MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao Cha Ishirini Na Moja

MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao Cha Ishirini Na Moja

NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Ishirini na Moja – Tarehe 4 Mei, 2020 (Bunge Lilianza Saa Nane Mchana) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH -KATIBU MEZANI: TAARIFA YA SPIKA Kwa mujibu wa Kanuni ya 33(2) ya Kanuni za Kudumu za Bunge, Toleo la Mwaka 2016, Waheshimiwa Wabunge kwa masikitiko makubwa Mheshimiwa Spika anapenda kuwajulisha kuwa Bunge letu limepatwa na msiba mwingine mkubwa wa kuondokewa na Mbunge na aliyekuwa Waziri wa Katiba na Sheria, Mheshimiwa Balozi Dkt. Augustine Philip Mahiga ambaye alifariki alfajiri ya kuamkia siku ya Ijumaa tarehe 1 Mei, 2020 Jijini Dodoma na kuzikwa tarehe 2 Mei, 2020 nyumbani kwake Tusamaganga, Iringa. Waheshimiwa Wabunge, pamoja na mengi mazuri na muhimu aliyoyafanya marehemu Mheshimiwa Balozi Mahiga mwaka 2003 mpaka 2010 akiwa Balozi wa Kudumu wa Tanzania katika Umoja wa Mataifa, alirejesha heshima ya Tanzania hadi kuwa moja ya nchi zilizounda Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa na yeye kuwa Mkuu wa Ujumbe wa Tanzania katika Baraza hilo. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Waheshimiwa Wabunge naomba sasa tusimame kwa muda wa dakika moja kama ishara ya kuomboleza kifo cha mwenzetu. (Hapa Wabunge walisimama kwa dakika moja kuomboleza kifo cha Mhe. Balozi Dkt. Augustine Phillip Mahiga) NAIBU SPIKA: Mwenyezi Mungu ailaze roho ya marehemu mahali pema peponi. Amina. Tukae. Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH -KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2020/2021. MHE. ZUBERI M. KUCHAUKA - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MIUNDOMBINU: Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano kwa mwaka wa fedha 2019/ 2020 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa mwaka wa fedha 2020/2021. NAIBU SPIKA: Ahsante sana. Nimwite Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni wa Wizara ya Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Hayupo. Katibu! 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH -KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU (Maswali yafuatayo yameulizwa na kujibiwa kwa njia ya mtandao) Na. 192 Ujenzi wa Maabara za Shule – Hanang MHE. DKT. MARY M. NAGU aliuliza:- Mwaka 2013 – 2015 Serikali ilihamasisha wananchi kujenga vyumba vya maabara katika shule mbalimbali Wilayani Hanang lakini hadi sasa maabara hizo hazijakamilika. Je Serikali ipo tayari kutoa fedha ili kukamilisha ujenzi wa maabara hizo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Mary Michael Nagu, Mbunge wa Hanang, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali ipo tayari kuunga mkono jitihada za wananchi katika ukamilishaji wa ujenzi wa maabara za shule za sekondari kwa ajili ya masomo ya sayansi. Katika bajeti ya mwaka wa fedha 2020/2021, Serikali imeidhinishiwa shilingi bilioni 42 kwa ajili ya ukamilishaji wa maabara zilizojengwa kwa nguvu za wananchi. Kati ya fedha hizo, Halmashauri ya Wilaya ya Hanang imeidhinishiwa Shilingi milioni 210 ambazo zitatumika kukamilisha maabara saba. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 193 Kuboresha Miundombinu ya Elimu Rufiji MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA aliuliza:- Shule nyingi katika Wilaya ya Rufiji zimechakaa kwani nyingi zilijengwa wakati wa Mkoloni. (a) Je, Serikali ina mpango gani wa kuzikarabati shule hizo? (b) Je, ni lini Serikali itaboresha miundombinu ya shule za Sekondari Muhoro na Ikwiriri ili ziwe za kidato cha Tano na Sita? WAZIRI WA NCHI, OFlSI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mohamed Omary Mchengerwa, Mbunge wa Rufiji, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali imeendelea kuzikarabati shule za msingi na sekondari katika Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji ambapo katika mwaka wa fedha 2017/ 2018 Halmashauri ilipatiwa kiasi cha Shilingi milioni 259 kwa ajili ya ukarabati wa Shule ya Sekondari Utete. (b) Mheshimiwa Naibu Spika, katika mwaka wa fedha 2017/2018 na 2018/2019, Halmashauri ya Wilaya ya Rufiji imepatiwa kiasi cha Shilingi milioni 256 kwa ajili ya ujenzi wa mabweni mawili (2), matundu 10 ya vyoo na kukamilisha maboma nane (8) ya madarasa katika Shule ya Sekondari Muhoro. Vilevile, katika mwaka wa fedha 2018/2019, Halmashauri ilipatiwa kiasi cha Shilingi milioni 60 kwa ajili ya ujenzi wa vyumba vitatu (3) vya madarasa katika Shule ya Sekondari Ikwiriri. Miundombinu hiyo imeboreshwa ili kuziwezesha shule hizo kuanza kudahili wanafunzi wa kidato cha tano. 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Na. 194 Mji wa Lamadi Kupewa Hadhi ya Mamlaka ya Mji Mdogo MHE. GIMBI D. MASABA aliuliza:- Mji wa Lamadi uliopo Wilaya ya Busega Mkoani Simiyu ni miongoni mwa Miji yenye sifa za kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo. Je, ni lini Serikali itautangaza Mji huo kuwa Mamlaka ya Mji Mdogo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Gimbi Dotto Masaba, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali inatambua uwepo wa miji inayokua kwa kasi ambayo inaweza kupewa hadhi ya Mamlaka za Miji Midogo ikiwemo Mamlaka ya Mji Mdogo wa Lamadi. Hata hivyo, kipaumbele cha Serikali kwa sasa ni kuendeleza maeneo mapya ya utawala yaliyoanzishwa tayari kwa kuyawekea miundombinu na huduma muhimu ili yaanze kutoa huduma kwa wananchi kabla ya kuanzisha maeneo mapya ya utawala. Na. 195 Serikali Kupunguza Kodi ya Huduma MHE. BONIVENTURA D. KISWAGA aliuliza:- Je, Serikali ina mpango gani wa kupunguza Kodi ya Huduma (Service Levy) kutoka 0.03 na kuwa 0.01 ili kuleta unafuu kwa wafanyabiashara nchini? 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Boniventura Destery Kiswaga, Mbunge wa Magu, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ushuru wa huduma (Service Levy) unaotozwa kwa Mujibu wa Sheria ya Fedha za Serikali za Mitaa, Sura 290, Kifungu cha 6(u) na 7(z). Kwa mujibu wa Sheria hiyo, Halmashauri zina hiari na uwezo wa kupanga kiwango cha Ushuru wa Huduma kisichozidi Asilimi 0.3 (not exceeding 0.3 %). Hivyo, Sheria imetoa mwanya wa kupunguza ushuru huo kulingana na mazingira ya biashara, uzalishaji na ulipaji wa kodi katika Halmashauri husika. Na. 196 Mafunzo ya Afya ya Uzazi Salama MHE. SABREENA H. SUNGURA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itawafikia Mama wa Tanzania kote kwa kuwapa mafunzo dhidi ya Afya ya Uzazi Salama? WAZIRI WA AFYA, MAENDELEO YA JAMII, JINSIA, WAZEE NA WATOTO alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Sabreena Hamza Sungura, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, katika juhudi za kuboresha huduma za afya ya uzazi, ni muhimu sana wanawake wote, hasa walio katika umri wa kuzaa, miaka 15 hadi 49 wapate elimu ya afya ya uzazi salama. Mafunzo haya hujumuisha, uzazi wa mpango, umuhimu wa kuhudhuria kliniki wakati wa ujauzito, huduma za dharura kwa matatizo yatokanayo na uzazi, magonjwa ya zinaa, virusi vya UKIMWI/VVU na madhara ya madawa ya kulevya. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, Wizara ya Afya imeendelea kutoa mafunzo ya uzazi salama kwa kupitia njia mbalimbali ikiwemo vipeperushi na mabango, vipindi vya redio na televisheni. Katika kipindi cha Januari hadi Juni, 2019, Wizara imeweza kutumia njia hizo za kuelimisha na kutoa mafunzo na kuwafikia jumla ya wanawake 1,480,900 Tanzania Bara. Kupitia mafunzo haya, Idadi ya akinamama wanaojifungulia katika vituo vya kutolea huduma imeendelea kuongezeka hadi kufikia asilimia 83 mwezi Machi, 2020 ikilinganishwa na asilimia 64 kwa kipindi kama hicho mwaka 2015/2016 Mheshimiwa Naibu Spika, lengo la Wizara ni kuwa, kufikia mwaka 2020, kila mwanamke aliye katika umri wa kujifungua atakuwa amefikiwa na elimu hii. Elimu hii itasaidia akinamama kuhudhuria kliniki mapema mara tu wanapogundua ni wajawazito na pia kujifungulia katika vituo vya kutolea huduma ili waweze kuhudumiwa na watoa huduma wenye ujuzi. Na. 197 Ufanisi wa Sospa Kuzuia Udhalilishaji kwa Mtoto wa Kike MHE. JANET Z. MBENE aliuliza:- Hivi karibuni limejitokeza suala lililozua mjadala mkubwa kuhusu wanafunzi kupata mimba na kusababisha kukatisha masomo yao, mwaka 1998 Bunge lilipitisha Sheria maalum ya makosa ya kujamiiana (SOSPA) ambayo ilibadili sheria kadhaa na kuweka sheria inayoshughulikia makosa ya udhalilishaji wa kingono na wa kijinsia iliyolenga kurudisha heshima, usalama na hadhi ya wanawake na watoto. (a) Je mpaka sasa ni watu wangapi waliotiwa hatiani na kufungwa kifungo kilichoainishwa kwenye sheria hiyo? (b) Je kati ya watu waliofungwa watu wazima ni wangapi na wanafunzi waliowapa mimba wanafunzi wenzao ni wangapi na wako wapi kwa sasa? 7 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) (c) Je kati ya watoto waliopo shuleni na ambao hawapo shuleni, ni wangapi waliobakwa au kurubuniwa na wangapi waliofanya nao mapenzi kwa hiari? WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Janeth Zebedayo Mbene, Mbunge wa Ileje, lenye sehemu (a), (b) na (c) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, mpaka sasa jumla ya watuhumiwa 456 wamekwishatiwa hatiani,

View Full Text

Details

  • File Type
    pdf
  • Upload Time
    -
  • Content Languages
    English
  • Upload User
    Anonymous/Not logged-in
  • File Pages
    377 Page
  • File Size
    -

Download

Channel Download Status
Express Download Enable

Copyright

We respect the copyrights and intellectual property rights of all users. All uploaded documents are either original works of the uploader or authorized works of the rightful owners.

  • Not to be reproduced or distributed without explicit permission.
  • Not used for commercial purposes outside of approved use cases.
  • Not used to infringe on the rights of the original creators.
  • If you believe any content infringes your copyright, please contact us immediately.

Support

For help with questions, suggestions, or problems, please contact us