Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document) Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Arobaini na Mbili – Tarehe 9 Agosti, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatayo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2011/2010 MHE. WILLIAM A. MGIMWA - MWENYEKITI WA KAMATI YA VIWANDA NA BIASHARA: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda na Biashara Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka 2010/2012 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MHE. GRACE S. KIWELU - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Viwanda na Biashara kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla hatujaendelea, naomba kulitaarifu Bunge kwamba Waziri Mkuu - Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda amesafiri kikazi kwenda Morogoro na inawezekana akarudi mchana wa leo. Kutokana hali hiyo, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameelekeza kuwa Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) atakaimu nafasi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu hadi wakati huo. Ahsante. (Makofi) MASWALI NA MAJIBU Na. 383 Matatizo ya Maji Maji Kata ya Mbokomu MHE. SUSAN J. LYIMO aliuliza:- Liko tatizo sugu la maji kwenye Kata ya Mbokomu hususan kwenye Vijiji vya Korini Kusini na Juu Tema pamoja na Vitongoji vyake ambalo halijapatiwa ufumbuzi. (a) Je, ni lini tatizo hilo litatatuliwa? (b) Kwa sababu vyanzo vya maji havikidhi mahitaji ya wakazi wa maeneo hayo: Je, Serikali haioni haja ya kuwa na vyanzo mbadala vikiwemo vile vya maji ardhini? NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:- 1 Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Susan Jerome Lyimo - Mbunge wa Viti Maalum lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, kama ilivyo kwa maeneo mengine ya nchi, Serikali inatekeleza programu ya Sekta ya Maendeleo ya Maji katika Halmashauri kupitia Mpango wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini. Katika mwaka 2010/2011 Halmashauri ya Wilaya ya Moshi iliidhinishiwa shilingi bilioni 2.2 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa vijiji 12 ambavyo vimechagua kutumia teknolojia ya mserereko (Gravity Scheme) kutoka kwenye mito ya maji iliyopo. Kati ya fedha hizo, shilingi milioni 320.5 zimepokelewa na kazi zilizokwishafanyika ni usanifu wa miradi ya vijiji husika na uandaaji wa makabrasha ya zabuni ambapo taarifa ya kazi hiyo iliwasilishwa kwa Waziri wa Maji ili kupata ridhaa ya kutangaza zabuni. Utekelezaji wa mradi huu unafanyika kwa lot tatu ambapo awamu ya kwanza inahusisha vijiji vya Korini Kaskazini na Korini Kusini vilivyoko katika Kata ya Mbokomu. Mradi huu ukikamilika, utaondoa tatizo la maji katika Kata ya Mbokomu na maeneo mengine ndani ya Halmashauri. Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2011/2012, Halmashauri imetenga shilingi milioni 704.7 kupitia mpango wa Sekta ya Maji kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika vijiji hivyo 12 vilivyochaguliwa. Mheshimiwa Naibu Spika, miradi mingine inayotekelezwa ndani ya Halmashauri ni Kirua Kahe Water Supply ambapo ujenzi unatagemea kukamilika Desemba, 2011. Kutakuwa na extension tatu zitakazotekelezwa kuanzia Aprili, 2012. Katika mradi huu kuna makubaliano kati ya Halmashauri na Mhisani aitwaye KfW Shirika la Ujerumani ambalo litahisaini mradi huo kwa gharama ya shilingi bilioni 3.7. Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wa vijiji nilivyovitaja hapo juu walihamasishwa na kuelimishwa kuhusu uchangiaji wa ujenzi wa miradi ya maji na kuhusishwa kuchagua technolojia inayowafaa na watakayoweza kulipia gharama za uendeshaji ambapo vijiji vyote 12 vilichagua teknolojia ya serereko. Hivyo, kwa kutumia mbinu shirikishi, wananchi wenyewe wanapewa nafasi ya kuamua teknolojia inayowafaa kwa kuzingatia dhana au uchangiaji na huduma za maji katika jamii. Vyanzo vya maji vinavyotumika kwa sasa ni Mto Mrusunga na uwezo wa chanzo hiki ni lita 44 kwa sekunde. MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa tatizo hili ni la muda mrefu sana na hata Naibu Waziri wa kipindi kilichopita Mheshimiwa Chiza aliwahi kwenda miaka mitatu iliyopita na akaahidi tatizo hilo litakamilishwa, lakini mpaka leo bado na swali langu bado halijajibiwa kwa sababu nimeuliza ni lini tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi? Kwa hiyo, nilikuwa nataka jibu la hilo. Pili, kwa kuwa mila na desturi za Wachaga ni pamoja na kufuga mifugo ya ndani, yaani hawatoi mifugo yao nje, na kwa maana hiyo, tatizo la maji ni kubwa sana, vile vile ikizingatiwa kwamba maeneo hayo kwa sasa hivi wazee wengi ndio wapo: Je, Mheshimiwa Naibu Waziri, haoni kwamba tatizo hilo ni kubwa sana na kwa hiyo, inabidi wawapatie maji hasa ikizingatiwa Mto Mrusunga ambao ni chanzo kikuu kwa sasa hivi hauna maji kabisa? (Makofi) NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, ni kwamba Halmashauri ya Moshi inatekeleza huu mradi kupitia program ya maji na imefikia hatua nzuri na mpaka sasa wameshatangaza tender ili kuweza kupata mkandarasi atakayeendelea kujenga katika awamu ya kwanza. Nimesema kwamba tuna bahati kwamba Shirika la Ujerumani limekubali kufadhili mradi huu kwa shilingi bilioni 3.7 na watafanya kwa awamu. Kwa hiyo, nina uhakika katika muda mpaka tufikie 2015 tatizo hili la maji litakuwa limekwisha. Maeneo mengine tutaendelea kuyapanua jinsi uwezo wa fedha utakavyokuwa unapatikana. Kuhusu Mto Mrugusunga ni kwamba maji ya mto ule yanatosha kwa kipindi cha masika. Lakini wakati wa kiangazi kuna tatizo la uharibifu wa mazingira, kwa hiyo, maji hupungua. Namwomba Mheshimiwa Lyimo asaidie pia kuhamasisha wananchi kuhifadhi mazingira ili tuwe na 2 maji endelevu na vyanzo vyetu vya maji viwe vinaweza kukidhi kwa muda wote wa mwaka mzima. (Makofi) Na. 384 Kupandishwa kwa Mipaka ya Wilaya MHE. DKT. ANTHONY G. MBASSA aliuliza:- Kulikuwa na suala la kupindishwa kwa mipaka ya Wilaya wakati Wilaya ya Chato ikimegwa toka Wilaya kongwe ya Biharamulo hususan katika Kijiji cha Nyantimba na taarifa za awali zilipelekwa TAMISEMI. Je, nini hatma ya suala hilo? WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Anthony Mbassa - Mbunge wa Biharamulo Magharibi kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2005 Serikali kupitia Tangazo Na. 337 ilitangaza kuundwa kwa Wilaya mpya ya Chato ambayo ilitokana na Wilaya mama ya Biharamulo. Mipaka ya Wilaya iliyowekwa ni ya asili kwa kutumia mito na milima. Aidha, tangazo hilo lilionyesha kuwa Kijiji cha Nyantimba ni kimoja na kipo katika Wilaya ya Biharamulo. Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2009 Serikali ilitoa tangazo la Serikali Na. 205 lilitangaza orodha ya vijiji vilivyokuwa vimesajiliwa na kuonyesha kuwa Kijiji cha Nyantimba kipo katika Wilaya zote mbili za Biharamulo na Chato isipokuwa tofauti pekee ni kwamba Kijiji cha Nyantimba kwa upande wa Biharamulo kina vitongoji vinne na kwa upande wa Wilaya ya Chato kina vitongoji vitano. Mheshimiwa Naibu Spika, mkanganyiko huu unatokana na tofauti iliyopo kati ya mpaka wa Wilaya na mpaka wa Jimbo la Uchaguzi la Chato. Serikali ilipoweka mpaka wa Wilaya ya Biharamulo na Wilaya mpya ya Chato haikuzingatia mpaka wa Jimbo, hivyo kuna sehemu ya Jimbo la Uchaguzi la Chato ambayo ilibaki upande wa Biharamulo na ni sehemu hii ambapo Kijiji cha Nyantimba kinapatikana. Aidha, kuna makosa ya kiuchapaji ambayo yalifanyika katika matangazo ya Serikali ya kukitaja Kijiji cha Nyantimba kuwepo katika Wilaya zote mbili wakati siyo sahihi, kwani kipo kijiji kimoja tu cha Nyantimba. Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, itawasilisha tena jambo hili kwa Tume ya Uchaguzi ili iweze kurekebisha mpaka wa Jimbo la Uchaguzi la Chato uendane na mpaka wa Wilaya ya Chato. Aidha, Serikali italifanyia pia marekebisho tangazo la Serikali Na. 205 ili kuondokana na kasoro zilizopo. MHE. DKT. ANTHONY G. MBASSA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa katika jibu la msingi Mheshimiwa Waziri ameonyesha kabisa kwamba Serikali imejichanganya na ilichapisha matangazo haya kimakosa:- (a) Je, Serikali haoni kwamba kipengele cha kwanza cha tangazo la Serikali Na. 337 lilikuwa sahihi kwa kupatia kijiji hiki Wilaya ya Biharamulo? (b) Kwa kuwa jopo la watalaam lilikaa na nyaraka zikaletwa TAMISEMI zikibainisha kabisa kijiji hiki kinapaswa kuwa Wilaya ya Biharamulo na siyo Chato: Je, haoni kwamba sasa ni wakati muafaka wa kupitia nyaraka na kutoa tamko katika Bunge hili kwamba kijiji hiki kinapaswa kirudi Biharamulo na siyo Chato? 3 WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa niaba ya Waziri Mkuu, napenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:- Kama nilivyosema kwenye jibu la msingi kwamba GN hizi zote karibuni zimechanganya. GN 337 yenyewe inagawa Wilaya ya Chato na Wilaya ya Biharamulo hiyo ni Wilaya. GN 205 imegawa Vijiji na Kata. Napo hapo kuna mchanganyiko. GN 190 ambayo imetaja Halmashauri ya Wilaya ya Chato Kijiji cha Nyantimba kiko katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato. Sasa kwa kuwa nyaraka zote hizi ziko TAMISEMI na kwa kuwa Kijiji cha Nyantimba sasa hivi kinapata huduma zote kutoka Chato, ni vyema na ni busara tukapitia zile nyaraka zote, lakini tukarudia pia kwa wananchi kuwauliza kwamba ni vyema wachague
Recommended publications
  • 9Aprili,2013
    9 APRILI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kwanza - Tarehe 9 Aprili, 2013 WIMBO WA TAIFA (Hapa Waheshimiwa Wabunge Waliimba Wimbo wa Taifa) (Mkutano Ulianza Saa 3.00 Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa msimame tena. Mtakumbuka kwamba wakati wa Vikao vyetu vya Kamati, kwa bahati mbaya sana tulimpoteza mpenzi wetu Mheshimiwa Salim Hemed Khamis. Kwa hiyo, tumkumbuke kwa dakika moja. (Hapa Waheshimiwa Wabunge walisimama kwa Dakika moja kumkumbuka Mheshimiwa Salim Hemed Khamis aliyekuwa Mbunge wa Chambani Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amin. Ahsanteni sana na karibuni tukae. 1 9 APRILI, 2013 Waheshimiwa Wanbunge, katika Mkutano wa Tisa, Bunge lilipitisha Muswada wa Sheria ya Serikali uitwao The Plant Breeders` Rights Bill, 2012, kwa taarifa hii napenda kulialifu Bunge hili Tukufu kwamba, Mswada huo umekwisha pata kibali cha Mheshimiwa Rais na kuwa Sheria ya nchi iitwayo: The Plant Breeders` Rights Act, 2012 Na. 9 ya mwaka 2012. Kwa hiyo, ule sasa ni sheria ya Nchi. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kuwasilisha mezani Taarifa ya Matoleo yote ya Gazeti la Serikali pamoja na nyongeza zake zilizochapishwa tangu Kikao cha mwisho cha Mkutano wa Bunge uliopita. Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. MASWALI NA MAJIBU Na. 1 Kujenga Barabara ya Old Moshi kwa Lami MHE. GODFREY W. ZAMBI (K.n.y. MHE. DKT. CYRIL A. CHAMI) aliuliza:- Je, Serikali itatekeleza lini ahadi ya kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Old Moshi inayoanzia Kiboriloni kupitia Kikarara, Tsuduni hadi Kidia? 2 9 APRILI, 2013 NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Hamsini na Mbili - Tarehe 22 Agosti, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kwa masikitiko makubwa natoa taarifa kwamba Mheshimiwa Mussa Hamisi Silima, Mbunge kutoka Baraza la Wawakilishi Zanzibar, jana Jumapili, tarehe 21 Agosti, 2011 majira ya jioni kama saa mbili kasorobo hivi walipokuwa wakirejea kutoka Dar es Salaam, yeye na familia yake walipata ajali mbaya sana katika eneo la Nzuguni, Mjini Dodoma. Katika ajali hiyo, mke wa Mbunge huyo aitwaye Mwanaheri Twalib amefariki dunia na mwili wa Marehemu upo hospitali ya Mkoa hapa Dodoma ukiandaliwa kupelekwa Zanzibar leo hii Jumatatu, tarehe 22 August, 2011 kwa mazishi yatanayotarajiwa kufanyanyika alasili ya leo. Kwa hiyo, naomba Waheshimiwa Wabunge tusimame dakika chache tumkumbuke. (Heshima ya Marehemu, dakika moja) (Hapa Waheshimiwa Wabunge walisimama kwa dakika moja) Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, amina. Ahsanteni sana, tukae. Kwa hiyo sasa hivi tunavyoongea Mheshimiwa Mbunge ambae nae pia ameumia vibaya na dereva wake wanaondoka na ndege sasa hivi kusudi waweze kupata yanayohusika kule Dar es Salaam na pia kule watakuwa na watu wa kuwaangalia zaidi. Lakini walikwenda Zanzibar kumzika kaka yake na Marehemu huyu mama. Kwa hiyo, wamemzika marehemu basi wakawa wanawahi Bunge la leo ndiyo jana usiku wamepata ajali. Kwa hiyo, watakaokwenda kusindikiza msiba, ndege itaondoka kama saa tano watakwenda wafuatao, watakwenda Wabunge nane pamoja na mfawidhi zanzibar yeye anaongozana na mgonjwa sasa hivi lakini ataungana na wale kwenye mazishi.
    [Show full text]
  • (Online Document) 1 BUNGE LA TANZANIA
    Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Sita – Tarehe 18 Mei, 2015 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kutokana na maagizo yaliyotolewa humu wiki iliyopita kuhusu Hati za kuwasilisha Mezani. Kama kuna kundi lolote, Kamati, Serikali au Upinzani hawajaleta Hati hazisomwi. Waziri wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais! Mheshimiwa Naibu Waziri! HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MUUNGANO): Randama za Makadirio ya Matumizi kwa Ofisi ya Makamu wa Rais na Taasisi zake kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma) pamoja na (Utawala Bora) kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS (MAHUSIANO NA URATIBU): Hotuba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. MHE. JASSON S. RWEIKIZA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA: 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma), (Utawala Bora na Mahusiano na Uratibu) kwa mwaka wa fedha 2014/2015 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. MHE. ESTHER N. MATIKO - MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI KWA OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA, UTAWALA BORA NA MAHUSIANO NA URATIBU: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Ofisi ya Rais (Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Utawala Bora na Mahusiano na Uratibu kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016 SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tunaanza maswali Ofisi ya Rais, Mahusiano na Uratibu, Mheshimiwa Engineer Athumani Mfutakamba.
    [Show full text]
  • Tanzania Human Rights Report 2016
    Tanzania Human Rights Report 2016 LEGAL AND HUMAN RIGHTS CENTRE & ZANZIBAR LEGAL SERVICES CENTRE NOT FOR SALE Tanzania Human Rights Report - 2016 Mainland and Zanzibar - i - Tanzania Human Rights Report 2016 Part One: Tanzania Mainland - Legal and Human Rights Centre (LHRC) Part Two: Zanzibar - Zanzibar Legal Services Centre (ZLSC) - ii - Tanzania Human Rights Report 2016 Publishers Legal and Human Rights Centre Justice Lugakingira House, Kijitonyama P. O. Box 75254, Dar es Salaam, Tanzania Tel: +255222773038/48, Fax: +255222773037 Email: [email protected] Website: www.humanrights.or.tz & Zanzibar Legal Services Centre P. O. Box 3360, Zanzibar, Tanzania Tel: +2552422384 Fax: +255242234495 Email: [email protected] Website: www.zlsc.or.tz Partners The Embassy of Sweden The Embassy of Norway Oxfam Rosa Luxemburg UN Women Open Society Initiatives for Eastern Africa Design & Layout Albert Rodrick Maro Munyetti ISBN: 978-9987-740-30-7 © LHRC & ZLSC 2017 - iii - Tanzania Human Rights Report 2016 Editorial Board - Part One Dr. Helen Kijo-Bisimba Adv. Imelda Urio Ms. Felista Mauya Adv. Anna Henga Researchers/Writers Paul Mikongoti Fundikila Wazambi - iv - Tanzania Human Rights Report 2016 About LHRC The Legal and Human Rights Centre (LHRC) is a private, autonomous, voluntary non- Governmental, non-partisan and non-profit sharing organization envisioning a just and equitable society. It has a mission of empowering the people of Tanzania, so as to promote, reinforce and safeguard human rights and good governance in the country. The broad objective is to create legal and human rights awareness among the public and in particular the underprivileged section of the society through legal and civic education, advocacy linked with legal aid provision, research and human rights monitoring.
    [Show full text]
  • Tarehe 12 Aprili, 2011
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Tano – Tarehe 12 Aprili, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Taarifa ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioisha tarehe 30 Juni, 2010 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Financial Statements of Local Government Authorities for the Financial Year ended 30th June, 2010). NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE.GREGORY G. TEU): Taarifa ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu kwa Mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2010 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Audit of the Financial Statement of the Central Government for the Year ended 30th June, 2010). Taarifa ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Hesabu zilizokaguliwa za Mashirika ya Umma kwa Mwaka 2009/2010 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Financial Statement of Public Authorities and other Bodies for the Financial Year 2009/2010). Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Ukaguzi wa Ufanisi na Upembuzi kwa kipindi kilichoishia tarehe 31 Machi, 2011 (The General Report of the Controller and Auditor General on the Performance and Forensic Audit Report for the Period ended 31st March, 2011).
    [Show full text]
  • MKUTANO WA ISHIRINI ___Kikao Cha Kumi Na Mbili
    Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA ISHIRINI __________ Kikao cha Kumi na Mbili - Tarehe 25 Mei, 2015 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. MHE. MAUA ABEID DAFTARI (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MAENDELEO YA JAMII): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2014/15 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) MHE. MOSES J. MACHALI (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI JUU YA WIZARA YA MAENDELEO YA JAMII, JINSIA NA WATOTO): Taarifa ya Msemaji wa Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Wizara ya Maendeleo ya Jamii, Jinsia na Watoto kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Kazi na Ajira kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016.
    [Show full text]
  • Consequences for Women's Leadership
    The Politics Behind Gender Quotas: Consequences for Women’s Leadership Equity in African Legislatures by Christie Marie Arendt B.A. in Interdisciplinary Studies in Social Science, May 2004, Michigan State University M.A. in International Affairs, May 2006, The George Washington University A Dissertation submitted to The Faculty of The Columbian College of Arts and Sciences of The George Washington University in partial fulfillment of the requirements for the degree of Doctor of Philosophy January 31, 2017 Dissertation directed by Kimberly J. Morgan Professor of Political Science and International Affairs The Columbian College of Arts and Sciences of The George Washington University certifies that Christie Marie Arendt has passed the Final Examination for the degree of Doctor of Philosophy as of December 16, 2016. This is the final and approved form of the dissertation. The Politics Behind Gender Quotas: Consequences for Women’s Leadership Equity in African Legislatures Christie Marie Arendt Dissertation Research Committee: Kimberly J. Morgan, Professor of Political Science and International Affairs, Dissertation Director Jennifer Brinkerhoff, Professor of International Affairs, International Business, and Public Policy & Public Administration Eric Kramon, Assistant Professor of Political Science and International Affairs, Committee Member ii © Copyright 2017 by Christie Marie Arendt All rights reserved iii Dedication To my parents, Anne and Steve Arendt, none of this was possible without your enduring love and support. iv Acknowledgments This dissertation benefitted from the encouragement and guidance of a number of people. As an alumna of The George Washington University’s Elliott School of International Affairs, I knew that GW would provide a perfect environment to pursue my doctoral studies.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Arobaini na Moja – Tarehe 5 Agosti, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. NAIBU WAZIRI WA KAZI NA AJIRA: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kazi na Ajira kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MHE. JENISTA J. MHAGAMA - MWENYEKITI WA KAMATI YA MAENDELEO YA JAMII: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Maendeleo ya Jamii kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Kazi na Ajira kwa Mwaka 2010/2011 Pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MHE. REGIA E. MTEMA - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA KAZI NA AJIRA: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Kazi na Ajira kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MASWALI NA MAJIBU Na. 373 Kuboreshwa kwa Maslahi ya Madiwani MHE. FELISTER A. BURA aliuliza:- Madiwani ni nguzo muhimu katika kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi na nia ya Serikali ni kuboresha maslahi ya Madiwani iil waweze kutimiza wajibu wao ipasavyo;- Je, ni lini maslahi ya Madiwani yataboreshwa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri Mkuu, ninaomba kujibu swali la Mheshimiwa Felister Bura, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba, Waheshimiwa Madiwani ni nguzo muhimu katika kufuatilia utekelezaji wa Ilani ya Uchaguzi wa Chama cha Mapinduzi.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao Cha Arobaini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Arobaini na Sita – Tarehe 15 Juni, 2020 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae, tunaendelea na Mkutano wetu wa 19, Kikao cha 46, bado kimoja tu cha kesho. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na: NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2020 (The Finance Bill, 2020). Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha kwa Mwaka wa Fedha 2020/2021 (Monetary Policy Statement for the Financial Year 2020/2021). MHE. ALBERT N. OBAMA - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI:Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti Kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2020 (The Finance Bill, 2020). 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. RHODA E. KUNCHELA - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO: Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Muswada wa Sheria ya fedha wa mwaka 2020 (The Finance Bill, 2020). MHE. DKT. TULIA ACKSON - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KANUNI ZA BUNGE: Azimio la Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kanuni za Bunge kuhusu Marekebisho ya Kanuni za Bunge SPIKA: Asante sana Mheshimiwa Naibu Spika, Katibu MASWALI NA MAJIBU (Maswali yafuatayo yameulizwa na kujibiwa kwa njia ya mtandao) Na. 426 Migogoro ya Mipaka MHE.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Arobaini na Saba – Tarehe 15 Agosti, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MWENYEKITI WA KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa Mwaka wa Fedha 2010/2011 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MASWALI NA MAJIBU Na. 416 Makubaliano Kati ya Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki MHE. JOYCE J. MUKYA aliuliza:- Makubaliano kati ya Serikali ya Tanzania na Jumuiya ya Afrika Mashariki (Kifungu 3(a) yaliyosainiwa Mkoani Arusha tarehe 14 Machi, 1996 yanatambua hadhi ya Wafanyakazi wa Kitanzania katika ngazi za Executives na Professional Staff ya kupata haki zao za msingi ikiwemo ile ya kumiliki pasi za kusafiria za kidiplomasia (Diplomatic Passports),
    [Show full text]
  • Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 MAJADILIANO YA BUNGE
    Nakala ya Mtandao (Online Document) MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA ISHIRINI __________ Kikao cha Ishirini na Moja - Tarehe 5 Juni, 2015 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, napenda kuchukua nafasi hii kuwapa pole wote kwa msiba uliotupata, msiba ulitokea wakati nikiwa Geneva ambapo tulikuwa na kikao cha Kamati Ndogo ya maandalizi ya Mkutano Mkuu wa Maspika wote duniani utakaofanyika mwezi wa Nane, sasa kuna Maspika kumi ndiyo tupo kwenye maandalizi ya mkutano huo na kilikuwa ni kikao chetu cha mwisho kabla ya mkutano huo. Kwa hiyo, wakati msiba unatokea nilikuwa huko, nilipewa taarifa na nilisikitika sana. Kwa hiyo, tutatangaza baadaye mchana, ni akina nani watakaokwenda kuzika kesho. Katibu! HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI (MHE. CHARLES M. KITWANGA): Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016. NAIBU WAZIRI WA MAJI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Maji kwa mwaka wa Fedha, 2015/2016. MHE. DAVID H. MWAKYUSA (k.n.y. MHE. PROF. PETER M. MSOLLA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa Fedha 2015/2016. MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED (k.n.y. MHE. MAGDALENA H. SAKAYA - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA MAJI): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Fedha kwa Wizara ya Maji kwa Mwaka wa Fedha 2015/2016.
    [Show full text]
  • Tanzania Human Rights Report 2015 Tanzania Mainland Legal and Human Rights Centre (LHRC) Tanzania Human Rights Report 2015
    Tanzania Human Rights Report 2015 Tanzania Mainland Legal and Human Rights Centre (LHRC) Tanzania Human Rights Report 2015 Publishers Legal and Human Rights Centre Justice Lugakingira House, Kijitonyama P.O. Box 75254, Dar es Salaam, Tanzania Tel: +255222773038/48, Fax: +255222773037 Email: [email protected] Website: www.humanrights.or.tz Partners - LHRC Accountability in Tanzania (AcT) The Embassy of Norway The Embassy of Sweden ISBN: 978-9987-740-25-3 © LHRC 2016 - ii - Tanzania Human Rights Report 2015 Editorial Board Dr. Helen Kijo-Bisimba Adv. Imelda Urrio Ms. Felista Mauya Adv. Anna Henga Mr. Castor Kalemera Researchers/Writers Mr. Paul Mikongoti Mr. Pasience Mlowe Mr. Fundikila Wazambi Design & Layout Mr. Rodrick Maro - iii - Tanzania Human Rights Report 2015 Acknowledgement Legal and Human Rights Centre (LHRC) has been producing the Tanzania Human Rights Report, documenting the situation in Tanzania Mainland since 2002. In the preparation and production of this report LHRC receives both material and financial support from different players, such as the media, academic institutions, other CSOs, researchers and community members as well as development partners. These players have made it possible for LHRC to continue preparing the report due to its high demand. In preparing the Tanzania Human Rights Report 2015, LHRC received cooperation from the Judiciary, the Legislature and the Executive arms of the State. Various reports from different government departments and research findings have greatly contributed to the finalization of this report. Hansards and judicial decisions form the basis of arguments and observations made by the LHRC. The information was gathered through official correspondences with the relevant authorities, while other information was obtained online through various websites.
    [Show full text]