MKUTANO WA NANE Kikao Cha Nne – Tarehe

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

MKUTANO WA NANE Kikao Cha Nne – Tarehe Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Nne – Tarehe 18 Juni, 2007 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, katika Orodha ya Shughuli za leo kuna jambo muhimu ambalo lilisahauliwa na imetulazimu turekebishe Orodha ya Shughuli za leo, kwa sababu zipo Hati za kuwasilisha mezani ambazo hazikuyatangulia maswali. Kwa hiyo, Nyongeza ya Orodha ya Shughuli za leo imetawanywa sasa hivi ni badiliko ambalo litahusu shughuli hizo. Kwa hiyo, sasa nitamwita Katibu kwa kutuongoza katika shughuli hizo. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- MHE. DR. ABDALLAH O. KIGODA – MWENYEKITI WA KAMATI YA FEDHA NA UCHUMI:- Taarifa ya Kamati ya Fedha na Uchumi kuhusu Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2006. Mpango na Maendeleo kwa mwaka 2007/2008 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2007/2008. MHE. KABWE Z. ZITTO – MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA MIPANGO, UCHUMI NA UWEZESHAJI:- Hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji kuhusiana na Hali ya Uchumi wa Taifa na mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo na mfumo wa matumizi ya Serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2007/2008. MHE. HAMAD RASHID MOHAMED – MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA FEDHA:- 1 Taarifa na Mapendekezo ya Kambi ya Upinzani kwa Bajeti ya mwaka wa Fedha 2007/2008. MASWALI NA MAJIBU Na. 30 Semina ya Viongozi Iliyofanyika Ngurdoto MHE. MHONGA SAID RUHWANYA aliuliza:- Kwa kuwa, mara tu baada ya Viongozi Watendaji kama vile Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuteuliwa walipewa Mafunzo ya kazi katika semina iliyofanyika Ngurdoto Arusha:- (a) Je, ni kiasi gani cha fedha kilitumika katika kugharimia semina hiyo na vyanzo vya fedha hizo ni vipi? (b) Je, semina hiyo ilisaidia kwa kiasi gani katika utendaji wa kazi zao za kila siku? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Mhonga Said Ruhwanya, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) naomba kutoa maelezo yafuatayo:- Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Nne, ilipata ushindi wa kishindo kwa nafasi ya Urais kwa asilimia 80.28 pamoja na Ubunge ikilinganishwa na Vyama vingine vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Ushindi huo peke yake ni changamoto kwa Serikali ya Awamu ya Nne. Matarajio ya wannachi ni makubwa kutokana na malengo yaliyomo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 kwani yaliwapa watu matumaini na hivyo wakaamua kutoa ushindi huo mkubwa. Katika kutekeleza majukumu yake kwa Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya. Rais alilazimika kupanga safu ya Viongozi wa kumsaidia ambapo Mawaziri wapya 19 kati ya 30, Manaibu Mawaziri wapya 26 kati ya 31, Wakuu Mikoa Wapya 15 kati ya 21 na Wakuu wapya wa Wilaya 47 kati ya Wakuu wa Wilaya 113 waliokuwepo katika Awamu ya Tatu waliteuliwa. Hivyo, ili kujibu matarajio makubwa ya jamii iliyotoa ushindi mkubwa kwa CCM ilikuwa ni muhimu kwa kuanzia kwa Viongozi hawa kukutana pamoja ili wawe na uelewa wa pamoja katika kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2005 kwa kuzingatia vipaumbele vya Taifa kupitia Semina Elekezi ya Ngurdoto. (Makofi) Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, sasa naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:- 2 (a) Mheshimiwa Spika, katika Semina Elekezi ya Ngurdoto iliyofanyika tarehe 22 – 27 Agosti, 2006 jumla ya Sh.1,602,000,000/= zilitumika. Vyanzo vya fedha hizo ni kutoka sehemu zifuatazo:- (i) Mfuko wa Kuboresha Utendaji (Performance Improvement Fund (PIF) – Shilingi milioni 500,000,000. Unaoratibiwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. (ii) Programu ya Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa (Local Government Reform Programme (LGRP) shilingi milioni 300,000,000. (iii) Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa (Local Government Support Programme (LGSP) shilingi 200,000,000/=. (iv) Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa shilingi 602,000,000/=. Hivyo kufanya jumla ya matumizi kufikia shilingi 1,602,000,000/=. (b) Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza katika maelezo ya utangulizi hapo juu, Semina Elekezi ya Ngurdoto ilikuwa ni sehemu ya kujenga uwezo kwa Viongozi ili kusaidia kuimarisha utendaji kazi Serikalini. Mafanikio katika utendaji yanaonekana wazi. Tutakubaliana wote kuwa mafanikio hayo hayakutokana na Semina Elekezi ya Ngurdoto pekee. Baada ya semina hiyo zilifuatia semina nyingine pamoja na mafunzo mbalimbali. Madhumuni makubwa ni kutekeleza kazi za Serikali kwa ufanisi zaidi. Mheshimiwa Spika, Semina hiyo imewasaidia Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Makatibu wa Tawala za Mikoa kukabiliana na changamoto mbalimbali katika utendaji kazi wao. Mada zilizowasilishwa zililenga katika utawala bora, mikakati ya kuboresha utendaji kazi Serikalini na ukuzaji wa uchumi na maendeleo ya jamii. Hivyo, Semina hivyo ilisaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha uongozi wa pamoja, usimamizi wa utendaji, uwajibikaji na udhibiti wa raslimali ndani ya Serikali kwa Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya. (Makofi) Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutoa mafunzo kwa watumishi wake katika ngazi zote ili kuzidi kuimarisha utendaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi. Ni dhahiri kwamba mafunzo yoyote yana gharama, lakini kikubwa ni kuhakikisha mafunzo hayo yanachochea maendeleo kwa wananchi. (Makofi) MHE. MHONGA SAID RUHWANYA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nilivyokuwa nafahamu mimi ni kwamba Wabunge wa CCM ni asilimia 69 na siyo asilimia 80. Naomba sasa niulize swali langu. (a) Licha ya Semina hiyo Elekezi ya Ngurdoto bado Semina Elekezi, Warsha na Kongamano yanaendelea na hata juzi tu swali kama hili liliulizwa. Kwa hiyo, ni fedha nyingi sana zinatumika ambazo zingeweza kufanyia mambo mengine. Je, Serikali itakubaliana na mimi kwamba Semina Elekezi hiyo ya Ngurdoto haikuwa na tija yoyote ndiyo maana mpaka leo Semina na Warsha zinaendelea? 3 (b) Kwa nini Serikali isipunguze warsha hizo na semina badala yake iweke utaratibu maalum wa mafunzo yenye tija ambayo yanaweza kusaidia utendaji kazi kuliko ilivyo hivi sasa warsha na kongamano imekuwa ni kero? (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, nia ya Semina ya Ngurdoto ilikuwa ni kutoa dira na mwelekeo wa Serikali ya Awamu Nne, na tuelewe kwamba mwajiri yeyote anapomwajiri mtu anataka tija katika Shirika lake au Taasisi yake. Kwa hiyo, hata Serikali ya Awamu ya Nne ilitoa Semina Elekezi ili kutoa mwelekeo na dira; na hata kwenye ajira unapomwajiri mtumishi unatoa Introduction course, orientation ili huyo mwajiriwa afuate matakwa ya shirika lako au Taasisi yako. Kwa hiyo, Mheshimiwa Rais aliona ni vyema kutoa Semina Elekezi ili kutoa mwelekeo na dira kwa Awamu ya Nne ya uongozi. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kuhusu (b) kero kwa upande wa semina na kongamano. Waheshimiwa Wabunge, ni ukweli usiyofichika kwamba semina na kongamano hazitolewi kiholela tu zinakuwa na mada maalum na zinakuwa na malengo maalum. Kwa hiyo, semina hizo kama semina za UKIMWI na Semina za Waheshimiwa Wabunge kujua mwelekeo wa Serikali zote zinaleta tija na siyo kubomoa. Mimi ninawaomba Waheshimiwa Wabunge, tusiziponde sana hizo semina bali tuelewa kwamba ni nia nzuri ya Serikali katika kujenga nchi yetu. (Makofi) SPIKA: Nadhani inatosha, tunahamia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo. Na. 31 Kuwaendeleza Vijana Kimichezo MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Nne imedhamiria kuimarisha na kuongeza viwango vya michezo nchini kama vile mpira wa miguu, mpira wa pete (netball), riadha, kareti, mpira wa kikapu n.k.; na kwa kuwa, vijana wengi wenye vipaji vya michezo wako Mikoani, Wilayani na Vijijini:- Je, Serikali ina mikakati gani ya kuwatafuta vijana hao na kuendeleza vipaji vya michezo walivyo navyo? NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO (MHE. JOEL N. BENDERA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa makofi mazuri ya kuashiria mambo mazuri. (Makofi) 4 Mheshimiwa Spika, kabla sijajibu swali la Mheshimiwa Anna Lupembe, kwa ruhusa yako nikuombe uniruhusu nitoe salam ama nitoe tamko la kuishukuru timu yetu ya Taifa kwa kubeba bendera vizuri katika kutetea Taifa letu. (Makofi) Mheshimiwa Spika, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, mtakumbuka tarehe 14 Juni, 2007 kwa niaba ya Serikali aliwakabidhi vijana bendera ya nchi ili waendelee katika kutafuta nafasi ya kushiriki katika finali za Kombe la Mataifa Uhuru ya Afrika kule Burkinafaso. Vijana hao wamefanya kazi nzuri, nyie wote ni mashahidi wameweza kutupatia ushindi wa goli moja bila na kutuweka katika mazingira mazuri ya kuweza kuendelea katika mashindano hayo. Naomba nitoe salamu hizo kwa niaba ya Waziri wangu na kwa niaba ya Serikali tuwapongeze kwa dhati kabisa kwa kazi nzuri ya kulitetea Taifa na kuiletea heshima nchi yetu. Naomba tuwaunge mkono tuwachangie ili waweze kufanya vizuri katika mechi ya mwisho tarehe 2 Septemba, 2007 tuwakungute Msumbiji magoli mengi ili tu-qualify kwenda Ghana. (Makofi) Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anna Lupembe, Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Serikali ya Awamu ya Nne imedhamiria kuendeleza na kuimarisha vipaji na kukuza viwango vya michezo yote hapa nchini. Kwa sasa Wizara yangu inaendelea na kutoa mafunzo mbalimbali kwa viongozi wa michezo katika kutambua vipaji kwa vijana nchini kote. Mheshimiwa Spika, ni vema ieleweke kuwa kukuza michezo kwa kuendeleza vipaji vya vijana ni njia mojawapo tu katika kuimarisha
Recommended publications
  • Did They Perform? Assessing fi Ve Years of Bunge 2005-2010
    Policy Brief: TZ.11/2010E Did they perform? Assessing fi ve years of Bunge 2005-2010 1. Introducti on On July 16th 2010, following the completi on of the 20th session of the Bunge, the President of Tanzania dissolved the 9th Parliament. This event marked the end of the term for Members of Parliament who were elected during the 2005 general electi ons. Now that the last session has been completed it allows us to look back and to consider how MPs performed during their tenure. Did they parti cipate acti vely and represent their consti tuencies by asking questi ons and making interventi ons, or were they silent backbenchers? The Bunge is the Supreme Legislature of Tanzania. The Bunge grants money for running the administrati on and oversees government programs and plans. The Bunge oversees the acti ons of the Executi ve and serves as watchdog to ensure that government is accountable to its citi zens. To achieve all this, Members of Parliament pass laws, authorize taxati on and scruti nize government policies including proposal for expenditure; and debate major issues of the day. For the Bunge to eff ecti vely carry out its oversight role, acti ve parti cipati on by Members of Parliament is criti cal. MPs can be acti ve by making three kinds of interventi ons: they can ask basic questi ons, they can ask supplementary questi ons and they can make contributi ons during debates. This brief follows earlier briefs, the last of which was released in August 2010. It presents seven facts on the performance of MPs, including rati ng who were the most acti ve and least acti ve MPs.
    [Show full text]
  • Coversheet for Thesis in Sussex Research Online
    A University of Sussex DPhil thesis Available online via Sussex Research Online: http://sro.sussex.ac.uk/ This thesis is protected by copyright which belongs to the author. This thesis cannot be reproduced or quoted extensively from without first obtaining permission in writing from the Author The content must not be changed in any way or sold commercially in any format or medium without the formal permission of the Author When referring to this work, full bibliographic details including the author, title, awarding institution and date of the thesis must be given Please visit Sussex Research Online for more information and further details Accountability and Clientelism in Dominant Party Politics: The Case of a Constituency Development Fund in Tanzania Machiko Tsubura Submitted for the Degree of Doctor of Philosophy in Development Studies University of Sussex January 2014 - ii - I hereby declare that this thesis has not been and will not be submitted in whole or in part to another University for the award of any other degree. Signature: ……………………………………… - iii - UNIVERSITY OF SUSSEX MACHIKO TSUBURA DOCTOR OF PHILOSOPHY IN DEVELOPMENT STUDIES ACCOUNTABILITY AND CLIENTELISM IN DOMINANT PARTY POLITICS: THE CASE OF A CONSTITUENCY DEVELOPMENT FUND IN TANZANIA SUMMARY This thesis examines the shifting nature of accountability and clientelism in dominant party politics in Tanzania through the analysis of the introduction of a Constituency Development Fund (CDF) in 2009. A CDF is a distinctive mechanism that channels a specific portion of the government budget to the constituencies of Members of Parliament (MPs) to finance local small-scale development projects which are primarily selected by MPs.
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 106 Sept - Dec 2013
    Tanzanian Affairs Text 1 Issued by the Britain-Tanzania Society No 106 Sept - Dec 2013 The Race for the State House President Obama’s Visit Surprises in Draft Constitution Tanzania in a Turbulent World Shangaa - Art Surprising the US Newspaper cover featuring twelve people said to be eying the Presidency. cover photo: Shirt celebrating the visit of President Obama to Tanzania. New cover design - we are trying a new printer who offers full colour. Comments welcome, and please send photos for future covers to [email protected] David Brewin: THE RACE FOR STATE HOUSE Americans usually start campaigning for the next election contest almost immediately after the completion of the previous one. Tanzania seems to be moving in the same direction. Although the elections are not due until late 2015, those aspirants who are considering standing for the top job are beginning to quietly mobilise their support. Speculation is now rife in political circles on the issue of who will succeed President Kikwete. Unlike some of his opposite numbers in other states, notably Zimbabwe, he is expected to comply with the law and retire at the end of his second term as all his predecessors have done. A number of prominent figures are expected to compete in the elections. One factor which could become crucial is a long established ‘under- standing’ that, if the president is a Muslim, as is President Kikwete, his successor should be a Christian. President Nyerere was a Catholic, former President Mwinyi is a Muslim and President Mkapa is also a Catholic. As both the Christian presidents have been Catholics the large Protestant community might be wondering when its time will come.
    [Show full text]
  • Tanzania Revenue Authority
    TANZANIA REVENUE AUTHORITY CUSTOMS AND EXCISE DEPARTMENT LIST OF LICENSED CUSTOMS AGENTS FOR THE YEAR 2014 S/NO LICENSE NO TIN AGENT NAME LOCATION CONTACT DIRECTORS EMPLOYEES Status 1 11665 101-103-854 21ST CENTURY FREIGHT CHAGGA STREET Box No :33072 1 .MARY JACOB SHIRIMA 1. REGINALD AMINIEL Active FORWARDERS LTD District :ILALA 2 .PETER WILLBARD SHIRIMA URIO Region :DAR ES 2. GEORGE MJIGABA SALAAM NDARO Email : 3. PETER WILLBARD 21centuryff@gmail. SHIRIMA com 4. ZULFA MUHAMED BYAMUNGU 5. XAVIER JOSEPH SETTEBE 6. DENIS ILDEPHONCE SEYIMBWA 7. JOSEPH FELIX MANJIRA 8. DOMINIC SIMON ASSEY 9. NATHANAEL NZINYANGWA MJEMA 10. RAMADHANI HAMISI ZAE 11. ASTARICO MTOBESYA RAPHAEL 12. RAMADHANI SEIF HASSAN 13. BRYTON STEVEN MFURU 14. NYANGI PETER KITENGA Printed Date: 4/2/2014 9:28:12 AM Page 1 of 143 2 11438 104-849-091 A & G HOLDINGS LIMITED Uhuru Street Box No :5730 1 .GORDON JOHNSON ODIERO 1. FAIZ ABEID FAIZ Active District :Ilala 2 .ATIENO LAURENCE MAINA 2. LILIAN SOSPITER Region :DAR ES KASHURA SALAAM 3. JOSEPH ISAYA OIRO Email : 4. EMANUEL MASIRORI aandgholdings@ya NYITAMBE hoo.com 5. REHEMA KHALPHAN KESSY 6. MUSSA KIMWAGA TUWANO 7. YUNUS ALLY YASIN 8. JOHNSON GORDON ODIERO 3 11388 101-014-711 A & M CLEARING & FORWARDING VUGA Box No :3283 1 .SALEH ALI NASSOR 1. SULEIMAN ALLY ALAWY Active SERVIRCES District :TOWN 2 .MANSOUR NASSOR SALIM 2. MANSOUR NASSOR Region :UNGUJA SALIM Email : 3. SALEH ALI NASSOR amcfszanzibar@ya hoo.com 4 11505 102-395-077 A AND HIS DCO LTD SAMORA/MKWEPU Box No :62417 1 .ANDERSON BIGIRWA 1.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge Mkutano Wa Kumi Na Nne
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA NNE Kikao cha Nne – Tarehe 30 Januari, 2009 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 39 Mtiririko wa Mikutano ya Bunge MHE. DR. HAJI MWITA HAJI aliuliza:- Kwa kuwa mkutano wa Bunge wa Kumi na mbili (12) umeisha hivi kairbuni:- (a) Je, Mkutano huo ni wa Bunge la ngapi tokea kuanza kwa Bunge la Tanzania? (b) Je, Mtiririko wa Bunge la Tanzania ukoje tokea kuanza kwake hadi kufikia Bunge hili ? WAZIRI WA NCHI OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Dr. Haji Mwita Haji, Mbunge wa Muyuni, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mkutano wa 12 wa Bunge uliokwisha ni wa Bunge la Tisa (9) tangu kuanza kwa Bunge la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. 1 (b) Bunge la kwanza la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania lilianza mwaka 1965 baada ya Muungano wa iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika na Jamhuri ya watu wa Zanzibar. Ikumbukwe kwamba Bunge la iliyokuwa Jamhuri ya Tanganyika ilidumu kwa muda mfupi sana. Kwa mujibu wa Ibara ya 65 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, toleo la 2005, maisha ya Bunge la Jamhuri la Muungano wa Tanzania ni muda wa miaka mitano. Mheshimiwa Spika, kwa kuzingatia masharti yaliyowekwa na Ibara ya 65, mtiririko wa maisha ya Bunge umekuwa kama ifuatavyo:- Mwaka 1965 – 1970 Bunge la Kwanza, 1970 – 1975 Bunge la Pili, 1975 -1980 Bunge la Tatu, 1980 – 1985 Bunge la Nne, 1985 – 1990 Bunge la Tano, 1990 – 1995 Bunge la Sita, 1995 – 2000 Bunge la Saba, 2000 – 2005 Bunge la Nane, 2005 – 2010 Bunge la Tisa.
    [Show full text]
  • 1 Bunge La Tanzania
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA NNE Kikao cha Kumi na Mbili – Tarehe 11 Februari, 2009 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Sammuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU (SERA, URATIBU NA BUNGE): Taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa Maazimio ya Bunge juu ya Zabuni ya Kuzalisha umeme wa Dharura ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Development Company LLC ya Houston, Texas – Marekani mwaka 2006. Taarifa ya Serikali kuhusu tatizo la Nishati ya Mafuta Nchini. NAIBU WAZIRI WA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Serikali kuhusu uendeshaji wa Shirika la Ndege Tanzania (ATCL). Taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa Maazimio ya Bunge juu ya uendeshaji usioridhisha wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) unaofanywa na Kampuni ya RITES ya India. Taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa Maazimio ya Bunge juu ya utendaji wa kazi usioridhisha wa kampuni ya Tanzania International Container Terminal Services (TICTS). Taarifa ya Serikali kuhusu utekelezaji wa Maazimio ya Bunge juu ya uuzwaji wa Nyumba za Serikali. 1 MWENYEKITI WA KAMATI YA NISHATI NA MADINI - (MHE. WILLIAM H. SHELLUKINDO): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Nishati na Madini kuhusu utekelezaji wa Maazimio ya Bunge juu ya Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa Dharura ulioipa ushindi Kampuni ya Richmond Development Company LLC ya Houston, Texas – Marekani mwaka 2006. MWENYEKITI WA KAMATI YA MIUNDOMBINU – (MHE. MOHAMED H. MISSANGA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Miundombinu kuhusu utekelezaji wa Maazimio ya Bunge juu ya uendeshaji usioridhisha wa Shirika la Reli Tanzania (TRL) unaofanywa na Kampuni ya RITES ya India.
    [Show full text]
  • Do They Work for Us? Eight Facts About Mps in Tanzania
    Policy Note: 01/2010 Do they work for us? Eight facts about MPs in Tanzania 1. Introduction The Bunge, Tanzania’s Parliament, is one of the most important institutions in the country. Its importance is reflected in the resources allocated to it. For 2009/10, Tanzania’s Parliament was allocated Tshs 62 billion. Since Parliament comprises of 320 members, this amount averages to Tshs 194 million per MP. Most MPs (231) are elected by their respective constituencies, but a significant number (88), or about 28% of all MPs, have been appointed: 75 as special seats legislators and 5 as representatives from the Zanzibar House of Representatives. In addition Parliament comprises the Attorney General and 8 appointees by the President. One of Parliament’s core functions is to oversee the executive branch of Government. Parliament is to ensure that the country is well governed, that services are properly delivered to citizens, and that money entrusted to the Government is well spent and accounted for. In Parliament, MPs can hold the Executive to account by making three kinds of interventions: MPs can ask basic questions, they can ask supplementary questions and they can make contributions during debates. This note assesses the performance of MPs by considering how actively they participated in the sessions of Parliament. The period covered are the seventeen sessions of Parliament from 2005 to 2009 (the 18th session which started on 26th January 2010 is not included). 2. Eight facts about performance of Parliament All MPs are in a position to ask questions or make contributions though serving Government Ministers are unlikely to do so.
    [Show full text]
  • Working Paper 98
    Working Paper 98 Democratisation in Tanzania: No Elections Without Tax Exemptions IDS_Master Logo Ole Therkildsen and Ane Karoline Bak June 2019 IDS_Master Logo_Minimum Size X X Minimum Size Minimum Size X : 15mm X : 15mm ICTD Working Paper 98 Democratisation in Tanzania: No Elections Without Tax Exemptions Ole Therkildsen and Ane Karoline Bak June 2019 Democratisation in Tanzania: No Elections Without Tax Exemptions Ole Therkildsen and Ane Karoline Bak ICTD Working Paper 98 First published by the Institute of Development Studies in June 2019 © Institute of Development Studies 2019 ISBN: 978-1-78118-566-7 This is an Open Access paper distributed under the terms of the Creative Commons Attribution Non Commercial 4.0 International license, which permits downloading and sharing provided the original authors and source are credited – but the work is not used for commercial purposes. http://creativecommons.org/licenses/by-nc/4.0/legalcode Available from: The International Centre for Tax and Development at the Institute of Development Studies, Brighton BN1 9RE, UK Tel: +44 (0) 1273 606261 Email: [email protected] Web: www.ictd.ac/publication IDS is a charitable company limited by guarantee and registered in England Charity Registration Number 306371 Charitable Company Number 877338 2 Democratisation in Tanzania: No Elections Without Tax Exemptions Ole Therkildsen and Ane Karoline Bak Summary A demand-supply framework has been developed and applied to Tanzania to explore the link between democratisation, economic liberalisation and the use of tax exemptions to fund political parties’ electoral campaigns. In Tanzania, the demand for this type of money has increased since one-party rule was abolished in 1992.
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 108 May - Aug 2014
    Tanzanian Affairs Text 1 Issued by the Britain-Tanzania Society No 108 May - Aug 2014 Operation Tokomeza Constitution Review - More Heat than Light Low Confidence in the Economy Mark Gillies: OPERATION TOKOMEZA Tokomeza – to scatter, or destroy, or to reduce to nothing. In the autumn of 2013, a report commissioned by the government’s Wildlife Division and the Frankfurt Zoological Society concluded that the elephant population of the Selous Game Reserve had dropped to 13,000, its lowest recorded level. This is a drop of 80% from the previ- ous survey in 2005, when there were an estimated 65-70,000 elephants. The cause of this decline was unrestrained, systematic poaching. At the current rate, in four years time there would no longer be any elephants left in the Selous. The Tanzanian government had no choice: it had to act. The result was Operation Tokomeza, a cross-services, multi-ministry attempt to end the poaching of large mammals in Tanzania. Initial success came in the form of increased seizures of illicit ivory, but this was soon overshadowed by horrific stories of beatings, sexual assault and even murder, some of which were recorded on mobile phones and Prior to his resignation, Natural Resources and Tourism minister, Ambassador Khamis Kagasheki, inspects tusks impounded at a Mikocheni house (DSM) cover photo by Dr Graeme Shannon Operation Tokomeza 3 posted on YouTube. MPs raised questions in Parliament, issuing a report that confirmed the existence of human rights abuses. The Minister for Natural Resources and Tourism, Hamisi Kagasheki, resigned, and three Ministers were sacked: the Minister for Home Affairs, Emmanuel Nchimbi, the Minister for Defence and National Service, Shamsi Vuai Nahodha and the Minister for Livestock Development, David Mathayo.
    [Show full text]
  • Hoja Ya Kutokuwa Na Imani Na Waziri Mkuu Orodha Ya Waheshimiwa Wabunge Walioweka Saini Zao Dodoma
    HOJA YA KUTOKUWA NA IMANI NA WAZIRI MKUU ORODHA YA WAHESHIMIWA WABUNGE WALIOWEKA SAINI ZAO DODOMA JINA LA MHESHIMIWA MBUNGE SAINI YAKE 1. Mhe. Anne Semamba Makinda, (CCM) SPIKA S.L.P 6958, DAR ES SALAAM. -0754/0784 465226 NJOMBE KUSINI 2. Mhe. Job Yustino Ndugai, (CCM) NAIBU SPIKA S.L.P 64, KONGWA. -0762 605951/ 0655 605951 KONGWA 1. Mhe. Mwanamrisho Taratibu Abama, (CHADEMA) S.L.P. 2455, ZANZIBAR. -0775 242006 VITI MAALUM 2. Mhe. Maida Hamad Abdallah, (CCM) S.L.P. 60, Wete. -0784 549061/0716 955024 VITI MAALUM 3. Mhe. Anna Margareth Abdallah, (CCM)-0784 338181 S.L.P. 314, MASASI/ S.L.P. 12433, DAR ES SALAAM. VITI MAALUM 4. Mhe. Rashid Ali Abdallah, (CUF) S.L.P 2, ZANZIBAR. -0776 720960 TUMBE 5. Mhe. Abdallah Sharia Ameir, (CCM) S.L.P. 2220, ZANZIBAR, 0777 419232 DIMANI 6. Mhe. Abdulsalaam Selemani Amer, (CCM) S.L.P. 35 MIKUMI. - 0784 291296/0773 291296 MIKUMI 7. Mhe. Bahati Ali Abeid (CCM) S.L.P. 3451 ZANZIBAR 0777 469244 VITI MAALUM 1 8. Mhe. Abdul-Aziz Mohamed Abood, (CCM) - 0758 500000 S.L.P. 127, Morogoro, 0754/0784 261888 MOROGORO MJINI 9. Mhe. Chiku Aflah Abwao, (CHADEMA) S.L.P. 759 IRINGA. - 0715/0784 599772 VITI MAALUM 10. Mhe. Khalfan Hilaly Aeshi, (CCM) -0786 060000 S.L.P 479 SUMBAWANGA, RUKWA. -0767 212111 SUMBAWANGA MJINI 11. Mhe. Rukia Kassim Ahmed, (CUF) S.L.P. 16217 DAR ES SALAAM 0773 178580 VITI MAALUM 12. Mhe. Lameck Okambo Airo, (CCM) S.L.P. 594, Mwanza, 0777 444305/ 0784444305 RORYA 13. Mhe.
    [Show full text]
  • Tanzania Parliament
    The information contained in this book is as comprehensive as the Members of Parliament were able to supply at the time of going to press. If you have any inquiries on this book or difficulties in contacting Members of Parliament or Parliamentary staff, please contact the Office of the Clerk of the National Assembly at the following addresses: Dodoma: P.O. Box 941 Tel. No. 026-2323115/2322761-5/2322771 Fax No. 026-2324218 E-mail: [email protected] Dar es Salaam: Zanzibar: P.O. Box 9133 P.O. Box 362 Zanzibar Tel: 022-2112065-7 Tel: 024 -2230782 Fax: 022 – 2112538 0773-193 802 E-mail: [email protected] Fax: 0773 -193 803 Website: www.parliament.go.tz Published by the Clerk of the National Assembly P.O. Box 9133, Dar Es Salaam, Tanzania Designed at:- Printed in Tanzania by: ECOMM TANZANIA by E.D.Kissuu ECOPRINT LTD. P.O.Box 21425,Dar es Salaam. P.O.Box 65182 Dar es Salaam, Tel.+255 22 286 3864 Tel:+255 713 607 207 Email: [email protected] Email: [email protected] Cover Design: Claire Lwehabura Photos: E.D.Kissuu and Patric M.Kakwaya ISBN NO. 9987-22-094-0 This book may not be reproduced without the permission of the Author: © Tanzania National Assembly 2005 PREFACE The Friedrich Ebert Foundation has for the third time financed the Directory after the General Elections as part of the cooperation that exists between the two Institutions. As in the previous directories, the publication will assist the Parliament’s initiative in its commitment to making the House transparent to the public as part of the Civic Education program.
    [Show full text]
  • FIRSTNAME MIDDLENAME SURNAME Pius Chipanda Msekwa Zakia Hamdani Meghji Wilson Mutagaywa Masilingi William Vangimembe Lukuvi Pius Yasebasi Ng'wandu Prof
    FIRSTNAME MIDDLENAME SURNAME Pius Chipanda Msekwa Zakia Hamdani Meghji Wilson Mutagaywa Masilingi William Vangimembe Lukuvi Pius Yasebasi Ng'wandu Prof. Philemon Mikol Sarungi Omar Ramadhan Mapuri Muhammed Seif Khatib Dr. Mary Michael Nagu Prof. Mark James Mwandosya Prof. Juma Athumani Kapuya Dr. Juma Alifa Ngasongwa Joseph James Mungai Dr. John Pombe Joseph Magufuli Jakaya Mrisho Kikwete Brg. Gen. Hassan Athumani Ngwilizi Harith Bakari Mwapachu Gideon Asimulike Cheyo George Clement Kahama Frederick Tluway Sumaye Edward Ngoyai Lowassa Edger Diones Maokola-Majogo Daniel Ndhira Yona Charles N. Keenja Basil Pesambili Mramba Dr. Asha-Rose Mtengeti Migiro Arcado Denis Ntagazwa Anna Margareth Abdallah Andrew John Chenge Dr. Abdallah Omar Kigoda Shamim Parkar Khan Dr. Maua Abeid Daftari Abdisalaam Issa Khatib Tatu Musa Ntimizi Pius P. Mbawala Mudhihir Mohamed Mudhihir Bujiku Philip Sakila Mizengo Kayanza Peter Pinda Zabein Muhaji Mhita Capt. John Zefania Chiligati Dr. Ibrahim Said Msabaha Dr. Hussein Ali Mwinyi Hezekiah Ndahani Chibulunje Dr. Festus Bulugu Limbu Hamza Abdallah Mwenegoha Dr. Anthony Mwandu Diallo Abdulkadir Shareef Rita Louise Mlaki Mohamed Rished Abdallah Zuhura Shamis Abdallah Alhaj Shaweji Abdallah Mohammed Abdi Abdulaziz Bahati Ali Abeid Khamis Awesu Aboud Kijakazi Khamis Ali Omary Mjaka Ali Fatma Said Ali Khamis Salum Ali Aziza Sleyum Ally Mohamed Abdully Ally Shaibu Ahmada Ameir Kheri Khatib Ameir Rostam Abdulrasul Azizi Faida Mohamed Bakar Elizabeth Nkunda Batenga Joel Nkaya Bendera Lydia Thecla Boma Dr. Batilda Salha Burian Robert Jacob Bazuka Margareth J. Bwana Kisyeri Werema Chambiri Dr. Aaron Daudi Chiduo Diana Mkumbo Chilolo Samuel Mchele Chitalilo Anatory Kasazi Choya Omar Saidi Likungu Chubi Paschal Constantine Degera Leonard Newe Derefa Ahmed Hassan Diria Abdullatif Hussein Esmail Abdallah Khamis Feruz Chifu Abdallah Fundikira Dr.
    [Show full text]