1458127169-Hs-7-3-20

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

1458127169-Hs-7-3-20 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) 12 APRILI, 2012 BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Tatu – Tarehe 12 Aprili, 2012 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tuendelee kusimama. Waheshimiwa Wabunge tutakumbuka kwamba tumepata misiba mikubwa hivi karibuni, kama ilivyo ada nitaomba tusimame kwa heshima ya mwakilishi wa Jimbo la Bububu Mheshimiwa Salum Amour Mtondoo. Lakini vile vile Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Mwita Kyaro, lakini vile vile Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu, Marehemu Harun Mahundi naomba tusimame kwa dakika moja tukiwakumbuka. (Hapa Waheshimiwa Wabunge walisimama kwa dakika moja kuwakumbuka waliotutangulia mbele ya haki) NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, shughuli za asubuhi ya leo naomba niwakumbushe Wabunge wote na Watanzania kwa ujumla kwamba leo tarehe 12/04/2012 ni siku ya Kumbukumbu ya kifo cha mpendwa wetu aliyekuwa Waziri Mkuu Ndugu yetu Edward Moringe Sokoine na Kumbukumbu yake Kitaifa leo itafanyika kule Morogoro ambako kutakuwa na ibada kwa ajili hiyo. 1 12 APRILI, 2012 Kutakuwa na basi ambalo litaondoka hapa kwenye saa nne. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge ambao watapenda kufanya hivyo tuingie katika usafiri huo. KIAPO CHA UTII Wabunge wafuatao waliapa Kiapo cha Utii na kukaa katika nafasi zao ndani ya Ukumbi wa Bunge. Mheshimiwa Cecilia Daniel Paresso Mheshimiwa Joshua Samwel Nassari (Hapa Wabunge walishangilia na kupiga vigelegele baada ya Kiapo) NAIBU SPIKA: Order. Katibu hatua inayofuata. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA URATIBU NA BUNGE: Taarifa ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Hesabu zilizokaguliwa za Serikali za Mitaa kwa Mwaka ulioishia Tarehe 30 Juni, 2011. (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Audit of the Financial Statements of the Local Government Authorities for the year ended 30 th June, 2011) NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. GREGORY GEORGE TEU): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ruhusa yako na kupitia kwako kabla ya kuwasilisha Hati Mezani naomba nitoe taarifa fupi ndani ya Bunge lako Tukufu kwamba katika mkutano wa Umoja wa Mataifa (The United National General Assembly) , uliofanyika Novemba, 2011. 2 12 APRILI, 2012 Mkutano huu uliridhia kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania Ndugu Ludovick Utoah, (The Controller and Auditor General of the United Republic of Tanzania) na ofisi yake kuwa mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi wa Mahesabu pamoja na programs mbalimbali za Umoja wa Mataifa kuanzia tarehe 1 Julai, 2012 kwa kipindi cha miaka 6 mfululizo. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Tanzania ataungana na wenzake kutoka Supreme Audit Institution ya China na Supreme Audit Institution ya Uingereza kuunda Bodi ya ukaguzi wa umoja wa Mataifa kwa kipindi chote cha miaka 6. Kupitia uteuzi huu Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi itapata fursa nzuri na uzoefu wa kujenga uwezo wa kushiriki issues mbalimbali za ukaguzi wa kimataifa na hii ni motisha kubwa kwa wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi. Hii ni heshima kubwa kwa ofisi na nchi kupata fursa hii ambayo nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Mataifa walikuwa wanainuia. Kupitia Ukaguzi huu nchi yetu itapafa fedha za kigeni yaani forex kupitia ada za ukaguzi zitakuwa zinalipwa na Umoja wa Mataifa. Serikali itatoa support kwa kadri itakavyoona inafaa katika kutekeleza jukumu hili la ukaguzi wa Umoja wa Mataifa. Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya pongezi hizi kwa niaba ya Waziri wa Fedha naomba sasa uniruhusu kuweka Mezani Hati zifuatazo:- Taarifa ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu kwa Mwaka ulioishia Tarehe 30 Juni, 2011 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Audit of the Financial Statements of the Central Government for the Year Ended 30 th June, 2011). Taarifa ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Juu ya Hesabu zilizokaguliwa za Mashirika ya 3 12 APRILI, 2012 Umma kwa Mwaka 2010/2011 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Audit of Public Authorities and Other Bodies for the Financial Year 2010/2011). Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Ukaguzi Jumuifu wa Ufanisi na Upembuzi kwa kipindi kilichoishia tarehe 31 Machi, 2012 (Report of the Controller and Auditor General of Tanzania on the Performance and Forensic Audit conducted for the period ending 31 st March, 2012). Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Juu ya Hesabu zilizokaguliwa za miradi ya Maendeleo kwa Mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2011 (Report of the Controller and Auditor General of Tanzania on the Audit of the Financial Statements of Donor Funded Projects for the year ended 30 th June, 2011). Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Ripoti ya Ufanisi inayohusu Ukaguzi wa Magari na Udhibiti wa Mwendo wa Magari katika kupunguza Ajali za Barabarani (A Performance Audit Report on the Management of Traffic Inspections and Speed Limits in Tanzania). Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Ukaguzi wa Ofisi za Balozi (Report of the Controller and Auditor General of Tanzania on the Audit of the Financial Statement of the Tanzania Embassies/Mission for the Year ended 30 th June, 2011). Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania kwa Mwaka 2010/2011 (The Annual Report and Accounts of the National Audit Office of Tanzania for the Period 2010/2011). 4 12 APRILI, 2012 NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha tunakushukuru sana. Swali la kwanza kwa siku ya leo litaulizwa na Mheshimiwa Mariam Ruben Kasembe. MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, … NAIBU SPIKA: Nitakupa nafasi baada ya kipindi cha Maswali na Majibu nitakupa nafasi. MHE. KABWE Z. ZITTO: Samahani, Kiongozi wa Kambi Upinzani Bungeni ndio anatakiwa kuanza kuuliza swali. NAIBU SPIKA: Kiongozi wa Upinzani Bungeni alisimama? Kiongozi wa upinzani Bungeni una swali? Sikukuona samahani. MASWALI KWA WAZIRI MKUU MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue nafasi hii kuomba/kutoa pole kwa Watanzania wote ambao wamefikwa na misiba ambayo ilikumba taifa siku za karibuni. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa muda mrefu yamekuwepo matamko mbalimbali yanayotokana na Viongozi wa Serikali na mengine yakitoka kwa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kwamba maeneo ambayo Watanzania wanachagua Vyama vya Upinzani kuwa wawakilishi wao katika vyombo vya maamuzi kama Madiwani na Wabunge hayatapata mgao wa fedha za maendeleo. (Makofi) Mheshimiwa Waziri Mkuu tunaomba sasa kauli yako kama kauli ya Serikali uwaeleze Watanzania kupitia Bunge hili kama ni kweli Serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi ina Sera ya Ubaguzi katika mgao wa pato la taifa na kama kweli Sera hiyo ipo ni kikao gani kinachokaa kufanya mgao huo zaidi ya Bunge la Bajeti ambalo sisi wote tunakaa hapa kwa maana ya wawakilishi wetu wa Tanzania kutoka Vyama vyote 5 12 APRILI, 2012 ambavyo vimepigiwa kura. Mheshimiwa Waziri Mkuu tunaomba utupe majibu hayo. ( Makofi ) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, ni lazima nionyeshe masikitiko yangu sana kwenye swali hili kwa sababu limeulizwa kijumla na linatoa picha kana kwamba anayoyasema ndio mambo yanayotekelezwa wakati anajua kabisa kwamba hiyo si kweli. Hakuna mahali popote hapa nchini ambako hatujapeleka fedha kulingana na mgao wa taifa bila kujali kama eneo hilo ni la CHADEMA la CU F au la Chama kingine chochote. (Makofi) Kwa hiyo, kidogo nimestushwa na hiyo kauli lakini basi labda niishie hapo tu. ( Makofi ) MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Waziri Mkuu, pamoja na masikitiko yako napenda kukufahamisha kwamba kauli kama hizi zimekuwa zinatolewa mara kwa mara na ninaweza nikatoa mifano halisi na mfano wa kwanza kauli hizi zimetolewa na Waziri Mheshimiwa Mary Nagu wakati wa Kampeni za Uchaguzi katika Jimbo la Arumeru Mashariki. Kauli kama hizi zimetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi katika Jimbo la Arumeru Mashariki, Mkoani Arusha. Matamshi kama haya yaliwahi kutolewa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa John Magufuli katika kampeni za Igunga. Mheshimiwa Waziri Mkuu ahadi kadhaa zimekuwa zinatolewa na Serikali wakati wa kampeni kipindi ambacho kinajulikana kabisa kwamba ni marufuku kwa watendaji wa Serikali kutoa kauli kama hizo na umarufuku huo unatiwa halali na hukumu iliyofanyika katika Jimbo la Kigoma Mjini kufuatia kauli iliyotolewa na Serikali pamoja na ziada ya Rais Mheshimiwa Mstaafu Mzee Mwinyi wakati wa ziara katika uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Mjini. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge sasa swali. 6 12 APRILI, 2012 MHE. FREEMAN A. MBOWE: Sasa Mheshimiwa Waziri Mkuu unatuambia vipi tutakapoweza kukudhihirishia kwamba kauli hizo zimetoka na utachukua basi hatua gani kwa Mawaziri wako ambao wametoa kauli hizo? ( Makofi ) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nafikiri Watanzania tuendelee kujenga demokrasia yetu tumejitahidi sana. Serikali hii itaendelea kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi hii katika mgao wake wote wa fedha. Sasa kama kuna kauli nyingine, kauli zinatoka, nyingine kwenye mapambano wakati wa chaguzi na nini mimi nasema tutaendelea kuheshimu Katiba na Sheria. ( Makofi ) MHE. MARIAM R. KASEMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali kwa Waziri Mkuu. Kwanza kabisa naomba nichukue nafasi hii kuwapa pole sana Wakulima wa Zao la Korosho popote walipo nchini na
Recommended publications
  • 25 JUNI, 2013 MREMA FULL.Pmd
    25 JUNI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Hamsini na Sita - Tarehe 25 Juni, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Ifuatazo Iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:- Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA (CCC) kwa Mwaka ulioshia tarehe 30 Juni, 2012 (The Annual Report and Audited Accounts of TCRA Consumer Consultative Council (TCRA – CCC) for the Year Ended 30th June, 2012). MASWALI NA MAJIBU Na. 457 Wakuu wa Mikoa/Wilaya Kuwa Wabunge MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA aliuliza:- Moja ya majukumu ya Bunge ni kuisimamia na kuishauri Serikali na pia Ibara ya 67(2)(g) ya Katiba ya Jamhuri 1 25 JUNI, 2013 ya Muungano wa Tanzania inaeleza kukoma kwa mtu kuwa Mbunge endapo mtu huyo amepewa madaraka ya Afisa Mwandamizi katika Utumishi wa Umma. (a) Je, ni kwa maana gani Wabunge ambao ni Wakuu wa Mikoa au Wakuu wa Wilaya wanatimiza majukumu yao ya Kibunge? (b) Je, ni kwa namna gani viongozi hao wanakiuka Ibara ya 67(2)(g)ya Katiba pamoja na kuwa wanateuliwa na Rais? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Christowaja Gerson Mtinda, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge ambao ni Wakuu wa Mikoa au Wilaya wanatimiza majukumu yao ya Kibunge kwa kuzingatia Ibara 63(3)(a) – (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
    [Show full text]
  • 1458125471-Hs-6-8-20
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Kumi na Tatu – Tarehe 10 Februari, 2010 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA UCHUMI (MHE. OMAR YUSSUF MZEE): Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Benki ya Posta Tanzania, kwa Mwaka 2008 [The Annual Report and Accounts of The Tanzania Postal Bank for the Year 2008]. The Mid-Term Review of the Monetary Policy Statement of The Bank of Tanzania for the Year 2009/2010. MWENYEKITI WA KAMATI YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini juu ya Taarifa ya Serikali Kuhusu Ubinafsishwaji wa Mgodi wa Kiwira. Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini Kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge Kuhusu Mchakato wa Zabuni ya Kuzalisha Umeme wa Dharura Ulioipa Ushindi Kampuni ya Richmond Development Company LLC. Houston Texas - Marekani Mwaka 2006. MWENYEKITI WA KAMATI YA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Kamati ya Miundombinu Kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelzaji wa Azimio la Bunge Kuhusu Uendeshaji Usioridhisha wa Shirika la Reli Tanzania uliofanywa na Kampuni ya RITES ya India. 1 Taarifa ya Kamati ya Miundombinu Kuhusu Taarifa ya Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge Kuhusu Utendaji wa Kazi Usioridhisha wa Kampuni ya TICTS. MASWALI NA MAJIBU Na. 145 Usimamizi wa Ukaguzi wa Fedha za Halmashauri MHE. HERBERT J. MNTANGI aliuliza:- Kwa kuwa, kiasi cha fedha kinachopelekwa katika Halmashauri za Wilaya, Manispaa na Jiji ni kikubwa na kinahitaji usimamizi wa ziada:- Kwa kuwa kitengo cha ukaguzi wa ndani kipo chini ya Mkurugenzi Mtendaji.
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA NANE Kikao Cha Kumi Na Tano
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Kumi na Tano – Tarehe 3 Julai, 2007 (Kikao Kilianza Saa 3.00 Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI:- Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, mkiangalia Order Paper yetu ya leo, hati za kuwasilisha Mezani iko, Ofisi ya Makamu wa Rais, yuko Mwenyekiti wa Kamati ya Maliasili na Mazingira, tumemruka Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba na Sheria na Utawala, halafu atakuja Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani Bungeni. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS (MAZINGIRA): Hotuba ya Bajeti ya Wizari wa Nchi, Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha wa 2007/2008. MWENYEKITI WA KAMATI YA MALIASILI NA MAZINGIRA: Taarifa ya Kamati ya Bunge ya Maliasili na Mazingira kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha uliopita pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2007/2008. MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA (MHE. RAMADHAN A. MANENO): Tarifa ya Kamati ya Bunge ya Katiba, Sheria na Utawala kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais – Muungano kwa mwaka wa Fedha 2006/2007 na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa Fedha 2007/2008. MHE. RIZIKI OMARI JUMA (k.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI): 1 Maoni ya Kambi ya Upinzani kuhusu Utekelezaji wa Ofisi ya Makamu wa Rais kwa Mwaka wa Fedha uliopita pamoja Maoni ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka 2007/2008.
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao Cha Thelathini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini na Sita – Tarehe 27 Mei, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nawaomba tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa 15, leo ni Kikao cha 36. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2019/2020. NAIBU WAZIRI WA MADINI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. CATHERINE V. MAGIGE - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI) Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini Kuhusu utekelezaji na Majukumu ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MHE. TUNZA I. MALAPO - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU WIZARA YA MADINI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni juu ya Wizara ya Madini kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Tunza Malapo, tunakushukuru. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na TAMISEMI, swali la kwanza litaulizwa na Mheshimiwa Azza Hilal, Mbunge wa Viti Maalum - Shinyanga.
    [Show full text]
  • Na Namba Ya Prem Jina La Mwanafunzi Shule Atokayo 1
    ORODHA YA WANAFUNZI WALIOCHAGULIWA KUJIUNGA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2021 WILAYA YA TEMEKE - WASICHANA A.UFAULU MZURI ZAIDI SHULE YA SEKONDARI KILAKALA - BWENI NA NAMBA YA PREM JINA LA MWANAFUNZI SHULE ATOKAYO 1 20140978513 GIFT JUMANNE MWAMBE SACRED HEART SHULE YA SEKONDARI MSALATO - BWENI NA NAMBA YA PREM JINA LA MWANAFUNZI SHULE ATOKAYO 1 20141212460 IQRA SUPHIAN MBWANA ASSWIDDIQ 2 20141196774 HADIJA SAMNDERE ABDALLAH KIZUIANI SHULE YA SEKONDARI TABORA WAS - BWENI NA NAMBA YA PREM JINA LA MWANAFUNZI SHULE ATOKAYO 1 20140161890 JANETH JASSON RWIZA HOLY CROSS 2 20140142894 CATHERINE JACKSON MUGYABUSO HOLY CROSS 3 20140158817 MARTHA FREDRICK KIULA KAMO 4 20141283912 VANESSA ARISTIDES MSOKA JOYLAND B.UFUNDI BWENI SHULE YA SEKONDARI MTWARA UFUNDI - BWENI NA NAMBA YA PREM JINA LA MWANAFUNZI SHULE ATOKAYO 1 20140246791 PRINCESSREBECA ALOYCE MOSHA SHALOM 2 20140293569 SUZAN DIOCRES PETER MWANGAZA ENG. MED. SHULE YA SEKONDARI TANGA UFUNDI - BWENI NA NAMBA YA PREM JINA LA MWANAFUNZI SHULE ATOKAYO 1 20140271585 FATUMA IBRAHIMU NASSORO SOKOINE 2 20141282072 ALAWIA ASHIRI KIBWANGA KIBURUGWA 3 20140813416 LUCY MARTIN NDEU MGULANI C.BWENI KAWAIDA SHULE YA SEKONDARI KAZIMA - BWENI NA NAMBA YA PREM JINA LA MWANAFUNZI SHULE ATOKAYO 1 20141358656 ASHURA ISSA NGULANGWA NZASA 2 20140961580 SHUFAA HAMADI TAMBARA UKOMBOZI 3 20140801607 NAIMA RAZACK MCHALAGANYA TAIFA 4 20140437650 HALIMA HASHIMU MPEGEA RUVUMA SHULE YA SEKONDARI LOWASSA- BWENI NA NAMBA YA PREM JINA LA MWANAFUNZI SHULE ATOKAYO 1 20141303924 RAHMA ALLY KWAKWADU MBANDE SHULE YA SEKONDARI LUGOBA-
    [Show full text]
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? With Partial Support from a TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? ACKNOWLEDGEMENTS This review was compiled and edited by Tanzania Development Research Group (TADREG) under the supervision of the Steering Group of Policy Forum members, and has been financially supported in part by Water Aid in Tanzania and Policy Forum core funders. The cartoons were drawn by Adam Lutta Published 2013 For more information and to order copies of the review please contact: Policy Forum P.O Box 38486 Dar es Salaam Tel: +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] ISBN: 978-9987 -708-09-3 © Policy Forum The conclusions drawn and views expressed on the basis of the data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. Every effort has been made to verify the accuracy of the information contained in this review, including allegations. Nevertheless, Policy Forum cannot guarantee the accuracy and completeness of the contents. Whereas any part of this review may be reproduced providing it is properly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. Designed by: Jamana Printers b TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TABLE OF CONTENTS POLICY FORUM’s OBJECTIVES .............................................................................................................
    [Show full text]
  • MKUTANO WA TATU Kikao Cha Hamsini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Hamsini na Sita – Tarehe 22 Juni, 2021 (Bunge Lilianza saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Waheshimiwa tunaendelea na Mkutano wetu wa Tatu, leo ni Kikao cha Hamsini na Sita na kabla hatujaendelea nitumie nafasi hii kuwashukuru sana wasaidizi wangu wote wakiongozwa na Mheshimiwa Naibu Spika, Mheshimiwa David Kihenzile, Mheshimiwa Zungu na Mheshimiwa Najma kwa kazi nzuri ambayo wameifanya wiki nzima kutuendeshea mjadala wetu wa bajeti. (Makofi) Sasa leo hapa ndio siku ya maamuzi ambayo kila Mbunge anapaswa kuwa humu ndani, kwa Mbunge ambaye Spika hana taarifa yake na hatapiga kura hapa leo hilo la kwake yeye. (Makofi) Katibu. NDG. NENELWA MWIHAMBI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Maswali na tunaanza na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Kwela. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 465 Ujenzi wa Makao Makuu ya Halmashauri Katika Mji wa Laela MHE. DEUS C. SANGU aliuliza:- Je, ni lini Serikali itakamilisha ujenzi wa Ofisi za Makao Makuu ya Halmashauri ya Sumbawanga katika Mji wa Laela baada ya agizo la Serikali la kuhamisha Makao Makuu? SPIKA: Majibu ya swali hilo muhimu la watu wa Kwela, Mheshimiwa Naibu Waziri - TAMISEMI, Mheshimiwa Dkt. Festo Dugange tafadhali. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deus Clement Sangu, Mbunge wa Jimbo la Kwela kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Halmashauri ya Wilaya ya Sumbawanga ni miongoni mwa Halmashauri 30 zilizohamia kwenye maeneo mapya ya utawala mwaka 2019.
    [Show full text]
  • 1458125147-Hs-6-4-20
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA SITA Kikao cha Nne – Tarehe 3 Februari, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA VIWANDA, BIASHARA NA MASOKO: Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Tume ya Ushindani kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010 [The Annual Report and Audited Accounts of Fair Competition Commission for the Financial year 2009/2010]. NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Serikali ya Utekelezaji wa Azimio la Bunge juu ya Uendeshaji wa Sekta Ndogo ya Gesi Nchini. MASWALI NA MAJIBU Na. 39 Uwekezaji wa Kibiashara wa Nchi ya Libya Tanzania MHE. JOSEPH O. MBILINYI aliuliza:- Aliyekuwa Kiongozi wa Libya Marehemu Kanali Muamar Gaddafi, alijulikana sana kwa kuwekeza mabilioni ya dolla kwenye nchi mbalimbali za Kiafrika, kibiashara na kijamii kama hoteli, barabara na misikiti: (a) Je, Tanzania ilifaidikaje na uwekezaji wa Gaddafi kibiashara hapa nchini? (b) Kwa kuwa, Serikali ya Tanzania haitambui Serikali ya mpito ya Libya. Je, ni nani anayesimamia uwekezaji wa biashara wa Marehemu Kanali Gaddafi hapa nchini? NAIBU SPIKA: Ahsante sana, mabadiliko hayo hayabadilishi maudhui ya swali. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, UWEKEZAJI NA UWEZESHAJI: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joseph Osmund Mbilinyi, Mbunge wa Mbeya Mjini, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa mujibu wa kumbukumbu zilizopo katika Kituo cha Uwekezaji nchini (TIC), Marehemu Kanali Muammar Gaddafi hakuwahi binafsi kuwekeza kibiashara hapa nchini.
    [Show full text]
  • Bspeech 2008-09
    HOTUBA YA WAZIRI WA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA, MHESHIMIWA STEPHEN MASATO WASIRA (MB) KUHUSU MAKADIRIO YA MATUMIZI YA FEDHA YA WIZARA YA KILIMO CHAKULA NA USHIRIKA KWA MWAKA 2008/2009 UTANGULIZI 1. Mheshimiwa Spika, naomba kutoa hoja kwamba Bunge lako Tukufu baada ya kuzingatia taarifa iliyowasilishwa hapa Bungeni leo na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Kilimo Mifugo na Maji inayohusu Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika, sasa lijadili na kukubali kupitisha makadirio ya Matumizi ya Kawaida na ya Maendeleo ya Wizara ya Kilimo Chakula na Ushirika kwa mwaka wa Fedha wa 2008/2009. 2. Mheshimiwa Spika, awali ya yote nitumie fursa hii kuungana na Watanzania wenzangu kumpongeza Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Jakaya Mrisho Kikwete kwa kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Umoja wa Afrika. Kuchaguliwa kwake, na mchango wake alioutoa tangu kuchaguliwa kwake kuwa Mwenyekiti wa Umoja huo umelijengea Taifa letu heshima kubwa katika medani ya kimataifa. Aidha, uongozi wake na juhudi zake za kupambana na maovu katika jamii yetu, licha ya kusimamia utekelezaji wa Ilani ya Chama cha Mapinduzi kwa ajili ya Uchaguzi wa Mwaka 2005 ni kielelezo dhahiri kuwa ni kiongozi anayejali haki na maendeleo ya nchi yetu. Juhudi zake hizo zimedhihirisha uwezo wake mkubwa wa kuongoza na utumishi wake uliotukuka aliouonyesha katika nyadhifa mbali mbali alizowahi kushika katika Serikali na Chama cha Mapinduzi. Wananchi wanaendelea kuwa na imani na matumaini makubwa kwa uwezo wake katika kuliongoza Taifa letu. 1 3. Mheshimiwa Spika, nitumie fursa hii pia kumpongeza Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda (MB) kwa kuteuliwa kwake kuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
    [Show full text]
  • Tarehe 4 Februari, 2013
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA KUMI Kikao cha Tano – Tarehe 4 Februari, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 53 Hospitali ya Wilaya ya Nyang’hwale Kupatiwa Watumishi MHE. JOSEPHINE T. CHAGULLA aliuliza:- Hospitali ya Karumwa ambayo ni ya Wilaya mpya ya Nyang’hwale haina watumishi wa kutosha kwani ina daktari mmoja, Manesi watatu na mtaalam mmoja wa Maabara:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupeleka watumishi wa kutosha katika hospitali hiyo? 1 NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Josephine Tabitha Chagulla, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kwamba Kituo cha Afya, Karumwa kilichoko katika Wilaya mpya ya Nyang’hwale kina Daktari mmoja, Manesi watatu na Mtaalam mmoja wa maabara. Kutokana na tatizo la upungufu wa watumishi wa sekta ya afya kuwepo katika hospitali, vituo vya afya na Zahanati zote nchini kikiwemo kituo cha afya Karumwa, Serikali imechukua jitihada za makusudi kuhakikisha kuwa udhahili wa wanafunzi wanaojiunga na fani za Udaktari na Uuguzi unaongezeka katika vyuo vikuu na vyuo vya ngazi ya Diploma na cheti. Aidha, Serikali imerejesha kada za chini za afya zilizokuwa zimefutwa. Mheshimiwa Naibu Spika, pamoja na jitihada hizo, hivi sasa Serikali kupitia Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii inawapanga wahitimu wa fani za afya moja kwa moja katika vituo vya kazi baada ya kibali kutolewa na Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kumi na Moja – Tarehe 22 Aprili, 2008 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Bodi ya Tumbaku Tanzania kwa mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2007 (The Annual Report and Audited Accounts of the Tanzania Tobacco Board for the year ended 30th June, 2007). WAZIRI WA ELIMU NA MAFUNZO YA UFUNDI: Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Bodi ya Mikopo ya Wanafunzi wa Elimu ya Juu kwa mwaka 2006/2007 (The Annual Report and Accounts of the Higher Education Students Loans Board (HESLB) for the year 2006/2007). Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Mamlaka ya Elimu Tanzania kwa Mwaka 2006/2007 (The Annual Report and Accounts of the Tanzania Education Authority for the year 2006/2007). MASWALI NA MAJIBU Na. 132 1 Hali mbaya ya Walimu na Shule za Msingi MHE. MOHAMED R. ABDALLAH (K.n.y. MHE. BENITO W. MALANGALILA) aliuliza:- Kwa kuwa, hivi sasa Serikali imetenga fedha nyingi katika Wizara ya Elimu na Mafunzo ya Ufundi, lakini pamoja na fedha hizo kutengwa bado hali siyo nzuri katika elimu ya msingi nchini:- (a) Je, Serikali inaelewa kuwa bado wapo walimu katika shule za msingi wanaoishi katika nyumba za nyasi? (b) Je, Serikali inaelewa kuwa wapo wanafunzi wanaosomea chini ya miti katika baadhi ya shule za msingi nchini? (c) Je, Serikali imechukua hatua gani katika kutatua matatizo hayo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu naomba kujibu swali la Mheshimiwa Benito William Malangalila, Mbunge wa Mufindi Kusini, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, Ofisi yangu haina taarifa rasmi kuhusu walimu wanaoishi katika nyumba za nyasi pamoja na kwamba tunaelewa kuwa kuna upungufu mkubwa wa nyumba za walimu hapa nchini.
    [Show full text]