Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Kumi na Nane – Tarehe 6 Julai, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA UTARATIBU): Mheshimiwa Spika, Kabla sijawasilisha Hati Mezani ninapenda kutumia dakika yako moja kutoa shukrani za dhati kabisa kwako. Kwanza kwa kuwa wa kwanza kutangaza msiba wa Mama yangu na vilevile kuwashukuru sana Waheshimiwa Wabunge wote ambao wameniletea rambirambi kwa namna moja au nyingine kwa njia ya sms na kwa simu na hii imefanyika kwa wananchi wengi nchini kote. 1 Mheshimiwa Spika, ninawashukuru sana wote sina kitu cha kufanya isipokuwa kuwaambia kuwa asanteni sana, nimepata faraja na Mama yetu tumemwweka mahali pema katika nyumba yake ya milele. Kwa hiyo, baada ya maelezo hayo mafupi na kwa kuwapongeza na kuwashukuru wote naomba sasa kuwakilisha Hati Mezani. Taaarifa ya Mpango wa Maendeleo wa Miaka Mitano, 2011/2012 - 2015/2016. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha, 2012/2013. MASWALI NA MAJIBU Na.143 Serikali Kujenga Nyumba za Walimu MHE. SULEIMAN M. N. SULEIMAN (K.n.y. MHE. LOLESIA J. BUKWIMBA) aliuliza:- Shule nyingi za msingi zina upungufu mkubwa wa nyumba za walimu hivyo kusababisha walimu kuishi katika mazingira magumu na kutoripoti katika shule kama Nyamsebhi, Mnekezi, Shibela, Kageye, Ntono na Nyasalala katika Jimbo la Busanda. 2 Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga nyumba za walimu katika shule hizo na nyingine ili kuboresha mazingira ya walimu kufanya kazi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lolesia Bukwimba, Mbunge wa Busanda kwa kutoa maelezo yafuatayo. Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Geita ina jumla ya shule za msingi za Serikali 271 na binafsi 6. Aidha, idadi ya walimu waliopo ni 3,531 na nyumba za walimu ni 770 ambazo hata hivyo hazitoshi. Serikali inatambua umuhimu wa kuwa na nyumba za kutosha za walimu ili kuboresha mazingira ya kuishi na kuwawezesha kufanya kazi zao ipasavyo. Kwa kuzingatia azma hiyo Serikali imekuwa ikitenga fedha na kuhamasisha wadau mbalimbali kuchangia katika ujenzi wa miundombinu ya shule ikiwemo ujenzi wa nyumba za walimu. Mheshimiwa Spika, katika kipindi cha mwaka 2006/2007 hadi 2009/2010 Serikali ilitoa jumla ya shilingi 22,800,000.00 kuchangia jitihada za wananchi wa Halmashauri ya Wilaya ya Geita kujenga nyumba za walimu zipatazo 25. Shule zilizonufaika na fedha hizi ni shule ya msingi Nyamisebhi, Shilabhela, Buyagu,Kageye, Mnekezi na shule ya msingi Nyalwanzaja. 3 Mheshimiwa Spika, Serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2010/2011 ilitenga kiasi cha shilingi bilioni 2 kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu katika shule za msingi. Kati ya kiasi hicho shilingi milioni 49 kilitengwa na kutumwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita kwa ajili ya ujenzi wa nyumba za walimu. Mheshimiwa Spika, naomba kuchukua fursa hii kuzihimiza Halmashauri kuweka kipaumbele katika ujenzi wa nyumba za walimu katika mipango yao ya bajeti na kusimamia vizuri matumizi ya fedha zinazotolewa na Serikali kwa ajili ya kazi hiyo ili kuboresha mazingira ya kazi za walimu. MHE. SULEIMAN M. N. SULEIMAN: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa tatizo la nyumba za walimu katika Jimbo la Geita liko sambamba kabisa na tatizo la nyumba za walimu katika Jimbo la Kishapu. Kwa sababu mfano wa nyumba za walimu katika Jimbo la Kishapu ni kama picha niliyokuonyesha. Je, Serikali inaridhika na walimu wa Jimbo Kishapu kuwa na nyumba ambazo zina mazingira magumu na hatimaye wakawa wanakimbia katika Jimbo letu kwa sababu wengi wao hawawezi kuishi katika nyumba za aina hii? (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu swali la nyongeza lililoulizwa na Mheshimiwa Nchambi kutoka Kishapu. 4 Serikali bado inao mpango mzuri wa kujenga nyumba za walimu kwenye maeneo yao. Mwaka huu wa fedha 2012/1213 tumetenga jumla ya shilingi bilioni 296 kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote nchini. Miongoni mwa fedha hizi sasa katika Halmashauri zile waweke kipaumbele kwenye maeneo yenye changamoto nyingi ikiwemo nyumba za walimu. Mheshimiwa Spika, ili kuwawezesha walimu ambao tunawapangia kazi katika maeneo hayo waweze kuishi kwenye nyumba. Hata hivyo kila Halmashauri kupitia bajeti zake za mapato ya ndani mbali ya hizi ambazo ni za Serikali nao tunatoa wito kuweka kipaumbele kwenye maeneo haya yale yote yenye changamoto katika sekta ya elimu kuwezesha sekta hii kufanya kazi yake vizuri. MHE. PAULINE P. GEKUL: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa kilio cha nyumba za walimu ni kubwa sana na tumeona kwamba TBA imekuwa ikitengewa fedha chache sana na Serikali kama tulivyoeleza katika bajeti kivuli jana cha Wizara ya Ujenzi. Ni kwanini Serikali isiiongezee TBA fedha za kutosha ili ijenge hizi nyumba za walimu? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, mpango wa ujenzi wa nyumba za walimu pamoja na ule ambao umewekwa chini ya Ofisi ya Waziri Mkuu lakini pia suala la TBA liko kwenye Wizara ambayo sasa hivi inawasilisha bajeti yake. Ninaomba sana Waheshimiwa Wabunge tuipitishe bajeti ya 5 Wizara ya Ujenzi ambayo pia ina kitengo cha TBA ili pia pia nayo iweze kuweka mipango endelevu ya ujenzi wa nyumba kwa ajili ya kutoa huduma kwa walimu kwenye maeneo yale ambayo wanaweza kuyafikia. MHE. FAIDA M. BAKAR: Mheshimiwa Spika, kwa kuwa, walimu wengi wana matatizo ya makazi na kwa kuwa, wengi wanaishi katika nyumba za kupanga. Je, Serikali itakubaliana na mimi kwamba sasa ni wakati muafaka wa kuwaongezea posho za makazi walimu hawa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU,TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Spika, Ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Faida Bakar. Ni kweli kwamba tumekuwa tukisikia kilio cha walimu wenyewe lakini hata Waheshimiwa Wabunge mmesema sana juu ya kuongeza maslahi ya walimu ili waweze kufanya kazi zao katika mazingira rahisi zaidi. Lakini ninapenda kusema kwamba mpango wa Serikali wa kuboresha maslahi ya walimu ili waweze kumudu kuishi na kufanya kazi yao vizuri tunao lakini yataweza kubodreka kadri fedha za Serikali zinavyoweza kupatikana ili kuweza kuboresha maslahi ya walimu kama ambavyo tumeweza kusema. (Makofi) Pia hata wakati tunachangia hoja ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwamba Serikali inayo azma njema ya kuweza kuboresha maslahi. Kwa hiyo, katika mipango hiyo ambayo inaendelea kadiri ya fedha zinavyoweza 6 kupatikana hilo ni eneo mojawapo ambalilo tutataka kuliboresha ili walimu waweze kufanya kazi zao vizuri. Na. 144 Ukamilishaji wa Ujenzi wa Shule za Sekondari Rombo MHE. MUSTAPHA B. AKUNAAY (K.n.y. MHE. JOSEPH R. SELASINI) aliuliza:- Kutokana na uhaba wa ardhi katika Kata ya Keni, Mrao Keryo, katika Jimbo la Rombo, wananchi wameamua kujenga shule za sekondari kwa mtindo wa ghorofa na shule hizo ni pamoja na sekondari za Keni, Bustani na Shimbi. Je, Serikali itakuwa tayari kuchukua shule hizo na kukamilisha ujenzi wake ili kuunga mkono juhudi za wananchi wa Rombo na kuwapa nafasi kuchangia miradi mingine? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Roman Selasini, Mbunge wa Rombo lakini pia kabla sijaanza kujibu swali lake ninatambua kabisa kuwa Mheshimiwa Mbunge mwenzetu alipata ajali mbaya sana iliyoweza kusababisha vifo vya watu wane akiwemo Mama yake Mzazi. 7 Kwa niaba ya Ofisi ya Waziri Mkuu tunampa pole sana na tunajua kuwa yeye bado yupo hospitalini tunamtakia uponaji mwema yeye na Mke wake, na sasa naomba nijibu swali lake nikijua kabisa anayo hamu ya kulisikia hili kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, mchango mmojawapo wa wananchi katika kufanikisha ujenzi wa sekondari za Kata ni kuwezesha upatikanaji wa ardhi kupitia Serikali za vijiji. Kutokana na ufinyu wa ardhi wananchi wa Rombo waliamua kujenga shule za Sekondari za Kata kwa mtindo wa ghorofa. Shule za sekondari za Kata zinazojengwa kwa mtindo wa ghorofa ni shule ya Sekondari Keni, inayojengwa katika Kata ya Keni, shule ya Sekondari Shimbi inayojengwa katika Kata ya Shimbi na shule ya Sekondari Bustani inayojengwa katika Kata ya Mrao Keryo. Mheshimiwa Spika, katika mwaka wa fedha 2010/2011 Serikali katika kuunga mkono jitihada za wananchi wa Rombo kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Rombo ilitoa jumla ya shilingi 625,000,000/= kwa ajili ya miradi ya maendeleo ya ya elimu katika Kata zote 41 za Serikali. Kwa kuzingatia gharama za ujenzi wa ghorofa shule hizo tatu zilipata mgao ufuatao:- (i) Shule ya Sekondari Bustani ilipewa 57,645,850/=; (ii) Shule ya Sekondari Keni ilipewa shilingi 53,995,850/=; na 8 (iii) Shule ya Sekondari Shimbi shilingi 53,995,850/=. Mheshimiwa Spika, ujenzi wa shule za sekondari za Kata ni ubia kati ya wananchi, Halmashauri na Serikali Kuu. Shule za Sekondari za Kata zinazojengwa ni mali ya Halmashauri husika. Katika mwaka wa fedha 2012/2013 Serikali imejenga jumla ya shilingi bilioni 296 kwa ajili ya miradi ya maendeleo katika Halmashauri zote nchini, Halmashauri ya Wilaya ya Rombo imetengewa jumla ya shilingi bilioni 2.2. Mheshimiwa Spika, natoa wito kwa Hamashauri kusimamia matumizi ya fedha hizi na kuhakikisha maelekezo sahihi ya kukamilisha miradi ya zamani
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages456 Page
-
File Size-