Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA ISHIRINI ___________ Kikao cha Kumi na Nane – Tarehe 1 Juni, 2015 (Kikao Kilianza Saa tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Lediana M. Mng‟ong‟o) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Randama za Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. MHE. GREGORY G. TEU (K. n. y. MHE. MARGARET S. SITTA - MWENYEKITI KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA ZA JAMII)•: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma za Jamii kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. MHE. GRACE S. KIWELU – MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya fedha kwa Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) MASWALI NA MAJIBU Na. 119 Fedha kwa Ajili ya Kutengeneza Mitaro ya Barabara MHE. ANNAMARYSTELLA J. MALLAC aliuliza:- Serikali imekuwa ikitenga fedha nyingi kila mwaka kwa ajili ya matengenezo ya barabara za Halmashauri za Miji na Wilaya ikiwemo za Mpanda na Sumbawanga ambazo huharibika mara kwa mara kwa sababu ya ukosefu wa mitaro:- Je, ni lini Serikali itatenga fedha za kutengeneza mitaro hiyo ili kuokoa fedha zinazotumika mara kwa mara kutengeneza barabara zinazosombwa na maji? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa AnnaMaryStella John Mallac, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa mitaro katika barabara za mijini. Katika Halmashauri ya Mji wa Mpanda kuanzia Mwaka wa Fedha 2012/2013 hadi Mwaka wa Fedha 2014/2015, jumla ya Sh. 502,000,000 zimetumika kujenga mitaro ya maji ya mvua. Kwa sasa Mji wa Mpanda una kilometa 20.2 za mitaro ya maji ya mvua. Hata hivyo kwa kuzingatia mtandao wa barabara uliopo katika mji huo wenye jumla ya kilometa 251.5 za mitaro ya maji na mvua zinahitajika kujengwa. Aidha, katika bajeti ya Mwaka wa Fedha 2015/2016 zimeombwa Sh. 150,000,000 za kuendeleza ujenzi wa mitaro ya maji ya mvua katika barabara za Mji wa Mpanda. Mheshimiwa Mwenyekiti, Halmashauri ya Manispaa ya Sumbawanga ina kilometa 204.55 za mtandao wa barabara za mijini na hivyo kufanya jumla ya kilometa 409.1 ziwe na uhitaji wa kuwekewa mitaro ya maji ya mvua. Kwa sasa Mji wa Sumbawanga una kilometa 13.5 za mitaro ya maji ya mvua ambapo ujenzi hufanyika kila mwaka wa fedha na kwa kutenga Sh. 50,000,000 za kujenga mita 500 za mitaro ya maji ya mvua katika maeneo korofi, barabara za kiwango cha lami na changarawe. MWENYEKITI: Swali la nyongeza Mheshimiwa AnnaMaryStella Mallac! MHE. ANNAMARYSTELLA J. MALLAC: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri naomba niongeze swali ili nipatiwe majibu. Mheshimiwa Mwenyekiti, imezoeleka sasa kwa Serikali, inapopanga bajeti inaweka fedha kwa wingi kwa maneno, lakini inapoamua kupeleka katika Halmashauri, inapeleka kwa uchache sana, yaani kidogo ambazo haziwezi kumalizia ile miradi na kuleta adha katika mitaa yetu kule, barabara za pale mjini, mvua inapokuja tena inaharibu hata kile kipolwa kidogo kilichokuwa kimetengenezwa. Sasa napenda kuiuliza Serikali, haioni kwamba kazi za kurudia rudia ni uharibifu wa fedha, vile vile ni kuwabebesha mzigo wa lawama Wakurugenzi wa Halmashauri husika? Ahsante. MWENYEKITI: Majibu, Mheshimiwa Naibu Waziri! 2 Nakala ya Mtandao (Online Document) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli katika nyakati kadhaa kunaweza kuwa kuna tatizo la upatikanaji wa fedha na ule mradi uliokusudiwa usitekelezwe kwa wakati halafu tukapata tatizo la mvua labda, halafu ikaharibu pia hata structure ile ya awali. Mikakati ya Serikali wakati wote ni kuhakikisha kwamba, mradi unapoanza unakamilika na pale ambapo tunatenga bajeti fedha itolewe ili iweze kukamilika. Kwenye eneo la barabara na maeneo ya miji tunavyo vyanzo viwili ambavyo tunavitumia mara nyingi katika kuboresha huduma zetu za barabara na mitaro yake. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kuna fedha ambayo inatengwa kupitia bajeti ya Halmashauri yenyewe lakini mbili tunayo ile miradi ya barabara ambayo tunatengewa fedha kila mwaka ili tuweze kuiimarisha. Kwa sababu ya uhitaji mkubwa wa matengenezo ya barabara, sasa tumeona tuhakikishe kwamba tunatenga fedha kwa mradi mmoja mmoja ambao unatakiwa kuanzwa na kukamilika badala ya utaratibu wa awali wa kuwa tunatenga kidogo barabara hii, kidogo barabara ile, badala yake fedha zinakuwa hazikamiliki, haziletwi kwa wakati kama ambavyo tumeeleza na tatizo limeshaelezwa mara nyingi na Wizara ya Fedha ikija hapa itaeleza utaratibu unaotumika katika kuleta fedha. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge jambo analolieleza tunalifahamu na tutahakikisha kwamba mradi ule tuliouanza tunaukamilisha. MWENYEKITI: Mheshimiwa Wenje, swali la nyongeza! MHE. EZEKIA D. WENJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru sana. Katika gharama ambazo Serikali inatumia kwenye Halmashauri zetu nchi nzima ni kutengeneza barabara ni fedha nyingi sana na hii inatokana na kwamba Halmashauri nyingi hazina grader kwa hiyo wanatafuta Wakandarasi kuja kutengeneza barabara za Halmashauri ambazo in real sense tunatumia hela nyingi sana. Hii ni kwa Halmashauri zote nchi hii ikiwemo na hata Halmashauri ya Jiji la Mwanza ninakotoka. Je, Serikali ina mkakati gani wa kutoa amri kwa Halmashauri zote nchi hii, kila Halmashauri ihakikishe inakuwa na grader linalofanya kazi ili kupunguza gharama za kutengeneza barabara kwa kuwapa makandarasi? MWENYEKITI: Mheshimiwa Naibu Waziri, majibu! NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Mheshimiwa Mwenyekiti, tunatambua kwamba Halmashauri zinazo kazi nyingi sana za barabara na mara nyingi hutumia wazabuni katika kurekebisha hata yale matengenezo madogo madogo. Sisi tunaamini kwamba Halmashauri inapoweza kuwa na mipango yake yenyewe, inapoona kwamba inatumia gharama nyingi kwenye zabuni mbalimbali na wanaweza kuwa na alternative ni suala la Madiwani kuona umuhimu wa ununuzi wa grader na kuweza kurekebisha kazi ndogo ndogo au zile muhimu badala ya kutumia wazabuni ambao gharama yake inakuwa kubwa zaidi. Mheshimiwa Mwenyekiti, nazungumza hili kwa sababu Halmashauri nyingi tumeona zimeshaanza kununua ma-caterpillar yake yenyewe na kufanya kazi za barabara iweze kukamilika. Kwa manufaa ya Wilaya ya Nyamagana ambayo pia Mheshimiwa Mbunge anaweza kushauri pale na tumeshawahi kutoa maelezo haya kwenye Halmashauri, pamoja na zilizotekeleza, sasa Nyamagana ione kupitia mipango yake ya ndani na kuona umuhimu wa kupunguza gharama kwa wazabuni, sasa iweze kununua vyombo vyake yenyewe. Kwa kuwa tuna Wahandisi, wataalam tunaweza kuajiri tu operator ili waweze kufanya zile kazi ndogo 3 Nakala ya Mtandao (Online Document) ndogo wao wenyewe badala ya kutumia wazabuni ambao pia gharama yake ni kubwa kama nilivyosema awali. MWENYEKITI: Mheshimiwa Ester Bulaya, nilikuona! MHE. ESTER A. BULAYA: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru. Nataka tu kuuliza swali dogo la nyongeza. Tunajua Serikali inatumia fedha nyingi katika ujenzi wa barabara. Hapa nazungumzia barabara kuu ya kutoka Mwanza kwenda Musoma. Kupitia lile eneo la Bunda kuna maeneo ambayo barabara kabla haijakabidhiwa tayari imeshaharibika. Sasa nataka kujua, hivi ni vigezo gani mnavyotumia kuwapata Wakandarasi ambao wanajenga barabara chini ya kiwango; barabara kabla haijakabidhiwa tayari imeshakatika? MWENYEKITI: Naibu Waziri wa Ujenzi, majibu, Mheshimiwa Mhandisi Lwenge! NAIBU WAZIRI WA UJENZI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba inawezekana kwa yeye jinsi alivyoona kwamba barabara imeharibika kabla haijakabidhiwa, lakini assessment siku zote tunaifanya barabara ikishakabidhiwa. Sasa kama bado Mkandarasi anaendelea kufanya kazi pale, unajuaje kama kipande hiki kimekwisha? Mpaka kikabidhiwe ndipo tunasema hiki kimekwisha na kimepokelewa. Barabara yoyote haiwezi kupokelewa kama haijafikia kiwango kinachotakiwa kulingana na mkataba ule. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa hiyo, suala hili ni jambo la usimamizi, sisi tunaendelea kufuatilia. Kwa hiyo, kama kweli anachokisema ndiyo hivyo basi tutakwenda kuona tuone kama hicho kipande kimekabidhiwa na kimeharibika kabla ya muda wake. Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. MWENYEKITI: Ahsante sana, tunakwenda swali linalofuata, Mheshimiwa Josephine Genzabuke. Samahani, samahani, swali linalofuata ni la Mheshimiwa Deo Filikunjombe. Mheshimiwa Esther Bulaya! Na. 120 Kufikisha Maji Safi na Salama Mji wa Ludewa MHE. ESTER A. BULAYA (K.n.y. MHE. DEO H. FILIKUNJOMBE) aliuliza:- Maji safi na salama ni muhimu kwa afya za wananchi:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka maji safi na salama katika Mji wa Ludewa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deo Filikunjombe, Mbunge wa Ludewa, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Mji wa Ludewa unakadiriwa kuwa na wakazi wapatao 13,000 ambapo kati yake ni asilimia