Tarehe 19 Mei, 2017

Tarehe 19 Mei, 2017

NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Ishirini na Tisa – Tarehe 19 Mei, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Tukae, Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE - KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Houtuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2017/2018. MHE. MATTAR ALI SALUM (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIFUGO, KILIMO NA MAJI): Taarifa ya Kamati ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2016/2017 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2017/2018. 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. SUSAN A. J. LYIMO (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. NAIBU SPIKA: Ahsante, Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE–KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU Na. 234 Posho ya Madaraka kwa Viongozi MHE. COSATO D. CHUMI aliuliza:- Serikali ilitoa Waraka Na.3 wa mwaka 2014 kuhusu Posho ya Madaraka kwa viongozi wa elimu wakiwemo Walimu Wakuu wa Shule za Msingi, Sekondari, Vyuo na Waratibu Elimu Kata lakini tangu waraka huo utolewe yapata karibu miaka miwili sasa posho hiyo haijaanza kulipwa. Je, ni lini Serikali itaanza kulipa posho hiyo ya viongozi wa elimu? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Cosato David Chumi, Mbunge wa Mafinga Mjini, kama ifuatavyo:- 2 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ilianza kutekeleza Waraka Na. 3 wa mwaka 2014 kuhusu Posho ya Madaraka kwa Viongozi kuanzia Julai, 2016. Walimu Wakuu wanalipwa kiwango cha shilingi 200,000 kila mwezi na Wakuu wa Shule na Warataibu wa Elimu Kata wanalipwa Posho ya Madaraka kwa kiwango cha shilingi 250,000 kwa mwezi. Kuanzia Julai, 2016 hadi Aprili, 2017, Serikali imelipa posho hiyo jumla ya shilingi bilioni 1.87. Posho hiyo inalipwa kwa viongozi hao kwa ajili ya kuimarisha usimamizi wa elimu katika ngazi ya shule nchini. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Cosato Chumi, swali la nyongeza. MHE. COSATO D. CHUMI: Mheshimiwa Naibu Spika, nakushukuru. Kwanza napenda kuipongeza Serikali kwa kuanza kutekeleza Waraka huo wa kuwalipa Posho ya Madaraka Walimu Wakuu wa Shule pamoja na Waratibu. Hata hivyo nina maswali mawili ya nyongeza. Mheshimiwa Naibu Spika, swali la kwanza, kwa kuwa posho hii kama ilivyoelezwa katika Waraka ni Posho ya Madaraka. Je, Serikali sasa haioni ni wakati muafaka kuanza kulipa posho hii kwa ajili ya viongozi wengine kama vile Afisa Elimu, Afisa Elimu Taaluma pamoja na Afisa Elimu Takwimu na Vifaa? (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kwa kuwa kazi ya ualimu ni zaidi ya kufundisha, kuna kufanya maandalio, kufundisha, kusahihisha, kupanga matokeo na mengine mengi tu. Je, Serikali haioni sasa ni wakati muafaka kurejesha ile tulikuwa tunaita Teaching Allowance kwa ajili ya kuwalipa walimu? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nimpongeze Mbunge kwa sababu swali hili ni concern ya 3 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) walimu wote na hii kwanza mwanzo ilikuwa inajitokeza na Serikali tuliamua kuitekeleza kama tulivyosema hapo awali. Suala la jinsi gani tuangalie Maafisa Elimu Taaluma, Maasifa Elimu Takwimu watapata posho hii, nadhani vyeo hivi ni vya kimuundo ambavyo viko katika Halmashauri zetu maana yake kuna hao vilevile kuna Maafisa Kilimo na Maafisa mbalimbali. Kwa sasa kwanza tuendelee na utaratibu wa sasa na pale itakapoonekana kuna haja ya kuweza kufanya mabadiliko tutafanya hivyo. Lengo letu kubwa ni kupandisha motivation ya wafanyakazi hasa watendaji wetu katika ngazi mbalimbali waweze kufanya kazi kwa ufanisi. Mheshimiwa Naibu Spika, katika jambo lingine la Teaching Allowance, hata Mheshimiwa Masoud alisimama hapa hoja yake ilikuwa ni hiyo hiyo, jambo hili tumelichukua. Bahati nzuri Waziri wetu hapa wa Utumishi kutoka Ofisi ya Rais nakumbuka mwezi Mei, 2017 alifanya mkutano rasmi wa uzinduzi wa Bodi hii. Sasa tunakwenda kuangalia suala zima la wafanyakazi katika mazingira mbalimbali maana hatuzungumzii walimu peke yake, tuna Mabwana Shamba, tuna watu wa kada mbalimbali ambao na wenyewe wako katika mazingira hayo magumu. Ndiyo maana Serikali kupitia Ofisi ya Rais, Utumishi inashughulikia jambo hili kwa upana wake lengo kubwa ni kuja na ajenda pana ya Kitaifa ni nini tufanye kutatua matatizo ya wafanyakazi walio katika mazingira mbalimbali ya utendaji wa kazi. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bilago. MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Suala la Teaching Allowance huwa halieleweki vizuri ndiyo maana linachanganywa na kada zingine. Teaching Allowance lengo lake ni ku-offset zile saa nyingi ambazo mwalimu anatumia kusahihisha madaftari au kazi za wanafunzi mpaka nyumbani kazi ambayo haifanywi na sekta zingine. Hakuna Bwana Kilimo anakwenda kusimamia… NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Bilago uliza swali. MHE. KASUKU S. BILAGO: Najenga hoja. 4 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU SPIKA: Usijenge hoja swali lako ni la nyongeza, kwa hiyo, utakuwa umeshalipanga tayari. Uliza swali lako ili tu-save muda. MHE. KASUKU S. BILAGO: Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali lazima iangalie Teaching Allowance kwa walimu kama kitu pekee kabisa. Je, ni lini sasa Serikali itakuja na mkakati rasmi wa kuwasaidia walimu hawa kupata hiyo Teaching Allowance? (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Waziri wa Utumishi na Utawala Bora majibu. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA NA UTAWALA BORA: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Wazir wa Nchi, Ofisi ya Rais - TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Bilago, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, nimueleze tu Mheshimiwa Bilago kwamba kama Serikali tunatambua umuhimu na thamani ya mwalimu na uzito na ugumu wa kazi wanayofanya na ndiyo maana ukiangalia katika kada za utumishi wa umma walimu wamepewa kipaumbele cha hali ya juu na bado hatutasita kufanya hivyo. Mheshimiwa Naibu Spika,nimhakikishie tu Mheshimiwa Mbunge, tumeanza zoezi la tathmini ya kazi, tunaangalia uzito, majukumu na aina za kazi kwa ujumla wake katika Utumishi wa Umma na posho zipi zitatakiwa kuwepo katika kada gani. Nimuombe Mheshimiwa Mbunge aendelee kuvuta subira, zoezi hilo la tathmini ya kazi litakamilika katika mwaka huu wa fedha na baada ya hapo tutaweza kuainisha na kupitia na kuhuisha miundo mbalimbali ya kiutumishi vilevile kuangalia ni posho zipi ambazo zinahitajika kuwepo ikiwemo na hiyo ya Teaching Allowance kwa mapana yake. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Daimu Mpakate, swali la nyongeza. 5 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. DAIMU I. MPAKATE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Makaimu Watendaji wa Vijiji karibu maeneo mengi ya Tanzania hawapewi posho. Je, Serikali haioni haja ya kuwapa posho Makaimu Watendaji wa Vijiji ili waweze kufanya kazi zao vizuri? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Naibu Spika, anachosema Mheshimiwa Mpakate ni kwamba katika maeneo mbalimbali ya vijiji vyetu watu wengi wanakaimu na kuna maeneo mengine walimu ndiyo walikuwa wanakaimu kama Watendaji wa Vijiji na tumetoa maelekezo katika Kurugenzi zetu kuacha kukaimisha Watendaji wa Vijiji hasa wale walimu kwa sababu wanaondoa nguvu kubwa sana ya ufundishaji. Katika jambo hili, kila Halmashauri tumeipa maelekezo na kila Mkurugenzi anajua ana watu wangapi wanakaimu sasa kupitia own source zao wataangalia utaratibu gani wa kufanya lakini lengo kubwa tunataka katika kila kijiji kazi ziweze kufanyika. NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea. Mheshimiwa Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa, Mbunge wa Viti Maalum sasa aulize swali lake. Na. 235 Kupandisha Madaraja Walimu Wanaojiendeleza MHE. DKT. MARY M. MWANJELWA aliuliza:- Je, nini mkakati na sera ya Serikali kwa wafanyakazi hususani walimu wanaojiendeleza katika kuwapandisha madaraja na kuwaongezea mishahara? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu. 6 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Mary Machuche Mwanjelwa, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa Kanuni za Kudumu za Utumishi wa Umma za 2009, watumishi wa umma hupandishwa vyeo kwa kuzingatia sifa na ufanisi na utendaji kazi. Mwalimu anapohitimu mafunzo yake anastahili kubadilishiwa muundo wake wa utumishi mfano, Mwalimu Daraja la III - Stashahada kwenda Daraja la II ngazi ya Shahada. Kupanda daraja kwa mtumishi kunategemea utendaji kazi utakaothibitishwa na matokeo katika Mfumo wa Wazi wa Upimaji Utendaji Kazi wa mtumishi husika yaani OPRAS system. Watumishi wote wanatakiwa kujaza fomu hizo na kupimwa utendaji wao wa kazi kama wanastahili kupandishwa daraja.

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    373 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us