Tarehe 3 Julai, 2017

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Tarehe 3 Julai, 2017 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Hamsini na Nane – Tarehe 3 Julai, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae, Katibu! NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI: Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Maelezo ya Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Mamlaka na Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Bill, 2017] Maelezo ya Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources Contracts (Review and Re-negotiation of Unconscionable Terms) Bill, 2017] 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. ESTER M. MMASI – (K.n.y. MHE. DOTTO M. BITEKO - MWENYEKITI WA KAMATI YA PAMOJA): Maoni ya Kamati ya Pamoja kuhusu Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources Contracts (Review and Re-negotiation of unconscionable Terms) Bill, 2017]. Maoni ya Kamati ya Pamoja kuhusu Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Bill, 2017). MHE. DAVID E. SILINDE – MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA: Maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Bill, 2017]. Maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwa Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources Contracts (review and Re-negotiation of Unconscionable Terms) Bill, 2017]. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Katibu! NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: 2 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MASWALI NA MAJIBU Na. 478 Mradi wa Maji Chankolongo – Geita MHE. LOLESIA J. M. BUKWIMBA aliuliza:- Je, ni lini mradi wa maji wa Chankolongo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita utakamilika? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lolesia Jeremia Maselle Bukwimba, Mbunge wa Busanda, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Geita ilianza kutekeleza mradi mpya wa maji wa Chankolongo mwaka 2014/2014 ukiwa ni mojawapo ya miradi ya vijiji 10 kwa kufanya usanifu upya na kusaini mikataba ya ujenzi mwezi Machi, 2014 wenye thamani ya shilingi bilioni 4.39 baada ya mradi wa awali wa Nyakagomba kushindikana hadi kuchakaa kwa miundombinu yake. Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi unalenga kutumia chanzo cha Ziwa victoria na utahudumia vijiji vinne vya Chankolongo, Chikobe, Chigunga na Kabugozo vyenye wakazi wapatao 24,724. Kazi yote ina mikataba sita iliyoandaliwa na kusimamiwa na COWI (T) Consulting Engineers and Planners kwa kushirikiana na Association with Environmental Consult Limited. kama Mtaalam Mshauri. Malipo yaliofanyika hdi ssa ni kiasi cha shilingi bilioni 1.99 ambayo ni sawa na asilimia 45.3 ya gharama ya mradi, ambapo utekelezaji umefikia asilimia 50. Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu ulikumbwa na changamoto kutokana na uwezo mdogo wa mkandasi (Fare 3 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Tanzania Limited) aliyekuwa akijenga choteo na kusambaza mabomba. Hata hivyo, Halmashauri ya Wilaya ya Geita imesukuma utekelezaji wa mradi huu ambapo mkandarasi (Fare Tanzania Limited) ameingia makubaliano (sub contract) na kampuni nyingine iitwayo Katoma Motor Factors Limited ambayo inaleta mabomba yote ya mradi pamoja na pampu ndani ya mwezi huu wa Julai 2017. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hali ya sasa mradi huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba, 2017. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lolesia Bukwimba, swali la nyongeza. MHE. LOLESIA J. M. BUKWIMBA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu kwa kunipa nafasi niuliza maswali mawili ya nyongeza. Kutokana na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri ni kweli kwamba changamoto bado ni kubwa sana katika Mradi huu wa Chankolongo. Pia kutokana na majibu yake na yeye mwenyewe amewahi kufika kwenye huo mradi, mradi huu ni wa muda mrefu sana kiasi kwamba wananchi mpaka sasa hawaelewi kinachoendelea juu ya mradi huu. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ningependa pia Mheshimiwa Waziri awahakikishie wananchi kwamba, je, ni kweli mwezi Desemba mwaka 2017 mradi huu utakamilika kutokana na changamoto zilizopo? Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa mradi huu unakusudia kuvuta maji kutoka Ziwa Victoria na ndani ya Jimbo la Busanda wananchi wana tatizo kubwa sana la maji na maji mengi yanayotumika kwa ajili ya uchenjuaji wa dhahabu ni machafu na wananchi wanapenda kupata maji safai na salama; je, mradi huu utawezesha kufikisha maji na katika Jimbo zima la Busanda? Napenda kupata majibu hayo. Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. 4 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli mimi na yeye Mbunge tulikwenda jimboni kwake ili kuukagua mradi huu na ni kweli mradi huu tumeukuta una changamoto nyingi sana na ndiyo maana kwa hatua tulizozifanya pale na kutoa maelekezo nilipofika site mpaka Engineer pale pamoja na Afisa Manunuzi amesimamishwa majukumu kutokana na mradi huu, kwa hiyo hatukulala kwenye mradi huu. Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, miezi michache iliyopita tulitoa maagizo kwamba choteo liweze kukamilika na mabomba yaweze kupatika. Kwa taarifa nilizozipata juzi ni kwamba lile choteo limekamilika maji yanatoka katika ziwa mpaka yanafika pale katika intake yenyewe, lakini usambaji wa mabomba umekuwa ukisua sua. Ndiyo maana Halmashauri ilivyosukuma, huyu sasa ameingia na hii kampuni nyingine ya Katoma Motor Factors Limited ambayo imefanya commitment ya kuleta mabomba yote bila hata ya kulipwa hata senti tano. Kwa hiyo mabomba yatafikishwa site ndani ya mwezi huu wa saba. Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa nilizozipata ni kwamba tayari mabomba haya yapo ndani ya meli na kwamba muda wowote yatafika hapa site. Kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge naomba nikuhakikishie kwamba kwa jinsi nilivyoongea na watendaji katika Halmashauri ya Geita ni kwamba tutasukuma ndani ya mwezi wa 12 mradi huu uweze kukamilika. Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu agenda ya pili, kwamba mradi huu ikiwezekana ufike kwenye maeneo mengine; wazo ni jema lakini naona kwanza jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba mradi huu unaweza kukamilika katika vile vijiji vya awali. Jambo hili likishakamilika hapa tutaweka mipango mingine ya namna ya kufanya; kwa 5 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) sababu chanzo hiki ni kikubwa sana ili kiweze kusaidia wananchi wa Busanda waweze kupata maji kama Mbunge wao anavyohangaika siku zote. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa David Silinde, swali la nyongeza. MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa kuwa tatizo la maji nchini ni kubwa na Tanzania ni moja ya nchi ambayo tuna sifa ya kuwa na Maziwa makubwa pamoja na mito mingi; yaani ni nchi ya Maziwa Makuu tofauti na zile nchi za kwenye jangwa kule kama Libya ambao wana maji zaidi ya asilimia 80. Sasa ni kwa nini Serikali isione aibu ya kushindwa kutatua hili tatizo kwa muda mrefu ilhali tuna maji mengi? Sasa hivi ukiangalia moja ya sifa ya nchi yetu ambayo tumekuwa tukijitamba na Serikali mmekuwa mkijisifu kwamba mmekuwa mkikusanya mapato mengi. Ni kwa nini sasa… NAIBU SPIKA: Mheshimiwa umeshauliza swali la kwanza umesema kwa nini Serikali isione aibu, ulishamaliza hilo swali, hilo ni la pili na hili ni la nyongeza. Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji majibu. NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imejitahidi, kila mwaka inatenga fedha na inazipeleka kwenye Halmashauri. Ni kazi ya Halmashauri kuhakikisha inatumia hiyo hela kuwapatia wananchi maji. Mheshimiwa Naibu Spika, nimeandaa kitabu kinachoonesha bajeti iliyotengwa katika Halmashauri na kiasi cha fedha ambacho Halmashauri imetumia. Halmashauri nyingi zimeshindwa kutumia fedha zilizotengwa kwenye bajeti. Sasa lawama hii iende kwa nani wakati sisi wenyewe ni Madiwani kwenye hizo Halmashauri? 6 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba nchi yetu ina maji ya kutosha kilichobaki ni kuweka fedha na kusambaza na Serikali inaendelea kuweka fedha. Imeweka fedha mwaka uliopita na mwaka huu fedha tayari ipo kwa ajili ya Halmashauri kuhakikisha kwamba mnatumia zile fedha kuwapa wananchi maji na Wizara ya Maji na Umwagiliaji imeshatoa maelekezo ya jinsi ya kufanya. Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niwaambie Waheshimiwa Wabunge Halmashauri yangu tayari imeshatengeneza mpango kazi leo tarehe 3 Julai, hebu jiulize wewe kwenye Halmashauri yako kwenye bajeti mpya je, mpango kazi umeshaanza kufanya? Ndugu zangu naomba sana bajeti ipo tusimamie Halmashauri waweze kutekeleza miradi ya maji hakuna haja ya kulaumiana. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zacharia Issaay, swali la nyongeza. MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji, hivi sasa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu katika majimbo yote mawili tulikuwa na mradi
Recommended publications
  • Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI NA SABA YATOKANAYO NA KIKAO CHA NNE (DAILY SUMMARY RECORD OF PROCEEDINGS) 7 NOVEMBA, 2014 MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI NA SABA KIKAO CHA NNE – 7 NOVEMBA, 2014 Kikao kilianza saa 3:00 Asubuhi kikiongozwa na Mhe. Job Y. Ndigai, Mb Naibu Spika ambaye alisoma Dua. MAKATIBU MEZANI 1. Ndg. Charles Mloka 2. Ndg. Lina Kitosi 3. Ndg. Hellen Mbeba I. MASWALI YA KAWAIDA Maswali yafuatayo yaliulizwa na wabunge na kupitia majibu Bungeni:- 1. Ofisi ya Waziri Mkuu – swali na. 38 la Mhe. Anne Kilango 2. Ofisi ya Waziri Mkuu – swali na. 39 la Mhe. Salum Khalfan Barwary 3. Ofisi ya Waziri Mkuu – swali na. 40 la Mhe. Moses Joseph Machali 4. Wizara ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi – swali na. 41. La Mhe. Omar Rashid Nundu 5. Wizara ya Maendeleo ya Mifungo na Uvuvi – swali na. 42. La Mhe. Hilda Ngoye 6. Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi – swali na. 43. La Mhe. Zitto Kabwe Zuberi 7. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Tecknolojia – swali na. 44 –la Mhe. Murtaza Mangungu 8. Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia - swali na. 45-la Mhe. Godfrey Mgimwa 9. Wizara ya Katiba na Sheria - swali na. 46 – la Mhe. Neema Mgaya Hamid 2 10. Wizara ya Katiba na Sheria- swali na. 47 – la Mhe. Assumpter Mshana 11. Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo – swali na. 48 la Mhe. Khatib Said Hji. 12. Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo - swali na. 49 la Mhe.
    [Show full text]
  • Madini News Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Toleo Na.2 Wa Tanzania Machi, 2020 HALIUZWI
    Toleo Na.2 // Machi 2020 Yaliyomo // Biteko - Nitasimama na Mzee Tume ya Leseni ya TanzaniteOne Imefutwa na Kisangani mpaka “asimame” Kurudishwa Serikalini - Biteko... Uk.04 ... Uk.08 Madini Bilioni 66.5 zapatikana tangu Wanawake Tume ya Madini kuanzishwa kwa masoko Wawakumbuka ya madini ... Uk.10 Yatima ... Uk.18 www.tumemadini.go.tz Tume ya Madini 2020 www.tumemadini.go.tz /TAHARIRI Salamu Kutoka kwa Waziri wa Madini Maoni ya Mhariri SEKTA YA MADINI INAIMARIKA, MAFANIKIO MASOKO TUENDELEZE USHIRIKIANO YA MADINI TUMEWEZA! Katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Wizara ya Madini ilipanga kutekeleza majukumu yake kupitia miradi Katika kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mbalimbali ikilenga katika kuimarisha Sekta ya Madini, hivyo kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa Taifa, Serikali kupitia uchumi wa nchi. Tume ya Madini kuanzia Machi, 2019 ilifungua masoko ya madini Katika Toleo lililopita nilielezea kwa kifupi kuhusu yale ambayo yamesimamiwa na kutekelezwa na Wizara na vituo vya ununuzi wa madini lengo likiwa ni kudhibiti utorosh- kwa kipindi cha takribani miaka miwili tangu kuanzishwa kwake. waji wa madini kwa kuwapatia wachimbaji wa madini nchini Katika Toleo hili nitaelezea kwa kifupi mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kipindi cha sehemu ya kuuzia madini yao huku wakilipa kodi mbalimbali kuanzia Julai, 2019 hadi Februari, 2020. Kama ambavyo nilieleza Bungeni katika Hotuba yangu wakati Serikalini. nikiwasilisha Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2019/2020, nilieleza kuwa, Wizara imepangiwa kukusanya Shilingi 470,897,011,000.00 katika Mwaka wa Fedha 2019/2020. Uanzishwaji wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa Napenda kuwataarifu wasomaji wa Jarida hili kuwa, hadi kufikia Februari, 2020 jumla ya Shilingi madini ni sehemu ya maelekezo yaliyotolewa kwenye mkutano wa 319,025,339,704.73 zimekusanywa ambazo ni sawa na asilimia 102 ya lengo la makusanyo ya nusu mwaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania, Dkt.
    [Show full text]
  • Online Document)
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Sita – Tarehe 4 Februari, 2020 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa tukae. Katibu tunaendelea Waheshimiwa Wabunge na Mkutano wetu wa Kumi na Nane, kikao cha leo ni kikao cha tano, Katibu NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati Zifuatazi Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Matoleo ya Gazeti la Serikali pamoja na Nyongeza zake yaliyochapishwa tangu Mkutano wa Bunge uliopita kama ifuatavyo:- (i) Toleo Namba 46 la tarehe 8 Novemba, 2019 (ii) Toleo Namba 47 la tarehe 15 Novemba, 2019 (iii) Toleo Namba 48 la tarehe 22 Novemba, 2019 (iv) Toleo Namba 49 la tarehe 29 Novemba, 2019 (v) Toleo Namba 51 la tarehe 13 Desemba, 2019 (vi) Toleo Namba 52 la tarehe 20 Desemba, 2019 (vii) Toleo Namba 53 la tarehe 27 Desemba, 2019 (viii) Toleo Namba 1 la tarehe 3 Januari, 2020 (ix) Toleo Namba 2 la terehe 10 Januari, 2020 (x) Toleo Namba 3 la tarehe 17 Januari, 2020 (xi) Toleo Namba 4 la terehe 24 Januari, 2020 MHE. JASSON S. RWEIKIZA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za MItaa kuhuus shughuli za Kamati hii kwa Mwaka 2019. MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE KATIBA NA SHERIA: Taarifa ya Kmaati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu shughuli zilizotekelezwa na Kamati hiyo kwa kipindi cha kuanzia Februari, 2019 hadi Januari, 2020.
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao Cha Thelathini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini na Sita – Tarehe 27 Mei, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nawaomba tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa 15, leo ni Kikao cha 36. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2019/2020. NAIBU WAZIRI WA MADINI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. CATHERINE V. MAGIGE - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI) Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini Kuhusu utekelezaji na Majukumu ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MHE. TUNZA I. MALAPO - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU WIZARA YA MADINI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni juu ya Wizara ya Madini kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Tunza Malapo, tunakushukuru. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na TAMISEMI, swali la kwanza litaulizwa na Mheshimiwa Azza Hilal, Mbunge wa Viti Maalum - Shinyanga.
    [Show full text]
  • Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Bunge La Tanzania Mkutano Wa Tatu Yatokanayo Na Kikao Cha Arobaini Na Saba 21 Juni, 2016
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA TATU YATOKANAYO NA KIKAO CHA AROBAINI NA SABA 21 JUNI, 2016 MKUTANO WA TATU - YATOKANAYO NA KIKAO CHA AROBAINI NA SABA TAREHE 21 JUNI, 2016 I. DUA: Saa 3.00 Asubuhi Naibu Spika (Mhe. Dkt.Tulia Ackson) alisoma Dua na Kuongoza Bunge. Makatibu Mezani: 1. Ndg. Theonest Ruhilabake 2. Ndg. Zainab Issa Wabunge wa Kambi ya Upinzani walitoka nje ya ukumbi wa Bunge baada ya dua kusomwa na Mhe. Naibu Spika. II. MASWALI: Maswali yafuatayo yaliulizwa na Waheshimiwa Wabunge na kujibiwa na Serikali:- OFISI YA WAZIRI MKUU: Swali Na.399 – Mhe. Raphael Masunga Chegeni [kny. Mhe. Salome Makamba] Swali la nyongeza: (i) Mhe. Raphael Masunga Chegeni (ii) Mhe. Abdallah Hamisi Ulega (iii) Mhe. Joseph Kasheku Musukuma (iv) Mhe. Mariam Nassoro Kisangi OFISI YA RAIS (TAMISEMI): Swali Na.400 Mhe. Oran Manase Njeza Swali la nyongeza: (i) Mhe. Oran Manase Njeza (ii) Mhe. Desderius John Mipata (iii) Mhe. Goodluck Asaph Mlinga Swali Na.401 – Mhe. Boniventura Destery Kiswaga Swali la nyongeza: (i) Mhe. Boniventura Destery Kiswaga (ii) Mhe. Augustino Manyanda Maselle (iii) Mhe. Richard Mganga Ndassa (iv) Mhe. Dkt. Dalali Peter Kafumu Swali Na. 402 – Mhe. Fredy Atupele Mwakibete Swali la Nyongeza: (i) Mhe. Fredy Atupele Mwakibete (ii) Mhe. Njalu Daudi Silanga (iii) Mhe. Halima Abdallah Bulembo (iv) Mhe. Azza Hilal Hamad 2 WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Swali Na.403 – Mhe Joseph Kakunda. kny Mhe. Ally Saleh Ally Swali la nyongeza: (i) Mhe. Joseph George Kakunda (ii) Mhe. Mussa Azzan Zungu (iii) Mhe. Cosato David Chumi (iv) Mhe.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA SABA Kikao Cha Ishirini Na Tano – Tarehe 15
    NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Ishirini na Tano – Tarehe 15 Mei, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu! NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. MWENYEKITI: Ahsante. Katibu. NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI: Maswali. 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MASWALI NA MAJIBU Na. 200 Mgongano wa Kiutendaji – Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma MHE. LEONIDAS T. GAMA aliuliza:- Wananchi wa Songea Mjini wamekuwa wakiitumia Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kama Hospitali yao ya Wilaya hivyo kufanya kuwepo na mgongano wa kiutendaji kati ya Mamlaka ya Mkoa inayoitambua Hospitali hiyo kama Rufaa ya ngazi ya Mkoa na Mamlaka ya Wilaya. Tarehe 10 Januari, 2016, Mheshimiwa Waziri wa Afya alifika kuona hali halisi na juhudi za wananchi wa Songea Mjini za kujenga Kituo cha Afya Mji Mwema ambacho kimefikia hatua kubwa, hivyo wakamwomba Waziri kituo hicho kipandishwe hadhi kuwa Hospitali ya Wilaya, Songea Mjini. (a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuiacha Hospitali ya Mkoa ifanye kazi ya Rufaa Kimkoa? (b) Je, Serikali haioni haja ya kupunguza msongamano katika hospitali hiyo kwa kuanzisha Hospitali ya Wilaya Songea Mjini? (c) Je, ni lini basi Serikali
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Kumi Na Tisa – Tarehe 29 Aprili, 2021
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Kumi na Tisa – Tarehe 29 Aprili, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa, tukae. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU WAZIRI WA MADINI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. SAADA MONSOUR HUSSEIN - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa maswali, tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Simon Songe Lusengekile, Mbunge wa Busega, sasa aulize swali lake. Na. 158 Serikali Kukamilisha Ujenzi wa Zahanati – Busega MHE. SIMON S. LUSENGEKILE aliuliza:- Wananchi wa Kata ya Imalamate Wilayani Busega wamejenga zahanati na kumaliza maboma manne kwa maana ya zahanati moja kila kijiji:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wananchi hao kuezeka maboma hayo ili waweze kupata huduma za afya kwenye zahanati hizo? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Thelathini
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Thelathini na Tano - Tarehe 2 Juni, 2016 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua (Hapa Waheshimiwa Wabunge wa Kambi ya Upinzani Walitoka Nje) NAIBU SPIKA: Tukae, Katibu. MBUNGE FULANI: Hamna posho ninyi. NAIBU SPIKA: Katibu. NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU MEZANI: Maswali. MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Aida Joseph Khenani, Mbunge wa Viti Maalum swali lake litaulizwa na Mheshimiwa Ally Keissy. Na. 284 Unyanyasaji Unaofanywa na Mgambo/Askari Kwa Wafanyabiashara Wadogo Wadogo MHE. ALLY K. MOHAMED (K.n.y. MHE. AIDA J. KHENANI) aliuliza:- Kumekuwa na hali ya ukiukwaji wa haki za binadamu unaofanywa na mgambo na askari polisi wanapotekeleza maagizo ya Serikali dhidi ya 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) wafanyabiashara wadogo wadogo hususan mama lishe, bodaboda pamoja na machinga. Je, Serikali inatoa tamko gani juu ya hali hiyo? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Aida Joseph Khenani, Mbunge wa Viti Maalum kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, mgambo wanafanya kazi kwa mujibu wa sheria ya polisi wasaidizi ya mwaka 1969 kwa kuzingatia sheria hiyo, Halmashauri zimeruhusiwa kuajiri askari ngambo kwa ajili ya kusaidia usimamizi wa Sheria Ndogondogo za Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji na Wilaya. Mheshimiwa Naibu Spika, askari mgambo anayefanya kazi katika Halmashauri anawajibika kuzingatia sheria za nchi pamoja na sheria ndogo ndogo zilizotungwa na Halmashauri.
    [Show full text]
  • Tarehe 4 Aprili, 2019
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Tatu – Tarehe 4 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Leo ni kikao cha tatu cha Mkutano wetu wa Kumi na Tano. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, AJIRA, KAZI VIJANA NA WAZEE NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA: Taarifa 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. HASNA S.K. MWILIMA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mfuko wa Bunge kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mfuko huo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MHE. DKT. JASMINE T. BUNGA - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Tume ya Uratibu na Udhibiti wa UKIMWI) kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 2 AGOSTI, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba mzime vipasa sauti vyenu maana naona vinaingiliana. Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri, tunaingia hatua inayofuata. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Leo ni siku ya Alhamisi lakini tulishatoa taarifa kwamba Waziri Mkuu yuko safarini kwa hiyo kama kawaida hatutakuwa na kipindi cha maswali hayo. Maswali ya kawaida yapo machache na atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Vita R. M. Kawawa. Na. 310 Fedha za Uendeshaji Shule za Msingi MHE. VITA R. M. KAWAWA aliuliza:- Kumekuwa na makato ya fedha za uendeshaji wa Shule za Msingi - Capitation bila taarifa hali inayofanya Walimu kuwa na hali ngumu ya uendeshaji wa shule hizo. Je, Serikali ina mipango gani ya kuhakikisha kuwa, fedha za Capitation zinatoloewa kama ilivyotarajiwa ili kupunguza matatizo wanayopata wazazi wa wanafunzi kwa kuchangia gharama za uendeshaji shule? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) imepanga kila mwanafunzi wa Shule ya Msingi kupata shilingi 10,000 kama fedha za uendeshaji wa shule (Capitation Grant) kwa mwaka.
    [Show full text]
  • Tarehe 4 Mei, 2021
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Ishirini na Mbili – Tarehe 4 Mei, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Tunaendelea na Mkutano wetu wa Tatu, leo ni Kikao cha Ishirini na mbili. Katibu! NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 2021/2022. MHE. HUSNA J. SEKIBOKO - K.n.y. MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI A KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa mwaka wa fedha 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. SPIKA: Ahsante sana, Mheshimiwa Husna Sekiboko kwa niaba ya Kamati. Katibu! NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Swali letu la kwanza leo tunaanza na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, swali hilo litaulizwa na Mheshimiwa Hassan Selemani Mtenga Mbunge wa Mtwara Mjini. Mheshimiwa Mtenga tafadhali uliza swali lako. Na. 179 Kujenga Barabara za Lami-Kata za Manispaa ya Mtwara Mikindani MHE. HASSAN S. MTENGA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kujenga barabara za lami katika Kata za Ufukoni, Magomeni na shangani Manispaa ya Mtwara Mikindani.
    [Show full text]
  • Muhtasari Juu Ya Biashara Na Haki Za Binadamu Tanzania Robo Tatu Ya Mwaka: Julai – Septemba 2020
    photo courtesy of Governance Links MUHTASARI JUU YA BIASHARA NA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA ROBO TATU YA MWAKA: JULAI – SEPTEMBA 2020 Tangu aingie madarakani mwaka 2005, Rais Magufuli ametilia mkazo kwenye maendeleo ya miundom- binu kama jambo muhimu katika kufikia malengo ya viwanda na maendeleo ya Tanzania. Ma- tokeo yake, miradi mingi ya miundombinu mikubwa imekuwa ikiendelea nchini, kuanzia miundombinu ya barabara, ukarabati wa mifumo ya reli na viwanja vya ndege nchini, na kuongeza na kuwa na aina nyingi ya nishati nchini kupitia mitambo ya gesi asilia na umeme wa maji, kwa kutaja tu kwa uchache. Wakati miradi ya miundombinu inaongeza mapato, ajira, ukuaji wa uchumi na, hivyo, maendeleo chanya, upanuzi wa haraka wa sekta unaweza pia kuleta athari hasi kwa jamii na mazingira ambamo miradi inatekelezwa. Mwaka 2017, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG), ilidokeza uhitaji wa ku- zingatia haki za binadamu kwenye sekta ya ujenzi inayokua kwa kasi nchini (Kumb. E.1). Mwezi Machi 2020, zaidi ya wadau 60 kutoka kwenye biashara, asasi za kiraia na serikali walihimiza kuweka kipaumbele katika sekta ya miundombinu ili kukuza heshima ya haki za binadamu nchini Tanzania (Kumb. E2). Matokeo mapya juu ya athari za miradi mikubwa ya miundombinu kwa haki za binadamu yanawasili- shwa kupitia chunguzi kifani mpya tano juu ya “Sauti za Watanzania”. Tafiti hizi zilitathmini athari za miradi mitatu ya usambazaji wa nishati: Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (mkoa wa Manyara; Kumb. E3), Mradi wa Umeme wa Maji wa Maporomoko ya Rusumo (mkoa wa Kagera; Kumb. E4) na miradi ya usambazaji wa nishati vijijini (mkoa wa Mwanza; Kumb.
    [Show full text]