Tarehe 4 Julai, 2017
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Hamsini na Tisa – Tarehe 4 Julai, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu. NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Maelezo ya Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2017 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) Bill, 2017). MHE. OMARY A. BADWEL (K.n.y. MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA): Maoni ya Kamati ya Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali Na. 4 wa mwaka 2017 (The Written Laws (Miscellaneous Amendments) No. 4 Bill, 2017) 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. ABDALLAH A. MTOLEA (K.n.y. MHE. TUNDU A.M. LISSU - MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KATIBA NA SHERIA): Maoni ya Msemaji Mkuu wa kambi Rasmi ya Upinzani wa Wizara ya Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali wa mwaka 2017 [The Written Laws (Miscellaneous amendments) Bill, 2017]. NAIBU SPIKA: Ahsante. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea. Katibu. NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Maswali, tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Marwa Ryoba Chacha, Mbunge wa Serengeti, sasa aulize swali lake. Na. 487 Ukosefu wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti MHE. MARWA R. CHACHA aliuliza:- Wilaya ya Serengeti ni kitovu cha utalii na ni Wilaya inayopata watalii wengi lakini haina Hospitali ya Wilaya na hivyo kuleta usumbufu kwa wageni pamoja na wakazi wa Serengeti:- Je, ni lini Hospitali ya Wilaya itakamilika? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais – TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Marwa Ryoba Chacha, Mbunge wa Serengeti, kama ifuatavyo:- 2 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuwa Halmashauri ya Wilaya ya Serengeti haina hospitali ya Wilaya, hivyo wananchi hutumia Hospitali Teule ya Nyerere yaani DDH ambayo inamilikiwa na Kanisa la Mennonite Tanzania. Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Serengeti ulianza mwaka 2009 katika Kijiji cha Kibeyo ambao unafanyika kwa awamu. Katika awamu ya kwanza, jumla ya shilingi bilioni 5.4 zilikadiriwa kutumika kwa ajili ya kuandaa michoro, kuanza ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje, pamoja na jengo la upasuaji (operating theater). Fedha hizo zinatarajiwa kupatikana kutoka vyanzo mbalimbali ikiwemo ruzuku kutoka Serikali Kuu, Mfuko wa Maendeleo wa Halmashauri, Benki ya Maendeleo ya Afrika, pamoja na mapato ya ndani ya Halmashauri (own source). Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasa uandaaji wa michoro pamoja na jengo la upasuaji lenye vifaa vyote (operating theater) vimekamilika na kukabidhiwa kwa Halmashauri tayari kwa matumizi. Aidha, ujenzi wa jengo la wagonjwa wa nje (OPD) upo katika hatua mbalimbali za ukamilishaji. Mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imeweka mpango wa kupeleka fedha ili jengo la wagonjwa wa nje (OPD) liweze kukamilika na kuanza kutoa huduma kwa wananchi. Mheshimiwa Naibu Spika, ni azma ya Serikali kukamilisha ujenzi wa hospitali mbalimbali za Wilaya hapa nchini ili kuwasaidia wananchi kupata huduma bora za afya. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Marwa Ryoba Chacha, swali la nyongeza. MHE. MARWA R. CHACHA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante, nina maswali mawili ya nyongeza. La kwanza tarehe 24 Mei, 2017 wakati Naibu Waziri akijibu swali langu lililokuwa linahusu kupeleka dawa kwenye vituo vya afya niliuliza swali la nyongeza lililokuwa linahusu hospitali hii ya Wilaya. Bahati nzuri Naibu Waziri amefika kwenye hospitali ile akaona, alisema kwamba wametenga 3 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) shilingi milioni 700 kwenda kumalizia OPD ambayo hiyo ingekuja kabla ya mwaka wa fedha 2016/2017 haujaisha. Mwaka wa fedha 2016/2017 umeisha. Alitamka kwenye Bunge hili, wananchi wa Serengeti walisikia zinaenda shilingi milioni 700 kumalizia OPD. Je, alilidanganya Bunge na wananchi wangu wa Serengeti? Kama siyo kwamba alidanganya, nini kilitokea? Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili… NAIBU SPIKA: Umeshauliza mawili Mheshimiwa. (Hapa baadhi ya Wabunge walizungumza bila mpangilio) NAIBU SPIKA: Umeshauliza mawili labda ulikuwa hujisikilizi. (Kicheko) Umeshauliza mawili, kwa hiyo, mwache Mheshimiwa Waziri ajibu hayo maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Naibu Waziri Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, mantiki ya kupeleka fedha Serengeti ilikuwa siyo kulidanganya Bunge na zoezi hili tutalifanya maeneo mbalimbali. Kama Serikali, tuna mpango na tumezungumza kwamba katika programu ya Serikali kwamba tutafanya katika sekta ya afya hasa vituo vya afya vile ambavyo vimeonekana ni changamoto kubwa katika maeneo mbalimbali. Mheshimiwa Naibu Spika, katika kipindi cha sasa, takribani vituo 142 tutavifanyia ujenzi huo ambayo ni equivalent pesa yake karibuni shilingi milioni 700 katika kila center kwa ajili ya kutengeneza miundombinu na kupeleka vifaa tiba. Mheshimiwa Naibu Spika, suala la kudanganya Bunge, jambo hilo halipo isipokuwa ni commitment ya Serikali. Kwa hiyo, jambo la msingi ni kwamba watu wa Serengeti wavute subira kwa sababu Serikali ina mipango yake na inatekeleza. 4 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Katika ujenzi huu sehemu nyingine tunafanya bulk procurement kuufanya ujenzi huu tupate mkandarasi wa pamoja kuhakikisha ujenzi huu unaenda sambamba katika maeneo yote na lengo letu kwamba tupate value for money na ubora wa majengo ule unaokusudiwa tuweze kuupata vizuri. Kwa hiyo, ni commitment ya Serikali kuhakikisha kwamba inapeleka huduma za afya kwa wananchi wake wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Japhary Michael. MHE. RAPHAEL J. MICHAEL: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali moja la nyongeza kwa Mheshimiwa Naibu Waziri. Mheshimiwa Naibu Spika, tatizo lililopo Serengeti linafanana na tatizo lililopo Manispaa ya Moshi na ukizingatia kwamba Manispaa ya Moshi ndiyo Makao Makuu ya Mkoa wa Kilimanjaro na ndiyo eneo ambalo watalii wote wanaoenda mlima Kilimanjaro hupitia pale. Tumekuwa na ombi la muda mrefu la kuomba Hospitali ya Wilaya Serikalini kwa zaidi ya miaka sita au saba hapa. Swali langu, je, Serikali itatusaidia lini kutekeleza ombi letu maalum la kujenga Hospitali ya Wilaya katika Manispaa ya Moshi? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli inawezekana kulikuwa na maombi maalum katika vipindi mbalimbali, lakini tufahamu kwamba haya maombi maalum mara nyingi sana siyo kama ile bajeti ya msingi. Kwa hiyo, inategemea kwamba ni jinsi gani Serikali kipindi hicho imepata fedha za kutosha ku-accommodate maombi maalum. Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, najua kwamba Moshi kweli hakuna Hospitali ya Wilaya, lakini ukiangalia vipaumbele vya Taifa hili hata ukiangalia katika maeneo 5 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) mengine kwa mfano kama Serengeti alipokuwa anazungumza ndugu yangu Mheshimiwa Marwa pale, wako tofauti sana na Moshi. Angalau Moshi mna alternative pale, watu wanaweza wakaenda KCMC au sehemu nyingine. Mheshimiwa Naibu Spika, kwa hiyo, tutaangalia jinsi tutakavyofanya. Ninyi kama Halmashauri ya Wilaya anzeni kufanya hiyo resource mobilization katika ground level na sisi tutaangalia jinsi gani tulifanye jambo hilo. Mheshimiwa Naibu Spika, hata hivyo, ndiyo maana katika kusaidia katika suala zima la Moshi kwa ujumla wake (Moshi Mjini na Vijijini) sasa hivi tunaenda kukiboresha kituo cha Uru Mashariki pale. Lengo kubwa ni kwamba kiweze kusaidiana na hospitali zile ambazo ziko pale kwa lengo kubwa lile lile la kuwasaidia wananchi wa Moshi waweze kupata huduma nzuri ya afya. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Flatei Massay, swali la nyongeza. MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la nyongeza. Kwa kuwa Mheshimiwa Waziri alifika Jimboni kwangu na amekiona Kituo cha Dongobesh na tukaleta ombi la kujengewa theater, je, Mheshimiwa lini sasa theater ile inajengwa ili wananchi wangu wapate matibabu hayo ya upasuaji? Ahsante. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli tuliweza kufika Dongobesh na kuweza kufanya tathmini ya changamoto kubwa inayokabili huduma ya afya katika eneo lile. Mheshimiwa Naibu Spika, kuhusu mpango wa Serikali ndiyo nimezungumza katika vituo 142 kwamba na 6 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Dongobesh ni miongoni mwa kituo ambacho tunaenda kukijengea theater; lakini siyo theater peke yake; tutajenga pale theater tutaweka na vifaa lakini halikadhalika tutaweka uboreshaji wa miundombinu kwa bajeti iliyotengwa pale Dongobesh. Kwa hiyo, naomba niwatoe hofu wananchi wa Dongobesh kwamba jambo hili kwa sababu manunuzi yake tumepeleka kwa ujumla, tufanye subira, ni commitment ya Serikali kwamba siyo muda mrefu sana kazi hii itaanza mara moja. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Venance Mwamoto, swali la nyongeza. MHE.VENANCE M. MWAMOTO: Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Naibu Waziri kwanza nimpe pongezi kubwa kwa kazi kubwa ambayo ametufanyia pale Kilolo kwa ujenzi wa hospitali, ni kilio