Chadema Blog: HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
1 More Next Blog» Create Blog Sign In T his site uses cookies from Google to deliver its services, to personalize ads and to analyze traffic. Information about your use of this site is shared with Google. By using this site, you agree to its use of cookies. LEARN MORE GOT IT MONDAY, MAY 27, 2013 HOTUBA YA MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI MHE. HALIMA JAMES MDEE (MB) KUHUSU MAPITIO YA UTEKELEZAJI WA BAJETI YA 2012/2013 NA MAKADIRIO YA MAPATO NA MATUMIZI YA WIZARA YA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI KWA MWAKA WA FEDHA 2013/14 I. UTANGULIZI Mheshimiwa Spika, hakuna ubishi kwamba ardhi ndio msingi mkuu wa uchumu wa taifa lolote, na kwa maana hiyo ardhi ni msingi maisha ya mwanadamu. Ardhi ni miongoni mwa vitu vikuu vine vinavyohitajika ili taifa liendelee. Hayati Mwalimu Julius Kambarage Nyerere aliwashi kusema “Ili taifa liendelee linahitaji watu, ardhi, siasa safi na uongozi bora” Mheshimiwa Spika, nimekuwa nikijiuliza kuhusu chimbuko la umasikini TEAM LOWASSA uliokithiri Tanzania kwa kuzingatia vigezo vya maendeleo alivyotoa Hayati Mwalimu Nyerere. Baada ya kufanya marejeo ya machapisho mbalimbali lakini pia baada yakupata uzoefu wa uongozi kama Mbunge wa Wananchi na hasa kama Waziri Kivuli kwa Arhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi, na kwa kuzingatia mwenendo halisi wa watawala hapa Tanzania nimegundua kuwa kiwazo kikubwa kwa maendeleo ya nchi yetu sio watu (watu wapo wengi sana takribani milioni 45), tatizo sio ardhi (hiyo ipo ya kutosha na ziada takribani [1] hekta milioni 94.3 ). Mheshimiwa Spika, tatizo ni “siasa safi na uongozi bora”. Tofauti na Kauli Mbiu mkakati za kisiasa enzi za Mwalimu, kwamba Sisa ni kilimo, Uhuru na Kazi, Kilimo cha Kufa na Kupona, sasa hivi tunashuhudia siasa za watawala za kuongeza umasikini wan chi hii “kwa ari na kasi zaidi, tunashuhudia watawala wakijigamba kwamba “wamethubutu na wameweza” kuwa mafisadi wa rasilimali za nchi hii. Mheshimiwa Spika, maneno niliyoyatumia hivi punde hayanifurahishi hata kidogo, lakini nimelazimika kuyasema kwa kuwa sioni watawala wa nchi hii wakifikiri namna ya kumkomboa mtanzania kutoka kwenye wimbi la umasikini, bali kila mmoja anajitahidi kujilimbikizia mali hasa kwa hofu ya kuondolewa madarakani (akakosa namna ya kuishi) kutokana na kuenea kwa kasi na kuungwa mkono kwa wingi na wananchi kwa chama kikuu cha upinzani nchini cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA). Mheshimiwa Spika, nasikitika sana kwamba badala ya Serikali ya CCM kutumia muda na rasilimali ilizo nazo kutatua matatizo sugu ya kiuchumi ya taifa hili (hususan uporaji wa ardhi ya wananchi), inatumia fedha nyingi za umma kupambana na CHADEMA ambayo inatetea maslahi ya wananchi. Mheshimiwa Spika, Nchii hii ina rasilimali nyingi sana ikiwemo ardhi ambazo zingeweza kuifanya Tanzania kuwa miongoni mwa nchi za ulimwengu wa pili kiuchumi, lakini tuna tatizo la uhaba wa viongozi wenye “ufahamu, maadili na busara” ya kutumia rasilimali hizi kwa maslahi ya taifa. Mheshimiwa Spika, kutokana na ombwe la uongozi katika taifa hili, na kutokana na “ubinafsi, ulafi na ufisadi” wa viongozi waliopewa dhamana ya kusimamia rasilimali za nchi yetu, leo taifa hili ni masikini, miaka hamsini na mbili baada ya uhuru. Mhshimiwa Spika, Kambi Rasmi ya Upinzani inayoongozwa na CHADEMA imekuwa ikibainisha mapungufu na kasoro nyingi katika masuala ya Ardhi, Nyumba na Maendeleo ya Makazi tangu mwaka 2011 hadi leo, lakini Serikali hii ya CCM imeendelea kuwa na shingo ngumu kuyafanyia kazi mapendekezo ya Kambi ya Upinzani jambo ambalo linaendelea kusababisha migogoro mingi na ufisadi katika umiliki na matumizi ya ardhi hapa nchini Mheshimiwa Spika, katika hotuba ya msemaji mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani katika bajeti ya wizara hii kwa mwaka wa fedha 2011/2012, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni ilianisha matatizo makubwa ya ardhi nyumba na maendeleo ya makazi na kuitaka Serikali kutafuta ufumbuzi kwa kuchukua GOOGLE+ FOLLOWERS hatua za haraka. Matatizo hayo yalikuwa kama ifuatavyo:- Chadema Blogtz Add to circles 1 . Uporaji wa ardhi ya Tanzania unaofanywa chini ya usimamizi wa Serikali kwa mbinu au hila ya uwekezaji, 2. Ufisadi wa ardhi unaofanywa na viongozi wa Serikali na Chama cha Mapinduzi kwa kuuziana ardhi kwa bei ya kutupwa, 3. Ukiukwaji mkubwa wa Sheria ya Ardhi namba 4 ya mwaka 1999 na Sheria namba 5 ya ardhi ya vijiji ambapo viongozi wa Serikali walikuwa wakigawa ardhiki holela bila kuzingatia matakwa ya sheria hizo, 4. Migogoro mikubwa ya ardhi baina ya wakulima na wafugaji ambayo kwa nyakati tofauti imepelekea umwagaji wa damu miongoni mwa wananchi, 5 . Matatizo makubwa katika tathmini ya malipo ya fidia kwa wananchi wanaotakiwa kuondoka katika maeneo yao kupisha matumizi mapya ya ardhi, 6 . Kuendelea kupanda kwa bei ya vifaa vya ujenzi jambo ambalo 3,219 have me in circles View all limesababisha wananchi kuendelea kuishi katika makazi duni na hivyo kuhatarisha usalama wao na kutweza utu wao, RASIMU YA KATIBA 2013 TOLEO 7. Serikali na taasisi zake kutolipa kodi za pango kwa wakati kwa LA PILI (JIPYA) Shrika la Nyumba la Taifa na hivyo kulirudhisha nyuma kimaendeleo, RASIMU YA KATIBA (TOLEO LA PILI) na 8. Wakala wa Taifa wa Utafiti wa Nyumba bora na Vifaa vya Ujenzi kushindwa kuleta mabadiliko kutokana na kuongezeka kwa nyumba zisizo bora ( kama vile nyumba za tembe, tope na nyasi) na kuongezeka kwa bei ya vifaa vya ujenzi Bonyeza Read More Kuendelea Mheshimiwa Spika, Aidha, katika bajeti ya wizara hii kwa mwaka 2012/2013, Kambi Rasmi ya Upinzani iliendelea kuipigania ardhi ya watanzania inayoporwa kwa kuitaka Serikali kufanya yafuatayo:- TEMBELEA JAMIIFORUMS 1 . Kuyarejesha kwa wananchi, mashamba yote yaliyobinafsishwa ambayo wawekezaji wameshindwa kuyaendeleza, 2. Kutatua mgogoro wa ardhi kati ya Hifadhi ya Taifa ya Tarangire na vijiji [2] [3] v y a Gijedabung, Ayamango na Gedamar katika Wilaya ya Babati Mkoani Manyara ambapo mamlaka ya hifadhi ilitoa amri kwa wananchi wa vijiji hivyo kuondoka kwa kuwa walikuwa wako ndani ya hifadhi, 3. Kutatua migogoro ya ardhi kati ya wafugaji na wakulima hasa katika MWANAHALISIFORUM Wilaya ya Karagwa na Biharamulo Mkoani Kagera ambapo wananchi walifukuzwa kwenye maeneo yao ya kilimo na maeneo hayo kugawiwa kwa wafugaji matajiri bila wananchi kuhusishwa, 4 . Kulipa fidia stahiki kwa wananchi wanaotakiwa kuondoka katika maeneo yao kupisha matumizi mapya ya ardhi hasa katika maeneo ya TEMBELEA WANABIDII GROUP Kibamba –Luguruni, Kwembe Kati na Kigamboni Mkoa wa Dar es Salaam, 5 . Kuandaa mpango mkakati na endelevu wa kukomesha uvamizi wa ardhi (hasa katika Manispaa ya Kinondoni ) unaofanywa na magenge ya watu wenye silaha wanaovamia maeneo ya watu, kuharibu mali na kuyakalia maeneo hayo kwa nguvu jambo linalosababisha uvunjifu wa amani na hatimaye vifo, ZIARA YA LOWASSA DSM 6 . Kubatilisha mkataba wa kifisadi kati Kampuni ya Uwindaji ya Game Frontiers of Tanzania Limited na Kampuni mbili za nje za uchimbaji madini za Uranium Resourses PLC na Western Metals, kufanya utafiti wa uchimbaji wa madini ya Uranium kwenye kitalu cha uwindaji katika kijiji cha Mbarang’andu kinyume cha sheria. 7 . Kuanzisha Mamlaka ya Udhibiti wa Kodi za Nyumba (Real Estate Regulatory Authority) ili kuratibu, kuweka viwango na miongozo ya kodi za nyumba ili kuwaondolea wananchi wapangaji wa nyumba adha kubwa ya gharama kubwa za pango zisizo na viwango. Mheshimiwa Spika, baada ya Serikali hii ya CCM kuoneka kutojali maslahi ya wananchi katika kumiliki na kutumia ardhi yao, na baada ya kuongezeka kwa kasi ya kugawa ardhi kwa wageni kwa hila ya uwekezaji, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni inayoongozwa na CHADEMA iliendelea kupambana kuitetea MSAFARA WA LOWASSA KWENDA KUCHUKUA FOMU YA URAIS ardhi ya Tanzania ili wananchi wawe wanufaika wa kwanza wa rasilimali ardhi. TUME YA UCHAGUZI Mheshimiwa Spika, Safari hii, Kambi Rasmi ya Upinzani ilileta hoja binafsi bungeni tarehe 8 Novemba, 2012 kwa ajili ya hatua za kibunge baada ya Serikali kuoneka kutojali uporaji wa ardhi ya wananchi unaofanywa kwa kisingizio cha uwekezaji. Mheshimiwa Spika, katika hoja hiyo, Bunge liliazimia kwamba : 1. Zoezi la ugawaji ardhi kwa wawekezaji wa nje na ndani lisitishwe hadi hapo tathmini ya kina itakapofanyika kubaini ni kiasi gani cha ardhi kipo mikononi mwa wawekezaji na wasio wawekezaji. 2. Tathmini ya kina ifanyike kuweza kubaini raia wa kigeni na wa ndani waliojipatia ardhi kinyemela kupitia serikali za vijiji kinyume na WATANZANIA WANATAKA matakwa ya sheria ya ardhi Na. 5 ya mwaka 1999. MABADILIKO Mheshimiwa Spika, baada ya mvutano mkali kati ya wabunge wa CCM wakiisaidia Serikali yao dhidi ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, hatimaye Serikali ilikubali kwa shingo upande kufanya tathimini ya ardhi iliyoko mikononi mwa wageni lakini ilikataa kusitisha uwagaji wa ardhi kwa wageni. Hata hivyo, Serikali ilitakiwa kuleta ripoti ya tathmini hiyo bungeni mwezi Aprili, 2013, lakini mpaka sasa Serikali haijafanya hivyo. Mheshimiwa Spika, kabla sijajielekeza katika mambo mahsusi yanayohusu wiza hii kwa mwaka wa fedha 2013/2014 napenda kuchukua nafasi hii kwa niaba ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuitaka Serikali ilieleze Bunge hili na CHADEMA- TANZANIA'S wananchi wote, kwamba imetatua kwa kiasi gani matatizo yaliyoainishwa hapo MOVEMENT FOR CHANGE juu na imetekeleza kwa kiasi gani mapendekezo ya Kambi Rasmi ya Upinzani yaliyoorodheshwa hapo juu (moja baada ya jingine) ya tangu mwaka 2011 hadi leo?. Aidha, Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni, inayoongozwa na CHADEMA inaitaka Serikali kulieleza Bunge hili imetekeleza vipi maazimio ya bunge ya tarehe 8 Novemba, 2012 yaliyoitaka Serikali kufanya tathmini ya ardhi iliyopo chini ya umiliki wa wageni