1458127169-Hs-7-3-20

1458127169-Hs-7-3-20

Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) 12 APRILI, 2012 BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Tatu – Tarehe 12 Aprili, 2012 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tuendelee kusimama. Waheshimiwa Wabunge tutakumbuka kwamba tumepata misiba mikubwa hivi karibuni, kama ilivyo ada nitaomba tusimame kwa heshima ya mwakilishi wa Jimbo la Bububu Mheshimiwa Salum Amour Mtondoo. Lakini vile vile Mkuu wa Majeshi Mstaafu Jenerali Mwita Kyaro, lakini vile vile Mkuu wa Jeshi la Polisi Mstaafu, Marehemu Harun Mahundi naomba tusimame kwa dakika moja tukiwakumbuka. (Hapa Waheshimiwa Wabunge walisimama kwa dakika moja kuwakumbuka waliotutangulia mbele ya haki) NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, shughuli za asubuhi ya leo naomba niwakumbushe Wabunge wote na Watanzania kwa ujumla kwamba leo tarehe 12/04/2012 ni siku ya Kumbukumbu ya kifo cha mpendwa wetu aliyekuwa Waziri Mkuu Ndugu yetu Edward Moringe Sokoine na Kumbukumbu yake Kitaifa leo itafanyika kule Morogoro ambako kutakuwa na ibada kwa ajili hiyo. 1 12 APRILI, 2012 Kutakuwa na basi ambalo litaondoka hapa kwenye saa nne. Kwa hiyo, Waheshimiwa Wabunge ambao watapenda kufanya hivyo tuingie katika usafiri huo. KIAPO CHA UTII Wabunge wafuatao waliapa Kiapo cha Utii na kukaa katika nafasi zao ndani ya Ukumbi wa Bunge. Mheshimiwa Cecilia Daniel Paresso Mheshimiwa Joshua Samwel Nassari (Hapa Wabunge walishangilia na kupiga vigelegele baada ya Kiapo) NAIBU SPIKA: Order. Katibu hatua inayofuata. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU SERA URATIBU NA BUNGE: Taarifa ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Hesabu zilizokaguliwa za Serikali za Mitaa kwa Mwaka ulioishia Tarehe 30 Juni, 2011. (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Audit of the Financial Statements of the Local Government Authorities for the year ended 30 th June, 2011) NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE. GREGORY GEORGE TEU): Mheshimiwa Naibu Spika, kwa ruhusa yako na kupitia kwako kabla ya kuwasilisha Hati Mezani naomba nitoe taarifa fupi ndani ya Bunge lako Tukufu kwamba katika mkutano wa Umoja wa Mataifa (The United National General Assembly) , uliofanyika Novemba, 2011. 2 12 APRILI, 2012 Mkutano huu uliridhia kwamba Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania Ndugu Ludovick Utoah, (The Controller and Auditor General of the United Republic of Tanzania) na ofisi yake kuwa mmoja wa Wajumbe wa Bodi ya Ukaguzi wa Mahesabu pamoja na programs mbalimbali za Umoja wa Mataifa kuanzia tarehe 1 Julai, 2012 kwa kipindi cha miaka 6 mfululizo. Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali wa Tanzania ataungana na wenzake kutoka Supreme Audit Institution ya China na Supreme Audit Institution ya Uingereza kuunda Bodi ya ukaguzi wa umoja wa Mataifa kwa kipindi chote cha miaka 6. Kupitia uteuzi huu Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi itapata fursa nzuri na uzoefu wa kujenga uwezo wa kushiriki issues mbalimbali za ukaguzi wa kimataifa na hii ni motisha kubwa kwa wafanyakazi wa Ofisi ya Taifa ya Ukaguzi. Hii ni heshima kubwa kwa ofisi na nchi kupata fursa hii ambayo nchi nyingi wanachama wa Umoja wa Mataifa walikuwa wanainuia. Kupitia Ukaguzi huu nchi yetu itapafa fedha za kigeni yaani forex kupitia ada za ukaguzi zitakuwa zinalipwa na Umoja wa Mataifa. Serikali itatoa support kwa kadri itakavyoona inafaa katika kutekeleza jukumu hili la ukaguzi wa Umoja wa Mataifa. Mheshimiwa Naibu Spika, baada ya pongezi hizi kwa niaba ya Waziri wa Fedha naomba sasa uniruhusu kuweka Mezani Hati zifuatazo:- Taarifa ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu kwa Mwaka ulioishia Tarehe 30 Juni, 2011 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Audit of the Financial Statements of the Central Government for the Year Ended 30 th June, 2011). Taarifa ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Juu ya Hesabu zilizokaguliwa za Mashirika ya 3 12 APRILI, 2012 Umma kwa Mwaka 2010/2011 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Audit of Public Authorities and Other Bodies for the Financial Year 2010/2011). Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Ukaguzi Jumuifu wa Ufanisi na Upembuzi kwa kipindi kilichoishia tarehe 31 Machi, 2012 (Report of the Controller and Auditor General of Tanzania on the Performance and Forensic Audit conducted for the period ending 31 st March, 2012). Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Juu ya Hesabu zilizokaguliwa za miradi ya Maendeleo kwa Mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2011 (Report of the Controller and Auditor General of Tanzania on the Audit of the Financial Statements of Donor Funded Projects for the year ended 30 th June, 2011). Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Ripoti ya Ufanisi inayohusu Ukaguzi wa Magari na Udhibiti wa Mwendo wa Magari katika kupunguza Ajali za Barabarani (A Performance Audit Report on the Management of Traffic Inspections and Speed Limits in Tanzania). Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Ukaguzi wa Ofisi za Balozi (Report of the Controller and Auditor General of Tanzania on the Audit of the Financial Statement of the Tanzania Embassies/Mission for the Year ended 30 th June, 2011). Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Ofisi ya Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali Tanzania kwa Mwaka 2010/2011 (The Annual Report and Accounts of the National Audit Office of Tanzania for the Period 2010/2011). 4 12 APRILI, 2012 NAIBU SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri wa Fedha tunakushukuru sana. Swali la kwanza kwa siku ya leo litaulizwa na Mheshimiwa Mariam Ruben Kasembe. MHE. KABWE Z. ZITTO: Mheshimiwa Naibu Spika, … NAIBU SPIKA: Nitakupa nafasi baada ya kipindi cha Maswali na Majibu nitakupa nafasi. MHE. KABWE Z. ZITTO: Samahani, Kiongozi wa Kambi Upinzani Bungeni ndio anatakiwa kuanza kuuliza swali. NAIBU SPIKA: Kiongozi wa Upinzani Bungeni alisimama? Kiongozi wa upinzani Bungeni una swali? Sikukuona samahani. MASWALI KWA WAZIRI MKUU MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Naibu Spika, kwanza nichukue nafasi hii kuomba/kutoa pole kwa Watanzania wote ambao wamefikwa na misiba ambayo ilikumba taifa siku za karibuni. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa muda mrefu yamekuwepo matamko mbalimbali yanayotokana na Viongozi wa Serikali na mengine yakitoka kwa Viongozi wa Chama cha Mapinduzi kwamba maeneo ambayo Watanzania wanachagua Vyama vya Upinzani kuwa wawakilishi wao katika vyombo vya maamuzi kama Madiwani na Wabunge hayatapata mgao wa fedha za maendeleo. (Makofi) Mheshimiwa Waziri Mkuu tunaomba sasa kauli yako kama kauli ya Serikali uwaeleze Watanzania kupitia Bunge hili kama ni kweli Serikali inayoongozwa na Chama cha Mapinduzi ina Sera ya Ubaguzi katika mgao wa pato la taifa na kama kweli Sera hiyo ipo ni kikao gani kinachokaa kufanya mgao huo zaidi ya Bunge la Bajeti ambalo sisi wote tunakaa hapa kwa maana ya wawakilishi wetu wa Tanzania kutoka Vyama vyote 5 12 APRILI, 2012 ambavyo vimepigiwa kura. Mheshimiwa Waziri Mkuu tunaomba utupe majibu hayo. ( Makofi ) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, ni lazima nionyeshe masikitiko yangu sana kwenye swali hili kwa sababu limeulizwa kijumla na linatoa picha kana kwamba anayoyasema ndio mambo yanayotekelezwa wakati anajua kabisa kwamba hiyo si kweli. Hakuna mahali popote hapa nchini ambako hatujapeleka fedha kulingana na mgao wa taifa bila kujali kama eneo hilo ni la CHADEMA la CU F au la Chama kingine chochote. (Makofi) Kwa hiyo, kidogo nimestushwa na hiyo kauli lakini basi labda niishie hapo tu. ( Makofi ) MHE. FREEMAN A. MBOWE: Mheshimiwa Waziri Mkuu, pamoja na masikitiko yako napenda kukufahamisha kwamba kauli kama hizi zimekuwa zinatolewa mara kwa mara na ninaweza nikatoa mifano halisi na mfano wa kwanza kauli hizi zimetolewa na Waziri Mheshimiwa Mary Nagu wakati wa Kampeni za Uchaguzi katika Jimbo la Arumeru Mashariki. Kauli kama hizi zimetolewa na Naibu Waziri wa Ardhi katika Jimbo la Arumeru Mashariki, Mkoani Arusha. Matamshi kama haya yaliwahi kutolewa na Waziri wa Ujenzi Mheshimiwa John Magufuli katika kampeni za Igunga. Mheshimiwa Waziri Mkuu ahadi kadhaa zimekuwa zinatolewa na Serikali wakati wa kampeni kipindi ambacho kinajulikana kabisa kwamba ni marufuku kwa watendaji wa Serikali kutoa kauli kama hizo na umarufuku huo unatiwa halali na hukumu iliyofanyika katika Jimbo la Kigoma Mjini kufuatia kauli iliyotolewa na Serikali pamoja na ziada ya Rais Mheshimiwa Mstaafu Mzee Mwinyi wakati wa ziara katika uchaguzi wa Jimbo la Kigoma Mjini. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mbunge sasa swali. 6 12 APRILI, 2012 MHE. FREEMAN A. MBOWE: Sasa Mheshimiwa Waziri Mkuu unatuambia vipi tutakapoweza kukudhihirishia kwamba kauli hizo zimetoka na utachukua basi hatua gani kwa Mawaziri wako ambao wametoa kauli hizo? ( Makofi ) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, mimi nafikiri Watanzania tuendelee kujenga demokrasia yetu tumejitahidi sana. Serikali hii itaendelea kutimiza wajibu wake kwa mujibu wa Katiba na Sheria za Nchi hii katika mgao wake wote wa fedha. Sasa kama kuna kauli nyingine, kauli zinatoka, nyingine kwenye mapambano wakati wa chaguzi na nini mimi nasema tutaendelea kuheshimu Katiba na Sheria. ( Makofi ) MHE. MARIAM R. KASEMBE: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali kwa Waziri Mkuu. Kwanza kabisa naomba nichukue nafasi hii kuwapa pole sana Wakulima wa Zao la Korosho popote walipo nchini na

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    260 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us