MKUTANO WA NANE Kikao Cha Nne – Tarehe

MKUTANO WA NANE Kikao Cha Nne – Tarehe

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Nne – Tarehe 18 Juni, 2007 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, katika Orodha ya Shughuli za leo kuna jambo muhimu ambalo lilisahauliwa na imetulazimu turekebishe Orodha ya Shughuli za leo, kwa sababu zipo Hati za kuwasilisha mezani ambazo hazikuyatangulia maswali. Kwa hiyo, Nyongeza ya Orodha ya Shughuli za leo imetawanywa sasa hivi ni badiliko ambalo litahusu shughuli hizo. Kwa hiyo, sasa nitamwita Katibu kwa kutuongoza katika shughuli hizo. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- MHE. DR. ABDALLAH O. KIGODA – MWENYEKITI WA KAMATI YA FEDHA NA UCHUMI:- Taarifa ya Kamati ya Fedha na Uchumi kuhusu Hali ya Uchumi wa Taifa kwa mwaka 2006. Mpango na Maendeleo kwa mwaka 2007/2008 na Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa mwaka 2007/2008. MHE. KABWE Z. ZITTO – MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA MIPANGO, UCHUMI NA UWEZESHAJI:- Hotuba ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Mipango, Uchumi na Uwezeshaji kuhusiana na Hali ya Uchumi wa Taifa na mapendekezo ya Mpango wa Maendeleo na mfumo wa matumizi ya Serikali katika kipindi cha mwaka wa fedha 2007/2008. MHE. HAMAD RASHID MOHAMED – MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA FEDHA:- 1 Taarifa na Mapendekezo ya Kambi ya Upinzani kwa Bajeti ya mwaka wa Fedha 2007/2008. MASWALI NA MAJIBU Na. 30 Semina ya Viongozi Iliyofanyika Ngurdoto MHE. MHONGA SAID RUHWANYA aliuliza:- Kwa kuwa, mara tu baada ya Viongozi Watendaji kama vile Wakuu wa Mikoa na Wilaya kuteuliwa walipewa Mafunzo ya kazi katika semina iliyofanyika Ngurdoto Arusha:- (a) Je, ni kiasi gani cha fedha kilitumika katika kugharimia semina hiyo na vyanzo vya fedha hizo ni vipi? (b) Je, semina hiyo ilisaidia kwa kiasi gani katika utendaji wa kazi zao za kila siku? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kabla ya kujibu swali la Mheshimiwa Mhonga Said Ruhwanya, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) naomba kutoa maelezo yafuatayo:- Mheshimiwa Spika, Serikali ya Awamu ya Nne, ilipata ushindi wa kishindo kwa nafasi ya Urais kwa asilimia 80.28 pamoja na Ubunge ikilinganishwa na Vyama vingine vilivyoshiriki Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2005. Ushindi huo peke yake ni changamoto kwa Serikali ya Awamu ya Nne. Matarajio ya wannachi ni makubwa kutokana na malengo yaliyomo kwenye Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005 kwani yaliwapa watu matumaini na hivyo wakaamua kutoa ushindi huo mkubwa. Katika kutekeleza majukumu yake kwa Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya. Rais alilazimika kupanga safu ya Viongozi wa kumsaidia ambapo Mawaziri wapya 19 kati ya 30, Manaibu Mawaziri wapya 26 kati ya 31, Wakuu Mikoa Wapya 15 kati ya 21 na Wakuu wapya wa Wilaya 47 kati ya Wakuu wa Wilaya 113 waliokuwepo katika Awamu ya Tatu waliteuliwa. Hivyo, ili kujibu matarajio makubwa ya jamii iliyotoa ushindi mkubwa kwa CCM ilikuwa ni muhimu kwa kuanzia kwa Viongozi hawa kukutana pamoja ili wawe na uelewa wa pamoja katika kutekeleza Ilani ya CCM ya mwaka 2005 kwa kuzingatia vipaumbele vya Taifa kupitia Semina Elekezi ya Ngurdoto. (Makofi) Mheshimiwa Spika, baada ya maelezo hayo, sasa naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mbunge, kama ifuatavyo:- 2 (a) Mheshimiwa Spika, katika Semina Elekezi ya Ngurdoto iliyofanyika tarehe 22 – 27 Agosti, 2006 jumla ya Sh.1,602,000,000/= zilitumika. Vyanzo vya fedha hizo ni kutoka sehemu zifuatazo:- (i) Mfuko wa Kuboresha Utendaji (Performance Improvement Fund (PIF) – Shilingi milioni 500,000,000. Unaoratibiwa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma. (ii) Programu ya Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa (Local Government Reform Programme (LGRP) shilingi milioni 300,000,000. (iii) Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa (Local Government Support Programme (LGSP) shilingi 200,000,000/=. (iv) Ofisi ya Waziri Mkuu, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa shilingi 602,000,000/=. Hivyo kufanya jumla ya matumizi kufikia shilingi 1,602,000,000/=. (b) Mheshimiwa Spika, kama nilivyoeleza katika maelezo ya utangulizi hapo juu, Semina Elekezi ya Ngurdoto ilikuwa ni sehemu ya kujenga uwezo kwa Viongozi ili kusaidia kuimarisha utendaji kazi Serikalini. Mafanikio katika utendaji yanaonekana wazi. Tutakubaliana wote kuwa mafanikio hayo hayakutokana na Semina Elekezi ya Ngurdoto pekee. Baada ya semina hiyo zilifuatia semina nyingine pamoja na mafunzo mbalimbali. Madhumuni makubwa ni kutekeleza kazi za Serikali kwa ufanisi zaidi. Mheshimiwa Spika, Semina hiyo imewasaidia Wakuu wa Mikoa, Wakuu wa Wilaya na Makatibu wa Tawala za Mikoa kukabiliana na changamoto mbalimbali katika utendaji kazi wao. Mada zilizowasilishwa zililenga katika utawala bora, mikakati ya kuboresha utendaji kazi Serikalini na ukuzaji wa uchumi na maendeleo ya jamii. Hivyo, Semina hivyo ilisaidia kwa kiasi kikubwa kuimarisha uongozi wa pamoja, usimamizi wa utendaji, uwajibikaji na udhibiti wa raslimali ndani ya Serikali kwa Ari Mpya, Nguvu Mpya na Kasi Mpya. (Makofi) Mheshimiwa Spika, Serikali itaendelea kutoa mafunzo kwa watumishi wake katika ngazi zote ili kuzidi kuimarisha utendaji na utoaji wa huduma bora kwa wananchi. Ni dhahiri kwamba mafunzo yoyote yana gharama, lakini kikubwa ni kuhakikisha mafunzo hayo yanachochea maendeleo kwa wananchi. (Makofi) MHE. MHONGA SAID RUHWANYA: Mheshimiwa Spika, ahsante. Nilivyokuwa nafahamu mimi ni kwamba Wabunge wa CCM ni asilimia 69 na siyo asilimia 80. Naomba sasa niulize swali langu. (a) Licha ya Semina hiyo Elekezi ya Ngurdoto bado Semina Elekezi, Warsha na Kongamano yanaendelea na hata juzi tu swali kama hili liliulizwa. Kwa hiyo, ni fedha nyingi sana zinatumika ambazo zingeweza kufanyia mambo mengine. Je, Serikali itakubaliana na mimi kwamba Semina Elekezi hiyo ya Ngurdoto haikuwa na tija yoyote ndiyo maana mpaka leo Semina na Warsha zinaendelea? 3 (b) Kwa nini Serikali isipunguze warsha hizo na semina badala yake iweke utaratibu maalum wa mafunzo yenye tija ambayo yanaweza kusaidia utendaji kazi kuliko ilivyo hivi sasa warsha na kongamano imekuwa ni kero? (Makofi) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA: Mheshimiwa Spika, nia ya Semina ya Ngurdoto ilikuwa ni kutoa dira na mwelekeo wa Serikali ya Awamu Nne, na tuelewe kwamba mwajiri yeyote anapomwajiri mtu anataka tija katika Shirika lake au Taasisi yake. Kwa hiyo, hata Serikali ya Awamu ya Nne ilitoa Semina Elekezi ili kutoa mwelekeo na dira; na hata kwenye ajira unapomwajiri mtumishi unatoa Introduction course, orientation ili huyo mwajiriwa afuate matakwa ya shirika lako au Taasisi yako. Kwa hiyo, Mheshimiwa Rais aliona ni vyema kutoa Semina Elekezi ili kutoa mwelekeo na dira kwa Awamu ya Nne ya uongozi. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kuhusu (b) kero kwa upande wa semina na kongamano. Waheshimiwa Wabunge, ni ukweli usiyofichika kwamba semina na kongamano hazitolewi kiholela tu zinakuwa na mada maalum na zinakuwa na malengo maalum. Kwa hiyo, semina hizo kama semina za UKIMWI na Semina za Waheshimiwa Wabunge kujua mwelekeo wa Serikali zote zinaleta tija na siyo kubomoa. Mimi ninawaomba Waheshimiwa Wabunge, tusiziponde sana hizo semina bali tuelewa kwamba ni nia nzuri ya Serikali katika kujenga nchi yetu. (Makofi) SPIKA: Nadhani inatosha, tunahamia Wizara ya Habari, Utamaduni na Michezo. Na. 31 Kuwaendeleza Vijana Kimichezo MHE. ANNA R. LUPEMBE aliuliza:- Kwa kuwa Serikali ya Awamu ya Nne imedhamiria kuimarisha na kuongeza viwango vya michezo nchini kama vile mpira wa miguu, mpira wa pete (netball), riadha, kareti, mpira wa kikapu n.k.; na kwa kuwa, vijana wengi wenye vipaji vya michezo wako Mikoani, Wilayani na Vijijini:- Je, Serikali ina mikakati gani ya kuwatafuta vijana hao na kuendeleza vipaji vya michezo walivyo navyo? NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI NA MICHEZO (MHE. JOEL N. BENDERA) alijibu:- Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa makofi mazuri ya kuashiria mambo mazuri. (Makofi) 4 Mheshimiwa Spika, kabla sijajibu swali la Mheshimiwa Anna Lupembe, kwa ruhusa yako nikuombe uniruhusu nitoe salam ama nitoe tamko la kuishukuru timu yetu ya Taifa kwa kubeba bendera vizuri katika kutetea Taifa letu. (Makofi) Mheshimiwa Spika, Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, mtakumbuka tarehe 14 Juni, 2007 kwa niaba ya Serikali aliwakabidhi vijana bendera ya nchi ili waendelee katika kutafuta nafasi ya kushiriki katika finali za Kombe la Mataifa Uhuru ya Afrika kule Burkinafaso. Vijana hao wamefanya kazi nzuri, nyie wote ni mashahidi wameweza kutupatia ushindi wa goli moja bila na kutuweka katika mazingira mazuri ya kuweza kuendelea katika mashindano hayo. Naomba nitoe salamu hizo kwa niaba ya Waziri wangu na kwa niaba ya Serikali tuwapongeze kwa dhati kabisa kwa kazi nzuri ya kulitetea Taifa na kuiletea heshima nchi yetu. Naomba tuwaunge mkono tuwachangie ili waweze kufanya vizuri katika mechi ya mwisho tarehe 2 Septemba, 2007 tuwakungute Msumbiji magoli mengi ili tu-qualify kwenda Ghana. (Makofi) Mheshimiwa Spika, baada ya kusema hayo, kwa niaba ya Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Anna Lupembe, Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Serikali ya Awamu ya Nne imedhamiria kuendeleza na kuimarisha vipaji na kukuza viwango vya michezo yote hapa nchini. Kwa sasa Wizara yangu inaendelea na kutoa mafunzo mbalimbali kwa viongozi wa michezo katika kutambua vipaji kwa vijana nchini kote. Mheshimiwa Spika, ni vema ieleweke kuwa kukuza michezo kwa kuendeleza vipaji vya vijana ni njia mojawapo tu katika kuimarisha

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    126 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us