Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Sita

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Sita Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Arobaini – Tarehe 28 Julai, 2009 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. MHE. MOHAMMED AMOUR CHOMBOH (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA VIWANDA NA BIASHARA): Taarifa ya Kamati ya Viwanda na Biashara kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko kwa Mwaka 2008/2009 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. MHE. KHADIJA SALUM ALLY AL-QASSMY (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO):- Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Randama za Makadirio ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. MASWALI NA MAJIBU 1 Na. 289 Mabaraza ya Ardhi ya Kata MHE. DR. FESTUS B. LIMBU aliuliza:- Kwa kuwa, Serikali imeanzisha Mabaraza ya Ardhi ya Kata katika Jimbo la Magu:- (a) Je, ni zipi stahili za Wajumbe wa Mabaraza hayo na wanasimamiwa na chombo gani? (b) Je, ni lini Wajumbe hao watapatiwa semina? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dokta Festus Bulugu Limbu, Mbunge wa Magu, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a)Mheshimiwa Mwenyekiti, Mabaraza ya Ardhi ya Kata ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria Mabaraza ya Kata sura ya 206 toleo la mwaka 2002. Pamoja na majukumu yake ya kawaida Mabaraza ya Kata yana madaraka ya kupokea na kusikiliza rufaa za migogoro ya ardhi kutoka katika Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji ambavyo vimo katika Kata husika. Mheshimiwa Mwenyekiti, stahili za Wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi ya Kata katika Jimbo la Magu ni kama ilivyo katika Wilaya zingine nchini. Kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 1999, na kama ilivyofafanuliwa na mwongozo wa sheria za Mahakama ya Ardhi wa mwaka 2005, posho za Wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi ya Kata zitalipwa kwa viwango vya sheria ya fedha ya Serikali za mitaa ya mwaka 1982. Chanzo cha fedha za posho zitakazotokana na vyanzo vya mapato vya mabaraza ya Kata kama vile faini gharama za kesi na mchango wa Halmashauri na wadau wengine. mabaraza haya yanasimamiwa na Halmashauri za Wilaya husika. Mpaka tulipokuwa tunaingia katika kikao hiki Wajumbe wa Baraza hili katika Wilaya ya Magu walikuwa wamepewa shilingi elfu kumi na nne ambayo ilikuwa ni flat rate (b)Mheshimiwa Mwenyekiti, Mabaraza ya Ardhi ya Kata katika Wilaya ya Magu yalipewa semina juu ya uendeshaji wa mabaraza haya katika mwaka wa fedha 2007/2008. Semina hizo ziliendeshwa na wawezeshaji kutoka katika ngazi ya Wilaya na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Wawezeshaji hawa walikuwa wa fani za ardhi, sheria na rasilimali watu. Baada ya mafunzo mabaraza haya yalipewa vitendea kazi vya msingi kama vile majalada au mafaili na karatasi. Kwa kuwa 2 muda wa kazi wa Wajumbe wa mabaraza haya ni miaka mitatu, Halmashauri ya Wilaya ya Magu itaendelea kutoa elimu na vitendea kazi vya msingi kwa Mabaraza haya ili kuongeza ufanisi katika utendaji . (c)Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu swali Na. 68 la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa Mbunge wa Namtumbo kwenye Mkutano wa Nane wa Bunge lako Tukufu, napenda kuzihimiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha uanzishwaji wa mabaraza hayo kwa kila Kata na Kijiji unafanyika. Vilevile ziandae mipango maalum ya kuwaelimisha na kuwawezesha watendaji wa mabaraza hayo katika kutekeleza majukumu yao. Hii ni pamoja na utoaji wa elimu kwa umma juu ya utumiaji wa mabaraza hayo.(Makofi) MHE. DR. FESTUS B. LIMBU: Mheshimiwa Mwenyekiti namshukuru sana Waziri kwa majibu mazuri, lakini naomba niulize maswali mawili ya nyongeza:- (a)Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri haoni kwamba kuruhusu Mabaraza haya kujilipa kutokana na faini itabidi waongeze sana faini ili wapate pesa za kujilipa, haoni kwamba hiyo ni hatari? (b)Mheshimiwa Mwenyekiti, toka mwaka 1974 ambapo vilianzishwa vijiji vya ujamaa mashamba yaligawiwa upya na baadhi ya watu wakawa wamehama, sasa hivi wanaanza kurudi kudai maeneo yaliyokuwa ya kwao wakati tayari yalishagawiwa na Serikali za vijiji kwa wananchi wapya, huo ni mgogoro mkubwa. Mheshimiwa Waziri anatoa kauli gani kuhusu hali hiyo?(Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, unaporuhusu watu walete vitu na pesa zinazopatikana katika kesi ile ndizo zitakazotumika kulipa mabaraza, mimi sidhani kama hili linawezekana kwa sababu katika haya mabaraza kipo kiwango cha mwisho kinachotamkwa pale kwamba ni shilingi elfu kumi. Kwa hiyo hata kama watataka wawatoze sana ili ziongezeke kule wakapate ishirini hakuna, utaratibu huu mwisho wake ni shilingi elfu kumi hawawezi kufanya kinyume cha hapo. Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili kuhusu mgogoro wa ardhi kwamba ardhi ilishagawanywa halafu baadaye tena inachukuliwa inapelekwa kwenye kesi, Mabaraza haya yanaanzia kwenye vijiji yanakwenda kwenye Kata na yanapotoka kwenye Kata yanakwenda kwenye Wilaya na moja kwa moja kesi zile zinakwenda Mahakama Kuu. Huu anaosema kwamba unakuwa ni mgogoro mkubwa maana yake ni kwamba kama kuna mtu yeyote anayetaka kulalamika atakwenda katika hatua hiyo kulingana na ukubwa wa mgogoro unaozungumzwa hapo. Na. 290 3 Kuboresha Kituo cha Afya cha Nanjirinji –Kilwa MHE. HASNAIN G. DEWJI aliuliza:- Kwa kuwa, Kituo cha Afya kilichopo Nanjirinji Wilayani Kilwa kimeanza kutoa huduma lakini mpaka sasa hakina dawa, wataalam na gari la wagonjwa. Je, Serikali ina mpango gani wa kukiboresha kituo hicho ili kiweze kutoa huduma kwa ufanisi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hasnain Gulamabas Dewji, Mbunge wa Kilwa Kusini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kituo cha Nanjirinji kilichojengwa kwa masaada wa TASAF na nguvu za wananchi kilikamilika mwishoni mwa mwaka 2008. Kituo hicho kinahudumia wananchi wapatao 35,000 na kinapokea rufaa kutoka kwenye zahanati za Nakiu, Likawage na Nainokwe. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Watumishi; Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kama ilivyo katika maeneo mengi hapa nchini ina upungufu wa Watumishi. Kama alivyoeleza jana Mheshimiwa Waziri wa Afya, wastani wa upungufu wa watumishi wa Afya Kitaifa ni asilimia 62. Idara ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ina watumishi 24 tu wakati mahitaji halisi ya Idara ni watumishi 689 kwa mujibu wa Ikama. Kituo cha Afya cha Nanjirinji kina watumishi saba ambao ni Mganga (Clinical Officer) mmoja, Muuguzi Mkunga mmoja na wahudumu wa Afya watano. Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya madawa katika Halmashauri ni nzuri, vituo vya Afya na zahanati kwa kupitia mpango mpya wa kuagiza madawa yanayohitajika (Integrated Logistic System –ILS) huagiza MSD na kupata mgao kila robo mwaka. Kituo kilipata mgao wake kama kawaida mwezi Disemba 2008 na mara ya mwisho ilikuwa mwezi Aprili 2009. Mgao unaofuata wa Julai unategemewa wakati wowote. Sasa hivi uagizwaji umeshafanywa na Mfamasia wa Wilaya. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa inao mpango wa kuboresha huduma katika kituo hicho. Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imewasilisha maombi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kuongezewa watumishi wenye sifa kwa mujibu wa Ikama. 4 Katika kuboresha huduma kwenye kituo hicho, Halmashauri itahamishwa wahudumu wa afya wawili kutoka Hospitali ya Wilaya kupelekwa Kituo cha Afya Nanjirinji mwezi Agosti, 2009. Vilevile, Halmashauri ina mpango wa kuongeza nyumba za watumishi kutoka nne zilizopo hadi sita katika Bajeti ya mwaka 2009/2010 ili kuongeza motisha kwa watumishi wanaopangwa kufanya kazi hapo. (Makofi) MHE. HASNAIN G. DEWJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mawili mazuri ya Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza; (a) Kwa kuwa, Nanjirinji ni porini na maeneo mengi ya vijiji vya jirani ni mbali na katika swali langu la msingi niliulizia gari la wagonjwa, naona Waziri amesahau kunijibu kuhusu umuhimu wa kuwa na magari ya wagonjwa. (b)Kwa kuwa, Lindi hakuna chuo cha kufundisha Manesi na Wakunga, Je, Serikali ina mpango gani kwa Mkoa wa Lindi kuwa na Chuo cha kufundishia Manesi na Wakunga NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, anachosema Mheshimiwa Dewji ni sahihi kwa sababu rekodi zetu hapa zinaonesha katika eneo lao kituo cha afya cha Njinjo kina ambulance, kituo cha afya Masoko kina ambulance, kituo cha afya cha Pande kina ambulance lakini kituo cha afya cha Nanjirinji hakina ambulance, kwa hiyo anachosema ni kweli. Mheshimiwa Mwenyekiti, hizo kilomita anazozisema ni nyingi nimezitafuta zinaonesha kwamba kutoka Masoko Kivinje ni kilomita 190 ambako ndiko kuna hospitali ya Wilaya. Vile vile ipo karibu na hospitali ya Ruango wanakwenda kilomita 70. Kwa hiyo ni kweli anachosema Mheshimiwa Mbunge. Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kuna zoezi linalofanyika la ambulance nitamshauri Waziri Mkuu na Waziri wa Nchi ili tuone uwezekano wa kupatiwa ambulance kwa sababu kwa kweli wana tatizo hawa. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante sana, namwona
Recommended publications
  • Jamhuri Ya Muungano Wa Tanzania Bunge La Tanzania
    JAMHURI YA MUUNGANO WA TANZANIA BUNGE LA TANZANIA MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI NA SABA YATOKANAYO NA KIKAO CHA KUMI NA NNE (DAILY SUMMARY RECORD OF PROCEEDINGS) 21 NOVEMBA, 2014 MKUTANO WA KUMI NA SITA NA KUMI SABA KIKAO CHA KUMI NA NNE – 21 NOVEMBA, 2014 I. DUA Mwenyekiti wa Bunge Mhe. Mussa Azzan Zungu alisoma Dua saa 3.00 Asubuhi na kuliongoza Bunge. MAKATIBU MEZANI – i. Ndg. Asia Minja ii. Ndg. Joshua Chamwela II. MASWALI: Maswali yafuatayo yaliulizwa na wabunge:- 1. OFISI YA WAZIRI MKUU Swali Na. 161 – Mhe. Betty Eliezer Machangu [KNY: Mhe. Dkt. Cyril Chami] Nyongeza i. Mhe. Betty E. Machangu, mb ii. Mhe. Michael Lekule Laizer, mb iii. Mhe. Prof. Peter Msolla, mb Swali Na. 162 - Mhe. Richard Mganga Ndassa, mb Nyongeza (i) Mhe Richard Mganga Ndassa, mb Swali Na. 163 - Mhe. Anne Kilango Malecela, mb Nyongeza : i. Mhe. Anne Kilango Malecela, mb ii. Mhe. John John Mnyika, mb iii. Mhe. Mariam Nassor Kisangi iv. Mhe. Iddi Mohammed Azzan, mb 2 2. OFISI YA RAIS (UTUMISHI) Swali Na. 164 – Mhe. Ritta Enespher Kabati, mb Nyongeza i. Mhe. Ritta Enespher Kabati, mb ii. Mhe. Vita Rashid Kawawa, mb iii. Mhe. Mch. Reter Msingwa, mb 3. WIZARA YA UJENZI Swali Na. 165 – Mhe. Betty Eliezer Machangu, mb Nyongeza :- i. Mhe. Betty Eliezer Machangu, mb ii. Mhe. Halima James Mdee, mb iii. Mhe. Maryam Salum Msabaha, mb Swali Na. 166 – Mhe. Peter Simon Msingwa [KNY: Mhe. Joseph O. Mbilinyi] Nyongeza :- i. Mhe. Peter Simon Msigwa, Mb ii. Mhe. Assumpter Nshunju Mshama, Mb iii. Mhe. Dkt. Mary Mwanjelwa 4.
    [Show full text]
  • Online Document)
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA ISHIRINI Kikao cha Arobaini na Sita – Tarehe 8 Julai, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa Z. Azzan) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, maswali na tunaanza na ofisi ya Waziri, Mheshimiwa Kayombo, kwa niaba yake Mheshimiwa Rage. Na. 321 Ofisi kwa ajili ya Tarafa-Mbinga MHE. ISMAIL A. RAGE (K.n.y. MHE. GAUDENCE C. KAYOMBO) aliuliza:- Wilaya ya Mbinga ina tarafa sita lakini tarafa zote hazina ofisi rasmi zilizojengwa:- Je, ni lini Serikali itajenga ofisi kwa Makatibu Tarafa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Gaudence Cassian Kayombo, Mbunge wa Mbinga Mashariki kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, Mkoa wa Ruvuma una jumla ya tarafa 24 yaani Tunduru wako saba, Mbinga wana tarafa sita, Nyasa wana tarafa tatu, Namtumbo wana tarafa tatu na Songea wana tarafa tano. Ni kweli tarafa za Wilaya ya Mbinga hazina ofisi rasmi zilizojengwa na Serikali. Ujenzi wa hizo ofisi unafanyika kwa awamu kulingana na upatikanaji wa fedha. Kwa sasa Mkoa wa Ruvuma umeweka kipaumbele katika ujenzi wa ofisi nne za tarafa katika Wilaya ya Nyasa na Tunduru. Tarafa hizo ni Luhuhu (Lituhi-Nyasa), Ruhekei (Mbamba bay-Nyasa), Mpepo (Tinga-Nyasa) na Nampungu (Nandembo-Tunduru). Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka wa fedha wa 2014/2015, Mkoa ulitenga shilingi milioni mia tatu kwa ajili ya ujenzi wa ofisi ya Tarafa ya Luhuhu (Lituhi), Ruhekei (Mbamba bay), Mpepo (Tingi) na Nampungu (Nandembo).
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 112 Sept - Dec 2015
    Tanzanian Affairs Issued by the Britain-Tanzania Society No 112 Sept - Dec 2015 ELECTION EDITION: MAGUFULI vs LOWASSA Profiles of Key Candidates Petroleum Bills Ruaha’s “Missing” Elephants ta112 - final.indd 1 8/25/2015 12:04:37 PM David Brewin: SURPRISING CHANGES ON THE POLITICAL SCENE As the elections approached, during the last two weeks of July and the first two weeks of August 2015, Tanzanians witnessed some very dra- matic changes on the political scene. Some sections of the media were even calling the events “Tanzania’s Tsunami!” President Kikwete addessing the CCM congress in Dodoma What happened? A summary 1. In July as all the political parties were having difficulty in choosing their candidates for the presidency, the ruling Chama cha Mapinduzi (CCM) party decided to steal a march on the others by bringing forward their own selection process and forcing the other parties to do the same. 2. It seemed as though almost everyone who is anyone wanted to become president. A total of no less than 42 CCM leaders, an unprec- edented number, registered their desire to be the party’s presidential candidate. They included former prime ministers and ministers and many other prominent CCM officials. 3. Meanwhile, members of the CCM hierarchy were gathering in cover photos: CCM presidential candidate, John Magufuli (left), and CHADEMA / UKAWA candidate, Edward Lowassa (right). ta112 - final.indd 2 8/25/2015 12:04:37 PM Surprising Changes on the Political Scene 3 Dodoma to begin the lengthy and highly competitive selection process. 4. The person who appeared to have the best chance of winning for the CCM was former Prime Minister Edward Lowassa MP, who was popular in the party and had been campaigning hard.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    NAKALA YA MTANDAO (ON LINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ BUNGE LA KUMI NA MOJA ___________ MKUTANO WA KWANZA Kikao cha Kwanza - Tarehe 17 Novemba, 2015 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) DKT. THOMAS D. KASHILILAH - KATIBU WA BUNGE: Naomba tukae. TANGAZO LA RAIS LA KUITISHA MKUTANO WA BUNGE DKT. THOMAS D. KASHILILAH - KATIBU WA BUNGE: Waheshimiwa Wabunge, kwa mujibu wa masharti ya Katiba, Mkutano huu wa Kwanza unaanza kwa Rais kuuitisha. Naomba kuchukua nafasi hii kusoma Tangazo la Rais kama ambavyo tumelipokea. Tangazo la Serikali Na. 513 la tarehe 6 Novemba, 2015. Kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Sura ya Pili, hati iliyotolewa kwa mujibu wa Ibara ya 90(1). Hati ya Kuitisha Mkutano wa Bunge Jipya. KWA KUWA, Uchaguzi Mkuu ulifanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 katika Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977; NA KWA KUWA, masharti ya Ibara ndogo ya kwanza ya Ibara ya 90 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, yanamtaka Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kuitisha Mkutano wa Bunge Jipya kabla ya kupita siku saba tangu Tume ya Uchaguzi kutangaza matokeo ya Uchaguzi Mkuu; NA KWA KUWA, matokeo ya Uchaguzi Mkuu uliofanyika tarehe 25 Oktoba, 2015 yalitangazwa na Tume ya Taifa ya Uchaguzi tarehe 29 Oktoba, 2015; HIVYO BASI, mimi John Pombe Joseph Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa mamlaka niliyonayo chini ya Ibara ya 90(1) ya 1 NAKALA YA MTANDAO (ON LINE DOCUMENT) Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania ya mwaka 1977, naitisha Mkutano wa Bunge Jipya la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ufanyike katika ukumbi wa Bunge uliopo Mjini Dodoma tarehe 17 Novemba, 2015 kuanzia saa tatu asubuhi.
    [Show full text]
  • Ruaha Journal of Business, Economics and Management Sciences, Vol.1, Issue 1, 2018  Ms Hadija Matimbwa , Faculty of Business and Management Science, RUCU Iii
    RUAHA JOURNAL of Business, Economics and Management Sciences Faculty of Business and Management Sciences Vol 1, Issue 1, 2018 A. Editorial Board i. Executive Secretarial Members Chairman: Dr. Alex Juma Ochumbo, Dean Faculty of Business and Management Sciences, RUCU Chief Editor: Prof. Robert Mabele, Faculty of Business and Management Sciences, RUCU Managing Editor: Dr.Venance Ndalichako, Faculty of Business and Management Sciences, RUCU Business Manager: Dr. Alberto Gabriel Ndekwa, Faculty of Business and Management Science, RUCU Secretary to the Board: Ms. Hawa Jumanne,Faculty of Business and Management Science, RUCU ii. Members of the Editorial Board Dr. Dominicus Kasilo, Faculty of Business and Management Science, RUCU Bishop Dr. Edward Johnson Mwaikali,Bishop of Mbeya, Formerly with RUCU Dr. Theobard Kipilimba, Faculty of Business and Management Science, RUCU Dr. Esther Ikasu, Faculty of Business and Management Science, RUCU ii Ruaha Journal of Business, Economics and Management Sciences, Vol.1, Issue 1, 2018 Ms Hadija Matimbwa , Faculty of Business and Management Science, RUCU iii. Associate Editors Prof. Enock Wicketye Iringa University,Tanzania. Dr. Enery Challu University of Dar es Dr. Ernest Abayo Makerere University, Uganda. Dr. Vicent Leyaro University of Dar es Salaam Dr. Hawa Tundui Mzumbe University, Tanzania. B. Editorial Note Ruaha Journal of Business, Economics and Management Sciences would like to wish all our esteemed readers on this first appearance A HAPPY NEW YEAR. We shall be appearing twice a year January and July. We hope you will be able to help us fulfill this pledge by feeding us with journal articles, book reviews and other such journal writings and stand ready to read from cover to cover all our issues.
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 114 May - Aug 2016
    Tanzanian Affairs Issued by the Britain-Tanzania Society No 114 May - Aug 2016 Magufuli’s “Cleansing” Operation Zanzibar Election Re-run Nyerere Bridge Opens David Brewin: MAGUFULI’S “CLEANSING” OPERATION President Magufuli helps clean the street outside State House in Dec 2015 (photo State House) The seemingly tireless new President Magufuli of Tanzania has started his term of office with a number of spectacular measures most of which are not only proving extremely popular in Tanzania but also attracting interest in other East African countries and beyond. It could be described as a huge ‘cleansing’ operation in which the main features include: a drive to eliminate corruption (in response to widespread demands from the electorate during the November 2015 elections); a cutting out of elements of low priority in the expenditure of government funds; and a better work ethic amongst government employees. The President has changed so many policies and practices since tak- ing office in November 2015 that it is difficult for a small journal like ‘Tanzanian Affairs’ to cover them adequately. He is, of course, operat- ing through, and with the help of ministers, regional commissioners and cover photo: The new Nyerere Bridge in Dar es Salaam (see Transport) Magufuli’s “Cleansing” Operation 3 others, who have been either kept on or brought in as replacements for those removed in various purges of existing personnel. Changes under the new President The following is a list of some of the President’s changes. Some were not carried out by him directly but by subordinates. It is clear however where the inspiration for them came from.
    [Show full text]
  • Bunge Newsletter
    BungeNe ewsletter Issue No 008 June 2013 New Budget Cycle Shows Relavance For the first time in recent Tanzania history the engage the government and influence it make sev- Parliament has managed to pass the next financial eral tangible changes in its initial budget proposals. year budget before the onset of that particular year. This has been made possible by the Budget Commit- This has been made possi- tee, another new innovation by Speaker Makinda. ble by adoption of new budget cycle. Under the old cycle, it was not possible to influence According to the new budget cycle, the Parliament the government to make changes in budgetary allo- starts discussing the budget in April as opposed to cations. That was because the main budget was read, old cycle where debate on the new budget started on debated and passed before the sectoral plans. After June and ends in the first or second week of August. the main budget was passed, it was impossible for the MPs and government to make changes in the When the decision was taken to implement the new sectoral budgets since they were supposed to reflect budget cycle and Speaker Anne Makinda announced the main budget which had already been passed. the new modalities many people, including Mem- bers of Parliament, were skeptical. Many stakehold- These and many other changes have been made possi- ers were not so sure that the new cycle would work. ble through the five components implemented under the Parliament five years development plan. “Govern- But Ms Makinda has managed to prove the doubt- ment and Budget Oversight and Accountability is one ers wrong.
    [Show full text]
  • 1458125471-Hs-6-8-20
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA TATU Kikao Cha Thelathini Na Saba
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ______________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Thelathini na Saba – Tarehe 6 Juni, 2016 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu! NDG. ZAINAB ISSA - KATIBU MEZANI: Maswali. MASWALI NA MAJIBU Na. 303 Upanuzi wa Hospitali ya Mkoa wa Pwani MHE. SILVESTRY F. KOKA aliuliza:- Upanuzi wa hospitali ya Mkoa ya Pwani ijulikanayo kama Hospitali ya Tumbi umesimama kwa takribani miaka mitatu, sasa nondo na zege la msingi na nguzo zinaoza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kukamilisha ujenzi wa hospitali hiyo ili kuondoa hasara na kuleta tija katika huduma ya afya Kibaha? 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Silvestry Francis Koka, Mbunge wa Kibaha Mjini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua changamoto zinazoikabili hospitali ya rufaa ya Tumbi – Kibaha ambazo zimesababishwa kwa sehemu kubwa na ufinyu wa majengo ya kutolea huduma na uchache wa vifaa tiba. Hadi sasa Serikali imetumia shilingi bilioni 5.98 kwa ajili ya upanuzi wa hospitali hiyo. Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali katika bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 imetenga shilingi bilioni 1.4 kwa ajili ya kuendeleza upanuzi wa hospitali ya Tumbi Kibaha ili kuboresha huduma za afya kwa wananchi. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Silvestry Koka, swali la nyongeza. MHE. SILVESTRY F. KOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, nashukuru. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali na kwa niaba ya wananchi wa Kibaha nishukuru kwa kutupatia hiyo 1.4 bilioni katika upanuzi wa hospitali hii, nina maswali mawili ya nyongeza.
    [Show full text]
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who Will Benefit from the Gas Economy, If It Happens?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013 Who will benefit from the gas economy, if it happens? Supported by: 2 TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? ACKNOWLEDGEMENTS Policy Forum would like to thank the Foundation for Civil Society for the generous grant that financed Tanzania Governance Review 2013. The review was drafted by Tanzania Development Research Group and edited by Policy Forum. The cartoons were drawn by Adam Lutta (Adamu). Tanzania Governance Reviews for 2006-7, 2008-9, 2010-11, 2012 and 2013 can be downloaded from the Policy Forum website. The views expressed and conclusions drawn on the basis of data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. TGRs review published and unpublished materials from official sources, civil society and academia, and from the media. Policy Forum has made every effort to verify the accuracy of the information contained in TGR2013, particularly with media sources. However, Policy Forum cannot guarantee the accuracy of all reported claims, statements, and statistics. Whereas any part of this review can be reproduced provided it is duly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. ISBN:978-9987-708-19-2 For more information and to order copies of the report please contact: Policy Forum P.O. Box 38486 Dar es Salaam Tel +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] Suggested citation: Policy Forum 2015.
    [Show full text]
  • Bunge La Tanzania
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Kwanza – Tarehe 9 Juni, 2009 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) WIMBO WA TAIFA (Hapa Wabunge Waliimba Wimbo wa Taifa) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta ) Alisoma Dua KIAPO CHA UAMINIFU Mbunge afuataye aliapa Kiapo cha Uaminifu na kukaa katika nafasi yake Bungeni:- Mheshimiwa Lolensia Jeremiah Maselle Bukwimba SPIKA: Ahsante sana, leo shamrashamra zimepita kiasi; nimetafuta ushauri wa sheria bado sijapewa kuhusu shamrashamra hizi kwa kiwango hiki kama inaruhusiwa kwa kanuni lakini hayo sasa ni ya baadaye. (Kicheko) T A A R I F A Y A S P I K A SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, katika Mkutano wa Kumi na Tano wa Bunge hili, tulipitisha Miswada mitano ya sheria iitwayo The Human DNA Regulation Bill, 2009, The Fertilizers Bill, 2009, The Insurance Bill, 2009, The Water Resources Management Bill, 2009 na The Water Supply and Sanitation Bill, 2009. Mara baada ya kupitishwa na Bunge na baadae kupita katika hatua zake zote za uchapishaji, Miswada hiyo ilipelekwa kwa Mheshimiwa Rais ili kupata kibali chake kwa mujibu wa Katiba. Kwa taarifa hii, nafurahi kuwaarifu Wabunge wote na Bunge hili Tukufu kwamba, tayari Mheshimiwa Rais amekwishatoa kibali kwa Miswada yote hiyo mitano na sasa ni sheria za nchi, ambapo The Human DNA Regulation Act, 2009 inakuwa ni Sheria Namba Nane ya Mwaka 2009; The Fertilizers Act, 2009 ni Sheria Namba Tisa ya 1 Mwaka 2009; The Insurance Act, 2009 ni Namba Kumi ya Mwaka 2009; The Water Resources Management, Act 2009 ni Namba Kumi na Moja ya Mwaka 2009; na Sheria Namba Kumi na Mbili ya Mwaka 2009 ni ile ya Water Supply and Sanitation Act, 2009.
    [Show full text]
  • Hotuba Ya Bajeti Ya Wizara Ya Mambo Ya Nje 2012/2013 Posted: Monday August 06, 2012 1:06 PM BT
    Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje 2012/2013 Posted: Monday August 06, 2012 1:06 PM BT HOTUBA YA WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA MHESHIMIWA BERNARD KAMILLIUS MEMBE (MB.), AKIWASILISHA BUNGENI MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO W A KIMATAIFA KWA MWAKA WA FEDHA 2012/2013 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, kufuatia taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kudumu ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), naomba sasa kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu lipokee, lijadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa mwaka wa fedha 2012/2013. 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote napenda kutumia fursa hii kukupongeza wewe binafsi kwa kuliongoza kwa umahiri mkubwa Bunge hili la Bajeti la mwaka 2012/2013. Napenda pia kuwapongeza Mheshimiwa Job Ndugai (Mb.), Naibu Spika na Waheshimiwa Wenyeviti wanaokusaidia kuongoza Bunge hili kwa kazi nzuri wanayoifanya. 3. Mheshimiwa Spika, kwa namna ya pekee nachukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, kwa uongozi wake mahiri wa Serikali ya Awamu ya Nne. Chini ya uongozi wake Taifa letu limeendeleza utamaduni wetu wa kudumisha amani, utulivu na mshikamano. Nawaomba Watanzania wote tuendelee kudumisha hali hiyo ili kuimarisha umoja wetu ambao ni tunu isiyopatikana kwa bei yoyote. 4. Mheshimiwa Spika, niruhusu niungane na Waheshimiwa Wabunge wengine wote walionitangulia kuwapongeza kwa dhati kabisa Waheshimiwa Wabunge wapya, Mawaziri na Naibu Mawaziri walioteuliwa na Mheshimiwa Rais mwezi Mei 2012. Nawapongeza Wenyeviti na Makamu Wenyeviti wa Kamati za Kudumu za Bunge waliochaguliwa kipindi hiki kutokana na mabadiliko yaliyotokea kwenye nafasi mbalimbali humu Bungeni na ndani ya Serikali.
    [Show full text]