Maendeleo Ya Kilimo Na Ushirika Kwa Kipindi Cha Miaka 50 Ya Uhuru Wa Tanzania Bara (1961 - 2011)
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011) JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA WIZARA YA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA MAENDELEO YA KILIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961 - 2011) KILIMO KWANZA “Tumethubutu, Tumeweza, Tunazidi Kusonga Mbele” a kkilimoilimo mmiakaiaka 550.indd0.indd a 111/16/111/16/11 110:34:230:34:23 AAMM TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE b kkilimoilimo mmiakaiaka 550.indd0.indd b 111/16/111/16/11 110:34:230:34:23 AAMM MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011) KAULI YA WAZIRI Kwanza kabisa napenda kumshukuru Mwenyenzi Mungu kwa kunipa uhai na kuniwezesha kuungana na Watanzania wenzangu katika maadhimisho haya ya Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara. Katika kuadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa nchi yetu, hatuna budi kuwakumbuka waasisi na viongozi wa Taifa letu ambao wametoa mchango mkubwa katika maendeleo ya kilimo tunachojivunia leo. Tangu Uhuru wa Tanzania Bara upatikane nchi yetu imepitia awamu nne za uongozi. Awamu ya kwanza iliongozwa na Baba wa Taifa na Rais wa Kwanza Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere ambaye alikuwa mstari wa mbele na mhimili mkubwa wa kuwaongoza Watanzania katika kudai Uhuru na hatimaye kuupata hapo Desemba 9, 1961. Mara baada ya nchi yetu kupata Uhuru, Serikali ilitoa kipaumbele cha kwanza katika kuendeleza kilimo kama uti wa mgongo wa uchumi wetu. Kilimo kiliajiri zaidi ya asilimia 90 ya wananchi wote na mazao ya katani, kahawa na pamba yaliongoza kulipatia Taifa fedha za kigeni. Hivyo ilibidi kilimo kiendelezwe kwa kutumia mbinu mbalimbali za kisiasa, kijamii na kiuchumi. Kati ya miaka ya 1961 na 1980, zilibuniwa kaulimbiu na maazimio mbalimbali kama vile “Chakula ni Uhai”, “Siasa ni Kilimo”, “Kilimo cha Kufa na Kupona”, “Mvua za Kwanza ni za Kupandia” ili kuhamasisha maendeleo ya kilimo, pamoja na kuhamasisha kilimo cha ujamaa. Awamu ya Pili iliongozwa na Rais Ali Hassan Mwinyi ambapo tulishuhudia mageuzi ya kiuchumi ambayo yalikuwa kichocheo kikubwa katika maendeleo ya kilimo ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Sera ya Kilimo ya mwaka 1983. Awamu ya tatu ya uongozi ilikuwa chini ya Rais Benjamin William Mkapa ambapo katika awamu hiyo kilimo kilipata msukumo wa kipekee na kuwa chenye mafanikio. Katika awamu hiyo utekelezaji wa Sera ya Taifa ya Kilimo na Mifugo ya mwaka 1997 na uanzishwaji wa Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo ulishuhudia kilimo kikikua kutoka chini ya asilimia 3 hadi asilimia 6. Awamu ya nne ya uongozi ambayo ipo chini ya Rais Daktari Jakaya Mrisho Kikwete, kilimo kimeendelea kupewa kipaumbele kikubwa, ikiwa ni pamoja na utekelezaji wa Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP) na Programu ya Mageuzi na Modenaizesheni ya Ushirika (CRMP) ambazo zimekuwa chachu ya kuleta mapinduzi ya kijani hapa nchini. Jambo kubwa la kujivunia kutokana na kilimo ni kuwa kwa sasa asilimia 95 ya mahitaji ya Taifa ya chakula kinazalishwa hapa hapa nchini. Aidha, Serikali imeweka mfumo wa kuhifadhi chakula kwa ajili ya matumizi wakati upungufu unapotokea. Akiba ya Taifa ya Chakula imekuwa ikiongezeka kila mwaka na uwezo wa Wakala wa Taifa wa Hifadhi ya Chakula unatarajia kufi kia tani 400,000 i kkilimoilimo mmiakaiaka 550.indd0.indd SSec2:iec2:i 111/16/111/16/11 110:34:240:34:24 AAMM TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE ifi kapo mwaka 2015 kutoka uwezo wa kununua na kuhifadhi tani 150,000 mwaka 2009. Aidha, mikakati mbalimbali inaendelea kutekelezwa hususan kuongeza eneo la kilimo cha umwagiliaji, matumizi ya zana bora za kilimo na kuongeza upatikanaji wa pembejeo zinazohitajika katika kuongeza uzalishaji na tija. Katika Miaka 50 ya Uhuru wa nchi yetu, pamoja na kuwa na changamoto nyingi za kisiasa, kijamii na kiuchumi, kilimo chetu kimeendelea kuwa nguzo kuu na mhimili wa Uchumi wa Taifa letu. Hivyo, tunapoadhimisha Miaka 50 ya Uhuru tunayo sababu ya kwenda kifua mbele tukiwa na kaulimbiu yetu inayosema KILIMO KWANZA- “Tumethubutu, Tumeweza, Tunazidi Kusonga Mbele”. Kutokana na uzoefu tulioupata kwa miaka 50, napenda kuwahakikishia Watanzania kuwa tutasonga mbele kwa haraka, tujitosheleze kwa chakula na tuwe wazalishaji wakubwa wa mazao ya chakula na biashara, tutakaotegemewa na majirani zetu wa EAC, SADC na soko la kimataifa. Katika miaka 50 ijayo vizazi vyetu vitajivunia Taifa tajiri linalojitegemea kiuchumi, kijamii na lenye nguvu za kisiasa hapa duniani. Profesa Jumanne A. Maghembe (Mb.) WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA ii kkilimoilimo mmiakaiaka 550.indd0.indd SSec2:iiec2:ii 111/16/111/16/11 110:34:250:34:25 AAMM MAENDELEO YA KLIMO NA USHIRIKA KWA KIPINDI CHA MIAKA 50 YA UHURU WA TANZANIA BARA (1961-2011) MUHTASARI Mwaka huu wa 2011, nchi yetu inaadhimisha Miaka 50 ya Uhuru wa Tanzania Bara uliopatikana tarehe 9 Desemba, 1961 kutoka kwa wakoloni wa Kiingereza. Katika kuadhimisha miaka hiyo 50 tangu Uhuru, juhudi mbalimbali zimefanyika na zinaendelea kufanyika ili kuendeleza sekta ya kilimo. Juhudi hizo ni pamoja na tafi ti mbalimbali za kilimo, huduma za ugani, mafunzo ya wataalam, mafunzo ya wakulima, ujenzi wa miundombimu ya umwagiliaji, mipango ya matumizi bora ya ardhi, matumizi ya zana bora na maendeleo ya ushirika. Muundo wa Wizara inayosimamia sekta ya kilimo umekuwa ukibadilika katika vipindi tofauti kukidhi mahitaji ya kipindi husika. Kiuongozi, kuanzia mwaka 1961 mpaka sasa (2011), Wizara imeongozwa na Mawaziri 16 na Naibu Mawaziri 8 (Jedwali Na. 1). Waziri wa kwanza aliyeongoza Wizara alikuwa Mheshimiwa Dereck Bryceson. Kwa sasa (2011) Wizara inaongozwa na Mheshimiwa Profesa Jumanne Maghembe na Naibu Waziri Mheshimiwa Injinia Christopher Chiza. Katibu Mkuu wa kwanza wa Wizara alikuwa Bwana Ibrahim Sapi Mkwawa. Tangu Uhuru hadi sasa (2011), Wizara inayosimamia kilimo imeongozwa na Makatibu Wakuu 22 na Naibu Makatibu Wakuu sita. Katibu Mkuu wa Wizara wa sasa (2011) ni Bwana Mohamed S. Muya akiwa na Naibu Makatibu Wakuu wawili ambao ni Bibi Sophia Kaduma na Injinia Mbogo Futakamba. Katika muundo wa sasa Wizara ina Idara 10 ambazo ni Utafi ti na Maendeleo; Mafunzo; Maendeleo ya Mazao; Matumizi Bora ya Ardhi; Zana za Kilimo; Umwagiliaji na Huduma za Ufundi; Sera na Mipango; Utawala na Rasilimali Watu; Usalama wa Chakula; na Maendeleo ya Ushirika. Pia, Wizara ina vitengo nane ambavyo ni Sheria; Fedha na Uhasibu; Teknolojia ya Habari na Mawasiliano (TEHAMA) , Ukaguzi wa Ndani; Usajili wa Haki Miliki za Wagunduzi wa Aina Mpya za Mbegu; Mawasiliano Serikalini; Mazingira; na Ugavi na Manunuzi. Vilevile, Wizara ina wakala, mamlaka na taasisi tisa na inasimamia bodi tisa za mazao. Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika ina majukumu ya kuhakikisha Taifa linajitosheleza kwa chakula na kwamba kilimo kinatoa mchango mkubwa katika uchumi na katika kuondoa umaskini. Katika kuhakikisha kwamba hayo yanatekelezwa, Wizara inaongozwa na Dira pamoja na Dhamira ya kutoa huduma bora za kilimo na ushirika, kujenga uwezo wa Serikali za mitaa, na kuweka mazingira mazuri kwa wadau na sekta binafsi ili kuchangia ipasavyo katika uzalishaji wenye tija kwa maendeleo endelevu ya kilimo na ushirika. Ndani ya kipindi cha Miaka 50 ya Uhuru yamekuwepo mabadiliko ya sera na mikakati ambayo yamekuwa yakianzishwa ili kutekeleza azma ya Serikali ya kuinua uchumi wa nchi kupitia sekta ya kilimo. Mabadiliko makuu ya sera yalitokea baada ya kutangazwa kwa Azimio la Arusha la mwaka 1967 lililosisitiza Siasa ya Ujamaa na Kujitegemea ambalo katika utekelezaji wake kaulimbiu mbalimbali zilibuniwa. Kaulimbiu hizo ni pamoja na Azimio la Iringa la “Siasa ni Kilimo” la mwaka 1972 lililosisitiza uanzishwaji wa mashamba makubwa ya vijiji yatakayoendeshwa kwa iii kkilimoilimo mmiakaiaka 550.indd0.indd SSec2:iiiec2:iii 111/16/111/16/11 110:34:250:34:25 AAMM TUMETHUBUTU, TUMEWEZA, TUNAZIDI KUSONGA MBELE kutumia zana bora, wanyamakazi na kilimo cha umwagiliaji. Azimio hilo lilifuatiwa na Operesheni Vijiji ambayo ilikuwa na lengo la kuwaweka wananchi pamoja ili wapate huduma muhimu kama vile maji, elimu na afya. Operesheni Vijiji kwa upande wa sekta ya kilimo iliambatana na kuanzishwa kwa mashamba makubwa ya vijiji na mashamba ya bega kwa bega. Mwaka 1974 ilizinduliwa “Kampeni ya Kilimo cha Kufa na Kupona” ambayo ililenga kuongeza uzalishaji wa chakula katika ngazi ya Kaya. Mazingira mbalimbali ya kiuchumi na kijamii yaliyoipata nchi yetu mwishoni mwa miaka ya 70 yalichangia kutofi kiwa kwa baadhi ya malengo ya kuimarisha kilimo kama ilivyotarajiwa. Hivyo, mwaka 1982 Serikali iliagiza ufanyike uchambuzi wa kubaini upungufu wa kisera uliosababisha kutofi kiwa kwa malengo ya kujitosheleza kwa chakula. Uchambuzi huo uliwezesha upatikanaji wa sera ya kwanza ya kilimo ya mwaka 1983 ambayo ililenga katika kuhakikisha upatikanaji wa chakula katika ngazi ya kaya na kuboresha kiwango cha lishe na maisha ya Watanzania. Sera hiyo ilifanyiwa marekebisho na kuunganishwa na sera ya mifugo na kupatikana kwa Sera ya Kilimo na Mifugo ya mwaka 1997 ambayo pia imefanyiwa marekebisho na ikishapitishwa itajulikana kama Sera ya Taifa ya Kilimo ya mwaka 2009. Mkakati wa Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDS) wa mwaka 2001, ambao unatekelezwa kupitia Programu ya Kuendeleza Sekta ya Kilimo (ASDP) kuanzia mwaka 2006, ikiwa na malengo makubwa mawili ambayo ni (i) Kuwawezesha wakulima na wafugaji kuongeza uzalishaji na tija (ii) Kujenga mazingira bora ya kisera na kisheria ili kuongeza uwekezaji wa sekta binafsi katika kilimo. Azimio la Kilimo Kwanza na Programu Kabambe ya Kuendeleza Kilimo Afrika (Comprehensive Africa Agriculture Development Program –CAADP) inalenga kuongeza rasilimali ili kuleta mapinduzi ya kilimo kwa kasi zaidi. Aidha, katika kuendeleza ushirika Sera ya kwanza ya Maendeleo ya Ushirika Tanzania ilipitishwa mwaka 1997 kwa ajili ya kutoa malengo ya jumla na mikakati muhimu kuhakikisha kwamba makundi ya watu maskini katika jamii yanakuwa na chombo cha kuaminika cha kuwezesha kufi kia malengo yake ya kiuchumi na kijamii. Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 2002 ilipitishwa, ili kuzingatia upungufu uliotokana na Sera ya Maendeleo ya Ushirika ya mwaka 1997. Sera hiyo inatekelezwa kupitia Programu Kabambe ya Mageuzi na Modenaizesheni ya Ushirika (CRMP) na Sheria ya Vyama vya Ushirika Na.20 ya mwaka 2003.