1 BUNGE LA TANZANIA ___MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA SABA Kikao Cha Hamsini Na Sita – Tarehe 29 Juni
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Hamsini na Sita – Tarehe 29 Juni, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Naomba tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wa Saba, Kikao cha Hamsini na Sita. Katibu! NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Mwaka ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Sekta ya Hifadhi ya Jamii kwa Mwaka 2015/2016 (The Annual Report of Social Security Regulatory Authority for The Year 2015/2016). 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Hati ya Uhamishaji Fedha Na. 1 ya mwaka 2016/2017 (Statement of Reallocation Warrant No. 1 of 2016/2017); na Hati ya Uhamishaji Fedha Na. 2 ya mwaka 2016/2017 (Statement of Reallocation Warrant No. 2 of 2016/2017). SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri Fedha na Mipango. Katibu! NDG. CHARLES MLOKA – KATIBU MEZANI: MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu; Mheshimiwa Waziri Mkuu karibu. (Makofi) Swali la kwanza litaulizwa na Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Morogoro Kusini Mashariki, ambaye ni Mheshimiwa Omary Tebweta Mgumba. Mheshimiwa Mgumba! MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Spika, nashukuru kwa kunipa nafasi hii kumuuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu swali la kwanza. Mheshimiwa Waziri Mkuu, wewe ndiye Kiongozi wa Serikali yetu ya Chama cha Mapinduzi ndani ya Bunge, lakini pia ndiye kiranja mkuu wa Serikali hii ya Awamu ya Tano. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kama unavyofahamu kuna wazabuni wengi katika Halmashauri zetu tunakotoka ambao sisi ni wawakilishi wao pamoja na Serikali Kuu, walifanya kazi ya kutoa huduma katika taasisi za Serikali na Serikali yenyewe kwa muda mrefu, wengine wana miaka miwili, mitatu, wengine mpaka mitano, lakini mpaka sasa hawajalipwa stahiki zao. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Waziri Mkuu ukizingatia mnamo tarehe 01 Juni ndani ya Bunge hili, uliliambia Bunge hili kwamba malipo yanachelewa ni kwa sababu wanafanya uhakiki, ambalo ni jambo zuri, kuwagundua wale ambao wanastahili kulipwa… SPIKA: Swali Mheshimiwa Mgumba, moja kwa moja! MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Spika, nataka kumuuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu, watu hawa wamesubiri kwa muda mrefu na ukaguzi umeshafanyika zaidi ya mara tano, nini kauli ya Serikali, watawalipa lini wazabuni wote waliotoa huduma ndani ya Serikali? SPIKA: Majibu ya swali hilo muhimu Mheshimiwa Waziri Mkuu tafadhali. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mgumba, Mbunge wa Morogoro Vijijini, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, upo ukweli kwamba, Serikali inadaiwa na wazabuni wetu waliokuwa wanatoa huduma kwenye maeneo mbalimbali. Wako ambao wametoa huduma kwenye Halmashauri za wilaya kwa maana ya huduma kwenye shule, kwenye magereza, lakini pia wako ambao wamefanya kazi za kutoa huduma kwenye Wizara mbalimbali. Na kwa mara ya mwisho nilikuwa hapa nilipata swali la aina hii linalowahusu wadai/wazabuni wa pembejeo, wote hawa ni watoa huduma ndani ya Serikali. Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba tumeweza kugundua kwamba baadhi ya madeni na baadhi ya wadai wachache miongoni mwao wametuletea taarifa za madai ambayo si sahihi sana. Na kweli, tulichokifanya tulitoa maagizo kwenye maeneo yote, ili kuhofu kupoteza fedha, kulipa fedha ambayo haikufanyiwa kazi kwa madai yale. Kwa hiyo, tumeendesha zoezi la uhakiki chini ya Wizara ya Fedha na taasisi yetu kupitia CAG, hasa kule kwenye 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) madeni makubwa ili kujiridhisha viwango vinavyotakiwa kulipwa kwa wazabuni hawa. Mheshimiwa Spika, tuliweka utaratibu kwamba angalao kufikia mwishoni mwa mwezi huu tuwe tumemaliza hilo zoezi la uhakiki halafu tuanze kulipa madeni haya. Kwa hiyo ni matarajio yangu kwamba Wizara ya Fedha watanipa taarifa, na Wizara zile zote ambazo zina madeni ya watoa huduma zitatoa taarifa ya viwango vya fedha, halafu sasa tusimamie Wizara ya Fedha kuweza kuwalipa hawa watoa huduma. Mheshimiwa Spika, nataka nitumie nafasi hii, kwanza niwashukuru kwa uvumilivu wao wadeni wote wanaotudai, lakini pili tuwasihi waendelee kutuvumilia na taratibu hizi kwa lengo lilelile nililokuwa nimelieleza awali la kuokoa fedha ambazo zinalipwa kwa watu ambao hawakutoa huduma. Hata hivyo bado tutaendelea kuwatumia watoa huduma kutoa huduma ndani ya Serikali kwenye maeneo ambayo wameendelea kutoa huduma na tuwahakikishie tu kwamba tutawalipa. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo, Mheshimiwa Mbunge kama wako watoa huduma kwenye eneo lako endelea kuwahakikishia kwamba Serikali tutlipa madeni. Ahsante sana. (Makofi) SPIKA: Mheshimiwa Mgumba, kuna haja ya nyongeza? Hebu tujaribu eeh, maana ahadi umeshapata! MHE. OMARY T. MGUMBA: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Kuna swali dogo tu la nyongeza. Mheshimiwa Spika, kwanza nimpongeze sana Mheshimiwa Waziri Mkuu kwa majibu mazuri ambayo kutoka Serikalini. Swali dogo la tu la nyongeza, kwa kuwa kama ulivyosema kwenye majibu yako ya msingi, kwamba mmegundua kuna watu ambao wameleta madai ambayo 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) si sahihi, lakini naamini pia kuna watu ambao watakuwa madai yao ni sahihi. Sasa nini kauli ya Serikali kwa wale ambao madai yao ni sahihi ambao wamekaa muda mrefu kiasi kwamba imewaongezea gharama kwa maana ya riba sehemu walizokopa, nani atalipa gharama hizi kwa ajili ya usumbufu uliotokea na gharama zilizoongezeka kwenye madeni hayo? (Makofi) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mgumba, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, kama ambavyo nimeeleza kwenye jibu la awali kwamba kwanza tunathamini sana kazi waliyoifanya katika kutoa huduma kwenye sekta zetu. Lakini mbili, tumewashukuru kwa uvumilivu kwa kipindi chote hiki ambacho sisi tunafanya uhakiki. Baadhi ya wadai nimepata nafasio ya kukutana nao hapa Dodoma wakati huu wa Bunge na kuzungumza nao na kuwaambia kwa nini tumechelewa kuwapa fedha zao, wale ambao kweli wana madai halali. Mheshimiwa Spika, lakini bado nirudi tena kusema kwamba, hatuna namna nyingine ya kufanya zaidi ya uchelewaji huu wa kulipa kwa sababu tuko kwenye zoezi la kuhakiki, ili tujiridhishe. Kama ingekuwa tumechelewa tu, kwamba hatuna kazi yoyote, tumeacha tu hapo kungekuwa na swali ambalo naamini unacholenga kingeweza kupata maelezo. Lakini bado niwahakikishie kwamba taratibu zinakamilika na tulisema tunakamilisha tarehe 30 Juni, yaani kesho tu tarehe 30 Juni, tunatarajia Wizara ya Fedha itapewa taarifa kutoka kwenye Wizara mbalimbali, kwamba madai yetu halali ni haya kwa ajili ya watu hawa kwa huduma waliyoitoa, baada ya hapo tunalipa tu na tutaendelea kuwapa nafasi zaidi ya kutoa huduma. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo niwahakikishie kwamba wataendelea kutoa huduma, hasa wale ambao ni waaminifu kwenye awamu ijayo hii ya mwaka wa fedha mpya wa mwaka 2017/2018. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Swali la pili kwa siku ya leo kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu linatoka kwa Mbunge wa Mbulu Mheshimiwa Flatei Gregory Massay. Mheshimiwa Massay tafadhali swali fupi. MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, nashukuru sana. Mheshimiwa Waziri Mkuu, hivi karibuni Serikali imefanya uhakiki wa vyeti fake na imeacha ma-gap na mapengo katika maeneo yetu hasa ya vijijini kwa upande wa afya. Je, lini sasa Serikali mtatusaidia ili vituo vyetu au zahanati ziweze kuendelea kutokana na nafasi hizo ambazo sasa zimechwa wazi? WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba arudie tena swali, maana kulikuwa na msikiko usio sahihi kwenye vipaza sauti vyetu. SPIKA: Tafadhali, kwa kifupi! MHE. FLATEI G. MASSAY: Mheshimiwa Spika, Serikali imefanya uhakiki wa watumishi ambao wana vyeti fake. Sasa baada ya uhakiki huo wengine wameacha vituo vya afya na zahanati zetu kule. Sasa swali langu, je, lini mtaajiri sasa, ili watu wetu kule wapate huduma, hasa kwenye maeneo ya afya ambako watumishi wameshaacha kazi kutokana na kwamba, walikuwa wana vyeti ambavyo havistahili kuendelea kuwepo? Ahsante. SPIKA: Kuziba mapengo ya mapungufu ya watumishi waliopunguzwa kutokana na vyeti fake. Mheshimiwa Waziri Mkuu, majibu! 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Flatei Massay, Mbunge wa Mbulu, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba tumepitisha zoezi hili la uhakiki wa vyeti kwa watumishi wetu na uhakiki huu baada ya kuwa tumekamilisha tulipata makundi matatu. Kundi la kwanza ni wale wenye vyeti fake moja kwa moja, kundi la pili ni wale wenye vyeti vinavyotumika na zaidi ya mtu mmoja, lakini kundi la tatu uko utata wa majina ambao umejitokeza kwenye vyeti hivi ambavyo wao wamepata nafasi ya kukata rufaa. Sasa wote hawa wameacha pengo kwa sasa, na ndilo ambalo Mheshimiwa Mbunge amelizungumzia, lini tunatoa ajira. Mheshimiwa Spika, Mheshimiwa Rais wetu Dkt. John Pombe Magufuli ametoa nafasi za ajira zaidi ya 50,000 ili kuziba mapengo haya ambayo yamejitokeza kwa wenye vyeti fake, lakini vilevile ili kuongeza tu ajira kwenye sekta nyingine kwa lengo la kuboresha utoaji huduma kwenye sekta mbalimbali. Mheshimiwa Spika, tayari vibali vimeshatolewa na Wizara ya Utumishi, tumeanza na idara ya elimu, tumesha ajiri walimu wa masomo ya sayansi wamekwenda kwenye vituo, tumetoa pia nafasi kwenye sekta ya afya na vibali hivi vitaendelea kutolewa kadri ya nafasi ambazo Mheshimiwa Rais ameahidi kwa Watanzania. Mheshimiwa Spika, ninaamini Rais wetu mpendwa kwa ahadi yake nafasi hizi ataendelea kuzitoa ili tuzibe mapengo na kuboresha pale ambako kuna upungufu