Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)

Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Arobaini na Mbili – Tarehe 9 Agosti, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatayo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2011/2010 MHE. WILLIAM A. MGIMWA - MWENYEKITI WA KAMATI YA VIWANDA NA BIASHARA: Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda na Biashara Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka 2010/2012 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MHE. GRACE S. KIWELU - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Viwanda na Biashara kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla hatujaendelea, naomba kulitaarifu Bunge kwamba Waziri Mkuu - Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda amesafiri kikazi kwenda Morogoro na inawezekana akarudi mchana wa leo. Kutokana hali hiyo, Mheshimiwa Waziri Mkuu ameelekeza kuwa Mheshimiwa Dkt. Mary Nagu - Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu (Uwekezaji na Uwezeshaji) atakaimu nafasi ya Mheshimiwa Waziri Mkuu hadi wakati huo. Ahsante. (Makofi) MASWALI NA MAJIBU Na. 383 Matatizo ya Maji Maji Kata ya Mbokomu MHE. SUSAN J. LYIMO aliuliza:- Liko tatizo sugu la maji kwenye Kata ya Mbokomu hususan kwenye Vijiji vya Korini Kusini na Juu Tema pamoja na Vitongoji vyake ambalo halijapatiwa ufumbuzi. (a) Je, ni lini tatizo hilo litatatuliwa? (b) Kwa sababu vyanzo vya maji havikidhi mahitaji ya wakazi wa maeneo hayo: Je, Serikali haioni haja ya kuwa na vyanzo mbadala vikiwemo vile vya maji ardhini? NAIBU WAZIRI WA MAJI alijibu:- 1 Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Susan Jerome Lyimo - Mbunge wa Viti Maalum lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, kama ilivyo kwa maeneo mengine ya nchi, Serikali inatekeleza programu ya Sekta ya Maendeleo ya Maji katika Halmashauri kupitia Mpango wa Maji Safi na Usafi wa Mazingira Vijijini. Katika mwaka 2010/2011 Halmashauri ya Wilaya ya Moshi iliidhinishiwa shilingi bilioni 2.2 kwa ajili ya utekelezaji wa mradi wa vijiji 12 ambavyo vimechagua kutumia teknolojia ya mserereko (Gravity Scheme) kutoka kwenye mito ya maji iliyopo. Kati ya fedha hizo, shilingi milioni 320.5 zimepokelewa na kazi zilizokwishafanyika ni usanifu wa miradi ya vijiji husika na uandaaji wa makabrasha ya zabuni ambapo taarifa ya kazi hiyo iliwasilishwa kwa Waziri wa Maji ili kupata ridhaa ya kutangaza zabuni. Utekelezaji wa mradi huu unafanyika kwa lot tatu ambapo awamu ya kwanza inahusisha vijiji vya Korini Kaskazini na Korini Kusini vilivyoko katika Kata ya Mbokomu. Mradi huu ukikamilika, utaondoa tatizo la maji katika Kata ya Mbokomu na maeneo mengine ndani ya Halmashauri. Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka 2011/2012, Halmashauri imetenga shilingi milioni 704.7 kupitia mpango wa Sekta ya Maji kwa ajili ya kuendelea na utekelezaji wa miradi ya maji katika vijiji hivyo 12 vilivyochaguliwa. Mheshimiwa Naibu Spika, miradi mingine inayotekelezwa ndani ya Halmashauri ni Kirua Kahe Water Supply ambapo ujenzi unatagemea kukamilika Desemba, 2011. Kutakuwa na extension tatu zitakazotekelezwa kuanzia Aprili, 2012. Katika mradi huu kuna makubaliano kati ya Halmashauri na Mhisani aitwaye KfW Shirika la Ujerumani ambalo litahisaini mradi huo kwa gharama ya shilingi bilioni 3.7. Mheshimiwa Naibu Spika, wananchi wa vijiji nilivyovitaja hapo juu walihamasishwa na kuelimishwa kuhusu uchangiaji wa ujenzi wa miradi ya maji na kuhusishwa kuchagua technolojia inayowafaa na watakayoweza kulipia gharama za uendeshaji ambapo vijiji vyote 12 vilichagua teknolojia ya serereko. Hivyo, kwa kutumia mbinu shirikishi, wananchi wenyewe wanapewa nafasi ya kuamua teknolojia inayowafaa kwa kuzingatia dhana au uchangiaji na huduma za maji katika jamii. Vyanzo vya maji vinavyotumika kwa sasa ni Mto Mrusunga na uwezo wa chanzo hiki ni lita 44 kwa sekunde. MHE. SUSAN A. J. LYIMO: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa tatizo hili ni la muda mrefu sana na hata Naibu Waziri wa kipindi kilichopita Mheshimiwa Chiza aliwahi kwenda miaka mitatu iliyopita na akaahidi tatizo hilo litakamilishwa, lakini mpaka leo bado na swali langu bado halijajibiwa kwa sababu nimeuliza ni lini tatizo hilo litapatiwa ufumbuzi? Kwa hiyo, nilikuwa nataka jibu la hilo. Pili, kwa kuwa mila na desturi za Wachaga ni pamoja na kufuga mifugo ya ndani, yaani hawatoi mifugo yao nje, na kwa maana hiyo, tatizo la maji ni kubwa sana, vile vile ikizingatiwa kwamba maeneo hayo kwa sasa hivi wazee wengi ndio wapo: Je, Mheshimiwa Naibu Waziri, haoni kwamba tatizo hilo ni kubwa sana na kwa hiyo, inabidi wawapatie maji hasa ikizingatiwa Mto Mrusunga ambao ni chanzo kikuu kwa sasa hivi hauna maji kabisa? (Makofi) NAIBU WAZIRI WA MAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza kabisa kama nilivyosema kwenye jibu la msingi, ni kwamba Halmashauri ya Moshi inatekeleza huu mradi kupitia program ya maji na imefikia hatua nzuri na mpaka sasa wameshatangaza tender ili kuweza kupata mkandarasi atakayeendelea kujenga katika awamu ya kwanza. Nimesema kwamba tuna bahati kwamba Shirika la Ujerumani limekubali kufadhili mradi huu kwa shilingi bilioni 3.7 na watafanya kwa awamu. Kwa hiyo, nina uhakika katika muda mpaka tufikie 2015 tatizo hili la maji litakuwa limekwisha. Maeneo mengine tutaendelea kuyapanua jinsi uwezo wa fedha utakavyokuwa unapatikana. Kuhusu Mto Mrugusunga ni kwamba maji ya mto ule yanatosha kwa kipindi cha masika. Lakini wakati wa kiangazi kuna tatizo la uharibifu wa mazingira, kwa hiyo, maji hupungua. Namwomba Mheshimiwa Lyimo asaidie pia kuhamasisha wananchi kuhifadhi mazingira ili tuwe na 2 maji endelevu na vyanzo vyetu vya maji viwe vinaweza kukidhi kwa muda wote wa mwaka mzima. (Makofi) Na. 384 Kupandishwa kwa Mipaka ya Wilaya MHE. DKT. ANTHONY G. MBASSA aliuliza:- Kulikuwa na suala la kupindishwa kwa mipaka ya Wilaya wakati Wilaya ya Chato ikimegwa toka Wilaya kongwe ya Biharamulo hususan katika Kijiji cha Nyantimba na taarifa za awali zilipelekwa TAMISEMI. Je, nini hatma ya suala hilo? WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Anthony Mbassa - Mbunge wa Biharamulo Magharibi kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2005 Serikali kupitia Tangazo Na. 337 ilitangaza kuundwa kwa Wilaya mpya ya Chato ambayo ilitokana na Wilaya mama ya Biharamulo. Mipaka ya Wilaya iliyowekwa ni ya asili kwa kutumia mito na milima. Aidha, tangazo hilo lilionyesha kuwa Kijiji cha Nyantimba ni kimoja na kipo katika Wilaya ya Biharamulo. Mheshimiwa Naibu Spika, mwaka 2009 Serikali ilitoa tangazo la Serikali Na. 205 lilitangaza orodha ya vijiji vilivyokuwa vimesajiliwa na kuonyesha kuwa Kijiji cha Nyantimba kipo katika Wilaya zote mbili za Biharamulo na Chato isipokuwa tofauti pekee ni kwamba Kijiji cha Nyantimba kwa upande wa Biharamulo kina vitongoji vinne na kwa upande wa Wilaya ya Chato kina vitongoji vitano. Mheshimiwa Naibu Spika, mkanganyiko huu unatokana na tofauti iliyopo kati ya mpaka wa Wilaya na mpaka wa Jimbo la Uchaguzi la Chato. Serikali ilipoweka mpaka wa Wilaya ya Biharamulo na Wilaya mpya ya Chato haikuzingatia mpaka wa Jimbo, hivyo kuna sehemu ya Jimbo la Uchaguzi la Chato ambayo ilibaki upande wa Biharamulo na ni sehemu hii ambapo Kijiji cha Nyantimba kinapatikana. Aidha, kuna makosa ya kiuchapaji ambayo yalifanyika katika matangazo ya Serikali ya kukitaja Kijiji cha Nyantimba kuwepo katika Wilaya zote mbili wakati siyo sahihi, kwani kipo kijiji kimoja tu cha Nyantimba. Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI, itawasilisha tena jambo hili kwa Tume ya Uchaguzi ili iweze kurekebisha mpaka wa Jimbo la Uchaguzi la Chato uendane na mpaka wa Wilaya ya Chato. Aidha, Serikali italifanyia pia marekebisho tangazo la Serikali Na. 205 ili kuondokana na kasoro zilizopo. MHE. DKT. ANTHONY G. MBASSA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa kuwa katika jibu la msingi Mheshimiwa Waziri ameonyesha kabisa kwamba Serikali imejichanganya na ilichapisha matangazo haya kimakosa:- (a) Je, Serikali haoni kwamba kipengele cha kwanza cha tangazo la Serikali Na. 337 lilikuwa sahihi kwa kupatia kijiji hiki Wilaya ya Biharamulo? (b) Kwa kuwa jopo la watalaam lilikaa na nyaraka zikaletwa TAMISEMI zikibainisha kabisa kijiji hiki kinapaswa kuwa Wilaya ya Biharamulo na siyo Chato: Je, haoni kwamba sasa ni wakati muafaka wa kupitia nyaraka na kutoa tamko katika Bunge hili kwamba kijiji hiki kinapaswa kirudi Biharamulo na siyo Chato? 3 WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Mheshimiwa Naibu Waziri, kwa niaba ya Waziri Mkuu, napenda kujibu maswali ya Mheshimiwa Mbunge kama ifuatavyo:- Kama nilivyosema kwenye jibu la msingi kwamba GN hizi zote karibuni zimechanganya. GN 337 yenyewe inagawa Wilaya ya Chato na Wilaya ya Biharamulo hiyo ni Wilaya. GN 205 imegawa Vijiji na Kata. Napo hapo kuna mchanganyiko. GN 190 ambayo imetaja Halmashauri ya Wilaya ya Chato Kijiji cha Nyantimba kiko katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato. Sasa kwa kuwa nyaraka zote hizi ziko TAMISEMI na kwa kuwa Kijiji cha Nyantimba sasa hivi kinapata huduma zote kutoka Chato, ni vyema na ni busara tukapitia zile nyaraka zote, lakini tukarudia pia kwa wananchi kuwauliza kwamba ni vyema wachague

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    124 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us