Majadiliano Ya Bunge ______

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Majadiliano Ya Bunge ______ NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ BUNGE LA KUMI NA MOJA MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Ishirini na Moja – Tarehe 6 Mei, 2019 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa tukae. Katibu. NDG. PAMELA PALLANGYO – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa mwaka wa fedha, 2018/2019. MWENYEKITI: Ahsante. Katibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. PAMELA PALLANGYO – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Swali letu la kwanza leo linaulizwa na Mheshimiwa Ruth Mollel, Mbunge wa Viti Maalum na linaelekezwa Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Na. 166 Athari za Mtambo wa Kuchoma Takataka za Hospitali na Dawa Zilizokwisha Muda – Mkuranga MHE. RUTH H. MOLLEL aliuliza:- Mtambo wa kuchoma takataka za hospitali na dawa zilizokwisha muda wake upo katika Kijiji cha Dundani Wilayani Mkuranga. Uchomaji unapofanyika moshi mzito huingia kwenye nyumba na maeneo ya wananchi wanaoishi karibu na mtambo huo na kuhatarisha afya zao:- Je, Serikali ina mkakati gani wa kunusuru afya na maisha ya wananchi wanaoishi karibu na mtambo huo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ruth Hiyob Mollel, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli kwamba upo mtambo wa kuchomea taka na dawa zilizokwisha muda wake uliojengwa na mwekezaji katika Kijiji cha Dundani, Wilaya ya Mkuranga. Hapo awali mtambo huo ulikuwa na kasoro za ujenzi ambapo Serikali ilimwagiza mwekezaji kuzirekebisha kwa ilani ya tarehe 18, Oktoba, 2017 yenye kumbu. Na. NEMC/HQ/EA/05/0702/VOL1/7 sambamba na 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kusimamisha shughuli za mtambo mpaka kasoro zitakapokuwa zimerekebishwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, marekebisho hayo yamefanyika na baada ya mamlaka zote, ikiwemo Serikali ya Kijiji cha Dundani kujiridhisha kwamba hakuna tena moshi unaoathiri mazingira, mtambo huo umeruhusiwa kuendelea na kazi na mpaka sasa hakuna taarifa yoyote iliyofika katika Ofisi ya Mkurugenzi Mtendaji, Wilaya ya Mkuranga kulalamikia shughuli za mtambo huo. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Mollel. MHE. RUTH H. MOLLEL: Mheshimiwa Mwenyekiti, pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri, pamoja na marekebisho ambayo yamefanyika, ni kwamba sasa ule moshi zamani ulikuwa unafika mbali, baada ya marekebisho ule moshi bado unatoka na bado unaathiri wananchi waliokuwa jirani, unasababisha watu kukohoa na harufu chafu kwa wananchi wanaozunguka lile eneo. Swali langu: Je, Serikali ilishafanya utafiti kwa sababu watu wanakohoa, tumejua ni madhara gani ya kiafya yanayosababishwa na moshi huo? Swali langu la pili; ni kwa nini sasa NEMC wasirudi tena kule Dundani na kuhakikisha kwamba ule moshi unatafutiwa namna ambayo itaudhibiti usiendelee kuchafua mazingira? MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Kandege. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza naomba nikiri kwamba Mheshimiwa Ruth Mollel ni Diwani wa kata husika, kwa hiyo, yeye ni mdau katika eneo hilo. Kama ambavyo nimejibu katika jibu langu la msingi, kwamba mpaka sasa hivi hakuna taarifa ambayo imekuja Ofisi ya Mkurugenzi ikionesha kwamba kuna kasoro ambazo 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Serikali inatakiwa irekebishe, naomba Mheshimiwa Mbunge kwa kutumia vikao vyake alipeleke hili. Mheshimiwa Mwenyekiti, hata hivyo, kwa sababu sisi tunajali afya ya mwananchi kuliko jambo lingine lolote, naomba nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge, pamoja na swali lake la pili kwamba angetaka NEMC waende kwa mara ya pili kutazama; kwa sababu mtaji wetu kwa mwananchi ni kuhakikisha kwamba ana afya bora, basi naomba nimhakikishie kwamba Serikali kwa kupitia NEMC tutakwenda kuchunguza na tujiridhishe pasi na mashaka kwamba hakuna madhara ambayo yanatokana na kichomea taka hiki. MWENYEKITI: Ahsante. Mheshimiwa Lubeleje. MHE. GEORGE M. LUBELEJE: Mheshimiwa Mwenyekiti, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ili niweze kuuliza swali moja la nyongeza. Kwa kuwa madawa yaliyokwisha muda wake (expired drugs) ni hatari sana katika maisha ya binadamu; na kwa kuwa baadhi ya maduka hayakaguliwi vizuri kuhakikisha kwamba madawa yaliyokwisha muda hayapo. Je, Mheshimiwa Waziri anasemaje kuhusu ukaguzi wa maduka yote ambayo yana madawa hayo yaliyokwisha muda wake? MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa maswali hayo Mheshimiwa Naibu Waziri wa Afya, Mheshimiwa Ndugulile. NAIBU WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO: Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mujibu wa taratibu zetu za afya, dawa zilizoisha muda au matumizi hazipaswi kutumika kwa matumizi ya binadamu. Mahospitali pamoja na wauzaji wa maduka binafsi wanatakiwa wazitenge tofauti na dawa ambazo zinaendelea kutumika ndani ya vituo vyetu vya kutolea huduma za afya lakini vilevile katika matumizi ya dawa za kuuzwa. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, kuna utaratibu maalum ambao umewekwa ambapo dawa na vifaa vya hospitali havichomwi tu kama takataka nyingine, vina utaratibu wake na utaratibu huu upo. Nitoe rai tu kuhakikisha kwamba mamlaka ambazo zinasimamia ikiwa ni pamoja na Mamlaka ya TFDA na Baraza la Famasia, basi wapite kuhakikisha kwamba wanatoa elimu hiyo na kuweka utaratibu mzuri wa uteketezaji wa hizi dawa ili zisije zikaingia katika mikono isiyo salama. MWENYEKITI: Ahsante. Waheshimiwa tunaendelea. Swali linalofuta linaulizwa na Mheshimiwa Vedastus Mathayo Manyinyi, Mbunge wa Musoma Mjini na linaelekezwa kwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Utumishi na Utawala Bora) Na. 167 Zoezi la Kuwaondoa Watumishi Wenye Vyeti Fake MHE. VEDASTUS M. MANYINYI aliuliza:- Serikali katika kuhakikisha inapata watumishi bora na wenye sifa iliamua kuwaondoa watumishi wasio na sifa pamoja na wenye vyeti feki, lakini zoezi hilo lilikumbwa na changamoto mbalimbali ambapo Afisa Utumishi aliwaondoa watumishi kwenye payroll bila sababu maalum na walipofuatilia Wizarani walirudishwa kazini:- (a) Je, kwa nini Serikali isiunde timu maalum ili ipite kila Halmashauri kupitia taarifa juu ya zoezi hili ili haki itendeke hasa kwa wale ambao hawana uwezo wa kwenda Wizarani? (b) Wapo watumishi ambao baada ya kuajiriwa kwa kutumia vyeti feki walijiendeleza kielimu zaidi ya Darasa la Saba na wameondolewa kwa kosa la udanganyifu wa vyeti: Je, Serikali haioni kuwa hao ni bora kuliko wale ambao hawakujiendeleza? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA alijibu:- 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Vedastus Mathayo Manyinyi, Mbunge wa Musoma Mjini, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa kushirikiana na waajiri na Baraza la Mitihani la Taifa, Serikali iliendesha zoezi maalum la kuhakiki vyeti vya ufaulu mtihani wa Kidato cha Nne, Kidato cha Sita na Ualimu. Kupitia zoezi hilo, watumishi 15,189 walibainika kuwa na vyeti vya kugushi na kuondolewa kwenye orodha ya malipo ya mshahara (payroll). Hata hivyo, baada ya kupokea malalamiko kutoka kwa watumishi na vyanzo vingine kuhusu watumishi kuondolewa kimakosa au kwa uonevu katika orodha ya malipo ya mishahara, Serikali imekuwa ikifanya ufuatiliaji wa karibu ikiwa ni pamoja na kuunda timu za ufuatiliaji wa utekelezaji wa zoezi hili. Jumla ya watumishi 4,160 waliobainika kuondolewa kimakosa au kwa uonevu wamerejeshwa kazini. Kati ya watumishi waliorejeshwa kazini 3,057 ni Watendaji wa Vijiji/Mtaa na Kata. (b) Mheshimiwa Mwenyekiti, watumishi wanaojiendeleza zaidi ya Darasa la Saba wanafanya vizuri na Serikali inahimiza watumishi kujiendeleza kielimu. Hata hivyo, kwa mujibu wa Kanuni ile ya D.12 ya Kanuni za Kudumu katika Utumishi wa Umma za mwaka 2009, ni makosa kwa mtumishi kujipatia ajira kwa njia ya udanganyifu. Hivyo Serikali ilielekeza waajiri kuwaondoa kwenye orodha ya malipo ya mishahara Watumishi wa Umma wote walioajiriwa kabla ya tarehe 20, Mei, 2004 ambao katika kumbukumbu zao rasmi za kiutumishi walijaza taarifa za udanganyifu kwamba walifaulu mitihani ya Kidato cha Nne, lakini hawakuthibitisha taarifa zao kwa kuwasilisha vielelezo vya sifa hizo kama vile taarifa binafsi (personal records). Hivyo, pamoja na watumishi hao kujiendeleza kielimu, uamuzi wao wa kutoa taarifa za udanganyifu unawaondolea 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) sifa ya uaminifu na uadilifu kwa Serikali na hivyo wanakosa sifa za kuendelea kuwa Watumishi wa Umma. Ahsante. MWENYEKITI: Mheshimiwa Manyinyi. MHE. VEDASTUS M. MANYINYI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa kupata nafasi ili niweze kuuliza maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza namshukuru Mheshimiwa Naibu Waziri, mkwe wangu, kwa majibu mazuri aliyoweza kunipatia, lakini (a) kwa kuwa Serikali imekiri kwamba kati ya watumishi 15,000 walioondolewa waligundua kwamba watumishi 4,160 waliondolewa kimakosa. Hawa ni wale waliopata nafasi ya kuja Dodoma, Utumishi na kwenda Dar es Salaam kwenye Tume. Wale ambao hawakuwa na uwezo, tafsiri yake ni kwamba wamebaki huko. (Makofi) Sasa swali; ni lini sasa Serikali itaunda tume ambayo angalau itakwenda kila Halmashauri au Mkoani
Recommended publications
  • Tarehe 30 Machi, 2021
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Kwanza – Tarehe 30 Machi, 2021 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) WIMBO WA TAIFA NA WIMBO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (Hapa Kwaya ya Bunge iliimba Wimbo wa Taifa na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: TAARIFA YA SPIKA NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nitaleta kwenu Taarifa ya Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Job Yustino Ndugai. Waheshimiwa Wabunge, kama ambavyo wote tunafahamu aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Dkt. John Pombe Joseph Magufuli alifariki dunia tarehe 17 Machi, 2021 katika Hospitali ya Mzena, Jijini Dar es Salaam alikokuwa akipatiwa matibabu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Waheshimiwa Wabunge, kufuatia msiba huo wananchi wa Tanzania walipata fursa ya kutoa heshima za mwisho kama ifuatavyo; tarehe 20 hadi 21 Machi, 2021 Mkoani Dar es Salaam, tarehe 22 Machi, 2021 Mkoani Dodoma ambapo pia ilifanyika hafla ya kitaifa. Tarehe 23 Machi, 2021 ilikuwa Zanzibar na tarehe 24 Machi, 2021 ilikuwa mkoani Mwanza. Waheshimiwa Wabunge, nazisikia kelele sina hakika kama wote tuko pamoja kwenye jambo hili zito lililolipata Taifa letu. Tarehe 25 hadi 26 mkoani Geita na Chato. Waheshimiwa Wabunge, mazishi ya aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Dkt. John Pombe Joseph Magufuli yalifanyika siku ya Ijumaa tarehe 26 Machi, 2021 nyumbani kwake Chato, Mkoani Geita. Waheshimiwa Wabunge, kwa kuwa leo ni siku ya kwanza kwa Bunge hili kukutana tangu ulipotokea msiba huo naomba Waheshimiwa Wabunge tusimame kwa dakika moja ili kumkumbuka mpendwa wetu.
    [Show full text]
  • Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Kumi na Mbili - Tarehe 30 Machi, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali leo tunaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Conchesta Rwamlaza, atauliza swali la kwanza. Na. 117 Mwakilishi wa Wazee katika Vyombo vya Maamuzi MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA aliuliza:- Kwa muda mrefu wazee wa nchi hii wamekuwa wakililia uwakilishi katika vyombo mbalimbali vya maamuzi kama vile Bunge, Halmashauri, Vijiji na kadhalika kama ilivyo kwa vijana, wanawake na watu wenye ulemavu ili sauti zao zisikike:- Je, ni lini Serikali itasikia kilio cha wazee hawa? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Utaratibu wa kupata wawakilishi katika vyombo vya maamuzi kama vile Bunge, umeelezwa katika Ibara ya 66 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977. Ibara hii imefafanua aina za Wabunge na namna ya kuwapata. Utaratibu wa kuwapata wawakilishi katika Halmashauri umeelezwa 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) katika Sheria ya Uchaguzi wa Serikali za Mitaa, Sura ya 292 yaani The Local Authority Election Act, Cap. 292. Aidha, utaratibu wa kuwapata wawakilishi katika vijiji hutawaliwa na Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura ya 287 na Sheria ya Serikali za Mitaa, Sura ya 288. Mheshimiwa Spika, wawakilishi wanaowakilisha makundi mbalimbali katika Bunge, Halmashauri na Vijiji, kwa mfano, wanawake, vijana, watu wenye ulemavu na kadhalika, wamekuwa wakipatikana kupitia mapendekezo yanayowasilishwa na vyama vya siasa kwenye vyombo vinavyosimamia uchaguzi katika ngazi hizo.
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 114 May - Aug 2016
    Tanzanian Affairs Issued by the Britain-Tanzania Society No 114 May - Aug 2016 Magufuli’s “Cleansing” Operation Zanzibar Election Re-run Nyerere Bridge Opens David Brewin: MAGUFULI’S “CLEANSING” OPERATION President Magufuli helps clean the street outside State House in Dec 2015 (photo State House) The seemingly tireless new President Magufuli of Tanzania has started his term of office with a number of spectacular measures most of which are not only proving extremely popular in Tanzania but also attracting interest in other East African countries and beyond. It could be described as a huge ‘cleansing’ operation in which the main features include: a drive to eliminate corruption (in response to widespread demands from the electorate during the November 2015 elections); a cutting out of elements of low priority in the expenditure of government funds; and a better work ethic amongst government employees. The President has changed so many policies and practices since tak- ing office in November 2015 that it is difficult for a small journal like ‘Tanzanian Affairs’ to cover them adequately. He is, of course, operat- ing through, and with the help of ministers, regional commissioners and cover photo: The new Nyerere Bridge in Dar es Salaam (see Transport) Magufuli’s “Cleansing” Operation 3 others, who have been either kept on or brought in as replacements for those removed in various purges of existing personnel. Changes under the new President The following is a list of some of the President’s changes. Some were not carried out by him directly but by subordinates. It is clear however where the inspiration for them came from.
    [Show full text]
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who Will Benefit from the Gas Economy, If It Happens?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013 Who will benefit from the gas economy, if it happens? Supported by: 2 TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? ACKNOWLEDGEMENTS Policy Forum would like to thank the Foundation for Civil Society for the generous grant that financed Tanzania Governance Review 2013. The review was drafted by Tanzania Development Research Group and edited by Policy Forum. The cartoons were drawn by Adam Lutta (Adamu). Tanzania Governance Reviews for 2006-7, 2008-9, 2010-11, 2012 and 2013 can be downloaded from the Policy Forum website. The views expressed and conclusions drawn on the basis of data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. TGRs review published and unpublished materials from official sources, civil society and academia, and from the media. Policy Forum has made every effort to verify the accuracy of the information contained in TGR2013, particularly with media sources. However, Policy Forum cannot guarantee the accuracy of all reported claims, statements, and statistics. Whereas any part of this review can be reproduced provided it is duly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. ISBN:978-9987-708-19-2 For more information and to order copies of the report please contact: Policy Forum P.O. Box 38486 Dar es Salaam Tel +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] Suggested citation: Policy Forum 2015.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TISA Kikao Cha Sita – Tarehe 14 Novemba, 2017
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA TISA Kikao cha Sita – Tarehe 14 Novemba, 2017 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Tukae, Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, VIJANA, AJIRA NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Matoleo ya Gazeti la Serikali pamoja na Nyongeza zake yaliyochapishwa tangu Mkutano wa Bunge uliopita kama ifuatavyo:- (i) Toleo Na. 35 la tarehe 01/09/2017 (ii) Toleo Na. 36 la tarehe 08/09/2017 (iii) Toleo Na. 37 la tarehe 15/09/2017 (iv) Toleo Na. 38 la tarehe 22/09/2017 (v) Toleo Na. 39 la tarehe 29/09/2017 (vi) Toleo Na. 40 la tarehe 06/10/2017 (vii) Toleo Na. 41 la tarehe 13/10/2017 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (viii) Toleo Na. 42 la tarehe 20/10/2017 (ix) Toleo Na. 43 la tarehe 27/10/2017 NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ENG. ATASHASTA J. NDITIYE): Maelezo ya Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania wa Mwaka 2017 (The Tanzania Telecommunications Corporation Bill, 2017) MHE. HAWA M. CHAKOMA (K.n.y. MHE. NORMAN A.S. KING - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU): Maoni ya Kamati ya Miundombinu kuhusu Muswada wa Sheria ya Shirika la Mawasiliano Tanzania wa Mwaka 2017 (The Tanzania Telecommunications Corporation Bill, 2017) MHE. QAMBALO W.
    [Show full text]
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? With Partial Support from a TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? ACKNOWLEDGEMENTS This review was compiled and edited by Tanzania Development Research Group (TADREG) under the supervision of the Steering Group of Policy Forum members, and has been financially supported in part by Water Aid in Tanzania and Policy Forum core funders. The cartoons were drawn by Adam Lutta Published 2013 For more information and to order copies of the review please contact: Policy Forum P.O Box 38486 Dar es Salaam Tel: +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] ISBN: 978-9987 -708-09-3 © Policy Forum The conclusions drawn and views expressed on the basis of the data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. Every effort has been made to verify the accuracy of the information contained in this review, including allegations. Nevertheless, Policy Forum cannot guarantee the accuracy and completeness of the contents. Whereas any part of this review may be reproduced providing it is properly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. Designed by: Jamana Printers b TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TABLE OF CONTENTS POLICY FORUM’s OBJECTIVES .............................................................................................................
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Kumi Na Tisa – Tarehe 29 Aprili, 2021
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Kumi na Tisa – Tarehe 29 Aprili, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa, tukae. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU WAZIRI WA MADINI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. SAADA MONSOUR HUSSEIN - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa maswali, tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Simon Songe Lusengekile, Mbunge wa Busega, sasa aulize swali lake. Na. 158 Serikali Kukamilisha Ujenzi wa Zahanati – Busega MHE. SIMON S. LUSENGEKILE aliuliza:- Wananchi wa Kata ya Imalamate Wilayani Busega wamejenga zahanati na kumaliza maboma manne kwa maana ya zahanati moja kila kijiji:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wananchi hao kuezeka maboma hayo ili waweze kupata huduma za afya kwenye zahanati hizo? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 2 AGOSTI, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba mzime vipasa sauti vyenu maana naona vinaingiliana. Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri, tunaingia hatua inayofuata. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Leo ni siku ya Alhamisi lakini tulishatoa taarifa kwamba Waziri Mkuu yuko safarini kwa hiyo kama kawaida hatutakuwa na kipindi cha maswali hayo. Maswali ya kawaida yapo machache na atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Vita R. M. Kawawa. Na. 310 Fedha za Uendeshaji Shule za Msingi MHE. VITA R. M. KAWAWA aliuliza:- Kumekuwa na makato ya fedha za uendeshaji wa Shule za Msingi - Capitation bila taarifa hali inayofanya Walimu kuwa na hali ngumu ya uendeshaji wa shule hizo. Je, Serikali ina mipango gani ya kuhakikisha kuwa, fedha za Capitation zinatoloewa kama ilivyotarajiwa ili kupunguza matatizo wanayopata wazazi wa wanafunzi kwa kuchangia gharama za uendeshaji shule? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) imepanga kila mwanafunzi wa Shule ya Msingi kupata shilingi 10,000 kama fedha za uendeshaji wa shule (Capitation Grant) kwa mwaka.
    [Show full text]
  • Miradiya Bilioni 788 Kutekelezwa
    Mwanza Urban Water Supply And Sanitation Authority Mwanza Urban Water Supply And Sanitation Authority NEWS BULLETIN Oktoba 2019 NEWS BULLETIN TOLEO NAMBA: O5 OKTOBA, 2019 www.mwauwasa.go.tz TUNATEKELEZA KWA VITENDO ZIARA YA WAZIRI MBARAWA KWENYE PONGEZI KWA MRADI WA MAJI MHANDISI MSALALA uk 8 ANTHONY SANGA uk 4 SERIKALI YA DKT. MAGUFULI NI YA VITENDO- PROF MKUMBO MIRADI YA BILIONI 788 KUTEKELEZWA KANDA YA ZIWA VICTORIA uk 2 Mwanza Urban Water Supply And Sanitation Authority NEWS BULLETIN Oktoba 2019 MIRADI YA BILIONI 788 KUTEKELEZWA KANDA YA ZIWA VICTORIA erikali inatekeleza miradi 17 ya maji yenye thamani ya Shilingi Bil- ioni 788 ikiwa ni hatua mojawapo ya utatuzi wa changamoto ya upa- tikanaji wa maji kwa kutumia maji ya Ziwa Victoria. Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo ali- yasema hayo Agosti, 2019 alipofa- nya ziara kwenye mradi wa maji wa Nyahiti, Wilaya Sya Misungwi Mkoani Mwanza kwa lengo la kujio- nea hatua iliyofikiwa ya utekelezwaji wake. Aliwaasa wananchi waendelee kuiamini Serikali ya Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwani hatua mbalimbali zinaendelea kuchukuliwa na Serikali yake kupitia Wizara ya Maji ya kuhakiki- sha huduma ya maji inafika kwenye maeneo yote yenye changamoto. “Tunaendelea hatua kwa hatua kutatua changamoto ya maji kwenye mikoa yote ya Tanza- nia Bara na kwa upande wa Kanda ya Ziwa tunate- keleza miradi 17 inayotumia maji kutoka Ziwa Vic- toria yeye thamani ya Bilioni 788,” alisema Profesa Mkumbo. Akiuzungumzia mradi wa maji wa Nyahi- ti, Profesa Mkumbo alisema gharama za utekeleza- ji wake ni Bilioni 13 na umekamilka kwa asilimia 97 na kwamba hatua iliyopo ni ya kuwaungan- Katibu Mkuu wa Wizara ya Maji, Profesa Kitila Mkumbo (kulia) akisikiliza maelezo ishia wananchi ambapo takriban wateja 2,150 ya utekelezaji wa mradi wa Nyahiti kutoka kwa aliyekuwa Mkurugenzi Mtendaji wataunganishwa kwenye awamu ya kwanza.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Ishirini na Nne – Tarehe 18 Julai, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita muuliza swali la kwanza nina matangazo kuhusu wageni, kwanza wale vijana wanafunzi kutoka shule ya sekondari, naona tangazo halisomeki vizuri, naomba tu wanafunzi na walimu msimame ili Waheshimiwa Wabunge waweze kuwatambua. Tunafurahi sana walimu na wanafunzi wa shule zetu za hapa nchini Tanzania mnapokuja hapa Bungeni kujionea wenyewe demokrasia ya nchi yetu inavyofanya kazi. Karibuni sana. Wapo Makatibu 26 wa UWT, ambao wamekuja kwenye Semina ya Utetezi na Ushawishi kwa Harakati za Wanawake inayofanyika Dodoma CCT wale pale mkono wangu wakulia karibuni sana kina mama tunawatakia mema katika semina yenu, ili ilete mafanikio na ipige hatua mbele katika kumkomboa mwanamke wa Tanzania, ahsanteni sana. Hawa ni wageni ambao tumetaarifiwa na Mheshimiwa Shamsa Selengia Mwangunga, Naibu Waziri wa Maji. Wageni wengine nitawatamka kadri nitakavyopata taarifa, kwa sababu wamechelewa kuleta taarifa. Na. 223 Barabara Toka KIA – Mererani MHE. DORA H. MUSHI aliuliza:- Kwa kuwa, Mererani ni Controlled Area na ipo kwenye mpango wa Special Economic Zone na kwa kuwa Tanzanite ni madini pekee duniani yanayochimbwa huko Mererani na inajulikana kote ulimwenguni kutokana na madini hayo, lakini barabara inayotoka KIA kwenda Mererani ni mbaya sana
    [Show full text]
  • Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Bunge La Tanzania
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA SABA YATOKANAYO NA KIKAO CHA THELATHINI NA MBILI 23 MEI, 2017 MKUTANO WA SABA KIKAO CHA THELATHINI NA MBILI TAREHE 23 MEI, 2017 I. DUA: Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) alisoma Dua Saa 3.00 Asubuhi na kuongoza Bunge. Makatibu mezani: 1. Ndugu Joshua Chamwela 2. Ndugu Neema Msangi II. HATI ZA KUWASILISHA MEZANI (1) Naibu Waziri wa Maliasili na Utalii – Mhe. Ramo Makani aliwasilisha Mezani:- - Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. (2) Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii – Mhe. Khalifa Salum Suleiman aliwasilisha Mezani:- - Taarifa ya Kamati ya Ardhi, Maliasili na Utalii kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Maliasili na Utalii kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017 pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. (3) Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Wizara ya Maliasili na Utalii – Mhe. Roman Selasini aliwasilisha Mezani:- - Taarifa ya Upinzani kuhusu Wizara ya Maliasili na Utalii juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. 1 III. MASWALI Maswali yafuatayo yaliulizwa na kujibiwa:- WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO Swali Na. 254: Mhe. Ritta Kabati (Kny. Mhe. Mahmoud H. Mgimwa) Nyongeza: Mhe. Ritta Kabati Mhe. Elias J. Kwandikwa Mhe. James Mbatia Mhe. Venance Mwamoto Swali Na. 255: Mhe. Ignas A. Malocha Nyongeza: Mhe. Ignas A. Malocha Mhe. Oran Njenza Mhe. Omary T. Mgimba Mhe. Adamson E. Mwakasaka Mhe. Zuberi Kuchauka Mhe.
    [Show full text]
  • 1 BUNGE LA TANZANIA ___MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA KUMI NA SABA Kikao Cha Nne – Tarehe 8 Novemba, 20
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA SABA Kikao cha Nne – Tarehe 8 Novemba, 2019 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Andrew J. Chenge) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae. Katibu. NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO NA MAZINGIRA): Taarifa ya Tatu ya Hali ya Mazingira Nchini (State of the Environment Report, 3). NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Taarifa ya Mwaka ya Tathmini ya Utendaji wa Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma kwa mwaka wa fedha 2018/2019 (The Annual Performance Evaluation Report on Public Procurement Regulatory Authority for the Financial Year 2018/2019). 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MWENYEKITI: Ahsante sana. Katibu. NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Swali letu la kwanza linaelekezwa Ofisi ya Rais – TAMISEMI. Linaulizwa na Mheshimiwa Justin Joseph Monko, Mbunge wa Singida Kaskazini. Na. 40 Kuwa na Uchaguzi Mdogo wa Serikali za Mitaa MHE. JUSTIN J. MONKO aliuliza:- Inapotokea Mwenyekiti wa Serikali ya Mtaa/Kijiji amefariki au kupoteza sifa ya kuwa Mwenyekiti wa Mtaa au Kijiji husika huongozwa na Kaimu Mwenyekiti:- Je, kwa nini Serikali haioni umuhimu wa kuwepo uchaguzi mdogo kama ilivyo kwa Madiwani na Wabunge? MWENYEKITI: Ahsante. Majibu kwa swali hilo, Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Waitara. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA
    [Show full text]