NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Hamsini na Nane – Tarehe 3 Julai, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae, Katibu! NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI: Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Maelezo ya Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Mamlaka na Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Bill, 2017] Maelezo ya Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources Contracts (Review and Re-negotiation of Unconscionable Terms) Bill, 2017] 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. ESTER M. MMASI – (K.n.y. MHE. DOTTO M. BITEKO - MWENYEKITI WA KAMATI YA PAMOJA): Maoni ya Kamati ya Pamoja kuhusu Muswada wa Sheria ya Mapitio na Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources Contracts (Review and Re-negotiation of unconscionable Terms) Bill, 2017]. Maoni ya Kamati ya Pamoja kuhusu Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017 (The Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Bill, 2017). MHE. DAVID E. SILINDE – MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA: Maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Mamlaka ya Nchi kuhusiana na Umiliki wa Maliasili wa Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources (Permanent Sovereignty) Bill, 2017]. Maoni ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani kwa Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Mapitio ya Majadiliano kuhusu Masharti Hasi katika Mikataba ya Maliasili za Nchi Mwaka 2017 [The Natural Wealth and Resources Contracts (review and Re-negotiation of Unconscionable Terms) Bill, 2017]. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Katibu! NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: 2 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MASWALI NA MAJIBU Na. 478 Mradi wa Maji Chankolongo – Geita MHE. LOLESIA J. M. BUKWIMBA aliuliza:- Je, ni lini mradi wa maji wa Chankolongo katika Halmashauri ya Wilaya ya Geita utakamilika? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lolesia Jeremia Maselle Bukwimba, Mbunge wa Busanda, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Geita ilianza kutekeleza mradi mpya wa maji wa Chankolongo mwaka 2014/2014 ukiwa ni mojawapo ya miradi ya vijiji 10 kwa kufanya usanifu upya na kusaini mikataba ya ujenzi mwezi Machi, 2014 wenye thamani ya shilingi bilioni 4.39 baada ya mradi wa awali wa Nyakagomba kushindikana hadi kuchakaa kwa miundombinu yake. Mheshimiwa Naibu Spika, Mradi unalenga kutumia chanzo cha Ziwa victoria na utahudumia vijiji vinne vya Chankolongo, Chikobe, Chigunga na Kabugozo vyenye wakazi wapatao 24,724. Kazi yote ina mikataba sita iliyoandaliwa na kusimamiwa na COWI (T) Consulting Engineers and Planners kwa kushirikiana na Association with Environmental Consult Limited. kama Mtaalam Mshauri. Malipo yaliofanyika hdi ssa ni kiasi cha shilingi bilioni 1.99 ambayo ni sawa na asilimia 45.3 ya gharama ya mradi, ambapo utekelezaji umefikia asilimia 50. Mheshimiwa Naibu Spika, mradi huu ulikumbwa na changamoto kutokana na uwezo mdogo wa mkandasi (Fare 3 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Tanzania Limited) aliyekuwa akijenga choteo na kusambaza mabomba. Hata hivyo, Halmashauri ya Wilaya ya Geita imesukuma utekelezaji wa mradi huu ambapo mkandarasi (Fare Tanzania Limited) ameingia makubaliano (sub contract) na kampuni nyingine iitwayo Katoma Motor Factors Limited ambayo inaleta mabomba yote ya mradi pamoja na pampu ndani ya mwezi huu wa Julai 2017. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hali ya sasa mradi huu unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi Desemba, 2017. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Lolesia Bukwimba, swali la nyongeza. MHE. LOLESIA J. M. BUKWIMBA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu kwa kunipa nafasi niuliza maswali mawili ya nyongeza. Kutokana na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri ni kweli kwamba changamoto bado ni kubwa sana katika Mradi huu wa Chankolongo. Pia kutokana na majibu yake na yeye mwenyewe amewahi kufika kwenye huo mradi, mradi huu ni wa muda mrefu sana kiasi kwamba wananchi mpaka sasa hawaelewi kinachoendelea juu ya mradi huu. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, ningependa pia Mheshimiwa Waziri awahakikishie wananchi kwamba, je, ni kweli mwezi Desemba mwaka 2017 mradi huu utakamilika kutokana na changamoto zilizopo? Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa mradi huu unakusudia kuvuta maji kutoka Ziwa Victoria na ndani ya Jimbo la Busanda wananchi wana tatizo kubwa sana la maji na maji mengi yanayotumika kwa ajili ya uchenjuaji wa dhahabu ni machafu na wananchi wanapenda kupata maji safai na salama; je, mradi huu utawezesha kufikisha maji na katika Jimbo zima la Busanda? Napenda kupata majibu hayo. Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante. 4 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli mimi na yeye Mbunge tulikwenda jimboni kwake ili kuukagua mradi huu na ni kweli mradi huu tumeukuta una changamoto nyingi sana na ndiyo maana kwa hatua tulizozifanya pale na kutoa maelekezo nilipofika site mpaka Engineer pale pamoja na Afisa Manunuzi amesimamishwa majukumu kutokana na mradi huu, kwa hiyo hatukulala kwenye mradi huu. Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, miezi michache iliyopita tulitoa maagizo kwamba choteo liweze kukamilika na mabomba yaweze kupatika. Kwa taarifa nilizozipata juzi ni kwamba lile choteo limekamilika maji yanatoka katika ziwa mpaka yanafika pale katika intake yenyewe, lakini usambaji wa mabomba umekuwa ukisua sua. Ndiyo maana Halmashauri ilivyosukuma, huyu sasa ameingia na hii kampuni nyingine ya Katoma Motor Factors Limited ambayo imefanya commitment ya kuleta mabomba yote bila hata ya kulipwa hata senti tano. Kwa hiyo mabomba yatafikishwa site ndani ya mwezi huu wa saba. Mheshimiwa Naibu Spika, taarifa nilizozipata ni kwamba tayari mabomba haya yapo ndani ya meli na kwamba muda wowote yatafika hapa site. Kwa hiyo Mheshimiwa Mbunge naomba nikuhakikishie kwamba kwa jinsi nilivyoongea na watendaji katika Halmashauri ya Geita ni kwamba tutasukuma ndani ya mwezi wa 12 mradi huu uweze kukamilika. Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu agenda ya pili, kwamba mradi huu ikiwezekana ufike kwenye maeneo mengine; wazo ni jema lakini naona kwanza jambo la msingi ni kuhakikisha kwamba mradi huu unaweza kukamilika katika vile vijiji vya awali. Jambo hili likishakamilika hapa tutaweka mipango mingine ya namna ya kufanya; kwa 5 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) sababu chanzo hiki ni kikubwa sana ili kiweze kusaidia wananchi wa Busanda waweze kupata maji kama Mbunge wao anavyohangaika siku zote. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa David Silinde, swali la nyongeza. MHE. DAVID E. SILINDE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwa kuwa tatizo la maji nchini ni kubwa na Tanzania ni moja ya nchi ambayo tuna sifa ya kuwa na Maziwa makubwa pamoja na mito mingi; yaani ni nchi ya Maziwa Makuu tofauti na zile nchi za kwenye jangwa kule kama Libya ambao wana maji zaidi ya asilimia 80. Sasa ni kwa nini Serikali isione aibu ya kushindwa kutatua hili tatizo kwa muda mrefu ilhali tuna maji mengi? Sasa hivi ukiangalia moja ya sifa ya nchi yetu ambayo tumekuwa tukijitamba na Serikali mmekuwa mkijisifu kwamba mmekuwa mkikusanya mapato mengi. Ni kwa nini sasa… NAIBU SPIKA: Mheshimiwa umeshauliza swali la kwanza umesema kwa nini Serikali isione aibu, ulishamaliza hilo swali, hilo ni la pili na hili ni la nyongeza. Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji na Umwagiliaji majibu. NAIBU WAZIRI WA MAJI NA UMWAGILIAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imejitahidi, kila mwaka inatenga fedha na inazipeleka kwenye Halmashauri. Ni kazi ya Halmashauri kuhakikisha inatumia hiyo hela kuwapatia wananchi maji. Mheshimiwa Naibu Spika, nimeandaa kitabu kinachoonesha bajeti iliyotengwa katika Halmashauri na kiasi cha fedha ambacho Halmashauri imetumia. Halmashauri nyingi zimeshindwa kutumia fedha zilizotengwa kwenye bajeti. Sasa lawama hii iende kwa nani wakati sisi wenyewe ni Madiwani kwenye hizo Halmashauri? 6 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba nchi yetu ina maji ya kutosha kilichobaki ni kuweka fedha na kusambaza na Serikali inaendelea kuweka fedha. Imeweka fedha mwaka uliopita na mwaka huu fedha tayari ipo kwa ajili ya Halmashauri kuhakikisha kwamba mnatumia zile fedha kuwapa wananchi maji na Wizara ya Maji na Umwagiliaji imeshatoa maelekezo ya jinsi ya kufanya. Mheshimiwa Naibu Spika, sasa niwaambie Waheshimiwa Wabunge Halmashauri yangu tayari imeshatengeneza mpango kazi leo tarehe 3 Julai, hebu jiulize wewe kwenye Halmashauri yako kwenye bajeti mpya je, mpango kazi umeshaanza kufanya? Ndugu zangu naomba sana bajeti ipo tusimamie Halmashauri waweze kutekeleza miradi ya maji hakuna haja ya kulaumiana. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Zacharia Issaay, swali la nyongeza. MHE. ZACHARIA P. ISSAAY: Mheshimiwa Spika, ahsante. Pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri wa Maji, hivi sasa Halmashauri ya Wilaya ya Mbulu katika majimbo yote mawili tulikuwa na mradi
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages305 Page
-
File Size-