Tarehe 19 Mei, 2017

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Tarehe 19 Mei, 2017 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Ishirini na Tisa – Tarehe 19 Mei, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Tukae, Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE - KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Houtuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2017/2018. MHE. MATTAR ALI SALUM (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIFUGO, KILIMO NA MAJI): Taarifa ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018. 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. SUSAN A. J. LYIMO (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. NAIBU SPIKA: Ahsante, Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE–KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 234 Posho ya Madaraka kwa Viongozi MHE. COSATO D. CHUMI aliuliza:- Serikali ilitoa Waraka Na.3 wa mwaka 2014 kuhusu Posho ya Madaraka kwa viongozi wa elimu wakiwemo Walimu Wakuu wa Shule za Msingi, Sekondari, Vyuo na Waratibu Elimu Kata lakini tangu waraka huo utolewe yapata karibu miaka miwili sasa posho hiyo haijaanza kulipwa. Je, ni lini Serikali itaanza kulipa posho hiyo ya viongozi wa elimu? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cosato David Chumi, Mbunge wa Mafinga Mjini, kama ifuatavyo:- 2 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilianza kutekeleza Waraka Na. 3 wa mwaka 2014 kuhusu Posho ya Madaraka kwa Viongozi kuanzia Julai, 2016. Walimu Wakuu wanalipwa kiwango cha shilingi 200,000 kila mwezi na Wakuu wa Shule na Warataibu wa Elimu Kata wanalipwa Posho ya Madaraka kwa kiwango cha shilingi 250,000 kwa mwezi. Kuanzia Julai, 2016 hadi Aprili, 2017, Serikali imelipa posho hiyo jumla ya shilingi bilioni 1.87. Posho hiyo inalipwa kwa viongozi hao kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa elimu katika ngazi ya shule nchini. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Cosato Chumi, swali la nyongeza. MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwanza napenda kuipongeza Serikali kwa kuanza kutekeleza Waraka huo wa kuwalipa Posho ya Madaraka Walimu Wakuu wa Shule pamoja na Waratibu. Hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwa posho hii kama ilivyoelezwa katika Waraka ni Posho ya Madaraka. Je, Serikali sasa haioni ni wakati muafaka kuanza kulipa posho hii kwa ajili ya viongozi wengine kama vile Afisa Elimu, Afisa Elimu Taaluma pamoja na Afisa Elimu Takwimu na Vifaa? (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa kazi ya ualimu ni zaidi ya kufundisha, kuna kufanya maandalio, kufundisha, kusahihisha, kupanga matokeo na mengine mengi tu. Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka kurejesha ile tulikuwa tunaita Teaching Allowance kwa ajili ya kuwalipa walimu? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mbunge kwa sababu swali hili ni concern ya 3 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) walimu wote na hii kwanza mwanzo ilikuwa inajitokeza na Serikali tuliamua kuitekeleza kama tulivyosema hapo awali. Suala la jinsi gani tuangalie Maafisa Elimu Taaluma, Maasifa Elimu Takwimu watapata posho hii, nadhani vyeo hivi ni vya kimuundo ambavyo viko katika Halmashauri zetu maana yake kuna hao vilevile kuna Maafisa Kilimo na Maafisa mbalimbali. Kwa sasa kwanza tuendelee na utaratibu wa sasa na pale itakapoonekana kuna haja ya kuweza kufanya mabadiliko tutafanya hivyo. Lengo letu kubwa ni kupandisha motivation ya wafanyakazi hasa watendaji wetu katika ngazi mbalimbali waweze kufanya kazi kwa ufanisi. Mheshimiwa Naibu Spika, katika jambo lingine la Teaching Allowance, hata Mheshimiwa Masoud alisimama hapa hoja yake ilikuwa ni hiyo hiyo, jambo hili tumelichukua. Bahati nzuri Waziri wetu hapa wa Utumishi kutoka Ofisi ya Rais nakumbuka mwezi Mei, 2017 alifanya mkutano rasmi wa uzinduzi wa Bodi hii. Sasa tunakwenda kuangalia suala zima la wafanyakazi katika mazingira mbalimbali maana hatuzungumzii walimu peke yake, tuna Mabwana Shamba, tuna watu wa kada mbalimbali ambao na wenyewe wako katika mazingira hayo magumu. Ndiyo maana Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Utumishi inashughulikia jambo hili kwa upana wake lengo kubwa ni kuja na ajenda pana ya Kitaifa ni nini tufanye kutatua matatizo ya wafanyakazi walio katika mazingira mbalimbali ya utendaji wa kazi. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bilago. MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Suala la Teaching Allowance huwa halieleweki vizuri ndiyo maana linachanganywa na kada zingine. Teaching Allowance lengo lake ni ku-offset zile saa nyingi ambazo mwalimu anatumia kusahihisha madaftari au kazi za wanafunzi mpaka nyumbani kazi ambayo haifanywi na sekta zingine. Hakuna Bwana Kilimo anakwenda kusimamia… NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bilago uliza swali. MHE. KASUKU S. BILAGO: Najenga hoja. 4 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Usijenge hoja swali lako ni la nyongeza, kwa hiyo, utakuwa umeshalipanga tayari. Uliza swali lako ili tu-save muda. MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali lazima iangalie Teaching Allowance kwa walimu kama kitu pekee kabisa. Je, ni lini sasa Serikali itakuja na mkakati rasmi wa kuwasaidia walimu hawa kupata hiyo Teaching Allowance? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Utumishi na Utawala Bora majibu. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Wazir wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bilago, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, nimueleze tu Mheshimiwa Bilago kwamba kama Serikali tunatambua umuhimu na thamani ya mwalimu na uzito na ugumu wa kazi wanayofanya na ndiyo maana ukiangalia katika kada za utumishi wa umma walimu wamepewa kipaumbele cha hali ya juu na bado hatutasita kufanya hivyo. Mheshimiwa Naibu Spika,nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge, tumeanza zoezi la tathmini ya kazi, tunaangalia uzito, majukumu na aina za kazi kwa ujumla wake katika Utumishi wa Umma na posho zipi zitatakiwa kuwepo katika kada gani. Nimuombe Mheshimiwa Mbunge aendelee kuvuta subira, zoezi hilo la tathmini ya kazi litakamilika katika mwaka huu wa fedha na baada ya hapo tutaweza kuainisha na kupitia na kuhuisha miundo mbalimbali ya kiutumishi vilevile kuangalia ni posho zipi ambazo zinahitajika kuwepo ikiwemo na hiyo ya Teaching Allowance kwa mapana yake. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Daimu Mpakate, swali la nyongeza. 5 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Makaimu Watendaji wa Vijiji karibu maeneo mengi ya Tanzania hawapewi posho. Je, Serikali haioni haja ya kuwapa posho Makaimu Watendaji wa Vijiji ili waweze kufanya kazi zao vizuri? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, anachosema Mheshimiwa Mpakate ni kwamba katika maeneo mbalimbali ya vijiji vyetu watu wengi wanakaimu na kuna maeneo mengine walimu ndiyo walikuwa wanakaimu kama Watendaji wa Vijiji na tumetoa maelekezo katika Kurugenzi zetu kuacha kukaimisha Watendaji wa Vijiji hasa wale walimu kwa sababu wanaondoa nguvu kubwa sana ya ufundishaji. Katika jambo hili, kila Halmashauri tumeipa maelekezo na kila Mkurugenzi anajua ana watu wangapi wanakaimu sasa kupitia own source zao wataangalia utaratibu gani wa kufanya lakini lengo kubwa tunataka katika kila kijiji kazi ziweze kufanyika. NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea. Mheshimiwa Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa, Mbunge wa Viti Maalum sasa aulize swali lake. Na. 235 Kupandisha Madaraja Walimu Wanaojiendeleza MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA aliuliza:- Je, nini mkakati na sera ya Serikali kwa wafanyakazi hususani walimu wanaojiendeleza katika kuwapandisha madaraja na kuwaongezea mishahara? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. 6 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za 2009, watumishi wa umma hupandishwa vyeo kwa kuzingatia sifa na ufanisi na utendaji kazi. Mwalimu anapohitimu mafunzo yake anastahili kubadilishiwa muundo wake wa utumishi mfano, Mwalimu Daraja la III - Stashahada kwenda Daraja la II ngazi ya Shahada. Kupanda daraja kwa mtumishi kunategemea utendaji kazi utakaothibitishwa na matokeo katika Mfumo wa Wazi wa Upimaji Utendaji Kazi wa mtumishi husika yaani OPRAS system. Watumishi wote wanatakiwa kujaza fomu hizo na kupimwa utendaji wao wa kazi kama wanastahili kupandishwa daraja.
Recommended publications
  • Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Bunge La Tanzania
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI NA SABA YATOKANAYO NA KIKAO CHA KUMI NA NNE (DAILY SUMMARY RECORD OF PROCEEDINGS) 21 NOVEMBA, 2014 MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI SABA KIKAO CHA KUMI NA NNE – 21 NOVEMBA, 2014 I. DUA Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu alisoma Dua saa 3.00 Asubuhi na kuliongoza Bunge. MAKATIBU MEZANI – i. Ndg. Asia Minja ii. Ndg. Joshua Chamwela II. MASWALI: Maswali yafuatayo yaliulizwa na wabunge:- 1. OFISI YA WAZIRI MKUU Swali Na. 161 – Mhe. Betty Eliezer Machangu [KNY: Mhe. Dkt. Cyril Chami] Nyongeza i. Mhe. Betty E. Machangu, mb ii. Mhe. Michael Lekule Laizer, mb iii. Mhe. Prof. Peter Msolla, mb Swali Na. 162 - Mhe. Richard Mganga Ndassa, mb Nyongeza (i) Mhe Richard Mganga Ndassa, mb Swali Na. 163 - Mhe. Anne Kilango Malecela, mb Nyongeza : i. Mhe. Anne Kilango Malecela, mb ii. Mhe. John John Mnyika, mb iii. Mhe. Mariam Nassor Kisangi iv. Mhe. Iddi Mohammed Azzan, mb 2 2. OFISI YA RAIS (UTUMISHI) Swali Na. 164 – Mhe. Ritta Enespher Kabati, mb Nyongeza i. Mhe. Ritta Enespher Kabati, mb ii. Mhe. Vita Rashid Kawawa, mb iii. Mhe. Mch. Reter Msingwa, mb 3. WIZARA YA UJENZI Swali Na. 165 – Mhe. Betty Eliezer Machangu, mb Nyongeza :- i. Mhe. Betty Eliezer Machangu, mb ii. Mhe. Halima James Mdee, mb iii. Mhe. Maryam Salum Msabaha, mb Swali Na. 166 – Mhe. Peter Simon Msingwa [KNY: Mhe. Joseph O. Mbilinyi] Nyongeza :- i. Mhe. Peter Simon Msigwa, Mb ii. Mhe. Assumpter Nshunju Mshama, Mb iii. Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa 4.
    [Show full text]
  • Madini News Rais Wa Jamhuri Ya Muungano Toleo Na.2 Wa Tanzania Machi, 2020 HALIUZWI
    Toleo Na.2 // Machi 2020 Yaliyomo // Biteko - Nitasimama na Mzee Tume ya Leseni ya TanzaniteOne Imefutwa na Kisangani mpaka “asimame” Kurudishwa Serikalini - Biteko... Uk.04 ... Uk.08 Madini Bilioni 66.5 zapatikana tangu Wanawake Tume ya Madini kuanzishwa kwa masoko Wawakumbuka ya madini ... Uk.10 Yatima ... Uk.18 www.tumemadini.go.tz Tume ya Madini 2020 www.tumemadini.go.tz /TAHARIRI Salamu Kutoka kwa Waziri wa Madini Maoni ya Mhariri SEKTA YA MADINI INAIMARIKA, MAFANIKIO MASOKO TUENDELEZE USHIRIKIANO YA MADINI TUMEWEZA! Katika Mwaka wa Fedha 2019/2020 Wizara ya Madini ilipanga kutekeleza majukumu yake kupitia miradi Katika kuhakikisha kuwa Sekta ya Madini inakuwa na mchango mbalimbali ikilenga katika kuimarisha Sekta ya Madini, hivyo kuwa na mchango mkubwa kwenye ukuaji wa mkubwa kwenye ukuaji wa uchumi wa Taifa, Serikali kupitia uchumi wa nchi. Tume ya Madini kuanzia Machi, 2019 ilifungua masoko ya madini Katika Toleo lililopita nilielezea kwa kifupi kuhusu yale ambayo yamesimamiwa na kutekelezwa na Wizara na vituo vya ununuzi wa madini lengo likiwa ni kudhibiti utorosh- kwa kipindi cha takribani miaka miwili tangu kuanzishwa kwake. waji wa madini kwa kuwapatia wachimbaji wa madini nchini Katika Toleo hili nitaelezea kwa kifupi mafanikio ya utekelezaji wa majukumu ya Wizara kwa kipindi cha sehemu ya kuuzia madini yao huku wakilipa kodi mbalimbali kuanzia Julai, 2019 hadi Februari, 2020. Kama ambavyo nilieleza Bungeni katika Hotuba yangu wakati Serikalini. nikiwasilisha Bajeti ya Wizara kwa Mwaka 2019/2020, nilieleza kuwa, Wizara imepangiwa kukusanya Shilingi 470,897,011,000.00 katika Mwaka wa Fedha 2019/2020. Uanzishwaji wa masoko ya madini na vituo vya ununuzi wa Napenda kuwataarifu wasomaji wa Jarida hili kuwa, hadi kufikia Februari, 2020 jumla ya Shilingi madini ni sehemu ya maelekezo yaliyotolewa kwenye mkutano wa 319,025,339,704.73 zimekusanywa ambazo ni sawa na asilimia 102 ya lengo la makusanyo ya nusu mwaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tazania, Dkt.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA KUMI Kikao Cha Saba – Tarehe 7 Februari, 2018
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI Kikao cha Saba – Tarehe 7 Februari, 2018 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa tukae, Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha (Mapitio ya Nusu mwaka 2017/2018) [Monetary Policy Statement (The Mid – Year Review 2017/2018)]. MHE. PETER J. SERUKAMBA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu Shughuli za Kamati kwa mwaka 2017. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. DANIEL E. MTUKA – K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu shughuli za Kamati kwa mwaka 2017. MWENYEKITI: Asante sana, Katibu tuendelee. NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 84 Kuimarisha Huduma za Kijamii maeneo ya Vijiji MHE. CECIL D. MWAMBE (K.n.y MHE. UPENDO F. PENEZA) aliuliza:- Je, Serikali imeweka mikakati gani kuimarisha huduma za umeme, maji, afya na elimu katika maeneo ya vijijini ili kuongeza uzalishaji katika maeneo hayo na kuzuia wimbi la watu kukimbilia mijini? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPH G. KAKUNDA) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi
    [Show full text]
  • MKUTANO WA SABA Kikao Cha Ishirini Na Tano – Tarehe 15
    NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Ishirini na Tano – Tarehe 15 Mei, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu! NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. MWENYEKITI: Ahsante. Katibu. NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI: Maswali. 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MASWALI NA MAJIBU Na. 200 Mgongano wa Kiutendaji – Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma MHE. LEONIDAS T. GAMA aliuliza:- Wananchi wa Songea Mjini wamekuwa wakiitumia Hospitali ya Mkoa wa Ruvuma kama Hospitali yao ya Wilaya hivyo kufanya kuwepo na mgongano wa kiutendaji kati ya Mamlaka ya Mkoa inayoitambua Hospitali hiyo kama Rufaa ya ngazi ya Mkoa na Mamlaka ya Wilaya. Tarehe 10 Januari, 2016, Mheshimiwa Waziri wa Afya alifika kuona hali halisi na juhudi za wananchi wa Songea Mjini za kujenga Kituo cha Afya Mji Mwema ambacho kimefikia hatua kubwa, hivyo wakamwomba Waziri kituo hicho kipandishwe hadhi kuwa Hospitali ya Wilaya, Songea Mjini. (a) Je, Serikali haioni umuhimu wa kuiacha Hospitali ya Mkoa ifanye kazi ya Rufaa Kimkoa? (b) Je, Serikali haioni haja ya kupunguza msongamano katika hospitali hiyo kwa kuanzisha Hospitali ya Wilaya Songea Mjini? (c) Je, ni lini basi Serikali
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 105 May - Aug 2013
    Tanzanian Affairs Text 1 Issued by the Britain-Tanzania Society No 105 May - Aug 2013 Even More Gas Discovered Exam Results Bombshell Rising Religious Tensions The Maasai & the Foreign Hunters Volunteering Changed my Life EVEN MORE GAS DISCOVERED Roger Nellist, the latest volunteer to join our panel of contributors reports as follows on an announcement by Statoil of their third big gas discovery offshore Tanzania: On 18 March 2013 Statoil and its co-venturer ExxonMobil gave details of their third high-impact gas discovery in licence Block 2 in a year. The new discovery (known as Tangawizi-1) is located 10 kilometres from their first two discoveries (Lavani and Zafarani) made in 2012, and is located in water depth of 2,300 metres. The consortium will drill further wells later this year. The Tangawizi-1 discovery brings the estimated total volume of natural gas in-place in Block 2 to between 15 and 17 trillion cubic feet (Tcf). Depending on reservoir characteristics and field development plans, this could result in recoverable gas volumes in the range of 10-13 Tcf from just this one Block. These are large reserves by international stand- ards. By comparison, Tanzania’s first gas field at Songo Songo island has volumes of about 1 Tcf. Statoil has been in Tanzania since 2007 and has an office in Dar es Salaam. It operates the licence on Block 2 on behalf of the Tanzania Petroleum Development Corporation (TPDC) and has a 65% working interest, with ExxonMobil Exploration and Production Tanzania Limited holding the remaining 35%. It is understood that under the Production Sharing Agreement that governs the operations, TPDC has the right to a 10% working participation interest in case of a development phase.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Hamsini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Hamsini na Sita – Tarehe 22 Juni, 2021 (Bunge Lilianza saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Waheshimiwa tunaendelea na Mkutano wetu wa Tatu, leo ni Kikao cha Hamsini na Sita na kabla hatujaendelea nitumie nafasi hii kuwashukuru sana wasaidizi wangu wote wakiongozwa na Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa David Kihenzile, Mheshimiwa Zungu na Mheshimiwa Najma kwa kazi nzuri ambayo wameifanya wiki nzima kutuendeshea mjadala wetu wa bajeti. (Makofi) Sasa leo hapa ndio siku ya maamuzi ambayo kila Mbunge anapaswa kuwa humu ndani, kwa Mbunge ambaye Spika hana taarifa yake na hatapiga kura hapa leo hilo la kwake yeye. (Makofi) Katibu. NDG. NENELWA MWIHAMBI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Maswali na tunaanza na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Kwela. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 465 Ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri Katika Mji wa Laela MHE. DEUS C. SANGU aliuliza:- Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Sumbawanga katika Mji wa Laela baada ya agizo la Serikali la kuhamisha Makao Makuu? SPIKA: Majibu ya swali hilo muhimu la watu wa Kwela, Mheshimiwa Naibu Waziri - TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt. Festo Dugange tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Jimbo la Kwela kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ni miongoni mwa Halmashauri 30 zilizohamia kwenye maeneo mapya ya utawala mwaka 2019.
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Kumi Na Tisa – Tarehe 29 Aprili, 2021
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Kumi na Tisa – Tarehe 29 Aprili, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa, tukae. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Ndani ya Nchi kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU WAZIRI WA MADINI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2021/2022. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. SAADA MONSOUR HUSSEIN - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2020/2021 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Katibu. NDG. MOSSY LUKUVI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa maswali, tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Simon Songe Lusengekile, Mbunge wa Busega, sasa aulize swali lake. Na. 158 Serikali Kukamilisha Ujenzi wa Zahanati – Busega MHE. SIMON S. LUSENGEKILE aliuliza:- Wananchi wa Kata ya Imalamate Wilayani Busega wamejenga zahanati na kumaliza maboma manne kwa maana ya zahanati moja kila kijiji:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuwasaidia wananchi hao kuezeka maboma hayo ili waweze kupata huduma za afya kwenye zahanati hizo? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri wa TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 2 AGOSTI, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba mzime vipasa sauti vyenu maana naona vinaingiliana. Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri, tunaingia hatua inayofuata. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Leo ni siku ya Alhamisi lakini tulishatoa taarifa kwamba Waziri Mkuu yuko safarini kwa hiyo kama kawaida hatutakuwa na kipindi cha maswali hayo. Maswali ya kawaida yapo machache na atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Vita R. M. Kawawa. Na. 310 Fedha za Uendeshaji Shule za Msingi MHE. VITA R. M. KAWAWA aliuliza:- Kumekuwa na makato ya fedha za uendeshaji wa Shule za Msingi - Capitation bila taarifa hali inayofanya Walimu kuwa na hali ngumu ya uendeshaji wa shule hizo. Je, Serikali ina mipango gani ya kuhakikisha kuwa, fedha za Capitation zinatoloewa kama ilivyotarajiwa ili kupunguza matatizo wanayopata wazazi wa wanafunzi kwa kuchangia gharama za uendeshaji shule? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) imepanga kila mwanafunzi wa Shule ya Msingi kupata shilingi 10,000 kama fedha za uendeshaji wa shule (Capitation Grant) kwa mwaka.
    [Show full text]
  • AUDITED FINANCIAL STATEMENTS for the YEAR ENDED 30Th JUNE 2017
    THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA PRIME MINISTER’S OFFICE DRUG CONTROL AND ENFORCEMENT AUTHORITY (VOTE 091) AUDITED FINANCIAL STATEMENTS FOR THE YEAR ENDED 30th JUNE 2017 AUDITED FINANCIAL STATEMENTS 1 FOR THE YEAR ENDED 30th JUNE 2017 Drug Satchets VISION To have a society with zero tolerance on drug abuse and trafficking. MISSION To protect the well-being of Tanzanians against drug and related effects by defining, promoting and coordinating the Policy of the Government of the URT for the control of drug abuse and illicit trafficking. CORE VALUES In order to achieve the above Vision and Mission, the Authority has put forward core values, which are reliability, cooperation, accountability, innovativeness, professionalism, confidentiality, efficiency and effectiveness. Heroin Cocain Cannabis Miraa Precursor Chemicals AUDITED FINANCIAL STATEMENTS i FOR THE YEAR ENDED 30th JUNE 2017 THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA PRIME MINISTER’S OFFICE DRUG CONTROL AND ENFORCEMENT AUTHORITY (VOTE 091) TABLE OF CONTENTS List of Acronyms ......................................................................................................................iii General Information .................................................................................................................iv Statement from the Honorable Minister for State, Prime Minister’s Office; Policy, Parliamentary Affairs, Labour, Employment, Youth and the Disabled ..........................1 Statement by the Accounting Officer .......................................................................................3
    [Show full text]
  • 16 MEI, 2013 MREMA 1.Pmd
    16 MEI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Ishirini na Saba – Tarehe 16 Mei, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. Waheshimiwa Wabunge Kikao cha Ishirini na Saba kinaanza. Mkutano wetu wa Kumi na Moja. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UCHUKUZI:- Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. 1 16 MEI, 2013 MHE. PROF. JUMA A. KAPUYA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA MIUNDOMBINU): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Uchukuzi kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013 na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MHE. PAULINE P. GEKUL (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA UCHUKUZI): Taaqrifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Uchukuzi Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MASWALI KWA WAZIRI MKUU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kama kawaida yetu siku ya Alhamisi tunakuwa na Kipindi cha Maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu na swali la kwanza la siku ya leo linaulizwa na Mheshimiwa Stephen Hilary Ngonyani. MHE. STEPHEN H. NGONYANI: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana. Kwanza nianze kwa kumpongeza Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa kunipa chakula cha msaada kule kwenye jimbo langu. Swali linalokuja ni hivi. Mheshimiwa Naibu Spika, Kitengo cha Maafa ni Kitengo ambacho kiko chini ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, nchi nzima kinajua jinsi unavyosaidia wananchi.
    [Show full text]
  • Muhtasari Juu Ya Biashara Na Haki Za Binadamu Tanzania Robo Tatu Ya Mwaka: Julai – Septemba 2020
    photo courtesy of Governance Links MUHTASARI JUU YA BIASHARA NA HAKI ZA BINADAMU TANZANIA ROBO TATU YA MWAKA: JULAI – SEPTEMBA 2020 Tangu aingie madarakani mwaka 2005, Rais Magufuli ametilia mkazo kwenye maendeleo ya miundom- binu kama jambo muhimu katika kufikia malengo ya viwanda na maendeleo ya Tanzania. Ma- tokeo yake, miradi mingi ya miundombinu mikubwa imekuwa ikiendelea nchini, kuanzia miundombinu ya barabara, ukarabati wa mifumo ya reli na viwanja vya ndege nchini, na kuongeza na kuwa na aina nyingi ya nishati nchini kupitia mitambo ya gesi asilia na umeme wa maji, kwa kutaja tu kwa uchache. Wakati miradi ya miundombinu inaongeza mapato, ajira, ukuaji wa uchumi na, hivyo, maendeleo chanya, upanuzi wa haraka wa sekta unaweza pia kuleta athari hasi kwa jamii na mazingira ambamo miradi inatekelezwa. Mwaka 2017, Tume ya Haki za Binadamu na Utawala Bora (CHRAGG), ilidokeza uhitaji wa ku- zingatia haki za binadamu kwenye sekta ya ujenzi inayokua kwa kasi nchini (Kumb. E.1). Mwezi Machi 2020, zaidi ya wadau 60 kutoka kwenye biashara, asasi za kiraia na serikali walihimiza kuweka kipaumbele katika sekta ya miundombinu ili kukuza heshima ya haki za binadamu nchini Tanzania (Kumb. E2). Matokeo mapya juu ya athari za miradi mikubwa ya miundombinu kwa haki za binadamu yanawasili- shwa kupitia chunguzi kifani mpya tano juu ya “Sauti za Watanzania”. Tafiti hizi zilitathmini athari za miradi mitatu ya usambazaji wa nishati: Bomba la Mafuta Ghafi la Afrika Mashariki (mkoa wa Manyara; Kumb. E3), Mradi wa Umeme wa Maji wa Maporomoko ya Rusumo (mkoa wa Kagera; Kumb. E4) na miradi ya usambazaji wa nishati vijijini (mkoa wa Mwanza; Kumb.
    [Show full text]
  • Briefing on “Business & Human Rights in Tanzania” – 2020
    photo courtesy of HakiArdhi BRIEFING ON “BUSINESS & HUMAN RIGHTS IN TANZANIA” – 2020 QUARTER 1: JANUARY – MARCH In March 2020, key stakeholders from civil society, the business community and various government agencies from Tanzania mainland and Zanzibar met in Dar es Salaam to discuss the topics of “land rights and environment” during the second Annual Multi-stakeholder Dialogue on Business and Human Rights (Ref.E1). “Land rights and environment” were identified as cross-cutting issues that affect the rights of many in various ways in Tanzania. Sustainable solutions for addressing the country’s many conflicts related to land are therefore essential to guarantee basic rights for all. During the multi-stakeholder meeting, four case studies on current issues of “land rights and envi- ronment” (Ref.E2) were presented by Tanzanian civil society organisations (Ref.E1). Their studies focussed on initiatives to increase land tenure security and on the tensions between conservation and rights of local communities. The studies confirm that land is indeed a critical socio-economic resource in Tan- zania, but a frequent source of tensions in rural areas due to competing needs of different land users, such as communities versus (tourism) investors or local communities versus conservation authorities (Ref. E2, E3). Women face a number of additional barriers acquiring land rights which affect their livelihoods (Ref.E4, E5). The absence of formalized land rights and land use plans in many regions of the country aids in sus- taining land-related challenges. Therefore, initiatives to address land tenure security (Ref.E5) can have positive effects on local communities (Ref.E6).
    [Show full text]