujenzi wa barabara hii kwa kiwango cha lami itaanza.

Mheshimiwa Kapteni Mstaafu alitoa shukrani kwa wananchi Jimbo la Newala kwa kazi nzuri inayofanywa na Wizara hii kuhakikisha Mkoa wa Mtwara unaunganishwa na Mikoa ya jirani ya Lindi na Ruvuma. Shukrani tunazipokea, pia anasema Wizara iendelee kutenga fedha mwaka huu ili kuongeza urefu wa barabara za Newala Mjini hususan upande wa kwenda Masasi hadi viwanda vya korosho.

Mheshimiwa Spika, katika mwaka huu wa fedha 2012/2013, Serikali imetenga Shilingi milioni 960 kwa ajili

358 ya kuanza ujenzi wa barabara za Mjini Newala kuelekea viwanda vya korosho.

Mheshimiwa Goodluck Ole-Medeye anaipongeza Wizara, pia anasema kutokana na hali mbaya ya barabara za Halmashauri ya Wilaya ya Arusha, anaomba upendeleo maalumu ili barabara hizo zitengenezwe ili kupitika mwaka mzima. Tunamwambia Mheshimiwa Ole-Medeye kwamba kuzipandisha barabara hizi ni lazima tufuate vigezo vilivyowekwa kwenye Sheria.

Mheshimiwa Rosweeter Kasikila anasema kasi ya utekelezaji wa miradi ya barabara kwa kiwango cha lami iongezwe ili ujenzi ukamilike kwa wakati. Barabara hizo ni ya Tunduma - Sumbawanga - Sumbwanga - Kasanga - Sumbwanga - Mpanda hadi kibaoni. Ushauri wake tumeupokea na tutasimamia.

Mheshimiwa Clara Diana Mwatuka anasema shukurani kwa Wizara kwa kujenga barabara ya Kibiti - Lindi na daraja la Mto Mbwinji – Nangoo. Shukurani tunazipokea. Vile vile kulikuwa na suala la kwamba Serikali ijenge barabara ya Mtwara - Newala - Masasi kwa kiwango cha lami. Serikali imetenga Shilingi milioni 790 katika mwaka wa fedha 2012/2013 kwa ajili ya kuanza upembuzi yakinifu na usanifu wa kina kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami mara baada ya usanifu kukamilika, tutaanza mchakato wa kujenga barabara hiyo.

Mheshimiwa Suzan Kiwanga anasema kwamba, barabara ya Kidatu - Ifakara kilomita 80 na Ifakara -

359 Mlimba hadi Madeke ijengwe kwa kiwango cha lami kutokana na umuhimu wake katika kilimo. Pia kama Waziri alivyosema, kwenye barabara katika majibu ya hoja yake, Serikali imekwishaanza mchakato wa ujenzi wa barabara hizi kwa kiwango cha lami kama ifuatavyo:-

Barabara ya Kidatu – Ifakara, Serikali imeanza mchakato wa kumpata Mhandisi mshauri kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa ujenzi wa Barabara ya Kidatu hadi Ifakara Mpaka Lumecha; barabara ya Ifakara - Mlimba Serikali itatekeleza ahadi kwa kutenga Shilingi milioni 61 kwa mwaka huu 2011/2012 na Shilingi milioni 40 kwa ajili ya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara ya Ifakara hadi Kihansi.

Mheshimiwa Spika, masuala ambayo Waheshimiwa Wabunge wengi wameongelea zaidi, ni kuomba barabara za lami. Hili ni jambo ambalo wote mnataka maendeleo, hata mimi Jimboni kwangu naomba barabara ya lami, Waziri Mkuu naye anaomba barabara ya lami, sasa tujenge uwezo wa uchumi ili barabara zote hizi tuzijenge na ziwe katika kiwango cha lami.

Waheshimiwa Wabunge, naunga mkono hoja hii na naomba ndugu zangu wote mtuunge mkono ili hoja hii iweze kupita na tuweze kufanya kazi ambazo mmetuagiza tuzifanye. Ninashukuru sana kwa kunipa nafasi.

TAARIFA

360 MHE. GODFREY W. ZAMBI: Taarifa.

SPIKA: Taarifa.

GODFREY W. ZAMBI: Mheshimiwa Spika, Naibu Waziri alipokuwa anajibu, amenitaja kama Weston Zambi. Sasa ili kuweka kumbukumbu sawa, naomba ifahamike sawasawa kuwa jina langu kamili ninaitwa Godfrey Weston Zambi. Weston ni jina la baba yangu.

SPIKA: Sawa. Kuna majina mengine pia naomba Hansard iweze kuweka sawa. Kuna mahali alitaja Mallac, siyo huyu. Yeye huyu anaitwa Ana MaryStella John Mallac. Kuna mwingine alitajwa Mheshimiwa Christopher Mtinda, lakini ni Christowaja Mtinda. Kwa hiyo, ni masahihisho hayo machache. Unajua ukishakuwa na majina mengi, inakuwa ngumu kutamka.

Waheshimiwa Wabunge, toka juzi mmeanza kuona akina mama wanakuja na kutoka hata kuwatambulisha inakuwa vigumu, maana wanabadilishana kupata nafasi katika Kumbi hizi. Hawa ni akina mama Wasabato ambao wameamua kuja kushuhudia shughuli za Bunge, kipindi hiki tulichonacho hapa. Kwa hiyo, wamekuja kwa makundi mbalimbali, siwezi hata kuwatambulisha.

Halafu tusifanye utani saa hivi! Saa 11.00 mnatakiwa kuwepo hapa. Wale wote ambao wameondoka ama wanatakiwa kuondoka hawaondoki leo, wataondoka kesho asubuhi na nitahakikisha kwamba wale ambao wameondoka

361 kuna adhabu yao itakuwepo, na mnaijua adhabu yenyewe.

Waheshimiwa Wabunge, kupitisha Wizara hizi ni muhimu, siyo wakati wa kuondoka ondoka. Wakati wa maamuzi tunatakiwa tuwe nusu au zaidi. Kwa hiyo, wale ambao wamepanga safari zao sasa hivi, naomba waahirishe mpaka kesho asubuhi kwasababu kazi yako ya kwanza ni Bunge na siyo vinginevyo. Haya mengine unayoyafanya, unafanya, lakini kazi yako ya kwanza ni Bunge. Kwa hiyo, naomba kabisa, na kama hamtakuwepo hapa, basi wote tunawajua, na hatua zitachukuliwa.

Naomba sasa nisitishe shughuli hizi mpaka saa 11.00 jioni..

(Saa 12.49 mchana Bunge lilifungwa mpaka Saa 11.00 jioni)

(Saa 11.00 jioni Bunge lilirudia)

WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, awali ya yote, napenda nikushukuru tena kwa kupata nafasi hii ili niweze kuzungumza na kuwatambua Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia katika hoja ya Wizara yangu.

Mheshimiwa Spika, wachangiaji waliochangia hapa Bungeni kwa kuongea ni Waheshimiwa Wabunge 39, waliochangia kwa maandishi ni Wabunge 144, waliochangia kwenye bajeti ya Wizara ya Fedha, Ofisi ya Waziri Mkuu na Wizara zilizotangulia

362 ni 68. Kwa hiyo, jumla ya wachangiaji wote waliochangia kuhusu masuala ya Wizara ya Ujenzi ni Wabunge 251.

Mheshimiwa Spika, nianze kuwatambua wale waliochangia kwa maandishi, nao ni hawa wafuatao:-

Mheshimiwa Gosbert B. Blandes, Mheshimiwa Felix F. Mkosamali, Mheshimiwa Mwigulu L. N. Madelu, Mheshimiwa Victor K. Mwambalaswa, Mheshimiwa Mch. Luckson N. Mwanjale, Mheshimiwa Faida Mohammed Bakar, Mheshimiwa Richard M. Ndassa, Mheshimiwa Dkt. Mary M. Nagu, Mheshimiwa Dkt. Kebwe S. Kebwe, Mheshimiwa Said J. Nkumba, Mheshimiwa Mch. Getrude P. Rwakatare, Mheshimiwa Amina Abdallah Amour, Mheshimiwa Christowaja G. Mtinda, Mheshimiwa Leticia M. Nyerere, Mheshimiwa Dunstan D. Mkapa, Mheshimiwa Hezekiah N. Chibulunje, Mheshimiwa Charles M. Kitwanga, Mheshimiwa Rashid Ali Abdallah, Mheshimiwa Henry D. Shekifu, Mheshimiwa Luhaga J. Mpina, Mheshimiwa Prof. Jumanne A. Maghembe, Mheshimiwa Ignas A. Malocha, Mheshimiwa Freeman A. Mbowe, Mheshimiwa Desderius J. Mipata, Mheshimiwa Benedict O. Nangoro, Mheshimiwa Prof. Peter M. Msolla na Mheshimiwa Selemani S. Jafo. (Makofi)

Wengine ni Mheshimiwa Rukia K. Ahmed, Mheshimiwa Abia M. Nyabakari, Mheshimiwa Aliko N. Kibona, Mheshimiwa Abdallah Sharia Ameir, Mheshimiwa Omari R. Nundu, Mheshimiwa Anna MaryStella J. Mallac, Mheshimiwa Stephen M. Wasira, Mheshimiwa Waride Bakari Jabu, Mheshimiwa Mhonga

363 S. Ruhwanya, Mheshimiwa Lucy P. Owenya, Mheshimiwa Majaliwa K. Majaliwa, Mheshimiwa Assumpter N. Mshama, Mheshimiwa Aggrey D. J. Mwanri, Mheshimiwa Fatuma A. Mikidadi, Mheshimiwa Godfrey W. Zambi, Mheshimiwa Augustino M. Masele, Mheshimiwa Mendrad L. Kigola, Mheshimiwa Livingstone J. Lusinde, Mheshimiwa Gregory G. Teu, Mheshimiwa Capt. George H. Mkuchika, Mheshimiwa Gudluck J. Ole-Medeye, Mheshimiwa Rosweeter F. Kasikila, Mheshimiwa Clara D. Mwatuka, Mheshimiwa Suzan L. Kiwanga. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Wabunge wengine ni Mheshimiwa Kombo Khamis Kombo, Mheshimiwa Amos G. Makalla, Mheshimiwa Dkt. Augustino L. Mrema, Mheshimiwa Said M. Mtanda, Mheshimiwa Ezekiel M. Maige, Mheshimiwa Nimrod E. Mkono, Mheshimiwa Abdulkarim E. Shah, Mheshimiwa Dkt. Mary M. Mwanjelwa, Mheshimiwa Moses J. Machali, Mheshimiwa Amina Mohamed Mwidau, Mheshimiwa Mkiwa A. Kimwaga, Mheshimiwa Hamad Ali Hamad, Mheshimiwa Dkt. David M. Mallole, Mheshimiwa Said A. Arfi, Mheshimiwa Yussuf Haji Khamis, Mheshimiwa John P. Lwanji, Mheshimiwa Kaika S. Telele, Mheshimiwa Abdul J. Marombwa, Mheshimiwa Ali Khamis Seif, Mheshimiwa Andrew J. Chenge na Mheshimiwa Herbert J. Mntangi. (Makofi)

Wengine ni, Mheshimiwa Agripina Z. Buyogera, Mheshimiwa Salim Hemed Khamis, Mheshimiwa Sylvester M. Mabumba, Mheshimiwa Horoub Muhammed Shamis, Mheshimiwa Mariam R. Kasembe, Mheshimiwa Martha M. Mlata, Mheshimiwa Philipo A.

364 Mulugo, Mheshimiwa Juma Sururu Juma, Mheshimiwa Faith M. Mitambo, Mheshimiwa Prof. Anna K. Tibaijuka, Mheshimiwa Cecilia D. Paresso, Mheshimiwa Eng. Ramo M. Makani, Mheshimiwa Dkt. Peter D. Kafumu, Mheshimiwa Nassib Suleiman Omar, Mheshimiwa Abdalla Haji Ali na Mheshimiwa Jason S. Rweikiza. (Makofi)

Wengine ni Mheshimiwa Ritta E. Kabati, Mheshimiwa James D. Lembeli, Mheshimiwa Albert O. Ntabalima, Mheshimiwa Juma Othman Ali, Mheshimiwa Cynthia H. Ngoye, Mheshimiwa Janet Z. Mbene, Mheshimiwa Ally K. Mohamed, Mheshimiwa Stephen H. Ngonyani, Mheshimiwa Vincent J. Nyerere, Mheshimiwa Thuwayba Idrisa Muhamed, Mheshimiwa Dkt. Festus B. Limbu, Mheshimiwa Mustapha B. Akunaay, Mheshimiwa Selemani J. Zedi, Mheshimiwa Mch. Israel Y. Natse, Mheshimiwa Eustace O. Katagira, Mheshimiwa Deo H. Filikunjombe, Mheshimiwa Aliko N. Kibona, Mheshimiwa John P. Lwanji, Mheshimiwa Angela J. Kairuki, Mheshimiwa Dkt. Antony G. Mbassa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, wengine ni Mheshimiwa Philemon K. Ndesamburo, Mheshimiwa Chacha M. Nyangwine, Mheshimiwa Jenista J. Mhagama, Mheshimiwa Rebecca M. Mngodo, Mheshimiwa Dkt. Lucy S. Nkya, Mheshimiwa Salome D. Mwambu, Mheshimiwa Maryam Salum Msabaha, Mheshimiwa Deogratias A. Ntukamazina, Mheshimiwa Salum K. Barwany, Mheshimiwa Dkt. Christine G. Ishengoma, Mheshimiwa Josephine J. Genzabuke, Mheshimiwa

365 Halima J. Mdee, Mheshimiwa Joyce J. Mukya na Mheshimiwa Esther N. Matiko. (Makofi)

Wengine ni Mheshimiwa Elizabeth N. Batenga, Mheshimiwa Prof. Kulikoyela K. Kahigi, Mheshimiwa Asha Mohamed Omari, Mheshimiwa Alphaxard K. N. Lugola, Mheshimiwa Kapt. John Z. Chiligati, Mheshimiwa John J. Mnyika, Mheshimiwa Margaret S. Sitta, Mheshimiwa Milton M. Mahanga, Mheshimiwa Felister A. Bura, Mheshimiwa Murtaza A. Mangungu, Mheshimiwa Riziki S. Lulida, Mheshimiwa Dkt. Pudensiana W. Kikwembe, Mheshimiwa Iddi M. Azzan, Mheshimiwa Joseph O. Mbilinyi, Mheshimiwa James F. Mbatia, Mheshimiwa Moza A. Saidy, Mheshimiwa Dkt, Terezya P. L. Huvisa na Mheshimiwa Sabreena H. Sungura. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, waliochangia kwa kuzungumza humu Bungeni ni Kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Anne K. Malecela ambaye ni Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu, Mheshimiwa Pauline P. Gekul, Mheshimiwa Jason S. Rweikiza, Mheshimiwa Fatuma A. Mikidadi, Mheshimiwa Dkt. Hadji H. Mponda, Mheshimiwa Zabein M. Mhita, Mheshimiwa Eustace O. Katagira, Mheshimiwa Abdul R. Mteketa, Mheshimiwa Omari R. Nundu, Mheshimiwa Mustapha B. Akunaay, Mheshimiwa Eng. Ramo M. Makani, Mheshimiwa Juma A. Njwayo, Mheshimiwa Said A. Arfi, Mheshimiwa Ignas A. Malocha, Mheshimiwa Dunstan D. Mkapa, Mheshimiwa Mendrad L. Kigola, Mheshimiwa Desderius J. Mipata, Mheshimiwa Dkt. Lucy S. Nkya, Donald K. Max, Mheshimiwa John M.

366 Cheyo, Mheshimiwa Aliko N. Kibona, Mheshimiwa Felix F. Mkosamali na Mheshimiwa Silvestry F. Koka. (Makofi)

Wengine ni Mheshimiwa Prof. Peter M. Msolla, Mheshimiwa Eugen E. Mwaiposa, Mheshimiwa Nimrod E. Mkono, Mheshimiwa Modestus D. Kilufi, Mheshimiwa Peter J. Serukamba, Mheshimiwa Freeman A. Mbowe, Mheshimiwa Mch. Peter S. Msigwa, Mheshimiwa Mhonga S. Ruhwanya, Mheshimiwa Jenista J. Mhagama, Mheshimiwa Haroub M. Shamis, Mheshimiwa AnnaMaryStella J. Mallac, Mheshimiwa Faith M. Mitambo, Mheshimiwa Stephen H. Ngonyani, Mheshimiwa James F. Mbatia, Mheshimiwa Rajab Mbarouk Mohammed, pamoja na Mheshimiwa Eng. Gerson H. Lwenge - Naibu Waziri wa Wizara ya Ujenzi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwanza kabisa, napenda niseme kwa dhati kabisa kwamba Waheshimiwa Wabunge wote waliochangia katika hoja ya Wizara ya Ujenzi wa Chama cha Mapinduzi, wa upande ule wa Upinzani, kwa ujumla wametoa michango yao mizuri sana nami nawapongeza sana. Kwa sababu michango yao mingi ilikuwa ni ya kutoa ushauri na mimi nasema kwa dhati kabisa kwamba Wizara yangu na sisi Watalaam kwa ujumla tumeipokea, tutaifanyia kazi katika kuhakikisha kwamba tunaiboresha zaidi, ili katika nyakati nyingine zinazokuja ushauri wote uliotolewa na Waheshimiwa Wabunge wote bila kujali itikadi zao za Vyama, tutayazingatia ili kuhakikisha kwamba Sekta ya Miundombinu inaendelea kufanya kazi vizuri zaidi na zaidi. Kwa hiyo, nawapongeza sana.

367 Mheshimiwa Spika, kwa maneno ya jumla, nchi yetu ni kubwa, ina jumla ya kilomita za mraba 949,000. Katika barabara ambazo ziko chini ya Wizara ya Ujenzi ni zaidi ya kilomita 35,000. Katika Kilomita hizo, zaidi ya kilomita 12,786 ndizo zinaitwa barabara kuu (Trunk Roads). Kilomita zaidi ya 22,214 ndizo zipo katika upande wa Regional Roads, zile nyingine zilizobaki ndiyo District Roads, Feeder Roads, na barabara nyingine zilizoko Vijijini.

Mheshimiwa Spika, ukiangalia hali halisi ya mtandao katika nchi yetu, napenda kuthibitisha mbele ya Bunge lako kwamba kuna kazi kubwa sana ambazo zinafanyika. Katika mtandao mzima wa barabara hadi sasa hivi, karibu zaidi ya kilomita 11,154 ndizo zinashughulikiwa katika kutengenezwa kwa kiwango cha lami.

Katika bajeti hii kwa ujumla, tumejitahidi sana ku- focus katika maeneo ambayo kwa ukweli yalikuwa hayana barabara nyingi za mtandao wa barabara za lami. Ndiyo maana ukichukua kwa mfano Mkoa wa Geita na Kagera, hata fedha za miradi inayoendelea kule kwa kujengwa kwa kiwango cha lami zimepungua. Hii ni kwa sababu barabara ya kutoka Geita mpaka Mtukura yote ni lami. Utaona pia kwamba katika Mkoa wa Mwanza karibu barabara zote kuu ni lami isipokuwa barabara moja ambayo ni kilomita 17 inayotoka Kisesa hadi Usagara, katika trunk Roads.

Mheshimiwa Spika, ukienda pia Mkoa wa Mara, barabara ambazo ni trunk roads zote ni lami isipokuwa

368 barabara ya kutoka Makutano, Fort Ikoma, hadi Mugumu ambayo ndiyo trunk roads. Ukienda Mkoa wa Kilimanjaro, barabara zote trunk roads ni lami, lakini hata ukienda Dar es Salaam pamoja na kwamba kuna matatizo mengi ya msongamano, lakini barabara zote ambazo ni trunk roads ziko chini ya TANROADS ambazo ni kilomita 140.4 zote ni lami. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ukienda Lindi barabara zote ambazo ni trunk roads ni lami ukiacha sehemu ambayo imebaki kutoka Somanga kuja kwenye daraja la Mkapa. Kwa hiyo, tumejaribu ku-focus katika maeneo mengine ambayo yalikuwa hayajafunguliwa kwa barabara za lami.

Mheshimiwa Spika, katika miaka miwili iliyopita Mkoa wa Rukwa na Katavi, ulikuwa na kilomita 14 tu za barabara ya lami, nazo zilikuwa ni zile za madaraja yaliyojengwa chini ya ufadhili wa World Bank. Mkoa wa Kigoma ulikuwa na kilomita 12 tu za lami pale Mjini, Mkoa wa Tabora ulikuwa na kilomita 100 nazo zipo kwa pembeni, ukianzia Nzega unakwenda mpaka Igunga mpaka Shelui labda na Tabora Mjini ambako palikuwa na kilomita kama tatu hivi za lami. Eneo lingine lote halikuwa na barabara za lami. Kwa hiyo, tumejaribu ku- focus katika maeneo hayo ili angalau nchi hii iweze kuwa reflected katika barabara za lami na hasa katika barabara kuu.

Mheshimiwa Spika, ndiyo maana utaona ukichukua Mkoa wa Kigoma, ukachukua na Mkoa wa Tabora, miradi iliyopo inayotengenezwa kwa barabara za lami ina-cost Shilingi bilioni 623.

369

Mheshimiwa Spika, nilimshangaa sana Mheshimiwa Mkosamali aliposema kwamba Mkoa wa Kigoma unaonewa, nikaona wakati mwingine hata majina yanafanana; kwa sababu hata ukipewa bado unaweza ukaamini tu kama hakipo. Kwa sababu kutoka Kigoma hata ukitoka Mwandiga kwenda Manyovu kwenye mpaka wa Burundi, mimi nimefika kule. Kilomita 60 zimefunguliwa na Mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete, ni lami. Lakini ukienda kwa upande wa Burundi, hakuna lami.

Mheshimiwa Spika, ukitoka pale Kigoma uje kuelekea barabara ya Uvinza ni lami, kuna kandarasi anafanya pale kilomita 76.6, lakini ule mtandao wote unakuja unatokea Nzega kuna Makandarasi. Ile portion iliyokuwa imebaki kwa Mheshimiwa Kapuya, ile barabara ya kutoka Kaliua kwenda Irundi nayo imetangazwa leo kwa ajili ya kuanza kujenga. Mkisoma kwenye magazeti ya leo, mtaona. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, unaona katika Mikoa hii ina fedha nyingi, lakini ukichukua Mkoa wa Rukwa pamoja na Katavi nao katika bajeti hii miradi inayoendelea ni Shilingi bilioni 589. Tumefanya hivyo kwa makusudi ili tuweze kuifungua kutoka Tunduma mpaka Sumbawanga ambako kuna jumla ya kilomita 231. Tufungue Sumbawanga mpaka Kisesa Kilomita 112 kwa lami, pote kuna Makandarasi; lakini tufungue kutoka Sumbawanga mpaka Mpanda na ikiwezekana ifike mpaka Mishamo kutoka pale Mpanda. Lengo letu ni kuunganisha ile barabara mpaka Uvinza ambayo ni trunk road. Lakini ikiwezekana pia tuunganishe ile

370 barabara kutoka Katavi ije mpaka Tabora ikipitia Sikonge kwa Mheshimiwa Nkumba. Hilo ndilo lengo letu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini ukienda Mkoa wa Mtwara na Ruvuma, napo kuna fedha nyingi zaidi ya Shilingi bilioni 580. Lengo ni kutaka kufungua ile sehemu ya kutoka Masasi - Mangaka ambayo ndiyo imekamilika kutengenezwa kwa lami. Kutoka pale Mangaka mpaka Mbamba Bay zaidi ya kilomita 667 ziwe ni lami zote. Ndiyo maana tumeweka Makandarasi pale wengi, lengo ni kuhakikisha hii Mikoa ambayo kwa siku nyingi watu wa maeneo yale wengine hata walikuwa hawajui rangi ya lami. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, tunafanya hivyo kwa maksudi kwa sababu Serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete ni Serikali ya Watanzania wote bila kubagua hata Vyama. Ndiyo maana hata Mheshimiwa Freeman Mbowe alikuwa anaomba hapa barabara. Hii ni kudhihirisha kwamba CCM ndiyo watawala, na ndiyo wenye barabara, na ndiyo wenye pesa. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, nami nimempongeza sana Mheshimiwa Mbowe, hata michango yake ni mizuri sana; ametambua kwamba bila CCM hata barabara yake haiwezi ikatengenezwa na anatingisha kichwa kwa kuonesha kwamba anakubali. Bahati nzuri ni rafiki yangu sana, nampenda sana. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, katika suala la Dar es Salaam, hili suala ni very complex. Ninafahamu michango ya

371 Wabunge kweli ni very concerned. Kutoka Upinzani, CCM michango yao yote ni mizuri sana. Lakini katika juhudi za Serikali ambazo zimefanywa, Mkoa wa Dar es Salaam tu miradi inayoendelea sasa hivi ina thamani ya Shilingi bilioni 899. Sasa Shilingi bilioni 899 investment yote ambayo iko Dar es Salaam, si kitu kidogo!

Mheshimiwa Spika, miradi yote nimeitaja hapa kwenye kitabu change. Kuna mradi ule wa BRT ambao kandarasi yuko pale Strasburg ameshaanza kufanya kazi. Ukikusanya na vile vituo pamoja na vituo vingine 29, kuna mini flyovers zaidi ya tatu.. Ni zaidi ya Shilingi bilioni 290 ambayo itahusisha kutoka Kimara kuja Fire kwenda Kariakoo kwenda Kivukoni na kuja kuunganisha mpaka Morocco pale. Katika maeneo mbalimbali, ile barabara itapanuliwa kuwa na njia tatu. Lakini kwenye maeneo ya Fire patakuwa na njia nane wala siyo mbili, wala siyo tatu. Ni njia nane! Kwa hiyo, wiki hii vitu hivi siyo vidogo. (Makofi)

Ukitoka Mwenge kwenda Tegeta kuna Shilingi bilioni 88 zimewekwa pale, na njia ile inapanuliwa kwa njia nne pamoja na service road. Lakini ukitoka Mwenge tena kuja Morocco pale kilomita 4.1. Katika bajeti ya mwaka huu, tumetenga fedha na penyewe patapanuliwa njia. Tunatengeneza daraja la Kigamboni Shilingi bilioni 240, tunaunganisha kutoka Barabara ya Kilwa mpaka Kariakoo kuna Shilingi bilioni 6.6, tumeweka pale, zitapanuliwa njia nne. Tumechukua barabara ndogo ndogo za Dar es Salaam ili ziweze kuhudumiwa na TANROAD moja kwa moja. Kuna Shilingi bilioni nne point something, TANROAD yenyewe Mkoa wa Dar es Salaam kuna

372 Shilingi bilioni 18, tumeamua tuanze kufanya usafiri wa majini. Tulivyopandisha bei ya vivuko watu wengine walilalamika. Mwaka huu ilikuwa tutegemee kukusanya Shilingi bilioni tano, mwaka huu tunakusanya Shilingi bilioni 7.9 na fedha nyingine tutazinunulia kivuko ambacho kitaanza kufanya kazi kutoka Dar es Salaam mpaka Bagamoyo tupunguze msongamano kwa ajili ya watu wa Dar es Salaam. Kuna vituo zaidi ya saba vinajengwa. (Makofi)

Sasa ukichukulia kwa ujumla, ndio unaweza ukaona kwamba kuna investment kubwa ambayo inafanyika. Sitaki kuitaja miradi yote kwa sababu ninajua time haitaniruhusu. Lakini nasema kwa dhati kwamba juhudi kubwa zinafanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi katika kuhakikisha kwamba barabara zinatengenezwa kwa kiwango cha lami.

Mheshimia Spika, wakati tunapata uhuru tulikuwa na kilomita 1300 tu. Katika miaka 50 yote iliyopita tulifikia kilomita 6,500; leo kilomita zinazojengwa ni 11,154. Kwa hiyo, baada ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete tutakuwa na kilomita karibu 17,000 za barabara za lami. Barabara hizi za lami ungezipeleka Burundi au Rwanda wangekosa mahali pa kulima kwa sababu ingekuwa kila mahali ni lami. (Makofi)

Kwa hiyo, juhudi ni kubwa sana zinazofanywa na Serikali ya Chama cha Mapinduzi inayoongozwa na Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete katika kutengeneza barabara katika nchi hii. (Makofi)

373 Mheshimiwa Spika, nimesema katika suala la Dar es Salaam ni very complex na mimi nataka niwe muwazi, na nataka nizungumze kwa ukweli. Ujenzi wa Barabara za Dar es Salaam zina matatizo sana. Unaweza ukatengeneza barabara, ukatengeneza service road; service road humo humo ndiyo watu wanafanya biashara; service road humo humo ndiyo magereji; lakini viongozi wapo wanaohusika na maeneo hayo. Nakumbuka Mheshimiwa Freeman Mbowe anasema hapa service road ni vizuri zikaachwa. Mimi nakubaliana naye kwamba watu wasifanye biashara kwenye service road.

Mheshimiwa Spika, kwenye masuala ya barabara, tuache siasa. Sheria zimepitishwa hapa ikiwemo Sheria Na. 13 ya mwaka 2007 na Sheria hii ya Road Reserve imeanza tangu mwaka 1932. Sasa ni vizuri tufike mahali tusimamie sheria. Kwa sababu huwezi ukajenga barabara wakati watu wengine wako kwenye barabara. Ni lazima tufike mahali tuamue, hata kama ni kwa machungu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, siku moja nilisema jengo la TANESCO liko kwenye road reserve, siyo uongo, liko kwenye road reserve! Hata kama nisipolibomoa mimi, siku moja litabomolewa tu unless tubadilishe sheria. Hata kama ni jengo la Serikali, ukweli unabaki pale pale, unless tufike siku moja tubadilishe sheria zetu kwamba kwa barabara za Dar es Salaam upana wake sasa utakuwa ni upana wa kupita bajaji. Lakini kama hii sheria ipo iliyopitishwa na Bunge, itabaki ni vile vile. (Makofi)

374 Tunapozungumzia kutengeneza barabara, hakuna sababu tena ya mtu mwingine anakwenda kupachika mabango barabarani. Wenzetu Kenya waliamua kabisa kuwa na Wizara inayoshughulikia Nairobi peke yake, wameweza kutengeneza flyover moja ya kutoka Theca mpaka Nairobi barabara nane kwenda juu. Inawezekana katika siku zinazokuja ni vizuri basi labda barabara zote za Dar es Salaam tukichukua mfano labda zisimamiwe tu na TANROAD. Hayo ni mawazo yangu, ili kusudi tunapoamua kuchukua hatua iwe ni hatua ya mwisho, pasitokee mtu mwingine wa kuingilia huku, ili kusudi mtu akishindwa kutengeneza barabara, apatikane mtu wa kulaumiwa mmoja. (Makofi)

Sasa hizi ndizo challenge tunazozipata kwa Dar es Salaam. Kwa sasa hivi tunataka kujenga Dar es Salaam Express Road ya kutoka Dar es Salaam kuja Chalinze kilomita 100 na kutoka Chalinze kuja mpaka Morogoro njia sita. Wawekezaji wameshajitokeza wengi kwa kujenga kwa PPP. Problem tunayoi-face, watu wamejenga kwenye road reserve na wapo hata wanasiasa wengine wanasema wafanyie biashara humo humo, watafanyia wapi? Hao hao ndio wamepitisha hiyo sheria. Wengine wako hapa, message sent and delivered. Nasema kwa uwazi kabisa. Siyo Mheshimiwa Mbowe! Mheshimiwa Mbowe anasimamia vizuri sana. (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, sasa ifike mahali kama tunataka kupunguza msongamano kwa Jiji la Dar es Salaam ambapo kwa magari yaliyosajiliwa yako zaidi ya milioni moja, ni lazima tuanze kuchukua hatua na vyama vyote tushirikiane kama ushirikiano

375 ulioonyeshwa kwenye Bunge hili, na kuunga mkono bajeti hii na ndiyo maana nimesema nawapongeza sana leo Wapinzani, wabarikiwe kabisa na Mwenyezi Mungu, kwa sababu wametoa mawazo mazuri tu. Kwa mwendo huu Serikali hii itakwenda vizuri, kwa sababu sasa tunapata mawazo mazuri kutoka Upinzani, wanazungumza wametulia, very constructive, Msemaji wa Barabara naye amezungumza vizuri, mama Yule; tukaona sasa CCM tuna-support tu, tunakwenda vizuri. CCM Hoyeee! CHADEMA Hoyee, kwa kuunga mkono hoja hii; CUF Hoyee! UDP Hoyee! TLP Hoyee! NCCR Hoyee! Na wengine wote. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, kwa sababu tunajenga nchi ya umoja kwa ajili ya maendeleo ya Watanzania, bahati nzuri barabara hazina siasa, wa CHADEMA atapita mle mle na wakati mwingine atafanya maandamano sawa sawa tu, vizuri, akaenda na atapita mpaka mwisho; Wa CCM atapita mle mle, wa CUF atapita mle mle, ndiyo uzuri wa barabara. Barabara inatuunganisha wote Watanzania. Ndio maana ninasema kwa dhati kabisa michango mikubwa sana iliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge leo naipongeza sana, na watalaam wangu wameichukua na tutaifanyia kazi bila kujali imetolewa na upande gani, kwa sababu lengo ni kutafuta solution ya matatizo yanayoikabili nchi yetu. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, sina uhakika kama ni muda mwingi sana, lakini labda nianze kujibu hoja zilizokuwa zikitolewa na Waheshimiwa Wabunge. Mheshimiwa Anne Kilango ametoa pongezi, amezungumzia juu ya masuala ya madeni. Bahati nzuri juzi tumemaliza

376 madeni yaliyokuwa yanadaiwa na makandarasi. Zimelipwa Shilingi bilioni 300 na Serikali. Issue yangu hapa ni kwamba makandarasi huwa wanalipwa certificate wanazofanya. Hakuna fedha utakayolipwa bila kufanya kazi. Mkandarasi yeyote anapokuwa kwenye site ni lazima a-produce certificate. Bila certificate huwezi ukalipwa fedha.

Kwa hiyo, wito wangu kwa makandarasi, wafanye kazi sana ili kusudi certificate watakazokuwa wanazileta Wizarani waweze kulipwa madeni yao. Ikiwezekana wamalize mapema kazi zao.

Pia kuna hoja kwamba miradi inayogharamiwa na Serikali isimamiwe na makandarasi wetu. Hili tumeanza na huu ulikuwa ni ushauri wa Kamati ya Miundombinu kuanzia mwaka 2011. Tumeanza na Daraja la Mbutu, sasa hivi kuna makandarasi wazalendo 13 wameungana wanatengeneza lile daraja kwa Shilingi bilioni 12.5 na hata hata cost zimekuwa chini zaidi kwa sababu kama tunge-involve Makandarasi wa nje ingegharimu zaidi ya Shilingi bilioni 20 hadi 25. Kwa hiyo, kutumia Wakandarasi wa ndani tuna-serve fedha. Lakini hata zile fedha kwa sababu ni Makandarasi wa ndani, zinakuwa na multiplying effect, akitoka pale anaweza akaenda kwa akina Mbowe akaenda akaoa akatoa mahari kwa sababu ni kandarasi wa humu humu. Anaweza akaenda kwa Wafipa kule akafanya hivyo hivyo. Kwa hiyo, ile fedha inabaki humu kuliko kandarasi wa nje. (Kicheko/Makofi)

377 Kwa hiyo, hili ni ushauri mzuri ambao ulitolewa na Kamati ya Miundombinu, tunawapongeza sana na tumeshaanza kufanya kazi. (Makofi)

Kuhusu msongamano wa magari, nimeshalizungumzia na hatua tumeshaanza kuzichukua, nimezieleza kwa kirefu sana katika hotuba yangu. Kuhusu matatizo ya mizani, tumeyaona kwa mfano, matatizo ya mizani pale Kibaha kwamba nayo inaweza ikawa chanzo cha kuleta msongamano katika Jiji la Dar es Salaam.

Mheshimiwa Spika, ule mzani wa Kibaha tunauhamisha, tunaupeleka eneo moja linaitwa Migwaza. Katika bajeti ya mwaka huu tumetenga fedha zaidi ya Shilingi milioni 4000 na kitu. Ule mzani tutakaoujenga Migwaza magari, yatakuwa yanapimwa huku yakiendelea kusafiri, hayatakuwa yanasimama. Kwa hiyo, ni mzani wa kisasa zaidi. Tumeweka fedha kwa ajili ya kuweka huo mzani. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, pia imezungumziwa TEMESA, kuhusu TBA kwamba ijenge nyumba za kuwakopesha wafanyakazi na kadhalika. TBA wameanza hii kazi, ndiyo maana katika bajeti ya mwaka huu wana miradi zaidi ya bilioni 101. Lakini pia watafanikiwa kupata mkopo wa zaidi ya Shilingi bilioni 180,000 ambapo wataanza kujenga nyumba katika miradi yao ya nyumba 10,000. Wataanza katika mwaka huu kujenga nyumba 2,500 katika Mikoa yote. TBA imeanza na ndiyo maana nasema kwamba wanaendelea vizuri na

378 palikuwa na matatizo kidogo kule, tumeanza kufanya reforms.

Msemaji wa Kambi ya Upinzani amezungumza vizuri tu, michango yake ni mingi, mizuri, na ndiyo maana nasema kwa kweli nilitakiwa tu niseme hapa, halafu nisimame, halafu nimalize nikakae, halafu watu wakamaliza tu, wakapitisha, tukaondoka, tukaenda kupumzika. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Msemaji wa Upinzani alizungumzia juu ya ubora wa barabara kwamba umepungua kidogo. Nasema haujapungua, lakini ikumbukwe pia kwamba katika barabara zilizokuwa za Halmashauri zaidi ya kilomita 4,400 zimerudishwa TANROAD. Kwa hiyo, nguvu zimekuwa nyingi zaidi za kushughulikia.

Suala la kwamba barabara nyingi zimekuwa zikijengwa chini ya kiwango; ni barabara chache. Unapokuwa na mradi wa kilomita 11,000, usitegemee kwamba wote watakuwa waaminifu. Hatufanyi kazi na malaika. Ndiyo maana barabara ya Kilwa ilipokosewa na Kampuni ya Kajima, tuliwaambia warudie, na sasa hivi wanarudia kwa gharama zao wenyewe. Barabara ya Sekenke kwenda Selous tumeshamu-instruct Consultant pale Kampuni ya Ufaransa pamoja na contract Chiko, sasa hivi wameanza kufanya mobilization, wanarudia kwa gharama zao ili kusudi wajifunze kwamba Tanzania siyo mahali pa kuja kuchukua na kuondoka. Kumrudisha Mkandarasi kwenda kurudia ni kazi ngumu inahitaji moyo na ndiyo maana wakati mwingine tunaugua mara moyo, mara

379 nini, lakini potelea mbali wakafanye tu kazi, shauri yao kule! Kwa hiyo, tunaendelea hivyo. (Makofi/Kicheko)

Barabara ya Nangurukuru - Mbwemku, Mkandarasi aliyemaliza pale ilibidi kazi airudie kazi kwa gharama zake. Lakini katika kila barabara inayotengenezwa na kukamilika huwa kuna grace period ya kati ya mwaka mmoja na miaka mitatu ya kukaa pale Mkandarasi anaiangalia. Tumeshawa- instruct mainjinia wetu kwamba ni lazima wasimamie hivyo. Katika siku zinazokuja, barabara itakayofeli kwa Mkoa fulani na wakati kuna Regional Manager kule, Regional Manager yule atakuwa amepoteza kazi ili kusudi wajifunze kusimamia barabara zilizo kwenye maeneo yao. Ni hatua ngumu kidogo, lakini ni lazima tufanye hivi ili kusudi tushikane vizuri, barabara zetu ziweze kutengenezwa kwa standard zinazotakiwa. (Makofi)

Pia kuna hoja kwamba miradi 26 haikupelekewa fedha. Miradi yote imepelekewa fedha. Tuna miradi zaidi ya 120. Sasa ina-depend yule mkandarasi alivyokuwa anafanya kazi. Aliyefanya kazi kidogo, amepelekewa fedha kidogo; aliyefanya kazi sana na certificate nyingi, amepelekewa fedha nyingi.

Mheshimiwa Spika, kuna hoja inayosema barabara nyingi zinachelewa kukamilika. Sina uhakika sana kwa sababu barabara inapoanza kujengwa ina process zake. Kuna feasibility study, kuna detail design, muda unakwenda, unakwenda kwenye construction. Ukishatangaza tenda, ni lazima ufuate masharti ya sheria za PPR. Lakini akishakwenda mtu kwenye site, ni

380 lazima apewe miezi isiyopungua sita kwa ajili ya kufanya mobilization. Kwa hiyo, mpaka ukija kufikia mkandarasi anafanya kazi na kumaliza, sometime zinachukua time. (Makofi)

Kuhusu special road construction kwamba Serikali ikamilishe ujenzi wa barabara zilizobaki, tutakamilisha. Ndiyo maana tunaomba wenzetu mtupitishie hii bajeti ili kusudi tuendelee kuzikamilisha. Msipopitisha hii bajeti, hatutakamilisha. Tutakamilisha lini? Lakini nashukuru kwamba Wabunge wote wa Upinzani waliokuwa wanachangia wameunga mkono hoja hii. Wengine hawakutaka kutamka kwa hadharani hapa, lakini wameandika kwa maandishi. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, kuna hili sakata la bomoabomoa, tumeshauriwa kwamba Serikali isitumie sheria tu. Sasa kwa nini tunapitisha sheria? Kama sakata la bomoabomoa tusitumie sheria tu, kwa nini tunapitisha sheria? Tuache kupitisha sheria humu! Actually wa kulaumiwa zaidi kuhusu bomoabomoa ni Wabunge mliopitisha hii sheria. Wala sio Magufuli, wala sio Serikali, kwa sababu kazi ya Serikali ni kutekeleza Sheria. Sheria hii imeanza tangu mwaka 1932 ikafanyiwa amendment mwaka 1939, ikafanyiwa amendment mwaka 1949, ikafanyiwa amendment mwaka 1954, ikafanyiwa amendment mwaka 1967 kupitia Cap. Namba 167 na ikatangazwa tarehe 6 Juni, 1967, imefanyiwa amendment mwaka 2007 kupitia Sheria namba 13. Yote inazungumzia upande wa barabara ni lazima uwe mita 30. Sasa tutatengenezaje barabara kama hakuna sheria hii? Ni lazima Watanzania na wapiga kura wetu tuwaeleze ukweli.

381 Mimi kuna wakati fulani kwenye Jimbo langu nilibomoa nyumba 157, nikaenda nikawaambia ninabomoa hizi nyumba, najua nitakosa kura za watu 157 na wake zao. Kwa hiyo, ni kama watu wa 300 na kitu. Mmoja niliyembomolea akazungumza kwenye Mkutano, akasema: “Mimi nitakupa kura.” Katika mwaka ule nilipita bila kupingwa. (Makofi)

Kwa hiyo, Watanzania wanaelewa kwa sababu wanapenda maendeleo. Ni lazima tufike mahali Watanzania tuwaeleze ukweli, hata kama ukweli ule unauma. Msema kweli ni mpenzi wa Mungu. Lakini ni ukweli pia katika hii sheria tumeona kuna maeneo fulani ambayo ni lazima tuyapitie ili kama patahitajika kufanya amendment tutazileta hapa Bungeni. Maeneo yale ni maeneo ya milimani. Ukienda kwa Mheshimiwa Mama Malecela pale na maeneo mengine ya milimani, kwa kweli ukichukua mita 30 zote, saa nyingine ni kuwapa punishment wananchi wale. Kwa hiyo, tutaangalia, tutatuma committee ya mainjinia na watalaam wapitie maeneo yote ambayo kwa kweli kwa msingi ule kwamba tunatakiwa kutengeneza barabara, tuangalie ni kwa namna gani tunaweza tukafanya mabadiliko. Lakini wale ambao wako sehemu pana, waondoke tu kwenye road reserve, watuachie tutengeneze barabara. Huo ndiyo ukweli na ukweli utabaki pale pale. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, kuna hoja kwamba fedha za TBA ni kidogo. TBA inatakiwa kujiendesha kibiashara na ndiyo maana tumewaambia kwa mwaka huu waanze kukopa benki na bahati nzuri kupitia Benki Kuu

382 wameanza kupata mwelekeo mzuri wa kuweza kupata benki ili kusudi wajenge nyumba zaidi.

Hoja nyingine ni TEMESA, kuhusu sera ya magari. Hilo nalo limezungumziwa. Mheshimiwa Rweikiza, kwanza amesema haungi mkono hoja na mimi nikasikatika kidogo, Mzilakende mwenzangu, Mbunge mwenzangu kutoka Kagera, anakataa kuunga mkono! Wengine wote wameunga mkono, mpaka wa Upinzani, yeye tu ndio amekataa! Anasema, kwa sababu barabara moja inayotoka Bukoba kwenda Kabango Bay haijajengwa kwa lami. Katika Mikoa ambayo barabara zake zote trunk road ni lami, ni pamoja na Kagera. Kutoka Bukoba mpaka Mtukura ni lami, ndiyo zilianza kujengwa.

Sasa huwezi ukajenga barabara za lami mbili zinazofuatana zote zinakwenda kwenye direction moja. Ukajenga Bukoba kwenda Kabango Bay lami, halafu ukajenga Bukoba kwenda Mtukura zote zinakwenda mpaka Uganda, lami, wakati wengine Wafipa kule hawajawahi hata kuona lami; wakati barabara ya kutoka Mbamba Bay ambayo ni trunk road hawajawahi kuona lami, wakati barabara za Tabora hakuna lami, wakati barabara ya kutoka Dodoma Makao Makuu ya nchi kwenda Iringa haijakamilika kuwa lami, wakati barabara ya kutoka hapa kwenda Babati, Arusha sio lami. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, huo ndiyo ukweli na ukweli unabaki ukweli. Kwa hiyo, hii barabara haijengwi sasa hivi kwa lami. Huo ndiyo ukweli na mimi nakueleza

383 kabisa ndugu yangu, haitajengwa kwa lami sasa hivi. (Makofi/Kicheko)

Tumalize sehemu nyingine, tutakuja kujenga, lakini pia mkataba uliowekwa kwenye barabara hii, hawakuweka TANROAD au Wizara ya Ujenzi, aliweka RAS wa Kagera mkataba mwaka 2008. Alimweka Kandarasi aliyekuwa anaitwa kwanza consultant, ilikuwa ni ITEKO na Kandarasi alikuwa ni kampuni moja inaitwa JESSEY, kwa gharama ya Shilingi bilioni 47. Katika mikataba ya Mkoa, hata Meneja wa TANROAD haruhusiwi kuweka mkataba wa zaidi ya Shilingi bilioni mbili. Ninafahamu Mheshimiwa Cheyo atalifuatilia hili. Limeshafika, basi limefika kwake. Shilingi bilioni 47, mwaka 2008, Ofisi ya RAS ya Mkoa baadaye ikakosa hizo hela, ikabidi wa-terminate ule mkataba mwaka 2010 na wanadaiwa fedha tu nyingine bila kufanyika kazi. Sasa nilitegemea Mheshimiwa Rweikiza akatoe Shillingi kwenye TAMISEMI, siyo Wizara ya Ujenzi kwa sababu RAS yuko TAMISEMI. Lakini akawaachia TAMISEMI wakapitisha bajeti yao, anakuja ananishikilia mimi. Ni kunionea! (Kicheko/Makofi)

Mheshimiwa Spika, lakini pia Mheshimiwa Rweikiza alizungumzia barabara nyingine ya kwenda Kijiji ambacho bahati nzuri nimewahi kufika kule, Kijiji cha Kyamalange na Mwenyekiti wa Kijiji kule anaitwa Mzee Kiaruzi. Nilipokuwa Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na Uvuvi, nilifika kule kuweka mradi mmoja uliokuwa unasimamiwa na Lake Victoria Fisheries Organisation kwa ajili ya masuala ya uvuvi. Barabara ya kwenda kule ni ya TAMISEMI kilometa tano, nayo ananishikia mimi Shilingi. Nilitegemea angalau angeweza

384 akaomba niipandishe hadhi kwa kutumia Sheria Namba 13 ya mwaka 2007, hata hajaniomba kuipandisha, ameshashika Shilingi. Kwa hiyo, na hiyo barabara siichukui kwa sababu hai-qualify Sheria Namba 13 ya mwaka 2007. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Spika, ni lazima tufike tuambizane ukweli! Alitakiwa ashike Shilingi ya TAMISEMI, siyo ya Wizara ya Ujenzi, kwa sababu waliohusika kuweka mkataba ule ni RAS. Ninashukuru PSE wanalifuatilia hilo.

Mheshimiwa Spika, mimi ni wa Kagera, lakini ni lazima niseme ukweli kwamba Kagera wana barabara nyingi pia za lami, na katika Wilaya ya Bukoba wana kilometa 48.4, mpaka hata kwenye ile barabara ya kutoka Katerero ukapitie pale Kyana - Basa, ukaenda Lutela - Ng’oma kule. Maendeleo ya barabara, napo pameshajengwa kilometa kama tano za lami. (Kicheko/Makofi)

MBUNGE FULANI: Wapi?

WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, lakini pia kuna ushauri mzuri tu umetolewa na Mheshimiwa Rweikiza, amesema Wizara hii iimarishe sana miundombinu ya reli ambapo tutazungumza na wenzetu wa mawasiliano. Kwa ujumla, mimi namwomba tu Mheshimiwa Rweikiza aunge mkono angalau hata yale maombi tuliyoyatoa kule tuweze kuanza kuyafikiria. Lakini barabara hii katika bajeti ya mwaka huu tumeweka zaidi ya Shilingi milioni 225.711, akisoma kwenye ukurasa wa 265 wa hotuba yangu,

385 atakuta fedha zile tumeziweka kwa ajili ya kufanya rehabilitation kwa kiwango cha changarawe.

Mheshimiwa Fatuma Mikidadi ameunga mkono hoja kwa asilimia mia moja, na mimi namshukuru sana. Alisema wiki hii barabara ya Kibita anaomba ikamilike. Tunasema tutaikamilisha kwa sababu mpaka sasa hivi Mkandarasi ameshapewa zaidi ya Shilingi bilioni 45, zilizobaki tena hata juzi amelipwa. Ni kwa bahati mbaya sana katika mradi ule wa kilometa 60, waliokuwa wafadhili wetu Kuwait Fund hawakuweza kutoa fedha zozote. Kwa hiyo, ikabidi tutumie malipo yote ya Mkandarasi kwa kutumia fedha za ndani. Tumejipanga vizuri, barabara hii itakamilika mwaka huu ili watu wawe wanatoka Dar es Salaam mpaka Lindi – Mingoyo - Mtwara kwa bajaji. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Mikidadi pia alizungumzia pia kuhusu mradi wa OPEC Fund. Mradi ule ulikamilika mwaka 2010. Kwa hiyo, miradi sasa hivi inayotengenezwa, inatengenezwa kwa fedha za Mfuko wa Barabara pamoja na za Wizara. Amezungumzia pia kuhusu barabara zilizopandishwa hadhi, maeneo ya barabara yake. Nampongeza sana Mheshimiwa.

Mheshimiwa Mponda aliunga mkono hoja, akazungumzia juu ya Morogoro kwamba ni eneo la chakula, na mimi nakubaliana naye kabisa. Amezungumzia juu ya kushukuru Serikali kwa kutenga fedha za kutosha kwa ajili ya ujenzi wa Daraja la Kilombero na mimi ninashukuru, kwa sababu ile ni ahadi ya Mheshimiwa Rais na ndiyo maana lile daraja

386 likajengwa kwa Shilingi bilioni 55. Lakini pia hata ile barabara nyingine inayokwenda kuunganisha mpaka kule Songea, zaidi ya kilometa 300 na kitu nayo itaanza kufanyiwa feasibility study kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami. Katika bajeti ya mwaka huu, tumeweka zaidi ya Shilingi milioni 1000 na kitu.

Mheshimiwa Mponda pia alizungumzia suala la kivuko, kwamba kimechakaa. Tunaelewa, lakini kwa sababu sasa tunajenga daraja, kile kivuko hakitatumika tena.

Mheshimiwa Mhita ametoa pongezi hasa kwa barabara za lami ambazo zimepangwa na barabara yake ya kutoka Bonga kuja Mayamaya kilometa 188.9. Fedha zipo chini ya African Development Bank, tutahakikisha tunapata Makandarasi wazuri, tutaigawanya katika sehemu mbili ili barabara hiyo nayo iweze kutengenezwa. Ile barabara ndiyo sehemu ya The Great Northern Road ambayo alikuwa anaizungumza Mheshimiwa Mbatia, ambapo katika sehemu iliyokuwa imebaki kutokea Cairo hadi Cape Town ilikuwa imebaki kutoka Bongo Mayamaya na kutoka Dodoma kwenda Iringa. Lakini zote hizi sasa zina Makandarasi. Kwa hiyo, The Great Northern Road sasa itapitika kama ambavyo mtu atatoka Cairo hadi Cape Town akipita kwenye barabara ya lami akitaka hata kwa baiskeli. (Makofi)

Mheshimiwa Mhita pia amezungumzia juu ya barabara ya Katech - Kondoa kwamba ichukuliwe na TANROAD. Amezungumzia mambo mengi. Kwa ujumla Mheshimiwa Mhita amezungumzia masuala mengi na

387 mimi nasema ushauri wake na maoni yake yote tumeyakubali.

Mheshimiwa Katagira naye amezungumzia mambo mengi, amezungumzia juu ya barabara ya Kyaka - Bungene zaidi ya kilometa 59.1 ambayo inajengwa kwa kiwango cha lami, tutaendelea kuijenga mpaka ile sehemu nyingine iliyobaki ya kuunganisha Ngara. Hiyo nataka kukuhakikishia Mheshimiwa Kategira.

Vile vile Mheshimiwa Katagira amezungumzia kuhusu barabara inayounganisha Kyerwa kwenda Uganda na hasa kwenye milima ile ya Rwabununka. Tumeweka kiasi fulani cha fedha katika kuhakikisha hiyo barabara nayo inashughulikiwa. Ushauri wake tunakubaliana nao, tunau-support na tutaufanyia kazi katika bajeti hii.

Mheshimiwa Mteketa ametoa pongezi kwa Daraja la Kilombero. Amezungumzia juu ya barabara ya kidatu - Ifakara na umuhimu, amezungumzia barabara ya Chita - Bofu na anaunga mkono, na mimi nakushukuru sana, kwa sababu usipounga mkono lile Daraja la Kilombero sasa halitapitika mtani wangu. Lakini tunashukuru umeunga mkono na yale yote uliyoyapendekeza hapa tutayazingatia katika bajeti ya mwaka huu.

Mheshimiwa Nundu, anaunga mkono hoja, anatoa pongezi kwa Serikali kwa kujenga barabara nyingi kwa lami. Nampongeza Mheshimiwa Nundu kwa kusimamia kazi yake vizuri katika Jimbo lake.

388 Amezungumzia juu ya barabara ya Tanga - Pangani ambayo inakuja, inatokezea Bagamoyo zaidi ya kilometa 178 ambayo nayo tumeanza kuifanyia feasibility study kwa ajili ya kujenga kwa kiwango cha lami. Amezungumzia juu ya wananchi wavumilivu, na kwamba barabara zilizo chini ya TAMISEMI zina hali mbaya, hasa za Halmashauri, anaomba zipelekewe TANROAD. Ombi lake hili kidogo tunaliona ni gumu, lakini nakubaliana na mapendekezo yaliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge wengi kwamba inawezekana sasa wakati umefika wa kuanzisha agency nyingine kwenye TAMISEMI ili tuwe na agency ya TANROAD, tuwe na agency nyingine ya TAMISEMI inayoshughulikia barabara kule. Kwa sababu ni ukweli usiofichika hata zile fedha zinazopelekwa za road fund katika Halmashauri za Wilaya nyingi, zinaliwa na zinapotea bure. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, tumekuwa tukipata orodha kutoka kwa Mwenyekiti wa road fund, Dkt. James Wanyancha, Halmashauri zile ambazo zimekuwa zikitumia vizuri kwa fedha za road fund na kwa mujibu wa sheria, fedha zile zinatakiwa kutumika kwa ajili ya matengenezo ya barabara tu. Lakini nyingine zinatumika hata kulipana safari, tuna mifano ya kutosha. Kwa hiyo, ninafikiri ninakubaliana kabisa na mapendekezo ya Waheshimiwa Wabunge kwa sababu hata na mimi barabara zangu kule Chato zinazosimamiwa na Halmashauri, nyingine ziko kwenye hali mbaya. Ndiyo maana pamekuwa na notion ya kila Mbunge kutaka barabara zitolewe kwenye Halmashauri zipelekwe TANROAD, na hii ni kwa sababu watu wa TANROAD wanafanya kazi nzuri. Kwa niaba

389 yenu Waheshimiwa Wabunge, naomba mniruhusu niwapongeze sana Ma-engineer wa TANROAD kwa kazi nzuri wanazofanya. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Akunaay anaishukuru Serikali. Msema kweli ni safi tu kushukuru, wala hakuna ubaya. Hata kwenye Biblia, neno kushukuru limeandikwa kwenye Zaburi karibu mara ishirini, thelathini, lakini huyu pia aliwahi kuwa Mjumbe wa Road Fund, na kushukuru ni mambo mazuri. Amezungumzia juu ya msongamo wa magari. Amesema Dar es Salaam magari, mizigo yasitishwe, yasiingie Mjini, baisikeli zitumike mahali pengine; ameshauri tuanzishe sate lite town. (Makofi)

Mheshimiwa Akunaay mimi nakupongeza kabisa, yaani ushauri wako wote huu ni mzuri na tunaupokea asilimia mia moja. Mheshimiwa Mbowe una watu wazuri sana huko wengine. (Makofi) Mheshimiwa Spika, ushauri wa Mheshimiwa Akunaay ni wa kweli tu, anazungumza ukweli tu kutoka moyoni kwa sababu anajua moyo wake unamuuma, huyo hata akihamia CCM tunampa tu kura. Ushauri wake tunaukubali kwa mikono miwili yote. (Makofi/Kicheko)

Mheshimiwa Eng. anasema pongezi kwa Wizara ya Ujenzi, kwa kupandisha daraja, anasema pongezi kwa kupata fedha za mabarabara, ametoa ushauri mwingi mpaka akaishia kutoa ushauri kwenye Engineer’s Registration Board kwamba tuanze ku-create ajira kwa Watanzania. Kwa bahati nzuri mwaka huu kuna ma-enginner 1000 ambao

390 watakwenda kwa ajili ya training kwenye miradi ya barabara na fedha zimetolewa, zipo kwenye bajeti ya mwaka huu. Kwa hiyo, nashukuru ushauri wake na amepongeza pia ujenzi unaoendelea kwenye barabara, akatoa concern yake juu ya barabara inayokwenda kwa kusuasua kwa Kandarasi mmoja anayefanya kazi kule. Tumeshaanza kuchukua hatua.

Mheshimiwa Juma Njwayo anasema yeye haungi mkono hoja kwa sababu fedha zilizotengwa za feasibility study na detail design hazitoshi. Ndugu yangu naomba uunge mkono tu, najua ulikuwa unachomekea tu pale. Tumeweka Shilingi milioni 700, ukikusanya na zile nyingine, kwa hiyo, barabara ya kutoka Mtwara kuja Tandahimba mpaka Masasi nayo tunaiweka kwenye programme kwa ajili ya kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami. Ningewaomba wapiga kura kwa Mheshimiwa Njwayo, wamwamini kwamba anatetea sana wananchi wa kule, na sisi tumeweka zaidi ya Shilingi milioni 700 kwa ajili ya kuijenga hii barabara kwa kiwango cha lami. Tunaanza na detail design. Nakuomba kabisa Ndugu yangu uipitishe ili kusudi angalau tuanze kufanya design, ikiwezekana mwaka kesho tuanze na yenyewe kuitengeneza kwa kiwango cha lami. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, ninasema kwa dhati kwamba, tuna nia nzuri na kwa sababu barabara ile ya kutoka Masasi kwenda Mtwara kwa kupitia Jimbo lako, ndiyo imepita kwenye maeneo ambayo ni very productive. Kwa hiyo, barabara ile ina umuhimu wa pekee kutengenezwa kwa kiwango cha lami. (Makofi)

391 Mheshimiwa Spika, barabara ya Ndundu - Somanga: Je, tatizo ni nini? Nimeshaeleza Mkandarasi aliyekuwa pale, wafadhili wetu walikuwa Kuwait Fund, hawakutoa fedha, ikabidi tutoe fedha zote sisi Serikali. Lakini pia Mkandarasi yule Mzee Karafi mwenyewe ambaye ndiye owner wa kampuni ile alifariki mwaka 2011. Kwa hiyo, kampuni ikawa na mtikisiko kidogo, lakini tumewabana vizuri na kwa sasa hivi tumepeleka Engineer wa kusimamia pale moja kwa moja. Kazi zitakamilika.

Kandarasi asisubirie amalize kazi ndipo aambiwe kurudia. Huo ni ushauri mzuri, lakini kwa wale tuliowaambia kurudia ni kwa sababu hatukuweza kuwaambia wakati huo. Lakini wakati mwingine hata barabara ikishamalizika, anaweza akafunika juu usione kama imeharibika ndani. Kwa hiyo, ikishaharibika na wakati ameshatoka, napo ni vizuri kumwambia kurudia. Anaweza akafunikafunika juu usielewe kila mahali na ndiyo maana huwa tunaweka grace period ya mwaka mmoja hadi miaka mitatu ya kuisimamia hiyo barabara. Kwa hiyo, sisi tutaendelea kuwasimamia, lakini pia na kurudia wale watakaokuwa wanashindwa na uturuhusu Mheshimiwa wawe wanarudia, kwa sababu ukirudia anapata hasara contractor na hivyo anakuwa anajifunza zaidi kwamba kosa la namna hiyo asilirudie mara nyingine.

Mheshimiwa Arfi naye ametoa pongezi, wako wengi tu, Makamu Mwenyekiti wa CHADEMA anatoa pongezi kwa bajeti ya Chama cha Mapinduzi. (Makofi)

392 Mheshimiwa Spika, huo ndiyo uzalendo wa kweli, huo ndiyo Utanzania wa kweli kwa sababu wanatambua kwamba barabara hazina siasa, ingawaje barabara nyingi zinajengwa na Chama cha Mapinduzi.

Ninakupongeza na ushauri wako ulioutoa Mheshimiwa Arfi tunauzingatia kwa kweli. Vile vile alizungumzia juu ya majengo ya TBA, Mikoa mipya: Je, nyumba hizo zitajengwa? Nami nasema kwa dhati kwamba TBA sasa waangalie namna ya kuanza kujenga nyumba mpya kwenye Mikoa hiyo mipya ikiwa ni pamoja na Mkoa anaotoka Mheshimiwa Arfi. Madeni ya Makandarasi yamelipwa, juzi tu tumelipa zaidi ya Shilingi bilioni 300. Matengenezo ya PMR kwa Mkoa wa Rukwa yamefanya kazi vizuri. Nami nampongeza huyu Kandarasi aliyefanya hiyo kazi. Wizara ipandishe daraja barabara za Wilaya. Katika kupandisha hapa madaraja, tunazingatia sheria.

Barabara inayotakiwa kupandishwa kuwa ya Mkoa, ni lazima iunganishe Mkoa, Wilaya na Wilaya, ile inapandishwa inakuwa rural road. Inayounganisha Makao Makuu ya Mkoa na Makao Makuu ya Mkoa mwingine inakuwa trunk road. Lakini katika bajeti hii, tumepanga tutapita barabara zote zilizoletwa na Waheshimiwa Wabunge, kwa sababu maombi ni mengi. Zile zitakazo-qualify kupandishwa, tutazipandisha, zile ambazo zitashindwa ku-qualify, tutawajulisha kwa nini zimeshindwa.

Vile vile Mheshimiwa Arfi amezungumzia juu ya Daraja la Mto Malagarasi, Daraja la Kikwete. Namjibu

393 kwamba, linakwenda vizuri. Kuhusu Serikali isikwamishe mradi huu; nasema hautakwama, utakamilika. Hata katika bajeti ya mwaka huu tumeweka fedha, pamoja na zile kilometa 48 za eneo hilo. Kwa hiyo, Daraja la Kikwete litamalizika. Otherwise nakushukuru sana kwa mchango wako na ushauri wako Mheshimiwa Arfi.

Mheshimiwa Malocha amesema barabara ya Kibaoni - Kamsamba ni vyema ikatengenezwa kwa lami, amesema Daraja la Mto Momba: Je, daraja hili litatengenezwa lini? Amezungumzia juu ya barabara ya Jimbo za Kwela, amezungumzia juu ya mradi wa PMRR, amezungumzia pongezi kwa Wizara na Serikali. Ushauri wako na maombi yako mengi ambayo umeyazungumza hapa, tumeyazingatia. Ni bahati mbaya, muda siyo mwingi sana na bado nina hoja nyingi tu za kujibu. Lakini nataka kukueleza Mheshimiwa Malocha, tumezingatia yale yote uliyoyaweka. (Makofi)

Mheshimiwa Dunstan Mkapa anaunga mkono, anazungumzia juu ya Masasi - Mangaka, anazungumzia ADB imetenga fedha za kutosha, amezungumzia fedha ziko kutoka Mangaka hadi Tunduru, ametoa pongezi, amesema Serikali iharakishe ujenzi wa barabara hii, Daraja la Halmashauri lijengwe na Wizara, barabara ya Ulinzi - Tia nayo ameizungumzia. Ni maombi mengi. Nataka kumhakikishia Mheshimiwa Mkapa kwamba tunayazingatia mengi, yale yatakayowezekana tutayashughulikia nataka, kumwahidi kwenye hilo.

394 Mheshimiwa Kigola ameunga mkono, anasema barabara ya Ngorongoro, amesema barabara za Mkoa Ejibalamaziwa, barabara ya Kasanga ni vyema kuwekwa kokoto. Sheria za barabara bado zina matatizo na anasema tutoe elimu ya kutosha, na sisi tutaendelea kweli kutoa elimu ya kutosha ili wananchi wengine wasionewe kwa sababu ya kutokujua. Ndiyo maana katika wale ambao tulikwishatoa maelezo hapa, wale waliokutwa na sheria ya mwaka 2007, kwa maana nyingine kwamba walikuwa wako kwenye road reserve kwa Sheria hii ya mwaka 2007, yaani zilipoongezwa zile mita 7.5, wale wote tunawalipa fidia. Ila wale walio ndani ya mita 22.5 wa sheria ile ya zamani ya mwaka 1932 ikafanyiwa amendment mpaka mwaka 1967 na kadhalika na kadhalika ambao wao hatuwalipi fidia kwa sababu wale ni wakorofi. Lakini wale waliokutwa kwa sheria ya mwaka 2007 sheria namba 13, wale wote tunapowagusa majengo yao pamoja na kwamba wako kwenye road reserve pamoja na kwamba ignorance of law is not defence, kwa ubinadamu wa Chama cha Mapinduzi wale wanalipwa fidia. (Makofi)

Mheshimiwa Mbowe ametigisha kichwa, basi kwa uzuri wa Chama cha Mapinduzi kwa kushirikiana na Vyama vya Upinzani vinavyoongozwa na Mheshimiwa Mbowe tutawalipa fidia. (Kicheko)

Mheshimiwa John Mipata amesema Tunduma – Sumbawanga, anampongeza Mheshimiwa Rais, na aliomba kwamba ni vyema fedha zikatengwa na kutosha barabara ya Kasanga. Nasema barabara hiyo nayo inakwenda vizuri. Pia alitoa pongezi kwa

395 ujenzi, pongezi nyingi nyingi tu kwa mradi wa PMR, akasema barabara za Halmashauri ni vizuri zipelekwe TANROADS na kadhalika. Tumezingatia ushauri wake, yale yatakayowezekana tutayachukua, yale yatakayoshindakana napo tutamjulisha Mheshimiwa Mipata.

Mheshimiwa , ameunga mkono, amezungumzia juu ya barabara ya Bigwa Kisaki, Mvuha, anaomba ijengwe kwa lami; amezungumzia juu ya Ngerengere Masaki, amezungumzia juu ya madaraja katika Wilaya ya Morogoro Vijijini, amezungumzia juu ya barabara za Halmashauri nazo zishughuliwe na TANROADS. Maombi yote haya tunayazingatia, tutayaangalia yale yatakayowezekana Mheshimiwa dada yangu Nkya tutayashughulikia, yale yatakayowezekana.

Mheshimiwa Donald Max ametoa pongezi, na ameomba paundwe TANROADS Vijijini, pia anaomba lami pale Geita. Nafikiri tutaangalia namna gani tunaweza kuweka pale Geita napo kwa sababu kuna mavumbi mengi hata kilomita moja, mbili kwa sababu ni ahadi ya Mheshimiwa ya Rais. Vile vile aliomba makalvati yale tuyabebe sasa, tutaangalia kama tutaweza hilo tuone ni namna gani ya kumsaidia.

Mheshimiwa Cheyo anasema leo atalala vizuri sana, nchi hii sasa inapitika kila mahali alipokuwa akigombea Urais wakati ule ilikuwa ni shida. Hawa ndio watu wanazungumza ukweli kabisa. Aliifahamu nchi hii wakati akigombea Urais kwenye miaka ile ya nyuma,

396 sasa anasema inapitika kila mahali. Nampongeza mzee wangu Cheyo. (Makofi)

Ni vyema kushukuru hata kama anayeongoza hiyo Serikali ni Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi, indirect umemshukuru Mheshimiwa Rais wetu ambaye ni mpendwa kwa kufanya kazi hizi. (Makofi)

Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Cheyo pia amepongeza kwa ujenzi wa madaraja katika Jimbo lake, tutayashughulikia kwa sababu Chama cha Mapinduzi hakina Chama katika kushughulikia maendeleo ya wananchi. Amezungumzia juu ya Mwingumbi - Bariadi. Ile barabara kwa mwaka huu tumetenga Shilingi milioni 7,000. Nataka kumhakishia Mheshimiwa Cheyo kwamba ile barabara tutaitengeneza. Mkandarasi alikuwa na matatizo kidogo, tumembana, na sasa hivi ameanza kufanya kazi. Kwa hiyo, tutatengeneza kutoka Lamadi hadi Bariadi kilomita 71.9, kutoka Bariadi - Mwigumbi nayo lazima itengenezwe kwa kiwango cha lami. Nakuhakikishia Mheshimiwa na kwa bahati nzuri fedha zipo, madeni ya Serikali kuwa na madeni ni kitu cha kawaida. Tajiri yeyote ni lazima uwe na madeni. Usipokuwa na madeni na wewe ni tajiri, siyo tajiri. (Makofi)

Hata Marekani wana madeni kila mahali. Fedha ziongezwe, barabara za Bariadi, yote hayo yote tumeyapongeza na pongezi kwa Mfuko wa Road Fund, wanafanya kazi nzuri. Ninakupongeza sana Mheshimiwa. Pongezi kwa kupunguza gharama, tunakupongeza. Mmakandarasi..... Eeeh!

397

(Hapa kengele ya kwanza ililia kuashiria muda wa Mzungumzaji kwisha)

WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Kibona alitoa pongezi na ameniombea, na amezungumzia barabara zake za Ileje, anasema hawajawahi kuona lami. Tutaangalia hata Ileje angalau namna ya kuweka hata water seal barabara ya lami. (Makofi)

Vile vile Mheshimiwa Kibona aliomba barabara ya TAMISEMI ziwe za Mkoa, anazungumzia juu ya barabara inayokwenda mpakani mwa Malawi, tumeyazingatia yote Mheshimiwa Kibona, mengine tutayajibu kwa maandishi kwa sababu time ni ndogo kweli, nimeshagongewa kengele hapa.

Mheshimiwa Mkosamali, ushauri wake mwingi ni mzuri, ila amezungumzia kwa barabara ya kutoka Kidahwe kwamba tumeitengea fedha ndogo. Hizo fedha zinatosha, tumetenga Shilingi milioni 3,500, Mkandarasi unapotangaza tenda, fedha anazotakiwa kulipwa ni advance payment, na Mkandarasi ni lazima awe na guarantee, advance payment kwa Shilingi bilioni 3.5 zinatosha. Ile barabara ni muhimu na mimi najua kabisa ni muhimu, lakini hizi ndizo za kuanzia katika bajeti ya mwaka huu.

Nataka kukuhakikishia Mheshimiwa Mkosamali kwamba barabara hii itajengwa kwa kiwango cha lami. Ila za pale mjini, hatuwezi tukajenga tena lami nyingine wakati tunajenga kilomita 300 halafu hiyo tuje tuibomoe. Kwa hiyo, kilomita 300 zote tutazijenga na

398 tutatangaza katika bajeti ya mwaka huu. Niamini Mheshimiwa Mkosamali, na uunge mkono. Usipounga mkono, hizi Shilingi bilioni 3.5 zitakwenda kwingine. (Makofi/Kicheko)

Sasa na mimi si nimchomekee kidogo! Yeye si alichomekea kidogo? Lakini otherwise Mheshimiwa Mkosamali ametoa ushauri mzuri tu, amezungumzia barabara ya Mabamba inayokwenda Burundi, umezungumzia juu ya ahadi ya Mheshimiwa Rais, yote yale tunayazingatia. Ushauri ni mzuri, umezungumzia juu ya TBA isimamie nyumba, amezungumzia juu ya DARTS, vikao vya Bodi, mengi ni mazuri tu Mheshimiwa Mkosamali na mimi, nakupongeza. Kwa hayo, barabara ile tutaijenga, naomba tu atuunge mkono apitishe hii bajeti, asitoe shilingi. (Makofi)

Mheshimiwa Koka, ametoa ushauri mzuri sana kwa barabara zilizoko kwenye Makao Kakuu ya Kibaha, nami ushauri wake nimeupokea. Ni kweli ni vizuri tutengeneze zile barabara angalau zitasaidia hata kupunguza msongamano katika Kiji la Dar es Salaam na maeneo mengine.

Mheshimiwa Koka umetoa ushauri mzuri, tutaangalia ni namna gani tunaweza tukazitengeneza zile barabara.

Mheshimiwa Spika, barabara ya Kongowe - Bagamoyo, Mji wa Kibaha na kadhalika, Mheshimiwa Prof. Msolla naye amezungumzia mengi, ametoa ushauri, amezungumzia juu ya diversion road, Mheshimiwa Eugen Mwaiposa amezungumzia mengi,

399 ametoa pongezi, amezungumzia juu ya barabara ya Ukonga - Chanika, nataka kusema Mheshimiwa tutazingatia ushauri wako na tutaangalia namna gani baadhi ya barabara nyingine tutazipandisha hadhi. (Makofi)

Mheshimiwa , amezungumzia juu ya barabara. Actually, Mheshimiwa Mkono bahati mbaya hayumo humu alipokuwa akizungumza ile barabara anayoizungumza. Leo imetangazwa tenda kwa ajili ya kujengwa kwa kiwango cha lami. Sasa akikataa sijui nimwambie Chief Executive sasa tufanyaje! Tumeweka Shilingi bilioni 3,000 kwa ajili ya kujenga barabara ya lami kutoka Makutano, kwenda Nate. Kwa hiyo, ninamwomba Mheshimiwa Mkono alipo asome hata kwenye gazeti la Uhuru, ataona barabara hii imetangazwa tenda kwa ajili ya kuanza kujengwa kwa kiwango cha lami.

Kwa hiyo, aunge mkono tu kaka yangu ambaye ninajua anazungumza kwa concern yake. Yupo mmoja anatingisha kichwa, anasema kwanini imetangazwa tenda? Imetengazwa tenda kwa sababu hata mwaka 2011 ilitengewa fedha. Kwa hiyo, asitingishe kichwa kwa kusema kwamba inatangazwaje tenda wakati bajeti haijapitishwa. Mwaka 2011 mkasome kwenye vitabu, barabara ile ilitengewa fedha. Kwa hiyo, ndiyo maana imetangazwa tenda na za mwaka huu zinaendelea. (Makofi)

Mheshimiwa Modestus Kilufi, ametoa pongezi kwa ujenzi wa barabara ya Mafinga, barabara yaani zote hizi anapongeza tu.

400

Mheshimiwa Serukamba naye anaunga mkono, Mheshimiwa Freeman Mbowe ametoa ushauri mzuri tu, nakubaliana nao na nam-support tu vizuri, amezungumzia barabara yake. Ile barabara tutaijenga na itakamilika.

Mheshimiwa Peter ametoa ushauri, tunakubaliana nao.

SPIKA: Mheshimiwa, muda.

WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Spika, baada ya maeneno haya mengi yote, naomba kutoa hoja. (Makofi)

(Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

SPIKA: Hoja hiyo imeungwa mkono sasa kabla hatujaingia kwenye hatua nyingine, napenda kutangaza kwamba Mheshimiwa Waziri Mkuu kama Kiongozi wa Shughuli za Serikali Bungeni amepata safari, lakini badala yake amemweka Mheshimiwa Samuel Sitta - Waziri Ushirikiano wa Afrika Mashariki, ni Kaimu katika nafasi hiyo. (Makofi)

Ni kawaida, Senior Minister ndiyo wanakaimu kama kiongozi hayupo. Kwa hiyo mkimwona amekaa pale na yeye pia msimfuate kuongea huko, kwa sababu anapaswa kusikiliza vinavyoendelea.

KAMATI YA MATUMIZI

401 MATUMIZI YA KAWAIDA

FUNGU 98 – WIZARA YA UJENZI

MWENYEKITI: Waheshimiwa tamaa yangu leo tuweze kufika kwenye kitabu cha nne kwa sababu kitabu cha nne ndiyo kina barabara, kwa sababu ndiyo kitabu cha maendeleo. Mking’ang’ania mshahara wa Waziri, basi kwenye maendeleo hamfiki, kwa hiyo repetition na kwa wale waliojibiwa tutumie muda wetu mzuri. Kitabu cha nne cha Maendeleo kwa barabara ndiyo mahali penyewe. Sasa mkianza mshahara wa Waziri wala hawezi kuahidi chochote pale kwa sababu ni mshahara wake tu. Kwa hiyo, tujitahidi kama tunaweza kufika kwenye kitabu cha nne itakuwa vizuri sana.

Kif. 1001 – Admin. and HR Management..……Tsh. 2,189,222,000/=

MWENYEKITI: Kama nilivyosema, we use wrongly kipindi cha mshahara wa Waziri, na mkisoma kanuni, kati yenu hakuna atakayefanikiwa kwa sababu anasema lazima suala liwe la kisera. Sasa ukiniuliza barabara ya kwako, barabara ya wapi, hiyo siyo sera. Kwa hiyo, mjue hapa nitakataa. Someni kanuni, inasema utauliza swali mahsusi linalohusiana na sera, siyo barabara yangu barabara yangu; hiyo hamna. Haya, tunaanza kuandika watu, kama hujajiandaa ufikirie kabisa.

402 Tuanze na Mheshimiwa Kombo, nimeshawaambieni mambo ya sera, tunakwenda hovyo, ni mambo ya sera sasa. Haya tuanze Mheshimiwa Kombo.

MHE. KOMBO KHAMIS KOMBO: Mheshimiwa Mwenyekiti, fungu…

MWENYEKITI: Mshahara wa Waziri tu, hamna fungu.

MHE. KOMBO KHAMIS KOMBO: Mshahara wa Waziri sub vote 1001….

MWENYEKITI: Sema tu mshahara wa Waziri tunaujua.

MHE. KOMBO KHAMIS KOMBO: Mshahara wa Waziri. Kwa kawaida fungu 220700 kodi huwa zinapanda, lakini hapa kodi zinaonyesha zimeshuka badala ya kupanda, ni kwa sababu gani? Wakati leo zinashuka ni kwa sababu kodi za ofisi hii ya Mheshimiwa Waziri ziendelee kushuka wakati kodi zinatakiwa zipande, au jengo ni bovu?

MWENYEKITI: Mmemwelewa? Anasema kwanini hesabu ya mwaka huu ni ndogo kuliko ya mwaka 2011 katika kifungu kile? Mheshimiwa Naibu Waziri.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, maelezo ni kwamba jengo ambalo tulikuwa tunatumia Wizara mbili sasa tumegawanya Wizara, kwa hiyo, imepungua tu. Ni jengo moja badala ya mawili, kwa hiyo, ndiyo maana figure imepungua.

403

MHE. SALIM HEMED: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Moja kati ya matatizo yanayosababisha msongamano kwa barabara ya Dar es Salaam Morogoro ni mzani wa Kibaha na Mikese. Nilijaribu kufanya utafiti kwa nchi jirani kuona wao wanafanya nini, nimegundua kwamba mizani hizi hazijengwi karibu na barabara kuu. Sasa Mheshimiwa Waziri amezungumza leo kwamba anataka kuondoa mzani wa Kibaha; Sasa huu mzani wa Mikese ambao vilevile ni kero: Je, tuko tayari kuondoa mizani hizi karibu na barabara ili tuzijenge mbali kuondoa msongamano?

WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, matatizo ya msongamano ya Dar es Salaam ni mengi ikiwa ni pamoja na mzani wa Kibaha. Tunaanza na mzani wa Kibaha kuuhamisha kuupeleka Migwaza.

MWENYEKITI: Mbona unasema Migwaza...

WAZIRI WA UJENZI: Vigwaza…

MWENYEKITI: Vigwaza…

WAZIRI WA UJENZI: Eeh! Kwa uhakika itasaidia sana kupunguza msongamano kule kwa sababu Kibaha na Dar es Salaam ni jirani sana. Ule wa Mikese tutaangalia hatua kwa hatua ili kusudi barabara isianze kuharibika tena kati ya Vigwaza kwenda Mikese.

MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchango wangu wa maandishi, nilishauri kuhusiana na namna bora ya kudhibiti uwezo

404 na ubora wa Makandarasi ili kuwa na tija na katika ujenzi wa barabara nchini.

Katika ushauri, nilitoa kwa kutambua kwamba Makandarasi wengi nchini wanakuwa registered na Contractors Registration Board. Makandarasi hawa wanapokuwa hawadhibitiwi vizuri, wanasababisha kwanza ubovu wa kazi wanazofanya, pili, upotevu mkubwa wa fedha za Serikali, na mwisho ufanisi katika utendaji mzima wa kazi unaokusudiwa.

Katika ushauri wangu, nilitambua kwamba Makandarasi huwa wanateuliwa na kupewa kazi hizo kwa kutumia Sheria ya Public Procurement ambapo vitengo vya ugani katika Taasisi za Umma zina-award zile contract kwa Makandarasi bila kulazimika kupitia kwa CRB.

Ushauri ambao ningeomba Mheshimiwa Waziri atupe ni kwa nini isiwe compulsory kwamba, kabla ya kutoa tender yoyote au kabla ya ku-award tender yoyote kwa Mkandarasi yeyote, Mamlaka ya CRB kwa maana ya Contractors Registration Board, ishirikishwe katika process nzima ya due diligence ili kuweza kutambua uwezo wa wakandarasi, historia ya wakandarasi, ikiwemo mitambo wanayotumia kwa kazi hiyo kama inalingana na uwezo wao kama walivyoandikishwa kwenye Bodi hiyo.

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ushauri aliutoa

405 Mheshimiwa Mbowe kwa bahati mbaya sana time haikutosha kuweza kumjibu.

Natambua kabisa, kupitia Sheria Namba 17 ya Mwaka 1997 ambayo ilifanyiwa amendment kwenye mwaka 2011, ilianzisha Contractors Registration Board ambapo hadi sasa Wakandarasi waliosajiliwa katika nchi nzima kuanzia Class One, Class Two hadi Class Seven wapo 9,041. Bodi ya Wakandarasi kupitia hiyo Contractors Registration Board, imekuwa ikichukua hatua kali kwa Wakandarasi ambao wameshindwa ku- perform kazi zao vizuri. Moja ya hatua zilizochukuliwa ni pamoja na kuwafukuza. Katika Hotuba yangu nimeeleza zaidi ya Wakandarasi elfu mbili na mia tano na sabini na wamefutiwa usajili, kwa hiyo, hawawezi kufanya kazi yoyote.

Katika hilo, Bodi ya Wakandarasi ambayo ipo chini ya Wizara ya Ujenzi, TANROAD na PPRA, ambazo zote zinafanya kazi kwa kushirikiana, huwa zina-coordinate katika kujua ni Wakandarasi gani ambao wako registered, ni Wakandarasi gani ambao wamefutiwa na ni Wakandarasi gani ambao hawatakiwi kufanya kazi. Hivi karibuni kuna orodha imeshatolewa na PPRA ambayo Wakandarasi hawatakiwi kupata kazi mahali popote. Kwa hiyo, huwa kuna communication ndani ya vyombo hivi katika kuhakikisha kwamba, Mkandarasi ambaye hapaswi kufanya kazi hawezi kupata kazi.

MWENYEKITI: Mnaona swali alilouliza Kiongozi wa Kambi ya Upinzani ni la Kisera na si kibarabara cha kule

406 Hai wala nini ni la Kisera correctly. Kwa hiyo, Mheshimiwa Chenge ni hao hao wanaitwaga pamoja. (Kicheko)

MHE. ANDREW J. CHENGE: Sisi ni ndugu pia. Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru kwa kunipatia nafasi. Serikali inatumia pesa nzingi sana kujenga barabara nchini. Ninapenda iiambie Kamati yako sasa kwamba katika mwaka huu tulioumaliza tunaingia katika mwaka 2012/2013, yaani mwaka mpya wa fedha ni madeni kiasi gani ya Wakandarasi ambao wamefanya kazi na certificates zao zimewasilishwa na ni deni gani, dead stock, kiwango chake sasa ni shilingi ngapi ili tujue katika utekelezaji wa bajeti hii sehemu kubwa ya kazi hiyo itakuwa ni kwenda kulipa deni.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda Serikali itueleze ili tuwe na picha kamili. Nakushukuru sana.

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa kwamba, Serikali inatumia fedha nyingi kuwalipa Wakandarasi wanaofanya kazi katika nchi hii na hasa kwa kuzingatia kwamba Miradi ya Barabara huwa ina gharama kubwa. Hii ni katika juhudi kubwa za Serikali zinazofanywa kuhakikisha kwamba inaimarisha mitandao ya barabara zake.

Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2010, yaani tulipokuwa tukianza mwaka 2011, wakati tunapitisha bajeti hii tuliingia na madeni ya shilingi

407 bilioni 320. Kwa hiyo, katika bajeti ya mwaka jana na mwaka huu, yameshughulikiwa sana na Serikali, madeni karibu yote yamemalizika na kwa sasa hivi fedha ambazo zinadaiwa na Wakandarasi kutokana na certificate hazizidi shilingi bilioni 50. Madeni ya mwisho yamelipwa shilingi bilioni 300 wiki iliyopita. Kwa hiyo, kwa maana nyingine nataka kusema kwamba, Serikali ya Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, inajitahidi kwa hali ya juu sana kulipa madeni ya Wakandarasi.

Ieleweke pia kwamba ili Mkandarasi alipwe kwa utaratibu wa kimkataba huwa ni lazima kwanza a- produce certificate na ile certificate ni lazima iwe verified na consultants ambao wako kule; inakwenda kuwa verified na TANROAD, inakuwa verified na Wizara na baadaye haya madeni yanakwenda kuwa verified na Hazina kwa ajili ya kulipa. Tunafanya hivyo kwa makusudi ili pasitokee malipo hewa kwa Wakandarasi ambao ni wababaishaji.

Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, nataka kukuthibitishia kwamba, kwa kiasi kikubwa madeni ya Wakandarasi yamepungua sana, jukumu lililobaki ni kwa Wakandarasi kufanya kazi. Kwa taarifa tulizonazo, hata lile deni lililobaki kidogo nalo inawezekana likakamilika mapema katika mwezi huu.

MHE. JAMES F. MBATIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Katika mchango wangu wa maandishi nilitaka kujua uimarishaji wa Kitengo cha Risk Management katika Wizara hii, kwa sababu yapo majanga ya aina mbalimbali yanayotokea na

408 mengine hakuna anayejua ni acts of God. Sasa inaonesha kwamba, kwenye Engineering Bureaus nyingi, Kitengo hiki huwa hakitiliwi mkazo au hakisimamiwi vizuri na huu ni uzoefu kwenye Mataifa mengi.

Hapa kwetu Tanzania, fedha nyingi zinatumika katika Miradi hii kwa vile life span ya Miradi mingi ambayo amesema inatoa grace period ya miaka mitatu Mkandarasi akiwemo kwenye Mradi. Sasa baada ya hapo kama Kitengo hiki hakitaimarishwa, kitaligharimu Taifa fedha nyingi na hii imekuwa ni udhaifu mkubwa katika departments nyingi za engineering.

Kwa hiyo, nilitoa ushauri wa namna hiyo kwamba; je, katika Wizara yetu ya Ujenzi uimarishaji wa Kitengo hiki kama kipo kinaimarishwa kiasi gani na kinatiliwa mkazo kiasi gani na utaalamu wake?

Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba ufafanuzi.

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, tuliupata ushauri wa Mheshimiwa Mbatia na sisi kama Wizara, tumeupokea ili tuweze kuufanyia kazi katika bajeti inayokuja.

MHE. DKT. AUGUSTINE L. MREMA: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mchango wangu kwa Wizara ya Ujenzi niliuliza Sera inayotumika kwenye mizani ya Njiapanda ya Himo. Mizani ile inapokea magari kutoka Nairobi kwenda Mombasa na Dar es Salaam kwenda Arusha na Mombasa, lakini imekuwa kero kubwa sana

409 na kila wakati kumekuwa na msururu wa magari kutoka Njiapanda kwenda Chekereni, kutoka Njiapanda kwenda Uchira na kutoka Njiapanda kwenda Himo.

Ninauliza hivyo kwa sababu hiyo mizani ina tabia za ajabu, magari yanapimwa Kibaha lakini yakifika pale yanaambiwa yamezidisha uzito, hata wakipunguza mizigo wanaambiwa bado wamezidisha uzito. Sasa tunashangaa mizani ile ikoje na tofauti yake na mizani ya Kibaha ni nini?

La pili, hata magari yasiyokuwa na bidhaa na mizigo nayo yanapimwa.

Tatu, mizani ile ipo barabarani na msongamano wa magari ni mkubwa. Naomba kuuliza kama hayo yote yanayofanyika ni utekelezaji wa Sera ya Wizara ya Ujenzi; ni usimamizi usiofaa; ama ni utekelezaji wa Ilani kama anavyosema rafiki yangu Mheshimiwa Mbowe pale; au tatizo ni nini? Tusaidieni kwa sababu imekuwa kero, watu wanalalamika na kunung’unika na wanakinung’unikia Chama cha Mapinduzi. Sasa ili mwendelee kutawala na mwendelee kuwa na sifa, hebu nisaidie pale Njiapanda tunafanyaje?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Mrema kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, mizani yoyote katika nchi hii inatawaliwa na Sheria Namba 30 ya Mwaka 1973, haitawaliwi na Ilani ya CCM wala Ilani ya TLP au ya CHADEMA, bali inatawaliwa na Sheria iliyopitishwa na

410 Bunge hili akiwemo Mheshimiwa Mrema. Kwa hiyo, tunatambua tatizo linalotokea kwenye mzani wa Himo, ambapo katika taratibu za mwaka huu Barabara ya kutoka Arusha - Moshi hadi Himo ni miongoni mwa barabara ambayo itaanza kufanyiwa design na ule mzani wa Himo ulivyokaa na hasa kwa sababu umekaa upande mmoja tu, tutaufanyia modification ili uhamishwe pale uwekwe mahali pazuri zaidi usi-create msongamano na hasa kwa sababu mzani ule upo karibu na Njiapanda tena ya kwenda Dar es Salaam na Njiapanda ya kwenda kwenye mpaka wa Kenya. Kwa hiyo, hilo tumelizingatia ili tusi-create kero kwa Watanzania bila kuzingatia vyama vyao.

MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Kikwembe.

MHE. DKT. PUDENSIANA W. KIKWEMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Katika mchango wangu wa maandishi, niliongelea suala la utengenezaji wa barabara. Ninafahamu kwamba, kabla ya kutengeneza barabara kuna stage mbalimbali mojawapo ikiwa ni upembuzi yakinifu na usanifu wa kina.

Katika Ilani ya Uchaguzi ya Chama cha Mapinduzi ya 2010, imeonesha kwamba, barabara kutoka Mpanda mpaka Kahama ilitakiwa mpaka kufikia 2015 iwe imeshafanyiwa upembuzi yakinifu na Daraja la Ugala liwe limeshajengwa lakini mpaka hivi sasa sijaona na huu ni mwaka wa pili wa kutekeleza Ilani ya Chama cha Mapinduzi.

411 Mheshimiwa Mwenyekiti, katika bajeti hii sijaona mpango wowote unaoongelea suala hilo. Ninaomba nipatiwe majibu kwa niaba ya Wananchi wa Mpanda na Kahama kwa ujumla.

MWENYEKITI: Hayo ndiyo maswali ambayo nilikuwa nayakataa. Nilianza na watu wengine mwone jinsi wanavyouliza. Katika hali ya kawaida kitu hiki hakiwezi kuwa katika bajeti hii, ni cha Sera tu lakini hakipo humu. Ndiyo maana nilianza na watu fulani fulani kwa sababu nilijua wao wataonesha njia, ukianza barabara za wapi na wapi nyingine kama hazipo ni hazipo tu na kama ipo angalia kwenye Mradi. Naomba hili lisijibiwe. Tunaendelea na Mheshimiwa Bura.

MHE. FELISTER A. BURA: Mheshimiwa Mwenyekiti, TBA kazi yake kubwa kwa sasa ni kujenga Nyumba za Serikali, za Wizara, Ofisi za Wakuu wa Mikoa na Wakuu wa Wilaya na kadhalika. Nina imani kwamba, ikipewa uwezo inaweza ikashiriki katika kufanya kazi kibiashara zaidi na hasa katika Halmashauri zetu ambapo kuna kujenga Zahanati, Shule, Nyumba za Walimu na hata majengo makubwa ya Serikali. Ninataka kujua ni lini Serikali itaiwezesha TBA sasa kushiriki katika kazi za kibiashara zaidi kuliko ilivyo hivi sasa?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali la Mheshimiwa Bura la kuiwezesha TBA, haya yote yanaendana na uwezo wa kibajeti, lakini kwa mujibu wa Sheria Namba 30 ya Mwaka 1997, iliyoanzisha Executive Agency ya TBA, moja ya jukumu la TBA ni pamoja na kujiendesha yenyewe. TBA imelitambua hili na imeanza kuji-reform

412 na ndiyo maana katika baadhi ya majengo sasa hivi yanayoshughulikiwa, imeanza kuingia ubia na wawekezaji binafsi.

TBA pia inaendelea kuyaendeleza majengo yake zaidi ya 2,013 yaliyopo nchi nzima. Imeshajenga zaidi ya nyumba 1,470 katika nchi nzima, lakini pia sasa kwa kutambua kwamba ni agency yenye uwezo wa kukopa na kukopeshwa, inafanya mpango wa kukopa fedha kutoka kwenye mabenki na ndiyo maana katika bajeti ya mwaka huu, tumeandika katika Kitabu chetu kwamba TBA watapata mkopo wa shilingi milioni 1,800 ili waweze kujenga nyumba katika maeneo mbalimbali.

Nakubaliana na hilo lakini limeanza kughulikiwa vizuri na TBA ambayo imeanza kujipanga vizuri katika kujiendesha kibiashara.

MHE. LEDIANA M. MNG’ONG’O: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Kwa muda mrefu tumekuwa tunazungumzia suala la barabara zetu kutokuwa na mahali pa kupumzikia abiria, matokeo yake kila tunaposafiri tunasimama na kwenda kujisaidia porini na matokeo yake wakati mwingine abiria kutekwa kwa sababu wameamua kusimama na kujisaidia.

Sasa naomba nimwulize Mheshimiwa Waziri kwamba; kwa kuwa tumezisikia barabara nyingi ambazo zipo kwenye bajeti hii; je, Wizara imekumbuka kuweka vituo vya kupumzikia katika barabara zote ikiwemo hizi ambazo zinajengwa sehemu mbalimbali mfano Iringa, Dodoma, Babati na nyinginezo ili tuwe na

413 vituo vinavyoeleweka kutoka mwanzo wa usanifu ili Private Public Partinership, wale Wabia, wakitaka kuungana na Serikali wawe wanajua ni wapi wanaweza kuwekeza mapema na wakati wanapotangaza tender za barabara wawe wanaelewa kwamba ni wapi ambapo vile vituo vimewekwa wakati wa ujenzi?

Naomba Waziri anijibu, maana tumezidi kuchagua mazingira na pia inaitia aibu nchi yetu ambayo imeendelea namna hii kuwa tunasimama porini.

MBUNGE FULANI: Kuchimba dawa!

MWENYEKITI: Kuchimba dawa na Sheria ya Mazingira pia inatakiwa kutekelezwa.

MHE. LEDIANA M. MNG’ONG’O: Kuchimba dawa!

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naielewa concern ya Mheshimiwa Mng’ong’o, lakini ujenzi wa barabara yoyote katika nchi hata katika nchi zilizoendelea, huwa huwezi ukaacha kutofautisha na uwekezaji wa watu wengine.

Ninapenda kutoa wito kwa Watanzania wanaotaka kufanya biashara hiyo ya kupumzika au kuchimba dawa katika maeneo ya barabara, kila barabara inapojengwa wafanye hiyo shughuli, kwa sababu huwezi kutengeneza mahali pa biashara na wakati huo huo unajenga barabara. Nazungumza hivi

414 kwa kuzingatia uwezo katika bajeti ndogo hii ya kutengeneza barabara.

Tulijaribu kufanya hivyo kwa kutengeneza barabara ya kutoka Makuyuni – Ngorongoro, ambapo tuliweka mahali pa kumpumzikia lakini tunajua katika biashara hii, yaani katika ujenzi wa barabara, Serikali peke yake haiwezi ikasimamia kila kitu na ndiyo maana ningewaomba Waheshimiwa Wabunge katika maeneo yao wale wanaotaka kufanya hii biashara ya kujenga hoteli mahali pa kumpumzikia na mahali pengine, basi wafanye hivyo na Wizara tutatoa maeneo kwa ajili ya kushughulikia hata kama ni kwenye road reserve.

MHE. DEO H. FILIKUNJOMBE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi hii.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ni Sera ya Chama cha Mapinduzi kuhakikisha kwamba, barabara za lami zinajengwa katika maeneo kadhaa hapa nchini. Mheshimiwa Waziri anawaambia nini kuhusu fedha hii na utekelezaji wake?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa ni Sera ya Chama cha Mapinduzi kuhakikisha inajenga barabara na ndiyo maana katika Ilani ya Uchaguzi ya Mwaka 2010, ukurasa wa 72 hadi 83 zinazungumzia masuala ya barabara. Ninachotaka kumweleza Mheshimiwa Filikunjombe ni kwamba, Serikali ya Chama cha Mapinduzi itaendelea kutengeneza barabara, ikiwa ni pamoja na barabara nyingine za

415 maeneo ambayo yalisahaulika na maeneo yake, lakini pia ikiwa ni pamoja na barabara nyingine za kutoka Njombe hadi Makete, zaidi ya kilomita 109, kwa sababu ndiyo Sera ya Chama cha Mapinduzi katika kuhakikisha inaunganisha Mikoa na Wilaya kwa barabara zinazopitika.

MHE. ALPHAXARD K. N. LUGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Barabara ambazo zimetajwa kwenye bajeti hii ni nyingi sana na katika majibu ya Mheshimiwa Waziri, amekuwa akitumia maneno upatikanaji wa fedha. Kwenye mchango wangu wa maandishi, kwa kuangalia masuala haya ya upatikanaji wa fedha, nilitaka kujua kwamba, pale ambapo fedha zitakuwa zinapatikana na pale ambapo watakuwa wanafanya maamuzi kwamba zinaanzia barabara gani, katika Ilani ya Chama cha Mapinduzi wamejipanga vizuri kuainisha barabara kuanzia ya kwanza katika priority na pale ndipo ambapo kuna Barabara ya kwanza iliyotajwa ya Nyamuswa – Kisolya - Bunda.

Sasa ninataka kujua kama fedha zikipatikana wataendelea na mtindo huo huo kwa kuanzia na Barabara ya Nyamuswa – Kisolya – Bunda? Ahsante sana. (Kicheko)

MWENYEKITI: Haya, yaani kwenye kile kitabu ndiyo walipanga ki-priority? Swali ndiyo hili kwamba haya yaliyopangwa ki-priority kwenye Ilani siyo barabara ile?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kujibu swali

416 la Mheshimiwa Lugola, ambaye bahati nzuri alikuwa mwanafunzi wangu Sengerema Sekondari na alikuwa mwanafunzi mzuri sana. Napenda kumthibitishia kwamba, yale yote yaliyopangwa kwenye Ilani ya Uchaguzi kuhusu barabara ikiwemo hata ile iliyotajwa mara ya kwanza ya kutoka Bunda hadi Kisolya, yenye jumla ya kilomita 118, nayo itajengwa kwa kiwango cha lami na ndiyo maana barabara nyingi zilizotajwa kwenye Ilani ya Uchaguzi zimeshamaliza kufanyiwa feasibility studies, ikiwa ni pamoja na hiyo barabara namba moja. Kwa mwaka huu wa fedha zimetengwa shilingi bilioni 1.9 kwa ajili ya kutangaza tender ili barabara hiyo na zingine zilizopo kwenye Ilani ya Uchaguzi zitengenezwe kwa kiwango cha lami. (Makofi)

MHE. MODESTUS D. KILUFI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nilitaka kujua umuhimu wa barabara zinapopangwa nini kinachoangaliwa, kwa sababu barabara nyingi zimekuwa zikipangiwa fedha lakini mwaka unapita na mwaka unaofuata zinapangiwa fedha tena pengine ndogo zaidi na bila utekelezaji. Wananchi wa maeneo yale wanakuwa na imani kwamba, barabara yao itajengwa kwa kiwango cha lami, lakini inafika muda mwaka unapita, bajeti nyingine inapita na ikipangiwa fedha ni kidogo, ambayo haitii matumaini kwamba, ile barabara itajengwa kwa kiwango cha lami. Sasa sijui inakuwaje; umuhimu unaangaliwaje? (Makofi)

MWENYEKI: Ahsante, swali zuri.

417 WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, hili tumelitambua na ndiyo maana bajeti ya mwaka jana ya Wizara ya Ujenzi ilikuwa shilingi trilioni 1.49 lakini bajeti ya mwaka huu ni shilingi trilioni 1.03. Nataka kumhakikishia Mheshimiwa Mbunge, yale yote tuliyoyaomba humu ndiyo yatakayotimizwa katika bajeti ya mwaka 2012/2013.

MHE. RIZIKI S. LULIDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda nimwulize swali Mheshimiwa Waziri kwamba, katika Sera ya Chama cha Mapinduzi ilitangazwa kuwa Mikoa ambayo iko nyuma kwa maendeleo ya barabara ukiwemo Mkoa wa Lindi, itapewa kipaumbele. Kipindi cha kiangazi barabara inapitika lakini kipindi cha masika wananchi ambao wanataka kwenda Liwale inabidi wazunguke mpaka Masasi ili kufika Lindi na Waziri akatoa ahadi akiwa Mchinga.

Je, Mheshimiwa Waziri anasemaje? Ahsante.

MWENYEKITI: Unauliza nini, maana Sera hapa ni kwamba; je, utaratibu wa kujenga barabara katika mikoa iliyoachwa nyuma unaendeleaje? Ndiyo Sera yenyewe hiyo na siyo habari ya kupitika sijui wapi sasa!

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutoa maelezo kwa Mheshimiwa Riziki. Kama alivyo-quote yeye mwenyewe Ilani ya uchaguzi na kama ambavyo mtaona katika Hotuba yangu ya Bajeti, ukurasa wa 81 hadi 92; fedha zilizotengwa nyingi zimeelekezwa katika Mikoa ambayo ilikuwa imeachwa nyuma ikiwepo ile ya

418 Kusini. Lengo ni kuhakikisha Mikoa hii inapata mawasiliano mazuri ya barabara zinazopitika katika kipindi chote cha mvua, masika, kiangazi, kipupwe na kadhalika. Kwa hiyo, huo ndiyo utekelezaji na hii bajeti, ime-reflect mwelekeo wa kuhakikisha kwamba, maeneo ambayo yalisahaulika kwa muda mrefu ni lazima yafunguliwe kwa barabara nzuri zaidi.

MHE. FELIX F. MKOSAMALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nina swali fupi kuhusu Sera za kutekeleza Ahadi za Rais. Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, amesema hizi barabara za Ahadi ya Rais za Kibondo Mjini hazitajengwa kwa sababu ya hii Barabara ya Nyakanazi – Kidawe, yenye kilomita 310, ambayo imetengewa shilingi bilioni 3.5. Nilitaka nimpe taarifa kwamba, hii barabara haipiti Kibondo Mjini, ni kilomita tano kutoka Kibondo Mjini. Sasa akisema hii ahadi haitatekelezwa maana yake anataka Wananchi wa Kibondo wasimwelewe vizuri Mheshimiwa Rais aliyeahidi pale. Naomba tu akubali ili mwaka kesho nimwunge mkono vizuri zaidi. (Kicheko)

MWENYEKITI: Swali lako halijibiwi kwa sababu siyo la Kisera. Mheshimiwa Machali. (Makofi)

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ukijaribu kufanya analysis ya Randama ya Makadirio ya Mpango na Bajeti kwa mwaka wa 2012/2013 inaonesha wazi kwamba, ni Sera ya Serikali kuhakikisha inajenga barabara zote ambazo zinaunganisha mikoa kwa kiwango cha lami. Ukijaribu pia kusoma vizuri na kufanya uchunguzi hata kwenye miradi ambayo imekwisha kutekelezwa katika maeneo

419 mbalimbali ya nchi yetu, utagundua kwamba, zile barabara ambazo zimekuwa zinafadhiliwa na Washirika wa Maendeleo kama vile MCC, JICA, ADB, World Bank na Washirika wengine zimekuwa na uhakika mkubwa sana wa kuweza kujengwa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ukiangalia pia kwenye ukurasa wa 126, barabara ya kutoka Kidawe – Nyakanazi ni moja ya barabara ambazo ziko kwenye mpango kama ilivyo kwenye barabara nyingine. Nataka ufafanuzi kutoka Serikalini; nini commitement ya Serikali kuhakikisha barabara hiyo nayo inaweza kupewa kipaumbele kwa kupewa fedha mapema iwezekanavyo hasa ikizingatiwa kwamba katika kipindi cha miaka miwili mfululizo iliyopita fedha zimekuwa zinatengwa lakini hazipelekwi huko? Sasa ili kuweza kutekeleza matakwa ya Sera na wananchi wakati mwingine wasione kwamba wanadanganywa kila wakati; Serikali inatuambia nini; itatoa kipaumbele au la?

MWENYEKITI: Siyo swali la Sera, halipati majibu. Mheshimiwa Mnyika. (Makofi/Kicheko)

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Katika mchango wangu wa maandishi, niliomba ufafanuzi wa Kisera wa Serikali kuhusiana na uondoaji wa tatizo la msongamano katika Jiji la Dar es Salaam. Nilitambua kwamba, msimamo wa Kisera wa Serikali ni kuwekeza kwenye Miradi ya muda mrefu ya Barabara Kuu ambayo kwa misingi ya msimamo wa Kisera inakwenda mpaka 2015/2016, wakati tatizo la foleni ni Janga la Kitaifa kuanzia sasa.

420

Nilieleza pia kwenye mchango wangu kuwa katika uandaaji wa bajeti, tunaongozwa na Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano. Sasa Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano ulitoa Mwongozo wa Kisera kuwa, mkakati mmojawapo wa kuondoa foleni Dar es Salaam ni kuharakisha ujenzi wa barabara za pembezoni za mzunguko (ring roards) ili watu wasilazimike kupita kwa wingi kwenye barabara kubwa. Ninaomba kupata ufafanuzi wa Kisera kutoka kwa Waziri; je, Wizara ipo tayari sasa kuandaa bajeti kwa kuzingatia Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano kwenye vipaumbele vya mwaka ambavyo vimewekwa ili kuweza kumaliza tatizo la foleni haraka zaidi?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, inawezekana labda ni bahati mbaya tu Mheshimiwa Mnyika hajasoma vizuri hotuba yangu, kwa sababu katika maelezo niliyoyatoa jana wakati nikiisoma hapa, suala la msongamano wala haliko Dar es Salaam tu, liko katika miji yote inayokua; Dar es Salaam, Mwanza, Arusha, Dodoma na maeneo mengine. Katika bajeti ya mwaka huu, nilieleza wazi kwamba, katika Miradi ya gharama kubwa inayotekelezwa kwa wingi, Mkoa ambao unaongoza katika nchi nzima ni Dar es Salaam. Miradi inayoendelea kule kwa ajili ya kupunguza msongamano kwa Dar es Salaam tu ina cost ya bilioni 899. Kwa hiyo, kama ni suala la Kisera, Sera imeanza kutekelezwa kwa kuzingatia Ilani ya uchaguzi katika kupunguza msongamano Dar es Salaam.

421 MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Awali ya yote, niseme Mheshimiwa Waziri hakujibu mambo ya msingi ambayo tuliyazungumzia katika Hotuba yetu ya Upinzani, amejibu yale mepesi na mazuri, mabaya ameyaacha.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nilihoji suala zima la shilingi 348,075,000,000 za mwaka jana ambazo zilitengwa katika bajeti na hazikueleweka zilikwenda wapi. Majibu yaliyotolewa ni kwamba, hizo fedha ni kwa ajili ya kuchangia sisi kama nchi pale ambapo tunachukua mikopo katika Miradi ya Maendeleo ya Barabara. Tukahoji, mwaka huu hizo fedha hazijatengwa na mwaka jana zimefanya kazi gani? Mheshimiwa Waziri hakuweza kutupa majibu, naomba atupatie majibu hizi fedha kwa nini mwaka huu hazikutengwa; na je, mwaka huu hatutakopa kwa ajili ya Miradi hiyo ya Maendeleo?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, namshangaa Mheshimiwa Mbunge kusema yalikuwa mabaya, kwa sababu mimi nayaona hayo ni mazuri tu. Hakuna mabaya na ndiyo maana nilimpongeza kwamba aliyoyachangia yote ni mazuri.

Zile fedha zilizowekwa kwa ajili ya special project katika bajeti ya mwaka jana ziliwekwa kwa ajili ya ku- reinfonce na kusaidia madeni yatakayokuwa yamejitokeza. Nimezungumza leo kwamba, bilioni 300 zimelipwa juzi kwa ajili ya kulipia madeni. Pia katika Miradi inayoendelea ya Wafadhili kuna Miradi mingine kwa mfano, Mradi wa Mheshimiwa Freeman Mbowe,

422 nataka niutolee mfano, bajeti ya kumaliza mradi ule ni shilingi bilioni 5.4, mpaka sasa hivi contractor ameshalipwa shilingi bilioni 1.59; kwa vyovyote Mkandarasi akifanya kazi kwa speed, fedha zilizokuwa zimetengwa zikawa ndogo, zile fedha ndizo zilizokuwa zinatumika kwa ajili ya kumlipa Mkandarasi. Kwa mwaka huu, hazikutengwa kwa sababu tunajua hatuna madeni, tumemaliza. Kwa hiyo, hatuwezi tukatenga fedha kwa kujua kwamba hatuna madeni. Ndiyo maana tumeomba hizi ambazo tunajua zitatosha. Kwa hiyo, hilo ulilolizungumza ni zuri tu, wala siyo baya, kama ulifikiri ni baya, ni makosa yako, sisi tunaliona ni zuri. (Makofi)

MHE. PROF. KULIKOYELA K. KAHIGI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana kwa kunipa nafasi niulize jambo dogo tu ili nipate ufafanuzi. Katika mchango wangu wa maandishi, niliuliza kuhusu Sera juu ya Wakandarasi ambao wanasababisha uharibifu katika majengo yaliyo karibu na maeneo ya migodi ya kokoto na pia wanaosababisha uchafuzi wa mazingira na hasa vyanzo vya maji. Nilitoa mfano wa Mgodi wa Kokoto wa Strabag ambao umesababisha uharibifu wa majengo ya Shule ya Msingi Busonzo katika Kata ya Busonzo, Bukombe na pia mgodi huo vumbi lake limesababisha uchafuzi wa vyanzo vya maji na Watendaji wa Halmashauri wanajua hili, lakini malalamiko ya wanakijiji hayajasikilizwa. Sasa naomba ufafanuzi kuhusu Sera juu ya jambo hili?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kutoa maelezo kwa Mheshimiwa Profesa Kahigi. Ni bahati

423 mbaya tu kwamba, maelezo yaliyotolewa na Waheshimiwa Wabunge na michango yao kulingana na muda tuliokuwa nao, tusingeweza kujibu yote. Tunakubali kwamba, alileta haya maelezo na bahati nzuri sisi Wizara huwa tunashirikiana sana na wenzetu wa Wizara ya Mazingira kuangilia ni lini athari zimetokea.

Mheshimiwa Mwenyekiti, lakini pia hili nalo lazima tulizingatie kwamba, wakati mwingine katika Miradi mikubwa inayofanyika, matatizo madogo madogo yanaweza kuwa yemejitokeza na hasa kwa barabara nzuri sana iliyojengwa ya kutoka Isaka – Bukombe – Lusahunga kupitia kwa Mheshimiwa Profesa Kahigi. Kwa hiyo, tutalichunguza na kuona hayo malalamiko yakoje na tunaweza tukayashughulikia kwa njia gani.

MHE. ESTHER N. MATIKO: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kwenye mchango wangu wa maandishi niliuliza kwamba, licha ya kwamba Mkoa wa Mara unachangia pato kubwa kwenye Pato la Taifa kupitia Mbuga ya Serengeti, Migodi tuliyonayo kama North Mara na mingine, kodi za Wananchi kwa maana ya Wafanyakazi, Wafanyabiashara na Wakulima, lakini tumekuwa tunapewa priority ndogo sana kwenye kugaiwa fedha kwa ajili ya matengenezo ya barabara.

Nilitaka nijue Serikali inatumia kigezo kipi kufanya allocation ya barabara?

MWENYEKITI: Allocation ya fedha kwenye barabara, Mheshimiwa Waziri.

424 WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, sisi Wizara hatujengi barabara za Majimbo wala za Mikoa, tunajenga Barabara za Kimataifa na ndiyo maana Trunk Roads na Regional Roards zinazosimamiwa na Wizara ni kilomita 35,000 katika nchi nzima.

Kwa Mkoa wa Mara, bahati nzuri barabara zote ambazo ni Trunk Roads ni za lami, isipokuwa barabara ya kutoka Makutano kwenda Mugumu. Kwa hiyo, tusingeweza kuanza kutengeneza Barabara za Mkoa na Wilaya, wakati kuna mikoa mingine barabara za lami hawajawahi kuziona. Kwa hiyo, tumeona tumalize kwanza, Trunk Roads za mikoa mingine ambayo haijaona barabara za lami, baadaye tutakapomaliza ndipo tutarudi kwenye Barabara za Mikoa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, na hiyo ndiyo Sera nzuri ya Chama cha Mapinduzi ya kugawana mapato madogo yanayopatikana kwa Taifa zima, badala ya kupeleka maendeleo ya barabara moja sehemu nyingine. Ndiyo maana utaona katika bajeti hii, Mkoa wa Kagera, Geita nilikotoka mimi, Mwanza, Mara na Shinyanga, fedha za Miradi inayoendelea ni ndogo ukilinganisha na mikoa mingine. Sababu ni moja tu kwamba, ukitoka Bukoba unaenda mpaka Mwanza kote ni lami, ukitoka Mwanza mpaka Sirari kwa Mheshimiwa anayezungumza ni lami na ukitoka Mwanza unapita Shinyanga yote ni lami, kwa hiyo, wale waliofaidika na barabara za lami kwa wakati ule, tuwaache na wengine wa sehemu nyingine wapate lami za Trunk Roards. (Makofi)

425

MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Moja ya maamuzi ya Bunge hili ni pamoja na ku-discourage matumizi ya foreign currencies katika shughuli za manunuzi nchini na ku- encourage shilingi itumike.

Katika mizani kumekuwa kukitozwa Dola za Kimarekani kwa watu wanaozidisha uzito. Je, Mheshimiwa Waziri haoni kwamba anachangia kuididimiza shilingi katika Taifa?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumjibu Mheshimiwa Mchungaji Msigwa, kama ifuatavyo:-

Mheshimiwa Mwenyekiti, Nchi ya Tanzania haiwezi ikawa isolated. Huwezi ukazikataa Dola, Euro, Kwacha au Shilingi. Kwa hiyo, kwa wale wanaozidisha uzito katika mizani kwa mfano, kwa nchi ambazo ni land locked; DRC, Burundi, Uganda na sehemu nyingine ni lazima walipe hizo dola kwa sababu tunaamini kama nchi tunapata faida zaidi. Hiyo ni hali halisi.

Pia katika masuala haya ya kutoza ushuru katika mizani, convention ya kawaida kutokana na rate iliyopo huwa inaruhusiwa. Kwa hiyo, hatuwalazimishi kulipa kwa dola, tunaangalia exchange rate iliyopo kwa sababu wakati mwingine mtu anafika pale na anakwambia yeye hana shilingi ana dola. Huwezi ukaikataa dola, unachofanya una-convent exchange rate iliyopo kwa wakati ule analipa halafu unakwenda unabadilisha kwenye T-shillings. Kwa hiyo, hiyo siyo

426 kwamba tunaichukia shilingi, tunaaipenda shilingi sana. Pia hili limefafanuliwa vizuri katika Sheria Na. 30 ya Mwaka 1973.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nimwambie tu Mheshimiwa Msigwa, ambaye bahati nzuri ni Mchungaji kwamba, tunaheshimu Sheria, ni kama vile zilivyo Amri Kumi za Mungu. Kwa hiyo, tunazingatia Sheria kama zilivyopitishwa, kama zina kasoro basi ziletwe Bungeni hapa na tuzifanyie mabadiliko. (Makofi)

MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Katika mchango wangu wa maandishi nilihoji Sera ya Serikali, pamoja na kuwa ni nzuri ya kuwajengea watumishi wake nyumba za kuishi kwa bei nafuu, lakini imeonekana kwamba, nyumba hizi specifically zile zilizokuwa chini ya TBA zimekuwa zikitumika kama urithi wa wale ambao walizipata mara ya kwanza. Kwa mfano, kuna Wabunge wengi ambao walibahatika kupata nyumba hizo kwa bahati nzuri au mbaya, hawakuweza kurudi tena Bungeni, lakini nyumba hizo wameendelea kuzihodhi na kuwarithisha ndugu zao au kupangisha kwa watu wengine. Kama ni Sera ya Serikali kuwajengea wananchi makazi especially watumishi wakiwepo Wabunge; Wizara inasemaje kuhusu kufanya uchunguzi yakinifu ili kujua ni akina nani wanamiliki nyumba hizo kinyume cha taratibu na wanazitumia vibaya matokeo yake Wabunge wanaishi kwa kutangatanga wanapanga nje ya nyumba? Ahsante.

MWENYEKITI: Kumbe unasemea hapa Dodoma!

427

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, tunauchukua ushauri wa Mheshimiwa Christowaja Mtinda, tutafuatilia ili tuone haki inatendeka kwa Waheshimiwa Wabunge wanaohitaji nyumba hapa Dodoma.

MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi. Kwa kuzingatia wingi wa wanawake nchini na kwa kuzingatia mahitaji ya wanawake ya capacity building nchini; ni lini Serikali itatilia maanani kuweka kiwango kikubwa kwa ajili ya kuwajengea uwezo wanawake nchini?

MWENYEKITI: Kiwango cha nini?

MHE. LETICIA M. NYERERE: Kiwango cha kuwa-train kwenye capacity building, maana nimeona kwenye Randama Wizara ya Ujenzi imeweka shilingi milioni 79 tu ambazo zinatosha ku-train wanawake watatu tu kwa mwaka.

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Wizara ya Ujenzi katika kuwajali akina mama na hasa katika masuala ya training, ipo juu na ndiyo maana hicho anachokizungumzia ni kuhusu kuwawezesha akina mama kushiriki katika Miradi ya Barabara. Ndiyo maana hadi hivi sasa kuna makampuni ya akina mama zaidi ya 160 ambayo yameshasajiliwa. Hata Mwenyekiti wa Wakandarasi Tanzania nzima ni mwanamama, Engineer Ngimbo. Kwa hiyo, hilo ni

428 katika kujali namna ya kuwawezesha akina mama katika kushiriki masuala ya biashara, lakini katika masuala ya kujiajiri wenyewe katika Miradi ya Ukandarasi.

MHE. CECILIA D. PARESSO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Katika mchango wangu wa maandishi, nilitaka kufahamu Wizara ina mkakati gani wa kuelekeza barabara za miji ambayo ni vitovu vya utalii ili ziweze kushughulikiwa na TANROADS badala ya Halmashauri. Ahsante.

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyosema ni vigumu kuzichukua barabara zote za utalii, barabara zote za TAMISEMI, zikashughulikiwa na TANROADS; unless tuje hapa Bungeni tutoe mapendekezo kwamba sasa fedha zinazopelekwa TAMISEMI ambazo ni zaidi ya asilimia 30 za Road Fund zihamishiwe TANROADS na barabara zote za Halmashauri na zinazoshughulikiwa kwenye utalii zihamishiwe huko kwa sababu kupanga ni kuchagua. Kwa hiyo, Wizara yetu inashughulikia barabara ambazo zipo chini ya Wizara yake, ambazo ni Regional Roads na Trunk Roads.

Pakitokea maamuzi mengine ya Kisera kupitia Waheshimiwa Wabunge kwamba, sasa wakati umefika wa barabara zote Tanzania zinakuwa chini ya TANROADS, sisi tutatekeleza, lakini kwa hivi sasa tunaziachia mamlaka zinazohusika na barabara hizo. Wale wanaoshughulika na utalii, TANAPA na kadhalika, washughulikie na barabara zao, TAMISEMI washughulikie barabara zao na sisi tushughulikie

429 barabara zetu. Hiyo ndiyo Sera ya mgawanyo wa kazi mzuri.

MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nilizungumza wakati wa mchango, pamoja na kazi nzuri ambayo Wizara imeifanya ya kuweka alama za mipaka katika Barabara zote Kuu nchini bado Wizara inatumia fedha nyingi kulipa fidia kwa ajili ya kuwahamisha wananchi pamoja na mali zao.

Sasa ni lini Wizara itaweka Sera Maalum na kutengeneza Master Plan ya Road Network ya nchi nzima ili kuwafanya wananchi popote katika Miji Mikubwa, Miji Midogo na hata katika Mitaa yetu kutambua kuwa sasa na hata kwa miaka mingi ijayo kwamba barabara zitapita maeneo gani wasiyaendeleze maeneo hayo na kufanya fedha za maendeleo kutumika kulipa fidia?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda kumjibu Mheshimiwa Koka, kama ifuatavyo:-

Master Plan za barabara zote katika nchi nzima zipo. Actually, kwa kupitia Sheria Na. 4 ya Ardhi ya Mwaka 1999, Sheria Na. 5 ya Vijiji ya Ardhi ya Mwaka 1999, Sheria ya Mipango Miji ya Mwaka 2007 na Sheria ya Road Reserve ambayo imepangwa ya Sheria Na. 13 ya Mwaka 2007, network ya barabara zote zipo na ndiyo maana tunazugumzia hapa kuhusu kilomita 35,000. Katika sheria ile inazungumzia wazi kwamba, kuna maeneo ambayo yako ndani ya Road Reserve

430 na kwa kutambua kwamba wananchi wasipate shida ndiyo maana Serikali imechukua gharama kubwa za kuweka plots au maeneo ya kuonesha kwamba hapa ni mwisho wa barabara. Hili ni lengo kubwa la kuwasaidia wananchi kwamba wasivamie maeneo hayo.

Pia katika barabara mpya hili haliwezi kuepukika kwa sababu unaweza ukawa na network ya kilomita 35,000 ukafika mahali ukahitaji barabara nyingine kutengeneza mahali ambapo ni kwenye makazi ya watu. Kila mahali tunapotengeneza barabara mpya kwa makazi ya watu, wale watu wanalipwa kwa mujibu wa Sheria hiyo Na. 13 ya Mwaka 2007, lakini pia kwa mujibu wa Sheria za Ardhi Na. 4 na 5 za Mwaka 1999, kifungu Na. 3(g).

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Ningependa kufahamu, katika mchango wangu wa maandishi niliishauri Serikali itengeneze Mkakati Maalum ambao unaweza ukaainisha gharama halisi za ujenzi wa barabara zote za lami ili ikiwezekana hata tuchukue mkopo ili tuweze kujenga barabara zote. Kwa sababu kadiri tunavyochelewa kujenga gharama zinazidi kupanda na ukiangalia sasa hivi kwa kipindi cha miaka mitano tuliyopita gharama zimeongezeka kwa zaidi ya shilingi bilioni 500 au 600.

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, hili suala limepokelewa na Serikali, wenzetu wa Tume ya Mipango na Wizara ya Fedha kama wataliona

431 linawezekana la kuchukua mikopo yote ili isi-bust na kadhalika, sisi hatuna tatizo. Wizara tukipewa fedha tunatekeleza tu hata zitoke wapi. Kwa hiyo, ushauri wako tutaufikisha kwa wanaohusika na bahati nzuri wapo wanakusikiliza, Serikali ikapata mkopo wa kutosha, nafikiri ni ushauri mzuri.

MHE. NYAMBARI C. M. NYANGWINE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Katika mchango wangu wa maandishi nilitaka kujua Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba barabara zote za mipakani, yaani zile security roads zinapitika kwa sababu barabara hizi ni muhimu sana kwa ulinzi na usalama wa nchi yetu?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, katika maelezo yetu tuliyoyatoa hapa, zimepangwa fedha almost shilingi bilioni 300 ambazo zitagawanywa katika Mikoa yote 25 ya Tanzania Bara. Nimeshatoa maelekezo kwa Regional Managers wote katika nchi nzima waweze kuangalia pia uwezekano wa namna gani wanaweza kuzifanyia services barabara zilizoko mpakani ili nazo ziweze kupitika lakini pia zitumike kwa ajili ya ulinzi wa nchi yetu.

MHE. MENDRAD L. KIGOLA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante sana. Napenda nimwulize Waziri kwamba; hapa Tanzania tuna wasomi wengi sana wanaosomea masuala ya barabara. Je, ni lini sasa tutafikia kipindi tuseme kwamba sasa hatutegemei wakandarasi kutoka nje tunategemea wakandarasi wa ndani?

432 WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kabisa katika nchi yetu tuna wasomi wengi sana. Mpaka leo ninavyozungumza, engineers ambao wapo registered ni zaidi ya 11,400 ambao wanasajiliwa na Engineers Registration Board, ambayo ipo chini ya Profesa Lema, ambaye ni Mwalimu wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam.

Kweli pia kwamba, tangu tupate Uhuru wakati huo tulikuwa na Wakandarasi wachache tu wa Kizalendo. Leo tunapozungumza tuna wakandarasi zaidi ya 9,041 waliosajiliwa. Almost karibu 95 per cent ni Wakandarasi Wazalendo. Tumeanza sasa kuwatumia wakandarasi wazalendo ili waweze kushiriki kikamilifu katika kazi ya barabara. Pia wakandarasi wa kigeni ambao wanapata kazi kupitia Sheria ambayo mmeipitisha hivi karibuni ya PPP inaruhusu makampuni ya Wakandarasi Wazalendo at least kuweza kushiriki katika kazi za barabara, nafikiri kati ya asilimia 15 na 25, kwa hiyo, tunalizingatia hili kwa sababu sasa tuna wataalamu wa kutosha.

MHE. JUMA A. NJWAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Nasimama ili kuweka mambo sawa sawa hapa kidogo. Wakati wa mchango wangu, sikuunga mkono hoja kwa sababu nyingi tu mojawapo ikiwepo barabara niliyokuwa nimeitaja ya Tandahimba – Newala – Mtwara kuwa ni ya Ilani na hivyo ni Sera ya CCM ya kupeleka huduma ya barabara karibu na wananchi na hasa kwenye matatizo. Pia Mheshimiwa Waziri kushindwa kutimiza ahadi yake ya kumaliza fedha zote safari hii kama alivyoniahidi mwaka jana.

433 Amejieleza vizuri, lakini pia shilingi milioni 700 ambazo zimetengwa kwenye barabara hizo, ukijumlisha na shilingi milioni 375 ni karibu shilingi 1,750,000,000. Kwa kuwa naamini Wizara yake haiwezi kukosa shilingi 425,000,000 kwa mwaka huu wa kumalizia barabara hiyo, basi nasimama kusema naunga mkono hoja. Ahsante. (Makofi)

MHE. DESDERIUS J. MIPATA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Katika mchango wangu wa maandishi nilihoji na kuomba ufafanuzi pale kunapokuwa na upanuzi au ujenzi wa barabara na inapotokea barabara inapita kwenye makaburi na Serikali kulazimika kuacha kuendeleza ujenzi wake na hatimaye kuhama na kuathiri makazi ya wananchi zaidi ya mitaa mitatu ambayo inakuwa ni gharama kubwa kuliko kuhamisha makaburi.

Nikatoa mfano kama ilivyotokea kwenye kijiji kimoja cha Chala, katika ujenzi wa barabara inayotoka Sumbawanga kwenda Kanazi, ambapo vijiji vyote vimeshapata fidia, lakini kwa sababu ya makaburi tu Serikali inakubali kubeba mzigo mkubwa wa gharama na imeshindwa kulipa mpaka sasa.

Mheshimiwa Mwenyekiti, nataka ufafanuzi.

MWENYEKITI: Suala la Sera la Ujenzi wa Barabara kwenye makaburi.

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, hawa watani zangu Wafipa sifahamu hayo makaburi yana nini. Katika

434 kutengeneza barabara huwa kuna mambo mengi yanaangaliwa wakati wa feasibitility study, detailed design mpaka inapofika wakati wa construction. Kwanza, huwa wanaangalia ni namna gani wanaweza kutengeneza barabara ambayo ni fupi zaidi kwa gharama chache zaidi, lakini pia wanaangalia cost ambazo zinakuwepo katika aidha wakipitisha mahali fulani ni kwa namna gani wanaweza wakalipa fidia na kadhalika na ndiyo maana utaona hata barabara hii ya Central Corridor haikupita katika Kijiji cha Iguguno. Unaona hii katika barabara ya kwenda Mwanza haikupita katika Mji wa Misungwi kwa sababu tulijua tukipitisha pale tutalipa compesation kubwa. Kwa hiyo, hayo yote huwa yanaangaliwa.

Katika ujenzi suala la makaburi wala siyo kitu kigeni, kwa sababu Barabara ya Kawawa tuliweza kuhamisha makaburi tukaunganisha barabara ya kwenda Airport kwa kuwalipa fidia na barabara ikapita. Kwa hiyo, sifahamu hayo makaburi ya watani zangu kule Sumbawanga yakoje, nitajaribu kufuatilia inawezekana labda waliogopa kwa sababu makaburi yana mambo yao, yana matambiko yao.

Ninachotaka kusema ni kwamba, barabara haiogopi makaburi. Kama barabara inapita kwenye makaburi na tunajua linaweza inatengenezwa kwa kuzingatia sheria na kadhalika, yale makaburi yanaweza kulipwa fidia. Tutajaribu kufuatilia ni kwa namna gani hiyo barabara ilifanya diversion na baadaye nitamjibu tu Mheshimiwa mtani wangu kuhusu hiyo barabara husika.

435 (Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1002 - Finance and Accounts Unit ...... Sh.759,954,900

MWENYEKITI: Mheshimiwa Leticia Nyerere. Sasa hapo itabidi mseme kifungu.

MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kasma 410200 - Acquisition of Vehicles and Transportation Equipment. Sijui kama ni typing error au ni nini; wameandika mwaka wa fedha huu ni shilingi 1,000. Naomba ufafanuzi.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu hiki tumeweka kama token, fedha zikipatikana tunaweza kununua gari.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1003 - Policy and Planning Division … …Sh.766,462,000

MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kasma ya 220400 - Medical Supplies and Services. Kwa mwaka wa fedha huu inaonekana shilingi 440,000/=. Naomba ufafanuzi kwa nini zimeshuka kiasi hicho. Nipate maelezo watatumia mbinu gani?

436 NAIBU WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu hiki fedha zimepungua kwa sababu ya ufinyu wa bajeti.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1004 - Government Communication Unit …Sh.321,156,100 Kif. 1005 - Procurement Management Unit …Sh.336,646,900 Kif. 1006 - Internal Audit Unit … … Sh. 247,410,900

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1007 - Legal Service Unit … … Shs.162,921,200

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Kasma 210100 - Basic Salaries - Pensionable Posts.

Ukiangalia pale mwaka 2010/11 ilikuwa ni takriban kama Sh. 37,644,089, lakini mwaka jana ilipungua na kuja Sh. 17,662,000. Mwaka huu imekuja kwenye shilingi 30,759,600, hata kwenye vifungu vingine pia umeona kwamba kwenye mwaka 2011/12 kumekuwa na hali kama ya kupungua kwenye fungu hili la mishahara. Sasa nilikuwa nataka kujua ni sababu gani ambayo imepelekea mwaka jana imeshuka na mwaka huu imeongezeka kwa kiasi ambacho kidogo ni kikubwa. Naomba ufafanuzi.

437 NAIBU WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kwamba, mwaka huu imepanda kidogo kutokana na ajira mpya na kuna nyongeza ya mshahara pia na kupandishwa vyeo.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 1008 – Information Communication Technology…...... Sh. 200,092,100

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 2002 – Technical Services Division … ..... Sh.9,085,193,300

MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kasma 220200 - Utilities Supplies and Services. Ninahoji kwa nini kuna sifuri watatumia mbinu gani?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, hiki Kitengo hakihusiki na mambo ya supplies yapo Utawala, kwa hiyo, hatuwezi kuwatengea fedha.

MWENYEKITI: Na ni miaka miwili mfululizo.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya

438 Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 2005 - Roads Development Division … Sh. 314,393,900

MHE. ANDREW J. CHENGE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana. Nataka kwenye hiyo Sub-Vote 2005, item 270800. Ukurasa wa 171 kwenye Hotuba ya Mheshimiwa Waziri, unaona fedha za Mfuko wa Barabara ni bilioni 376.4. Sasa hapa kuna ongezeko ambalo nimejaribu kuangalia kwenye vitabu nashindwa ku-reconcile hizi figure ambazo zipo kwenye Kitabu cha Hotuba ya Waziri na kwenye item hii hapa. Sijui kama nimeeleweka?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi fedha ni za Mfuko wa Barabara na katika fedha hizi asilimia 70 huwa zinaenda Wizara ya Ujenzi na asilimia 30 zinaenda TAMISEMI. Road Fund kwa ujumla ipo chini ya Wizara ya Ujenzi. Kwa hiyo, ndiyo maana fedha hizi zimewekwa hapa na ukiangalia kwenye kitabu cha maelezo, zile zinazokwenda Wizara ya Ujenzi ni shilingi bilioni 300.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 2006 - Transport Services Division …. …. … …Sh. 0

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

439

Kif. 5002 - Safety and Environment Division … … … …Sh. 662,993,700

MHE. LETICIA M. NYERERE: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Kasma 410500 - Acquisition of Household and Institutional Equipment. Nilikuwa nahoji kwa nini kuna 12.5 million wakati miaka miwili ya fedha hapakuwa na amount yoyote? Naomba maelezo.

NAIBU WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kifungu hiki ni kwa ajili ya ununuzi wa samani za ofisi. Kwa sababu baada ya kutenganisha Wizara, Ofisi imekuwa haina samani kwa hiyo inabidi tuzinunue, ndiyo maana mwaka jana hazikuwepo.

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nilitaka kujua tu kwenye item 220900, ambayo ni kwa ajili ya training, nimeona kama hakuna fedha yoyote ambayo imetengwa this time. Sasa hatuna mahitaji tena ya kufanya training?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, masuala ya training tumeyapeleka Utawala.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

MATUMIZI YA MAENDELEO

Fungu 98 – Wizara ya Ujenzi

440

MWENYEKITI: Tukifika kifungu hiki maana yake fedha zilizotengwa ni kwa Mradi huo. Sasa usianze kusema mimi mbona ya kwangu hapa haionekani; inayoonekana ndiyo hiyo iliyoko hapo. Ndiyo utaratibu wenyewe, maana ukisoma ile Kanuni inasema wakati wa Kamati ya Matumizi huwezi kuongeza fedha na kama ukitaka kuhamisha ni fungu zima, kitu ambacho siyo rahisi. Kwa hiyo, unaweza ukasema tu kwamba Mradi huu hela hizi zimetengwa, kwa mfano, HIV wasipoeleza maeneo gani ambayo hiyo shughuli inahusika.

Kif.1001 - Administration and HR Management … … …Sh. 0 Kif.1003 - Policy and Planning Division …. …. … … …. ...Sh. 992,472,000 Kif. 2002 - Technical Services Division … … … … …Sh.14,149,336,000

(Vifungu vilivyotajwa hapo juu vilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif.2005 - Roads Development Division … … …. … Sh. 673,346,584,000

MHE. JUMA. A. NJWAYO: Mheshimiwa Mwenyekiti, ukurasa wa 295, item 4143 - Ndundu Somanga Road. Imetengewa shilingi bilioni 4.077. Tumekuwa na masikitiko makubwa na wananchi wanalamika sana kwenye eneo hili. Malalamiko ni mengi, sasa nilitaka kujua hizi hela naziona bado ni kidogo, ndiyo zinamaliza tatizo la pale kwamba hatutarudi tena

441 hapa kuomba hela? Sisi tungependa ahadi ya Mheshimiwa Waziri ya Oktoba mwaka huu kuwa imemaliza barabara. Ahsante.

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, Mradi huu wa kilometa 58, gharama ya Mradi mzima ni shilingi bilioni 59. Kandarasi yupo kwenye site. Mpaka hivi sasa ameshalipwa zaidi ya bilioni 45. Hizi fedha zilizotengwa ni kwa ajili ya bajeti ya mwaka huu. Pia Mkandarasi anapokuwa kwenye site anapomaliza kazi huwa halipwi fedha zote, zinabaki fedha zingine zinashikiliwa na Serikali mpaka grace period ya kuangalia ule Mradi unapokamilika na huwa kati ya mwaka mmoja mpaka mitatu. Kwa hiyo, zile zitakazokuwa zimebaki akimaliza mwaka huu zitakuwa zinasubiri mpaka ile time ya kuangalia barabara ile itakapokamilika, ndiyo maana utaona katika Barabara za Nangurukuru Wakandarasi walimaliza miaka mitatu iliyopita lakini katika bajeti ya mwaka huu tumewapangia kuwalipa malipo yao ya mwisho, ikiwa ni pamoja na Daraja la Umoja ambalo limefunguliwa zaidi ya miaka miwili iliyopita, mwaka huu ndiyo tumeweka fedha za kumalizia Miradi yao kwa sababu kipindi kile cha uangalizi kimeisha. Kwa hiyo, Mkandarasi huyu pamoja na kwamba anadai fedha hizo zote, hatapewa zote mpaka atakapomaliza kazi na ile grace period ya miaka mitatu atakapokaa pale.

MHE. MHONGA S. RUHWANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Mimi nipo katika kifungu kidogo 4164, ambacho kinaelezea Barabara ya Kidahwe – Kasulu – Kibondo – Nyakanazi. Nimesimama kuomba

442 commitment ya Serikali na nasema hivyo kwa sababu ya historia ya nyuma juu ya ukamilishaji wa barabara hii na pesa ambazo zimekuwa zikitoka kidogo kidogo na wakati mwingine. Kutokana na historia ya nyuma kwamba katika kipindi cha Bunge la Tisa, miaka yote mitano majibu yalikuwa … natumia neno ambalo ulisema hukutaka nilitumie kwamba, yalikuwa kama ya ulaghai, ambayo kila mara tulikuwa tunaambiwa tupo kwenye usanifu, upembuzi yakinifu, usanifu wa kina. Sasa hivi katika ukurasa wa 31 katika Kitabu chake cha Hotuba amesema, usanifu umekamilika na maandalizi ya kutangaza zabuni za kazi ya ujenzi kwa sehemu ya Kidahwe – Kasulu – Nyakanazi yanaendelea. Sasa nataka kujua ili jibu hili lisiwe kama la miaka yote hii mitano kwamba mpango unaendelea wa kutangaza zabuni. Ninataka kujua commitment ya Serikali; Mpango Mkakati wake ni kumaliza barabara hii kwa kiwango cha lami muda wa miaka mingapi ili tuache kusimama simama na kuuliza kuhusu barabara hii.

MWENYEKITI: Kwa hiyo umeondoa neno ulaghai?

MHE. MHONGA S. RUHWANYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, sawa.

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, commitment ya Serikali ni pamoja na kuweka hizi fedha na ndiyo vimeandikwa kwenye Vitabu vya Hazina, tumeweka shilingi bilioni 3.5 kwa ajili ya kuanza Barabara ya Nyakanazi – Kidahwe. Hiyo ndiyo commitment ya Serikali.

443 MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru. Nami nakwenda kwenye kasma hiyo hiyo ya 4164 - Barabara ya Kidahwe – Kasulu – Kibondo – Nyakanazi.

MWENYEKITI: Mheshimiwa Machali, Kanuni inakataa please.

MHE. MOSES J. MACHALI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni swali lingine.

MWENYEKITI: Hapana. Akishauliza mwenzio kuhusu kasma ile ile, Kanuni inasema haurudii. Naomba msome Kanuni, kwa sababu alipouliza yule basi tayari swali lako limekwisha. Sasa tunaendelea na Mheshimiwa Nkumba.

MHE. SAID J. NKUMBA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Mimi nataka nipate ufafanuzi kwenye Kitabu cha Maendeleo Sub-Vote 2005, item 4148, zimetengwa shilingi bilioni 1.2, lakini kwenye Hotuba ya Mheshimiwa Waziri na bahati nzuri kwenye majibu ya Mheshimiwa Waziri amejibu kwamba, Tabora –Sikonge, kilometa 70 zipo shilingi bilioni moja na Ipole – Koga – Mpanda zipo shilingi bilioni 1.2. Kwa hesabu zake hapa kwenye Kitabu cha Hotuba ni shilingi bilioni 2.2. Ninataka nipate ufafanuzi; fedha hizi shilingi bilioni 1.2 ambazo najua ndizo zitakazokuwa zimetengwa kwa ajili ya shughuli hizi za maendeleo ambazo zimeoneshwa kwenye Kitabu hapa na ahadi hii nayo naweza kwenda kuitumia kwa sababu ni ahadi ambayo ametolea kama maelezo ya hotuba. Sasa

444 naomba nipate ufafanuzi. Hii bilioni moja ipo wapi kwenye Kitabu hiki cha Maendeleo au ataitoa wapi?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, naelewa concern ya Mheshimiwa Nkumba. Fedha zilizotengwa katika item hii ni zile zinazotokana na development. Zile zingine 1.2 zimetengwa kutokana na fedha zinazotokana na Mfuko wa Barabara, ambazo zipo kwenye viambatanisho hivi. Fedha za Mfuko wa Barabara bahati nzuri kifungu chake tumeshakipitisha na kiliulizwa na Mheshimiwa Chenge. Miradi yake huwezi ukaiandika yote kwa sababu ina-cover nchi nzima. Kwa hiyo, namhakikishia Mheshimiwa Nkumba kwamba, Mradi ule una 2.4 billion. 1.2 ni kutoka kwenye development na another 1.2 ni kutoka kwenye Road Fund.

MHE. CAPT. JOHN Z. CHILIGATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kuniona. Nipo kwenye Sub- Vote 2005, kifungu kidogo 4118, kuhusu Dodoma Manyoni Road. Nilitaka kupata ufafanuzi kwamba, kwa kuwa Barabara ya Dodoma – Manyoni – Singida imepita pembeni mwa Mji huo wa Manyoni na wakati wa kuizindua Barabara hiyo, Waziri Mkuu alitoa ahadi kwamba kile kipande cha barabara ya zamani ambacho kinapita katikati ya Mji wa Manyoni, ambacho kina urefu wa kama kilomita tano tu nacho kingewekwa lami. Mwaka jana niliuliza Waziri akasema pesa hazikuwekwa lakini akaahidi kwamba mwaka huu zingewekwa na kwa sababu ni rafiki yangu wa siku nyingi nikamwamini. Sasa sehemu ya fedha

445 zilizotengwa katika kasma hii zitatekeleza ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi fedha zilizopo katika kifungu hiki, shilingi milioni 230 ni kwa ajili ya kumalizia kulipa deni la Mkandarasi kwa kuwa time ya kuangalia ule Mradi imekamilika, ambazo ni shilingi milioni 230. Ile ahadi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu na ambapo nimezungumza na Mheshimiwa Chiligati, ya kuanza kutengeneza barabara iliyokuwa ya zamani bado ipo pale pale na nina uhakika tutaangalia kwa kutumia fedha za Mfuko wa Barabara, ambazo kwa bahati nzuri katika mwaka huu tuna shilingi bilioni 300 ili tuanze kutengeneza barabara yake ya Manyoni kwa awamu.

MHE. JOHN J. MNYIKA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Kasma 4138, ukurasa wa 296 - Decongestion of Dar es Salaam Road na ndicho kifungu kinachohusika na kupunguza msongamano kwa kutumia barabara za pete na barabara za mzunguko. Sasa nimeisoma Hotuba ya Waziri, ukurasa wa 115, ambao unazungumzia kuhusu hizi barabara na zimetengenezwa orodha za barabara za Dar es Salaam. Vilevile nimesoma Mpango wa Taifa wa Miaka Mitano, ukurasa wa 131, ambao ndiyo unatoa mwongozo wa mgao wa fedha kwenye kifungu hiki. Sasa ukiangalia kwa mwaka wa fedha uliopita, kifungu hiki kilitengewa shilingi bilioni tano wakati Mpango wa Taifa ulihitaji kifungu hiki kitengewe shilingi bilioni 68. Nilipouliza mwaka jana niliambiwa ilikuwa ni kipindi cha mpito, mwaka huu pesa zingeongezwa. Mwaka huu

446 kimetengewa shilingi bilioni 10.5 na kwa mujibu wa Mpango wa Taifa tulioupitisha Bungeni mwaka huu, kilitakiwa kitengewe shilingi bilioni 31.

Kwa hiyo, ukichanganya shilingi bilioni 31 ya mwaka huu na shilingi bilioni 68 ya mwaka jana, in total hizi barabara zilipaswa zitengewe shilingi bilioni 100 na hapa ndiyo nazungumzia barabara kama ya Goba kupunguza foleni ya Morogoro Road au barabara ya ahadi ya Rais ya Kimara kupitia Bonyokwa, Mavurunza, Maramba Mawili na nyinginezo ambazo orodha imetajwa lakini kiwango cha pesa ni kidogo sana ukilinganisha na ilivyopaswa kupangwa na Mpango na ikilinganishwa vilevile na commitment ambazo Serikali imepitisha.

Napenda kupata ufafanuzi kutoka kwa Mheshimiwa Waziri, kutokana na umuhimu wa hizi barabara kwenye kupunguza foleni kwa haraka kwa dharura ni kwa nini kiwango kisizingatie Mpango wa Taifa wa Maendeleo wa Miaka Mitano?

MWENYEKITI: Swali sasa hivi fedha ni za nini? Naomba kwanza nitumie Kanuni ya 104(2), kuongeza dakika 30 baada ya muda wa kawaida wa kuahirisha Bunge. Mheshimiwa Waziri.

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, nilieleza Miradi inayoendelea Dar es Salaam kwa ajili ya kupunguza msongamano ina gharama ya shilingi bilioni 899. Miradi iliyotajwa katika item hii, nataka nimfafanulie Mheshimiwa Mnyika ni Barabara ya Round About

447 Msimbazi –Twiga, ina milioni 1,000. Ubungo Terminal – Kigogo ina milioni 1,073, Jet – Vituka –Devis Corner ina milioni 1,200, Ubungo Maziwa – External ina milioni 777, Kimara Kilungule – External ina milioni 1,000, Mbezi Malamba Mawili – Kinyerezi – Banana na nafikiri huko ndiko kwake milioni 2,000, Tegeta Kibaoni – Wazo – Goba – Mbezi Morogoro ina milioni 2,100, Tangibovu – Goba milioni 1000, Kimara Baruti milioni 577. Hizi ni katika vile visehemu vya barabara za pembeni.

Katika Miradi mikubwa inayoendelea kwa Dar es Salaam katika kupunguza msongamano nilieleza kwamba, kuna Barabara ya Kimara – Mjini mpaka Kariakoo kwenda Morocco gharama ya ule Mradi ni bilioni 240. Kuna vituo vya mabasi zaidi ya vinane na vituo vidogo vidogo 29, cost yake ni bilioni 47. Kuna Mradi wa kutoka Tegeta kwenda Morocco kwa kupitia Mwenge kuna bilioni 88. Kuna Daraja la Kigamboni kuna bilioni 214, kuna barabara nyingine hata ya kupitia Bagamoyo kwenda Msata ina bilioni 89 na Miradi mingine mingine. Kuna fly-overs bilioni 2000 na kadhalika. Hizi ni baadhi ya barabara ambazo tumezitaja ambazo zimetayarishwa kwenye kasma hii zingine zipo kwingine.

Katika Miradi mingine ambayo inaendelea mingine inafadhiliwa na wafadhili. Nafikiri kwa hayo machache ameelewa.

MWENYEKITI: Samahani, Kanuni niliyoongezea muda ni 104(1) siyo kifungu kidogo cha (2).

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya

448 Matumizi bila mabadiliko yoyote)

MWENYEKITI: Kifungu nilichoongezea muda ni cha 104, kifungu cha kwanza, siyo cha pili.

Kif. 2006 - Transport and Service Division …… …… …………. Sh. 0

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

Kif. 5002 - Safety and Environment Division …… …. Sh. 5,459,880,000

MWENYEKITI: Mheshimiwa Zambi, halafu atafuata Mheshimiwa Mangugu.

MHE. GODFREY W. ZAMBI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninashukuru kwa kunipa nafasi. Kifungu hicho hicho cha 5002, kifungu kidogo cha 4136 - Road Safety Activities. Kwa uelewa wangu ni kwamba, kifungu hiki ndicho kinachohusika na shughuli kama vile alama za barabarani, ufyekaji wa majani barabarani, lakini pia uwekaji wa matuta ndivyo ninavyoelewa. Kama hivyo ndivyo, labda Waziri anaweza kutusaidia.

Ninafurahi kuwa kifungu hicho kimetengewa hela nyingi sana za kutosha karibu bilioni 4.3, lakini inasikitisha kwamba, barabara zetu nyingi matuta yaliyowekwa hayana standard, ukipita kwa mfano pale Morogoro, mengine ni makubwa mno na tumeshawahi kulalamika humu Bungeni kwamba

449 yapunguzwe yawe na viwango sawasawa lakini mpaka leo hakijafanyika chochote.

Mheshimiwa Mwenyekiti, hata magari mengine yanaharibika barabarani na inachukua muda mrefu sana kuondolewa. Mtakumbuka kuwa mwaka juzi kule Mkoani Morogoro Kikundi cha Five Stars, wale wanamuziki waliokuwa wanatoka Mbeya, walifariki kwa sababu gari lingine liliharibika na lilichukua muda mrefu kuondolewa. Sasa wakati tunatenga pesa nyingi kwa ajili ya shughuli hizo barabarani na wakati huo pia unakuta alama nyingi za barabarani hazipo; Waziri anatuhakikishiaje au nachukua hatua gani kuhakikisha kwamba barabara zetu zinakuwa na matuta ambayo yana standard, majani barabarani yanafyekwa na magari yanayoharibika yanaondolewa immediately ili kuondoa madhara yanayoweza kupatikana? Ahsante.

MWENYEKITI: Kwamba hizi hela ni za haya aliyoyasema? Ndiyo swali lenyewe.

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza, kifungu hiki hakihusiki na kufyeka majani na kutengeneza matuta. Kifungu hiki kinahusika na kujenga mzani katika eneo la Vigwaza na ndiyo maana kuna fedha za wafadhili pale tunahamisha Mzani wa Kibaha tunapeleka Vigwaza na ule mzani utakuwa wa kisasa, utakuwa unapima magari yakiwa kwenye mwendo. Fedha ambazo zimetengwa kwa ajili ya kufyeka majani, rehabilitation, matuta na kadhalika, zimetengwa kupitia fedha za Mfuko wa Barabara ambazo

450 zimegawanywa kwa Regional Managers wote lakini ninataka kumhakikishia kuwa suala la matuta kwa mfano yale ambayo siyo standard, tumeliona na tumechukua concern ya Waheshimiwa Wabunge, tutayafanyia kazi, ikiwa ni pamoja na mengine kuyapunguza kwa sababu uwekaji wa matuta kila mahali nalo ni tatizo.

Mheshimiwa Mwenyekiti, ninapenda pia nitoe wito kwa wananchi, panapotokea ajali watu wanakwenda kuweka matuta; huku ni kuvunja Sheria. Kwa hiyo, tutaweka alama za barabarani, watu wasiende kwenye barabara na kuanza kuchimba na kuweka magogo. Tutaanza kuchukua hatua kwa watu wanaoingia kwenye barabara na kulazimisha kuweka matuta kwa sababu wanatulazimisha kuvunja Sheria. (Makofi)

MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kifungu hicho cha 5002, kifungu kidogo cha 6212, nimeona hili ni eneo ambalo kuna road safety na hizo alama nyingine za usalama barabarani. Serikali imekuwa ikitumia gharama kubwa sana kuweka na kununua alama za barabarani lakini kumezuka mtindo ambao siyo kwa kiungwana, ambapo watu wanang’oa zile alama na kwenda kuuza kama chuma chakavu. Ukiangalia kimsingi wanaosababisha hili siyo wale ambao wanang’oa, wanaosababisha ni wale ambao wananunua. Sisi kama Serikali kwa nini tusiwabane wanunuzi ili hivi vitu visiwe na soko kwa sababu huwezi kukuta mtu anabandua lami kwenda kuiuza kwa sababu haina soko?

451

Nilitaka kujua Mheshimiwa Waziri pamoja na kutenga pesa hizi milioni 800 zinahusika pia na ku- enforce watu ambao wanafanya vitendo vya kihalifu?

MWENYEKITI: Swali ni kwamba shilingi milioni 800 ni za nini hapa?

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, hizi fedha ni kwa ajili ya Kitengo cha Road Safety na Environment. Katika Wizara ya Ujenzi tuna Kurugenzi inayohusika na masuala ya mazingira. Kabla Mradi wa Barabara haujaanza kutengenezwa, lazima pawepo na assessment za kimazingira na kuona ule Mradi hauna effect ya masuala ya environment, lakini zingine zinazobaki ni katika control ya masuala mengine ya support katika mambo ya safety, tukishirikiana na Wizara ya Mambo ya Ndani na Wizara nyingine.

Suala alilolizungumza ni la ukweli, Serikali inalichukua lakini Polisi pia watakuwa wamelichukua ili pawepo na ukaguzi hata kwenye viwanda vinavyohusika na kutengeneza vyuma chakavu ili hatua zichukuliwe.

(Kifungu kilichotajwa hapo juu kilipitishwa na Kamati ya Matumizi bila mabadiliko yoyote)

(Bunge lilirudia)

T A A R I F A

452

WAZIRI WA UJENZI (BARABARA NA VIWANJA VYA NDEGE): Mheshimiwa Spika, naomba kutoa Taarifa kwamba, Bunge lako Tukufu, limekaa ya Matumizi, limeyapitia Makadirio na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013, kifungu kwa kifungu na kuyapitisha bila mabadiliko yoyote.

Hivyo basi, naomba sasa Bunge lako liyakubali makadirio haya.

Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja. (Makofi)

WAZIRI WA MAMBO YA NDANI: Mheshimiwa Spika, naafiki.

(Hoja ilitolewa iamuliwe) (Hoja iliamuliwa na Kuafikiwa)

(Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Ujenzi (Barabara na Viwanja vya Ndege) kwa mwaka 2012/2013 yalipitishwa na Bunge)

SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kwanza kabisa, ninaomba niwaopongeze wote kwa namna tulivyofanya kazi vizuri leo mpaka tumemaliza vitabu vyote ni kwa sababu ya kufuata Kanuni. Kwa mujibu wa Kanuni, katika mshahara wa Waziri hausemi tuseme kila kitu halafu mgeangalia jinsi mlivyo-handle mshahara wa Waziri, tumetoa masomo kwa Watanzania kuhusu Sera zinazohusiana na masuala mazima ya barabara, kwa sababu tulipokuwa tunajadiliana kila mtu alikuwa anataja kwake ilikuwa

453 sawa tu, lakini hapa mwisho mmezungumza Sera, sasa imewasidia hata watu wengine kujua Sera katika maeneo haya inasema nini. Kwa hiyo, tumefanya kazi ya Kibunge na hivyo tumefika mpaka kwenye Kitabu cha Nne. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, naomba kuchukua nafasi hii kuwapongeza wote. Ninapenda tufanye hivyo kila wakati, tusiwe watu wa kupoteza muda bila sababu. La pili, tuwapongeze Mheshimiwa Waziri, Naibu Waziri na Watendaji Wakuu wote, kwa kufanya kazi nzuri ya kuendesha shughuli nzima ya ujenzi wa barabara na nyumba katika nchi yetu. Ninaamini sifa mlizopata kwa Waheshimiwa Wabunge hapa, mtaziendeleza kwa vitendo kusudi tutakapokutana tena mwaka mwingine, tuwe tunazungumzia mambo mengine. Kuna ushauri mkubwa mkubwa ulifanyika hapa, nadhani Wizara itazingatia; kwa mfano, kuweza kukopa fedha za kutosha ili kutengeneza barabara nyingi kwa wakati mmoja na wakati huo mwendelee kulipa Serikali. Ninadhani ni ushauri mzuri na masuala ya Dar es Salaam kama alivyosema, ninaamini mtaangalia vizuri kwa sababu ni kero kwa kila mtu, ninatamani watu wahamie Dodoma kuliko kubakia Dar es Salaam. (Makofi)

Waheshimiwa Wabunge, kwa hiyo, ninadhani haya ni mambo machache tu ambayo mnatakiwa kuyafanya. Vinginevyo, nina tangazo dogo hapa kwamba, Waheshimiwa Wabunge Wanamichezo wa upande wa Simba na Yanga kuwa, safari yao ya kwenda Dar es Salaam kwenye Tamasha la Michezo itakuwa kesho saa kumi na moja alfajiri. Usafiri

454 umeandaliwa utakuwepo katika Viwanja vya Bunge hapa. Kwa hiyo, wachezaji mnaombwa kuzingatia muda huo ni saa kumi na moja; ukija umewahi ndiyo vizuri na ukichelewa utaachwa. Wanasema Kamati za Ufundi kwa timu zote mbili zimeshatangulia kwa ajili ya maandalizi, moja imetokea Pemba na nyingine imetokea Sumbawanga. (Kicheko)

Wananilazimisha mimi eti nimesema asubuhi msipoingia hapa nitawapa adhabu eti ulikuwa ujanja wangu; mimi sina timu, ninyi watu atakayeshinda kesho nitakuwa timu hiyo hiyo itakayoshinda. Kwa hiyo, ninaomba niwashukuru sana kwa ushirikiano tulioupata kwa muda wa siku mbili hizi. Mimi mwenyewe ninaondoka kesho, mimi ni Mjumbe wa Kamati ya Utendaji ya Bunge la SADC, kwa hiyo, ninatakiwa kuwepo kule Siku ya Jumanne, Mheshimiwa Naibu Spika atakuwepo hapa Jumatatu na Wenyeviti, ninaomba muwape ushirikiano wa hali ya juu sana, makosa yaliyotokea kwa mmoja mmoja sisi wenyewe tutakaa pamoja tutakubaliana yasirudiwe.

Waheshimiwa Wabunge, ninaomba ushirikiano mlionipa mimi na wenzangu muwape, tunajenga Bunge letu lenye heshima na nidhamu, tafadhali naomba muwape ushirikiano wa kutosha.

Waheshimiwa Wabunge, ninaahirisha Kikao cha Bunge mpaka Jumatatu, saa tatu asubuhi.

(Saa 1.52 usiku Bunge liliahirishwa mpaka Siku ya Jumatatu, Tarehe 9 Julai, 2012 Saa Tatu Asubuhi)

455

456