Tarehe 2 Februari, 2021
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA PILI Kikao cha Kwanza – Tarehe 2 Februari, 2021 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) WIMBO WA TAIFA NA WIMBO WA JUMUIYA YA AFRIKA MASHARIKI (Hapa Kwaya ya Bunge Iliimba Wimbo wa Taifa na Wimbo wa Jumuiya ya Afrika Mashariki) SPIKA: Ahsante sana Kwaya yetu ya Bunge. Excellent. (Makofi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Naomba tukae. Wabunge wapya wabakie hapo nje mpaka tutakapowakaribisha. Wengine tuchukue nafasi zetu haraka. Waheshimiwa Wabunge, kabla hatujaanza kikao chetu, naomba kutoa pole kwenu wote kwa kuondokewa na Mbunge mwenzetu Mheshimiwa Marehemu Martha Jachi Umbulla, Mbunge wa Viti Maalum kutoka Mkoa wa Manyara aliyefariki tarehe 21 Januari, 2021 nchini India alikokwenda kwa ajili ya kupata matibabu na kuzikwa tarehe 26 Januari, 2021 nyumbani kwake Dongobesh, Mkoani Manyara. Waheshimiwa Wabunge, kwa heshima naomba tusimame kwa dakika moja tumwombee ili Mwenyezi Mungu ampumzishe kwa amani. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (Hapa Waheshimiwa Wabunge walisimama kwa muda kwa ajili ya kumwombea Marehemu Mhe. Martha Jachi Umbulla) SPIKA: Bwana alitoa, Bwana ametwaa. Jina lake lihimidiwe. Amina. Tunaweza kukaa. Najua muda mrefu mmekuwa hamko pamoja, lakini hiyo isiwe sababu ya kutosikilizana ndugu zangu Waheshimiwa. Sasa mko Bungeni kila mmoja anayepiga story aache, anayegeuza kiti, aangalie mbele kwa Spika. Naomba tuwe na utulivu ndani ya ukumbi. Waheshimiwa Wabunge, baada ya kuahirisha Mkutano wa Kwanza wa Bunge kwa mujibu wa Kanuni ya 30(2)(b) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, kwa nyakati tofauti tofauti tulifanya shughuli za kuapisha Kiapo cha Uaminifu Wabunge 27 kuwa Wabunge wa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kama ifuatavyo:- Wabunge 19 Viti Maalum kutoka CHADEMA, Wabunge wanne wa Majimbo kutoka Chama cha ACT Wazalendo na Wabunge watano wa kuteuliwa na Rais. Sasa nawakaribisha humu ndani kwa kuanza na Wabunge watano wa kuteuliwa ambao ni Mheshimiwa Humphrey Polepole, Mheshimiwa Riziki Saidi Lulida, Mheshimiwa Dkt. Dorothy Onesphoro Gwajima, Mheshimiwa Dkt. Leonard Madaraka Chamuriho na Mheshimiwa Profesa Shukrani E. Manya. Wabunge hawa wa kuteuliwa watano naomba waingine ndani ya Ukumbi wa Bunge sasa. (Makofi) (Hapa Wabunge wa Kuteuliwa na Rais waliingia Ukumbini) SPIKA: Ahsante sana. Pia tuliwaapisha Wabunge wanne kutoka Chama cha ACT Wazalendo, nao nitawaomba waingie kama wako hapo nje, Mheshimiwa Khalifa Mohamed Issa, Mheshimiwa Khatib Said Haji, Mheshimiwa Omar Ali Omar na Mheshimiwa Salum Mohamed Shaafi. (Makofi) 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (Hapa Wabunge kutoka Chama cha ACT Wazalendo waliingia Ukumbini) SPIKA: Ahsanteni sana, pia tuliwaapisha Wabunge 19 wa Viti Maalum kutoka CHADEMA ambao naomba niwataje kwanza halafu ndiyo waingie; Mheshimiwa Halima James Mdee, Mheshimiwa Grace Victor Tendega, Mheshimiwa Esther Nicholaus Matiko, Mheshimiwa Cecilia Daniel Paresso, Mheshimiwa Ester Amos Bulaya, Mheshimiwa Agnesta Lambert Kaiza, Mheshimiwa Nusrat Shaaban Hanje, Mheshimiwa Jesca David Kishoa, Mheshimiwa Hawa Subira Mwaifunga, Mheshimiwa Tunza Issa Malapo, Mheshimiwa Asya Mohamed, Mheshimiwa Felista Deogratius Njau, Mheshimiwa Naghenjwa Livingstone Kaboyoka, Mheshimiwa Sophia Hezron Mwakagenda, Mheshimiwa Kunti Yusuph Majala, Mheshimiwa Stella Simon Fiyao, Mheshimiwa Anatropia Rweikiza Theonest, Mheshimiwa Salome Wycliffe Makamba na Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza. Sasa nawaomba waingie ndani ya ukumbi wa Bunge, wachukue nafasi ya viti vyao. (Makofi) (Hapa Wabunge wa Viti Maalum kutoka CHADEMA waliingia Ukumbini) SPIKA: Ahsante sana. Baada ya kuwakaribisha wenzetu hao ambao kwa niaba yenu ningependa kuwapongeza sana kwa kupata fursa ya kuwa Waheshimiwa Wabunge Kikatiba. Sasa tuendelee na shughuli. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU): Hotuba ya Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli aliyoitoa wakati wa ufunguzi wa Bunge la Kumi na Mbili, tarehe 13 Novemba, 2020. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Jenista Mhagama, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu. Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: Maswali. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla hamjaanza kuulizana maswali, nafikiri mnaweza mkauona ukumbi wetu kwa wale ambao mna jicho la kuweza kuangalia kumbukumbu mtaona kuna kazi kubwa sana ambayo imefanyika hapa. Huko juu taa karibu zote zilikuwa zimekufa, hata mzingo huo mwingine, lakini pia rangi na sasa hivi hata ukidondosha sindano chini unaiona. Naomba tumpigie makofi Katibu na timu yake kwa kazi nzuri. (Makofi) Sasa kweli huu ni mjengo kweli kweli! Ndiyo maana watu wanapambana kweli kweli kuja mjengoni hapa maana mjengo unapendeza. Ahsante sana. (Makofi) Tunaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI, swali letu la kwanza kabisa kwa Bunge la Kumi na Mbili amepewa heshima Mheshimiwa Boniface Mwita Getere, Mbunge wa Bunda kuliuliza. Mheshimiwa Getere. Sijui yuko upande gani sasa maana mnakaa upya. Ahsante nimekuona. MASWALI NA MAJIBU MHE. BONIFACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, naomba swali langu namba 295 lipate majibu. SPIKA: Naomba urudie, maana hilo swali lako mimi silifahamu. Angalia Order Paper. Na. 1 Tatizo la Madawati MHE. BONIFACE M. GETERE aliuliza:- 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, Serikali inachukua hatua gani endelevu za kuondoa tatizo sugu la upungufu wa madawati kwenye baadhi ya shule za msingi na sekondari nchini? SPIKA: Swali lako ni namba moja kabisa, sio 295, hapana, Kwa hiyo kila muuliza swali lazima uwe umeshaangalia swali lako ni namba ngapi ili uweze kuliuliza. Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Waziri wa TAMISEMI. Mheshimiwa Silinde tafadhali na yeye ni mara ya kwanza anajuka kujibu maswali, kwa hiyo makofi ni muhimu. (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, ahsante. Kabla sijaanza kujibu swali namba moja la Mheshimiwa Mwita Getere, naomba kwa idhini yako nitoe shukrani kwanza kwa Mwenyezi Mungu kwa kuniwezesha kushinda uchaguzi, lakini vilevile kuweza kuingia ndani ya Bunge. Pia kwa kipekee kabisa nimshukuru sana Mheshimiwa Rais Dkt. John Pombe Joseph Magufuli kwa imani kubwa ambayo amenionesha kwangu mpaka kuniteua kuwa Naibu Waziri katika Ofisi ya Rais, TAMISEMI ambayo nahudumu. (Makofi) Mheshimiwa Spika, vilevile naomba nikishukuru chama changu Chama Cha Mapinduzi kwa imani yake kubwa ambayo wameionesha kwangu kwa kunipa nafasi ya kugombea na mwisho wa siku kunisaidia kampeni na kushinda kwa kishindo. Nakishukuru sana. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa kipekee kabisa niishukuru familia yangu. Mama yangu mzazi kwa kuwa nami katika kipindi chote mpaka kufikia hatua hii ambayo leo nimefikia… SPIKA: Sasa majibu! NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Spika, 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) sasa naomba nijibu swali la Mheshimiwa Mwita Getere, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI naomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniface Mwita Getere, Mbunge wa Bunda kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, changamoto ya wanafunzi kukosa madawati katika shule za msingi na sekondari imetokana na mwitikio mkubwa wa wazazi kuandikisha wanafunzi shuleni baada ya Serikali kuanzisha mpango wa utoaji wa elimu bila malipo ambapo idadi ya wanafunzi wanaoandikishwa kwenye shule za msingi na sekondari umeongezeka maradufu. Mheshimiwa Spika, Serikali imeendelea kutoa fedha kwa ajili ya ununuzi wa madawati ambapo mpaka sasa mwaka 2015 kulikuwa na madawati 3,024,311 na mpaka sasa hivi kufikia mwezi Septemba 2020 Serikali imeongeza madawati kufikia madawati 8,095,207 ambapo kumekuwa na ongezeko la madawati 5,070,899. Mheshimiwa Spika, katika kukabiliana na upungufu wa madawati, Serikali imeendelea kuchukua hatua mbalimbali ikiwa ni pamoja na kutenga fedha kwa ajili ya utengenezaji wa madawati kwenye miradi yote inayotengewa fedha za ukamilishaji wa vyumba vya madarasa kwa shule za msingi na sekondari na kuhamasisha wananchi na kuwashirikisha wadau na asasi mbalimbali katika utengenezaji wa madawati pamoja na kuendelea kutenga fedha ya matengenezo ya madawati kwenye Halmashauri kupitia mapato ya ndani. Nashukuru sana. SPIKA: Mheshimiwa Mwita Getere, Mbunge wa Bunda kama unalo swali la nyongeza. MHE. BONIFACE M. GETERE: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la kwanza kwenye Bunge lako hili la Kumi na Mbili. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, suala la madawati limekuwa ni suala sugu sana katika nchi yetu. Swali langu la kwanza, nataka kujua Serikali ina mpango gani sasa wa kuwa na mfuko maalum au mfuko wa kudumu ambao utafanya hili tatizo la madawati liweze kupungua katika nchi yetu na hasa katika Jimbo langu la Bunda, upungufu wa madawati kwenye shule za msingi na sekondari ni mkubwa sana? Mheshimiwa Spika, swali la pili, sasa hivi nchi yetu kuna wanafunzi wanaenda shuleni hasa sekondari. Kuna mkanganyiko wa kusema twende na madawati, wengine wananunua wazazi, wengine wanasema Serikali inaleta. Mheshimiwa Spika, nini tamko la Serikali kwenye suala hili la madawati katika shule za sekondari? (Makofi) SPIKA: Majibu ya maswali hayo, Mheshimiwa Naibu Waziri, TAMISEMI, Mheshimiwa David Silinde, tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE: DAVID E. SILINDE): Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Naomba nimjibu Mheshimiwa Boniface Mwita