6 Novemba 2013
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILINO YA BUNGE ________ MKUTANO WA KUMI NA TATU Kikao cha Saba – Tarehe 6 Novemba, 2013 (Mkutano Ulianza saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua TAARIFA YA SPIKA SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, napenda kuwatangazia kwamba kwa mujibu wa Kanuni ya 30(1) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, toleo la Aprili, 2013 na Ibara ya 91 (2) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete anakusudia kulihutubia Bunge siku ya Alhamisi tarehe 7 Novemba, 2013 kuanzia saa 10.00 jioni. Wote mnaombwa kuwepo ukumbini siku hiyo ili kumsikiliza Mheshimiwa Rais. Katibu! HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Chuo Kikuu Mzumbe kwa Mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2012 [The Annual Report and Accounts of Mzumbe University for the Year ended 30th June, 2012]. 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali, tunaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu. Namwita Mheshimiwa Vicent Joseph Nyerere aulize swali lake. Na. 82 Ujenzi wa Hospitali ya Mkoa wa Mara MHE. VICENT J. NYERERE aliuliza:- Kwa miaka miwili mfululizo Serikali imekuwa ikitenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara, lakini mpaka sasa kazi haijaanza. Je, ni nini kimekwamisha ujenzi huo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vicent Josephat Nyerere kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ujenzi wa Hospitali ya Rufaa ya Mkoa wa Mara ulianza kupitia nguvu za wananchi mwaka 1980 na kusimama mwaka 1987, baada ya wananchi kushindwa kuendeleza ujenzi huo kutokana na kuongezeka kwa gharama za ujenzi. Baada ya juhudi za kumpata mwendelezaji kutokufanikiwa, mwaka 2010 hoja ilijengwa kupitia Kamati ya Ushauri ya Mkoa (RCC) na kukubaliwa. Mheshimiwa Spika, mapendekezo ya gharama za kukamilisha ujenzi yaliingizwa katika mpango wa miaka mitano wa maendeleo wa Mkoa wa Mara kuanzia mwaka wa fedha 2012/2013 hadi 2016/2017 inayokadiriwa kuwa Shilingi bilioni 37 mpaka utakapokamilika. Mwaka wa fedha 2012/2013 jumla ya Shilingi bilioni 2.1 zilitengwa na kutolewa na Serikali, na mwaka 2013/2014 zilitengwa ambapo hadi kufikia mwezi Oktoba, 2013 Shilingi milioni 500 zimetolewa kwa 2 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI)] ajili ya kuendeleza mradi. Kazi nyingine zinazofanyika ni ujenzi wa uzio kuzunguka eneo la Hospitali kwa gharama ya Shilingi milioni 250 kupitia bajeti ya matumizi ya kawaida. Mheshimiwa Spika, awali Mkoa uliomba Mfuko wa Hifadhi ya Jamii ya TASAF ndiyo wajenge. Hata hivyo, mfuko haukuweza kuafikiana na Mkoa kwa kuwa walikuwa na miradi mingine ya ujenzi inayoendelea. Hivyo, hatua zilizochukuliwa na Mkoa ni kutangaza zabuni ili kumpata Mkandarasi ambapo Zabuni ilitangazwa katika gazeti la Daily News la Tarehe 21 Mei, 2013. Taratibu za kumpata Mkandarasi ziko katika hatua za mwisho. MHE. VINCENT J. NYERERE: Mheshimiwa Spika, nashukuru. Kwa kuwa, Serikali inatumia fedha nyingi sana kuwatibu watu nje nikiwemo mimi mwenyewe, na Hospitali ya Apollo ilionyesha nia ya kuwekeza katika Hospitali hapa Tanzania; kwa nini Serikali isiwasiliane na watu wa Apollo kwa ajili ya kuwapo Hospitali hii ili shughuli ya ujenzi wa Hospitali iende haraka? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Vicent Nyerere kama ifuatavyo:- Ni kweli kwamba tunatumia gharama kubwa sana kupeleka wagonjwa nje na kwa sasa hivi Serikali iko katika hatua za kuziboresha hospitali zetu kuhakikisha kwamba magonjwa mengi ambayo yanawapeleka wagonjwa nje yanatibiwa humu humu ndani. Yeye mwenyewe ni shahidi kwamba sasa hivi Muhimbili wanafanya operation ya moyo na hata vitengo vingi ambavyo wagonjwa wetu walikuwa wanapelekwa nje vimeimarishwa. Ukienda Moi sasa hivi huduma nyingi kwa kweli, kwa kiasi kikubwa zinapatikana Muhimbili na katika hospitali zetu za Rufaa za Bugando na KCMC. SPIKA: Mheshimiwa Conchesta nimekuona! 3 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) MHE. CONCHESTA L. RWAMLAZA: Mheshimiwa Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Mheshimiwa Spika, yako majengo mengi ambayo yamejengwa katika Hospitali za Mikoa na yamekamilika bila kutumika. Kwa mfano, Hospitali ya Mkoa wa Singida, kuna jengo la Hospitali ya Tumbi lakini pia kuna jengo la Siha. Ni lini Serikali sasa itaruhusu au kutoa pesa ili majengo haya yaweze kutumika ili huduma ziwepo kwa ajili ya wananchi? (Makofi) SPIKA: Ahsante kwa swali zuri. Mheshimiwa Waziri wa Nchi, majibu! WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, ni kweli kuna majengo mengi yamekamilika na yanahitaji kutumika na Mheshimiwa aliyeuliza swali, mwenyewe ni Mjumbe wa Kamati ya TAMISEMI na ana ushahidi kwamba katika bajeti ya mwaka huu Tumbi, Hospitali ya Singida na Siha tumezitengea pesa ambazo zitawawezesha kununua vifaa ili ziweze kutumika. SPIKA: Naomba tuendelee na swali linalofuata, Mheshimiwa Diana Chilolo. Na. 83 Ujenzi wa Kituo cha Afya Shelui MHE. DIANA M. CHILOLO aliuliza:- Wakati wa kampeni za Urais mwaka 2010, Mheshimiwa Rais aliahidi kujenga Kituo cha Afya Kata ya Shelui na tayari wananchi chini ya uongozi wa Kata hiyo walishaanza kuchangia mfuko wa ujenzi huu na kufyatua tofali; na ahadi hii Serikali imeiachia Halmashauri ya Wilaya ya Iramba ambayo ina mapato madogo sana kupitia vyanzo vyake:- 4 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [MHE. D. M. CHILOLO] Je, Serikali itakuwa tayari kutoa fedha kupitia Mfuko wa MMAM ulioko Halmashauri? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Diana M. Chilolo, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, miradi ya ujenzi wa Zahanati na Vituo vya Afya huibuliwa na wananchi wenyewe kupitia Mpango wa Fursa na Vikwazo katika Maendeleo (O&OD) na kutekelezwa kwa ubia wa wananchi na Halmashauri. Halmashauri huchangia gharama kidogo za utekelezaji wa miradi hiyo kwa kuwezesha upatikanaji wa vifaa pamoja na usimamizi. Halmashauri ya Wilaya ya Iramba kwa kushirikiana na wananchi, imeanza ujenzi wa Kituo hicho cha Afya ambapo vifaa yakiwemo matofali 3,000 na mifuko ya Saruji 70 vimeandaliwa na ujenzi upo katika hatua ya msingi. Mheshimiwa Spika, katika bajeti ya mwaka 2013/2014, Halmashauri imetenga Shilingi milioni 80 kutokana na fedha za ruzuku ya maendeleo katika Serikali za Mitaa (LGCDG) kwa ajili ya ujenzi huo. Wananchi watachangia Shilingi milioni 40 ili kukamilisha utekelezaji wa mradi huu ambapo unatarajiwa kugharimu Shilingi milioni 120 katika awamu ya kwanza. Aidha, katika mwaka huu Halmashauri imeweka kipaumbele kwa ajili ya kukamilisha ujenzi wa nyumba tano za watumishi katika Zahanati za Mwendui, Gembena na Kisharita kwa gharama ya Shilingi milioni 75.0, kukamilisha majengo ya wagonjwa wa nje (OPD) katika Zahanati tatu za Kata ya Urughu kwa gharama ya Shilingi milioni 60.0 na kukamilisha majengo ya Zahanati za Misuna na Kisimba kwa gharama ya Shilingi milioni 50.5. Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Iramba itaendelea kutenga fedha kila mwaka kadri zitakavyopatikana ili kukamilisha ujenzi huo. 5 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Diana Chilolo swali la nyongeza. MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri, nina swali moja dogo la nyongeza. Kwa kuwa, changamoto ya kujenga Kituo cha Afya hiki ilitokana na ahadi ya Mheshimiwa Rais kuahidi kujenga Kituo cha Afya hapo; na kwa kuwa jitihada hizi alizozisema Mheshimiwa Waziri, mpaka sasa hivi wananchi wana tofali 6,000 mpaka leo hii na wana Shilingi milioni tano za kuchangishana wenyewe na ahadi ya Serikali ilikuwa itenge kuanzia bajeti hii ambayo tunaitumia sasa: Je, kwa kusubiria bajeti ya mwaka kesho, hatuoni kwamba wananchi hawa tunawakatisha tamaa na wanakuwa hawana imani na ahadi ya Mheshimwa Rais? Je, Serikali itakuwa tayari kutafuta pesa popote kuweka nguvu ya ujenzi wa Kituo hiki cha Afya kwenye Mji? Shelui ni mji mdogo... SPIKA: Aise! Uliza swali. MHE. DIANA M. CHILOLO: Mheshimiwa Spika, naomba majibu. SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Nchi, majibu! WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Spika, ni kweli ni ahadi ya Mheshimiwa Rais na inavyotakiwa ahadi za Mheshimiwa Rais tuweke katika mipango yetu na hapo hapo Serikali inaangalia kwamba inatoa pesa kutoka katika vyanzo gani. Katika jibu langu la msingi, nimesema katika bajeti ambayo tunayo ya mwaka 2013/2014 Halmashauri imetenga Shilingi milioni 80 kutoka katika pesa za ruzuku ya Serikali za Mitaa. Ukishasema ruzuku, maana yake inatoka Serikali kuu na siyo kutoka vyanzo vya Halmashauri. Kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge napenda nikuhakikishie kwamba ahadi 6 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) [WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI)] ya Mheshimiwa Rais inatekelezwa na Serikali imeanza kutoa pesa. Katika bajeti hii imeanza imeanza kwa Shilingi milioni 80 na bajeti zinazofuata pia itaendelea kutenga. SPIKA: Ahsante. Mheshimiwa Zambi, swali la nyongeza. MHE. GODFREY W. ZAMBI: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipatia nafasi ili niulize swali