jarida la Toleo la 09 WIZARA YA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO

Limeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - GCU | www.habari.go.tz | Juni

Mwaka wa Vipaji

Wizara HabariTz Wizara_habaritz Wizara_HabariTZ Wiza ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo SERIKALI KUBORESHA MAZINGIRA YA SANAA NA MICHEZO

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Mhe. katikati ya mwezi Juni 2021 akiwa Jijini Mwanza akizungumza na vijana alisema kuanzia mwezi Desemba mwaka huu wasanii wataanza kulipwa Mirabaha yao kupitia kazi za Sanaa zinazochezwa katika redio, runinga na mitandao ya kijamii.

Kauli hiyo ya Mhe. Rais na Serikali imekuwa jibu la kilio cha wasani kwa muda mrefu, huku maamuzi hayo ya Serikali yamekuja wakati ambapo sekta ya Sanaa, Utamaduni na Michezo zinaa- jiri vijana wengi.

“Tumeanzisha Mfuko wa Maendeleo ya Michezo ili kusaidia timu zetu za Taifa, tumefuta kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika nyasi bandia. Hivyo, majiji na Manispaa changamkieni fursa hii kupata viwanja bora”. Pia Mheshimiwa Rais alilipigia chapuo suala hili.

Aidha, Mhe. Rais alitoa wito kwa (CCM) kutumia fursa hiyo kuboresha viwanja ambavyo inavimiliki katika mikoa na majiji yote nchini ili kuweka mazingira sahihi ya kuendesha michezo nchini.

Sisi Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tunayachukulia maagizo ya Mhe. Rais aliy- oyatoa kwa Wizara akiwa Jijini Mwanza kwa uzito wake kuanzisha vituo vya michezo (Sports Academy) kila Mkoa ili kukuza vipaji na Sekta ya Michezo hapa nchini.

Tunaamini maagizo haya yamekuja wakati sahihi kwa mfano suala la mrabaha lililokuwa kero kubwa kwa wasanii, ni vizuri wafanyabiashara, wadau wa wasanaa na jamii kwa ujumla tushiriki- ane kuhakikisha wasanii wanapata haki zao ili kuikuza sanaa ya kitanzania na kuibua fursa nyingi zaidi za ajira.

Kwa upande wa taasisi zinazomiliki viwanja vya michezo kama ilivyoagizwa na Mhe. Rais, wale wasio na uwezo wa kuboresha viwanja hivyo wawape fursa hiyo wenye uwezo wa kufanya hivyo huku kwa Upande wa Sport Academy, tayari suala hili limeshaingizwa katika bajeti ya mwaka wa fedha 2021/2022.

Tunaimani kwa upande wetu sisi kama Wizara yenye dhamana ya sekta za Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo tutatoa ushirikiano wote unaohitajika kuhakikisha kuwa shabaha ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan kuboresha mazingira ya michezo, sanaa na utamaduni yanaboreshwa inatimia kwa kila mdau kutimiza wajibu wake ipasavyo.

www.habari.go.tz Wasanii kuanza kulipwa mi baha mwezi Desemba, 2021 Na Shamimu Nyaki, Dodoma

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa “Tumeanzisha Mfuko wa Maende- Utamaduni, Sanaa na Michezo Tanzania Mhe. Samia Suluhu leo ya Michezo ili kusaidia timu zetu kuanzisha vituo vya michezo Hassan amesema kuanzia mwezi za Taifa, tumefuta kodi ya Ongeze- (Sports Academy) kila Mkoa ili Desemba mwaka huu wasanii wata- ko la Thamani (VAT) katika nyasi kukuza vipaji na sekta ya michezo anza kulipwa mirabaha yao kupitia bandia, hivyo majiji manispaa chan- hapa nchini. kazi za Sanaa zinazochezwa katika gamkieni fursa hii kupata viwanja redio, runinga na mitandao ya bora” amesisitiza Mhe. Samia. Awali Waziri wa Habari, Utamad- kijamii. uni, Sanaa na Michezo Mhe. Inno- Aidha, Mhe. Rais ametoa wito kwa cent Bashungwa ametoa wito kwa Mhe. Samia amesema hayo Juni 15, Chama cha Mapinduzi kutumia wafanyabiashara na watoa huduma 2021 Jijini Mwanza alipokuwa fursa hiyo kuboresha viwanja kutumia wasanii katika kutangaza anazungumza na vijana wa Mkoa ambavyo inavimiliki katika mikoa huduma na biashara zao kwa kuwa huo kwa niaba ya vijana wote na majiji yote nchini ili kuweka wasanii wana wafuasi na ushawishi nchini, ambapo amesema Sekta ya mazingira sahihi ya kuendesha mkubwa katika jamii, huku akisisiti- Sanaa, Utamaduni na Michezo inaa- michezo nchini. za vijana ambao wanavipaji kuvi- jiri vijana wengi hivyo Serikali inen- onyesha ili viwapatie ajira. delea kuimarisha sekta hizo. Vilevile ameiagiza Wizara ya Habari

01 WHUSM | JUNI 2021 SEKTA YA HABARI

Tanzania yamlilia Kaunda Adeladius Makwega, DODOMA

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa vuguvugu za ukombozi wa Bara kuwa mzee amefariki dunia, Tanzania Samia Suluhu Hassan zima la Afrika kwa kushirikiana kwa ninawaomba tumuombee.” ametoa pole kwa Rais wa Zambia karibu na Rais wa Kwanza wa Edgar Lungu kutokana na msiba wa Tanzania pamoja na Msiba huo umewagusa watu Rais wa Kwanza wa Taifa la hilo viongozi wengine wa Afrika wa mbalimbali akiwamo nahodha wa Keneth Kaunda. wakati huo. zamani wa timu ya Taifa ya Zambia (K.K Eleven) Kalusha Bwalya “Nimesikitishwa na msiba huo wa Miaka ya 1950, Kaunda alikuwa mtu aliyenusurika kifo katika ajali ya Rais wa Kwanza wa Zambia muhimu katika vuguvugu la kupiga- ndege iliyogharimu maisha ya watu Kenneth Kaunda, Mungu amlaze nia uhuru wa Rhodesia ya Kaskazini 30 wakiwamo wachezaji 18 viongozi pahala pema peponi.” Taarifa hiyo (sasa Zambia) kutoka kwa Uingere- na makocha wa timu hiyo timu imemnukuu Mhe. Rais Samia. za. mwaka 1993 ambaye amewapa pole taifa lote la Zambia, familia ya Mzee Tanzania inamkumbuka Kenneth Kifo chake ni pigo kwa taifa lake na Kaunda, Wazambia wote na Waaf- Kaunda maarufu kama (KK) Afrika kwa ujumla ambapo Vyombo rika kwa ujumla na kuwaomba ambaye alikuwa Rais wa kwanza wa vya Habari na wengine wakinukuu wawe na faraja katika kipindi hiki Zambia, mzalendo, mwanaharakati ukurasa wa facebook wa mtoto kigumu. Apumzike kwa amani. za Ukombozi wa Bara na mwana mkubwa wa Mzee Kaunda anayefa- mwema wa Afrika aliyeipenda hamika kama Kambarage ambaye hatua iliyopelekea kuunga mkono anabainisha, “Nina huzuni kubwa

WHUSM | JUNI 2021 02 Somo la Elimu kwa Michezo kufundishwa kwa wanafunzi wote nchini Na John Mapepele, Mtwara

Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muun- Amesema, Serikali inaendelea na wa Rais Mhe. Samia Suluhu Hassan gano wa Tanzania Mhe. Kassim jitihada za kuanzisha tahasusi za wa kuwahimiza wananchi kufanya Majaliwa ameelekeza somo la Elimu Michezo kwa wanafunzi wa Kidato mazoezi ili kuepuka magonjwa kwa Michezo lifundishwe kwa cha 5 na 6 ili kupata mafaniko katika yasiyo ya kuambukizwa, huku wanafunzi wote katika Shule za sekta na kuchangia katika maende- akisisitiza kuendelea kuunda vikun- Msingi na Sekondari. leo ya uchumi wa viwanda. di vya mazoezi ya ukakamavu (Jog- ging) na matamasha mbalimbali ya Waziri Mkuu ametoa maelekezo “Nasisitiza Wizara husika kuangalia michezo pamoja na kujijengea hayo Juni 08, 2021 Mkoani Mtwara mitaala iliyopo kama inakidhi mahi- utamaduni wa kufanya mazoezi alipofungua mashindano ya taji ya sasa na kuchukua hatua stahi- mara kwa mara. Michezo na Taaluma kwa Shule za ki pale ambapo kutaonekana kuna Msingi na Sekondari (UMI- upungufu, nihimize kuboreshwa TASHUMTA na UMISSETA) ambapo kwa vyuo vya ualimu ili viimarishe amesema matarajio ya Serikali ni masomo ya Elimu kwa Michezo kuona wanafunzi wakionyesha hatua itakayomuwezesha kila uwezo na nidhamu ya hali ya juu ili mhitimu kuwa na ujuzi wa ufundis- kuleta mafanikio kwa taifa. haji wa michezo”amesisitiza Waziri Mkuu. Pia Mhe. Majaliwa amesisitiza wito

03 WHUSM | JUNI 2021 SEKTA YA HABARI

Mhe. Majaliwa: Tufanye mazoezi tuimarishe Afya zetu Na Shamimu Nyaki, DODOMA

Waziri Mkuu wa Tanzania Mhe. ya kutuhamasisha umuhimu wa Aidha, Mhe. Majaliwa ametoa rai Majaliwa amewaa- kufanya mazoezi ili kuimarisha afya kwa watanzania kushiriki mazoezi, sa watanzania kujijengea utaratibu na hatimaye kuongeza ufanisi kuzingatia mlo sahihi kwakua kinga wa kufanya mazoezi mara kwa katika kazi zetu, pamoja na kujikin- ni bora kuliko tiba ambapo pia ame- mara ili kujiepusha na magonjwa ga na magonjwa yasiyoambukiza sisitiza kuundwa kwa vikundi vya pamoja na kuimarisha afya zao. ambayo wengi tumekua wahan- mazoezi ya ukakamavu (Jogging) ga”amesema Mhe. Majaliwa. pamoja na kushiriki matamasha Waziri Mkuu ameyasema hayo, Juni mbalimbali ya michezo. 12, 2021 Jijini Dodoma alipozindua Waziri Mkuu ameongeza kuwa, Bonanza la Michezo (Pamoja magonjwa hayo ambayo Bonanza) lilioandaliwa na Benki ya yanachangiwa kwa kiasi kikubwa na CRDB kwa kushirikiana na Bunge la matumizi ya vilevi, kutoshiriki Tanzania ambalo limehusisha mbio mazoezi au kufanya shughuli za fupi, mazoezi ya viungo pamoja na kutumia nguvu pamoja na kutozin- michezo mbalimbali katika Uwanja gatia lishe bora yamekua chanzo wa Jamhuri Jijini hapo. cha gharama kubwa za afya kwa Serikali na kupoteza nguvu kazi ya “Bonanza hili limeandaliwa kwa ajili Taifa.

WHUSM | JUNI 2021 0204 Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akifanya mazoezi kwenye Bonanza la Michezo (Pamoja Bonanza) lilioandaliwa na Benki ya CRDB kwa kushirikiana na Bunge la Tanzania hivi karibuni. SEKTA YA HABARI

Serikali kuanzisha Kituo cha Michezo katika Chuo cha Michezo Malya Na John Mapepele, MTWARA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Habari, Utamaduni, Sanaa na vya Michezo vya Kitaifa, vilabu, Sanaa na Michezo Mhe. Innocent Michezo, Ofisi ya Rais, TAMISEMI watalaam wa kuvumbua vipaji Bashungwa amesema Wizara na Wizara ya Elimu, Sayansi na (scouters) kutoka Taasisi ya inatarajia kuanzisha kituo maalum Teknolojia katika ngazi mbalimbali Mbwana Samatta pamoja na wata- cha kuendelezea michezo katika kuanzia ngazi ya mawaziri, makati- laam kutoka Sweden wamealikwa ili Chuo Cha Maendeleo ya Michezo bu wakuu na wataalam" amesema kupata fursa ya kuona vipaji katika Malya ili kuendeleza vipaji vina- Waziri Bashungwa. mashindano hayo. vyopatikana. Waziri Bashungwa amesema, Katika ufunguzi huo, Naibu Waziri Waziri Bashungwa amesema hayo matarajio ya Serikali ni kusimamia Ofisi Ya Rais TAMISEMI Mhe. David Juni 08, 2021 Mkoani Mtwara michezo vizuri katika ngazi ya chini Silinde amesema malengo makuu ya wakati wa ufunguzi wa mashindano ambayo itakuwa ni chimbuko mashindano hayo ni pamoja na ya Michezo na Taaluma kwa Shule kubwa la kuvuna vipaji ambavyo kutekeleza azma ya Serikali ya za Msingi na Sekondari (UMI- vitaendelezwa hatimaye kupata Awamu ya Sita ya kukuza vipaji vya TASHUMTA na UMISSETA) yaliyo- wachezaji wenye weledi, watakaoc- michezo kwa kuibua na kujenga fanywa na Waziri Mkuu wa Tanza- heza timu za Taifa, lakini pia umoja wa kitaifa, mshikamano na nia Mhe. Kassim Majaliwa. watakaocheza michezo ya kulipwa, upendo baina ya wanafunzi wangali na kupatia ajira. katika umri mdogo ili kuimarisha "Muamko na hamasa mnayoiona taaluma ya michezo kwa wanafunzi leo hii, ni ushirikiano wa Wizara ya Katika mashindano hayo, vyama na kuwajengea ujuzi na maarifa.

WHUSM | JUNI 2021 0206 Naibu Waziri Gekul: Wiza inagusa hisia za watu wengi Na Shamimu Nyaki, Dodoma

Naibu Waziri wa Habari, Utamad- kuunganisha watanzania. Kupitia isho la Mpira wa Miguu Tanzania, uni, Sanaa na Michezo Mhe. Pauline michezo wananchi wanaimarisha Shirikisho la Riadha Tanzania, Gekul amesema Sekta za Wizara afya zao na kupunguza bajeti ya Chama cha Michezo ya Jadi Tanza- hiyo zinagusa hisia na maisha ya dawa ambapo tayari Serikali nia na Chama cha Mpira wa Miguu watu wengi katika maisha ya kila kushirikiana na Wadau zipo shule za cha Wilaya ya Mpanda vilipitiwa, siku. kulea vipaji vya michezo”amesema kuboreshwa na kuidhinishwa na Mhe. Gekul. Msajili wa Vyama vya Michezo.127 Mhe. Gekul amesema hayo wakati ikiwa ni hatua ya kuimarisha anachangia na kujibu maswali ya Mhe. Gekul amesema Baraza la michezo. Wabunge wakati wa kujadili hoja ya Michezo la Taifa (BMT) ambalo Waziri Mhe. ndiyo waratibu wa michezo nchini Ili kuboresha michezo nchini, Mhe. alipowasilisha Hotuba ya Makadirio mpaka sasa limesajili vyama vya Gekul ameongeza kuwa Chuo cha ya Mapato na Matumizi ya Wizara michezo 12, vilabu 89, taasisi tano za Michezo Malya kimehuisha mitaala hiyo hivi karibuni Bungeni Jijini kimichezo, wakuzaji vipaji vya ya ufundishaji ambayo sasa Dodoma ambapo takriban Wabunge michezo 11 vituo vya michezo vine inaendana na mahitaji ya soko la 25 wamechangia hotuba hiyo moja na mawakala wamichezo 21. michezo ndani na nje ya nchi hatua kwa moja na Wabunge wanne ambayo itaongeza idadi ya michezo wamechangia kwa maandishi. Aidha, ameongeza kuwa marekebi- inayofundishwa ikiwemo mpira wa sho ya Katiba ya Kamati ya Olimpiki kengele kwa ajili ya watu wenye “Hii ni Wizara inayogusa hisia za Tanzania (TOC), Vyama vya uoni hafifu, mpira wa meza na watu, huburudisha, elimisha na michezo vinne ambavyo ni Shirik- vinyoya.

07 WHUSM | JUNI 2021 SEKTA YA HABARI

Tanzania Mwenyeji Mashindano ya Mchezo wa Kabbadi Na Octavian Kimario, DAR ES SALAAM

Mashindano ya Afrika ya mchezo "Natoa rai kwenu kuzishirikisha Mhe. Gekul ameongeza kuwa wa Kabaddi kwa mwaka 2021 yana- sekta nyingine katika fursa hii Serikali inaendelea kuipa kipaum- tarajiwa kufanyika hapa nchini muhimu, mfano sekta ya Utalii, bele michezo mbalimbali inayofan- kuanza Juni 29 hadi 5 Julai, 2021 wanaweza kutumia fursa iliyopo ya vizuri ndani na nje kwakuwa katika Ukumbi wa Ubungo Plaza kutangaza vivutio vya Utalii vilivyo- inasaidia kutangaza nchi, kuibua Jijini Dar es salaam. po nchini kwa mataifa ambayo vipaji pamoja na kuzalisha ajira kwa yanakuja kushiriki mashindano vijana. Naibu Waziri wa Habari, Utamad- haya," amesema Mhe. Gekul. uni Sanaa na Michezo Mhe. Pauline Mashindano hayo yanatarajiwa Gekul Juni 21, 2021 ametembelea Aidha, Mhe. Gekul amewataka kushirikisha nchi sita Kenya, Mauri- kambi ya timu ya taifa ya mchezo wachezaji waliopo kambini kufanya tius, Misri, Cameroon Zimbambwe huo katika shule ya Sekondari mazoezi kwa bidii ili kulibakisha na wenyeji Tanzania ambapo Nguva wilayani Kigamboni Jijini kombe la mashindano hayo nyum- wageni kutoka katika nchi zaidi ya Dar es Salaam, ambapo amewataka bani, huku akipongeza wadhamini 20 za Afrika wanatarijiwa kuwasili waratibu wa mchezo huo kutoa waliojitokeza kudhamini kambi hiyo hapa nchini kwa ajili ya kuratibu na elimu ili jamii iutambue mchezo na kutoa rai kwa wadhamini zaidi kushuhudia mashindano hayo. huo. kujitokeza.

WHUSM | JUNI 2021 08 Wasanii wa kizazi kipya wafunika UMITASHUMTA, UMISSETA Na Joseph Kigingi, MTWARA 2021

Wasanii wa muziki wa kizazi kipya, umati uliofurika katika kiwanja cha Maua Sama na Chegge Chigunda taarabu na singeli wamekuwa mion- Nangwanda Sijaona. wamekonga nyoyo za wanamichezo goni mwa kitutio kikubwa walipo- wa UMISSETA na kuleta hamasa panda kutoa burudani wakati ufun- Akifungua mashindano hayo, kubwa kwa wanamichezo na wadau guzi na ufungaji wa Mashindano ya Mheshimiwa Waziri Mkuu ame- mbalimbali wa mkoa wa Mtwara Michezo na Taaluma kwa Shule za pongeza ubunifu wa waandaji wa walipotumbuiza jukwaani Juni 21, Msingi Tanzania (UMITASHUMTA) mashindano ya mwaka huu kwa 2021 kwenye ufunguzi wa Mashin- na Sekondari (UMISSETA) kwenye kuwashirikisha wasanii ili kuja dano ya Michezo na Taaluma kwa Uwanja wa Nangwanda Sijaona kutoa burudani katika kipindi cha Shule za Sekondari Tanzania (UMIS- mjini Mtwara na kuyafanya mashin- mashindano haya na kuonesha SETA) kwenye Uwanja wa Nang- dano ya mwaka huu kuwa na ham- vipaji na vipawa walivyopewa na wanda Sijaona mjini Mtwara. nasa kubwa tofauti na mashindano Mwenyezi Mungu. yote ya awali. Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Aidha, wakati wa ufungaji wa mash- Utamaduni, Sanaa na Michezo, Dkt. Mashindano ya UMISHUMTA yaliy- indano ya UMITASHUMTA wasanii Hassan Abbasi, amesisitiza kuwa ofunguliwa Juni 08, 2021 na Waziri wa kundi la Mr.Bluu na Msaga mashindano haya yataendelea Mkuu, wa Jamhuri ya Muungano Sumu na vikundi vya kwaya na kutumbuizwa na wasanii mbalimba- wa Tanzania Mhe. KassimMajaliwa ngoma za asili kutoka mikoa li kutoka ndani na nje ya Mkoa wa Majaliwa ambapo kundi la wasanii mbalimbali vilipanda jukwani na likiongozwa na Ibrah kutoka Konde kutoa burudani mwanana. Mtwara, ambapo burudani pia Gang, Beka Flavour, Peter Msechu kutoka vikundi vya ngoma za asili, na Linah Sanga, msanii maarufu wa Pia, wasanii mbalimbali wa muziki kwaya na Sanaa nyingine vitaende- Singeli Dulla Makabila na Mfalme wa kizazi kipya, wakiongozwa na lea kuonesha umahiri wao. wa taarabu Mzee Yusuf waliteka

09 WHUSM | JUNI 2021 SEKTA YA HABARI

Bilion 1.5 zatengwa kwa ajili ya mfuko wa maendeleo ya Utamaduni na Sanaa Na Richard Mwamakafu, MWANZA

Waziri wa Habari,Utamaduni, zinaendelea na utaratibu wa kurudi- Aidha, Mhe. Bashungwa ametumia Sanaa na Michezo Mhe. Innocent sha Bahati Nasibu ya Taifa ili ya nafasi hiyo kuwapongeza Wasanii Bashungwa amesema katika Bajeti mapato yaende kwenye Mfuko wa nchini pamoja na Wanahabari kwa Kuu ya Serikali takriban Shilingi Maendeleo ya Michezo. kazi nzuri wanazofanya kwa masla- Bilioni 1.5 zimetengwa kwa ajili ya hi ya Taifa ambapo amewataka Mfuko wa Maendeleo ya Utamad- Ametumia nafasi hiyo pia kum- kuendelea kumuunga mkono Mhe. uni na Sanaa. shukuru Mhe. Rais kwa kuondoa Rais katika kuleta maendelo ende- Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) levu nchini. Mhe. Bashungwa amesema hayo kwenye nyasi bandia nchini ili miun- Juni 14, 2021 Jijini Mwanza katika dombinu ya michezo iweze kupen- ziara ya Rais wa Tanzania Mhe. deza na kuwa katika hali nzuri Samia Suluhu Hassan ya kukagua na ambapo kwa kuanza italenga kuzindua miradi mbalimbali ya viwanja vya majiji na kadiri fedha maendeleo ambapo ameeleza kuwa itakavyopatikana viwanja vya wizara hiyo kwa kushirikiana kwenye Manispaa na Halmashauri Wizara ya Fedha na Mipango vitafikiwa.

WHUSM | JUNI 2021 0210 Bunge lapitisha takriban sh. bilioni 54 kwa Wiza ya Habari Na Eleuteri Mangi, Dodoma

Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Bajeti hiyo imepitishwa Mei 31, 2021 Maendeleo ya Michezo Malya, Tanzania limepitisha na kuidhinisha Jijini Dodoma baada ya kuwasilish- ujenzi wa eneo Changamani la Bajeti ya Wizara Habari, Utamad- wa na Waziri mwenye dhamana ya Michezo Dodoma, ujenzi wa eneo uni, Sanaa na Michezo jumla ya Wizara hiyo Mhe. Innocent Changamani la Michezo Dar es Sh.Bilioni 54 741,802,000 ili iweze Bashungwa na kujadiliwa na Salaam, ujenzi wa vituo vya mazoezi kutekeleza majukumu yake kwa Wabunge kwa mujibu wa ratiba ya na kupumzika wananchi na mwaka ujao wa fedha. Bunge. ukarabati wa Taasisi ya Sanaa na Utamaduni Bagamoyo. Katika fedha hizo, Sh. Kwa upande miradi ya maendeleo, 19,146,653,000 zimepangwa kutu- Mhe. Bashungwa amebainisha Miradi mingine ni ukarabati wa mika kwa ajili ya mishahara, kiasi kuwa Wizara itatekeleza miradi Chuo Maendeleo ya Michezo Malya, cha Sh. 14,880,149,000 matumizi mbalimbali ikiwemo Programu ya Upanuzi wa Usikivu TBC, kufunga mengineyo na kiasi cha Sh. Urithi wa Ukombozi wa Bara la Mtambo Mpya wa Kisasa wa 20,715,000,000 zitaelekezwa Afrika, Mfuko wa Utamaduni na Uchapaji pamoja na Mradi wa Elimu kwenye miradi ya maendeleo. Sanaa Tanzania, Ujenzi wa Chuo cha kwa Umma.

11 WHUSM | JUNI 2021 SEKTA YA HABARI

Wiza ya Habari yavuka lengo ukusanyaji mapato mwaka 2020/2021 Na Eleuteri Mangi, DODOMA

Wizara ya Habari, Utamaduni, Waziri mwenye dhamana ya Wizara imeanzisha Mfuko wa Utamaduni Sanaa na Michezo imevuka lengo la hiyo, Mhe. Innocent Bashungwa na Sanaa Tanzania ambao ulisajiliwa ukusanyaji mapato kwa kukusanya amesema hayo Mei 31, 2021 Bungeni Septemba 30, 2020 kwa lengo la jumla ya kiasi cha Sh.1, 080,109,491 Jijini Dodoma alipokuwa akiwasili- kuwawezesha watendaji wa kazi za ambazo ni sawa na asilimia 113 hadi sha Hotuba ya Makadirio ya kiutamaduni na Sanaa katika mitaji kufikia Mei, 2021 kutoka Sh. Mapato na Matumizi ya Fedha kwa na kuwajengea uwezo wa kitaalamu 960,000,000/= kiasi ambacho Mwaka 2021/2022. ili kuwawezesha kuandaa bidhaa kilikadiriwa kukusanywa kwa bora zinazomudu ushindani kitaifa mwaka 2020/21. Katika Sekta ya Utamaduni, Wizara na kimataifa.

WHUSM | JUNI 2021 12 Serikali kuondoa VAT kwenye nyasi bandia Na Eleuteri Mangi, Dodoma

Serikali imependekeza kusamehe “Serikali imekubali kuongeza tozo “Nimefurahi Bajeti ya mwaka huu Kodi ya Ongezeko la Thamani (VAT) katika Sports Betting kutoka imependekeza mapato ya michezo kwenye Nyasi bandia kwa ajili ya asilimia 25 hadi 30 ya mapato ya ya kubahatisha yachangie Mfuko viwanja vya mpira vilivyopo kwenye sasa ili asilimia tano iliyoongezeka wa Maendeleo ya Michezo, pia Miji. iende moja kwa moja katika Mfuko kurejeshwa kwa Bahati Nasibu ya wa Maendeleo ya Michezo” amese- Taifa ambayo itachangia Mfuko wa Hayo yamesemwa na Waziri wa ma Dkt. Mwigulu. Maendeleo ya Sanaa na Utamaduni” Fedha na Mipango Dkt. Mwigulu amesema Mhe. Bashungwa. Nchemba Juni 10, 2021 Bungeni Kwa upande wake Waziri wa Jijini Dodoma alipokuwa anawasili- Habari, Utamaduni, Sanaa na sha Bajeti Kuu ya Serikali ambapo Michezo Mhe. Innocent Bashungwa amesema kuwa msamaha huo ameshukuru maamuzi hayo ya utahusisha ridhaa kutoka Shirikisho Serikali ambayo yanaenda kuende- la Mpira wa Miguu Nchini (TFF). leza sekta ya michezo nchini.

13 WHUSM | JUNI 2021 SEKTA YA HABARI

Serikali yampongeza Diamond Platnumz Na Freddy Mwakikato, DODOMA

Waziri wa Habari, Utamaduni, Sanaa kutaka wananchi wahamasishwe ili inees ili msanii huyo ashinde tuzo na Michezo Mhe. Innocent kumpigia kura kwa wingi msanii hiyo ambapo washindi watatangaz- Bashungwa amempongeza Msanii huyo kwa kuteuliwa kugombea tuzo wa Juni 27, 2021. Nasib Abdul (Diamond Platnumz) za BET kwa kuwa ameitanganza nchi kwa kutajwa kuwania tuzo za heshi- kote ulimwenguni. Diamond Platnumz ni msanii pekee ma kipengele cha Wasanii waliofan- kutoka Afrika Mashariki aliyeingia ya vizuri Kimataifa zilizotangazwa Ili kufanikisha msanii Diamond katika orodha ya Wasanii wanaowa- hivi karibuni na Black Entertainment Platnumz kupata tuzo hiyo, Mhe. nia tuzo hiyo duniani. Wasanii Television (BET) kwa mwaka 2021. Bashungwa amesema Wizara kupitia wengine ni Burna Boy na Wizkid BASATA inawahimiza Wabunge, kutoka Nigeria, Aya Nakamura na Mhe. Bashungwa ametoa pongezi Watanzania pamoja na wadau Youssoupha kutoka Ufaransa, hizo alipokuwa akijibu hoja ya Mhe. wengine ndani na nje ya nchi kumpi- Headie One na Young T & Bugsey Mbunge wa ga kura kwa wingi kupitia link ya kutoka Uingereza pamoja na Emicida Maswa Mashariki Mei 31, 2021 ya https://www.bet.com/-awards/nom- wa Brazil.

WHUSM | JUNI 2021 02 Sasisha - Update Ta kilishi - Computer Kimemeshi - charger kitumi - device maunzi laini - software maunzi ngumu - Hardware kizinza - display kichakata maneno - wordprocesser sakinisha - install wavuti wa walimwengu - World wide web (WWW) pakua - download chakata - process vinjari - browser nui - mode kikusa - interface prog mu tumizi - application 1. Kuanzisha Bodi ya Ithibati ya Wanahabari, Baraza Huru la Habari na Mfuko wa Mafunzo kwa Wanahabari,

2. Kufunga mitambo ya masafa ya FM ya TBC katika mikoa ya Njombe, Songwe na Simiyu na Wilaya za Kilwa na Serengeti pamoja na kupanua usikivu wa redio katika maeneo ya Unguja na Pemba,

3. Kuendelea na ujenzi wa majengo ya Makao Makuu ya TBC eneo la Vikonje Jijini Dodoma na kuimarisha Chaneli ya Tanzania Safari.

4. Kampuni ya Magazeti ya Serikali (TSN) itanunua mtambo mpya na wa kisasa wa uchapaji na kuwekeza zaidi kwenye habari mtandao.

5. Kuimarisha Muundo wa TCRA ili kusimamia utangazaji.

6. VKuhuisha na kukamilisha Sera ya Maendeleo ya Utamaduni ya mwaka 1997 pamoja na kuchapisha na kusambaza kitabu cha Mwongozo wa Maadili na Utamad- uni wa Taifa,

7. Kuratibu Programu ya Urithi wa Ukombozi wa Afrika iliyoasisiwa na azimio la Umoja wa Afrika mwaka 2011,

8. Kuendeleza mikakati ya kukitangaza na kubidhaisha Kiswahili

9. Kujenga jengo la kisasa la Ofisi za Mfuko wa Maendeleo ya Utamaduni na Sanaa Jijini Dodoma zitakazotumiwa na taasisi za BASATA, Bodi ya Filamu Tanzania, COSOTA na BAKITA ili kuanza kuwawezesha wasanii kimitaji na mafunzo kwa wadau wa mfuko huo ambao umetengewa kiasi cha Sh.1, 500,000,000,

10. Baraza la Sanaa la Taifa (BASATA) litaimarisha ukusanyaji wa mapato kwa kuan- zisha mfumo wa kielektroniki utakaopanua wigo kwa kuwafikia wadau wa maeneo yote ya nchi wanaohitaji kupata huduma za usajili na vibali,

11. Baraza litatoa vitambulisho kwa wasanii kuwarahisishia kupata huduma mbalim- bali ikiwemo Bima ya afya na huduma za kifedha kwa kuwa vitambulisho hivyo vitaunganishwa na mifumo ya taasisi zingine, 12. Kuweka mfumo wa kisheria ya Taasisi ya Hakimiliki Tanzania (COSOTA) utak- aowezesha kutozwa kwa tozo ya Blank Tape Remuneration/Levy pamoja na mfumo wa kufuatilia matumizi ya kazi za sanaa hususan muziki na filamu katika vyombo vya habari na kukamilisha mfumo wa kielekroniki (online platform) kwa ajili ya kusam- baza kazi za wasanii,

13. Kuanzisha Tamasha Maalum la Michezo ya wanawake ili kuimarisha ushiriki wa wao katika michezo na kuibua vipaji vyao pamoja na kuzindua Mkakati wa Taifa wa Maendeleo ya Michezo na kusimamia utekelezaji wake,

14. Kuendelea kushirikiana na OR TAMISEMI na Wizara ya Elimu, Sayansi na Tekno- lojia, kusimamia shule maalumu za michezo zitakazotengwa katika mikoa yote ya Tanzania Bara na kusimamia ufundishwaji wa somo la michezo kwenye shule za msingi na sekondari ikiwa ni pamoja na tahsusi zenye somo la michezo ili kukuza taaluma hiyo nchini,

15. Kuratibu michezo ya UMISSETA na UMITASHUMTA kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia pamoja na kuratibu Siku Maalumu ya Michezo Kitaifa ili kuhamasisha michezo kwa jamii,

16. Kufanya maboresho na kupanua Chuo cha Maendeleo ya Michezo Malya ili kuki- fanya chuo cha michezo cha kimataifa (sports academy). Toleo la 09

Limeandaliwa na Kitengo cha Mawasiliano Serikalini - GCU Wiza ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo

www.habari.go.tz