MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao Cha Ishirini Na Moja

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao Cha Ishirini Na Moja NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Ishirini na Moja – Tarehe 4 Mei, 2020 (Bunge Lilianza Saa Nane Mchana) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH -KATIBU MEZANI: TAARIFA YA SPIKA Kwa mujibu wa Kanuni ya 33(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Mwaka 2016, Waheshimiwa Wabunge kwa masikitiko makubwa Mheshimiwa Spika anapenda kuwajulisha kuwa Bunge letu limepatwa na msiba mwingine mkubwa wa kuondokewa na Mbunge na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga ambaye alifariki alfajiri ya kuamkia siku ya Ijumaa tarehe 1 Mei, 2020 Jijini Dodoma na kuzikwa tarehe 2 Mei, 2020 nyumbani kwake Tusamaganga, Iringa. Waheshimiwa Wabunge, pamoja na mengi mazuri na muhimu aliyoyafanya marehemu Mheshimiwa Balozi Mahiga mwaka 2003 mpaka 2010 akiwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, alirejesha heshima ya Tanzania hadi kuwa moja ya nchi zilizounda Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na yeye kuwa Mkuu wa Ujumbe wa Tanzania katika Baraza hilo. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Waheshimiwa Wabunge naomba sasa tusimame kwa muda wa dakika moja kama ishara ya kuomboleza kifo cha mwenzetu. (Hapa Wabunge walisimama kwa dakika moja kuomboleza kifo cha Mhe. Balozi Dkt. Augustine Phillip Mahiga) NAIBU SPIKA: Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina. Tukae. Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH -KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2020/2021. MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU: Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2019/ 2020 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/2021. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Nimwite Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Hayupo. Katibu! 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH -KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU (Maswali yafuatayo yameulizwa na kujibiwa kwa njia ya mtandao) Na. 192 Ujenzi wa Maabara za Shule – Hanang MHE. DKT. MARY M. NAGU aliuliza:- Mwaka 2013 – 2015 Serikali ilihamasisha wananchi kujenga vyumba vya maabara katika shule mbalimbali Wilayani Hanang lakini hadi sasa maabara hizo hazijakamilika. Je Serikali ipo tayari kutoa fedha ili kukamilisha ujenzi wa maabara hizo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Mary Michael Nagu, Mbunge wa Hanang, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ipo tayari kuunga mkono jitihada za wananchi katika ukamilishaji wa ujenzi wa maabara za shule za sekondari kwa ajili ya masomo ya sayansi. Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021, Serikali imeidhinishiwa shilingi bilioni 42 kwa ajili ya ukamilishaji wa maabara zilizojengwa kwa nguvu za wananchi. Kati ya fedha hizo, Halmashauri ya Wilaya ya Hanang imeidhinishiwa Shilingi milioni 210 ambazo zitatumika kukamilisha maabara saba. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 193 Kuboresha Miundombinu ya Elimu Rufiji MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA aliuliza:- Shule nyingi katika Wilaya ya Rufiji zimechakaa kwani nyingi zilijengwa wakati wa Mkoloni. (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuzikarabati shule hizo? (b) Je, ni lini Serikali itaboresha miundombinu ya shule za Sekondari Muhoro na Ikwiriri ili ziwe za kidato cha Tano na Sita? WAZIRI WA NCHI, OFlSI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa, Mbunge wa Rufiji, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuzikarabati shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji ambapo katika mwaka wa fedha 2017/ 2018 Halmashauri ilipatiwa kiasi cha Shilingi milioni 259 kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Sekondari Utete. (b) Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2017/2018 na 2018/2019, Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji imepatiwa kiasi cha Shilingi milioni 256 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili (2), matundu 10 ya vyoo na kukamilisha maboma nane (8) ya madarasa katika Shule ya Sekondari Muhoro. Vilevile, katika mwaka wa fedha 2018/2019, Halmashauri ilipatiwa kiasi cha Shilingi milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu (3) vya madarasa katika Shule ya Sekondari Ikwiriri. Miundombinu hiyo imeboreshwa ili kuziwezesha shule hizo kuanza kudahili wanafunzi wa kidato cha tano. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 194 Mji wa Lamadi Kupewa Hadhi ya Mamlaka ya Mji Mdogo MHE. GIMBI D. MASABA aliuliza:- Mji wa Lamadi uliopo Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu ni miongoni mwa Miji yenye sifa za kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo. Je, ni lini Serikali itautangaza Mji huo kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Gimbi Dotto Masaba, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua uwepo wa miji inayokua kwa kasi ambayo inaweza kupewa hadhi ya Mamlaka za Miji Midogo ikiwemo Mamlaka ya Mji Mdogo wa Lamadi. Hata hivyo, kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni kuendeleza maeneo mapya ya utawala yaliyoanzishwa tayari kwa kuyawekea miundombinu na huduma muhimu ili yaanze kutoa huduma kwa wananchi kabla ya kuanzisha maeneo mapya ya utawala. Na. 195 Serikali Kupunguza Kodi ya Huduma MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupunguza Kodi ya Huduma (Service Levy) kutoka 0.03 na kuwa 0.01 ili kuleta unafuu kwa wafanyabiashara nchini? 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniventura Destery Kiswaga, Mbunge wa Magu, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ushuru wa huduma (Service Levy) unaotozwa kwa Mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290, Kifungu cha 6(u) na 7(z). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, Halmashauri zina hiari na uwezo wa kupanga kiwango cha Ushuru wa Huduma kisichozidi Asilimi 0.3 (not exceeding 0.3 %). Hivyo, Sheria imetoa mwanya wa kupunguza ushuru huo kulingana na mazingira ya biashara, uzalishaji na ulipaji wa kodi katika Halmashauri husika. Na. 196 Mafunzo ya Afya ya Uzazi Salama MHE. SABREENA H. SUNGURA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itawafikia Mama wa Tanzania kote kwa kuwapa mafunzo dhidi ya Afya ya Uzazi Salama? WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sabreena Hamza Sungura, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, katika juhudi za kuboresha huduma za afya ya uzazi, ni muhimu sana wanawake wote, hasa walio katika umri wa kuzaa, miaka 15 hadi 49 wapate elimu ya afya ya uzazi salama. Mafunzo haya hujumuisha, uzazi wa mpango, umuhimu wa kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito, huduma za dharura kwa matatizo yatokanayo na uzazi, magonjwa ya zinaa, virusi vya UKIMWI/VVU na madhara ya madawa ya kulevya. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Afya imeendelea kutoa mafunzo ya uzazi salama kwa kupitia njia mbalimbali ikiwemo vipeperushi na mabango, vipindi vya redio na televisheni. Katika kipindi cha Januari hadi Juni, 2019, Wizara imeweza kutumia njia hizo za kuelimisha na kutoa mafunzo na kuwafikia jumla ya wanawake 1,480,900 Tanzania Bara. Kupitia mafunzo haya, Idadi ya akinamama wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma imeendelea kuongezeka hadi kufikia asilimia 83 mwezi Machi, 2020 ikilinganishwa na asilimia 64 kwa kipindi kama hicho mwaka 2015/2016 Mheshimiwa Naibu Spika, lengo la Wizara ni kuwa, kufikia mwaka 2020, kila mwanamke aliye katika umri wa kujifungua atakuwa amefikiwa na elimu hii. Elimu hii itasaidia akinamama kuhudhuria kliniki mapema mara tu wanapogundua ni wajawazito na pia kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma ili waweze kuhudumiwa na watoa huduma wenye ujuzi. Na. 197 Ufanisi wa Sospa Kuzuia Udhalilishaji kwa Mtoto wa Kike MHE. JANET Z. MBENE aliuliza:- Hivi karibuni limejitokeza suala lililozua mjadala mkubwa kuhusu wanafunzi kupata mimba na kusababisha kukatisha masomo yao, mwaka 1998 Bunge lilipitisha Sheria maalum ya makosa ya kujamiiana (SOSPA) ambayo ilibadili sheria kadhaa na kuweka sheria inayoshughulikia makosa ya udhalilishaji wa kingono na wa kijinsia iliyolenga kurudisha heshima, usalama na hadhi ya wanawake na watoto. (a) Je mpaka sasa ni watu wangapi waliotiwa hatiani na kufungwa kifungo kilichoainishwa kwenye sheria hiyo? (b) Je kati ya watu waliofungwa watu wazima ni wangapi na wanafunzi waliowapa mimba wanafunzi wenzao ni wangapi na wako wapi kwa sasa? 7 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (c) Je kati ya watoto waliopo shuleni na ambao hawapo shuleni, ni wangapi waliobakwa au kurubuniwa na wangapi waliofanya nao mapenzi kwa hiari? WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Janeth Zebedayo Mbene, Mbunge wa Ileje, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasa jumla ya watuhumiwa 456 wamekwishatiwa hatiani,
Recommended publications
  • 1458137638-Hs-4-4-20
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE KIKAO CHA NNE – TAREHE 14 JUNI, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 37 Ardhi Iliyotolewa Kujenga Shule ya Msingi Kiraracha MHE. AUGUSTINO L. MREMA aliuliza:- Mzee Pauli Sananga Lekule wa Kijiji cha Kiraracha, Kata ya Marangu, Wilaya ya Moshi Vijijini, alitoa ardhi yake ikatumika kujenga shule ya msingi Kiraracha, Marangu miaka 10 iliyopita akiahidiwa na Serikali kupewa eneo jingine kama fidia lakini mpaka sasa hajapewa eneo jingine kama fidia jambo lililomfanya aione Serikali haikumtendea haki. Je, ni lini Serikali itamlipa haki yake kutokana na makubaliano hayo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Augustino Lyatonga Mrema, Mbunge wa Vunjo kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua kuwa Ndugu Pauli Sananga Lekule wa Kijiji cha Kiraracha, Kata ya Marangu Magharibi, alitoa ardhi yake kwa ajili ya ujenzi wa shule ya msingi Kiraracha, Kata ya Marangu Magharibi kwa ahadi ya kufidiwa eneo lililoko Njia panda. Aidha eneo ambalo Halmashauri ya Wilaya ya Moshi ilitarajia kumfudia Ndugu Lekule lipo katika mgogoro na kesi bado inaendelea Mahakama Kuu. 1 Mheshimiwa Spika, kwa kuwa eneo lililopimwa viwanja na kutarajia mlalamikaji lipo katika mgogoro wa kisheria kati ya Halmashauri na wananchi, Serikali inaendelea kufuatilia mwenendo wa kesi na mara shauri litakapomalizika Mahakamani mhusika atapewa eneo lake. Mheshimiwa Spika, katika jitihada za Serikali kuhakikisha shauri hili haliendelei kuchukua muda mrefu, Halmashauri ya Wilaya ya Moshi imeunda timu kwa ajili ya kufuatilia na kuharakisha shauri hili ili ikiwezekana limalizike nje ya Mahakama ili Ndugu Lekule Sananga aweze kupata haki yake mapema.
    [Show full text]
  • Tarehe 28 Juni, 2017
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Hamsini na Tano – Tarehe 28 Juni, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- MHE. GEORGE M. LUBELEJE (K.n.y. MHE. KAPT. MST. GEORGE H. MKUCHIKA - MWENYEKITI WA KAMATI YA HAKI, MAADILI NA MADARAKA YA BUNGE): Taarifa ya Kamati ya Haki, Maadili na Madaraka ya Bunge kuhusu Shauri la Kudharau Mamlaka ya Spika linalomhusu Mheshimiwa Joshua Samwel Nassari, Mbunge na Shauri la Kusema Uwongo Bungeni linalomhusu Mheshimiwa Conchesta Leonce Rwamlaza, Mbunge. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Katibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali tutaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu. Mheshimiwa Mgeni Jadi Kadika, Mbunge wa Viti Maalum, kwa niaba yake Mheshimiwa Mheshimiwa Mwanne Mchemba. Na. 452 Mradi wa MIVARF MHE. MWANNE I. MCHEMBA (K.n.y. MHE. MGENI JADI KADIKA) aliuliza:- Mradi wa MIVARF ni wa Muungano na Makao Makuu yapo Arusha ambapo kazi yake kuu ni kujenga masoko, miundombinu ya barabara, kuongeza thamani na kupeleka maendeleo vijijini:- Je, ni kwa kiasi gani mradi huu umechangia kuleta maendelezo Zanzibar? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA) alijibu: Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mgeni Jadi Kadika, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, MIVARF ni programu inayohusika na miundombinu ya masoko, uongezaji thamani ya mazao na huduma za kifedha vijijini.
    [Show full text]
  • Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Tatu – Tarehe 8 Mei, 2014 (Mkutano Ulianza Saa tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job J. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA, UTAWALA BORA NA MAHUSIANO NA UTARATIBU: Randama za Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Utawala Bora na Mahusiano na Uratibu kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MASWALI NA MAJIBU Na. 20 Kuhamisha Soko la Mwika MHE. DKT. AUGUTINE L. MREMA aliuliza:- Soko la Mwika liko barabarani na kuna hatari ya wananchi kugongwa na magari:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutafuta eneo kubwa na kuhamisha soko hilo ili kukwepa athari hizi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Augustino Lyatonga Mrema Mbunge wa Vunjo kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Soko la Mwika liko katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi karibu na barabara. Soko hili lina ukubwa wa ekari 2.5 na idadi ya wafanyabiashara wanaotumia soko hili ni kati ya 1,000 hadi 1,500. Kimsingi kuna ongezeko kubwa la wafanyabiashara kufuatia mahitaji ya walaji ambao wanajumuisha wananchi wa Kata ya Mwika Kaskazini na Mwika Kusini. Kwa kutambua changamoto ya soko hili kuwa karibu na barabara, Halmashauri inaandaa mpango wa kuboresha soko hilo ili liwe la kisasa na kuondoa athari za ajali katika eneo hilo.
    [Show full text]
  • Tarehe 9 Mei, 2019
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Ishirini na Nne – Tarehe 9 Mei, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu. NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. ASHA MSHIMBA JECHA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2018/ 2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. QAMBALO W. QULWI – NAIBU MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI KUHUSU WIZARA YA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Kuhusu Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. NAIBU SPIKA: Ahsante. Waheshimiwa tunaendelea. Katibu. NDG. JOSHUA CHAMWELA – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Maswali, tutaanza na Ofisi ya Rais, TAMISEMI. Mheshimiwa Yahaya Omary Massare, Mbunge wa Manyoni Magharibi sasa aulize swali lake. Na. 196 Serikali Kuzipatia Waganga Zahanati za Jimbo la Manyoni Magharibi MHE. YAHAYA O. MASSARE aliuliza:- Wananchi wa Manyoni Magharibi kwa kushirikiana na Serikali kupitia miradi mbalimbali ikiwemo TASAF wamejenga zahanati katika Vijiji vya Gurungu, Sanjaranda, Kitopeni, Ipande, Doroto, Itagata, Kalangali, Makale, Mwamagembe na Kintanula, lakini mpaka sasa zahanati hizi hazina Waganga:- Je, ni lini Serikali itazipatia zahanati hizo Waganga, ili wananchi wapate huduma kufuatana na sera yake? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, majibu.
    [Show full text]
  • Tarehe 28 Aprili, 2017
    NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Kumi na Nne – Tarehe 28 Aprili, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa, tukae. Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Tutaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Ester Michael Mmasi, Mbunge wa Viti Maalum, kwa niaba yake Mheshimiwa Stanslaus Mabula. Na.110 Vigezo vya Kurasimisha Vibali vya Ajira na Kuishi Nchini MHE. STANSLAUS S. MABULA (K.n.y. MHE. ESTER M. MMASI) aliuliza:- Pamoja na juhudi za Serikali katika kulinda ajira za vijana wa Kitanzania, Serikali kupitia Sheria ya Ajira ya Wageni Na. 1 ya mwaka 2015 ilirasimisha vibali vya kuishi na ajira kwa wageni batili wapatao 317 kati ya 779. Je, ni vigezo gani vilivyotumika katika urasimishaji wa vibali hivyo wakati vijana wengi wa Kitanzania hususan 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wahitimu wa vyuo vikuu wanahangaika katika kupata ajira ili wafurahie faida ya taaluma zao? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU (KAZI, VIJANA NA AJIRA) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ester Mmasi, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Sheria ya Kuratibu Ajira kwa Wageni Nchini Na.1 ya mwaka 2015 ilianza kutumika tangu tarehe 15/9/2015. Sheria hii imeweka utaratibu maalum kwa mtu anayetaka kumuajiri raia wa kigeni kuomba kibali cha ajira kwa Kamishna wa Kazi ambaye ndiye mwenye mamlaka pekee ya utoaji wa vibali vya ajira kwa wageni nchini.
    [Show full text]
  • Tarehe 28 Mei, 2021
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Thelathini na Tisa– Tarehe 28 Mei, 2021 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Mkutano wetu wa Tatu, leo ni Kikao cha Thelathini na Tisa. Katibu. NDG. BAKARI KISHOMA – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- NAIBU WAZIRI WA HABARI, UTAMADUNI, SANAA NA MICHEZO: Randama ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo kwa mwaka wa fedha 2021/2022. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri Michezo. Katibu. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. BAKARI KISHOMA – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na Ofisi ya Rais - TAMISEMI, swali la Mheshimiwa Dkt. Pius Stephen Chaya, Mbunge wa Manyoni Mashariki. Na. 321 Ujenzi wa Hospitali ya Wilaya ya Manyoni MHE. DKT. PIUS S. CHAYA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kuanza ujenzi wa Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni kwa sababu Hospitali iliyopo haikidhi mahitaji kutokana na uchakavu na ongezeko la watu? SPIKA: Majibu ya swali hilo muhimu kwa watu wa Manyoni, Mheshimiwa Naibu Waziri Dkt. Festo Dugange. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. DKT. FESTO J. DUGANGE) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais -TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Pius Stephen Chaya, Mbunge wa Jimbo la Manyoni kama ifuatavyo: Mheshimiwa Spika, Serikali inatambua uwepo wa hospitali 43 kongwe na chakavu za Halmashauri ikiwemo Hospitali ya Halmashauri ya Wilaya ya Manyoni.
    [Show full text]
  • Tarehe 13 Juni, 2017
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Arobaini na Sita – Tarehe 13 Juni, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Yustino Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Tukae. Katibu! NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Maswali tunaanza na TAMISEMI, swali la Mheshimiwa Joram Ismael Hongoli, Mbunge wa Lupembe. Mheshimiwa Hongoli! Na. 374 Mahitaji ya Kidato cha Tano – Shule ya Sekondari Lupembe MHE. JORAM I. HONGOLI aliuliza:- Shule ya Sekondari ya Lupembe iliyopo Halmashauri ya Wilaya ya Njombe ni ya muda mrefu na tulishaomba na kufanya maandalizi ya kuwa na Kidato cha Tano kwa Mchepuo wa CBG. Je, ni lini Serikali itaanzisha Kidato cha Tano katika Shule hiyo? 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joram Ismael Hongoli, Mbunge wa Lupembe, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Shule ya Sekondari ya Lupembe ni miongoni mwa shule mpya 22 ambazo zimeombewa kibali Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia ili iweze kupokea wanafunzi wa kidato cha tano katika mwaka 2017. Hivyo, shule hiyo itaanza kupokea wanafunzi wa kidato cha tano baada ya kupatikana kwa kibali kilichoombwa kufuatia ukaguzi wa miundombinu ya shule iliyofanyika. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri kwa jibu zuri na fupi kabisa. Mheshimiwa Hongoli Mbunge wa Lupembe swali la nyongeza. MHE. JORAM I. HONGOLI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana. Pamoja na majibu mazuri ya Naibu Waziri naomba niulize maswali mawili ya nyongeza.
    [Show full text]
  • 1 Bunge La Tanzania
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Kumi na Tatu – Tarehe 27 Juni, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 121 Chama Tawala Kuzuiwa Kutekeleza Sera Zake MHE. MOHAMED H. MISSANGA aliuliza:- Baada ya Uchaguzi Mkuu wa mwaka 2010 Chama cha Mapinduzi (CCM) ambacho kilishinda, kilipewa ridhaa ya kuongoza nchi na kutekeleza Ilani yake ya Uchaguzi ambayo inaeleza kuwa wananchi wanayo haki ya kuchangia katika Miradi ya Maendeleo nchini:- (a) Je, Serikali haioni kuwa si haki kwa Vyama vya Upinzani kuwakataza wananchi wasichangie Miradi mbalimbali ya Maendeleo na kwamba hali hiyo inazuia Chama Tawala kutekeleza sera zake? (b) Je, Serikali haioni kuwa hali hiyo inaweza kuchangia wafadhili kusitisha misaada yao kwa kukosekana ushiriki wa wananchi katika miradi hiyo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu napenda kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed H. Missanga, Mbunge wa Singida Magharibi, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika, shughuli za Vyama vya siasa hapa nchini zinatawaliwa na Sheria ya Vyama vya Siasa Na. 5 ya mwaka 1992 na marekebisho yake mbalimbali pamoja na Kanuni za Maadili ya Vyama vya Siasa za mwaka 2007. Hivyo, ni wajibu wa 1 Vyama vyote vya siasa kuzingatia sheria na Kanuni hizo katika kudumisha amani, utulivu na mshikimano uliopo kijamii. Mheshimiwa Spika, baada ya Uchaguzi Mkuu wa 2010, Chama cha Mapinduzi (CCM) kilishinda na kupata ridhaa ya wananchi kuongoza nchi kwa kipindi kingine cha miaka mitano.
    [Show full text]
  • 16 Aprili, 2012 1 Bunge La Tanzania
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) 16 APRILI, 2012 BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Tano – Tarehe 16 Aprili, 2012 (Mkutano ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na. 52 Ahadi ya Rais Kununua Gari la Wagonjwa (Ambulance) - Kituo cha Afya Mlangali MHE. DEO H. FILIKUNJOMBE aliuliza:- Mwaka 2008, Rais wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania Mheshim iwa Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete, aliahidi kuwapatia wananchi wa Mlangali gari jipya la wagonjwa Ambulance:- 1 16 APRILI, 2012 (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kutekeleza ahadi hiyo? (b) Je, gari hilo linaweza kupatikana leo baada ya Bunge kuahirishwa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Deo Haule Filikunjombe Mbunge wa Ludewa lenye sehemu (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, nakubaliana na Mheshimiwa Mbunge kwamba Mheshimiwa Rais mwaka 2008 aliahidi kutoa gari kwa ajili ya kituo cha afya Mlangali katika Halmashauri ya Wilaya ya Ludewa. Kwa kuzingatia ahadi ya Mheshimiwa Rais na adha ya usafiri waliyo nayo wananchi wa Mlangali, tarehe 1 Aprili, 2011 Serikali ilipeleka gari la kubebea wagonjwa katika kituo cha Afya Mlangali kwa ajili ya kuhudumia wagonjwa wanaohitaji rufaa. Gari lililonunuliwa ni Toyota Land Cruiser Hardtop lenye Na. Za usajili SM 9192. Gari hili lilikabidhiwa kituo cha afya Mlangali tangu Septemba, 2011. 2 16 APRILI, 2012 Mheshimiwa Spika, nachukua nafasi hii na fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Deo Filikunjombe kwa jitihada kubwa alizofanya kwa wananchi wake wa Ludewa kwa kuamua kununua magari mawili (hiace ) ambapo yanatumika kusafirishia wagonjwa wa rufaa katika Wilaya ya Ludewa.
    [Show full text]
  • UNDP TANZANIA MID-TERM EVALUATION of the LEGISLATIVE SUPPORT PROJECT PHASE II (2017-2021) November 2019
    UNDP TANZANIA MID-TERM EVALUATION OF THE LEGISLATIVE SUPPORT PROJECT PHASE II (2017-2021) November 2019 Disclaimer The Mid-term Evaluation of “UNDP TANZANIA LEGISLATIVE SUPPORT PROJECT PHASE II 2017-2021” has been drafted by Tim Baker and Chris Awinia. The views expressed in this document are those of the authors and do not necessarily represent the views of these institutions. Project Title Legislative Support Project (LSP), Phase II Atlas ID Award 00095419, Project 0009425 Corporate Outcome Citizen expectations for voice, development, the rule of law and accountability are met by stronger systems of democratic governance Corporate Outputs Output 1: Increase the capacity of the National Assembly to effectively scrutinise legislation and its implementation and to monitor government performance in a participatory manner Output 2: More effective parliamentary scrutiny of government budget and expenditure, including monitoring of the Sustainable Development Goals (SDGs) Output 3: Enhance the capacity of the National Assembly to engage citizens and represent their interests in the work of the parliament Output 4: The National Assembly is more effectively engaged in strategic leadership, transparency and external engagement Output 5: Gender is mainstreamed in all functions of the National Assembly Country Tanzania Project Dates Start: 01 January 2017 Planned end: 31 December 2021 Project Budget USD $12,765,600 Funding Source DFID, Royal Danish Embassy, One Fund, Embassy of Ireland, TRAC Implementing party National Assembly Tanzania 2 Table
    [Show full text]
  • Tarehe 3 Mei, 2016
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Kumi na Moja – Tarehe 3 Mei, 2016 (Bunge lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae, Katibu. NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH - KATIBU MEZANI: Hati za kuwasilisha Mezani. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA KILIMO, MIFUGO NA UVUVI: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi pamoja na Taasisi zake kwa mwaka wa fedha 2016/2017. MHE. NDAKI M. MASHIMBA (K.n.y MWENYEKITI WA KAMATI YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi kwa mwaka wa fedha 2015/2016 pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017. 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) MHE. DKT. IMMACULATE S. SEMESI (K.n.y MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KUHUSU KILIMO, MIFUGO NA UVUVI): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Kilimo, Mifugo na Uvuvi juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2016/2017. NAIBU SPIKA: Tunaendelea, Katibu NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH - KATIBU MEZANI: Maswali MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Ofisi ya Rais, TAMISEMI, Mheshimiwa Joseph Michael Mkundi, Mbunge wa Ukerewe aulize swali lake. Na. 83 Huduma za Afya Katika Wilaya ya Ukerewe MHE. JOSEPH M. MKUNDI aliuliza:- Wilaya ya Ukerewe inajumuisha visiwa
    [Show full text]
  • MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao Cha Saba – Tarehe 9
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Saba – Tarehe 9 Aprili, 2020 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. EMMANUEL MPANDA - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU (Maswali yafuatayo yameulizwa na kujibiwa kwa njia ya mtandao) Na. 55 Kuwajengea Uwezo Wanawake na Vijana Nchini MHE. CATHERINE N. RUGE aliuliza:- Mheshimiwa Naibu Spika, kumekuwepo na jitihada zinazofanywa na Taasisi zisizo za Serikali katika kuwahamasisha na kuwajengea uwezo wanawake na vijana kuwania nafasi mbalimbali za uongozi katika chaguzi nchini:- (a) Je ni nini mkakati wa Serikali kulifanya kundi hili kushiriki na kupata nafasi za kugombea katika chaguzi zijazo? 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (b) Sera ya vijana katika Jumuiya ya Afrika Mashariki inahitaji uwepo wa Mabaraza ya vijana kwa nchi wanachama: Je, ni lini Baraza hili litaanzishwa? WAZIRI MKUU alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Catherine Nyakao Ruge, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, katika kuhakikisha kuwa vijana wanahamasishwa na kujengewa uwezo wa kuwania nafasi za uongozi katika chaguzi zijazo, Serikali inatekeleza mikakati ifuatayo:- (i) Inaratibu programu ya ujasiri na Stadi za maisha kwa vijana, ambapo kupitia programu hizi, vijana wanapatiwa mafunzo yanayolenga kuwaandaa kuwa na uthubutu, kujiwekea malengo na kufanya maamuzi sahihi kuhusu maisha yao ikiwa ni pamoja kushiriki katika masuala ya uongozi kwenye ngazi mbalimbali. (ii) Kupitia Mbio za Mwenge wa Uhuru, vijana wamekuwa wakihamasishwa kushiriki katika nafasi za uongozi, mathalani, katika kipindi cha mwaka 2016 - 2019 jumla ya vijana wakimbiza Mwenge wa Uhuru 30 waliofanya kazi hiyo kwa weledi na uzalendo wa hali ya juu wameweza kupata nafasi za uongozi za kisiasa na za kiutendaji katika ngazi mbalimbali.
    [Show full text]