Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Sita

Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Sita

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _____________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Arobaini – Tarehe 28 Julai, 2009 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. MHE. MOHAMMED AMOUR CHOMBOH (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA VIWANDA NA BIASHARA): Taarifa ya Kamati ya Viwanda na Biashara kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko kwa Mwaka 2008/2009 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. MHE. KHADIJA SALUM ALLY AL-QASSMY (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO):- Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Viwanda, Biashara na Masoko kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. NAIBU WAZIRI WA AFYA NA USTAWI WA JAMII: Randama za Makadirio ya Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. MASWALI NA MAJIBU 1 Na. 289 Mabaraza ya Ardhi ya Kata MHE. DR. FESTUS B. LIMBU aliuliza:- Kwa kuwa, Serikali imeanzisha Mabaraza ya Ardhi ya Kata katika Jimbo la Magu:- (a) Je, ni zipi stahili za Wajumbe wa Mabaraza hayo na wanasimamiwa na chombo gani? (b) Je, ni lini Wajumbe hao watapatiwa semina? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dokta Festus Bulugu Limbu, Mbunge wa Magu, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a)Mheshimiwa Mwenyekiti, Mabaraza ya Ardhi ya Kata ni chombo ambacho kimeundwa kwa mujibu wa Sheria Mabaraza ya Kata sura ya 206 toleo la mwaka 2002. Pamoja na majukumu yake ya kawaida Mabaraza ya Kata yana madaraka ya kupokea na kusikiliza rufaa za migogoro ya ardhi kutoka katika Mabaraza ya Ardhi ya Vijiji ambavyo vimo katika Kata husika. Mheshimiwa Mwenyekiti, stahili za Wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi ya Kata katika Jimbo la Magu ni kama ilivyo katika Wilaya zingine nchini. Kwa mujibu wa Sheria ya Ardhi ya Vijiji Na. 5 ya mwaka 1999, na kama ilivyofafanuliwa na mwongozo wa sheria za Mahakama ya Ardhi wa mwaka 2005, posho za Wajumbe wa Mabaraza ya Ardhi ya Kata zitalipwa kwa viwango vya sheria ya fedha ya Serikali za mitaa ya mwaka 1982. Chanzo cha fedha za posho zitakazotokana na vyanzo vya mapato vya mabaraza ya Kata kama vile faini gharama za kesi na mchango wa Halmashauri na wadau wengine. mabaraza haya yanasimamiwa na Halmashauri za Wilaya husika. Mpaka tulipokuwa tunaingia katika kikao hiki Wajumbe wa Baraza hili katika Wilaya ya Magu walikuwa wamepewa shilingi elfu kumi na nne ambayo ilikuwa ni flat rate (b)Mheshimiwa Mwenyekiti, Mabaraza ya Ardhi ya Kata katika Wilaya ya Magu yalipewa semina juu ya uendeshaji wa mabaraza haya katika mwaka wa fedha 2007/2008. Semina hizo ziliendeshwa na wawezeshaji kutoka katika ngazi ya Wilaya na Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU). Wawezeshaji hawa walikuwa wa fani za ardhi, sheria na rasilimali watu. Baada ya mafunzo mabaraza haya yalipewa vitendea kazi vya msingi kama vile majalada au mafaili na karatasi. Kwa kuwa 2 muda wa kazi wa Wajumbe wa mabaraza haya ni miaka mitatu, Halmashauri ya Wilaya ya Magu itaendelea kutoa elimu na vitendea kazi vya msingi kwa Mabaraza haya ili kuongeza ufanisi katika utendaji . (c)Mheshimiwa Mwenyekiti, kama nilivyojibu swali Na. 68 la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa Mbunge wa Namtumbo kwenye Mkutano wa Nane wa Bunge lako Tukufu, napenda kuzihimiza Halmashauri zote nchini kuhakikisha uanzishwaji wa mabaraza hayo kwa kila Kata na Kijiji unafanyika. Vilevile ziandae mipango maalum ya kuwaelimisha na kuwawezesha watendaji wa mabaraza hayo katika kutekeleza majukumu yao. Hii ni pamoja na utoaji wa elimu kwa umma juu ya utumiaji wa mabaraza hayo.(Makofi) MHE. DR. FESTUS B. LIMBU: Mheshimiwa Mwenyekiti namshukuru sana Waziri kwa majibu mazuri, lakini naomba niulize maswali mawili ya nyongeza:- (a)Mheshimiwa Mwenyekiti, Waziri haoni kwamba kuruhusu Mabaraza haya kujilipa kutokana na faini itabidi waongeze sana faini ili wapate pesa za kujilipa, haoni kwamba hiyo ni hatari? (b)Mheshimiwa Mwenyekiti, toka mwaka 1974 ambapo vilianzishwa vijiji vya ujamaa mashamba yaligawiwa upya na baadhi ya watu wakawa wamehama, sasa hivi wanaanza kurudi kudai maeneo yaliyokuwa ya kwao wakati tayari yalishagawiwa na Serikali za vijiji kwa wananchi wapya, huo ni mgogoro mkubwa. Mheshimiwa Waziri anatoa kauli gani kuhusu hali hiyo?(Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, unaporuhusu watu walete vitu na pesa zinazopatikana katika kesi ile ndizo zitakazotumika kulipa mabaraza, mimi sidhani kama hili linawezekana kwa sababu katika haya mabaraza kipo kiwango cha mwisho kinachotamkwa pale kwamba ni shilingi elfu kumi. Kwa hiyo hata kama watataka wawatoze sana ili ziongezeke kule wakapate ishirini hakuna, utaratibu huu mwisho wake ni shilingi elfu kumi hawawezi kufanya kinyume cha hapo. Mheshimiwa Mwenyekiti, suala la pili kuhusu mgogoro wa ardhi kwamba ardhi ilishagawanywa halafu baadaye tena inachukuliwa inapelekwa kwenye kesi, Mabaraza haya yanaanzia kwenye vijiji yanakwenda kwenye Kata na yanapotoka kwenye Kata yanakwenda kwenye Wilaya na moja kwa moja kesi zile zinakwenda Mahakama Kuu. Huu anaosema kwamba unakuwa ni mgogoro mkubwa maana yake ni kwamba kama kuna mtu yeyote anayetaka kulalamika atakwenda katika hatua hiyo kulingana na ukubwa wa mgogoro unaozungumzwa hapo. Na. 290 3 Kuboresha Kituo cha Afya cha Nanjirinji –Kilwa MHE. HASNAIN G. DEWJI aliuliza:- Kwa kuwa, Kituo cha Afya kilichopo Nanjirinji Wilayani Kilwa kimeanza kutoa huduma lakini mpaka sasa hakina dawa, wataalam na gari la wagonjwa. Je, Serikali ina mpango gani wa kukiboresha kituo hicho ili kiweze kutoa huduma kwa ufanisi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Hasnain Gulamabas Dewji, Mbunge wa Kilwa Kusini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kituo cha Nanjirinji kilichojengwa kwa masaada wa TASAF na nguvu za wananchi kilikamilika mwishoni mwa mwaka 2008. Kituo hicho kinahudumia wananchi wapatao 35,000 na kinapokea rufaa kutoka kwenye zahanati za Nakiu, Likawage na Nainokwe. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa upande wa Watumishi; Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa kama ilivyo katika maeneo mengi hapa nchini ina upungufu wa Watumishi. Kama alivyoeleza jana Mheshimiwa Waziri wa Afya, wastani wa upungufu wa watumishi wa Afya Kitaifa ni asilimia 62. Idara ya Afya katika Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa ina watumishi 24 tu wakati mahitaji halisi ya Idara ni watumishi 689 kwa mujibu wa Ikama. Kituo cha Afya cha Nanjirinji kina watumishi saba ambao ni Mganga (Clinical Officer) mmoja, Muuguzi Mkunga mmoja na wahudumu wa Afya watano. Mheshimiwa Mwenyekiti, hali ya madawa katika Halmashauri ni nzuri, vituo vya Afya na zahanati kwa kupitia mpango mpya wa kuagiza madawa yanayohitajika (Integrated Logistic System –ILS) huagiza MSD na kupata mgao kila robo mwaka. Kituo kilipata mgao wake kama kawaida mwezi Disemba 2008 na mara ya mwisho ilikuwa mwezi Aprili 2009. Mgao unaofuata wa Julai unategemewa wakati wowote. Sasa hivi uagizwaji umeshafanywa na Mfamasia wa Wilaya. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali kupitia Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa inao mpango wa kuboresha huduma katika kituo hicho. Halmashauri ya Wilaya ya Kilwa imewasilisha maombi Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi wa Umma, kuongezewa watumishi wenye sifa kwa mujibu wa Ikama. 4 Katika kuboresha huduma kwenye kituo hicho, Halmashauri itahamishwa wahudumu wa afya wawili kutoka Hospitali ya Wilaya kupelekwa Kituo cha Afya Nanjirinji mwezi Agosti, 2009. Vilevile, Halmashauri ina mpango wa kuongeza nyumba za watumishi kutoka nne zilizopo hadi sita katika Bajeti ya mwaka 2009/2010 ili kuongeza motisha kwa watumishi wanaopangwa kufanya kazi hapo. (Makofi) MHE. HASNAIN G. DEWJI: Mheshimiwa Mwenyekiti, nashukuru kwa majibu mawili mazuri ya Naibu Waziri, nina maswali mawili ya nyongeza; (a) Kwa kuwa, Nanjirinji ni porini na maeneo mengi ya vijiji vya jirani ni mbali na katika swali langu la msingi niliulizia gari la wagonjwa, naona Waziri amesahau kunijibu kuhusu umuhimu wa kuwa na magari ya wagonjwa. (b)Kwa kuwa, Lindi hakuna chuo cha kufundisha Manesi na Wakunga, Je, Serikali ina mpango gani kwa Mkoa wa Lindi kuwa na Chuo cha kufundishia Manesi na Wakunga NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Mwenyekiti, anachosema Mheshimiwa Dewji ni sahihi kwa sababu rekodi zetu hapa zinaonesha katika eneo lao kituo cha afya cha Njinjo kina ambulance, kituo cha afya Masoko kina ambulance, kituo cha afya cha Pande kina ambulance lakini kituo cha afya cha Nanjirinji hakina ambulance, kwa hiyo anachosema ni kweli. Mheshimiwa Mwenyekiti, hizo kilomita anazozisema ni nyingi nimezitafuta zinaonesha kwamba kutoka Masoko Kivinje ni kilomita 190 ambako ndiko kuna hospitali ya Wilaya. Vile vile ipo karibu na hospitali ya Ruango wanakwenda kilomita 70. Kwa hiyo ni kweli anachosema Mheshimiwa Mbunge. Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa hivi kuna zoezi linalofanyika la ambulance nitamshauri Waziri Mkuu na Waziri wa Nchi ili tuone uwezekano wa kupatiwa ambulance kwa sababu kwa kweli wana tatizo hawa. (Makofi) MWENYEKITI: Ahsante sana, namwona

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    221 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us