Tarehe 12 Septemba, 2019
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA KUMI NA SITA Kikao cha Nane – Tarehe 12 Septemba, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na Mkutano wetu wa Kumi na Sita na Kikao cha leo ni Kikao cha Nane, Katibu. NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI SPIKA: Hati za Kuwasilisha Mezani, naomba nimwite Mheshimiwa Waziri wa Ujenzi, Uchukuzi na Mawasiliano. Namuona Naibu Waziri, Mheshimiwa Elias Kwandikwa. NAIBU WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO (MHE. ELIAS J. KWANDIKWA): Taarifa ya Mwaka na Hesabu zilizokaguliwa za Mfuko wa Barabara kwa Mwaka 2015/2016 (The Annual Report and Audited Report of Roads Fund Board for the year 2015/2016). 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Naibu Waziri. Sasa naomba nimuite Mwanasheria Mkuu wa Serikali, Mheshimiwa Prof. Kilangi tafadhali. MWANASHERIA MKUU WA SERIKALI: Maelezo ya Mwanasheria Mkuu wa Serikali kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 6) wa Mwaka 2019 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 6), Bill, 2019]. SPIKA: Ahsante sana. Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo, anakuja Mwenyekiti mwenyewe, Mheshimiwa Andrew Chenge. (Makofi) MHE. ANDREW J. CHENGE – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA SHERIA NDOGO: Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Sheria Ndogo kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 6) wa Mwaka 2019 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 6), Bill, 2019]. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Mwenyekiti wa Kamati. Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni Kuhusu Wizara ya Katiba na Sheria, Mheshimiwa Cecilia Paresso. MHE. CECILIA D. PARESSO (K.n.y MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU WIZARA YA KATIBA NA SHERIA): Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Muswada wa Sheria ya Marekebisho ya Sheria Mbalimbali (Na. 6) wa Mwaka 2019 [The Written Laws (Miscellaneous Amendments) (No. 6), Bill, 2019]. SPIKA: Ahsante sana. Katibu. 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Maswali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Mheshimiwa Waziri Mkuu, karibu. (Makofi) Ahsante sana. Muuliza swali wa kwanza atakuwa Mheshimiwa Mbunge wa Jimbo la Mlalo, Mheshimiwa Rashid Abdallah Shangazi. Mheshimiwa Shangazi tafadhali. MHE. RASHID A. SHANGAZI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa nafasi hii. Mheshimiwa Waziri Mkuu, Serikali ya Awamu ya Tano imehamasisha sana shughuli za kilimo na wananchi wamehamasika sana, lakini hivi karibuni limetokea tatizo kubwa sana la ufungaji wa mazao kwa mtindo wa lumbesa lakini pia kuwepo na vifungashio ambavyo havina viwango stahiki. Jambo la kusikitisha sana ni kwamba Mamlaka za Serikali, hasa Wakala wa Vipimo na Mizani, pia Serikali katika ngazi za Halmashauri, Wilaya na Mikoa zimeshindwa kabisa kudhibiti tatizo hili la ufungaji wa mazao kwa mtindo wa lumbesa. Je, Serikali ipo tayari kuanzisha operesheni maalum nchi nzima kudhibiti tatizo hili ambalo kwa kweli linawanyong’onyeza wakulima na kuwaletea lindi la umaskini? (Makofi) SPIKA: Ahsante sana. Majibu ya swali hilo Mheshimiwa Waziri Mkuu tafadhali. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Shangazi, Mbunge wa Mlalo kule Lushoto, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kwamba Serikali imeendelea kusisitiza wakulima wetu nchini wanapolima mazao yao waweze kunufaika kutokana na masoko yaliyo sahihi. Tunaanza kuona baadhi ya wanunuzi kutofuata sheria, 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kanuni na taratibu za manunuzi ya mazao hayo pindi wanapokwenda kwa wakulima. Mheshimiwa Spika, nimefanya ziara Wilaya ya Karatu eneo maarufu linalozalisha mazao la Lake Eyasi, eneo la Eyasi kule chini. Moja kati ya malalamiko ambayo wakulima waliyatoa ni kama ambavyo Mheshimiwa Shangazi ameeleza, lakini Serikali imeweka utaratibu wa mazao yote yanayolimwa na kuingia kwenye masoko, lazima masoko hayo yatumie vipimo halisi ili liweze kulipa bei stahiki na mkulima aweze kunufaika. (Makofi) Mheshimiwa Spika, tunaposema vipimo stahiki maana yake kuna vipimo ambavyo tunavitumia, inaweza kuwa ni kipimo cha ndoo ambazo tunajua kuna ndoo za lita tano, kumi, ishirini, na ni rahisi pia kukadiria na bei ambayo inawekwa na wakulima inakuwa ndiyo bei sahihi. Pia kuna vifungashio kama vile magunia ya kilo hamsini, kilo mia, nayo pia ni sehemu ya vipimo halisi lakini muhimu zaidi ni kutumia mizani ambayo haina utata. Mheshimiwa Spika, sasa imetokea wanunuzi kuwalazimisha wakulima baada ya kile kipimo halisi kuongeza tena nundu inayojulikana kwa jina la lumbesa kama ambavyo Mheshimiwa Mbunge ameeleza, hii haikubaliki. Tumetoa maelekezo sahihi kwa Wakuu wa Mikoa wote, Wakuu wa Wilaya wote, Wakurugenzi na Maafisa Kilimo na Maafisa Ushirika wanaosimamia masoko kwenye ngazi hizo za wakulima wawe wasimamizi wa biashara inayofanywa na wanunuzi kwa mkulima pindi anapouza mazao yake ili kujiridhisha kwamba vipimo vyote vinatumika na siyo kuongeza nundu zaidi ya kipimo ambacho kinatakiwa, kwa sababu kufanya hivyo tunamnyonya mkulima na mkulima anapata hasara kwenye mazao hayo. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa hiyo utayari wa Serikali upo na tumeshatoa maelekezo kwa Wakuu wa Wilaya. Kwa hiyo nirudie tena kutoa wito kwa Maafisa Kilimo, Ushirika, Wakuu Wa Wilaya, Wakuu wa Mikoa kwenye maeneo yao 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wasimamie biashara hii na kuendesha operesheni kwenye maeneo yote ya masoko ili kujiridhisha kwamba mazao yetu yananunuliwa kwa vipimo kama ambavyo vimekubalika. Huo ndiyo msisitizo wa Serikali na tutaendelea kusisitiza wakati wote. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana, tunaendelea. Mheshimiwa Mariam Nasoro Kisangi, uliza swali lako. MHE. MARIAM N. KISANGI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kunipa nafasi nami niweze kuuliza swali kwa Mheshimiwa Waziri Mkuu. Mheshimiwa Waziri Mkuu, katika miezi ya karibuni katika Mikoa mbalimbali ya nchi yetu kumekuwa na changamoto kubwa ya kupanda kwa gharama za maji bila kuzingatia uasilia, kuletewa bili zisizo sahihi, kukatiwa maji bila utaratibu na kukosa maji kwa muda mrefu kisha unaletewa bili kubwa. Kero hiyo imejitokeza katika Mikoa mbalimbali katika nchi yetu ikiwemo Mikoa ya Dar es Salaam, Manyara, Dodoma, Tanga, Mwanza na Mikoa mingine mingi na hasa katika maeneo ya Mijini. Je, Serikali inatoa kauli gani kwa wananchi wake waliokumbwa na kero hiyo? SPIKA: Ahsante sana. Mheshimiwa Waziri Mkuu majibu kwa swali hilo tafadhali. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mariam Kisangi, Mbunge wa Mkoa wa Dar es Salaam, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, alichosema Mheshimiwa Mbunge, yako maeneo yanajitokeza kwamba mamlaka tulizozipa mamlaka hiyo ya kusimamia maji kwenye maeneo yao, tunazo mamlaka ambazo tunazianzisha sasa za RUWA za vijijini na kwenye ngazi za Wilaya, lakini zipo mamlaka ambazo zimechukua maeneo makubwa kwenye ngazi za 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mikoa, pia tuna Kamati za Maji ambazo zinasimamia miradi hii kwenye maeneo ya vijiji na maeneo mengine yote. Mheshimiwa Spika, kumejitokeza wimbi la mabadiliko ya bei. Ni kweli upo utaratibu ndani ya Serikali kwamba mamlaka hizo zinapoona zinahitaji kuboresha huduma zinaweza kufanya mapitio ya bei zao. Lakini kinachotokea sasa ni kwamba zipo mamlaka zinapita zaidi ya kiasi. Mheshimiwa Spika, nimefanya ziara Mkoani Simiyu na hapa karibuni nilikuwa kwenye Wilaya ya Maswa, moja kati ya malalamiko niliyoyapokea kwa wananchi pale ni kupanda kwa bei kutoka shilingi 5,000 wanayoilipa kwa mwezi mpaka shilingi 28,000. Sasa bei hizi hazina uhalisia, hakuna sababu ya mamlaka kutoza fedha yote hiyo na kuwafanya wananchi wakose maji. Mheshimiwa Spika, Serikali ndiyo inatekeleza hii miradi na inatoa fedha kwa lengo la kuwapa huduma wananchi ili wapate huduma ya maji. Mamlaka tumewapa jukumu la kusimamia mradi huo na kuhakikisha kwamba angalau wanaweza kufanya marekebisho, matengenezo pale ambapo kunatokea uharibifu. Kwa hiyo, gharama haziwezi kuwa kubwa kiasi hicho na wala wao hawapaswi kutoza wananchi ili kurudisha gharama za mradi kwa sababu Serikali haijadai gharama ya kuendesha mradi huo kwa wananchi. (Makofi) Mheshimiwa Spika, kwa bahati nzuri jana nilikuwa na Waziri wa Maji nikimwambia hili la kwamba lazima afuatilie Mamlaka ya EWURA ambayo ina mamlaka ya kukaa na hizo mamlaka zetu za maji kufanya mapitio ya bei. Bei zinazotakiwa kuwekwa ni zile ambazo mwananchi wa kule kijijini anaweza kuzimudu lakini siyo kwa kupandisha bei kutoka shilingi 5,000 mpaka shilingi 28,000, jambo ambalo halina uhalisia. Mheshimiwa Spika, kwa hiyo nataka nimhakikishie Mheshimiwa Mbunge na Waheshimiwa Wabunge wote na Watanzania kwa ujumla, tutaendelea kusimamia Mamlaka 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) zote za Maji, lakini Serikali itaendelea kutoa huduma za maji, nataka tujiridhishe kila Mtanzania anapata maji kwenye maeneo yake kwa usimamizi wa mamlaka hizi, lakini hatutaruhusu na hatutakubali kuona Mtanzania anatozwa gharama kubwa za maji kiasi hicho. Huku tukiwa tunatoa wito kwamba lazima tuchangie maji ili tuweze kuendesha miradi hii pale ambapo tunatakiwa kununua diesel, tunatakiwa tununue tepu ya kufungulia maji au bomba linapopasuka, lazima mamlaka zile ziweze kufanya ukarabati huo, lakini siyo kwa kutoza fedha kiasi hicho.(Makofi) Mheshimiwa Spika, masharti ambayo yapo mnapotaka kuongeza bei ni kwamba mamlaka hizo zinapodhamiria jambo hilo ni lazima kwanza zitoe taarifa EWURA, mbili kwenye vikao hivyo lazima Kamati