Nakala Ya Mtandao (Online Document)
NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Kumi na Mbili - Tarehe 30 Machi, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali leo tunaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Conchesta Rwamlaza, atauliza swali la kwanza. Na. 117 Mwakilishi wa Wazee katika Vyombo vya Maamuzi MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza:- Kwa muda mrefu wazee wa nchi hii wamekuwa wakililia uwakilishi katika vyombo mbalimbali vya maamuzi kama vile Bunge, Halmashauri, Vijiji na kadhalika kama ilivyo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ili sauti zao zisikike:- Je, ni lini Serikali itasikia kilio cha wazee hawa? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Utaratibu wa kupata wawakilishi katika vyombo vya maamuzi kama vile Bunge, umeelezwa katika Ibara ya 66 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Ibara hii imefafanua aina za Wabunge na namna ya kuwapata. Utaratibu wa kuwapata wawakilishi katika Halmashauri umeelezwa 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) katika Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 yaani The Local Authority Election Act, Cap. 292. Aidha, utaratibu wa kuwapata wawakilishi katika vijiji hutawaliwa na Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura ya 287 na Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura ya 288. Mheshimiwa Spika, wawakilishi wanaowakilisha makundi mbalimbali katika Bunge, Halmashauri na Vijiji, kwa mfano, wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na kadhalika, wamekuwa wakipatikana kupitia mapendekezo yanayowasilishwa na vyama vya siasa kwenye vyombo vinavyosimamia uchaguzi katika ngazi hizo.
[Show full text]