Mikesha Ya Peshwaar

Author(s):

Sayyid al-Musawi al-Shirazi [1]

Publisher(s):

Al Itrah Foundation [2]

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Peshawar Nights. Asili ya kitabu hiki ni cha lugha ya Kifarsi kwa jina la, Shab’ha-ye Peshawar. Sisi tumekiita, Mikesha ya Peshawar.

Mikesha ya Peshawar ni nakala ya mjadala kati ya wanavyuoni mbalimbali wa Kisunni na mwanachuoni mmoja wa Kishia mzaliwa wa Shiraz () aitwaye Abdu ‘l-Fani Muhammad al-Musawi Sultanu ‘l-Wa’idhiin, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 31 tu. Mjadala huu ulifanyika katika mji wa Peshawar ambao wakati huo ilikuwa ni sehemu ya Bara Hindi na hivi sasa ni sehemu ya . Ulifanyika kuanzia tarehe 27 Januari 1927 na kuundelea kwa mikesha kumi ndani ya msikiti ambako watu zaidi 200 walihudhuria kila usiku. Mjadala huu ulifanywa kwa muundo mzuri wa kuheshimiana pande zote bila ya kuvunjiana heshima. Mwandishi mwenyewe amejiita katika kitabu hiki kama “Da’i” yaani mtu anayewaombea mema watu wengine, sisi tumelitafsiri neno hilo kama “Muombezi”.

Get PDF [3] Get EPUB [4] Get MOBI [5]

Translator(s):

Dr. M. S. Kanju [6]

Topic Tags:

Ahl al-Bayt [7] History [8] Shi'a [9]

Person Tags:

Prophet Muhammad [10] Sayyid Muhammad al-Musawi al-Shirazi [1] Fatimah al-Zahra [11] Neno La Mchapishaji

Kitabu kilichoko mikononi mwako ni tarjuma ya kitabu cha Kiingereza kiitwacho, Peshawar Nights. Asili ya kitabu hiki ni cha lugha ya Kifarsi kwa jina la, Shab’ha-ye Peshawar. Sisi tumekiita, Mikesha ya Peshawar.

Mikesha ya Peshawar ni nakala ya mjadala kati ya wanavyuoni mbalimbali wa Kisunni na mwanachuoni mmoja wa Kishia mzaliwa wa Shiraz (Iran) aitwaye Sayyid Abdu ‘l-Fani Muhammad al-Musawi Sultanu ‘l-Wa’idhiin, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 31 tu. Mjadala huu ulifanyika katika mji wa Peshawar ambao wakati huo ilikuwa ni sehemu ya Bara Hindi na hivi sasa ni sehemu ya Pakistan. Ulifanyika kuanzia tarehe 27 Januari 1927 na kuundelea kwa mikesha kumi ndani ya msikiti ambako watu zaidi 200 walihudhuria kila usiku. Mjadala huu ulifanywa kwa muundo mzuri wa kuheshimiana pande zote bila ya kuvunjiana heshima. Mwandishi mwenyewe amejiita katika kitabu hiki kama “Da’i” yaani mtu anayewaombea mema watu wengine, sisi tumelitafsiri neno hilo kama “Muombezi”.

Masharti ya mjadala yalikuwa kwamba ni vianzo vile tu vinavyokubaliwa na madhehebu zote ndivyo vitakavyorejelewa. Mjadala huu uliandikwa na kuripotiwa na waandishi wanne katika magazeti ya kila siku, na baadaye ukachapishwa kama kitabu huko Tehran, Iran.

Huu ulikuwa ni mjadala uliopangwa vizuri, wa kielimu na utumiaji wa vipawa vya akili ambapo kila hoja iliyotolewa ilitumika elimu na akili kuiwasilisha mpaka pande zote zikaridhika.

Katika kuwasilisha hoja zake, mwanachuoni huyu mkubwa wa Kishia alitumia rejea za vitabu vingi maarufu vya Kisunni na ambavyo si maarufu sana lakini vyenye kuaminika. Rejea na vitabu hivyo vimeorodheshwa kwa wingi sana ndani ya kitabu hiki ili msomaji aweze kuvirejelea. Lakini kwa bahati mbaya sana, mengi ya matoleo mapya ya vitabu hivyo yamefanyiwa mabadiliko na baadhi ya sehemu kuondolewa, hususan zile zinazounga mkono madai ya Shia. Ufuatao hapa chini ni mfano mdogo tu wa yanayofanywa katika vitabu hivyo:

Katika ukurasa wa 301 wa juzuu ya 3 ya Tafsir al-Kashshaaf iliyokusanywa chini ya maelekezo ya Sheikh Mustafa al-Halabi (toleo la pili, 1319 A.H. liliochapishwa na Main Government Printing House ya Amiriah Bulaq ya Misir), kuna beti zinazojitokeza ambazo kwazo Jarullah Zamakhshari, mfasiri wa al- Kashshaaf, alitangaza wazi imani yake katika uhalali wa Ushia. Lakini katika chapisho la 1373 A.H. lililochapishwa na Printing House Istiqamah bi’l-Qahara, shairi lililotajwa halionekani tena.

Marehemu Allamah Sayyid S. Akhtar Rizvi katika kitabu chake Uimamu uk. 37, anaandika kushangazwa kwake kutokana na maneno yaliyoondolewa katika kitabu cha at-Tarikh cha at-Tabari, chapa ya Leiden (ya mwaka 1879 Masihia) ambayo imeyanakili maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.) aliyoyatumia wakati wa karamu maarufu ya ndugu wa karibu aliyoitayarisha mwenyewe. Maneno ya mwisho aliyoyasema Mtukufu Mtume (s.a.w.) katika karamu hiyo yalikuwa haya:

“Enyi watu wangu! Huyu ni ndugu yangu, wasii wangu na khalifa wangu miongoni mwenu; msikilizeni na mtiini.” Lakini katika chapa ya Misri (ya mwaka 1963 Masihia) - chapa ambayo inayodaiwa kuwa imechekiwa na ile ya Leiden - maneno haya muhimu: “wasii wangu na khalifa wangu” yamebadilishwa na kuwa “kadha wa kadha” na kusomeka hivi: “Huyu Ali ni ndugu yangu na kadha wa kadha.” Huu ni msiba mkubwa.

Sultanu ‘l-Wa’idhiin, mwandishi wa kitabu hiki, amedondoa rejea nyingi kutoka katika matoleo ya zamani, hivyo, msomaji asishangae kutokuona rejea hizo katika matoleo mapya. Huu ni mchezo umefanywa na unaendelea kufanywa mpaka leo. Na lengo ni kuficha ukweli.

Hata hivyo, ‘ukweli siku zote unaelea’; matoleo ya zamani yapo mengi na yamehifadhiwa kwenye maktaba zetu.

Ni muhimu kufikia kila aina ya maoni katika kujaribu kuamua ukweli. Uislamu kimsingi uko dhidi ya kufuata kibubusa. Mjadala huu umefanywa ili kuwaelemisha Waislamu kwa ujumla juu ya madhehebu za Kiislamu ili kujenga maoni yao kuhusu mtazamo mzuri wa mtu mwenyewe.

Ni muhimu mtu kuelewa hoja za wale ambao hakubaliani nao. Inawezekana kusemwa kwamba wale ambao hawaelewi kabisa mtazamo wa maoni tofau- ti, hawaelewi kwa ukamilifu (mtazamo) wa kwao wenyewe. Hili tena ni jaribio letu kubwa la kutoa kitabu kikubwa kinachohusu mjadala juu ya madhehebu za Kiislamu.

Tumekiona kitabu hiki ni chenye manufaa sana, hususan wakati huu wa maendeleo makubwa ya elimu katika nyanja zote, ambapo uwongo, ngano za kale na upotoshaji wa historia ni mambo ambayo hayana nafasi tena katika akili za watu.

Kutokana na ukweli huo, Taasisi yetu ya Al-Itrah Foundation imeona bora kukichapisha kitabu hiki kwa lugha ya Kiswahili, kwa madhumuni yake yaleyale ya kuwahudumia Waislamu, hususan wazungumzaji wa Kiswahili.

Tunamshukuru ndugu yetu, Dr. M. S. Kanju kwa kukubali jukumu hili la kukitarjumi kitabu hiki. Vilevile tunawashukuru wale wote walioshiriki kwa njia moja au nyingine hadi kufanikisha kuchapishwa kwa kitabu hiki.

Mchapishaji: Al-Itrah Foundation S. L. P. 19701 Dar-es-Salaam, Tanzania Peshawar(Mikesha Ya Peshawar)

Sultanu’l-Wa’izin Shirazi, mwanachuo mkubwa wa Iran, alitembelea India mwaka wa 1927 (1345 A.H.) wakati akiwa na umri wa miaka 30. Alipata makaribisho makubwa popote alipokwenda. Watu walinufaika kutokana na ujuzi wake wa hadithi, historia, na tafsiri juu ya Qur’ani Tukufu.

Alishauriwa kuingia katika mjadala wa kidini tarehe 23 Rajab, 1345 A.H., na watu wa imani nyingine katika eneo la Peshawar, eneo ambalo lilikuwa ni katika India na ambalo leo ni eneo la Pakistan. Mjadala ulifanyika kwa muda wa mikesha kumi mfulululizo.

Washiriki wakubwa wawili kutoka upande mwingine walikuwa ni wanachuoni maarufu wa Kabul, Hafidh Muhammad Rashid na Sheikh Abdul’s-Salam. Waandishi wanne waliandika taarifa za mjadala huo mbele ya watu takirban 200 (Shia na Sunni).

Magazeti ya sehemu hiyo yaliandika taarifa za mjadala huo kila siku asubuhi iliyofuatia. Sultanu’l- Wa’idhin alikusanya maelezo ya magazeti kuhusu mjadala huo katika kitabu nchini Iran, na kuchapishwa Tehran kama Shabhaye-Peshawar, au Peshawar Nights ifuatayo ni tarjuma ya kitabu hicho:

Mkutano Wa Kwanza

(Usiku wa Alhamisi, 23 Rajab, 1345 A.H.)

Hafidh Muhammad Rashid, Sheikh Abdu’s-Salam, Sayyid Abdu’l-Hayy, na wanachuoni wengine wa eneo hilo walihudhuria. Mjadala ulianza mbele ya mkusanyiko mkubwa. Katika majarida na magazeti, walimuita mwandishi kama “Qibla-o-Ka’ba,” lakini katika kurasa hizi nimejiita mwenyewe kama “Muombezi” na Hafidh Muhammad Rashid kama “Hafidh.”

Hafidh: Tumefurahishwa sana kupata fursa hii ili kujadili nukta za msingi ambazo kwazo tunahitilafiana. Kwanza lazima tuamue jinsi tutakavyo endesha mjadala huu.

Muombezi: Niko tayari kushiriki katika mjadala huu kwa masharti kwamba tunaweka kando mawazo yote tuliyokuwa nayo kabla (juu ya imani zetu), na kujadili masuala kwa mantiki, kama ndugu.

Hafidh: Mimi pia niruhusiwe kutoa sharti moja: kwamba mjadala wetu uwe chini ya msingi wa maamrisho ya Qur’ani Tukufu.

Muombezi: Sharti hili halikubaliki kwa vile Qur’ani Tukufu ni yenye habari nyingi katika maelezo machache ambayo maana zake za ndani lazima zitafsiriwe kwa kurejea kwenye matukio mengine na hadithi.

Hafidh: Sawa, hili ni wazo la maana, lakini vile vile ni muhimu kwamba rejea zote zifanywe kwenye hadithi na matukio ambayo chimbuko lake ni juu ya ushahidi usiopingika. Lazima tujizuie kutokana na kurejea kwenye vyanzo vyenye mashaka.

Muomezi: Imekubalika. Kwa mtu kama mimi, ambaye ana fahari ya kutosha kudai uhu- siano na Mtume, sio haki kwenda kinyume na mifano iliyowekwa na jadi wangu, Mtume wa Uislamu. Ametambulishwa katika Qur’ani kama ifuatavyo:

{واﻧﱠﻚَ ﻟَﻌﻠَ ﺧُﻠُﻖ ﻋﻈﻴﻢ {4

“Na hakika una tabia njema kabisa.” (68:4)

Vile vile sio vizuri kutenda dhidi ya maamrisho ya Qur’ani Tukufu ambayo inasema:

{ادعُ اﻟَ ﺳﺒِﻴﻞ رﺑِﻚَ ﺑِﺎﻟْﺤﻤﺔ واﻟْﻤﻮﻋﻈَﺔ اﻟْﺤﺴﻨَﺔ ۖ وﺟﺎدِﻟْﻬﻢ ﺑِﺎﻟﱠﺘ ﻫ اﺣﺴﻦ ۚ{125

“Waite watu katika njia ya Mola wako kwa hikima na mauidha mema, na ujadiliane nao kwa nama iliyo bora…” (16:125)

Uhusiano Na Mtukufu Mtume

Hafidh: Samahani, unatoa rejea kwenye uhusiano wako na Mtukufu Mtume. Hiyo inajulikana sana, lakini naomba kwamba unifahamishe nasaba yako ili nipate kujua vipi jadi yako kinasaba imefikia kwa Mtume.

Muombezi: Nasaba ya jadi yangu humfikia Mtume kupitia kwa Imamu Musa Kadhim kama ifuatavyo: Muhammad, mtoto wa Ali Akbar (Ashrafu’l-Waidhin), mtoto wa Mujahid al-Waidhin, mtoto wa Ibrahim, mtoto wa Salih, mtoto wa Abi Ali Muhammad, mtoto wa Ali (ajulikanye kama Mardan), mtoto wa Abi’l- Qasim Muhammad Taqi, mtoto wa (Maqbulu’d-Din) Husein, mtoto wa Abi Ali Hasan, mtoto wa Muhammad bin Fadhullah, mtoto wa Is’haq, mtoto wa Hashim, mtoto wa Abi Muhammad, mtoto wa Ibrahim, mtoto wa Abi’l-Fiyan, mtoto wa Abdallah, mtoto wa Hasan, watoto wa Ahmad (Abu Tayyib), mtoto wa Abi Ali Hasan, mtoto wa Abu Ja’far Muhammad al-Hari (Nazil-e-Kirman), mtoto wa Ibrahim Az-Zarir (ajulikanaye kama Mujab), mtoto wa Amir Muhammad al-Abid, mtoto wa Imamu Musa Kadhim, mtoto wa Imamu Muhammad Baqir, mtoto wa Imamu Ali Zainu’l-Abidin, mtoto wa Imamu Husein, mtoto wa Amir’l-Muminin, Ali bin Abi Talib.

Hafidh: Safu hii ya nasaba hufikia kwa Amir’l-Muminin, Ali bin Abi Talib (Mungu ambariki) ingawa umesema kwamba huishia kwa Mtukufu Mtume. Kwa kweli, pamoja na nasaba hii unapaswa kujiita miongoni mwa jamaa za Mtukufu Mtume na sio miongoni mwa kizazi chake cha moja kwa moja. Dhuria ni yule ambaye moja kwa moja anaungana na Mtume.

Muombezi: Safu ya jadi wetu hufikia kwa Mtume kupitia kwa Bibi Fatima Zahra, mama wa Imamu Husein. Sielewi ni kwa nini unasisitiza mno juu ya nukta hii.

Hafidh: Nafikiri nimeeleweka vibaya. Ni mtazamo wangu kwamba dhuria hutambuliwa kutoka upande wa kiume tu. Nanukuu ubeti wa Kiarabu: “Watoto wangu, wajukuu, na mabinti wanatokana na mimi, lakini watoto wa binti wangu hawatokani na mimi.” Kama unaweza kuthibitisha vinginevyo, tafadhali fanya hivyo.

Muombezi: Kuna ushahidi imara, kutoka katika Qur’ani na kutoka katika hadithi, kuthibitisha nukta yangu.

Hafidh: Tafadhali usimulie ili tupata kuelewa.

Muombezi: Wakati ulipokuwa unaongea sasa hivi, nimekumbuka mazungumzo kati ya Harun ar- Rashid, Khalifa wa Kibani Abbas, na Imamu wetu Musa Kadhim juu ya suala hili. Imamu alitoa jibu la kuridhisha kiasi kwamba Khalifa mwenyewe alilikubali.

Hafidh: Ningependa kusikia kuhusu mazungumzo hayo.

Muombezi: Abu Ja’far Muhammad Bin Ali, mwenye lakabu ya Sheikh Saduq, katika karne ya nne A. H., katika kitabu chake Uyun-e-Akbar ar-Ridha (vyanzo vikubwa vya Ridha), na Abu Mansur Bin Ali Tabarsi, katika kitabu chake Ihtijajj, anatoa maelezo kinaganaga ya mazungumzo ambayo yalifanyika kati ya Harun ar-Rashid na Imamu Musa Ja’far katika baraza ya Khalifa. Khalifa alimuuliza Imamu: “Unawezaje kudai kwamba wewe ni dhuria wa Mtukufu Mtume? Mtume hana dhuria. Inakubaliwa kwamba dhuria ni kutoka upande wa kiume na sio upande wa kike. Wewe ni kizazi cha bint yake.” Imamu akasoma Aya ya 84-85 kutoka Sura ya 6 ya Qur’ani Tukufu:

ووﻫﺒﻨَﺎ ﻟَﻪ اﺳﺤﺎق وﻳﻌﻘُﻮب ۚ ﻛ ﻫﺪَﻳﻨَﺎ ۚ وﻧُﻮﺣﺎ ﻫﺪَﻳﻨَﺎ ﻣﻦ ﻗَﺒﻞ ۖ وﻣﻦ ذُرِﻳﺘﻪ داۇود وﺳﻠَﻴﻤﺎنَ واﻳﻮب وﻳﻮﺳﻒ {وﻣﻮﺳ وﻫﺎرونَ ۚ وﻛﺬَٰﻟﻚَ ﻧَﺠﺰِي اﻟْﻤﺤﺴﻨﻴﻦ {84

{وزَﻛﺮِﻳﺎ وﻳﺤﻴ وﻋﻴﺴ واﻟْﻴﺎس ۖ ﻛﻞ ﻣﻦ اﻟﺼﺎﻟﺤﻴﻦ {85

“Na tukampa (Ibrahim) Is’haqa na Yakuub, wote tukawaongoa. Na Nuh tulimuongoa zamani, na katika kizazi chake Daudi na Suleimani na Ayub na Yunus na Musa na Harun. Na hivi ndivyo tuwalipavyo wafanyao mema. Na Zakaria na Yahya na Isa na Ilyasa, wote walikuwa miongoni mwa watu wema.” (6:84-85)

Imamu akamuuliza Khalifa: “Ni nani aliyekuwa baba wa Isa?” Harun akajibu kwamba Isa alikuwa hana baba. Imamu akasema: “Kulikuwa hakuna yeyote aliyekuwa baba yake, na bado Allah alimjumuisha Isa katika dhuria wa mitume kupitia Mariamu. Hivyo hivyo ame- tujumuisha sisi katika dhuria wa Mtume kupitia kwa jadi wetu Bibi Fatima.” Aidha, Imamu Fakhur’d-Din Razi, katika kitabu chake Tafsir-e-Kabir, juzuu ya 4, uk. 124, anasema kuhusiana na aya hii kwamba, inathibitisha kwamba Hasan na Husein ni watoto wa Mtume wa Uislamu.

Kwa vile katika aya hii Mungu amemdhihirisha Isa kama kizazi cha Ibrahim, na Isa hana baba, uhusiano huu ni kutoka upande wa mama. Katika hali hiyo hiyo, Hasan na Husein ni dhuria wa kweli wa Mtume. Imamu Musa alimuuliza Harun kama anataka uthibitisho zaidi. Khalifa akamuambia Imamu aendelee. Imamu akasoma Aya ya 61 kuto- ka Sura ya 3 ya Qur’ani Tukufu: “Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikia ilmu, waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake wetu na wanawake wenu, na sisi na ninyi, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo,”

Aliendelea, akisema kwamba hakuna mtu hata mmoja ambaye amewahi kudai kwamba katika tukio hilo la maapizano (Mubahila) dhidi ya Wakiristo wa Najran kwamba Mtume alimchukuwa pamoja na yeye mtu yeyote isipokuwa Ali Bin Abi Talib, Fatima, Hasan na Husein. Kwa hiyo hufuatia kwamba “sisi” (anfusana) maana yake ni Ali Bin Abi Talib. “Wanawake” (nisa’ana) maana yake Fatima na “Watoto” (abna’ana) maana yake Hasan na Husein, ambao Allah amewatambulisha kama watoto wa Mtume mwenyewe. Kwa kusikia hoja hii, Harun aliguta, “Hongera, Ewe Abu’l-Hasan.” Kwa uwazi mantiki hii huthibitisha kwamba Hasan na Husein (watoto wa Bibi Fatima) ni watoto wa Mtukufu Mtume.

Nyongeza Ya Ushahidi Kuthibitisha Kwamba Kizazi Cha Fatima Ni Dhuria

Wa Mtukufu Mtume.

Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali, mmoja wa wanachuoni wenu wakubwa, katika kitabu chake Sharh’l-Nahju’l- Balagha, na Abu Bakr Razi katika tafsir yake, wameionesha aya hiyo hiyo wakithibitisha kwamba Hasan na Husein wanatoka upande wa mama yao, ni watoto wa Mtukufu Mtume katika njia ile ile ambayo Allah katika Qur’ani Tukufu amemjumuisha Isa katika kizazi cha Ibrahim kutoka upande wa mama yake, Mariamu.

Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i, katika kitabu chake Kifayatu’t-Talib; Ibn Hajar Makki katika ukurasa wa 74 na 93 wa Sawa’iq Muhiriqa, kutoka kwa Tabrani na Jabir Bin Abdullah Ansari, na Khatib Khawarizmi katika Manaqib kutoka kwa Ibn Abbas - wote wanasimulia kwamba Mtume alisema: “Allah ameumba dhuria wa kila Mtume kutokana na kizazi chake mwenyewe, lakini dhuria wangu waliumbwa katika kizazi cha Ali.” Vile vile Khatib-e-Khawarizmi katika Manaqib; Mir Seyyid Ali Hamadani Shafi’i katika Mawaddatu’l-Qubra; Imamu Ahmad Bin Hanbal, katika Musnad, na Sulayman Hanafi Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda wanasimulia katika maneno hayohayo kwa zaidi au pungufu, kwamba Mtukufu Mtume amesema: “Watoto wangu hawa wawili, ni maua mawili ya ulimwengu huu, na wote wawili ni Maimamu, imma wawe ni Maimamu kwa wazi au kimya kimya wakiwa wamekaa nyumbani.”

Na Sheikh Sulayman Hanafi, katika Yanabiu’l-Mawadda, ameitoa sura ya 57 kwenye suala hili na akaonesha hadithi nyingi kutoka kwa wanachuoni wake mwenyewe, kama Tabrani, Hafidh Abdu’l-Aziz Ibn Abi Shaiba, Khatib-e-Baghdadi Hakim, Baihaqi, na Tabari - wote wanasimulia katika maneno yanayohitalifiana kidogo kwamba Hasan na Husein ni watoto wa Mtume.

Kuelekea mwisho wa sura hiyo hiyo, Abu Salih anaandika: Hafidh Abdu’l-Aziz Bin Al- Akhzar, Abu Nu’aim, Tabari Ibn Hajar Makki katika ukurasa wa 112 wa Sawa’iq Muhriqa, kutoka kwa Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i mwishoni mwa jalada la 1, baada ya sura

100 za Kifayatu’t-Talib, na Tabari katika simulizi ya Imamu Hasan anasimulia kwamba Khalifa wa pili, Umar Bin Khattab, alisema: “Nilimsikia Mtume akisema kwamba katika Siku ya Hukumu kila ukoo utatenganishwa isipokuwa kizazi changu. Kila kizazi cha binti ni kutoka upande wa baba isipokuwa kizazi cha Fatima, ambacho kimeunganishwa na mimi. Mimi ni baba yao na jadi wao.” Sheikh Abdullah Bin Muhammad Bin Amir Shabrawi Shafi’i, katika kitabu chake Kitabu’l-Ittihaf bi Hubbi’l-Ashraf, alinukuu hadithi hii kutoka kwa Baihaqi na Darqutni kutoka kwa Abdullah Bin Umar, na yeye kutoka kwa baba yake, kwenye harusi ya Ummu Kulthum. Na Jalalu’d-Din Suyuti akinukuu kutoka kwa Tabrani katika kitabu chake Ausat, amesimulia kutoka kwa Khalifa Umar na Sayyid Abu Bakr Bin Shahabu’d-Din Alawi katika ukurasa wa 39-40 wa sura ya 3 ya Rishfatu’s- Sadi min bahra Fadha’il Bani Nabiu’l-Hadi (iliyopigwa chapa katika Maktabi A’lamiyya, Misr 1303 A.H.) huthibitisha kwamba dhuria wa Fatima ni kizazi cha Mtume wa Uislamu.

Kwa hiyo, ubeti ambao umeunukuu hauna nguvu mbele ya ushahidi wote huu wa kinyume chake. Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i, katika kitabu chake Kifayatu’t-Talib, anathibitisha kwamba watoto wa binti wa Mtume ni watoto wa Mtukufu Mtume. Halikadhalika, kuna hadithi nyingine nyingi ambazo huthibitisha kwamba watoto wa Bibi Fatima ni watoto wa Mtume. Safu yetu ya jadi huenda mpaka kwa Imamu Husein; kwa hiyo, sisi ni dhuria wa Mtume.

Hafidh: Hoja yako ni ya mantiki na kuridhisha. Watu walitawanyika kwa ajili ya Swala ya Isha. Wakati wa mapumziko Nawab Abdu’l- Qayum Khan, ambaye anatokana na familia sharifu ya Kisunni, alitaka ruhusa kumuuliza Muombezi maswali fulani.

Kwanini Shia Wanachanganya Swala Zao

Nawab: Kwa nini Shia wanachangana Swala ya Dhuhr na Alasir na Maghari na Isha? Hii sio sawa kulingana na matendo ya ibada ya Mtukufu Mtume.

Muombezi: Kwanza kabisa, miongoni mwa wanachuoni wenu kuna tofauti nyingi za maoni kuhusu suala hili. Pili, unasema tunakwenda kinyume na mwenendo wa Mtume. Hapa umekosea kwani Mtukufu Mtume amezoea kuswali Swala zake katika njia zote, wakati mwingine kwa kuzitengenisha na wakati mwingine kwa kuzichanganya.

Hapo Nawab Swahib aliwageukia wanachuoni wake, aliwauliza kama ni kweli kwamba Mtume aliswali katika njia zote.

Hafidh: Ndio alifanya hivyo, lakini ni wakati tu alipokuwa safarini au wakati kama kuna vikwazo vingine fulani, kama mvua. Vinginevyo, wakati alipokuwa nyumbani siku zote alikuwa akiswali swala zake kwa kuzitenganisha.

Muombezi: Imeandikwa katika vitabu vyenu wenyewe vya hadithi kwamba Mtume ali- zoea kusali Swala zake kwa kuzitenganisha na halikadhalika kwa kuzichanganya akiwa nyumbani na bila kikwazo chochote. Hadithi nyingi zinathibitisha ukweli huu. Muslim Bin Hajjaj katika Sahih yake, katika mlango wa “Jam’a Baina’s-Salatain fi’l-Hadhar,” anasema kwamba Ibn Abbas alisema: “Mtume alizoea kuswali Swala ya Dhuhr na Alasir kwa kuziunganisha na halikadhalika hivyo hivyo kwa Swala za Magharib na Isha bila ya kuwa na kikwazo cha kufanya hivyo, au wakati alipokuwa nyumbani.” Tena Ibn Abbas alisimulia:

“Tuliswali rakaa nane za Dhuhr na Alasir na baadae rakaa saba za Magharib na Isha kwa kuziunganisha tukiwa pamoja na Mtume.” Hadithi hiyo hiyo imesimuliwa na Imamu Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake jalada la kwanza, ukurasa wa 221. Halikadhalika, Imamu Muslim ananukuu idadi ya hadithi kuhusiana na suala hili.

Anamnukuu Abdullah Bin Shaqiq akiwa amesema kwamba siku moja Abdullah Ibn Abbas alikuwa anahutubia baada ya Swala ya Alasir mpaka jua likazama na nyota zikawa zinaonekana. Watu wakapiga makelele, “Swala, Swala,” lakini Ibn Abbas hakuwajali. kisha mtu mmoja wa Bani Tamimi alipiga kelele, “Swala, Swala.” Ibn Abbas akasema: “Unanikumbusha mimi kuhusu Sunna, lakini mimi mwenyewe nimemuona Mtume akikusanya Swala za Dhuhr na Alasir halikadhalika Magharib na Isha.” Abdullah Bin Shaqiq alisema alikuwa hana hakika kuhusu maneno haya na alikwenda kwa Abu Huraira kumuuliza kuhusu maneno hayo. Alithibitisha kile alichokisema Ibn Abbas.

Kupitia sanad nyingine ya wasimuliaji, Abdullah Bin Shaqiq alisimulia kutoka kwa Aqil kwamba siku moja Abdullah Ibn Abbas aliwahutubia watu juu ya mimbari. Alibaki pale kwa muda mrefu mpaka giza likaingia. Wakati mtu mmoja alipopiga kelele mara tatu, “Swala, Swala, Swala,” Abdullah Ibn Abbas alikasirika na akasema: “Ulaaniwe wewe. Unathubutu kunikumbusha mimi kuhusu Swala, ingawaje wakati wa Mtukufu Mtume tuli- zoea kukusanya Swala za Adhuhr na Alasir na halikadhalika Magharib pamja na Isha.” Zarqani katika Sharhe Mawatta cha Imamu Malik, jalada la 1, katika sura ya Jama’a Baina’s-Salatain, ukurasa wa 263, anaeleza, “Nisa’i alisimulia kutoka kwa Amru Bin Haram kutoka kwa Abi Sha’atha kwamba Ibn Abbas aliswali Dhuhr na Alasir na halikadhalika Magharib na Isha kwa pamoja mjini Basra bila kukawia au kitendo chochote kati yao. Alisema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliswali katika njia hii hii.”

Vile vile Muslim katika Sahih yake na Malik katika Mawatta, sura ya Jam’a Baina’s- Salatain, na Imamu Hanbal katika Musnad wanamnukuu Ibn Abbas kutoka kwa Sa’id Bin Jabir kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliswali Swala zake za Dhuhr na Alasir pamoja mjini Madina bila kulazimishwa kufanya hivyo kwa hofu au hali mbaya ya hewa. Abu Zubair akasema alimuuliza Abu Sa’id kwa nini Mtume alikusanya Swala hizo mbili. Sa’id akasema yeye vile vile alimuuliza Ibn Abbas swali kama hilo hilo.

Ibn Abbas alijibu kwamba alikusanya Swala hizo mbili ili kwamba wafuasi wake wasije wakawekwa katika uzito na shida zisizo na sababu. Vile vile, katika hadithi nyingine nyingi, Ibn Abbas inasimuliwa kwamba alisema Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Uislamu alikusanya Swala za Dhur na Alasir halikadhalika na Magharib na Isha bila kulazimishwa kufanya hivyo. Hadith hizi katika Sahihi zenu na vitabu vyingine sahihi huthibitisha kuruhusiwa uku- sanyaji wa Swala mbili, nyumbani au safarini.

Hafidh: Hakuna nukuu kama hiyo ya hadithi katika Sahih Bukhari.

Muombezi: Kwa sababu waandishi wote wa Sahih, kama vile Muslim, na Nisa’i, Ahmad Bin Hanbal, na wafasir wa Sahih mbili, ya Muslim, Bukhari, na wanachuoni wengine wakubwa wa ki-Sunni wamenukuu mambo haya, hii inatosha kwetu kuishindisha nukta yetu. Lakini kwa kweli Bukhari vile vile ameziandika hadithi hizi katika Sahih yake, lakini kwa hila ameziweka mbali na sehemu zao husika, ile sehemu inayohusika na ukusanya- ji wa Salat mbili.

Kama utaipitia ile milango ya “Bab-e-Ta’akhiru’dh-Dhuhur li’l-Asr Min Kitabe Mawaqtu’s-Salat” na “Bab-e-Dhikru’l-Isha wa’l-Atma” na Bab-e-Waqitu’l- Maghrib,” utaziona hadithi zote hizi humo. Hadithi hizi kuandikwa chini ya kichwa cha habari: “Ruhusa na Mamlaka ya Kisheria ya kukusanya Salat mbili” huthibitisha kwamba ni imani ya kawaida ya wanachuoni wa madhehebu hizi mbili.

Usahihi wa hadithi hizi umekwisha kubaliwa katika vitabu vya Sahih. Kwa sababu hiyo, Allama Nuri katika Sharhe Sahih Muslim, Asqalani, Qastalani, Zakariyya-e-Razi katika sharhe ambayo imeandikwa juu ya Sahih Bukhari, Zarqani katika Sharhe yake juu ya Muwatta - kitabu cha Imamu Malik, na wengine wamesimulia hadithi hizi. Baada ya kunukuu hadithi ya Ibn Abbas, walikubali usahihi wake na wakakiri kwamba hadithi hizi ni uthibitisho wa kukubalika kwa kukusanya Salat mbili.

Nawab: Imewezekanaje kwamba hadithi hizi zimekuwa katika matumizi tangia wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini wanachuoni wamechukuwa njia nyingine?

Muombezi: Hali hii haikomei kwenye nukta hii peke yake. Utaona mifano mingi kama hii baadae. Katika suala hili, Mafaqih wa ki-Sunni, kwa wazi bila ya kufikiria kwa makini, au kwa sababu nyingine ambazo mimi sizielewi, wametoa maelezo yasiyoleweka kukinzana na hadithi hizi. Kwa mfano, wanasema kwamba huenda hadithi hizi huzungumzia hali zinazohusiana na hofu, hatari, mvua, au upepo mkali. Baadhi ya wanachuoni wenu wa zamani, kama Imamu Malik, Imamu Shafi’i, na baadhi ya wanachuo wa Madina wametoa maelezo kama hayo hayo. Namna hii, pamoja na ukweli kwamba hadithi ya Ibn Abbas kwa uwazi kabisa inasema kwamba ukusanyaji wa Swala mbili ulikuwa unafanywa bila kikwazo cha hofu au uwezekano wa kunyesha mvua.

Wengine wamesema kwamba huenda mawingu yalikuwa yametanda angani, na wale waliokuwa wakisali hawakujua ni saa ngapi. Pengine walipomaliza kusali Swala yao ya Adhuhur, mawingu yalitawanyika, na wakaona kwamba ilikuwa ni wakati wa Swala ya Alasir. Hivyo wakalazimika kusali Adhuhuri na Alasiri kwa pamoja. Sidhani maelezo zaidi yasiyo yamkinika yanaweza kupatikana.

Pengine wafasiri hawa hawakujali kufikiria kwamba mtu aliyekuwa akisali Swala hizo ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Uislamu. Mawingu hayakumaanisha kwake kile ambacho kingemaanishwa kwa wengine. Anajua sababu zote na matokeo. Mbali na ukweli kwamba maelezo haya hayaridhishi, ukusanyaji wa Swala za Mahgarib na Isha unakataa maelezo yao. Katika wakati huo mawingu hayana uhusiano na suala hili. Kama tulivyosema, hadithi ya Ibn Abbas kwa uwazi inaeleza kwamba khutuba yake iliendelea kwa muda mrefu mpaka wasikilizaji wakapiga kelele, “Swala, Swala.”

Walimkumbusha kwamba nyota zimetokea na kwamba ilikuwa ni wakati wa Swala. Lakini aliichelewesha Swala ya Magharibi kwa makusudi ili aje kuswali zote, Magharib na Isha kwa pamoja. Abu Huraira vilevle alithibitisha kitendo hiki, akisema kwamba Mtume vile vile aliswali kwa nama hiyo hiyo. Maelezo ya uwongo kama hayo, katika mwanga wa mwongozo wa dhahiri, husikitisha.

Wanachouni wenu wenyewe wameyapuuza hayo. Sheikhu’l- Ansari, katika kitabu chake, Tuhfatu’l-Bari fi Sharhe Sahihu’l-Bukhari katika sura ya Salatu’z-Dhuhr ma’l-Asr wa’l-Magharib ma’l- Isha ukurasa wa 292, jalada la 2, na halikadhalika Allama Qastalani, katika ukurasa wa 93 jalada la 2 la Irshadu’s-Sari fi Sharhe Sahihu’l-Bukhari, na hivyo hivyo na washereheshaji wengine wa Bukhari wanakiri kwamba aina hii ya maelezo ni kinyume na maana ya wazi ya hadithi na kwamba kusisitiza kwamba kila Swala iswaliwe peke yake ni mashrti yasiyo na msingi. Nawab: Basi mgogoro huu umejitokeza vipi mpaka madhehebu mbili za Waislamu kila moja inataka kumwaga damu ya mwenzake, na kulaumu kitendo cha mwenzake?

Muombezi: Unasema kwamba madhehebu hizi mbili ni adui kwa kila mmoja, lakini sikubaliani na wewe. Sisi Mashi’a hatumdharau mwanachuoni yeyote au mtu wa kawaida katika ndugu zetu Masunni. Tunasikitika kwamba propoganda za Makhariji, Manasibi na Bani Umayyah zimeathiri nyoyo za baadhi ya watu. Kwa bahati mbaya sana, baadhi ya Masunni wanawachukulia ndugu zao Mashi’a, ambao wako pamoja nao kwa kuhusiana na Qibla (Ka’aba), Kitabu Kitukufu (Qur’ani), Mtume, utekelezaji wa matendo ya dini, na kujiepusha kutokana na madhambi, kuwa kama Marafidhi (watofautishaji), waabudu masanamu, na makafiri.

Amma kwa swali lako kuhusu vipi tofauti hizi zilivyojitokeza, labda hili tunaweza kulijadili katika mikutano yetu ya baadae. Kuhusu kusali Swala kwa kutenganisha au kwa pamoja, wanachuoni wa sheria wa ki- Sunni wenye kutegemewa wamenukuu hadithi ambazo huruhusu kusali Adhuhuri na Alasiri na Magharibi na Isha kama jambo la wepesi, wasaa au usalama. Sijui kwa nini baadhi ya watu hawaoni kwamba inaruhusika kusali Swala mbili pamoja pasi na kuwa na udhuru wowote. Baadhi ya wanachuo, kama Abu Hanifa na wafuasi wake wameikataza katika hali yoyote, iwe kuna udhuru au la, au Swala iwe inasaliwa wakati mtu akiwa safarini au nyumbani.

Shafi’i, Maliki, na Hanbali, pamoja na hitilafu zao zote katika kanuni za msingi na zisizo za msingi, wameruhusu ukusanyaji wa Swala wakati wa safari ya halali. Lakini Maulamaa wa ki-Shi’a, wakiwa katika utii wa Imamu na kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wameruhusu bila masharti yoyote ukusanyaji wa Swala mbili kwa pamoja.

Hakika kusali Swala katika wakati ulioanishwa kwa kila Swala ni bora kuliko kuzisali kwa wakati mmoja, kama ambavyo imeelezwa kwa uwazi katika vitabu vya tafsir vinavyoshughulika na matatizo ya utekelezaji wa masuala ya dini vilivyoandikwa na Maulamaa wa ki-Shi’ah. Kwa vile watu mara nyingi wanakuwa na shughuli nyingi katika mambo yao wenyewe na wasi wasi, wanaogopa huenda wakazikosa Swala zao. Kwa hiyo, kwa nafasi zao na kuepuka uzito na shida, Mashi’a wanasali Swala zao mbili katika wakati mmoja, mapema au kwa kuahirisha, katika wakati ule ule uliotengwa kwa ajili ya Swala. Sasa nafikiri kiasi hiki kinatosha kuwapa mwanga ndugu zetu Masunni ambao hutuangalia kwa hasira. Bila shaka tunaweza kurudi kwenye majadiliano yetu kuhusu misingi, ambapo baadae masuala yanayohusu ibada yatatatuliwa.

Jinsi Wazazi Wa Allama Walivyohama Kutoka Hijazi Kwenda Iran

Hafidh Sahib alimuomba Allama Sultanu’l-Wa’idhin amueleze ni vipi wazazi wake walivyohama kutoka Hijazi kwenda Iran. Alieleza historia ya wahenga wake ambao - uawa huko Shirazi kwa amri ya mfalme wa ki-Banu Abbas. Makaburi yao mpaka sasa bado yanawavutia mahujaji kutoka sehemu za mbali. Maarufu miongoni mwao ni Sayyid Amir Muhammad Abid, Sayyid Amir Ahmad ( Charagh), na Sayyid Alau’d-Din Husein, wote ni watoto wa Imamu Musa Kadhim. Maelezo kuhusu familia yake yanaondolewa hapa.

Jinsi Kaburi La Amiru’l-Mu’minin Ali (A.S.) Lilivyogunduliwa.

Vile vile ulitajwa ungunduzi wa kaburi la Amiru’l-Mu’minin ‘Ali (as).

Hafidh: Lakini kaburi la Amiru’l-Mu’minin liligunduliwa katika hali gani miaka 150 baada ya kifo chake?

Muombezi: Kwa sababu uonevu wa Banu Umayya ulikuwa mkali sana wakati wa mwisho wa uhai wa ‘Ali, hivyo aliagiza katika wosia wake kwamba azikwe kwa siri wakati wa usiku, na kwamba isiachwe alama yoyote ya kaburi hilo.

Ni jamaa zake wachache tu wa karibu na watoto wake ndio waliohudhuria mazishi yake. Asubuhi ya tarehe 21 Ramadhan siku ambayo ilikuwa ndio azikwe, misafara miwili ilitayarishwa. Mmoja ulielekezwa kwenda Makka, na mwingine kwenda Madina. Hii ndio sababu iliyofanya kwa miaka mingi kaburi lake lisijulikane, isipokuwa kwa jamaa zake wachache na watoto wake tu.

Hafidh: Kwanini eneo la kaburi hilo likafanywa siri?

Muombezi: Huenda ni kwa sababu ya hofu ya tabia isiyo ya dini ya Banu Umayya. Walikuwa maadui makhususi wa jamaa ya kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w). Wangeweza kulivunjia heshima kaburi lake.

Hafidh: Lakini inawezekana kwamba Mwislamu, hata kama ni adui kiasi gani, anaweza kulifanyia vurugu kaburi la ndugu yake Mwislamu?

Muombezi: Umesoma historia ya Banu Umayya? Kuanzia siku ambayo utawala huu mbaya uliposhika madaraka, mlango wa maonevu ulifunguliwa miongoni mwa Waislamu. Subuhana-LLAH! Maovu yalioje waliyoyafanya! Damu iliyoje waliyoimwaga, na heshima zilizoje walizozivunja!

Kwa aibu kubwa, wanachuoni wenu wakubwa wameandika jinai zao nyingi. Allama Maqrizi Abu’l-Abbas Ahmad bin Ali Shafi’i ameandika maovu ya Banu Umayya yanayoumiza moyo kabisa katika kitabu chake Annaza’ Wa’t-takhasum fima baina Bani Hashim wa Bani Umayya.

Bani Umayya Na Utiaji Najisi Wa Makuburi

Kwa mfano wa yale waliyokuwa na uwezo nayo, nitaonesha matukio mawili: Kuuwawa shahidi kwa Zaid bin Ali bin Husein, ajulikanaye kama Zaid Shahid, na kuuwawa shahidi kwa mtoto wake, Yahya. Wanahistoria wote wa Shi’a na Sunni wameandika kwamba wakati Hisham bin Malik alipokuwa Khalifa, alitenda maovu mengi. Mwishowe, Zaid bin Ali, mtoto wa Imamu Zainu’l-Abidin na anayejulikana sana kama mwanachuo mkubwa na mwanatheolojia mchamungu, alikwenda kumuona Khalifa kutafuta haki kwa ajili ya manung’uniko ya Bani Hashim.

Lakini punde tu Zaid alipowasili, Khalifa badala ya kumsalimu kama mtoto wa moja kwa moja wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alimtukana kwa lugha ya kuchukiza sana ambayo siwezi kuirudia hapa.

Kwa sababu ya kudhalilishwa huku alikofanyiwa, Zaid aliondoka na kwenda Kufa, ambako aliunda jeshi dhidi ya Bani Umayya. Gavana wa Kufa, Yusuf bin Umar Thaqafi, alitoka na jeshi kubwa kumkabili. Zaid alisoma shairi lifuatalo: “Maisha ya udhalilifu na kifo cha heshima, vyote ni chembe zenye uchungu, lakini kama moja wapo lazima ichanguliwe, chaguo langu ni kifo cha heshima.”

Ingawa alipigana kishujaa, Zaid aliuwawa katika mapigano hayo. Mtoto wake, Yahya, alichukua mwili wake kutoka kwenye uwanja wa vita na akamzika mbali kutoka mjini karibu na ukingo wa mto, na kusabibisha maji kupita juu yake. Hata hivyo, kaburi hilo liligunduliwa, na chini ya amri ya Yusuf mwili huo ulifukuliwa, kichwa cha Zaid kilikatwa na kupelekwa Syria kwa Hisham.

Katika mwezi wa Safar, 121 A.H., Hisham aliamuru mwili mtakatifu wa mtoto huyu wa Mtume (s.a.w.w) uwekwe kwenye kiunzi cha kunyongea ukiwa uchi kabisa.

Kwa muda wa miaka minne ulikaa kwenye kiunzi cha kunyongea. Baadae, wakati Walid bin Yazid bin Abdu’l-Malik bin Marwan alipokuwa Khalifa katika mwaka wa 126 A.H., aliamrisha kwamba mifupa ile itolewe kutoka kwenye kiunzi cha kunyongea, ichomwe, na jivu lake lisambazwe juu lichukuliwe na upepo.

Mtu huyu aliyelaaniwa alitenda uovu kama huu huu kwenye mwili wa Yahya bin Zaid wa Gurgan. Mtu huyu mtukufu vile vile alipinga uonevu wa Bani Umayya. Yeye pia aliuwawa katika medani ya vita. Kichwa chake kilipelekwa Syria na kama alivyofanyiwa mtukufu baba yake, mwili wake ulitundikwa kwenye kiunzi cha kunyongea kwa muda wa miaka sita.

Marafiki na maadui wote kwa pamoja walilia walipouona mwili wake. Waliu’d-Din Abu Muslim Khorasani, ambaye alipigana dhidi ya Bani Umayya kwa niaba ya Bani Abbas, aliuchukuwa mwili wake na kuuzika huko Gurgan, ambako ni sehemu ya kuhiji ().

Matendo Maovu Ya Ufalme Huu

Kwa kuzingatia maovu ya ufalme huu uliolaaniwa, mwili wa Amiru’l-Muminin, ‘Ali (as) ulizikwa wakati wa usiku, na hakuna alama ya kaburi hilo iliyoachwa. Kaburi likabakia bila kuonekana mpaka wakati wa Khalifa Harun ar-Rashid. Siku moja Harun alikwenda kuwinda katika eneo la Najaf, ambako paa waliishi kwa wingi. Wakati mbwa walipofukuza paa, walichukua hifadhi juu ya kilima kidogo (kilichotutumka juu ya ardhi) cha Najaf, kilima ambacho mbwa hao hawakuweza kukipanda.

Mara nyingi wakati mbwa waliporudi nyuma, paa waliteremka chini, lakini wakati mbwa wanapowarukia tena, wale paa huchukua tena hifadhi juu ya kile kilima. Harun akatuma watu wake kwenda Najaf kuuliza. Walimleta mzee mmoja kwake na Khalifa akauliza kuhusu siri ya kwa nini mbwa hawakupanda juu kilima.

Kugunduliwa Kwa Kaburi Tukufu La Ali.

Yule Mzee akajibu kwamba anaielewa Siri yake, lakini alikuwa anaogopa kuitoa. Khalifa akamhakikishia usalama wake, na yule mzee akamwambia: Siku moja nilikuja hapa pamoja na baba yangu, ambaye alipanda juu ya kilima na akaswali pale. Nilipomwuuliza kuna nini pale, akasema kwamba waliwahi kuja pale na Imam Ja’far Sadiq kwa ajili ya Ziara. Imam alisema kwamba hili ni kaburi Tukufu la Mheshimiwa babu yake, Amur’l Mu’miniina Ali, na kwamba muda mfupi litakujajulikana.”

Kwa amri ya Khalifa sehemu ile ilichimbuliwa, na alama za kaburi zikaonekana wazi pamoja na ubao wenye maandishi ya Ki-Syria yenye maana; “Kwa jina la Allah, Mwenye rehema, Mwenye kurehemu. Kaburi hili limetayarishwa na Mtume Nuh kwa ajili ya Ali, wasii wa Muhammad miaka 700 kabla ya gharika.”

Khalifa Harun alitoa heshima zake kwenye sehemu ile na akaamuru ule udongo urudish- we. Kisha akasali rakaa mbili. Alilia sana na akajilaza juu ya kaburi. Baadae, kwa amri yake, taarifa ya tukio lote ilitolewa kwa Imam Musa Kadhim huko Madina. Imam alithibitisha kwamba kaburi hilo ni la Mheshimiwa babu yake, Amiru’l-Mu’minin Ali, lipo mahala hapo. Kisha Harun akaamuru jengo la mawe lijengwe juu ya kaburi tukufu la Amiru’l-Mu’minin, ambalo lilikuja kujulikana kama “Hajar Harun.” Kwa wakati huo habari zilisambaa na Waislamu wakaizuru sehemu hiyo tukufu.

Ibrahim Mujab, babu yake mkubwa wa Sultani’l-Wa’idhin (Muombezi) pia alitoka Shiraz kwa ajili ya Ziara hii tukufu na baada ya kukamilisaha Ziara hii, yeye akafariki huko Karbala. Alizikwa karibu na kaburi tukufu la Babu yake Mkubwa, Imam Husein. Kaburi lake liko pembe ya Kaskazini Mashariki ya kuba lake tukufu na linazuriwa mara kwa mara na wapenzi wake.

Khitilafu Kuhusu Sehemu Aliyozikwa Amiru’l- Mu’minin.

Hafidh: Pamoja na maneno haya ya kuthibitisha na yenye nguvu, nafikiri kwamba kaburi la Ali (R.A) haliko Najaf. Wanachuoni wanatofautiana juu ya nukta hii. Baadhi wanasema liko kwenye Ikulu mjini Kufa; baadhi wanasema liko kwenye Kibla ndani ya Msikiti Mkuu wa Kufa; baadhi wanasema liko kwenye lango linalojulikana kama Ba-e-Kinda katika Msikiti wa Kufa; baadhi wanashikilia kwamba liko ndani ya Rahba huko Kufa; na bado wengine wanasema liko pembeni mwa kaburi la Fatima huko Baqi. Katika yetu, pia kuna sehemu karibu na Kabul inajulikana kama Kuba la Ali. Kutokana na maelezo fulani, mwili Mtukufu wa Ali uliwekwa kwenye Kasha na ukalazwa juu ya mgongo wa ngamia na ukapelekwa kuelekea Madina.

Kikundi cha watu kikanyakua lile kasha, wakidhania lina vitu vya thamani. Wakati wanalifungua, wakaona mwili ule Mtukufu, wakaule- ta Kabul, na ukazikwa katika sehemu hii. Ndio maana watu wanaitukuza sehemu hii.

Muombezi: Tofauti zilitokea kwa sababu ya maelezo ya wasia wake, ambao umeweka sharti kwamba matayarisho ya mazishi yake yatatize sehemu yake ya kuzikwa. Inasimuliwa na Imam Ja’far Sadiq kwamba katika wakati wake wa kufa, Amiru’l- Mu’minin alimwambia mtoto wake, Imam Hasan kwamba baada ya kumzika Najaf, ata- yarishe makaburi manne kwa ajili yake katika sehemu nne tofauti. Katika Msikiti wa Kufa, katika Rahba, katika nyumba ya Ju’da Hira, na Ghira. Shia wanakubali kwamba kaburi lake tukufu liko Najaf. Chochote walichojifunza kutoka kwa Ahli Bait ni sahihi. Watu wa nyumba wanajua vizuri zaidi kuhusu kinachohusiana na nyumba yao.

Kwa hakika nawashangaa wanachuo wenu ambao wamezitelekeza simulizi za Kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika kila jambo. Hawakuuliza kuhusu mahala pa kaburi la baba kwa watoto wake wenyewe ili kuelewa ukweli. Ni hakika kabisa kwamba watoto wanajua zaidi kuhusu kaburi la baba yao kuliko wengine. Kama nadharia hizi za sasa zingekuwa sawsawa, Maimam Watukufu wangewajulisha wafuasi wao juu ya hilo.

Lakini wamelithibitisha mahala lilipo Najaf, wamezuru hiyo sehemu wao wenyewe, na wamewahimiza sana wafuasi wao kuizuru sehemu hiyo. Sibt Ibn Jauz katika kitabu chake “Tadhkira” amezitaja tofauti hizi. Anasema: Maoni ya sita ni kwamba liko Najaf katika ile sehemu inayojulikana sana, ambayo kwa kawaida hufanyiwa Ziara. Kwa yote yaliyojitokeza, haya ndio maoni ya sawasawa.”

Halikadhalika, wanachuo wenu wengine kama Khatibu-e-Khawarizmi katika “Munaqib,” Muhammad bin Shafi’i katika “Matalibu’s- Su’ul”, Ibn Abi’l-Hadid katika “Sharhe Nahaju’l-Balagha”, Firuzabadi katika “Qamus,” yake chini ya neno Najaf, na wengine, wameshikilia kwamba kaburi la Amirul’-Mu’minin liko Najaf.

Mkutano Wa Pili, Ijumaa Usiku 24 Rajab, 1345 A.H.

Hafidh: Nilivutiwa mno na mazungumzo yako yenye maelekezo kuhusu mtiririko wa jadi yako. Nakiri kwamba wewe ni kizazi (dhuria) cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini nashangaa ni vipi mtu mwenye elimu kama wewe unakuwa chini ya ushawishi wenye ushusha hadhi wa maadui.

Ukiwa mwenye kuziacha njia za jadi wako Maarufu, umefuata njia za makafiri wa Iran. Ninachomaanisha hapa kwa njia za maadui wapumbavu ni yale mambo mapya ya uzushi (Bid’a) yaliyoingizwa katika Uislamu kupitia kwa Mayahudi.

Muombezi: Tafadhali hebu elezea ni nini unachomaanisha.

Dhana Potofu Kuhusu Asili Ya Madhehebu Ya Shia.

Hafidh: Historia yote ya Mayahudi imeharibiwa na hila. Abdullah bin Saba ‘San’a’i, Ka’bu’l-Ahbar, Wahhab Ibn Munabba, na wengine waliukiri Uislamu, na wakajifanya wanakubali hadith za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hivyo kusababisha ghasia miongoni mwa Waislamu.

Khalifa wa tatu Uthman bin Affan, aliwaandama na wakakimbilia Misri, ambako walianzisha madhehebu yajulikanayo kama Shia. Walieneza taarifa za uongo kuhusu Khalifa Uthman na kuandika hadith za uongo za kumaanisha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteuwa Ali kuwa Khalifa na Imamu.

Kwa kuanzishwa madhehebu haya vurugu zilienea, ambazo zilipelekea kuuwawa kwa Khalifa Uthman na kuchukuliwa kwa cheo cha ukhalifa na Ali. Kikundi kilichokuwa na uadui kwa Uthman kikasimama juu kumpendelea Ali. Wakati wa Ukhalifa wa Bani Umayya, wakati watu wa familia ya Ali na wafuasi wake walipokuwa wanauwawa, kikundi hiki kilijificha.

Bado, baadhi ya watu, kama Salman Farsi, Abu Dharr Ghifari, na Amar Yasir, waliunga mkono mwenendo wa Ali. Mashindano haya yaliendelea mpaka wakati wa Harun’ar- Rashidi, na hasa mwanae Ma’mun-ar-Rashidi Abbas, ambaye alimshinda ndugu yake kwa msaada wa wa-Irani, na kisha wakaeneza wazo la kwamba Ali alikuwa ni bora kuliko makhalifa wengine, Wa-Irani, wakiwa na uadui na Waarabu ambao waliwashinda, wakapata fursa ya kuwapinga Waarabu kwa kutumia jina la dini. Mashi’a wakapata nguvu katika kipindi cha Wadailami na Wafalme wa Ki-Safavid na hatimaye wakatambuliwa.

Basi wakajulikana rasmi kama madhehebu ya Shia. Wazoroasta wa Iran bado wanajiita Mashia. Kwa ufupi, madhehebu ya Shia yalianzishwa na Myahudi, Abdullah bin Saba. Vinginevyo kusingekuwa na neno kama Shia katika Uislamu. Babu yako, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alilichukia neno hilo.

Kusema kweli madhehebu ya Shia ni sehemu ya imani ya Kiyahudi. Nashangaa kwa nini umeacha njia za haki za jadi wako na ukafuata njia ya waliokutangu lia, ambao wamefuata njia za Kiyahudi. Ilikupasa ufuate Qur’ani Tukufu na mfano wa babu yako, Mtume (s.a.w.w.).

Ni Upuuzi Kumhusisha Abdullah Bin Saba’ Na Mashi’a

Muombezi: Ni kitu kisicho cha kawaida kwa mtu msomi kama wewe kutegemeza hoja zake katika misingi ya uongo kabisa. Hakuna maana kwako wewe kulihusisha jina la Abdullah bin Saba na Mashia. Abdullah bin Saba alikuwa Myahudi, na kutegemeana na vyanzo (rejea) vya Shia, yeye ni mnafiki na analaaniwa vikali. Ikiwa kwa wakati fulani alitokea kuwa rafiki wa Ali, ni uhusiano gani aliokuwa nao na Mashia? Kama mwizi atavaa guo ya Mwanachuo, akapanda juu ya mimbari, na akasababisha madhara kwa Uislamu, utayachukia mafundisho na kuwaita Wanachuoni wezi? **

** Huu ulikuwa mwaka wa 1927 (1345 A.H.), katika miaka ya hivi karibuni imebainika kwamba kulikuwa hakuna mtu anayeitwa Abdullah Ibn Saba, huu ulikuwa ni ubunifu wa mtu aliyekuwa akiitwa Seif. Ukweli huu umetokana na utafiti uliofanywa na mwanachuoni mtafiti, Al-Askari. Soma kitabu chake: “Abdallah bin Saba’ na ngano nyinginezo”

Kwa kweli Waislamu wa Madhehebu ya Shia kamwe hawajakuwa ni kikundi cha Siasa tu. Walikuwa wakati wote wanaunda madhehebu ya dini, ambayo hayakuanzishwa, kama unavyosema, katika wakati wa Ukhalifa wa Uthman, lakini lililinganiwa kutokana na maneno na maamrisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika wakati wake mwenyewe.

Wakati ambapo wewe unajadili kwa msingi wa ushahidi wa kubuni wa maadui, mimi nitanukuu kwa ajili yako Aya kutoka Qur’ani Tukufu na similizi za waandishi wenu wenyewe kuonyesha hali ya ukweli halisi. Maana Ya Neno Shi’a

Muombezi: Shi’a kama ujuavyo, kilugha ina maana ya “Mfuasi.” Mmoja wa maulamaa wenu mkubwa, Firuzabadi katika kitabu chake “Qamusu’l-lughat,” anasema:

Jina la Shi’a kwa kawaida lina maana ya kila mtu ambaye ni rafiki wa Ali na Ahlul-Bait wake. Jina hili ni lao peke yao.” Maana hii hii hasa inatolewa na Ibn Athir katika “Nihayatul’l-Lugha.” Kutokana na Sharh zenu wenyewe, neno Shia lina maana ya “wafuasi wa Ali ibn Abu Talib,” na lilikuwa likitumika katika njia hii katika wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Kwa kweli alikuwa ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe ambaye alilitambulisha neno Shi’a kwa maana ya “Mfuasi wa Ali bin Abu Talib.” Na neno hili lilikuwa likitumiwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye kuhusu yeye Allah (s.w.t.) Anasema:

{وﻣﺎ ﻳﻨْﻄﻖ ﻋﻦ اﻟْﻬﻮﱝ {3

{انْ ﻫﻮ ا وﺣ ﻳﻮﺣ {4

“Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake). Hayakuwa haya ila ni Wahyi uliofunuliwa.” (53: 3-4)

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaita wafuasi wa Ali “Shia,” “waliokombolewa” na “waliookolewa.”

Hafidh: Kiko wapi kitu kama hicho? Sisi hatujakiona kamwe.

Muombezi: Sisi tumekiona na hatufikirii kuwa ni sawa kuficha ukweli. Allah (s.w.t.) Amewalaani wafichaji na hao akawaita ni watu wa motoni. Allah (s.w.t.) Anasema:

“Hakika wale wanaficha hoja zilizo wazi na uongozi ambao tumeuteremsha baada ya kuzibainisha kwa watu kitabuni, hao anawalaani Allah na wanawalaani wenye kulaani.” (2:159) “Hakika wale wafichao aliyoyateremsha Allah katika Kitabu wakafadhilisha thamani ndogo, hao hawali matumboni mwao isipokuwa moto, wala Allah hatawasemeza Siku ya Kiyama wala hatawatakasa, na watapata adhabu iliyo kali.”

Hafidh: Kama tunaijua kweli na tukaificha nakubali kwamba tunastahili laana kama ilivyofunuliwa katika aya hizi tukufu.

Muombezi: Natumaini utaziweka akilini Aya hizi mbili ili kwamba usije ukashindwa nguvu na tabia au kutovumilia. Hafidh Abu Nu’aim Isfahani ni moja wa watu wenu maarufu sana katika wasimuliaji wa hadith. Ibn Khallikan amemsifu katika kitabu chake “Wafayatu’l Aayan” kama Huffadh mkubwa (Mtu wa hikma) na mmoja kati ya wasimuli- aji wa hadith aliyeelimika sana. Vile vile anaelezea kwamba jalida kumi za kitabu chake “Hilyatu’l–Aulya” ni miongoni mwa vitabu vizuri mno vya kufundishia. Salahu’d-din Khalil bin Aibak Safdi anaandika katika “Wafiy bi’l-Wafiyat” kuhusu yeye: “Mfalme wa wasimuliaji wa hadith, Hafidh Abu Nu’aim, alikuwa wa mbele sana katika ilmu, uchamungu, na uaminifu.

Alikuwa na nafasi ya hali ya juu katika usimuliaji na uelewaji wa hadhith. Kitabu chake kilicho bora sana ni “Hiliyatul’-Auliya” katika jalida kumi, zikiwa na chimbuko kutoka Sahih mbili (Bukhari na Muslim).” Muhammad bin Abdullah al- Khatab amemsifu katika “Rijali’l-Mishkati’l-Masabin.” akisema kwamba ni miongoni mwa wasimuliaji hadith wa mbele ambaye simulizi zake ni za kuaminika kabisa.

Kwa ufupi, Mwanachuo na Muhadithina huyu mwenye kuheshimika na fahari ya Maulamaa wenu, anasimulia kutoka kwa Abdullah ibn Abbas kupitia nyororo yake mwenyewe ya wasimuliaji katika Kitabu chake “Hilyatu’l-Auliya” kama ifuatavyo: “Wakati aya ifuatayo ya Qur’ani Tukufu ilipoteremshwa:

{انﱠ اﻟﱠﺬِﻳﻦ آﻣﻨُﻮا وﻋﻤﻠُﻮا اﻟﺼﺎﻟﺤﺎتِ اوﻟَٰﺌﻚَ ﻫﻢ ﺧَﻴﺮ اﻟْﺒﺮِﻳﺔ {7

ﺟﺰاوﻫﻢ ﻋﻨْﺪَ رﺑِﻬِﻢ ﺟﻨﱠﺎت ﻋﺪْنٍ ﺗَﺠﺮِي ﻣﻦ ﺗَﺤﺘﻬﺎ اﻧْﻬﺎر ﺧَﺎﻟﺪِﻳﻦ ﻓﻴﻬﺎ اﺑﺪًا ۖ رﺿ اﻟﻪ ﻋﻨْﻬﻢ ورﺿﻮا ﻋﻨْﻪ ۚ ذَٰﻟﻚَ ﻟﻤﻦ {ﺧَﺸ رﺑﻪ {8

‘(Na kwa) wale ambao wanaamini na kufanya mema, hakika hao ndio wabora wa viumbe. Malipo yao kwa Mola wao ni bustani zipitazo mito chini yake, watakaa humo milele. Allah yuko radhi nao na wao wako radhi Naye, na hayo ni kwa yule amchae Mola.’” (98: 7– 8)

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akizungumza na Ali, alisema: “Ewe Ali, wabora wa viumbe (khairi’l-Bariyya) katika Aya hii tukufu inakuashiria wewe na wafuasi (Shi’a) wako. Katika siku ya ufufuo, wewe na wafuasi (Shi’a) wako mtapita daraja ambayo kwamba Allah atakuwa radhi nanyi na ninyi mtakuwa radhi Naye.”

Sifa Zaidi Za Shi’a

Halikadhalika, Abu’l-Muwayyid Muwafiq Bin Ahmad Khawarizmi katika sura ya 17 ya Manaqib yake; Hakim Abu’l-Qasim Abdullah Bin Abdullahi’l-Haskani, katika Shawahidu’t-Tanzil; Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib, uk. 119, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira, uk. 31, Munzir Bin Muhammad Bin Munzir, na hususan Hakim, wamesimulia kwamba Hakim Abu Abdullah Hafidh (mmoja wa maulamaa wenu wakubwa) alisema, akitegemea juu ya ushahidi wa wasimuliaji kurudi nyuma hadi kufikia kwa Yazid Bin Sharafi’l-Ansari, mwandishi wa Amiru’l-Mu’minin Ali Bin Abi Talib kwamba Ali alisema kwamba wakati wa kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Mtume aliegema kwenye kifua cha Ali na akasema: “umeisikia ile aya tukufu: ‘Wale ambao wameamini na wakafanya matendo mema, hao ndio bora wa viumbe.’ (98:7) Hawa ni Shi’a wako. Sehemu yangu ya kukutania na wewe itakuwa ni kwenye Chemchemu ya Kauthar (katika Pepo). Wakati viumbe wote watakapokusanyika kwa ajili ya hesabu, uso wako utang’ara, na utatambulishwa siku hiyo kama kiongozi wa watu wenye nyuso angavu.”

Jalalud-Din Suyuti katika Durru’l-Mansur anamnukuu Abu’l-Qasim Ali Bin Hasan (anayejulikana zaidi kama Ibn Asakir Damishqi) ambaye anamnukuu Jabir Bin Abdullah Ansari, mmoja wa masahaba wakubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akisema kwamba yeye na watu wengine walikuwa wamekaa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati Ali Bin Abi Talib alipoingia ndani. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Naapa kwa Yule ambaye anamiliki uhai wangu kwamba mtu huyu (Ali) na wafuasi wake watapata wokovu katika Siku ya Ufufuo.” Wakati huo huo aya hiyo hapo juu ilishushwa.

Katika sharhe hiyo hiyo, Ibn Adi anamnukuu Ibn Abbas akisema kwamba wakati aya hiyo hapo juu iliposhuka, Mtume akasema kumuambia Amiru’l-Mu’minin, Ali: “Wewe na waafuasi wako mtakuja Siku ya Ufufuo katika hali ambayo kwamba wote mtaridhia juu ya Allah, na Allah ataridhika nanyi.”

Katika Manaqib ya Khawrizmi, ifuatayo ilisimuliwa kutoka kwa Jabir Bin Abdullah Ansari: “Nilikuwa kwenye hadhara ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati Ali alipoungana nasi, na wakati ule Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Huyu ambaye amekujieni ni ndugu yangu.’ Kisha, akaelekea Ka’ba, Mtume akachukua mkono wa Ali na akasema: “Naapa kwa Yule ambaye anamiliki uhai wangu, huyu Ali na wafuasi wake watakuwa wamepata wokovu katika Siku ya Hukumu.’

Kisha akasema: ‘Ali ndiye wa mbele zaidi yenu wote katika imani, mwenye kuzingatia mno kuhusu dhamana za Allah, mwadilifu kupita wote katika kuamua mambo ya watu, na mwadilifu kupita wote katika kugawa masurufu miongoni mwa watu, na aliye juu zaidi ya wote kwa cheo mbele ya Allah.’” Katika wakati huo aya hiyo hapo juu ilishushwa.

Katika Sura ya 11 ya Kitabu chake “Sawa’iq” Ibn Hajar anamnukuu Hafidh Jamalu’d-Din Muhammad Bin Yusuf Zarandi Madani (Mwanachuo mkubwa wa madhehebu yenu) akisema kwamba: Wakati Aya hiyo hapo juu ilipoteremshwa, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ewe Ali, Wewe na Shi’a wako ndio wabora wa viumbe walioumbwa.

Wewe na Mashi’a wako mtakuja Siku ya Hukumu katika hali ambayo nyote mkiwa mmeridhia kwa Allah, na Allah atakuwa radhi nanyi. Maadui zako watakuwa wamechukizwa mno, na mikono yao itakuwa imefugwa kuzunguuka shingo zao.” Kisha Ali akauliza, ni nani maadui zangu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu, “Yule ambaye ana uadui kwako na ambaye anakutukana.”

Allama Samhudi, katika Jawahiru’l-Iqdain, kwa idhini ya Hafidh Jamalu’d-Din Zarandi Madani na Nuru’d-Din Ali bin Muhammad bin Ahmad Maliki Makki, ajulikanaye kama Ibn Sabbagh, ambaye anaheshimiwa kama mmoja wa Wanachuo wenu Mashuhuri na mnadharia mkubwa wa mambo ya dini, katika kitabu chake “Fusulu’l-Muhimma” anasimulia kutoka kwa Abdullah bin Abbas, kwamba wakati Aya hii iliyo kwenye mjadala ilipoteremshwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumuambia Ali; “Ni wewe na Mashi’a wako. Wewe na wao mtakuja Siku ya Hukumu mkiwa mmefurahi mno na mmeridhia, ambapo maadui zako watakuja na huzuni kubwa na mikono iliyofungwa.”

Mir Seyyed Ali Hamadani Shafi’i, mmoja wa wanachuo wenu mashuhuri katika kitabu chake “Mawaddatul’l-Qurba” na mwanachuo anayejulikana vizuri sana kwa upinzani wake juu ya Shia, Ibn Hajar katika kitabu chake “Sawa’iq-e-Muhriqa”, anasimulia kutoka Ummu’l-Mu’minina Umm Salma, mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwamba Mtume alisema:

“Ewe Ali, wewe na Mashia wako mtaishi Peponi; wewe na Mashia wako mtaishi katika Pepo.” Mwanachuo anayejulikana sana wa Khawarizm, Muwaffaq bin Ahmad, kati- ka kitabu chake “Manaqib” Sura ya 19, anasimulia kutoka rejea zinazoaminika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumuambia Ali: “Katika umma wangu wewe ni kama Masihi Isa Mwana wa Mariamu.”

Taarifa hii inaonyesha kwamba, kama vile wafuasi wa Mtume Isa (A.S.) walivyogawanyi- ka katika makundi: Waumini wa kweli wajulikanao kama Hawari’in, Mayahudi, na wapi- ga chuku (wenye kutia maneno chumvi) ambao wanamshirikisha yeye na Allah; katika njia hiyo hiyo Waislamu watakuja kugawanyika katika makundi matatu. Mojawapo litakuwa Shi’a, waumini wa kweli. Kundi lingine litakuwa la maadui wa Ali, na kundi la tatu litakuwa la wenye kukuza cheo chake.

Sifa Za Shia Zathibitishwa Kutoka Kwenye Vitabu Vya Sunni.

Kufikia hapa watu walitawanyika katika kuitikia mwito wa Swala ya Isha. Baada ya Swala Mulla Abdu’l- Hayy alirudi na Sherhe ya Suyuti, Mawaddatu’l-Qurba, Musnad ya Imam Ahmad bin Hanbal, na Manaqib ya Khawarizmi. Alisoma kutoka kwenye vitabu hivyo hadith alizokuwa amezinukuu Muombezi katika mijadala yake kwa njia ya uthibitisho. Kwa vile rejea zangu zilikuwa sawa sawa, muonekano wa nyuso za wale wote ambao wako katika kambi ya upinzani ulibadilika. Wakati huo huo walikuta hadith nyingine katika Mawaddatu’l-Qurba.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema, “Ewe Ali, Siku ya Hukumu wewe na Mashi’a wako mtakuja mbele za Allah mkiwa mmefurahi mno na kuridhia, ambapo adui yako atakuja na huzuni kubwa na mikono ikiwa imefungwa.” Muombezi: Hizi ni hoja zilizo wazi zinazoungwa mkono na Kitabu cha Allah, na hadith sahihi, na Ta’arikh. Kuungwa mkono kwa upande wangu kunakuja kutoka kwenye vitabu vya wanachuo wenu mashuhuri. Haya ni kwa nyongeza juu ya simulizi nyingi ambazo zimo katika vitabu na Sherhe za Shi’a. Kwa kutumia vitabu hivivilivyoko mbele yenu sasa, ninaweza kuendelea kuwasilisha hoja ziungazo mkono nukta iliyo kwenye mjadala mpaka kesho asubuhi, kwa rehema za Allah; lakini nafikiri kwamba hoja nilizowasilisha zipaswe kuwa zinatosha kuondoa mashaka yenu kuhusu Mashi’a. Watukufu mliohudhuria, sisi Mashia sio Mayahudi. Sisi ni wafuasi wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.).

Mwanzilishi wa neno Shi’a kwa maana ya “Wafuasi wa Ali” hakuwa mlaaniwa huyu Abdullah bin Saba, bali ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Kamwe hatumfuati mtu binafsi bila rejea zenye hoja za kumuunga mkono. Mmesema kwamba ilikuwa ni baada ya Uthman ndio neno “Shi’a” lilipoanza kutumika kuashiria wafuasi wa Ali. Kwa kweli, hata wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Masahaba kadhaa maarufu wenye kutajika walikuwa wakiitwa Mashi’a.

Hafidh Abu Hatim Razi katika kitabu chake “Az-Zainat” ambacho amekiandika kwa ajili ya kufafanua maana ya maneno fulani na Semi zinazotumika miongoni mwa Wanachuo, anasema kwamba neno la kwanza jipya ambalo lilikuja kukubaliwa na wote katika Uislamu wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lilikuwa ni “Shia.” Neno hili lilitumika kwa masahaba maarufu wanne: Abu Dharr Ghifar, Salman Farsi, Mikdadi bin Aswad Kindi, na Ammar Yasir. Hadith nyingi zaidi zilinukuliwa katika kuunga mkono nukta hii hii.

Sasa ni juu yenu kufikiria vipi iliwezekana kwamba wakati wa Mtume (s.a.w.w.) Wanne kati ya masahaba wake wakubwa waliitwa Shi’a. Kama Mtume (s.a.w.w.) alifikiria kuwa neno hilo ni la uzushi (bida’a), kwanini hakuwakataza watu kulitumia? Ukweli ni kwamba watu walisikia kutoka kwa Mtume (s.a.w.w) mwenyewe kwamba wafuasi (Mashi’a) wa Ali walikuwa ni wakazi wa Peponi. Walikuwa na fahari nalo na kwa uwazi wakajiita wenyewe Mashi’a.

Cheo Cha Salman, Abu Dharr, Mikdadi Na Ammar

Umesimulia Hadith kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) isemayo: “Hakika masahaba wangu ni kama nyota; yeyote katika wao mtakayemfuata, mtakuwa mmeongozwa sawa-sawa.

Abu’l-Fida anaandika katika kitabu chake cha Tarikh kwamba watu hawa wanne, ambao walikuwa masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walijitenga, pamoja na Ali kula kiapo cha utii kwa Abu Bakar, siku ile ya Saqifa. Kwa nini hamchukulii kukataa kwao kula kiapo kuwa kunafaa kuigwa?

Maulamaa wenu wenyewe wameandika kwamba walipendwa na Allah na Mtume Wake. Sisi tunawafuata kama walivyomfuata Ali.

Kwa hiyo kutokana na hadith yenu wenyewe, sisi tuko katika njia ya Mwongozo. Kwa ruksa yenu, na kutilia maanani uchache wa muda, ninawasilisha kwenu simulizi chache katika kuunga mkono hoja yangu kwamba watu hawa wanne walipendwa na Allah na Mtume (s.a.w.w.).

Abu Nu’aim Isfahami katika “Hilyatu’l-Auliya”, Juz. 1, uk. 172 na Ibn Hajar Makki katika hadith ya tano ya hadith arobaini zilizosimuliwa katika “Sawa’iqul- Muhriqa” kwa kumtukuza Ali, iliyosimuliwa kutoka kwa Tirmidhi, na Hakim kutoka kwa Buraida, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) alisema: “Hakika, Allah ameniamuru mimi kuwapenda watu wanne na amenijulisha kwamba Yeye mwenyewe anawapenda.”

Wakati watu walipomuuliza ni kina nani watu hao wanne, alisema: “AIi ibn Abu Talib, Abu Dharr, Mikdadi na Salman.” Tena, Ibn Hajar katika Hadithi ya 39 amesimulia kutoka kwa Tirmidhi na Hakim kutoka kwa Anas bin Malik kwamba Mtume amesema: “Pepo inashauku juu ya watu watatu, Ali, Ammar, na Salman.” Je, vitendo vya Sahaba hawa Mashuhuri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) sio vya mfano wa kuigwa na Waislamu wengine? Je, sio aibu kwamba kwa maoni yenu Sahaba wamewekewa mpaka kwa wale tu waliocheza mchezo wa Saqifa, au ambao wameukubali mpango wake bila kupinga, ambapo wengine ambao wamepinga hila za Saqifa wanaonekana kama wasiokuwa waaminifu? Na ikiwa ni hivyo, basi hadith uliyoinukuu ingekuwa na maneno haya: “Hakika wachache kati ya Sahaba wangu ni kama nyota .”

Sababu Za Wa-Irani Kuupokea Ushi’a.

Umekuwa sio mwema katika kusema kwamba, “Ushia ni Dini ya kisiasa, na kwamba Mazoroasta wa Iran wameukubali kwa ajili ya kujiokoa kutoka umiliki wa Waarabu, umesema hivyo katika upofu wa kufuata watangulizi wako. Nimekwishathibitisha kwamba ni dini ya Uislamu, dini ambayo Mtume (s.a.w.w.) ameiweka amana mikononi mwa wafuasi wake. Kwa kweli, wale ambao bila kibali chochote kutoka kwa Mtume (s.a.w.w.), wakaweka msingi wa Saqifa, walikuwa ndio wenyewe wanasiasa na sio wafuasi wa famil- ia Tukufu ya Mtume (s.a.w.w.).

Ni tabia ya Wa-Iran kwamba wao hutazama mambo kwa kuyachunguza. Wakati watakaposadikishwa na ukweli wake, wanayakubali, kama ambavyo waliukubali Uislamu wakati Iran iliposhindwa na Waarabu. Hawakulazimishwa kufanya hivyo. Waliuacha Uzoroasti na kwa uaminifu kabisa wakaushika Uislamu.

Halikadhalika, wakati waliporidhishwa na mantiq na huduma za Ali zenye thamani isiokadirika, wakaukubali Ushi’a. Kinyume na maelezo ya waandishi wenu wengi,Wairani hawakumkubali Ali wakati wa Ukhalifa wa Harun-r-Rashid au Maamunu’r-Rashid. Walimkubali Ali wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Salman Farsi alikuwa mmoja wa wafuasi waaminifu kabisa wa Ali.

Alifikia kiwango cha juu cha Imani. Maulamaa wa Madhehebu zote kwa makubaliano ya pamoja wameandika kwamba Mtume amesema: “Salman anatokana na Ahlul Bait wetu (yaani ni mmoja wa watu wa Nyumba yangu).” Kwa sababu hii aliitwa “Salman Muhammad” na yeye inakubalika kabisa kuwa ni mfuasi thabiti mwenye kumuunga Ali, na mpinzani mkali wa Saqifa.

Kama, kutegemeana na vitabu vyenu wenyewe, sisi tukimfuata yeye, basi tuko katika njia iliyonyooka. Alizisikia aya za Qur’ani na maneno ya Mtume (s.a.w.w.) kuhusu Ali na kiwazi kabisa akaelewa kwamba utii kwa Ali ulikuwa ni utii kwa Mtume (s.a.w.w.) na kwa Allah (Swt). Alimsikia mara kwa mara Mtume akisema: “Mwenye kumtii Ali ananitii mimi; na mwenye kunitii mimi anamtii Allah (Swt); ambaye ana uadui kwa Ali ni adui kwangu; na ambaye ana uadui kwangu ni adui kwa Allah (Swt).

Kila Mu-Iran, hata hivyo, ambaye alikwenda Madina na kusilimu, iwe wakati wa Mtume au baadae, alizitii amri za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa sababu hii Khalifa wa pili akashindwa kuvumilia na akaweka vikwazo vingi juu ya Wairan. Shida hizi na taabu zilizaa uadui ndani ya nyoyo zao. Walihoji ni kwanini Khalifa awanyime haki za Uislamu kinyume na amri zilizowekwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Shukurani Za Wa-Iran Juu Ya Huruma Za Ali.

Mbali na hali hizi, Wa-Irani walikuwa na shukurani sana kwa Ali kwa huruma zake kuhu- siana na matendo waliyofanyiwa mabinti wa kifalme waliotekwa na Waarabu. Wakati wafungwa wa Mada’in (Taisfun) walipoletwa mjini Madina, Khalifa wa pili aliamuru kwamba wafungwa wote wa kike wafanywe kuwa watumwa wa Waislamu. Ali alilikataza hili na akasema kwamba mabinti wote wa kifalme ni wafungwa wa kipekee na wanapaswa wapewe heshima.

Wawili kati ya wale wafungwa walikuwa ni mabinti wa mfalme Yazdigerd wa Iran na hawakuweza kufanywa watumwa. Khalifa akauliza ni nini kifanywe. Ali akasema kwamba kila mmoja yapasa aruhusiwe kuchagua mume miongoni mwa Waislamu. Kwa ajili hiyo, Shahzanan alimchagua Muhammad ibn Abu Bakar (ambaye alilelewa na Ali), ambapo yule binti mfalme mwingine, Shahbanu alimchagua Imam Husain, mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wote walikwenda kwenye nyumba za watu hawa baada kufungishwa ndoa kisheria. Shahzanan alizaa mtoto wa kiume, Qasim Faqih, baba wa Ummi Farwa, ambaye alikuwa mama wa Imam wetu wa Sita, Ja’afar as- Sadiq. Imam Zainu’l-Abidin, Imam wetu wa nne alizaliwa na Shahbanu.

Hivyo mwanzo wa Ushia haukuwa na uhusiano wowote na wakati wa Harun na Ma’amun au na Utawala wa Ufalme wa Safavid katika Iran, kama ulivyosema mapema. Ulitangazwa wazi karne saba kabla ya Ufalme wa Safavid (yaani karne ya 4 A.H) wakati wa-Dailami (wa-Buwayyid) walipokuwa watawala. Katika mwaka wa 694 A.H. Falme ya Iran ilikuwa ikitawaliwa na Ghazan Khan Mughal (ambaye jina lake la Kiislamu lilikuwa Mahmud). Tokea wakati huo, Imani juu ya Ahlul Bait wa Mtume (s.aw.w.) ilidhihirisha kama jambo la kawaida, Ushia ulikua kwa uimara kabisa. Baada ya kifo cha Ghazan Khan Muqhal mnamo mwaka wa 707 A.H., ndugu yake, Muhammad Shah Khuda Bandeh akawa mtawala wa Iran. Aliandaa mjadala wa kidini (Mdahalo) kati ya Alama Hilli, Mwanachuo msomi wa Kishia, na Khwaja Nidhamu’d-Din Abdul’l-Maliki Maraghe’i, Kadhi Mkuu wa (Madhehebu) Shafii na Mwanachuo mkubwa wa Kisunni wa wakati huo.

Midahalo Kati Ya Allama Hilli Na Kadhi Mkuu Kuhusu Uimamu.

Nukta ya mdahalo huu ilikuwa ni Uimamu. Allama Hilli alitoa hoja zenye nguvu sana kuthibitisha kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi alitemfuatia mara moja Mtume (s.a.w.w.) bila mwanya, na kwa kuridhisha kabisa akabainisha uwongo wa madai ya ule upande mwingine, kiasi kwamba wale wote waliohudhuria walitosheka kabisa na jinsi ya ukweli wa Allama. Khwaja Nidhamu’d-Din alikubali kwamba hoja za Allama haziwezi kukanushwa. Lakini akasema kwamba, kwa vile alikuwa akifuata njia za wakubwa wake waliomtangulia, haikuwa vizuri kuiacha. Aliona kwamba ilikuwa ni muhimu kudumisha mshika- mano miongoni mwa Waislamu. Mfalme Wa Irani Aliikubali Iman Ya Kishi’a.

Mfalme alisikiliza hoja hizo kwa usikivu makini, mwenyewe akaukubali msimamo wa Shi’a, na akatangaza uhalali wa Ushia katika Iran. Hatimaye alitangaza kwa nagavana wa mikoa kwamba Khutuba za kila juma (zinazotolewa misikitini) zinapaswa zitangaze haki ya Ali kama mrithi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Vile vile aliamuru kwamba Kalimah iandikwe kwenye dinari (Sarafu za dhahabu) katika njia hii: “La ilaha illa llah Muhammad Rasulullah, Aliyan Waliyyullah,” maana yake, “Hakuna Mungu ila Allah; Muhammad ni Mtume wa Allah na Ali ni Walii wa Allah.” (makamu au mlezi wa watu aliyeteuliwa kiungu). Katika njia hii mizizi ya Ushi’a ilisimama kwa umadhubuti kabisa.

Karne saba baadae, wakati wafalme wa Ki-Safavid walipoingia madarakani, utando wa ujinga na ushabiki usio na maana katika dini viliendelea kuondolewa, Ushi’a ukashamiri kila mahali katika nchi ya Iran. Ndio, wako Mazoroasti katika Iran na wale wanaotia chimvi cheo cha Ali na kumfikiria yeye kuwa ni Mungu. Lakini haipasi kuwahusisha na watu wa kawaida wa Iran, ambao wana imani katika Allah na Mtume Muhammad kama Mtume wa mwisho. Hawa wanamfuata Ali na watoto wake kumi na moja kama ilivyoamrishwa na Mtume (s.a.w.w.).

Hafidh: Ni kitu cha kushangaza kwamba ingawa kiasili umetokea Hijaz (Arabia) na umeishi Iran kwa muda mfupi, bado unawaunga mkono Wairani, na kuwaita wafuasi wa Ali, ambaye yeye mwenyewe alikuwa mtiifu kwa Allah. Lakini Mashia wa Iran wanamchukulia Ali kama ni Mungu.

Hapa kuna baadhi ya beti kutoka kwa washairi wa Kiiran wakiashiria hoja hii, ambapo Ali mwenyewe alilaani imani kama hizi. Mwisho wa beti hizi unaonyesha Ali akisema: “Nani anasaidia wakati wa matatizo! Ni mimi ambaye ni Mungu! Ni mimi.” Ubeti wa mshairi mwengine unasema: “Kulingana na iman ya wale ambao wana akili na wanamtambua Mungu, Mungu ni Ali na Ali ni Mungu.”

Muombezi: Nashangaa kwanini, bila kufanya uchunguzi, uweze kuwatuhumu Wairani wote kuwa wanamchukulia Ali kama Mungu. Wanachuo wenu wenyewe wamefanya madai ya kishabiki kama haya. Wamesema kwamba Mashi’a wanamwabudu Ali na kwa ajili hiyo wao ni Makafiri. Kwa hiyo kuwaua wao ni wajib. Matokeo yake Waislamu wa na Turkistan kwa ukatili mkubwa wakamwaga damu za Waislamu wa Iran.

Watu wa kawaida miongoni mwa Masunni mara kwa mara wanapotoshwa na baadhi ya Ulamaa wenu, na watu wenu wanawachukulia Wairani kuwa ni Makafiri. Katika wakati uliopita, watu wenu Wa-Turkomania wameshambulia msafara wa Wairani karibu na Khorasan, wakawanyang’anya na kuwaua watu, na kusema kwamba, yeyote atakayeua marafidh saba (yaani Shi’a) atakuwa na uhakika wa kwenda peponi.

Yakupasa uweke akilini kwamba lawama za kuhusika na mauaji haya zinakuwa moja kwa moja juu ya viongozi wenu, ambao huwaambia Masunni wasio na elimu kwamba Mashi’a wanamuabudu Ali.

Uislamu Unakataza Kujigamba Kuhusu Nasaba.

Nikirejea kwenye nukta yako ya kwanza kwamba, kwa kuwa mwanzoni nilihusiana na Arabia, Makka ma Madina, kwanini niwaunge mkono Wairani. Nakuambia kwamba mimi sina tabia ya ushabiki wa kitaifa.

Mtume wetu (s.a.w.w.) amesema: “Waarabu wasijigambe kwamba wao ni bora kwa wasio Waarabu na kinyume chake; na weupe wasijigambe kwa ubora kwa weusi na kinyume chake. Ubora uko tu katika elimu na uchaji. Katika Qur’ani Tukufu Allah (swt) anasema:

ﻳﺎ اﻳﻬﺎ اﻟﻨﱠﺎس اﻧﱠﺎ ﺧَﻠَﻘْﻨَﺎﻛﻢ ﻣﻦ ذَﻛﺮٍ واﻧْﺜَ وﺟﻌﻠْﻨَﺎﻛﻢ ﺷُﻌﻮﺑﺎ وﻗَﺒﺎﺋﻞ ﻟﺘَﻌﺎرﻓُﻮا ۚ انﱠ اﻛﺮﻣﻢ ﻋﻨْﺪَ اﻟﻪ اﺗْﻘَﺎﻛﻢ ۚ انﱠ اﻟﻪ {ﻋﻠﻴﻢ ﺧَﺒِﻴﺮ {13

“Enyi watu! Hakika tumekuumbeni ninyi mume na mke; na tumekufanyeni mataifa na makabila ili kwamba mpate kujuana; hakika aliye mbora sana miongoni mwenu mbele ya Allah ni yule amchae Allah zaidi…” (49:13).

Vile vile katika Sura hiyo hiyo ndani ya Qur’ani Anasema:

{اﻧﱠﻤﺎ اﻟْﻤﻮﻣﻨُﻮنَ اﺧْﻮةٌ ﻓَﺎﺻﻠﺤﻮا ﺑﻴﻦ اﺧَﻮﻳﻢ ۚ واﺗﱠﻘُﻮا اﻟﻪ ﻟَﻌﻠﱠﻢ ﺗُﺮﺣﻤﻮنَ {10

“Kwa hakika Waumini wote ni ndugu, basi patanisheni baina ya ndugu zenu na mcheni Allah ili mrehemiwe.” (49:10).

Kwa hiyo, watu wote, Waasia, Waafrika, Wazungu, Waamerika weupe, weusi, wekundu au manjano, makabila yote ambayo ni Waislamu ni ndugu, na hakuna hata mmoja anayeweza kudai ubora juu ya mwingine. Kiongozi mkubwa wa Waislamu, Mwisho wa Mitume, alitenda juu ya msingi huu. Alionyesha mapenzi yake makhususi kwa Salman Farsi wa Iran, Suhaib wa Asia ndogo, na Bilal wa Abysinia (Uhabeshi – Ethiopia ya sasa).

Na kwa upande mwingine alimpuuza Abu Lahab (ambaye jina lake lina maana ya Baba wa Miali ya Moto), ami yake mwenyewe ambaye amelaaniwa katika Sura ya Qur’ani Tukufu ambayo inasema:

{ﺗَﺒﺖ ﻳﺪَا اﺑِ ﻟَﻬﺐٍ وﺗَﺐ {1

“Imeangamia mikono miwili ya Abu Lahab! Naye amekwisha angamia…” (111:1). Uislamu Vile Vile Unakataza Ubaguzi (Wa Aina Zote).

Ulimwengu umeshuhudia matatizo ya taratibu mbaya mno katika nchi za Maghribi ambayo yalikuwa ni matokeo ya ubaguzi wa rangi. Katika nchi hizo weusi hawaruhusiwi kwenye mahoteli, migahawa, makanisa, na sehemu nyingine za mikusanyiko iliyokusudiwa kwa weupe tu. Uislamu ulipiga marufuku taratibu hizo za kikatili miaka 1300 iliyopita na kutangaza kwamba Waislamu, bila kujali kabila, rangi, au utaifa wote ni ndugu. Hivyo Waarabu wakienda kombo, nitawalaumu, na nitakuwa rafiki wa Mashi’a wa Iran.

Pili, umewahusisha Mashabiki (wakereketwa) wa Kiiran (Maghullat) na Mashi’a ambao ni Madhubuti, wenye kuabudu Mungu Mmoja (yaani Allah) na kumfuata Ali kutokana na Maamrisho ya Mtume (s.a.w.w.) Tunamchukulia Ali kama mja mcha Mungu wa Allah na aliyechaguliwa na Allah kuwa mrithi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Lawama Kwa Mashabiki Washupavu (Maghullat).

Aidha, tunawapuuza wale ambao iman zao ni kinyume na sisi, kama Saba’iyya, Khitabiyya, Gharabiyya, Allawiyya, Mukhammasa, Bazighiyya, Nussairiyya, ambao wametawanyika nchini Irani kote, Mosul, na Syria. Sisi Mashi’a tuko tofauti nao na tunawaona wao kuwa ni Makafir.

Katika vitabu vyote vilivyoandikwa na Maulamaa wa Kishi’a na Wanachuo wa Shari’ah, Maghulamu wamechanganywa pamoja miongoni mwa Makafir, kwa vile imani yao ni kinyume na misingi ya Ushi’a. Kwa mfano, wanahoji kwamba, kwa vile kuingia kwa roho katika umbo la mwili inawezekana (kama Jibril alivyoweza kujitokeza mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika umbo la Dahiyya-e-Kalbi), ilikuwa ni Mapenzi ya Allah kwamba Nafsi yake tukufu ionekane katika umbo la mwanadamu, katika mwili wa Ali.

Kwa sababu hii wanakiona cheo cha Ali kuwa ni kikubwa kuliko cha Mtume. Jambo kama hilo lilijitokeza wakati wa Ali mwenyewe. Baadhi ya watu kutoka India na Sudan walikuja kwake na kutamka kwamba yeye alikuwa Mungu. Mara kwa mara Ali aliwakataza kushikilia itiqadi hii, lakini hakuna athari iliyotokea (hawakuacha).

Hatimaye, kama ilivyoandikwa katika vitabu vingi vya Tarekh, Ali aliamrisha wauwawe ndani ya visima vya moshi. Maelezo ya habari hii yameandikwa katika Baharu’l-Anwar, Juz. 7, na mwanachuoni mkubwa, Agha Muhammad Baqir Majlis. Amir’l-Mu’miniina na Maimam wengine waliwalaumu vikali sana watu kama hawa. Ali alisema: “Ee Allah ninakibeza kikundi cha Ghulat, kama vile Isa alivyowabeza Wakristo.

Ikiwezekana uwatelekeze hao daima.” Katika wakati mwengine alisema: “Kuna makundi mawili ambayo yatapatwa na vifo vya kufedhehesha, na mimi siwajibiki nao (kwa vile ninavidharau vitendo vyao): Hao ni wale wanaozidisha mipaka halali ya mapenzi kwangu, na hao ni Ghullat, na wale ambao bila sababu yoyote ile, wana uadui juu yangu. Nawachukia wale ambao wanatukuza cheo changu kupita mipaka yake halisi.”

Vilevile alisema: “Kuna makundi mawili yaliyojihusisha na mimi yatapata shida ya kifo cha aibu: Moja ni lile lililo na watu ambao wanasema ni marafiki na kunitukuza kupita mipaka ya halali; jingine lina maadui ambao wanatweza hadhi yangu.”

Mashi’a wanawalaumu wale ambao wanamtukuza Ali na Ahlul Bait wake kupita mipaka iliyoamriwa na Allah na Mtume (s.a.w.w.). Maulamaa wetu kwa pamoja wamewachukulia wote hao kwamba ni Makafir. Hairuhusiwi kuhudhuria mazishi yao au koleana nao. Vilevile wananyimwa kurithi mali ya Waislamu; sadaka na kodi za kidini haziwezi kupewa wao. Qur’ani Tukufu inawalaumu katika maneno haya:

“Sema: Enyi watu wa Kitabu msipite kiasi katika dini yenu bila ya haki. Walamsifuate matamanio ya watu waliokwisha potea toka zamani, na wakapoteza wengi, na wenyewe wakapotea njia iliyo- sawa.” (al-Maidah; 5:77).

Allama Majlisi katika Kitabu chake “Baharu’l-Anwar” Juz. 3 ambacho ni ensaklopidia (kitabu cha maarifa yote) ya itiqad ya Shi’a, ameandika hadith nyingi kuwalaumu Ghullat. Imam Ja’far Sadiq (a.s.) ananukuliwa akisema, “Sisi ni waja wa Allah, ambaye ametuumba na akatufanya sisi kuwa bora kwa viumbe wake wengine. Hakika sisi tutakufa na tutasimama mbele ya Allah kwa ajili ya hesabu. Yule ambaye ni rafiki ya Ghullat ni adui yetu; na yule ambaye ni adui yao huyo ni rafiki yetu. Maghullat ni makafir na Washirikina; laana naiwe juu yao.”

Kiongozi mkubwa wa dini wa Mashia vilevile amemnukuu Imam huyu huyu akisema: “Laana ya Allah iwe juu ya wale ambao wanadai Utukufu na Umungu kwa Ali. Kwa jina la Allah, Ali alikuwa ni mja mtiifu wa Allah. Laana iwe juu ya wale waliotukashifu sisi; baadhi ya watu wanasema mambo kuhusu sisi ambavyo sisi wenyewe hatuyasemi. Tunasema wazi kwamba hatuna uhusiano nao.”

Sheikh Saduq (Abu Ja’far Muhammad bin Ali) Faqih mwenye kuheshimiwa sana (Mwanachuo Shari’ah) wa Mashia, anamnukuu Zarara bin A’yun, mwandishi wakuamini- ka wa Kishia, ambaye alikuwa Hafidh na Sahaba wa Imam Muhammad Baqir na Imam Ja’far Sadiq, akisema: “Nilimueleza Imam Ja’far Sadiq kwamba mmoja kati ya watu anayejulikana kwake, huamini katika Tufiidh (uwakilishi wa mamlaka ya Mungu). Imam akasema: ‘Ina maanishwa nini kwa Tufwidh?,’ Nikajibu. ‘Yule mtu anasema kwamba, Allah alimuumba Muhammad na Ali na kisha akakabidhi Mamlaka yake kwao juu ya mambo ya watu. Hivyo wao ndio waumbaji, watoaji wa chakula, wao wahuishaji na wao ndio wenye kufisha.’

Mtukufu Imam akasema: “Adui huyo wa Allah, anaongopa. Wakati utakaporudi kwake, msomee Aya hii kutoka katika Qur’ani Tukufu “…… au wamemfanyia Allah washirika ambao wameumba kama alivyoumba Yeye, kwa hiyo alivyoviumba vikawababaisha (akili)? Sema Allah ndiye Muumbaji wa kila kitu na ni mmoja tu, Mwenye Enzi Kuu.” (13:16). Mashi’a Wako Tofauti Na Ghullat.

Sisi Shi’a ni tofautli na Ghullat. Waache wadai kwamba wao ni Mashi’a, Mwenyezi Mungu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali, na kizazi chao wanawachukia.

Ali alimuweka mkubwa na Ghullat jela kwa muda wa siku tatu, na akamuamuru atubie kwa uovu wake.

Alipokataa Ali alimfanya achomwe mpaka akafa. Kama huwezi kutoa angalau kitabu kimoja ambacho ndani yake Ghullat wametukuzwa, basi angalau uwalaumu Maulamaa wasio wavumilivu ambao wanawapotosha Masunni kuhusu Mashi’a.

Ufafanuzi Kuhusu Heshima Kwa Maimam.

Hafidh: Ushauri wako wa Kindugu unafaa kufikiriwa. Lakini tafadhali, je unaweza kufafanua nukta nyingine zaidi? Umesema muda wote kwamba hamuwatukuzi Maimam wenu kupita kiasi. Mnawaona Ghullat kama watu duni (wasiostahili heshima) na wanaofaa kwenda jahannamu, lakini unatumia maneno yasiyostahili kwa mintarafu ya Maimam wenu.

Umesema “Rehema za Allah ziwe juu yao”, ingawa unajua kwamba, kwa mujibu wa Qur’ani, neno hili limetengwa kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tu. Qur’ani inasema:

{انﱠ اﻟﻪ وﻣَﺋﺘَﻪ ﻳﺼﻠﱡﻮنَ ﻋﻠَ اﻟﻨﱠﺒِ ۚ ﻳﺎ اﻳﻬﺎ اﻟﱠﺬِﻳﻦ آﻣﻨُﻮا ﺻﻠﱡﻮا ﻋﻠَﻴﻪ {56

“Hakika Allah na Malaika wake wanamtakia Rehema Mtume. Enyi ambao mmeamini mtakieni rehema juu yake na Msalimuni kwa (uzuri) wa Salamu.” (33:56).

Mwendo wako huo unakiuka kiwazi kabisa hukumu ya Qur’ani. Neno lako hilo ni Uzushi (bida’a).

Muombezi: Aya hii haitukatazi kumuombea rehema mtu wengine yoyote. Tunaamrishwa kumuombea Rehema Mtume. Katika Aya nyingine ya Qur’ani Tukufu, Allah anasema. “Amani na iwe juu ya watu wa Ya Sin (Ahl Ya Sin),” yenye maana ya kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Ama kwa Mitume wengine wa Allah, kuombea rehema hakukutolewa pamoja na vizazi vyao popote katika Qur’ani. Kuombea rehema kumetolewa tu kwa Mitume wa Allah.

{ﺳَم ﻋﻠَ ﻧُﻮح ﻓ اﻟْﻌﺎﻟَﻤﻴﻦ {79

“Amani na Salaam kwa Nuh miongoni mwa Mataifa.” (37: 79).

{ﺳَم ﻋﻠَ اﺑﺮاﻫﻴﻢ {109 “Amani na Salaam kwa Ibrahim.” (37:109)

{ﺳَم ﻋﻠَ ﻣﻮﺳ وﻫﺎرونَ {120

Amani na Salaam kwa Musa na Haruni.”(37:120).

Watu Wa Ya Sin Inawahusu Watu Wa Muhammad

Wafasiri wote na Wanachuo wa madhehebu yenu wenyewe wanakiri kwamba Allah amemuita Mtume kwa jina Ya Sin. Hivyo basi Ahli (watu wa) Ya Sin maana yake ni watu wa Muhammad. Miongoni mwa wengine, Ibn Hajar Makki, Mwanachuo wa Kisunni mchungu sana kwa Shia, anasema katika “Sawa’iq Muhriqa” chini ya aya zilizonukuliwa katika kuwasifu Ahlul Bait, kwamba kikundi cha Wafasiri wamemnukuu Ibn Abbas (Mfasiri, na mkubwa wa Waumini) akisema kwamba Ahl Yasin maana yake ni Ahl Muhammad. Kwa hiyo, Salaam, maamkuzi ya amani kwa Ahli Ya Sin yana maana Salaam kwa Ahli Muhammad. Imam Fakhru’d-Bin Razi anaandika: “Ahli Bait wa Mtume wako sawa naye katika mambo matano:

1) Salaam: Salaam kwa Mtume na Salaam kwa Ahli Ya Sin (Ahli Muhammad) ni kitu kimoja.

2) Salawat (kutakia rehma) katika Swala kwa Mtume na Ahlul Bait wake, ambako ni laz- ima.

3) Tohara: Allah Anasema katika sura ya “Ta Ha” (20:1): “(Ewe Mtume) Msafi na tohara:” Ile aya ya tohara iliteremshwa katika kuwatukuza Ahlul-Bait (33:33).

4) Uharamu wa Sadaka: Sadaka haiwezi kupokelewa imma na Mtume au Ahlul-Bait wake. Mapenzi:

5) Mapenzi: Mapenzi kwa Mtume maana yake nimapenzi kwa Ahlul Bait wake.

Allah Anasema:

{ﻗُﻞ انْ ﻛﻨْﺘُﻢ ﺗُﺤﺒﻮنَ اﻟﻪ ﻓَﺎﺗﱠﺒِﻌﻮﻧ ﻳﺤﺒِﺒﻢ اﻟﻪ وﻳﻐْﻔﺮ ﻟَﻢ ذُﻧُﻮﺑﻢ ۗ{31

“Sema: kama mnampenda Allah, basi nifuateni mimi, Allah atakupendeni ninyi…”(3:31)

Na kuhusu Ahlul Bait Allah Anasema:

{ﻗُﻞ  اﺳﺎﻟُﻢ ﻋﻠَﻴﻪ اﺟﺮا ا اﻟْﻤﻮدةَ ﻓ اﻟْﻘُﺮﺑ ۗ{23 ۗ

“Sema: Sikuombeni malipo yoyote kwa haya bali Mapenzi kwa Ndugu wangu wa karibu” (42:23). Salawat Juu Ya Muhammad Na Aali - Muhammad Ni Sunna (Iliyokokotezwa),

Na Katika Swala Za Faradhi Ni Wajibu.

Wengi wa wasimuliaji wa Hadith hususan Bukhari katika Sahih yake Juz. 3, na Muslim katika Sahih yake Juz. 1 Sulayman Balkhi katika Kitabu chake “Yanabiu’l-Mawadda”, na hata Ibn Hajar katika Kitabu chake “Sawa’iqi” wanamnukuu Ka’b bin Ajza akisema: “Wakati Aya: ‘Hakika, Allah na Malaika wake wanamtakia rehema (wanamswalia) Mtume” (33:56) ilipoteremshwa, tulimuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), namna gani tutaomba rehema kwa ajili yako, Ewe Mtume wa Allah,?” Mtume akajibu, “Ombeni juu ya rehema (Swalawat) zenu kwa namna hii. “Ee Allah teremsha rehema kwa (Mtume) Muhammad na Aali Muhammad.’”

Imam Fakhru’d-Din Razi, katika Juzuu ya 6, ya Kitabu chake “Tafsir-e-Kabir” pia anasimulia hadithi kama hiyo. Ibn Hajar, akisherhesha juu ya hadith hiyo, anaonyesha kwamba, ni wazi kutoka katika Hadithi hii kwamba kuomba rehema kwa ajili ya Mtume ni sawa sawa na kuomba rehema kwa kizazi chake pia. Vilevile anamnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Msiniswalie (Msiniombee) Swalawat kigutu.”

Alipoulizwa anamaanisha nini kwa Swalawat kigutu; akasema: “Msiseme, ‘Allahumma swali Ala Muhammad,” (Ewe Allah Mrehemu Muhammad) bali semeni, Allahumma swali Ala Muhammad wa Ala Aali Muhammad.”

Dailami anaandikwa kwamba, Mtume alisema: “Sala zetu hubakia zimezuiliwa mpaka tuombe Swalawat juu ya Mtume na Ahlul (watu) wake” Imam Shafi’i anasema: Enyi Ahlul Bait (watu wa Nyumba ya Mtume) Allah Amefanya mapenzi kwenu kuwa ni wajib (lazima) kwetu sisi katika Qur’ani Tukufu.

Kwa mintarafu ya ubora wenu, Cheo na Sifa zenu, inatosha kujua kwamba kama mtu hakuomba Swalawat (rehema) kwa ajili yenu, Sala yake haikubaliwi.” Kama Swalawat kwa ajili ya Mtume na Dhuria (kizazi) wake inaachwa kwa makusudi, basi swala hiyo ya wajib inakataliwa. Na Mtukufu Mtume amesema: “Sala ya wajib ni nguzo ya iman; kama Sala ikikubaliwa, matendo mengine yote (ya ibada) yanakubaliwa; kama imekataliwa, matendo yote mengine yanakataliwa.”

Kuomba Swalawat kwa ajili ya Ahlul-Bait ni Sunna iliyokokotezwa na ni namna ya ibada ambayo ilikuwa ikifanywa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Tunaona fahari kufanya kile ambacho Qur’ani Tukufu na Mtume (s.a.w.w.) wametuarimsha sisi kufanya. Mkutano Wa Tatu – Jumamosi Usiku 25 – Rajab 1345 A.H.

Hafidh: Kwa msingi wa mazungumzo yako ya usiku wa jana naona kwamba Mashi’a wamegawanyika katika idadi ya matapo. Tafadhali tujulishe tujue ni lipi katika hayo matapo unalikubali, ili mipaka ya majadiliano yetu iwe katika tapo hilo.

Mashia Hawakugawanyika Katika Matapo

Muombezi: Mimi sikusema kwamba Mashi’a wamegawanyika katika matapo. Mashi’a wamejitoa kwa Allah (s.w.t.) na ni wafuasi wa Mtume na kizazi chake. Ni kweli baadhi ya matapo yamejichukulia jina la Shi’a ili kuwapotosha watu. amechukua manufaa ya jina la Shi’a, wakahubiri imani potofu na kueneza mkanganyiko. Watu wasio na ujuzi wame- husisha majina yao miongoni mwa Mashi’a. Ziko faraka nne za namna hiyo, mbili katika hizo zimebakia: Zaidiyya, Kaysaniyya, Qaddahiyya na Ghullat.

Zaidiyya

Zaidiyya wanamfuata Zaid bin Ali bin Husein. Wanamchukulia mtoto wa Imam Zainu’l- Abidin, aitwaye Zaid kuwa ndiye Mrithi wake. Kwa wakati huu watu hawa wanapatikana kwa idadi kubwa nchini Yemen na majirani waizungukao. Wanaamini kwamba miongoni mwa Dhuria wa Ali na Fatima, Yeye ndiye “Imam ambaye ni mwanachuo, mcha Mungu, na shujaa.

Anachomoa upanga na kusimama dhidi ya maadui,” Katika wakati wa Khalifa dhalimu wa Kibani Umayya, Hisham ibn Abdul-Malik, Hadhrat Zaid alisimama dhidi ya wale waliokuwa katika mamlaka na akauwawa Shahidi na kwa ajili hiyo akakubaliwa na Zaidiyya kama Imam. Ukweli ni kwamba Zaid alikuwa na cheo cha juu zaidi kuliko hicho ambacho Zaidiyya wanakidai kwa ajili yake. Alikuwa ni Sayyid mashuhuri wa ukoo wa Bani Hashim, na alikuwa akijulikana kwa ucha Mungu wake, hekima, Sala, na ushujaa. Alipitisha mikesha mingi bila usingizi akikesha kusali na alifunga mara kwa mara. Mtume (s.a.w.w.) alitabiri Shahada yake (kifo cha kishahidi), kama ilivyosimuliwa na Imam Husein:

“Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaweka mkono wake Mtakatifu kwenye mgongo wangu na akasema: “Ewe Husein haitachukuwa muda mrefu atazaliwa mtu miongoni mwa Dhuria wako.

Atakuwa anaitwa Zaid; atauwawa kama Shahid. Katika siku ya ufufuo, yeye na Masahaba zake wataingia Peponi, wakiweka miguu yao juu ya shingo za watu.” Lakini Zaid mwenyewe hakudai kamwe kuwa yeye ni Imam. Ni masingizio yasiyo na msingi kwa watu kusema kwamba alidai. Kusema kweli, yeye alitambua Imam Muhammad Baqir kama Imam na alitoa utii wake kiukamilifu kwake.

Ilikuwa ni baada tu ya kufariki kwa Imam Muhammad Baqir ndipo watu wajinga wakatwaa itiqad ya kwamba: “Siye Imam yule akaaye nyumbani na kujificha machoni mwa watu; Imam ni yule ambaye ni Dhuria wa Hadharat Fatima, ambaye ni mwenye elimu, na ambaye anachomoa upanga na kusimama dhidi ya adui, na kulingania (kuwaita) watu upande wake. Zaidiyya wamegawanyika katika faraka Tano: Mughairiyya; Jarudiyya; Zakariyya; Khashbiyya; na Khaliqiyya.

Wa-Kaysaniyya Na Imani Yao.

Tapo la pili ni la Kaysaniyya. Hawa ni Masahaba wa Kaysan, Mtumwa wa Ali bin Abu Talib, ambaye alimuacha huru. Watu hawa wanaamini kwamba baada ya Imam Hassan na Imam Hussain, Muhammad Hanafiyya mtoto mwingine (wa kiume) anayefuatia kwa umri, wa Amir’l-Mu’minina, Ali (A.S.) alikuwa ndiye Imam. Lakini Muhammad Hanafiyya mwenyewe kamwe hajadai hivi.

Alikuwa akiitwa Muaminifu wa Watiifu. Alikuwa akijulikana sana kwa elimu yake, Ucha Mungu, Utiifu, Ibada, na mtiifu kwenye maamrisho ya Mwenyezi Mungu. Baadhi ya watu wajinga hutoa ushahidi ambao waliuita upinzani wake kwa Imam Zainul’l-Abidin. Walidai kwamba Muhammad Hanafiyya alidai kuwa ni Imam. Ukweli ulikuwa vinginevyo. Hajadai kamwe kuwa ndiye Imam. Alitaka kuwaonyesha wafuasi wake wajinga cheo na hadhi ya Imam wa nne, Zaimul’l-Abidin. Matokeo yalikuwa kwamba, katika msikiti huohuo Mtukufu (wa Makka) wakati Hajaru’l-Aswad (jiwe jeusi) lilipothibitisha Uimamu wa Imam Zainul’l-Abidin, kama ilivyoandikwa kwa mpangilio katika vitabu vya Ta’rikh, Abu Khalid Kabuli, mkubwa wa wafuasi wa Muhammad Hanafiyya pamoja na wafuasi wengine, walimkubali Imam Zainu’l-Abidin kama Imam.

Lakini kundi la watu walaghai walipotosha watu wa kawaida na wajinga kwa kusema kwamba Muhammad Hanafiyya alionyesha tu adabu, kwamba mbele za Bani Umayya ilikuwa inapendeza mno kwa Muhammad Hanafiyya kufanya kama alivyofanya.

Baada ya kufariki Muhammad Hanafiyya, watu hawa walisema hakufa, na kwamba amejificha katika pango la Mlima Rizwi, na kwamba atakujatokea baadae kuujaza ulimwengu kwa haki na amani. Tapo hili lina matapo mengine madogodogo: Mukhtariyya; Karbiyya; Ishawiyya na Harabiyya.

Lakini leo hakuna lililopo hata moja kati ya hayo.

Qaddahiyya Na Imani Yao.

Tapo la tatu, Gaddahiyya, Wanajiita wenyewe Shia, lakini ni kundi la Makafiri.

Kitapo hiki kilianzishwa Misri na Ma’mum Ibn Salim (au Disan) ajulikanae kama Qada na Issa Chahar Lakhtan (Yesu wa sehemu nne.) Walijitolea kutafsir Qur’ani Tukufu na kumbukumbu za Ta’rikh kwa kulingana na matakwa yao. Wanashikilia kwamba kuna kanuni mbili za dini: moja ya siri na nyingine ya wazi. Kanuni ya siri ilitolewa na Allah kumpa Mtume Muhammad. Mtume akaitao kwa Ali, naye akaitoa kwa dhuria wake na kwa Mashia halisi. Wanaamini kwamba, wale wanaoijua ile kanuni ya siri wamesamehewa katika Sala na kumuamudu Allah.

Wamesimamisha dini yao katika nguzo saba. Wanaamini Mitume saba, na Maimamu saba, Imam wa saba akiwa yuko Ghaibuni. Wanangojea kujitokeza kwake. Wamegawanyika katika vijikundi viwili.

1) Nasiriyya ambao walikuwa Masahaba wa Nasiri Khusru Alawi, ambaye kwa mashairi yake, hotuba na vitabu alivuta watu wengi kwenye ukafiri. Walienea katika Tabaristan yote kwa idadi kubwa.

2) Sabahiyya (wanaojulikana katika nchi za Magharibi kama ‘Assassins,’ yaani wauaji). Walikuwa ni Masahaba wa Hasan Sabba, mwenyeji wa Misri ambaye amekuja Iran, na ambaye alisababisha matukio ya misiba na huzuni ya Alamut, ambayo ilisababisha kuuwawa kwa idadi kubwa ya watu. Matapo haya yamehifadhiwa kwenye vitabu vya Ta’rikh.

Ghullat Na Imani Zao

Tapo jingine ni lile la Ghullat, ambalo ndio kundi potovu zaidi katika matapo yote. Wanajulikana kwa makosa kama ni Shi’a. Kwa kweli hawa wote ni makafiri. Wamegawanyika katika vijikundi Saba: Saba’iyya; Mansuriyya; Gharabiyya; Bazishiyya; Yaqubiyya; Isma’iliyya na Azdariyya.

Sio Shi’a Ithna Shariyya tu (wanoamini katika Maimam kumi na mbili), bali Waislamu wote ulimwenguni wanaikataa imani yao.

Shi’a Imamiyya Ithnashariyya Na Imani Yao.

Hili ndilo kundi Sahihi la Shi’a, ambalo linaamini Maimamu kumi na mbili baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Matapo haya mengine hayana kinachofanana na kundi letu; wamejichukulia tu jina la Shi’a.

Imani Katika Allah Na Mitume

Kundi la Shi’a Imamiyya wanamini kuwepo kwa Allah Mwenye Enzi zote daima Milele. Ni mmoja, kwa maana kamilifu ya upweke wa uhalisi wa kuwako kwake. Yeye ni mmoja, hana mfano wake. Yeye ni muumba wa vitu vyote vilivyopo. Hakuna chenye kulingana au kuwa sawa na Yeye katika hali yoyote. Manabii watukufu na Mitume walitumwa kuwaeleza watu kuhusu Allah, namna ya kumuabudu Yeye, na jinsi ya kumjua Yeye. Mitume wote walihubiri na kuongoza watu kwa mujibu wa Mafundisho yaliyowekwa mbele na Mitume wakubwa watano: Nuh, Ibrahim, Musa, Issa na mwisho wa wote, Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) ambaye dini yake itabakia mpaka Siku ya Kiyama. Imani Katika Adhabu, Malipo, Jahannamu, Pepo, Na Siku Ya Kiyama.

Mwenyezi Mungu Mtukufu ameweka malipo kwa ajili ya matendo yetu, ambayo yatatole- wa kwetu katika Pepo au Jahanamu. Siku iliyowekwa kwa malipo ya matendo yetu inaitwa “Siku ya Malipo.” Wakati maisha ya Ulimwengu huu yatakapokoma, Allah (s.w.t.) atawafufua viumbe wa ulimwengu kuanzia wa mwanzo mpaka mwisho. Atawafanya wakusanyike katika Mashar; sehemu ya kukusanyikia Roho zote. Baada ya hesabu ya haki, kila mtu atapewa malipo au adhabu kwa kulingana na matendo yake.

Mambo haya yametabiriwa katika vitabu vyote vya Mwenyezi Mungu: Taurat, Zaburi, Injili na Qur’ani Tukufu. Kwetu sisi Kitabu cha Mwongozo kilicho sahihi zaidi ni Qur’ani Tukufu ambayo imefika kwetu kutoka wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) bila mabadiliko yoyote. Tunatenda juu ya amri zilizomo ndani ya Qur’ani Tukufu, na tunataraji malipo kutoka kwa Allah. Tunaamini katika amri zote zile za wajib ambazo zimo katika Qur’ani, kama Sala, Saumu, Zaka, Hija na Jihad.

Imani Katika Kanuni Za Ibada:

Halikadhalika, tunaamini katika Kanuni za utendaji wa ibada, ikiwa ni pamoja na ibada za wajibu na za Suna na amri nyingine zote ambazo zimetufikia kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tumejizatiti kushikamana nazo na kuzitekeleza kwa kadri ya uwezo wetu. Na tunajiepusha kutokana na madhambi yote, makubwa au madogo kama ulevi, kamari, uasherati, kulawiti, riba kuua, udhalimu ambavyo vimekatazwa katika Qur’ani Tukufu na Hadith.

Imani Katika Maimamu:

Sisi Shi’a vilevile tunaamini kwamba, kama ambavyo kuna mjumbe kutoka kwa Allah ambaye anazifikisha kwetu sisi kanuni na maamrisho, na ambaye ameteuliwa na kujulishwa kwetu na Allah (s.w.t.), vilevile kuna mrithi, Khalifa, au Mlinzi wa dini, ambaye anach- aguliwa na Allah na anatambulishwa kwetu kupitia kwa Mtume wa Allah. Kwa ajili hiyo Mitume wote wa Allah waliwajulisha warithi wao kwa Umma zao. Wa mwisho wa Mitume watukufu, ambaye alikuwa ndiye mkamilifu zaidi na aliye nyanyuliwa daraja ya juu zaidi kuliko Mitume wote wa Allah, aliacha kwa ajili ya wafuasi wake viongozi kusaidia watu kuepukana na matatizo.

Kwa mujibu wa hadith zilizothubutu, aliwajulisha kwa watu warithi wake kumi na mbili. Wa kwanza wao akiwa ni Ali bin Abu Talib (A.s.). Imam wa mwisho, ni Mahdi (A.f) ambaye yupo ulimwenguni, lakini yuko kwenye Ghaib (amefichwa kwenye macho ya watu), atatokeza katika muda usiojulikana baadae, wakati atakapoujaza ulimwengu uliovu- rugika kwa haki na amani.

Shi’a Imamiyya vilevile Wanaamini kwamba hawa Maimamu kumi na mbili wameteuliwa na Allah na wamejulishwa kwetu kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa mwisho. Wa mwisho katika Maimam watukufu ametoweka katika macho ya watu (kwa amri ya Mwenyezi Mungu), kama vile Maimam wengine walivyotoweka katika wakati wa Mitume waliopita, kama ilivyoelezwa katika vitabu vingi vilivyoandikwa na Maulamaa wenu.

Kiumbe huyu Mtakatifu amehifadhiwa na Allah (s.w.t.) ili kwamba siku moja aweze kuujaza ulimwengu na haki. Kwa ufupi, Shi’a wanaamini katika yale yote ambayo yamo katika Qur’ani Tukufu na katika hadith Sahihi. Ni mwenye kushukuru sana kwa Allah kwamba nimefuata imani hizi, sio kwa upofu tu wa kufuata wazazi wangu, bali kwa ukweli wenye mantiki na kuchunguza.

Hafidh: Mheshimiwa Maulana, hakika nina wiwa na wewe kwa kuweza kueleza imani za Shi’a, lakini kuna Hadith na Dua katika vitabu vyenu ambazo zinakwenda kinyume na maelezo yako na kuonyesha upotofu wa Mashi’a.

Muombezi: Tafadhali kuwa wazi zaidi.

Kanusho Juu Ya Hadith Ya Ma’rifa

Hafidh: Katika “Tafsir-e-Safi”, kilichoandikwa na mmoja wa Wanachuo wenu mwenye cheo cha juu, Faiz Kashi, mna hadith isemayo kwamba: “Siku moja Imam Husain; Shahid wa Karbala, akihutubia Masahaba wake alisema: “Enyi watu, Allah (s.w.t.) hakuumba waja Wake, bali kumjua Yeye.

Wakati wakimjua Yeye, wanamuabudu Yeye, wakati wakimwabudu Yeye, wanakuwa kinyume na kuabudu kitu kingine chochote.” Mmoja wa Masahaba akasema: “Maisha ya Baba yangu na Mama yangu na yawe mhanga kwa ajili yako! Ewe Mtoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)! Nini hasa maana ya kumjua Allah?” Mtukufu Imam akajibu, “Kwa kila mtu kumjua Allah ina maana kumjua Imam wake wa Zama, ambaye lazima atiiwe.”

Muombezi: Kwanza, lazima tuchunguze nyororo ya wasimuliaji ili kuthibitisha kama ni Sahihi. Hata kama ni sawa kwa kutegemeana na wasimuliaji, bado Aya za Qur’ani Tukufu na Hadith halisi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haziwezi kueleweka vibaya kwa sababu ya madai ya mtu mmoja.

Kwa nini usizichunguze hadith na simulizi za Maimam wetu Watukufu, na mijadala ya kidini kati ya viongozi wetu wa dini na makafiri, ambayo tayari imethibitisha Upweke wa Allah?

Kwa nini huangalii vitabu vikuu na Sharhe hasa za Shi’a kama vile -e- Mufazzal. Tawhid-e- Saduq, Biharu’l-Anwar (Kitabu cha Tawhid) cha Allama Majlisi na vitabu vingine vilivyoandikwa na Maulamaa wa Kishi’a ambavyo vimejaa hadith za mfululizo (juu ya Tawhid) kutoka kwa Maimam wetu watukufu?

Kwa nini usiangalie katika An-Naktu’l-Itiqadiyya, cha Sheikh Mufid (Amefariki 413 A.H.) mmoja wa Maulamaa wa Kishi’a, na pia kitabu chake Awa’ilu’l-Maqalat fi’l-Madhahib wa’l-Mukhtarra au Ihtajaj cha Mwanachuo wetu mashuhuri, Abu Mansur Ahmad bin Ali bin Abu Talib Tabrasi? Kama ungefanya hivyo, ungepata kujua jinsi gani Mtukufu Imam wetu Ridha (A.S.) alivyothibitisha Umoja wa Allah.

Si haki kuchukua baadhi ya taarifa zenye mashaka kwa ajili ya kutaka tu kuwazulia uongo Mashi’a. Vitabu vyenu wenyewe vina mambo ya vichekesho na maoni yasioeleweka kiakili.

Kwa kweli hadith za ajabu ajabu zimo katika vitabu vyenu Sahihi zaidi - Sahihi Sitta (yaani vile vitabu sita vya hadith vinavyokubalika kwenu ninyi).

Hafidh: Kwa kweli, maneno yako ni ya kuchekesha sana maadam unaona makosa katika vitabu ambavyo umaarufu na usahihi wake si wa kutiliwa mashaka, hususan Sahihi Bukhar, na Sahih Muslim. Maulamaa wetu wanakubaliana kwamba hadith zote zilizomo humo ni za kweli. Kama mtu akivikataa vitabu hivi viwili, anaikataa Madhehebu halisi ya Sunni. Baada ya Qur’ani Tukufu, Sunni wanategemea juu ya usahihi wa vitabu hivi, viwili.

Pengine bila shaka umeona maelezo ya Ibn Hajar Makki mwanzoni mwa kitabu chake Sawa’iq al- Muhriqa, sura ya “Matukio” (Matukio ya ukhalifa wa Abu Bakar) kama ilivyoandikwa na Bukhar na Muslim katika Sahih zao mbili, ambavyo ndio vitabu sahihi zaidi na vya kutegemewa baada ya Qur’ani Tukufu kwa mujibu wa makubaliano ya pamoja ya wafuasi (yaani, Ummah).

Anasema kwamba maadam ummah wote uko pamoja kati- ka kuzikubali hadith za vitabu hivyo, chochote ummah wanachokubaliana kwa shauri moja hakiwezi kutiliwa mashaka. Juu ya msingi wa makubaliano haya, hadith zote zilizomo katika vitabu hivi zinakubalika bila kutiliwa mashaka. Kwa hiyo, hakuna mtu anayeweza kujasiri kudai kwamba vitabu hivi vina mambo ya ajabu na ya kuchekesha.

Hadith Za Ajabu Katika Sahihain – Bukhari Na Muslim.

Muombezi: Kwanza, kwamba vitabu hivi vinakubaliwa na umma wote, kunapingwa kwa uwazi kabisa. Madai yako kuhusiana na rejea kutoka kwa Ibn Hajar, peke yake ni ya ajabu, kwa kuwa Waislamu milioni 100 hawaikubali nukta yake.

Kwa hiyo, makubaliano ya pamoja ya umma katika suala hili ni kama makubaliano ya pamoja yaliyodaiwa na watu wenu katika suala al ukhalifa. Pili, ninayosema yametegemezwa kwenye sababu zenye msingi thabiti. Kama utavichunguza vitabu hivyo bila kuwa na mawazo ya chuki, utashangaa sana.

Wengi wa maulamaa wenu wakubwa, kama vile Darqutni, Ibn Hazam, Allama Abu’l-Fazl Ja’far bin Tha’labi katika Kitabu’l-Imta’ fi Akhamu’s-’, Sheikh Abdul’Qadir bin Muhammad Qarshi katika Jawahiru’l-Mazay’a fi Tabqatu’l-Hanafiyya, na wengineo, pamoja na maulamaa wote wa Kihanafia wamevilaumu vitabu hivi viwili (Sahihain) na wamekiri kwamba vina idadi kadhaa ya hadith dhaifu na zisizothibiti. Lengo la Bukhari na Muslim lilikuwa ni kukusanya hadith; sio kuhukumu usahihi wake.

Baadhi ya Wanachuo wenu watafiti kama vile Kamalu’d-Din, Ja’far bin Sa’lih wamechukuwa taabu kubwa katika kuonyesha kasoro na makosa ya hadithi na wameweka misingi yenye nguvu katika kuunga mkono matokeo ya utafiti wao.

Hafidh: Ningelilikaribisha suala la kama utazionyesha hoja hizo ili kwamba hadhara hii ipate kujua ukweli.

Muombezi: Nitaonyesha mifano michache tu.

Rejea Zinazoonyesha Kuhusu Kuonekana Kwa Allah

Kama mnataka kusoma Hadith za kupotosha kuhusu Allah kuchukua mwili wa kibinadamu (au kuingia katika mwili wa mwanadamu), ambazo zinatetea kwamba Yeye (Allah), kama kiumbe mwenye mwili, anaweza kuonekana katika ulimwengu huu, au ataonekana katika ulimwengu jao wa Akhera, (kama inavyoaminiwa na Tapo la Suni yaani Hanbaliyya na Ashariyya) mnaweza mkarejea kwenye vitabu vyenu wenyewe, hususan Sahih Bukhari, Juz. 1, uk. 100 katika Mlango wa Fadhla-s-Sujud Min Kitabu’l-Adhan, na katika Sahih Muslim Juz. 4, uk. 92 Babu’s-Sira Min Kitabu‘r-Riqaq na vilevile tena kwenye hiyo Sahih Muslim Juz. 1 uk. 86 Sura ya Isbatu’l-Ruyatu’l-Mu’Minin Rabbahum Fi’l-Akhira; na Musnad ya Imam Hanbal Juz. 2, uk. 275. Mtapata maelezo ya kutosha ya namna hii katika vitabu hivyo.

Kwa mfano, Abu Huraira anasema: “Makelele na kishindo cha ukali wa moto vitakithiri, hautatulia mpaka Allah aweke mguu Wake humo. Kisha Jahannam itasema: “Basi, basi! hiyo inanitosha; inanitosha.” Vilevile Abu Huraira anasimulia kwamba kikundi cha watu walimuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); “Je, tutamuona Muumba wetu hiyo Siku ya Malipo?” Akajibu: “Bila shaka. Je, wakati wa mchana wakati anga inapokuwa haina mawingu, jua lina kuumizeni wakati mnapoliangalia?” Wakasema, “Hapana!” Yeye akase- ma tena: “Je, wakati wa usiku mnapoungalia mwezi mpevu wakati anga ni nyeupe, unakuumizeni?” Wakasema, “Hapana!”

Aliendelea: “Hivyo wakati mtakapomuona Allah Siku ya malipo hamtadhurika, kama vile tu ambavyo hamdhuriki muangaliapo hivi (jua na mwezi). Wakati Siku ya Hukumu itakapofika, itatamkwa na Allah kwamba kila umma wamfuate Mungu wao. Hivyo kila mtu ambaye alikuwa akiabudu masanamu au kitu kingine kisichokuwa Allah, Aliye Mmoja, ataingizwa katika moto wa Jahannamu. Kadhalika kila mmoja wa watu wema na wabaya watalipwa katika moto isipokuwa wale waliomuabudu Allah, Mmoja Mkamilifu. Watalala katika moto wa Jahannamu.

Katika muda huo Allah atatokeza katika umbo Makhususi mbele za watu ili kwamba wapate kumuona. Kisha Allah atawaambia kwamba Yeye ndiye Mola wao. Kisha Waumini watasema, “Tunajikinga na uungu wako. Sisi ni miongoni mwa wale ambao walikuwa hawaabudu kitu chochote isipokua Allah Mwenye mamlaka ya juu.” Allah atasema katika kuwajibu, “Mnayo dalili yoyote kati yenu na Allah ambapo kwamba mnaweza kumuona Yeye na kumtambua?” Watasema, “ndio!” Kisha Allah atawonyesha mguu wake uliowazi (bila kiatu). Hapo waumini watanyanyua vichwa vyao kuelekea juu na watamuona katika hali ileile kama waliyomuona nayo kwa mara ya kwanza. Kisha Allah atasema kwamba, Yeye ndiye Muumba wao. Wote kwa pamoja watakubali kwamba Yeye ndiye Mola wao.”

Sasa ni juu yenu ninyi kuamua iwapo maelezo namna hii ni sawa na ukafiri au hapana, kwamba Allah atajitokeza kiumbo mbele za watu na atafunua mguu Wake!

Na nukta kubwa sana yenye kuunga mkono hoja yangu ni kwamba Muslim bin Hajjaj anaanza kuandika sura katika Sahih yake kuhusu uhakika wa kuonekana Allah (s.w.t.), na amenukuu simulizi za kubuni kutoka kwa Abu Huraira, Zaid bin Aslam; Suwaid bin Sa’id, na wengine. Na baadhi ya maulamaa wakubwa wa madhehebu yenu wenyewe kama Dhahabi katika ‘Mizanu’l-Itidal’ na Suyuti katika kitabu chake Kitabu‘l-Lu-ualia’l- Masnu’a fi haditha’l-Muzu’a, na Sibt ibn Jauzi katika Al-Muzu’a; wamethibitisha juu ya hoja za Msingi kwamba simulizi (Hadith) hizi ni za kubuni.

Qur’ani Tukufu Inakataa Dhana Ya Kuonekana Kwa Allah.

Hata kama kusingelikuwa na uthibitisho dhidi ya madai hayo hapo juu. Aya ya Qur’ani Tukufu inakataa waziwazi dhana ya kuonekana kwa Mwenyezi Mungu. Allah (s.w.t.) Anasema:

{ ﺗُﺪْرِﻛﻪ اﺑﺼﺎر وﻫﻮ ﻳﺪْرِكُ اﺑﺼﺎر ۖ وﻫﻮ اﻟﻠﱠﻄﻴﻒ اﻟْﺨَﺒِﻴﺮ {103

“Macho hayamfikii, bali yeye anayafikia macho…” (6:103)

Tena, wakati Nabii Musa alipolazimishwa na wana Israel kwenda sehemu yake ya Sala na amuombe Allah “Ajidhihirishe kwake,” Qur’ani Tukufu inaandika tukio hili kama ifuatavyo:

{ﻗَﺎل ربِ ارِﻧ اﻧْﻈُﺮ اﻟَﻴﻚَ ۚ ﻗَﺎل ﻟَﻦ ﺗَﺮاﻧ وﻟَٰﻦ اﻧْﻈُﺮ{143

“…(Musa) akasema: “Mola wangu nionyehse (nafsi Yako) ili nikuone,” Akasema: “Huwezi (Ukathubutu) kuniona…” (7:143).

Seyyid Abdu’l-Hayy (Imam wa wa jama’at ya Ahli Sunna): Je! Hii sio kweli kwamba Ali Alisema: “Siwezi kumuabudu Mungu ambaye simuoni?” Wakati Ali anasema kitu cha namna hiyo, ina maana kwamba Allah anaweza kuonekana. Hoja Na Hadith Kuhusu Kutokuonekana Kwa Allah

Muombezi: Rafiki Mheshimiwa, umeondoa sentensi moja nje ya fuo la maneno haya. Nitakusomea matini yote. Hadith hii imeandikwa na Sheikh mashuhuri, Muhammad Ibn Yaqub Kulain katika kitabu chake “Usul al-Kafi,” (juzuu juu ya tawhid), na hivyo hivyo Sheik Saduq katika kitabu chake juu ya Tawhid, Sura ya Ibtal Aqida Ruyatullah. Imam Ja’far as-Sadiq ananukuliwa akisema, mwanachuo mmoja wa Kiyahudi alimuuliza Amir’l-Mu’minin, Ali (A.S.) iwapo amemuona Allah katika wakati wa Sala. Imam akajibu: “Hawezi kuonekana kwa macho haya ya kiumbo.

Ni moyo ndio unaomuona Yeye, kwa mwanga wa uhalisi wa kuamini na kusadiki.” Kutokana na majibu ya Ali ni kwamba yeye anachomaanisha kwa kumuona Allah, sio kumuona kwa macho, bali kwa mwanga wa imani ya kweli. Kuna ushahidi mwingine mwingi uliotegemezwa juu ya hoja na mambo yaliyoandikwa ya kuthibitisha maoni yetu juu ya nukta hii.

Zaidi ya hayo, mbali na wanachuo wa Kishi’a, maulana wenu wenyewe, kama Qadhi Baidhawi na Jarullah Zamakhshari, wamethibitisha katika Sharhe zao kwamba haiwezekani kwa Allah kuonekana. Yeyote ambaye anaamini juu ya kuonekana kwa Allah, katika ulimwengu huu au ulimwengu ujao, anaamini kwamba ni kiumbe mwenye mwili. Kuamini hivyo ni ukafiri.

Rejea Zaidi Ya Hadith Za Ajabu Ajabu Katika Vitabu Viwili Vya Hadith

Mnafikiria vitabu vyenu sita vya Hadith, khususan vile vya Bukhari na Muslim, kama vitabu vya Ufunuo. Natamani kwamba mngeviangalia kwa busara na msivuke mipaka katika kuvisifu kwenu. Bukhari, katika Sura ya “Kitab-e-Ghusl,” na Muslim katika Sehemu ya 2 ya Sahih yake (Sura ya fadhil za Mtume Musa), na Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake, Sehemu ya 2 uk. 315, na maulamaa wenu wengine wamemnukuu Abu Huraira akisema: “Miongoni mwa wana wa Israel ilikuwa ni desturi yao kuoga pamoja bila nguo, hivyo kwamba kila mmoja aliangalia utupu wa mwenziwe. Hawakufikiria kama kuna kizuizi katika hilo. Mtume Musa ndiye aliyekuwa akiingia kwenye maji peke yake, hivyo kwamba hakuna aliyeweza kuona sehemu zake za siri.

“Wana wa Israeli walizoea kusema kwamba Mtume Musa alikuwa na hitilafu katika sehe- mu zake za siri, hivyo alijiepusha kuoga nao. Siku moja Mtume Musa alikwenda mtoni kuoga. Alivua nguo zake, akaziweka juu ya jiwe na akaingia mtoni. Lile jiwe likakimbia na nguo zake. Musa akalikimbiza lile jiwe akiwa uchi, akipiga makelele: ‘Nguo zangu! Ewe jiwe nguo zangu.’ Wana wa Israel wakamuona Musa akiwa uchi na wakasema: ‘Kwa jina la Allah Musa hana hitilafu katika tupu zake.’

Kisha lile jiwe likasimama, na Musa akarudishiwa nguo zake. Kisha Musa akalipiga lile jiwe kwa nguvu sana kiasi kwamba lile jiwe likalia kwa sauti kubwa mara sita au mara saba kwa maumivu.” Kweli mnaamini kitu kama hicho kinawezekana kwa Nabii Musa (A.S.), au kwamba jiwe, kitu kisicho na uhai, lingeweza kuchukua nguo zake? Kwa hakika itakuwa haiwezekani kwa Mtume kukimbia uchi mbele za watu.

Nitasimulia Hadith nyingine iliyoandikwa katika Sahih ambayo ni ya kichekesho zaidi. Bukhari anamnukuu Abu Huraira katika Sahih yake (Juz. 1, uk. 158 na Juz. 2, uk. 153), na tena katika Sura ya “Kifo cha Mtume Musa,” na Muslim vilevile anamnukuu huyo huyo (Abu Huraira) katika Sahih yake Juz. 2, uk. 309 katika Sura ya Fadhila za Musa akisema: “Malaika wa Mauti alikuja kwa Mtume Musa na akamtaka akubali mwito wa Mola wake. Aliposikia hivi, Musa alimchapa kofi kali la uso kiasi kwamba jicho lake moja liling’oka.

Hivyo alirudi kwa Allah na akalalamika kwamba amemtuma kwa mtu ambaye hataki kufa, na ambaye amemng’oa jicho lake moja. Allah akaponya jicho lake na akamuamuru arudi tena kwa Musa na amuambie kwamba, kama anataka maisha marefu, yapasa aweke mkono wake juu ya mgongo wa fahali wa ng’ombe. Ataishi miaka mingi kama idadi ya nywele zitakazofunikwa na mkono wake.”

Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake, Juz. 2 uk. 315, na Muhammad bin Jarir Tabari, katika kitabu chake chaTarikh, Juz. 1, chini ya kichwa cha habari, “Kifo cha Mtume Musa,” ametoa maelezo haya haya kutoka kwa Abu Hurira pamoja na nyongeza kwamba kufikia wakati wa Musa, Malaika wa mauti alikuwa akitoa roho (za watu) katika mwili kiwaziwazi. Lakini baada ya Musa kumchapa kofi la uso, alikuja bila kuonekana.”

Sasa ni juu yenu kuamua ni kichekesho gani hiki ambacho kimewekwa katika vitabu hivi viwili vya hadith, ambavyo mnaviita kuwa ni vya usahihi zaidi kuliko vitabu vyote baada ya Qur’ani Tukufu. Riwaya nilizoelezea hakika zinadhalilisha heshima za Mitume wa Allah.

Ama kwa Abu Huraira, sizishangai simulizi zake. Maulamaa wenu wenyewe wanakiri kwamba, ili apate kujaza tumbo lake kwa vyakula vyenye ladha vilivyotolewa na Mu’awiya, alibuni hadithi za uongo. Kwa sababu ya uzushi wake, Khalifa Umar alimpiga viboko. Ni jambo la kushangaza kwamba watu wenye akili wanaamini ngano kama hizi za kuchekesha.

Sasa ngoja turudi kwenye majadiliano yetu kuhusu hadith uliyonukuu. Ni dhahiri, mtu mkweli akiona hadith pekee (iliyosimuliwa na mtu mmoja) atailinganisha na hadith nyingine sahihi. Imma ataisahihisha au ataikataa moja kwa moja kuliko kuitumia kama msingi wa kuwashambulia ndugu zake wa madhehebu nyingine na kuwaita makafir.

Kwa vile kitabu Tafsiri-e-Safi hatunacho hapa, hatuwezi kusema chochote kuhusu usahihi wa hadith hii.

Hata kama ni kweli, yatupasa kutegemea juu ya kanuni kwamba, kama tunajua athari, tunaweza kujua sababu. Yaani, kama tunamjua Imam kama Imam, kwa hakika tunajua utambulisho wa Allah, katika njia ileile, ambayo kama mtu anamjua Waziri Mkuu, anamjua Mfalme. Ni kwa kuhusu kanuni hii kwamba Sura ya “Tawhid” na Aya nyingine za Qur’ani Tukufu zilishuka. Zaidi ya hayo, kuna Hadith nyingi kuhusu upweke wa Allah zilizosimuliwa na Imam Husain mwenyewe na Maimamu wengine. Kumjua Imam wetu ni namna kubwa ya Ibada ya Allah. Maana hiyo hiyo imetolewa katika “Ziarat-e-Jami’a”, ambayo imefika kwetu kutoka kwa Mtukufu Imam. Tunaweza kuitafsiri pia kwa njia nyingine, kama wanachuo walivyofanya katika mambo kama haya. Mtekelezaji yoyote wa kitendo anaweza kuelewe- ka kwa asili ya kitendo chake.

Kwa vile Mtume na kizazi chake walifikia daraja ya juu kabisa katika uwezo wa kibinadamu, hakuna wengine wenye fadhila au ubora kama wao. Kwa kuwa hawa ndio njia dhahiri zaidi ya kumjua Allah, yeyote awajuaye hawa, anamjua Allah. Kama walivyosema wenyewe: “Ni kwa kupitia kwetu sisi, kwamba Allah anaweza kutumikiwa.” Tunaamini kwamba Ahlul Bait wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wametufundisha elimu kuhusu Allah na njia zinazostahili za kumuabudu Yeye. Wale ambao hawakuwafuata wamepotea njia.

Hadith Ya Thaqalain (Vizito Viwili).

Kusisitiza jambo hili hili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema katika hadith inayokubali- wa na madhehebu zote. “Enyi watu (wafuasi) wangu! Mimi ninakuachieni kwa ajili yenu vitu viwili vizito (vya rejea): Kitabu cha Allah na Ahlul Bait wangu. Mtakapokuwa mumeshikamana na viwili hivi, kamwe, kamwe hamuwezi kupotea baada yangu, kwani kwa hakika viwili hivi kamwe havitatengana mpaka vinifikiea kwenye chemchem ya Kauthar.”

Hafidh: Hatutegemei juu ya hadith hii, ambayo unajaribu kuirudia. Kuna uzushi mwingi katika vitabu vyenu na mifano ya ushirikina, kama vile kutafuta kutekelezewa haja zetu kutoka kwa Maimamu zaidi kuliko kutoka kwa Allah. Ushirikina ni nini? Ushirikina una maana ya kumgeukia mtu mwingine yeyote au kitu zaidi kuliko kwa Allah kwa ajili ya kutekelezewa haja zetu. Imeonekana kwamba Mashi’a kamwe hawamuombi Allah. Wanawaomba Maimam. Hili si chochote, bali ni ushirikina.

Muombezi: Ninasikitika kwamba unapotosha ukweli. Labda ningeruhusiwa nikuelezeni ushirikina ni nini kwa mujibu wa maulamaa wakubwa wa Kiislamu na kwa mujibu wa aya za Qur’ani Tukufu.

Ushirikina Na Aina Zake:

Ushirikina ni wa aina mbili: Ushirikina wa wazi na ushirikina uliofichika. Ushirikina wa wazi una maana ya kumshirikisha mtu au kitu na Nafsi Kamili ya Allah au kumshirikisha na sifa Zake. Kumfanyia Allah washirika maana yake kushirikisha kitu na Upweke Wake na kuukiri ushirikishaji huu kwa ulimi, kama Sanamiyya (waabudu sanamu) au Mazorostania, ambao wanaamini katika kanuni mbili:

Nuru na giza. Wakristo pia wanafanya hivyo. Wanaamini katika utatu na kuugawanya uungu katika sehemu tatu - Baba, Mwana, na Roho Mtakatifu. Wanaamini katika tabia tofauti za kila mmoja, na mpaka watatu hawa waungane, bila hivyo uungu wenyewe hautakuwa kamili. Qur’ani Tukufu inakataa imani hii, na Allah (s.w.t.) anaelezea upweke wake katika maneno haya: {ﻟَﻘَﺪْ ﻛﻔَﺮ اﻟﱠﺬِﻳﻦ ﻗَﺎﻟُﻮا انﱠ اﻟﻪ ﺛَﺎﻟﺚ ﺛََﺛَﺔ ۘ وﻣﺎ ﻣﻦ اﻟَٰﻪ ا اﻟَٰﻪ واﺣﺪٌ ۚ{73

“Kwa hakika wamekufuru wale waliosema: Hakika Allah ni Mmoja katika watatu; hali hakuna mungu ila Allah Mmoja….” (al-Maida; 5: 73).

Kushirikisha vitu na sifa za Uungu, maana yake ni kuamini kwamba sifa Zake, kama elimu Yake au nguvu ziko tofauti na, au ni nyongeza katika Nafsi Yake Kamilifu. Ashariyya wa Abu’l-Hasani Ali bin Ismail Ashari Basari, wanaelezewa na Maulamaa wenu wakubwa, kama Ali bin Ahmad katika kitabu chake Al- na Minhaju’l-Adilla fi Aqa’idi’l-Mila, Uk. 57 kuwa wanaamini kwamba Sifa za Allah ni nyongeza katika Nafsi Yake kamilifu, na kwamba ni za milele. Hivyo yeyote mwenye kuamini kwa njia yeyote ile kwamba tabia au sifa yeyote ya Allah ni nyongeza katika Nafsi yake kamilifu, huyo ni mshirikina.

Kila sifa Yake ni yenye asili kwake. Ushirikina katika matendo ya mtu, ina maana kumshirikisha mtu mwingine katika Dhati Yake Yenye kujitosheleza Daima dumu. Mayahudi wanaamini kwamba Allah aliumba viumbe na kisha akajiweka mbali na viumbe Wake. Katika kuwalaumu watu hawa, aya ifuatayuo iliteremshwa:

{وﻗَﺎﻟَﺖِ اﻟْﻴﻬﻮد ﻳﺪُ اﻟﻪ ﻣﻐْﻠُﻮﻟَﺔٌ ۚ ﻏُﻠﱠﺖ اﻳﺪِﻳﻬِﻢ وﻟُﻌﻨُﻮا ﺑِﻤﺎ ﻗَﺎﻟُﻮا ۘ ﺑﻞ ﻳﺪَاه ﻣﺒﺴﻮﻃَﺘَﺎنِ ﻳﻨْﻔﻖ ﻛﻴﻒ ﻳﺸَﺎء ۚ{64

“Na Mayahudi wanasema: Mkono wa Allah umefungwa! Mikono yao itafungwa (kwa pingu) na watalaaniwa kwa yale wanayoyasema. Bali, mikono yake yote iwazi; Hutoa apendavyo…” (5:64).

Ghullat wanaunda kundi lingine la washirikina. Pia wao wanaitwa Mufawwiza. Wanaamini kwamba, Allah ameweka au kuaminisha Mamlaka ya mambo yote kwa Maimam watukufu. Kwa mujibu wao, Maimam ni waumbaji na pia hutupatia sisi riziki. Kwa uwazi, wale wanaomuona mtu kuwa mshirika katika Mamlaka ya Uungu ni mshirikina.

Ushirikina Katika Swala:

Ushirikina katika Sala, ina maana ya mtu kugeuza mazingatio yake wakati wa swala kwa makusudi kuelekea kwa kiumbe aliyeumbwa badala ya kuelekea kwa Allah. Kama mtu akikusudia kuomba kwa kiumbe aliyeumbwa, huyo ni mshirikina. Qur’ani Tukufu inakataza haya katika maneno haya.

{ﻓَﻤﻦ ﻛﺎنَ ﻳﺮﺟﻮ ﻟﻘَﺎء رﺑِﻪ ﻓَﻠْﻴﻌﻤﻞ ﻋﻤً ﺻﺎﻟﺤﺎ و ﻳﺸْﺮِكْ ﺑِﻌﺒﺎدة رﺑِﻪ اﺣﺪًا {110

“…Anayetarajia kukutana na Mola Wake, naafanye vitendo vizuri, na asimshirik- ishe yeyote katika ibada ya Mola wake.” (18:110). Aya hii inaonyesha kwamba sharti la msingi wa imani ni kwamba mtu lazima afanye lolote lile ambalo ni zuri na asije kumshirikisha yeyote pamoja na Allah katika kutoa utii na ibada Kwake. Kwa maneno mengine, yule ambaye anasali au kutekeleza Hija, au kufanya kitendo chochote kizuri kwa ajili tu ya kujionyesha kwa watu uzuri wake, ni mshirikina.

Amewashirikisha wengine pamoja na Allah katika jambo la kutekeleza vitendo vyake. Kuonyesha kujikinai kwa matendo mazuri ni ushirikina mdogo, ambao hutangua vitendo vyetu vizuri.

Imepata kuelezwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Jiepusheni na ushirikina mdogo.” Watu wakamuuliza, “Ewe, Mtume wa Allah, ni nini ushirikina mdogo? Akajibu: “Al-riya wa’s-sama” (yaani, kuonyesha watu au kuwafanya wasikie juu ya ibada yako kwa Allah).

Vile vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kitu kibaya mno ninachokuhofieni kwenu ni ushirikina uliofichika; hivyo kuweni na hadhi ya juu yake kwa kuwa miongoni mwa wafuasi wangu ushirikina ni wa siri mno kuliko kutambaa kwa mdudu chungu juu ya jiwe gumu katika usiku wa giza.”

Tena alisema: “Mtu ambaye anatekeleza ibada ya Sala kwa njia ya majivuno, ni mshirikina. Mtu ambaye anafunga au kutoa sadaka au kutekeleza Hija au kumuachia mtumwa huru ili kuonyesha kwa watu uadilifu wake au kujipatia jina zuri, ni mshirikina.”

Na kwa vile mistari hii ya mwisho inaelekeza kwenye mambo ya roho, umechanganywa katika ushirikina uliojificha.

Hafidh: Tunaona katika maelezo yako mwenyewe kwamba kama mtu atafanya maombi kwa kiumbe yeyote aliyeumbwa ni mshirikina. Hivyo Mashia nao ni washirikina, kwa vile wanafanya maombi kwa Maimamu watukufu na watoto wao.

Kuhusu Kuomba Au Ahadi:

Muombezi: Kama tunataka kuyakinisha imani ya jumuiya moja, hatupasi kutegemea juu ya watu wasio na ujuzi wa jumuiya hiyo. Yatupasa kusoma vitabu vyao vya kuaminika.

Kama unapenda kuuchunguza Ushi’a, usianze na Shi’a omba omba barabarani, wapigao makelele ya “Ya! Ali, Ya! Imam Ridha,” na kwa hoja hiyo, ukatangaza kwamba Mashi’a ni washirikina. Halikadhalika, kama mtu mjinga atafanya maombi au kiapo kwa jina la Maimamu au watoto wao, haipasi kuukashifu Ushi’a wote. Kama utasoma vitabu vya Sheria vya Shi’a, utaona kwamba hamna hata dalili moja ya ushirikina, au mambo ya upumbavu.

Msisitizo juu ya Upweke wa Allah uko wazi kila mahali. Vitabu mashuhuri zaidi, “Sharhe ya Lum’a, na Shara’i, vinapatikana kwa wingi na unaweza ukavichunguza. Katika Sura ya “Ahadi” (ya nadhiri) maelezo sahihi ya wanasheria wa Kishia yanatajwa katika vitabu vyote vilivyotajwa hapo juu na katika vitabu vingine vingi. Kwa kuwa nad- hir ni aina ya maombi, ni lazima kuwa na nia kwamba ni kwa ajili ya kujikurubisha kwa Allah (Kurbata ila llah).

Kuna Sharti mbili kwa nadhiri sahihi: Nia ya moyo na kutamka au kwa maelezo ya maneno ya lugha yoyote ile itakayokuwa. Kuhusu sharti la kwanza, nia ya moyo lazima iwe kwa ajili ya Allah. Sharti la Pili hukamilisha sharti la kwanza; mtu ambaye anafanya Nadhiri lazima aseme kwa maneno kwamba, ni kwa ajili ya Allah.

Kwa mfano, kama anaahidi kufunga au kuacha kunywa (ulevi), lazima aweke nia kwa kutumia maelezo ya maneno ambayo yana neno ‘lillah’ (kwa ajili ya Allah) bila ya hivyo nadhiri itakuwa batili.

Nadhiri Kwa Jina La Allah.

Kama tunafanya nadhiri isiyo kwa jina la Allah, bali kwa mtu mwingine, ikiwa amekufa au yuhai, au tukimchanganya pamoja na jina la Allah, hata kama ni Imam au mtoto wake, nadhir hiyo si sahihi. Kama hili likifanywa kwa makusudi na kwa kujua basi huo ni ushirikina wa dhahiri, kama ilivyo wazi kutoka kwenye Aya, “...Na usimshirikishe yoyote katika ibada ya Mola Wako.” (18:110). Wanasheria (mafakihi) wa Kishi’a wanakubali kwamba, kufanya nadhiri kwa jina la mtu yoyote pamoja na Mitume au Maimam ni kosa. Kama ikifanywa kwa makusudi ni ushirikina.

Nadhiri yoyote lazima ifanywe katika jina la Allah, ingawa tumerehusiwa kufanya wakai wowote tunapopenda. Kwa mfano, kama mtu kwa jina la Allah atachukua mbuzi kumpeleka kwenye nyumba makhususi au sehemu ya ibada au kwenye kaburi la Imam au mtoto wa Imam na akamtoa dhabihu, hakuna madhara ndani yake.

Vilevile, kama akiahidi na kutoa fedha au nguo kwa jina la Allah kumpa Seyyid (mjukuu wa Mtume) maalum, au kutoa sadaka kumpa yatima, au muombaji, hakuna madhara ndani yake. Kwa kweli, kama mtu anaahidi kufanya nadhiri tu kwa ajili ya Mtume au Imam, au mtoto wa Imam au kwa ajili ya watu wengine, hiyo inakatazwa.

Ikifanywa kimakusudi, ni ushirikina. Ni wajibu wa kila Mtume au mwenye mamlaka ya kidini kuwaonya watu kama Qur’ani Tukufu inavyosema:

{ﻗُﻞ اﻃﻴﻌﻮا اﻟﻪ واﻃﻴﻌﻮا اﻟﺮﺳﻮل ۖ ﻓَﺎنْ ﺗَﻮﻟﱠﻮا ﻓَﺎﻧﱠﻤﺎ ﻋﻠَﻴﻪ ﻣﺎ ﺣﻤﻞ وﻋﻠَﻴﻢ ﻣﺎ ﺣﻤﻠْﺘُﻢ ۖ وانْ ﺗُﻄﻴﻌﻮه ﺗَﻬﺘَﺪُوا ۚ{54

“Sema: Mtiini Allah na mtiini Mtume, na kama mkigueka basi juu yake kinabakia kile alichobebeshwa juu yake na juu yenu hubakia kile mlichobebeshwa juu yenu …” (24:54).

Ni wajibu wa watu kusikiliza kile anachokisema Mtume wa Allah na kukitekeleza. Walakini, kama mtu hajali kufuata mafundisho ya Kimungu na hayatekelezi, haiwezi kudhuru imani au kanuni ambazo ndani yake imani imesimamishwa. Ushirikina Uliofichika: Kujionyesha Katika Sala.

Aina ya pili ya ushirikina ni ule ushirikina uliofichika, kama vile kufanya kujionyesha Sala zetu au namna zingine za utiii kwa Allah. Tofauti kati ya ushirikina huu na ule ushirikina wa katika Sala, ni kwamba kuhusu suala la ushirikina katika Sala tunashirikisha kitu kingine au kiumbe pamoja na Allah.

Kama mtu ataelekeza nia yake kwenye kitu kingine mbali na Allah, katika Ibada ya Sala, au kama kwa ushauri wa Shetani, akawa na picha bandia ya Mungu katika mawazo yake, au kama kiongozi wake ndio kiini cha nia yake, basi ni mshirikina.

Hakuna isipokuwa Allah Ndiye apasaye kuwa mlengwa wa nia katika ibada zetu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba, kama mtu atafanya kitendo kizuri na akafanya mtu mwingine kuwa mshirika pamoja na Allah ndani yake, basi kitendo chake chote ni kwa ajili ya yule mshirika. Allah anachukia kitendo hicho na mtendaji wake pia. Vile vile imesimuliwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba,

“Kama mtu akifanya ibada ya Sala, au kufunga, au kutekeleza Hija na ana mawazo kwamba kufanya kwake hivyo watu watamsifu, “basi hakika, amefanya mshirika pamoja na Allah katika kitendo chake.”

Vilevile imesimuliwa kutoka kwa Imam Ja’far Sadiq kwamba kama mtu atafanya kitendo kwa kumuogopa Allah, au kwa ajili ya malipo ya Akhera na akachangaya ndani yake rid- haa ya binaadamu, basi mtendaji wa kitendo hicho ni mshirikina.

Ushirikina Kuhusiana Na Kisababisho

Aina moja ya ushirikina ni ile ambayo huhusishwa kwenye kisababisho, kwa kuwa watu wengi huweka matumaini yao na hofu juu ya kisababisho cha pili. Huu pia ni ushirikina, lakini unasameheka. Ushirikina una maana yakufikiri kwamba uwezo wote kiasili unatokana na kisababisho cha pili. Kwa mfano, jua hustawisha vitu vingi ulimwenguni, lakini kama mtu atafikiria uwezo huu ni wa msingi katika jua (yaani asili yake inatokana na jua lenyewe), basi huu ni ushirikina.

Walakini, kama tunaamini kwamba jua limepata uwezo huu kutoka kwa Allah, na kwamba jua ni kisababisho cha pili tu cha ukarimu wake, basi huu kamwe sio ushirikina. Bali hasa ni namna ya Ibada, kwa kuwa kutafakari juu ya ishara za Allah ni mwanzo wa kumwabudu Allah. Utajo umefanywa katika Aya za Qur’ani Tukufu kwenye ukweli huu kwamba yatupasa kutafakari juu ya ishara za Allah kwa kuwa hii huongozea kwenye mazingatio juu ya Allah.

Kwa njia hiyo hiyo, kutegemea juu ya kisababisho cha pili (nadhari ya mfanya biashara kwenye biashara, au nadhari ya mkulima kwenye shamba lake) humfanya mtu kuwa mshirikina kama kwa sababu hii atageuza mazingatio yake kunyume kutoka kwa Allah.

Kwa msingi wa maelezo ya ushirikina ya hapo juu, ni upi katika mifano iliyoelezwa hapo ambao unafikiri unatumika kwa Mashi’a? Ni kwa namna gani kutokana na mtazamo wa Sala, imani au hadithi za Shi’a ambayo umeiona, inayoweza kuwafanya washambuliwe kwa ushirikina?

Hafidh: Nakiri kwamba yote uliyosema ni sawasawa, lakini kama utachukua taabu ya kufikiri kidogo, utakubali kwamba kutegemea juu ya Maimam ni ushirikina. Kwa kuwa haitupasi kutafuta njia yoyote ya kibinadamu kumfikia Allah, yatupasa kumwomba Allah moja kwa moja kwa ajili ya kutaka msaada.

Kwanini Mitume Walitafuta Misaada Kutoka Kwa Watu?

Muombezi: Inashangaza kwamba unapuuza niliyokuwa nikisema hapa wakati wote huu. Je ni ushirikina kufanya maombi kwa watu wengine kwa ajili ya kutekelezewa haja zetu? Kama hii ingekuwa kweli, umma wote wa binadamu kwa ujumla basi ni wa kishirikina. Kama kuomba msaada kwa wengine ni ushirikina, kwa nini Mitume waliomba misaada kutoka kwa watu? Yakupasa uzichunguze aya za Qur’ani Tukufu ili upate kujua kipi ni kweli na sahihi. Aya zifuatazo zinafaa kuzingatiwa:

“Akasema: ‘Enyi wakuu! Ni nani atakayeniletea kiti chake cha enzi kabla hawajakuja kwangu, hali ya kuwa wamekwisha sslimu amri?’ Mjasiri mmoja miongoni mwa majini akasema: ‘Mimi nitakuletea kabla hujainuka mahali pako hapo na mimi bila shaka ninazo nguvu za hayo (na) ni muaminifu.’ ‘Akasema yule aliyekuwa na ilmu ya Kitabu: ‘Mimi nitakuletea kabla ya kupepesa jicho lako’ basi alipokiona kimewekwa mbele yake alisema: ‘Haya ni kwa fadhila za Mola wangu…..’” (28; 38-40)

Uletaji wa kiti cha Enzi cha Bilqis (Malikia wa Sheba) kwa Sulaiman ulikuwa hauwezekani kwa kila kiumbe. Kwa kukiri kabisa, ilikuwa sio kawaida, na Mtume Sulaiman, pamoja na kujua kwake kwamba ilihitaji uwezo wa Ki-Mungu, hakumuomba Allah kuleta kiti hicho cha enzi, bali aliomba viumbe wa kawaida tu kumsaidia. Ukweli huu unaonyesha kwamba kuomba msaada wa wengine sio ushirikina.

Allah, kisababisho cha kwanza, ndiye Muumba wa visababisho vya ulimwengu huu. Ushirikina ni jambo la moyo. Kama mtu anaomba msaada wa mwingine na hamfikirii yeye kuwa ni Allah au mshirika Wake, haikatazwi. Hali hii ni ya kawaida kila mahali. Watu huenda kwenye nyumba za wengine na kuomba msaada bila kuchukua jina la Allah.

Kama nikienda kwa Daktari na nikamuomba aniponyeshe, je, nitakuwa mshirikina? Tena kama mtu anakufa maji, na akapiga kelele za kuomba msaada hivi atakuwa ni mshirikina? Hivyo tafadhali kuwa muadilifu na usipoteze ukweli. Jumuiya yote ya Shi’a inaamini kwamba, kama mtu atafikiria kizazi cha Mtume kuwa ni Allah au washirika katika Dhati (Nafsi) Yake, hakika yeye ni mshirikina. Utakuwa umewasikia Mashi’a wakiwa katika shida wakilia, “Ya Ali, nisaidie!” Ya Husain, nisaidie!” Lakini ukweli ni kwamba, kwa kuwa ulimwengu ni nyumba ya visababisho vya pili, tunawafikiria wao kama njia ya kutolewa katika shida. Tunaomba msaada wa Allah kupitia kwao.

Hafidh: Badala ya kumuomba Allah moja kwa moja, kwa nini muombe visababisho?” Muombezi: Matarajio yetu ya kudumu kuhusu haja zetu, dhiki, na hofu yamewekwa juu ya Allah, Mkamilifu. Lakini Qur’ani Tukufu inasema yatupasa kumfikia Allah, kupitia baadhi ya njia (visababisho) za kupelekea.

{ﻳﺎ اﻳﻬﺎ اﻟﱠﺬِﻳﻦ آﻣﻨُﻮا اﺗﱠﻘُﻮا اﻟﻪ واﺑﺘَﻐُﻮا اﻟَﻴﻪ{35

“Enyi ambao mmeamini! Mcheni Allah na tafuteni njia ya kumfikia Yeye…” (5:35).

Dhuria Watukufu Wa Muhammad Ni Njia (Wasyla – Visababisho)

Ya Neema Za Mungu.

Sisi Shi’a hatuwachukulii kizazi cha Mtume kama ufumbuzi wa matatizo yetu yote. Tunawaona wao kama wacha Mungu zaidi katika waja wa Allah na kama njia za neema za Mungu. Tunajiambatanisha wenyewe kwenye ile familia bora zaidi kwa mujibu wa maamrisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hafidh: Kwa nini unasema kwamba, maneno: “Njia ya kumfikia (Wasyla)” katika Aya hiyo hapo juu yanawahusu kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?”

Muombezi: Katika hadith nyingi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), amependekeza kwetu, kwamba katika shida zetu tuwaombe watoto wake kama njia ya kumfikia Allah. Wengi wa Maulamaa wenu, kama Hafiz Abu Nu’aimi Isfahani katika kitabu chake “Nuzulu’l-Qur’ani fi Ali” (Ufunuo katika Qur’ani kuhusu Ali), Hafiz Abu Bakr Shiraz katika kitabu chake “Ma Nazala mina’l-Qur’ani fi Ali” na Imam Ahmad Tha’labi katika Tafsir (Sharhe) yake anasema kwamba Wasilat (njia ya kumfikia) katika aya hiyo hapo juu ina maana ya watoto wa Mtume (s.a.w.w.).

Maneno haya yamekuwa wazi kwenye hadith nyingi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ibn Abi’l-Hadid Mutazali, mmoja wa Mualamaa wenu maarufu, anase- ma katika “Sherhe Nahjul’l-Balagha” yake, Juz. 4, Uk, 79, kwamba Bibi Fatima Zahra, alitaja maana ya maneno ya Aya hii mbele ya Muhajirina na Ansari, wakati anatoa khutuba yake yenye kuhusu kunyang’anywa shamba lake la Fadak, katika maneno haya: “Namshukuru Allah Ambaye kwamba Ukuu Wake na Nuru Yake, Wakazi wa mbinguni na ardhini hutafuta njia ya kumfika Yeye. Miongoni mwa viumbe Wake sisi ni njia (Wasilat) ya kumfikia Yeye.”

Hadith Ath-Thaqalain (Hadith Ya Vizito Viwili).

Miongoni mwa hoja zetu nyingi zinazokubaliwa kuhusu uhalali wa kufuata kwetu kizazi cha Mtume ni “Hadith ath-Thaqalain” - vizito viwili, ambayo usahihi wake umekubaliwa na Madhehebu zote. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kama mtashikamana na viwili hivi, kamwe, hamtapotea baada yangu.” Hafidh: Nafikiri umekosea wakati unaposema kwamba hadith hii ni sahihi na kwamba inakubaliwa na wote kwa kuwa haijulikani kwa Maulamaa wetu mashuhuri. Kuthibitisha haya naweza kusema kwamba, msimuliaji mkubwa wa hadith wa madhehebu yetu, Muhammad bin Ismaili Bukhari, haisimulii katika Sahih yake, ambacho ndio kitabu sahi- hi zaidi baada ya Qur’ani.

Muombezi: Sikukosea kuhusu hadith hiyo. Usahihi wa hadith hii tukufu umekubaliwa na Maulamaa wenu wenyewe. Hata Ibn Hajar Makki, pamoja na uchungu wake na chuki, anakubali ukweli wake. Yakupasa uangalie katika “Sawai’q Muhriqah (Sehemu ya 2, Sura ya 2, Uk. 89-90, chini ya aya ya 4) ambamo ndani yake, baada ya kunukuu maelezo ya Tirmidhi, Imam Ahmad bin Hanbali, Tabrani, na Muslim, anasema:

“Elewa kwamba hadith inayohusu kujiambatanisha na Thaqalain - vizito viwili (Ahlul-Bait wa Mtume na Qur’ani) imesimuliwa katika njia nyingi. Wasimuliaji wa hadith hii idadi yao ni zaidi ya ishirini, wote ni Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Kisha anasema kwamba kuna baadhi ya khitilafu ya namna ambayo kwayo hadith hii imesimuliwa. Wengine wanasema kwamba ilisimuliwa wakati Mtume yuko kwenye Hija yake ya mwisho huko Arafa; baadhi wanasema ilisimuliwa Madina, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yuko kwenye kitanda alichofia na chumba chake kilikuwa kimejaa Masahaba wake; wengine wanasema kwamba ilisimuliwa huko Ghadir-Khum; na wengine wanasema ilisimuliwa baada ya kurudi kwake kutoka Ta’if.

Baada ya kusema yote haya, yeye (Hajar Makki) mwenyewe anafafanua kwamba hakuna khitilafu ya wazi katika hadith yenyewe. Ama kwa tofauti ya sehemu, huenda ilikuwa kwamba Mtume amerudia kusimulia hadith hii katika nyakati tofauti na mara kwa mara (sehemu mbalimbali) kwa ajili ya kusisitiza ukubwa wa Qur’ani na kizazi chake kitukufu.

Umesema kwamba, kwa kuwa Bukhari hakuisimulia hadith hii katika Sahih yake, basi usahihi wake ni wa mashaka. Lakini hadith hii, ingawa haikuandikwa na Bukhari, imesimuliwa kiujumla na maulamaa wakubwa wa madhehebu yenu, pamoja na Muslim bin Hajjaj na waandishi wengine wa vitabu sita vya hadith, ambao wameziandika katika vitabu vyao kwa ukamilifu sana, na hawategemei ukusanyaji wa Bukhari tu peke yake.

Kama unakubali uadilifu wa Maulamaa wako wote mwenyewe, ambao wote walitambuliwa na Masunni waliopita, yapasa ukubali hadithi hii kwamba ni ya kweli, ambayo kwa sababu fulani haikuandikwa na Bukhari.

Hafidh: Hakuna sababu ya kuunga mkono kutokuiandika hadith hii. Bukhari alikuwa makini sana katika suala la kusimulia hadithi. Alikuwa ni mwanachuo mwangalifu sana, na kama aliona hadith, kwa mtazamo wa maudhui au chanzo chake, kuwa yenye madhara au kutokubalika na akili za kawaida, yeye hiyo hakuiandika.

Muombezi: Kama mithali inavyosema: “Kupenda sana kitu humfanya mtu kuwa kipofu na kiziwi.” Waheshimiwa Masuni wamekosea hapa, una shauku kubwa katika upendo wako kwa Imam Bukhari. Unasema alikuwa mchunguzi sana wa mambo, na kwamba simulizi zilizomo katika Sahih yake ni za kuaminika na kustahiki sifa ya Wahayi (Ufunuo). Lakini ukweli ni kinyume chake. Nyororo ya riwaya zilizotajwa na Bukhari zina watu ambao mara kwa mara wameshutumiwa kama waongo.

Hafidh: Madai yako sio ya kweli. Unashusha elimu na uwezo wa Bukhar, ambavyo ni tusi kwa madhehebu yote ya Sunni.

Muombezi: Kama uchunguzi ulioko juu ya msingi wa elimu ni matusi, basi wengi wa Maulamaa wenu maarufu ni watu ambao wamekebehi ile nafasi ya juu ya elimu na maarifa. Ningependa kukushauri uvichunguze mwenyewe vitabu vilivyoandikwa na waandishi wakubwa na maulamaa wa madhehebu yenu ambao wameandika Sherhe juu ya Sahih Bukhari, k.m. “Al-Lu’ali’l- Masnu’a fi hadith’l-Mazu’a” ya Suyuti, “Mizanu’l-ibtidal” na “Talkhisu’l-Mustadraka” ya Dhahabi; “Tandhkiratu’l-Mazu’a” ya Ibn Jauzi, “Tarikh Baghdad” kilichokusanywa na Abu Bakar Ahmad bin Ali Khatib Baghadad, na vitabu vingine vya “Ilm Rijal” (vinavyoitwa, makala juu ya sifa za wasimuliaji) vilivyoandikwa na maulamaa wenu wengi wakubwa. Kama utasoma vitabu hivi, hutathubutu kusema kwamba nimemkebehi Imam Bukhari.

Bukhari Na Muslim Wameandika Hadith Nyingi Zilizosimuliwa Na Wazushi.

Nilichosema ni hiki: Vitabu hivi viwili, Sahih Bukhari na Sahih Muslim, vina hadithi zili- zosimuliwa na waongo. Kama utavichunguza Sahih Muslim na Sahih Bukhari katika mwanga wa vitabu vya “Rijal” (yaani vitabu vyenye kuelezea maisha na tabia za wasimuliaji wa hadith), utaona kwamba wameandika hadith nyingi zilizosimuliwa kutoka kwa watu ambao walikuwa waongo wakubwa, kwa mfano Abu Huraira, muongo mwenye sifa mbaya, Ikrima Kharji, Sulaiman bin Amri, na wengine wa namna hiyo hiyo.

Bukhari hakuwa makini katika kuandika Hadith kama unavyofikiri. Hakuiandika “Hadith ya Thaqalain” ambayo wengine wameiandika, lakini hakusita kuandika ngano za kufedhehesha na matusi kuhusu Mtume Musa akimpiga kofi la uso Malaika wa Mauti, Mtume Musa akikimbia akiwa uchi mbele za watu akifukuza jiwe, na juu ya kuonekana kwa Allah (s.w.t.).

Fikiria ngano nyingine ya kudhihaki na matusi iliyoandikwa na Bukhari katika Sahih yake, Juz. 2, uk. 120, Sura ya “Al’Lahr Bi’l-Harb,” na Muslim katika Sahih yake Juz. 1, akimnukuu Abu Huraira akisema kwamba siku ya Idd baadhi ya mabedui kutoka Sudani walikusanyika katika Msikiti wa Mtume. Waliwaburudisha watazamaji kwa michezo na maonyesho yao.

Mtume akamuuliza Aisha (Mke wake - Mama wa Waumini) kama angependa kuona hayo maonyesho. Aisha, akasema anapenda kuyaona. Mtume akamfanya (Aisha) apande juu ya mgongo wake kwa hali ambayo kichwa chake kilikuwa juu ya mabega yake na uso wake juu ya kichwa cha Mtume. Ili kumfurahisha Aisha, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akiwaomba wachezaji kuonyesha mchezo (dansa) nzuri zaidi. Mwishowe Aisha alichoka, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuacha ateremke chini! Amua mwenyewe iwapo ngano kama hii haifedheheshi.

Kama Bukhari alikuwa makini kuhusu kusimulia mambo, je, ilikuwa inafaa kwa upande wake kuandika ngano za kipuuzi kama hizi katika Sahih yake? Lakini ni mpaka sasa unaviainisha vitabu hivi kuwa ndio sahihi zaidi baada ya Qur’ani Tukufu. Hakika Bukhari alichukua tahadhari maalum kuliacha jambo la Uimamu na Umakamu wa Ali (a.s.) na hivyo hivyo suala la Ahlul-Bait. Huenda aliogopa maelezo kama hayo yangeweza yakatu- mika siku moja kama silaha dhidi ya wapinzani wa Ahlul-Bait.

Hadith Nyingi Sahihi Zihusuzo Ahlul-Bait Ziliepukwa Kwa Makini Sana.

Hivyo wakati tukilinganisha Sahih Bukhari na Sahih nyinginezo, tunafikia kwenye uamuzi juu ya suala hili kwamba hadith yoyote yenye kuwahusu Ahli Bait, hata iwe sahihi vipi na kuungwa mkono kikamilifu na waandishi katika mwanga wa Qur’ani, Bukhari kwa makusudi alishindwa kuiandika.

Kwa mfano, kuna Aya nyingi za Qur’ani Tukufu, ambazo zina muelekeo wa moja kwa moja juu ya Ahadith (Hadhithu’l-Wilaya katika siku ya Ghadir; Hadith Inzar Yaumu’d-Dar; Hadithu’l-Muwakhat; Hadithus-Safina; Hadith Babu’l-Hitta n.k.) ambazo zinahusu, heshima juu yao, na umakamu wao dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hizi Bukhari ameziacha kwa uangalifu na umakini sana.

Na kwa upande mwingine, zile zinazoitwa eti ni “Hadith” ambazo zinawatweza Mitume, hususan Mtume wetu na kizazi chake kilicho safi, zimeandikwa katika kitabu chake bila hata kufikiria kidogo kwamba zimesimuliwa na waongo.

Vyanzo Vya Hadith Ya Thaqalain.

Ama kwa hadith ya Thaqalain (Vizito viwili), ambayo Bukhari hakuiandika katika kitabu chake, vitabu vingine sahihi vya madhehebu yenu vimeisimulia. Kusema kweli, hata yule mwanahadith mkubwa, Muslim, ambaye anafikiriwa kuwa sawa na Bukhari, yeye pia ameisimulia.

Wanachuo wengine ambao wameisimulia hadith hii ni hawa wafuatao: Muslim bin Hajaji katika “Sahih” yake Juz. 7, uk. 122; Abu Dawud katika “Sahih” yake; Tirmidhi katika “Sunan” yake, sehemu ya 2, uk. 307; Nisa’i katika “Khasa’is” yake uk. 30; Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad” yake Juz. 3, uk. 14-17, Juz. 4, uk. 26 na 59 na Juz. 5, uk. 182 na 189; Hakim katika “Mustadrak” Juz. 3, uk. 109 na 148; Hafidh Abu Nu’aim Isfahani katika Hilyatu’l-Auliya, Juz. 1, uk. 355; Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira yake, uk. 182; Ibn Athir Jazari katika “Usudu’l-Ghaiba”, Juz. 2, uk. 12 na Juz. 3, uk. 147; Hamidi katika “Jama’Baina-s-Sahihain” Razin katika “Jama’Baina-s-Siha-e-Sitta”; Tabran katika “Tarikh al-Kabir”; Dhahabi katika Talkh is-e-Mustadrak. Ibn Abd Rabbih katika “Iqdu’l-Faridh” yake; Muhammad bin Talha Shafi’i katika “Matalibu’s-Su’ul”; Khatib Khawarizmi katika “Manaqib” Sulayman Balkhi Hanafi kati- ka “Yanabiu’l-Mawaddatu”, uk. 18, 25, 29, 30, 31, 32, 34, 95, 115, 126, 199 na 230, pamo- ja na tofauti ndogo katika maneno; Mir Seyyid Ali Hamadani katika “Mawadda” ya pili ya “Mawaddatu’l-Qurba;” Ibn Abi-l-Hadid katika “Sherh Nahju’l- Balaghah”; Shablanji katika “Nuru’l-Absar” uk. 99; Nuru’d-Din Sabbagh Maliki katika “Fusulu’l- Muhimma” uk. 25; Hamwaini katika “Fara’idu’s-Simtain”; Imam Tha’labi katika “Tafsir Kasfu’l-Bayan”; Sam’ani na Ibn Maghazili Shafi’i katika “Manaqib”; Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’l-Talib”, Sura ya 1, katika maelezo ya usahihi wa Khutuba ya Ghadir Khum na vilevile katika Sura 62, uk. 130; Muhammad bin Sa’ad Khatib katika “Tabaqat”, Juz. 4, uk. 8; Fakhru’d-Din Razi katika “Tafsir Kabir” Juz. 3, chini ya Aya I’tisma (3:103), uk. 18; Ibn Kathir Damishqi katika “Tasfir” Juz. 4 chini ya aya ya Mawadda (42:23), uk. 113, Ibn Hajar Makki katika “Sawa’iq-e-Muhriqah” uk. 75, 87, 90, 99 na 136 pamoja na tofauti ya maneno.

Kuna wanachuo wengine kadhaa wa madhehebu yenu ambao majina yao siwezi kuyataja katika mkutano huu kutokana na uhaba wa muda. Wengi wa wanachuo wenu wameisimulia hadith hii muhimu kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa wingi sana na kwa mfu- atano usiokatika wa usimuliaji kutoka kwa mmoja hadi mwingine kiasi kwamba imepata hadhi ya hadith inayosimuliwa mara kwa mara.

Kwa mujibu wa hadith hii, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema yafuatayo: “Ninaacha kati yenu vitu viwili vizito; Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Ahlul-Bait wangu. Kama mtaambatana na viwili hivi, kamwe, kamwe hamtapotea. Viwili hivi havitatengana mpaka vije vinifikie kwenye Haudhi ya Kauthar.”

Kwa msingi wa hadith hii Sahihi, tunaona kwamba yatupasa kutafuta mshikamano kwenye Qur’ani Tukufu na Ahlul-Bait wa Muhammad (s.a.w.w.).

Sheikh: Hadith hii ya Mtume imesimuiliwa na Salih bin Musa bin Abdullah bin Ishaq, kupitia nyororo yake ya wasimuliaji waaminifu, akisema kwamba Abu Huraira ameisimulia katika njia hii: “Ninakuachieni vitu viwili vizito: Kitabu cha Allah (Qur’ani Tukufu) na Sunna zangu (Mwenendo)….”

Muombezi: Unanukuu tena hadith kutoka kwa mkorofi yule yule ambaye amepuuzwa na wakosoaji wa Shi’a (Kama Dhahabi, Yahaya, Imam Nisai, Bukhari na Ibn Adi, n.k.). Je, hutosheki na rejea za kuaminika ambazo nimezifanya kutoka Maulamaa wenu wenyewe wakubwa kuhusu hadith hii? Unanukuu maneno yasiyokubalika ya Hadith japokuwa Mashi’a na Masunni wote kwa pamoja wamekubali kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ametumia maneno, “Kitabu cha Allah na kizazi changu”, na sio “Sunna zangu.”

Kusema kweli “Kitabu” (Qur’ani) na “Sunna” (mwenendo) vyote vinahitaji tafsir. Kwa hiyo Sunna haiwezi kuelezea Qur’ani Tukufu.

Hivyo kizazi cha Mtume ambao ndio sawa na Qur’ani Tukufu ndio Wafasir halisi wa Qur’ani Tukufu na Sunna za Mtume (s.a.w.w.) vilevile. Hadith Ya Safina.

Sababu nyingine inayotufanya tutafute kushikamana na kizazi cha Mtume ni hadith sahih, “Hadith ya Safina”, ambayo imesimuliwa na Maulamaa wenu wote wakubwa, takriban bila kuacha hata mmoja, na mlolongo usiovunjika.

Zaidi ya Wanachuo wenu mia moja wenyewe wameisimulia hadith hii: Muslim bin Hajjaj katika “Sahih” yake, Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad”, Hafidh Abu Nu’aim kati- ka “Hilyatu’l-Auliya.” Ibn Abdi’l-Birr katika “Isti’ab.” Abu Bakar Khatib Baghdadi kati- ka “Ta’rikh Baghdad”; Mohammed bin Talha, Shafi’i katika “Matalibu’s-Suul;” Ibn Athir katika “Nihaya” Sibti Ibn Jauzi katika “Tadhkira”; Ibn Sabbagh Makki katika “Fusulu’l- Muhimma”; Allama Nuru’d-Din Samhudi katika “Ta’rikhu’l-Madina” Sayyid Mu’min Shablanji katika “Nuru’l-Absar;” Imam Fakhni’d-Din Razi katika “Tafsir Mafatihu’l- Ghaib”, Jalalu’d-Din Sayuti katika “Durru’l-Manthur”; Imam Tha’labi katika “Tafsir Kasfu’l-Bayan”, Tabrani katika “Ausat”; Hakim katika “Mustadrak” Juz. 3, uk, 151; Sulayman Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 4, Mir Seyyid Ali Hamadani katika “Mawaddatu’l-Kurba” Mawadda ya 2; Ibn Hajar Makki katika “Sawa’iqu’l-Muhrikah” chini ya Aya 8; Tabari katika “Tafsir” yake, na vilevile katika “Tarikh” yake; Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’l-Talib.” Sura ya 100, uk. 233.

Maulamaa wengine wengi wa madhehebu yenu wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mfano wa Ahlul-Bait wangu ni ule wa Safina ya Nuh. Ambaye ataipanda ataokolewa; ambaye anaipa mgongo atazama na kuangamia.”

Imam Muhammad bin Idris Shafi’i amerejea kwenye Hadith hii Sahih katika beti zake za mashairi ambazo Allama Fazil Ajib ameziandika katika “Dhakhiratu’l-Ma’al.” Imam Shafi’i, ambaye anatambuliwa kama mmoja wa wanachuo maarufu wa madhehebu ya Suni, anakiri kwamba, kushikamana kwetu na familia iliyotoharishwa ya Mtume ni njia ya wokovu wetu kwa sababu, kati ya Madhehebu sabini za Uislam, ile madhehebu ambayo inafuata kizazi cha Mtume ndiyo peke yake itakayopata wokovu.

Kutafuta Njia Ya Kumfikia Allah Sio Ushirikina.

Umesema kwamba kutafuta njia ya kumfikia Allah ni ushirikina. Kama hii ilikuwa kweli, kwa nini Umar bin Khatib alitafuta msaada wa Allah (swt.) kupitia kwa kizazi cha Mtume?

Hafidh: Khalifa Umar kamwe hajafanya hivyo.

Muombezi: Katika nyakati za shida Umar alitafuta msaada wa kizazi cha Mtume, Alimwomba Allah kupitia kwao, na mahitaji yake yalitekelezwa. Ninarejea kwenye matukio mawili tu. Ibn Hajar Makki anaandika katika “Sawa’iq-e-Muhriqah,” baada ya Aya ya 14 (kutoka kwenye Tarikh Damascus) kwamba katika mwaka wa 17 Hijria watu waliswali kwa ajili ya kuomba mvua lakini hawakufanikiwa.

Khalifa Umar akasema kwamba angesali kwa ajili ya mvua siku ifuatayo kupitia njia ya kumfikia Allah. Asubuhui yake alikwenda kwa Abbas, ami yake Mtume na akasema: “Toka nje ili tuweze kumuomba Allah kupitia kwako kwa ajili ya mvua.”

Abbas alimuomba Umar akae kidogo ili kwamba hio njia ya kufikia kwa Allah ipatikane. Basi, Bani Hashim (Ahlul-Bait) walijulishwa. Kisha Abbas akatoka nje pamoja na Ali, Imam Hassan na Imam Husein. Bani Hashim wengine walikuwa nyuma yao. Abbas akamwambia Umar kwamba mtu yoyote mwingine asiongezwe kwenye kundi lao.

Kisha walikwenda sehemu ya kuombea ambapo Abbas alinyanyua mikono yake kwa ajili ya maombi na akasema: “Ya Allah! Wewe ndio umetuumba sisi, na unajua kuhusu vitendo vyetu. Ya Allah! Kama ulivyokuwa Mwema kwetu mwanzoni, hivyo kuwa Mwema kwetu mwishoni.” Jabir anasema kwamba du’a yao ilikuwa bado haijakwisha wakati mawingu yalipojitokeza na ikaanza kunyesha. Kabla hawajafika nyumbani kwao, walikwishalowa.

Bukhari pia anasimulia kwamba, siku moja wakati wa ukame Umar bin Khatib alimuom- ba Allah kupitia kwa Abbas bin Abdu’l-Muttalib na akasema: “Tunatuma maombi sisi wenyewe kupitia kwa ami yake Mtume wetu; hivyo, Mwenyezi Mungu tunyeshee mvua.” Kisha ilianza kunyesha. Ibn Abi’l-Hadid Mutazili katika “Sherhe Nahju’l-Balaghah” (Chapa ya Misri), uk. 256, anaandika kwamba Khalifa Umar alikwenda pamoja na Abbas, ami yake Mtume, kumuomba Allah kwa ajili ya mvua.

Katika maombi yake kwa ajili ya mvua, Khalifa Umar alisema: “Ya Allah! Tunaleta maombi wenyewe kupitia kwa ami yake Mtume Wako, na kwa jadi yake na kwa watu wao maarufu waliobakia. Hivyo linda cheo cha Mtume wako kupitia kwa Ami yake. Tulikuwa tumeongozwa Kwako kupitia kwa Mtume, ili kwamba tutafute msaada wao na kufanya toba.”

Kama kuwatafuta kizazi cha Mtume na kuwaendea kwa ajili ya haja zetu katika njia ya Allah ni ushirikina, basi Khalifa Umar alikuwa mshirikina wa kwanza. Kizazi cha Muhammad (s.a.w.w.), kutoka wakati wa Mtume mpaka leo hii, wamekuwa ndio njia ya kupitia (Wasilat) katika du’a na maombi yetu kwa Allah. Tunawachukulia tu kama watu wacha-Mungu sana na walio karibu mno na Allah. Kwa hiyo tunawaona wao ni njia ya kutufikisha kwa Allah. Na uthibitisho mzuri wa hili ni vitabu vyetu vya Dua zilizoelezwa na Maimam wetu Ma’asum. Tunakubali maelekezo ya Maimam wetu.

Hapa ninavyo vitabu viwili: “Zadu’l-Ma’ad” cha Allama Majlisi na “Hidayatuz-Za’irin” cha Sheikh Abbas Qummi, ambavyo ninavitoa kwako ili uvichunguze. (Wote wawili Hafidh na Sheikh walichunguza vitabu vile). Waliisoma Du’a ya Tawassul, na waliona kwamba Ahlul-Bait wa Mtume walikuwa ni sehemu ya du’a. Kila mahali walikuwa wametajwa kama njia ya kufikia kwa Allah.

Katika muda ule Mulla Abdu’l-Hayy alisoma Du’a yote ya Tawassul, iliyoelezwa na Maimam watoharifu na kunukuliwa na Muhammad bin Babawayh Qummi. Dua Ya Tawassul.

Haya ni maombi kwa Allah. Kama Ali ambavyo ametajwa hapa, na Maimam wote wametajwa kwa hali hiyo hiyo. Athari ya Ahlul-Bait wa Mtume inatafutwa kutufikisha kwa Allah. Wanatajwa namna hii: “Ewe Bwana wetu na kiongozi wetu! Tunatafuta msaada wako wa kutufikisha kwa Allah. Ewe unayeheshimika zaidi mbele ya Allah: Tuombee sisi Kwake.” Ahli Bait wote wa Mtume wametajwa katika hali hiyo hiyo.

Mashia Hawawasingizii Masunni.

Wakati du’a hii ilipokuwa ikisomwa, baadhi ya mabwana waungwana wa Kisuni waliguta kwa mshangao na butwaa na masikitiko juu ya kutoelewana kukubwa kulikosababiwa na watu. Muombezi akauliza: Je, kuna dalili yoyote ya ushirikina katika du’a hii? Je, jina tukufu la Allah halipatikani kila mahali? Ni watu wenu wangapi wasioelewa na wasio wavumilivu ambao wamewauwa Mashi’a wa watu masikini, wakiamini kwamba wameua mshirikina? Lawama juu ya mambo haya moja kwa moja ni juu ya maulamaa kama ninyi wenyewe.

Je, umewahi kusikia hata siku moja kwamba Shi’a mmoja amemuua Sunni? Ukweli ni kwamba maulamaa wa Kishi’a hawaenezi sumu.

Hawajengi chuki baina ya Shi’a na Sunni, na wanaona kuua kwamba ni dhambi kubwa. Katika mambo ya tofauti ya imani kati yao, wanafafanua misimamo kwa majadiliano yaliyojengeka juu ya msingi wa elimu na mantiki, na kufanya ijulikane kutokana na mazungumzo yao kwamba Sunni ni ndugu zao.

Maulamaa Wa Kisuni Wanawaita Mashi’a Makafiri.

Kwa upande mwingine, matendo ya maulamaa mashabiki wa Sunni wanafaa kuangaliwa. Wafuasi wa Abu Hanifa, Maliki bin Anas, Muhammad bin Idris Shafi’i na Ahmad bin Hanbal, ambao wanazo tofauti za wazi kabisa, wanawaita wafuasi wa Ali bin Abi Talib na Imam Ja’far bin Muhammad makafiri na washirikina.

Wanachuoni wengi wakubwa na wacha Mungu wa Kishi’a waliuwawa mashahidi kwa fat’wa zilizotolewa na Maulamaa wa Kisuni. Kinyume chake hakuna mfano wa ukatili kama huo kwa upande wa Ulamaa wa Kishi’a. Maulamaaa wenu mara kwa mara hutoa maneno ya kuwalaani Mashia, lakini hutaona popote laana juu ya Masunni katika vitabu vilivyoandikwa na Maulamaa wa Kishi’a.

Hafidh: Hutendi haki. Unachochea chuki bure. Toa mfano mmoja tu wa mwanachuo wa Kishi’a aliyeuwawa kwa hukumu ya maulamaa wetu! Nani katika Mualamaa wetu aliyetoa maneno ya laana juu ya Shi’a?

Muombezi: Kama ingekuwa nielezee kirefu matendo ya Maulamaa wenu au ya watu wenu wa kawaida, mkutano mmoja usingekuwa mrefu wa kutosha. Nitarejea tu kwenye mifano michache yenye kuhusiana na matendo yao ili ujue kwamba mimi sichochei chuki, bali naonyesha ukweli.

Kama utavichunguza vitabu vya Maulamaa wenu mashabiki, utaona sehemu ambazo wamelaani Mashi’a. Kwa mfano, angalia vitabu vya Tafsiri vya Imam Fakhrud-Din Razi.

Wakati anapopata wasaa tu, kwa mfano kuhusiana na Aya za Wilayat, huandika kwa kurudia rudia: “Laana iwe juu ya Marafidhi, laana iwe juu ya Marafidhi,” lakini maulamaa wetu hata mara moja hawajaandika mambo kama hayo juu ya ndugu zetu Masunni.

Mfano wa vitendo vya kikatili vya maulamaa wenu kuhusu maulamaa wa Kishi’a ni zile hukumu ya Makadhi wakubwa wawili wa Syria (Burhanud-Din Maliki na Ibad bin Jama’at Shafi’i) dhidi ya mmoja wa Mwanasheria (Faqih) mkubwa, Abu Abdullah Muhammad bin Jamalu’d-bin Makki Amili.

Mwanachuo yule mkubwa alikuwa akijulikana katika wakati wake kwa ucha Mungu wake na elimu ya Sheria.

Mfano wa uwanachuo wake ni kitabu chake, “Lum’a,” ambacho alikiandika kwa muda wa siku saba bila kuwa na kitabu chochote mkononi mwake juu ya Sheria (Fiqih) isipokuwa “Mukhtasar Nafi’.” Zaidi ya hayo, wanachuo wa madhehebu haya manne (Hanafi, Maliki, Shafi’i na Hanbal) walikuwa miongoni mwa wanafunzi wake.

Kwa sababu ya maonevu ya Massuni, mara kwa mara alifanya Taqiyya (kujigeuza na kuficha mwelekeo wakati wa hatari), na hakutangaza Ushi’a wake waziwazi. Kadhi Mkuu wa Syria, Ibad bin Jama’at, ambaye ameweka uhusuda dhidi yake, alimzungumza vibaya kwa mtawala wa Syria (Baidmar) na akamshutumu kuwa yeye ni Rafidhi na Shi’a.

Mwanachuo huyu maarufu akatiwa nguvuni.Baada ya kutaabikia ufungwa na mateso ya mwaka mmoja, kwa fat’wa ya Makadhi hawa wawili (Ibnu’l-Jama’at na Burhanud-Din) yeye akauawa na mwili wake ukatundikwa kwenye kiunzi. Kwa vile walitangaza kwamba kuna Rafidh ni Kafiri yuko juu ya miti ya kunyongea, watu wa kawaida waliupiga mawe mwili ule. Baadae, mwili ule ulichomwa na jivu lake likasambazwa.

Miongoni mwa maulamaa na wanasheria wa Kishi’a wa kujivunia wa Syria katika karne ya 10 Hijriya, alikuwa Sheikh Zainu’d-Din bin Nuru’d-bin Ali bin Ahmad Amili. Alikuwa akijulikana sana miongoni mwa marafiki na maadui kwa elimu yake na uadilifu. Akiwa mtunzi wa vitabu vingi, alijiweka mbali na ulimwengu na akaandika vitabu 200 juu ya masuala mbalimbali.

Ingawa aliishi maisha ya kujitenga, bado maulamaa wa Kisunni walijenga chuki juu yake, na wivu juu ya umaarufu wake miongoni mwa watu. Mkubwa katika wapinzani wake alikuwa Kadhi Sa’ida, ambaye aliandika kwa Mfalme Sultan Salim malalamiko yafuatayo: “Hakika kuna mtu anaishi katika jimbo la Syria ambaye ni mzushi, mtu ambaye hahusiki na mojawapo ya madhehebu manne.” Sultani Salim aliamrisha kwamba mwanasharia huyo aletwe mbele ya mahakama huko Istanbul (Uturuki). Alitiwa nguvuni ndani ya Msikiti Mtukufu wa Makka na alifanywa mfungwa siku arubaini mjini Makka.

Katika safari ya baharini kuelekea Istanbul, alikatwa kichwa na mwili wake ukatupwa baharini. Ni kichwa chake tu ndicho kilichopelekwa kwa mfalme

Waheshimiwa Mabwana! Nakuulizeni kwa shauku moyoni, kwa jina la Allah mseme iwapo mlipata kusikia tabia ya namna hiyo kwa upande wa Maulmaa wa Kishi’a dhidi ya Sunni kwa sababu ya kutofauta madhehebu ya Shi’a.

Ni hoja gani mtakayoleta kuthibitisha kwamba iwapo mtu akiacha kufuata yoyote katika madhehebu manne, yeye anakuwa ni kafiri na kwamba kuuawa kwake yeye ni wajib? Je, ni mantiki kufuata madhehebu ambayo yamekuja kuweko karne kadhaa baada ya Mtume, ambapo wale wanaofuata kanuni iliyokuwepo tangu wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wanaamriwa wauawe?

Mashia Na Madhehebu Manne Ya Sunni.

Tafadhali hebu semeni kwa jina la Allah, iwapo hawa Maimam wanne Abu Hanafi, Malik, Shafi’i na Hanbal, walikuwa hai wakati wa uhai wa Mtume. Je, waliipata misingi ya dini kutoka kwa Mtume moja kwa moja?

Hafidh: Hakuna hata mmoja aliyedai hayo kuwa hivyo.

Muombezi: Je, Amir’l-Mu’minin Ali hakuwa mwenzi wa wakati wote wa Mtume, na je, hakutangaza kuwa Yeye ni lango la Jiji la Elimu?

Hafidh: Yeye kwa hakika alikuwa mmoja kati ya masahaba maarufu sana wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na katika hali zingine yeye alikuwa ni mbora kuliko wao wote.

Muombezi: Je, hivi hatuna haki, kwa hiyo, ya kushikilia kwamba kumfuata Ali ni wajibu? Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alisema kwamba kumtii Ali ni sawa na kumtii yeye na kwamba yeye Ali alikuwa ni Lango la Elimu? Vile vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba yoyote yule anayetaka kupata elimu yapasa aende kwenye mlango wa Ali.

Vilevile, kwa mujibu wa “Hadith ath-Thaqalain” na “Hadith as-Safina,” ambazo zinatambuliwa na wote Sunni na Shi’a kugeuka kutoka kwenye njia iliyoonyeshwa na Ahlul-Bait wa Mtume itatuongozea kwenye maangamizi. Utovu wa utii, au uadui dhidi ya Ahlul-Bait wa Mtume ni sawa sawa na utovu wa utii kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe.

Licha ya yote haya, Maulamaa wa Kishi’a hawajaonyesha ukosa subira wa namna hiyo kwa angalau hata Sunni wa kawaida, achilia mbali kwa maulamaa wao. Tulikuwa siku zote tukiwasihi Mashi’a kwamba Masunni ni ndugu zetu katika Uislamu na yatupasa kubakia tumeungana (yaani kulinda umoja wetu).

Kwa upande mwingine mara kwa mara maulamaa wa Kisunni wamekuwa wakiwachochea watu wao, wakisema kwamba Mashi’a ni wazushi, Marafidhi,Ghullat, au Mayahudi. Wanasema kwamba, kwa kuwa hawa Shi’a hawafuati mmoja katika Maimam wanne wa Kisunni (Abu Hanifa, Malikki, Shafi’i na Hanbali), basi ni makafiri. Ukweli ni kwamba wale wanaowafuata Ahlul-Bait wa Mtume (s.a.w.w.) wameongozwa sawasawa.

Mauaji Ya Mashi’a Huko Irani Na Afghanistan.

Waturuki, Bani Khawarizim, Wa-Uzbeg na wa-Afghan waliwateka nyara na kuwauwa Mashi’a wasio na hatia. Muhammad Amin Khan Uzbeg, ajulikanaye kwa jina la Khan Khawa, na Abdullah Khan Uzbeg waliwaua kikatili na kuwapora Mashi’a na wakakiri kuwa wamelifanya hilo.

Maulamaa wa Kisunni walitangaza kwamba Mashi’a ni makafiri na kwamba wanaweza kuuawa kwa mjibu wa ya dini. Ma-Amiri (viongozi) wa Afghanistani waliwatendea Mashi’a kwa namna hiyo hiyo.

Katika mwaka wa 1267 Hijiriyya siku ya Ashura (Mwezi 10 Muharam), Masunni walishambulia ukumbi katika Qandahar, ambako Mashi’a walikuwa wanaomboleza mauaji ya mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Waliwaua Mashi’a wengi kwa ukatili mkubwa, wakiwemo watoto, na wakapora mali zao. Kwa miaka mingi Mashi’a waliishi maisha ya dhiki na walikatazwa kuendesha ibada zao za kidini.

Katika siku ya Ashura wachache wao walikwenda kwenye kumbi za siri na waliombeleza mauaji ya Imam Husein (A.S) kisirisiri kabisa, na wale wengine walikuwa wakichinjwa kwenye nyanda za Karbala. Ilikuwa ni Mfalme Amanullah Khan aliyeondoa kikwazo hicho juu ya Shi’a na akawatendea upole.

Kuuwawa Shahidi Kwa Shahid Thalis.

Katika makaburi ya Akbarabad (Agra) India, pale amelala Mwanachuo Mchamungu mno wa Kishi’a, Qadhi Seyyid Nurullah Shustari. Aliuawa kishenzi sana akiwa na umri wa miaka 70 katika mwaka wa 1019 Hijiriya na Mfalme Jahangir, kufuatia fat’wa kutoka kwa wanachuo wa Kisunni kwamba Yeye alikuwa Rafidh.

Hafidh: Unatushambulia (kwa maneno) bila sababu yoyote. Mimi mwenyewe nimeshtushwa mno kusikia vitendo vya kuchukiza mno vya watu wajinga, lakini matendo ya Mashi’a pia yalikuwa yanahusika na matukio haya.

Muombezi: Unaweza kunieleza ni matendo gani ya Mashi’a ambayo yalifanya kuwa halali kwao kuuwawa?

Hafidh: Kila siku maelfu ya watu wanasimama mbele za makaburi ya waliokufa na kuwaomba msaada. Je, kitendo hiki sio mfano wa kuabudu wafu? Kwa nini Maulamaa wasikataze wakati mamilioni ya watu hao wakiweka mapaji yao ya nyuso zao kwenye ardhi wakisujudu katika kuwaabudu wafu? Nashangaa ni kwa vipi bado unayaita mambo haya kuwa sio shirki.

Wakati majadiliano na Mawalana Hafidh yakiendelea, faqihi wa Kihanafi, Agha Sheikh Abdus-Salam alikuwa anakichunguza Hidayatuz-Za’irin. Akasema kwa msisitizo mzito, “Tazama hapa! (akikionyesha kile kitabu).

Ulamaa wako anasema kwamba wakati mahujaji wanapomaliza Ziarat katika Makuba ya Maimam, wanapaswa kuswali rakaa mbili za Sala ya Ziarat.

Huenda hawaikusudii Sala hii kwa jina la Allah; vinginevyo, nini maana ya Sala ya Ziarat? Huu sio ushirikina kufanya ibada ya Sala kwa ajili ya Imam? Mahujaji wanaosimama na kuelekeza nyuso zao kwenye makaburi na kusali ni ushahidi mzuri wa ushirikina. Hiki ni kitabu chenu Sahihi. Unaweza ukatetea hali yenu hii?”

Muombezi: Mbona unajiingiza katika mazungumzo ya kitoto! Hivi umewahi kuwako kwenye Ziarat hizo na kuwaona Mahujaji hao ana kwa ana?

Sheikh: Hapana.

Muombezi: Sasa ni vipi ukaweza kusema kwamba mahujaji hao wanaswali wakiwa wameelekeza nyuso zao kwenye kaburi, na kusema kwamba swala hii ya Ziarat ni dalili ya ushirikina?

Sheikh: Kitabu hiki kinasema kwamba waswali Swala ya Ziarat kwa ajili ya Imam.

Muombezi: Hebu lete hicho kitabu nikiangalie. Ngoja nisome maelekezo kuhusu Ziarat, mpaka tufikie kipengele cha Sala ambacho ndio hoja ya kukataa kwako. Wakati wowote ukiona dalili ya ushirikina, tafadhali ionyeshe. Na iwapo utaona alama za kuamini na kuabudu Mungu Mmoja kuanzia juu mpaka chini usije ukajisikia vibaya kwa hilo, bali sema kwamba ulikuwa umeelewa vibaya. Kitabu kiko hapa mbele yenu.

Maelekezo Kuhusu Ziarat:

Maekelezo ni kama yafutayo: “Wakati mwenye kufanya Ziarat afikapo handaki la Kufa, anasimama pale na kusoma kisomo kifuatacho” Allah ni Mkubwa mno, Allah ni mkubwa mno Mwenye ukubwa, Utukufu, Sifa njema, na rehema. Allah ni Mkubwa Mno juu zaidi ya kile ambacho nakiogopa. Allah ni Mkubwa mno. Yeye ni msaada wangu; Kwake Yeye nategemea na Kwake Yeye yako matumaini yangu na Kwake Yeye naelekea.’ Wakati mwenye kufanya Ziarat akifika lango la Najaf, yampasa kusoma: ‘Sifa zote njema ni za Allah, ambaye ametuongoza katika hili, tusingekuwa ni wenye kuongoka kama Allah asingetuongoza.’ Wakati akifika lango la Uwanja wa Mtukufu yampasa asome, baada ya kumtukuza Allah:

‘Nashuhudia kwamba hakuna Mungu isipokuwa Allah, aliye Mmoja. Yeye hana mshirika. Na pia ninashuhudia kwamba, Muhammad ni mja na Mtume Wake.

Ametuletea kweli kutoka kwa Allah. Na pia nashuhudia kwamba Ali ni mja wa Allah na ndugu yake Mtume wa Allah. Allah ni mkubwa mno, Allah ni mkubwa mno, Allah ni Mkubwa mno. Hakuna Mungu isipokuwa Allah, na Allah ni Mkubwa mno. Shukrani zote ni Zake kwa mwongozo na msaada Wake kuitikia kile alichofunua juu ya njia kuelekea Kwake.’

Wakati Mwenye kufanya Ziarat akifika kwenye lango la Quba, yampasa asome: ‘Ninashuhudia kwamba hakuna Mungu isipokuwa Allah, aliye Mmoja. Yeye hana Mshirika pamoja Naye…’ mpaka mwisho.

Wakati, baada ya kwisha kuomba ruhusa ya Allah, ya Mtume, na ya Maimam, mwenye kufanya Ziarat hufika ndani ya Quba, husoma Ziarat mbalimbali ambazo zina maamkuzi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kwa Amir’l-Mu’minin. Baada ya Ziarat, husali rakaa sita (za Sunna), rakaa mbili kwa ajili ya Amir’l- Mu’minin na rakaa mbili kwa ajili ya Nabii Adam na mbili kwa ajili ya Nabii Nuh ambao wamezikwa katika eneo hilo hilo.”

Salat-Ziarat Na Dua Baada Ya Sala.

Je, utekelezaji wa ibada ya Sala kama sadaka kwa ajili ya roho za wazazi na waumini wengine, haikuamrishwa juu yetu? Je, maamrisho haya ni ushirikina? Vilevile ni kwa ajili ya ubinaadamu kwamba wakati mtu anapokwenda kumuona rafiki humpatia zawadi fulani. Kuna Sura katika vitabu vya Madhehebu zote ambamo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anatuamrisha kutoa zawadi kuwapa waumini.

Hivyo mwenye kufanya Ziara anapofika kwenye kaburi la mpendwa bwana wake na anajua kwamba kitu alichokuwa amekipenda zaidi ilikuwa ni Sala, anasali rakaa mbili katika njia yake ya kufikia kwa Allah na anaitoa Sala ile kama zawadi kwa ajili ya roho ya bwana wake huyo. Je, huo ni ushirikina? Baada ya kusoma kanuni za msingi wa Sala hii, pia soma du’a iliyoko baada ya Sala, ili kwamba mashaka yako yote yaondoke.

Du’a Baada Ya Sala:

Ibada ya Dua ni kwamba baada ya kumaliza Sala katika kichwa cha kaburi la Imam aliyezikwa pale, na nyuso zetu kuelekea Kibla (sio kuelekea kwenye kaburi), tunasoma du’a ifuatayo, “Ewe Allah! Sala hii nimeifanya zawadi kwa bwana na kiongozi wangu, Mtume Wako na ndugu yake Mtume Wako, Amir’l- Mu’minin Ali bin Abu Talib.

Ewe Allah, teremsha rehema na amani Yako juu ya Muhammad na kizazi chake. Zikubali rakaa mbili hizi za Sala kutoka kwangu na unijazi, kama ambavyo ungewajazi watendaji wa matendo mema.

Ewe Allah! Nimeitoa Sala hii (kama Sadaka) kwa ajili Yako, na nimerukuu na kusujudu mbele yako Wewe kwa kunyenyekea Kwako. Wewe ni Mmoja ambaye huna mshirika. Hairuhusiwi kusali, kurukuu au kusujudia chochote isipokuwa Wewe. Wewe ni Allah, uliye Mkuu na hakuna mungu isipokuwa Wewe.”

Mabwana waheshimiwa! Kwa jina la Allah, kuweni waadilifu. Kuanzia muda ule mwenye kuzuru anapoweka mguu wake juu ardhi ya Najaf, mpaka baada ya kusali sala yake ya Ziarat, yeye anajishugulisha katika kumkumbuka Allah swt.

Sheikh: Inashangaza kwamba huoni yalioandikwa hapa: “Busu kizingiti cha mlango na kisha ingia ndani ya haram ya Kuba.” Tumesikia kwamba wakati wenye kufanya Ziarat wakifika kwenye mlango wa kuba la Maimam wao, wanakwenda Sijida kwa heshima. Je kusujudu huku sio kwa ajili ya Ali? Je, sio ushirikina wakati tunasujudia mwingine asiyekuwa Allah?

Muombezi: Kama mimi ndio ningekuwa ni wewe, nisingelisema neno. Ningenyamaza kimya mpaka mkutano wa mwisho wa mjadala huu na kusikiliza mantiki ya majibu yangu. Lakini nitakuambia kwa ufupi mara nyingine tena kwamba, kubusu kizingiti au sakafu ya makuba ya Maimam sio ushirikina. Umelitafsiri vibaya neno “kubusu” na kuliona kuwa ni sawa na kusujudu. Wakati unasoma kitabu hicho mbele yetu unadiriki kufanya mabadiliko ya ugeuzaji maana ya maneno kama huu, sijui ni jinsi gani utatusingizia wakati utakapokuwa peke yako ukiwahutubia watu wasio na elimu.

Maelekezo yaliyomo katika kitabu hiki na vitabu vinavyohusu Du’a na sehemu za Ziarat ni kwamba mwenye kufanya Ziarat, kama namna ya kuonyesha heshima, inampasa kubusu kizingiti sio kusujudu. Vipi unafikiria kubusu na kusujudu kuwa ni kitu kimoja? a, ni wapi umeona ima katika Qur’ani tukufu au katika hadith yoyote kwamba kubusu kizingiti cha Kuba la Mtume au Imam kumekatazwa? Hivyo kama huna jibu la maana kwa swali hili, usipoteze wakati wetu.

Na, kama unavyosema “umesikia” kwamba wafanyao Ziarat husujudu kwa heshima. Kwa uhakika hukuwaona kwa macho yako wakifanya hivi. Qur’ani tukufu inasema, “Enyi ambao kwamba mmeamini! Akikujieni fasiki na habari, ichunguzeni, msije mkadhuru watu kwa ujinga, kisha mkawa ni wenye kusikitika kwa yale muliyoyafanya.” (49:6).

Kwa mujibu wa amri hii ya Qur’ani Tukufu, hatupasi kutegemea maelezo ya watu waovu. Yatupasa kufanya juhudi kubwa kujua ukweli, hata ikiwezekana kufanya safari ili kupata habari ya kweli moja kwa moja.

Wakati nilipokuwa Baghdadi, nilikwenda kwenye makaburi ya Abu Hanifa na Sheikh Abdul’Kadir Jilani na nikaona watu walivyofanya. Ilikuwa vibaya zaidi kuliko ulivyoelezea kuhusu Mashi’a wanavyofanya, lakini kamwe sijal- izungumza hili. Nilipofika kwenye kaburi la Abu Hanifa hapo Mu’azza’m, niliona kundi la Masunni wakirudia rudia kubusu Sakafu, badala ya kizingiti, na kujigaragaza kwenye sakafu. Lakini kwa kuwa hawakuonekana kwa mahabithi, na kwa sababu sikuwa na sababu za kuwalaumu, kwamwe sikuitaja habari hii kwa mtu yoyote. Nilielewa kwamba walikuwa wakifanya hivyo kwa ajili ya mahaba sio kama ibada.

Ewe bwana mheshimiwa! Hakika hakuna Shi’a mcha-Mungu ambaye amediriki kusujudu kwa yeyote isipokuwa Allah. Kama, kwa vyovyote vile iwavyo, kama tunaanguka chini ya ardhi katika hali kama ya kusujudu na kusugua mabapa ya nyuso zetu juu yake (bila kuwa na nia ya kuabudu), hiki ni kitu kidogo sana. Kuinama mbele ya mtu mtukufu bila kumfikiria kuwa yeye ni Allah, au kuanguka chini juu ya ardhi na mtu kusugua uso wake juu yake, sio ushirikina. Ni matokeo ya mahaba makubwa.

Sheikh: Inakuwaje kwamba tunaposhuka chini juu ya ardhi na kuweka paji letu la uso juu yake, kwamba kitendo hiki kisiweze kuwa sawa na kusujudu?

Muombezi: Kusujudu kunategemea juu ya nia, na nia ni jambo la moyo. Ni Allah peke yake ndiye anayejua nia zetu za moyoni. Kwa mfano tunaweza kuona watu wamelala chini juu ya ardhi kwa hali kama ya kusujudu.

Ni kweli kwamba kusujudia yeyote asiyekuwa Allah sio sawasawa, hata ikiwa bila nia yoyote. Walakini, kwa kuwa hatujui nia za mioyo yao, hatuwezi kuiita hiyo kuwa ni Sijida ya Ibada.

Kusujudu Kwa Ndugu Zake Yusufu Mbele Yake.

Kwa hiyo, kusujudu katika hali iliyo sawa na Sijida ya ibada (lakini bila nia yake), kuonyesha heshima kwa mtu sio ushirikina. Kwa mfano nduguze Nabii Yusufu walisujudu mbele yake. Wakati huo Mitume wawili walikuwepo, Ya’qub na Yusufu, lakini hawakuwakataza kufanya hivyo. Allah (s.w.t.) Anasema katika Suratul-Yusufu ya Qur’ani Tukufu.

{ورﻓَﻊ اﺑﻮﻳﻪ ﻋﻠَ اﻟْﻌﺮشِ وﺧَﺮوا ﻟَﻪ ﺳﺠﺪًا ۖ وﻗَﺎل ﻳﺎ اﺑﺖِ ﻫٰﺬَا ﺗَﺎوِﻳﻞ روﻳﺎي ﻣﻦ ﻗَﺒﻞ ﻗَﺪْ ﺟﻌﻠَﻬﺎ رﺑِ ﺣﻘﺎ ۖ{100

“Na aliwainua wazazi wake na kuwaweka katika kiti cha Ufalme, na wote wakaporomoka kumsujudia, na akasema; “Ewe Baba yangu, hii ndiyo hakika ya ndoto yangu ya zamani; bila shaka Mola wangu ameithibitisha …..” (12:100).

Aidha, Qur’ani Tukufu inasema katika sehemu nyingi kwamba Malaika walifanya Sajida mbele ya Mtume Adam. Hivyo kama kusujudu namna hiyo ni ushirikina, basi nduguze Mtume Yusufu na Malaika wa Allah walikuwa washirikina. Ni Iblis aliyelaaniwa peke yake ndiye ambaye hakuwa mshirikina! Kuwaomba Maimamu Sio Kuwaabudu Wafu.

Sasa napenda kumjibu Mheshimiwa Hafidh, ambaye amesema kwamba maombi mbele ya makaburi ya Maimam ni sawa sawa na kuwaabudu wafu. Unauliza kwa nini Mashi’a wanaomba msaada kwenye makaburi ya Maimam. Pengine unaamini kwamba hakuna maisha baada ya kifo na unasema: “Kilicho kufa kimeangamia moja kwa moja.” Allah (s.w.t.) anaelezea katika Qur’ani Tukufu mawazo potovu haya,

Anasema:

{انْ ﻫ ا ﺣﻴﺎﺗُﻨَﺎ اﻟﺪﱡﻧْﻴﺎ ﻧَﻤﻮت وﻧَﺤﻴﺎ وﻣﺎ ﻧَﺤﻦ ﺑِﻤﺒﻌﻮﺛﻴﻦ {37

“Hakuna ila maisha yetu haya ya dunia, tunakufa na kuishi, basi, wala sisi si wenye kufufuliwa.” (23:37).

Kama mjuavyo nyote, wale wanaoamini katika Allah wanajua kwamba kuna maisha baada ya kifo. Wakati mwanadamu akifa, mwili wake unakuwa hauna uhai, lakini, tofauti na wanyama, roho na hisia ya kusema hubakia katika viwiliwili vilivyo sawa na hivi, lakini halisi zaidi na watarehemiwa au kuadhibiwa katika hali ya mpito (barzakh) au mahali pa mateso.

Mashahidi na wale waliouawa katika njia ya Allah watafurahia neema maalum. Hii imesimuliwa katika Qur’ani Tukufu:

“Na usiwadhanie wale waliouawa katika njia ya Allah kuwa ni wafu; bali wahai na wanaruzukiwa kwa Mola wao, wanafurahia aliyowapa Allah kwa fadhila zake, na wanafurahia kwa hilo hilo wale ambao wameachwa nyuma yao, bado hajajiunga nao; ya kwamba haitakuwa hofu juu yao wala hawatahuzunika.” (3: 169-170).

Ninatafakari juu ya maneno haya: “Wahai (na) wanaruzukiwa kwa Mola wao……” (3: 169) Wao wanatujibu, lakini kwa vile kusikia kwetu kumefunga kwa mapazia ya ulimwengu wa kimaada hatusikii sauti zao. Kwa ajili hiyo katika salaam (ziarat) kwa Imam Husein, tunasema; “Ninashuhudia kwamba unasikia ninayosema na kwamba unajibu.” Je, umesoma Khutuba na 85 katika Nahju’l-Balagha? Kizazi cha Mtume wametambulishwa kama ifuatavyo: “Enyi watu huu ni usemi wa Mtume:

Yeyote anayekufa miongoni mwetu sio mfu, na yeyote ambaye anaoza (baada ya kufa) kutoka miongoni mwetu kwa hakika haozi.’” (Nahjul-Balaghah Tarjuma ya Kiingereza, Juz. 1, uk. 130 iliyochapishwa na Peer Muhammad Ebrahim Trust, Karachi.) Hivyo ni kwamba, katika uwanja wa mwanga na mambo ya Kiroho, Ahlul-Bait wanaishi na wanabakia wenye kudumu milele.

Kwa ajili hiyo, Ibn Abi’l-Hadid Mutazali na Sheikh Muhammad Abdul, Mufti mashuhuri wa Misri, wakisherehesha hadith hiyo hapo juu, wanasema kwamba, dhuria wa Mtume (s.a.w.w.) hawakufa kwa namna walivyokufa wengine. Hivyo tunaposimama mbele ya makaburi ya Maimam, hatusimami mbele za wafu, na hatuzugumzi wafu. Tunasimama mbele za walio hai na kuzungumza na wanaoishi. Kwa ajili hiyo sisi sio waabuduo wafu.

Tunamuabudu Allah. Je huamini kwamba Imam Ali, Imam Husain, na mashahidi wa Badr, Hunain, Uhud na Karbala walitoa muhanga maisha yao katika njia ya Allah kwa ajili ya haki? Je, hawakuwakabili madhalimu wa Kiquraishi, Bani Umayya, Yazid na wafuasi wake, ambao lengo lao lilikuwa ni kuifulitia mbali Dini.

Kama vile ule uimara wa masahaba wa Mtume na mihanga ya mashahidi wa Badri, Hunain, na Uhud ulivyopelekea kushindwa kwa ukafiri, kwa njia hiyo hiyo uamuzi imara wa Imam Husain kutoa mhanga maisha yake, uliimarisha Uislamu. Kama Imam asingesimama imara dhidi ya nguvu za uovu, mwana kulaaniwa Yazid angeuharibu Uislamu na angeweza kupenyeza ukafiri wake katika Umma wa Kiislamu.

Sheikh: Inashangaza kwamba, unamwita Khalifa wa Waislamu Yazid bin Mu’awiya kuwa ni kafir. Yakupasa uelewe kwamba Mu’awiya bin Abu Sufyan alimchagua yeye kuwa Khalifa. Khalifa wa Pili Umar bin Khattab na Khalifa wa tatu Uthman aliyedhulimiwa, walimchagua Mu’awiya kuwa Amir (Gavana) wa Syria. Kwa sababu ya uwezo na vipaji vyao, watu waliwakubali kuwa Makhalifa kwa uaminifu kabisa.

Hivyo uhusishaji wako wa makhalifa wa Uislamu kuwa ni makafiri una maana kwamba hukuwatukana tu Waislamu wote ambao wamewakubali kama makhalifa, bali vile vile umewatukana Makhalifa waliopita ambao wamewaidhinisha wao kuwa makhalifa au magavana. Kwa kweli walifanya makosa, ambayo yalitokea wakati wa ukhalifa wao.

Mjukuu wa Mtume, Imam Husain, aliuwawa, lakini hili lilisamehewa. Kwa vile walitubia, Allah Mwingi wa rehema, aliwasamehe. Imam Ghazali na Damiri wameshughulika na nukta hii kwa uan- galifu kabisa katika vitabu vyao na wamethibitisha usafi wa khalifa Yazid.

Muombezi: Kamwe sikutaraji kwamba ushabiki wako utakwenda mbali kiasi hicho mpaka kutetea kusudi la mlaaniwa Yazid. Unasema kwamba kwa vile wakubwa wao waliowatangulia waliona inafaa kuwafanya ma-Amir au watawala, basi Waislam wote ili- wapasa wawakubali.

Kauli hii haileti maana yoyote. Tunasema kwamba Khalifa yapasa awe safi (aliyeepukana kabisa na madhambi yote) na kuteuliwa ki-Ungu ili kwamba tusije tukadumu katika ukandamizwaji. Unasema kwamba Ghazali na Damiri wametetea nafasi ya Yazid. Lakini walikuwa mashabiki kama ulivyo wewe.

Hakuna mtu mwenye akili timamu ambaye atathubutu kamwe kujaribu kutetea matendo ya mlaaniwa Yazid. Unasema kwamba Yazid alifanya “kosa” katika kumuua Imam Husain.

Lakini kumuuwa mtoto kipenzi mno wa Mtume, kuchanganya pamoja na watu 72, wakiwemo watoto wadogo na wazee, na kuwachukua mateka mabinti wacha-Mungu wa Mtume vichwa wazi na nyuso wazi, haikuwa “kosa” la hivi hivi tu. Ulikuwa ni ukatili usiosemeka. Aidha, jinai zake hazikuishia kwenye chinja chinja hii ya kutisha peke yake. Kuna mifano mingi mingine ya ukafiri wake.

Ukafiri Wa Yazid.

Miongoni mwa mambo yanayothibitisha ukafir wa Yazid ni beti zake mwenyewe za kishairi. Kwa mfano anaandika hivi:

“Kama kunywa (pombe) kunakatazwa katika dini ya Muhammad, basi na iwe hivyo; mimi nitaukubali Ukristo.”

“Ni ulimwengu huu tu, kwa ajili yetu. Hakuna ulimwengu mwingine. Haipasi sisi kuzuiliwa starehe za ulimwengu huu.”

Beti hizi zinajitokeza katika mkusanyiko wa kazi zake za kishairi, na Abu’l-Faraj bin Jauzi ameyaandika katika kitabu chake “Radd Ala’l-Muta’asibu’l-Anid.” Anasema tena:

“Mwenye kututishia na hekaya za siku ya mwisho, muache afanye hivyo. Haya ni mambo ya uongo, yanayotunyima sisi starehe zote za sauti na muziki.”

Sibt Ibn Jauzi anaandika katika kitabu chake “Tadhkira,” uk. 748 kwamba, wakati dhuria wa Mtume walipoletwa Syria kama mateka, Yazidi alikuwa amekaa katika ghorofa ya pili ya kasri yake. Yeye alisoma beti mbili zifuatazo:

“Wakati machela za ngamia zilizobeba wafungwa zilipotokea, kunguru alilia (ndege mbaya katika Uarabu). Nilisema: “Ewe Kunguru, kama ulie au usilie, nimelipa kisasi juu ya Mtume.”

“Kisasi” huelekeza kwenye ukweli kwamba, wazee wake na jamaa zake wa karibu wali- uawa katika vita vya Badr, Uhud, na Hunain. Aliwachukulia kisasi cha vifo vyao kwa kuwaua watoto wa Mtume.

Ushahidi mwingine wa Ukafir wake ni kwamba alipofanya hafla ya kusherehekea Shahada ya Husain, alisoma beti za Kikafir za Abdullah bin Uzza Ba’ri. Sibt Ibn Jauzi, Abu Raihan, na wengine wameandika kwamba Yazid alitamani wazee wake wangekuwepo, ambao wote walikuwa makafir, na waliuawa katika vita vya Badr kwa amri ya Mtume.

Yazid alisema: “Natamani watu wa ukoo wangu ambao waliuawa huko Badr, na wale ambao wame- waona watu wa ukoo wa Khazraj wakilia

(katika vita ya Uhud) kwa ajili ya majeraha ya michomo mikali (ya panga, mikuki na mishale), wangekuwa hapa. Wangelinishangilia kwa sauti na kusema: ‘Ewe Yazid mikono yako kamwe isipooze,’ kwa sababu nimewauwa wakuu wa ukoo wake( yaani ukoo wa Mtume). Nimefanya hivyo kama kisasi cha Badr, ambacho sasa kimekamilika.

Bani Hashim walicheza mchezo tu na serikali. Hakukuja ujumbe kutoka kwa Allah, wala ufunuo wowote. Nisingekuwa wa familia ya Khandaq kama nisingechukua kisasi juu ya dhuria wa Mtume. Tumeyalipa kisasi mauaji yaliyofanywa na Ali kwa kumuuwa mtoto wake, mpanda farasi na simba mwerevu.

Ruhusa Ya Kumlaani Yazid Iliyotolewa Na Maulamaa Wa Kisunni.

Wengi wa Maulamaa wenu wanamuona Yazid kama kafiri. Hata Imam Ahmad bin Hanbal na Maulamaa wengine wengi wakubwa wa madhehebu yenu wameshauri kwamba laana juu yake zinapaswa kuelezwa. Abdur-Rahman Abul-Faraj bin Jauzi ameandika kitabu juu ya somo hili, Kitabul-Radd Ala’l- Muta’asibu’l-Anidul-Mani’an La’n-e-Yazid La’natullah. Ni Maulamaa mashabiki wachache tu wa madhehebu yenu, kama Ghazali, wameonyesha upendeleo kwa Yazid, na wamebuni makinzano yasiyo na maana kwa ajili ya kumtetea.

Hata hivyo, wengi wa Maulmaa wenu, wameiona tabia yake isiyo ya kidini na ya kidhal- imu. Muslim anasema kwamba, kama Khalifa; Yazid alidiriki kuiangamiza dini, Mas’udi katika kitabu chake “Muruju’z- Dhahab, “Juz. 2, anasema kwamba tabia ya Yazid ilikuwa sawa na ile ya Firauni, lakini ni kwamba Firauni alikuwa muadilifu zaidi kwa watu wake kuliko alivyokuwa Yazid.

Utawala wa Yazid ulileta fedheha juu ya jina zuri la Uislam. Uovu wake ulikuwa ni pamoja na kunywa pombe, kumuua mtoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kumlaani mshika Makamu wa Mtume Ali, kubomoa nyumba ya Allah (Masjidu’l-Haram) na mauaji ya halaiki. Amefanya uhalifu usiohisabu dhidi ya Sheri ‘ah ya dini, na dhambi ambazo hazisameheki.

Nawab: Yazid alihusika vipi na mauwaji ya halaiki?

Muombezi: Wanahistoria wengi wamelisimulia jambo hili. Sibt Ibn Jauzi katika kitabu chake “Tadhkira” uk. 63, anasema kwamba baadhi ya watu wa Madina walikwenda Syria katika Mwaka wa 62 A.H. Walipoyagundua matendo maouvu ya Yazid walirudi Madina na kuvunja kiapo cha utiifu kwake, wakamlaani, wakamfukuza, gavana wake, Uthman bin Abi Sufyani. Abdullah bin Hanzala ( Ghusilu’l- Mala’ikat) alisema:

“Enyi watu, hatukuasi dhidi ya Yazidi mpaka tulipothibitisha kwamba si mtu mwenye kufuata dini. Aliua watoto wa Mtume, alnajihusisha kinyume na sheria na mama zake, binti zake, na dada zake, anakunywa pombe, na hajishughulishi na ibada ya Sala.”

Habari hizi zilipomfikia Yazid, alituma jeshi kubwa la watu wa Syria chini ya Mulsim bin Uqba dhidi ya watu wa Madina. Mauaji ya Waislamu yaliendelea kwa muda wa siku tatu. Jeshi la Yazidi liliua watu 700 waungwana wa Kikuraish, Muhajirina, na Ansar, na watu 10,000 wa kawaida.

Naona aibu kusema jinsi Waislamu walivyonyanyaswa. Nitanukuu kifungu kimoja tu katika ‘Tadhkira,’ ya Sibti Ibn Jauzi uk. 163, kilichosimuliwa na Abu’l- Hasan Mada’an:“Baada ya mauwaji ya halaiki ya watu wa Madina, wanawake 1000 wasiolewa walizaa watoto.” Je, Yazid Anapaswa Kulaaniwa?

Sheikh: Madai haya yanaonyesha madhambi yake. Madhambi yanasameheka na yanaweza kufidiwa, na Yazid alionyesha hali ya kutubia. Allah ambaye ndiye Mwenye kusamehe madhambi amemsamehe. Basi kwa nini wakati wote unamlaani na kumuita muovu?

Muombezi: Baadhi ya mawakili hubishana juu ya kesi ya wateja wao mpaka dakika ya mwisho kwa sababu wamepokea malipo kutoka kwao, ingawaje wanaelewa vizuri ustahili wa kesi yenyewe. Lakini nashindwa kuelewa kwa nini unapendelea mno kumtetea Yazid, mbele ya mauaji yake ya watoto wa Mtume wa Allah na kuwaua kwake watu wa Madina. Aidha, maelezo yako kwamba alionyesha kutubia hayathibitiki.

Je kukataa kwake misingi muhimu ya Uislamu siku ya ufufuo, Wahyi na Utume hakustahili laana yetu kwake? Je, Allah hakuwalaani madhalimu? Kama hoja hizi hazitoshi kwa mawakili wa Yazid bin Mu’awiya, kwa ruhusa yako nitanukuu hadith kutoka kwa Maulamaa wenu maarufu.

Bukhari na Muslim katika “Sahih” zao, Allama Samhudi katika “Ta’rikhu’l-Madina,” Abu’l-Faraj bin Jauzi katika Kitabu‘r-Radd Ala’l-Muta’asibul-Anid,” Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira-e-Khawasul-Umma, Imam Ahmad bin Hanbali katika “Musnad” na wengine wanamnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Kama mtu yeyote atawatishia na kuwaonea watu wa Madina, Allah atamtishia (yaani Siku ya Malipo). Atalaaniwa na Allah, Malaika, na wanadamu wote. Na katika Siku ya Malipo, Allah hatayakubali matedno yake yoyote.

Vilevile Mtume amesema: “Laana iwe juu ya yule mwenye kuutishia mji wangu (watu wa Madina).” Je, mauaji haya ya halaiki hayakuwatishia wale watu wa Madina? Kama yalifanya basi kubali pamoja na Mtume, Malaika na watu wote kwamba yule mfanya mauovu mbaya alilaaniwa na atakuwa akiendelea kulaaniwa mpaka Siku ya Kiyama.

Wengi wa ulamaa wenu wamemlaani Yazid. Abdullah bin Muhammad bin Amir Shabrawi Shafi’i katika “Kitabu’l-Ittihaf bi Hubbi’l Ashraf Raji’ba La’n-e-Yazid” uk. 20, anaandika kwamba wakati jina la Yazid lilipotajwa mbele ya Mulla Sa’d Taftazan, yeye alisema: “Laana iwe juu yake na wafuasi na wasaidizi wake.”

Allama Samhudi katika kitabu chake “Jawahirul-Iqdain” ananukuliwa akisema; “maulamaa kwa ujumla wamekubaliana kwamba, inaruhusiwa kumlaani aliyemuua Imam Husein, au aliyetoa amri ya yeye kuuliwa, au yule aliyeridhia mauaji yake, au yule aliyekubali kuuliwa kwake.”

Ibn Jauzi, Abu Ya’la na Salih bin Ahmad, wakihoji kutoka kwenye Aya za Qur’ani wanaandika kwamba: “Imethibitika kwamba imeruhusiwa kumlaani Yazid. Ni wajibu wa Waislamu wote kwamba yawapasa kujua haki alizonazo Imam Husein juu yao.

Na ni vipi, kwa nguvu ya kupatwa kwake na mateso ya udhalimu na uonevu, yeye alivyounyweshea mti wa Uislamu kwa damu yake mwenyewe na damu ya familia yake. Vinginevyo, mti ule uliobarikiwa ungekufa kwa sababu ya udhalimu wa Bani Umayyah. Alikuwa ni Husain ambaye aliupatia Uislamu uhai mpya.

Nasikitika kwamba badala ya kuitambua huduma hii ambayo watu hawa watukufu wameitoa kwa Uislamu, mnazua makinzano kuhusu wafanya ziara ambao wanazuru makaburi yao na kuwaita wenye kuabudu wafu. Mara nyingi tunasoma kwamba katika sehemu muhimu za nchi, kama Paris, London, Berlin, na Washington kuna makaburi ya kumheshimu “Askari asiyejulikana.”Inasemekana kwamba, kuteseka kwa uonevu wa adui na kwa kuihami nchi yake, alijitoa muhanga maisha yake.

Lakini hakukuwa na alama juu ya mwili wake au nguo kuonyesha utambulisho wa familia yake au mji anakotoka. Kwa sababu alitoa maisha yake kwa ajili ya kuitetea nchi yake, ingawaje alikuwa hajulikani, alistahiki heshima. Wakati mfalme au mtu yeyote mashuhuri anapotembelea miji hii, huzuru hilo kaburi la “Askari asiyejulikana” na kuweka mashada ya maua juu yake.

“Askari asiyejulikana” anapata heshima zaidi, lakini nasikitika kwamba, badala ya kuwa- heshimu wafanya Ziara wanaozuru makaburi ya wanachuoni Waislamu wacha-Mungu sisi tunawashutumu. Baadhi yao waliijua Qur’ani yote kwa moyo.

Walitoa mhanga maisha yao kuutetea Uislamu. Watu hawa ni pamoja na mawakala (wadhamini) wa Allah, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) .

Kuvunjwa Heshima Ya Makaburi:

Baadhi ya Waislamu wameyabomoa kabisa makaburi kama hayo na wakapika chai juu ya masanduku yaliyopangwa juu ya makaburi hayo. Tukio kama hilo lilitokea mwaka wa 1216 A.H. katika Siku ya Iddi’l- Ghadir, wakati wengi wa wakazi wa Karbala huenda Najaf kwa ajili ya ziara.

Ma-Wahhabi wa Najaf waliishambulia Karbala na wakawauwa Mashi’a. Wakayabomoa makaburi ya wale waliotoa mhanga maisha yao kwa ajili ya Uislamu. Karibu wakazi 5,000 wa Karbala, ikiwa ni pamoja na Maulamaa, wazee, wanawake, watoto, waliuawa.

Hazina ya Imam Husain iliporwa na vito vya thamani, taa za dhahabu, na mazulia ya thamani yalichukuliwa. Sanduku la thamani lililokuwa juu ya kaburi hilo lilichomwa moto na chai ikapikwa juu yake. Watu wengi walichukuliwa kama wafungwa. Ole kwa Waislamu kama hao!

Masikitiko yalioje kwamba katika nchi zote zilizostarabika, makaburi ya wafalme, wanachuo, na hata askari wasiojulikana yanaheshimiwa, lakini Waislamu ambao wanategemewa kuonyesha hisia nzuri za umuhimu wa kuhifadhi makaburi, ya wale ambao ni fahari yao, huyapora na kuyabomoa kama washenzi.

Katika mji wa Makka na Madina, Wahhabi walibomoa makaburi ya mashahidi wa Uhud, pamoja na la Hamza, na jadi zake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kama Abdu’l-Muttalib, Abdullah, na wengineo.

Vile vile walibomoa makaburi ya familia ya Mtume, watoto wake, kama Imam Hasani, Imam Zainu’l- Abidin, Imam Muhammad Baqir, Imam Ja’far Sadiq, Bibi Fatima binti ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na wengi wengine wa ukoo wa Bani Hashim na Maulamaa watukufu. Bado wanajiita wao ni waislamu.

Hakika wao wanajenga ma-Quba makubwa kwa ajili ya watu wao mashuhuri na wafalme. Ukweli ni kwamba, Maulmaa wa madhehebu zote wamenukuu hadithi nyingi zikitutaka tuzuru makaburi ya waumini ili kwamba yasalimike kutokana na kuharibika.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alizuru makaburi ya waumini na akamuomba Allah kwa ajili ya wokovu wao.

Dhuria Wa Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Ni Mashahidi Katika Njia Ya

Allah Na Wako Hai

Je, Unafikiri familia ya Mtume iliyotukuka ambao walitoa maisha yao katika njia ya dini ni mashahidi? Kama utasema sio mashahidi, ni nini hoja yako? Kama ni mashahidi, vipi utawaita kuwa wao, ni “Wafu?” Qur’ani Tukufu inaeleza kwamba:

{ﺑﻞ اﺣﻴﺎء ﻋﻨْﺪَ رﺑِﻬِﻢ ﻳﺮزَﻗُﻮنَ {169

“Wako hai ( na) wanaruzukiwa na Mola wao.” (3:169).

Hivyo kwa mujibu wa Qur’ani na hadith, watu wale watukufu wako hai, Hivyo, sisi sio waabudu wafu. Hatuwasalimii wafu, tunawatukuza walio hai.

Na hakuna Shia yoyote, msomi au asiye msomi, ambaye anawafanya wao kama waondoaji wa matatizo moja kwa moja. Huwachukulia kama waja wacha Mungu na njia ya kufikisha kwa Allah.

Tunaweka mahitaji yetu mbele za Maimam wanyofu ili kwamba wamuombe Allah atuhurumie waja wake. Wakati tukisema, “Ewe Ali, nisaidie, “Ewe Husain, nisaidie” ni kama tu, mtu ambaye anataka kumfikia Mfalme. Anaweza kwenda kwa waziri Mkuu na kuomba amsaidie.

Hakika hamfanyi waziri mkuu huyo wa kama kimbilio la mwisho kwa kuondoa matatizo yake. Kusudio lake pekee ni kumfikia mfalme kupitia kwake, kwa vile kwa kutokana na cheo chake, anaweza kuonana na mfalme kwa urahisi sana. Shi’a hawawachukuli dhuria wa Mtume kama washirika katika vitendo vitukufu; wanawachukulia wao kama waja Wake wacha-Mungu. Daraja Ya Maimamu Ma’sumin

Kwa vile ni wawakilishi wa Mwenyezi Mungu wanawakilisha mahitaji ya shida zao Kwake. Kama ombi linastahili, Yeye hulikubali. Vinginevyo, jazaa yake itatolewa kesho akhera. Nukta moja haipasi kuachwa bila maelezo: Mashi’a wanachukulia cheo cha Maimam Ma’sum kama cha juu kuliko mashahidi wengine wa Uislamu.

Hafidh: Taarifa hii inahitaji maelezo. Ni tofauti gani kati ya Maimam wenu na Maimam wengine wote isipokuwa tu kwamba wao wana uhusiano na Mtume?

Muombezi: Kama utaitazama nafasi ya Uimam, utoana tofauti iliyowazi kati ya dhana ya Uimam inavyochukuliwa na Mashi’a na ile ya Masunni.

Mkutano Wa Nne Jumapili Usiku 26 Rajab; 1345 A.H

Mjadala Kuhusu Uimamu:

Muombezi: Ninyi watu wema mnayo habari kwamba neno “Imam” lina maana nyingi. Kilugha lina maana ya “Kiongozi.” Imam al-Jama’at maana yake ni “yule mwenye kuongoza Sala za Jamaa.”

Anaweza pia kuwa kiongozi wa watu katika mambo ya siasa au ya kiroho. Imam al-Jum’a maana yake ni yule mtu mwenye kuongoza sala ya Ijumaa. Kwa hiyo, Sunni wafuasi wa madhehebu nne na sheria, wanawaita viongozi wao “Maimam” kama vile Imam Abu Harifa, Imam Maliki, Imam Shafi’i, na Imam Hanbal.

Wana-itiqadi na mafaqihi hawa ni viongozi wao katika mambo ya dini na wameweka Sheria za dini kwa mujibu wa utafiti wao au kwa mujibu wa kukisia kwao kuhusu uhalali wa matendo. Kwa hiyo wakati tunapovichunguza vitabu vya Fiqih vya Maimamu hawa wanne, tunakuta tofauti nyingi miongoni mwao zinazohusu misingi ya imani na Kanuni za utekelezaji wa imani.

Halikadhalika Madhehebu yote yana viongozi kama hao, na miongoni mwa Mashi’a, maulamaa na mafuqahaa wanashikilia nafasi kama hizo hizo.

Kwa kutoweka kwa Imam wetu wa zama aliye hai, wao wanatoa matamko ya kisheria kwa kutegemea elimu yao ya Qur’ani Tukufu, Hadithi sahihi za Mtume, na Maimamu wa kitume. Lakini hatuwaiti Maimamu kwa sababu Uimam ni wa washika makamu (wa Mtume) kumi na wawili peke yao - dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kuna tofauti nyingine, Sunni baadae walifunga mlango wa ijtihad (juhudi ya kutafsiri sheria).

Kuanzia karne ya tano A.H wakati ambapo, kwa amri ya Mfalme, maoni yaliyoelezewa na Maulamaa na Mafuqhaa yalikusanywa, huu uitwao uimamu uliishilizwa kwa maimamu wanne. Na madhehebu manne (Hanafi, Maliki, Shafi’i, na Hanbali) yakaanzishwa. Watu walilazimishwa kufuata kati ya moja ya hiyo, kama ilivyo desturi kwa wakati huu wa sasa.

Haijulikani ni kwa misingi ipi kumfuata Imam mmoja kunapendekezwa. Sifa gani Imam wa Mahanafi alizonazo ambazo Imam wa Maliki hanazo? Ni sifa gani alizonazo Imam wa Shafi’i alizonazo ambazo Imam wa Hanbal hana.Na kama ulimwengu wa Kiislamu utalaz- imishwa wenyewe kufungwa kwenye kufuata moja ya Madhehebu manne, basi maendeleo ya Jumuiya ya Kiislamu yatakuwa yamefungwa kabisa, ingawaje kwamba Uislamu hutufundisha kwamba yatupasa kusonga mbele pamoja na nyakati.

Iufanya hivi, tunahitaji uongozi wa Maulamaa. Kuna mambo mengi ambayo haitupasi kufuata hukumu ya Mujtahidi aliyekufa. (Kuanzia Jihad, kujitahidi, humaanisha katika hali hii, mtu anayejitahidi kutafsiri na kuunda taratibu na Sheria, kwa vile Ijtihad inahusika kwenye njia ya kujitahidi), bali inapasa kumgeukia mujtahid aliye hai kwa ajili ya kupata mwongozo. Mujitahidi wengi wamezaliwa baadae miongoni mwenu, ambao walikuwa na cheo cha juu katika elimu kuliko wale “Maimam wanne.” Sijui kwa nini upendeleo una- tolewa kwa wale waliopita ili kwamba si wengine ila wao tu waweze kufuatwa na haki za wengine kupuuzwa. Katika fiqih ya Shi’a, Mujtahid katika kila zama, mpaka wakati wa kujitokeza kwa Mtukufu Imam wa zama zetu, wao wanayo haki ya kufanya jitihada. Katika kuhusu matatizo mapya, hatuwezi kufuata hukumu ya Mujtahid aliyekufa.

Kuweka Mipaka Kwenye Madhehebu Manne Hakuna Msingi.

Ni ajabu kwamba mnawaita Mashi’a wazushi na waabudu wafu. Wao wanafuata amri za Maimamu kumi na wawili, dhuria wa Mtume (s.a.w.w.). Aidha haijulikani ni kwa misingi ipi mnajaribu kuwalazimisha Waislamu wawafuate Ashariyya au Mu’tazala kuhusiana na msingi (Usul) ya imani na mmoja kati ya Maimamu wanne katika sheria za matawi (Furu’) ya imani.

Wale ambao hawawafuati wanaitwa marafidhi. Kwa vile Abu’l-Hasan Ash’ari, Abu Hanifa, Malik bin Anas, Muhammad bin Idris Shafi’i, na Ahmad bin Hanbali walikuwa sawa na Maulamaa na mafaqihi wa Kiislamu wengine wengi, na kwa vile hakuna amri kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ya kuwafuata wao, mipaka ya kuwafuata wao tu yenyewe ni uzushi (bida’a). kama ningelileta madai haya, ungelisema nini katika kujibu?

Hafidh: Kwa vile Maimamu hawa walikuwa wana daraja ya juu ya utii kwa Allah, uchaji, ukweli, na uadilifu, pamoja na elimu kubwa mno ya Fiqih imekuwa lazima kwetu sisi kuwafuata.

Muombezi: Hatulazimiki na mantiki kujifunga sisi wenyewe kuwafuata wao peke yao. Wengi wa Maulamaa wenu wengine walikuwanazo sifa sawa kama hizi. Mpaka wa kuwafuata wao peke yao ni kebehi kwa Maulamaa wengine wenye sifa sawa na zao. Hatuwezi kulazimishwa kufuata mtu mmoja yeyote au watu wengine bila maelekezo ya kimamlaka kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hakuna ruhusa kama hiyo kutoka kwa Mtume kuhusu Maimamu wenu wanne. Basi vipi muiwekee dini mpaka (kizuizi) kwenye madhe- hebu haya manne tu?

Ushi’a Kulinganishwa Na Madhehebu Manne.

Katika mikesha michache tu iliyopita uliyaita madhehebu ya Shi’a kuwa ni ya “kisiasa” na ukasema kwamba kwa vile hayakuwepo wakati wa Mtume - kwamba yalikujakuwepo wakati wa Ukhalifa wa Uthman - ilikuwa ni haramu kuyafuata. Usiku wa kabla ya jana tulithibitisha kwamba Ushi’a uliasisiwa wakati wa Mtume (s.a.w.w) kwa maelekezo yake mwenyewe.

Kiongozi wa Mashi’a, Amirul-Mu’minin Ali alilelewa na kufundishwa na Mtume tangu utotoni na kupata elimu yake ya dini kutoka kwake. Kwa mujibu wa riwaya zilizomo kwenye vitabu sahihi vyenu wenyewe, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amemwita yeye “Lango la Elimu.”

Kwa dhahiri kabisa alisema: “Utii kwa Ali ni utii kwangu, na kutomtii Ali ni kutomtii mimi.” Katika mkusanyiko wa watu 70,000 alimteua kuwa Amir na Khalifa, na akawaamrisha Waislamu wote, wakiwemo Umar na Abu Bakr, kula kiapo cha utii kwake.

Lakini haifahamiki ni vipi madhehebu yenu Manne yalivyokuja kuanzishwa, wala ni yupi kati ya Maimamu wanne aliyemuona Mtume au kama kuna ruhusa yoyote iliyosimuliwa kutoka kwa Mtume kuhusu wao ili angalau kuweza kueleza ni kwa nini Waislamu waweze kulazimika kuwafuata wao. Bila sababu za kukufungeni mnawafuata wakubwa zenu na hamusemi chochote cha kupasisha Uimamu wao isipokuwa tu kwamba walikuwa mujtahid wakubwa, watu wenye elimu na uchamungu.

Lakini, ikiwa sifa hizi zipo kwa kiwango cha juu sana katika kizazi cha Mtume, hivyo basi sio wajibu kwetu sisi kuwafuata wao? Hivi hizi madhehebu zisizo na kiungo na Mtume ndio za uzushi au Madhehebu iliyoasisiwa na Mtume na kuongozwa na dhuria wake ndiyo ya uzushi?

Katika njia hiyo hiyo, kuna Maimamu wengine kumi na mmoja, ambao kuhusu wao kuna Hadithi mbali mbali zinazoonyesha kwamba wao ndio wanaolingana na Qur’ani Tukufu. Katika Hadith al-Thaqalain imeelezwa wazi kwamba: “Yeyote ambaye atashikamana na viwili hivi ataokolewa na yule ambaye atakaa mbali navyo amepotea. Katika “Hadithus- Safina.” Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Yule ambaye hukaa mbali navyo ataangamia na kupotea.” Ibn Hajar katika “Sawa’iq” (Bab-e-Wasiyyatu’n –Nabi, uk.135) ananukuu hadithi kutoka kwa Mtume isemayo kwamba: “Qur’ani na dhuria wangu ni dhamana zangu; kama mtashikamana wenyewe kwenye viwili hivi, kamwe hamtapotea.”

Kwa kuliunga mkono hili, Ibn Hajar ananukuu hadithi nyingine kutoka kwa Mtume kuhusu Qur’ani Tukufu na dhuria wake watoharifu: “Msivuke mipaka ya Qur’ani na dhuria wangu; wala msiwapuuze. Vinginevyo mtaangamizwa. Na msiwafundishe dhuria wangu kwa vile wao wanajua zaidi kuliko mlivyo ninyi.”

Baada ya hivi, Ibn Hajar akatoa maelezo kwamba, hadithi hizo hapa juu huthibitisha kwamba dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni bora kuliko wengine wote katika elimu na katika kutekeleza wajibati za kidini.”

Maimamu Wanne Wa Kisunni Wametangazana Kuwa Makafiri.

Walakini hata hivyo, inashangaza kwamba, pamoja na kujua kwamba dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni wabora kuliko wengine wote, Masunni wanamfuata Abu’l Hasan Ash’ari katika misingi ya dini na Maimamu wanne katika kanuni za utekelezaji wa Imani. Kufuata mwenendo huo ni kwa sababu ya ushabiki na kiburi. Na hata kama tukijaalia kuwa usemayo ni kweli, kwamba Maimamu wenu wanne wana haki ya ninyi kuwakubali kwa sababu walikuwa wanachuo na wachamungu, basi kwanini kila mmoja wao akamlaumu mwengine kwa ukafiri?

Hafidh: Wewe umkali sana. Unasema kila kinachokuja kwenye akili. Unawasingizia Maimamu wetu. Maelezo haya ni ya uwongo. Kama kuna kilichosemwa dhidi yao, ni kutoka kwa Maulamaa wa Kishi’a. Kutoka upande wetu hakuna chochote kilichosemwa dhidi yao. Tumeonyesha heshima kwao.

Muombezi: Ni dhahiri wewe hukusoma vitabu vya Maulamaa wako. Maulamaa wenu maarufu wenyewe wameandika vitabu vinavyohusu kukataa kwao. Hata hawa maimamu wanne wameshutumiana wenyewe kwa wenyewe kwa kukiuka sheria za dini.

Hafidh: Maulamaa hao ni akina nani? Nini maelezo yao?

Muombezi: Masahaba wa Abu Hanifa, Ibn Hajar (Ali bin Ahmad Andalusi aliyekufa 456 A.H.), na wengine wamekuwa kila mara wakiwasuta Imamu Maliki na Muhammad bin Idris Shafi’i. Kadhalika wafuasi wa Imam Shafi’i, kama Imamu’l-Haramain, Imam Ghazali na wengine wamemshutumu Abu Hanifa na Malik. Hebu ngoja nikuulize kitu: Hawa walikuwa watu aina gani – Imam Shafi’i, Abu Hamid bin Muhammad Ghazali, na Jarullah Zamakhshari?

Hafidh: Walikuwa Mafuqaha wakubwa, wanachuo wasomi, watu wachamungu, na Maimamu wetu.

Shutuma Za Maulamaa Wa Kisunni Kwa Abu Hanifa:

Muombezi: Imam Shafi’i amesema: “Hajapata kuzaliwa mtu wa kuchukiza katika Uislamu kama Abu Hanifa.” Vilevile amesema: “Nimeangalia katika vitabu vya wafuasi wa Abu Hanifa, na nikaona mna kurasa 130 zenye mambo yenye kukinzana na Qur’ani Tukufu na Sunna.”

Abu Hamid Ghazali katika kitabu chake “Manqul-fi Ilmi’l-Usul” anasema: “Kwa hakika Abu Hanifa amepotoa kanuni ya dini, kaifanya njia yake kuwa ya mashaka, amebadilisha mpangilio wake, na amechanganya sheria katika hali ambayo kanuni iliyoelezwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) imeharibika kabisa. Mtu mwenye kufanya hivyo makusudi na kuiona hiyo kuwa ni halali; ni kafiri. Mtu mwenye kuifanya na hali akijua, ni fasiq.

Kwa mujibu wa Mwanachuo huyu mkubwa, Abu Hanifa alikuwa ama yeye ni kafir au fasiq. Vitabu vingi vingine vinamshutumu Abu Hanifa. Jarullah Zamakshari, mwandishi wa “Tafsirul’al-Kash’shaf” na mmoja wa Maulamaa wenu wachamungu, anaandika katika “Rabiu’l-Abrar” kwamba Yusufu bin Asbat alisema:

“Abu Hanifa alizikataa karibu Hadith 400 za Mtume wa Uislamu.” Yusufu akaeleza kwamba: “Abu Hanifa alisema: Lau Mtume wa Uislamu angenifahamu, mengi ya maneno yangu angeyakubali.”

Maulamaa wenu wenyewe wametoa shutuma za namna hiyo kwa Abu Hanifa na kwa hao Maimamu wengine watatu. Zinaweza kupatikana katika “Mutahawwal” cha Ghazali,

‘Nuqtu’sh-Sharifa” cha Shafi’i, “Rabiu’l-Abrar” cha Zamakhshari, na “Muntazim” cha Ibn Jauz. Imam Ghazil anasema katika “Mutahawwal” yake: “Kuna makosa mengi katika vitabu vya Abu Hanifa. Hakuwa na elimu ya balagha, nahau, au hadith.” Vilevile anaandika: “Kwa vile hakuwa na elimu ya hadith, alitegemea juu ya kukisia mwenyewe. Kiumbe wa kwanza aliyetenda kwa kukisia alikuwa ni Shetani.”

Ibn Jauzi anaandika katika “Muntazim” yake: “Ulamaa wote wameungana katika kumshutumu Abu Hanifa. Kuna Makundi matatu ya wakosoaji kama hao: kundi moja linashikilia kwamba imani yake katika misingi ya Uislamu ilikuwa haina uhakika; kundi lingine linasema kwamba, hakuwa na kumbukumbu imara na hakuweza kukumbuka hadith; kundi la tatu linaamini kwamba alitenda kwa kukisia na kwamba maoni yake yalikuwa siku zote tofauti na hadith za kweli.”

Maulamaa wenu wenyewe wemewalaumu Maimamu wenu. Maulamaa wa Kishi’a hawakuwahusisha na chochote, isipokuwa kile Maulamaa wenu wenyewe walichosema kuhusu wao.

Kwa upande mwingine, hakuna tofauti ya maoni miongoni mwa Ulamaa wa Kishi’a kuhusiana na nafasi za hao Maimamu kumi na mbili.

Tunawaona Maimamu watukufu kama wanafunzi wa fundisho moja. Maimamu hawa - wote walitenda kwa mujibu wa sheria za Ki-Mungu ambazo yule mwisho wa Mitume aliwapa. Kamwe hawakutenda kwa kukisia au kuafiki uzushi. Walichosema au kufanya kilikubaliana na maneno ya Mtume. Hivyo, hakukuwa na tofauti miongoni mwao.

Uimam Kwa Mujibu Wa Shi’a Una Maana Ya Uwakilishi Wa Allah.

Kwa mujibu wa ufafanuzi uliotolewa na Maulamaa, Uimamu au Uwakilishi wa Allah, ni moja ya misingi ya Uislamu. Tunaamini kwamba Uimamu ni uwakilishi wa Allah kwa viumbe wote na Khilafat-e-Rasul (Makamu/warithi wa Mtume) kwa ulimwengu huu na ujao. Kwa hiyo, ni wajibu kwa wanadamu wote kufuata wapangaji wake katika mambo yote, ya kidunia na hali kadhalika ya kiroho.

Sheikh: Ingelikuwa vizuri kama usingelitamka kidhahiri kwamba Uimamu umeingizwa katika misingi ya imani, kwa vile Maulamaa wakubwa wa Uislamu wanakataa kuwekwa kwake humo. Umewekwa katika shuruti za matendo ya imani. Maulamaa wenu wameufanya sehemu ya misingi.

Muombezi: Maelezo yangu haya, hayakomei kwenye Imam wa Mashi’a tu. Hata Maulamaa wenu wakubwa wanayo imani kama hiyo. Mmoja wao ni mfasiri wenu mashuhuri Qadhi Baidhawi, ambaye anasema katika kitabu chake “Minhaju’l-Usul” kuhusiana na mjadala juu ya masimulizi ya Hadithi: “Uimamu ni moja ya kanuni za msingi za imani, ambazo kuzikataa na ukinzano juu yake hupelekea kwenye ukafir na uzushi.”

Mulla Ali Qushachi anasema katika kitabu chake “Sharh-e-Tajrid.” Uimamu kwa jumla ni Uwakala wa Allah kwa mambo yote ya ulimwengu huu na dini, kama Ukhalifa wa Mtume.” Na Qadhi Ruzbahan, mmoja wa washupavu mno (Shabiki) wa Maulamaa wenu anaashiria kwenye maana hiyohiyo.

Anasema: “Uimamu kwa mujibu wa wafuasi wa Abu’l-Hasan Ash’ari ni uwakilishi wa Mtume wa Uislamu kwa ajili ya kuimarisha imani na kulinda salama maslahi ya Jumuiya ya Kiislamu. Wafuasi wote wanafungwa katika wajibu wa kufuata maamrisho yake.”

Ungekuwa Uimamu sio sehemu ya shuruti za matendo ya imani, Mtume asingesema kwamba: “Yeyote yule anayekufa bila kujua Imamu wake wa zama, anakufa kifo cha kijahilia.”

Hii imenukuliwa na Maulamaa wenu maarufu, kama Hamidi katika “Jam’i-Bainu’s- Sahihain” na Mulla Sa’d Taftazani katika “Sharhe Aqa’id-e-Nasafi.” Kutoelewa sharti hata moja la utekelezaji wa imani hakuwezi kuwa sawa na ujinga ulioelezwa na Baidhawi kuhusu kutokujua misingi, yaani kwamba ujinga wake ni sababu ya ukafir.

Kwa hiyo Uimamu ni moja ya misingi ya imani na ni hatua ikamilishayo Utume. Kwa ajili ya hiyo, kuna tofauti kubwa kati ya dhana ya Uimamu wetu na ile inayotafsiriwa na ninyi.

Mnawaita Maulamaa wenu Maimamu, kama vile Imam Adhma, na Imam Maliki. Lakini hii ni maana ya mdomo. Sisi pia tunatumia neno Imam-e-Juma’a, Imam-e-Ja-ma’at.

Hivyo wanaweza wakawepo mamia ya Maimamu kwa wakati mmoja, lakini katika maana ya kitaalamu (kiistilahi) ambayo kwayo tunatumia neno “Imam,” ina maana muwakilishi wa Allah. Katika maana hii kuna Imam mmoja tu kwa wakati mmoja. Sifa bora za elimu, Maadili, ushujaa, upenzi kwa Allah, na uchamungu zimekamilishwa ndani yake.

Anawashinda binadamu wote katika tabia zote na hushikilia hali ya kutofanya makosa. Dunia haitakuwa bila Imam wa aina hiyo mpaka siku ya malipo. Imam wa ubora kama huo anakuwa katika kiwango cha juu kabisa cha mafanikio ya kiroho. Imam kama huyo anaidhinishwa na Allah na anateuliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hushinda viumbe wote pamoja na Mitume waliopita.

Hafidh: Kwa upande mmoja unawashutumu Maghulat, na kwa upande mwingine wewe mwenyewe kiububusa unawasifu Maimamu na kuiona nafasi yao ya juu zaidi kuliko ile ya Mitume. Akili ya kawaida inalikataa hili, na Qur’ani Tukufu vilevile imeeleza kwamba Mitume wamewekwa katika nafasi ya juu zaidi. Nafasi yao iko baina ya uhuru wa ki-ungu na lile lenye kuwezekana. Kwa vile maelezo yako hayaungwi mkono na akili, hayawezi kukubaliwa.

Cheo Cha Uimam Ni Juu Zaidi Kuliko Cha Utume Wa Kawaida.

Muombezi: Bado hujaniuliza ni kwa misingi ipi nimeyatoa maelezo haya, na kwa hiyo unasema ni ya bila hekima. Ushahidi mzuri kwa maelezo yangu ni Qur’ani Tukufu, ambayo ikizungumzia maisha ya Mtume Ibrahim, inasema kwamba, baada ya kumpa mitihani mitatu (ya maisha, mali, na watoto), Allah alikusudia kufanya cheo chake cha juu zaidi. Kwa vile Utume na Cheo cha Khalil (Rafiki) havikuruhusu dhahiri cheo cha juu, nafasi ya Uimamu ndiyo iliyokuwa nafasi pekee ya Cheo cha juu ambayo hata Mtume wa Allah anaweza kuaminishwa. Qur’ani Tukufu inasema: “Na wakati Mola Wake alipomjaribu Ibrahim na maneno fulani, aliyatekeleza.

Alisema:

{ﻗَﺎل اﻧّ ﺟﺎﻋﻠُﻚَ ﻟﻠﻨﱠﺎسِ اﻣﺎﻣﺎ ۖ ﻗَﺎل وﻣﻦ ذُرِﻳﺘ ۖ ﻗَﺎل  ﻳﻨَﺎل ﻋﻬﺪِي اﻟﻈﱠﺎﻟﻤﻴﻦ {124

“Hakika nitakufanya Imam wa watu. Ibrahimu akasema: Na dhuria wangu? Akasema ahadi yangu haiwafikii madhalimu.” (2:124).

Aya hii ambayo inaonyesha nafasi ya Uimamu, pia inathibitisha kwamba cheo cha Uimamu ni cha juu kuliko cha Utume. Kwa vile nafasi ya Mtume Ibrahimu ilinyanyuliwa kutoka Utume kwenda Uimamu.

Hafidh: Hii ina maana, kwa mujibu wa maelezo yako, ni kwamba nafasi ya Ali ilikuwa ya juu kuliko ile ya Mtume wa Mwisho. Hivi ndivyo Maghulat walivyoamini, kama wewe mwenyewe ulivyokiri.

Mitume Wa Kawaida Na Wale Maalumu:

Muombezi: Sina maana ya hivyo ulivyohitimisha wewe. Kama ujuavyo kuna tofauti kubwa kati ya Utume wa kawaida na Utume maalumu. Cheo cha Uimamu ni cha juu zaidi kuliko cheo cha Utume wa kawaida, lakini kiko chini kuliko cha Utume Maalumu. Mtume wa mwisho ndiye kiwango cha hali ya juu cha utume maalum.

Nawab: Nisamehe kwa kuingilia kwangu. Je; Mitume wote hawakutumwa na Allah? Hapana shaka wote wana cheo kile kile. Qur’ani Tukufu inasema: “Hatutofautishi baina ya yeyote kati ya Mitume.” (2:285). Basi kwanini umetofautisha baina yao na ukagawa Utume katika makundi mawili; kawaida na maalumu?

Muombezi: Hakika, Aya hii ni kweli iko sawa sawa katika fuo lake. Yaani, kwa kiasi kufanikisha lengo la Utume kuhusikavyo (ambako kuna maana ya kufundisha watu kuhusu kuwepo kwa Allah. Siku ya Malipo na kuzifunza akili zao), Mitume wote kutoka Adamu mpaka mwisho wa Mitume, wako sawa. Lakini wanatofautiana katika sifa, mafanikio na cheo.

Tofauti Katika Daraja Za Mitume.

Je, Mtume ambaye ametumwa kuongoza watu 1,000 ni sawa na yule aliyepelekwa kuongoza watu 30,000, au kwa yule aliyetumwa kuongoza wanadamu wote? Hebu tuchukue mfano. Hivi, Mwalimu wa wanafunzi wa darasa la kwanza ni sawa na Mwalimu wa darasa la nne?

Je, Walimu wa madarasa ya juu ni sawa na Maprofesa au Walimu wa Chuo Kikuu? Wote wako katika Utawala mmoja na kufanya kazi chini ya mpango mmoja wa jumla, lengo lao likiwa kuelimisha wanafunzi. Bado, kwa kuzingatia elimu ya Walimu hao, hawako sawa.

Kila mmoja yuko tofauti na mwingine kwa mujibu wa kisomo, uwezo, na mafanikio yake. Kwa mtazamo wa lengo la Utume, Mitume wote wa Allah wako sawa sawa. Walakini, kwa sababu ya tofauti katika daraja na elimu, wako tofauti. Qur’ani Tukufu inasema:

{ﺗﻠْﻚَ اﻟﺮﺳﻞ ﻓَﻀﻠْﻨَﺎ ﺑﻌﻀﻬﻢ ﻋﻠَ ﺑﻌﺾٍ ۘ ﻣﻨْﻬﻢ ﻣﻦ ﻛﻠﱠﻢ اﻟﻪ ۖ ورﻓَﻊ ﺑﻌﻀﻬﻢ درﺟﺎتٍ ۚ{253

“Tumewafanya baadhi ya Mitume kuwazidi wengine; Miongoni mwao wako ambao Allah amesema nao, na baadhi yao Amewatukuza kwa (vyeo vingi) daraja.” (2: 253).

Mwanachuo wenu wenyewe Jarullah Zamakshari anasema katika kitabu chake, “Tafsir-e- kush-Shaf” kwamba, Aya hiyo hapo juu ina maana Mtume wetu alikuwa bora katika daraja kwa wengine wote kwa sababu ya sifa zake maalumu, muhimu zaidi ni ambayo kwamba alikuwa wa mwisho wa Mitume.

Nawab: Nimefurahi umelitatua tatizo hili, lakini nina swali lingine, ingawa kwa namna nyingine halihusiki hapa. Tafadhali tueleze kwa ufupi sifa makhususi za Utume maalumu.

Muombezi: Kuna sifa nyingi za pekee kwa Utume Maalumu, na kuna sababu nyingi mno zinazothibitisha vipi Mtume mmoja kati yao wote ndiye Mtume maalum wa Allah. Kwa hakika hatua hiyo huishiliza duru la Utume.

Lakini mikutano hii haikupangwa kuthibitisha Utume wa Allah kwa Waislamu. Kama ingekuwa tuijadili nukta hii kikamilifu, tungetoka nje ya nukta yetu ya Uimamu. Walakini kwa ufupi hata hivyo, nitajadili nukta hii. Sifa Za Utume Maalum:

Ukamilifu wa ubinadamu umo katika ukamilifu wa nafsi. Ukamilifu wa kimaadili na kiroho hauwezi kufikiwa bila kutakasa nafsi. Ukamilifu huu hauwezekani mpaka mtu aongozwe kwa uwezo wa hekima. Hapo ndipo mtu ataweza kupanda juu na juu zaidi pamoja na nguvu ya elimu na utendaji sahihi mpaka anafikia kilele cha ubinadamu, kama ilivyoelezwa na Ali.

Yeye alisema: “Mtu aliumbwa na uwezo wa kuongea ambayo ni asili ya ubinadamu. Kama mazungumzo yamepambwa na elimu na vitendo, hufanana na kuwepo ufalme wa ki-mbinguni ambao ndiyo asili ya kuumbwa kwa mwanadamu.

Wakati mazungumzo yake yanapofikia pahala pa kujizuia na yanaondokana na mata yote ya maumbile, inakuwa moja pamoja na ufalme wa ki-mbinguni. Kisha huachana na ulimwengu wa kihayawani na kufikia hatua ya juu sana ya ubinaadamu.” Uwezo wa mtu wa kuzungumza humfanya bora kwa viumbe vyote. Lakini kuna sharti moja lililoambatanishwa kwalo, kwamba uisafishe nafsi yake na uchafu wote kwa elimu na matendo sahihi. Sehemu hizi mbili ndani ya mtu ni kama mbawa mbili za ndege, ambaye huruka juu angani kutokana na nguvu za mbawa zake.

Hivyo hivyo kiwango cha mtu cha mafanikio ya ubinadamu hupanda kutokana na elimu yake na matendo sahihi. Kuvuka mipaka ya hali ya kinyama na kufikia nyanja ya matendo ya kibinadamu hutegemea juu ya ukamilifu wa nafsi. Mtu ambaye hukusanya ndani yake stadi za elimu na matendo sahihi na akafikia thuluthi ya tabaka tatu za watu (watu wa kawaida, watu bora na watu bora zaidi), hufikia daraja la chini kabisa la Utume. Wakati mtu kama huyo anapokuwa shabaha ya hisani maalumu za Allah, anakuwa Mtume.

Naam, kwa kweli Utume vilevile una daraja tofauti. Mtume anaweza kufikia daraja ya juu zaidi katika tabaka hizi tatu. Cheo hiki ni cha juu sana katika nyanja ya uwezekano, ambayo wenye busara (wataalamu) huiita Hekima ya Kwanza, na ambayo ni Athari ya Kwanza au Matokeo ya Mwanzo. Hakuna cheo cha juu kama hiki katika miliki ya viumbe.

Nafasi hii imeshikwa na wa mwisho wa Mitume, ambaye ni wa kwanza, hakuna kama yeye isipokuwa kile Chanzo cha Awali. Wakati Mtume alipopandishwa kwenye daraja hii ya juu zaidi, Utume ulikomelezwa. Uimamu ni daraja la chini kuliko daraja ya juu zaidi ya utume, lakini ni hatua ya juu kuliko daraja zote nyingine za Utume. Kwa vile Ali alipandishwa kwenye hatua ya juu kuliko ya Utume na alikuwa mmoja katika nafsi pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), aliaminishwa kazi ya Uimamu na hivyo kuwa mbora kwa Mitume wote waliopita.

Hafidh: Sehemu ya mwisho ya maneno yako inachanganya. Kwanza, unasema Ali alikuwa katika ngazi ya Utume, pili, kwamba alikuwa nafsi moja na Mtume Muhammad, tatu, kwamba alikuwa bora kwa Mitume mingine. Nini hoja zako kuthibitisha ukweli wa maneno yako? Hoja Za Cheo Cha Utume Kwa Ajili Ya Ali Kutoka Kwenye Hadith Manzila.

Muombezi: Kwamba Ali amepata cheo cha Utume yaweza kuthibitishwa kwa kurejea kwenye hadith ya Manzila (Hadith inayohusu vyeo), ambayo imesimuliwa kwa kauli moja kwa kadri ya maneno yanayofanana. Wa mwisho wa Mitume watukufu amerudia mara nyingi na katika mikusanyiko tofauti. “Je, huridhiki kwamba kwangu wewe ni kama Harun alivyokuwa kwa Musa, isipokuwa tu kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu?” Na wakati mwingine aliwaambia wafuasi wake. “Ali kwangu mimi ni kama alivyokuwa Hauna kwa Musa.”

Hafidh: Usahihi wa hadith hii haukuthibitishwa. Hata kama ingethibitishwa kuwa ni kweli itakuwa ni simulizi pekee na kwa hiyo haikubaliki.

Usahihi Wa Hadith Ya Manzila Kutoka Kwenye Rejea Za Kawaida.

Muombezi: Katika kutoa taarifa kuhusu usahihi wa hadith hii, nitarejea kwenye vitabu vyenu. Hii sio simulizi ya pekee. Imethibitishwa na maulamaa wenu mashuhuri, kama Suyuti, Hakim Nishapuri, na wengine, ambao wamethibitisha kutegemeka kwake kwa vyanzo vinavyokubaliwa kwa pamoja. Baadhi yake ni hivi vifuatavyo:

(1) Abu Abdullah Bukhari katika Sahih yake Juz. 111, Kitab Ghazawa, gahazawa Tabuk; uk. 54, na ndani ya kitabu chake “Bida’u’l-Khalq”, uk. 180; (2) Muslim bin Hajjaj katika Sahih yake iliyochapishwa Misri, 1290 A.H. Juz. 11, chini ya kichwa cha habari, “Ubora wa Ali;” uk. 236-7; (3) Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad Juz. 1 “Sababu za kutoa jina la Husain”, Uk. 98, 118, 119 na maelezo chini ya kurasa ya kitabu hicho hicho, Sehemu ya 5 uk. 31; (4) Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i katika “Khasa’isi’l-Alawiyya” uk. 19; (5) Muhammad bin Sura Tirmidhi katika Jami’ yake; (6) Hafidh Ibn Hajar Asqalani kati- ka “Isaba.” Juz. 11, uk. 507; (7) Ibn Hajar Makki katika “Sawa’iq Muhriqa” Sura ya 9, Uk. 30& 34; (8) Hakim Abu Abdullah Muhammad bin Abdullah Nishapuri katika “Mustadarak”, Juz. 11, Uk. 109; (9) Jalalu’d-Din Suyuti katika “Tarikhu’l-Khulafa” uk. 65; (10) Ibn Abd Rabbih katika “Iqdu’l-Farid” Juz. 11, uk. 194; (11) Ibn Abdu’l-Birr katika “Isti’ab”, Juz. 11, uk. 473; (12) Muhammad bin Sa’d Katib Waqidi katika “Tabaqatu’l-Kubra;” (13) Imam Fakhru’d-Din Radhi katika “Tafsir Mafatihu’l-Ghaib”; (14) Muhammad bin Jarir Tabari katika “Tafsir” yake, na pia katika “Tarikh” yake; (15) Seyyed Mu’min Shablanji katika “Nuru’l-Absar”, uk. 68; (16) Kamalu’d-Din Abu Salim Muhammad bin Talha Shafi’i katika “Matalibu’s-Su’ul”, uk. 17; (17) Mir Seyyed Ali bin Shahabu’d-Din Hamadani katika “Mawaddatu’l-Qubra”, kuelekea mwisho wa Mawadda 7; (18) Nuru’d-Din Ali bin Muhamma Maliki Makki, ajulikanaye kwa jina la Ibn Sabbagh Maliki katika “Fusulu’l Muhimma” uk. 23 na 125; (19) Ali bin Burhanu’d-Bin Shafi’i katika “Siratu’l-Halabiyya” Juz. 11, uk, 49; (20) Sheikh Sualyman Balkh Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, (21) Mulla Ali Muttaqi katika “Kanzu’l-Ummal”, Juz. VI, uk. 152 –153; (22) Ahmad bin Ali Khatib katika “Ta’rikh Baghdad”; (23) Ibn Maghazili Shafi’i katika “Manaqib”; (24) Muwaffaq bin Ahmad Khawarizmi katika “Manaqib”; (25) Ibn Jazari Ali bin Muhammad katika “Usudu’l-Ghaiba”; (26) Ibn Kathir Damishqi katika “Tarikh” yake; (27) Ala’u’d- Daula Ahmad bin Muhammad katika “Urwatu’l-Wuthqa”; (28) Ibn Athir Mubarak bin Muhammad Shaibani katika “Jami’ul’-Usul”; (29) Ibn Hajar Asqalani katika “Tahdhibu’t- Tahdhib”; (30) Abu’l-Qasim Husain bin Muhammad Raghib Isfahani katika “Muhadhiratu’l-Udaba”; Juz. 11, uk. 212.

Maulamaa wenu wengi wengine wakubwa wameisimuliwa hadith hii muhimu pamoja na tofauti kidogo ya maneno kutoka kwa Masahaba wengi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama vile:

(1) Umar bin Khattab, (2) Sa’d bin Ali Waqqas (3) Abdullah bin Abbas; (4) Abdulllah bin Mas’ud; (5) Jabir bin Abdullah Ansari, (6) Abu Huraira; (7) Abu Sa’id Khurdri; (8) Jabir bin Sumra; (9) Maliki bin Huwairi’s, (10) Bara’a bin Azib; (11) Zaid bin Arqam; (12) Abu Rafi; (13) Abdullah bin Ubai; (14) Abu Suraiha, (15) Hudhaifa bin Assad, (16) Anas bin Malik, (17) Abu Huraira Aslami, (18) Abu Ayyub Ansari, (19) Sa’id bin Musayyab (20) Habib bin Abi Thabit, (21) Sharhbil bin Sa’d; (22) Ummi Salma (Mke wa Mtume); (23) Asma bint Umais, (Mke wa Abu Bakar); (24) Aqil bin Abi Talib (25) Muawiyya bin Abu Sufyan, na wengi wa Sahaba wengine.

Kwa ufupi wote hawa wameisimuliwa pamoja na tofauti kidogo ya maneno kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ewe Ali, wewe uko kwangu mimi kama Harun alivyokuwa kwa Musa, isipokuwa kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu.” Je, Maulamaa wote hawa wakubwa – na kuna wengi sikuwataja – hawatoshi kuthibitisha kwamba hadithi hii imekubaliwa kwa pamoja kuwa ya kweli? Je, utathibitisha sasa kwam- ba ulikuwa katika kutokuelewa?

Kwa vile unachukua mwelekeo wa wasiwasi kuhusu ukweli wa hadith hii, yakupasa uangalie katika Kitabu “Kifayatu’t-Talib fi Manaqib-e-Ali Bin Abu Talib,” Sura ya 7, kilichoandikwa na Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i, ambaye ni mmoja wa Maulamaa wenu Maarufu mno wa madhehebu yenu. Baada ya kunukuu hadith sita zenye kumtukuza Ali, mwandishi huyu akaisherehesha (uk.149) hadith hii kama ifuatavyo:

“Hii ni hadithi ambayo usahihi wake umekubaliwa na wote. Imesimuliwa na Maimamu wenye elimu zaidi na Huffadh (wajuao Qur’ani Tukufu kwa moyo), kama vile Abu Abdullah Bukhari katika Sahih yake, Muslim bin Hajjaj katika Sahih yake, Abu Dawud katika Sunan yake, Abu Isa Tirmidhi katika Jami’ yake, Abu Abdu’r-Rahman katika Sunan yake, Ibn Maja Qazwini katika Sunan yake. Wote hawa kwa pamoja wamekubali usahihi wake. Hakim Nishapuri amesema kwamba hadith hii imeingia katika hatua ya Mutawatir.”

Nina hakika kwamba sihitaji kutoa ushahidi zaidi kuonyesha kwamba hadith hii ni Sahihi.

Hafidh: Mimi sikukosa maadili ya kidini, hivyo siwezi kukataa mantiki yako ya kiakili, lakini hebu vuta mazingatio kwenye kauli ya mwanachuo na mwana itikadi mkubwa, Abu’l-Hasan Amadi, ambaye ameikataa hadith hii.

Muombezi: Nashangaa kwa nini mtu mwenye elimu kama wewe, baada ya kusikia maoni ya Maulamaa wako mashuhuri, utaamini taarifa ya mtu muovu ambaye alikuwa hata kuswali haswali.

Sheikh: Mtu yuko huru kuelezea imani yake. Kama mtu akielezea maoni yake, haitupasi sisi kumkashifu. Haipendezi kwa wewe kumzulia uongo badala ya kutoa majibu yenye mantiki kwenye maelezo yake.

Muombezi: Umenielewa vibaya. Simlaumu mtu yeyote kinyume cha haki. Si kuwa ninaishi katika wakati wa uhai wa Amadi. Maulamaa wenu wenyewe wameelezea kwamba alikuwa ni mtu aliyekuwa hana dini. Sheikh: Ni wapi ambapo Ulamaa wetu wamesema kwamba alikuwa ni mtu asiyekuwa na dini?

Amadi Haaminiki Kama Msimuliaji Wa Hadithi.

Muombezi: Ibn Hajar Asqalani ameandika katika Lisanu’l-Mizan: “Saif Amadi Mutakallim Ali bin Abi Ali, mwandishi, alifukuzwa kutoka Damascus kwa sababu ya maoni yake yasiyokuwa ya kidini, na ni kweli kwamba alikuwa hasali.”

Na Dhahabi, ambaye pia ni mmoja wa Maulamaa wenu Maarufu, ameandika hivyohivyo katika “Mizanu’l-Itidal.” Amesema kwamba Amadi alikuwa mzushi. Kama Amadi asingekuwa muovu na mzushi asiyekuwa na dini, asingeweza kutoa maneno ya kashfa kuhusu Sahaba wote wa Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.), ikiwa ni pamoja na Khalifa wenu wenyewe, Umar bin Khatab (mmoja wa wasimuliaji wa hadithi hii). Sio haki kabisa kwamba mnawaona Mashi’a kuwa na taksiri kwa sababu ya kutokubali hadith zilizoandikwa katika “Sihah.” Kama hadithi imetolewa kutoka vyanzo sahihi, inakubaliwa hata kama iko kwenye “Sihah.” Lakini hadithi iliyothibiti, ambayo imeandikwa na Bukhari, Muslim, na waandishi wengine wa “Sihah” inakataliwa na Amadi, hamuoni taksiri kwayo.

Kama unataka kujua kwa ukamilifu hoja zinazohusu usahihi na vyanzo vya hadith hii kutoka kwenye maandishi ya Maulamaa wenu, na kama uko tayari kuwalaumu watu kama Amadi, unaweza ukaangalia jalada za “Abaqatu’l-Anwar”, zilizoandikwa na mwanachuo mkubwa na mfasiri, Allama Mir Seyyed Hamid Husain Dihlawi.

Yakupasa uangalie hususan hadith ya Manzila ili uweze kujua kwamba vipi mwanachuo huyu mkubwa wa Kishi’a alivyokusanya vyanzo kutoka kwa wanachuo wenu wa Shariah na wakathibitisha kutegemeka kwa hadhi hii.

Hafidh: Umesema kwamba mmoja wa wasimuliaji wa Hadithi hii alikuwa Umar bin Khattab. Ningetaka kujua zaidi kuhusu habari hii.

Kuthibitishwa Hadith Ya Manzila Na Umar Bin Khattab.

Muombezi: Abu Bakar Muhammad bin Ja’afaru’l-Mutiri na Abu’l-Laith bin Muhammad Samarqandi Hanafi, katika vitabu vyao, Majalis, Muhammad bin Abdu’r-Rahman Dhahabi katika “Riadhu’n- Nadhara”, Mulla Ali Muttaqi katika “Kanzu’l-Ummal” na wengine, wamesimulia kutoka kwa Ibn Abbas akisema kwamba siku moja Umar bin Khattab alisema: “Liache jina la Ali (yaani usimzungumze Ali sana kwa ubaya) kwa sababu nimesikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kwamba Ali alikuwa na sifa tatu.

Kama ningekuwa na moja kati ya sifa hizi, ningeihifadhi zaidi kuliko kitu chochote kifikiwacho na mwanga wa jua juu yake. Siku moja mimi; Abu Bakar, Abu Ubaida Jarra na baadhi ya Sahaba wengine tulikuwepo, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amepumzika kwa kumuegemea Ali bin Abu Talib. Alipiga bega la Ali na kusema: “Ali! Kiasi imani inavyohusika, wewe ni wa kwanza wa Waumini wote, na kiasi Uislam unavyohusika, wewe umechukua nafasi ya kuongoza!’

Kisha akasema: ‘Ali! Uko kwangu mimi kama alivyokuwa Harun kwa Musa. Na ni muongo ambaye anafikiri ni rafiki yangu kama yeye ni adui yako.”

Je, inaruhusiwa katika imani yenu kukataa maneno ya Khalifa Umar? Kama hairuhusiwi, kwa nini unaamini taarifa za ajabu za mtu kama Amadi?

Nafasi Ya Simulizi Pekee Katika Madhehebu Ya Sunni.

Ningali bado sijajibu moja ya madai yako. Umesema kwamba hadith hii ni simulizi pekee, na kwa ajili hiyo haikubaliki. Kama tukisema kitu hicho kwa mujibu wa mtindo wa watu ambao tunao katika maoni, tutakuwa wenye haki. Lakini inanishangaza kusikia kitu hiki kutoka kwako, kwa sababu katika madhehebu yenu hata simulizi pekee inatosha kuthibitisha ukweli wa jambo.

Kama mtu akikataa kukubali usahihi wa simulizi pekee, kwa mujibu wa maulamaa wenu atakuwa si muumini. Maliku’l-Ulama Shahabu’d-Din Daulatabadi amesema katika “Hidayatu’S-Sa’da”: “Kama mtu anakataa kukubali riwaya pekee au rai na akasema kwamba haikubaliki, huyo ni kafir.

Kama akisema simulizi pekee hii sio sahihi, na rai hii haikuthibiti, atakuwa mtenda kosa, sio kafir.

Hafidh: Tumetoka kwenye mada yetu ya msingi. Tafadhali hebu tueleweshe ni vipi utaweza kuthibitisha kwa Hadith hii ya Manzila kwamba Ali alishika cheo cha Utume.

Sifa Za Ali.

Muombezi: Hadith hii inathibitisha kwamba Ali anazo sifa tatu:

(1) Cheo cha Utume. (2) Cheo cha Mrithi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); na (3) Nafasi yake ya juu miongoni mwa Sahaba wote wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Kama alivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wafuasi wa Ali walimfananisha na Harun, ambaye alikuwa Mtume, aliwekwa kuwa Khalifa wa Musa, na alikuwa mbora juu ya Bani Israel wote.

Nawab: Harun alikuwa Mtume? Muombezi: Ndiyo. Nawab: Unaweza kuonyesha Aya kutoka kwenye Qur’ani yenye kuunga mkono nukta hii?

Muombezi: Allah ameutaja Utume wake katika Aya nyingi. Anasema: “Hakika tumekuletea wahyi kama tulivyompelekea wahyi Nuh na manabii baada yake. Na tulimpelekea Ibrahim na Ismail na Is’haq na Yakub na makabila; na Isa na Ayub na Yunus na Harun na Suleiman na Daud tukampa Zaburi.” (4:163) Na halafu tena Anasema: “Na mtaje Musa katika Kitabu, hakika yeye alikuwa mwenye kusafishwa, na alikuwa Mtume, Nabii. Na tukamwita upande wa kulia wa mlima, na tukamsongeza kuzungumza naye kwa siri. Nasi tukampa katika rehema zetu nduguye Harun, Nabii.” (19:51-53)

Hafidh: Hivyo kwa mujibu wa hoja yako, Muhammad na Ali wote walikuwa Mitume. Muombezi: Mimi sikuelezea katika njia unayoelezea wewe. Kwa kweli wewe mwenyewe unajua kwamba kuna tofauti kubwa ya maoni kuhusu ni Mitume wangapi walikuwepo. Baadhi wanadai kwamba walikuwepo 120,000 - au hata zaidi.

Lakini wote hao katika nyakati zao husika walikuwa wamegawanyika katika makundi na walikuwa (daraja ya) chini kwa Mtume mkuu ambaye kwake kilifunuliwa kitabu kitukufu kikiwa na sheria mpya za dini. Watano miongoni mwao walikuwa ni Mitume wakuu: Nuh, Ibrahim, Musa, Isa, na mwisho wa Mitume wote, Muhammad, ambaye cheo chake kilikuwa ndio cha juu zaidi.

Harun alikuwa mmoja wa wale Mitume ambao hawakuwa wa kudumu au wa kujitegemea. Alikuwa chini ya Sharia (mfumo wa kidini) ya ndugu yake Musa. Ali alifikia cheo cha Utume lakini hakupandishwa kwenye cheo hicho cha Mtume kwa asili yake yenyewe kwa vile alikuwa chini ya Shari’a ya Muhammad.

Katika hadith hii ya Manzila, madhumuni ya Mtume yalikuwa ni kuwaambia watu kwamba, kama vile ambavyo Harun amefikia Cheo cha Utume lakini alikuwa chini ya Musa, Ali alifikia cheo cha Utume. Uimamu ulipasishwa kwake, lakini alikuwa chini ya Muhammad (s.a.w.w.).

Umuhimu Wa Cheo Cha Ali.

Katika Sharhe yake juu ya Nahju’l-Balagha, Ibn Abi’l-Hadid anasema kuhusiana na hadith hii kwamba kwa kutaja cheo cha Harun katika kumlinganisha na Musa, Mtume alionyesha kwamba Ali bin Abu Talib alishika cheo hicho. Vivyo hivyo, Muhammad bin Talha Shafi’i, katika “Matalibu’s-Su’ul”, uk. 19, baada ya kuelezea cheo na nafasi ya Harun, anasema: “Maana hasa ya jambo hili ni kwamba, nafasi ya Harun katika kuhusiana na Musa ilikuwa kwamba Harun alikuwa ndugu yake, muwakilishi wake, mshirika katikaUtume, na wasii wake au Mshika Makamu wakati Musa alipokuwa safarini.

Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alikuwa vilevile katika hadith hii alionyesha kwamba, Ali alikuwa nayo nafasi ile ile kama aliyokuwa nayo Harun, isipokuwa Utume, ambao umeondolewa kwa kusema kwake: “Hakutakuwa na Mtume baada yangu.”

Kwahiyo, imethibitishwa kwamba Ali alikuwa ndugu yake Mtume, waziri (msaidizi) muwakilishi, na mrithi au Makamu wake, kama ilivyoelezewa na Mtume katika safari yake ya Tabuk. Hadith hii kwa umoja inakubaliwa kuwa ni ya kweli. Maoni kama haya yameelezewa na Ibn Sabbagh Maliki katika “Fusulu’l- Muhimma” uk. 29, na wengine wengi wa Maulamaa wenu mashuhuri.

Hafidh: Nafikiri madai yako kwamba kama Mtume wetu asingekuwa Muhuri (mwisho) wa Mitume, Ali angeishika nafasi hiyo, ni (madai) ya kipekee kwako wewe mwenyewe. Hakuna mtu mwingine aliyesema hivyo.

Muombezi: Madai haya hayakuishia kwangu na kwa Maulamaa wa Kishi’a tu. Maulamaa wenu wenyewe wamekuwa na maoni kama haya. Mmoja wa Maulamaa wenu wakubwa ni Mulla Ali bin Sultan Muhammad Harawi Qari.

Katika kitabu chake “Mirqat- e-Sharh bar Mishkat”, yeye anasema, akitoa maoni juu ya hadith ya Manzila; “Kuna dalili katika Hadith hii kwamba, kama kungekuwa na Mtume wa Allah baada ya mwisho wa Mitume, basi angelikuwa ni Ali.” Mwingine katika ulamaa wenu mashuhuri ambaye ameitafsiri Hadith hii kwa njia hii hii ni yule mwanachuoni ajulikanaye sana, Jalalu’d-Din Suyuti.

Anaandika kuelekea mwisho wa kitabu chake “Baghiatu’l’-Wu’az fi Tabaqatu’l- Huffadh”, akitoa Sanad (nyororo) ya wapokezi mpaka kufikia kwa Jabir Abdallah Ansari, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia Amiru’l-Muuminiina Ali. “Angelikuwepo Mtume yoyote baada yangu, basi angelikuwa ni Wewe!” Kwa nyongeza, Mir Seyyed Ali Hamadani Faqih Shafi’i anasema katika Mawaddad ya Pili ya Mawadda Sita katika kitabu chake “Mawaddatu’l-Qurba,” akinukuu riwaya kutoka kwa Anas bin Malik, kwamba Mtume alisema: “Hakika, Allah amenifanya mimi Mkuu kwa Mitume wote, akanichagua mimi kwa ubora, na akanifanyia mimi wasii, binamu yangu Ali.

Kupitia kwake yeye akaimarisha mabega yangu, kama vile mabega ya Musa yalivyoimarishwa na Harun. Yeye (Ali) ni makamu wangu na msaidizi wangu.

Kama kungelikuwepo na Mtume yoyote baada yangu, angelikuwa ni Ali, lakini hakutakuwa na Mtume baada yangu.”

Hivyo unaona kwamba siko peke yangu katika kudai cheo cha Utume kwa Ali. Mtume na Maulamaa wenu wamelikubali hilo. Kwa vile alikuwa na cheo cha Harun na kwa vile muda wa Utume ulikuwa umefikia kikomo Ali alikuwa mwenye kufaa zaidi kwa Ukhalifa. Moja ya dalili za utukufu wa cheo cha Ali ilikuwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliruhusu mlango wa nyumba ya Ali kubakia kufunguka kuelekea Msikitini.

Maneno haya yalisababisha mshangao na bumbuazi miongoni mwa Masunni. Muombezi akauliza kwa nini inakuwa hivyo.

Nawab: Ijumaa iliyopita tulikwenda Msikitini kusali. Hafidh Sahib akatueleza kuhusu ubora wa khalifa Abu Bakar. Alisema kwamba yeye aliruhusiwa kuweka mlango wa nyumba yake kuelekea Msikitini. Tunashangaa kusikia wewe ukisema kwamba ruhusa hii ilikuwa kwa Ali pekee. Tafadhali hebu ifafanue nukta hii.

Muombezi: (Akimgeukia kwa Hafidh Sahib) Ulitoa kauli hii?

Hafidh: Ndio Imesimuliwa kwenye hadith Sahih zetu, kama iliyoelezwa na Sahaba mchamungu na mwadilifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abu Huraira. Mtume aliagiza kwamba: “Milango yote ifunguliwayo kuelekea Msikitini ifungwe isipokuwa mlango wa nyumba ya Abu Bakr, kwani Abu Bakr anatokana na mimi na mimi ninatokana na Abu Bakr.”

Muombezi: Hakika unajua kwamba kwa sababu ya ubora wa Amiru’l-Mu’minina, Ali, Bani Ummaya walifanya juhudi endelevu kwa kupitia njia za siri na hususani kupitia kwa watu wenye kujipendekeza na kumsifu sifu mno Mu’awiya, kama Abu Huraira na Mughira ili kubuni hadith kama hizo. Aidha, wafuasi wa Abu Bakr, kwa sababu ya kumuunga mkono kwao yeye, waliziimarisha hadith hizi za kughushi.

Ibn Abi’l-Hadid, katika Sherhe yake ya Nahju’l-Balagha Jz. 1, na tena katika Jz. 3, uk. 17, anaeleza kwa urefu kwamba miongoni mwa hadith nyingi za kughushi ni hii ielezeayo kuhusu kufungwa kwa milango ya nyumba zote inayoelekea Msikitini isipokuwa ule wa Abu Bakr.

Kinyume na hadith hii ya kughushi, ziko hadith nyingi sahihi, ambazo zimesimuliwa sio tu katika vitabu Sahih vya Shi’a, lakini vilevile katika vitabu vya kutegemewa vya Mualamaa wenu wenyewe, kama “Sahih.”

Nawab: Kwa vile ni suala la ubishani, huku Hafidh Sahib akisema ni pekee kwa Abu Bakr, na wewe ukisema ni pekee kwa Ali, tungefurahia kama ungenukuu kutoka vitabu vyetu ili kwamba tuweze kulinganisha rejea zako na zile za Hafidh Sahib.

Hadith Ambayo Kwa Amri Ya Mtume Milango Ya Nyumba Inayoelekea Msikitini Ilifungwa Isipokuwa Mlango Wa Nyumba Ya Ali.

Muombezi: Vyanzo vifuatavyo vimesimulia kwamba, Mtume aliamrisha kwamba ile milango ya nyumba zote inayofunguka kuelekea Msikitini ifungwe isipokuwa mlango wa nyumba ya Ali: Ahmad bin Hanbal katika Musnad. Jz. 1 uk. 175, Jz. 2 uk. 26 na Jz. 4, uk. 369; Imam Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i katika “Sunan” na katika “Khasa’isi’l-Alawi” uk. 13 – 14; Hakim Nishapuri katika “Mustadrak”, Jz. 3, uk. 117- 125 na Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira” uk. 24 – 25 wameshuhudia usahihi wa Hadithi hii juu ya msingi wa Sanad za wasimuliaji wa Tirmidhi na Ahmad. Halafu, Ibn Athri Jazri katika “Athna’l-Matalib”, uk, 12, Ibn Hajar Makki, katika “Sawa’iq Muhriqa”, uk. 76; Ibn Hajar Asqalani katika “Fathu’l-Bari” Jz. 7, uk. 12, Tibrani katika “Ausat”, Khatib Baghdadi katika kitabu chake cha “Tarikh” Jz. 7, uk. 205, Ibn Kathir kati- ka “Tarikh” Jz. 7, uk. 342, Muttaqi Hindi katika “Kanzu’l-Ummal”, Jz. 6, uk. 408; Haithami katika “Majima’uz-Zawa’id”, Jz. 9, uk. 65; Muhibu’d-Din Tabari katika “Riyadh” Jz. 2, uk, 451; Hafidh Abu Nu’aim katika “Fadha’ilu’s-Sahaba” na katika “Hilyatu’l-Auliya” Jz. 4, uk. 183; Jalalu’d-Din Suyuti katika “Ta’rikhu’l-Khulafaa”, uk. 116, katika “Jamu’l- Jawami”, katika “Khasa’isul-Kubra” na katika “La’aliu’l-Masunu’a” Jz. 1, uk, 181; Khatib Khawarizmi katika “Manaqib”, Hamwaini katika “Fara’id”, Ibn Maghazili katika “Manaqib”, Munawi Misri katika “Kunuzu’d-Daqa’iq”, Sulayman Balkh Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, uk. 87, alitumia sura yote nzima ya 17 kwa suala hili hasa peke yake, Shahabu’d-Din Qastalani katika “Irshad Bari”, Jz. 6, uk. 81, Halabi kati- ka “Siratu’l-Halabiyya” Jz. 3, uk. 374 na Muhammad bin Talha Shafi’i katika “Matalibu’s- Su’ul” na wengine wengi, hususan kutoka miongoni mwa masahaba mashuhuri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wamesimulia kitu hicho hicho. Kwa mfano Khalifa Umar bin Khattab, Abdulla Ibn Abbas, Abdullah bin Umar, Zaid bin Arqam, na Jabir bin Abdullah Ansari wamethibitisha usahihi wa hadith hii.

Baadhi ya maulamaa wenu mashuhuri, kwa ajili ya kuepusha watu kutokana na kupotezwa na Bani Umayya wamesisitiza ukweli wa hadith hii. Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i, katika kitabu chake “Kifayatu’t-Talib” Sura ya 50, ameshughulika na hadith hii chini ya kichwa cha habari maalum. Akinukuu kutoka vyanzo sahihi anasema kwamba, kwa vile idadi ya milango ya masahaba wa Mtume ilifunguka kuelekea Msikitini, na kwa vile Mtume amepiga marufuku watu wote kuingia Msikitini na hali ya janaba au haidh, aliagiza kwamba milango yote ya nyumba ifungwe isipokuwa mlango wa nyumba ya Hadhrat Ali.

Yeye alisema: “Fungeni milango yote bali acheni mlango wa nyumba ya Ali ubakie wazi.” Muhammad bin Yusuph Shafi’i anasema kwamba ni Ali pekee yake ambaye kwam- ba aliruhusiwa kuingia na kukaa ndani ya Msikiti katika hali ya janaba. Aliendelea kusema: “Kwa ufupi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kuufanya upendeleo huu wa kipekee juu ya Ali ilikuwa ni heshima kubwa mno. Inaonyesha kwamba Mtume alijua kwamba Ali, Fatima, na dhuria wao walikuwa huru kabisa kutokana na uchafu kama inavyoonyeshwa wazi na ‘aya ya tohara’ katika Qur’ani Tukufu.”

Maneno haya ya mwanachuo wa Ki-Shafi’i yanaweza kulinganishwa na hadith iliyotajwa na Hafidh Sahib. Tukiachilia mbali vyanzo vyote Sahihi tulivyonukuu, kama mnao uthibitisho wowote wa utohara wa Abu Bakr, tafadhali utoeni. Ukweli ni kwamba hata Bukhari na Muslim katika ukusanyaji wao wa hadithi wameonyesha ukweli huu kwamba mtu aliyanajisika hawezi kukaa ndani ya Msikiti. Mtume alisema: “Hairuhusiwi kwa mtu yeyote ambaye sitohara kukaa ndani ya Msikiti isipokuwa kwa mimi na Ali.”

Labda ningeruhusiwa hapa kunukuu hadith kutoka kwa Khalifa wa pili Umar bin Khattab, ambayo imeandikwa na Hakim katika “Mustadrak”, uk. 125, na Sulaiman Balkhi katika. Yanabin’l-Mawadda Sura ya 56, uk. 210, na wengineo, kama Imam Ahmad bin Hanbal, Khatib Khawarizmi, Ibn Hajar, Suyuti, na Ibn Athir Jazri. Yeye alisema: “Hakika Ali bin Abi Talib alikuwa nazo sifa tatu za pekee, kama ningekuwa na mojawapo kati ya hizo, ingelikuwa ni bora zaidi kwangu mimi kuliko ngamia wa manyoya mekundu:-

(1) Mtume alimuozesha binti yake kwake, (2) Mtume aliagiza kwamba milango ya nyumba zote inayofunguka kuelekea msikitini ifungwe, isipokuwa mlango wa nyumba ya Ali; (3) Mtume alimpa bendera (ya Uislamu) siku ya vita ya Khaibar.”

Kutokana na maelezo haya, ni wazi sasa kwamba Ali alikuwa sawa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika sifa zote, kama vile tu Harun alivyokuwa kwa Musa. Hivyo wakati Musa alipomuona anafaa kwa kazi hii, alimuomba Allah kumfanya mshirika katika ujumbe wake, ili kwamba aweze kuwa Waziri wake. Vivyo hivyo, wakati Mtume alipoona kwamba hakuna yoyote miongoni mwa wafuasi wake wote mwenye kustahiki kama Ali, alimuomba Allah amfanye Ali kuwa Waziri na mshirika wake.

Nawab: Kuna hadith zaidi zinazohusu suala hili? Muombezi: Ndio, nyingi zinapatikana kuhusiana na suala hili katika vitabu vyenu wenyewe. Nawab: Niko tayari kuzisikiliza mradi ninyi pia (akionyesha upande wa Maulamaa wa upande mwingine) mtataka kusikiliza. Hafidh: Hakuna ubaya. Kusikiliza Hadith ni tendo la ibada kama simulizi yenyewe hiyo.

Wakati Akiwa Kwenye Rukuu Katika Sala Ali Alitoa Pete Kumpa Masikini.

Muombezi: Ibn Maghazili faqih Shafi’i katika “Manaqib” yake, Jalalu’d-Din Suyuti katika Durrul-Manthur mwana theolojia mashuhuri, Ahmad Tha’labi katika “Kashfu’l- Bayan,” Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkiratu’l-Khawasu’l-Umma”, kuhusiana na Aya ya Wilayat wananukuu kutoka kwa Abu Dharr Ghifari na Asma bint Umais (mke wa Abu Bakr) kwamba, wamesema kwamba siku moja walikuwa wanasali Sala ya Adhuhuri msik- itini wakati Mtume alikuwepo. Akaja masikini akaomba sadaka. Hakuna aliyempa chochote. Ali alikuwa anarukuu (katika Sala). Wakati alipoonyesha kidole chake, masikini alitoa ile pete kutoka kwenye kidole chake.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyaona yaliyotokea, akanyanyua kichwa chake kuelekea mbinguni akasema: “Ya! Allah, Ndugu yangu Musa alikuomba: ‘Ya! Allah, nifungulie kifua changu na nifanyie wepesi kazi yangu. Chagua kwa ajili yangu msaidizi kutoka kwenye familia yangu, Harun ndugu yangu.’” Ilifunuliwa Aya kumuambia Musa kwamba du’a yake imekubaliwa.

Allah akachagua kwa ajili yake msaidizi na akaimarisha mikono yake na akawapa uwezo na mamlaka kiasi kwamba hakuna hata mmoja aliyeweza kuwashinda nguvu. “na Musa akasema kumwambia ndugu yake Harun: ‘Chukua mahala pangu miongoni mwa watu, na utendee wema wala usifuate njia ya waharibivu’” (7: 142)

Cheo Cha Harun Kama Mtume Kadhalika Kama Khalifa.

Hafidh: Umesema kwamba Harun alikuwa ni mshirika wa Musa katika Utume. Ilikuaje tena akafanywa kuwa Khalifa wake? Mshirika katika Utume hushikilia nafasi ya juu kuliko ile ya ukhalifa au umakamu. Kama mshirika ni Mtume, na akafanywa kuwa Khalifa, huku ni kushusha cheo chake.

Muombezi: Kanuni ya Utume inahusika kwa Musa, na Utume wa Harun ulikuwa chini ya ule wa Musa. Lakini kuhusu kuhubiri alikuwa mshirika wake, kama ilivyo dhahiri kutokana na ombi la Musa, lililoandikwa katika Qur’ani: “Musa akasema: Ewe Mola Wangu! Nikunjulie kifua changu, na unifanyie kazi yangu kuwa nyepesi, na ulifungue fundo lililo katika ulimi wangu, wapate kufahamu maneno yangu.

Na unipe waziri katika watu wangu, Harun, ndugu yangu. Kwake niongeze nguvu zangu, na umshirikishe katika kazi yangu.” (at-Taha; 20: 25-32)

Vivyo hivyo, Ali alikuwa mmoja ambaye mbali na kuwa daraja ya Utume alikuwa ni mshirika wa Mtume katika hatua zote na sifa maalum.

Hafidh: Nimeshangazwa kukusikia unavyoitia chumvi nafasi ya Ali. Wote tumeshitush- wa. Umesema hivi punde tu kwamba Ali alikuwanazo sifa zote za Mtume.

Muombezi: Maelezo haya sio ya kutia chumvi. Ni ya ukweli. Makamu wa Mtume, kutokana na akili ya kuwaida, yapasa awe mfano wa Mtume. Hata Maulamaa wenu wakubwa wameelezea itiqad kama hii hii. Imam Tha’labi, katika Sherhe yake, ali- ithibitisha nukta hii.

Na yule mwanachuo mkubwa wa Kisunni, Alim Fadhili Seyyed Ahmad Shahabu’d-Din, katika Kitabu chake “Tauzihu’d-Dala’il” amerejea kwenye nukta hii kama ifuatavyo: “Sio siri kwamba Amiru’l-Mu’minin alifanana na Mtume wa Allah, katika nyingi ya sifa nzuri, matendo yasiyo ya kibinafsi, tabia, maombi kwa Allah, na njia zote tukufu za maisha. Hii imethibitishwa na riwaya sahihi na vianzo vya kutegemea, na haihitaji uthibitisho wowote au hoja. Baadhi ya Maulamaa wamezihisabu kuwa ni sawa sifa zile ambazo Ali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa nazo.”

Miongoni mwa sifa walizoshirikiana wote ni nasaba yao safi. Na tukihoji kutokana na aya ya tohara, tunaona kwamba Ali ni sawa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika utohara (Aya hii iliteremshwa kwa ajili ya watu watano: Muhammad, Ali, Fatima Hasan na Husain). Ali, kama Mtume alikuwa Mwakilishi wa Allah. Kwa mujibu wa madhehebu zote, aya ifu- atayo iliteremshwa kwa ajili ya Ali.

“Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na walioamini; ambao hushika Swala na hutoa Zaka nao wakiwa wamerukuu.” Ali alikuwa sawa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika utendaji kazi za Utume na kuhubiri, kama suala la Suratul-Bara’at linavyoonyesha. Mtume alimpa Abu Bakr baadhi ya aya za Sura hii na akamwagiza akazisome kwa watu wakati wa Hija. Mara Malaika Jibril ali- tokea mbele ya Mtume na akamwambia kwamba ni mapenzi ya Allah kwamba jambo la Qur’ani tukufu linapaswa kupelekwa ama na Mtume mwenyewe, au mtu ambaye ana- tokana naye. Ali alikuwa anafanana na Mtume katika wajibu wake kama Muakala wa Allah. Mtume Mwenyewe alisema: “Nimeamrishwa na Allah nitangaze hivi kwenu.”

Kisha akakamata mkono wa Ali na kusema: “Jueni nyote, yule ambaye ni mimi ni Maula kwake (yaani, ambaye mimi ni mwenye kutawalia mambo yake). Ali vilevile ni Maula (Bwana) wake.” Aidha, nafsi ya Ali imetangazwa kuwa ni nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aya ya kuapizana (Mubahila) inasema:

ﻓَﻤﻦ ﺣﺎﺟﻚَ ﻓﻴﻪ ﻣﻦ ﺑﻌﺪِ ﻣﺎ ﺟﺎءكَ ﻣﻦ اﻟْﻌﻠْﻢ ﻓَﻘُﻞ ﺗَﻌﺎﻟَﻮا ﻧَﺪْعُ اﺑﻨَﺎءﻧَﺎ واﺑﻨَﺎءﻛﻢ وﻧﺴﺎءﻧَﺎ وﻧﺴﺎءﻛﻢ واﻧْﻔُﺴﻨَﺎ واﻧْﻔُﺴﻢ ﺛُﻢ {ﻧَﺒﺘَﻬِﻞ ﻓَﻨَﺠﻌﻞ ﻟَﻌﻨَﺖ اﻟﻪ ﻋﻠَ اﻟْﺎذِﺑِﻴﻦ {61 “Watakaokuhoji katika haya baada yakukufikia ilmu hii waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zenu na wanawake zetu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Mwenyezi Mungu iwashukie waongo. (3: 61)

Tukirudi kwenye wakati ule ndani ya Msikiti, wakati Ali alipompa masikini pete yake na Mtume akamuomba Allah, akimuomba Yeye amfanye Ali kuwa mshirika wake katika Utume wake.

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaomba: “Ya Allah! Mimi ni Muhammad, mchaguliwa Wako na Mtume Wako. Kifungulie kifua changu. Na nifanyie wepesi kazi yangu na unichagulie msaidizi kutoka kwenye familia yangu, Ali. Imarisha mgongo wangu kupitia kwake.”

Abu Dharr amesimulia: “Kwa jina la Allah! Du’a ya Mtume ilikuwa haijafikia mwisho, Malaika Jibril akatokea na kumfunulia Aya hii: “Hakika rafiki yenu mlinzi ni Mwenyezi Mungu na Mtume Wake na walioamini, ambao wanadumisha Swala na kutoa Zaka huku wakiwa wamerukuu. (5: 55)

Du’a ya Mtume ilikubaliwa, na Ali aliteuliwa kama waziri wake. Muhammed bin Talha Shafi’i, katika “Matalibus-Su’ul”, uk. 19, amelishughulikia suala hili kwa urefu. Juu ya hayo, Hafidh Abu Nu’aim Isfahan katika “Manaqatu’l-Mutaharin”, Sheik Ali Ja’far kati- ka “Kanzu’l-Barahin”, Imam Ahmad Bin Hanbal katika “Musnad”, Seyyed Shahabu’d- Din katika “Tauzihu’d-Dala’il”, Jalalu’d-Din Suyuti katika “Durrul- Mansur”, na wanachuo wenu wengine mashuhuri wa madhehebu yenu wameisimulia hii katika vitabu vyao. Baadhi yao wamesimulia kutoka kwa Asma bint Umais (Mke wa Abu Bakr), na baadhi kutoka kwa masahaba wengine.

Ifuatayo imesimuliwa na Abdullah Ibn Abbas. “Mtume alitushika mikono mimi na Ali. Alisali rakaa nne, na akiwa amenyoosha mikono yake Mbinguni, akasema: “Ya Allah! Musa mtoto wa Imran, alikuomba umteulie msaidizi na kuifanya nyepesi kazi yake.

Mimi ni Muhammad. Nakuomba ufungulie kifua changu na uifanye nyepesi kazi yangu. Ufanye ulimi wangu kuwa fasaha ili watu wapate kuelewa maneno yangu. Niteulilie msaidizi kutoka kwa familia yangu, Ali. Niimarishe mgongo wangu kupitia kwake, na mshirikishe pamoja nami katika kazi yangu! Nilisikia sauti ikisema: ‘Ewe Muhammad! Nimelikubali ombi lako.’

Kisha Mtume akamshika Ali mkono na akasema: “Nyanyua mikono yako kuelekea juu mbinguni na umuombe Allah ili kwamba ajaalie kitu juu yako.’ Ndipo Ali akanyanyua mikono yake juu na kusema: ‘Ya Allah! Niahidi mimi kwa upande wako kwamba utanichukuwa mimi katika upendo Wako.” Mara Malaika Jibril akatokea na kule- ta Aya ifuatayo katika Suratul-Mariam: “Hakika wale waliomini na wakatenda mema, Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma atawajaalia mapenzi Yake juu yao.” 19: 96

Wakati masahaba wa Mtume waliposhangazwa na hili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akase- ma: “Kwa nini mnashangaa? Qur’ani Tukufu ina vigawanyo vinne: Robo moja inatuhusu sisi Ahlul-Baiti, robo moja inahusiana na mambo ya halali; robo moja ni kwa ajili ya mambo ya haramu; na robo moja inahusu maagizo na Sheria. Naapa kwa jina la Allah kwamba, kuna Aya nyingi katika Qur’ani ambazo zimeshushwa kwa kumsifu Ali.” Sheikh: Hata kama hadith hii itachukuliwa kama ni Sahih, haiashirii cheo maalum kwa Ali. Hadith hiyo hiyo imesimuliwa kuwahusu Khalifa Abu Bakr na Khalifa Umar. Qaz’a bin Suwaid amesimulia kutoka Ibn Malika ambaye anamnukuu Ibn Abbas akisema kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema; “Abu Bakr na Umar wako kwangu mimi kama alivyokuwa Harun kwa Musa.”

Muombezi: Yakupasa uangalie tabia za baadhi ya wasimuliaji wenu (wa hadith). Wakati mwingine unahoji kutokana na similizi za Amadi na wakati mwingine kutoka kwenye zile za yule mwongo mwenye sifa mbaya na mzushaji; Qaz’a bin Suwaid, pamoja na kwamba mualamaa wenu mashuhuhuri wamempuuza.

Allama Dhahabi, katika “Mizanul-l’tidal”, katika maelezo ya habari za Qaz’a bin Suwaid na Ammar bin Harun, wanaipuuza hadith hii na kusema kimkato tu: “Huu ni uwongo.” Wakati Maulamaa wenu wanampuuza Qaz’a, hadith anazosimulia inapasa zipuuzwe. Linganisha Hadith hii ya Qaz’a bin Suwaid na Sanad ya Hadith ambayo nimenukuu kutoka kwa maulamaa wenu mashuhuri mno wa madhehebu yenu na uamue mwenyewe ni hadith ipi unaikubali.

Mkutano Wa Tano; Jumanne Usiku 27 Rajab 1345, A.H.

Hafidh: Kutoka kwenye mazungumzo yako fasaha ya usiku uliopita ninahitimisha kwamba ulitaka kuthibitisha kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi anayefuatia mara moja wa Mtume, ingawa ukweli ni kwamba hadith hii ina maana makhususi tu. Ilisimuliwa wakati wa safari ya Tabuk. Hakuna uthibitisho kwamba ina maana ya jumla.

Muombezi: Katika Hadith hii neno “Manzila” (Cheo) linatumika katika maana ya jumla. Neno hili kwa kuonyesha upekee, huthibitsha kwa uwazi kwamba maelekezo ni ya maana ya jumla. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtaja Ali sambamba na neno “Mtume” na akaelezea Manzila yake (Yaani cheo chake) akitumia usemi, “isipokuwa kwamba haku- takuwa na Mtume baada yangu.”

Maulamaa wengi wakubwa na waandishi wamenukuu hadith hii hii kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye inasemekana alimuambia Ali: “Je, huridhiki kwamba kwangu wewe ni kama Harun alivyokuwa kwa Musa isipokuwa kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu?”

Muda wa kutokuepo kwake kwa siku arobaini, Musa hakuacha mambo katika uamuzi wa wafuasi wake. Alimchagua Harun, mtu bora miongoni mwa Bani-Israil kukaimu kama Khalifa wake na mrithi. Vivyo hivyo, Mtume wa mwisho, ambaye dini yake ni kamili zaidi, alikuwa na sababu kubwa zaidi za kuwalinda watu wake kutokana na machafuko ya dhamira zao huru.

Alihifadhi Sheria ya dini ili kwamba isije ikapitia katika mikono ya watu wasio na ujuzi, wale ambao wangeweza kuigeuza kwa mujibu wa matamanio yao. Watu wasio na ujuzi wangetegemea juu ya kukisia kwao na kusababisha migawanyiko katika mambo ya Sheria.

Hivyo, katika hadith hii tukufu Mtume anasema “Ali yuko kwangu mimi kama alivyokuwa Harun kwa Musa,” akithibitisha kwamba Ali alishikilia viwango vile vile vya daraja na mamlaka, sawa kama Harun alivyokuwa. Ali alikuwa bora kwa Umma wote na kwa ajili hiyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamchagua kuwa msaidizi wake na mrithi wake.

Hafidh: Uliyosema kuhusu Hadith hii hayana ubishani. Lakini kama utaangalia jambo hili kwa uangalifu, utakubali kwamba hadith hii haina maana ya jumla. Maana yake imekomea kwenye Vita vya Tabuk wakati Mtume alipomteua Ali kuwa Khalifa wake kwa muda maalum.

Hadith Ya Manzila Imesimuliwa Mara Nyingi:

Muombezi: Ungeweza kuwa ni mwenye haki katika maneno yako kama hadith hii inges- imuliwa wakati wa vita vya Tabuk tu. Lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliirudia hadith hii katika sehemu tofauti. Ilisimuliwa wakati undugu miongoni mwa watu tofauti katika Muhajirina (wahamiaji) ulipoanzishwa katika mji wa Makka. Ilisimuliwa vilevile katika mji wa Madina wakati undugu ulipoanzishwa kati ya Muhajirina na Ansar.

Katika nyakati zote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimchagua Ali kama ndugu yake, akisema, “Wewe kwangu mimi ni kama alivyokuwa Harun kwa Musa isipokuwa kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu.”

Hafidh: Kadiri nilivyochunguza mimi, hadith ya Manzila ilisimulwa wakati wa vita vya Tabuk tu. Mtume alimuacha Ali katika nafasi yake hali iliyofanya Ali kuhuzunika. Mtume akamliwaza kwa maneno haya. Nafikiri umepotoshwa.

Muombezi: Hapana, mimi sijakosea. Vitabu vyenu wenyewe vya Sahih vimeisimulia Hadith hii. Miongoni mwao ni Mas’ud (Mwandishi wa kutegemewa kwa mujibu wa mad- hehebu zote) ambaye ameandika katika “Muruju’dh-Dhahab”, Jz. 2, uk. 49; Halabi katika “Siratu’l-Halabiyya”, Jz. 2, uk. 26 na 120, Imam Abdu’r-Rahman Nisa’i katika “Khasa’isu’l-Alawiyya”, uk. 19, Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira”, uk. 13-14, Sulaiman Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 9 na 17, na vingine vingi vimesimulia hadith hii.

Wote wanasema kwamba, “Mbali na sehemu mbili za kuanzisha undugu (Makka na Madina kati ya Masahaba) imesimuliwa pia katika sehemu nyingine nyingi.

Kwa hiyo, hadith hii sio ya kutafsiriwa katika maana ya kukomea yenye mipaka au kwa tukio moja makhususi tu. Maana yake ya jumla ni jambo lililothubutu. Ni kupitia Hadithi hii ambapo Mtukufu Mtume alitangaza katika matukio yanayostahili umakamu wa Ali baada yake. Moja ya matukio hayo lilikuwa lile la vita ya Tabuk.

Hafidh: Inawezekana vipi Masahaba wa Mtume waliisikia Hadith hii katika maana yake ya jumla, wakijua kwamba ilikuwa na maana ya kwamba umakamu wa Ali uliridhiwa na Mtume na bado baada ya kifo cha Mtume, wakawa maadui na wakamkubali mtu mwingine kuwa Khalifa?

Muombezi: Nina marejeo mengi ya kuunga mkono jibu langu kwa swali lako, lakini majibu mazuri zaidi kwa wakati huu ni kuiangalia mitihani ya Harun katika hali inayqfanana kama hii hii. Qur’ani inaeleza kwamba, wakati Musa alipomteua Harun kuwa makamu wake, aliwakusanya mbele yake Bani-Israil (kwa mujibu wa baadhi ya taarifa watu 70,000 walikusanyika).

Musa alisisitiza kwamba, wakati wa kutokuwepo kwake yawapasa kumtii Harun, Khalifa na makamu wake. Kisha Musa alikwenda juu mlimani kuwa peke yake na Allah. Kabla ya mwezi kupita, Samiri alichochea fitna miongoni mwa Bani Isra’il.

Alitengeneza ndama (wa ng’ombe) wa dhahabu na Bani Israil wakiwa wamemuacha Harun, walikusanyika mbele ya msaliti Samiri katika idadi kubwa. Ilikuwa ni muda mfupi tu umepita kabla ya tukio hili, Bani Israil, hawa hawa walimsikia Musa akisema kwamba wakati wa kutokuwepo kwake Harun atakuwa Khalifa wake na kwamba yawapasa kumtii.”

Hata hivyo watu 70,000 walimfuata Samiri. Nabii Harun kwa nguvu sana alipinga kitendo hiki na kuwakataza wasijiingize katika matendo hayo ya dhambi, lakini hakuna hata mmoja aliyemsikiliza. Aya ya Sura ya A’raf inaeleza kwamba, wakati Musa aliporudi, Harun alimwambia: “Ewe mtoto wa mama yangu! Hakika watu hawa wameniona mimi mnyonge na walikuwa karibu waniuwe….” (7: 150)

Harun Alikuwa Ni Mrithi (Makamu) Wa Musa Aliyeteuliwa.

Bani Isra’il wenyewe waliyasikia maelekezo ya wazi kutoka kwa Musa, lakini Musa alipokwenda juu mlimani, Samiri akaitwaa fursa hiyo. Alitengeneza ndama wa dhahabu na kuwapoteza Bani Isra’il.

Kufanana Kwa Hali Ya Mambo Kati Ya Ali Na Harun.

Hali kadhalika, baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), baadhi ya watu ambao walikuwa wamemsikia akisema kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi wake, waligeuka dhidi ya Ali. Imam Ghazali ameelezea jambo hili katika mwanzo wa Makala yake ya nne kati- ka “Sirru’l-Alamin.” Anaeleza kwamba baadhi ya watu walirejea kwenye hali yao ya mwanzo ya ujinga.

Kwa hali hii, kuna kufanana kukubwa kati ya hali ya Harun na ile ya Ali. Kama wengi wa wanahistoria wenu wenyewe, Abu Muhammad Abdullah bin Muslim bin Qutayba Bahili Dinawari, Kadhi maarufu sana wa Dinawar, katika “Al-Imama wa Siyasa” Jz. 1, uk. 14 anasimulia kwa urefu matukio ya Saqifa. Anasema kwamba, walitishia kuchoma nyumba ya Ali na wakamchukua mpaka Msikitini kwa mabavu na kutishia kumuua isipokuwa achukue kiapo cha utii kwao. Ali alikwenda kwenye kaburi tukufu la Mtume na akarudia maneno yale yale ya Qur’ani ambayo Harun alimwambia Musa:

{ﻗَﺎل اﺑﻦ ام انﱠ اﻟْﻘَﻮم اﺳﺘَﻀﻌﻔُﻮﻧ وﻛﺎدوا ﻳﻘْﺘُﻠُﻮﻧَﻨ{150

“Yeye (Harun) akasema: Ewe Mtoto wa Mama yangu! Hakika watu hawa waliniona mimi mnyonge na walikuwa karibu waniuwe…” (7: 150).

Nawab: Wakati Umakamu wa Ali ulikuwa umethibitishwa, kwanini Mtume atumie maneno ambayo yalidokezea hiyo maana tu? Kwa nini hakutangaza wazi kwamba Ali alikuwa ndiye makamu wake, ili kwamba kusiweze kuja kutokea pingamizi lolote baada yake?

Muombezi: Nilikuambieni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alielezea ukweli katika njia zote. Hili liko dhahiri kutoka vitabu vyenu, ambavyo vimeandika hadith nyingi mno kuhusiana na suala hili. Watu wasomi wanaelewa kwamba kidokezo ni chenye nguvu sana kuliko maelezo ya vivi hivi tu, hususan pale kidokezo hicho kikiwa chenye mzizi wa kina mno kiasi kwamba kina maana nyingi sana ndani yake”

Nawab: Umesema kwamba kuna Hadith nyingi za wazi zilizoandikwa na Maulamaa wenu zinazohusu umakamu wa Ali. Tafadhali, je unaweza kutuelezea zaidi kuhusu hili? Tunaambiwa kwamba hakuna hadith ambayo inathibitisha Umakamu wa Ali.

Muombezi: Ziko hadith nyingi zinazohusu Ukhalifa katika vitabu vyenu wenyewe vya uhakika.

Hadith Ya Karamu Ya Ndugu Na Mtume Kumchagua Ali Kama Khalifa Wake.

Kati ya hadith zote zinazohusu umakamu wa Ali, hadith ya Karamu ndiyo ya muhimu zaidi. Katika siku ambayo Mtume alitangaza Utume wake, alitangaza pia kwamba Ali alikuwa Mrithi wake. Maulamaa wa Madhehebu yenu, wakiwemo Imam Ahmad bin Hanbal, Muwaffaq bin Ahmad Khawarizmi, Abu Ja’far Muhammad bin Jarir Tabari, Ibn Abi’l-Hadid Mutazali na kundi la wengine wamesimulia kwamba wakati Aya ya 214 ya Sura ya Shu’ara: “Na waonye jamaa zako wa karibu”, (26:214) ilipoteremshwa, Mtume alikaribisha Makuraish arubaini (miongoni mwa ndugu zake), nyumbani kwa Abu Talib.

Aliweka mbele yao mguu wa mbuzi, mkate na kikombe cha maziwa.Walicheka na kusema: “Ewe Muhammad! Hukuandaa chakula chakutosha hata kwa mtu mmoja.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Anzeni kula kwa jina la Allah.” Wakati walipokula na wakawa wameshiba vya kutosha, waliambizana: “Muhammad amewarogeni na chakula hiki.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasimama katikati yao na kusema; “Enyi kizazi cha Abdu’l-Muttalib! Allah Mwenye uwezo wote amenituma mimi kama Mjumbe kwa viumbe wote kwa jumla na hususan kwenu ninyi. Nakutakeni ninyi mutamke kauli mbili ambazo ni nyepesi na rahisi kwa ulimi, lakini katika mizani ya matendo ni nzito. Kama mtatamka kauli hizo mbili, mutakuwa mabwana wa nchi za Waarabu na wasio kuwa Waarabu.

Kupitia kauli hizo mtakwenda Peponi na mtapata kinga kutokana na Moto wa Jahannam. Maelezo hayo mawili ni:

Kwanza, kutoa shahada kwa Upweke wa Allah, na Pili kutoa Shahada kwa Utume wangu. Wa kwanza ambaye ataukubali wito wangu na kunisaidia katika kazi yangu atakuwa ndugu yangu, msaidizi wangu, mrithi wangu, na Makamu wangu baada yangu.

Mtume alirudia maneno haya ya mwisho mara tatu, na mara zote tatu hakuna aliyejibu isipokuwa Ali, akisema, “Mimi nitakusaidia, Ewe Mtume wa Allah.” Hivyo Mtume akatangaza: “Huyu Ali ni ndugu yangu, na yeye ndiye mrithi wangu, na Khalifa miongoni mwenu.

Uthibitisho Kutoka Ulamaa Wa Kisunni Na Waandishi Wa Ulaya.

Mbali na Maulamaa wa Kiislamu wa Kishia na Kisunni, Wanahistoria wengi walio waadilifu wa mataifa mengine wameelezea kwa kirefu Karamu hii. Walikuwa hawana upendeleo wa kidini, wakiwa wao sio Shia wala Sunni.

Mmoja wa Waandishi hawa ni mwana-Historia na Mwanafilosophia wa Kiingereza wa Karne ya kumi na tisa, Thomas Carlyle katika kitabu chake “Heroes and Hero-worship” ametoa maelezo ya kina juu ya karamu iliyofanyika nyumbani kwa Abu Talib. Baada ya maelezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali alisimama na akabainisha imani yake kwa Mtume.

Kwa ajili hiyo Ukhalifa uliwekwa juu yake. Waandishi wengine wa Ulaya wamethibitisha jambo hili, wakiwa ni pamoja na George Sale wa Uingereza na Hashim, Mkristo wa Syria katika kitabu chake “Maqalatu’l-Islam”, na Bw. John Davenport katika kitabu chake “Muhammad and the Qur’an.”

Wote wanakubali kwamba mara tu baada ya tangazo la Utume wake, alimuita Ali Ndugu yake, Msaidizi, Makamu na Khalifa wake. Aidha, Hadith nyingi zinathibitisha kwamba Mtume alisisitiza jambo hili katika matukio mengine mengi.

Hadith Za Wazi Na Dhahiri Kuhusu Ukhalifa Wa Ali.

(1) Imam Ahmad Ibn Hanbal katika “Musnad” yake na Mir Seyyed Ali Hamadani Shafi’i katika “Mawaddati’l-Qurba” kuelekea mwisho wa Mawadda ya nne, wameandika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema; “Ewe Ali! Utatekeleza majukumu kwa niaba yangu, na wewe ni makamu wangu juu ya wafuasi wangu.” (2) Imam Ahmad Ibn Hanbal katika “Musnad”, Ibn Maghazili Faqih Shafi’i katika “Manaqib” na Tha’labi katika “Tafsir” yake wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumwambia Ali: “Ewe Ali! Wewe ni ndugu yangu, Makamu, Mrithi na Mlipa madeni wangu.”

(3) Abu Qasim Husain bin Muhammad (Raghib Ispahani) katika “Mahadhiratu’l Udaba wa Muhawaratu’Sh-Shu’ara wa’l-Balagha” (kilichochapishwa Amira-e-Shazafiyya, Seyyed Husain Afandi, 1326 A.H.), sehemu ya 2, uk. 213, ananukuu kutokea kwa Ibn Malik kwamba Mtume amesema: “Hakika rafiki yangu, msaidizi, makamu na mbora wa watu ambaye ninamuacha nyuma yangu, ambaye atalipa deni langu na kutimiza ahadi yangu ni Ali bin Abu Talib.”

(4) Mir Seyyed Ali Hamadani katika “Mawaddatu’l-Qurba.” Katika mwanzo wa Mawadda ya sita, anasimulia kutoka kwa Khalifa wa Pili, Umar bin Khattab, kwamba wakati Mtume alipoanzisha uhusiano wa Kindugu miongoni mwa Masahaba, alisema: “Huyu Ali ni ndugu yangu katika dunia hii na kesho Akhera; yeye ni mrithi wangu kutoka miongoni mwa jamaa zangu na makamu wangu miongoni mwa umma wangu; yeye ndiye mrithi wa elimu yangu na mlipaji wa deni langu, chochote anachoniwia mimi, nami nawiwa naye, faida yake ni faida yangu na hasara yake ni hasara yangu; yoyote aliye rafiki yake ni rafiki yangu,mtu ambaye ni adui yake ni adui yangu.”

(5) Katika Mawadda hiyo hiyo, ananukuu hadith kutoka kwa Anas bin Malik, ambayo nimeitaja mapema. Kuelekea mwisho wake anasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema; “Yeye (Ali) ni Makamu wangu na Msaidizi.”

(6) Muhammad bin Ganji Shafi’i ananukuu Hadith kutoka kwa Abu Dharr Ghifari katika Kitabu chake, “Kifayatu’t-Talib” kwamba Mtume amesema: “Bendera ya Ali, Kiongozi wa Waumini, Kiongozi wa watu wenye nyuso zenye kung’ara, na Makamu wangu, itakuja kwangu katika chemchem ya Kauthari.”

(7) Baihaqi, Khatib Khawarizmi, na Ibn Maghazili Shafi’i wanaandika katika “Manaqib” zao kwamba alisema kumuambia Ali: “Sio sawasawa kwamba mimi niondoke kuwaacha watu bila ya wewe kuwa Makamu wangu kwa vile wewe ndiye bora zaidi wa Waumini baada yangu.”

(8) Imam Abu Abdur-Rahman Nisa’i mmoja wa Maimam wa vitabu sita (Siha) vya hadith, anasimulia kwa urefu kutoka kwa Ibn Abbas fadhila za Ali kuhusiana na hadith Na. 23 katika “Khasa’isu’l-Alawi.” Baada ya kuelezea cheo cha Mtume Harun, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema kumwambia Ali: “Wewe ni Makamu wangu baada yangu kwa kila Muumini.” Hadith hii na nyingine ambazo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ametumia maneno “baada yangu” zinathibitisha wazi kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi wa mara tu.

(9) Kuna “Hadith ya Uumbwaji,” ambayo imesimuliwa katika njia mbalimbali. Imam Ahmad Ibn Hanbal katika “Musnad” yake, Mir Seyyed Ali Hamadani katika “Mawadda-tul-Qurba”, Ibn Maghazili Shafi’i katika “Manaqib”, na Dailami katika “Firdaus” wamemnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Mimi na Ali tumeumbwa kwa Nuru Takatifu moja miaka 14,000 kabla Nabii Adam hajaumbwa. Kutoka kwenye mgongo wa Adam na kupitia kizazi chake kitukufu, Nuru hiyo ilirithiwa na Abdu’l- Muttalib, na kutoka kwake iligawanywa na kurithiwa na Abdullah (baba yake Mtume) na Abu Talib (baba yake Ali). Mimi nilipewa Utume, na Ali alipewa Ukhalifa.”

(10) Hafiz Abu Ja’far Muhammad bin Jarir Tabari (amekufa 310 A.H.) anaandika katika kitabu chake “Kitabu’l-Wilaya” kwamba Mtume amesema mwanzoni mwa khutuba yake maarufu pale Ghadir Khum; “Malaika Jibril amenifikishia amri ya Allah kunitaka kwamba nisimame sehemu hii na kuwajulisha watu kwamba Ali bin Abu Talib ni ndugu yangu, wasii wangu, na Khalifa wangu baada yangu. Enyi watu! Allah amem- fanya Ali kuwa Walii (mlezi) wenu, na Imam (kiongozi). Utii kwake ni wajibu juu ya kila mmoja wenu; amri yake ni yenye mamlaka ya juu; maneno yake ni kweli tupu; laana iwe juu yake yule ambaye anampinga, rehma ya Allah iwe juu ya yule ambaye amemfanya rafiki.”

(11) Sheikh Suleyman Balkhi katika “Yanabiu’l-Mawadda” anaelezea kutoka katika kitabu cha “Manaqib” cha Ahmad, na yeye kutoka kwa Ibn Abbas, hadith inayoelezea fadhila nyingi za Ali. Ninainukuu yote hapa. Ibn Abbas anasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ewe Ali! Wewe ni Mchukuzi wa Elimu yangu, Walii na rafiki yangu, Wasii wangu, Mrithi wa elimu yangu na khalifa wangu. Wewe ndiye mdhamini wa urithi wa Mitume wote waliotangulia. Wewe ni msiri wa Allah katika ardhi hii na hoja ya Allah kwa viumbe wote. Wewe ni nguzo ya Iman na mlezi wa Uislam. Wewe ni taa katika giza; nuru ya muongozo, na kwa ajili ya watu wa ulimwengu wewe ni bendera iliyonyanyuliwa juu kabisa.

Ewe Ali! Yeyote akufuatae wewe atakuwa ameokolewa; yule ambaye hakutii wewe ataangamia; wewe ni njia ing’aayo, na iliyonyooka; wewe ni Kiongozi wa watu wasafi, na Kiongozi wa Waumini; kwa yeyote yule ambaye mimi ni mwenye kutawaliwa mambo (Maula) wake wewe pia ni maula (bwana) kwake; na mimi ndiye Maula (Bwana) wa kila muumini; (Mwanaume na Mwanamke). Ni rafiki yako tu yule aliyezaliwa katika ndoa halali. Allah hakunipeleka mbinguni kuzungumza Naye bila kuniambia, ‘Ewe Muhammad! fikisha salamu zangu kwa Ali na muambie kwamba ni Imam wa rafiki zangu na nuru ya waabuduo!’ Hongera Ewe Ali, juu ya ubora huu wa ajabu.”

(12). Abu Mu’ayyid Muwafiqu’d-Din, msemaji mzuri wa Khawarizm, katika kitabu chake “Fadha’il’l- Amirul-Mu’minin,” kilichochapishwa mwaka 1313 A.H., Sura ya 19 uk. 240, ananukuu nyanzo ambavyo vimesimulia kwamba Mtume amesema: “Wakati nilipofika Sidratu’l-Muntaha (Kituo cha juu sana wakati wa Mir’raji) nilisemeshwa hivi: ‘Ewe Muhammad! Wakati ulipowajaribu watu, ni yupi uliyemuona mtiifu zaidi.’ Nikasema ‘Ali!’ Kisha Allah akasema: ‘Umesema kweli Muhammad!’ Tena akaendelea kusema:

“Umechagua Makamu ambaye atafikisha elimu yako kwa watu, na kuwafundisha waja wangu kutoka Kitabu Changu yale mambo ambayo hawayajui?’ Nikasema, ‘Ewe Allah! Yoyote utakayemchagua Wewe, nami nitamchagua.’ Yeye akasema: nimekuchagulia Ali juu yako. Ninamfanya yeye Makamu na Wasii wako.’ Na akampamba Ali na elimu Yake na uvumilivu. Yeye ni Kiongozi wa Waumini ambaye hakuna hata mmoja anayeweza kuwa sawa naye katika cheo miongoni mwa watangulizi wake au warithi wake.’” Kuna hadith nyingi kama hizi katika vitabu vyenu Sahih. Baadhi ya Maulamaa wenu waadilifu, kama Nizzam Basri, wameukubali ukweli huu. Salahu’d-Din Safdi katika kitabu chake “Wafa-Bi’l-Wafiyya”, kuhusiana na maelezo ya Ibrahim bin Sayyar bin Hani Basri, ajulikanae kama Nizzam Mu’tazali, anasema: Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alithibitisha Uimama wa Ali na akamchagua kuwa Imam. Masahaba wa Mtume walikuwa na habari kamili juu ya hili, lakini Umar kwa ajili ya Abu Bakr, aliufunika Uimamu wa Ali kwa pazia.”

Ni wazi kutoka katika vitabu vyenu, hadith na tafsiri za Qur’ani kwamba Ali alishika nafasi ya juu sana ya ubora. Khatib Khawarizmi anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas katika “Manaqib”, Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i katika kitabu chake “Kifayatu’t-Talib”, Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira” yake, Ibn Sabbagh Maliki katika “Fusulu’l-Mawadda”, Suleiman Balkhi Hanafi katika ‘Yanabiul-Mawadda’ na Mir Seyyed Ali Hamadani katika “Mawaddatu’l-Qurba”, Mawadda ya 5, nakala kutoka kwa Khalifa wa Pili, Umar bin Khattab – wote wakithibitisha pamoja na tofauti kidogo tu ya maneno kwamba Mtume alisema: “Kama miti yote ingelikuwa ni kalamu, kama bahari ingelikuwa ni wino, kama majini wote na watu wangekuwa waandishi - hata hivyo sifa za Ali bin Abu Talib zisingeweza kuorodheshwa zote.”

Tabia Za Masahaba.

Sheikh Abdu’s-Salam: (Akimgeukia Hafidh Muhammad Rashid Sahib). Niruhusu niseme kitu kwa ufupi. (Akigeuka kumwangalia Muombezi). Kamwe hatuzikatai sifa za hali ya juu za Ali, lakini kuweka mipaka ya utukufu kwake peke yake sio sawa, kwa vile Masahaba wakubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa kila mmoja, ni watu wa uadilifu. Unajiingiza katika mazungumzo ya upande mmoja, ambayo yanawapoteza watu. Niruhusu kunukuu hadith moja juu ya sifa zao ili ukweli juu ya jambo hili uweze kudhi- hirishwa.

Muombezi: Mimi sijishughulishi na mambo na watu, Aya za Qur’ani tukufu na hadith sahihi zinatuelekeza katika muelekeo mmoja. Ninaapa kwa Jina la Allah kwamba mimi simpendi au kumchukia yeyote kimbumbumbu. Ninawaomba wasikilizaji kunisimamisha kama wakati wowote nitakimbilia njia yoyote ambayo ni kinyume na hoja au busara. Hadithi zinazokubaliwa na madhehebu zote ziwe ndio za kutegemewa.

Sizikatai sifa nzuri za masahaba waadilifu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini yatupasa kutafuta miongoni mwao mmoja ambaye ni bora juu ya umma wote. Mjadala wetu sio wa kuhusu watu wema kwa kuwa wema ni wengi. Yatupasa kutafuta ni yupi aliyekuwa na sifa bora zaidi baada ya Mtume ili kwamba tuweze kumfuata yeye.

Sheikh: Unaleta vikwazo visivyo muhimu. Katika vitabu vyenu hakuna hata hadith moja yenye kuwasifu makhalifa. Tutahojiana vipi juu ya msingi huo?

Muombezi: Katika usiku wa kwanza wa majadiliano yetu, utakumbuka kwamba Hafidh Sahib mwenyewe aliukubali mjadala juu ya masharti kwamba hoja zetu zitegemee juu ya Aya za Qur’ani na juu ya Hadith zinazokubaliwa na Madhehebu zote. Kwa vile ninavyo vitabu vyenu Sahih, mimi nilikubali sharti hili. Kama ambavyo nyote mtathibitisha, sijatoka katika msimamo huo. Katika kuunga mkono hoja zangu nimesoma Aya za Qur’ani tu na Hadith zilizoandikwa katika vitabu Sahih vya Maulamaa wenu mashuhuri.

Wakati mlipoweka sharti hili, hamkujua kwamba mtakuja kunaswa baadae. Hata hivyo, bado sitaki sharti hili lichukuliwe kikamilifu moja kwa moja. Niko tayari kusikiliza hadith zenu za upande mmoja kama ni Sahih. Kisha tutaweza kuyaamua mambo kwa haki. Mimi sina kusita katika kuukubali ukweli kwenye kulinganisha fadhail za Ali.

Sheikh: Umetaja hadith inayohusu umakamu wa Ali lakini ukasahau ukweli kwamba kuna hadith nyingi kuhusu Abu Bakr.

Muombezi: Kwa kuzingatia akilini kwamba Maulamaa wenu wakubwa, kama vile Dhahabi, Suyuti na Ibn Abi’l-Hadid wameelezea kwamba Amawi - wafuasi wa Mu’awiyya na wa Abu Bakr wamebuni hadith nyingi katika kumtukuza Abu Bakr, unaweza kutaja hadithi moja kutoka miongoni mwa nyingi ya hizo ili kwamba mtu muadilifu aweze kua- mua juu ya usahihi wake.

Hadith Katika Kumtukuza Abu Bakr.

Sheikh: Kuna Hadith Sahihi iliyosimuliwa na Umar bin Ibrahim bin Khalid, ambaye anasimulia kutoka kwa Isa bin Ali bin Abdullah bin Abbas, na yeye kutoka kwa baba yake, na yeye kutoka kwa babu yake, Abbas, kwamba Mtume wa Uislamu alimwambia bwana huyo, “Ewe Ami yangu! Allah amemfanya Abu Bakr kuwa khalifa wa dini yake. Hivyo msikilize na umtii ili kwamba uweze kupata wokovu.” Muombezi: Hii ni Hadith iliyokataliwa.

Sheikh: Ni Hadith iliyokataliwa kwa vipi?

Muombezi: Maulamaa wenu mashuhuri wenyewe wameikataa. Kwa sababu wasimuliaji wa hadith hii walikuwa ni waongo wenye sifa mbaya na waghushaji, Maulamaa wenu hawaioni kama inastahili kukubalika. Dhahabi katika “Mizanul-I’tidal”, akiandika kuhusu Ibrahim bin Khalid, na Khatib Baghdadi akiandika kuhusu Umar bin Ibrahim anasema: “Yeye ni muongo mkubwa.” Na Hadith iliyosimuliwa na muongo haikubaliki.

Sheikh: Imesimuliwa kutoka vyanzo vya kuaminika kwamba mmoja wa masahaba wachamungu wa Mtume, Abu Huraira, alisimulia kwamba, Jibril alijitokeza mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akasema: “Allah anakutolea salaam, Anasema, ‘Nimemridhia Abu Bakr; muulize kama na yeye pia ameniridhia Mimi au laa.’”

Muombezi: Yatupasa kuwa waangalifu sana kuhusu kutaja Hadith. Nataka usikilize Hadith ambayo Maulamaa wenu wenyewe, kama Ibn Hajar (ndani ya Isaba) na Ibn Abdu’l-Bar (katika Isti’ab) wananukuu kutoka kwa Abu Huraira kwamba Mtume amesema: “Kuna wengi ambao huninukuu vibaya, na mwenye kunitafsiri vibaya makazi yake ni motoni. Wakati hadithi inaposimuliwa kwenu kwa niaba yangu ni lazima muipime na Qur’ani.”

Hadith nyingine inayokubaliwa na Madhehebu zote, imesimuliwa na Imam Fakhru’d-Din Radhi katika “Tafsir Kabir” Jz. 2, uk. 271 anasimulia kwamba Mtume amesema: “Wakati hadith kutoka kwangu inapoelezewa kwenu, iwekeni mbele ya Kitabu cha Allah kama ikikubaliwa na Qur’ani Tukufu, ikubalini. Vinginevyo, ikataeni.” Vitabu vya maulamaa wenu wenyewe mashuhuri vinaeleza kwamba mmoja wa wale ambao walighushi hadith kwa jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alikuwa huyu mtu aliyekataliwa, Abu Huraira, ambaye umemuita mchamungu.

Sheikh: Sikutarajia mtu wa kiwango chako kusema maneno ya kuzua kuhusu masahaba wa Mtume.

Muombezi: Unataka mimi nitishwe na neno “Sahaba”, lakini umekosea kama unafikiri neno “Sahaba” lazima libebe heshima. Kweli usahaba na Mtume unaongezea fadhila za mtu, lakini hili hutegemea juu ya sharti kwamba Sahaba huyo ni mtiifu kwa Mtume. Kama anakwenda kinyume na maelekezo ya Mtume, basi kwa hakika atakataliwa. Je, Munafiqina (wanafiki) hawakuwa miongoni mwa Masahaba wa Mtume? Ndiyo, walikuwemo, na wote walilaaniwa.

Sheikh: Haikuthibishwa kwamba walikataliwa. Kama walikataliwa ni uthibitisho gani kwamba watakwenda motoni? Je, kila mtu aliyekataliwa au kulaaniwa atakwenda motoni? Mtu aliyelaaniwa ni yule ambaye kwa mujibu wa Sheria ya wazi ya Qur’ani Tukufu, au Hadith ya Mtume ametangazwa hivyo (kuwa atakwenda motoni).

Tabia Ya Abu Huraira Na Laana Yake:

Muombezi: Kuna sababu za wazi kuonyesha kwamba Abu Huraira alikuwa sio mtu wa kuaminika. Maulamaa wenu wenyewe wamethibitisha ukweli huu. Moja ya sababu ya kulaaniwa kwake ni kwamba, kwa mujibu wa maneno ya Mtume, alikuwa rafiki wa mwana kulaaniwa wa mlaaniwa Abu Sufyan. Abu Huraira alikuwa mmoja wa wanafiki. Katika baadhi ya nyakati huko Siffin alisali Sala iliyoongozwa na Amiru’l-Mu’minin Ali.

Wakati mwingine alikaa katika meza ya chakula ya Mu’awiya kula chakula chake cha ghali. Kama ilivyoelezwa na Zamakhashari katika “Rabiu’l-Abrar” na Ibn Abi’l-Hadid katika Sherhe ya “Nahju’l- Balagha, wakati Abu Huraira alipoulizwa sababu za sera yake hii ya udanganyifu, yeye alisema; “Chakula cha Mu’awiyya ni kitamu sana na chenye ladha, na Sala nyuma ya Ali ni bora zaidi.”

Maulamaa wenu wenyewe, kama vile Sheikhu’l-Islam Hamwaini katika “Fara’id” Sura ya 37, Khawarizmi katika “Manaqib” Tibrani katika “Ausar”, Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’t-Talib” (na kundi la wengine), wananukuu kutoka kwa huyu huyu Abu Huraira na wengine kwamba Mtume amesema: “Ali yu pamoja na Haki na Haki iko pamoja na Ali.” Wakati alipomuacha Ali na kwenda kubembeleza hisani za Mu’awiya, hakuwa wa kulaaniwa. Kama mtu si tu hanyamazi aonapo matendo maovu ya Mu’awiya, bali hushirikiana naye hasa na humsaidia ili kuendeleza nafasi yake mwenyewe ya kilimwengu na kujaza tumbo lake, hivi huyo sio mtu wa kulaaniwa?

Abu Huraira huyo huyo mwenyewe anasimulia (kama ilivyoandikwa na Maulamaa wenu mashuhuri, kama Hakim Nishapuri katika Mustadrak, Jz. 2, uk. 124, Imam Ahmad bin Hanbali, Tibrani, na wengine), kwamba Mtume amesema: “Ali yu pamoja na Qur’ani na Qur’ani iko pamoja na Ali. Viwili hivi havitatengana mpaka vinifikie katika Chemchem ya Kauthar. Ali anatokana na mimi na mimi ninatokana na Ali. Yule ambaye anamtweza Ali, hunitweza mimi. Yule ambaye hunitweza mimi, anamtweza Allah.” Mu’awiya katika hutuba zake za Sala ya Ijumaa alimlaani Ali, Hasan, na Husein. Aliagiza kwamba katika mikusanyiko yote, watu hawa watukufu sharti walaaniwe.

Hivyo kama mtu kiukamilifu amejishirikisha na watu walaanifu kama hawa na yu aridhia matendo yao, huyu si wa kulaaniwa? Na wakati anashirikiana na watu hawa, kama huwasaidia kwa kughushi hadith na kulazimisha watu watoe laana dhidi ya watu watukufu, huyu si wa kulaaniwa?

Sheikh: Je, ni busara kwetu sisi kukubali masingizio haya, kwamba masahaba waamini- fu wa Mtume, wanaghushi hadith na waweze kuwalazimisha watu wamlaani Ali?

Muombezi: Kwa kweli ni vigumu kuamini kwamba sahaba mwaminifu angeweza kufanya kitu kama hicho. Kama yeyote katika Masahaba amefanya kitu kama hicho, ina maana kwamba hakuwa muaminifu. Kuna Hadithi nyingi zilizosimuliwa na Maulamaa wenu wenyewe kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Yule ambaye anamtweza Ali, hunitweza mimi na Allah.”

Sheikh: Kwa kuwa mkweli, wakati unawasingizia masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kusema kwamba, walighushi hadith, vipi tunaweza kutumaini kwamba hutahusisha maarubu mabovu kwa Maulamaa wa vyeo vya juu wa Kisunni? Ninyi Mashi’a mna tabia inayofahamika ya kuwakashifu watu maarufu.

Muombezi: Huna haki katika kuhusisha vitu kama hivyo kwetu. Historia ya Uislamu ya miaka 1400 iliyopita inathibitisha kinyume chake. Kuanzia mwanzo wa karne ya kwanza ya Uislamu, Bani Umayya wamewatukana Maimam Maasum, dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na wafuasi wao Mashi’a. Hata leo, maulamaa wenu mashuhuri wanasimulia hadith za kashfa dhidi ya Mashi’a katika vitabu vyao ili kuwapoteza watu.

Sheikh: Ni ulamaa gani wa Sunni aliyewakashifu Mashi’a?

Kashfa Za Ibn Abd Rabbih Dhidi Ya Mashi’a.

Muombezi: Mmoja wa Maulamaa waandishi wenu wakubwa, Shahabu’d-Bin Abu Umar Ahmad bin Muhammad bin Abd Rabbih Qartabi Andalusi Maliki (aliyefariki 48 A.H.), katika Indu’l-Farid yake Jz. 1, uk. 269, amewaita Mashi’a Mayahudi wa Umma huu.” Anasema kwamba, kama vile Mayahudi walivyokuwa maadui wa Wakristo, Mashi’a ni maadui wa Uislamu. Anadai kwamba, Mashi’a kama walivyo Mayahudi, hawaukubali ukweli kwamba mke aweza kutalikiwa mara tatu kutoka kwa mtu huyo huyo, wala hawaikubali sheria ya Edda.

Wote hapa, Mashi’a na Masunni ambao wana uzoefu na rafiki zao Shi’a watayacheka madai haya. Utaona katika vitabu vyote vya fiqih ya Kishi’a mashariti kuhusu talaka tatu na Edda baada ya talaka.

Vilevile anatuhumu kwamba Mashi’a, kama walivyo Mayahudi, ni maadui wa Jibril, kwa sababu Jibril amewasilisha maagizo ya Allah (Wahyi) kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), badala ya Ali (kicheko miongoni mwa wasikilizaji Mashi’a). Sisi Mashi’a tunamwamini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Tunaamini kwamba maagizo ya Allah yaliteremshwa kwake kupitia kwa Malaika Jibril, ambaye cheo chake ni cha juu zaidi kuliko kile kilichohusishwa kwake na mwandishi huyu asiye maana.

Kashfa Zilizotolewa Na Ibn Hazm.

Mwingine kati ya Maulamaa wenu wakubwa ni Abu Muhammad Ali bin Ahmad bin Said Ibn Hazm Andalusi (amekufa 456 A.H.), ambaye ameandika kimakhususi dhana potofu kuhusu Mashi’a katika kitabu chake mashuhuri “Kitabu’l-Fasil fi’l-Milal Wa’n-Nihal.” Kwa mfano anasema Shi’a sio Waislamu, ni waasi, wafuasi wa Mayahudi na Wakristo. Katika Juzuu ya 4, uk. 182, anaandika kwamba:

“Kwa mujibu wa Mashi’a, ni halali kuoa wanawake tisa.” Riwaya hii inaweza kukanushwa kwa urahisi sana kwa kuangalia vitabu vya Shi’a ambavyo kwa uwazi vimeeleza kwamba ni haramu kuwa na zaidi ya wanawake wanne katika ndoa ya kudumu, kwa wakati mmoja. Kuna tuhuma nyingi zinazofanana na hizi, zisizo na msingi wa mambo machafu yaliyohusishwa na Mashi’a katika kitabu chake hiki, ambayo ungeona aibu kuyasikia.

Kashfa Zilizotolewa Na Ibn Taimiyya

Mmoja wa Ulamaa wenu mtovu wa dini zaidi ni Ahmad bin Abdu’l-Halim Hanbali, ajulikanaye kama Ibn Taimiyyah (amekufa 728 A.H.). Alikuwa na dhamira mbaya kupita kiasi juu ya Mashi’a, Amru’l-Mu’minin Ali, na kizazi cha Mtume. Kitabu chake “Minhaju’s- Sunna” kimejaa uadui mkali dhidi ya Ali na kizazi cha Mtume.

Yeyote yule ambaye ana ufahamu wa ukweli japo kidogo angeshangazwa kusikia uongo wake. Kwa mfano anaandika kwamba: “Hakuna kundi kubwa la waongo kama madhehebu ya Shi’a, na ni kwa sababu hii kwamba waandishi wa vitabu vya Sahih (Sihah Sita) hawakuingiza katika vitabu vyao Hadith zilizosimuliwa na wao.”

Katika Juz. ya 10, uk. 23 anasema kwamba, Mashi’a wanaamini katika misingi minne ya dini - Tauhidi, Adili, Nubuwat na Uimam. Kwa kweli katika vitabu vya itiqad vya Shia, vinavyopatikana kila mahali, imeandikwa kwamba itiqad ya Shia ina misingi mitatu: Tauhid, Nubuwat, na Ma’ad (Siku ya malipo); Adil ni sehemu ya Tauhid na Uimam ni sehemu ya Nubuwat. Katika juzuu ya 1, Uk. 131, anaeleza kwamba Mashi’a hawakusanyiki misikitini. Hawasali Sala ya Ijumaa au Sala za jamaa. Kama wakisali wanasali kila mtu peke yake. (kicheko miongoni mwa Mashi’a).

Lakini kwa hakika tunaweka mkazo mkubwa katika Sala za jamaa. Katika miji mingi ya Iraq na Iran, ambayo ni vituo vya Mashi’a, misikiti yetu inajaa watu wanaoabudu wakisali sala za Jamaa. Katika ukurasa huohuo, anaandika kwamba Mashi’a hawafanyi Hijja kwenye Al-Kaaba.

“Hija yao ni ya kuzuru makaburi tu, ambayo wanaiona ni bora kuliko kwenda kuhiji Makka. Wanawalaani wale ambao hawafanyi Ziara kwenye makaburi.” (kicheko). Vitabu vya du’a vya Shi’a vina Sura maalum kwa ajili ya dua za hijja unaoitwa Kitabu’l-Hajj.

Wanatheolojia wa Kishi’a, wameandika vitabu vingi wakielezea kanuni kwa ajili ya Hijja, ambamo maelekezo maalum yametolewa kutekeleza taratibu za Hijja.

Hadithi nyingi kutoka kwa Maimamu wetu zinasisitiza kwamba, kama Muislamu (Shi’a au Sunni) anao uwezo na bado akashindwa kutekeleza Hija anatengwa katika Uislamu. Wakati akifa anaambiwa: “Kufa kifo chochote unachoweza, kiwe kifo cha kiyahudi, Kikristo, au cha muabudu moto.”

Unaweza kuamini kwamba mbele ya maelekezo kama hayo Mashi’a wangejiepusha na kutekeleza Hija? Kwa nyongeza juu ya tafsiri hizi potovu, mtu huyu muovu amesema kwamba mwanachuo mkubwa wa Kishia, Muhammad bin Muhammad bin Nu’man (Sheikh Mufid) ameandika “Manasikhu’l-Hajj li’l- Mashahid.”

Jina sahihi la kitabu hicho ni “Mansikhu’z-Ziarat”, ambacho kinapatikana kila mahali na ambacho kina maelekezo kuhusu kuzuru sehemu za Ziarat, pamoja na Ma Kuba matukufu ya wastahiki Maimamu.

Kama utaviangalia vitabu hivi vya Ziarat, utaona kwamba kutembelea kwenye makaburi ya Mtukufu Mtume na Maimamu kunapendekezwa, sio wajibu.

Uthibitisho mzuri dhidi ya tuhuma za mtu huyu mtovu wa dini ni mwendo unaofuatwa na Mashi’a, ambao huenda kuhiji kwa maelfu kila mwaka. Shutuma nyingine bandia ya muongo huyu, yaweza kupatikana katika juzuu ya 1, uk. 11, ambako anasema kwamba Mashi’a wanaita mbwa wao kwa majina ya Abu Bakr na Umar na kila siku wanawalaani (hao Abu Bakr na Umar). (Kicheko miongoni mwa Mashi’a). Hiki ni kichekesho.

Kwa mujibu wa itiqad ya Shia, mbwa ni najisi kabisa. Nyumba ya Muislam yenye mbwa hukosa baraka za Allah. Kwa hiyo, Waislamu Mashi’a wanakatazwa kabisa kufuga mbwa isipokuwa kwa masharti makhususi (kuwinda, kuilinda nyumba, au kuchunga mbuzi). Moja ya sababu nyingi za kutopatana kati ya Yazid na mjukuu wa Mtume, Imam Husain, ilikuwa kwamba Yazid alikuwa mpenzi wa mbwa na akiwafuga bila kuwa na sababu nzuri.

Ibn Taimiyya vilevile anaandika kwamba, kwa vile Mashi’a wanangojea kutokeza kwa yule wa mwisho wa Maimam wao, katika sehemu nyingi, hususan katika Sardab (Sakafu chini ya nyumba) ya Samara (ambako Mtukufu Imam alitoweka), ameandaliwa farasi kwa ajili yake. Wanamuita Imam wao ajitokeze, wakisema kwamba wamejiandaa kikamilifu kumtumikia Yeye.

Vilevile anaandika kwamba Mashi’a hugeuka kuelekea upande wa mashariki wakati wa siku za mwisho wa Ramadhani na kumwita Imamu ajitokeze. Baadhi yao huacha hata Sala zao za faradhi; wakifikiri kwamba kama watajishughulisha na kusali Sala zao na Imam akajitokeza wangeweza kukosa kumtumikia kwao. (Kicheko kwa Sunni na Mashi’a).

Hatushangazwi sana na Hadith za kuchekesha za mtu huyu muovu. Bali tunashangazwa na tabia za maulamaa wa sasa wa Misri na Damaskas ambao, bila kuwauliza Mashi’a ambao wanaishi nao, wanafuata upumbavu wa mtu kama Ibn Taimiyya. Itakuwa inachosha sana kutoa orodha ndefu ya riwaya zisizo sahihi za Ibn Hajar Makki, Hafidh, na Kadhi Ruzbahan. Vitabu yao vinajulikana, ingawa katika mtazamo wa usahihi, hivyo havina thamani.

Kwa mfano “Milal Wa’n-Nihal” cha Muhamma Ibn Abdu’l-Karim Shahrastani (amekufa 548 A.H.), katika macho ya wanachuoni, hakina thamani hata kidogo. Mtu hataweza kuona chochote ndani yake isipokuwa itiqad bandia kabisa zilizohusishwa kwa Mashi’a, kama kumuabudu Ali na imani ya kuhama kwa roho (baada ya kufa kuingia katika mwili mwingine). Ni wazi hakuwa mtu mwenye elimu. Akiandika kuhusu Shi’a Ithnashariyya, yeye anasema kwamba, kaburi la Ali Ibn Hadi Muhamma Naqi, ambaye amekuja baada ya Imam Muhammad Taqi, liko Qum.

Lakini hata watoto wadogo wanajua kwamba Kuba Tukufu la Imam Ali Naqi liko ubavuni mwa kuba la Mtoto wake, Imam Hasan Askari huko Samarra. Sidhani kwamba rejea nyingine zaidi za namna hii ni muhimu kuthibitisha kwamba ulamaa wa Kisunni wamebuni riwaya za uongo kuhusu Mashi’a. Na siko peke yangu katika kulenga shutuma dhidi ya uaminifu wa Abu Huraira. Maulamaa wa Kisunni wamefichua tabia zake mbaya katika vitabu vyao wenyewe.

Tabia Za Abu Huraira Na Hadith Zinazotaka Alaaniwe.

Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali katika Sherhe yake ya “Nahaju’l-Balagha,” Jz. 1, uk. 358, na katika Jz. 4, anasimulia kutoka kwa Sheikh na mwalimu wake, Imam Abu Ja’far Asqalani, kwamba Mu’awiyya bin Abu Sufyani aliandaa kikundi cha masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na watoto wa masahaba hao kwa lengo la kughushi hadith.

Miongoni mwa wale waliobuni hadith chafu dhidi ya Ali walikuwa Abu Huraira, Amr bin Aas, na Mughira Ibn Sha’ba. Akitoa maelezo juu ya ngano hizi, Ibn Abil-Hadid anasimulia kwamba, wakati mmoja Abu Huraira aliingia Msikiti wa Kufa na kuona kundi kubwa la watu ambao walikuja kumpokea Mu’awiya. Alipaza sauti yake kwenye lile kundi la watu: “Enyi watu wa Iraq. Mnafikiri kwamba nitasema uongo katika kumpinga Allah na Mtume Wake na kujinunulia moto wa Jahanam? Sikieni kutoka kwangu nilivyosikia kutoka kwa Mtume. ‘Kila Mtume ana Haram (Sehemu takatifu ya kuishi) na Haram yangu ni Madina.

Mtu ambaye anahusika na uzushi katika mji wa Madina analaaniwa na Allah, na Malaika Wake, na pamoja na wanadamu wote!’ Naapa kwa jina la Allah, kwamba Ali alihusika na uzushi.” (Yaani, Ali alichochea mfarakano miongoni mwa watu, hivyo, kwa mujibu wa Mtume, anapaswa kulaaniwa).

Wakati Mu’awiya alipolifahamu hili (kwamba Abu Huraira amefanya kitu kama hicho kwa ajili yake na amekifanya katika makao makuu ya Ali, Kufa), alimuita, akampa zawadi, na akamfanya Gavana wa Madina. Je, matendo yake mabaya hayatoshi kuthibitisha kwamba anastahili laana? Je, ni sahihi kwamba mtu ambaye amemfanyia ubaya mbora zaidi wa Makhalifa achukuliwe kama mchamungu kwa sababu tu amewahi kuwa sahaba wa Mtume?

Sheikh: Ni katika sababu zipi ambazo Mashi’a wanamuona kuwa kalaaniwa?

Muombezi: Kuna hoja nyingi katika kuunga mkono maoni yetu. Mojawapo ya hizo ni kwamba, mwenye kumtukana Mtume, kwa mujibu wa madhehebu zote amelaaniwa. Kwa mujibu wa Hadith ambayo nimeitaja mapema, Mtukufu Mtume amesema: “Mwenye kumtukana Ali, hunitukana mimi, Mwenye kunitukana mimi humtukana Allah.” Ni dhahiri kwamba Abu Huraira alikuwa mmoja wa wale ambao, sio tu amemtukana Ali bin Abu Talib, bali ambaye alighushi hadith kuwachochea wengine kumtukana yeye.

Njama Ya Abu Huraira Na Busr Bin Artat Katika Mauwaji Ya Waislamu.

Vilevile tunamlaani Abu Huraira kwa kula njama kwake na Busri Ibn Artat katika mauaji ya maelfu ya Waislamu. Imesimuliwa na wanahistoria wenu wenyewe, akiwemo Tabari, Ibn Athir, Ibn Abi’l-Hadid, Allama Samhudi, Ibn Khaldum, Ibn Khallikan, na wengine kwamba Mu’awiyya alimtuma yule katili Busri Ibn Artat pamoja na wanajeshi wa Syria

4,000 kwenda Yemen kupitia Madina kuwasaga watu wa Yemen na Mashi’a wa Ali. Washambuliaji hawa waliwaua maelfu ya Waislamu katika mji wa Madina, Makka, Ta’if, Jabala (Mji wa Tihama), Najran, Safa, na vitongoji vyake. Hawakuwaacha vijana au wazee wa Bani Hashim au Shi’a wa Ali.

Waliwaua hata watoto wadogo wawili wa binamu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Ubaidullah bin Abbas Gavana wa Yemen, ambaye alikuwa ameteuliwa na Ali. Inasemekana kwamba zaidi ya Waislamu 30,000 waliuwawa kwa amri ya dhalimu huyu.

Bani Umayya na wafuasi wao walitenda ukatili huu wa kiwendawazimu. Mpendwa wenu Abu Huraira alishuhudia unyama huu na hakuwa kimya tu, bali pia aliuunga mkono kikamilifu.

Watu wasio na hatia kama Jabir bin Abdulla Ansari, na Abu Ayyub Ansari walitafuta pa kukimbilia. Hata nyumba ya Abu Ayyub Ansari ambaye alikuwa mmoja wa masahaba wakubwa wa Mtume, ilichomwa moto. Wakati Jeshi hili lilipoelekea Makka, Abu Huraira alibakia Madina. Sasa naomba mtueleze, kwa jina la Allah, iwapo mtu huyu mlaghai ambaye alikuwa katika usahibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa miaka mitatu, na ambaye amesimulia zaidi ya Hadith 5,000 kutoka kwa Mtume, hakusikia hadithi zile mashuhuri zinazohusu mji wa Madina?

Maulamaa wa madhehebu zote (kama Allama Samhudi katika “Ta’rikhu’l-Madina,” Ahmad bin Hanbal katika “Musnad” Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira” uk. 163) wamenukuu kutoka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye amesema mara kwa mara: “Yule ambaye atawatishia watu wa Madina na mateso, atatishwa na Allah na atalaaniwa na Allah, Malaika Wake, na wanadamu wote. Allah hatakubali kitu chochote kutoka kwake.

Na alaaniwe yule mwenye kuwatisha watu wa Madina. Kama mtu yeyote atawadhuru watu wa Madina, Allah atamyeyusha kama risasi katika moto.”

Sasa ni kwa nini Abu Huraira alijiunga na jeshi lile ambalo liliiangamiza Madina? Kwa nini alibuni hadith zenye upinzani kwa makamu sahihi wa Mtume? Na kwa nini aliwachochea watu kumtukana yule mtu ambaye kuhusu yeye Mtume amesema: “Kumtukana yeye ni kunitukana mimi?”

Wewe amua iwapo kama mtu ambaye amebuni hadith kwa jina la Mtume hakuwa mwenye kulaaniwa? Sheikh: Umekosa huruma, sio vyema kwako kumwita Sahaba muaminifu mno wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mtovu wa dini na mzushi.

Laana Ya Abu Huraira Na Kupigwa Kwake Na Umar.

Muombezi: Siko peke yangu ambaye “sina huruma” kwa Abu Huraira. Mtu wa kwanza ambaye hakuwa na huruma naye alikuwa Khalifa wa Pili, Umar bin Khattab. Ibn Athir na Ibn Abi’l-Hadid katika Sherhe yake ya Nahjul’l-Balagha, Jz. 3, uk. 104 (iliyochapishwa Misri) na wengine wengi wameeleza kwamba Khalifa Umar alimchagua Abu Huraira kuwa gavana wa Bahrain katika mwaka wa 21 A.H., watu wakamjulisha Khalifa kwamba Abu Huraira amejikusanyia mali nyingi na amenunua farasi wengi.

Kwa ajili hiyo Umar akamuondoa madarakani katika mwaka wa 23 A.H. Mara tu Abu Huraira alipoingia kwenye baraza, Khalifa akasema: “Ewe adui wa Allah na adui wa Kitabu Chake! Umeiba mali ya Allah?

Alijibu: “Sikuiba, bali watu wamenipa zawadi.” Ibn Sa’ad katika “Tabaqat” Jz. 4, uk. 90, Ibn Hajar Asqalani katika “Isaba”, na Ibn Abdi-e-Rabbih katika “Iqdu’l-Farid” Jz. 1, wanaandika kwamba Khalifa alisema: “Wakati nilipokufanya Gavana wa Bahrain, ulikuwa huna hata kiatu katika miguu yako, lakini sasa nimesikia kwamba umenunua farasi kwa dinari 1,600. umeipataje mali hii.’ Alijibu, ‘Hizi ni zawadi za watu ambazo faida yake imekuwa marudufu zaidi.’

Uso wa Khalifa uligeuka kuwa mwekundu kwa hasira, na alimpiga viboko kwa nguvu sana kiasi kwamba mgongo wake ulivuja damu. Kisha akaamuru zile dinari 10,000 ambazo Abu Huraira alizikusanya huko Bahrain zichukuliwa kutoka kwake na ziwekwe kwenye mfuko wa Baitu’l-Mal.” Hii haikuwa mara ya kwanza kwa Umar kumchapa Abu Huraira. Muslim anaandika katika Sahih yake Jz. 1, uk. 34, kwamba wakati wa uhai wa Mtume, Umar bin Khattab alimpiga Abu Huraira kwa nguvu sana mpaka akaanguka chini. Ibn Abi’l-Hadid anaandika katika Sherhe yake ya “Nahjul’l-Balagha” Jz. 1, uk. 360: “Abu Ja’far Asqalani amesema: Kwa mujibu wa watu wetu mashuhuri (Yaani Wanachuoni), Abu Huraira alikuwa mtu muovu.

Hadith zilizosimuliwa na yeye hazikukubaliwa. Umar alimchapa na kiboko na akamwambia kwamba alikuwa amebadilisha hadith na alihusisha maneno ya uongo kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).’” Ibn Asakir katika kitabu chake “Ta’rikh Kabir”, na Muttaqi katika “Kanzu’l-Umma” wanasimulia kwamba Khalifa Umar alimchapa viboko, alimkemea na akamkataza kusimulia hadith kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Umar alisema: “Kwa sababu unasimulia hadithi nyingi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) una uwezo tu wa kuhusisha uongo kwake. - Yaani mtu anatazamia mtu muovu kama wewe kutoa uongo tu kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hivyo ni lazima uache kusimulia Hadith kutoka kwa Mtume; vinginevyo nitakupeleka katika nchi ya Dus.” (Kabila katika Yemen ambalo kwamba Abu Huraira anatokana nalo). Ibn Abi’l-Hadid, katika Sherhe yake ya “Nahju’l-Balagha”, Jz. 1, uk. 360 (iliyochapishwa Misri) anasimulia kutoka kwa mwalimu wake, Imam Abu Ja’far Asqalini, kwamba Ali alisema: Jihadharini na muongo mkubwa miongoni mwa watu, Abu Huraira Dusi.”

Ibn Qutayba, katika “Ta’wil-e-Mukhtalifu’l-Hadith,” na Hakim katika Mustadrak Jz. 3, na Dhahabi katika “Talkhisu’l-Mustadrak” na Muslim katika Sahih yake, Jz. 2, wakielezea kuhusu tabia za Abu Huraira, wote wanasema kwamba Aisha alikuwa alipingana naye mara kwa mara na kusema: “Abu Huraira ni muongo mkubwa ambaye hughushi hadith na kuzihusisha na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

“Kwa ufupi sio sisi peke yetu ambao tumemkataa Abu Huraira. Kwa mujibu wa Khalifa Umar, Amirul’l- Muuminiina Ali, Ummu’l-Muuminina Aisha, na Masahaba wengine na wafuasi wa Mtume, wamesema kwamba alikuwa sio muaminifu kabisa.

Kwa ajili hiyo, Masheikh wa madhehebu ya Mutazila na Maimam wao, na ulamaa wa Kihanafia kwa kawaida wanakataa hadith zilizosimuliwa na Abu Huraira.

Aidha, katika Sherhe yake ya Sahih Muslim, Jz. 4, Nadwi anasisitiza nukta hii: “Imam Abu Hanifa amesema: ‘Masahaba wa Mtukufu Mtume kwa ujumla walikuwa ni wacha-Mungu na wanyofu. Ninaikubali kila hadith yenye ushahidi iliyosimuliwa na wao, lakini sizikubali hadith ambazo chanzo chake ni Abu Huraira, Anas Ibn Malik, au Samara bin Jundab.”

Tunamkataa Abu Huraira yule yule, ambaye Khalifa Umar alimchapa viboko na kumuita mwizi na muongo. Alikataliwa na Ummu’l-Mu’minina Aisha, Imam Abu Hanifa, na masahaba wengi na wafuasi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tunamkataa Abu Huraira huyo huyo ambaye alikataliwa na kuitwa muongo na Bwana wetu, kiongozi wa wenye kuabudu Mungu mmoja, Ali, na akakataliwa na Maimamu watukufu na dhuria wa Mtume.

Tunamkataa Abu Huraira ambaye alikuwa muabudu tumbo, ambaye pamoja na kujua ubora wa Ali, alimpuuza. Alimpendelea mfadhili wake, mlaaniwa Mu’awiya, alikaa kwenye meza yake ya chakula na kula vyakula vitamu naye, na akatunga hadithi za kumpinga Ali.

Kwa mtazamo wa mjadala wetu mpaka sasa, ninyi na mimi tunawajibika kuangalia kwamba wakati hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ikiwa kwenye mjadala, yatupasa kwanza kuirejesha kwenye Qur’ani Tukufu. Kama hadith inakubaliana na Qur’ani, yatupasa kuikubali, vinginevyo la.

Majibu Kwa Hadith Idhaniwayo Kwamba Allah Alisema, “Nimeridhishwa Na Abu Bakr - Je Na Yeye Ameridhika Na Mimi?”

Hadithi ambayo umeisimulia mapema (ingawa ni ya upande mmoja) yaweza kurejeshwa kwenye Qur’ani Tukufu. Kama hakuna pingamizi, hapana shaka tutaikubalia. Hata hivyo, aya moja ya Qur’ani inasema: “Na hakika tumemuumba mwanadamu, nasi tunajua yanayopita katika nafsi yake; nasi tukaribu naye zaidi kuliko mshipa wake wa shingo.” (50:16)

Mnatambua kwamba Hablu’l-Warid (mshipa wa shingo) ni usemi wa kawaida utumiwao kuelezea ukaribu uliozidi mno. Maana ya Aya hii ni kwamba, Allah ni Mjuzi wa yote. Hakuna kinachofichika kwake, hata kiwe ndani kiasi gani katika moyo wa mtu. Allah anajua siri za nyoyo zetu.

Na katika Sura ya “Yunus” Anasema: “Na hushughuliki katika kazi yoyote, wala hasomi humo (kitu chochote) katika Qur’ani, wala hamfanyi kitendo chochote, isipokuwa sisi tunakuwa mashahidi juu yenu mnaposhughulika nayo. Hakifichikani kwa Mola wako kitu chochote (hata) kilicho sawa na uzito wa mdudu chungu, la katika ardhi wala katika mbingu. Wala (hapana) kidogo kuliko hicho wala kikubwa, isipokuwa kimo katika kitabu (cha Allah) kielezacho (kila kitu).” (10:61).

Kwa mujibu wa Aya hizi, na kwa mujibu wa akili ya kuzaliwa, hakuna kinachofichikana kwa Allah. Anajua mtu anachofanya au kufikiri. Sasa linganisha hadithi hii na Aya hizi mbili na uone kama zinaweza kupatanishwa. Itawezekana vipi kwamba Allah Mwenye Nguvu zote asijue furaha ya Abu Bakr, kiasi kwamba Yeye mwenyewe awajibike kumuuliza kama ameridhishwa Naye au la? Akili ya kuzaliwa na Qur’ani Tukufu vinaonyesha kwamba “Hadith” hii ni ya uwongo.

Hadith Zenye Kumsifu Abu Bakr Na Umar Na Kutostahili Kwao.

Sheikh: Hakuna shaka kwamba Mtume alisema: “Allah atajionyesha kwa watu wote kwa ujumla na makhususi kwa Abu Bakr.” Vilevile alisema: “Allah hakuweka kitu chochote kwenye kifua changu ambacho hakukiweka kwenye kifua cha Abu Bakr.” Vilevle alisema: “Mimi na Abu Bakr ni kama farasi wawili ambao wanalingana sawa katika mbio.” Alisema tena: “Katika anga kuna malaika 80,000 ambao huomba rehma kwa ajili ya yule ambaye ni rafiki wa Abu Bakr na Umar. Na katika usawa wa upande mwingine wa anga kuna Malaika 80,000 ambao humlaani yule ambaye ni adui wa Abu Bakr na Umar.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vilevile alisema: “Abu Bakr na Umar ni wabora wa wanadamu wote kuanzia mwanzo mpaka mwisho.”

Cheo cha Abu Bakr na Umar kinaweza kupimwa kutokana na Hadithi ambayo kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Allah ameniumba mimi kutokana na nuru Yake, Abu Bakr kutokana na nuru yangu, na Umar kutokana na nuru ya Abu Bakr. Umar ni taa ya watu wa Peponi.”

Kuna hadithi nyingi kama hizo ambazo zimeandikwa katika vitabu vyetu Sahihi. Nimesimulia Hadithi chache tu ili kwamba ujue Cheo halisi cha makhalifa.

Muombezi: Maana ya hadhithi hizi huongozea kwenye uasi na ukafiri wa kidini, ambavyo inadhihirisha wazi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kusema vitu kama hivyo. Hadithi ya kwanza inaonyesha kwamba Allah ana mwili na ni ukafiri kuamini kwamba Allah ana mwili. Hadithi ya pili inaonyesha kwamba Abu Bakr alishiriki katika yale yaliyoteremshwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hadithi ya tatu inamaanisha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa hali yoyote hakuwa mbora zaidi kwa Abu Bakr. Hadithi nyingine inapingana na hadithi nyingi, ambazo zinakubaliwa na madhehebu zote, kwamba watu wabora zaidi wa ulimwengu huu ni Mtume Muhammad na kizazi chake.

Mbali na ukweli huu wa wazi, Maulamaa wenu mashuhuri kama Muqaddas katika kitabu chake “Tadhkiratu’l-Muzu’a”, Firuzabadi Shafi’i katika kitabu chake “Safaru’s-Sa’adat”, Hasan bin Athir Dhahabi katika kitabu chake “Mizanul-l’tidal”, Abu Bakr Ahmad bin Ali Khatib Baghdad katika kitabu chake cha “Ta’rikh”, Abu’l-Faraj Ibn Jauzi katika “Kitabu’l- Muzu’a”, na Jalalu’d-Din Suyuti katika “Al’Lu’ali’l-Masnu’a fi’l-Abadusi’l-Muzu’a” - wote wamehitimisha kwamba Hadithi hizi ni zakutungwa. Zinapingana na Qur’ani Tukufu na akili ya kuzaliwa.

Sheikh: Lakini hebu angalia hadithi nyingine, ambayo hakika ni sahihi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Abu Bakr na Umar ni Mabwana wa wazee wa Peponi.”

Muombezi: Kama utaichunguza kwa karibu zaidi Hadith hii inayotarajiwa, unaweza ukaona kwamba, mbali na ukweli kwamba ulamaa wenu wenyewe wameikataa, hadithi hii haiwezekani kuwa inatoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kila mtu anajua kwamba pepo haitaingiwa na wazee. Hakuna mabadiliko ya kidogo kidogo huko. Kuna riwaya nyingi zinazokubaliwa na madhehebu zote zinazohusiana na jambo hili. Moja ya hizo ni suala la Ashja’iyya, mwanamke mzee ambaye alikuja kwa Mtume.

Katika maongezi yake, Mtume alisema: “Wanawake wazee hawataingia Peponi.” Yule mwanamke alihuzunika sana na akasema, huku akilia: “Ewe Mtume wa Allah, hii ina maana mimi sitaingia Peponi.” Alipokwisha kusema hivi, akaondoka. Mtume akasema: “Muambieni kwamba siku hiyo atakuwa kijana na ataingia Peponi.” Kisha akasoma Aya ifuatayo kutoka kwenye Qur’ani Tukufu:

{اﻧﱠﺎ اﻧْﺸَﺎﻧَﺎﻫﻦ اﻧْﺸَﺎء {35

{ﻓَﺠﻌﻠْﻨَﺎﻫﻦ اﺑﺎرا {36

{ﻋﺮﺑﺎ اﺗْﺮاﺑﺎ {37

{ﺻﺤﺎبِ اﻟْﻴﻤﻴﻦ {38

“Hakika tumewafanya wakuwe katika umbo (jipya), na tumewafanya vijana kama kwamba ndiyo kwanza wanaolewa, wanapendana na waume zao (walio) hirimu moja na wao, kwa ajili ya watu wa kheri. (56: 35 – 38).

Katika Hadithi nyingine inayokubaliwa na wote ninyi na sisi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Wakati wakazi wa Peponi watakapoingia Mbinguni, watakuwa vijana na nyuso safi halisi, nywele za kipilipili, macho ya haiba, umri wa miaka 33.”

Sheikh: Maelezo yako ni kweli kama yalivyo, lakini hii ni hadithi Makhususi (yaani maalumu kwa ajili ya Abu Bakr na Umar).

Muombezi: Sielewi. Una maana gani kwa kusema “Hadith Makhususi.” Una maana kwamba Allah atapeleka kikundi cha wazee Peponi ili kwamba Abu Bakr na Umar waweze kuwa mabwana zao? Isitoshe, ulamaa wenu mashuhuri wanaiona Hadith hii kuwa ni ya kutungwa. Mtume ametupa utaratibu kwa ajili ya kuthibitisha Hadithi. Nilisema mapema kwamba Hadithi yoyote ambayo haipatani na Qur’ani ni ya kupuuzwa. Wanachuoni wetu sisi wanakataa Hadithi nyingi zinazodaiwa kutokana na Mtume na Maimamu Watukufu katika misingi ya kanuni iliyotamkwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.):

“Wakati wowote itakapoelezwa Hadith kwamba inatoka kwangu, irejesheni kwenye Qur’ani Tukufu; kama inakubaliana nayo, ikubalini, vinginevyo, ikataeni”.

Kwa ajili hiyo, wanachuoni wetu hawakubali hadith ambazo hazikubaliani na Qur’ani Tukufu. Nilieleza mapema kwamba Maulamaa wenu wameandika vitabu juu ya kukataa Hadithi za kutungwa.

Kwa mfano Sheikh Majdu’d-Din Muhammad bin Yaqub Firuzabadi katika “Safaru’s- Sa’ada” (uk. 142), Jalalu’d-Din Suyuti katika “Kitabu’l-Lu’ali”, Ibn Jauzi katika “Muzu’a”, Muqaddasi katika “Tadhkiratu’l- Muzu’a”, na Sheikh Muhammad bin Darwish (Mashuhuli kwa jina la Hul-e-Beiruti) katika “Asna’l-Talib” - wote wamesema kwamba nyororo ya wasimuliaji wa hadith isemayo kwamba Abu Bakr na Umar ni mabwana wa wazee wa peponi humchanganya Yahya bin ‘Anbasa. Dhahabi anasema kwamba, “huyu Yahya ni msimuliaji asiyeaminika, na Ibn Jan anashikilia kwamba Yahya alikuwa akitunga hadithi.”

Hivyo, mbali na hoja zangu zilizopita, hata Maulamaa wenu wanaiona kuwa ni hadithi ya uwongo. Kwa kweli, inawezekana kwamba ilitungwa na wafuasi wa Abu Bakr, familia ya Umayya. Ili kuwadhalilisha Bani Hashim na kizazi cha Mtume, walikuwa wakitunga Hadith sambamba na zile sahihi zilizosimuliwa kwa kuitukuza familia ya Mtume.

Mtu kama Abu Huraira, ili kupata mwanya wa kuingia kwenye kundi maalum la kiutawala la Bani Umayya, mara kwa mara alighushi hadithi.

Kwa sababu ya uadui wao kwa kizazi cha Mtume, walitunga hadithi sambamba na zile zinazokubaliwa na Maulamaa wote wa Shi’a na Sunni.

Nawab: Ni Hadithi ipi inayokubaliwa katika suala hili?

Hadith Ya Kwamba Hasan Na Husein Wote Ni Mabwana Wa Vijana Wa Peponi.

Muombezi: Hadith iliyo Sahihi ni kwamba Mtume alisema: “Hasan na Husein ni mabwana wa vijana wa peponi, na baba yao ni mbora zaidi yao.” Maulamaa wengi wamesimulia Hadith hii. Kwa mfano Khatib Khawarizmi katika “Manaqib”, Mir Seyyid Ali Abu Abdu’r-Rahman Nisai katika “Khasa’is-il-Alawi” (hadithi tatu), Ibn Sabbagh Maliki kati- ka “Fusulu’l-Muhimma”, uk. 159, Sulaiman Balki Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 54, Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira”, akinukuu kutoka kwa Tirmidhi, Ibn Maja na Imam Ahmad Hanbal, Sibt Ibn Jauzi katika uk. 133 wa “Tadhkiratul-Mawadda,” Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad, Tirmidhi katika “Sunan” na Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’l-Talib” Sura ya 97, wameandika hadithi hii na huyu wa mwisho akaongeza kwamba, msimuliaji mkubwa wa hadith, Imam Abdu’l-Qasim Tibrani, vilevile ameiandika Hadith hii katika “Mu’ajamu’l-Kabir” na akaorodhesha wasimuliaji wake mbalimbali wote, kama vile Amir’l-Mu’minina Ali, Umar bin Khattab (Khalifa wa Pili), Hudhaifa Yamani, Abu Sa’id Khudri, Jabir bin Abduullah Ansari, Abu Huraira, Usama bin Zaid, na Abdullah bin Umar.

Baada ya hapo. Muhammad bin Yusufu amesema kwamba ni hadith sahihi isiyo na ubis- hani. Kutovunjika muala wa nyororo ya wasimuliaji wa hadith hii ni uthibitisho wa kuwa kwake Sahihi. Aidha, Hafidh Abu Nu’aim Isfahani katika “Hilyatu’l-Auliya” Ibn Asakir katika “Tarikh Kabir” Jz. 4, uk. 206, Hikam katika “Mustadrak”, Ibn Hajar Makki katika “Sawa’iq-Muhriqa” - kwa ufupi, Maulamaa wenu mashuhuri wote wamethibitisha usahihi wa hadith hii.

Sheikh: Lakini hebu angalia hadith hii, ambayo usahihi wake hakuna atakayeukataa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Katika taifa lolote atakaloishi Abu Bakr, sio sahihi kwa mtu yoyote kufadhilishwa kuliko yeye.” Hadithi hii inathibitisha kwamba Abu Bakr ni bora kwa Umma wote.

Muombezi: Nasikitika kwamba unakubali hadith bila udadisi hata kidogo. Hadith hii ingelikuwa imesimuliwa na Mtume, yeye mwenyewe angetenda kwa mujibu wake. Lakini alitoa kipaumbele kwa Ali mbele ya macho ya Abu Bakr. Je, Abu Bakr hakuwepo wakati wa Mubahila pale ambapo Ali alichaguliwa kama nafsi ya Mtume? Katika vita vya Tabuk, wakati Abu Bakr mtu mzima na mzoefu zaidi alikuwepo, kwa nini Mtume akamfanya Hadhrat Ali naibu na Khalifa wake?

Kwa nini Abu Bakr aliondolewa kwa amri ya Mungu na kupendelewa Ali, wakati mtu mzima huyu alipotumwa kwenda Makka kulingania Uislamu na kuzisoma Aya kutoka Sura ya tisa ya Qur’ani “Baraat (Tawba)?” Wakati Abu Bakr alikuwepo kwa nini Mtume alimchukua Ali kwenda pamoja naye Makka kuvunja Masanamu, akamfanya apande juu ya mabega yake, akimuamrisha avunje sanamu la Hubal? Kwa nini wakati Abu Bakr alikuwepo Mtume akamtuma Ali kwenda kuhubiri miongoni mwa watu wa Yemen? Mwisho, kwa nini Mtume akamfanya Ali kuwa Mrithi na Makamu wake badala ya Abu Bakr?

Sheikh: Kuna hadithi yenye nguvu sana kutoka kwa Mtume ambayo haiwezi kupingwa. Imesimuliwa na Amr bin Aas ambaye amesema: “Siku moja nilimuuliza Mtume. ‘Ewe Mtume wa Allah! Ni nani unayempenda sana miongoni mwa wanawake?’

Akajibu: ‘Aisha.’ Nikasema: ‘Nani unayempenda sana miongoni mwa wanaume?’ Akajibu, ‘Baba yake Aisha, Abu Bakr.’” Kwa vile Mtume amempendelea Abu Bakr juu ya watu wote, basi alikuwa mbora kwa umma wote. Ukweli huu wenyewe, peke yake ni uthibitisho wenye kuvutia zaidi wa kuonyesha uhalali wa ukhalifa wa Abu Bakr.

Majibu Kwa Hadith Inayodhaniwa Kwamba Abu Bakr Na Aisha Walipendelewa Zaidi Na Mtume.

Muombezi: Mbali na ukweli kwamba hadithi hii imetungwa na wafuasi wa Abu Bakr, haipatani na Hadith Sahihi ambazo zinakubaliwa na Madhehebu zote. Hadith hii inapasa kuangaliwa kwa mitazamo miwilii. Kutoka upande wa Ummu’l-Mu’minina Aisha na kutoka upande wa Abu Bakr. Mtume asingeweza kusema kwamba kati ya wanawake wote alimpenda Aisha zaidi. Nimekwisha sema tangu mwanzo kwamba hii inakinzana na Hadithi nyingi Sahihi zilizomo kwenye vitabu vyote vya Sunni na Shia.

Sheikh: Ni hadithi zipi zinazopingana na riwaya hii?

Muombezi: Kuna hadithi nyingi kuhusu Mama wa Maimamu; Fatima Zahra, zilizosimuli- wa na Maulamaa wenu wenyewe, ambazo zinapingana na maelezo yako. Hafidh Abu Bakr Baihaqi katika Kitabu chake cha “Ta’rikh”, Hafidh Ibn Abdu’l-Bar katika “Isti’ab”, Mir Seyyid Ali Hamadani katika “Mawaddatu’l-Qurba”, na wengine miongoni mwa Maulamaa wenu, wamesimulia kwamba Mtume mara kwa mara amesema: “Fatima ni mbora wa wanawake wote na wa umma wangu.”. Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad”, na Hafidh Abu Bakr Shirazi katika “Nuzulu’l- Qur’ani Fi Ali” anasimulia kutoka kwa Muhammad bin Hanafiyya, na yeye kutoka kwa Amirul-Mu’minina Ali, Ibn Abdu’l-Bar katika “Isti’ab”, katika maelezo juu ya Fatima, yaliyosimuliwa katoka kwa Ummu’l-Mu’minina Khadija, kutoka kwa Abdu’l-Warith Bin Sufyani na kutoka kwa Abu Dawud na Anas Bin Malik, Sheikh Sulaimani Balkhi Hanafi katika Sura ya 55 ya “Yanabiu’l-Mawadda”, Mir Seyyid Ali Hamadani katika “Mawaddatu’l-Qurba”, Mawadda ya 13 - hawa na wasimuliaji wengine wa Hadith wameelezea kutoka kwa Anas Bin Malik kwamba, Mtume alisema:

“Kuna wanawake wanne walioshinda wote wa ulimwengu: Mariam, bint wa Imran; Asiya, bint wa Mazahim; Khadija, bint wa Khalid; na Fatima, binti wa Muhammad”.

Khatib katika “Ta’rikh Baghdad;” anasimulia kwamba Mtume aliwatangaza wanawake hawa wanne kuwa ni wabora wa wanawake wote wa ulimwengu. Kisha akamtangaza Fatuma kuwa ni mbora wao wote ulimwenguni na Akhera.

Muhammad bin Ismaili Bukhari katika “Sahihi” yake, na Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad” yake wanasimulia kutoka kwa Aisha bint Abu Bakr kwamba Mtume alisema kumwambia Fatima:

“Ewe Fatima, ninakupa habari njema kwamba Allah amekufanya mbora wa wanawake wote duniani na amekufanya wewe kuwa ndiye mtakatifu zaidi wanawake wote wa Uislamu.”. Vilevile Bukhari katika “Sahihi” yake, sehemu ya 4, uk. 64 Muslim katika Sahih yake Jz. 2, katika Mlango wa “Fadhail za Fatima,” Hamidi katika “Jam’a Bainus-Sahihain” yake, Abdi katika “Jam’a Bainu’s- Sihahu-s-Sitta” hawa na wengine wengi wamesimulia kutoka kwa Ummu’l-Mu’miniina Aisha kwamba Mtume alisema: “Ewe Fatima! hufurahi kwam- ba wewe ni Bibi wa wanawake wote wa ulimwengu?”

Ibn Hajar Asqalani amenukuu maneno hayo hayo katika kitabu chake “Isaba” kuhusiana na maisha ya Fatima pamoja na maelezo: “Wewe ni mbora wa wanawake wote wa ulimwengu.”

Vilevile, Bukhari, Muslim, Imam Ahmad Bin Hanbal, Tibrani na Sulaiman Balkhi Hanafi - wote wameiandika hadith hii.

Aya Juu Ya Mapenzi Kwa Familia Ya Mtume.

Kwa nyongeza, Bukhari na Muslim; kila mmoja katika Sahih yake, Imam Tha’labi katika Tafsir yake, Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad”, Tibrani katika Mu’jamu’l-Kabir, Sulaimani Balkh Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 32 kutoka kwenye “Tafsir” ya Ibn Abi Hatim, “Manaqib” ya Hakim, Wasit na Wahidi, “Hilyatu’l-Auliya” cha Hafidh Abu Nu’aim Isfahani na Fara’id ya Hamwaini, Ibn Hajar Makki katika “Sawa’iq, Muhriqa” chini ya Aya ya 14 kwa idhini ya Ahmad, Muhammad bin Talha Shafi’i katika “Mutalibu’s-Su’ul” uk. 8, Tabari katika Tafsir, Wahidi katika Asbabun-Nuzul, Ibn Maghazil katika “Manaqib”, Muhibu’d-Din Tabari katika “Riyazu’n-Nuzra”, Mu’min Shablanji kati- ka “Nuru’l-Absar,” Zamakhshari katika “Tafsir”, Imam Fakhru’d-Din Razi katika “Tafsir Kabir”, Sayyid Abu Bakr Shahabu’d-Din Alawi katika “Rishfatu’s-Sadi min Bahr-e- Faza’il-e-Baniu’l-Nabi’i’l-Hadi” Sura ya 1 uk. 22 –23 kutoka “Tafsir” ya Baghawi, “Tafsir” ya Tha’labi, “Manaqib” ya Ahmad, “Tafsir Kabir” na “Ausat” vya Tibrani na Sadi, Sheikh Abdullah bin Muhammad bin Amir Shabrawi Shafi’i katika “Al-Ittihaf” uk.5 kutoka kwa Hakim, Tibrani na Ahmad, Jalalu’d-Din Suyuti katika “Ihya’u’-l-Mayyit” kutoka Tafsir za Ibn Mudhir, Ibn Abi Hatim, Ibn Mardawaih, na “Mu’jamu’l-Kabir” cha Tibrani; na Ibn Abi Hatim na Hakim - kwa ufupi, wengi wa maulamaa wenu mashuhuri (ukiondoa wafusi wachache wa Bani Umayya na maadui wa Ahlul Bait), wamesimulia kutoka kwa Abdullah bin Abbas na wengine, kwamba wakati Aya ifuatayo ya Qur’ani Tukufu ilipoteremshwa:

“Sema: Siombi malipo yoyote kwa haya bali mapenzi kwa jamaa zangu; na anayefanya wema tutamzidishia wema…” (42:23).

Kikundi cha Masahaba wakauliza, “Ewe Mtume wa Allah! ni nani hao jamaa zako ambao mapenzi kwao yamefanywa wajibu juu yetu na Allah?” Mtume Akajibu, “Ni Ali, Fatima, Hasan na Husein.” Baadhi ya Hadith zina maneno, “na watoto wao” yaani watoto wa Hasan na Husein.

Kukubali Kwa Shafi’i Kwamba Mapenzi Kwa Ahlu Bait Ni Wajibu.

Hata Ibn Hajar (mtu shupavu sana asiye mvumilivu) katika kitabu chake “Sawa’iq-Muhriqa” uk. 88, Hafidh Jamalu’d-Din Zarandi katika “Mi’raju’l-Rasul”, Sheikh Abdullah Shabrawi katika “Kitabu’l-Ittihaf”, uk. 29, Muhammad Bin Ali Sabban wa Misir katika “As’afu’r-Raghibin”, uk. 119, na wengine wamesimulia kutoka kwa Imam Muhammad Bin Idris Shafi’i, ambaye ni mmoja wa Maimamu wenu wanne na kiongozi wa kidini wa madhehebu ya Shafi’i, kwamba alikuwa akisema:

“Enyi Ahli Bait wa Mtume wa Allah! Mapenzi kwenu yamefanywa wajibu kwetu na Allah kama ilivyokuja katika Qur’ani Tukufu (akirejea aya iliyotajwa hapo juu).

Inatosha kwa hadhi yenu kwamba, kama mtu hatatoleeni salamu katika Sala, Sala yake haitakubaliwa.” Sasa ninakuuliza, inawezekana hadithi ya upande mmoja iliyoelezwa na wewe ikasimama dhidi ya Hadith zote hizi Sahihi ambazo zimekubaliwa na madhehebu yote ya Sunni na Shia?

Dhana Potofu Kuhusu Mapenzi Ya Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Kwa Aisha.

Kuhusu mapenzi ya Mtume kwa Aisha, unafikiri kwamba kwa sababu ya matamanio yake ya kimwili alimpenda Aisha zaidi kuliko Fatima? Ni kweli kwamba Aisha alikuwa mke wake na kwa hiyo ni Ummu’l-Mu’minina (Mama wa Waumini) kama wake wengine wa Mtume. Lakini je, inakubalika kwamba alimpenda Aisha zaidi kuliko alivyompenda Fatima, ambaye mapenzi kwake yamefanywa wajibu katika Qur’ani Tukufu, ambaye kwa ajili yake iliteremshwa aya ya utakaso na ambaye alijumuishwa kwenye Mubahila? Hakika unajua kwamba Mtume na warithi wake hawakushawishiwa na matamanio ya kimwili, na kwamba walimgeukia Allah peke yake.

Kujifunga huku kulikuwa kwa makhususi kabisa ni halisi hasa kwa yeye mwisho wa Mitume. Aliwapenda wale ambao Allah aliwapenda. Je, yapasa sisi kuzikataa hadithi hizi sahihi ambazo zimekubaliwa na Maulamaa wa madhehebu zote, na ambazo zinakubaliana na Aya za Qur’ani Tukufu, au tuichukulie Hadith ambayo umesimulia hivi punde tu kuwa ni ya kutungwa? Unadai kwamba Mtume amesema alimpenda Abu Bakr zaidi kuliko mtu mwingine yoyote. Lakini dai hili vilevile liko mbali na hadithi Sahihi nyingine nyingi ambazo zimesimuliwa na Maulamaa wenu wenyewe, ambao wamesisitiza kwamba, kwa mujibu wa Mtume, mtu aliyependwa sana alikuwa ni Ali.

Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Alimpendelea Ali Kuliko Watu Wengine Wote.

Sheikh Suleiman Balkhi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 55, anasimulia kutoka kwa Tirmidhi hadith ya Buraida kwamba, kwa mujibu wa Mtume, mwanamke aliyependwa zaidi alikuwa ni Fatima na mwanaume aliyependwa zaidi sana alikuwa ni Ali. Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’t- Talib” Sura ya 91, anaandika kutoka kwa Ummu’l-Mu’minina Aisha kwamba alisema: “Allah hakuumba mtu yeyote ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpenda zaidi kuliko Ali.”

Anaongeza kusema kwamba, hii ndio hadith ambayo Ibn Jarir katika Manaqib yake na Ibn Asakir Damishqi katika tarjuma yake wameisimulia kutoka kwa Ali.

Muhyi’d-Din na Imamu’l-Haramain Ahmad Bin Abdullah Shafi’i wanasimulia kutoka kwa Tirmidhi katika “Dhakha’iru’l-Uqba” kwamba watu walimuuliza Aisha ni mwanamke yupi aliyekuwa anapendwa zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na yeye akajibu, “Fatima.” Kisha aliulizwa kuhusu mwanaume aliyependwa zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akajibu, “Ni mume wake, Ali bin Abu Talib.” Tena alisimulia kutoka “Mukhalis” cha Dhahabi, na Hafidh Abu’l-Qasim Damishqi na yeye kutoka kwa Aisha kwamba alisema yeye Aisha: “Sijaona mwanaume aliyependwa zaidi na Mtume kuliko Ali, wala mwanamke aliyependwa zaidi kama Fatima.”

Kwa nyongeza, Sheikh huyu anasimulia kutoka kwa Hafidh Khajandi na yeye kutoka kwa Ma’azatu’l- Ghifariyya kwamba alisema: “Nilikwenda kuonana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwenye nyumba ya Aisha ambapo Ali alikuwa nje ya nyumba hiyo. Mtume akamuambia Aisha, “Huyu (Ali) ndiye kipenzi mno kwangu na mwenye kuheshimika zaidi miongoni mwa wanaume wote, Tambua haki yake na mpe heshima kwa cheo chake.”

Sheikh Abdullah bin Muhammad bin Amir Shabrawi Shafi’i ambaye ni mmoja wa Maulamaa wenu mashuhuri, ameandika katika “Kitabu’l-Ittihaf bi Hubbi’l-Ashraf,” uk. 9, Sulaiman Balkhi katika “Yanabiu’l-Mawadda” na Muhammad bin Talha Shafi’i katika Matalibu’s-Su’ul, uk. 6, kutoka kwa Tirmidhi, na yeye kutoka kwa Jami bin Umar - wote wamesimulia ifuatavyo: “Nilikwenda kwa Ummu’l- Mu’minina Aisha pamoja na shangazi yangu (dada yake baba), na tulimuuliza, ni nani ambaye alikuwa akipendwa zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Yeye alijibu, ‘Miongoni mwa wanawake alikuwa ni Fatima na miongoni mwa wanaume, ni mumewe Ali bin Abi Talib.’” Hadithi hii hii imesimuliwa na Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i katika “Mawaddatu’l- Kurba” Mawadda ya 2, pamoja na tofauti kidogo kwamba Jami bin Umar alisema kwamba alipokea jibu hili kutoka kwa shangazi yake.

Halikadhalika, Khatib Khawarizmi amesimulia hadithi hii kutoka kwa Jami bin Umar, na yeye kutoka kwa Aisha mwishoni mwa sura ya 4 ya Manaqib yake, Ibn Hajar Makki, kati- ka “Sawa’iq Muhriqa”, kuelekea mwishoni mwa sura ya 2, baada ya kuandika hadithi 40 juu ya fadhila za Ali, anasimulia hadith ifuatayo kutoka kwa Aisha: “Miongoni mwa wanawake, Fatima alikuwa ndiye mwanamke aliyependwa zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na miongoni mwa wanaume ni mume wake.”

Muhammad bin Talha Shafi’i, katika “Matalib-us-Su’ul”, uk. 7, baada ya ya kuandika Hadith mahususi mbali mbali juu ya suala hili, anaelezea hitimisho lake mwenyewe katika maneno yafuatayo: “Hadith hizi sahihi na zisizokifani huthibitisha kwamba Fatima alikuwa mwenye kupendwa zaidi na Mtume kuliko wanawake wote.

Ni mwenye cheo cha juu zaidi ya wanawake wote wa Peponi na pia wa mbele zaidi juu ya wanawake wa Madina.” Hadithi hizi za kuaminika, kwa uwazi zinathibitisha kwamba katika viumbe wote, Ali na Fatima walikuwa ndio wenye kupendwa zaidi na Mtume. Uthibitisho mwingine wa Mtume kumpendekeza zaidi Ali kuliko wanaume wengine ni ile “Hadith ya Ndege” (Hadith-e-Ta’ir). Hadithi hii inajulikana sana na kukubaliwa sana kiasi kwamba hatuhitaji kutaja vyanzo vyake vyote. Nitataja tu baadhi ya hivyo.

Hadithi Ya Ndege Aliyebanikwa:

Wengi wa ulamaa wenu, kama Bukhari, Muslim, Tirmidhi, Nisa’i, na Sijistani katika “Sahih” zao, Imam Ahmad bin Hanbali katika “Musnad” yake, Ibn Abi’l-Hadid katika Sherhe yake ya “Nahju’l-Balagha”, Ibn Sabbagh Maliki katika “Fusulu’l-Muhimma,” na Sulaiman Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda,” Sura ya 8, na kundi la waandishi wengine waaminifu wameiandika “Hadith-e-Ta’ir” katika vitabu vyao. Wanathibitisha kwamba hadithi hii ilielezewa na wasimuliaji wa Hadith 24, kutoka kwa Anas bin Maliki. Ibn Sabbagh Maliki katika “Fusulu’l-Muhimma” anaandika kuhusu hadith hii katika maneno haya: “Katika vitabu vya Hadith Sahihi na riwaya za kuaminika, Hadith-e-Ta’ir, kutoka kwa Anas bin Malik ni haipingiki.” Sibt Ibn Jauzi, katika uk. wa 23 wa kitabu chake “Tadhkira” na “Sunan” ya Tirmidhi na Mas’udi katika uk. wa 49 juzuu ya 2 ya “Muruju’dh-Dhahab”, wameangalia hususan katika sehemu ya mwisho ya hadithi hii ambayo ina dua ya Mtume na kukubaliwa kwake na Allah.

Imam Abdu’r-Rahman Nisa’i katika hadith ya tisa katika kitabu chake “Khasa’isu’l-Alawi” na Hafidh Bin Iqda na Muhammad bin Jarir Tabari, wote wamerejea kwenye nyororo isiyokatika ya wasimuliaji na kwenye vyanzo sahihi vya hadith hii, wakisema kwamba ilisimuliwa na masahaba 35 wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka kwa Anas bin Malik. Kwa ufupi, Maulamaa wenu wote mashuhuri wamethibitisha usahihi wa hadith hii na wameijumuisha kwenye vitabu vyao. Allama Sayyid Hamid Husain ameweka juzuu nzima ya kitabu chake “Abaqatu’l- Anwar” kwa ajili ya Hadithi hii tu. Alikusanya vyanzo vyote vya kuaminika kutoka kwa Maulamaa wenu mashuhuri na kwa wazi kabisa akathibitisha usahihi wa hadith hii.

Kwa mujibu wa Hadith hii, siku moja mwanamke mmoja alileta zawadi ya ndege aliyebanikwa kwa Mtume. Kabla ya kumla, Mtume akiwa amenyoosha mikono yake juu, akamuomba Allah hivi: “Ee Allah! Kati ya viumbe wako wote, mlete mtu ambaye ni mpenzi zaidi kwako na kwangu, ili kwamba ale pamoja nami ndege huyu wa kubanikwa.” Ndipo Ali akaingia ndani akala ndege yule wa kubanikwa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Baadhi ya vitabu vyenu, kama vile “Fusulu’l-Muhimma” cha Malik, “Ta’rikh” cha Hafidh Nishapuri, “Kifayatu’t-Talib” cha Ganji Shafi’i na “Musnad” ya Ahmad Bin Hanbal, n.k. ambamo Hadith hii imesimuliwa kutoka kwa Anas bin Malik, vimeandikwa kwamba Anas bin Malik alisema “Mtume alikuwa bado hajamaliza dua yake wakati Ali alipoingia nyum- bani pale, lakini nikamficha jambo lile. Wakati Ali alipoingiza mguu wake mara ya tatu, Mtume akiniamrisha nimuache aingie ndani. Wakati Ali alipoingia Mtume akasema: “Baraka za Allah ziwe juu yako; ni kitu gani kimekuleta kuja kwangu? Ali akamueleza kwamba alikuja kwake mara tatu lakini aliruhusiwa kuingia safari hii tu. Mtume akaniuliza ni kitu gani kimenifanya niwe hivyo, na nikajibu: “Ukweli ni kwamba, niliposikia dua yako, nilitamani kwamba heshima hii ingekwenda kwa mmoja wa kabila langu.” Sasa nakuulizeni enyi waungwana iwapo dua ya Mtukufu Mtume ilikubaliwa au kukataliwa na Allah.

Sheikh: Ni wazi Allah aliikubali kwa vile aliahidi katika Qur’ani tukufu kwamba angekubali dua ya Mtume. Aidha, Allah alijua kwamba Mtume asingeweza kuomba dua isiyofaa. Hivyo Allah aliyakubali maombi yake kila wakati.

Muombezi: Allah alimpeleka Ali, mtu anayestahiki zaidi katika viumbe Wake, kwa Mtume. Wanachuoni wenu wenyewe wamethibitisha tukio hili. Muhammad bin Talha Shafi’i katika Kitabu chake “Matalib-Us- Su’lu”, Sura ya 1, sehemu ya 5, uk. wa 15, amethibitisha cheo cha juu cha Ali kama mwenye kupendwa zaidi na Allah na Mtume juu ya msingi wa “Hadith ya Bendera (Riyat)” na “Hadith ya Ndege.”

Katika kuhusiana na hilo anasema: “Nia ya Mtume ilikuwa kwamba watu waelewe cheocha kipekee na cha hali ya juu cha Ali, ambaye alifikia upeo wa juu zaidi wa kuweza kufikiwa na wacha Mungu.”

Vilevile Hafidh na Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i (aliyekufa 658 A.H.) anaandika katika kitabu chake, Kifayatu’t-Talib Sura ya 33, akizungumzia fadhila za Ali ibn Abi Talib, kwamba hadith hii kwa uwazi kabisa inathibitisha kwamba Ali alikuwa kipenzi sana katika viumbe kwa Allah.

Baadae anasema kwamba Hakim Abu Abdullah Hafidh Nishapuri ameisimulia hii “Hadith-e-Ta’ir” ya Anas kutoka wasimuliaji 86 na vile vile akaandika na majina ya wasimuliaji wote 86 (Tazama Kifayatu’t- Talib, Sura ya 32). Ile hadith ambayo umenukuu wewe, ukiilinganisha na Hadith zilizosimuliwa na Maulamaa wenu wa daraja za juu (isipokuwa washupavu wakorofi wachache), haiwezi kutegemewa na ingekataliwa na watu wenye elimu.

Sheikh: Nina wasiwasi kwamba umeamua kwa akili yako kutokubali tunayo yasema.

Muombezi: Unawezaje kuhusisha chuki kama hizo kwangu? Unaweza ukatoa mfano mmoja tu ambapo umetoa hoja yenye nguvu na mimi bila sababu nikaikataa? Ninaapa kwamba katika mijadala ya kidini na Mayahudi, Wakristo, Wahindu na Wabrahmin na Mabahai wasio na elimu wa Iran, Makadian wa India na wayakinifu (wenye kuamini vitu vyenye kuonekana, kugusika na kuhisiwa tu) – katika hali zote hizi mimi sijawahi kufanya ukaidi katika hoja zangu. Kamwe sijawahi kuwa mbishi kwa makafir hawa – vipi nitaweza kufanya hivyo kwenu ninyi, ndugu zangu katika Uislamu?

Sheikh: Tumesoma maelezo ya mjadala wako na Wahindu na Wabrahmin wa Lahore katika magazeti. Tulivutiwa mno na maelezo hayo. Ingawa tulikuwa hatujakutana na wewe, tulijisikia tumeungana na wewe kimaadili. Natumaini kwamba Allah atakuongoza wewe na sisi kwenye njia iliyonyooka. Tunaamini kwamba kama kuna wasiwasi wowote kuhusu Hadith fulani, inatupasa, kwa mujibu wa ushauri wako, kuirejesha kwenye Qur’ani Tukufu.

Hata hivyo, kama unahoji ubora wa khalifa Abu Bakr na muundo wa ukhalifa wa makhalifa wakubwa, na kama utaziona hadith kuwa ni zenye mashaka, je, utasita vilevile kuamini hoja ambayo imetegemea juu ya Qur’ani Tukufu?

Muombezi: Allah asitujaalie siku tutakayotilia shaka ukweli uliotegemea juu ya Qur’ani Tukufu au Hadith Sahihi. Walakini, wakati tutakapokuwa tumeingia kwenye mjadala wa kidini na Taifa lolote au Jumuiyya, wao vilevile wanahoji kutoka kwenye Aya za Qur’ani Tukufu kuthibitisha mtazamo wao. Kwa vile Aya za Qur’ani zina daraja mbalimbali za maana, Mtume wa mwisho, ili kuwalinda watu dhidi ya kutoelewana, hakuiacha Qur’ani kama chanzo pekee tu cha mwongozo.

Kama inavyokubaliwa na madhehebu zote (Shia na Sunni), yeye mwenyewe (Mtume) alisema: “Nawaachieni vitu viwili vizito: “Kitabu cha Allah (Qur’ani) na kizazi changu. Kama mtashikamana na viwili hivi, kamwe, hamtapotea baada yangu. Hakika viwili hivi kamwe havitatengana mpaka vinifikie kwenye chemchem ya Kauthar.”

Kwa sababu hii, maana ya ufunuo wa Qur’ani Tukufu yapasa itafutwe ama kutoka kwa Mtume, fasir mkuu wa Qur’ani Tukufu, au baada yake, kutoka kwa wale walio sawa na Qur’ani Tukufu, dhuria watukufu wa Mtume. Qur’ani Tukufu inasema: “Basi waulizeni wenye kumbukumbu ikiwa ninyi hamjui.” (21:7).

“Watu Wenye Kumbukumbu” Ni Ahli Muhammad Dhuria Wa Mtukufu Mtume (S.A.W.W.).

Ahlu’dh- maana yake watu wenye kumbukumbu, ambao ni Ali na Maimamu watukufu, kizazi chake, ambao wako sawa na Qur’ani. Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi katika kitabu chake “Yanabiu’l- Mawada”, Sura ya 39, akinukuu kutoka “Tafsir-e-Kasfu’l- Bayan” ya Imam Tha’labi, anasimulia kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah Ansari, ambaye amesema: “Ali amesema: ‘Sisi dhuria wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni watu wa kumbukumbu.’” Kwa vile “Dhikr, Kumbukumbu”, ni moja ya majina ya Qur’ani Tukufu, familia hii inajumuisha na watu wa Qur’ani.

Kama ilivyoelezwa na Maulamaa wa kwenu na wa kwetu, Ali amesema: “Niulizeni kitu chochote mnachotaka kabla sijakuacheni. Niulizeni kuhusu Kitabu kitukufu (Qur’ani) kwa vile ninajua kuhusu kila Aya ndani yake – iwe imeteremshwa wakati wa usiku au wakati wa mchana, katika tambarare au katika milima. Kwa jina la Allah, hakuna Aya ya Qur’ani Tukufu iliyoteremshwa bali najua iliteremshwa kuhusu nini.

Allah (S.w.t.) amenijaalia mimi kuwa na ulimi fasaha na akili yenye busara.” Kwa hiyo, kutegemeza hoja juu ya Aya za Qur’ani tukufu, yapasa iwe kwa mujibu na maana yake sahihi na tafsir iliyotolewa na wale wenye uwezo wa kutoa tafsir ya kuaminika. Vinginevyo, kila mtu atatoa tafsir yake ya Aya za Qur’ani, kwa mujibu wa upeo wa elimu yake na imani, na hii itaishia tu kwenye hitilafu za maoni na mgongano wa mawazo. Pamoja na hoja hii katika akili, naomba usome hizo Aya zako.

Aya Za Qur’ani Tukufu Kuhusu Kuchaguliwa Kwa Makhalifa Wanne,

Na Majibu.

Sheikh: Allah anasema kwa uwazi katika Qur’ani Tukufu:

ﻣﺤﻤﺪٌ رﺳﻮل اﻟﻪ ۚ واﻟﱠﺬِﻳﻦ ﻣﻌﻪ اﺷﺪﱠاء ﻋﻠَ اﻟْﻔﱠﺎرِ رﺣﻤﺎء ﺑﻴﻨَﻬﻢ ۖ ﺗَﺮاﻫﻢ رﻛﻌﺎ ﺳﺠﺪًا ﻳﺒﺘَﻐُﻮنَ ﻓَﻀً ﻣﻦ اﻟﻪ {ورِﺿﻮاﻧًﺎ ۖ ﺳﻴﻤﺎﻫﻢ ﻓ ۇﺟﻮﻫﻬِﻢ ﻣﻦ اﺛَﺮِ اﻟﺴﺠﻮدِ ۚ{29

“Muhammad ni Mtume wa Allah, na walio pamoja naye ni wenye nyoyo thabiti mbele ya makafiri, na wenye kuhurumiana wao kwa wao, utawaona wakiinama kwa kurukuu na kusujudu (katika Sala), wakitafuta fadhila za Allah na radhi (yake). Alama zao ni katika nyuso zao kwa taathira (athari) ya kusujudu…” (48:29).

Kwanza Aya hii huthibitisha ubora wa Abu Bakr. Pili huonyesha nafasi za makhailfa wanne kinyume na inavyodaiwa na madhehebu ya Shi’a kwamba Ali alikuwa Khalifa wa kwanza. Aya hii bila ubishani inaelezea kwamba Ali alikuwa Khalifa wa nne. Muombezi: Hakika Aya hii haitoi dalili yoyote ya wazi kuhusu namna ya kuchaguliwa makhalifa au kuhusu ubora wa Abu Bakr. Kwa hiyo, lazima uonyeshe ni sehemu ipi katika Aya hii ambapo maana hiyo imefichwa.

Sheikh: Mwanzoni mwa Aya hii, usemi (usemao) “na walio pamoja naye” huashiria kwa yule mtu maarufu ambaye alikuwa na Mtume ‘usiku wa pango.’

Utaratibu wa kupokezana nafasi ya ukhalifa pia iko wazi katika aya hii. “Walio pamoja naye” ina maana ya Abu Bakr, ambaye alifuatana na Mtume kwenye Pango la Thawr katika usiku wa Hijra. Usemi, “wenye nyoyo thabiti mbele ya makafir” maana yake ni Umar Bin Khattab, ambaye alikuwa mkali sana kwa makafir. Usemi, “wenye kuhurumiana wao kwa wao” huashiria kwa Uthman bin Affan, ambaye alikuwa mpole sana.” Usemi, “alama zao ni katika nyuso zao kwa athari ya kusujudu” huashiria kwa Ali. Ni wazi kwamba Ali ni Khalifa wa nne, sio wa kwanza, kwa vile Allah amemtaja katika sehemu ya nne.

Muombezi: Nashangaa vipi nitaweza kujibu ili kwamba nisije nikalaumiwa kwa kujipendelea mwenyewe. Hakuna tafsir za Qur’ani, ukichukua pamoja na zile za maulamaa wenu wakubwa, ambazo zimetafsiri maneno haya kama ulivyofasili wewe. Aya hii ingekuwa inahusu utaratibu wa Ukhalifa, siku ya kwanza baada ya kifo cha Mtume, wakati Ali, Bani Hashim, na masahaba mashuhuri wa Mtume walipoweka vipingamizi na wakakataa kula kiapo cha utii kwa Khalifa, basi hoja zisizo za msingi zisingetolewa pale.

Wangeweza kutoa jibu la kunyamazisha kwa kusoma aya hii tukufu pale pale. Kwa hiyo, ni wazi kwamba tafsiri yako ni mawazo yaliyokuja baadaye. Hakuna yeyote katika wafasiri wakubwa wa madhehebu yenu, kama Tabari, Imam Tha’labi, Fadhil Nishapuri, Jalalu’d- Din Suyuti, Qadhi Baihawi, Jarullah Zamakhshari, Imam Fakhru’d-Din Radhi, au wengine ambao wameitafsir hivyo.

Nashindwa kuelewa jinsi unavyoipata maana hii. Wapi na kutoka kwa nani maana hii ilitolewa? Aya hii, kielimu na mtazamo wa kifundi, vilevile vinakwenda kinyuma na unavyosema.

Sheikh: Sikutarajia kwamba utakuwa mpinzani hivyo kwenye aya iliyo na maana ya wazi kiasi hicho. Hakika kama una lolote la kusema dhidi ya hivi unaweza ukatueleza tujue ili kwamba ukweli halisi uweze kuthibitishwa.

Muombezi: Ukichukulia ujenzi wa kinahau wa aya hii, kama tutaitafsiri maana yake kama ulivyofanya wewe, itakuwa na maana kwamba ama Muhammad ni Abu Bakr, Umar, Uthman na Ali au kwamba Abu Bakr, Umar, Uthman na Ali ni Muhammad!

Hata wanafunzi wanaoanza wanajua kwamba aina hii ya tafsir ya kinahau sio sahihi. Mbali na hayo, kama aya hii inaashiria kwa Makhalifa wanne, kungekuwa na kiungo “na” kupatanisha maneno ili kupata hiyo maana yako, lakini haiko hivyo.

Wafasiri wote wa madhehebu yenu wenyewe wanasema kwamba aya hii inaashiria kwa waumini wote. Aidha, sifa zilizotajwa katika aya hii kwa wazi kabisa zinaashiria kwa mtu mmoja tu, ambaye alikaa na Mtume kuazia mwanzo kabisa na sio watu wanne. Na kama tukisema mtu huyu mmoja alikuwa Amir’l- Mu’minina Ali, itakuwa sawasawa zaidi kulingana na akili za kuzaliwa na hadith kuliko kutaja wengine wowote.

Hoja Kutokana Na “Aya Ya Pango” Na Majibu Yake.

Sheikh: Ina shangaza kwamba unadai ati hujiingizi katika hoja zenye kupotosha, ingawa maoni yako ni ya kupotosha hasa. Allah anasema katika Qur’ani tukufu: “Kama hamtam- nusuru, basi Allah alimnusuru walipomtoa wale waliokufuru, yeye akiwa wa pili wake walipokuwa wote katika pango alipomwambia Sahibu y ake. ‘Usihuzunike kwa hakika Allah yu pamoja nasi, Allah akamteremshia utulivu wake na akamnusuru kwa majeshi msiyoyaona…’” (9: 40).

Kwanza, Aya hii inaunga mkono aya iliyopita na huthibitisha kwamba usemi “na walio pamoja naye”, huashiria kwa Abu Bakr ambaye alikuwa na Mtume katika Pango katika usiku wa Hijra, Pili, ukweli kwamba alikuwa na Mtukufu Mtume, yenyewe ni uthibitisho mkubwa wa fadhila na ubora wa Abu Bakr kwa umma wote. Mtume aliweza kutabiri kwamba Abu Bakr alikuwa Mrithi wake, na kwamba kuwepo kwa Khalifa baada yake ni muhimu.

Kwa hiyo, alitambua kwamba ilimpasa kumhifadhi Abu Bakr kama ambavyo angejihifadhi yeye mwenyewe. Hivyo, alimchukua kuwa naye ili kwamba Abu Bakr asije akakamatwa na maadui. Huduma kama hii haijafanywa kwa Mwislamu mwingine yeyote. Hii inathibitisha wazi haki yake ya ukhalifa kuliko wengine.

Muombezi: Kama ungeangalia Aya hii kwa busara zaidi, ungeona kwamba uamuzi wako ni wa makosa.

Sheikh: Unaweza kutoa sababu dhidi ya hitimisho ambalo tumelitoa?

Mombezi: Ningekuomba uliache suala hili kwa muda huu kwa sababu maneno huzaa maneno. Baadhi ya watu wenye chuki wanaweza wakafasiri maoni yetu kwa nia mbaya. Sitaki kuchochea chuki. Mtu anaweza akasema tunataka kuwavunjia heshima makhalifa, ingawa cheo cha kila mmoja kimewekwa, na sio muhimu kufanya tafsir zisizo na maana.

Sheikh: Unakuwa mkwepaji. Elewa kwamba hoja yenye maana haizai chuki; huondoa kutokuelewana.

Muombezi: Kwa vile umetumia neno “Mkwepaji,” ninalazimika kujibu, ili uweze kujua kwamba silikwepi suala hili. Nilitaka kudumisha utaratibu wa mjadala wetu. Natumaini kwamba hutaona makosa kwa upande wangu. Umetoa utetezi wa kizembe sana kwamba Mtume alijua kwamba Abu Bakr atakuwa Khalifa wake baada yake. Kwahiyo, ilikuwa muhimu kwake kuokoa maisha yake, na hivyo akamchukuwa ili awe pamoja naye. Ukweli Kuhusu Abu Bakr Kufuatana Na Mtukufu Mtume (S.A.W.W.).

Majibu kwa maelezo yako ni rahisi. Kama Abu Bakr angekuwa Khalifa pekee baada ya Mtume, maoni kama hayo yangewezekana, lakini mnaamini katika makhalifa wanne. Kama hoja yako hii ni sahihi, na kama ilikuwa muhimu kwa Mtume kulinda usalama wa Khalifa, basi Mtume angeondoka nao wote wanne kutoka mjini Makka. Kwa nini aliweza kuwaacha wale watatu, mmoja wao katika hali ya hatari ya kulala katika kitanda cha Mtume, ambavyo ilikuwa ni hatari katika usiku ule wakati maadui zake walikuwa wamekusanyika ili kumuua?

Kwa mujibu wa Tabari (Sehemu ya tatu ya “Tarikh”) Abu Bakr hakuwa na habari za harakati za Mtume za kuondoka Makka. Wakati alipokwenda kwa Ali na kumuuliza kuhusu Mtume, alimueleza kwamba Mtume amekwenda kule pangoni. Ali akamwambia kwamba kama alikuwa na shughuli yoyote naye, alipaswa amkimbilie. Abu Bakr alikimbia na akamkuta Mtume njiani. Na hivyo akafuatana naye. Mtiririko huu wa matukio unaonyesha kwamba Mtume hakukusudia kumchuka Abu Bakr kuwa naye. Aliungana naye katikati ya njia bila ruhusa ya Mtume.

Kwa mujibu wa taarifa nyingine, Abu Bakr alichukuliwa katika safari hiyo kwa kuhofia asije akasababisha matatizo na kutoa habari kwa maadui. Maulamaa wenu wenyewe wameukiri ukweli huu. Kwa mfano, Sheikh Abu’l-Qasim bin Sabbagh, ambaye ni mmoja katika maulamaa wenu anayejulikana sana wa madhehebu yenu, ankiandika katika kitabu chake Al-Nur-Wa’l-Burhan kuhusu maisha ya Mtume, anasimulia kutoka kwa Muhammad bin Ishaq, na yeye kutoka kwa Hasan bin Thabit Ansari, kwamba alikwenda Makka kufanya Umra kabla ya kuhama kwa Mtume.

Aliona kwamba Maquraishi makafiri walikuwa wamewaandama masahaba wa Mtume. Mtume akamuamrisha Ali kulala katika kitanda chake, na kwa kuogopa kwamba Abu Bakr angetoa siri hii kwa makafiri, Mtume akamchukua awe pamoja naye.

Mwisho, ingelikuwa vizuri kama ungeonyesha ni ushahidi gani uliopo katika Aya hii, unaoonyesha ubora wa Abu Bakr au iwapo kufuatana na Mtume katika safari ni uthibitisho kwamba mtu anayo sifa ya Ukhalifa.

Sheikh: Ushahidi upo. Kwanza, usuhuba wa Mtume na kwamba, Allah amemuita saha- ba wa Mtume, yenyewe ni sifa tosha. Pili, Mtume mwenyewe amesema: “Hakika Allah yu pamoja nasi.” Tatu, uteremshwaji wa utulivu juu yake kutoka kwa Allah, kama ilivyotajwa katika Aya hii, ni uthibitisho wa kuvutia zaidi wa ubora wa Abu Bakr. Kwa hiyo, nukta zote hizi zikiwekwa pamoja huonyesha ubora wake kwa wengine kuhusiana na ukhalifa.

Muombezi: Hakuna anayesita kuikubali nafasi ya Abu Bakr, Mwislam mtu mzima, mmoja wa masahaba mashuhuri na baba wa mke wa Mtume. Hata hivyo, sababu hizi hazithibitishi ubora wake katika ukhalifa. Kama utajaribu kuthibitisha nukta yako hii kwa maelezo haya mbele ya watu waadilifu wasio na upendeleo, utakuwa unavutia lawama nzito.

Watasema kwamba usuhuba na watu wema sio uthibitisho wa sifa au ubora. Kwa mfano, mara kwa mara tunaona kwamba watu wabaya hufuatana na watu wema, na kundi la makafiri hufuatana na Waislamu katika safari. Pengine umesahau Qur’ani Tukufu inavyosema kuhusu Mtume Yusufu ambaye amesema:

{ﻳﺎ ﺻﺎﺣﺒ اﻟﺴﺠﻦ اارﺑﺎب ﻣﺘَﻔَﺮِﻗُﻮنَ ﺧَﻴﺮ ام اﻟﻪ اﻟْﻮاﺣﺪُ اﻟْﻘَﻬﺎر {39

“Enyi wafungwa sahibu wenzangu wawili! Je! waungu wengi wanaofarikiana ndio bora au Mwenyezi Mungu, Mmoja Mwenye nguvu?” (12:39).

Kuhusu Aya hii, wafasiri wamesema kwamba wakati Yusufu alipopelekwa jela, siku hiyo hiyo mpishi wa Mfalme na mtunza mvinyo ambao wote walikuwa makafiri, vilevile walitiwa jela pamoja naye. Kwa muda wa miaka mitano watu hawa watatu (waumini na makafiri kwa pamoja ) waliishi pamoja kama maswahiba. Wakati akiwahubiria, Yusufu aliwaita sahiba zangu.

Je, usuhuba huu wa Mtume Yusufu ulifanya hata mara moja hali ya kuwaona makafiri hawa wawili kama watu bora au wenye heshima? Je, usuhuba wao na Mtume Yusufu ulileta mabadiliko katika Iman zao? Maandishi ya Wafasiri na wanahistoria yanatuambia kwamba, baada ya miaka mitano ya usahaba, waliachana kila mmoja katika hali ile ile.Aya nyingine ya Qur’ani Tukufu inasema:

{ﻗَﺎل ﻟَﻪ ﺻﺎﺣﺒﻪ وﻫﻮ ﻳﺤﺎوِره اﻛﻔَﺮت ﺑِﺎﻟﱠﺬِي ﺧَﻠَﻘَﻚَ ﻣﻦ ﺗُﺮابٍ ﺛُﻢ ﻣﻦ ﻧُﻄْﻔَﺔ ﺛُﻢ ﺳﻮاكَ رﺟً {37

“Sahiba wake akamuambia na hali ya kuwa anajibishana naye: Je! Unamkufuru, Yule aliyekuumba kwa udongo, kisha kwa tone la manii, kisha akakufanya mtu kamili?” (18:37)

Wafasiri wanakubaliana kwamba aya hii inazungumzia ndugu wawili, mmoja alikuwa muumini, ambaye jina lake lilikuwa Yahuda. Mwingine alikuwa kafir jina lake lilikuwa Bara’tus. Jambo hili limeelezewa vilevile katika “Tafsir-e-Kabir” na Imam Fakhru’d-Din Razi, ambaye ni mmoja katika Maulamaa wenu.

Ndugu hawa wawili walizungumza pamoja, maelezo ambayo hayataweza kutolewa hapa. Hata hivyo Allah amewaita wote wawili (Muumin na Kafiri). “Masahibu.” Je, yule kafiri alipata faida kutokana na usuhuba wake na Muumini? Kwa hakika hapana. Hivyo usuhuba peke yake sio msingi wa mtu kudaiwa kuwa ni bora. Kuna mifano mingi yenye kuunga mkono maoni haya.

Maneno Ya Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) “Allah Yuko Pamoja Nasi” Sio Uthibitisho Wa Ubora Wa Abu Bakr.

Umesema pia kwamba kwa vile Mtume alimuambia Abu Bakr, “Allah yuko pamoja nasi.” kwamba huo ni uthibitisho wa ubora wa Abu Bakr na haki yake ya Ukhalifa! Waweza ukayafikiria tena maoni yako. Watu wanaweza wakakuuliza, kwa mfano, “Je, Allah anakuwa na waumini na mawalii tu, na sio na makafir?” Unajua sehemu yoyote ambayo Allah hayupo? Je, hivi Allah hayupo na kila mtu? Chukulia kwamba muumini na kafiri wako pamoja katika mkusanyiko. Qur’ani inasema:

اﻟَﻢ ﺗَﺮ انﱠ اﻟﻪ ﻳﻌﻠَﻢ ﻣﺎ ﻓ اﻟﺴﻤﺎواتِ وﻣﺎ ﻓ ارضِ ۖ ﻣﺎ ﻳﻮنُ ﻣﻦ ﻧَﺠﻮﱝ ﺛََﺛَﺔ ا ﻫﻮ راﺑِﻌﻬﻢ و ﺧَﻤﺴﺔ ا ﻫﻮ {ﺳﺎدِﺳﻬﻢ و ادﻧَ ﻣﻦ ذَٰﻟﻚَ و اﻛﺜَﺮ ا ﻫﻮ ﻣﻌﻬﻢ اﻳﻦ ﻣﺎ ﻛﺎﻧُﻮا ۖ{7

“Je! Huoni kwamba Allah anajua vilivyomo mbinguni na vilivyomo ardhini? Haupatikani mnong’ono wa watu watatu ila yeye huwa ni wanne wao, wala watano ila yeye huwa ni wa Sita wao, wala wachache kuliko hao wala zaidi ila Yeye huwa pamoja nao, popote walipo…”(58:7).

Kwa mujibu aya hii na wa akili ya kawaida, Allah yupo na kila mtu.

Sheikh: Maelezo “Allah yupo pamoja nasi” Yana maana kwamba walikuwa wapenzi mno wa Allah kwa sababu wamesafiri katika njia ya Allah kwa madhumuni ya kuhifadhi dini yake. Baraka za Allah zilikuwa pamoja nao.

Muombezi: Lakini hakika maelezo haya hayathibitishi kwamba mtu anazo baraka za milele. Allah Mwenye nguvu hutizama matendo ya watu. Imetokea mara kwa mara kwamba wakati fulani, watu walifanya matendo mema na wakawa ni wenye kupokea rehema kutoka kwa Allah.

Baadae wakamuasi Allah na ikawapata adhabu ya Mungu. Ibilis kama unavyojua, alimuabudu Allah kwa maelfu ya miaka na akapata upole kutoka Kwake. Hata hivyo mara tu alipoasi amri yake, akalaaniwa. Qur’ani Tukufu inasema:

{ﻗَﺎل ﻓَﺎﺧْﺮج ﻣﻨْﻬﺎ ﻓَﺎﻧﱠﻚَ رﺟِﻴﻢ {34

{وانﱠ ﻋﻠَﻴﻚَ اﻟﻠﱠﻌﻨَﺔَ اﻟَ ﻳﻮم اﻟﺪِّﻳﻦ {35

“Akasema: Basi toka humo, na hali ya kuwa wewe ni mwenye kufukuzwa… Na kwa yakini itakuwa laana juu yako mpaka Siku ya Malipo.” (15:34-35).

Kumradhi, hakuna madhara katika kutoa mifano, madhumuni yangu ni kufafanua hii nukta. Historia imejaa mifano mingi ya wale ambao walikuwa karibu na Allah, lakini ambao baada ya kujaribiwa, walilaaniwa. Bal’am Bin Ba’ur, kwa mfano, wa hirimu moja na Musa, alitokea kuwa karibu sana na Allah kiasi kwamba Allah alimfunulia lile Ism-e- A’dhim (jina tukufu la Allah, ambalo kupitia hilo chochote kinachoombwa kinakubaliwa upesi sana na Allah).

Alimuomba Allah kwa njia ya Ism-e-A’dhim na akasababisha shida ikampata Musa katika Bonde la Tia! Lakini wakati wa majaribio, Bal’am alizidiwa nguvu na mahaba ya vitu vya ulimwengu. Alimfuata Ibilis na akalaaniwa.

Wafasiri wametoa maelezo kamili ya tukio hili. Imam Fakhru’d-Din Razi katika Tafsir yake sehemu ya 4, uk. 463, ameelezea habari hii kutoka kwa Ibn Abbas, Ibn Mas’ud, na Mujahid. Allah katika Qur’ani Tukufu anatueleza hivi: “Na wasomee habari za yule tuliyempa Aya zetu kisha akajivuna nazo. Na shetani akamuandama na akawa miongoni mwa waliopotea.”

Barsisa Abid.

Au angalia la Barsisa Abid, ambaye mwanzoni alimwabudu Allah kiasi kwamba akakuwa Mustajabu’d- da’wa (mtu ambaye maombi yake hukubaliwa). Hata hivyo,wakati muda wa majaribio ulipofika, alishindwa.

Akipotezwa na Shetani, akafanya zinaa na msichana, akanyongwa, na akafa kafiri, Qur’ani inamzungumzia katika maneno haya:

{ﻛﻤﺜَﻞ اﻟﺸﱠﻴﻄَﺎنِ اذْ ﻗَﺎل ﻟْﻧْﺴﺎنِ اﻛﻔُﺮ ﻓَﻠَﻤﺎ ﻛﻔَﺮ ﻗَﺎل اﻧّ ﺑﺮِيء ﻣﻨْﻚَ اﻧّ اﺧَﺎف اﻟﻪ رب اﻟْﻌﺎﻟَﻤﻴﻦ {16

{ﻓَﺎنَ ﻋﺎﻗﺒﺘَﻬﻤﺎ اﻧﱠﻬﻤﺎ ﻓ اﻟﻨﱠﺎرِ ﺧَﺎﻟﺪَﻳﻦ ﻓﻴﻬﺎ ۚ وذَٰﻟﻚَ ﺟﺰاء اﻟﻈﱠﺎﻟﻤﻴﻦ {17

“Ni kama shetani, anapomwambia mtu: kufuru; na anapokufuru akamwambia: Mimi si pamoja na wewe, hakika namuogopa Allah, Mola wa walimwengu. Basi mwisho wa wote wawili hao ikawa waingie motoni wakae humo, na hiyo ndiyo jaza ya madhalimu.” (59:16-17).

Hivyo kama mtu aliwahi kufanya matendo mema wakati fulani, haina maana kwamba mwisho wake utakuwa mzuri. Ni kwa sababu hii kwamba tunaelekezwa kusema katika maombi yetu: “Matendo yetu na yawe na mwisho mwema.”

Sheikh: Kwa hakika sikutarajia mtu mwenye heshima kama wewe kutoa mfano wa shetani, Bal’am Ba’ur na Barsisa.

Muombezi: Samahani, nimekwishaeleza kwamba hakuna madhara katika kutoka mifano. Kwa kweli ni lazima tuitoe katika mijadala ya kielimu ili kuthibitisha ukweli. Allah awe shahidi yangu: Kamwe sikukusudia kumtweza yeyote kwa kutoa mifano hii. Madhumuni yangu ni kuthibitisha hoja yangu tu. Sheikh: Aya hii kwa wazi kabisa huthibitisha ubora wa Abu Bakr kwa sababu inasema: “Hivyo Allah akamteremshia utulivu juu yake….” (9:40). Kijina hapa humuashiria Abu Bakr, ambacho huthibitisha ubora wake.

Muombezi: Umeielewa vibaya, kijina kilichotumiwa baada ya “Sakina” (utulivu) huashiria kwa Mtume. Utulivu uliteremshwa kwake na sio kwa Abu Bakr, kama ilivyo dhahiri katika sentensi inayofuatilia ambapo Allah anasema: “…na akamnusuru kwa majeshi msiyoyaona…” (9:40) ukweli ni kwamba majeshi ya Malaika wasioonekana yalikuwa kwa ajili ya kumsaidia Mtume, sio Abu Bakr.

Sheikh: Nakubali kwamba msaada wa Mungu ulikuwa kwa ajili ya Mtume, lakini Abu Bakr akiwa pamoja na Mtume, hakuwa bila rehma.

Kuteremshwa Kwa Utulivu Kulikuwa Kwa Ajili Ya Mtume Wa Allah.

Muombezi: Kama upewaji wa rehma za Mungu umeashiria kwa watu wawili, nahau ya Kiarabu ingehitaji kwamba vijina vilivyotumika vingehusisha watu wawili katika misemo yote ya Aya hii. Lakini vijina hivi vinaashiria kwa mtu mmoja, Mtume, na rehma za Allah zilikuwa kwa ajili yake. Kama kupitia kwake yeye, upewaji wa rehma ungekusudiwa vilevile kwa ajili ya wengine, majina yao yangetajwa. Hivyo, uteremshaji wa utulivu katika aya hii ni kwa ajili ya Mtume peke yake.

Sheikh: Mtume wa Allah alikuwa hana haja ya kupewa utulivu wa Mungu. Alikuwa hauhi- taji kwa sababu alikuwa amehakikishiwa rahma za Mungu. Hivyo upewaji wa utulivu ulikuwa kwa ajili ya Abu Bakr.

Muombezi: Kwa misingi gani wewe unasema kwamba Mtume alikuwa hategemei upewa- ji wa rehma za Mungu? Hakuna mtu - awe Mtume Imam au Walii ambaye anajitegemea kwa (upewaji wa) rehma za Mungu. Pengine umesahau Qur’ani Tukufu inasema nini kuhusu tukio la Hunain.“Kisha Allah akateremsha utulivu wake juu ya Mtume wake na juu ya waliomini…” (9:26).

Kitu hicho hicho kimesemwa katika Sura ya 48 (Fat’h) aya ya 26, ya Qur’ani Tukufu. Waumini wamejumuishwa baada ya Mtume katika aya hii, kama vile katika “aya ya Pango.” Kama Abu Bakr angekuwa mwenye kustahiki kupewa utulivu, ima kijina kwa ajili ya watu wawili kingetumika, au jina lake lingetajwa mbalim- bali.

Jambo hili liko wazi kabisa kiasi kwamba Maulamaa wenu wenyewe wanakiri kwamba kijina kilichofungamanishwa na utulivu hakiashirii kwa Abu Bakr. Unaweza kuitazama “Naqzu’l-Uthmaniyya” kilichoandikwa na Sheikh Abu Ja’far Muhammad bin Abdullah Iskafi, ambaye ni mmoja wa Maulamaa mashuhuri na masheikh wa Mu’tazil. Mwanachuo huyu anaukana moja kwa moja uongo wa Abu Uthman Jahiz. Ibn Abi’l-Hadid vilevile ameandika baadhi ya majibu hayo katika Sharh yake ya Nahju’l-Balagha Jz. 3, uk. 253- 281. Kwa nyongeza, kuna usemi katika Aya hii, ambao maana yake halisi ni kinyume na hoja yako. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Abu Bakr: “Usihuzunike.” Usemi huu unaonyesha Abu Bakr alikuwa muoga.

Je, woga huu ulikuwa unafaa kusifiwa au hapana? Kama ingelikuwa hivyo, Mtume asingemzuia yeyote kufanya tendo jema. Mwakilishi wa Allah ana sifa makhususi. Muhimu zaidi ya hizo, kama ilivyotajwa katika Qur’ani Tukufu, ni kwamba haogopi kubadilika kwa maisha. Anafanya uvumilivu na ushujaa. Qur’ani Tukufu inasema: “Sikilizeni (eleweni)! Hakika vipenzi vya Allah hawatakuwa na khofu wala hawatahuzunika.” (10:62).

Mkutano Wa Sita Jumanne Usiku 28 Rajab 1345 A.H.

Bwana Ghulam Imamain, mfanyabiashara wa Kisunni mwenye kuheshimika, alikuja katika sehemu ya mkutano kabla ya jua kuzama. Alitaja sababu yake ya kuja. Alisema kwamba yeye na watu wengine walivutiwa sana na maelezo ya Muombezi. Akasema kwamba amesikia ukweli ambao hajapata kuusikia kabla yake.

Yeye na baadhi ya Sunni wengine walikuwa na majadiliano yasiyopendeza na Maulamaa wao, ambao hawakuweza kukanusha hoja za Muombezi lakini ambao kwa ukaidi wameng’angania msimamo wao. Wakati wa Sala ya Magharibi ulipowadia, Bw.Ghulam Imamain alisali Sala zote Magharibi na Isha nyuma ya Muombezi. Wakati wengine walipowasili, mjadala ulianza na ushauri wa Nawab Sahib.

Nawab: Tafadhali endelea na mazungumzo ya usiku wa jana. Tafsir ya ile aya ilikuwa haikukamilika.

Muombezi: (Akiangalia upande wa Maulamaa wa Kisunni). Mradi na nyie mliruhusu hilo.

Hafidh: (Kwa hasira kidogo). Hakuna madhara. Kama kuna kitu kimebakia kusemwa, tuko tayari kukisikiliza.

Muombezi: Usiku uliopita nilithibitisha kwa mtazamo wa kinahau kwamba maelezo ya baadhi ya wafasiri wanaosema kwamba aya hii huonyesha namna ya kuamua ukhalifa yalikuwa hayakubaliki. Sasa nitaelezea kutokana na mtazamo mwingine.

Sheikh Abdu’s-Salam Sahib alisema usiku uliopita kwamba kuna sifa nne zilizotajwa katika aya hii. Sifa hizi, alisema, zinaonyesha kwamba aya hii iliteremshwa kwa habari ya Makhalifa wanne wa kwanza na kwamba aya hii inaonyesha mpango wa ukhalifa. Majibu yangu kwa hoja hii ni: kwanza, wafasir wenye kuaminika hawajawahi kutoa maelezo kama hayo kuhusu maana halisi ya aya hii. Pili, nyote mnajua kwamba wakati sifa inapohusish- wa na mtu inaenda sawasawa na tabia yake, hapo ndipo (sifa hiyo) itakuwa na maana. Kama tutayaangalia mambo kwa busara zaidi, tunaona kwamba ni Ali tu ambaye alikuwa na sifa hizo zilizoelezewa katika aya hii. Sifa hizi kwa njia yoyote haziafikiani na hizo zilizotajwa na Sheikh Sahib.

Hafidh: Aya zote hizo ulizokwishasimulia kuhusu Ali hazikutosha? Unataka sasa kwa ujanja wako wa ufasaha wa kusema kuthibitisha kwamba aya hii tukufu vilevile iliteremshwa kwa kumtukuza Ali? Kama ni hivyo, hebu tujulishe ni vipi haikubaliani na ukhalifa wa makhalfa wanne wa kwanza.

Aya Mia Tatu Zenye Kumtukuza Ali.

Muombezi: Sijahusisha Aya ya Qur’ani Tukufu kwa kumtukuza Ali kwa uongo. Umechanganya mambo. Unaweza ukapuuza ukweli kwamba tafsiri zenye kujulikana vizuri na vitabu vyenye kuaminika vilivyoandikwa na Maulamaa wenu wenyewe vimeta- ja aya nyingi za Qur’ani Tukufu zikiwa ni za kumtukuza Ali? Unawezaje kuona kuwa ni kitu cha pekee kwangu? Je, Hafidh Abu Nua’im Isfahani, muandishi wa “Ma-Nazala nina’l-Qur’ani Fi Ali”, na Hafidh Abu Bakr Shirazi, muandishi wa “Nuzulu’l- Qur’ani Fi Ali”, walikuwa Mashi’a? Je, wafasiri wakubwa, kama Imam Tha’labi, Jalalu’d-Din Suyuti, Tabari, Imam Fakhru’d-Din Radhi, na Maulamaa wengine wenye sifa kubwa, kama Ibn Kathir, Muslim, Hakim, Tirmidhi, Nisa’i, Ibn Maja, Abu Dawdi, Ahmad Bin Hanbal, na hata Ibn Hajar asiye mvumilivu, ambaye amekusanya katika kitabu chake “Sawa’iq” Aya za Qur’ani zilizoteremshwa kumsifia Ali pia walikuwa Shi’a? Baadhi ya ulamaa kama,Tabari, na Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i mwanzoni mwa kitabu chake sehemu ya 62, anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas, na Muhadith wa Syria katika kitabu chake “Tarikh-e-Kabir”, na wengine wameandika Aya nyingi kiasi kama mia tatu za Qur’ani Tukufu zenye kumtukuza Ali. Je, watu hawa walikuwa Mashi’a au wanatokana na maula- maa wenu wakubwa?

Hatuhitaji kuhusisha kwa uongo aya ya Qur’ani tukufu kwa ajili ya kuthibitisha cheo cha Amir’l- Mu’minina Ali. Maadui zake (Bani Umayya, Nawasib na Khawarij) wamezuia fadhila zake zisitajwe na marafiki zake wakasita kusimulia ubora wake kwa kuogopa matokeo yake. Bado, vitabu vimejaa fadhila zake na vinatoa mwanga juu ya mambo yote ya kufanikiwa kwake.

Kwa vyovyote inavyohusika aya hii, sikujitia katika “ujanja wa ufanisi wa kusema.” Nimefichua ukweli, nikitoa hoja kutoka katika vitabu vyenu. Mmeona mpaka hapo kwamba sikutoa hoja kutoka kwenye riwaya za waandishi wa Kishi’a. Hata kama vitabu vya Shi’a viwekwe kando, bado nitathibitisha ubora wa kipekee wa Ali. Niliyosema kuhusu Aya hii yanakubaliana na maoni ya Maulamaa wenu wenyewe.

Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i amenukuu “Hadith ya kufanana” katika kitabu chake “Kifayatu’t- Talib” Sura ya 23, kutoka kwa Mtume yenye maana kwamba Ali alikuwa anafanana na Mitume. Anasema kwamba sababu ya Ali kuitwa kwamba anafanana na Mtume Nuh katika hekima ni kwamba Ali alikuwa mkali dhidi ya makafiri na mpole kwa waumini. Allah amezitaja sifa hizi katika Qur’ani Tukufu.

Ali ambaye siku zote alikuwa pamoja na Mtume, alikuwa “mkali dhidi ya makafiri na mwenye huruma kwa waumini.” Na ukichukulia, kama Sheikh Sahib anavyosema: kwamba usemi “Na wale ambao wako pamoja naye” unamuashiria Abu Bakr kwa sababu kwa muda wa siku chache alikuwa na Mtume ndani ya Pango, Hivi mtu kama huyo anaweza kuwa sawa na yule aliyekuwa na Mtume tangu utotoni na kupata maelekezo kutoka kwake?

Ali Ni Wa Kwanza Kutangaza Imani Juu Ya Mtume Wa Allah.

Aidha, katika tukio muhimu la kutangaza Utume wake, hakuna aliyemuunga mkono Muhammad isipokuwa Ali. Maulamaa wenu mashuhuli, kama Bukhari na Muslim, kati- ka “Sahih” zao, Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad” yake, na wengine wengi, kama vile Ibn Abdi’l-Birr katika “Isti’abi”, Jz. 3, uk. 32, Imam Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i katika “Khasa’isu’l-Alawi”, Sibt Ibn Jauzifi katika Tadhkira, uk. 63, Sheikh Suleimam Balkhi Hanafi ndani ya “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 12, kwa kunukuu kutoka kwa Tirmidhi na Muslim, Muhammad bin Talha Shafi’i katika “Matalibu’s-Su’ul” Sura ndogo - 1, Ibn Abi’l- Hadid katika “Sharh Nahju’l-Balagha”, Jz. 3, uk. 258, Tirmidhi katika “Jam’e- Tirmidhi”, Jz. 2, uk. 314, Hamwaini katika “Fara’id”, Mir Seyyed Ali Hamadani katika “Mawaddatu’l-Qurba”, na hata yulu shabiki Ibn Hajar katika “Sawa’iq-e-Muhriqa”, na wanachuoni wengine mashuhuri, wameandika pamoja na tofauti kidogo ya maneno, kutoka kwa Anas bin Malik na wengine kwamba:

“Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipewa Utume wa Allah siku ya Jumatatu, na Ali akatangaza imani yake kwake siku ya Jumanne.” Vilevile imesimuliwa tena kwamba: “Utume wa Allah ulitangazwa siku ya Jumatatu na Ali akasali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) siku ya Jumanne.” Na halafu tena, “Ali alikuwa mtu wa kwanza kutangaza imani yake kwa Mtume.” Vilevile Tabari, Ibn Abi-Hadid, Tirmidhi, na wengine wanasimulia kutoka kwa Ibn Abbas kwamba “Ali alikuwa wa kwanza kusali.”

Kufundishwa Kwa Ali Tangu Utotoni Na Mtume.

Ninakuombeni muangalie wanachuoni wenu, Nuru’d-Din Bin Sabbagh Malik, katika “Fusulu’l- Muhimma.” Sura ya “Tarbiatu’n-Nabi”, uk, 16, na Muhammad Bin Talha Shafi’i, katika “Matalibu’s- Su’ul”, Sura ya 1, uk. 11, na wengine walichosimulia. Katika wakati mmoja wa ukame hapo Makka, Mtume alimwambia ami yake, Abbas, kwamba, kaka yake, Abu Talib, ana watoto wengi na kwamba uwezo wake wa kujikimu kimaisha ulikuwa ni mdogo. Mtume Muhammad alipendekeza kwamba kila mmoja wao amuombe Abu Talib ampe mtoto mmoja ili kusaidia kupunguza mzigo mzito alionao. Abbas alikubali. Walikwenda kwa Abu Talib na pendekezo lao, na akakubali. Abbas akamchukuwa Ja’far-e- Tayyar kuwa chini ya malezi yake na Mtume akamchukuwa Ali. Malik akaendelea, “Ali alibakia moja kwa moja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka alipotangazwa kuwa Mtume wa Allah.”

Ali alitangaza Imani yake kwake, na akamfuata kama Mtume wa Allah, wakati huo Ali akiwa na umri wa miaka kumi na tatu tu. Alikuwa mwanaume wa kwanza kuukubali Uislamu.

Mke wa Mtume Khadija alikuwa mtu wa pekee aliyemkubali Mtume kabla ya Ali. Katika Sura hiyo hiyo, Malik anaelezea kwam- ba Ibn Abbas, Jabir Ibn Abdullah Ansari, Zaid ibn Arqam, Muhammad ibn Munkadar, na Rabi’atu’l-Marai wamesema kwamba mtu wa kwanza kumuamini Mtume baada ya Khadija alikuwa ni Ali. Anasema Ali aliutaja ukweli huu, ambao umesimuliwa na Maulamaa wenu.

Alisema: Muhammad, Mtume wa Allah ni ndugu yangu na mtoto wa Ami yangu; Hamza Bwana wa mashahidi, ni Ami yangu; Fatima binti ya Mtume ni mke wangu; na watoto wawili (wanaume) wa binti yake ni watoto wangu kwa Fatima. Nani kati yenu amechangia sifa kama hizi nilivyo mimi? Nilikuwa wa kwanza kabisa katika kuukubali Uislamu wakati nilikuwa bado mtoto tu. Mtume alitangaza katika siku ya Ghadir-e-Khum kwamba ilikuwa ni wajibu kunikubali mimi kama kiongozi wenu. (Kisha akasema mara tatu) “Ole kwa yule ambaye atamkabili Allah kesho (Siku ya Kiyama), kama akiwa amenifanyia mimi ukatili wowote ule.”

Muhammad Bin Talha Shafi’i katika “Matalibu’s-Su’ul”, sehemu ya 1, Sura ya 1, uk. 11, na wengine wengi katika Maulamaa wenu, wamesimulia kwamba maelezo haya yalikuwa ni majibu ya barua ya Mu’awiya aliyomuandikia Ali ambayo kwayo alijigamba kwamba baba yake alikuwa kiongozi wa kabila lake wakati wa “zama za ujinga” na kwamba kati- ka Uislamu Yeye (Mu’amiya) alikuwa ni Mfalme.

Mu’awiya vilevile alisema kwamba yeye alikuwa “mjomba wa waumini” mwandishi wa wahayi (ufunuo), na mtu sifa njema.” Baada ya kusoma barua hii, Ali akasema: “Mtu wa tabia hii – mtoto wa mwanamke ambaye alitafuna maini - anajigamba mbele yangu! (kuhusu mama yake Mu’awiyya - Hindi ambaye baada ya Vita vya Uhud akiwa na hasira kali alichana maiti ya Hamza, akakata ini lake, na akalitafuna). Hata hivyo, Mu’awiyya ingawa alikuwa mpinzani mkali wa Ali, hakuweza kuzikataa sifa hizi.

Aidha, Hakim Abu’l-Qasim Haskani, mmoja wa Maulamaa wenu, anasimulia kutoka kwa Abdu’r- Rahman Bin Auf, kuhusu aya hiyo hapo juu ya Makuraishi kumi waliokubali Uislamu, kwamba Ali alikuwa wa mbele zaidi miongoni mwao. Ahmad Bin Hanbal, Khatib Khawarizmi, na Sulayman Balkhi Hanafi, wanasimulia kutoka Anas bin Malik kwamba Mtume alisema: “Malaika walinitakia rehma mimi na Ali kwa muda wa miaka saba, kwani kwa muda huo hakuna sauti iliyotamka Upweke wa Allah isipokuwa yangu na ya Ali.”

Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali katika “Sherh-e-Nahjul-Balagha”, Jz. 1, uk. 373-5, ameandika Hadith nyingi mbalimbali zilizosimuliwa kupitia wanachuoni wenu zenye maana kwamba Ali alikuwa wa mbele zaidi katika jambo la Uislamu.

Baada ya kuandika vifungu mbalimbali vya maneno na simulizi anahitimisha kwa kusema: “Hivyo mukhtasari wa yote tuliyoeleza ni kwamba Ali ni wa kwanza miongoni mwa watu kuhusu Uislamu. Maoni kinyume na haya ni mara chache kuyasikia, na hayana maana kwetu kuyazingatia.”

Imam Abdu’r-Rahman Nisa’i, mwandishi wa moja ya vitabu sita Sahih vya hadith, ameandika katika “Khasa’isu’l-Alawi” hadith sita za mwanzo juu ya suala hili na amethibitisha kwamba mtu wa mbele zaidi katika Uislamu na wa kwanza kusali na Mtume alikuwa Ali. Kwa nyongeza, Sheikh Sulayman Balkh Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda.” Sura 12, ameandika hadith 31 kutoka kwa Tirmidhi, Hamwaini, Ibn Maja, Ahmad Bin Hanbal, Hafidh Abu Nu’ami, Imam Tha’labi, Ibn Maghazili, Abu’l-Muwayyid Khawarizmi, na Dailami, ambayo hitimisho lake ni kwamba Ali alikuwa wa kwanza katika umma wote wa Kiislamu kukubali Uislamu.

Hata shupavu mchungu Ibn Hajar Makki ameandika katika “Sawa’iq-Muhirika”, Sura ya 2 Hadith juu ya Suala hili hili, ambazo baadhi ya hizo zimekubaliwa na Sulayman Balkhi Hanaf katika kitabu chake “Yanabiu’l-Mawadda” kuelekea mwisho wa kufunga Sura ya 2, amesimuluia hadith juu ya suala hilo hilo, baadhi yake ambazo zimekubaliwa na Suleiman Balkhi Hanafi ndani ya Yanabiul’Mawadda yake.

Zaidi ya hayo, ndani ya Yanabiul’Mawadda, kuelekea mwisho wa Sura ya 12, amesimulia kutoka Ibn Zubair, Makki na yeye kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah Ansari, Hadith kuhusu sifa za Ali, ambayo ningependa kuitoa hapa kwa ruhusa yenu ili kuhitimisha hoja yangu.

Mtume alisema: “Mwenyezi Mungu alinichagua mimi kuwa Mtume na akanifunulia maandiko matakatifu. Mimi nikamwambia, ‘Ee Allah, Mola Wangu, ulimtuma Musa kwa Firauni, Musa akakuomba umfanye ndugu yake, Harun, Waziri wake ambaye angeweza kuimarisha mkono wake, ili maneno yake yapate kushuhudiwa.

Sasa nakuomba, Ee Allah, uchague kwa ajili yangu kutoka miongoni mwa familia yangu Waziri ambaye ataimarisha mkono wangu. Mfanye Ali kuwa Waziri wangu na ndugu yangu, ingiza ushujaa kwenye moyo wake, na mpe nguvu juu ya maadui. Ali alikuwa mtu wa kwanza kuniamini na kushuhudia Utume wangu na mtu wa kwanza kutamka Upweke wa Allah sambamba pamoja na mimi.’

Baadae niliendelea kumuomba Allah. Kwa hiyo Ali ni kiongozi wa warithi (wangu). Kumfuata yeye ni rehma; kufa ukiwa na utii kwake ni Shahada. Jina lake huonekana katika Taurat pamoja na jina langu; mke wake, mwaminifu zaidi, ni binti yangu; watoto wake wawili wa kiume, ambao ni mabwana wa vijana wa Peponi, ni watoto wangu.

Baada yao, Maimam wote ni wawakilishi wa Allah juu ya viumbe baada ya Mitume; na ni milango ya elimu miongoni mwa watu wangu. Yeyote ambaye atawafuata ameokolewa kutokana na moto wa Jahanam; yeyote ambaye atawafuata ameongozwa katika njia iliyonyooka; yeyote ambaye amejaaliwa na Allah kuwa na mapenzi kwao hakika atapelekwa Peponi. Hivyo, watu wenye akili, chukueni tahadhari.’”

Ningeweza kunukuu hadith za namna hiyo usiku wote, ambazo zote zimeandikwa na Maulamaa wenu. Lakini nafikiri hii inatosha. Ni Ali peke yake aliyefuatana na Mtume tangu utotoni, na kwa hiyo ni sawa kwamba tunamuona ni mtu aliyeashiriwa katika maneno, “Wale ambao wako pamoja naye”, na sio mtu ambaye alifuatana na Mtume kwa safari ya siku chache tu.

Imani Ya Ali Akiwa Bado Mtoto Tu.

Hafidh: Umethibitisha Nukta yako, na kamwe hakuna hata mtu mmoja ambaye amekataa kwamba Ali alikuwa mbele zaidi katika kuukubali Uislamu. Lakini ukweli huu haumfad- hilishi yeye kuwa mwenye sifa zaidi kwa kumlinganisha na Masahaba wengine. Kweli, Makhalifa wakubwa walikubali imani katika Uislamu miaka kadhaa baada ya Ali, lakini imani yao ilikuwa tofauti na bora zaidi kuliko yake. Sababu yenyewe ni kwamba Ali alikuwa mtoto tu, na hawa walikuwa watu wazima. Ni dhahiri kwamba, imani ya watu wazima, wenye busara ilikuwa bora zaidi kuliko ile ya mtoto. Kwa nyongeza, imani ya Ali ilikuwa ya ufuataji wa kibubusa na imani ya watu hawa ilijengwa juu ya akili. Imani inayopatikana kwa akili ni bora kuliko imani ya upofu. Kwa vile mtoto ambaye hayuko chini ya wajibu wa kidini wa kutekeleza ibada, haikiri imani isipokuwa kwa kufuata kwa upofu, hivyo Ali, ambaye alikuwa mtoto tu wa miaka kumi na tatu, alikiri imani yake kwa upofu tu wa kufuata.

Muombezi: Mazungumzo kama hayo kutoka kwa mtu msomi kama wewe kwa hakika yanashangaza. Nashangaa jinsi gani nitaivunja hoja kama hiyo. Kama ningekuwa niseme kwamba umechukuwa msimamo kama huo kwa ukorofi tu, ingekuwa dhidi ya tabia yangu kuhusisha sababu kama hiyo kwa mtu msomi. Ngoja nikuulize Swali: je, kuukubali Uislamu kwa Ali kulitegemea juu ya kupenda kwake mwenyewe binafsi au kwa kulinganiwa ya Mtume?

Hafidhi: Kwa nini unachukuwa mtizamo mkali kama huu juu ya namna tunavyoongea, kwani tunapokuwa na mashaka ni lazima tuyajadili. Kwa kujibu swali lako, nakiri kwamba Ali aliukubali Uislamu kwa ulinganio wa Mtume.

Muombezi: Wakati Mtume alipomlingania Ali akubali Uislamu, yeye hakujua kwamba mtoto hafungwi na majukumu ya kidini? Kama ukisema kwamba alikuwa hajui utakuwa unahusisha na ujinga na kama alijua na akamhubiria Ali hata hivyo, basi kitendo chake kilikuwa cha upuuzi. Ni dhahiri kwamba, kuhusiha upuuzi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni ukafir kwa vile Mtume ni Ma’sum (hakosei wala hatendi dhambi). Allah anasema kuhusu yeye katika Qur’ani Tukufu: “Wala hasemi kwa matamanio (ya nafsi yake). Hayakuwa haya ila ni Wahyi uliofunuliwa (kwake)” (53:3-4).

Mtume alimuona Ali ni mtu wa kufaa kulinganiwa kuukubali Uislamu. Mbali na hili, ujana si lazima kutanguliwa na hekima. Utu uzima huchukuliwa maanani kuhusiana na utekelezaji wa wajbat za kidi- ni, lakini sio mambo yanayohusiana na hekima. Imani inahusiana na mambo yanayo endana na hekima na sio sheria za kidini. Hivyo Imani ya Ali wakati wa utoto ni sifa kwa ajili yake kama vile Allah anavyotuambia katika Qur’ani Tukufu kuhusu Isa katika maneno haya: “Hakika mimi ni Mtumishi wa Allah: Allah amenipa kitabu na amenifanya Nabii.” (19:30).

Vilevile katika Sura hiyo anasema kuhusu Mtume Yahaya: “Na tulimpa hekima angali mtoto.” (19:12). Seyyed Ali Humairi Yamani, (alikufa 179 A.H.) anaonyesha ukweli huu katika mashairi yake. Ansema: “Kama vile Yahaya alivyofikia cheo cha Utume katika utoto wake, Ali ambaye alikuwa mrithi wa Mtume na baba wa watoto wake, vilevile alifanywa mwakilishi wa Allah na mlezi wa watu akingali mtoto.”

Sifa na heshima inayotolewa na Allah haitegemei juu ya umri. Hekima na akili hutegemea juu ya hali ya kuzaliwa. Nashangazwa na maelezo yako kwa vile hoja kama hizo zilitole- wa na Manasibi na Makhariji kwa kuchochewa na Bani Umayya. Waliishusha imani ya Ali kwamba ilikuwa ya utii wa kibubusa kwa yale aliyofundishwa.

Hata wanachuo wenu wameikubali sifa ya Ali kwa namna hii. Muhammad bin Talha Shafi’i, Ibn Sabbagh Maliki, Ibn Abi’l-Hadid na wengine wamenukuu mashairi ya Ali. Katika moja ya mashari yake anasema: “Nilikuwa wa kwanza na wa mbele zaidi miongoni mwenu katika kuukubali Uislamu wakati nilipokuwa mtoto mdogo tu.”

Kama imani ya Ali katika umri mdogo kama huo haikua bora, Mtume asingeielezea namna hiyo. Sulayman Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 55, uk. 202, anasimulia kutoka kwa Ahman Bin Abdullah Shafi’i akinukuu kutoka kwa Khalifa wa pili, Umar Bin Khattab, ambaye alisema:

“ Abu Bakr, Abu Ubaida Jarra na Kundi la watu waliokuwepo pamoja na Mtume wa Allah aliposhika bega la Ali na kusema: “Ewe Ali! Wewe ni wa kwanza na wa mbele zaidi miongoni mwa waumini wote na Waislamu katika kuukubali Uislamu, Wewe kwangu mimi ni kama alivyokuwa Harun kwa Musa.”

Vilevile Imam Ahmad Bin Hanbal anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas, ambaye amesema yeye, Abu Bakr, Abu Ubaida Bin Jarra, na wengine walikuwa pamoja na Mtume wakati alipoweka mkono wake katika bega la Ali na akasema: “Wewe uko mbele zaidi katika imani ya Uislamu miongoni mwa Waislamu wote, na uko kwangu Mimi kama Harun alivyokuwa kwa Musa, Ewe Ali! Anayefikiria kwamba mimi ni rafiki yake ambapo ni adui yako, huyo ni muongo.” Ibn Sabbagh Maliki ameandika hadith kama hiyo katika “Fusulu’l-Muhimma”, uk. 125, kutoka “Khasa- isu’l-Alawi” kama simulizi ya Abdullah bin Abbas, na Imam Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i anaeleza katika “Khasa’isu’l-Alawi” kwamba alisema: “Nimemsikia Umar bin Khattab akisema, ‘Litajeni jina la Ali kwa heshima kwa sababu nimemsikia Mtume akisema kwamba Ali anazo sifa tatu. Mimi (Umar) natamani kwamba ningelikuwa na moja tu kati ya hizo kwa sababu kila moja ya sifa hizo ni yenye thamani kubwa sana kwan- gu kuliko kitu chochote katika ulimwengu huu.”

Ibn Sabbagh amesimulia kama ifuatavyo kwa nyongeza ya walivyoandika wengine. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kuhusu Ali, “Yeye ambaye anakupenda wewe hunipenda mimi, na ambaye ananipenda mimi, Allah Humpenda, na yeyote apendwaye na Allah, humuingiza Peponi. Lakini yule ambaye ni adui kwako ni adui kwangu, na ambaye ni adui kwangu, Allah ni adui kwake na humhukumu kwenda Motoni.”

Kujitangaza kwa Ali kuwa Mwislamu hata ambapo alikuwa bado mdogo huthibitisha ubora wa hekima na sifa yake, ambayo hakuna Mwislamu mwingine anayeweza kuipata. Tabari katika kitabu chake cha Ta’rikh ananukuu kutoka Muhammad Bin Sa’ad Bin Abi Waqqas, ambaye alisema: Nilimuuliza Baba yangu iwapo Abu Bakr alikuwa wa kwanza wa Waislamu. Yeye akasema, ‘Hapana, zaidi ya watu hamsini waliingia Uislam kabla ya Abu Bakr; bali alikuwa mbora kwetu kama Mwislam.’” Vilevile anaandika kwamba Umar Bin Khattab aliingia Uislamu baada ya wanaume arobaini na tano na wanawake ishirini na moja. “Ama kwa aliyekuwa mbele zaidi katika Uislamu na Imani, alikuwa ni Ali Bin Abi Talib.” Imani Ya Ali Ilikuwa Ni Sehemu Ya Asili Yake Hasa:

Mbali na ukweli kwamba, Ali alikuwa wa mbele katika kuingia Uislamu, alikuwa na sifa nyingine, ya kipekee kwake, na ya muhimu zaidi kuliko sifa zake nyingine.

Uislamu wa Ali ulitokana na asili yake, ambapo ule wa wengine umetokea tu baada ya kuwa makafir huko nyuma. Tofauti na Waislamu wengine na masahaba wa Mtume, Ali hajawahi kamwe kuwa Kafir. Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika “Ma-Nazalu’l-Qur’ani fi Ali”, na Mir Seyyed Ali Hamadani katika “Mawaddatu’l-Qurba” wanasimulia kwamba Ibn Abbas amesema: “Naapa kwa jina la Allah kwamba hakuna mtu hata mmoja ambaye alikuwa hakuabudu masanamu kabla ya kuingia Uislamu isipokuwa Ali. Ali, alikubali Uislamu akiwa kamwe hajapata kuabudu masanamu.”

Muhammad Bin Yusuph Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’t-Talib”, Sura ya 24 anamnukuu Mtume akisema: “Wale ambao walitangulia kuikubali imani katika upweke wa Allah miongoni mwa wafuasi wa Mitume walikuwa ni watu watatu ambao hawajawahi kamwe kuwa washirikina:

Ali bin Abi Talib, mtu aliyetajwa katika Suratu Yaa-Sin, na Muumini katika watu wa Firauni. Wale wakweli (ma-Sidiq) ni Habib-e-Najjar, miongoni mwa kizazi cha Yaa Sin, Hizqil (Sawaiq al-Muhriqah, hadith ya 30 kati ya zile 40 kuhusu sifa za Ali, Yanabiu’l-Mawadda, Jz. 42, Nahjul-Balaghah, Jz. 2, uk. 451) miongoni mwa kizazi cha Firauni, na Ali bin Abi Talib, ambaye amewapita wote.” Mir Seyyed Ali Hamadani katika “Mawadda-tu’l-Qubra”, Mawadda ya 7, Khatib Khawarizmi katika “Manaqib” na Imam Tha’labi katika “Tafsir” yake anasimulia kutoka kwa Khalifa wa pili, Umar Bin Khattab: “Nashuhudia kwamba nimemsikia Mtume akisema, ‘Kama Mbingu Saba zingewekwa pamoja katika mizani moja na imani ya Ali katika nyingine, hakika imani ya Ali ingezidi uzito ile nyingine.’”

Nukta hiyo hiyo iliwekwa katika mashairi yaliyotungwa na Sufyani bin Mus’ab bin Kufi kama ifuatavyo: “Kwa jina la Allah, nashuhudia kwamba Mtume alituambia: ‘Haipasi kubakia bila kutojulikana na kwa mtu yeyote kwamba kama imani za wale wote wanaishi juu ya ardhi ingewekwa katika kipimio kimoja cha mizani na ile ya Ali katika kingine, imani ya Ali ingezidi uzito ile ya wengine.”

Ali Aliwapita Masahaba Wengine Wote Na Umma Wote Katika Ubora.

Mir Seyyed Ali Hamadani Shafi’i amendika hadith nyingi katika Mawaddatu’l-Qurba yake, ambazo zinaunga mkoni ubora wa Ali. Katika Mawadda ya Saba ananukuu kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mbora wa watu wa ulimwengu wote katika kipindi changu ni Ali.”

Wengi wa Maulamaa waadilifu wameukubali ubora wa Ali. Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh yake ya “Nahju’l-Balagha” Jz. 3, uk. 40, anasema kwamba Abu Ja’far Iskafi, kiongozi wa madhehebu ya Mu’tazil, alitangaza kwamba Bashir bin Mu’amar, Abu Musa, Ja’far Bin Mubashir, na maulamaa wengine wa Baghdad wanaamini kwamba, “Mtu bora zaidi miongoni mwa Waislamu wote alikuwa Ali bin Abu Talib, na baada yake mtoto wake Hasan, kisha mtoto wake Husain, baada yake ni Hamza na baada yake ni Jafar Bin Abi Talib.” Anaendelea kusema kwamba kiongozi wake Abu Abdullah Basri, Sheikh Abu’l-Qasim Balkhi, na Sheikh Abu’l-Hasan Khayya wanayo imani hiyo hiyo kama Abu Ja’far Iskafi kuhusiana na ubora wa Ali. Anaelezea imani ya madhehebu ya Mu’tazil ikisema.

“Mtu bora baada ya Mtume wa Allah ni mrithi (makamu) wa Mtume, mume wa Fatima, Ali; baada yake, ni watoto wake wawili Hassan na Husain; baada yao, Hamza, na baada yake Ja’far (Tayyar).”

Sheikh: Kama ungejua maelezo ya maulamaa yenye kuunga mkono ubora wa Abu Bakr, usingesema maneno haya.

Imani Ya Ali Ni Bora Kuliko Ya Abu Bakr.

Muombezi: Maulamaa wote wa kutegemewa, wa Kisuni wameukubali ubora wa Ali. Kwa mfano, unaweza ukarejea “Sharh Nahju’l-Balagha” ya Ibn Abi’l-Hadid, Jz. 3, uk. 264, ambamo maelezo hayohayo yamenukuliwa kutoka kwa Jahiz kwamba imani ya Abu Bakr ilikuwa bora kuliko ile ya Ali. Walakini, Abu Ja’far Askafi, mmoja wa maulamaa wakubwa wa madhehebu ya Mu’tazil alikataa madai haya, akisema kwamba imani ya Ali ilikuwa bora kwa ile ya Abu Bakr na masahaba wengine wote. Abu Ja’far amesema: “Hatukatai ubora wa masahaba, lakini kwa hakika hatumchukulii yeyote kati yao kuwa mbora kuliko Ali.” Ali alikuwa wa cheo cha juu sana kiasi kwamba kutaja jina lake sambamba na masahaba wengine haifai.

Kwa kweli sifa za masahaba haziwezi kulinganishwa na sifa tukufu mno za Ali. Mir Seyyed Ali Hamadani anasimulia katika “Mawadda” yake ya 7 kutoka kwa Ahmad Bin Muhammadu’l-Karzi Baghdadi, ambaye amesema kwamba alisikia kutoka kwa Abdullah bin Ahmad Hanbal, ambaye alimuuliza baba yake Ahmadi Bin Hanbal kuhusu cheo cha Masahaba wa Mtume. Yeye akamtaja Abu Bakr, Umar na Uthman na akasimama. Kisha Abdallah akamuuliza baba yake. “Liko wapi jina la Ali bin Abu Talib?” Baba yake akajibu, “Yeye ni katika dhuria watukufu wa Mtume. Hatuwezi kutaja jina lake (kwa jinsi alivyo maarufu) sambamba pamoja na watu wale.”

Tunaona katika Qur’ani Tukufu kwamba katika aya ya Mubahila, Ali anatajwa kama nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kuna hadithi yenye kuunga mkono habari hii, ambayo imeandikwa katika “Mawadda” ya 7 hiyohiyo, iliyosimuliwa kutoka kwa Abdullah Bin Umar Bin Khattab.

Alisema kwamba siku moja walipokuwa wakihesabu majina ya masahaba, yeye alimtaja Abu Bakr, Umar, na Uthman. Mtu mmoja akasema, “Ee Abdu’r-Abdur- Rahman! Kwa nini umeliacha jina la Ali? Yeye alijibu “Ali ni mmoja wa dhuria wa Mtume. Hawezi kuchanganywa na mtu yoyote yule. Yuko katika kundi namna moja na Mtume wa Allah.”

Ngoja nisimulie hadith nyingine kutoka katika “Mawadda” hiyo hiyo. Imesimuliwa kuto- ka kwa Jabir Bin Abdullah Ansari kwamba siku moja wakiwepo mbele ya Muhajirina na Ansari, Mtume alimwambia Ali:

“Ewe Ali! Kama mtu atatekeleza Sala zake kamili kwa Allah, na kisha akatia shaka kwamba wewe na familia yako ni bora kwa viumbe wengine wote, makazi yake yatakuwa Jahanam.” (Baada ya kusikia hadith hii, wale wote waliokuwepo pale, hususan Bw. Hafidhi, walionyesha kutubu, isije wakawa miongoni mwa wenye kutia mashaka).

Nimerejea hadith chache tu. Chaguo lenu linaelekea kuwa ni kuzikataa hadith zote hizi sahihi, ambazo zimeandikwa kwenye vitabu vyenu, au kukubali kwamba imani ya Ali ilikuwa bora kuliko ile ya masahaba wote, pamoja na ya Abu Bakr na Umar. Vilevile naomba muiangalie hadith hii (inayokubaliwa na madhehebu zote) ambamo Mtume alisema wakati wa Ghazawa-e-Ahzab (hujulikana vilevile kama vita vya Handaq), wakati Ali alipomuua Amru Ibn Abdu-e-Wudd kwa pigo moja la upanga wake:

“Pigo moja la Ali katika vita vya Khandaq limempatia fadhila zaidi kuliko malipo ya matendo mema ya umma wote (majini na watu) mpaka Siku ya Hukumu.” Kama pigo moja la upanga wake lilikuwa bora katika fadhila kuliko Sala za majini na watu zikichanganywa zote pamoja hakika ubora wake hauwezi kuhojiwa na yeyote isipokuwa na mashupavu waovu.

Ali Kama Nafsi Ya Mtukufu Mtume (S.A.W.W.).

Ingekuwa hakuna uthibitisho mwingine wa ubora wa Ali kwa Masahaba wote na Wanadamu wote kwa ujumla, Aya ya Mubahila inatosha kuthibitisha ubora wake. Inamtaja Ali kama “nafsi” ya Mtume. Mtukufu Mtume alikuwa kwa kukubalika kabisa ni mbora zaidi kwa wanadamu wote kuanzia mwanzo mpaka mwisho.

Kwa hiyo, neno “anfusana” (nafsi zetu) katika aya hiyo linaloashiria kwa Ali huthibitisha kwamba pia alikuwa bora kwa wanadamu wote kuanzia mwanzo mpaka mwisho. Huenda sasa mtakubali kwamba ule usemi, “Na wale ambao wapo pamoja naye”, utajo wake ni kwa Ali. Yeye alikuwa pamoja na Mtume kabla ya mtu yeyote yule kuanzia mwanzo wa Uislamu.

Ama kwa nini Ali hakufuatana na Mtume katika usiku wa kuhama kutoka Makka, ni wazi kwamba Mtume alimkabidhi Ali majukumu muhimu zaidi. Hakuna aliyekuwa muaminifu kama Ali. Aliachwa nyuma kurudisha kwa wenyewe mali zilizowekwa amana kwa Mtume.

(Jukumu la pili la Ali lilikuwa ni kuipeleka familia ya Mtume na Waislamu wengine Madina. Na hata ingawa Ali hakuwa pamoja na Mtume katika pango usiku ule, alitekeleza jukumu muhimu zaidi kwa vile alilala katika kitanda cha Mtume). Aya Ya Qur’ani Yenye Kumsifu Ali Kwa Kulala Kwake Katika Kitanda Cha Mtume Katika Usiku Wa Hijra.

Wanachuoni wenu wenyewe wametaja sifa za Ali katika tafsir zao (za Qur’ani). Kwa mfano, Ibn Sab’i Maghribi katika Shifa’u’s-Sudur, Tibrani katika “Ausat” na “Kabir”, Ibn Athir katika “Usudu’l-Ghaiba”, Jz. 4, uk. 25, Nuru’d-Din Sabbagh Maliki katika “Fusuli’l- Muhimma Fi Ma’rifati’l-’aimma”, uk. 33, Abu Ishaq Tha’labi, Fazil Nishapuri, Fakhru’d-Din Radhi na Jalalu’d-Dini Suyuti, kila mmoja katika Tafsir yake, Hafidh Abu Nu’aim Isphahani, muhadithina maarufu wa Ki-Shafi’i katika “Ma-Nazala’l-Qur’an fi Ali”, Khatib Khawarizmi katika “Manaqib” Sheikhul-Islam Ibrahim bin Muhammad Hamwaini katika “Fara’id”, Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’t-Talib”, Sura ya 62, Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad”, Muhammad bin Jarir kupitia vyanzo mbalimbali, Ibn Hisham katika “Siratu’n-Nabi”, Hafidh Muhadith wa Damascus katika “Arba’in Tiwal”, Imam Ghazali, katika “Ihya’u’l-Ulum”, Jz. 3, uk. 223, Abu’s-Sa’adat katika “Fadha’ilu’l-Irati’t-Tahira”, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharhe “Nahju’l-Balagha”, Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhikira” na wengine katika maulamaa wenu mashuhuri, wanasimulia kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokusudia, kwa amri ya Allah, kuondoka Makka na kwenda Madina, alimtaka Ali ajifunike shuka lake la kijani na alale katika kitanda chake.

Kwa hiyo, Ali akalala pahali pa Mtume kisha Mwenyezi Mungu akawaambia Malaika Jibril na Mikael kwamba amewafanya wao kuwa ndugu, na kwamba mmoja wao ataishi muda mrefu kuliko mwingine. Aliwauliza ni nani alikuwa tayari kumpa ndugu yake maisha yake ya ziada, ambayo kadiri yake hakuna mmoja wao aliyejua. Walimuuliza (Allah) iwapo chaguo hilo ni wajibu. Walielezwa kwamba sio wajibu. Hakuna hata mmoja wao aliyechagua kuachana na maisha yake ya ziada. Kisha yakafuata maneno haya matukufu: “Mimi nimeumba undugu kati ya mwakilishi wangu Ali na Mtume wangu Muhammad. Ali amejitolea kutoa mhanga maisha yake kwa ajili ya maisha ya Mtume. Kwa kulala katika kitanda cha Mtume, anayalinda maisha ya Mtume. Sasa ninyi wote mnaagizwa kwenda duniani kumuokoa kutokana na mbinu za uovu wa maadui.”

Kwa hiyo, wote wakaja duniani. Jibril akakaa kichwani kwa Ali na Mikaeli miguuni kwake. Jibril akasema, “Hongera, Ewe mwana wa Abu Talib! ambaye kwako Mwenyezi Mungu anajivunia mbele ya Malaika Zake.” Baada ya haya, Aya ifuatayo ikateremshwa kwa Mtume. “Na kuna aina ya watu ambao hutoa maisha yao kuzitafuta radhi ya Allah; na Allah ni mwingi wa upole kwa waja (wake).” (2:207).

Sasa nakusihini waheshimiwa, kuingalia aya hii kwa uangalifu wakati mtakaporudi nyumbani usiku na kutoa uamuzi wenu wenyewe. Je, ubora kwa haki ni wa yule ambaye alibakia pamoja na Mtume katika safari ya siku chache, akionyesha woga na huzuni, au kwa yule ambaye alihatarisha maisha yake usiku ule kishujaa na kwa furaha, kwa ajili ya usalama wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Imam Ja’far Askafi, mmoja wa maulamaa wakub- wa na viongozi wa Mu’tazil, anathibitisha, (kama ilivyosimuliwa katika Sharhe ya “Nahaju’l- Balagha” na Abi’l-Hadid Jz. 3, uk. 269-281), kwamba kulala kwa Ali katika kitanda cha Mtume kulikuwa bora zaidi kuliko muda mfupi wa Abu Bakr aliokaa pamoja na Mtume.

Anasema: “Maulamaa wa Kiislamu kwa pamoja wanashikilia kwamba, kwa ukweli halisi, ubora wa Ali katika usiku ule ulitukuka mno kiasi kwamba hakuna mtu angeweza kuufikia isipokuwa Ishaka na Ibrahimu wakati walipokuwa tayari kutoa maisha yao mhanga katika kutii mapenzi ya Allah.” (Wafasiri wengi, maulamaa na wanahistoria wanaamini kwamba alikuwa ni Ismail ambaye alijitoa mhanga na sio Ishaka).

Katika ukurasa wa 271 wa Sharhe ya Nahaju’l-Balagha, maelezo ya Abu Ja’far Askafi katika kumjibu Abu Athman Jahiz Nasib yameandikwa. Anasema: “Nilikwisha kuthibitisha mapema kwamba kulala kwa Ali katika kitanda cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika usiku wa kuhama kulikuwa bora zaidi kuliko kule kwa Abu Bakr kubakia pamoja na Mtume katika Pango. Ili kusisitiza hoja yangu, nitaithibitisha katika mitazamo mingine miwili: Kwanza, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah akiwa na mkuruba wa karibu na wa siku nyingi na Ali, alimpenda mno. Kwa hiyo alihisi kupotea kwa upendo wakati walipotengana.

Kwa upande mwingine, Abu Bakr alipata fursa ya kwenda pamoja na Mtume. Kwa vili Ali alikuwa na uchungu wa kutengana kwao, malipo yake yaliongezeka kwa sababu jinsi maumivu yanavyokuwa makali zaidi katika utumushi, ndivyo yanavyopata malipo makubwa zaidi.

Pili, kwa vile Ali alikusudia kuondoka Makka na hata aliwahi mara moja kuondoka peke yake, hali yake kama raia kule iliongezeka kuwa ngumu. Hivyo wakati akiondoka Makka pamoja na Mtume, hamu yake ya kuondoka ilitimia. Kwa ajili hiyo hakuna ubora wa kimaadili kama huo kwa ajili yake kama ulivyo kwa Ali, ambaye alivumilia machungu makali katika kuhatarisha maisha yake mbele ya panga zilizochomolewa za maadui.

Ibn Sab’a Maghrib anasema katika kitabu chake “Shifa’u’s-Sudur” kuhusu ushujaa wa Ali: “Kuna umoja kamili (wa makubaliano) miongoni mwa maulamaa wa Kiarabu kwamba katika usiku wa Hijra, kulala kwa Ali katika kitanda cha Mtume kulikuwa bora zaidi ya kutoka pamoja naye. Ali alijifanya mwenyewe mwakilishi wa Mtume na akahatarisha maisha yake kwa ajili ya Mtume. Hoja hii ni wazi mno kiasi kwamba kamwe hakuna hata mtu mmoja aliyeikataa isipokuwa wale waliopatwa na uwenda wazimu au ushabiki.” Nitakomeshea hapa na kurudi kwenye nukta yangu muhimu. Umesema kwamba, maneno ya Qur’ani “Wakali dhidi ya makafir” (48:29) yanamuashiria Khalifa wa pili, Umar Bin Khattab.

Lakini dai hili haliwezi kukubaliwa kwa sababu tu kwamba umesema hivyo. Ni lazima tuamue iwapo sifa hii ni katika tabia yake au laa. Kama ndivyo, niko radhi kuikubali. Kwa hakika ukali unaweza kuonyeshwa katika njia mbili: Katika majadiliano ya kidini ambayo kwayo kwa nguvu ya hoja, maulamaa wa upande mwingine wananya- mazishwa. Pili, unaweza kuonyeshwa katika uwanja wa vita.

Kwa kadiri mijadala ya kielmu ihusikanavyo, hakuna mfano hata mmoja katika historia ambapo Umar ameonyesha ukali wowote. Katika kiwango chochote, sijaona taarifa yoyote ya kihistoria yenye kuonyesha kwamba Umar alionyesha ukali katika majadiliano ya kielimu. Nitawashukuruni kama mtanionyesha mfano wowote. Kwa kweli, maulamaa wenu, wamekubali kwamba alikuwa ni Ali ambaye aliyatatua yale matatizo ngumu ya kisheria na kufutu mas’ala ya kidini wakati wa kipindi cha Makhalifa watatu. Ingawaje Bani Umayya na wafuasi mbumbumbu wa Abu Bakr walibuni hadithi zisizo na idadi kwa niaba yao, hawakuweza kuficha ukweli kwamba wakati watu wa imani nyingine walipokuja kwa Abu Bakar, Umar, au Uthman, kutatua matatizo magumu, makhalifa hawa waliyapeleka matatizo hayo kwa Ali.

Ali aliwapa majibu ya kuvutia kiasi kwamba watu wengi wasiokuwa Waislamu waliingia Uislamu. Ukweli kwamba Abu Bakr, Umar na Uthman walikubali ubora wa Ali unatosha kuthibitisha hoja yangu.

Wanachuoni wenu wameandika kwamba Khalifa Abu Bakr alisema: “Niondoeni, niondoeni, kwa vile mimi sio bora kuliko ninyi alimuradi Ali yuko kati yenu.” Kwa uchache kabisa, takriban mara sabini, khalifa Umar alikiri: “Kama Ali asingekuepo Umar angeangamia.” Mazingira mengi yenye hatari yametajwa kwenye vitabu, lakini mimi sitaki kueleza sana juu ya nukta hii. Kunaweza kuwa na mambo mengi muhimu ya kujadili.

Nawab: Ni habari gani zaweza kuwa za muhimu zaidi kuliko hii? Je, mambo haya yametajwa katika vitabu vyetu? Kama yametajwa tafadhali tueleze tupate kujua.

Muombezi: Maulamaa waadilifu wa madhehebu yenu wanakubali kwamba, mara kwa mara Umar alikiri kwamba Ali alikuja kumuokoa.

Ushahidi Kuhusu Maneno Ya Umar:

“Kama Ali Asingekuwepo, Umar Angeangamia.”

Qadhi Fadhlullah Bin Ruzbahan, yule shabiki shupavu, katika kitabu chake “Ibtalu’l- Batil;” Ibn Majar Asqalani katika “Tihdhibu’l-Tahdid”, kilichochapishwa Hyderabad Daccan, uk. 337; Ibn Hajar katika Isaba, Jz. 2, iliyochapishwa Misir uk. 509; Ibn Qutayba Dinawari katika “Ta’wil-e-Mukhtalafu’l-Hadith” uk. 201-202, Ibn Hajar Makki katika Sawa’iq-e-Muhriqa uk. 78; Hajj Ahmad Afindi katika “Hidayatu’l- Murtab” uk. 146 na 152, Ibn Athir Jazari katika “Usudu’l-Ghaiba”, Jz. 4, uk. 22; Jalalu’d-Din Suyuti katika “Ta’rikhu’l-Khulafa”, uk. 66; Ibn Abdu’l-Birr Qartabi katika “Isti’ab” Jz. 2, uk. 474; Seyyed Mu’min Shablanji katika “Nuru’l-Absar” uk.73; Shahabu’d-Din Ahmad bin Abdu’l-Qadir A’jili katika “Dhakhiratu’l-Ma’al”; Muhammad bin Ali As-Subban katika Is’afu’r-Raghibin, uk.152; Nuru’d-Din bin Sabbagh Maliki katika “Fusulu’l-Muhimma”, uk. 18; Nuru’d-Din Ali bin Abdullah Samhudi katika “Jawahiru’l-Iqdani”; Ibn Abi’l- Hadid Mu’tazil katika “Sharhe Nahaju’l-Balagha”, Jz. 1, uk. 6. Allama Qushachi katika Sharhe-e-Tarid, uk. 407, Khatib Khawarizmi katika “Manaqib”, uk. 46 & 60 Muhammad bin Talha Shafi’i katika “Matalibu’s-Su’ul” Sura ndogo ya 6, uk. 29, Imam Ahmad bin Hanbal katika “Fadha’il” halikadhalia na “Musnad”; Sibt Ibn Jauzi katika “Fadhkira” uk. 85 na 87 Imam Tha’labi katika “Tafsir Kafshu’l-Bayan”, Allama Ibn Qayyim Jauzi katika “Turuqi’l-Hakim”, akiandika hukumu za Ali kuanzia uk. 41 mpaka uk. 53; Muhammd bin Yusufu Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’t-Talib”, Sura ya 57; Ibn Maja Qazwini katika “Sunan” yake; Ibn Maghazili Shafi’i katika “Manaqib”; Ibrahim bin Muhammad Hamwaini katika “Fara’id”; Muhammad bin Ali bin Hasani’l-Hakim katika “Sharh-e- Fat’hil-Mubin”; Dailami katika “Firdaus” Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 14, Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika “Hilyatu’l- Auliya”, halikadhalika katika “Ma-Naza-la’l-Qur’an fi Ali”, na kundi la maulamaa wakub- wa wa madhehebu yenu, pamoja na tofauti ndogo katika maneno, wamesimulia usemi wa Umar, “Kama Ali asingekuwepo, Umar angeangamia.”

Mwanachuoni mkubwa, Ganji Shafi’i, katika sura ya 57, ya “Kifayatu’t-Talib Fi Manaqib Ali Bin Abu Talib”, baada ya kusimulia baadhi ya hadith sahihi anaelezea kutoka kwa Hudhaifa bin Yaman kwamba, “Siku moja yeye Hudhaifa alikutana na Umar, akamwuliza (yeye Hudhaifa): Ulijisikiaje hali yako wakati ulivyoamka asubuhi?” Hudhaifa akasema, “Niliamka asubuhi nikiichukia haki, nikipenda fitina, kushuhudia kitu kisichoonekana; kujifunza kwa moyo kitu kisichoumbwa, kusali bila kuwa na wudhuu, na kujua kwamba, kilichokuwa changu hapa duniani, sio kwa ajili ya Allah katika Mbingu.’

Umar alikasirishwa sana na maneno haya na alikusudia kumuadhibu Hudhaifa wakati Ali alipoingia ndani. Aliona dalili za hasira kwenye uso wa Umar na akauliza kwa nini alikuwa amekasirika hivyo. Umar akamueleza (maneno ya Hudhaifa) na Ali akasema: “Hakuna ubaya wowote kuhusu maneno haya.

Alichosema Hudhaifa ni sawa sawa: Haki maana yake kifo, ambacho anakichukia; fitna maana yake mali na watoto ambavyo anavitaka; na anaposema kwamba anashuhudia ambavyo hakuviona, hii ina maana kwamba anashuhudia upweke wa Allah, kifo, siku ya malipo, Pepo, Moto, daraja juu yake inayoitwa Sirat, ambavyo hakuna hata kimoja kati ya hivyo alichokiona.

Anaposema anajifundisha kwa moyo ambacho hakikuumbwa, hii huashiria kwenye Qur’ani. Anaposema kwamba anasali bila wuudhu, hii huashiria katika kumswalia Mtume wa Allah (kumtakia rehema na amani) ambako kuna ruhusiwa bila wuudhu; wakati akisema anacho kitu duniani ambacho si kwa ajili ya Allah Mbinguni, hii huashiria kwa mke wake, kwa vile Allah hana mke au watoto. Kisha Umar akasema: “Umar angepotea kama Ali asingetokea.’”

Ganji Shafi’i anasema kwamba maelezo ya Umar yanathibitika kwa mujibu wa riwaya za wasimuliaji wengi wa hadith. Mwandishi wa “Manaqib” anasema kwamba Khalifa Umar, mara kwa mara alisema: “Ewe Abu’l-Hasan! (Ali). Sitakuwa sehemu ya jamii bila wewe.” Vilevile alisema: “Wanawake hawana uwezo wa kuzaa mtoto kama Ali.”

Muhammad bin Talha Shafi’i katika “Matalibu’s-Su’-ul” na Sheikh Sulayman Balkh Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 14, akisimulia kutoka kwa Tirmidhi, ameandika riwaya yenye kinaganaga kutoka kwa Ibn Abbas ambapo mwisho wa riwaya hiyo anasema: “Masahaba wa Mtume walikuwa wakitafuta hukumu za kidini kutoka kwa Ali, na walikubali maamuzi yake. Hivyo, Umar Bin Khattab alisema katika nyakati mbalimbali, “Kama isingekuwa ni Ali, Umar angeangamia.”

Katika mambo ya kidini na mijadala ya kielimu Umar hakuonyesha ukali wowote. Kinyume chake, alikiri udhaifu wake mwenyewe na kumkubali Ali kama kimbilio lake. Hata Ibn Hajar Makki katika sura ya 3 ya “Sawa’iq-Muhriqa”, akielezea kutoka kwa Ibn Sa’d anamnukuu Umar akisema: “Naomba msaada wa Allah katika kuamua yale matati- zo magumu ambayo kwamba Abu’l-Hasan (Ali) hayupo.”

Ushujaa Wa Khalifa Umar Haujaonekana Kamwe Katika Uwanja Wowote Wa Vita.

Amma kuhusu ukali wa Umar katika uwanja wa vita, historia haikuandika mfano wowote juu ya hilo. Kinyume chake, wanahistoria wa madhehebu zote wanasimulia kwamba wakati wowote Umar alipokabiliana na adui mwenye nguvu, yeye alikimbia. Matokeo yake, Waislamu wengine pia walikimbia na mara kwa mara jeshi la Kiislamu lilishindwa.

Hafidh: Umezidisha pole pole ukosefu wa uungwana. Umemtukana Khalifa Umar ambaye alikuwa ni fahari ya Waislamu na ambaye katika zama zake Waislamu walipataushindi mkubwa. Kwa sababu ya Umar, jeshi la Waislamu lilishinda vita vyao. Unamuita muoga na kusema kwamba alikimbia kutoka uwanja wa vita na kwamba kushindwa kwa jeshi la Kiislamu kulikuwa ni kwa sababu yake! Je, ni sahihi mtu wa hadhi kama yako kumsingizia Khalifa Umar?

Muombezi: Nina wasiwasi kwamba umekosea. Ingawa umekuwa na mimi kwa mikesha mingi, hujanielewa bado. Pengine unafikiria ni kwa sababu ya chuki kwamba ndio ninalau- mu au kusifu watu. Sio hivyo. Kuna kuwiwa kukubwa katika mijadala ya kidini, ambako kumekuwa ni chanzo cha upinzani miongoni mwa Waislamu kwa karne nyingi. Mijadala kama hiyo mara kwa mara uchochea hali ya uovu, ambayo haipatani na maamrisho ya Qur’ani. Qur’ani kwa uwazi inasema:

“Enyi ambao mmeamini! Jiepusheni sana na dhana (kama iwezekanavyo) kwani baadhi ya dhana katika hali nyingine ni dhambi.” (49:12). Unafikiria kwamba maelezo yangu yamechochewa na uovu.Ukweli ni kinyume chake. Sijatamka neno kinyume cha ambavyo maulamaa wenu wameandika. Umesema hivi punde tu kwamba nimemtukana Khalifa Umar.

Lakini kulikuwa hakuna hata chembe ya dalili ya matusi. Niliyosema yanaoana na kumbukumbu za Historia. Sasa nalazimika kutoa mtazamo ulio wazi ili kunyamazisha upinzani huu.

Ushindi Haukuwa Kwa Sababu Ya Sifa Binafsi Za Umar.

Umesema Khalifa Umar alikuwa anahusika na ushindi wa Waislamu. Hakuna mtu anayekataa kwamba Waislamu walipata ushindi mkubwa wakati wa Ukhalifa wa Umar. Lakini kumbuka kwamba kwa mujibu wa maulamaa wenu mashuhuri, kama Qadhi Abu Bakr Khatib, katika kitabu chake, Ta’rikh Baghdad, Imam Ahmad Bin Hanbal katika “Musnad”, Ibn Abi’l-Hadid katika “Sharhe Nahju’l-Balagha” na waandishi wengine wengi, Khalifa Umar alitafuta mwongozo kutoka kwa Ali katika mambo yote ya kiutawala na kijeshi.

Na alikuwa akitenda kwa kufuata ushauri wa Ali. Kwa nyongeza, kulikuwa na tofauti katika ushindi wa Kiislamu kwa vipindi tofauti. Namna ya kwanza inarejea kwenye ushindi wakati wa kipindi cha Mtume mwenyewe, ambao ulikuwa kimsingi kwa sababu ya Ushujaa wa Ali. Kila mtu anakubali kwamba Ali alikuwa shujaa zaidi wa mashujaa. Kama hakupigana katika vita, ushindi haukupatikana.

Kwa mfano katika vita vya Khaibar, alipata maradhi ya macho, na ilikuwa haiwezikani kwa yeye kwenda kwenye mapigano.Waislamu walirudia rudia kushindwa kila walipokwenda kwenye uwanja wa mapambano, mpaka alipotibiwa na Mtume, Ali aliwaendea maadui mpaka akaziteka ngome za Khabar. Katika vita vya Uhud, wakati Waislamu wakivunja safu na kukimbia, alikuwa ni Ali aliyesimama imara.

Bila woga, alimkinga Mtume kutokana na maadui mpaka sauti iliyojificha ikatangaza, “Hakuna upanga kama Dhu’l-fiqah, na hakuna kijana shujaa kuliko Ali.”

Namna ya pili ya ushindi inahusiana na vile vita ambavyo vilipiganwa baada ya kifo cha Mtume. Ushindi huu ulikuwa ni kutokana na ushujaa wa maaskari mashuhuri wa Kiislamu na ubingwa wao wa kupanga. Lakini hapa hatuhusiki na ushindi wa Kiislamu wa wakati wa Ukhalifa wa Umar. Maudhui yetu ni kuhusu ujasiri wa Umar mwenyewe. Hauthibitishwi na ushahidi wowote wa kihistoria.

Hafidh: Ni matusi kudai kwamba Umar alikimbia kutoka uwanja wa mapambano, na kwamba hii ilipelekea kushindwa kwa Waislamu.

Muombezi: Kama kuonyesha ukweli wa kihistoria kuhusu mtu ni matusi, basi matusi haya yameandikwa na maulamaa wenu.

Hafidh: Ni wapi maulamaa wetu walipoandika kwamba Khalifa Umar alikimbia kutoka Uwanja wa mapambano? Ni wakati gani alisababisha kushindwa kwa Waislamu?

Kushindwa Kwa Abu Bakr Na Umar Katika Vita Vya Khaibar.

Muombezi: Kwa vile Ali alikuwa akiumwa macho katika siku ya kwanza ya vita vya Khaibar, Mtume alimpa Abu Bakr bendera ya Waislamu, ambaye aliongoza jeshi la Waislamu dhidi ya Mayahudi. Alirudi akiwa ameshindwa baada ya muda mfupi wa mapambano. Siku iliyofuata bendera ya Waislamu ilitolewa kwa Umar, lakini kabla hajafika sehemu ya mapambano, alikimbia kwa woga.

Hafidh: Maelezo haya ni uzushi wa Shi’a.

Muombezi: Vita vya Khaibar vilikuwa ni tukio muhimu la maisha ya Mtukufu Mtume, lililosimuliwa kwa kinaganaga na wanahistoria wa madhehebu zote. Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika “Hilyatu’l-Auliya” Jz. 1, uk. 62, Muhammad Bin Talha Shafi’i katika “Matalibu’s-Su’ul”, uk. 40, kutoka katika “Sira” cha Ibn Hisham, Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’t-Talib”, Sura ya 14, na maulamaa wenu wengi wengine wameandika tukio hili.

Lakini simulizi iliyo sahihi zaidi ni ile ya wanachuoni wawili wakubwa. Muhammad bin Ismail Bukhari, ambaye ameandika katika Sahih yake Jz. 2 iliy- ochapishwa Misir 1320 A.H., uk. 100, na Muslim Bin Hujjaj, ambaye anaandika katika Sahih yake, Jz. 2, iliyochapishwa Misir 1320 A.H., uk. 324, kwamba, “Khalifa Umar alikimbia kutoka Uwanja wa mapambano katika safari mbili.”

Miongoni mwa thibitisho nyingi zilizo wazi juu ya nukta hii ni beti zilizo za wazi za Ibn Abi’l-Hadid wa madhehebu ya Mu’tazila zijulikanazo kama “Alawiyyat-e-Sab’a” katika kumsifu Ali. Kuhusu “lango la Khaibar”, anasema: “Je, umesikia hadithi ya ushindi wa Khaibar? Miujiza mingi imefunganishwa pamoja ambayo huchanganya hata akili zenyes busara! Hawa wawili (Abu Bakr na Umar) walikuwa hawana mapenzi kwayo, au maarifa, ya kubeba bendera (kuongoza jeshi). Hawakujua siri za kutunza heshima ya bendera, waliifunika na twezo na wakakimbia ingawa walijua kwamba kukimbia kutoka kwenye uwanja wa mapambano ni sawa sawa na ukafiri.

Walifanya hivyo kwa sababu ya mmoja wa wanajeshi shujaa wa Kiyahudi, kijana mrefu na upanga wa wazi mkononi, akiwa amepanda juu ya farasi mwenye umbo refu, akiwashambulia kama mbuni dume aliyesisimuliwa, ambaye amepata nguvu kutokana na hewa ya msimu wa kuchipua na uoto wake wa mimea. Alikuwa kama ndege mkubwa ambaye amejipamba kwa rangi za kupendeza na aliyekuwa akienda kuelekea kwa mpenzi wake. Mng’aro wa moto wa kifo kutoka kwenye upanga wake na mkuki uliangaza na kuwatishia watu wawili hawa.” Ibn Abi’l-Hadid akizungumza nao (Abu Bakr na Umar) anaendelea kusema: “Nakuombeeni msamaha juu yenu, kwa kule kushindwa na kukimbia kwenu, kwa vile kila mtu anachukia kifo na kupenda uhai. Kama wengine wote, ninyi pia hamkukipenda kifo ingawa hakuna kinga kutokana na kifo. Lakini hamkuweza kujihatarisha na kifo.” Lengo langu sio kumkashifu mtu yeyote, ninasimulia ukweli wa kihistoria kuonyesha kwamba Khalifa hakuwa na ushujaa kama huo ambao angestahiki sifa ya “Mkali dhidi ya Makafir.” Ukweli ni kwamba yeye alikimbia kutoka uwanja wa mapambano.

Sifa hii katika mjadala inamhusu Ali peke yake, ambaye katika kila vita alikuwa mkali dhidi ya makafiri. Ukweli huu umethibitishwa na Allah kwenye Qur’ani Tukufu. Yeye Anasema:

“Enyi mlioamini! atakayeiacha dini yake miongoni mwenu, basi hivi karibuni Mwenyezi Mungu ataleta watu wengine ambao atawapenda, nao watampenda, wanyenyekevu kwa waumini, na wenye nguvu kwa makafiri. Watapiganaia dini ya Mwenyezi Mungu, wala hawataogopa lawama ya wenye kulaumu. Hiyo ndiyo fadhila ya Mwenyezi Mungu, humpa amtakaye, na Mwenyezi Mungu ni Mwenye wasaa, Mwenye kujua.” (5:54-56).

Hafidh: Inashangaza kwamba unajaribu kuhusisha aya hii na Ali. Hii inazungumzia wau- mini ambao wanazo sifa hizi na vipenzi wa Allah.

Muombezi: Ingekuwa vizuri kama ungeniuliza ni hoja gani ningeweza kutoa kuunga mkono maneno yangu. Jibu langu ni kwamba kama aya hii ingeteremshwa katika kuwasifu waumini, wasingekimbia kamwe kutoka uwanja wa mapambano. Hafidh: Je, ni haki kuwalaumu waumini na masahaba wa Mtume (lawama) ya kukimbia kutoka kwenye hatari? Watu hawa walipigana kishujaa katika vita.

Muombezi: Sio mimi niliyewaita “Wakimbiaji.” Historia inawaonyesha kama hivyo. Pengine umesahau kwamba katika vita vya Uhud na Hunain waumini wote na masahaba kwa ujumla, pamoja na masahaba wakubwa wa Mtume, walitafuta usalama kwa kukimbia.

Kama ilivyosimuliwa na Tabrini na wengine, wao walimuacha Mtume peke yake kati ya makafiri. Je, inawezekana kwamba wale waliogeuka na kuwapa maadui migongo wakimuacha Mtume peke yake kuwakabili maadui walikuwa wapenzi wa Allah na Mtume Wake?

Siko peke yangu katika kudai kwamba Aya hii iko katika kumsifu Ali. Abu Ishaq Imam Ahmad Tha’labi, ambaye mnamchukulia kama mkubwa wa wasimuliaji wenu wa Hadith, anaandika katika kitabu chake “Kashfu’l-Bayan” kwamba aya hii imeteremshwa katika kumsifu Ali kwa sababu hakuna mtu mwingine aliyekuwa na sifa zilizotajwa ndani yake.

Hakuna mwanahistoria - wa kwetu au wa nje - ambaye ameandika kwamba katika vita 36 vilivyopiganwa na Mtume, Ali hakuserereka kamwe hata katika moja. Katika vita vya Uhud, wakati masahaba wengine wote walipokimbia, na jeshi la adui lenye askari 5000 likawashambulia Waislamu, mtu pekee aliyebakia kwenye sehemu yake mpaka ushindi ulipopatikana alikuwa ni Ali.

Ingawa alijeruhiwa sehemu mbalimbali na kuvuja damu kwa wingi, aliwakusanya wale ambao walikuwa wamekimbia na kuendelea kupigana mpaka ushindi ulipopatikana.

Hafidh: Huna aibu kuhusisha “kukimbia” kwa masahaba wakubwa? Masahaba wote kwa ujumla na hasa Abu Bakr na Umar kwa ushujaa walimzunguuka Mtume na kumlinda.

Muombezi: Hukujifunza historia kwa uangalifu. Kwa ujumla, wanahistoria wameandika kwamba, katika vita vya Uhud Hunain na Khaibar masahaba wote walikimbia. Nimekueleza kuhusu Khaibar.

Amma kuhusu Hunain, Hamid katika “Jam-e-Banu’s- Sahihain” na Halabi katika “Siratu’l-Halabiyya”, Jz. 3, uk. 123, anasema kwamba masahaba wote walikimbia isipokuwa wanne: Ali na Abbas walikuwa mbele ya Mtume, Abu Sufyan Bin Harith alishika hatamu za farasi wa Mtume, na Abdullah Bin Mas’ud alisimama upande wake wa kushoto. Kukimbia kwa Waislamu huko Uhud hakukukataliwa na mtu yeyote.

Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’t-Talib” Sura ya 27, kwa vyanzo vyake mwenyewe, anamnukuu Abdullah Bin Mas’ud akisema kwamba Mtume amesema: “Wakati wowote Ali anapopelekwa peke yake katika pambano, nilimuona Jibril upande wake wa kulia, Mikael upande wake wa kushoto, na wingu likimfunika kutoka juu mpaka Allah Alipomfanya mshindi.”

Imam Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i anasimulia hadith 202 katika kitabu chake “Khasa’is-e- Alawi” kwamba Imam Hasan, akiwa amevaa kilemba cheusi alikuja kwa watu na akasimulia sifa za baba yake, akisema kwamba katika vita vya Khaibar, wakati Ali alipokwenda kuelekea ile ngome, “Jibril alikuwa akipigana upande wake wa kulia na Mikael upande wake wa kushoto.

Alimkabili adui kwa ushujaa mkubwa mpaka alipopata ushindi na akawa anastahiki mapenzi ya Allah.”

Ali Alikuwa Mwenye Kupendwa Na Allah Na Mtukufu Mtume (S.A.W.W.).

Katika Aya hii Allah anasema kwamba Yeye anawapenda wale ambao wana sifa hizi na kwamba wao pia wanampenda Yeye. Sifa hii ya kupendwa na Allah ni ya kipekee kwa Ali. Kuna ushahidi mwingi sana wenye kuunga mkono mtazamo huu. Miongoni mwa hadithi nyingi zinazohusiana na jambo hili ni ile inayosimuliwa na Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’t-Talib”, Sura ya 7.

Anasimulia kupitia vyanzo vyake mwenyewe, kutoka kwa Abdullah ibn Abbas, ambaye amesema kwamba, siku moja alikuwa amekaa na baba yake, Abbas mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati Ali alipoingia hapo na kumsalimia. Mtume akasimama, akamchukua mikononi mwake, akambusu katikati ya macho yake na akamfanya akae upande wake wa kulia. Kisha Abbas akamuuliza Mtume kama anampenda Ali. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu, “Ewe ami yangu mheshimika! Wallahi, Allah anampenda zaidi kuliko ninavyompenda mimi.”

Hadith Ya Bendera Katika Ushindi Wa Khaibar.

Uthibitisho wenye nguvu wa Ali kupendwa na Allah, na wa ushujaa wake katika uwanja wa vita, ni “Hadith-e-Rayat” (Hadith ya Bendera) ambayo ni sehemu ya mkusanyiko wenu wa Hadith. Hakuna hata mmoja wa Maulamaa wenu mashuhuri aliyeikataa.

Nawab: Ni nini Hadith-e-Rayat? Tafadhali kama ikiwezekana inukuu pamoja na vyanzo vyake.

Muombezi: Maulamaa na wanahistoria mashuhuri wa madhehebu hizi mbili (Shia na Sunni) wamesimulia “Hadith-e-Rayat.” Kwa mfano, Muhammad Bin Isma’il Bukhari katika Sahih yake Jz. 2 ‘Kitabu’l-Jihad Wa’s-Siyar,’ Sura Du’au’n-Nabi, vilevile katika Jz.

3 ‘Kitabu’l-Maghazi’, Sura ya Ghazawa-e-Khaibar. Muslim Bin Hajjaj katika Sahih yake, Jz. 2, uk. 324; Imam Abdu’r-Rahman Nisa’i katika “Khasa’isu’l-Alawi” Tirmidh katika “Sunan” yake; Ibn Hajar Asqalani katika “Isaba”, Jz. 2, uk. 508; Muhaddith-e-Sham kati- ka “Ta’rikh”; Ahmad bin Hanbal katika “Musnad”; Ibn Maja Qazwini katika “Sunan” yake; Sheikh Sulayman Balkh Hanafi katika “Yanabiu’l- Mawadda” Sura ya 6; Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira”; Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Matalibu’s-Su’ul”; Hafidh Abu Nu’aim Isfani katika “Hilyatu’l-Auliya”; Abu Qasim Tibran katika “Ausat” na Abu Qasim Husain bin Muhammad (Raghib Isfahani) katika “Muhadhiratu’l-Uda-ba” Jz. 2, uk. 212. Kwa ufupi, kwa hakika karibu wanahistoria wenu wote na Muhadathina wameandika hadith hii, hivyo kwamba Hakim anasema: “Hadith hii imefikia hatua ya makubaliano ya pamoja.” Tabrini anasema: “Ushindi wa Ali katika Khaibar unathibitish- wa na umoja wake.”

Wakati jeshi la Waislamu lilipoizingira ngome ya Khaibar, lilishindwa mara tatu chini ya uongozi wa Abu Bakr na Umar, na wakakimbia. Masahaba walivunjika moyo sana. Ili kuwatia moyo masahaba Mtume alitamka kwamba Khaibar itatekwa. Alisema: “Kwa jina la Allah, kesho nitampa bendera mtu ambaye atarudi na ushindi. Ni mtu ambaye husham- bulia kwa kurudia rudia na kamwe haondoki kwenye uwanja wa mapambano na kamwe harudi nyuma mpaka apate ushindi. Yeye anampenda Allah na Mtume Wake, na Allah na Mtume Wake, wanampenda yeye.” Usiku ule masahaba hawakuweza kulala, wakifikiria ni nani angepewa upendeleo huu maalum. Asubuhi, kila mmoja alivaa nguo za kijeshi na wakajitokeza mbele ya Mtume. Mtume akauliza: “Yuko wapi ndugu yangu na mtoto wa ami yangu, Ali Bin Abu Talib?” Walimwambia: “Ewe Mtume wa Allah, yeye anaumwa na macho sana kiasi kwamba hawezi hata kusogea.” Mtume akamtuma Salman amuite Ali. Salman akamshika Ali mkono akampeleka kwa Mtume.

Alimsalimia Mtume na baada ya kumrudishia salaam, Mtume akamuuliza, “una hali gani Ewe Abu’l- Hasan?” Akajibu, “Yote ni kheri kwa baraka za Allah. Naumwa kichwa na maumivu makali katika macho kiasi kwamba siwezi kuona chochote.” Mtume alimuomba aje karibu. Wakati Ali aliposogea karibu, Mtume aliweka mate ya kinywa chake mwenyewe kwenye macho ya Ali na akamuombea. Punde tu macho yake yakawa meupe na maumivu yake yakatoweka kabisa. Akampa Ali bendera ya ushindi.

Ali alielekea kwenye ngome za Khaibar, akapigana dhidi ya Mayahudi, akauwa wanajeshi wao mashujaa kama vile Marhab, Harith, Hisham na Alqama, na akazishinda ngome za Khaibar zilizokuwa hazishindiki.

Ibn Sabbagh Malik katika “Fusulu’l-Muhimma” uk. 21, amenukuu taarifa hii kutoka vitabu sita vya hadith, ambapo Muhammad bin Yusufu Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’l-Talib” Sura ya 14, baada ya kuisimulia hadithi hii anasema kwamba mtunga mashairi mkuu wa Mtume, Hassan bin Thabit, alikuwepo wakati wa tukio hili. Alitunga mashairi kumsifu Ali:

“Ali alikuwa akiumwa macho. Kwa sababu kulikuwa hakuna tabibu, Mtume alimtibia kwa mate yake mwenyewe. Hivyo wote muuguzi na mgonjwa walibarikiwa. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:‘Leo nitampa Bendera mpanda farasi aliye hodari mno, shujaa na muungwana, mwenzi wangu katika mapambano. Anampenda Allah na Allah anampenda; hivyo kupitia kwake Yeye Allah atatufanya tuzishinde ngome.’ Baada ya hili, akiwaacha wote pembeni, alimchagua Ali na akamfanya mrithi wake.”

Ibn Sabbagh Maliki anasimulia kutoka “Sahih Muslim” kwamba Umar bin Khattab amesema: “Kamwe sijatamani kuishika bendera lakini siku ile nilikuwa na hamu kubwa nayo.

Nilirudia rudia kujifanya nionekane mbele ya Mtume, nikitamani kwamba huenda pengine akaniita na kwamba nikaweza kubarikiwa heshima hii. Lakini alikuwa ni Ali ambaye ali- itwa na Mtume na utukufu ukaenda kwake.” Sibt Ibn Jauzi ameandika riwaya hii katika kitabu chake “Tadhkira”, uk. 15, na Imam Abdur-Rahman Ahmad Bin Ali Nisa’i katika “Khasa’isu’l-Alawi”, baada ya kusimulia hadithi kumi na mbili juu ya habari ya Ali kushika bendera kule Khaibar, ananukuu riwaya hiyo katika hadith ya kumi na nane kuhusu matumaini ya Umar kuipata bendera.

Vilevile Jalalu’d-Din Suyuti katika kitabu chake “Ta’rikhu’l-Khulafa”, Ibn Hajar Makki, katika “Sawa’iq” na Ibn Shirwaini katika kitabu chake “Firdausu’l-Akbar” anasimulia kwamba Umar Bin Khattab amesema: “Ali amejaaliwa mambo matatu na kama ninge- likuwa na moja tu ningelipendelea kuliko ngamia wote walioko katika miliki yangu:- Ndoa ya Ali na Fatima; kukaa kwake msikitini katika hali yoyote na hii haikuruhusiwa kwa yeyote isipokuwa Ali, na kushika kwake bendera katika vita vya Khaibar.”

Hoja yangu, kutegemea juu ya riwaya za Muhadithina wenu, inathibitisha kwamba maneno katika Aya - “Yeye (Allah) anawapenda na wao vilevile wanampenda Yeye” - yanahumhusu Ali. Muhammad Bin Yusufu Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’t-Talib”, Sura ya 13, anasimulia kwamba Mtume amesema: “Kama mtu anataka kumtazama Adam, Nuh na Ibrahim, na amtazame Ali.” Anasema kwamba, Ali ndiye yule anayesemwa na Allah kati- ka Qur’ani Tukufu: “Na wale ambao wako pamoja naye ni wakali dhidi ya makafiri, (na) wenye kuhurumiana wenyewe kwa wenyewe.” (48:29).

Ama kwa kauli yako kwamba kifungu cha maneno katika aya hii “kuhurumiana wenyewe kwa wenyewe” kinamhusu Uthman na huonyesha nafasi yake kama Khalifa wa tatu, hii haiungwi mkono na ushahidi wa kihistoria. Kwa kweli, tabia yake ilikuwa ni kinyume chake kabisa. Kuna hoja nyingi zenye kuthibitisha jambo hili, lakini nitasimama hapa. Mambo ambayo yangesemwa yanaweza kuchochea uhasama.

Hafidh: Kama utaishia kwenye rejea sahihi tu, hakuna sababu kwa nini tuchukizwe. Muombezi: Nitataja tu baadhi ya hizo.

Tabia Ya Uthman Na Namna Ya Maisha Ikilingan- Ishwa Na Ile Ya Abu Bakr

Na Umar.

Ibn Khaldun, Ibn Khallikan, Ibn A’sam Kufi (imeandikwa vilevile katika Siha-e-Sitta), Mas’ud katika “Muruju’dh-Dhahab” Jz. 1, uk. 435, Ibn Hadid katika “Sharhe Nahju’l- Balagha Jz. 1, na wengine katika Maulamaa wenu wanathibitisha kwamba wakati Uthman Bin Affan alipokuwa Khalifa, alikkwenda kinyume na mifano iliyowekwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na vilevile dhidi ya mwendo wa Abu Bakr na Umar. Madhehebu zote zinakubaliana kwamba katika Kamati ya Ushauri (Shura) ambayo kwayo alichaguliwa kuwa Khalifa, Abdur-Rahman Bin Auf alimlisha kiapo cha kutegemea juu ya kitabu cha Allah, Suna ya Mtume, na mwendo wa Abu Bakr na Umar.

Moja ya masharti ya kiapo chake ilikuwa kwamba Uthman hatawaacha Bani Umayya kuingilia (mambo ya uongozi) wala hangewapa mamlaka yoyote. Lakini nafasi yake (ya uongozi) ilipoimarika aliyavunja masharti haya. Kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu na hadith za kuaminika, kuvunja makubaliano (Mkataba) ni dhambi kubwa. Maulamaa wenu wenyewe wanasema kwamba Khalifa Uthman alivunja ahadi yake. Katika Ukhalifa wake wote alitenda kinyume na mwendo wa Abu Bakr na Umar. Aliwapa Bani Ummaya Mamlaka kamili juu ya maisha ya watu na mali zao.

Utajiri Wa Khalifa Uthman.

Hafidh: Ni katika njia gani alitenda dhidi ya mafunzo na matendo ya Mtume na mwendo wa Abu Bakr na Umar?

Muombezi: Muhadith mashuhuri, Mas’ud katika kitabu chake “Muruju’dh-Dhahab” Jz. 1, uk. 433, na wanahistoria wengine wameandika kwamba Uthman alijenga nyumba ya kipekee ya mawe yenye milango iliyotengenezwa kwa mti wa msandali. Alijikusanyia utajiri mkubwa, ambao aliutoa kiufujaji kwa Bani Umayya na wengine. Kwa mfano kodi ya kidini (Khums) kutoka Armania, ambayo ilitekwa katika kipindi chake ilitolewa kwa mlaaniwa Marwan bila idhini yoyote ya kidini.

Vile vile alimpa dirham 100,000 kutoka Baitul-mal (hazina ya Umma). Alimpa Abdullah Bin Khalid dirham 400,000, dirham 100,000 kwa Hakam Bin Abi’l-Aas, ambaye alilaaniwa na kuhamishwa na Mtume, na dirham 200,000 kwa Abu Sufyani (kama ilivyoandikwa na Ibn Abi’l-Hadid katika “Sherhe Nahju’l- Balagha.”, Jz. 1, uk. 68).

Katika siku aliyouawa, mali yake binafsi ilifikia dinari 150,000 na dirham milioni 20 taslimu. Alimiliki mali huko Wadiu’l-Qura na Hunain yenye thamani ya dinari 100,000 na kundi kubwa la ng’ombe, kondoo na ngamia. Kama matokeo ya matendo yake, Bani Umayya walio mbele walilimbikiza utajiri mkubwa utokanao na juhudi za watu.

Kwa Khalifa wa Uislam kujikusanyia utajiri kama huo wakati watu wengi wanateseka kwa njaa kwa hakika ilikuwa ni kosa. Aidha tabia hii ilikuwa inapingana kabisa na mwenendo wa masahaba wenzake, Abu Bakr na Umar. Uthman aliahidi katika Kamati ya Ushauri (Shura) kwamba angefuata nyayo zao. Mas’ud katika kitabu chake “Muruju’dh-Dhahab” anasema kuhusu Khalifa Uthman kwamba, wakati Khalifa Umar alipokwenda na mwanae Abdullah kuhiji, matumizi yao katika safari yao ya kwenda na kurudi yalikuwa dinari 16.

Alimwambia mwanae kwamba wamekuwa wafujaji. Kama utalinganisha mwendo wa ulaji mdogo wa Umar na matumizi ya kifujaji ya Uthman, utakubali kwamba mwendo wa maisha ya Uthman ulikuwa kinyume na kiapo chake katika ile Kamati ya Ushauri.

Khalifa Uthuman Aliwapa Moyo Watenda Maovu Miongoni Mwa Bani Umayya.

Uthmani vilevile aliwapa Bani Umayya mamlaka juu ya maisha na heshima za watu. Hatimaye, machafuko yalijitokeza katika ardhi za Waislamu. Aliwachagua watu wake anao wapendelea katika nafasi za juu kinyume na matakwa ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abu Bakr na Umar. Kwa mfano alimpa nafasi za juu ami yake, Hakam Bin Aas, mtoto wake, Marwan ambao wote walihamishwa na kulaaniwa na Mtume.

Hafidh: Unaweza ukathibitisha kwamba walilaaniwa?

Muombezi: Kuna njia mbili za kuthibitisha kwamba walilaaniwa. Allah aliwaita Bani Umayya “Mti uliolaaniwa” katika Qur’ani Tukufu (17:60). Imam Fakhuru’d-Din Razi, Tabari, Qartabi, Nishapuri, Suyuti, Shawkani, Alusi, Ibn Abi Hatim, Khatib Baghdad, Ibn Mardawaih, Hakim, Maqrizi, Baihaqi na wengine katika maulamaa wenu wanasimulia kutoka Ibn Abbas kwamba “Mti uliolaaniwa” katika Qu’an unahusu kabila la Umayya. Katika ndoto, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliona nyani wakipanda na kushuka katika mimbari yake (na kufukuza watu kutoka Msikitini).

Alipoamka, Malaika Jibril akateremsha Aya hii na kumueleza Mtume kwamba nyani wale walikuwa Bani Umayya, ambao watanyang’anya Ukhalifa wake baada yake. Sehemu yake ya kusalia na mimbari vitabakia katika mamlaka yao kwa miezi elfu. Imam Fakhni’d-Din Razi anasimulia kutoka Ibn Abbas kwamba Mtume alitaja jina la Hakam Bin Aas. Kwa hiyo amelaaniwa kwa vile ana- tokana na “Mti uliolaaniwa.”

Kuna Hadith nyingi kutoka vyanzo vya Sunni kuhusu kulaaniwa kwao.Hakim Nishapuri, katika “Mustadrak” Jz. 4, Uk. 437 na Ibn Hajar Makki katika “Sawa’iq-e-Muhriqa”, ananukuu kutoka kwa Hakim hadith ifuatayo kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). “Hakika muda mfupi tu familiya yangu itatawanyishwa na kuuawa na Umma wangu. Bani Umayya, Bani Mughira, na Bani Makhzum ni makatili zaidi katika maadui zetu.” Mtume Akasema kuhusu Marwan, akiwa mtoto wakati huo, “Huyu ni mjusi, mtoto wa mjusi, mwenye kulaaniwa, mtoto wa aliyelaaniwa.”

Ibn Hajar anaelezea kutoka kwa Umar bin Murratu’l-Jihni, Halabi katika “Siratu’l- Halabiyya”, Jz. 1, uk. 337; Baladhuri katika “Ansab”, Jz. 5, uk. 126; Sulayman Balkhi katika “Yanabiu’l-Mawadda”; Hakim katika “Mustadrak”, Jz. 4, uk. 481; Damiri katika “Hayatu’l-Haiwan”, J. 2, uk. 291; Ibn Asakir katika kitabu chake cha “Ta’rikh”; Imamu’l- Haram Muhyi’d-Din Tabari katika “Dhakha’iru’l-Uqba” na wengine wamesimulia kutoka kwa Umar bin Murratul-Jihni kwamba Hakam Bin Aas alitaka mazungumzo na Mtume. Mtume alipoitambua sauti yake, akasema: “Muacheni aingie ndani. Laana iwe juu yake na juu ya kizazi chake, isipokuwa wale ambao wanaamini, na watakuwa wachache.”

Imam Fakhri’d-Din Razi, katika kitabu chake “Tafsir-e-Kabir”, Jz. 5, akiandika kuhusu Aya ya “Mti uliolaaniwa...... ” na namna yake, anarejea kwenye kauli ya Aisha ambaye alisema kumuambia Marwan: “Allah alimlaani baba yako wakati upo kwenye mbegu zake za uzazi; hivyo na wewe vilevile ni sehemu yake yule ambaye amelaaniwa na Allah.”

Allama Mas’ud, anasema katika kitabu chake “Muruju’dh-Dhahab”, Jz. 1, uk. 435, kwamba Marwan bin Hakam alilaaniwa na kuhamishwa na Mtume. Alihamishwa kutoka Madina. Hakuruhusiwa kuingia Madina wakati wa Ukhalifa wa Abu Bakr na Umar, lakini Uthman alipokuwa Khalifa, alitenda kinyume cha mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abu Bakr, na Umar na akamruhusu kuingia Madina. Alimuweka karibu sana naye mwenyewe pamoja na Bani Umayya wote na akawafanyia upendeleo.

Nawab: Hakam Bin Abil-Aas alikuwa ni nani, na kwanini alihamishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Muombezi: Hakam Bin Aas alikuwa ni ami yake Khalifa Uthman. Kwa mujibu wa Tabari, Ibn Athir, na Baladhuri, ambaye anaandika katika “Ansab”, Jz. 5, uk. 17, yeye alikuwa ni jirani yake Mtume Zama za Jahiliyya. Alimtukana Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hususan baada ya tangazo lake la Utume. Alitembea nyuma ya Mtume na kumdhihaki kwa kumuigiza miondoko ya utembeaji wake.

Hata wakati wa Sala, alikuwa akimyooshea kidole kwa dharau. Baada ya kulaaniwa na Mtume, alibakia katika hali ya kupooza wakati wote na hatimaye akapoteza hali ya utimamu akili. Baada ya kutekwa Makka, alikuja Madina na inavyoonekana aliingia Uislamu, lakini mara kwa mara alimtukana Mtume.

Wakati alipokwenda nyumbani kwa Mtume, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mara moja alitoka nje ya nyumba yake na akasema “Mtu yeyote asiombe msamaha kwa niaba yake. Sasa yeye na watoto wake, Marwan na wengine wanapaswa waondoke Madina.” Kwa hiyo, mara moja Waislamu wakamtoa na kumfukuzia Ta’if. Wakati wa kipindi cha Abu Bakr na Umar, Uthman alimsaidia, akisema kwamba alikuwa ni ami yake na kwamba inapaswa aruhusiwe kurudi Madina. Lakini hawa wengine hawakulikubali shauri hili, wakisema kwamba kwa vile alilaaniwa na kuhamishwa na Mtume hawatamruhusu kurudi.

Wakati Uthman alipokuwa Khalifa, aliwarudisha wote. Ingawa watu wengi walilipinga shauri hili; Uthman alionyesha upendeleo maalum kwa jamaa zake na wengine anaowapenda. Alimfanya Marwan kuwa msaidizi wake na Afisa Mkuu wa Baraza lake. Alijikusanyia karibu yake waovu wengi wa kabila la Umayya na akawateua kushika nafasi za juu (katika serikali). Matokea yake ni kwamba, kwa mujibu wa utabiri wa Umar, wao ndio walihusika na janga lililompata Uthman.

Miongoni mwa watu walioteuliwa na Uthman alikuwa Walid bin Aqaba bin Abi Mu’ith ambaye alipelekwa Kufa kuwa Gavana. Kwa mujibu wa riwaya ya Mas’ud katika “Muruju’dh-Dhahab”, Jz. 1, Mtume alisema kuhusu Walid: “Hakika yeye ni mmoja wa wale watakaokwenda motoni.” Alijitumbukiza waziwazi kabisa katika matendo maovu. Kwa mujibu wa maelezo ya Mas’ud katika “Muruju’dh- Dhahab”, Abdu’l-Fida katika “Ta’rikh” yake, Suyuti katika “Ta’rikhu’l-Khulafa”, uk. 104, Abu’l-Faraj katika “Aghani” Jz. 4, uk. 128, Imam Ahmad bin Hanbal katika “Musnad”, Jz. 1, uk. 42 Yaqubi katika “Ta’rikh” yake Jz. 2, uk. 142; Ibn Athir vilevile katika Usudul- Uqba, Jz. 5, uk. 91 na wengine walisema kwamba, wakati wa ugavana wake huko Kufa, Walid alipitisha usiku mzima akifanya ufuska. Alikuja msikitini kwa ajili ya Sala ya Alfajiri akiwa amelewa na akasalisha rakaa nne za Sala ya asubuhi (badala ya mbili) kisha akawageukia watu na kusema “Uzuri ulioje wa asubuhi hii! Ningetaka kuendeleza Sala hii kama mutaridhia”.

Baadhi wanasema kwamba alitapika kwenye kibla ya msikiti kitendo ambacho kilileta maudhi makubwa kwa watu ambao walilalamika kwa Khalifa Uthman. Mmoja wa watu hawa wanaojulikana sana ni Mu’awiya, ambaye alifanywa kuwa Gavana wa Syria. Walid aliondolewa na badala yake akateuliwa Sa’id Bin Aas kama Gavana wa Kufa. Wakati watu walizipogundua sera za Uthman, sera zilizo kinyume na mafunzo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), walighadhibika. Walichukuwa hatua ambazo hatimae zilisabisha matokeo yake mabaya kama hayo. Uthman alihusika na kifo chake mwenyewe kwa sababu hakufikiria athari za matendo yake. Alipuuza ushauri wa Ali na akawa amepotezwa na wadanganyifu wenye kujipendekeza. Ibn Abi’l-Hadid ananukuu mazungumzo kati ya Umar na Ibn Abbas katika Sherhe ya “Nah’ju’l-Balagha”, Jz. 3, uk. 106. Khalifa Umar alisema kitu kuhusu kila mmoja wa wajumbe sita wa Kamati ya Ushauri na akaonyesha udhaifu wao.

Wakati jina la Uthmani lilipotajwa, baada ya kushusha pumzi mara tatu, Umar akasema kwamba, “Kama Ukhalifa utamfikia Uthman atawaweka watoto wa Abi Mu’it (Bani Umayya) juu ya watu. Kisha Waarabu watasimama na kuasi dhidi yake na kumuua.’

Ibn Abi’l-Hadid anakubaliana na uchambuzi wa Umar. Wakati Uthman alipokuwa Khalifa aliwakusanya karibu yake Bani Umayya. Aliwateuwa kuwa magavana na wakati walipoyachezea vibaya mamlaka yao, alifumba macho. Khalifa Uthman hakutaka hata kujinasua mwenyewe kutokana na Marwan.Watu wakichemka kwa kutoridhika, waliasi dhidi yake na mwishowe wakamuua.

Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Aliwalaani Abu Sufyan, Mu’awiya Na Mtoto

Wake Yazid.

Itasaidia sana kama utasoma kitabu maarufu cha Historia cha Jarir Tabari, mmoja wa maulamaa wenu wakubwa, ambaye ameandika: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuona Abu Sufyani akiwa amepanda punda. Mu’awiya alikuwa anaivuta kwa mbele, na mtoto wake Yazid, alikuwa anaisukuma kwa nyuma. Mtume akasema: “Laana iwe juu ya mpan- daji, mvutaji na msukumaji.” Maulamaa wenu mashuhuri, kama Tabari na Ibn A’sam Kufi wamemuona Khalifa Uthman kuwa ni mwenye makosa kwa kutomuua Abu Sufyan wakati alipoukana Uislamu, Wahyi (ufunuo), na kuwepo kwa Jibril.

Baada ya kumkemea Abu Sufyan kidogo, Uthman akalitupa kando suala hili. Nitawaomba vilevile muangalie Khutba ya 163 ya “Nahju’l-Balagha” na simulizi ambayo Ibn Abi’l-Hadid katika Sherhe yake ya “Nahju’l-Balagha” Jz. 2, (iliyochapishwa Misr) uk. 582, ananukuu kutoka “Tar’rikh-e-Kabir”, ya Tabari kwamba baadhi ya masahaba katika majimbo mbalimbali waliandika barua wakishawishi watu kutangaza vita vya Jihad, ili kujilinda kutokana na uonevu wa kikatili wa Uthman. Katika mwaka 34 A.H. watu wenye malalamiko dhidi ya maofisa walioteuliwa na Uthman walikuja Madina kwa Ali na wakamuomba aingilie kati. Uthman Hakukubali Ushauri Wa Ali.

Ali alikwenda kwa Uthman na akamuonya kuhusu matokeo ya kutisha ya kuendelea na sera zake hizo. Ali alisema, “Nakuambia kwa ajili ya Allah, usije ukajifanya wewe mwenyewe kuwa ni kiongozi wa umma huu aliyeuawa. Imesemekana kwamba kiongozi mmoja wa umma huu atauwawa, ambapo baada yake milango ya umwagaji damu na mauaji itabakia wazi mpaka Siku ya Kufufuliwa.”

Lakini Marwan na masahaba wa ki-Bani Umayya walipuuza ushauri wa Ali. Baada ya Ali kuondoka, Uthman aliamuru watu kukusanyika Msikitini. Alikwenda kwenye mimbari na badala ya kuwatuliza watu, aliwachokoza zaidi. Matokeo yakawa kama Khalifa Umar alivyotabiri. Uthman akauawa na waasi. Tofauti na Abu Bakr na Umar ambao walifuata ushauri wa Ali, Uthman alipuuza onyo lake na matokeo yake yakampata yaliyompata.

Uthman Aliwapiga Masahaba Wa Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Bila Huruma

Aidha, Uthman aliwapiga Masahaba ambao walipinga uonevu wake. Miongoni mwao alikuwa ni Abdulla Bin Mas’ud, ambaye alikuwa Hafidhi, Qari (msomaji Qur’ani) Mtunza Hazina ya Umma, Mwaandishi ambaye aliandika Aya zilizoteremshwa, na mmoja wa masahaba wakubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aliheshimiwa sana na Abu Bakr na Umar, ambao wote walichukuwa ushauri kutoka kwake. Ibn Khaldun katika Ta’rikh yake ameeleza kwamba, Khalifa Umar alisisitiza kwamba Abdullah abakie naye kwa sababu alikuwa na elimu kamili ya Qur’ani Tukufu na kwa sababu Mtume alimsifia sana. Ibn Abi’l-Hadid na wengine wameandika jambo hilo hilo.

Maulamaa wenu wanakubali kwamba wakati Uthman alipokusudia kukusanya Qur’ani Tukufu, alichukuwa nakala zote kutoka kwa waandishi. Alidai vilevile nakala ya Qur’ani Tukufu kutoka kwa Abdullah bin Mas’ud. Abdullah hakumpa nakala yake hiyo. Uthman alikwenda mwenyewe nyumbani kwake na akaichukuwa hiyo nakala ya Qur’ani Tukufu kutoka kwake kwa nguvu.

Baadae wakati Abdullah alipogudua kwamba, kama ilivyofanywa kwa nakala nyingine za Qur’ani Tukufu, na nakala yake pia imechomwa moto, alihuzunika mno. Katika mikusanyiko ya kijamii na kidini alisimulia hadith za shutuma ambazo alizijua kuhusu Uthman. Wakati habari hizi zilipomfikia Uthman, aliamrisha watumwa wake, wakampiga sana kiasi kwamba meno yake yalivunjika na alibakia kitandani. Baada ya siku tatu alikufa kwa majeraha yake. Ibn Abi’l-Hadid anaandika kwa kina kuhusu ukweli huu kutoka Jz. 1, uk. 67 na 226 wa Sharh “Nahju’l-Balagha” (iliyochapishwa Misir) chini ya “Ta’n VI” na akaendelea kusema kwamba Uthman alikwenda kumuangalia Abdullah aliyekuwa anaumwa.

Walizungumza pamoja kwa muda. Uthman akasema, “Ewe Abdu’r-Rahman! Niombee msamaha kwa Allah.” Abdullah akasema, “Namuomba Allah achukue haki yangu kutoka kwako.” (yaani haki ifanyike). Wakati Abu Dharr, sahaba wa karibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alipohamishiwa Rabza, Abdullah alikwenda kumuaga.

Kwa sababu hii, Abdullah alipigwa viboko arubaini. Hivyo Abdullah akamsisitizia Ammar Yasir kwamba Uthman asikubaliwe kumsalia Abdulla Sala ya jeneza. Ammar Yasir alikubali, na baada ya kifo cha Abdullah, alisali Sala ya jeneza pamoja na kikundi cha masahaba. Uthman alipogundua mpango huu wa mazishi, alikuja kwenye kaburi la Abdullah na aka- muuliza Ammar kwanini alisali Sala ya jeneza. Akajibu kwamba alilazimika kufanya hivyo kwa sababu Abdullah aliusia hivyo.

Ammar Alipigwa Kwa Amri Ya Uthman.

Mfano mwingine wa ukatili wa Uthman ulikuwa ni kumpiga kwake Ammar Yasir. Maulamaa wa madhehebu zote wanasimulia kwamba wakati uonevu wa Bani Umayya ulipozidi, baadhi ya masahaba wa Mtume walimuandikia Uthman, wakimtaka awe na huruma.

Walisema kwamba, kama ataendelea kuwasaidia magavana wake hao makatili wa ki-Bani Umayya hatakuwa anaudhuru Uislamu tu, bali yeye mwenyewe pia atajitia katika matokeo mabaya sana. Walimtaka Ammar Yasir kufikisha kwa Uthman ile barua ya malalamiko kwa vile Uthman mwenyewe alikubali uadilifu wa Ammar. Walikuwa wamemsikia Uthman mara kwa mara akisema kwamba, Mtume amesema kwamba imani ilikuwa imechanganyika na nyama na damu ya Ammar. Hivyo Ammar aliichukua barua ile na kuipeleka kwa Uthman.

Wakati alipowasili, Uthman alimuuliza, “Je, una shughuli na mimi?” Akajibu , “Sina shughuli ya namna ya kibinafsi. Bali kikundi cha masahaba wa Mtume wameandika katika barua hii mapendekezo fulani na ushauri kwa ajili ya ustawi wako. Wameyatuma kwako kupitia kwangu.”

Baada ya kusoma misitari michache, Uthman akaitupa ile barua chini. Ammar akasema: “Ilikuwa sio vizuri kwako wewe kufanya hivyo. Barua kutoka kwa masahaba wa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) inastahiki heshima. Kwa nini umeitupa chini? Ingelikuwa vizuri kwako wewe kuisoma na kuijibu.”

“Unaongopa” Uthman alisema kwa sauti kali. Kisha akaamuru watumwa wake kumpiga, na Uthman mwenyewe akampiga teke la tumbo. Alianguka chini, akazimia; jamaa zake wakaja wakamchukua, wakampeleka kwenye nyumba ya Ummu’l-Mu’Minin Umm Salma (mmoja wa wake za Mtume). Kuanzia adhuhuri mpaka usiku wa manane alikuwa bado amezimia. Makabila ya Hudhail na Bani Makhzun waligeuka dhidi ya Uthman kwa sababu ya ukatili wake kwa Abdullah Bin Mas’ud na Ammar Yasir.

Uthman alikuwa katili vilevile kwa Jandab Bin Junada, anayejulikana kama Abu Dhar Ghifari, mmoja wa masahaba karibu mno wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na mtu mwenye elimu. Muhadithina wakubwa na wanahistoria wa madhehebu zote wamesimulia kwamba mzee huyu wa miaka tisini alihamishwa isivyo halali kutoka sehemu hii kwenda sehemu nyingine kwa fedheha kubwa - kutoka Madina kwenda Syria, kutoka Syria kwenda Madina tena, kisha kutoka Madina kwenda kwenye Jangwa la Rabza. Alipanda ngamia asiye na matandiko akifuatana na binti yake tu. Alikufa katika (jangwa) la Rabza katika hali ya umasikini na ya kutelekezwa. sMaulamaa na wanahistoria wenu wakubwa, pamoja na Ibn Sa’d katika “Tabaqat”, Jz. 4, uk. 168, Bukhari katika “Sahih” yake, mlango wa “Kitab-e-Zaka”; Ibn Abi’l-Hadid kati- ka Sherhe yake ya “Nahju’l-Balagha”, Jz. 1, uk. 240 na Jz. 2, uk. 375 – 87, Yaqubi katika kitabu chake cha Ta’rikh Jz. 2, uk. 148; Abu’l-Hasan Ali Bin Husain Mas’ud, muhadithi- na na mwanahistoria mashuhuri wa Karne ya Nne katika kitabu chake “Muruju’dh- Dhahab”, 1, uk. 438; na wengine wengi wamesimulia ukatili wa Uthman.

Imeelezwa kwa mapana jinsi gani alivyomfanyia ubaya Abu Dharr mtu mwenye moyo safi, mtu aliyepend- wa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na vilevile jinsi gani Abdullah Bin Mas’ud, Hafidh na mwandishi wa Wahyi, alivyopigwa viboko arobaini kwa sababu alikwenda kumuaga Abu Dharr Ghifari. Hali ya ufidhuli wa aina hiyo hiyo ulionyeshwa kwa Ali kwa sababu hizo hizo.

Hafidh: Kama Abu Dharr alipatishwa mateso, ni kwa sababu ya maofisa wakorofi. Khalifa Uthman, ambaye alikuwa mpole sana na mwenye moyo laini, alikuwa hana habari na matukio haya.

Muombezi: Utetezi wako kwa Khalifa Uthman ni kinyume na ukweli. Mateso aliyopata Abu Dharr ilikuwa ni kwa ajili ya amri za wazi za Uthman mwenyewe. Kuthibitisha ukweli huu, anachohitaji mtu ni kurejea kwa Maulamaa wenu tu.

Kwa mfano unaweza ukaangalia “Nihaya” kitabu cha Ibn Athir, Jz.1, na kitabu chake, “Ta’rikh-e- Yaqubi” na hususan uk. 241 wa Jz. 1, ya “Sharhe Nahju’l-Balagha” cha Ibn Abi’l-Hadid. Wanachuoni hawa wameinakili barua ya Uthman iendayo kwa Mu’awiyya. Wakati Mu’awiyya alipopeleka taarida yenye uovu dhidi ya Abu Dharr kutoka Syria, Uthman alimuandikia hivi:

“Mlete Jundab (Abu Dharr) kwangu juu ya ngamia asiye na matandiko, peke yake, na mtu katili atakayemswaga ngamia huyo mchana na usiku.”

Wakati alipofika Madina, miguu yake Abu Dharr ilikuwa imechubuka na kutoa damu. Na bado Maulamaa wenu wamesimulia hadith isemayo kwamba Abu Dharr alitajwa makhususi kabisa na Mtume kama mtu ambaye kila mwanadamu lazima ampende. Hafidh Abu Nu’aim Isfahani katika “Hilyatu’l-Auliya”, Jz. 1, uk. 172; Ibn Maja Qazwini katika “Sunan” yake Jz. 1, uk. 66; Sheikh Sulayman Balkhi Shafi’i katika “Yanabiu’l- Mawadda”, Sura ya 59, akisimulia hadithi ya tano kati ya hadith arobaini zilizoandikwa katika “Sawa’iq-Muhriqa” na Ibn Hajar Makki kama sahihi, zikiwa zimechukuliwa kutoka kwa Tirmidhi na Hakim, kama ilivyosimuliwa na Buraida, na yeye kutoka kwa baba yake; Ibn Hajar Asqalani katika “Isaba”, Jz. 3, uk. 455; Tirmidh katika “Sahihi” yake, Jz. 2, uk. 213; Ibn Abdi’l-Birr katika “Isti’ab”, Jz. 2, uk. 557; Hakim katika “Mustadrak”, Jz. 3 uk. 130; na Suyuti, katika “Jam’u’s-Saghir” wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:“Allah ameniamrisha mimi kuwapenda watu wanne; na amenijulisha kwamba Yeye pia anawapenda.” Watu wakasema “Ewe Mtume wa Allah tueleze majina yao.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema “Ni Ali, Abu Dharr, Miqdad, na Salman.” Je, haki itaruhusu kwamba watu kama hao wapendwao na Allah kutendewa ukatili hivyo na kuyaita matendo hayo kuwa ni huruma?

Hafidh: Historia imesimulia kwamba Abu Dharr alikuwa mtu mvurugaji. Aliendesha propaganda kali huko Syria yenye kumpendelea Ali, akawatanabahisha watu wa Syria juu ya cheo cha Ali, na akasema kwamba alikuwa amemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi wake.

Kwa sababu aliwaita wengine wanyang’anyi na akasema kwamba Ali alikuwa Khalifa wa haki aliyeteuliwa na Allah, Khalifa Uthman, ili kulinda umoja na kuepusha matatizo, alilazimika kumuita kutoka Syria (arudi Madina). Kama mtu anajaribu kusababisha fitna miongoni mwa watu, ni jukumu la Khalifa kumuondoa kutoka sehemu hiyo.

Muombezi: Kama mtu anasema kweli, ni haki kumhamisha na kumtesa kwa sababu anafanya hivyo? Je, Uislamu unaturuhusu kumlazimisha mtu mzee kupanda ngamia aliyekonda, asiye na matandiko, ikiswagwa kwa nguvu na mtumwa mwenye harara, bila kusimama kwa ajili ya kupumzika, hivyo kwamba anawasili mashukio yake akiwa amechubuka na kuvuja damu?

Je, hii inaonyesha upole na moyo wa wema? Mbali na hilo kama Uthman alitaka kudumisha umoja na kuepusha matatizo kwa nini asiwaondoe Bani Umayya wahalifu, kama Marwan, ambaye alilaaniwa na kuhamishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Walid mpotovu na fuska wa dhahiri (afanyaye maovu bila kuficha) ambaye alisalisha akiwa amelewa na ambaye alitapika kwenye kibla ya msikiti? Kwa nini asiwaondoe wanasiasa madhalimu kutoka kwenye serikali yake, watu ambao wamewaonea watu, ambao mwishowe wakaasi na kumuuwa Uthman.

Hafidh: Unawezaje kusema kwamba Abu Dharr alisema kweli? Unajuaje kwamba aliyosema yako katika misingi ya elimu iliyo sawa na kwamba hakubuni hadithi kwa jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Muombezi: Tunasema hivyo kwa sababu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alithibitisha ukweli wa Abu Dharr. Maulamaa wenu wenyewe wameandika kwamba Mtume alisema: “Abu Dharr miongoni mwa watu wangu ni kama Isa miongoni mwa Bani Isra’il katika ukweli, utii na Ucha Mungu.” Muhammad Bin Sa’d mmoja wa Maulamaa wa cheo cha juu na muhadithina wa madhehebu yenu, ndani ya “Tabaqat”, Jz. 4, uk. 167- 168; Ibn Abdu’l-Birr katika “Isti’ab”, Jz. 1, Sura ya Jundab, uk. 84; Tirmidh katika “Sahih” yake Jz. 2, uk. 221; Hakim katika “Mustadrak”, Jz. 3, uk. 342; Ibn Hajar katika “Isaba” Jz. 3, uk. 662; Muttaqi Hindi katika “Kanzu’l-Ummal”, Jz. 6, uk. 169; Imam Ahmad Bin Hanbal katika “Musnad” Jz. 2 uk.163 na 175; Ibn Abil’-Hadid katika “Sherhe Nahju’l- Balagha” Jz. 1, uk. 241; kutoka kwa Mahidi; Hafidh Abu Nu’aim Isfahani katika “Hilyatu’l-Auliya” na mwandishi wa “Lisanu’l-Arab”, juu ya vyanzo mbali mbali vya kutegemewa wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ardhi haikuzaa wala mbingu haikufunika mtu muaminifu zaidi kuliko Abu Dharr.”

Kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anathibitisha uaminifu wa mtu, tunaweza kuwa na uhakika kwamba mtu yule alisema kweli. Wala Allah hamuiti mtu mpenzi wake, yule ambaye ni muongo. Kama kungalikuwa na mfano mdogo tu wa Abu Dharr kusema uwongo, Maulamaa wa mwanzo wa madhehebu yenu wangeuandika kama walivyoandika kuhusu Abu Huraira na wengine. Mtume alithibitisha uaminifu wake na vilevile akatabiri mateso yake. Hafidh Abu Nu’aim Isfahani katika “Hilyatu’l Auliya”, Jz. 1 uk. 162, anasimulia kutoka vyanzo vyake mwenyewe kwamba Abu Dharr alisema kwamba alikuwa amesima- ma mbele ya Mtume wakati alipomuambia: “Wewe ni mcha-Mungu, mara tu baada yangu utapatwa na shida.”

Nikauliza:“Katika njia ya Allah? Akasema: “Ndio, katika njia ya Allah! Nikasema: “naikaribisha (naikubali) amri ya Allah!” Hakika shida aliyopata sahaba mtukufu Abu Dharr katika jangwa kwa amri ya Mu’awiyya, Uthman na jamaa zao Bani Umayya ilikuwa ni shida ile ile aliyotabiri Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hadith: “Masahaba Wote Ni Kama Nyota” Inamhusu Na Abu Dharr Vilevile.

Kwa kweli nashangaa kauli zako zenye kupingana zenyewe. Kwa upande mmoja unasimulia hadith kutoka kwa Mtume kwamba, “Masahaba wangu wote ni kama nyota, kama mkimfuata yeyote miongoni mwao mtaokolewa.”

Kwa upande mwingine, wakati mmoja wa Masahaba watukufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anateswa na kufa katika huzuni, wewe unamtetea mkosaji! Yakupasa ama upuuze maelezo ya maulamaa wenu, au ukubali sifa zilizotajwa katika aya iliyo katika mjadala kwamba hazihusiani na wale waliowatesa masahaba watukufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hafidh: Abu Dharr alichagua kwenda Rebza kwa hiari yake mwenyewe.

Muombezi: Maelezo kama hayo yanaakisi majaribio ya maulamaa wenu mashabiki kuficha matendo mabaya ya viongozi wao. Kuhamishwa Abu Dharr kwa nguvu kwenda Rabza kunajulikana wazi sana. Kama mfano, nitaishia kunukuu riwaya moja, ambayo imesimuliwa na Imam Ahmad Bin Hanbal katika “Musnad” Jz. 5, uk. 156, Ibn Abi’l-Hadid katika “Sharhe Nahju’l-Balagha” Jz. 1, uk. 241, na Waqid katika kitabu chake cha Ta’rikh kutoka kwa Abu’l-Aswad Du’ili.

Abu Dharr aliulizwa kuhusu Safari yake ya Rabza. Abu Dharr akasema kwamba, “ali- hamishwa kwa nguvu na kupelekwa kuishi porini”. Akaendelea: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alinijulisha kuhusu hili. Siku moja nililala Msikitini. Mtume akaja na akaniuliza kwa nini nimelala msikitini. Nikasema kwamba usinginzi umenipitia tu.

Akaniuliza nitafanya nini kama nitahamishwa kutoka Madina. Nikasema ningekwenda kwenye nchi takatifu ya Syria. Akaniuliza nitafanya nini kama nitahamishwa huko pia. Nikasema nitarudi msikitini.

Aliniuliza tena ningefanya nini kama ningefukuzwa kutoka hapa pia. Nikasema: Nitachomoa upanga na kupigana. Aliniuliza kama ningependa aniambie kitu ambacho kingekuwa kwa manufaa kwangu. Niliposema ‘Ndio’ yeye akaniambia: ‘Nenda sehemu yoyote watakayokupeleka!’ Hivyo nikasikiliza alivyoniambia na nikamtii. Baada ya hivi Abu Dharr akasema, kwa Jina la Allah, wakati Uthman atakapokwenda mbele ya Allah atasimama akiwa ni mwenye dhambi kuhusiana na suala langu.’”

Upole Na Ukarimu Wa Ali Bin Abu Talib:

Kama utayachunguza mambo kwa akili huru iliyo wazi, utakubali kwamba Ali alikuwanazo sifa za huruma na upole kwa kiwango cha hali ya juu sana. Wanahistoria wote, pamo- ja na Ibn Abi’l-Hadid, wameeleza kwamba wakati Ali alipochukua Ukhalifa, aliondoa mambo mabaya na mazushi ambayo yaliingizwa ndani (ya Uislamu).

Aliwaondoa maofisa wasiomjua Mungu wa Ki-Bani Umayya, ambao waliyakandamiza majimbo wakati wa kipindi cha Ukhalifa wa Uthman.

Wanasiasa wachoyo walimshauri aahirishe uamuzi wake huo wa kuwondoa maofisa hao mpaka Ali atakapojiimarisha zaidi katika mamlaka. Mtukufu Imam akasema: “Naapa kwa Jina la Allah kwamba sitaruhusu hila za kijanja kama hizo.

Mnasisitiza kwamba nitumie njia za upatanisho, lakini hamjui kwamba jinsi wanavyoendelea kubakia katika mamlaka wakiniwakilisha mimi, wataendelea kutenda mabaya yale yale ya kidhalimu na ukatili ambao nitawajibika kwenye Mahakama ya haki ya Mungu. Siwezi kuruhusu udhalimu huu.” Uondoaji wa maofisa uliofanywa na Ali ulipelekea uhasama kwa watu wenye uchu wa madaraka, kama Mu’awiyya, na wakaitayarisha njia ya vita vya Jamal na Siffin. Kama Talha na Zubair wangechaguliwa kama magavana, wasingelichochea ghasia kule Basra na kuacha vita vya Jamal kutokea.

Upole na ukarimu wake ulienea sawasawa kwa marafiki na maadui. Uthman alikuwa katili sana kwake (zaidi kuliko alivyokuwa Abu Bakr na Umar), lakini waasi walipolazimisha kizuizi kwenye Ikulu ya Uthman, wakizuia maji na chakula, aliomba msaada kwa Ali. Ali aliwatuma watoto wake, Hasan na Husein, wakiwa na mikate na maji.

Ibn Abi’l-Hadid anaelezea tukio hili kwa kina katika Sharhe “Nahju’l- Balagha.” Khalifa Uthman alikuwa na sifa ya kutoa Sadaka na kusaidia wengine, lakini ilikuwa kwa jamaa zake tu, kama Abu Sufyani, Hakam Bin Abi’l-As na Murwan Bin Hakam. Aliwamwagia pesa na zawadi kutoka hazina ya Umma bila kibali cha kidini.

Lakini Amirul-Mu’minina Ali kamwe hakutoa zaidi ya kilichostahiki, hata kwa jamaa zake wa karibu. Kaka yake mkubwa, Aqil, alikuja kwake na kutaka pesa zaidi kuliko kawaida ya alivyokuwa akipewa.

Ali hakusikiliza ombi lake. Aqil alisisitiza na akasema kwamba kwa vile Ali alikuwa Khalifa na alikuwa na mamlaka kamiki juu ya mambo inapasa haja zake zitekelezwe. Kama onyo kwa kaka yake, Ali akapasha moto kipande cha chuma kwa siri na akakiweka karibu na mwili wa Aqil. Alipiga kelele kama mtu aliye katika maumivu makali, akiogopa kuwa ataungua. Ali akasema: “Wacha waombolezaji waomboleze kifo chako, ewe Aqil! Ulinywea wakati chuma kilichopashwa moto na mwanadamu kiliposogazwa karibu yako, na bado unanisogeza mimi kunielekeza kwenye moto ambao Allah ameumba kwa ghadhabu yake. Je, ni sawa wewe utafute hifadhi kutokana na maumivu haya ya kawaida, na kwamba mimi nisijihifadhi mwenyewe na Moto wa Jehanamu?”

Upole Wa Ali Kwa Marwan Na Abdullah Bin Zubair:

Hata baada ya kuwashinda maadui zake, Ali bado alikuwa mpole kwao. Mlaaniwa Marwan, mtoto wa mlaaniwa Hakum alikuwa ni adui muovu wa Ali. Lakini Ali alipomshinda Marwan katika vita ya Jamal, alimsamehe. Abdullah Bin Zubair alikuwa ni adui mwingine muovu.

Alimtukana Ali wazi wazi, na Abdullah aliposoma Khutuba yake kule Basra mbele za watu, alisema: “Hakika Ali Bin Abu Talib ni fisadi, duni, na bahili.” (Allah atuepushie mbali). Lakini Mtukufu Imam aliposhinda vita vya Jamal na mtu huyu muovu alipoletwa kama mateka mbele yake, Ali hakusema hata neno kali dhidi yake. Ali alimgeuzia kando uso wake na akamsamehe.

Upole Wa Ali Kwa Aisha

Mfano mzuri wa huruma ya Ali ulikuwa ni mwenendo wake kwa Aisha. Jinsi alivyokuja uso kwa uso kupigana naye na kumshutumu kungemkasirisha mtu duni. Lakini Ali alipomshinda, alimshughulikia kwa heshima. Alimpa Muhammad bin Abu Bakr, kaka yake Aisha, jukumu la kuangalia ustawi wake. Kwa maagizo yake, wanawake ishirini wenye nguvu waliovaa kama wanaume walimsindikiza Aisha mpaka Madina. Alipofika Madina, alielezea shukurani zake kwa wanawake hao na wake za Mtume.

Alisema kwamba siku zote atabakia mwenye shukurani kwake. Alikiri kwamba, ingawa alikuwa katili kwake na alikuwa amehusika na ghasia kiasi hicho, hakusema neno lolote baya dhidi yake.

Alisema alikuwa na lalamiko moja tu dhidi yake. Alishangaa kwa nini alimsafirisha kwenda Madina huku akisindikizwa na wanaume. Wanawake wale vijakazi mara moja walivua mavazi yao ya kiume. Ikajulikana wazi kwamba mpango huu ulifanywa kwa madhumuni ya kulinda mali zao kutokana na majambazi.

Mfano mwingine wa huruma za Ali ni jinsi alivyomshughulikia Mu’awiyah katika vita vya Siffin. Jeshi la askari 12,000 la Mu’awiyah liliufunga mto wa Euphrate. Wakati jeshi la Ali lilipoona kwamba njia waliyokuwa wanaitegemea ya kupatia maji ilikuwa imeshikwa, Ali alituma ujumbe kwa Mu’awiyah akisema kwamba Mu’awiyah hapaswi kufunga njia ya kufikia maji. Mu’awiyah alijibu kwamba atawanyima kutumia maji.

Ali akamtuma Malik Ashtar na kikosi cha askari. Alisukuma nyuma jeshi la Mu’awiyah na kuifungua njia ya kuufikia mto Euphrate. Masahaba wakasema: “Ewe Ali! Na sisi tulipize na tuwanyime maji, ili kwamba maadui wafe kwa kiu na vita vitakuwa vimekwisha.” Ali akasema: “Hapana! Kwa jina la Allah, sitalipiza kwa kufuata mfano wao. Waacheni askari wao wapate njia ya kufikia mto Euphrate.”

Maulamaa wenu wenyewe, kama Tabari katika kitabu chake “Ta’rikh”, Ibn Abi‘l-Hadid katika “Sharhe Nahju‘l-Blagha”, Suleimani Balkhi katika “Yanabiu‘l-Mawadda”, Sura ya 15, Mas‘udi katika “Murju‘dh- Dhahab”, na wanahistoria wengine wameandika kwa urefu kuhusu uugwana wa Ali. Unaweza ukachunguza maelezo haya na kisha ukaamua ni nani anayeelekea kulengwa na aya hii: “Na wakahurumiana wenyewe kwa wenyewe…” Katika aya iliyoko kwenye mjadala, Muhammad, Mtume wa Allah, ndiye mlengwa na kinacho fuatilia ni arifu yake.

Sifa zote zile ni kwa ajili ya mtu huyo huyo. Kuwa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kuwa mkali dhidi ya makafiri katika medani ya vita na katika mijadala ya kielimu, kuwa na huruma kwa marafiki na maadui – sifa zote hizi hurejea kwa mtu ambaye kamwe hajamuacha Mtume au hata kufikiria kumuacha.

Mtu huyo ni Ali Bin Abi Talib. Nilikwisha sema mapema kwamba, mwanachuo mkubwa, Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi‘i ameandika katika kitabu chake “Kifayatu‘t-Talib” kwamba katika ayah ii Allah anamsifia ‘Ali.

Sheikh: Kuna majibu mengi kwa maelezo yako, lakini umetafsri tu visivyo aya hii. Usemi “na wale ambao wako pamoja naye” ni wa wingi na hauwezi kuonyesha mtu mmoja tu. Kama sifa zilizotajwa katika aya zinamuonyesha mtu mmoja tu, kwanini vijina vikawa kwa wingi?

Muombezi: Kwanza, unasema kwamba kuna majibu mengi kwa maelezo yangu. Kama hiyo ilikuwa kweli, basi kwa nini usiyataje? Kunyamaza kwako ni uthibitisho kwamba hakuna “mjibu mengi” kwa maelezo yangu. Pili, ulichosema hivi punde tu ni hoja potofu.

Unajua kwamba katika luhga zote ikiwemo Kiarabu utumiaji wa wingi kwa ajili ya mmoja ni kitu cha kawaida kama dalili ya heshima. Kuna mifano mingi ya utumiaji huu katika Qur’ani Tukufu kama aya hii: “Hakika walii wenu ni Allah na Mtume wake na walio amini ambao husimamisha Salat na hutoa zaka na huku wamerukuu.” (5:55) Inakubaliwa na wote kwamba aya hii imeshuka kwa ajili ya Ali.

Wafasiri na muhadithina, kam vile Imamu Fakhru‘d-Din Razi katika “Tafsir Kabir”, juzuu ya 3, uk. 431; Imamu Abu Ishaq Tha‘labi katika kitabu chake “Kashfu ‘l-Bayan”; Jarullah Zamakhshari katika “Tafsir Kashshaf”, juzuu ya 1, uk. 422; Tabari katika “Tafsir” yake, juzuu 6, uk. 186; Abu‘l-Hasan Rammani katika “Tafsir” yake; Ibn Hawazin Nishapuri katika “Tafsir” yake; Ibn Sa‘dun Qartabi kati- ka “Tafsir” yake, juzuu ya 6, uk. 221; Nasafi Hafiz katika “Tafsir” yake, uk.496 (kwa njia ya ufafanuzi kwenye Tafsir ya Khazin Bahgdadi); Fazil Nishapuri katika “Gharibu‘l-Qur’ani”, juzuu ya 1, uk.461; Abu‘l-Hasan Wahidi katika “Asbabu’n-Nuzul”, uk. 148; Hafiz Jassas katika “Tafsir Ahkamu’l-Qur’ani,” uk. 542; Hafiz Abu Bakr Shirazi katika “Fima Nazala Mina’l-Qur’ani Fi Amiru’l-mu’minin”; Abu Yusuf Abdu’s-Salam Qazwini katika “Tafsir Kabir”; Kadhi Baidhawi katika “Anwar’t-Tanzil”, juzuu ya 1, uk. 345; Jalalu’d-Din Suyiti katika “Durr’l-Mansur”, juzuu ya 2, uk. 239; Kadhi Shukani San’a’i katika “Tafsir Fathu’l-Qadir”; Sayyid Muhammad Alusi katika “Tafsir” yake, juzuu ya 2, uk. 329; Hafiz Ibn Abi Shaiba Kufi katika “Tafsir” yake; Abu’l-Baraka katika “Tafsir” yake, juzuu ya 1, uk. 496; Hafiz Baghawi katika katika “Ma’alimu’t-Tanzil”; Imamu Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i katika “Sahih” yake.

Muhammad bin Talha Shafi’i katika “Matalibu’s-Su’ul”, uk. 31; Ibn Abi’l-Hadid katika “Sharhe Nahju’l- Balagha”, juzuu ya 3, uk. 375; Khazin Ala’u’d-Din Baghdadi katika “Tafsir” yake, juzuu ya 1, uk. 496; Suleimani Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, uk. 212; Hafiz Abu Bakr Baihaqi katika “Kitab Musnnaf”;

Razin Abdari katika “Jam’Bainu’s- Siha Sitta”; Ibn Asakir Damishiq katika “Ta’rikh Sham”; Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira”, uk. 9; Kadhi Azuda’ili katika “Mawaqif”; uk.276; Sayyid Sharif Jurjani katika “Sharhe Mawaqif”; Ibn Sabbagh Malik katika “Fusu’l-Muhimma”, uk. 123; Hafiz Abu Sa’d Sam’ani katika “Fadha’il’s-Sahaba”; Abu Ja’far Askafi katika “Nagzi’l-Uthmaniyya”; Tibrani katika “Ausat”; Ibn Maghazili Faqih Shafi’i katika “Manaqib”; Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’t-Talib”; Mulla Ali Qushachi katika “Sharhe Tajrid”; Sayyid Muhammad Mu’min Shablanji katika “Nuru’l-Absar”, uk. 77; Muhibu’d-Din Tabari katika “Riyazu’n-Nuzra”, juzuu ya 2, uk. 247, halikadhalika na wengine wengi miongoni mwa wanachuoni wenu maarufu, wote wamesimesimulia kutoka kwa Said, Mujahid Hasan Basri, A’mash, Atba Bin Hakim, Ghalib Ibn Abdullah, Qais Bin Rabi’a, Abaya Bin Rab’i , Abdullah Ibn Abbas, Abu Dharr Ghifari, Jabir Ibn Abdullah Ansari, Ammar, Abu Rafi, na Abdullah Bin Salam, na wengine wanakiri kwamba aya hii iliteremshwa katika kumsifia Ali.

Aya hii inaashiria kwenye wakati ambao Ali alitoa pete yake kumpa muombaji wakati akiwa kwenye rukuu. Hapa vile vile maneno yapo katika wingi kwa staha na heshima juu ya cheo cha Wilaya (walii), na kuthibitisha kwamba Ali alikuwa Imamu na mrithi wa Mtume (s.a.a.w.).

Msisitizo wa neno “In’nama”, hutoa maana ya – uamuzi wa Allah – wa mwisho na uliopangwa, yaani, uamuzi wa Allah kwamba Walii wa waumini lazima awe ni Allah, Mtume Wake (Muhammad), na waumini ambao hutoa sadaka huku wakiwa wanasali, huyu wa mwisho akiashiriwa bayana kuwa ni Ali.

Sheihk: Hakika utakubali kwamba tafsiri yako haikuthubutu kwa vile kuna maoni tofauti kuhusu hilo. Baadhi wanasema huashiria kwa Ansar, baadhi wanasema ni katika kumsifia Ibadat Bin Samit, na baadhi wanasema kwamba inaashiria kwa Abdullah Bin Salam.

Muombezi: Kwa hakika inashangaza kwamba mwanachuo kama wewe unaweza kupingana na ulamaa wako mwenyewe. Unachukua maoni ya wajinga wachache na wasioaminika ambao riwaya zao zinakataliwa. Wanachuoni wenu wakubwa kwa pamoja wametamka kwa dhati kuthibitisha juu ya nukta hii, watu kama Fazil Taftazani na Mulla Ali Qushachi, ambaye anasema katika kitabu chake, Sharhe Tajrid:

“Kwa mujibu wa maoni ya pamoja ya wafasiri, aya hii iliteremshwa katika kumsifia Ali, ambaye wakati akiwa kwenye rukuu katika Sala, alitoa pete yake kumpa muombaji.” Mashaka Na Utata Kuhusu “Aya Ya Walii” Na Ufafanuzi Wake

Sheikh: Katika mlolongo wa mazungumzo yako kuhusiana na aya hii, umejaribu kuthibisha kwamba Ali alikuwa ndiye mrithi wa mara moja wa Mtume (s.a.w.w.), ingawa neno “Wali” katika aya hii lina maana ya “rafiki” au “mwenye kupendwa sana”, na sio “Imamu” au “Mrithi.” Kama maoni yako ni yenye kukubalika kwamba “Wali” maana yake ni “mrithi” na “Imamu”, basi kwa mujibu wa kanuni iliyokubaliwa, haikomei kwa mtu mmoja, bali wengine wanakuwemo pia, Ali akiwa mmoja mionmgoni mwao.

Vile vile katika aya, “Hakika walii wenu ni Allah, na Mtume Wake, na wale ambao wameamini…” utumiaji wa (sarufi) wingi huonyesha watu kwa ujumla. Kusema kwamba muundo wa wengi ni kuonyesha heshima, haina maana bila hoja yenye nguvu, mfano wa ki-Qur’ani, au chanzo kingine.

Muombezi: Umeulewa vibaya msemo “…Walii wenu…” “Wali” ni (sarufi ya) umoja, “kum” (wenu) ni wingi ambao huashiria kwa watu na haioneshi umoja. Naam hakika, “Wali” ni kwa ajili ya mtu ambaye ni mlezi kwa jamii nzima katika zama zote. Pili, katika aya ambayo iko kwenye mjadala, pale ambapo wingi umetumika, baadhi ya mashabiki wamesema kwamba haiwezi kutafsiriwa kama umoja kama katika aya “…wale ambao wanasimamisha Sala…” pingamizi hili nililijibu mapema.

Nilisema kwamba, waandishi wakubwa mara nyingi wametumia umoja kumaanisha wingi. Vile vile umedai kwamba muundo wa (sarufi ya) umoja katika aya hii huashiria watu kwa ujumla. Tunasema kwamba, kwa mujibu wa msisitizo wa neno “hakika”, anayeashiriwa ni Ali, lakini hatukusema kwamba kuhusika huko ni kwa aina ya pekee tu kwake.

Wengine kutoka nyumba ya Mtume wanakuwemo pia. Kwa mujibu wa hadithi zilizo sahihi, Maimamu wote wa kizazi cha Mtume wamejumuishwa katika aya hii. Jarullah Zamakhshari anaandika katika “Kashshaf” kwamba aya hii iliteremshwa makhususi katika kumsifia Ali, lakini ule wingi uliotumika ndani yake, unamaanisha kwamba wengine lazima wamfuate.

Sheikh: Katika aya hii neno “Wali” haswa lina maana ya “msaidizi.” Kama lingekuwa na maana ya “mlezi” ambayo hujumuisha na cheo cha mrithi, basi angeliteuliwa wakati wa uhai wa Mtume (s.a.w.w.).

Muombezi: Cheo cha Ali ni cha kudumu. Ujengaji wa sentensi kisarufi na neno “Wali” uliotumika kama sifa, huthibitisha cheo cha kudumu cha Ali. Ukweli huu unaungwa mkono zaidi na Mtume kwa kumtangaza Ali kama makamu wake wakati wa safari ya Tabuk na kamwe hakulifuta tangazo hilo.

Mtazamo wetu unaimarishwa zaidi na Hadith-e-Manzila (Hadithi ya cheo) ambayo Mtukufu Mtume amerudia mara nyingi kuisimulia: “Ali kwangu mimi ni kama Harun alivyokuwa kwa Musa,” ambayo nimeilezea katika mikesha iliyopita. Hii yenyewe ni uthibitisho mwingine kwa Ali wa kuwa kwake Walii au Makamu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati wa uhai wa Mtume na baada ya kufa kwake.

Sheikh: Kama ingekuwa tulipe suala hili mazingatio yanayostahili, tungelikiri kwamba aya hii haimzungumzii Ali. Cheo chake ni kikubwa kuliko kile tunavyotaka kukithibitsha kutoka kwenye aya hii. Haithibitishi ubora wowote juu yake, bali hukiangusha chini cheo chake.

Muombezi: Sio wewe wala mimi – si yeyote katika Umma – pamoja na wale masahaba wakubwa wa Mtume, ambaye ana haki yoyote ya kuingilia tafsiri halisi za aya hizi. Aya za Qur’ani hazikuteremshwa kwa mujibu wa matakwa yetu. Kama baadhi ya watu wakitafsiri maana zao kwa kuegemeza juu ya maoni yao au wakataja tukio au habari ambayo imeteremshiwa, basi kwa hakika hao sio watu wa dini.

Kwa mfano, wafuasi wa Abu Bakr wanasema kwamba kwa mujibu wa hadithi iliyosimuliwa na mghushaji mkorofi Akrama, aya hii iliteremshwa kwa ajili ya Abu Bakr. Unaweza ukatueleza ni jinsi gani aya hii inavyoangusha cheo cha Ali?

Sheikh: Moja ya tabia za murwa wa cheo cha Ali ni kwamba, wakati anaposali kamwe hageuzi hadhari yake kwenye kitu kingine. Wakati fulani Ali alijeruhiwa katika vita. Kiwembe cha mshale kilibakia mwilini, na ilikuwa haiwezikani kukiondoa bila kusababisha maumivu makali. Lakini aliposimama kwa ajili sala, kiwembe cha mshale kiliondolewa, na kwa sababu ya kuzama katika ibada yake kwa Allah, hakusikia maumivu. Kama wakati wa kusali alitoa pete yake kumpa muombaji, kulikuwa na dosari kubwa kati- ka Sala yake.

Itaezakana vipi mtu ambaye amezama katika rehema ya Allah na wakati huo huo andoe hadhari yake kutoka kwa Allah kwa ajili ya kuitikia sauti ya omba omba? Aidha, katika kutenda kila jambo jema na kutoa sadaka kuweka nia ni kitu cha lazima. Wakati wa kusali hadhari ya mtu lazima iwe imeelekea kwa Allah peke Yake.

Inawezekana vipi kwamba nia yake imegeuka kutoka kwenye Sala na kugeuka kumuelekea kiumbe? Kwa vile tunakiona cheo cha Ali kuwa ni cha juu sana, hatukubali tafsiri yako.

Na kama alitoa chochote kwa omba omba, basi kwa hakika haikuwa wakati wa Sala, kwa vile rukuu maana yake ni kunyenyekea mbele ya Allah.

Muombezi: Umejifunza vizuri jinsi ya kusoma, lakini umeikosa njia ya kuendea kwenye maombi. Pingamizi hili ni dhaifu kuliko hata utando wa buibui. Kwanza, kitendo cha Ali kwa njia yoyote hakiangushi chini cheo chake. Kwa hakika kumsikiliza omba omba ili kumpa sadaka, ni chanzo cha ubora.

Katika hali hii, alikusanya sala yake ya kimwili na ya kiroho pamoja na sala ya kiyakinifu. Sala zote zilikuwa katika njia ya Allah. Ndugu wapenzi! Uharibifu ambao unanyongesha Sala ni ule ambao unatokana na fikra binafsi.

Kuzingatia sala nyingine, wakati ambapo unasali Sala mahususi, ni dalili ya ubora. Kwa mfano, kama wakati wa ibada ya Sala, mtu akalia kwa mapenzi makubwa ya jamaa zake, Sala yake itakuwa batili. Lakini kama akilia kwa mapenzi makubwa ya Allah, au kwa kumuogopa Yeye, basi hiyo ni dalili ya ubora. Umesema kurukuu maana yake ni kunyenyekea kwa unyofu kwa Allah. Maana hii inaweza ikatumika kwa matukio mengine.

Lakini kama ukisema kwamba kurukuu katika Sala, ambako ni hakika na lazima, kunabeba maana hiyo hiyo ya kilugha, watu wasomi watakudharau. Vile vile umejaribu kuondoa au kupuuza maana ya wazi ya aya. Umeitolea maana ya kistiari, ingawa unajua kwamba neno hilo huelezea kitendo kinachohitajika cha ibada ya Sala, ambacho ni kuinama mpaka viganja kufikia magoti. Na ukweli huu umekubaliwa na maulamaa wenu wakubwa, kama nilivyoelezea mapema.

Fadhil Qushachi, katika Sharhe Tjrid, anaelezea maoni ya wafasiri kwa ujumla kwamba Ali, wakati anarukuu katika Sala, alitoa pete yake kumpa omba omba. Tukiweka kila kitu pem- beni, tafadhali tueleze iwapo aya hii ilitaremshwa kwa kusifu au kwa kulaumu?

Sheikh: Ni wazi ilikuwa kwa kusifia.

Muombezi: Hivyo wakati maulamaa wa madhehebu zote wamesema kwamba aya hii iliteremshwa kwa kumsifia Ali, na kwamba ina ridhaa ya Allah (swt), kwa nini ulete ukinzani usio na maana, ukubaliane na Makhawariji washabiki, ambao maoni yao yameduk- izwa kwenye akili yako safi tangu utotoni? Kwa nini hukubali ukweli huu?

Sheikh: Samahani! Kwa vile wewe ni mzungumzaji fasaha, mara nyingi unatumia vidokezo na rejea ambazo zinaweza kujenga mawazo ambayo yanaweza kuleta matokeo yasiyofurahisha katika akili za watu ambao hawana elimu ya kutosha juu ya masuala haya. Ingekuwa vyema kama ungejizuia kutokana na lugha kama hizo.

Muombezi: Katika mazungumzo yangu hakuna chochote ila ukweli. Allah awe shahidi wangu, kamwe sijakusudia kutumia madokezo au rejea zisizo za moja kwa moja. Hakuna haja ya kufanya hilo. Chochote ninachotaka kusema, nakisema kwa wazi. Tafadhali nieleze ni vidokezo gani unavyomaanisha.

Sheikh: Muda mfupi uliopita wakati wa mazungumzo yako kuhusiana na aya iliyoko kwenye mjadala, ulisema kwamba sifa zilizotajwa ndani yake ni za kipekee kwa Ali Bin Abu Talib ambaye kuanzia mwanzo mpaka mwisho wa uhai wake, kamwe hajawa na shaka katika imani yake. Kwa namna hii unaonesha kwamba wengine walikuwa na hatia ya ukana mungu.

Je, wale makhalifa wakubwa au masahaba kuna yeyote aliyekuwa na shaka katika imani zao? Bila shaka hao masahaba, kama alivyokuwa Ali, kamwe hawajautilia shaka ukweli wa Uislamu. Hata mara moja hawajakengeuka katika mafindisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Muombezi: Kwanza, kamwe sijatumia maneno ambayo wewe umeyatumia sasa hivi. Pili, unaelewa kwamba kuthibitisha kitu kwa mtu fulani haina maana ya kutothibitisha kitu hicho kwa watu wengine. Tatu, ingawa unajaribu kunikosoa, nafikiri wengine hawana kitu kama hicho katika akili zao.

Allah awe shahidi wangu, sikufanya rejea yoyote isiyo ya moja kwa moja kwa kitu chochote, wala sijafikiria kufanya hivyo. Na kama kitu chochote kilitokea kwenye akili yako, ungeweza kuniuliza kuhusu kitu hicho kwa faragha.

Sheikh: Namna ya uzungumzaji wako huonyesha kwamba kuna nukta fulani ambazo unazinyamazia. Nakuomba utufahamishe kilichoko akilini mwako na kutupa rejea sahihi kwa unachosema.

Muombezi: Ni wewe uliyejenga kitu hicho akilini mwetu; unasisitiza kwamba suala hili lijadiliwe. Nakuomba tena, liache suala hili na uache kusisitiza juu yake.

Sheikh: Kama kulikuwa na kitu chochote cha usafihi, imekwisha. Sasa huna jinsi ila kujibu. Kama hutatoa jibu la wazi, ima la kukubali au kukataa, basi nitawajibika kuamua kwamba uliyoyasema yalikuwa hayana msingi wowote.

Muombezi: Hakuna chochote cha usafihi katika maelezo yangu, lakini kwa vile unasisitiza, sina jinsi isipokuwa kuufichua ukweli. Ulamaa wenu wakubwa wanakubali kwamba masahaba wa Mtume ambao imani yao ilikuwa bado haijakamilika, mara kwa mara walionyesha kuwa na mashaka. Baadhi yao walilea shaka hiyo na uasi wa kidini. Baadhi ya aya ziliteremshwa kwa ajili ya kuwalaumu.

Kwa mfano, walikuwepo munafiqin (wanafiki) ambao katika kulaumiwa kwao Sura nzima ya Qur’ani Tukufu iliteremshwa. Lakini masuala kama hayo hayapaswi kujadiliwa waziwazi. Nakuomba tena ujizuiye kuindama nukta hii. Sheikh: Una maana kwamba wale makhalifa wakubwa walikuwa ni miongoni mwa wale waliokuwa na mashaka.

Muombezi: Kama majibu yangu yatasababisha hisia mbaya miogoni mwa watu wasio na elimu, wewe ndiye utakayebeba lawama. Umesema sasa hivi, “Useme hivi au umesema kwamba.” Lakini tena, ni maulamaa wenu wenyewe ndio ambao wamesimulia mambo haya.

Sheikh: Wameandika kuhusu suala gani, na ni katika tukio gani makhalifa wameonesha shaka yao, na ni watu gani ambao walitia shaka? Tafadhali tujulishe.

Muombezi: Watu wengi walikuwa na shaka kubwa sana, lakini wakarudi kwenye imani yao ya asili. Baadhi yao wakang’ang’ania katika shaka zao. Ibn Maghazili Shafi’i, katika kitabu chake “Manaqib,” na Hafidh Abu Abdullah Muhammad Bin Abi Nasir Hamidi katika “Jam’Bainu’s-Sahihain-e-Bukhari”, na Muslim wanaandika: “Umar Bin Khattab alisema,‘Sijapata kuutilia mashaka utume wa Muhammad kama nilivyofanya siku ya Hudaibiyya.’” Maelezo haya yanaonyesha kwamba aliutilia shaka utume wa Muhammad zaidi ya mara moja.

Nawab: Samahani. Ni tukio gani katika Hudaibiyya ambalo lilimfanya awe na shaka kuhusu Mtume?

Muombezi: Mtume aliona usiku mmoja kwenye ndoto kwamba alikwenda Makka pamoja na mashaba zake kufanya Umra. Asubuhi yake, aliposimulia ndoto hii kwa masahaba zake, walimuomba aitafsiri ndoto hiyo. Mtume akasema, “Mwenyezi Mungu akipenda tutakwenda Makka kuitekeleza ibada hii Insha’allah.” Lakini hakuainisha ni wakati gani itafanyika.

Akiwa na nia ya kuizuru Nyumba ya Allah, Mtume aliondoka na masahaba zake kuelekea Makka katika mwaka ule ule.

Wakati walipofika Hudaibiyya (kisima kilicho karibu na Makka), Maquraishi walikuja pale na kuwazuia wasiendelee mbele. Kwa vile Mtume hakuenda kule akiwa amejiandaa kupigana, alijitolea kufanya amani nao.

Mkataba ulisainiwa na Mtume akarudi Madina. Katika tukio hili, Umar alikuwa na mashaka. Alikwedna kwa Mtume na akasema: “Je, wewe sio Mtume wa Allah na mtu mkweli? Je, wewe hukutuambia kwamba utakwenda Makka na kufanya Umra kisha unyoe kichwa chako na upunguza ndevu zako? Kwa nini sasa umeshindwa kufanya hivi?”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuuliza iwapo yeye aliweka muda kwa ajili ya hilo au kama aliwaambia kwamba atakwenda kule katika mwaka ule ule. Umar akakiri kwamba Mtume hakuainisha wakati. Mtume akasema kwamba alichowaambia ni sahihi, na Mungu akipenda watakwenda Makka siku zijazo na ndoto yake itatimizwa.

Hakika wakati kwa ajili ya utekelezaji wa tafsiri ya ndoto, uwe mapema au baadae utetagemea juu ya utashi wa Allah (swt). Kisha kwa uthibitisho wa maelezo ya Mtume, Jibril alijitokeza na kuteremsha aya ifuatayo ya Qur’n Tukufu:

“Hakika Allah amemtimizia Mtume Wake ndoto kwa haki. Bila shaka ninyi mtauingia Msikiti Mtukufu, insha-Allah kwa amani, na hali mmenyoa vichwa vyenu na (baadhi) mmepunguza nywele. Hamtakuwa na hofu. Yeye anajua msiyoyajua. Basi atakupeni kabla ya haya ushindi karibuni.” 48:27.

Ushindi hapa una maana ya ushindi wa Khaibar. Hii ilikuwa kwa ufupi tukio la Hudaibiyya ambalo kwa kweli lilikuwa ni mtihani kwa waumini na kwa watu wanaoyumba.

Kufikia hapa ulifuatia mjadala wa iwapo tuendelee na mjadala au la, kwa ajili ya ratiba ya wageni wa ki- Sunni kutoka Afghanistan na halikadhalika na Muombezi, matokeo yake ambayo ilikuwa ni uamuzi wa kuendelea.

Mkutano Wa Saba Jumatano Usiku 29 Rajab, 1345 A.H.

Sayyid Abdu’l-Hayy (Imam wa Msikiti wa jamaa wa Sunni): Mikesha fulani iliyopita ulitoa maelezo fulani ambayo kwamba Hafidh Sahib alitaka uthibitisho, lakini kwa ujanja ulikwepa kujibu au ulifanya watu miogoni mwetu wachanganyikiwe, na suala lote likawa ni lenye kukera.

Muombezi: Tafadhali nifahamishe ni lipi kati ya maswali yenu ambalo limeachwa bila kujibiwa, kwani sikumbuki ni suala gani unalolirejelea.

Sayyid: Wewe hukusema katika baadhi ya mikesha iliyopita kwamba Ali alikuwa na umoja wa ‘nafsi’ pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hivyo alikuwa mbora wa cheo kwa mitume wote?

Muombezi: Ni kweli. Hayo yalikuwa ni maelezo yangu, na ni katika imani yangu.

Sayyid: Basi kwa nini hukujibu swali letu?

Muombezi: Umekosea sana. Inashangaza kwamba umekuwa ukisikiliza kwa ukaribu majadiliano yetu, lakini bado sasa unanilaumu kwa kuchukuwa njia ya ujanja au kuchanganya akili zenu. Kama utaangalia kwa makini utaelewa kwamba sijasema kitu chochote cha kupotosha, lakini ma-Mulla hawa wasomi waliuliza maswali ambayo nililazimika kuyajibu. Sasa kama una swali lolote la kuuliza, unaweza kufanya hivyo, na kwa msaada wa Allah, nitalijibu.

Sayyid: Tunataka kujua vipi inawezekanaje kwamba watu wawili wanaweza kuungana kiasi kwamba muungano wao unawafanya kuwa mtu mmoja na yule yule.

Tofauti Kati Ya Muungano Wa Kuwazika Na Muungano Halisi

Muombezi: Kwa hakika, haiwezikani kwa watu wawili kuunda muungano halisi. Wakati niliposema kwamba Amiru’l-Muminina Ali ana muungano wa “nafsi” pamja na Mtume, hupaswi kuuchukualia kama muungano halisi, kwa sababu kamwe hakuna mtu aliyedai hivyo, na kama mtu yeyote akiuamini atakuwa amekosea kabisa. Muungano nilioutaja ni wa kuwazika tu, sio halisi, na unakusudia kuonesha kwamba wote wawili wana ubora ule ule wa nafsi na muruwa, sio mwili huo mmoja.

Hafidh: Basi kwa mujibu wa kauli hii wote lazima watakuwa ni mitume, na kutokana na usemavyo, wahayi lazima utakuwa umekuja kwa wote.

Muombezi: Hiyo ni dhana potofu ya dhahiri. Hakuna Shi’a hata mmoja mwenye imani kama hiyo. Nisingetegemea wewe kujiingiza katika mazungumzo kama haya na kupoteza wakati wetu. Nimekuelezeeni tu kwamba wanahusiana katika masuala yote ya sifa na ubora, isipokuwa sifa zile ambazo kuziondoa kwake kuna amri au misingi makhususi. Jambo hilo la pekee ni utume na sifa zake zote zilizoambatanishwa nao - mojawapo ikiwa ni upokeaji wa wahayi, na kwa kupitia huo ni mawasilisho ya Maamrisho ya Mungu.

Pengine umesahau maelezo yangu katika mikesha iliyopita, ambamo nilithibitisha kupitia Hadithi ya Cheo (Manzila) kwamba Ali alikuwa na cheo cha utume, lakini kwamba alifu- ata na alipasika kwenye dini na mafundisho yaliyofundishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Cheo chake katika utume hakikuwa zaidi ya kile cha Harun wakati wa Musa.

Hafidh: Lakini kama unaamini katika usawa wa Ali pamoja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika mambo yote ya sifa na ubora, inafuatia kwamba lazima uamini usawa wake katika masuala ya utume na sifa zilizoambatanishwa nao.

Muombezi: Inaweza kuelekea hivyo, lakini kama unafikiria kwa makini utaona kwamba sio hivyo. Kama nilivyothibibitisha mapema kutoka kwenye aya za Qur’ani, utume ni wa vyeo tofauti, na Manabii na Mitume wa Allah wanazidiana kati ya mmoja na mwingine katika ubora wa vyeo. Kama Qur’ani Tukufu inavyoeleza kwa uwazi: “Mitume hao Tumewatukuza baadhi yao juu ya wengine…” (2:253). Na kikamilifu zaidi katika cheo kwa Mitume wote ni cheo maalumu cha Muhammad, kama Allah alivyosema: “Muhammad sio baba wa yeyote katika wanaume wenu, bali ni Mtume wa Allah na mwisho wa Manabii, na Allah ni mjuzi wa kila kitu” (33:40).

Ni kwa ukamilifu huo wa utume ambao umepelekea kwenye ukomo wa utume. Hivyo katika sifa hii ya ukamilifu, hakuna mtu yeyote anayeweza kujumuishwa humo. Katika mambo mengine yote ya ubora, kuna ushirikiano na usawa, ambao kwamba kuna uthibitisho mwingi.

Sayyid: Unaweza ukaleta hoja yoyote kutoka kwenye Qu’an kuthibitisha madai haya?

Aya Ya Maapizano (Mubahila) Inathibitisha Umoja Wa Nafsi Ya Ali Na Ya Mtukufu Mtume (S.A.W.W.)

Muombezi: Hakika, hoja yetu ya kwanza ni kutoka Qur’ani Tukufu, ambayo ni ushahidi wa ki-Mungu wenye nguvu sana, yaani aya ya maapizano (Ayatul-Mubahila) ambayo kwayo Allah anasema:

ﻓَﻤﻦ ﺣﺎﺟﻚَ ﻓﻴﻪ ﻣﻦ ﺑﻌﺪِ ﻣﺎ ﺟﺎءكَ ﻣﻦ اﻟْﻌﻠْﻢ ﻓَﻘُﻞ ﺗَﻌﺎﻟَﻮا ﻧَﺪْعُ اﺑﻨَﺎءﻧَﺎ واﺑﻨَﺎءﻛﻢ وﻧﺴﺎءﻧَﺎ وﻧﺴﺎءﻛﻢ واﻧْﻔُﺴﻨَﺎ واﻧْﻔُﺴﻢ ﺛُﻢ {ﻧَﺒﺘَﻬِﻞ ﻓَﻨَﺠﻌﻞ ﻟَﻌﻨَﺖ اﻟﻪ ﻋﻠَ اﻟْﺎذِﺑِﻴﻦ {61

“Watakao kuhoji katika haya baada ya kukufikia elimu hii waambie: Njooni tuwaite watoto wetu na watoto wenu, na wanawake zetu na wanawake zenu, na nafsi zetu na nafsi zenu, kisha tuombe kwa unyenyekevu tutake laana ya Allah iwashukie waongo.” (3:61)

Maulamaa wenu wakubwa, kama vile Imamu Fakhuru’d-Din Razi, Imamu Abu Ishaq Tha’labi, Jalalu’d- Din Suyuti, Qadhi Baidhawi, Jarullah Zamakhshari, Muslim bin Hujjaj, na wengine wengi, wameandika kwamba aya hii tukufu iliteremshwa siku ya maapizano, ambayo ilikuwa mwezi 24 au 25 Dhu’l-Hijja katika mwaka wa 9 A.H.

Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipowalingania Uislamu Wakristo wa Najran, wao waliwateua watu wao wenye elimu sana kama vile Seyyed, Aqib, Jasiq, Alqama na kadhalika, idadi yao ikiwa ni zaidi ya watu sabini na wakawatuma kwenda Madina pamoja na watu 300 kati ya wafuasi wao, ili kukutana na Mtukufu Mume na kujifunza Uislamu ulikuwa ni nini. Waliingia katika mjadala wa kielimu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na walishangazwa na hoja zake nzito.

Alithibitisha ukweli wa ujumbe wake kutoka kwenye vyanzo vyao vyenye kuaminika na akasema kwamba, Isa mwenyewe alitabiri kuwasili kwake (Muhammad) kwa ishara mbali mbali, na Wakristo walikuwa wanangojea kutimia kwa utabiri wa Isa ambao kwa mujibu wake, mtu huyo atatokea akiwa amepanda ngamia kutokea milima ya Faran (katika Makka) na atahamia kwenye sehemu iliyopo kati ya ‘Ayr na Uhud (ambayo ilikuwa ni Madina).

Hoja hzi ziliwavutia sana Wakristo, lakini mapenzi yao ya heshima za kidunia yaliwazuia kuukubali ukweli. Basi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaeleza amri ya Allah, ambayo walikubaliana nayo kama njia ya kumaliza mjadala na kwa ajili ya kubainisha kati ya wakweli na waongo.

Kuwasili Kwa Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Kwa Ajili Ya Maapizano

Kwa mujibu wa makubaliano yao ya pamoja, siku iliyofuatia kundi lote la Wakristo, pamoja na wanachuoni wao zaidi ya sabini, walimngojea Mtume nje ya milango ya Madina. Walitegemea kwamba yeye angekuja kwa fahari na idadi kubwa ya wafuasi wake ili kuwahofisha.

Lakini milango ilipofunguliwa, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijitokeza akiwa na kijana wa kiume kuliani kwake, mwanamke mwenye heshima kushotoni kwake, na watoto wawili mbele yake.

Walibakia chini ya mti, wakiwakabili Wakristo. Asqaf, mtu mwenye elimu zaidi mwiongoni mwa Wakristo, aliuliza hao ni watu gani ambao Muhammad ame- toka nao. Alijulisha kwamba kijana wa kiume ni mkwe wake na binamu yake, Ali Bin Abi Talib, yule mwanamke ni binti yake, Fatima, na watoto wawili ni watoto wa binti yake, Hasan na Husein.

Wakati akiwahutubia Wakristo, kiongozi wao, Asqaf, alisema: “Tazameni, jinsi Muhammad anavyojiamini! Amekuja pamoja na jamaa zake wa karibu, watoto, na wapenzi wake, kwenye shindano hili la kiroho la kuapizana. Kwa jina Mungu, kama angelikuwa na shaka au hofu kuhusu msimamo wake, kamwe asingewachagua hawa. Sasa siwashauri kuingia kwenye mashindano dhidi yake. Lau si kuwa na hofu na Mfalme wa Rumi, tungeikubali imani ya Uislamu. Ingelifaa zaidi kukubaliana nao juu ya masharti yao na kurudi nyumbani.” Wote walikabaliana naye. Kwa hiyo, Asqaf alituma ujumbe kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akisema: “Hatutaki kushindana na wewe, bali tunataka kufanya amani na wewe.” Mtume alikubali mapendekezo yao.

Mkataba uliandikwa na Amiru’l-Muminin, Ali Ibn Abi Talib. Wakristo walikubali kulipa kodi ya mwaka katika muundo wa daraya 2,000, kila moja ikiwa na thamani ya takriban dirham 40 (dirham moja ilikuwa sawa na ½ wakia ya dhahabu), na mithqal 1000 za dhahabu (mithqal ilikuwa sawa na 1/6 wakia ya dhahabu).

Nusu ya hii ilkubaliwa ilipwe mwezi wa Muharram na nusu nyingine katika mwezi wa Rajab. Baada ya mkataba kusainiwa na pande zote, Wakristo walirudi nyumbani kwao. Wakati wakiwa njiani, mmoja wa wanachuo wao aitwaye Aqib alisema kuwaambia masahaba zake: “Kwa jina la Mungu, ninyi na mimi tunajua kwamba huyu Muhammad ni Mtume yule yule wa Mungu ambaye alikuwa akitazamiwa, na chochote anachosema kinatoka kwa Mungu.

Naapa kwa jina la Mungu kwamba yeyote aliyeshindana na Mtume wa Mungu aliangamia, na hakuna katika vijana wao na wazee wao aliyebakia hai. Kwa hakika kama tungeshindana nao, wote sisi tungeliuawa na asingebakia hai Mkristo yeyote ulimwenguni. Kwa jina la Mungu, wakati nilipowaangalia niliziona nyuso ambazo kama zingemuomba Mungu, wangeweza kusogeza milima.

Hafidh: Ulichosema ni kweli kabisa na kinakubaliwa na Waislamu wote, lakini hakina uhusiano na suala tunalojadili, yaani, kwamba Ali alikuwa ameungana kiroho na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Stahili Ya Ali, Fatima, Hasan Na Husein Inathibitishwa Na Aya Ya Maapizano

Muombezi: Ninahoji kutokana na neno “nafsi zetu” katika aya hii tukufu, kwani kutokana na aya hii masuala mengi yanatatuliwa.

Kwanza, njia ya haki iliyolinganiwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) imethibitishwa. Yaani, kama asingekuwa katika upande wa haki, asingethubutu kutoka kuja kwenye shindano wala wale Wakristo maarufu wasingelikimbia kutoka kwenye uwanja wa Mubahila.

Pili, vile vile aya hii huthibitisha kwamba Hasan na Husein walikuwa ni watoto wa Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kama nilivyokwishataja katika mazungumzo yangu katika usiku wa kwanza.

Tatu, huthibitisha kwamba Amiru’l- Mu’minin, Ali, Fatima, Hasan na Husein walikuwa kiroho ndio watu watukufu zaidi miongoni mwa viumbe wote, na wapenzi mno wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwani hata wanachuoni washabiki na wapinzani wakubwa wa madhehebu yenu, kama Zamakhshari, Baidhawi, na Fakhru’d-Din Razi, na wengine wameandika katika vitabu vyao.

Hususani Jarullah Zamkhshari, akiandika kuhusu aya hii tukufu, anatoa maelezo yanayojitosheleza kuhusu kukusanyika kwa “viumbe watano” hawa na kusema kwamba, aya hii ni uthibitisho mkubwa wa ubora wa Ashab-i-Ayba, watu watano ambao walikusanyika chini ya blanketi pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Nne, inaonesha kwamba Amiru’l-Muminin, Ali aliwapita masahaba wengine wote kwa ubora na cheo, kwa sababu Allah amemuita katika aya hii tukufu kama nafsi ya Mtume. Ni dhahiri kwamba, maneno “nafsi zetu” hayamaanishi nafsi ya Mtume mwenyewe, kwa sababu kuita maana yake kumwita mtu mwingine; mtu kamwe haambiwi ajiite mwenyewe. Kwa hiyo, neno hili huelekeza kwa mtu mwingine ambaye ni kama nafsi ya Mtume mwenyewe.

Na kwa vile, kwa mujibu wa maoni ya pamoja ya wafasiri wa kuaminika na muhadithina wa madhehebu zote, hakuna mwingine yeyote isipokuwa Ali, Fatima, Hasani na Husein ndio walikuwepo pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika maapizano, usemi katika aya hii tukufu, “watoto wetu na watoto wenu, wanawake wetu na wanawake wenu” huashiria Hasan na Husein na Fatima kwa mpangilio huo, na mtu mwingine angeweza kutambuliwa kama “nafsi zetu” katika kundi hili tukufu alikuwa ni Amiru’l- Muminin, Ali. Kwa hiyo, maneno haya “nafsi zetu” huthibitisha muungano wa nafsi kati ya Mtume Muhammad na Ali.

Kwa vile mungano halisi wa nafsi mbili hauwezikani, Allah kumuita Ali ‘nafsi’ ya Mtume Muhammad maana yake ni muungano wa kutwaliwa wa nafsi mbili.

Unajua vizuri sana kwamba kimsingi ni bora kulitambua neno kwa dhana ya karibu kuliko na ile ya mbali, na dhana ya karibu sana maana yake kuhusiana katika fadhila zote isipokuwa zile ambazo zimeondolewa kwa sababu fulani. Na tayari tumekuambieni kwamba ni utume maalumu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na upewaji wa Wahyi juu yake, ambavyo ni vitu vya kipekee kwake tu. Kwa hiyo, hatumchukulii Ali kama mshirika wake kuhusiana na sifa hizi mbili.

Lakini kwa mujibu wa aya hii tukufu, Ali anashirikiana pamo- ja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika fadhila nyingine zote, na kwa uhakika Allah (swt) amemjaalia Ali kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa baraka Zake zote. Hii peke yake inathibitisha muungano wa nafsi zao, ambao tulitaka kuuthibitisha.

Hafidh: Kwa nini unasisitiza kwamba aya hii haimaanishi kuita ‘nafsi’ yake mwenyewe? Kwa nini dhana hii isiwe bora kuliko dhana nyingine?

Muombezi: Ni matumaini yangu kwanba hutapoteza muda katika mazungumzo yasiyo na mantiki na kutoka nje ya njia ya uadilifu. Kwa kweli uadilifu huhitaji kwamba kama tumekubaliana juu ya nukta fulani, lazima tuendelee mbele. Sikutegemea mtu wa cheo chako na elimu yako kujiingiza katika mjadala bandia. Kama ujuavyo wewe mwenyewe na kwa mujibu wa wanachuoni wote, nafsi moja inafananishwa na nafsi nyingine kwa njia ya dhana. Miogoni mwa watu wasomi ni kawaida kudai muungano wa dhana, kama nilivyoeleza mwanzo.

Mara kwa mara inaonekana kwamba mtu mmoja anamuambia mwingine: “Wewe ni maisha yangu na nafsi yangu mwenyewe.” Hususan katika lugha ya hadith na simulizi, uhusiano huu mara kwa mara umekuwa ukielezewa kuhusu Amiru’l-Muminin, Ali, na kila simulizi kama hiyo ikuchukuliwa kwa peke yake ni uthibitisho wa kuonesha ukweli wa msimamo wangu.

Simulizi Zaidi Na Hadith Kama Ushahidi Wa Umoja Wa Msingi Wa Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Na Ali

Imamu Ahmad bin Hanbal, katika Musnad yake, Ibn Maghazili, mwanachuoni wa ki-Shafi’i katika Manaqib yake, na Muwafiq Ibn Ahmad Khawarizmi katika Manaqib yake, wanasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali; yeyote anayempenda yeye, amenipenda mimi; na ambaye ananipenda mimi, amempenda Allah.” Vile vile Ibn Maja katika Sunan yake, sehemu ya 1, uk. 92; Tirmidhi katika Sahih yake; Ibn Hajar katika kitabu cha Hadithi cha 5 cha “Hadithi Arobaini” zinazohusu fadhaila za Amiru’l-Muminin zilizosimuliwa katika Sawa’iq kutoka kwa Imamu Ahmad Bin Hanbal, Tirmidhi, Imamu Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i, na Ibn Maja; Imamu Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, juzuu ya 4, uk. 164; Muhamad Ibn Yusuf Ganji Shafi’i katika sura ya 67 ya Kifayatu’t-Talib kutoka Musnad ya Ibn Samak, juzuu ya 4, na Mu’jim Kabir cha Tibrani; na Imamu Abudu’r-Rahman Nisa’i katika Khasa’is, na Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda kutoka kwenye Mishkat – wote wamesimulia kutoka kwa Jash Bin Junada as-Saluni kwamba wakati wa hijja ya muago, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kule Arafa: “ Ali anatokana na mimi, na mimi natokana na Ali. Hakuna mtu anayenifidia mimi (yaani, hakuna awezaye kufanya kazi ya ujumbe wangu) isipokuwa mimi na Ali.”

Sulaimani Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawaddat, sura ya 7, anasimulia kutoka Zawa’id-e-Musnad cha Abdullah Bin Ahmad Bin Hanbal kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumuambia Ummu’l-Mu’minin Salma: “Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali. Nyama yake na damu yake inatokana na nyama yangu na damu yangu. Yuko kwangu mimi kama alivyokuwa Harun kwa Musa. Ewe Umm Salma! Sikiliza, na uwe shahidi kwamba huyu Ali ni bwana na mkuu wa Waislamu.” Hamidi katika kitabu chake Jam’Bainu’s-Sahihain na Ibn Abi’l-Hadid katika Sharhe- Nahju’l-Balagha wanasimulia kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali. Ali kwangu mimi ni kama kichwa kilivyo kwa mwili; mtu anayemtii yeye, ananitii mimi; na mtu anayenitii mimi, anamtii Allah.”

Muhammad Bin Jarir Tabari katika Tafsir yake na Mir Sayyid Ali Hamdani, mwanachuoni wa ki-Shafi’i, katika Muwadda ya 8 cha Muwaddatu’l-Qurba, wanasimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alisema: “Hakika Allah (swt) aliisaidia imani hii ya ki-Islamu kupitia Ali, kwa vile yeye anatokana na mimi, na mimi natokana na yeye, na aya hii tukufu imeteremshwa kwa ajili yake.

‘Basi je, yeye ni kama mtu ambaye ana dalili za wazi kutoka kwa Mola wake na kufuata ushahidi kutoka Kwake?’” (11:17)

Sheikh Sulaimani Balkhi Hanafi ameainisha katika sura ya 17 ya kitabu chake Yanbiu’l-Mawdda kuhusu suala hili hili chini ya maelezo mafupi: “Kuhusu Ali kuwa kama nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hadithi kwamba Ali anatokana na mimi, na mimi natokana na Ali.’” Katika sura hii amesimulia hadithi 24 katika njia tofauti na kwa maneno tofauti kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye alisema Ali alikuwa kama nafsi yake mwenyewe.

Kuelekea mwishoni mwa sura hii, alisimulia hadithi kutoka kwenye Manaqib kama ilivyosimuliwa na Jabir, ambaye alisema kwamba, alimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kwamba, Hadhrat Ali anazo sifa ambazo kwamba kama mtu anakuwa na moja kati ya hizo, ingelitosha kuthibitisha murwa wa mtu huyo na ubora wake.

Na kwa sifa hizo ilimaanishwa hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusiana na yeye kama vile: “Yeyote yule ambaye mimi ni mwenye kumtawalia mambo yake basi huyu Ali ni mwenye kutawalia mambo yake”, au “ Ali yuko kwangu mimi kama alivyokuwa Harun kwa Musa”, au “Ali anatokana na mimi na mimi natokana na Ali” au “Ali yuko kwangu mimi kama nafsi yangu ilivyokuwa kwangu, utii kwake ni utii kwangu”, au “Kupigana dhidi ya Ali ni kupigana dhidi ya Allah, na kufanya amani na Ali ni kufanya amani Allah”, au “Rafiki wa Ali ni rafiki wa Allah, na adui wa Ali ni adui wa Allah”, au Ali ni Hujjat (udhihirisho) wa Allah juu ya viumbe Wake”, au “ Mapenzi kwa Ali ni imani, na uadui dhidi yake ni ukafiri”, au “Kundi la Ali ni kundi la Allah, nakundi la maadui wa Ali ni kundi la Shetani;” au “Ali yuko pamoja na haki, na haki pamoja naye, (na hivyo) havitengani”, au “ Ali ndiye mgawaji wa Pepo na Moto”, au “Mtu anayejitenga na Ali, amejitenga na mimi, na anayejitenga na mimi, anajitenga na Allah”, au “Wafuasi wa Ali wataokolewa Siku ya Hukumu.”

Mwishowe, alinukuu hadithi nyingine yenye maelezo marefu kutoka kwenye Manaqib ambayo mwishoni mwake Mtume anasema: “Naapa kwa jina la Allah ambaye ameweka utume juu yangu, na kunifanya mimi mbora wa viumbe Wake: Ewe Ali! Hakika wewe ni Hujjat (udhihirisho) wa Allah kwa ajili ya watu, mdhamini Wake, mjuzi wa siri Zake, na Khalifa juu ya waja Wake.”

Kuna hadithi nyingi kama hizo kwenye vitabu vyenu. Maneno “nafsi zetu” kwa uwazi huonesha ushirikiano wa karibu kati ya Mtume na Ali katika masuala yote ya ubora.

Nafikiri kwamba aya hii ni ushahidi tosha wa msimamo wangu. Aidha, swali lako la pili linajibiwa na aya hiyo hiyo. Tumethibisha kwamba, ukiondoa utume na Wahyi, ambavyo vinamhusu Mtume tu peke yake, Ali alishirikishwa pamoja naye katika masuala yote ya ubora. Vile vile ina maana kwamba katika sifa za hali ya juu za ubora Ali alikuwa mbora zaidi ya Masahaba na kwa mtu yeyote katika umma huu. Kwa hakika aya hii inathibitisha kwamba anawapita Mitume wote wengine waliopita, kama vile ambavyo Mtume anawapi- ta Mitume wote wengine.

Kwa Vile Mtukufu Mtume Alikuwa Mbora Kwa Mitume Wote Wengine Na Ali Pia Alikuwa Mbora Kwao

Katika Ihya’u’l-Ulum ya Imam Ghazali, Sharhe Nahjul-Balaghah ya Ibn Abil-Hadid Mu’tazil, Tafsir ya Imam Fakhrud-Din Razi, na Tafsir za Jarullah Zamakhshari, Baidhawi, Nishapuri na kadhalika, utaikuta hadith hii ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Wanachuoni wa umma wangu ni kama mitume wa Bani-Israili.” Katika hadith nyingine amesema: “Ulamaa wa umma wa Mtukufu Mtume walikuwa sawa au bora kuliko mitume wa Bani-Israil kwa sababu tu kwamba chanzo chao cha elimu kilikuwa ndio kiini hasa cha elimu, Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.).

Kwa hiyo, Ali ibn Abi Talib bila shaka alikuwa mbora kwa mitume, kwa vile Mtukufu Mtume amesema: “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni lango lake.” Vile vile amesema: “Mimi ni nyumba ya hekima na Ali ni lango lake.” Wakati Ali mwenyewe alipoulizwa kuhusu jambo hili, yeye alieleza baadhi ya vipengele vya ubora wake kwa mitume wa Bani-Israil.

Mnamo mwezi 20 ya Ramadhan, wakati Ali alipokuwa katika kitanda chake cha umauti kufuatia lile shambulizi la Abdul-Rahman Ibn Muljim Muradi, alimtuma Imam Hasan kuwaita wale Mashi’a waliokuwa wamejikusanya kwenye mlango wa nyumba yake. Walipoingia ndani, walikuzunguka kitanda chake huku wakilia kimya kimya. Ali akasema: Mnaweza kuuliza swali lolote mnalolitaka kabla sijakuacheni, lakini maswali yenu yawe mafupi.” Mmoja wa wale waliokuwepo pale alikuwa ni Sa’sa’a bin Suwhan.

Wanachuoni wenu maarufu kabisa kama Ibn Abdul-Birr na Ibn Sa’ad, wameandika kuhusu maisha na tabia yake, wamemtegemea yeye Sa’sa’a, wakithibitisha kwamba yeye alikuwa ni mtu mwenye elimu kubwa.

Sa’sa’a alimwambia Ali: “Naomba unifahamishe ni nani mbora, ni wewe au Adam.” Imam Mtukufu akasema: “Haifai kwa mtu kujisifia mwenyewe, lakini kulingana na kauli adili- fu: ‘Na neema za Mola Wako alizokujaalia zisimulie,’ ninakwambia kwamba mimi ni bora kuliko Adam.” Alipoulizwa ni kwa nini imekuwa hivyo, Ali alieleza kwamba Adam alikuwa na kila namna ya huruma, starehe na neema kwa ajili yake ndani ya Pepo.

Alitakiwa tu kujizuia kutokana na chakula kile kilichokatazwa. Lakini hakuweza kujizuia na akala kutoka kwenye mti ule. Matokeo yake yeye alifukuzwa kutoka peponi. Mwenyezi Mungu hakumkataza yeye Ali kutokana na kula ngano (ambayo, kwa mujibu wa imani ya Kiislam ndio ‘mti’ uliokatazwa).

Lakini kwa kuwa yeye hakuwa na mwelekeo kwenye dunia ya mpito, yeye alijizuia kwa hiari yake mwenyewe kula ngano. (Hoja ya kauli hii ya Ali ilikuwa kwamba ubora wa mtu mbele ya Mwenyezi Mungu ulitegemea kwenye uchamungu na utii, na kwamba kilele cha uchamungu kinaegemea katika kujizuia hata kwa kile ambacho kinaruhusiwa kihalali).

Sa’sa’a akauliza: “Ni nani mbora, wewe ama Nuh?” Ali akajibu: “Mimi ndiye mbora. Nuh aliwalingania watu wake kumuabudu Mwenyezi Mungu lakini hawakutii. Kitendo chao cha aibu kilikuwa ni kumtesa yeye. Yeye aliwalaani na akamuomba Mwenyezi Mungu:

‘Ewe Mola Wangu! usiabakishe hata mtu mmoja juu ya ardhi miongoni mwa madhalimu hawa.’ Baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ingawaje watu walinisababishia matatizo makubwa, mimi sikuwalaani kamwe. niliyabeba mateso yao kwa subira kubwa.” Sa’sa’a akauliza: “Ni nani aliye mbora, wewe ama Ibrahim?” Ali alijibu: “Mimi na mbora, kwani Ibrahim alisema:

‘Mola Wangu! nionyeshe jinsi unavyofufua wafu. (Mungu) Akasema: Kwani huamini? Akasema: Hasha! bali ili moyo wangu utue ..... (2:260) Imani yangu ilikuwa kiasi kwamba nilisema: ‘Hata kama pazia la yale yaliyo ghaibu linge- funuliwa, imani yangu isingeongezeka.’”

Sa’sa’a akauliza: “Ni nani mbora, wewe au Musa?” Imam Mtukufu akajibu: “Mimi ndiye mbora, kwani wakati Mwenyezi Mungu Mtukufu alipomtuma Musa kwenda Misri kumlingania Firauni kwenye haki, Musa alisema: ‘Mola Wangu! Kwa hakika niliuwa mmoja wao, kwa hiyo naogopa wataniuwa. Na ndugu yangu Harun ni fasihi zaidi ulimi wake kuliko mimi. Basi mtume aende pamoja nami kunisaidia, ili anisadikishe. Hakika mimi na hofu watanikadhibisha.’ (28: 33-34)

Mtukufu Mtume aliniagiza mimi, kwa amri ya Allah kwenda Makka kuzisoma aya za Sura ya Al-Bara’a kutoka juu ya Ka’aba kwa makafiri wa Quraishia.

Mimi sikuwa na hofu, ingawaje kulikuwa na watu wachache ambao walikuwa hawajapoteza ndugu yao wa karibu kwa upanga wangu. Kwa kuitii amri yake, niliitekeleza kazi hiyo peke yangu. Nilizisoma aya za al-Bara’at na nikarejea.” Sa’sa’a akauliza tena: “Ni nani mbora, wewe au Isa (ibn Mariam)?” Ali akasema: “Mimi ni mbora, kwani wakati Mariam alipokuwa mjamzito kwa Rehma za Mwenyezi Mungu, na wakati wake wa kujifungua ukakaribia, ulishushwa wahyi kwake: ‘Ondoka katika Nyumba hii tukufu, kwani Nyumba hii ni nyumba ya ibada, sio mahali pa kuzalia watoto.’

Matokeo yake aliondoka kwenye Nyumba tukufu hiyo na akaenda kwenya kichaka ambako alijifungua mtoto Isa. Lakini wakati mama yangu mimi, Fatima binti al-Asad, alipojisikia uchungu wa uzazi ndani ya eneo la Ka’aba tukufu, aling’ang’ania kwenye ukuta na akamuomba Mwenyezi Mungu kwa jina la Nyumba ile na mjenzi wa Nyumba ile, ili apunguziwe maumivu yake. Mara ufa ukajitokeza katika ukuta huo, na mama yangu akasikia sauti ya kimuujiza ikimwambia, “Ewe Fatima! Ingia kwenye Nyumba ya Ka’aba.” Yeye akaingia ndani na mimi nikazaliwa ndani ya Ka’aba tukufu.’”

Kioo Cha Mitume Yote Kama Ilivyoonyeshwa Na Hadith Ya Ufananisho

Imesimuliwa vilevile katika vitabu vya ulamaa wenu kwamba Ali alikuwa ni kioo cha sifa za hali ya juu za mitume wote waliotangulia. Ibn Abil-Hadid Mu’tazili ndani ya Sharhe Nahjul-Balaghah yake, Jz. 11, uk. 449, Hafidh Abu Bakr Faqih Shafi’i, Ahmad bin Husein Baihaqi katika Manaqib, Imam Ahmad bin Hanbal ndani ya Musnad, Imam Fakhrud-Din Razi katika Tafsir al-Kabir kuhusiana na aya ya Mubahila, Muhui’d-Din ndani ya Yawaqit al-Jawhir, suala la 32, uk. 172; Sheikh Suleyman Balkhi Hanafi katika Yanabiul-Mawadda, mwanzoni mwa Sura ya 40 kwa idhini ya Musnad ya Ahmad bin Hanbal, Sahih ya Baihaqi, na Sharhil-Mawaqif wa’t-Tariqatil-Muhammadiyya, Nuru’d-Din Maliki katika Fusulul- Muhimma, uk. 120; kutoka kwa Baihaqi; Muhammad bin Talha Shafi’i ndani ya Matalibus-Su’ul uk. 22; na Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatut-Talib, Sura ya 23, wamesimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pamoja na tofauti kidogo ya maneno, hapa na pale, akisema kwamba: “Yeyote anayetaka kuiona elimu ya Adam, uchamungu wa Nuh, unyenyekevu wa Ibrahim, utukufu wa Musa, au ule utiifu wa Isa (Yesu), anaweza kumuangalia Ali ibn Abi Talib.”

Mir Seyyed Ali Hamadani amesimulia hadith hiyohiyo pamoja na nyongeza kidogo katika Mawaddatul- Qurba yake, Mawadda 8. Anasimulia kutoka kwa Jabir kwamba Mtume (s.a.w.w.) amesema. “Kwa hakika Mwenyezi Mungu amekusanya sifa tisini za mitume kwa Ali, ambazo hakumpa mtu mwingine yeyote.”

Yule Hafidh mkubwa Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i, baada ya kunukuu hadith hii, anatoa maelezo haya: “Ali alikuwa sawa na Adam katika elimu kwa vile Mwenyezi Mungu amemfundisha Adam kila kitu, kama anavyosema ndani ya Qur’ani Tukufu, ‘Na akamfundisha Adam majina .....’(2:31).

Hali kadhalika, Ali alikuwa na elimu ya mambo yote. Kwa sababu ya elimu iliyoshuka moja kwa moja kutoka kwa Allah swt., Adam alipewa ukhalifa wa Allah, kama Qur’ani tukufu inavyosema: “..... Nitajaalia khalifa juu ya ardhi..... (2:30).

Kwa kuwa elimu ya Adam iliongozea kwenye ubora wake, hivyo kwamba hata Malaika walisujudu kwa heshima juu yake, Ali pia alikuwa mtukufu sana wa viumbe wote na khalifa baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Elimu ya Ali ni sawa na ya Nuh kwa vile Ali alikuwa mkali dhidi ya makafiri na mpole kwa waumini. Allah amemsifia ndani ya Qur’ani:

“Na wale walio pamoja naye wana nyoyo imara dhidi ya makafiri, na wapole miongoni mwao wenyewe.” (48: 29).

Huu ni ushahidi mwingine kwamba aya hii ilishuka kwa kumsifia Ali, kama nilivyosema mapema. Nuh alikuwa mkali sana kwa makafiri, kama Qur’ani tukufu anavyosema: “Na Nuh akasema: ‘Mola Wangu! usibakishe hata mkazi mmoja juu ya ardhi miongoni mwa makafiri.’” (71:26).

Ali alikuwa sawa na Ibrahim katika utulivu wa moyo. Qur’ani tukufu inasema: “Kwa hakika, Ibrahim alikuwa mpole sana wa moyo.” (9:114).

Ali alikuwa na sifa zote ambazo Mitume wengine walikuwa nazo mmoja mmoja. Hadithi hii inayokubaliwa na wote huthibitisha kwamba Ali alikuwa na fadhail za hali ya juu sana, ambazo kila moja ya hizo ilikuwa sawa na sifa za juu sana za Mitume. Ni wazi kwamba, mtu ambaye alikuwa na fadhaila za juu sana za mitume wote, basi aliwapita wote kwa cheo. Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 40, ananukuu kutoka kwenye Manaqib ya Khawarizmi kutoka kwa Muhammad Bin Mansur, ambaye alisema kwamba alimsikia Ahmad Ibn Hanbal akisema: “Kulikuwa hakuna sifa kama hizo kwa Sahaba yeyote wa Mtume, kama zilivyokuwa kwa Ali Bin Abu Talib.” Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i vile vile anasimulia maneno yenye maana hiyo hiyo. Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali katika Sharhe-Nahju’l-Balagha, juzuu ya 1, uk. 46, anasema: “Ali alikuwa ndiye mtu mwenye kufaa sana katika nafasi ya Wilaya (Ulinzi) kwa fadhaili za ubora wake. Ukimuondoa tu Mtume wa Allah, alikuwa ni mtu mwenye kustahiki sana kwa cheo cha Khalifa.”

Ali kwa hakika alikuwa mwenye kustahiki zaidi kwa Ukhalifa, lakini aliwekwa kando kwa mbinu za kisiasa za watu duni. Angalau wangelimjulisha Ali kwamba walikuwa wakifanya mkutano huko Saqifa Bani Sa’da kuangalia juu ya suala muhimu la kumchangua Khalifa. Hawakufanya hivyo ili kumnyima haki yake ya urithi.

Kukubaliwa Kwa Abu Bakr Na Watu Wote

Hafidh: Je, sisi ni madhalimu au ni wewe? Unasema kwamba masahaba waliwachagua wale ambao wamepora Ukhalifa. Kwa hakika unafikiri kwamba sisi ni wajinga ambao kibubusa tunawafuata wazee wetu. Lakini kuna uthibitisho gani wenye nguvu kama “Ijma” – makubaliano ya wote kwa ujumla? Masahaba wote na Umma, pamoja na Ali, walimchagua Abu Bakr na wakala kiapo cha utii kwake.

Kwa hakika makubaliano ya pamoja ya watu ni ya mwisho na kukubaliana nayo ni lazima. Mtume alisema: “Watu wangu hawakubaliani katika (jambo lenye) kosa; watu wangu hawakubaliani katika upotofu wa kutoka kwenye njia iliyonyooka.” Hivyo hatukuafuata wazee wetu kibubusa. Ukweli ni kwamba katika siku ya kwanza baada ya kifo cha Mtume, Umma kwa pamoja uliamua katika mkutano kumsimamisha Abu Bakr kama Khalifa. Kwa sababu ilikuwa ni ukweli uliokubaliwa, lazima na sisi tuukubali.

Mumbezi: Tafadhali tujulishe Ukhalifa umeegemezwa katika misingi ipi?

Hafidh: Iko wazi. Uthibitisho mzuri wa kuwepo ukhalifa baada ya Mtume ni “Ijma” (makubaliano ya wote kwa ujmla) ya Umma ambayo kwayo ukhalifa umekuja kupatikana. Mbali na haya, sifa bora sana kwa Abu Bakr na Umar kwa ajili ya ukhalifa ilikuwa ni kuko- maa kwao kiumri. Ali, pamoja na fadhaili zote na ukaribu kwa Mtume, ilikuwa arukwe kwa sababu ya ujana wake.

Na, ili kuwa waadilifu na wenye haki, haikuwa sawa kwa kijana kuyaweka pembeni madai ya masahaba watu wazima. Na hatuchukilii kuachwa huku kwa Ali kama ni kushindwa kwake, kwani ubora wake kwa upande mwingine hukubaliwa na wote. Vile vile kuna hadithi iliyosimuliwa na Khalifa Umar kutoka kwa Mtume, ambaye alisema: “Utume na uongozi haviwekwi pamoja katika familia moja.” Kwa hiyo, Ali alinyimwa ukhalifa kwa sababu anatokana na familia ya Mtume. Alikuwa hafai kwa ajili ya cheo hicho.

Hoja Dhidi Ya Uhalali Wa “Ijmai”

Muombezi: Nimeshangaa kwamba unaweza kuleta hoja za kijinga kama hizi. Kwanza, unasema kwamba Ijmai, makubaliano ya Umma, ndio hoja yenye nguvu zaidi, na kwa kuunga mkono nukta yako umesimulia hadithi. Neno ‘ummai’ maana yake ‘umma wangu,’ hivyo hadithi hiyo (tujaalie kuwa ni ya kweli) inamaniisha kwamba wakati umma wote unapokubaliana kwenye jambo fulani, uamuzi wao hauwezi kuwa na makosa. Siwezi kukubaliana na hili. Allah aliutofautisha ummah huu kwa sababu ya ukweli kwamba mion- goni mwao kutakuwepo na kundi lililoongoka. Mwakilishi wa Allah atakuwa miongoni mwao. Wakati umma unapokusanyika pamoja, kundi lile lililoongoka litakuwa miongoni mwao.

Lakini hadithi hii (hata kama ni ya kweli) haioneshi ushahidi wowote kwamba Mtume aliitoa haki yake mwenyewe na kuruhusu ummah kuchagua Khalifa. Na hata kama Mtume alikuwa ameuchia ummah kuchagua Khalifa, haki hii itakuwa inaachiwa ummah wote. Kwa vile Waislamu wote hunufaika kutokana na Ukhalifa, lazima wangelikuwa na haki ya kuelezea maoni yao katika kumchagua Khalifa. Kwa hiyo, kukusanyika kwa ummah wote baada ya Mtume kufariki kungelikuwa muhimu ili kwamba kwa idhini yao ya pamoja, mtu mkamilifu angeweza kuchaguliwa kuwa Khalifa. Je, kulikuwapo na mkusanyika kama huo wa Waislamu? Je, hii ndiyo njia ambayo Abu Bakr aliyofikia kuwa ukhalifa?

Hafidh: Abu Bakr alibakia kwenye ukhalifa kwa zaidi kidogo ya miaka miwili. Wakati wa kipindi hiki Waislamu kwa jumla walikula kiapo cha utii kwake. Hii yenyewe ina maana ya maoni ya pamoja miongoni mwao, ambayo ni uthibitisho wa uhalali wa Ukhalifa wake.

Muombezi: Unajaribu kuliepuka suala lenyewe. Swali langu halikuwa kuhusu kipindi chote cha Abu Bakr. Nilikuwa nauliza kuhusu uamuzi uliochukuliwa katika Saqifa ya Bani Sa’da. Je, mkusanyiko ule pale ulikusanya ummah wote, au kulikuwa na watu wachache tu ambao walikula kiapo cha utii?

Hafidh: Ni dhahiri kwamba kulikuwa na masahaba wachache mashuhuri wa Mtume, laki- ni baadae Ijmai ilipita.

Muombezi: Je, Mtume, mtu anayefaa zaidi kuongoza ummah, aliitoa haki yake kwa upande wa ummah wake? Je, alitoa haki yake ili kwamba watu wa ukoo wa Aus, ambao walikuwa maadui kwa ukoo wa Khazraj, wale kiapo cha utii kwa ajili ya hofu ya maadui wao kushika madaraka? Je, aliacha haki yake ili kwamba watu wake waunde serikali kwa misingi ya hofu na ulafi? Je, unaweza kuita kikundi hiki kidogo cha watu kuwa ndio ummah? Je, Waislamu wa Makka, Yemen, Jeddah na miji mingine hawakuwa sehemu ya ummah? Je, hawakuwa na haki ya kutoa maoni yao kuhusiana na ukhalifa? Kama kulikuwa hakuna hila, kwa nini wasingojee na kupata msimamo wa Waislamu wote katika suala muhimu kama hili la Ukhalifa? Katika njia hii, Ijmai kwa maana yake halisi ingewza kupatikana. Hata leo, ili kusimamisha serikali ya kidemokrasi au kuchagua kiongozi wa taifa, hufanyika uchaguzi mkuu.

Wananchi wanapiga kura zao, na kiongozi anachaguliwa kwa wingi wa kura. Viongozi wa nchi zilizostaarabika na watu wote wastaarabu watauche- ka utaratibu wenu huu wa “Ijmai” usio na mpangilio mzuri.

Hafidh: Kwa nini unajiigiza katika mazungumzo yasiyopendeza? Ijmai ina maana kwamba kulikuwa na mkusanyiko wa watu wenye akili na masahaba wakubwa ambao waliku- tana ndani ya Saqifa. Muombezi: Unasema kwamba Ijmai ilimaanisha kwamba kulikuwa na mkusanyiko wa watu wenye akili na masahaba wakubwa wa Mtume, lakini huna msingi wowote kwa maelezo haya isipokuwa hadithi uliyoitaja. Ni wapi hadithi imetaja watu wenye akili au masahaba wakubwa? Narudia kwamba neno “umma” maana yake ni umma wote, sio idadi ndogo ya Masahaba, hata kama wakiwa wana elimu.

Hata kama unayosema yakiwa ni kweli, kwamba “Ijmai” maana yake “mkusanyiko wa watu wenye akili na masahaba wakubwa,” je, watu wenye akili na masahaba wakubwa wa Mtume walikomea kuwa ni hao watu wachache tu ambao walikusanyika chini ya paa dogo la Saqifa siku hiyo? Je, kulikuwa hakuna watu wengine wenye akili na masahaba wakubwa katika ulimwengu wa ki-Islamu? Na je, wote kwa pamoja walipiga kura kwa ajili ya Khalifa?

Hafidh: Kwa vile suala la Khalifa lilikuwa ni jambo nyeti, watu walikuwa wanahofia kwamba huenda kukatokea machafuko. Ilikuwa haiwezekani kuwaarifu Waislamu katika sehumu nyingine. Wakati Abu Bakr na Umar waliposikia kwamba baadhi ya Ansar wamekusanyika kule, na wao vile vile walikwenda kule kuzungumza. Kwa sababu Umar alikuwa mwanasiasa mweledi, aliona kwamba inafaa kwa ummah kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr.

Wengine walimfuata na kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr, lakini kikundi cha Ansar na watu wa ukoo wa Khazraj wanaomuunga mkono Sa’d Bin Ubaida, hawakula kiapo cha utii na wakaondoka Saqifa. Hiyo ndio ilikuwa sababuya kwa nini walifanya haraka.

Muombezi: Hivyo na wewe unakubali, kama wanahistoria na maulamaa wenu walivyokubali, kwamba katika siku ya Saqifa, wakati mashauri ya msingi yalipokuwa yanafanyika kulikuwa hakuna “Ijmai”. Kwa ajili ya maslahi ya kisiasa, Abu Bakr alimpendekeza Umar na Abu Ubaida Bin Jarra, na wao pia, kwa kulirudisha pendekezo hilo, wal- itaja jina la Abu Bakr, wakimuambia kwamba yeye anastahiki zaidi kwa nafasi hiyo. Wao mara moja tu wakala kiapo cha utii kwake.

Baadhi ya watu wa ukoo wa Aus waliokuwa pale vile vile walikula kiapo cha utii kwa Abu Bakr kwa msimamo wao wa uadui dhidi ya ukoo wa Khazraj, na vile vile walihofia kwamba Sa’d bin Ubaida angeweza vinginevyo kuwa Amir. Kwa njia hii uungaji mkono ulipanuka na kuwa mkubwa. Hata hivyo, kama Ijmai ingekuwa ni hoja yenye nguvu kuweza kutegemewa, wangelisubiri mpaka umma wote – au, kama ulivyosema: watu wenye akili – wakusanyike pale kupata idhini ya umma wote.

Hafidh: Nimekuambia kwamba hofu ya machafuko ililazimisha kundi hili kutenda kama walivyofanya. Watu wa ukoo wa Aus na Khazraj wamekusanyika katika Saqifa na walikuwa wakigombana wenyewe kwa wenyewe. Kila mmoja wao anataka kuamua uhuru wa dola ya ki-Islamu kwa ajili yao wenyewe.

Muombezi: Nakubaliana na unayoyasema. Muhammad Bin Jarir Tabari (tazama Ta’rikh yake, Jz. 2, uk. 457) na wengine wameandika kwamba, Waislamu hawakukusanyika chini ya Saqifa kumchagua Khalifa wao. Koo za Aus na Khazraj zilitaka kujichagulia Amir wao wenyewe. Abu Bakr na Umar wakanufaika kutokana na tofauti zao. Kama kweli walikusanyika kujadili Ukhalifa, kwa kweli wangeliwaita Waislamu wote kutoa maoni yao juu ya suala hilo. Kama ulivyosema: Hawakuwa katika hali ya kuweza kuwajulisha Waislamu wote, na muda ulikuwa unakimbia. Ilikuwa kweli kwamba walikuwa hawana mawasiliano ya mara moja na Makka, Yemen, Ta’if, au miji mingine ya mbali ya Waislamu.

Lakini je, walikuwa hawana hata njia ya kuwasiliana hata na Jeshi la Usama Bin Zaid, ambalo lilikuwa limepiga kambi nje kidogo ya Madina? Hivi wasingeweza kuwaarifu masahaba wakubwa wa Mtume ambao walikuwa kule? Mmoja wao alikuwa mtu maarufu, Kamanda wa jeshi la Waislamu, aliyechguliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Abu Bakr na Umar walikuwa chini yake.

Wakati Usama aliposikia kwamba, kwa hila watu watatu wamemchagua Khalifa bila kuwashauri watu wengine, au hata kuwajulisha, na kwamba walikuwa wamekula kiapo cha utii kwa mtu moja, alipanda farasi wake mpaka kwenye mlango wa Msikiti na akesema kwa sauti kubwa: “Vurugu yote hii ni ya nini? Kwa amri ya nani mmemchagua Khalifa? Kulikuwa na umuhimu gani, wa watu wachache ambao bila kuwashauri masahaba, wamemchagua Khalifa?”

Umar akajitokeza mbele kumtuliza na kusema: “Usama! Kazi hiyo imekwisha. Kiapo cha utii kimekwishatolewa. Usisababishe vurugu sasa miongoni mwa watu.

Na wewe mwenyewe pia ule kiapo cha utii.” Usama akakasirika, na kusema: “Mtume amenifanya mimi Amir wenu,” akasema. “Inawezekana vipi Amir aliyeteuliwa na Mtume atoe heshima ya utii kwa watu wa chini ambao waliwekwa chini ya amri yake?” Ingawa mengi zaidi yalitokea, kiasi hiki kidogo kinatosha kuthibitisha hoja yangu.

Ali Alikosa Kuarifiwa Kwa Makusudi Kuhusu Mkutano Wa Saqifa

Kama unasema kwamba Jeshi la Usama vile vile lilikuwa mbali na mji wa Madina na kwamba muda ulikuwa unakimbia, je, utadai kwamba umbali kutoka Saqifa na Msikitini na kwenye makazi ya Mtume vile vile ulikuwa mkubwa? Kwa nini hawakumuarifu Ali, au Abbas ami yake Mtume mwenye kuheshimiwa? Kwa nini hawakuwashauri Bani Hashim, kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Hafidh: Katika namna zote hali wakati ule ilikuwa ngumu kiasi kwamba hawakuthubutu kuwa wazembe na kuondoka Saqifa.

Muombezi: Samahani, walikuwa nao muda wa kutosha. Waliacha makusudi kumuarifu Ali, Bani Hashim, na masahaba wakubwa.

Hafidh: Unasemaje kwamba walifanya makusudi kuacha kuwaarifu?

Muombezi: Dalili moja ya wazi ni kwamba Umar alifika kwenye mlango wa nyumba ya Mtume lakini hakuingia ndani. Hafidhi: Kwa hakika kisa hiki kimebuniwa na Marafidhi.

Muombezi: Angalia ukurasa wa 456 Ta’rikh, ya Muhammad Bin Jarir Tabari, Jz. 2, mmoja wa Maulamaa wenu wakubwa. Anaandika kwamba Umar alifika mlangoni kwa nyumba ya Mtume lakini hakuingia ndani. Alituma ujumbe kwa Abu Bakr: “Njoo haraka; nina shughuli muhimu na wewe.” Abu Bakr akamtumia jibu kwamba hakuwa na muda. Umar akutuma ujumbe mwingine: “Tunakabiliwa na mgogoro. Kuwepo kwako ni muhimu.” Abu Bakr akatoka nje na Umar akamueleza kwa siri kuhusu kukusanyika kwa Ansar ndani ya Saqifa na akasema kwamba walipaswa kwenda huko mara moja.

Wote wakaondoka, na njiani wakakutana na Abu Ubaida wakamchukuwa na kuongozana naye. Kwa ajili ya Allah hebu jaribu kuwa muadilifu. Kama walikuwa hawakupanga njama, kwa nini Umar aende mpaka kwenye mlango wa nyumba ya Mtume na kisha asiingie ndani? Wangeliweza kuomba msaada. Je, katika Umma wote alikuwepo Abu Bakr tu, ambaye alikuwa na hakima zote, na kwamba masahaba wengine na kizazi cha Mtume walikuwa ni wageni ambao hawakustahiki kujulishwa kuhusu suala hili?

Je, Ijma yenu hii kwa haki inaundwa na watu watatu? Ni wapi katika sehemu yoyote ya ulimwengu ambako utaratibu kama huu unakubalika? Tuchukulie kwamba watu watatu au kikundi chochote cha watu, wakakusanyika katika mji na wakaunda Ijma na kisha wakamchagua kiongozi wa nchi.

Je, ni wajibu juu ya Maulamaa na wasomi wa miji mingine yote kuwatii? Au hata kama baadhi ya watu wenye ujuzi na wasomi ambao hawakuchaguliwa na wengine kutoa mawazo, je, ni lazima kwamba wasomi na maulamaa wote waliobakia wawafuate wao? Je, ni sahihi kukandamiza hisia za umma wote kwa tabia ya vitisho vya kundi moja la watu? Kama kwa upande mwingine, katika mijadala ya kielimu, kundi la watu wakafichua kwamba Ukhalifa haukithibitshwa na sheri za dini au za asili, ni haki kuwaita Rafidhi?

Unasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliliacha suala la Ukhalifa juu ya umma au kwa “wasomi” wa Umma, kama unavyoita. Je, wasomi wa Umma wanaundwa na Abu Bakr, Umar na Abu Ubaida Jarra? Kila mmoja akipendekeza jina la mwingine, na kisha wawili kati yao wakamkubali wa tatu. Na hiyo ikawa mwisho. Je, ni wajibu kwa Waislamu wote kuwafuata wao? “Wachache,” “wengi,” na “Ijma” humaanisha vitu tofauti kabisa.

Kama mkutano wa kushauriana unafanywa kwa ajili ya kuangalia tatizo fulani, na idadi ndogo ya watu ikatoa wazo moja, ambapo ile idadi kubwa ya watu ikatoa wazo jingine, kisha inasemwa kwamba, moja ni maoni ya wachache. Maoni ya idadi kubwa ya watu yanaitwa maoni ya wengi, na kama wote (bila tofauti yoyote) wakatoa kauli moja, inaitwa “Ijmai”.

Je Ijmai ilifikiwa ndani ya Saqifa au baadae Msikitini, au baada ya hapo katika mji wa Madina? Kama, hata hivyo, kwa kustahi matakwa yako, tukiondolea mbali haki za umma wote na kusema kwamba maoni ya wasomi na masahaba wa Mtume yalikuwa yanatosha kwa ajili ya Ijmai, nauliza je! Kulikuwa na Ijmai amabayo kwamba wasomi wote na masahaba mashuhuri wa Mtume walishiriki? Je, kikundi kidogo kile kule Saqifa kilikubaliana wote katika maoni yao? Jawabu lake lazima litakuwa ni hapana. Mwandishi wa “Mawaqif” mwenyewe amekiri kwamba kulikuwa hakuna Ijmai wakati wa Ukhalifa wa Abu Bakr, na kwa yakini vile vile kulikuwa hakuna maoni ya wote miongoni mwa wanachuoni wa Madina. Sa’d Bin Ubaida Ansari, kizazi chake, masahaba mashuhuri wa Mtume, Bani Hashim wote, rafiki zao, na Ali Bin Abu Talib, - wote walimpinga Abu Bakr kwa muda wa miezi sita. Watu hawa katu hawakula kiapo cha utii kwake.

Mjini Madina, makazi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hakuna Ijmai iliyofikiwa ambayo kwayo wasomi na masahaba walimuunga mkono Abu Bakr kama Khalifa. Wanahistoria wenu mashuhuri wenyewe, kama Imamu Fakhru’d-Din Razi, Jalalu’d-Din Suyuti, Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali. Tabari, Bukhari na Muslim, wameandika kwamba Ijma kamwe haikutokea hapo Madina.

Bani Hashim, Bani Umayya, na masahaba kwa ujumla – isipokuwa hao watu watatu walio- taja hapo juu – hawakuwepo Saqifa ili kupiga kura zao. Aidha, wengi waliupinga uamuzi huo kwa nguvu sana. Kusema kweli, baadhi ya masahaba wakubwa ambao walikataa kula kiapo cha utii kule Saqifa, walikwenda msikitini na kulalamika kwa Abu Bakr. Miongoni mwa muhajirina walikuwa ni; Salman Farsi, Abu Dharr Ghifari, Mikidadi bin Aswad Kindi, Ammar-e-Yasir, Buraida Aslami, na Khalid Bin Sa’id Bin Aas Amawi.

Miongoni mwa Ansari walikuwa; Abu’l-Hathama bin Tihan, Khuzaima Bin Thabit Dhu’sh- Shahadatain, Abu Ayyub Ansari, Ubai bin Ka’b, Sahl Bin Hunaif, Uthman Bin Hunaif, ambao walipingana na Abu Bakr ndani ya Msikiti. Nimetoa tu kwa mukhtasari mfupi juu ya matukio haya.

Hakuna Ijmai ya aina yoyote iliyofikiwa. Ijma inayosemwa ya wasomi na masahaba mashuhuri wa Madina ni uwongo mtupu.

Kwa kutegemea juu ya vyanzo vyenu wenyewe, nitakupa ordha ya majina ya wale ambao walipinga Ukhalifa. Ibn Hajar Asqalani na Baladhuri, kila mmoja katika Ta’rikh yake, Muhammad Bin Khawind Shah katika kitabu Rauzatu’s-Safa, Ibn Abdu’l-Birr katika Isti’ab na wengine wanasema kwamba , Sa’d Bin Ubaida na sehemu ya Makhawarij na kikundi cha Makuraishi hawakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr.

Aidha, watu kumi na nane ambao walikuwa Masahaba wakubwa na mashuhuri wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hawakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Walikuwa ni Mashi’a wa Ali Bin Abu Talib. Majina ya watu hao kumi na nane ni haya yafuatayo:

1. Salman Farsi 2. Abu Dharr Ghifari 3. Mikidadi Bin Aswad-e-Kindi 4. Ammar Yasir 5. Khalid Bin Sa’idbin al-Aas 6. Buraida Aslami 7. Ubaid Bin Ka’b 8. Khuzaima Bin Thabit Dhu’sh-Shahadatain 9. Abu’l-Hathama Bin Tihan 10. Sahl Bin Hunaif 11. Uthmani Bin Hunaif Dhu’sh-Shahadatain 12. Abu Ayyub Ansari 13. Jabir Ibn Abdullah Ansari 14. Hudhaifa bin Yaman 15. Sa’d Bin Ubaida 16. Qais Bin Sa’d 17. Abdullah Bin Abbas 18. Zaid Bin Arkam

Na Yakubi anaandika katika Ta’rikh yake: “ Kikundi cha Muhajirina na Ansari kilijitenga bila kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr, na walikuwa ni wafuasi wa Hadhrat Ali. Miongoni mwao walikuwa ni Abbas Bin Abu’l-Muttalib, Fazl Bin Abbas, Zubair Ibnu’l-‘Awwam Bin As, Khalid Bin Sa’id, Miqdadi Bin Umar, Salman Farsi, Abu Dharr Ghifari, Ammar Yasir, Bara’a Bin Azib, na Ubai Bin Ka’b.

Je, watu hawa hawakuwa wasomi wa Umma? Ali, Abbas, ami yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na watu wengine mashuhuri wa ukoo wa Bani Hashim – je, watu hawa hawakuwa ni wenye busara na waaminifu? Ilikuwa Ijma ya aina gani hiyo, ambayo ilifanyika bila ushauri wa watu hawa? Wakati Abu Bakr anachaguliwa kwa siri siri, na Masahaba wengine mashuhuri hawakujulishwa, je, hii inakuwa ni Ijma? Au ni njama za kisiasa?

‘Hadith Thaqalain’ Na ‘Hadith Safina’

Aidha, Bani Hashim, familia ya Mtume, hawakuwepo pale Saqifa. Uamuzi wao wa thamani hauwezi kukataliwa kwa mtazamo wa hadithi iliyosimuliwa katika mikesha iliyopita, na inayokubaliwa na madhehebu zote. Mtukufu Mtume alisema: “Ninakuachieni kati yenu vitu viwili vizito: Kitabu cha Allah (Qur’ani Tukufu) na Ahlul Bayt wangu (watu wafamilia tukufu: Ali, Fatimah, na kizazi chao).

Kama mkishikama na viwili hivi, kamwe, kamwe hamtapotea baada yangu.” Watu hawa hawakuunga mkono Ukhalifa wa Abu Bakr. Kwa nyongeza, kuna hadithi nyingine mashuhuri ijulikanayo kama Hadith- e-Safina, ambayo niliitaja katika mikesha iliyopita.

Mtume alisema: “Ahlul Bayt wangu ni kama safina ya Nuh. Yeyote anayeipanda ameokolewa, na anayeipa mgongo ameangamia.” Hadithi hii inaonesha kwamba, kama ambavyo watu wa Nuh waliokolewa kutokana na mafuriko makubwa kwa Safina yake, watu wa Mtume wetu wataokolewa kutokana na mabalaa kwa kushikamana na watu wa familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Ibn Hajar katika kitabu chake “Sawa’iq-e-Muhriqa”, Sura ya 50, akifafanua juu ya aya ya 4, (kati ya aya tano anazofafanua), ananukuu hadithi mbili kutoka kwa Ibn Sa’d kuhusu wajibu wa kuwafuata Ahlul Bayt watukufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Katika moja ya hadithi hizo Mtume alisema: “Mimi na Ahlul Bayt wangu ni mti wa Peponi ambao matawi yake yako katika ardhi; hivyo mwenye kutafuta njia ya kuelekea kwa Allah lazima ajiambatan- ishe nao.”

Katika hadithi ya pili Mtume alisema: “Miongoni mwa Umma wangu katika kila zama kuna watu waadilifu kutoka kwenye Ahlul Bayt wangu ambao huondoa uchafu unaoletwa kwenye dini na watenda maovu na ambao hufutilia mbali madai ya uwongo ya wenye kuchupa mipaka na tafsir za watu wasio elimika.

Naifahamike kwenu kwamba Maimamu wenu kwa hakika ndio wale ambao wataokuelekezeni kwa Allah. Hiyvo lazima muwe waangalifu kuhusu wale mnaowachukuwa kuwa viongozi wenu.”

Kiini cha hadithi za aina hii ni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anauambia Umma wake: “Mpaka muwafuate Ahlul Bayt wangu, vinginevyo maadui watakupotezeni.” Watu ambao wangeweza kushawishi Ijmai, kiapo cha utii, na uteuzi wa Khalifa, walipinga utaratibu ulioulezea.

Sasa hiyo ilikuwa ni Ijmai ya aina ngani? Masahaba wakubwa, wasomi, na kizazi cha Mtume walikuwepo hapo Madina wakati wa Saqifa. Hivyo hakuna shaka kwamba suala hili halikuamuliwa kwa wingi wa kura, wachilia mbali Ijma. Ibn Abdu’l-Birr Qartabi, mwanacuoni mkubwa wa madhehebu yenu, katika kitabu chake “Isti’ab”, Ibn Hajar katika “Isaba”, na Maulamaa wengine wanaandika kwamba, Sa’d Bin Ubaida, ambaye alikuwa ni mgombea wa Ukhalifa, kwa msimamo mkali kabisa alikataa kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr na Umar. Hakutaka kusababisha vurugu, hivyo aliondoka na kwenda Syria.

Kwa mujibu wa riwaya katika “Rauzatu’s-Safa”, kwa uchochezi wa mtu maarufu, yeye aliuawa. Kwa mujibu wa wanahistoria, mtu ambaye alitenda jinai hiyo ni Khalid Bin Walid. Baada ya kumuua Malik Bin Buwaira na kumuoa mke wake, wakati wa mwanzo wa Ukhalifa wa Abu Bakr, Umar akawa ni mwenye kumchukia sana, wakati Umar alipokuwa khalifa, Khalid akamuua Sa’d Bin Ubaida kwa ajili ya kutaka kupata upendeleo wa Umar.

Hafidh: Kwa vile kulikuwa na hatari ya vurugu, na hawakuweza kupata mawasiliano kwa umma wote, walilazimika kutegemea juu ya hao watu wachache waliokuwepo Saqifa ambako kiapo cha utii kilichukuliwa. Baadaye Umma waliuridhia (Ukhalifa huo).

Muombezi: Kama kulikuwa hakuna njia za kuwasiliana na Masahaba mashuhuri wa Mtume (saw), na wasomi wa Umma ambao walikuwa nje ya Madina, tafadhali tuambie kwa ikhlasi: Kama kulikuwa hakuna njama katika suala hili, kwa nini wasiwaite wale walio kuwepo mjini Madina kwenye mkutano wa Saqifa? Je, haikuwa ni muhimu kwao kupata ushauri wa Abbas, Ali ibn Abu Talib, na Bani Hashim? Je, maoni ya Umar na Abu Ubaida Bin Jarra yalitosha kwa ulimwengu wote wa ki-Islam? Hoja yako iliyotegemea juu ya Ijma, iwe ya jumla au makhususi, haikubaliki. Wasomi na Masahaba wakubwa hawakushiriki kwayo, badala yake waliipinga.

Kama nilivyosema: ‘Ijmai’ maana yake ni kwamba asiwepo hata na mtu mmoja ambaye hakubaliani na wengine. Katika ‘Ijma’ hii umekiri kwamba wasomi kwa ujumla hawakushiriki. Imamu Fakhru’d-Din Razi katika “Nihayatu’l-Usul” anasema kwamba, kulikuwa hakuna Ijmai ya makubaliano katika Ukhalifa wa Abu Bakr na Umar, mpaka baada ya kuuawa kwa Sa’d Bin Ubaida.

Nashindwa kuelewa vipi unaiita Ijmai hii ya kuwazika kuwa ni uthibitisho kwa ajili ya uhalali wa Ukhalifa. Dai lako la pili, kwamba Abu Bakr alikuwa mtu mzima kuliko Ali na kwa hiyo alikuwa anafaa zaidi kwa ajili ya Ukhalifa ni dhaifu kuliko hoja ya kwanza.

Kama umri ulikuwa sharti juu ya Ukhalifa, basi walikuwepo watu wazima wengi kuliko Abu Bakr na Umar. Kwa hakika Abu Qahafa, baba yake Abu Bakr alikuwa mkubwa kuliko mtoto wake, na alikuwa yu hai wakati ule. Kwa nini asichaguliwe kuwa Khalifa?

Hafidh: Umri wa Abu Bakr ukiungana na uwezo wake, ulimfanya kuwa chaguo la sawa sawa. Wakati kulikuwa kuna mzee, mwenye ujuzi, mtu anayependwa na Mtume katika Umma, kijana mdogo asiye na uzoefu hawezi kupewa amana ya uongozi.

Muombezi: Kama hiyo ingekuwa ni kweli, basi shabaha ya upinzani wako ni Mtume mwenyewe. Wakati alipoondoka kwenda kwenye vita vya Tabuk,wanafiki kwa siri walipanga kufanya maasi mjini Madina wakati akiwa hayupo. Kwa hiyo aliteua mtu mzoefu kushika nafasi yake ili aweze kudhibiti hali mjini Madina na kuivunja ile mipango ya wanafiki. Nakuomba utueleze, Mtume alimuacha nani katika nafasi yake mjini Madina kama mrithi na Khalifa wake?

Hafidh: Inajulikana sana kwamba alimfanya Ali khalifa na mrithi wake.

Muombezi: Je, Abu Bakr, Umar na masahaba wengine wazee zaidi hawakuwepo Madina wakati huo? Ndio. Na bado Mtume akamfanya kijana mdogo, Ali, kuwa Khalifa na mrithi wake.

Kwa ajili ya kusoma baadhi ya aya za Sura ya Al-Bara’a, ya Qur’ani Tukufu kwa watu Makka, mtu pengine angefikiri kwamba, mtu mzoefu lazima angekuwa anafaa kwa kazi hiyo. Lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimurudisha mzee Abu Bakr kutoka kwenye nusu ya safari yake, na akamuamuru yule kijana mdogo, Ali kutekeleza jukumu hili muhimu. Mtukufu Mtume akasema kwamba Allah amemwambia kwamba mtu wa kuwasilisha hiyo Qur’ani tukufu lazima awe ni yeye mwenyewe Mtume au mtu ambaye anatokana naye.

Halikadhalika, kwa ajili ya kuwaongoza watu wa Yemen, kwa nini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtuma Kiongozi wa Waumini Ali badala ya mzoefu zaidi Abu Bakr, Umar, au wengine waliokuwepo pale? Na katika matukio mengi kama haya, wakati wakiwepo Abu Bakr, Umar na wengine, alimteua Ali kutekeleza majukumu makubwa.

Hivyo ina maana kwamba ukhalifa unaousisitiza ni ustahili. Imenijia hivi punde tu kwamba uthibitisho wa nguvu wa kukataliwa kwa ukhalifa wa watu hawa ni upinzani wa ile inayoitwa ijmai kwa Ali, ambaye kwa mujibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alikuwa ni mwenye kubainisha kati ya haki na batili.

Maulamaa wenu mashuhuri wamesimulia hadithi nyingi kuhusiana na suala hili. Sheikh Suleimani Balhki Hanafi katika kitabu chake “Yanabiul-Mawadda”, Sura ya 16 akinukuu kutoka “Kitabu’s-Sabi’in-Fi- Fadha’il-e-Amiru’l-Mu’minin,” Imamu’l-Haram Abu Ja’far Ahmad bin Abdullah Shafi’i, katika hadithi ya 12 iliyosimuliwa kutoka Firdaus ya Dailami ya hadithi ya sabini, Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i katika Mawaddatu’l-Qurba, Mawadda ya 6, Hafidh katika kitabu chake “Amali”, Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika kitabu chake “Kifayatu’t-Talib,” Sura 44 anasimulia pamoja na hitilafu ndogo kati- ka maneno, kutoka kwa Ibn Abbas, Abi Laila Ghifari, na Abu Dharr Ghifari kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema (kifungu cha mwisho kikiwa sawa katika kila hadithi): “Punde tu baada ya kuondoka kwangu kwenye ulimwengu huu, yatatokea machafuko.

Wakati yakitokea, lazima mumfuate Ali Bin Abi Talib kwa vile atakuwa mtu wa kwanza kukutana na mimi na kupeana mikono na mimi katika Siku ya Hukumu. Yeye ametukuka kwa daraja na ni mwenye kubainisha kati ya haki na batili.”

Wakati Mtume alipofariki, machafuko makubwa yalitokea. Muhajirina na Ansar walitaka kupata Khalifa kutoka upande wao. Kwa mujibu wa maelekezo ya Mtume, Umma uli- paswa kumleta Ali ili kwamba aweze kubainisha kati ya haki na batili.

Hafidh: Hadith hii ina simulizi pekee (Hadith Ahad) na kwa hiyo si ya kutegemewa.

Muombezi: Nilikwisha jibu pingamizi lako kuhusu hadithi pekee. Maulamaa wa ki-Sunni huchukulia hadithi kama hiyo kama hoja ya msingi, hivyo huwezi kuikataa katika misingi hiyo. Mbali na hilo, sio hadithi hiyo pekee katika jambo hili.

Kuna riwaya nyingi kama hizo zilizosimuliwa na Maulamaa wenu wenyewe ambazo zinaelekeza kwenye maana hiyo hiyo, ambzo baadhi yake nimezitaja katika mikesha iliyopita. Kwa kuzingatia kikwazo cha muda wetu kuwa mfupi, nitakomea katika kutaja tu hapa baadhi ya majina ya waandishi. Moja ya riwaya hizi inasimuliwa na Muhammad Bin Talha Shafi’i katika kitabu chake “Matalibu’s-Su’ul”, Tabari katika “Tafsir Kabir,” Baihaqi katika “Sunan” yake, Nur’d-Din Maliki katika kitabu chake “Fusul’l-Muhima”, Hakim katika kitabu chake “Mustadrak,” Hafidh Abu Na’im katika kitabu chake “Hilya”, Ibn Asakir katika kitabu chake “Ta’rikh Ibn Asakir”, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharhe yake ya “Nahju’l-Balagha”, Tabrani katika kitabu chake “Ausat”, Muhibu’d-Din katika kitabu chake “Riyaz”

Hamwaini katika kitabu chake “Fara’id”, Suyuti katika kitabu chake “Durr-e-Mansur”, kutoka kwa Ibn Abbas, Salman, Abu Dharr na Hudhifa – wote wanasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akinyoosha mkono wake kuelekea kwa Ali Bin Abi Talib, alisema:

“Hakika huyu Ali ndiye mtu wa kwanza ambaye alitangaza imani yake kwangu na wa kwanza ambaye atakayepeana mikono na mimi katika Siku ya Hukumu. Yeye ni Siddiq-e-Akbar (mkweli mkubwa) na Faruq wa Umma huu (mtambuzi wa Umma huu). Atabainisha kati ya haki na batili.” Hadith “Ali Yuko Pamoja Na Haki Na Haki Iko Pamoja Na Ali”

Muhammad Bin Yusuf Ganji katika Sura ya 44 ya kitabu chake “Kifayatu’t-Talib” anasimulia hadithi hiyo hiyo pamoja na nyongeza ya maneno: “Na ni mtawala juu ya waumini na ni mlango wangu kwa ajili ya kupitia waumini; na ni Khalifa (mrithi) wangu baada yangu.”

Ganji Shafi’i anasema kwamba Muhadith-e-Sham (mwanahadithi wa Syria) anazo hadithi mia tatu zenye kumsifia Ali. Vile vile imeandikwa na Muhammad Bin Talha Shafi’i katika kitabu chake “Matalibu’s-Su’ul”, Khatib Khawazimi katika “Manaqib,” Sam’ani katika “Fadha’ilu’s-Sahaba”, Ibn Sabbagh Malik katika “Fusulu’l-Muhimma”, Khatib Baghdadi katika “Ta’rikh-e-Baghdad”, Jz. 14, uk. 21, Hafidh Mardawaih katika “Manaqib”, Dailami katika “Firdaus”, Ibn Qutayba katika “Imama wa’s-Siyasa”, Jz. 1, uk.111, Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’t-Talib”, Imamu Ahmad Hanbal katika “Musnad”, na maulamaa wenu wengi wamesimulia kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali popote ageukiapo.” Katika vitabu hivyo hivyo vile vile kuna hadith nyingine iliyosimuliwa na Sheikh Sulemani Qunduzi Hanafi, katika Sura ya 20 ya “Yanabiu’l-Mawadda”, kutoka kwa Hamwaini kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali.”

Hafidh Abi Nai’im Ahmad ibn Abdullah Ispahani katika kitabu chake “Hiyatu’l-Auliya” Jz. 1, uk. 63, anasimulia kwamba, Mtume alisema: “Enyi kundi la Ansar! Je, nikuelekezeni kwa mtu ambaye kama mkishikamana naye kamwe hamtapotea?” Wote wakasema: “Ndio, Ewe Mtume wa Allah”. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Mtu huyo ni Ali. Mpendeni kama mnavyonipenda mimi, na mheshimuni kama mnavyoniheshimu mimi, yale niliyokuambieni yalikuwa ni amri ya Allah iliyosimuliwa kwangu na Jibril.”

Lengo la ujumla la hadithi hizi ni kuonyesha dalili za upendeleo wa Mtume kuhusiana na mrithi wake. Mtume aliamrisha Umma wake kugeukia kwa Ali baada yake na kumfuata yeye. Kwa mwanga wa hadithi kama hizi, tueleze upinzani wa Ali kwa Abu Bakr una maanisha nini kwako. Kwa hakika inasikitisha sana na kushangaza kwamba haraka kubwa mno ilifanywa katika siku ya Saqifa. Kila mtu mwenye akili ambaye anajua yaliyotokea katika siku hiyo amefadhaika mno. Kama kulikuwa hakuna njama, kwa nini wasingoje (angalau kwa saa chache) ili kwamba Ali Bin Abi Talib, Bani Hashim, na Abbas waweze kuelezea maoni yao juu ya Ukhalifa?

Hafidh: Kulikuwa hakuna njama. Kwa vile walihofia vurugu, walifanya haraka kuamua suala la Ukhalifa kwa ajili ya usalama wa Uislamu.

Muombezi: Una maana kwamba Abu Ubaida Jarra, mchimba kaburi wa zamani wa Makka, na wengine walikuwa na wasiwasi zaidi na usalama wa Uislamu kuliko Abbas, ami yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anayeheshimiwa, na Ali Bin Abi Talib? Una maana kwamba kama wangelingojea kwa muda kidogo, au kama Abu Bakr na Umar, wakiwashughulisha watu, wangemtuma Abu Ubaida kumjulisha Abbas na Ali juu ya hali hii mbaya, hilo lingefanya Uislamu uangamie? Tafadhali jaribu kuwa mkweli. Kama wangewakaribisha watu wanaostahili huko Saqifa, nafasi yao ingelikuwa salama zaidi. Kusingelikuwa na hitilafu katika Uislamu kama ilivyo leo.

Baada ya miaka 1335, sisi ndugu wa ki-Islamu tusingezozana wenyewe kwa wenyewe kama tulivyo usiku huu, bali tungekuwa tumeungana katika kumpinga adui yetu wa pamoja. Sehemu kubwa ya msingi wa jengo hili lenye kasoro la Uislamu uliwekwa siku hiyo. Ilikuwa ni kwa ajili ya haraka za watu wale watatu za kutaka kukamilisha mipango yao ya siri.

Nawab: Bwana mheshimiwa, tafadhali tueleze kwa nini walifanya haraka. Kwa nini wasi- wajulishe hata watu waliokuwa Msikitini au katika nyumba ya Mtume?

Muombezi: Sababu sio za kutafuta mbali. Walifanya haraka kwa sababu walijua kwamba kama wakingojea Waislamu wote waje, au angalau hata watu mashuhuri wa jeshi la Usama Bin Zaid, masahaba mashuhuri wa Mtume waliokuwepo mjini Madina, au Bani Hashim, jina la Ali, miongoni mwa mwa mengine, lingependekezwa. Uwezekano wa kisiasa wa Abu Bakr na Umar ungelipunguzwa sana.

Hivyo basi waliharakisha mipango yao ili kwamba, wakati ambapo Bani Hashim na masahaba mashuhuri wakiwa wanajishughulisha na taratibu za mazishi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wao walifanikiwa katika kumteua Abu Bakr kuwa Khalifa juu ya msingi wa kura za watu wawili! Waliucheza mchezo huo, na usiku huu hapa ninyi watu wazuri mnaupa jina la “ijmai!” Hata ulamaa wenu wakubwa, kama Tabari, Ibn Abil-Hadid na wengine wameandika kwamba Umar alisema: “Ukhalifa wa Abu Bakr ulisimamishwa kwa haraka sana. Allah atusaidie!”

Amma kwa madai yenu mengine, ambayo mnayatoa kutoka kwa khalifa Umar, kwamba utume na utawala haviwezi kuchanganywa kwenye familia moja, vile vile yanakataliwa kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu:

{ام ﻳﺤﺴﺪُونَ اﻟﻨﱠﺎس ﻋﻠَ ﻣﺎ آﺗَﺎﻫﻢ اﻟﻪ ﻣﻦ ﻓَﻀﻠﻪ ۖ ﻓَﻘَﺪْ آﺗَﻴﻨَﺎ آل اﺑﺮاﻫﻴﻢ اﻟْﺘَﺎب{54

“Au wanawahusudu watu kwa yale aliyowapa Allah kutokana fadhila Zake? Basi tuliwapa ukoo wa Ibrahim Kitabu na hikma na tukawapa mamlaka makubwa.” (4:54)

Hadithi hii ambayo inahusishwa na Khalifa Umar, ni ya kubuniwa. Mtume kamwe hajasema neno lenye kukinzana na amri ya Qur’ani Tukufu. Aidha, ukhalifa hauwezi kutenganishwa na utume kwa sababu Khalifa wa kweli ni mfano wa sheria ya Mungu inayofanya kazi ulimwenguni. Kuuchukulia ukhalifa kama kazi ya kisiasa tu iliyotenganishwa na utume ndio kosa lenyewe hasa lililofanywa na Abu Bakr na Umar.

Kama Harun, ndugu yake Mtume Musa, angeweza kuondolewa kwenye ukhalifa wa Musa, Ali vile vile angeweza kunyimwa ukhalifa wa Mtume. Na kwa vile utume na ukhalifa, kwa mujibu wa Qur’ani, vilichanganywa juu ya Musa na Harun, hapana shaka ulichanganywa juu ya Muhmmad na Ali. Hadithi yenu hii ilibuniwa na Bani Umayya. Kama utume na ukhalifa usingeweza kuchanganywa katika familia moja, basi kwa nini katika Majilis-e- Shura (Kamati ya ushauri) Khalifa Umar alimpendekeza Ali kwenye ukhalifa? Hata hivyo, ninyi vile vile mnamkubali kuwa ni Khalifa wenu wa nne!

Ni ukinzano wenye kushangaza kwamba kwa kumetegemea juu ya hadithi ya Umar, mnakataa kuchanganywa utume na ukhalifa, lakini wakati Umar mwenyewe alipoidhinisha hali hii miaka michache baadae, mkaiunga mkono! Je, mnaweza kupinga na kuunga mkono pendekezo lile lile moja? Mnasema kwamba utume na utawala havichanganywi katika familia moja, ingawa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amefanya kuwa ni wajibu kwa Umma wake kufuata kizazi chake. Alisema kwamba kuwa na uadui nao ni kupotea njia.

Amesema katika mara nyingi, “Ninakuachieni vitu viwili vizito: Kitabu cha Allah (Qur’ani Tukufu) na Ahulul-Bayt wangu. Kama mkifungamana na viwili hivi, kamwe hatapotea baada yangu.” Hadithi hii sahihi imekubaliwa na madhehebu zote. Nimeitaja katika mikesha iliyopita pamoja na vyanzo vyake.

Hadithi Ya Safina – Hadithi Ya Saqifa

Wakati wa mafuriko makubwa yeyote yule ambaye alichukuwa hifadhi katika safina ya Huh aliokolewa. Yeyote yule ambaye aliipa mgongo akaacha kuipanda aligharikishwa, ikiwa ni pamoja na mtoto wa Nuh. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vile vile aliwatambulisha kizazi chake kama Safina ya Nuh, akimaanisha kwamba watu wa umma wake katika wakati wa mitihani lazima wajiambatanishe na kizazi chake.

Kwa hiyo, kwa mujibu wa maamrisho haya ya wazi, umma katika hitilafu zao zote, wanapaswa kutafuta manufaa ya Ahlul-Bayt wa Mtume. Ali Bin Abu Talib, kwa mujibu wa Mtume alikuwa ndiye msomi zaidi na mtu bora zaidi miongoni mwao. Kwa nini hawakumjulisha wakapata kushauriana naye? Lakini wapi! Hawakufanya hivyo. Wanasiasa walinyakuwa mamlaka na wakamnyima Ali haki yake ya kudumu.

Sheikh: Ni kwa misingi ipi unasema kwamba wangelimfuata Ali na kwamba maoni na ijmai ya masahaba ingelipaswa kuachwa?

Muombezi: Sijasema kwamba maoni ya Masahaba na ijma yao haipaswi kuheshimiwa. Tofauti moja kati yenu na mimi ni kwamba mara tu mnaposikia jina la sahaba, hata kama akiwa ni mnafiki, kama Abu Huraira, ambaye Khalifa Umar alimpiga na kumuita mwongo, mnamuinamia kwa heshima. Nawaheshimu mashaba wale tu ambao wanachukuana na masharti ya uswahiba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Aidha nimeonesha kwamba kulikuwa hakuna ijma ndani Saqifa. Kama mnaweza kupinga hoja yangu, sasa ni wakati wa kufanya hivyo. Nitakubaliana na muafaka wa hadhara hii. Kama mnaweza kuonyosha kutoka kwenye vitabu nyenu kwamba ndani ya Saqifa, umma wote au watu wasomi wenye akili wa umma walikusanyika pamoja na kukubaliana kwamba Abu Bakr awe Khalifa, tutakuwa tayari kulibali hilo.

Na kama ukiondoa watu wawili (Umar na Abu Ubaida) na watu wachache wa kabila la Aus, hakuna mtu mwingine aliyekula kiapo cha utii, lazima mkubali kwamba sisi Mashi’a tumeongozwa sawasawa. Tunaliacha kwenye maoni ya kisomi kuamua iwapo masahaba watatu walikuwa na haki ya kushikilia hatamu za umma wote. Wawili walikula kiapo kwa wa tatu, na baadae wakawatishia wengine kwa panga, moto, na fadheha, kuwalazimisha kukubali utashi wao.

Je, Ijmai Inapaswa Kukubaliwa Kwa Sababu Ya Kigezo Cha Yaliyopita?

Sheikh: Hatujui kama kulikuwa na uzembe kwa upande wao kwa sababu hatukuwepo kule siku hiyo. Katika muda huu mrefu hatuwezi kutambua walikuwa katika shinikizo la aina gani. Leo pamoja na hali hiyo kuwa ni ukweli uliothibiti, sio neno iwapo kama ijma ilikamilishwa katika hatua za pole pole. Hatupaswi kupinga. Lazima tukubaliane na watu wale na tufuate njia waliyotuonyesha.

Muombezi: Uzuri ulioje wa hoja hiyo! Unatutaka sisi tufikirie kwamba Uislamu hauna misingi? Kama watu wawili au watatu wakiunda mpango na wakaungwa mkono na watu wengine, je, ni jukumu la Waislamu kuwafuata wao? Je, hiyo ndio maana ya dini ya Mtume wa Uislamu? Qur’ani Tukufu inasema: “…Basi wabashirie waja wangu, wale ambao husikiliza maneno, wakafuata lililo bora lao…” (39:17-18)

Uislamu umesimama juu ya misingi ya kweli na hoja, sio juu ya kufuata kibubusa, naam kwa hakika si kwa kumfuata Abu Ubaida, mchimba kaburi. Mtume alituonesha njia. Alisema kwamba wakati umma ukiwa umegawanyika, lazima tumfuate mtu ambaye ameongozwa. Unatuuliza ni kwa nini ni wajibu juu yetu kumfuata Ali. Tunajibu kwamba wajubu huo umetegemea juu ya aya za Qur’ani na hadithi zilizoandikwa katika vitabu vyenu wenyewe.

Hadithi Za Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Zinazowahimiza Waumini Kumfuata Ali

Kuna hadithi nyingi ambazo hufanya wajibu juu ya umma kumfuata Ali. Mojawapo ya hizo imesimuliwa na Ammar-e-Yasr, ambayo imeandikwa na maulamaa wenu wafuatao katika vitabu vyao: Hafidh Abi Nu’aim Ispahani katika “Hilya”; Muhammad Bin Talha Shafi’i katika “Matalibu’s-Su’ul”; Baladhuri katika “Ta’rikh”; Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, Sura ya 43, kutoka kwa Hamwaini; Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i katika “Mawaddatu’l-Qubra”, Mawadda ya 5; Dalami katika “Firdaus”. Wanasimulia hadithi ndefu yenye maelezo kinaganaga ambayo haiwezi kusimuliwa hapa kwa ukamilifu. Inaweza kuelezewa kwa ufupi tu kwamba, wakati walipomuuliza Abu Ayyub kwa nini alikwenda kwa Ali na hakuchukua kiapo cha utii kwa Abu Bakr, yeye ali- jibu kwamba siku moja alikuwa amekaa na Mtume wakati Ammar-e-Yasir alipokuja na kumuuliza Mtume swali.

Katika kuendelea na mazungumzi yao, Mtume akasema: “Ewe Ammar! Kama watu wote watakwenda njia mmoja, na Ali peke yake akaenda njia nyingine, itakupasa kumfuata Ali. Ewe Ammar! Ali hatakuruhusu wewe kupotea kutoka kwenye njia ya mwongozo na hatakuongoza kwenye upotovu; Ewe Ammar! Utii kwa Ali ni utii kwangu, na utii kwangu ni utii kwa Allah.” Katika mwanga wa Maamrisho haya, na katika mwanga wa upinzani wa Ali kwa Abu Bakr, je, watu siwangemfuata Ali? Hata kama Bani Hashim, Bani Umayya, Masahaba mashuhuri, watu wajuzi wenye elimu wa umma, Muhajirina, na Ansari wasingekuwepo pamoja naye (na walikuwa pamoja naye) watu wangelimfuata Ali.

Hafidh: Wakati wa mjadala wetu, umesema vitu viwili vya ajabu. Kwanza, umerudia rudia kumuita Abu Ubaida “mchimba kaburi.” Unaweza kuthibitisha kwamba hii ilikuwa taaluma ya bwana mkubwa huyu? Pili, umesema kwamba Ali, Bani Hashim, na masahaba hawakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr, walimpinga. Lakini wanahistoria na wanahadithiwote wameandika kwamba Ali, Bani Hashim na masahaba wa Mtume walikula kiapo cha utii kwa Abu Bakr.

Muombezi: Sio sisi peke yetu tunaodai kwamba Abu Ubaida alikuwa mchimba kaburi. Imo katika vitabu vyenu wenyewe. Unawza kurejea kwenye Al-Bidayya wa’n-Nihaya, Jz. 5, uk. 266-267 (kitabu) kilichokusanywa na Ibn Kathir Shami, ambaye anasema kwamba, kwa vile Abu Ubaida amezoea kuchimba kaburi za watu Makka, Abbas alimtuma mtu kumtafuta Abu Talha, mchimba kaburi wa Madina, na mtu mwingine kumtafuta Abu Ubaida, ili kwamba wote wawili waweze kuchimba kaburi la Mtume.

Kulazimishwa Kwa Ali Na Bani Hashim Kula Kiapo Baada Ya Miezi Sita

Unasema kwamba Ali, Bani Hashim, na masahaba wa Mtume walikula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Umesoma maneno “walikula kiapo cha utii,” lakini hukuelewa ni kwa nani na vipi walivyokula kiapo. Wanachuoni wenu wote wa hadithi na wanahistoria wakubwa wameandika kwamba Ali na Bani Hashim walikula kiapo cha utii (kwa nje), lakini hilo limefanywa baada ya miezi sita, na hata hivyo chini ya vitisho vikubwa.

Hafidh: Sio vyema kwa mtu mtukufu kama wewe kutumia maneno ambayo hutumiwa na Mashi’a wa kawaida kwamba, Ali aliburuzwa kutoka kwenye nyumba yake na alitishiwa kuuawa kama asingekula kiapo cha utii. Ukweli ni kwamba katika siku chache za mwan- zo za ukhalifa kwa utashi na kwa furaha alikubali ukhalifa wa Abu Bakr.

Muombezi: Ali na Bani Hashim hawakula kiapo cha utii kwa mara moja. Wanahistoria wenu wameandika kwamba Ali alikula kiapo cha utiibaada ya kifo cha Hadhrat Fatima. Bukhari katika katika Sahih yake, Jz. 3, Sura ya Ghazawa Khaibar, uk. 37, na Muslim Bin Hujjaj, katika Sahih yake, Jz. 5, uk. 154, wameandika kwamba Ali alikula kiapo cha utii baada ya kifo cha Fatima.

Baadhi ya maulamaa wenu wanaamini kwamba Fatima alikufa siku 75 baada ya kifo cha Mtume. Ibn Qutayba vile vile anashikilia maoni hayo hayo, lakini wanahistoria wenu wengi wanadai kwamba alikufa miezi sita baada ya kufariki kwa Mtume. Kwa hiyo ina maana kwamba kiapo cha Ali kilikuja wakati fulani baada ya miezi 3 au 6 baada ya kufariki kwa Mtume.

Mas’udi katika kitabu chake “Muruju’s-Sahab”, Jz. 1, uk. 414, anasema: “Hakuna mtu kutoka Bani Hashim aliyekula kiapo cha utii kwa Abu Bakr mpaka baada ya kifo cha Bibi Fatima. Ibrahim Bin Saqafi anasimulia kutoka kwa Zuhri kwamba Ali hakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr mpaka miezi sita baada ya alipofariki Mtume, na watu hawakuwa na ujasiri wa kumshawishi isipokuwa baada ya kifo cha Bibi Fatima. Ibn Abi’l-Hadid katika Sharhe Nahju’l-Balagha anasimulia jambo hilo hilo.

Kwa hali yoyote, maulamaa wenu wenyewe wanasisitiza kwamba kiapo cha Ali hakikuwa cha haraka bali kilikuja tu baada ya muda fulani kupita na hata hivyo ni wakati mazingira yalipomlazimisha kufanya hivyo. Ibn Abi’l-Hadid, katika Sharhe Nahju’l-Balagha, Jz. 2, uk. 18, anasimulia kutoka kwa Zuhri, kutoka kwa Aisha, ambaye amesema: “Ali hakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr kwa muda wa miezi sita, na hakuna mtu kutoka Bani Hashim aliyekula kiapo mpaka Ali alipofanya hivyo.”

Ahmad Bin A’sam-e-Kufi Shafi’i katika “Futuh” na Abu Nasr Hamidi, katika “Jam’a Bainu’s-Sahihain” anasimulia kutoka kwa Nafiy, akinukuu kutoka Zuhri, ambaye alisema: “Ali hakula kiapo cha utii mpaka baada ya miezi ya kufariki kwa Mtume (s.a.w.w.).”

Ali Aliburuzwa Kutoka Nyumbani Kwake Na Nyumba Yake Ikachomwa Moto

Hafidh: Ni wapi maulamaa wetu waliposema kwamba Ali aliburuzwa kutoka kwenye nyumba yake na nyumba ikachomwa moto, kama kwa kawaida inavyoaminiwa na Mashi’a? wanalisimlia hili kwa mhemuko mkubwa katika majlis zao za kidini. Vile vile huchochea hisia za watu kwa kusema kwamba Fatima aliteswa na hatimaye akaharibu mimba yake.

Muombezi: Waheshimiwa mliohudhuria mnawashutumu Mashi’a, mkijaribu kuficha makosa ya viongozi wenu waliotangulia. Mnasema kwamba hadithi hizi zimebuniwa na Mashi’a. Ukweli ni kwamba kwa amri ya Abu Bakr, Umar na wenzake walikwenda nyumbani kwa Ali, wakamtisha kwa upanga, wakamburuza mpaka Msikitini na wakamlazimisha kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Ukweli huu umeandikwa na maulamaa wenu wenyewe. Kama mnataka, nitakusimulieni. Hatusemi kitu chochote kutoka kwenye vitabu vyetu. Tunasema kile mnachosema ninyi.

Hafidh: Ndio, tafadhali endelea. Tuko tayari kusikiliza.

Hoja Kumi Na Mbili Zinazounga Mkono Ukweli Kwamba Ali Alichukuliwa Kupelekwa Msikitini Kwa Ncha Ya Upanga

Muombezi:

(1) Abu Ja’far Baladhuri Ahmad Bin Yahya Bin Jabir Baghdadi, mmoja wa wanahadithi na wanahistoria wenu wa kutengemewa, anaandika katika kitabu chake cha Ta’rikh - Historia kwamba, wakati Abu Bakr alipomuita Ali ili kula kiapo cha utii, Ali alikataa. Abu Bakr alimtuma Umar akiwa na kijinga kwenda kuchoma moto nyumba ya Ali.

Fatima akaja mlangoni na kusema: “Ewe mtoto wa Khattab! Umekuja kuichoma nyumba yangu?” Akasaema: “Ndio, hili lina athari zaidi kuliko kitu chochote alichokifanya baba yako.”

(2) Izzu’d-Din Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazili, na Muhammad Bin Jarir Tabari, wanasimulia kwamba Umar alikwenda kwenye mlango wa nyumba ya Ali pamoja na Usay Bin Khuza’i, Salama Bin Aslam na kikundi cha watu. Kisha Umar akaita, “Tokeni nje! Vinginevyo nitaichoma nyumba yenu!”

(3) Ibn Khaziba anataarifu katika kitabu chake “Kitab-e-Gharrar” kutoka kwa Zaid Bin Aslam, ambaye alisema: “Nilikuwa mmoja wa wale waliokwenda pamoja na Umar tukiwa na vijinga vya moto mpaka kwenye mlango wa nyumba ya Fatima. Wakati Ali na watu wake alipokataa kula kiapo cha utii, Umar alimuambia Fatima: ‘Yeyote yule aliyeko ndani ya nyumba atoke nje.

Vinginevyo nitaichoma nyumba na yeyote aliyemo ndani.’ Ali, Hasani, Husein, Fatima, na kikundi cha Masahaba wa Mtume, na Bani Hashim walikuwemo ndani. Fatima akasema: ‘Utaichoma nyumba yangu moto pamo- ja na mimi mwenyewe na watoto wangu?’ Akasema: ‘Ndio, Wallahi, kama hawatoki nje na kula kiapo cha utii kwa Khalifa wa Mtume.’”

(4) Ibn Abd Rabbih, mmoja wa maulamaa wenu mashuhuri, anaandika katika kitabu chake “Iqdu’l- Farid,” Jz. 3, uk. 63, kwamba Ali na Abbas walikuwa wamekaa nyum- bani kwa Fatima. Abu Bakr akamuambia Umar: “Nenda ukawalete watu hawa. Kama wakikataa kuja, pigana nao.” Hivyo Umar akaenda nyumbani kwa Fatima na vijinga vya moto. Fatuma akaja mlangoni na akasema: “Umekuja kuchoma nyumba yetu?” Akasema: “Ndio…” na kadhalika.

(5) Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazili katika sharhe yake ya Nahju’l-Balagha, Jz. 1, uk. 134, akinukuu kutoka kitabu cha Jauhari, “Kitab-e-Saqifa” ameandika kwa kinaganaga kuhusu suala la Saqifa-e-Bani Sa’ad: “Bani hashim na Ali walikuwa wamekusanyika nyumbani kwa Ali. Zubair pia alikuwemo kwa vile naye alijiona kama ni mmoja wa Bani Hashim. Ali alizoea kusema, ‘Zubair alikuwa siku zote pamoja nasi mpaka wato- to wake walipokuwa wakubwa. Wao wakamgeuza dhidi yetu’. Umar akaenda nyumbani kwa Fatima na kikundi cha watu. Usayd na Salma vile vile walikuwa pamoja naye.

Umar akawataka watoke nje wachukue kiapo cha utii. Wao wakakataa. Zubair akachomoa upanga wake na akatoka nje. Umar akasema: ‘Mkamateni mbwa huyu.’ Salma Bin Aslam akamnyang’anya upanga huo na akautupa kiambazani. Kisha wakambururuza Ali kumpeleka kwa Abu Bakr. Bani Hashim wengine wakamfuata na walikuwa wanangojea kuona Ali atafanya nini.

Ali alikuwa akisema kwamba yeye ni mtumishi wa Allah na ndugu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hakuna aliyemsikiliza. Walimpeleka kwa Abu Bakr, ambaye alimtaka kula kiapo cha utii kwake. Ali akasema: ‘Mimi ndiye ninayestashiki zaidi katika nafasi hii, na sitakula kiapo cha utii kwako. Ni wajibu juu yako kula kiapo cha utii kwangu. Umeichukuwa haki hii kutoka kwa Ansar kwa kutegemea uhusiano wako na Mtume (s.a.w.w.). Na mimi vile vile, kwa msingi huo huo, nalalamika dhidi yako. Hivyo kuwa muadilifu. Kama unamuogopa Allah, kubali haki yangu, kama Ansar walivyofanya kwa yako. Vinginevyo, itakupasa ukubali kwamba unanidhulumu kwa makusudi.’

Umar akasema: ‘Hatutakuacha mpaka ule kiapo cha utii.’ Ali akasema: ‘Mmekula njama wote vizuri sana. Leo unamuunga mkono, ili kwamba kesho aweze kuurudsha ukhalifa kwako. Naapa Wallahi kwamba sitakubaliana na maombi yenu na sitakula kiapo cha utii (kwa Abu Bakr). Yeye anapaswa atoe kiapo cha utii kwangu.’

Kisha aliwageukia watu na akasema: ‘Enyi Muhajirina! Muogopeni Allah. Msipore haki ya mamlaka ya familia ya Muhammad. Haki hiyo imeamriwa na Allah. Msimuondoe mtu anayestahiki kutoka katika nafasi yake. Kwa jina la Allah sisi Ahlul-Bayt tuna mamlaka makubwa katika suala hili kuliko mlivyo ninyi. Kuna mtu miongoni mwenu ambaye ana ujuzi juu ya Kitabu cha Allah (Qur’ani), Sunna ya Mtume, na sheria za dini yenu.

Ninaapa Wallahi sisi tunavyo vitu vyote hivi. Hivyo msifuate nafsi zenu mkaja mkapotea kutoka kwenye ukweli.’” Ali alirudi nyumbani bila kula kiapo cha utii na akajitawisha mwenyewe nyumbani kwake mpaka Fatima alipofariki. Hapo tena, alilazimishwa kula kiapo cha utii.

(6) Abu Muhammad Abudullah Bin Muslim bin Qutayba Bin Umar Al-Bahili Dinawari, ambaye alikuwa mmoja wa maulamaa na Kadhi rasmi wa mji wa Dinawari, anaandika katika kitabu chake mashuhuri “Ta’rikhu’l-Khulafati Raghibin wa Daulati Bani Umayya”, kijulikanacho kama “Al-Imama wa’s-Siyasa”, Jz. 1, uk. 13: “Wakati Abu Bakr alipofahamu kwamba kundi la watu walio na uadui kwake wamekusanyika katika nyumba ya Ali, alimtuma Umar kwao. Wakati Umar alipompigia kelele Ali atoke nje na kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr, wote walikataa kutoka nje.

Umar alikusanya kuni na kusema ‘Naapa kwa jina la Allah, ambaye ana uhai wangu katika miliki Yake, amma mtatoka nje, au nitaichoma nyumba pamoja na wote waliomo ndani.’ Watu wakasema: “Ewe Abu Hafsa! Fatima vile vile yumo ndani.’ Akasema: ‘Hata akiwemo, nyumba nitaichoma moto tu.’

Hivyo wote wakatoka nje na kula kiapo cha utii, isipokuwa Ali, ambaye alisema: ‘Nimeweka nadhiri kwamba, mpaka nitakapomaliza kuikusanya Qur’ani, sitatoka nje ya nyumba wala kuvaa nguo kiukamilifu.’ Umar hakulikubali hili, lakini malalamiko ya huzuni ya Fatima na kubezwa na wengine, kulimlazimisha kurudi kwa Abu Bakr.

Umar alimhimiza kumlazimisha Ali atoe kiapo cha utii. Abu Bakr alimtuma Qanfaz mara kadhaa kumuita Ali, lakini safari zote alikatishwa tamaa. Mwishowe Umar, na kundi la watu walikwenda kwenye mlango wa nyumba ya Fatima. Wakati Fatima aliposikia sauti zao, alipiga kelele: ‘Ewe baba yangu, Mtume wa Allah!

Ni mateso gani haya tunayopata kuto- ka kwa mtoto wa Khattab na mtoto wa Abi Quhafa!’ Wakati watu hao walipoyasikia malalamiko ya Fatima, baadhi yao walirudi nyuma mioyo yao ikiwa imevunjika, lakini Umar alibaki pale na baadhi ya watu wengine mpaka mwishowe wakamburuza Ali kutoka nje ya nyumba.

Walimchukuwa Ali na kumpeleka kwa Abu Bakr, na akamuambia achukue kiapo cha utii kwake. Ali alisema: ‘Kama sikula kiapo cha utii kwako utanifanya nini?’ Wakasema: ‘Tuna apa kwa jina la Allah kwamba tutaivunja shingo yako.’ Ali akasema: ‘Mtamuuwa mtumishi wa Allah na ndugu wa Mtume?’ Umar akasema: ‘Wewe sio ndugu wa Mtume wa Allah.’ Wakati haya yakijiri, Abu Bakr alinyamaza kimya. Kisha Umar akamuuliza Abu Bakr iwapo yeye (Umar) alikuwa hafuati amri yake katika suala hili. Abu Bakr akasema kwamba muda Fatima yuko hai hatamlazimisha Ali kula kiapo cha utii kwake. Kisha Ali aliweza kufikia kaburi la Mtume, ambako akiomboleza na kulia, alimueleza Mtume kile ambacho Harun alimueleza ndugu yake (Mtume Musa), kama ilivyoandikwa katika Qur’ani Tukufu:

{ﻗَﺎل اﺑﻦ ام انﱠ اﻟْﻘَﻮم اﺳﺘَﻀﻌﻔُﻮﻧ وﻛﺎدوا ﻳﻘْﺘُﻠُﻮﻧَﻨ{150

‘..Ewe mtoto wa mama yangu! Hakika watu hawa wamenidharau, na wakakaribia kuniuwa…’( 7:150)

Fatima Aliwaambia Abu Bakr Na Umar Kwamba Anawalaani

Hao Wote Katika Kila Sala

Baada ya kuelezea Suala hili kwa urefu, Abu Muhammad Abdullah Bin Qutayba anasema kwamba Ali hakula kiapo cha utii na akarudi nyumbani. Baadae Abu Bakr na Umar walik- wenda nyumbani kwa Fatima kumbembeleza na kuomba msamaha wake.

Fatima akasema: ‘Allah awe ni shahidi wangu kwamba ninyi wawili mmenikosea. Ninawalaani katika kila Salat, na nitaendelea kuwalaani mpaka nitakapomuona baba yangu na kumlalamikia dhidi yenu.”

(7) Ahmad Bin Abdu’l-Aziz ni mmoja wa maulamaa wenu. Ibn Abi’l-Hadid anaandika kuhusu yeye katika maneno yafuatayo: “Alikuwa mtu msomi, mwanahadithi na mwandishi mkubwa.” Yeye anaandika katika kitabu chake, Kitab-e-Saqifa, na Ibn Abi’l- Hadid Mu’tazili vile vile anamnukuu katika Sharhe Nahju’l- Balagha, Jz. 1, uk. 9, kutoka kwa Abi’l-Aswad, ambaye amesema:

“Kundi la Masahaba na Muhajirina mashuhuri walielezea kuhusu kuudhiwa kwao na ukhalifa wa Abu Bakr na wakauliza ni kwa nini wao hawakushauriwa. Vile vile Ali na Zubair walionyesha hasira zao, wakakataa kula kiapo cha utii na wakarudi nyumbani kwa Fatima. Fatima alilia kwa nguvu na akawasihi kwa taadhima sana, lakini bila mafanikio yoyote. Walichukuwa upanga wa Ali na wa Zubair wakazirusha kwenye ukuta na kuzivunjilia mbali. Kisha wakawaburuza mpaka Msikitini na kuwalazimisha kula kiapo cha utii.”

(8) Jauhari anasimulia kutoka kwa Salma bin Abdu’r-Rahman kwamba wakati Abu Bakr aliposikia kwamba Ali, Zubair, na kundi la Bani Hashim walikuwa wamekusanyika nyumbani kwa Fatima, alimtuma Umar kwao. Umar alikwenda mpaka mlangoni mwa nyumba ya Fatima na akaita kwa sauti kubwa: “Tokeni nje, vinginevyo, naapa nitai- choma nyumba yenu!”

(9) Jauhari, kwa mujibu wa Ibn Abi’l-Hadid katika sharhe ya Nahaju’l-Balagha, Jz. 2, uk.

19, anasimulia kutoka kwa Sha’bi: “Wakati Abu Bakr aliposikia kuhusu mkusanyiko wa Bani Hashim katika nyumba ya Ali, alimuambia Umar: ‘Wewe na Khalid nendeni mkamlete Ali na Zubair waje wale kiapo cha utii.’ Hivyo Umar aliingia nyumbani kwa Fatima na Khalid akabakia nje. Umar akamuambia Zubair ‘Upanga huu ni wa nini?’ Akajibu, ‘Nimeupata kwa ajili ya kula kiapo kwa Ali.’

Umar akaunyakua upanga ule na kuutupa kwenye jiwe ndani ya nyumba na kuuvunja. Kisha akamtoa nje kwa Khalid. Alirudi tena ndani ya nyumba ambako kulikuwa na watu wengi, akiwemo Miqdadi, na Bani Hashim wote. Akimsemesha Ali, alisema: ‘Nyanyuka! Ninakupeleka kwa Abu Bakr. Lazima ule kiapo cha utii kwake.’ Ali akakataa. Umar akamburuza mpaka kwa Khalid. Khalid na Umar wakamlazimisha katika barabara ambayo ilikuwa imejaa watu ambao walishuhudia kitendo hiki. Wakati Fatima alipoona tabia hii ya Umar, yeye pamoja na wanawake wengi wa Bani Hashim (ambao walikuja kumliwaza), walitoka nje.

Walikuwa wakiomboleza na kulia kwa vilio vya sauti ya juu. Fatima alikwen- da msikitini ambako alimuambia Abu Bakr: ‘Mapema ilioje umewafukuza Ahlul Bayt wa Mtume wa Allah. Naapa kwa jina la Allah, sitazungumza na Umar mpaka nitakapomuona Allah (yaani Siku ya Hukumu).’

Fatima alionesha kuchukizwa kwake mno na Abu Bakr na hakuzungumza naye kwa muda wote uliokuwa umebakia wa maisha yake.” (Tazama Sahih Bukhari, sehemu ya 5 na 7).

(10) Abu Walid Muhibu’d-Din Muhammad bin Muhammad Bin Ash-Shahna Al-Hanafi (amekufa 815 A.H.), mmoja wa maulamaa wenu wakubwa anaandika katika katika kitabu chake, “Raudhatu’l-Manazir Fi Khabaru’l-Awa’il wa’l-Awakhir” kuhusiana na suala la Saqifa: Umar alikwenda nyumbani kwa Ali akiwa amejiandaa kuichoma nyumba moto pamoja na wote waliokuwemo ndani yake. Umar alisema: Ingieni kwenye kile ambacho umma umeingia.”

Tabari, katika kitabu chake Ta’rikh Jz. 2, uk. 443, anasimulia kutoka kwa Ziyad Bin Kalbi kwamba, “Talha, Zubair, na baadhi ya Muhajirin walikuwa nyumbani kwa Ali. Umar bin Khattab alikwenda huko na kuwataka watoke nje. Kama hawakutoka, alisema, angeichoma nyumba moto.”

(12) Ibn Shahna, katika “Hashiyya-e-Kamil” ya Ibn Kathir, Jz. 11, uk. 112, anaandika kuhusiana na suala la Saqifa kwamba: “Baadhi ya Masahaba wa Mtume, na Bani Hashim, Zubair, Atba Bin Abi Lahab, Khalid Bin Sa’id Bin As, Mikidadi Bin Aswad Kindi, Salman Farsi, Abu Dharr Ghifari, Ammar Bin Yasir, Bara’a Bin Azib, na Ubai Bin Ka’b walikataa kula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Walijikusanya katika nyumba ya Ali. Umar Bin Khattab alikwenda kule kwa nia ya kuichoma nyumba. Fatima akamlalamika. Umar akasema: “Ingia kule ambako wengine wameingia.”

Hizi ni sampuli tu za ukweli mwingi wa kihistoria ulioandikwa na wanahistoria wenu. Suala hili lilikuwa linajulikana sana kiasi kwamba washairi wa zamani wamelitaja. Mmoja wa washairi wenu, Hafidh Ibrahim wa Misr, anasema katika shairi la kumsifu Umar: “Hakuna mtu mwingine bali Abu Hafsa (Umar) ambaye angelikuwa na ujasiri wa kumuambia mkuu wa ukoo wa Adnan (Ali) na jamaa zake, akisema: ‘Kama mkishindwa kula kiapo cha utii, nitaichoma nyumba yenu, hata Fatima mwenyewe.’”

Hafidhi: Hadithi hizi zinaonyesha tu kwamba walichukuwa vijinga vya moto kuwatisha na kuwatawanyisha wapinzani wa ukhalifa. Kusema kwamba nyumba ya Ali ilichomwa moto na matokeo yake Fatima kuharibu mimba yake, ni maneno yaliyobuniwa na Mashi’a.

Riwaya Kuhusu Kuharibika Mimba Ya Fatima

Muombezi: Ungesoma Kitab-e-Isbatu’l-Wasiyya, kilichokusanywa na Abi’l-Hasan Ali Bin Husain Mas’udi, mwaandishi wa Muruju’dh-Dhahab. Aliandika kwa urefu sana kuhusu tukio la siku hiyo: “Walimzingira Ali na kuchoma mlango wa nyumba yake. Walimburuza kumtoa nje ya nyumba na wakambana mbora wa wanawake, Fatima, kati ya mlango na ukuta kwa nguvu sana kiasi kwamba Muhsin, mtoto wake ambaye alikuwa hajazaliwa, akafa kwa mimba yake kuharibika.”

Mashi’a hawakuyabuni mambo haya. Kilichotokea kimehifadhiwa katika kurasa za historia. Kuharibika kwa mimba ni habari za kweli.

Vile vile unaweza kurejea kwenye Sharhe Nahju’l-Balagha, Jz, 3, uk. 351. Ibn Abi’l-Hadid anaandika kwamba alimuambia mwalimu wake, Abu Ja’far Naqib, kwamba wakati Mtume alipoelezwa kwamba Hubbar Bin Aswad amevipiga vitoto vya binti yake (vikiwa tumboni bado) kwa mkuki, ambapo kwa sababu hiyo Zainab akaharibu mimba yake, Mtume aliruhusu yeye auwawe. Abu Ja’far akasema: ‘Lau Mtume wa Allah angelikuwa hai bado, kwa hakika angeamuru adhabu ya kifo vile vile kwa yule ambaye amemtisha Fatima kiasi kwamba mtoto wake Muhsin, alikufa kwa mimba yake kuharibika.’”

Hafidhi: Sielewi inasaidia lengo gani la manufaa kwa kusimulia visa hivi. Mambo ya aina hii husababisha kutokuelewana kwa pande hizi mbili.

Muombezi: Unakataa kusimulia kwangu mambo haya. Lakini ninafanya hivi kukana shutuma za waandishi waovu wanaowapoteza ndungu zetu ambao hawana ujuzi, na kuwaiTa Mashi’a makafir na kusema kwamba mambo haya yalikuwa ni ubunifu wa Mashi’a. Hatusemi kitu chochote kuhusu Ali mbali na kile ambacho Mtume amesema kuhusu yeye.

Tuliwaeleza katika mikesha iliyopita kwamba tunamchukulia Ali kama mja mtiifu wa Allah, makamu na mrithi wa Mtume aliyeteuliwa kwa utaratibu wa Mungu. Unadai kwamba hakuna maana ya kusimulia mambo haya. Kama msingezileta nukta hizi, tusingezijadili.

Kama msingesema usiku huu kwamba hizi ni imani za Shia bila hoja ya msingi kwazo, nisingelazimika kuiambia hadhara hii kwamba hizi ni imani za maulamaa wa ki-Sunni wasio na upendeleo.

Nawab: Mheshimiwa, tunaamini kwamba Husein, ash-Shahid, alikuwa ameongoka sawa-sawa na kwamba aliuawa kwa dhulma na maofisa wa Bani Umayya. Lakini kuna baadhi ya watu, hususan miongoni mwa vijana wetu, ambao wanasema kwamba vita vya Karbala vilikuwa ni vya kijeshi (kisiasa), na sio kadhia ya kidini. Inasemekana kwamba Husein Bin Ali alielekea Kufa kutafuta mamlaka, na ni jukumu la kila serikali kuzima hatari kama hizo.

Kwa hiyo, Yazid alizuia tishio hili. Walimtaka Mtukufu Imamu kula kiapo cha utii bila masharti kwa Khalifa Yazid, ambaye kwamba utii kwake ilikuwa ni wajibu. Walimtaka aende Syria akaishi kule na Khalifa kwa heshima au arudi mjini kwake (Madina).

Lakini hakufuata ushauri wao, na hatimaye aliuawa. Wanahitimisha kwamba maombolezo yoyote kwa ajili ya mtu wa kidunia kama huyu, ambaye aliuawa kwa ajili ya mapenzi yake ya mamlaka, sio tu hayana maana, bali pia ni bid’a. Je, una jibu kwenye nukta hii? Unakanusha vipi wazo la kwamba vita vya Karbala havikuwa kilele cha harakati za kisiasa?

Imamu Husein Kamwe Hakutamani Nguvu Za Kisiasa

Muombezi: Kila tendo zuri au baya linategemea elimu yetu juu ya Allah. Wapinzani lazi- ma kwanza wamtambue Allah, na kisha lazima wakubali Kitabu cha Mungu, Qur’ani. Kutokana na kukubali huko, ina maana kwamba tunatambua kwamba chochote kile kilichoko ndani ya Kitabu ni sahihi. Mtu yeyote anayeamini kwamba Husein Bin Ali alishaw- ishiwa na malengo ya kidunia anakataa ukweli wa Qur’ani Tukufu. Allah (swt) ametoa ushahidi wa usafi wa Husein katika Qur’ani Tukufu. Anasema: “…Allah anapenda kuwaondoleeni uchafu, Enyi watu wa nyumba (Ahlu’l-Bayt)! Na kuwatakaseni kwa utakaso ulio safi kabisa…” (Qur’ani; 33:33).

Maulamaa wenu wengi, kama Muslim, Tirmidhi, Tha’labi, Sijistani, Abu Nu’aim Isfahani, Abu Bakr Shirazi, Suyuti, Hamwani, Ahmad Bin Hanbal, Zamakhshari, Baidhawi, Ibn Athir, na wengine wameshikilia kwamba aya hii iliteremshwa kwa kuwatukuza wale watukufu watano, Ahlu’l-Bayt (watu wa Nyumba): Muhammad, Ali, Fatima, Hasan na Husein. Aya hii ndio uthibitisho mkubwa wa kutokukosea (Ma’sum) na usafi wa watu hawa watukufu. Uchafu mkubwa sana ni mapenzi ya mamlaka ya kidunia. Kuna hadithi nyingi kutoka kwa Mtume na Maimamu zinazolaumu hamu ya mamalaka ya kidunia na utekelezaji wa matamanio yetu maovu.

Mtume alisema: “Mapenzi na urafiki na dunia ni mzizi wa maovu yote.” Abu Abdillah Husein hakuwa na mapenzi na mamlaka ya kidunia. Kwa kweli hakuhatarisha maisha yake na maisha ya familia yake kwa ajili ya kupata utawala wa mpito katika dunia hii. Kama kusimama kwa Husein dhidi ya Yazid kulikuwa kwa ajili ya mamlaka ya kilimwengu tu, Mtume asingeamuru watu kumsaidia. Maulamaa wenu wenyewe wanathibitisha nukta hii. Sheikh Suleimani Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda” kutoka katika vitabu vya historia vya Bukhari, Baghawi, na Ibnu’s-Sikkin kutoka Dhakha’iru’l-Uqba ya Imamu’l-Haram Shafi’i, na Sirat-e-Mulla wanasimulia kutoka kwa Anas Bin Harith Bin Bayya, ambaye amesema kwamba alimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Hakika, mtoto wangu Husein atauawa katika ardhi ya Karbala. Kila mtu kati yenu ambaye atakuwepo wakati huo lazima amsaidie.”

Taarifa inaendelea: “Anas Bin Harith alifika Karbala na kwa kutii amri ya Mtume, aliuawa shahidi pamoja na Imamu Husein.” Kwa hiyo ina maana kwamba kule Karbala Imamu Husein alisimama kwa ajili ya haki na sio kwa mapenzi ya dunia hii. Kuandaa safari kwa Imamu Husein akiwa na kundi dogo, wakiwemo wanawake na watoto wadogo, ni ishara nyingine kuonesha kwamba alitoka nyumbani kwake sio kwa madhumuni ya kupata mamlaka.

Kama hiyo ingekuwa ndio nia yake, angelikwenda Yemen, ambako anaungwa mkono na wengi. Yemen ingelikuwa ni kituo cha kimantiki cha kuanzishia shughuli za kijeshi. Kwa hakika rafiki zake mara nyingi wamemshawishi kwenda Yemen, lakini walikuwa hawatambui madhumuni yake. Lakini Imamu Husein alijua kwamba hakuna njia ya kupa- ta mafanikio ya dhahiri. Safari yake ilianza na watu 84, wakiwemo wanawake na watoto, akilenga kwenye msingi mzuri. Ule mti mtukufu – la ilaha ill’allah (hakuna mungu isipokuwa Allah) – ulipandwa na babu yake, ukarutubishwa na damu yake na damu ya mashahidi wa Badir, Uhud, na Hunain. Mti huo uliaminishwa kwa mtunza bustani mzuri, Ali Bin Abu Talib, ambaye alizuiwa kwa vitisho vya mauaji na uchomaji moto mali wa makusudi.

Matokeo yake ilikuwa kwamba ile chemchem ya Tawhid (upweke wa Mungu) na utume ukakumbwa na mbadiliko ya kipupwe. Taratibu utawala wa bustani ukaangukia mikononi mwa Bani Umayya waovu.

Kuanzia ukhalifa wa Uthman Bin Affan, Bani Umayya wakahodhi utawala wa dola. Abu Sufyan, mzee na kipofu, lakini daima hamu yake ya mamlaka ilikuwa kali, alipiga kelele kwenye baraza ya Bani Umayya: “Enyi Bani Umayya! Uzuieni ukhalifa kwenye familia yenu wenyewe.

Pepo na moto ni ngano za watu wa kale. Enyi Bani Umayya! Ukamateni ukhalifa kama mpira. Naapa kwa kile ambacho nakiapia, kwamba kila siku nimetamani utawala huu kwa ajili yenu. Uchungeni ili kwamba uwe ni urithi wa vizazi vyenu.”

Makafiri hawa waliwaondoa watunza bustani sahihi kutoka kwenye bustani. Maji ya uhai yalisimamishwa na mti mtukufu ulisinyaa mpaka wakati wa utawala wa Yazid, wakati ulipoonekana kuelekea kufa.

Imamu Huseini akasafiri kwenda Karbala kuinyweshea ile bustani ya utume na kuimarisha ule mti mtukufu wa la ilha ill’Allah. Baadhi ya watu wanahoji kwa nini Imamu Husein asipandishe bendera ya upinzani mjini Madina. Hawajui kwamba angebakia Madina malengo yake yangelibakia bila kueleweka. Imamu Husein alikwenda Makka katika mwezi wa Rajabu alihutubia maelfu ya watu, akiwambia kwam- ba Yazid alikuwa anaung’oa mti wa Tawhid. Alisema kwamba Yazid ambaye alidai kuwa Khalifa wa Waslamu, alikuwa anauharibu msngi wa Uislamu. Akiwa ametawaliwa na ulevi wa pombe na kamari, Yazid alijiburudisha kwa kucheza na mbwa na manyani. Imamu Husein aliona kutoa mhanga maisha yake ni muhimu kwa ajili ya kuuhifadhi Uislamu.

Imamu Husein Alikataa Ushauri Wa Kuuacha Ujumbe Wake

Marafiki wa Imamu Husein na jamaa zake wamshawishi asiende Kufa, wakisema kwam- ba watu wa Kufa waliomtaka aende kule wana sifa mbaya wasioaminika. Watu wengi walikusanyika kwa Bani Umayya na kupokea pesa na upendeleo wa kisiasa kwa malipo ya kuwaunga mkono kwao. Kwa hiyo, kwa mujibu wa wengi wa wafuasi wake, Imamu Husein hakuwa na nafasi ya kuweza kuwashinda.

Walimuomba aache safari yake hiyo. Walimhimiza aende Yemen ambako alikuwa na wafuasi wengi, na ambako angeweza kuishi kwa amani. Lakini Huseini hakuweza kuelezea ukweli wa hali yake. Hata hivyo, alimtosheleza kila mmoja kwa jibu fupi.

Aliwaambia marafiki wa karibu na jamaa zake, kama ndugu yake, Muhammad Bin Hanafiyya: Unasema jambo sahihi. Mimi vile vile najua kwamba sitapata umiliki wa dhahiri, lakini siendi kwa ajili ya ushindi wa kidunia. Ninakwenda ili nikauawe. Natamani kwamba kwa kupitia nguvu yangu ya kuteseka kwa uonevu, ningeweza kuung’oa msingi wa udhalimu na ukatili. Nimemuona babu yangu, Mtume, katika ndoto akiniambia: ‘Fanya safari ya kwenda Iraq. Allah (swt) anataka kukuona wewe ukiuliwa.’”

Muhammad Bin Hanafiyya na Ibn Abbas wakasema: “Kama hivyo ndivyo, kwa nini unakwenda na wanawake?” Akajibu: “Babu yangu amesema kwamba Allah anataka kuwaona wao wakiwa mateka. Hivyo, kutokana na amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ninawachukuwa na kwenda nao.” Kutekwa kwa wanawake kutakuwa ndio sehemu ya maamuzi ya kuuliwa kwake shahidi.

Watauonesha ulimwengu ukatili wa Bani Umayya kwa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Bibi Zainabu binti wa Ali na Fatima, alitoa hotuba fasaha ya malalamiko katika baraza ya Yazid iliyojaa watu, ambapo mamia ya watu, wakiwemo watu maarufu, watu wakubwa kutoka Bani Umayya, na mabalozi wa nje, walisheherekea ushindi wao.

Imamu wa nne, Zainu’l-Abidin Ali Ibn Husein, naye vile vile alitoa hotuba ya madai fasa- ha juu ya haki na uadilifu katika mimbari ya Msikiti wa Bani Umayya, mbele ya Yazid. Baada ya kumtukuza Allah (swt) Zainu’l-Abidin alisema: “Enye watu! Sisi kizazi cha Mtume Muhammad, tumejaaliwa na Allah sifa sita na tumefanywa wabora kwa viumbe wote kwa kupewa fadhila saba.

Tumepewa elimu, uvumilivu, ujasiri, haiba yenye kupendeza, ufasaha, ushujaa, na tunapendwa na waumini. Sisi ni bora juu ya kila mtu kwa sababu Mtume Muhammad anatokana na sisi; Siddiq Ali Bin Abu Talib anatoka kwetu; Ja’far-e-Tayyar anatoka kwetu; Hamza anatoka kwetu, wajukuu wawili wa Mtume, Hasan na Husein, wanatoka kwetu; na Mahdi wa uma huu (Imam-e-Hujjat Bin Hasan) anatokana na sisi. Mtu ambaye hanijui mimi anapaswa ajue kuhusu familia yangu na hadhi yake; mimi ni mtoto wa Mtume wa Allah aliyetukuka mno na mbora, Muhammad Mustafa!”

Kisha kutoka kwenye mimbari ileile ambayo Mu’awiya na Yazid waliitumia kumtukana Ali, Imamu alimtukuza babu yake mashuhuri wa kupigiwa mfano, Ali Bin Abu Talib, mbele ya Yazid na wakuu wa Bani Umayya.

Watu wengi wa Syria hawajawahi kusikia sifa za Ali na fadhila zake. Imamu akasema: “Mimi ni mtoto wa mtu yule ambaye alipigana mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); ambaye awalipiga makafiri kule Badir na Hunain; ambaye katu hakupoteza imani yake kwa Allah japo kwa sekunde.

Mimi ni mtoto wa mtu mchamungu mno zaidi wa waumini wote, mrithi wa mitume, muuaji wa makafir, mtawala wa Waislamu, rehema ya waabuduo, mfalme wa wale ambao wanalia kwa hofu juu ya Allah, mvumilivu mno wa wavumilivu, mbora wa wanaotekeleza Salat.

Mimi ni mtoto wa mtu ambaye alisaidiwa na Jibril na Mikail. Mimi ni mtoto wa mtu yule ambaye alikuwa mlinzi wa heshima ya Waislamu na mkataji vichwa vya makafir. Ni mtoto wa mtu yule ambaye alipigana vita takatifu dhidi ya maadui, ayelikuwa fahari ya Makuraishi, mtangulizi wa wale walioukubali ujumbe wa Allah na Mtume Wake, wa kwanza kati ya wale walioukubali Uislamu, ulimi wa hekima ya Allah, msaidizi wa dini ya Allah, mlinzi wa amri za Allah, bustani ya hekima ya Allah, hazina ya elimu Yake.

Mimi ni mtoto wa mkuu wa wenye subira, mvunjaji wa vizuizi, ambaye moyo wake ulikuwa imara zaidi, ambaye maamuzi yake yalikuwa imara zaidi, ambaye tabia yake ilikuwa imara sana kuliko mtu yeyote. Alikuwa simba mkali kwenye uwanja wa vita, ambaye aliwakata maadui na kuwaangusha chini kwa upanga wake na kuwatawanya kama upepo mkali unavyotawanya majani makavu.

Alikuwa ndiye shujaa zaidi miongoni mwa watu wa Hijaz, jasiri zaidi miongoni mwa watu wa Iraq, Mwislamu safi zaidi, yeye ambaye alikula kiapo cha utii kule Aqaba, shujaa wa Badir na Hunain, mtu jasiri zaidi wakati wa kiapo cha utii chini ya mti, mtoa kafara wa aina yake, ya kipekee wakati wa kuhama kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mkuu wa ulimwengu wa ki-Arabu, mlinzi wa Ka’ba Tukufu, baba wa wajukuu wawili wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hizi ni sifa za babu yangu, Ali Bin Abu Talib.

Mimi vile vile ni mtoto wa Khadijatul-Kubra; mimi ni mtoto wa Fatima Zahra; mimi ni mtoto wa yule ambaye ameuawa kwa dharuba nyuma ya shingo; mimi ni mtoto wa yule ambaye aliutoka ulimwengu huu akiwa na kiu; mimi ni mtoto wa yule ambaye alinyimwa maji wakati ambapo maji yaliruhusiwa kwa viumbe waliobakia. Mimi ni mtoto wa yule ambaye mwili wake haukuoshwa wala kuvishwa sanda; mimi ni mtoto wa yule ambaye kichwa chake kitukufu kilinyanyuliwa katika ncha ya upanga; mimi ni mtoto wa yule ambaye wanawake wake walikashifiwa na kunyanyaswa waziwazi katika ardhi ya Karbala na kuchukuliwa mateka. Mimi ni mtoto wa yule ambaye wanawake wake waliletwa Syria kama mateka.”

Kisha Imamu alilia kwa sauti kubwa, na kuendelea: “Mimi ni…Mimi ni…” yaani, aliendelea kueleza fadhila za wahenga zake waliomtangulia na mateso ya mtukufu baba yake na Ahlu’l-Bayt. Kama matokeo ya hotuba yake hii, watu walilia sana. Baada ya kuliwa shahidi kwa Imamu Husein, majlis ya kwanza (kikao cha maombolezo) kwa ajili ya mateso ya kikatili aliyoyapata Imamu Husein ilifanyika katika Msikiti huu mkuu wa Bani Umayya.

Imamu Zainu’l-Abidin, baada ya kusimulia sifa za Ali mbele ya maadui, alitoa maelezo yenye kugusa nyoyo juu ya mateso aliyopata mtukufu baba yake ambayo yalisababisha kilio kikubwa cha kuumiza kutoka kwa watu wa Syria mbele ya Yazid. Alitishika sana na kuondoka Msikitini pale. Ilikuwa ni kutoka Msikitini hapa, kutokana na hotuba ya Imamu, ndipo watu wakasimama dhidi ya Yazid. Kwa sababu ya kelele za upinzani mkubwa wa watu, Yazid alilazimika kumlaani Ubaidullah Bin Marjana kwa kitendo chake kiovu. Hatimaye, ngome ya dhulma ya Bani Umayya iliteketezwa. Leo hatuoni katika Syria yote kaburi hata moja la Bani Umayya.

Tukirudi kwenye swali lako, Imamu Husein mara kwa mara alitabiri kuuawa kwake shahi- di. Wakati mmoja aliwahi kusimulia mjini Makka, mnamo siku ya Tarwia (siku ya 8 ya Dhu’l-Hijja 60 A.H.), akisema: “Kifo kimeambatanishwa kwa kila mmoja wa kizazi cha Adamu kama mkufu ulivyoambatanishwa kwenye shingo ya msichana. Nina shauku ya kukutana na wahenga wangu kama vile Yaqub alivyokuwa kwa ajili ya kukutana na Yusuf. Sehemu ambayo nitafia imekwishateuliwa kwa ajili yangu, na lazima niende kwenye sehemu hiyo. Ninawaona chui mwitu wakiniuwa, wakichana vipande vipande mwili wangu kati ya Nawawi’s na Karbala.”

Imamu Husein alijua kwamba hatafika Kufa, makao makuu ya Iraqi (zama hizo). Alijua kwamba atauawa na watu ambao walikuwa kama wanyama wakali, wakikata mwili wake vipande vipande. Alifanya safari hiyo kwa madhumuni ya kufa shahidi na sio kwa sababu za kisiasa.

Njiani humo aliwambia watu juu ya kifo chake kinachomngojea. Aliwaeleza marafiki zake na jamaa zake kwamba mfano mmoja ulikuwa unatosha kuthibitihsa jinsi ulimwengu huu usivyokuwa na thamani. Alisema kwamba baada ya Nabii Yahya kukatwa kichwa chake, kichwa hicho kiliwasishwa kwa mzinifu. Alisema kwamba kichwa chake yeye hivi punde kitachukuliwa kupelekwa kwa mlevi, Yazid.

Fikiria suala hili kwa muda. Hur Bin Riyahi pamoja na kikosi cha farasi cha askari 1000 waliizuia njia ya Husein. Kufa ilikuwa umbali wa maili thalathini tu. Hurr alikuwa ameteuliwa na Ubaidullah Ibn Ziyad kumzuia Imamu Husein. Hurr alikuwa asimuachie andelee kwenda Kufa wala kuachana naye bila kupata maelekezo zaidi. Kwa nini Imamu alijisalimisha kwa Hurr? Kama Husein alikuwa akitafuta mamlaka ya kisiasa, kwa hakika asingeweza kuzuiwa na Hurr, ambaye alikuwa hana zaidi ya askari 1000. Imamu alikuwa na askari 1300.

Hali ya kuwa angewashinda, Imamu angelifika Kufa, ambako ana watu wengi wanaomuunga mkono. Kutoka huko hali ya kuwa jeshi limeongezeka nguvu, angeweza kukabiliana na adui na kupata umiliki. Lakini alikubali amri ya Hurr, alisimama pale katika jangwa akizunguukwa na adui. Baada ya siku nne majeshi ya nyongeza ya adui yaliwasili pale, na mtoto wa Mtume akalazimika kustahamili mateso ya ukatili. Ushahidi mzuri katika kuunga mkono maoni yangu ni hotuba ya Imamu katika usiku wa kuamkia Siku ya Ashura. Mpaka usiku ule askari 1300 walikuwa wako tayari kupigana kwa ajili yake.

Husein aliwakusanya watu hao pamoja na akawaambia: “Wale ambao wamekuja kwa ajili ya kupata faida ya kidunia, basi wajue kwamba yeyote atakayebakia hapa kesho katika ardhi hii atauawa. Adui ana haja na mimi peke yangu; naondoa nguvu ya kifungo cha utii kutoka katika shingo zenu. Huu sasa ni usiku, na mnaweza kuondoka katika giza hili la usiku.” Wengi walikubali pendekezo lake na wakaondoka. Watu 42 tu walibakia, 18 Bani Hashim na 24 Masahaba.

Baada ya usiku wa manane, askari 30 wa adui walielekea kwenye kambi ya Imamu kwa ajili ya mashambulizi ya usiku, lakini walipom- sikia Husein akisoma Qur’ani Tukufu, walijawa na jazba na wakaungana na Imamu. Hawa ndio wale watu 72 waliojitolea mhanga maisha yao Siku ya Ashura. Wengi wao walikuwa wachamungu, na wengi walikuwa ni wasomaji wa Qur’ani Tukufu.

Leo mhanga mtukufu wa Husein unakubaliwa na marafiki na maadui kwa pamoja. Hata wale ambao ni wageni katika dini yetu wamevutia na ushujaa wake. Katika Da’iratu’l- Ma’rif ya Kifaransa, kuna makala ndefu yenye anwani ya “Mashahidi watatu” iliyoandikwa na mwanachuo mwanamke wa Kiingereza. Dhamira yake ni kwamba katika historia yote kumekuwa na mashahidi watatu, ambao kwa kujitolea kwao mhanga maisha yao, wamekuwa kivutio kikubwa katika kuendeleza njia ya haki. Wa kwanza alikuwa ni Socrates, na wa pili alikuwa ni Yesu - Isa Masihi (mwandishi alikuwa ni Mkristo). Sisi Waislamu, kwa hakika tunaamini kwamba Isa hakusulubiwa. Qur’ani Tukufu kwa uwazi inasema:

وﻗَﻮﻟﻬِﻢ اﻧﱠﺎ ﻗَﺘَﻠْﻨَﺎ اﻟْﻤﺴﻴﺢ ﻋﻴﺴ اﺑﻦ ﻣﺮﻳﻢ رﺳﻮل اﻟﻪ وﻣﺎ ﻗَﺘَﻠُﻮه وﻣﺎ ﺻﻠَﺒﻮه وﻟَٰﻦ ﺷُﺒِﻪ ﻟَﻬﻢ ۚ وانﱠ اﻟﱠﺬِﻳﻦ اﺧْﺘَﻠَﻔُﻮا ﻓﻴﻪ {ﻟَﻔ ﺷَﻚٍّ ﻣﻨْﻪ ۚ ﻣﺎ ﻟَﻬﻢ ﺑِﻪ ﻣﻦ ﻋﻠْﻢ ا اﺗّﺒﺎعَ اﻟﻈﱠﻦ ۚ وﻣﺎ ﻗَﺘَﻠُﻮه ﻳﻘﻴﻨًﺎ {157

{ﺑﻞ رﻓَﻌﻪ اﻟﻪ اﻟَﻴﻪ ۚ وﻛﺎنَ اﻟﻪ ﻋﺰِﻳﺰا ﺣﻴﻤﺎ {158

“Na hawakumuuwa wala hawakumsulubisha, bali walifananishwa kwao (mtu mwingine, kama Isa), na kwa hakika wale ambao wanatofautiana kwalo wana shaka juu ya hilo. Hawana elimu kuhusiana nalo, bali hufuata dhana tu. Kwa yakini hawakumuuawa. Hasha! Allah alimchukuwa juu Kwake.” (Qur’ani 4:157-158)

Shahidi wa tatu, anaandika mwanamke huyu, alikuwa ni Husein, mjukuu wa Muhammad. Anaandika: “Wakati tunapokusanya matukio ya kihistoria na kuyaangalia yale mazingira ambamo watu hawa watatu walitoa maisha yao, tunakubali kwamba mhanga wa Husein uliipita ile mingine miwili. Ukweli ulikuwa kwamba, Socrates na Yesu walitoa tu maisha yao wenyewe kwa kafara katika njia ya Mungu, lakini Husein alitoka nyumbani kwake kwenda nchi ya mbali ya jangwa kwenda kuzunguukwa na adui.

Yeye na familia yake yote waliuawa mashahidi kwa ajili ya kutetea njia ya haki. Aliwapeleka rafiki na jamaa zake kumkabili adui na kutoa mhanga maisha yao kwa ajili ya dini ya Allah. Hii kwa hakika ilikuwa ni ngumu mno kuliko kutoa maisha yake mwenyewe.”

Mfano wa dhahiri zaidi wa mateso ya udhalimu aliyopata Husein ulikuwa ni yale mauaji ya kikatili ya mtoto wake mdogo wa miezi sita. Alimbeba mtoto mikononi mwake akiomba maji kwa ajili yake (ambayo yalikuwa mengi), lakini maadui wakatili wale, badala ya kumpa maji, walimuuwa mtoto yule kwa mshale. Ushenzi huu wa maadui unathibitisha kwamba Imamu Husein alikuwa ni muathiriwa wa udhalimu.

Uvumilivu wake wa kushangaza ulivunjilia mbali kabisa nguvu za Bani Umayya na uliwashutumumbele ya ulimwengu. Ilikuwa ni kwa ajili ya mihanga yake na Ahlu’l-Bayt wake watukufu ambapo dini ya Muhammad ilipata uhai mpya.

Nawab: Kwa hakika tunawiwa mno na wewe. Tumevutiwa sana na maelezo yako ya mambo yanayomhusu Imamu Husein. Mpaka sasa tulikuwa tunafuata watu wengine na tulikuwa tunazikosa fadhila za ziarat (kuzuru kaburi tukufu la Imamu). Tumeambiwa kwamba kuzuru kaburi la Imamu Husein ni bida’a “uzushi.” Ama kwa hakika ni bida’a nzuri iliyoje hiyo, kwa vile humfanya mtu awe na ari na kumsaidia aelewe ukweli kuhusu kizazi cha Mtume.

Maana Halisi Ya Bida’a (Uzushi)

Muombezi: Neno “bidat,” lina asili yake katika madhehebu ya maulamaa wa ki-Sunni na ya Nasib na Khawarij, ambao walikuwa ni maadui waliothibitika wa Ali. Wameiita ziarat “bida’a” bila kufikiria ukweli kwamba bida’a inahusian na jambo linalohusu Mtume au Ahlul’Bayt wake, ambalo halikuamriwa na Allah.

Hata hivyo, kuhusu suala la kuzuru kaburi la Husein, kuna hadithi nyingi katika vitabu vya maulamaa wenu wenyewe. Nitakomea kwenye hadithi moja mashuhuri iliyoandikwa katika vitabu vyote vya maqatil na hadith mukhtar.

“Siku moja Mtume alikuwa nyumbani kwa Aisha wakati Husein alipoingia ndani. Mtume alimchukuwa mikononi mwake, akambusu na kumnusa. Aisha akasema: ‘Maisha ya baba yangu na mama yangu yawe mhanga kwa ajili yako! Kiasi gani unampenda Husein!’

Mtume akasema: ‘Hujui kwamba mtoto huyu ni sehemu ya ini langu na ua langu?’ Baada ya hapo Mtume akaanza kulia.

Aisha akauliza sababu ya kulia kwake. Mtume akajibu kwamba alibusu mahali ambako Bani Umayya watakuja kumjeruhi Husein. Aisha akauliza kama watamuuwa.

Akasema, ‘Ndio atauawa. Hawatapata usaidizi wangu (kesho akhera). Aliyebarikiwa ni yule anayekwenda kuzuru kaburi lake baada ya shahada yake.’ Aisha akamuuliza Mtume, ni malipo gani yatakuwa kwa ajili ya ziarat hiyo. Mtume akasema: ‘Itakuwa ni sawa na hijja yangu moja.’ Aisha akasema, ‘Hijja moja ya kwako!’ Akasema, ‘Hapana, mbili,’ Aisha alipoonesha mshangao tena, akasema, ‘Hapana, Hijja nne.’

Jinsi alivyozidi kuonesha mshangao ndivyo malipo yalivyozidi kuongezeka, mpaka mwishowe akasema, ‘Aisha! Kama mtu atakwenda kuzuru kabutri la Husein, Allah atampa malipo sawa na Hijja 90 na Umra 90 zilizofanywa na mimi.’ Kisha Aisha akanyamaza.’” Sasa nakuulizeni, Ziarat kama hiyo ni uzushi (bida’a)?

Faida Za Kuzuru Makaburi Ya Maimamu Watukufu

Kuna faida nyingine ambazo hupatikana kwa kuzuru makuburi ya Maimamu. Sehemu za ndani kabisa za eneo la kaburi, zinazoitwa haram, hubakia wazi kwa ajili ya wangeni usiku na mchana. Haram hizo na misikiti karibu yake kwa kawaida huwa zinakutwa zimejaa mahujaji na wafanyao ibada.

Wale ambao wamezoea kusali si zaidi ya Salat za wajibu mara nyingi hufanya jitihada maalumu za kiibada wakati wa kuzuru makaburi matukufu. Wanamuomba Allah kwa unyofu na kusoma Qur’ani. Je, ibada kama hiyo ni bida’a?

Nawab: Kwa hakika hatuna wa kumlaumu isipokuwa sisi wenyewe kama hatukuyaangalia mambo haya kwa ukaribu zaidi. Miaka michache iliyopita nilikwenda Baghdad kuzuru kaburi la Imam A’Dham Abu Hanifa na Abdu’l-Qadir Jilani. Siku moja nilikwenda kutembea karibu ya Kadhmain (sehemu aliyozikwa Imamu wa saba, Musa Ibn Ja’far Al-Kadhim na Imamu wa tisa, Muhammad Ibn Ali at-Taqi).

Wakati niliporudi, wenzangu walinilaumu vikali sana. Nashangaa kwamba kuzuru makuburi ya Imam A’dham huko Mu’dham, Sheikh Abdu’l-Qadir huko Baghdad, la Khwaja Nidhamu’d-Din huko India, la Sheikh Akbar Muhyi-d-Din Ibn Arabi huko Misr kunaweza kuchukuliwa kwamba kunastahili malipo ya thawabu. Kila mwaka watu wengi miongoni mwa madhehebu ya Sunni huzuru sehemu hizi ingawa Mtume kamwe hajalipendekeza hilo. Inawezekana vipi kwamba ziarat kwenye kaburi la Shahidi mkuu, mjukuu wa Mtume, ambayo Mtume ameipendekeza, iambiwe kuwa ni bida’a?

Naamua kwa dhati kabisa kwamba, Allah akipenda, mwaka huu nitakwenda kuzuru kaburi la mjukuu kipenzi cha Mtume, Husein. Nitamuomba Allah anisamehe makosa yangu yaliyopita.

Mkutano Wa Nane; Alkhamisi Usiku ( 1 Shaban, 1345 A.H.)

Sayyid Abdu’l-Hayy: Mheshimiwa, usiku uliopita ulichangia katika kutokuelewana miongoni mwa Waislamu.

Muombezi: Nieleze jinsi nilivyofanya hivyo.

Sayyid: Wakati unaelezea “sisi wenyewe”, uliwagawanya Waislamu kwenye makundi mawili: Waislamu na waumini. Lakini waislamu wote ni kitu kimoja na wako sawa. Wale wanaosema maneno “Hakuna mungu isipokuwa Allah na Muhammad ni Mjumbe Wake,” hao ni ndugu.

Hawapasi kutenganishwa katika makundi mawili kwa sababu hili lina mad- hara kwa Uislamu. Mashi’a wanajiita wenyewe waumini, na wanatuita sisi Waislamu. Lazima utakuwa umeona kwamba kule India Mashi’a wanaitwa waumini na Masunni wanaitwa Waislamu.

Ukweli ni kwamba ‘Uislamu na ‘Iman’ ni maneno yanayofanana kwa sababu Uislamu maana yake kukubali amri za dini. Utambuzi huu ndio ukweli wa ‘Iman.’ Umma wote umekubali kwamba Uislamu ni Iman halisi. Umekwenda kinyume na maoni ya wengi.

Tofauti Kati Ya Uislamu Na Imani

Muombezi: Kwanza, rejea yako juu ya watu wa kawaida haina maana ya watu wa umma wote kwa ujumla. Inarudi kwa watu wa kawaida wa kundi la Masunni. Pili, maelezo yako kuhusu Uislamu na Imani sio sahihi. Sio Mashia tu wanaohitalifiana na Masunni bali hata ma-Ash’ari, Mu’tazali, Mahanafi, na Mashafii vile vile wana maoni tofauti kuhusu hilo.

Tatu, mimi kwa kweli sielewi ni kwa nini mwanachuoni kama wewe unakimbilia pingamizi zisizo na maana. Mgawanyo huu katika makundi mawili umefanywa na Allah katika Qur’ani Tukufu. Pengine umesahau lile suala linalohusiana na Masahaba wa kuliani na Masahaba wa kushotoni waliotaja katika Qur’ani Tukufu ambayo inasema: “Wakaaji wa jangwani wanasema: ‘tumeamini.’ Sema: ‘Hamjaamini bali semeni, tumenyenyekea (tumesilimu); lakini imani bado haijaingia nyoyoni mwenu.’” (Qur’ani; 49:14)

Kwa hakika lazima uelewe kwamba aya hii iliteremshwa katika kuwalaumu lile kabila la jangwani la Bani Asad, ambao walikuwa Waislamu kwa majina tu. Wakati wa mwaka wa ukame, walijazana mjini Madina, na ili kupata msaada walidai kwamba wao ni waumini. Lakin nyoyoni mwao walikuwa si waumini kwa Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aya hii inathibitisha kwamba kuna makundi mawili ya Waislamu.

Waislamu waaminifu, ambao wamekubali uhalisi wa Imani, na wale ambao wanatamka imani maneno kwa mdomo tu. Katika nyanja yetu ya kijamii kundi la mwisho wanapasika na usalama na manufaa ya sheria zilizokusudiwa kwa Waislamu wote.

Lakini, kwa mujibu wa amri za Qur’ani Tukufu, hawapasiki na malipo yoyote katika akhera. Kutamka kwao kwamba hakuna mungu ispokuwa Allah na Muhammad ni Mjumbe Wake, na kujionyesha kwao katika jambo la kwamba wao ni Waislamu, hakuna maana ya kweli.

Sayyid: Umesema sawa, lakini Uislamu bila Imani hauna maana, kama vile ambavyo Imani bila Uislamu haina ubora. Allah anasema katika Qur’ani Tukufu: “Na msimwambie anayekutoleeni salamu: ‘Wewe sio muumini...... ’” (Qur’ani; 4:94).

Aya hii inathibitisha kwamba lazima tumtendee mtu kwa mujibu wa mtu anavyoonekana kwa nje. Kama mtu yeyote atasema, “Hakuna mungu isipokuwa Allah na Muhammad ni Mjumbe wa Allah,” lazima tukubali imani yake. Hii yenyewe ni ushahidi mzuri kwamba Uislamu na Imani ni maneno yanayofanana.

Muombezi: Aya hii iliteremshwa kuhusiana na mtu mahususi, imma Usama Bin Zaid au Muhallam Bin Jasama-e-Laisi, ambaye inasemekana aliuwa mtu katika vita, mtu ambaye ametamka, “Hakuna mungu isipokuwa Allah.” Aliuawa kwa dhana kwamba alitamka maneno haya kwa woga. Lakini kwa vile unafikiri kwamba iko katika hali ya ujumla, sisi vile vile tunawaona Waislamu wote kuwa ni safi.

Labda kwa kweli pale tunapowaona wakikiuka ile misingi ya dini. Lakini kuna tofauti kati ya Uislamu na Imani kwa sababu kuna daraja mbali mbali za Imani. Imam Ja’far Bin Muhammad As-Sadiq anasema katika hadithi ya Umar na Zubair: “Amma kuhusu Imani kuna masharti, daraja, na hatua. Baadhi ya hizo ni dhaifu na udhaifu wao uko wazi; baadhi ni nzuri zenye uzito; baadhi zimetimia na zimefikia ukamilifu.”

Imani dhaifu ni hatua ya kwanza kabisa ambayo kwamba mtu hupita kuingia katika Uislamu kutoka kwenye ukafiri. Daraja za juu za Imani zinawezekana. Rejea zake zimeta- jwa katika baadhi ya hadithi. Miongoni mwao ni hadithi katika Usul Kafi na Nahju’l- Balagha kutoka kwa Amir wa Waumini (Ali) na Ja’far Bin Muhammad As-Sadiq ambaye amesema: “Allah ameigawanya Imani katika daraja saba ambazo ni wema, ukweli, kusadikisha kwa moyo, kujisalimisha kwenye utashi wa Allah, utii, elimu, na uvumilivu.

Sifa hizi saba zimegawanywa bila ulingano miongoni mwa wanadamu. Mtu ambaye anazo sifa zote hizi ni muumini kamili. Kwa hiyo, Uislamu uko katika kundi la kwanza la Imani, ambamo kuna tamko la mdomo la imani katika utume wa Muhammad na Upweke wa Allah. Imani haijaingia katika moyo wa mtu kama huyo. Mtume wa Allah alikiambia kikundi cha watu: ‘Enyi watu! Ninyi ni miongoni mwa wale ambao mmekubali Uislamu kwa ndimi zenu, lakini bado kwa nyoyo zenu.’”

Ni dhahiri kwamba Uislamu na Imani viko tofauti. Lakini hatutakiwi kupekuwa nyoyo za watu wengine. Nilisema usiku uliopita kwamba dalili ya muumini ni vitendo vyake.

Lakini hatuna haki ya kuchunguza kuhusu vitendo vya Waislamu. Hata hivyo tunalazimika kuonyesha tabia za Imani, ili kwamba wale ambao wamezama katika usingizi waweze kutiwa moyo wa kutekeleza wajibu wao. Hivyo wataelewa ukweli wa Imani na watajua kwamba wokovu katika akhera utakuja tu kwa kufanya matendo mema, kama hadithi inavyosema: “Imani maana yake kukiri kwa ulimi, kusadikisha katika moyo, na kutenda kwa viungo vyetu.” Kukiri kwa ulimi na kusadikisha moyoni ni vitangulizi vya vitendo.

Naam tunajua kwamba ulimwengu huu mbaya ni utangulizi tu wa ulimwengu ujao. Njia ya wokovu kwa ajili ya mtu huyo imefungwa katika akhera mpaka awe ni mtu mwenye kufanya matendo mema hapa duniani. Allah (swt) anasema katika Qur’ani Tukufu:

{واﻟْﻌﺼﺮِ {1

{انﱠ اﻧْﺴﺎنَ ﻟَﻔ ﺧُﺴﺮٍ {2

{ا اﻟﱠﺬِﻳﻦ آﻣﻨُﻮا وﻋﻤﻠُﻮا اﻟﺼﺎﻟﺤﺎتِ وﺗَﻮاﺻﻮا ﺑِﺎﻟْﺤﻖ وﺗَﻮاﺻﻮا ﺑِﺎﻟﺼﺒﺮِ {3

“Naapa kwa Zama! Hakika mwanadamu yumo katika hasara, isipokuwa wale walioamini na wakatenda matendo mema…” (103:1-3)

Kwa ufupi, kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu, uchamungu ndio msingi wa Imani. Na kama mtu hana matendo mema katika sifa yake, kukubali kwake kwa mdomo au kusadikisha kwenye moyo bado kutamuacha mbali na Imani. Kama ni kweli kwamba inatupasa kumchukulia kila mtu kuwa ni Mwislamu, yule ambaye anasema , “Hakuna mungu isipokuwa Allah na Muhammad ni Mjumbe wa Allah,” kwa nini mnawachukilia Mashi’a kama makafiri?

Hakika Mashi’a wanaamini katika upweke wa Allah, utume wa Muhammad, Kibla moja, Kitabu kimoja. Wanatekeleza matendo yote ya wajibu, wanatekeleza saumu kama ilivyoelekezwa, wanakwenda kuhiji, wanatoa khums na zakat (kodi za kidini), wanaamini kufufuliwa katika mwili, na Siku ya Hukumu.

Je, ninyi sio ndio mnaosababisha utengano miongoni mwa Waislamu? Mnawatenga mamilioni ya Waislamu na kuwaita makafiri ingawa hamna hata chembe ya ushahidi kuun- ga mkono madai yenu. Hamtambui kwamba hizi ni mbinu za maadui ambao wanataka kusababisha migogoro miongoni mwa Waislamu kwa njia za uwongo kama huu.

Ukweli ni wamba hatuna tofauti katika misingi ya imani isipokuwa katika Uimamu na ukhalifa. Na vipi ingekuwa kama kungekuwa na tofauti katika matendo ya imani? Hitilafu kama hizo zipo miongoni mwa madhehebu zenu nne, nazo ni mbaya zaidi kuliko zile zilizoko kati yetu na ninyi. (haitakuwa sahihi sasa kuonyesha tofauti kati ya madhehebu za Hanafia na Maliki au kati ya Shafi’i na Hanbal.).

Kwa maoni yangu mimi, ninyi hamna hata chembe ya ushahidi kuthibitisha ushirikina au ukafiri wa Mashi’a. Kosa pekee la Mashi’a lisilosameheka, kwa mujibu wa kile walichoeneza Khawariji na Manasibi, kwa njia ya Bani Umayyah ni kwamba Shi’a hawapoto- shi katika kutafsir hadithi.

Hawawapi nafasi watu kama Abu Huraira, Anas, na Samura kuwa kati ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na sisi. Hata maulamaa wenu wenyewe na makhalifa wenu wakubwa waliwashutumu kama waongo.

Kosa kubwa wanalohusihswa nalo Mashia ni kwamba wanafuata kizazi cha Mtume, Ali na Maimamu kumi na mbili, na sio hao Maimamu wanne. Lakini ninyi hamna ushahidi kutoka kwa Mtume unaoonyesha kwamba ni lazima Waislamu wawafuate Ash’ari, au Mu’tazali katika misingi ya imani na Maliki, Hanafi, Hanbal nau Shafi’i katika matendo ya ibada.

Kwa upande mwingine kuna maelekezo mengi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yanayotuambia kwamba kizazi na Ahlul’l-Bayt wa Mtume wanalingana na Qur’ani Tukufu, na kwamba umma lazima ushikamane nao.

Miongoni mwa hadithi hizo ni ‘Hadith Thaqalain’, ‘Hadth-e-Safina’, ‘Hadith-e-Bab-e-Hitta’. Je, unaweza kunukuu hadthi moja tu ambayo kwayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema kwmba baada yake yeye watu wake lazima wamfuate Abu’l-Hasan Ash’ari na Wasil Bin Ata, na kadhalika, katika misingi ya imani na mmojawapo wa Maimamu wanne – Malik Bin Anas, Ahmad Bin Hanbal, Abu Hanifa, au Muhammad Bin Idris Shafi’i katika matendo ya ibada?

Sheikh Suleiman Balkhi Hanafi katika kitabu chake Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 4, anasimulia kutoka kwa Fara’id Hamwaini akinukuu kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Amirul-Mu’minin (Ali): “Ewe Ali! Mimi ni Jiji la elimu na wewe ni Lango lake. Hakuna mtu awezaye kuingia katika jiji bila kwanza kuingia katika lango.

Ni mwongo yule anayedai kunipenda mimi ambapo akiwa ni adui yako, kwa sababu wewe watokana na mimi na mimi natokana na wewe. Nyama yako ni nyama yangu, damu yako ni damu yangu, nafsi yako ni nafsi yangu, haiba yako ndio haiba yangu mimi.

Amebarikiwa yule mtu ambaye anakutii wewe, ole wake yule ambaye anakuasi wewe. Rafiki yako ni mwenye kunufaika, na adui yako yuko kwenye hasara. Mtu ambaye yuko pamoja na wewe amefuzu, na mtu ambaye yuko mbali na wewe amepotea. Baada yangu mimi, wewe na Maimamu wote katika kizazi chako ni kama Safina ya Nuh: ambaye atapanda humo ataokolewa, na yeyote yule ambaye atakataa kupanda humo ataangamia. Mfano wao (Maimamu) ni kama nyota: wakati nyota moja inapozama, nyingine hutokeza. Mpangilio huu utaendelea mpaka Siku ya Kiyama.”

Imeelezewa wazi kabisa katika Hadith-e-Thaqalain (inayokubaliwa na madhehebu zote) kwamba “Kama mtashikamana na Ahlul’-Bayt, kamwe hamtapotea.” Hata shupavu Ibn Hajar Makki anaandika katika matokeo ya utafiti wake katika Sawa’iq Muhriqa, Sura ya 2 sura ndogo,1, uk. 92, kuhusiana na aya ya Qur’ani Tukufu: {وﻗﻔُﻮﻫﻢ ۖ اﻧﱠﻬﻢ ﻣﺴﯩﻮﻟُﻮنَ {24

“Na wasimamisheni hakika hao wataulizwa. (37:24)

Na Sheikh Suleiman Balkhi Hanafi vie vile amenukuu kutoka kwenye Sawa’iq katika kitabu chake Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 95, uk. 296, (kilichochapishwa Istanbul) akisema kwamba hadithi hii imesimuliwa katika njia tofauti. Ibn Hajar anasema: “Hakika, hadithi ya kushikamana na ‘Vitu Viwili Vizito’ (Thaqalain) imesimuliwa katika njia tofauti, imesimuliwa na Masahaba zaidi ya 25 wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Ibn Hajar anasema kuhusiana na aya hiyo hapo juu ya Qur’ani kwamba Siku ya Hukumu, watu watauliza kuhusu Wilayat ya Ali na kizazi cha Mtume.

Anaandika kwamba kwa mujibu wa baadhi ya vyanzo, hadithi hii ilisimuliwa katika siku ya Arafa, na baadhi wanasema ilisimuliwa wakati Mtume yuko katika kitanda cha mauti na nyumba yake ikiwa imejaa Masahaba wake. Wengine wanasema ilikuwemo ndani ya hotuba yake ya mwisho baada ya Hija ya muago.

Ibn Hajar anatoa maoni yake kuhusiana na sehemu mbalimbali ilikosimuliwa hadithi hii: “Hakuna kutokulingana katika uwezekano kwamba Mtume katika kupenda kwake kuonesha Utukufu wa Qur’ani na kizazi chake kitukufu, alirudia rudia hadithi hii katika sehemu hizi na nyingine tofauti. Imesimuliwa kwa usahihi kabisa kwamba Mtume alisema: ‘Ninakuachieni miongoni mwenu vitu viwili vizito: kama mkivifuata, kamwe hamtapotea. Na viwili hivyo ni Kitabu cha Allah (Qur’ani) na Ahlul-Bayt wangu.’

Tabrani ameisimulia hadithi hii na nyongeza hii: “Angalieni jinsi mtakavyojihusisha na viwili hivi: Qur’ani na Ahlul’l-Bayt, hivyo msijaribu kuwatangulia, vinginevyo mtaangamia. Msiwapuuze, vinginevyo mtaharibikiwa. Msijaribu kuwafundisha, kwani wao wanajua zaidi kuliko ninyi.”

Hata Ibn Hajar mshupavu, baada ya kunukuu kutoka kwa Tabrani na wengine, anaandika: “Mtume aliita Qur’ani na kizazi chake, ‘Vizito Viwili ’ kwa sababu viwili hivi ni vizito mno na vitukufu katika kila kipengele.” Mtume vile vile alisema: “Namshukuru Allah ambaye ameijaza mioyo ya Ahlul’l-Bayt wangu kwa hekima.” Na Mtume vile vile alisema katika hadithi iliyotajwa huko mwanzoni: “.....Na kamwe msijaribu kuwafundisha (kizazi changu) kitu chochote kwa vile ni wenye elimu zaidi ya ninyi wote.

Muwaone ni bora kwa maulamaa wenu wote kwa sababu Allah amewaumba safi (watoharifu) na amewatambulisha kwenye umma kuwa na uwezo za kimiujiza na sifa nyingi nyingine zisizo na idadi.”

Kuna nukta moja katika hadithi hii ambayo inasisitiza kushikamana kwa Ahlul’l-Bayt: yaani, kwamba mfuatano wa vizazi vya Ahlul’l-Bayt, hautakatika mpaka Siku ya Hukumu. Inashangaza kwamba baadhi ya watu wanakiri kwamba watu wa Ahlul’l-Bayt wana elimu kubwa lakini wanakiuka amri za Mtume na kuwafanya kama viongozi wao; wale watu wengine ambao hawana haki ya kutangulizwa. Je, mnaweza ninyi au sisi kubadisha Qur’ani Tukufu? Je, tunaweza kuchangua kitabu kingine chochote?

Sayyid: Hapana, haiwezekani kamwe. Hii ni amana ya Mtukufu Mtume, ujumbe mtukufu, na chanzo kikuu kabisa cha mwongozo.

Muombezi: Mwenyezi Mungu akubariki! Umezungumza kweli kabisa. Wakati tukiwa hatuwezi kuibadili Qur’ani tukufu na kuiwekea kitabu kingine badala yake, kanuni hiyo hiyo ni lazima ifuatwe kuhusiana na wale ambao wanalingana na hiyo Qur’ani tukufu. Hivyo, ni kwa mujibu wa kanuni gani ambayo kwamba wale ambao hawatokani na kizazi cha Mtume walikubaliwa kuwapita wale wa kizazi chake?

Nataka jibu rahisi kwa swali hili ili tuweze kujua iwapo kwamba wale makhalifa watatu - Abu Bakr, Umar, na Uthman - walitokana na Ahlul-Bayt wa Mtume (s.a.w.w.), na kwamba walijumuishwa katika hadith zile tulizozitaja (ya Thaqalain, Safina na Bab-e-Hitta). Kama wameingizwa, basi lazima tuwafuate, kwa mujibu wa maagizo ya Mtume.

Seyyed: Hakuna anayeamini kwamba yeyote kati ya makhalifa hao, mbali na Ali, walikuwa wameingizwa kwenye Ahlul-Bayt wa Mtume. Kama ilivyo, makhalifa hao watatu waliotajwa walikuwa ni masahaba wazuri wa Mtume (s.a.w.w.)

Muombezi: Je, Mtume alituambia tufuate mtu maalum au kikundi cha watu? Ikiwa kundi moja linasema kwamba ni jambo lenye manufaa kufuata watu wengine, hivi tumtii Mtume ama tufuate uangalifu kama ulivyoamuliwa na umma?

Seyyed: Ni dhahiri kwamba utiifu kwa Mtume ni wajibu wa lazima.

Muombezi: Baada ya kwamba Mtume ametuelekeza tufuate Qur’ani tukufu na kizazi chake, kwa nini wamependelewa kufuatwa wengineo? Je, Abul-Hasan Ali bin Isma’il Ash’ari, Wasil bin Ata, Malik bin Anas, Abu Hanifa, Muhammad Idris Shafi’i na Ahmad Hanbal walitokana na kizazi cha Mtume au Amirul-Mu’minin Ali na wale kumi na moja toka kwenye kizazi chake?

Seyyed: Ni wazi kabisa, hakuna ambaye amewahi kamwe kusema kwamba watu hawa wanatokana na kizazi cha Mtume, lakini walikuwa mafaqihi maarufu na watu wachamungu wa umma.

Muombezi: Lakini kwa mujibu wa makubaliano ya pamoja ya umma, maimamu hawa kumi na mbili ni kizazi cha moja kwa moja cha Mtukufu Mtume. Ulamaa wenu wenyewe wanakubali kwamba wao wanalingana na Qur’ani tukufu, na kwamba utii kwao unaongoza kwenye uongofu. Zaidi ya hayo, Mtukufu Mtume alisema kwamba wao ndio wenye elimu zaidi kati ya watu.

Kwa kuzingatia kanuni hizi mbili zenye nguvu, ni majibu gani watakayotoa wakati Mtume atakapowauliza ni kwa nini walikiuka miongozo yake yeye, na wakawaachia watu wengine kukitangulia kizazi chake? Kuna maagizo yoyote kutoka kwa Mtume kwamba hawa Ashari na Mu’tazila wawafuate viongozi wao au kwamba Maliki, Hanbali, Hanafi na Shafi’i wawafuate viongozi wao katika matendo ya ibada? Hakuna yoyote kiasi kwamba aliyataja majina yao kwa miaka 300 baada ya kifo cha Mtume. Ni baada ya hapo tu, kwa sababu za kisiasa au nyinginezo ambazo mimi sizitambui, wao ndipo wakatokea uwanjani. Lakini hawa Maimam na kizazi cha Mtukufu Mtume walikuwa wakijulikana vema wakati wa uhai wa Mtume mwenyewe. Ali, Hasan, Husein na Fatima walikuwa wakijulikana kama Ahlul- Kisa’a, yaani “watu wa chini ya shuka.” Walikuwa ni wao ambao kwa sifa zao ile “Aya ya Utakaso” - Ayat-Tathiira - ilishuka kwa ajili yao. Hivi inafaa kweli, kuwaita wale wanaowafuata Ali, Hasan, Husein na wale Maimam wengine kuwa ni makafiri? Mmewafadhilisha wale ambao hawatokani na kizazi cha Mtume juu ya wale ambao walikuwa mafaqihi wakamilifu, wa kupigiwa mfano.

Ni majibu gani mtakayotoa kwenye mahakama tukufu ya haki mtakapoulizwa ni kwa nini mliwapotosha watu, kwa nini mliwaita wafuasi wa Ahlul-Bayt makafiri na wazushi?

Mnatutia makosani kwa sababu sisi sio wafuasi wa kanuni za kiimani za wa-Hanafi, Maliki, Hanbali au Shafi’i. Na bado hamumfuati Ali, licha ya maagizo ya wazi na ya dhahiri kabisa kutoka kwa Allah na Mtume wake kwamba mnapaswa kufanya hivyo. Bila ya sababu nzuri za maana, mnafuata moja ya madhehebu nne hizi na mmeifunga milango elimu ya sharia - fiqh.

Sayyed: Tunategemea juu ya Maimam hawa wanne kwa namna ileile kama ninyi mnavyotegemea kwa Maimam kumi na mbili.

Muombezi: Vizuri sana! ni jambo zuri kiasi gani hilo ulilosema! Idadi ya Maimam kumi na mbili haikuainishwa na Mashi’a au ulamaa wao karne nyingi baada ya kifo cha Mtume. Hadithi nyingi zilizosimuliwa na kutoka kwenye vyanzo vya wote, Shi’a na Sunni, zinathibitisha kwamba Mtume mwenyewe aliiainisha idadi hiyo ya Maimam kuwa ni kumi na mbili.

Miongoni mwa ulamaa wenu ambao wamesimulia jambo hili ni Sheikh Sulayman Qanduzi

Hanafi, ambaye anaandika katika Yanabiul-Mawadda yake, Sura ya 77, kuhusiana na tamko hili: “Watakuwepo makhalifa kumi na mbili baada yangu.”

Yahya bin Hasan katika Kitabul-Umma amesimulia kwa njia ishirini kwamba Mtukufu Mtume amesema kwamba warithi wake watakuwa ni kumi na mbili kwa idadi, na wote watatokana na Quraishi. Imesimuliwa kwa njia tatu ndani ya Sahih Bukhari, katika njia tisa ndani ya Sahih Muslim, kwa njia tatu ndani ya Sunnan Abu Dawuud, kwa nji moja ndani ya Sunnan-Tirmidhi, na kwa njia tatu ndani ya Jam’- e-Bainas-Sahihain ya Hamidi.

Wako ulamaa wenu wengi, kama vile Hamwaini katika Fara’id, Khawarizmi na ibn Maghazili kila mmoja katika Manaqib yake, Imam Tha’labi katika Tafsiir yake na ibn Abil-Hadid ndani ya Sharh Nahajul- Balaghah, na Sayyid Ali Hamadani Shafi’i katika Mawaddatul-Qubra, Mawadda 10.

Wote wamesimulia hadithi kumi na mbili zilizosimuliwa na Abdullah ibn Abbas, Ubaya bin Rabi’i, Za’id bin Haritha, Abu Huraira na Amirul- Mu’minin Ali. Wote hawa wanasimulia kwa njia tofauti, lakini maneno yale yale kwamba Mtume amesema kwamba idadi ya warithi wake na Maimam watakuwa w12 na kwamba wote watatokana na Maquraishi.

Baadhi ya hadith zinasema kwamba wao watatokana na Bani Hashim. Katika baadhi ya riwaya yale majina mahususi ya warithi kumi na mbili hao pia yametajwa. Wengine wao wanatoa idadi tu. Nimetoa kati ya hadith nyingi za ulamaa wenu. Sasa je, mnaweza kuta- ja hadith moja tu ambayo inaashiria kwamba idadi ya warithi wake watakuwa wanne tu? Hata kama ingekuwepo hadith moja tu kama hiyo, sisi tutaikubali kuliko ile ya kwetu wenyewe.

Bila kuzingatia ukweli kwamba hamuwezi kunukuu hadith hata moja kuhusu maimam wenu wanne, kuna tofauti kubwa sana kati ya Maimam wa Shi’a na hao Maimam wenu. Maimam wetu kumi na mbili ni warithi walioteuliwa ki-mbinguni.

Kuhusu maimam wenu, ni kiasi hiki tu kinachoweza kukubalika: walikuwa na elimu ya fiqhi (sharia za kiislam) na waliweza kutafsiri Qur’ani tukufu na hadith. Baadhi yao, kama Abu Hanifa, kulingana na kukiri kwa ulamaa wenu wenyewe, walikuwa hawakujuishwa miongoni mwa wasimuliaji wa hadith, mafaqih, au mujtahidi, bali walikuwa ni watu waliotegemea juu ya rai zao wenyewe.

Hii peke yake ni ushahidi wa kukosa kwao kuwa na elimu. Kwa upande mwingine, Maimam wa Shi’a ni waongozaji walioteuliwa ki-mbinguni, warithi walioagizwa, wa Mtukufu Mtume.

Kwa kweli katika kila zama wanakuwepo baadhi ya mafaqihi wenye elimu ya hali ya juu na wanachuoni miongoni mwa Mashi’a ambao wanazitafsiri amri za Allah, wakizingatia Qur’ani tukufu, hadith na makubaliano ya maoni.

Tunafuata fat’wa za ulamaa kama hao. Ingawa mafaqihi wenu walikuwa wanafun- zi wa, na walipata nyingi ya elimu yao, kutoka kwa Maimam wa Shi’a, ninyi mnawafuata wahenga wenu ki-kichwakicha tu, wale kati ya wanafunzi wao, ambao walikengeuka kut ka kwenye misingi ya elimu na wakategemea kukisia kwao. Sayyed: Unawezaji kudai kwamba Maimam wetu walipata manufaa ya elimu yao kutoka kwa Maimam wenu?

Muombezi: Ni ukweli wa kihistoria kwamba Imam Ja’far as-Sadiq aliwazidi wengine wote katika elimu. Yule Aalim mashuhuri, Nuru’d-Din bin Sabbagh Maliki anakiri ndani ya kitabu chake, Fusulul-Muhimma kwamba Mtukufu Imam alikuwa akijulikana na kuonekana wazi kwa elimu yake. Yeye anaandika: “Watu walipata elimu ya nyanja mbali mbali kutoka kwake. Watu walikuja kutoka nchi za mbali kupata maelekezo. Akajulikana sana katika nchi zote na ulamaa walisimulia hadith nyingi kutoka kwake kuliko kwa mtu mwingine wa Ahlul-Bayt .....”

Kundi kubwa la watu mashuhuri wa umma, kama Yahya bin Sa’id ibn Jarih, Malik bin Anas, Sufyan Thawri, Abu Ainiyya, Abu Ayyub Sijistani, Abu Hanifa, na Saba - wote wamesimulia hadith zake.

Kamalu’d-Din Abi Talha pia anaandika katika Manaqib yake kwamba maulamaa maarufu na viongozi wa kidini wamenukuu hadith kutoka kwa mtukufu Imam na wamepata elimu kutoka kwake. Miongoni mwao anataja majina ya wale waliotajwa kwenye Fusulul-Muhimma. Hata maadui walikiri fadhaili za mtukufu Imam. Kwa mfano, Maliki katika Fusulul-Muhimma na hususan Sheikh Abu Abdu’r-Rahman Salmi katika Tabaqatul- Masha’ikh yake anaandika:

“Hakika, Imam Ja’far as-Sadiq aliwapita wenzie wote wa wakati wake. Alikuwa na elimu ya kisilika na ujuzi katika dini, uchamungu kamilifu katika ulimwengu, kujizuia kutokana na matamanio yote ya kidunia, na hekima ya kina kikubwa.”

Na Muhammad bin Talha Shafi’i ameziandika sifa hizi zote za mtukufu Imam katika Matalibus-Su’ul yake, Sura ya 6, uk. 81: “Mtu huyu mwenye elimu kubwa alitokana na viongozi mashuhuri wa Ahlul- Bayt. Alijaaliwa na elimu nzito na alikuwa wakati wote katika hali ya kumkumbuka Allah. Alisoma Qur’ani tukufu mara kwa mara na alitoa tafsiri yake.

Wafuasi wake walijikusanyia lulu kutoka kwenye bahari ya elimu yake. Aligawanya muda wake wakati wa mchana na usiku katika miundo mbalimbali ya ibada. Kumtembelea yeye kulikuwa kama ukumbusho wa akhera.

Kuisikiliza hotuba yake kulimuongoza mtu kupata uchamungu, na kufuata maelekezo kulimuongozea mtu kwenye kupata pepo. Uso wake mng’aavu ulijulisha kwamba alitokana na familia ya Mtukufu Mtume. Usafi wa vitendo vyake pia ulionyesha kwamba anatokana na Ahlul-Bayt wa Mtume.

Wengi wa ula- maa wamepokea hadith na kupata elimu kutoka kwake. Miongoni mwao walikuwa ni Yahya bin Sa’id Ansari, ibn Jarih, Malik bin Anas, Sufyan Thawri, Ibn Ainiyya, Sha’ba na Ayyub Sijistani. Wote walishukuru kwa bahati njema na fursa ya kusoma kutoka kwake.”

Kuhusishwa Kwa Ushi’a Na Imam Ja’far As-Sadiq

Nawab: Mashi’a wanaamini katika Maimamu kumi na mbili. Kwa nini Ushi’a unahusish- wa na jina la Imam Ja’far Sadiq na kuitwa madhehebu ya Ja’far?

Muombezi: Kila Mtume, kwa mujibu wa amri ya Mungu, huteua mrithi wake. Muhammad alimtangaza Ali kuwa mrithi wake na akaamuru umma kumtii yeye. Lakini baada ya kifo cha Mtume, Ukhalifa ulichukuliwa na Abu Bakr, Umar na Uthman.

Wakati wa ukhalifa wao, isipokuwa wakati wa siku za mwanzo, Abu Bakr na Umar walimtaka ushauri Ali juu ya masuala yote mazito na kutenda kwa kufuata ushauri wake.

Aidha, maulamaa wakubwa na wanachuoni maarufu wa dini nyingine ambao walikuja Madina kwa ajili ya kutafuta elimu ya dini walikinaishwa kabisa na majadiliano yao na Ali. Katika maisha yake yote, Ali aliendelea kuuhudumia Uislamu katika njia nyingi. Baada ya kuuliwa kwake shahidi, wakati Bani Umayya walipokuwa watawala, uimamu kwa ukatili mkubwa ukakandamizwa. Imam Hasan Mujtaba, Imam Husein, Imam Zainu’l-Abidin, na Imam Muhammad Baqir walikuwa waathirika wa ukatili mkubwa wa Bani Umayya. Njia zote za kuwafikia wao zilifungwa isipokuwa kwa wafuasi wao wachache, wengine hawakuweza kunufaika kutokana na elimu yao. Kila mmoja wao aliuawa.

Hata hivyo, wakati wa mwanzo wa karne ya pili baada ya Hijra, chini ya shinikizo kubwa la ukatili wa Bani Umayya, watu waliasi dhidi ya yao. Mapigano makali ya umwagaji damu yalifuatilia kati ya Bani Abbas na Bani Ummaya. Wakati ambapo Bani Umayya walikuwa wamejishughulisha katika kuulinda utawala wao, hawakuweza kuendeleza unovu wao kwa Ahlul’l-Bayt. Kwa hiyo, Imam Ja’far akajitokeza kutoka kwenye kule kutengwa alikokuwa amefanyiwa na Bani Umayya. Aliwaelekeza watu kuhusiana na sheria za dini.

Wapenda elimu 4000 walijikusanya kuizunguka mimbar yake na kuzima kiu yao kutoka kwenye bahari ya elimu isiyo na kikomo ya mtukufu Imam. Baadhi ya masahaba zake wameandika kanuni mia nne ambazo zinajulikana kama ‘Usul-e-Arba Mia – yaani hukumu mia nne. Yafi’iy Yamani anaandika kwamba Imam Ja’far aliwapita wote katika elimu yake. Jabir Ibn Hayyan Sufi, aliandika mkusanyo wa kurasa elfu moja, akiorodhesha takriban vijitabu 500 juu ya mafundisho ya Imamu Ja’far.

Baadhi ya mafaqihi wakubwa wa ki-Sunni vile vile walikuwa ni wanafunzi wake. Abu Hanifa, Malik Bin Anas, Yahya Bin Sa’id Ansari, Ibn Jarih, Muhammad Bin Ishaq, Yahya Bin Satid Qattan, Sufyan Bin Uyayna, Sufyan Thawri – wote hawa walinufaika kutoka kwenye elimu yake kubwa mno. Ukubwa huu wa uchanuaji wa elimu ulitokea wakati huu kwa sababu Bani Umayya walizuiya mwenendo wa wazazi wake, na kwa bahati mbaya Bani Abbas wangeliwazuiya kizazi chake kuzungumza kwa uhuru.

Ukweli wa wa Ushi’a uliwekwa wazi na sifa za Ahlul’l-Bayt wa Muhammad zilitangazwa na Imamu Ja’far Sadiq. Kwa hiyo, madhehebu hii ikaja kujulikana kama “Ja’faria,” lakini hakuna tofauti kati ya Imamu Ja’far na yeyote katika Maimamu wanne miongoni mwa wahenga zake waliomtangulia au Maimamu sita waliokuja baada yake. Wote walikuwa viongozi wa kiro- ho waliowekwa na Mungu.

Ingawa marafiki na maadui wote kwa pamoja walitambua ubora wake katika elimu na ukamilifu wake katika sifa zote, viongozi wenu waliopita walikataa kumfanya kama mwanachuoni mkubwa wa dini na mtu mkamilifu wa zama zake.

Walikataa kutambua madhehebu yake sambamba na madhehebu nyingine nne ingawa yeye alishikilia daraja la juu zaidi katika elimu uchaji kama ilivyokubaliwa na maulamaa wenu wenyewe. Kwa vile alitokana na Ahlul’l-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alikuwa na haki ya kupata kipaumbele juu ya wengine.

Pamoja na mambo yote haya, maulamaa wenu washupavu wameonesha dharau sugu kama hii kwa kizazi cha Mtume wao kiasi kwamba wanachuoni wenu wa daraja za juu kama Bukhari na Muslim, hawakuweza kuandika hata hadithi moja kutoka kwa faqih huyu au Ahlul-Bayt. Aidha, hawakunukuu hadithi yoyote kutoka kwa Imam yoyote au Sa’dat (mabibi) wa kizazi kitukufu: Alawi, Husaini, Abidi, Musawi, Ridhawi, au kutoka kwa maulamaa kama hawa na mafuqahaa kama, Zaid Bin Ali Bin Husein, yule Shahid, Yahaya Bin Zaid, Muhammad Bin Abdullah, Husein Bin Ali, Yahya Bin Abdullah bin Hasan na kaka yake Idris, Muhammad Bin Ja’far Sadiq, Muhmmad Bin Ibrahim, Muhammad Bin Zaid, Abdullah Bin Hasan, Ali Bin Ja’far (Arizi) na wengine, wote hao ambao walikuwa maula- maa na mafaqih wakubwa na ambao walitokana na familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Kwa upande mwingine, wamenukuu hadithi kutoka kwa watu kama Abu Huraira, ambaye tabia yake mnaijua ninyi wote, na kutoka kwa yule mwongo mkubwa na mzushi, Akrama, yule Khawariji. Maulamaa wenu wenyewe wamethibitisha kwamba watu hawa walikuwa waongo na bado wanakubali hadithi zao kwa mioyo yao yote. Ibn Bayyit anaandika kwamba Bukhari amenukuu hadithi nyingi kufikia kiasi cha hadithi 12,000 kutoka kwa Khawariji na Nasibiyya, kama Imamu bin Hattan, mwenye kuvutiwa na Ibn Muljim, muuwaji wa Amir wa Waumini.

Wafuasi wa Imam-e-Adhma (Abu Hanifa), Imamu Malik, Imamu Shafi’i na Imamu Hanbal huwaona hawa kama Waislamu safi ingawa hakuna hata mmoja aliyetokana na Ahlul-Bayt wa Mtume, na kila mmoja wa madhehebu zile iko huru kuchukuwa njia zake mwenyewe ingawa kuna tofauti kubwa katika misingi na halikadhalika katika matendo ya ibada miongoni mwao.

Ni masikitiko makubwa kiasi gani kwamba wanawaita wafuasi wa Ja’far Bin Muhammad As-Sadiq makafiri! Na katika sehemum zote zinazotawaliwa na Masunni, ikiwemo Makka, ambayo kwa kuihusu Allah anasema: “Yeyote anaingia humo yuko huru,” hawako huru kuelezea imani yao au kutekeleza Sala zao.

Hivyo ninyi watu wema mnapaswa muelewe kwamba sisi Shi’a sio chanzo cha hitilafu zilizoko katika Uislamu; hatukuleta mtengano miongoni mwa Waislamu. Kusema kweli, migogano mingi hutokea upande wenu. Ni niyni mnaowaita Waislamu milioni 100 makafiri, ingawa ni waumini waaminifu sambamba na ninyi.

Hafidh: Ni kweli, kama ulivyosema, kwamba mimi sio mtu dhalimu. Nakubali kwamba kumekuwepo na vitendo viovu kwa sababu ya ushupavu. Ningependa kusema bila kujidai au kumpendeza yeyote kwamba nimenufaika sana kutokana na mazungumzo yako na nimejifundisha vya kutosha.

Lakini kwa idhini yako, niruhusu niseme kitu kimoja, ambacho ni malalamiko, na halikadhalika ni utetezi wa madhehebu stahiki ya Sunni. Unaweza kuniambia ni kwa nini wahubiri na maulamaa wa ki-Shi’a kama wewe hamchungi watu wenu wa kawaida kutokana na kutoa maneno ambayo hupelekea kwenye ukafiri? Matokeo yake ni kwamba wengine hupata nafasi ya kutumia neno kafiri dhidi yao.

Mtu anaweza kuwa shabaha ya mashambulizi kwa sababu ametoa maelezo yasiyo sahihi. Hivyo ninyi watu vile vile msiwafanye Masunni kuwa shabaha ya mashambulizi yenu. Mashi’a husema mambo ambayo huathiri nyoyo za Masunni, ambao kwa kulipiza huhusisha ukafiri kwa Mashi’a. Muombezi: Naomba unieleze ni maelezo gani au vitendo gani hupelekea kwenye ukafiri vinavyofanywa na Mashi’a?

Hafidh: Mashi’a kuwakosoa Masahaba wakubwa na baadhi ya wake safi wa Mtume, ni dhahiri hicho ni kitendo cha ukafiri. Kwa vile Masahaba wamepigana kwa miaka mingi pamoja na Mtume dhidi ya makafiri, ni wazi kwamba huduma yao ilikuwa safi kabisa kutokana na maadili yasiyokamilika. Kwa hakika wanastahiki Pepo, hususan wale ambao walipata baraka za Mungu. Kwa muijibu wa Qur’ani Tukufu : “Hakika Allah aliridhishwa sana na waumini wakati walipokula kiapo cha utii kwako chini ya mti” (Qur’ani 48;18) Hakuna shaka kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaheshimu. Mtu ambaye anakataa ubora wao hakika amepotea. Qur’ani inasema: “Wala hazungumzi kwa mata- manio yake. Hayakuwa haya ila ni ufunuo uliofunuliwa.” (Qur’ani; 53:3-4) Mtu kama huyo anamkataa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Qur’ani Tukufu, na mtu ambaye anamkataa Mtume na Qur’ani Tukufu hapana shaka yoyote ni kafiri.

Muombezi: Nilitegemea kwamba nukta kama hizo zisingeletwa katika mkutano huu wa hadhara. Majibu yangu yanaweza kuwafikia watu wasio na elimu na wanaweza wakaeneza propaganda potovu. Ingekuwa vizuri kama tungejadili masuala haya kwa faragha. Nitakuja kwako siku moja na tutalitatua tatizo hili kwa faragha.

Hafidh: Nasikitika, lakini watu wetu wengi katika mikesha kadhaa iliyopita wamesisitiza kwamba nukta hii ijadiliwe. Majadiliano yako siku zote ni yenye busara. Kama utatoa majibu mazuri yenye mvuto, hakutakuwa na matokeo mabaya. Vinginevyo ukubali kushindwa na hoja yetu.

Nawab: Ni sawa sawa. Wote tunataka suala hili litatuliwe hapa hapa na sasa hivi.

Muombezi: Nakubaliana tu matakwa yenu. Si kutarajia mtu mwenye uwezo kama wewe, baada ya maelezo kamili ambayo nimeyatoa katika usiku wa masiku yaliyopita juu ya suala la ukafiri ungeihusisha madhehebu ya Shi’a na ukafiri. Tayari nimewasilisha kwa ukamilifu uthibitisho kwamba Shi’a Ithna Ashari ni wafuasi wa Muhammad na kizazi chake kitukufu. Umeleta masuala mbalimbali. Nitajibu kila moja ya hayo kwa kuyatenganisha.

Kuwalaumu Masahaba Haina Maana Ya Ukafiri

Kwanza umesema kwamba ukosoaji wa Mashi’a juu ya Masahaba na baadhi ya wake wa Mtume hupelekea kwenye ukafiri. Sielewi msingi wa maelezo haya. Kama ukosoaji unaungwa mkono na ushahidi, unaweza kukubaliwa. Na hata kama mtu akitoa madai ya uwongo, hii haimfanyi kuwa kafiri. Ataitwa mwenye dhambi, kama mtu anayekunywa pombe au anayefanya zinaa. Na hakika kila kosa dhidi ya sheria ya Mungu linasameheka. Ibn Hazm Zahiri Andalusi (amezaliwa 456 A.H.) anasema katika kitabu chake Al-Fasl fi’l- milal wa’n- Nihal sehemu ya 3, uk. 227: “Kama mtu anamtukana Sahaba wa Mtume kwa ujinga, si wa kulaumiwa. Kama akifanya hivyo hali ya kuwa ana elimu juu ya hilo, ni mwenye dhambi kama wenye dhambi wengine ambao hufanya zinaa, wizi, nk.

Naam kama akiwalaani kwa makusudi, kwa vile walikuwa Masahaba wa Mtume, atakuwa kafiri kwa sababu tabia kama hiyo ni sawa na uadui dhidi ya Allah na Mtume Wake. Vinginevyo, kuwatukana tu Masahaba hakuwezi kuwa sawa na ukafiri.”

Kwa hiyo, Khalifa Umar alimuomba Mtume amruhusu kumkata kichwa Hatib, aliyekuwa mnafiki, ingawa alikuwa ni mmoja wa Masahaba wakubwa, muhajir, na mbaye alishiriki katika vita ya Badir. Kwa kule kumtukana na kumhusisha na unafiki, Umar hakuitwa kafiri.

Basi vipi inawezekana kwamba Mashi’a waitwe makafiri kwa kuwatukana baadhi ya Masahaba, tukichukulia kwa muda huu kwamba unayosema ni sahihi. Aidha, maulamaa wakubwa wa madhehebu yenu wameikataa nukta yenu hii.

Miongoni mwao ni Kadhi Abdu’r-Rahman Shafi’i, ambaye katika kitabu chake Muwafiq amekataa hoja ya maulamaa wenu washupavu kuhusu ukafiri wa Mashi’a. na Muhammad Ghazali anaandika kwamba kwalaani na kuwatukana Masahaba kamwe sio ukafiri; hata kuwalaani Masheikh wawili (Bukhari na Muslim) hakuwezi kuwa sawa na ukafiri.

Mulla Sa’d Taftazani anaandika katika Sharhe Aqa’id-e-Nas’i kwamba, “ baadhi ya watu wasio na uvumilivu wanasema kwamba wale ambao wanawatukana Masahaba ni makafiri. Ni vigumu kukubali mtazamo huo. Ukafiri wao hauthibitishwi kwa sababu baadhi ya maulamaa wamewapendelea, wakapuuza matendo yao maovu, na kutoa utetezi wa kipumbavu katika kuwaunga mkono.

Wamesema kwamba Masahaba wa Mtume walikuwa hawana dhambi yoyote, ingawa maelezo haya yalikuwa kinyume na ukweli wa mambo. Wakati mwingine walipigana wenyewe kwa wenyewe. Husda na kupenda madaraka mara kwa mara kuliwasababishia kufanya matendo maovu.

Hata baadhi ya Masahaba wakubwa hawakuwa huru kutokana na vitedno viovu. Hivyo, kama kwa msingi wa ushahidi fulani mtu akawakosoa, hapaswi kulaumiwa kwa hilo. Baadhi ya watu, kwa sababu waliwapendelea Masahaba walificha maovu yao, lakini baadhi wameandika matendo yao maovu na kuwalaumu.”

Mbali na hili, Ibn Athir Jazari, mwandishi wa Jam’ul-Usul, amewajumuisha Mashi’a kati- ka madhehebu ya ki-Islamu, basi mnawezaje kuwaita makafiri? Wakati wa kipindi cha Makhalifa wa kwanza, baadhi ya watu waliwalaani Masahaba kwa ajili ya matendo yao maovu. Hata hivyo, Makhalifa hawakuamuru wauawe kwa ukafiri wao.

Kwa hiyo, Hakim Nishapuri katika kitabu chake “Mustadrak”, sehemu ya 4, uk. 335, 354, Imamu Ahmad Hanbal katika “Musnad”, sehemu ya 1, uk. 9, Dhahabi katika “Talkhise Mustadrak”, Kadhi Ayaz katika “Kitab-e-Shifa”, sehemu ya 4, sura ya 1, na Imamu Ghazali katika “Ihya’u’l- Ulum”, Jz. 2, anataarifu kwamba wakati wa Ukhalifa wa Abu Bakr, mtu mmoja alikuja kwake na akatoa lugha chafu na laana dhidi yake kiasi kwamba wale waliokuwepo pale walishikwa na hasira. Abu Barza Salmi alimuomba Khalifa kama angemruhusu ili amuuwe yule mtu kwa sababu amekuwa kafiri. Abu Bakr alisema kwamba haiwezekani kufanya hivyo kwa vile hakuna mtu yeyote isipokuwa Mtume anayeweza kupitisha hukumu kama hiyo.

Makhalifa Wenyewe Hawakuchukulia Kulaniwa Wao Kuwa Ni Ukafiri

Kwa kweli, mabwana wakubwa wa ki-Sunni huwakiuka hata wale ambao wanawaunga mkono. Makhalifa wenyewe walisikia matusi lakini hawakuwalaumu watu kwa ukafiri au kuamuru wauawe. Aidha, kama kumlaani Sahaba ni sababu ya ukafiri, kwa nini msimuite Mu’awiya na wafuasi wake makafiri? Walimlaani na kumtukana mkamilifu zaidi wa Masahaba, Ali Bin Abu Talib. Kuwa na uchaguzi wa upendeleo katika suala hili huonesha tu kwamba lengo lako ni kitu kingine. Unataka kupigana dhidi ya Ahlul-Bayt na wafuasi wao! Kama kuwalaani Masahaba ni ukafiri, kwa nini msimlaumu Ummu’l- Mu’minin Aisha kwa ukafiri? Wanahistoria wenu wote wamesema kwamba alikuwa mara kwa mara akimtukana Khalifa Uthman na kwa uwazi akatangaza: “Muuwenu mzee huyu mpumbavu, kwani hakika amekuwa kafiri.” Hata hivyo, kama Shi’a atasema kwamba ilikuwa vema kwamba Uthman aliuawa kwa sababu alikuwa kafiri, mara moja mtasimama dhidi yake.

Lakini wakati Aisha alipomuambia Uthman mbele yake kwamba yeye ni Na’thal na kafiri, Khalifa hakumkataza kufanya hivyo wala Masahaba hawakumkemea. Wala ninyi hamuoni kwamba alifanya kosa.

Nawab: Mheshimiwa, unamaanisha nini kwa neno Na’thal?

Muombezi: Firuzabadi, ambaye ni mmoja wa maulamaa wenu mwenye daraja ya juu, anatoa maana yake katika Qamusu’l-Lughat kama ‘mzee mjinga’. Vile vile kulikuwa Myahudi aliyekuwa na ndevu ndefu mjini Madina aliyekuwa akiitwa kwa jina hilo, ambaye alifananishwa na Uthman. Mfafanuzi juu ya Qamus, Allama Qazwini, vile vile anatoa maana hiyo hiyo, anasema kwamba Ibn Hajar katika kitabu chake Tabsiratu’l-Muntaha, anaandika, “Nathal Myahudi mwenye ndevu ndefu aliyeishi Madina; alifanana sana na Uthman.”

Khalifa Abu Bakr Alimtukana Ali

Mwisho, kama mtu anayemtukana Sahaba ni kafiri, kwa nini Khalifa Abu Bakr, mbele ya Masahaba na mkusanyiko wa Waislamu, alimtukana Sahaba bora zaidi, Ali Bin Abi Talib? Mnatukuza sifa za Abu Bakr ingawa mlipaswa kumlaumu.

Hafidh: Kwa nini unamsingizia lawama hii ya uwongo? Ni lini Khalifa Abu Bakr alimtukana Khalifa Ali? Muombezi: Samahani! Sisi hatusemi kitu chochote mpaka tuwe tumefanya utafiti wa kutosha. Pengine ungetazama Sharhe Nahjul-Balagha, Jz. 4, uk. 80, ambapo imeandikwa kwamba Abu Bakr, akimdhihaki Ali kutoka kwenye mimbari ya Msikiti, alisema: “Yeye (Ali) ni mbwa mwitu, ushahidi wake ambao ni mkia wake.

Anasababisha matatizo, anapu- uza umuhimu wa matatizo makubwa, na kuchochea watu kufanya vurugu. Anaomba msaada kutoka kwa wanyonge na kukubali usaidizi kutoka kwa wanawake. Yeye ni kama Ummi’t-Tahal (kahaba mmoja wa siku za ujahilia, kama alivyoelezwa na Ibn Abil-Hadid) ambaye kwamba wanaume wa familia yake walikuwa wanapenda kufanya naye zinaa.”

Sasa mnaweza kulinganisha matusi ya Abu Bakr kwa Ali na ukosoaji unaofanywa na Mashi’a dhidi ya Masahaba. Kama kumtukana Sahaba yeyote ni sawa na ukafiri, basi Abu Bakr, binti yake Aisha, Mu’awiya na wafuasi wake wanapaswa kuitwa makafiri. Kama hakumfanyi mtu kuwa kafiri, basi huwezi kuwaita Mashi’a makafiri kwa jambo hilo.

Khalifa Umar Alishikilia Kwamba Kumlaani Mwislamu Sio Ukafiri

Aidha, kwa mujibu wa hukumu za wanachuoni wenu wakubwa na Makhalifa, wale ambao wanawatukana Makhalifa sio makafiri. Imam Ahmad Hanbal katika Musnad yake, Jz. 3, Ibn Sa’d Katib katika Kitab-e-Tabaqat, Kadhi Ayaz katika kitabu chake Shifa, sehemu ya 4 ya sura ya 1, wanasimulia kwamba, gavana wa Khalifa Umar, Ibn Abdul-Aziz, aliandika kutoka Kufa kwamba mtu mmoja amemtweza na kumtukana Umar Ibn Khattab, Khalifa wa pili.

Gavana huyo alitaka ruhusa ya kumuuwa huyo mtu. Umar Ibn Khattab akajibu kwamba hairuhusiwi kumuua Mwislamu kwa kutukana au kumlaani Mwislamu yeyote isipokuwa mtu ambaye anamtukana Mtume.

Kwa Mujibu Wa Abul-Hasan Ash’ari Hata Kumuita Allah Au Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Kwa Majina Mabaya Sio Ukafiri

Baadhi ya maulamaa wenu wakubwa, kama, Abu’l-Hasan Ash’ari na wafuasi wake, wanaamini kwamba kama mtu ana imani katika moyo wake na bado akaonyesha ukafiri (km. Kwa kuabudu kiyahudi au kikristo, kwa mfano) au akasimama na kupigana dhidi ya Mtume, au akamuita Allah au Mtume kwa majina mabaya, hata hivyo sio kafiri. Imani maana yake kuamini ndani ya moyo na kwa vile hakuna mtu anayeweza kuujua moyo wa mtu mwingine, haiwezi kusemwa iwapo ule ukafiri wa dhahiri unatoka moyoni au la. Maulamaa wa ki-Ash’ari vile vile wamejadili masuala haya katika vitabu vyao. Ibn Hazm Andalusi ameandika kwa urefu kuhusu nukta hizi katika kitabu chake Kitabu’l-Fazl (sehemu ya 4, uk. 204, 206). Kwa kuzingatia ukweli huu, ninyi mna haki gani ya kuwashutumu Mashi’a kwa ukafiri? Masahaba Wengi Walitukanana Wenyewe Kwa Wenyewe Lakini Hawakuchukuliwa Kama Makafiri

Katika vitabu vyenu sahihi, kama Musnad cha Imamu Ahmad Bin Hanbal, Jz. 2, uk. 236; Siratul- Halabiyya, Jz. 2, uk. 107, Sahih Bukhari, Jz. 2, uk. 74, Sahih Muslim, Kitab-e-Jihad wa Asbabu’n-Nuzul Wahid, uk. 118, kuna hadithi nyingi zinzoonesha kwamba Masahaba wengi walitukanana wenyewe kwa wenyewe mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Lakini Mtume hakuwaita watu hawa makafiri. Aliwaonya. (hadithi za kuhusu mizozo hii na uadui wa wao kwa wao zimeandikwa katika vitabu vya Sunni tu, sio katika vitabu vya Shi’a).Kwa mtazamo wa maneno haya, natumaini kwamba mmetosheka kwamba kulaani au kumtukana Sahaba yeyote hakumfanyi mtu kuwa kafiri. Kama tunamlaani mtu fulani bila sababu, tutakuwa ni watenda dhambi, sio makafiri. Na kila dhambi inaweza kusamehewa.

Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Aliyajua Matendo Yote Mabaya Na Mazuri Ya Masahaba

Pili, umesema kwamba Mtume aliwaheshimu na kuwastahi Masahaba wake. Hii ni sahihi. Kwa nyongeza, Waislamu wote na wasomi wanakubali kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alijua matendo mema na mabaya ya watu. Aliyaridhia matendo yao mema. Kwa hiyo, aliheshimu uadilifu wa Nushirwan na ukarimu wa Hatim Ta’i. Kama alimheshemu mtu fulani, ilikuwa ni kwa sababu ya matendo yake mazuri.

Lakini kule kuridhiwa anakooneshwa mtu kwa kufanya tendo jema, hakuthibitishi kwamba mwisho wake utakuwa wa mafanikio.

Pengine atafanya matendo mabaya siku za baadae. Kama akifanya, kumkemea kabla ya kufanya, sio uadilifu, hata kama ingejulikana kwamba atafanya uovu katika siku zijazo.

Ali alijua uovu na mwisho wa ushenzi wa mlaaniwa Abdu’r-Rahman Ibn Muljim Muradi na kwa kurudia rudia alimuambia kwamba yeye ndiye muuaji wake. Wakati mmoja kwa uwazi alisema: “Napenda aishi, lakini amedhamiria kuniua mimi, na rafiki huyu muovu anatokana na ukoo wa Murad.”

Maelezo haya yameandikwa na Ibn Hajar Makki kuelekea mwisho wa sehemu ya 1 ya Saw’iq, uk. 72. Bado Ali hakukusudia kumuadhibu. Hivyo, hadithi ambayo inaonesha kwamba stahili ya kitendo makhususi au maelezo sio lazima iwe yenye athari wakati wote unaokuja.

Sifa Ya Kuwa Mmojawapo Kwenye Bai’at-E-Ridhwan

Tatu, umesema kwamba kwa vile Masahaba walikuwa katika Bai’at-e-Ridhwan na wakachukua kiapo chao cha utii kwa Mtume, hawakustahili lawama, bali walistahiki kusifiwa kwa sababu wao ndio wanaorejewa kwenye aya tukufu uliyoisoma (48:18).

Wanachuoni watafiti na maulamaa wametoa maoni kwa mapana sana juu ya suala hili, wakisema kwamba ridhaa ya Mungu ya aya hii inahusika tu kwenye kitendo kile makhususi, Bai’at (kiapo cha utii), na kwamba haiendelei bila kikomo.

Ninyi wenyewe mnaelewa kwamba wakati wa tukio la Bai’at kule Hudabiyya, walikuwepo watu 1500, ambao kati yao baadae idadi ya watu walijumuishwa katika ‘aya za unafiki.’

Allah aliwaahidi moto wa milele. Je, inawezekana kwambwa Allah na Mtume wameweza kuridhia baadhi ya watu na kwamba baadhi yao (ya watu hao hao) waje wabakia motoni milele? Kwa hiyo ina maana kwamba ile ridhaa ya Mungu hakuwa kwa ajili ya Bai’at-e-Shajara (kiapo cha utii chini ya mti) peke yake, bali ilitegemea juu ya imani nyofu na matendo mema.

Wale ambao wameamini katika upweke wa Mungu (Tawhid) na Utumme (Nubwat) na wakala kiapo cha utii walistahiki radhi za Mungu. Walitangazwa kuwa watu wa Peponi. Lakini wale waliokula kiapo cha utii bila imani, au ambao hawakula kiapo, wanastahili ghadhabu Yake. Hakika, Masahaba walifanya matendo mazuri, na kwa ajili ya matendo yao mazuri (kama kula kiapo chini ya mti) lazima wasifiwe. Na hata kama muumini, awe yeye ni Sahaba au la, akifanya kosa, anaweza kukosolewa.

Mashi’a Wanakubali Ubora Wa Masahaba

Madhehebu ya Shi’a siku zote imeelezea matendo mema ya Masahaba. Aidha, hukubali matendo mema hata ya wale ambao wamekuwa ni shabaha ya ukosoaji mkali. Kwa mfano, inatambua kile kiapo chao cha utii cha chini ya mti, kuhama kwao pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kushiriki kwao katika vita, lakini vile vile hulaumu na kushutumu matendo yao mabaya.

Hafidh: Ninashangazwa kukusikia wewe ukisema kwamba, Masahaba wa Mtume walifanya matendo maovu. Mtume alitangaza kila mmoja wao ni mlezi na kiongozi wa jumuiya. Alisema katika hadithi mashuhuri kwamba: “Hakika masahaba wangu ni kama nyota; kama mnafuta yeyote kati yao, mtakuwa mmeongoka.” Imani yenu kwa dhahri sio ya kawaida, na hatukubali imani isiyo ya kawaida.

Hadithi Ya “Kuwafuata Masahaba” Yachunguzwa

Muombezi: Ninalazimika kujadili baadhi ya vipengele vya hadithi hii kabla sijaendelea kujibu. Kwa kweli, hakika hatuwezi kuzungumza kuhusu chanzo, usahihi, au udhaifu wa hadthi kwa njia ya kukosoa, kwani tutatoka kwenye mada kuu. Majadiliano yetu yataan- galia kwenye maana yake. Wale amabao wamebarikiwa heshima ya kumuona Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), au ambao wamesimulia hadithi kutoka kwake, wanaitwa Sahaba, iwe walikuwa ni wahamiaji (Muhajir) kutoka Makka au wale waliowasaidia (Ansar) kule Madina au wengine. Kutokuelewana kukubwa mwiongoni mwenu ni kwamba, kwa sababu ya nia zenu nzuri juu ya

Masahaba, mnawachukuliya wote kuwa wameepukana na makosa yote ingawa ukweli ni kinyume chake. Miongoni mwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), walikuwepo wema na wabaya, ambao Allah na Mtume Wake walikuwa wanawafahamu vizuri sana. Hili linaweza kuthibitishwa vizuri na ile Sura ya Munafiqun (wanafiki) na aya za sura nyingine, kama Tawba ambayo vile vile inajulikana kama Al- Bara’a (Kinga) na Ahzab (koo), ambazo ziliteremshwa kwa ajili ya kuwalaumu Masahaba ambao walikuwa wanafiki na waovu.

Maulamaa wenu mashuhuri wenyewe wameandika katika baadhi ya makosa na matendo mabaya ya Masahaba katika vitabu vyao sahihi. Hisham Bin Muhammad Sa’yib Kalbi, mmoja wa ulamaa mashuhuri wa madhehebu yenu ameandika kitabu juu ya makosa na kasoro za Masahaba. Wanafiki ambao wamelaumiwa na Allah (swt) na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa ndumila kuwili, ambao walikuwa Waislamu kwa nje tu.

Nyoyo zao zilikuwa imechafuliwa na dhulma na upotofu; na wote hao walijumuishwa katikakundi la Masahaba. Hivyo tutawezaje kuwa na nia njema kwa Masahaba wote? Na vipi tutakuwa na hakika kwamba kumfuata yeyote kati yao kutahakikisha uwongofu? Je, sio ukweli kwamba katika suala la Aqaba kulikuwa na Masahaba ambao walionekana kuwa waaminifu lakini walikusudia kumuua Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Suala La Aqaba Na Mpango Wa Kumuua Mtukufu Mtume (S.A.W.W.)

Hafidh: Baadhi ya maulamaa wanalichukilia suala la Aqaba kuwa ni ubunifu wa Mashi’a.

Muombezi: Ni vibaya sana kwako wewe kutegemea juu ya imani za baadhi ya watu ambao wana mawazo ya ki-Khawariji na Manasibi. Suala hili kwa uwazi kabisa linaju- likana kwa wote kiasi kwamba maulamaa wenu wenyewe wamelikubali. Tafadhali hebu rejea kwenye Dala’ilu’n-Nubuwat kilichoandikwa na Hafidh Abu Bakr Ahmad Bin Husain Baihaqi Shafi’i, ambaye ni mmoja wa wanachuoni na mafaqihi wenu maarufu.

Ameandika kisa cha Batn-e-Aqaba kwa nyororo (sanad) sahihi ya wasimuliaji; na vile vile Imamu Ahmad Bin Hanbal, kuelekea mwisho wa Jz. 5 ya Musnad yake, anataarifu kutoka kwa Abu Tufail, na Ibn Abi’l-Hadid anaandika katika Sharhe yake ya Nahju’l-Balagha, na ina- julikana kwa maulama wote kwamba, Mtukufu katika usiku huo alilaani kikundi cha Masahaba.

Nawab: Lilikuwa ni jambo gani, na ni nani hao ambao walitaka kumuua Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Muombezi: Maulamaa wakubwa wa madhehebu zote wameandika kwamba njiani wakati Muhammad anarudi kutoka vita ya Tabuk, wanafiki kumi na wanne walikula njama ya kumuua. Mpango ulikuwa ni kumsukuma kutoka kwenye ngamia wake angukie kwenye mporomoko wakati akipita Aqaba wakati wa usiku, uchochoro mwembamba ambao mtu mmoja tu anaweza kupita. Wakati walipojaribu kutekeleza mpango wao Malaika Jibril alimjulisha Mtume juu ya mpango huo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamtuma Hudhaifa Nakha’I kujificha nyuma ya mlima.

Wakati wale wahaini walipowasili na kuzungumza wenyewe pamoja, aliwatambua wote. Saba miongoni mwao wanatokana na Bani Umayya. Hudhaifa alirudi kwa Mtume na kuwataja wote.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuamuru kuiweka siri njama hiyo, na akasema Allah ndiye mlizi wao. Katika sehemu ya kwanza ya usiku Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alianza safari, akifuatiwa na jeshi lake.

Ammar-e-Yasr alimwongoza ngamia kwa mbele na Hudhaifa alikuwa akimswaga kwa nyuma. Wakati walipofikia kile kichochoro chembamba, wale wanafiki walimtupia ngamia mifuko yao ya ngozi iliyojaa mchanga (au makopo ya mafuta), ikatoa sauti kubwa, wakidhania kwamba mnyama yule aliyetishika atamtupa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) chini ya ule mporomoko mkali.

Lakini Allah (swt) alimkinga na wahaini wakakimbia na kutokomea katika kundi. Je, watu hawa hawakuwemo mwiongoni mwa Masahaba? Je, ni kweli kwamba kuwafuata wao maana yake ni njia ya wokovu? Wakati tunapozungumza kuhusu Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah kwa nini tufumbie macho makosa yao?

Mtume Kamwe Hakutuamrisha Tuwafuate Waongo

Mikesha iliyopita nilitaja tabia ya Abu Huraira, nikiwaeleza kwamba Khalifa Umar alimtandika viboko kwa sababu alizoea kusimulia hadithi za uwongo kutoka kwa Mtume. Je, hakuwa miongoni mwa Masahaba? Je, hakusimulia idadi kubwa ya hadithi kwa uongo? Halikadhalika, hawakuwa Masahaba wengine kama Sumra Bin Junda wamejumuishwa miongoni mwao? Je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah anaweza kuamuru jumuiya kufuata waongo na waghushaji?

Kama hadithi hii ni sahihi, yaani, kwamba kama tukimfuata yeyote katika masahaba, tutaongoka, basi tafadhali tujulishe ni yupi tumfuate, kama masa- haba wawili wanakwenda njia mbili tofauti.

Au kama kuna makundi mawili kila moja linapigana dhidi ya jingine, au kila moja kinyume na jingine, ni yupi ambaye itatupasa sisi kumuunga mkono?

Hafidh: Kwanza, masahaba watukufu wa Mtume wa Allah hakuwa maadui wenyewe kwa wenyewe. Na hata kama mmoja alimpinga mwingine, lazima tuupime ukweli huo vizuri. Yule ambaye ni safi na ambaye maelezo yake yana mantiki zaidi anapaswa kufuatwa.

Muombezi: Kama, kwa mujibu wa maelezo yako, tunafanya uchunguzi makini na kuona kwamba mmoja wao ni ni safi na yuko katika upande wa haki, basi kundi la upande mwingine la masahaba lazima liwe chafu na kwenye upande wa makosa. Basi hadithi hii kimsingi inapoteza sifa kwa sababu haiwezikani kwamba masahaba wasiokubaliana wanaweza wote kuwa vyanzo vya uongofu.

Upinzani Wa Masahaba Huko Saqifa

Kama hadithi hii ni sahihi kwa nini mnaleta upinzani dhidi ya Mashi’a, kwa sababu wao wamefuata kundi la Masahaba kama Salman, Abu Dharr, Mikidadi, Ammar-e-Yasir, Abu Ayyub Ansar, Hudhaifa Nakha’i na Khuzaima Dhu’sh-Shahadatain, nk., ambao nimewataja katika mikesha iliyopita? Kwa hakika watu hawa hawakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Kwa hiyo, kati ya Masahaba waliopingana wenyewe kwa wenyewe, ni nani waliokuwa upande wa haki? Kwa vyovyote vile kundi moja lilikuwa upande wa makosa ingawa hadithi uliyonukuu hutuambia kwamba tunaweza kufuata yeyote kati ya Masahaba na kuongoka.

Upinzani Wa Sa’d Bin Ubaida Kwa Abu Bakar Na Umar

Je, Sa’d Bin Ubaid hakuwa mmoja wa Masahaba ambao hawakula kiapo kwa Abu Bakr na Umar? Wanahistoria wote wa Shi’a na Sunni kwa pamoja wanashikilia kwamba yeye alikwenda Syria na akaishi kule mpaka katikati ya kipindi cha Ukhalifa wa Umar, ndipo ali- uawa. Kwa hiyo kumfuata yeye na kumpinga Abu Bakr na Umar, kwa mujibu wa hadithi hii, ni njia ya wokovu.

Talha Na Zubair Walimkabili Ali Huko Basra

Je, Talha na Zubair sio miongoni mwa Masahaba waliokula kiapo cha utii chini ya mti? Je, hawakumpinga mrithi wa haki Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Khalifa wa nne anayekubaliwa kwa mujibu wa imani yenu? Je, hawakuwa Masahaba hawa ni wenye kuhusika na umwagaji wa damu ya Waislamu wasio idadi? Sasa, tafadhali tujulishe ni lipi katika makundi haya mawili ya Masahaba ambao walipigana wenyewe kwa wenyewe ambalo kweli limeongoka. Kama utasema kwamba, kwa vile makundi yote yalikuwa na utii yalikuwa katika upande wa haki, utakuwa umekosea. Haiwezikani kudai kwamba makundi yanayopingana yote yawe yameongoka.

Kwa hiyo ina maana kwamba Masahaba ambao walikuwa upande wa Ali walikuwa kwa hakika wao ndio walioongoka. Kundi lililokuwa ule upande mwingine lilichukuwa njia ya makosa; na huu ni uthibitisho mwingine wa kukataa maelezo yako kwamba Masahba wale wote ambao walikuwepo katika Bai’at-e- Ridhwan, chini ya mti, walikuwa wameongoka.

Miongoni mwa wale ambao walikula kiapo cha utii walikuwa hawa wawili, Talha na Zubair, ambao vile vile walipigana dhidi ya khalifa wa haki. Kwa hakika wamepigana dhidi ya mtu ambaye kuhusu yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ewe Ali, kupigana dhidi yako ni kupigana dhidi yangu.” Je, hii si sawa na kupingana dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Basi vipi unasema kwamba neno Ashab au kuwepo chini ya mti wa kiapo ni uthibitisho wa wokovu? Mu’awiya Na ‘Amr Ibn Al-As Walizoea Kumlaani Na Kumtukana Ali

Muawiya na Amr al-As walikuwa Masahaba lakini bado walipigana dhidi ya mrithi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumlaani na kumtukana Ali katika mikutano ya hadhara na hata katika hutuba zinazotolewa baada ya Sala ya Ijumaa. Walifanya hivyo licha ya ukweli, kama ilivyoandikwa na maulamaa wakubwa wa madhehebu yenu katika vitabu vyao sahihi, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alirudia rudia kusema: “Yule ambaye anamtukana au kumlaani Ali, ananitukana mimi. Yule ambaye ananitukana mimi anamtukana Allah.”

Mwanachuoni Taftazani kwa kinaganaga alishughulikia suala hili katika Sharhe Maqasid. Yeye anaandika kwamba kwa vile Masahaba walikuwa maadui wenyewe kwa wenyewe, baadhi yao walikuwa wamepotea kutoka kwenye njia ya haki. Baadhi yao kwa ajili ya husda na matamanio ya kidunia, walifanya aina zote za makosa ya kiukatili.

Ni wazi kwamba Masahaba wengi, ambao hawakuwa ma’sum (wasiokosea) walifanya matendo maovu. Lakini baadhi ya maulamaa kwa sababu wanawapendelea, walijaribu kuficha makosa yao. Kuna hoja nyingi za kukataa hadithi hii iliyoko kwenye mjadala. Hakuna shaka kwamba hadithi hii ni ya kughushi. Maulamaa wenu wengi wameonyesha wasiwasi wao kuhusu usahihi wa vyanzo vyake.

Vyanzo Vya Hadithi “Masahaba Wangu Ni Kama Nyota” Ni Dhaifu

Baada ya kunukuu hadithi hii katika kitabu chake Sharhu’sh-Shifa, Jz. 2. uk. 91, Kadhi Ayaz anasema kwamba Darqutni katika kitabu chake Faza’il na Ibn Abdu’l-Birr wasema kwamba hadithi hii sio sahihi.

Vile vile imesimuliwa kutoka kwa Abd Bin Hamid katika Musnad yake ambaye ananukuu kutoka kwa Abdullah Ibn Umar kwamba Bazar alikataa kukubali usahihi wa hadithi hii. Vile vile alisema kwamba Ibn Adi ananukuu katika kitabu chake Kamil pamoja na rejea zake mwenyewe kutoka kwa Nafi, na yeye kutoka Abdullah Ibn Umar, kwamba vyanzo vya hadithi hii ni dhaifu sana. Baihaqi vile vile ameelezwa kwamba aliandika kuwa habari ya hadithi hii inajulikana sana lakini vyanzo vyake ni dhaifu.

Miongoni mwa vyanzo vya hadithi hii ni Harith Bin Ghazin, ambaye tabia yake inaju- likana, na Hamza Ibn Abi Hamza Nussairi, ambaye alishutumiwa kwa kuongopa. Udhaifu wa hadithi hii uko wazi. Ibn Hazm vile vile anasema kwamba hadthi hii ni ya kubuni na ni yenye kukataliwa. Hivyo katika majadiliano yetu hatuwezi kutengemea juu ya hadithi kama hii yenye nyororo (asnad) dhaifu ya vyanzo. Hata tukichukulia kwamba hadithi hii ilikuwa sahihi, isingeweza kutumika katika maana ya ujumla; ingeashiria tu kwa wale Masahaba watiifu na wachamungu ambao kwa mujibu wa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wamefuata Kitabu cha Allah na kizazi kitukufu cha Mtume. Masahaba Hawakuwa Ma’sum (Wasio Kosea)

Nikiwa nimeyasema haya, kama nitawakosoa baadhi ya Masahaba, msinichukulie mimi kama si mwadilifu. Hata hivyo wao walikuwa ni wanadamu, na iliwezekana wao kukosea.

Hafidh: Sisi pia tunaamini kwamba Masahaba hawakuwa ma’sum, lakini wakati huo huo ni ukweli unaokubalika kwamba wote kwa pamoja walikuwa ni watu wema. Hawakufanya makosa yoyote.

Muombezi: Madai yako ni mno, kama ukisisitiza kwamba wote walikuwa waadilifu na walioepukana na makosa, kwa vile katika vitabu sahihi vilivyoandikwa na maulamaa wenu wanahoji dhidi ya hilo. Wanatuambia kwamba hata baadhi ya Masahaba wakubwa wakati mwingine walifanya makosa.

Hafidh: Hatuzitambui taarifa kama hizo. Tafadhali tueleze kuhusu taarifa hizo kama unaweza.

Muombezi: Tukiyaacha yale waliyoyafanya wakati wa zama za ujinga (yaani, kabla ya kuja kwa Uislamu), wamefanya maovu mengi baada ya kusilimu. Inatosha kutaja tukio moja tu kwa njia ya mfano. Maulamaa wenu wakubwa wanaandika katika vitabu vyao sahihi kwamba katika ule mwaka wa kuiteka Makka (8 A.H.) baadhi ya wale Masahaba wakubwa walijiingiza katika burudani ya sherehe na shamra shamra na kwa siri wakany- wa pombe.

Hafidh: Hiki kwa hakika ni kisa cha kubuni. Wakati pombe ilikuwa imetangazwa kuwa ni haramu, Masahaba wa kuheshimika hawakuhudhuria japo hafla kama hizo, sembuse kuta- ja unywaji wa tembo.

Muombezi: Haikubuniwa kamwe na wapinzani. Kama itakuwa imebuniwa kwa hali yoyote ile, basi ilifanywa hivyo na ulamaa wenu wenyewe.

Nawab: Kama kulikuwa na hafla kama hiyo, majina ya huyo mwenyeji na wageni vilevile yatakuwa yametajwa. Unaweza kuelezea nukta hiyo?

Muombezi: Ndio, maulamaa wenu wenyewe wameielezea hiyo.

Kunywa Pombe Kwa Masahaba Kumi Katika Mkutano Wa Siri

Ibn Hajar katika kitabu chake Fathu’l-Bari, Jz. 10, uk. 30, anaandika kwamba Abu Talha Zaid Bin Sahl alitayarisha hafla ya pombe katika nyumba yake na akakaribisha watu kumi. Wote walikunywa pombe na Abu Bakr alisoma baadhi ya mashairi kuwasifia baadhi ya makafiri ambao waliuliwa katika vita ya Badr.

Nawab: Je, majina ya wageni yametajwa vile vile? Kama ndivyo, tafadhali tujulishe.

Muombezi: (1) Abu Bakr Bin Abi Kuhafa, (2) Umar Ibn Khattab, (3) Abu Ubaida Garra, (4) Ubai Bin Ka’b, (5) Sahl Bin Baiza, (6) Abu Ayyub Ansari, (7) Abu Talha (mwandaaji), (8) Abu Dajjana Samak Bin Kharsa, (9) Abu Bakr Bin Shaghuls, (10) Anas Bin Malik, ambaye alikuwa na umri wa miaka 18 wakati ule na ambaye alikuwa ndiye mgawaji wa pombe hiyo. Baihaqi katika Sunan yake, Jz. 8, uk. 29 vile vile amesimulia kutoka kwa Anas mwenyewe kwamba yeye alikuwa ndiye mdogo kuliko wote wakati huo na alikuwa akiwapimia pombe. (Kufikia hapa kukawa na vurumai kubwa ndani ya mkutano huo.)

Sheikh: Naapa kwa jina la Allah kwamba kisa hiki kimebuniwa na maadui!

Muombezi: Umehamaki sana na umetoa kiapo cha kufuru! Lakini hauko katika makosa ya moja kwa moja kabisa. Masomo yako yana kikomo. Kama ungesoma kwa mapana zaidi, ungejua kwamba maulamaa wako mwenyewe wameandika yote haya. Sasa yakubidi uombe msamaha wa Allah.

Sasa ninalazimika kuelezea mambo kwa mujibu wa maelezo ya maulamaa wenu wenyewe. Muhammad Bin Isma’il Bukhari katika Sahih yake (akifafanua juu ya Ayat-e-Khamr, ‘aya inayohusu pombe’, katika sura ya Ma’ida ya Qur’ani Tukufu); Muslim Ibn Hajar katika Sahih yake (Kitab-e-Ashraba Bab-e- Tahrimu’l-Khamr); Imamu Ahmad Bi Hanbal katika Musnad yake, Jz. 30, uk. 181 na 227; Ibn Kathir katika Tafsir yake, Jz. 11, uk. 93; Jalalu’d- Din Suyut katika Durr’l-Mansur, Jz. 2, uk. 321; Tabari katika Tafsir yake, J. 7, uk. 24; Ibn Hajar Asqalani katika Isaba, Jz. 4, uk. 22 na Fathu’l-Bari, Jz. 10, uk. 30; Badru’-d-Din Hanafi katika Umdatu’l-Qari, Jz. 10, uk. 84; Baihaqi katika Sunan yake, uk. 286 na 290; na wengine wameandika ukweli huu pamoja na maelezo marefu.

Sheikh: Pengine mambo haya yalitokea kabla pombe haijafanywa haramu.

Muombezi: Tunayoyapata kutoka kwenye vitabu vya Tafsir na historia yanaonesha kwamba hata baada ya aya za kuharamisha pombe baadhi ya Waislamu na Masahaba waliendelea kunywa pombe iliyokatazwa.

Muhammad Bin Jarir Tabari anasimulia katika Tafsir-e-Kabir, Jz. 2, uk. 203, kutoka kwa Abil Qamus Zaid Bin Ali, ambaye alisema Allah ameteremsha mara tatu aya zinazokataza pombe. Katika aya ya kwanza anasema:

{ﻳﺴﺎﻟُﻮﻧَﻚَ ﻋﻦ اﻟْﺨَﻤﺮِ واﻟْﻤﻴﺴﺮِ ۖ ﻗُﻞ ﻓﻴﻬِﻤﺎ اﺛْﻢ ﻛﺒِﻴﺮ وﻣﻨَﺎﻓﻊ ﻟﻠﻨﱠﺎسِ واﺛْﻤﻬﻤﺎ اﻛﺒﺮ ﻣﻦ ﻧَﻔْﻌﻬِﻤﺎ ۗ{219

“Wanakuuliza kuhusu ulevi na kamari. Sema: katika hivyo mna dhambi kubwa na manufaa kwa watu, lakini dhambi zake ni kubwa kuliko manufaa yake…” (2:219)

Lakini Waislamu hawakuacha pombe mara moja. Wakati mmoja watu wawili, wakiwa wamelewa, walisali Swala zao na kuzungumza mambo yasio kuwa na maana, aya nyingine iliteremshwa, isemayo:

{ﻳﺎ اﻳﻬﺎ اﻟﱠﺬِﻳﻦ آﻣﻨُﻮا  ﺗَﻘْﺮﺑﻮا اﻟﺼَةَ واﻧْﺘُﻢ ﺳﺎرﱝ ﺣﺘﱠ ﺗَﻌﻠَﻤﻮا ﻣﺎ ﺗَﻘُﻮﻟُﻮنَ{43

“Enyi ambao mmeamini! msikaribie Sala hali mmelewa, mpaka myajue mnayo yasema…” (4:43) Hata baada ya aya hii, unywaji wa pombe uliendelea, lakini watu hawakusali wakiwa wamelewa. Siku moja mtu mmoja alikunywa pombe (kwa mujibu wa taarifa ya Bazar, Ibn Hajar na Ibn Mardawiyya mtu huyo alikuwa ni Abu Bakr) na akatunga shairi kwa ajili ya makafiri ambao waliuawa katika vita ya Badir.

Wakati Mtume aliposikia hili alikasirika sana. Alikwenda kule inakofanyika hafla hiyo na akataka kumpiga. Yule mtu akasema, “Naomba kinga ya Allah kutokana na ghadhabu ya Allah na Mtume Wake. Allah awe shahidi yangu, sitakunywa pombe tena.” Kisha aya ifuatayo ikateremshwa:

{ﻳﺎ اﻳﻬﺎ اﻟﱠﺬِﻳﻦ آﻣﻨُﻮا اﻧﱠﻤﺎ اﻟْﺨَﻤﺮ واﻟْﻤﻴﺴﺮ واﻧْﺼﺎب وازْم رِﺟﺲ ﻣﻦ ﻋﻤﻞ اﻟﺸﱠﻴﻄَﺎنِ ﻓَﺎﺟﺘَﻨﺒﻮه ﻟَﻌﻠﱠﻢ ﺗُﻔْﻠﺤﻮنَ {90

“Enyi ambao mmeamini! Bila shaka ulevi, na kamari na kuabudu masanamu na kupiga ramli, ni uchafu katika kazi ya shetani. Basi jiepusheni navyo, ili mpate kufanikiwa.” (5:90).

Miongoni mwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwepo wazuri na wabaya kama ambavyo wapo miongoni mwa Waumini na Waislamu wengine. Wale miongoni mwao ambao walijaribu kumtii Allah na Mtume Wake walifikia daraja ya juu. Wale ambao walifuata tamaa za kidunia walikuwa wakidharauliwa na wengine. Hivyo wale ambao wanakosoa Masahaba wa kidunia, wanafanya hivyo kwa sababu fulani.

Yale matendo maovu ya baadhi ya masahaba, ambayo yameandikwa katika vitabu sahihi vya maulamaa wenu wenyewe, vile vile yanafaa kulaumiwa kwa mujibu wa ushahidi wa Qur’ani Tukufu. Mashi’a wanawalaumu katika misingi hiyo. Kama kuna majibu ya mantiki kwenye hoja hii, tuko tayari kuikubali.

Uvunjaji Kiapo Wa Masahaba

Inashangaza kwamba hata baada ya kusikia sifa zao za kulaumika (nimetaja chache tu kati ya nyingi) bado mnaendelea kuniuliza kuhusu maovu yao! Sasa ningependa kuwasilisha mfano mwingine wa matendo yao ya kuchikiza, ambayo yameandikwa katika vitabu vyote vya madhehebu zote: “Uvunjaji wa kiapo”. Allah amelifanya ni wajibu suala la mtu kutekeleza ahadi. Anasema: “Na timizeni ahadi ya Allah mnapo ahidi, wala msivunje viapo baada ya kuvithibitisha…” (16:91)

Na tena Allah amewaita wale ambao wanaovunja kiapo walaaniwa. Anasema: “Na wale ambao wanavunja ahadi ya Allah baada ya kuzifunga, na wanayakata yale ambayo Allah ameamrisha yaungwe, na wanafanya ufisadi katika nchi; hao ndio watakaopata laana, na watapata nyumba mbaya.” (13:25)

Hivyo ni wazi kutoka kwenye aya za Qur’ani Tukufu na kutoka katika idadi kubwa ya hadithi kwamba kuvunja kiapo ni dhambi kubwa, hususan kiapo kilichofanywa kwa Allah na Mtume wake. Uzito wa kosa hili ulikuwa mkubwa sana kwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hafidh: Ni kiapo gani cha utii ambacho Masahaba walifanya na Mtume na wakakivunja? Itawezaje kuwa chini ya mashambulizi ya aya za Qur’ani? Nadhani kwamba kama utaliangalia suala hili kwa makini utakubali kwamba mambo yote haya ni ubunifi mtupu wa Mashi’a. Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa wameepukana na makosa yote haya.

Katika Qur’ani Tukufu “Wakweli” Humaanisha Muhammad Na Ali

Muombezi: Nimekuambieni mara kwa mara kwamba Mashi’a wamejifunga kuwafuata viongozi wao. Vinginevyo hawawezi kuwa Mashi’a. Qur’ani Tukufu imetoa ushahidi wa ukweli wa viongozi wao. Maulamaa wenu mashuhuri kwa mfano, Imamu Tha’labi na Jalalu’d-Din Suyut katika vitabu vyao vya Tafsir, Hafiz Abu Nu’aim Ispahani katika kitabu chake Ma Nazal mina’l-Qur’ani fi Ali, Khatib Khawarizmi katika Manaqib, Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, sura ya 39, akisimulia kutoka kwa Khawarizmi, Hafiz Abu Nu’aim na Hamwaini na Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib, sura ya 62, wote wamenukuu kutoka kwenye kitabu cha historia cha mwanachuoni mkubwa Muhaddith-e-Sham kwamba katika aya Tukufu,

{ﻳﺎ اﻳﻬﺎ اﻟﱠﺬِﻳﻦ آﻣﻨُﻮا اﺗﱠﻘُﻮا اﻟﻪ وﻛﻮﻧُﻮا ﻣﻊ اﻟﺼﺎدِﻗﻴﻦ {119

“Enyi mlioamini! Mcheni Allah na kuweni pamoja na wakweli”. (9:119)

Wakweli maana yake Muhammad na Ali. Hivyo wafuasi wa familia hii tukufu hawawezi kuwa waongo au waghushaji kwa sababu ni yule mtu tu ambaye hana sababu za kweli na na zenye nguvu ndiye anaweza kusema uwongo au kughushi visa vya uwongo na kupata kitu cha kutegemea juu ya njia hii. Wanachosema Mashi’a kimeandikwa na maulamaa wenu wenyewe.

Kwanza mnapaswa kuwakataa maulamaa wenu, ambao wameandika mambo haya. Lau maulamaa wenu wasingeandika kuhusu uvunjaji wa kiapo wa Masahaba katika vitabu vyao sahihi, nisingelitaja hilo katika mkutano huu. Hafidh: Ni nani katika maulamaa wa ki-Sunni ambaye ameandika kwamba Masahaba walivunja kiapo cha utii. Maneno matupu hayawezi kusaidia.

Muombezi: Mimi sio ninazungumza tu. Hoja yangu ni yenye mantiki kamili. Masahaba walivunja kiapo chao cha utii mara nyingi. Walivunja kiapo cha utii ambacho kwacho Mtume wa Allah aliwaamuru wao, cha muhimu zaidi ni kiapo cha utii kule Ghadir-e-Khum.

Hadithi Ya Ghadir Na Asili Yake

Maulamaa wote, wa Shi’a na Sunni wanakubali kwamba, katika mwaka wa 10 wa Hijra, Mtume wa Allah akiwa anarudi kutoka kwenye hija yake ya mwisho, aliwakusanya pamoja Masahaba wote pale Ghadir- e-Khum siku ya 18 Dhi’l-Hijja. Baadhi ya wale ambao walikuwa wametangulia waliitwa warudi kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wale ambao walikuwa nyuma walingojewa. Maulamaa wenu wengi wanahistoria na vyanzo vya Shi’a wanaioa idadi ya watu 70000, na baadhi ya maulamaa wenu wengine, kwa mfano, Tha’labi katika kitabu chake cha Tafsir, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkirat’u-Khasa’isi’l- Umma fi Ma’rifati’l-Aimma na wengine wameandika kwamba walikuwepo watu 120,000 waliokusanyika pale.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliamuru itengenezwe mimbari. Alipanda katika mimbari na akatoa hotuba ndefu, ambayo sehemu yake kubwa ikiwa imejaa sifa na tabia za Amir’l-Muminin. Alisoma takribani aya zote zilizoshuka kwa ajili ya kumsifu Ali na akawakumbusha watu cheo kitukufu cha umakamu wa Amirul-Mu’minin.

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Enyi watu! Je, mimi sina mamlaka zaidi juu ya nafsi zenu kuliko ninyi wenyewe?” Rejea hii ni kwenye aya tukufu, “ Mtume ni bora zaidi kwa waumini kuliko nafsi zao…” (33:6)

Mkusanyiko ule ukajibu kwa sauti moja “Hakika, Ewe Mjumbe wa Allah!” Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akatangaza: “Yule ambaye mimi ni (maula kwake) mwenye kumtawalia mambo yake, huyu Ali ni (maula kwake) mwenye kumtawalia mambo yake.” Baada yakusema hivi alinyoosha mikono yake na akaomba kwa Allah. “Ewe Allah, kuwa rafiki kwa yule ambaye ni rafiki kwake (yaani Ali) na kuwa adui kwa yule ambaye ni adui kwake (yaani Ali) msaidie yule ambaye anamsaidia yeye na mtelekeze yule ambaye anamtelekeza yeye.”

Kisha hema lilikitwa kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alimuamuru Kiongozi wa waumini Ali kukaa ndani ya hema. Umma wote uliamriwa kutoa kiapo cha utii kwa Ali.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema kwamba ametoa maelekezo haya kulingana na amri ya Allah. Mtu wa kwanza kutoa kiapo ni siku hiyo alikuwa ni Umar. Kisha Abu Bakr, Uthmani, Talha, na Zubair walifuatia, na watu wote hawa waliendelea kutoa kiapo cha utii kwa muda wa siku tatu (yaani wakati ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alibakia pale).

Hafidh: Unaweza kuamini kwamba tukio la umuhimu kama wa namna hiyo limetokea kama inavyodaiwa na wewe na kwamba hakuna hata mmoja katika maulamaa maarufu aliyelisimulia hilo?

Muombezi: Sikutazamia maelezo kama haya kutoka kwako. Habari ya Ghadir Khum iko wazi kama mwanga wa mchana na hakuna yeyote ila shupavu na mtu mkaidi ndiye awezaye kuleta fedheha kwa kukataa tukio kama hili. Suala hili muhimu limeandikwa kwenye kumbukumbu na maulamaa wenu wote wachamungu katika vitabu vyao sahihi. Ningependa kutaja hapa baadhi ya majina ya waandishi na vitabu vyao ili uelewe kwam- ba maulamaa wenu wote maarufu walitegemea hadithi hii.

1. Imam Fakhru’d-Din Razi – Tafsir-e-Kabir Mafatihu’l-Ghaib. 2. Imam Ahmad Tha’alabi – Tafsir-e-Kashfu’l-Bayan. 3. Jalalu’d-Din Suyuti – Tafsir-e-Durru’l-Manthur. 4. Abu’l-Hasan Ali Bin Ahmad Wahidi Nishapuri – Asbabu’n-Nuzul. 5. Muhammad Bin Jarir Tabari – Tafsiru’l-Kabir. 6. Hafidh Abu Nu’aim Ispahani – Ma Nazal Mina’l-Qur’ani fi Ali na Hilyatu’l-Auliya. 7. Muhammad Bin Isma’il Bukhari – Ta’rikh, Jz. 1, uk. 375. 8. Muslim Bin Hajjaj Nishapuri – Sahih, Jz. 2, uk. 325. 9. Abu Dawud Sijistani – Sunan. 10. Hafidh Ibnu’l-Iqda – Kitabu’l-Wilaya. 11. Ibn Kathir Shafi’i Damishqi – Ta’rikh. 12. Imam Ahmad Ibn Hanbal – Musnad Jz. 4, uk. 281&371. 13. Abu Hamid Muhammad Bin Muhammad Al-Ghazali – Sirru’l-Alamin. 14. Ibn Abdu’l-Birr – Isti’ab. 15. Muhammad Bin Talha Shafi’i – Matalibu’s-Su’ul, uk. 16. 16. Ibn Maghazili Faqih Shafi’i – Manaqib. 17. Nuru’d-Din Bin Sabbagh Maliki – Fusulu’l-Muhimma. 18. Husain Bin Mas’ud Baghawi – Masabihu’s-Sunna. 19. Abu’l-Mu’ayyid Muwafiq Bin Ahmad Khatib Khawarizmi – Manaqib. 20. Majdu’d-Din Bin Athir Muhammad Bin Muhammad Shaibani – Am’u’l-Usul. 21. Hafidh Abu Abdu’r-Rahman Ahmad Bin Ali Nisa’i – Khasa’isu’l-Alawi na Sunan. 22. Sulaiman Balkhi Hanafi – Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 4. 23. Shahabu’d-Din Ahmad Bin Hajar Makki – Sawa’iq Muhriqa na Kitabu’l-Manhu’l- Malakiyya, hususan Sawa’iq, sehemu ya 1, uk. 25. pamoja na ushupavu wake mkubwa, anasema: “Hii ni hadithi ya kweli; ukweli wake hauwezi kutiliwa shaka. Hakika imesimuliwa na Tirmidhi, Nisa’i na Ahmad, na kama ikichunguzwa, vyanzo vyake ni vizuri vya kutosha.”

24. Muhammad Bin Yazid Hafiz Ibn Maja Qazwini – Sunan. 25. Hafidh Abu Abdullah Muhammad Bin Abdullah Hakim Nishapuri – Mustadrak. 26. Hafidh Sulaiman Ibn Ahmad Tabrani – Aust. 27. Ibn Athir Jazari – Usudu’l-Ghaiba. 28. Yusuf Sibt Ibn Jauzi – Tadhkiratu’l-Khasa’isu’l-Umma, uk. 17. 29. Abu Umar Ahmad Bin Abi Abd Rabbih – Iqdu’l-Farid. 30 Allama Samhudi – Jawahiru’l-Iqdain. 31. Ibn Taimiyya Ahmad Bin Abdu’l-Halim– Minhaju’s-Sunna. 32. Ibn Hajar Asqalani – Fathu’l-Bari na Tahdhibu’t-Tahdhib. 33. Abdu’l-Qasim Muhammad Bin Umar Jarrullah Zamakhshari – Rabiu’l-Abrar. 34. Abu Sa’id Sijistani – Kitabu’d-Darayab Fi Hadithi’l-Wilaya. 35. Ubaidullah Bin Abdullah Haskani – Du’atu’l-Huda ila Ada Haqqi’l-Muwala. 36. Razin Bin Mu’awiya Al-Abdari – Jam Bainu’s-Sahihi’s-Sitta 37. Imam Fakhru’d-Din Razi anasema katika Ktabu’l-Arba’in kwamba jumuiya yote kwa pamoja wanathibitisha hadithi hii. 38. Muqibili – hadithu’l-Mutawatira. 39. Suyut – Ta’rikhu’l-Khulafa. 40. Mir Sayyid Ali Hamadani – Mawaddatu’l-Qurba. 41. Abu Fath Nazari – Khasa’is’u’l-Alawi 42. Khwaja Parsa Bukhari – Faslu’l-Khitab. 43. Jamaluddin Shirazi – Kitabu’l-Arba’in. 44. Abdul Ra’ufu’l-Manawi – Faizu’l-Qadir fi Sharh-i-Jamiu’s-Saghir. 45. Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i – Kifayatu’t-Talib, sehemu ya 1. 46. Yahya Bin Sharf-Nauwi – Tahzibu’l-Asma wa’l-Lughat. 47. Ibrahim Bin Muhammad Hamwaini – Fara’idu’s-Simtain. 48. Kadhi Fadhlullah Bin Ruzhahan – Ibtalu’l-Batil. 49. Shamsuddin Muhammad Bin Ahmad Sharbini – Siraju’l-Munir. 50. Abul Fath Shahristani Shafi’i – Milal wa’n-Nihal. 51. Hafidh Abu Bakr Khatib Baghdadi – Ta’rikh. 52. Hafidh Ibn Asakir Abul-Qasim Damishqi – Ta’rikh-i-Kabir. 53. Ibn Abi’l-Hadid Mutazali – Sharhe Nahju’l-Balagha 56. Ala’uddin Samnani – Urwatu’l-Wuthqah. 57. Ibn Khaldun – Muqaddima. 58. Mawlana Ali Muttaqi Hindi – Kanzu’l-Ummal.

59. Shamsuddin Abul Khair Damishiqi – Asanu Matalib. 60. Sayyid Sharif Hanafi Jurjani – Sharh-i-Mawaqit 61. Nizamuddin Nishapuri – Tafsir-I-Ghara’ibu’l-Qur’ani.

Hadithi Ya Ghadir Imesimuliwa Na Tabari, Ibn Iqda Na Haddad

Nimesimulia vyanzo nilivyoweza kukumbuka. Lakini zaidi ya Maulamaa wenu wakubwa mia tatu wameisimulia hadithi ya Ghadir, aya za baligh (kuhubiri), kamalu’d-Din (ukamilifu wa dini), na mazungumzo katika eneo la Msikiti, kutoka kwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zaidi ya mia moja.

Kama tungetakiwa kueleza majina ya wasimuliaji wote hawa, yangetengeneza kitabu kamili. Hata hivyo, kiasi hiki, kinatosha kuthibitisha kwamba hadithi hii inakubaliwa na wote kama hadithi ya kweli.

Baadhi ya Maulamaa wenu wakubwa wameandika vitabu juu ya suala hili. Kwa mfano, mufasir mashuhuri na mwanahistoria wa karne ya nne hijiriya, Abu Ja’far Muhammad Bin Jarir Tabari (amekufa 310 A.H.), anatoa maelezo kamili ya hadithi ya Ghadir katika kitabu chake “Kitabu’l-Wilaya” na ameisimulia kupitia sanad sabini na tano za wapokezi.

Hafidh Abu’l-Abbas Ahmad Bin Sa’id Abdu’r-Rahman Al-Kufi, mashuhuri kwa jina la Ibn Iqda (amekufa 333 A.H.), amesimulia hadithi hii sharif katika kitabu chake “Kitabu’l- Wilaya” kupitia sanad 125 za wapokezi kutoka kwa Masahaba 125 wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ibn Haddad Hafidh Abu ‘l-Qasim Haskani (amekufa 492 A.H.), katika kitabu chake “Kitabu’l-Wilaya”, amesimulia kwa urefu hadithi ya Ghadir sambamba na kushuka kwa aya za Qur’ani. Kwa ufupi, wanachuoni wenu wote wateule na maulamaa wa daraja za juu (isipokuwa idadi ndogo ya wapinzani washupavu - wakaidi), wamenukuu asili ya hadithi hii kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.),ambaye alimtangaza Ali kama makamu wake siku ya mwezi 18 Dhu’l-Hijja katika mwaka wa hija yake ya mwisho.

Vile vili ni ukweli kwamba Khalifa Umar alikuwa wa kwanza miongoni mwa Masahaba kuonesha furaha yake juu ya tukio hili. Huku akiwa ameushika mkono wa Ali, alisema: “Hongera ewe Ali! Asubuhi hii imeleta neema kubwa kwako. Umekuwa maula wangu na maula wa waumini wote wanaume na waumini wanawake.”

Ushauri Wa Jibril Kwa Umar

Mwanafiqh wa ki-Shafi’i, Mir Sayyid Ali Hamadani wa karne ya nane hijiriyya, mmoja wa wanachuoni wa kutengemewa wa madhehebu yenu, anaandika katika kitabu chake “Mawaddatu’l-Qurba,” Mawadda ya 5, kwamba idadi kubwa ya Masahaba wamemnukuu Khalifa Umar katika sehemu tofauti akisema:

“Mtume wa Allah alimfanya Ali Maula, mkuu na kiongozi wa taifa (la ki-Islamu). Alitangaza katika mkutano wa hadhara kwamba yeye (Ali) ni maula wetu. Baada ya kuomba kwa ajili ya rafiki zake na kuwalaani adui zake, alisema: ‘Ewe Allah! Wewe ni shahidi wangu.’ (yaani, ‘Nimekamilisha jukumu langu la utume.’).

Katika tukio hili kijana wa kupendeza mwenye kunukia uzuri alikuwa amekaa kando yangu. Aliniambia, ‘Hakika Mtume wa Allah amefungamana na agano ambalo hakuna yeyote wa kulivunja isipokuwa mnafiki. Hivyo Umar! Jiepushe kutokana na kulivunja.’

Nilimueleza Mtume wa Allah kwamba wakati anaongea na mkusanyiko ule wa watu, kijana wa kupendeza, mwenye kunukia uzuri alikuwa amekaa kando yangu na kwamba aliniambia kitu kama hicho.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema, ‘hakuwa wa kizazi cha Adam, bali alikuwa Jibril, (ambaye alitokea katika umbo hilo). Alitaka kusisitiza kuhusu nukta ambayo nimeitangaza kuhusu Ali.’”

Sasa nataka kutafuta haki kutoka kwenu, je, ilikuwa sahihi kwa wao kuvunja angano imara na Mtume wa Allah ndani ya miezi miwili, kuenda kinyume na kiapo chao kitakatifu cha utii kwa Ali, kuchoma moto nyumba yake, kuchomoa panga dhidi yake, kumfedhehesha, kumburuza mpaka msikitini kumlazimisha kula kiapo cha utii?

Hafidhi: Sikutengemea kwamba mwanachuoni wa kuheshimiwa na Sayyid mstaarabu kama wewe ungelihusisha mambo ya kidunia kwa Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwatangaza wao kwamba ni chanzo cha uongofu kwa ajili ya umma wakati aliposema: “Masahaba wangu ni kama nyota; kama mkimfuata yeyote kati yao, mtaongoka.”

Hadithi Ya “Kuwafuata Masahaba” Sio Sahihi

Muombezi: Kwanza ningekuomba usirudie kitu kile kile kila mara. Punde tu ulihoji kutoka kwenye hadithi hii hii na nimekupa majibu yake.

Masahaba kama watu wengine walikuwa ni wenye kufanya makosa. Hivyo wakati wanathibishwa kwamba wao sio masum (wasiokosea), kwa nini mtu ashangae, kama pamoja na ushahidi sahihi, mambo ya kidunia yanahusishwa kwao? Pili ili kuisafisha akili yako, nitakupa majibu tena, ili kwamba usije ukategemea juu ya hadithi hiyo baadae. Kwa mujibu wa utafiti wa maulamaa wenu wakubwa, hadithi hii si ya kutegemewa, kama nilivyoelezea mapema.

Kadhi Ayaz Maliki ananukuu kutoka kwa maulamaa wenu wakubwa kwamba kwa vile wasimuliaji wa hadithi hii hujumuisha majina ya watu wajinga na wasio na elimu, Harith Bin Qazwin na Hamza Bin Abi Hamza Nasibi, ambao wameonekana kuwa ni waongo, hadithi hii haifai kusimuliwa. Vile vile, Kadhi Ayaz, katika Sharh-e-Shifa na Baihaki katika kitabu chake “Kitab”, wametamka kwamba hadithi hii ni ya kughushi na wamekichukulia chanzo chake kama kisichoaminika.

Baadhi Ya Masahaba Walikuwa Ni Watumwa Wa Tamaa Zao Na Waligeuka

Dhidi Ya Haki

Tatu, kamwe sijasema kitu chochote cha ukorofi, ninasema tu kile ambacho maulamaa wenu wamekiandika. Nakushauri usome Sharh-e-Maqasid ya Fazil Taftazani, ambamo ndani yake anaelezea kwa uwazi kwamba kuna mifano mingi ya uadui miongoni mwa Masahaba, ambayo huoneshsa kwamba baadhi yao walikuwa wamegeuka kuwa watenda dhambi na madhalimu. Hivyo tunaona kwamba watu si wakuheshimiwa tu kwa sababu eti walikuwa Masahaba wa Mtume.

Heshima ya kweli iko kwenye matendo yao na tabia zao. Kama hawatokani na wanafiki, bali walikuwa watii na waaminifu kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakika lazima watukuzwe na waheshimiwe. Tutaweka mavumbi ya miguu yao kwenye macho yetu.

Hivyo, enyi wapenda haki, je, mnathibitisha kwamba hadithi nyingi kwenye vitabu vyenu sahihi zinazohusu kupigana dhidi ya Amiru’l-Mu’minin Ali, kama vile asemavyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Kupigana dhidi ya Ali ni kupigana dhidi yangu,” zote hizi ni za uwongo? Au mnakiri kwamba hadithi hizi ni za kweli kikamilifu hasa? Je, hazikuandikwa pamoja na vyanzo vya kuaminika katika vitabu vyenu vya maulamaa wenu wenyewe wa mashuhuri?

Hatuhitaji kutaja kwamba hadithi hizi zimeandikwa na maulamaa wa ki-Shi’a pamoja na maoni kamili ya wote pamoja katika vitabu vyao vyote. Kama mnakubali hadithi hizi, lazima mkubali kwamba Masahaba wengi walikuwa wachupa mipaka na wenye dhambi kama Mu’awiya. Umar Ibn As, Abu Huraira, Samra Bin Jundab, Talha, Zubair wote hawa ambao waliasi na wakipigana dhidi ya Ali, kwa kweli waliasi dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe.

Na kwa vile wamepigana dhidi ya Mtume, kwa hakika walipotea kutoka kwenye njia iliyo nyooka. Hivyo, kama tunasema kwamba baadhi ya Masahaba walikuwa watumwa wa tamaa zao, hatukuwa tumekosea, kwa sababu tulichokisema kilikuwa ni kweli. Mbali na hili, hatuko wenyewe tu katika kushikilia kwamba baadhi ya Masahaba walikuwa wenye dhambi, madhalimu na wachupa mipaka. Tunategemeza msimsmo wetu juu ya vitabu vya maulamaa wenu wenyewe wakubwa.

Maoni Ya Imamu Ghazali Kuhusu Masahaba Kuvunja Kiapo Kilichochukuliwa Siku Ya Ghadir-E-Khum.

Kama utachunguza kitabu cha “Sirru’l-Alamin” kilichokusanywa na Abu Hamid Bin Muhammad Ghazali Tusi, kamwe hutapinga kile ambacho ninasema. Hata hivyo, ninalaz- imika kunukuu sehemu ya tansifu yake ya nne kwa kuunga mkono maelezo yangu.

Anasema: “Ushahidi na mantiki vikawa na mwanga, na kuna makubaliano ya wote pamoja miongoni mwa Waislamu kuhusiana na matini (maandiko) ya hotuba ya katika siku ya Ghadir-e-Khum kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: ‘Yule ambaye ni maula kwake (ambaye namtawalia mambo yake), Ali ni maula wake (mwenye kumtawalia mambo yake).’

Kisha Umar mara moja akasema, ‘Hongera, hongera, Ewe Abu’l-Hasani! Wewe ni maula wangu na vile vile maula wa waumini wote wanaume na wanawake.’”

Aina hii ya pongezi kwa uwazi inaonesha kukubaliwa kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na kukubaliwa kwa uongozi na ukhalifa wa Ali. Lakini baadae walizidiwa na tamaa zao za kidunia. Kupenda utawala na mamlaka kuliwanyima huruma.

Walijichukulia wenyewe kumchagua Khalifa kule Saqifq-e-Bani Sa’dat. Walitaka kupandisha bendera ya kizazi chao wenyewe na kuteka nchi ili kwamba majina yao yaweze kuhifadhiwa katika historia. Walilewa tamaa ya madaraka. Walipuuza maamrisho ya Qur’ani, na maagizo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Waliuza dini yao kwa ajili ya dunia hii. Biashara mbaya iliyo- je waliyofanya na Allah!

Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa katika kitanda chake alichofia aliomba apewe kalamu na wino ili kwamba aweze kufafanua suala mrithi. (Allah anisamehe kwa kulisema hili), Lakini Umar alisema: “Muacheni mtu huyu. Anaweweseka.” Hivyo wakati ambapo Qur’ani Tukufu na hadithi hazikuweza kuwasaidia, walitegemea juu ya Ijma (makubaliano ya wote pamoja).

Lakini hii vile vile ni batili kwa sababu Abbas, kizazi chake, Ali, mke wake na watoto wao hawakujihusisha na wale ambao wamekula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Halikadhalika, watu wa Saqifa vile vile walikataa kula kiapo kwa Khazraji, na Ansar vile vile waliwakataa wao.

Enyi watu mnaoheshimiwa! Tafadhali kumbukeni, Mashi’a hawadai chochote isipokuwa kile ambacho maulamaa wenu wa haki wanacho kidai.

Lakini kwa vile mnatuchukia sisi, mnaona makosa katika yale tunayo yasema, hata yawe ya mantiki kiasi gani. Lakini kamwe hamuwalaumu maulamaa wenu ni kwa nini wameandika mambo kama haya ingawa kwa kweli wameufichua ukweli na wakachapisha ukweli huu kwenye kurasa za historia.

Sheikh: Sirru’l-Alamin haikuandikwa na Imamu Ghazali. Cheo chake kilikuwa cha juu sana kwa yeye kuweza kuandika kitabu kama hicho, na maulamaa wakubwa hawaamini kwamba kitabu hiki kiliandikwa na yeye.

Sirru’l-Alamin Ni Kitabu Cha Imamu Ghazali

Muombezi: Maulamaa wenu wengi wamekiri kwamba kitabu hiki kiliandikwa na Imamu Ghazali. Yusufu Sibt Ibn Jauzi alikuwa muangalifu sana katika rejea zake kwa wanachuoni wengine (na vile vile alikuwa mshabiki wa dini yake). Katika kitabu chake “Tadhkira Khawasu’l-Umma”, uk. 36, anajadili kutoka kwenye maelezo hayo hayo ya Imamu Ghazali katika kitabu chake “Sirru’l-Alamin” na ananukuu dondoo hiyohiyo ambayo nimeinukuu.

Kwa vile hakuna maoni yaliyofanywa kuhusu maelezo hayo, inaonesha kwanza, kwamba anakubali kitabu hiki kimeandikwa na Imamu Ghazali. Pili, vile vile anakubaliana na maoni yake, ambayo kwa ufupi nimeyaelezea, ingawa yeye mwenyewe ameyaelezea kwa urefu. Kama asingekubaliana nayo angeyatolea ufafanuzi.

Lakini hakika maulamaa wenu mashabiki wanapokutana na maelezo kama haya ya manachuoni wakubwa na wakashindwa kuyakataa kimantiki, amma husema kwamba kitabu hicho hakikuandikwa na mwandishi huyo, au kwamba ni ubunifu wa Mashi’a. Au hata wakati mwingine wanakwenda mbali zaidi kufikia kusema kwamba watu hawa waadilifu wote walikuwa wenye dhambi na makafiri.

Rejea Kwenye Cheo Cha Ibn Iqda

Kuna ushahidi kwamba maulamaa wenu wengi waliteswa kwa sababu tu walisema ukweli. Maulamaa mashabiki na watu wasio wasomi wa madhehebu yenu huchukulia kuwa ni haramu kusoma vitabu visivyofuata desturi na kanuni. Wandishi wa vitabu kama hivyo waliweza hata kuuawa kama ilivyokuwa kwa Hafidh Ibn Iqda Abu’l-Abbas Ahmad bin Muhammad Bin Sa’id Hamadani ambaye alikufa 303 A.H.

Alikuwa mmoja wa maulamaa wenu wakubwa. Wanachuoni mashuhuri wa madhehebu yenu, kama Dhahabi na Yafi’i, wamemkubali na wakasema kwmba amejifunza hadithi 300,000 pamoja na vyanzo vyao, na kwamba alikuwa mchamungu mkubwa. Katika mkusanyiko wa hadhara katika mji wa Kufa na Baghdad katika karne ya tatu A.H., alisimulia kwa uwazi makosa ya Masheikh wawili (Abu Bakr na Umar). Kwa sababu hiyo watu wakamuita Rafizi na wakajizuia kunukuu hadithi kutoka kwake. Ibn Kathir Dhahabi na Yafi’i wanaandika kuhusu yeye: “Sheikh Ibn Iqda alikaa katika Msikiti wa Basra (Msikiti maarufu ulioko kati ya Baghdad na Kadhmain) na akasimulia kasoro na makosa ya Masheikh wawili (Abu Bakr na Umar) kwa watu. Kwa ajili hii hadithi zilizosimuliwa na yeye zimekataliwa.

Vinginevyo hakuna shaka ya yeye kwamba ni mtu mkweli na mchamungu.” Al-Khatib Baghdad vile vile alimsifia katika “Ta’rikh” yake lakini mwishoni akasema: “Kwa vile alielezea kasoro na makosa ya Masheikh wawili (Abu Bakr na Umar) yeye alikuwa ni Rafizi.” Hivyo watu nyie msiwe katika mawazo kwamba ni Mashi’a tu ambao wanafichua ukweli wa masuala haya. Maulamaa wenu wakubwa kama Imamu Ghazali na Ibn Iqda walizoea kuonyesha kasoro katika Masahaba wakubwa.

Rejea Kuhusu Kifo Cha Tabari

Katika kila zama ya historia kumekuwa na mifano ya maulamaa ambao wameteswa au kusumbuliwa kwa sababu ya kuongea au kuandika kwao ukweli. Kwa mfano yule mfasiri na mwanahistoria maarufu, Muhammad Ibn Jarir Tabari, ambaye alikuwa ni fahari ya maulamaa wenu, alikufa katika mwaka wa 310 A.H. mjini Baghdad.

Lakini kwa sababu utawala uliogopa machafuko ya raia, walikataa jeneza lake kutolewa mchana. Alizikwa kwa lazima wakati wa usiku ndani ya nyumba yake mwenyewe.

Kuuwawa Kwa Nasa’i

Mfano mwingine wa mateso ulikuwa ni kuuawa kwa Imamu Abdu’r-Rahman Ahmad Ibn Ali Nasa’i. Alikwa ni mtu wa heshima na anachukuliwa kama mmoja wa Maimamu wa Sahih Sitta (vitabu sahihi sita). Anatokana na maulamaa wenye vyeo vikubwa wa madhehebu yenu katika karne ya tatu A.H. Wakati alipofika Damascus katika mwaka wa 303

A.H., aliona kwamba, kwa sababu ya Bani Umayya, wakazi wa sehemu ile walikuwa wakilikashifu jina la Amiru’l-Mu’minin Ali Bin Talib kwa uwazi kabisa baada ya kila salat ya faradhi, hususan katika hotuba za salat za jamaa. Alisikitishwa sana kwa kuiona hali hii na aliamua kukusanya hadithi zote za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zenye kumsifia Amirru’l-Mu’minin pamoja na nyororo za vyanzo vyao, zote zile ambazo alizikumbuka.

Kutokana nazo hizo, aliandika kitabu, “Khasa’isu’l-Alawi,” katika kutetea cheo kitukufu na sifa bora za Ali. Alikuwa kila mara akiwasomea watu kutoka juu ya mimbari, hadith kutoka kwenye kitabu chake, zenye sifa za Mtukufu Imam Ali.

Siku moja wakati alipokuwa anasimulia sifa za hali ya juu za Ali, kundi la wafanya vurugu lilimburuza kutoka kwenye mimbari na kumpiga sana.

Walimpiga mateke kwenye korodani zake na kukamata kwa nguvu uume wake, wakamburuza nje ya Msikiti na wakamtupa mtaani kwenye barabara. Kwa matokeo ya majereha haya alikufa baada ya siku chache. Mwili wake ulichukuliwa ukapelekwa Makka ambako alizikwa. Matukio haya ni matokeo ya uadui na ujinga.

Sasa naomba msamaha kwamba nimesukumwa nje mbali kidogo kuto- ka kwenye nukta yangu. Nilichomaanisha ni kwamba nafasi ya Wilayat (Umakamu) wa Amiru’l-Mu’minin haikuandikwa na maulamaa wa ki-Shi’a peke yao tu. Maulamaa wenu mashuhuri vile vile wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mbele ya watu 70,000 au 120,000, alinyanyua mkono wa Ali na akamtambulisha kama Imamu (Kiongozi na mlezi) wa watu.

Mashaka Ya Sunni Kuhusu Maana Ya Maula

Hafidh: Hakika hukuna shaka kuhusu tukio hili na matini ya hadithi hii, lakini wakati huo huo haina umuhimu ambao ufasaha wako wa hisia unaonesha. Mbali na hili, kuna baadhi ya mashaka kuhusiana na matini ya hadithi hii. Kwa mfano neno maula, umetuambia kwamba lina maana: “Mtu ambaye ana mamlaka makubwa juu ya wengine”, ingawa inajulikana kwamba katika hadithi hii maula maana yake “mpenzi, msaidizi na rafiki.”

Mtume alijua kwamba Ali alikuwa na maadui wengi na hivyo alitaka kuwashauri watu kwamba yeyeyote yule ambaye alimpenda au alikuwa rafiki au msaidizi wake, Ali vile vile alimpenda na alikuwa rafiki yake na msaidizi wake.

Sababu iliyomfanya atake kiapo cha utii kwa watu ilikuwa kwamba hakutaka wao wamsabibishie Ali matatizo.

Muombezi: Nafikiri wakati mwingine bila sababu unachukuwa tabia ya viongozi wako waliokutangulia. Kama utaufikiria ukweli huu kwa makini, ukweli wa suala hili utakuwa wazi.

Hafidhi: Ni mambo gani yanayothibitisha maoni yako? Tafadhali tujulishe.

Maana Ya Maula Kama “Kiongozi” “Bwana” Kutokana Na Aya Ya - Ya Ayyuha’r-Rasul Baligh.

Muombezi: Ushahidi wa kwanza ni Qur’ani Tukufu na uteremshwaji wa aya: “Ewe Mtume! Fikisha uliyoteremshiwa kutoka kwa Mola wako. Na ikiwa hukufanya hayo basi hukufikisha ujumbe wake. Na Allah atakulinda na watu…” (5:67)

Hafidh: Utadai vipi kwamba aya hii iliteremshwa siku hiyo na kwa madhumuni haya? Muombezi: Maulamaa wenu wote wanaoheshimika wameikubali: Jalalu’d-Din Suyuti: “Durru’l-Mansur;” Jz. 2, uk. 298; Hafidh Ibn Abi Hatim Razi: “Tafsir-e-Ghadir”; Hafidh Abu Ja’far Tabari: “Kitabu’l-Wilaya”; Hafidh Abu Abu Abdullah Mahamili: “Amali”; Hafidh Abu Bakr Shirazi: “Ma Nazala mina’l-Qur’an Fi Amiri’l-Mu’minin”; Hafidh Abu Sa’id Sijistani: “Kitabu’l-Wilaya”; Hafidh Ibn Mardawiyya: “Tafsir-e-Ayah”; Hafidh Abul- Qasim Haskani: “Shawahidu’t-Tanzil”; Abu’l-Fatha Nazari:“Khasa’isu’l-Alawi”; Mu’inu’d- Din Meibudi: “Sharh-e-Diwan”; Kadhi Shekani: “Fathu’l-Ghadir”; Jz. 3, uk. 57; Sayyid Jamalu’d-Din Shirazi: “Arba’in”; Badru’d-Din Hanafi: “Umdatu’l-Qari Fi Sharh-e-Sahih Bukhari”, Jz. 8, uk. 584; Ahmad Tha’labi: “Tafsir Kashfu’l-Bayan”; Imamu Fakhru’d-Din Razi: “Tafsir-e-Kabir”, Jz. 3, uk. 636; Hafidh Abu Nu’aim Ispahani: “Ma nazala mina’l-Qur’ani Fi Ali; Ibrahim bin Muhammad Hamwaini: “Fara’idu’s-Simtain”; Nizamu’d-Din Nishapuri, Tafsir, Jz. 6, uk. 170; Sayyid Shahabud-Din Alusi Baghdadi: “Ruhu’l-Ma’ani, Jz. 2, uk. 348; Nuru’d-Din Bin Sabbagh Maliki: “Fusulu’l-Muhimma”, uk. 27; Ali Bin Ahmad Wahidi: “Asbabu’n-Nuzul”, uk. 150; Muhammad Bin Talha Shafi’i: “Matalibu’s-Su’ul”, uk. 16; Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i: Mawadda ya 5 kutoka “Mawaddatu’l-Qurba”; Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi: “Yanabiu’l-Mawadda”, sura ya 39. Kwa ufupi, kwa kadiri ninavyojua mimi, maulamaa wenu mashuhuri thalathini wameandika katika vitabu vyao sahihi na katika sharhe zao kwamba aya hii tukufu iliteremshwa siku ya Ghadir-e-Khum kumhusu Amiru’l-Mu’minin Ali.

Hata Kadhi Fazl Bin Ruzbahan, pamoja na uadui wake na ushabiki, anaandika: “Hakika imethibitishwa katika vitabu vyetu sahihi kwamba wakati aya hii ilipoteremshwa, Mtume wa Allah akiwa ameushika mkono wa Ali alisema: ‘Kwa yeyote yule ambaye mimi ni maula (bwana) wake, huyu Ali vile vile ni maula wake.’”

Hata hivyo, inashangaza kwamba Kadhi huyu huyu mpotofu katika “Kashf Ghumma” ana- toa taarifa ya ajabu kutoka kwa Razi Bin Abdullah: “Wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tulizoea kusoma aya hii hivi: ‘Ewe Mtume wetu (Muhammad) fikisha yale uliy- oteremshiwa kutoka kwa Mola wako, yaani kwamba Ali ni bwana wa waumini. Kama hutafanya, basi utakuwa hukufikisha ujumbe wake.’”

Vile vile Suyuti katika Durru’l-Mansur kutoka kwa Ibn Mardawiyya, Ibn Asakir na Ibn Abi Hatim kutoka kwa Abu Sa’id Khudiri, Abdullah Ibn Mas’ud (mmoja wa waandishi wa Wahyi) na Kadhi Shukani katika Tafsir-e-Fathu’l-Ghadir wanasimulia kwamba wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wao vile vile walisoma aya hiyo katika njia hiyo hiyo.

Kwa ufupi hili onyo lililomo katika aya hii linasema: “Kama hukufanya basi utakuwa hukufikisha ujumbe (kabisa)…” huonesha kwamba ujumbe ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliamriwa kuutoa ulikuwa wa umuhimu mkubwa sana.

Kwa hakika ulikuwa ni muhimu kwa ukamilifu wa utume wenyewe. Kwa hiyo, kwa hakika suala katika mjadala lilikuwa habari ya uimamu, utunukiaji wa mamlaka juu ya mtu ambaye angewaongoza watu kwa mujibu wa mafundisho ya Uislamu baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kushuka Kwa Aya “Siku Ya Leo Nimekukamil- Ishieni Dini Yenu”

Pale Ghadir-E-Khum

Mazingira ya pili ambayo yanathibitisha nukta yangu ni kule kushuka kwa aya:

{اﻟْﻴﻮم اﻛﻤﻠْﺖ ﻟَﻢ دِﻳﻨَﻢ واﺗْﻤﻤﺖ ﻋﻠَﻴﻢ ﻧﻌﻤﺘ ورﺿﻴﺖ ﻟَﻢ اﺳَم دِﻳﻨًﺎ ۚ{3

“Siku ya leo nimekukamilishieni dini yenu na kukutimizieni neema yangu kwenu na kuwachagulieni Uislamu kuwa ndio dini yenu.” (5:3)

Hafidh: Lakini ni jambo linalokubalika kwamba aya hii iliteremshwa siku ya Arafa, na hakuna hata mmoja katika maulamaa aliyedai kwamba aya hii iliteremshwa siku ya Ghadir.

Muombezi: Nakuomba usifanye haraka isiyo na maana katika kuukataa ukweli huu. Kama mambo yalivyo, nakubali kwamba baadhi ya maulamaa wenu wamesema kwamba aya hii iliteremshwa siku ya Arafa, lakini idadi kubwa ya ulamaa wenu waheshimika vile vile wamesema kwamba iliteremshwa siku ya Ghadir.

Vile vile baadhi ya ulamaa wenu wana maoni ya kwamba pengine aya hii iliteremshwa mara mbili, mara ya kwanza pale mwishoni mwa siku ya Arafa na tena siku ya Ghadir.

Kwa hiyo, Sibt Ibn Jauzi anasema katika Khawasu’l-Umma, uk. 18: “Inawezekana kwamba aya hii iliteremshwa mara mbili, mara ya kwanza katika siku ya Arafa na mara nyingine katika siku ya Ghadir- e-Khum, kama vile aya ya: ‘Kwa jina la Allah Mwingi wa rehema Mwenye kurehemu, ilivyoteremshwa mara mbili, mara ya kwanza mjini Makka na mara nyingine tena mjini Madina.”

Wanachuoni wenu wakuaminika, kama Jalalu’d-Din Suyuti katika “Durru’l-Mansur,” Jz. 2, uk. 256 na Itqan, Jz. 1, uk. 31; Imamu ‘l-Mufassirin Tha’labi katika “Kashfu’l-Bayan”; Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika “Ma Nuzala Mina’l-Qur’ani Fi Ali”; Abu’l-Fatha Nazari katika “Khasa’isu’l-Alawi”; Ibn Kathir Shami katika “Tafsir” Jz. 2, uk. 41 akimfu- ata Hafidh Ibn Mardawiyya: Muhammad Bin Jarir Tabari, Mwanachuo, mfasiri na mwanahistoria wa karne ya tatu A.H. katika “Tafsir-e-Kitabu’l-Wilaya”; Hafidh Abul’l- Qasim Haskani katika Shawahid-ut-Tanzil; Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira-e-Khawasu’l- Umma uk. 18; Abu Ishaq Hamwaini katika “Fara’idus-Simtain” sura ya 12; Abu Sa’id Sijistani katika “Kitabu’l-Wilaya”; Al-Khatib-e-Baghdadi katika “Ta’rikh-e-Baghdad, Jz. 8, uk. 290; Ibn Maghazili Faqih Shafi’i katika “Manaqib”, sura ya 14 na Maqtalu’l-Husain, sura ya 4, wote wameandika kwamba katika siku ya Ghadir-e-Khum Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteuwa Ali kwa amri ya Mungu kwenye cheo cha Wilaya (Makamu).

Aliwaeleza watu kila kile ambacho aliamriwa kukisema kuhusu Ali na akainua mikono yake juu kiasi kwamba weupe wa makwapa yake ulionekana. Aliwahutubia watu hivi: “Mpongezeni Ali kwa sababu ni Amir wa waumini. Jumuiya yote ilitekeleza amri hii. Walikuwa hawajaachana kila mmoja kuchukua njia yake wakati aya iliyotajwa hapo juu iliposhuka.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifurahishwa mno kwa kuteremshwa aya hii. Hivyo, wakati akiwahutubia watu alisema: “Allah ni Mkubwa, Ambaye ameikamilisha dini kwa ajili yao na amekamilisha neema Zake kwao na ameridhishwa na Utume wangu na umakamu wa Ali baada yangu.”

Imamu Haskani na Imamu Ahmad Bin Hanbal wametoa maelezo kamili ya tukio hili. Kama ninyi, waheshimiwa, mngeacha mawazo yenu yaliyojipandikiza juu ya suala hili, mtaweza kuzielewa aya tukufu na hadith, ambazo huonesha kwamba neno “Maula” maana yake walii (bwana) yaani, mtu aliye na mamlaka juu ya wengine wote.

Kama maula au wali haikumaanisha mtu ambaye ana mamlaka makubwa juu ya wengine, neno liliofuatia “baada yangu” lingekuwa halina maana. Na maneno haya ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyarudia rudia kuyasema kutoka kwenye ulimi wake mtuku- fu, yanathibitisha kwamba maula na wali humaanisha “mtu ambaye ana mamlaka makubwa juu ya wengine wote”, kwa sababu alisema kwamba cheo kile haswa kilitolewa kwa Ali baada yake.

Tatu, unaweza kuyaangalia yale mazingira. Katika jangwa lile lenye joto, ambako kulikuwa hakuna hifadhi kwa ajili ya wasafiri, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akakusanya umma wote. Watu walikaa kwenye vivuli vya ngamia, miguu yao ikiwa imefunikwa, katika joto kali linalochoma la jua. Katika hali hii Mtume alitoa hotuba ndefu, ambayo Khawarizmi na Ibn Mardawiyya katika “Manaqib” zao na Tabari katika “Kitabu’l-Wilaya” na wengine wameisimulia.

Je, inaleta maana kufikiria kwamba Mtume angetaka maelfu ya wafuasi wake kukaa siku tatu katika jangwa linalochoma kwa ajili ya kula kiapo kwa Ali kuonesha tu kwamba Ali alikuwa rafiki yao? Kwa hakika hakukuwa na mtu hata mmoja katika jumuiya yote ambaye alikuwa bado haujui ule uhusiano wa karibu kati ya Mtume na Ali au hajasikia kuhusu habari zake (kama nilivyokwishaeleza mapema).

Kuteremshwa kwa aya ya Qur’ani iliyoko kwenye mjadala kwa mara ya pili, hususan katika mazingara tofauti pamoja na maelekezo hayo makali kwamba watu wangeweza kuwekwa kwenye takilifu kubwa na mashaka, isingeweza kuwa na maana tu kwamba lazima wao wawe marafiki wa Ali.

Itakuwa utekelezaji huu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ama ulikusudiwa kuonesha umuhimu mkubwa sana, au ulikuwa ni upuuzi. Na hakika Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yuko mbali na matendo yote ya kipuuzi.

Kwa hiyo ni jambo la busara kuhitimisha kwamba, matayarisho haya hayakufanywa hivi hivi kwa ajili ya kuelekeza tu kwamba watu lazima wafanye urafiki na Ali. Kwa hakika tukio hili linaashiria kukamilika kwa ujumbe wa Mtume: kuthibitishwa kwa Uimamu, chanzo cha mwongozo wa umma baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Maoni Ya Sibt Ibn Jauzi Kuhusu Maana Ya Neno Maula

Baadhi ya ulamaa wenu mashuhuri wasifika wamikiri kwamba maana ya msingi ya neno Maula ni “bwana.” Miongoni mwao ni Sibt ibn Jauzi, ambaye baada ya kutoa maana kumi za neno hilo katika kitabu chake Tadhkiratul-Khawas, Sura ya 2, uk. 20, anasema kwamba kati ya zote hizo, ile maana ya kumi ndio inayoendana na kile alichokimaanisha Mtukufu Mtume kukisema.

Yeye anasema: “Hadithi hii inamaanisha haswa utii; hivyo hii maana ya kumi ndio iliyo sahihi, na yenyewe ina maana ya ‘bwana mwenye mamlaka juu ya wengine.’ Kwa hiyo hadithi hii ina maana ya yeyote yule ambaye mimi ni bwana (maula) kwake, Ali pia ni bwana (maula) kwake.’”

Katika kitabu cha Marajul-Bahrein Hafidh Abul-Faraj Yahya bin Sa’id Saqafi anaitafsiri kwa maana kama hiyo hiyo. Yeye anasimulia hadithi hii kwa vyanzo vyake kutoka kwa viongozi wake, ambao wamesema kwamba, Mtukufu Mtume, akiwa amemshika Ali mkononi alisema:

“Yeyote yule ambaye mimi ni bwana (Maula) juu ya nafsi yake, Ali naye pia ni bwana (Maula) juu ya nafsi yake.” Sibt ibn Jauzi anasema, “Hadith ya Mtukufu Mtume inayosema kwamba Ali anayo mamlaka au ni bwana juu ya nafsi za waumini wengine inathibitisha wazi Uimam au Umakamu wa Ali na kwamba utiifu kwake yeye ni wajibu.”

Maoni Ya Ibn Talha Shafi’i Kuhusu Maana Ya Neno Maula

Muhammad Bin Talha Shafi’i katika “Matalibus-Su’ul” katikati ya sehemu ya 5, sura ya 1, uk. 16, anasema kwamba neno maula lina maana nyingi, kwa mfano: “bwana”, “msaidizi”, “mrithi”, “muaminifu”, na kiongozi”. Kisha anasema kwamba hadithi hii tukufu inaitolea tafsri ya ndani aya ya Mubahila, (3:61). Ndani yake Allah (swt) amemuita Ali ‘nafsi’ ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kulikuwa hakuna utenganisho kati ya nafsi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na nafsi ya Ali kwa vile amezichanganya mbili hizi kwa kijina kiashiri- acho kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Muhammad Bin Talha anaongeza: “Katika hadithi hii Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anaonesha kwamba wajibu wowote walionao waumini kumhusu yeye, wanao wajibu huo vile vile kumhusu Ali. Kwa vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni hakika alikuwa bwana wa waumini katika mambo yao yote, msaidizi wao, kiongozi, na mtawala – yote haya yakiwa vidoke- zo vya neno maula – basi ina maana kwamba alimaanisha kitu hicho hicho kwa Ali (as).

Na hii kwa hakika ni nafasi ya juu sana, cheo kitukufu mno, ambacho kilitolewa maalumu kwa Ali. Ni kwa sababu hii kwamba Siku ya Ghadir Khum ilikuwa ni siku ya idd (siku kuu) shangwe kwa ajili ya wapenzi na marafiki wa Ali.”

Hafidh: Kwa mujibu wa maelezo yako, kwa vile neno maula lina maana nyingi, itakuwa ni makosa kuamua kwamba lilitumika katika suala hili kuonesha maana moja “bwana”, na kuziweka kando hizo maana nyingine.

Muombezi: Unatambua vema kanuni za msingi za wanachuoni kwamba wakati ambapo neno linaweza kuwa na maana nyingi tofauti, linakuwa na maana moja tu ya msingi na kwamba maana nyingine zinakuwa ni vinyambulika.

Kwa mfano, walii wa nikah (ndoa) maana yake mtu anayesimama kama wakili, au mdhamini. Walii wa mwanamke ni mume wake, walii wa mtoto ni baba yake ambaye ana mamlaka kamili juu yake. Wali ahd (mrithi mstahiki) wa mfalme maana yake “mtu ambaye haki yake ya kutawala haiwezi kukataliwa kama ataishi baada ya baba yake.”

Mbali na hili pingamizi lako linakurudia wewe, juu ya ni kwa nini umeweka mpaka kwenye maana yake “rafiki” na “msaidizi” wakati lina maana nyingine nyingi.

Hivyo hili uainishaji huu bila ya lengo maalumu ni batili. Pingamizi ulilofanya linakurudia wewe mwenyewe na sio kwetu kwa sababu maana ambazo tumezibainisha hazikukosa kuwa na lengo maalum lililoainishwa.

Aya za Qur’ani Tukufu, hadith, na maoni ya wanachuoni, vyote vinathibitisha maana hiyo hiyo tuliyoitoa. Miongoni mwa hizi ni zile sababu ambazo maulamaa wenu wakubwa, kama Sibt Ibn Jauzi, Muhammad Ibn Abi Talha Shafi’i wamezitoa kuhusiana na maana yake.

Aidha, imesimuliwa kwa idadi kubwa ya hadithi kutoka kwenye vyanzo vyenu na vyangu kwamba aya hii tukufu ilikuwa inasomwa hivi kimaana: “Ewe Mtume wa Allah! Fikisha kile ambacho kimeteremshwa kwako kutoka kwa Mola wako kuhusu wilaya ya Ali (umakamu) na kuwa kwake bwana wa waumini.”

Jalalu’d-Din Suyuti, ambaye ni mmoja wa maulamaa wenu mashuhuri amekusanya hadithi hizi kwenye kitabu chake, “Durru’l-Mansur”.

Hoja Aliyoitoa Ali Ndani Ya Msikiti Wa Kufa Iliyoko Juu Ya Msingi Wa

Hadith Ya Ghadir

Kama hadith hii na neno maula havikuwa uthibitisho wa Ali kama Imamu na Khalifa, Amirul-Mu’minin asingerudia mara kwa mara kuhoji kutokana nayo. Kwa hakika katika mikutano ya kamati za washauri alizirejea kama ushahidi wa Uimamu wake, kama walivyoandika: Khatib Khawarizmi katika “Manaqib” yake uk. 217; Ibrahim Ibn Muhammad Hamwaini katika “Fara’id” sura ya 58; Hafidh Ibn Iqda katika “Kitabu’l- Wilaya”; Ibn Hatim Damishqi katika “Durru’n-Nazim”, na Ibn Abi’l-Hadid katika “Sharhe-e- Nahju’l-Balagha, Jz. 2, uk. 61. Cha umuhimu haswa ni ule ushahidi uliotolewa na masahaba thelathini kule Rahba. Maulamaa wenu mashuhuri wamesimulia majadiliano aliyoyafanya Ali pamoja na Waislamu kule Rahba-e-Kufa (yaani, katika uwanja wa msikiti wa Kufa). Ifuatayo ni sehemu ya orodha ya wale ambao wameandika tukio hili:

Imam Ahmad Hanbal katika “Musnad” yake sehmu ya 1, uk. 129; Ibn Athir Jazari katika “Asadu’l- Ghiba,” Jz. 3, na Jz. 5, uk. 206 na 276; Ibn Qutayba katika “Ma’arif” uk. 194; Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’l-Talib”; Ibn Abi’l-Hadid katika “Sharh-e-Nahju’l-Balagha”, Jz. 1, uk. 362; Hafidh Abu Nu’aim Isfahani katika “Hilyatu’l- Auliya, Jz. 5, uk. 26; Ibn Hajar Asqalani katika “Isaba,” Jz. 2, uk. 408; Muhbu’d-Din Tabari katika “Dhakh’ir-e-Uqba”, uk. 67; Imamu Abdur-Rahman Nisa’i katika “Khasa’isu’l-Alawi”, uk. 26; Allama Samhudi Katika “Jawahiru’l-Iqdain”; Shamsu’d-Din Jazari katika “Asnu’l-Matalib”, uk, 3; Sulaimani Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l- Mawadda, sura 4; Hafidh Ibn Iqda katika “Kitabu’l-Wilaya. Ali alisimama mbele ya watu na akawataka kutoa ushahidi kuhusu kile walichosikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kuhusu yeye pale Ghadir-e-Khum.

Mashaba thelathini, pamoja na watu wa Badir kumi na mbili (wale ambao wamepigana katika vita ya Badr), walisimama na wakasema kwamba waliona katika Siku ya Ghadir-e-Khum Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiushika mkono wa Ali akiwaambia watu: “Je, mnajua kwamba ninayo mamlaka makubwa juu ya waumini kuliko waliyonayo katika nasi zao wenyewe?” wote wakasema:

“Ndio.” Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Kwa yeyote yule ambaye mimi ni maula wake (mwenye kumtawalia mambo yake), basi huyu Ali ni maula wake (mwenye kumtawalia mambo yake).”

Hali Ya Huzuni Kwa Wale Ambao Hawakuthibitisha Hadith Ya Ghadir

Watu watatu kutoka katika mkusanyiko huu hawakutoa ushahidi wa tukio hili. Mmoja wao alikuwa Anas Bin Malik, ambaye alisema kwamba amedhoofika kwa uzee amesahau mambo yote kuhusu tukio hilo. Ali aliwalaani watu wale watatu.

Alisema: “Kama mnasema uwongo, Allah akupeni ukoma, ambao hata vilemba vyenu havitaweza kuuficha.” Haukupita muda Anas aliposimama kutoka sehemu aliyokuwa amekaa ukoma ukatokea mwilini mwake. (kwa mujibu wa baadhi ya taarifa alipatwa na upofu na ukoma pamoja).

Hoja Ya Nne: “Je, Mimi Sina Mamlka Makubwa Juu Yenu Kuliko Mliyo

Nayo Kwenu Wenyewe?”

Muombezi: Nne, njia ambayo hadithi hii imesimuliwa yenyewe inaonesha kwamba neno maula maana yake ni “bwana”. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika hotuba yake kule Ghadir, aliwauliza watu: Je mimi sina mamlaka makubwa juu yenu kuliko mliyonayo kwenu wenyewe?”

Hii inarejea kwenye yale maneno ya Qur’ani Tukufu: “Mtume ana mamlaka makubwa juu ya waumini kuliko waliyo nayo juu yao wenyewe.” (33:6) Aidha, kuna hadithi ya kutengemewa katika vitabu vya madhehebu zote ambayo inansmu- lia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakuna muumini ambaye kwamba sina mamlaka makubwa juu yake katika ulimwengu huu na katika Akhera, kuliko aliyonayo mwenyewe.” Wote wakajibu kwa sauti moja kwamba ana mamlaka makubwa juu yao kuliko waliyonayo wao wenyewe.

Baada ya hapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Yule ambaye mimi ni mawla (namtawalia mambo yake) huyu Ali ni mawla wake (mwenye kumtawalia mambo yake). Hivyo kutokana na muktadha wa hadithi hii hufuatia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimaanisha “mamlaka” au “ubwana juu ya wengine” wakati alipotumia neno maula.

Hafidh: Katika vitabu vingi hakuna kumbukumbu kama hiyo ya Mtume kuwa amewahi kusema maneno haya: Je, mimi sina mamlaka juu yenu kuliko mliyonayo juu yenu wenyewe?”

Muombezi: Katika kusimulia hadithi ya Ghadir, wasimuliaji wametumia maneno tofauti kidogo, lakini kadiri ya hadithi za Shi’a zinavyohusika, maulamaa wote wa ki-Shi’a wanasema kwamba matini na muktadha wa hadithi ya Ghadir ni kama ilivyosimuliwa hapo juu.

Na katika vitabu sahihi vingi vya Sunni, vilivyoandikwa na maulamaa wenu wakubwa, kama Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira-e-Khawasu’l-Umma” uk. 18; Imamu Ahmad bin Hanbal katika “Musnad” yake; Nuru’d-Din Sabagh Maliki katika “Fusulu’l-Muhimma”; na kundi la wengi wengine ambao wamesimulia hadithi ya Ghadir, maneno “Je, mimi sina mamlaka makubwa juu yenu kuliko mliyonayo wenyewe” hupatikana humo.

Sasa kwa ajili ya baraka nawasilisha hapa Tarjuma ya hadihti hii ambayo imesimuliwa na Imamu Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, Jz. 4, uk. 281, kutoka kwa Bara’a Bin Azib. Yeye alisema: Nilikuwa nasafiri na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tulifika Ghadir. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akatangaza: ‘Kusanyikeni kwa ajili ya Sala.’ Ilikuwa ni kawai- da kama kulikuwa na kitu muhimu ambacho kilikuwa kitokee punde, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaamuru watu kukusanyika kwa ajili ya Sala.

Wakati watu wakiwa wamekwishakutanika na Sala imekwisha kutekelezwa, Mtume alizoea kutoa hotuba. Sehemu maalumu ilitayarishwa kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kati kati ya miti miwili. Baada ya kumalizika kwa Sala Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiwa amenyanyua mkono wa Ali juu kupita kichwa chake, alizungumza na watu waliokusanyika pale:

‘Je, mnajua kwamba mimi ni bwana wa waumini na nina haki zaidi juu ya kuliko waliyo nayo wao wenyewe juu ya nafsi zao.’ Wote wakasema, ‘Ndio, tunajua hivyo.’ Alisema tena, ‘Je, mnajua kwamba nina haki zaidi juu ya klia muumini kuliko aliyo kuwa nayo yeye mwenyewe?’ Wote wakajibu, ‘Ndio tunalijua hilo.’ Baada ya hapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema, ‘Yeyote yule ambaye mimi ni maula wake (mwenye kumtawalia mambo yake) huyu Ali ni maula wake (mwenye kumtawalia mambo yake).’ Kisha akamuomba Allah: ‘Ewe Allah! Kuwa rafiki kwa yule ambaye ni rafiki kwake (yaani, Ali) na kuwa adui kwa yule ambaye ni adui kwake.’

Mara tu kufuatia hili, Umar Bin Khattab alikutana na Ali na akasema, ‘Hongera, Ewe mwana wa Abu Talib! Sasa umekuwa maula wa waumini wote wanaume na wanawake.’”

Vile vile Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i katika “Mawaddatu’l-Qurba” Mawadda ya 5; Sulaimani Balkhi katika “Yanabiu’l-Mawadda” na Hafidhi Abu Nu’aim katika kitabu chake “Hilya” wameandika hadithi hii pamoja na tofauti kidogo katika maneno.

Hafidhi Abu’l-Fatha, ambaye kutoka kwake Ibn Sabbagh vile vile amenukuu katika kitabu chake Fusulu’l-Muhimma, amesimulia hadithi hii katika maneno haya: “Enyi watu! Allah Swt ni Maula wangu, nami ninayo mamlaka makubwa juu yenu kuliko mliyonayo juu yenu wenyewe. Inakupaseni mfahamu kwamba yeyote yule ambaye mimi ni maula kwake na huyu Ali vile vile ni maula wake.”

Ibn Maja Qazwini kaika “Sunan” yake na Imamu Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i katika kitabu chake “Ahadith” (uk. 81, 83, 93, 24) wameisimulia hadithi hii kwa namna hiyo hiyo. Na Zaid Ibn Arqam anaandika katika hadithi yake Na. 84 kwamba Mtume wa Allah alisema katika hotuba yake: “Je, mnajua kwamba ninayo mamlaka makubwa juu ya waumini wote, wanaume na wanawake, kuliko waliyonayo wao wenyewe?”

Wote wakasema: “Tunashuhudia kwamba unayo mamlaka makuu juu ya kila muumini kuliko aliyonayo yeye mwenyewe.” Katika wakati huo Mtume akasema: “ Kwa yeyote yule ambaye mimi ni maula (bwana) kwake huyu Ali vile vile ni maula (bwana) wake.” Kisha akaunyoosha mkono wa Ali. Kwa nyongeza Abu Bakr Ahmad Bin Al-Khatib Baghdadi (amekufa 462 A.H.), katika kitabu chake “Ta’rikh-e- Baghdad, Jz,. 8, uk. 289, 290, amesimulia hadithi ndefu kutoka kwa Abu Huraira kwamba kama mtu yeyote atafun- ga siku ya mwezi 8 Dhu’l-Hijja (Siku ya Ghadir), atalipwa malipo ya funga ya miezi sita. Kisha hapo akaindika hadithi hiyo hapo juu katika njia hiyo hiyo.

Mashairi Ya Hasan Mbele Ya Mtukufu Mtume

Mazingira ya tano kuthibitisha wilaya (umakamu) ya Ali ni usomaji wa mashairi ambayo Hasan Bin Thabit aliyasoma kwa ruhusa ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), katika mkusanyiko wa watu ambapo cheo cha Ali cha umakamu kilitajwa. Sibt Ibn Jauzi na wengine wameandika kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliposikia beti hizo, alisema: “Ewe Hasan! Kadiri unavyoendelea kutusaidia au kutusifia sisi kwa ulimi wako, basi ruhul-quds yule roho tukufu naye vile vile atakuwa anakusaidia wewe.”

Mfasiri mashuhuri na msimuliaji wa hadithi wa karne ya nne A.H., Hafidh Ibn Mardawiyya (amekufa 352 A.H.), katika “manaqib” yake; mkuu wa Mimamu, Muwaffaq Bin Ahmad Khawarizmi katika “Manaqib” yake na “Maqtalu’l-Husain,” sehemu ya 4; Jalalu’d-Din Suyuti katika “Risalatu’l-Azhar fi ma Aqdahu’sh- Shu’ara” na wengi katika wanachuoni wenu, wasimuliaji wa hadithi, na wanahistoria wanasimulia kutoka kwa Abu Sa’id Khudri kwamba katika Siku ya Ghadir-e-Khum, baada ya hotuba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na uteuzi wa Ali kama mrithi wake, Hasan Bin Thabit alisema: “Je, unaniruhusu nisome mashairi juu ya tukio hili?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema:

“Ndio, soma pamoja na baraka za Allah.” Hivyo alisimama sehemu iliyonyanyuka kidogo na akasoma kwa mfululizo beti zilizotungwa.maana ya beti hizo ni kama ifuatavyo:

“Katika Siku ya Ghadir-e-Khum Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwakusanya watu pamoja, na niliisikia sauti yake ikiwaita. Mtume akawambia, ‘Ni nani maula wenu na walii?’ Watu wakasema kwa uwazi, ‘Allah ni Maula wetu na wewe ni walii (mlinzi) wetu na hakuna anayekataa ukweli huu.’ Hivyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuambia Ali: “Simama! Ninaridhika na wewe kuwa imamu (makamu) na hadi (mlezi) baada yangu.

Hivyo yeyote yule ambaye mimi ni maula wake huyu Ali vile vile ni maula wake. Kwa hiyo, ninyi watu wote lazima muwe watiifu na waminifu katika kumsaidia yeye.’ Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaomba kwa Allah: ‘Ewe Allah! Kuwa rafiki kwa yule ambaye ni rafiki kwake (Ali) na kuwa adui kwa yule ambaye ni adui kwake.’”

Mashairi haya ni ushahidi wa wazi kwamba siku ile masahaba wa Mtume hawakulitafsiri neno maula katika njia nyingine yoyote isipokuwa ya Imamu na kwamba Ali atakuwa Khalifa baada ya Mtume kufariki.

Kama neno maula halikuwa na maana ya Imamu au bwana juu ya wengine, basi Mtume mara moja angelimkatiza Hasan wakati anasoma ubeti, “Ninaridhika na wewe kuwa Imamu na mlezi baada yangu”, na angemuambia kwamba amekosea na kwamba hakuwa na maana kwamba Ali atakuwa Imamu na mrithi baada yangu, na kwamba kwa neno maula alimaanisha “rafiki” au “msadizi”.

Lakini kwa kweli Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuunga mkona kwa kusema, “Ruhu’l-Qudus naye vile vile atakusaidia.” Mbali na hili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa uwazi alielezea nafasi ya uima- mu au wilaya (umakamu) wa Ali katika hotuba yake.

Inakubidi uichunguze hotuba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyoitoa kaita Siku ya Ghadir-e-Khum na ambayo imeandikwa kwa ukamilifu na Abu Ja’far Muhammad Ibn Jarir Tabari (amekufa 310 A.H.) katika kitabu chake “Kitabu’l-Wilaya”.

Anaandika kwamba Mtume alisema: “Sikilizeni na mtii. Hakika, Allah swt ni Maula wenu na Ali ni imamu wenu. Mpaka Siku ya Hukumu uimamu utabakia kwenye familia yangu, kizazi cha Ali.”

Masahaba Wavunja Ahadi Yao Waliyoweka Siku Ya Ghadir

Maana yoyote mtakayoitoa kwa neno maula, ni ukweli unaokubalika kwamba Masahaba waliweka ahadi kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika siku ile. Kuna kupatana kabisa kati ya madhehebu hizi mbili juu ya nukta hii. Basi kwa nini walivunja ahadi hiyo? Hata tukichukulia tu kwa muda huu kwamba kwa kusema maula Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimaanisha “rafiki” au “msaidizi” tu, kwa kumuogopa Allah hebu tuambieni kama mnafikiri kwamba urafiki ule ulimaanisha kwamba waje wachome moto nyumba ya Ali, kuitishia familia yake, na na kumtishia yeye kwa panga zilizochomolewa!

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitoa maelekezo ya wazi kwamba Masahaba lazima wale kiapo cha utii kwa Ali. Unafikiria kwamba alikusudia kwamba wao kwa hiyo waje wamtese mkwe wake mwenyewe? Baada ya kifo cha Mtume, hawakuvunja kiapo chao? Je, wale waliovunja kiapo, kwa maoni yenu ninyi, hivi walitimiza masharti ya urafiki? Je, waliisoma aya 25 sura ya 13, Al-Ra’d (Radi) ya Qur’ani Tukufu? “Na wale wanaovunja ahadi za Allah baada ya kuzifunga, na wanakata yale ambayo kwamba Allah ameamrihsa yaungwe, na wanafanya ufisadi katika nchi; hao ndio watakaopata laana, na watapata makazi mabaya.” (13:25)

Masahaba Wavunja Ahadi Kule Uhud, Hunain, Na Hudaibiyya

Katika vita ya Uhud na Hunain, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipowafanya Masahaba wote waahidi kwamba siku hiyo hawatakimbia, je, sio hakika kwamba walikimbia? Walikimbia kutoka kwenye uwanja wa vita na wakamuacha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kukabiliana na adui. Hili limeandikwa na wanahistoria wenu wenyewe, kama Tabari, Ibn Abi’l-Hadid, na Ibn A’same Kufi. Je, huku sio kuvunja kiapo chenye uzito mkubwa?

Naapa kwa Allah kwamba mnawatoa makosa bure Mashi’a wakati tunaposema yale tu ambayo wanahistoria wenu mashuhuri wameyasema.

Mashi’a Wanawalaumu Masahaba Wale Tu Ambao Vitendo Vyao Havikuwa Vya Haki

Sielewi ni kwa nini ninyi watu mmekuwa mkitushambulia kwa karne nyingi. Mnachoandika chochote ninyi kinakubaliwa, lakini kama tukiandika yale ambayo maulamaa wakubwa wa Sunni waliyo andika, tunaitwa makafiri kwa sababu tu tunakosoa dhulma za baadhi ya Masahaba.

Hata hivyo, kama ukosoaji wa Masahaba humaanisha Urafidha, basi kwa dhahiri Msahaba wote walikuwa Marafidhi, kwa sababu wote kila mmoja alikosoa vitendo vibaya vya mwenziye. Hata Abu Bakr na Umar walifanya hivyo.

Baadhi ya Masahaba wa Mtume walikuwa waumini wachamungu na walikuwa waki- heshimiwa sana. Wengine waliendekeza matamanio yao machafu na walilaumiwa. Kama unataka ushahidi wa kihistoria wa ukweli huu, nashauri kwamba usome Sharh-e-Nahju’l- Balagha ya Abi’l-Hadid, Jz. 4, uk. 454, 462, na usome majibu ya marefu ya Zaid kwa ukinzani wa Abu’l-Ma’ali Juwaini, ambayo Abu Ja’far Naqib ameyaandika.

Hapo ndipo utakapojua ni kiasi cha migogoro ilyokuwepo miongoni mwa Masahaba, ambao kwa hakika walilaaniana wenyewe kwa wenyewe kama waovu na makafiri.

Kukimbia Kwa Masahaba Kule Hudaibiyya

Katika maelezo yake ya suala la Hudaibiyya, Ibn Abi’l-Hadid, katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha, na wengine miongoni mwa wanahistoria wenu vile vile wameandika kwamba, baada ya kukamilika kwa mkataba ule wa amani, Masahaba wengi akiwemo Umar Bin Khattab, walionesha kuchukia kwao kuhusiana na masharti ya mkataba.Walimueleza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba walikuwa hawakuridhika na mkataba wa amani na walitaka kupigana. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawaambia kama walitaka kupigana walikuwa wako huru kufanya hivyo. Hivyo walishambulia. Lakini Masahaba wakashindwa vibaya na wakakimbia milimani na hawa hata hawakurudi kumlinda Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ndipo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali achomoe upanga na kuwafukuza Makuraishi.

Walipomuona Ali mbele yao, Makuraishi walirudi nyuma. Baadae Masahaba waliokimbia walirudi na kuomba msamaha kwa Mtume.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawaambia: “Kwani mimi sikujueni ninyi! Nyie sio watu wale wale ambao walitetemeka kwa hofu katika vita vya Badir mpaka Allah swt akatuma malaika kwa ajili ya kutusaidia! Ninyi sio Masahaba wangu wale wale ambao katika Siku ya Uhud mlikimbia milimani na mkaniacha bila ulinzi? Ingawa niliendelea kuwaita, lakini ninyi hamkurudi.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawahesabia udhaifu wao wote, na waliendelea kuelezea masikitiko yao kwa ajili ya vitendo vyao. Ibn Abi’l-Hadid anasema mwishoni mwa kazi yake ya kuandika kwamba karipio hili lilielekezwa haswa dhidi ya Umar, ambaye hakuamini ahadi zozote zilizowekwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kisha anaandika kwamba, kwa mwanga wa maelezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Khalifa Umar lazima alikimbia kutoka kwenye vita ya Uhud kwa sababu katika mazungumzo yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alilitaja hilo pia.

Sasa mnaweza mkaona wenyewe kwamba kama tukielezea ukweli huu, ambao umeandikwa na maulamaa wenu wakubwa kama Abi’l-Hadid na wengine, mara moja tunalengwa kushambuliwa (eti) kwa sababu tumemtukana Khalifa, lakini hakuna kikwazo kwa Abi’l- Hadid. Kwa kweli hatuna nia ya kumtukana mtu yeyote. Sisi tunasimulia mambo ya kihistoria tu, na mnatuangalia kwa macho ya dharau. Mnayapuuza mambo hayo.

Mashi’a Watatafuta Fidia Ya Hali Ya Mambo Siku Ya Hukumu

Mashi’a watakuwa na malalamiko mengi Siku ya Hukumu dhidi ya Ulamaa wenu. Ulimwengu utatoweka, lakini lazima msimame mbele ya Mahakama Adilifu ya Allah kwa ajili ya kujibu uonevu wenu.

Hafidh: Tafadhali niambie ni kwa uonevu upi ambao mtatafuta haki Siku ya Hukumu?

Muombezi: Kuna mifano ambayo naweza kuionesha. Wakati Siku ya Hukumu Tukufu itakapowadia, kwa hakika nitaitafuta haki.

Hafidh: Nakuomba usichochee mihemuko ya (watu) wengine. Tuambie ni uonevu gani uliokupata.

Muombezi: Uonevu na dhulma sio jambo geni leo kwetu sisi. Lakini msingi wake ulijengwa mara tu baada ya kufariki kwa babu yetu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Haki ya bibi yetu mdhulumiwa, Fatima Zahra ambayo aliachiwa na baba yake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa ajili ya kuwalea watoto wake, iliporwa. Hakuna kujali kokote kulikofanywa kwa ajili ya malalamiko na upingaji wake wa dhati. Hatimaye alifariki katika ujana wake akiwa amevunjika moyo.

Hafidh: Tafadhali, unawachochea watu bila sababu yoyote. Tuambie ni haki gani ya Fatima iliyoporwa? Tafadhali kumbuka kwamba kama utashindwa kuthibitisha dai lako, kwa kiasi fulani utashindwa katika Mahakama Tukufu ya Haki. Jione uko katika Mahakama ya Mungu ya Uadilifu na utetee kesi yako.

Muombezi: Siku moja tutakuwa mbele ya Mahakama Tukufu. Tunategemea kupata haki. Kama wewe pia unayo hisia ya uadilifu, basi yakupasa kama hakimu muadilifu kusikiliza hoja yangu bila chuki. Naamini utakubali uhalali wa dai letu.

Hafidh: Naapa kwamba sina chuki au ukaidi. Hakika umeona katika mikesha hii kwamba sihoji kipumbavu. Wakati niliposikia hoja zenye mantiki nilizikubali.

Kunyamaza kwangu kwenyewe kulikuwa kunaonesha kwamba nimekubaliana na mwenendo huu wa haki. Kwa asili mimi sio mtu wa kupenda mizozo.

Nakiri kwamba kabla sijakutana na wewe hapa, nilitaka nikushinde. Lakini nimevutiwa mno na usafi wako, upole wako, tabia nzuri, wepesi na hisia ya kweli, kiasi kwamba nimeweka nadhiri mbele ya Allah kwamba nasalimu amri kukubali ukweli wote wenye mantiki ingawa msimamo huu utavunja mioyo juu ya matarajio ya wengine.

Niamini mimi, sioyule mtu wa ule usiku wa kwanza. Nakueleza kwa ukweli na uwazi kabisa kwamba hajo zako zimeacha athari ya ndani mno katika moyo wangu. Kwa dhati kabisa natumaini kwamba nitaweza kufa pamoja na mapenzi na upendo kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kizazi chake, ili kwamba niweze kusimama kwa furaha na kuridhia mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Muombezi: Naam, hakika msimamo kama huo ulikuwa unategemewa kwa mwanachuoni kama wewe. Hakika mimi pia nimevutiwa sana na maelezo yako, na imejengeka kwangu hisia ya urafiki kwa upande wako. Sasa ningependa kuleta ombi kwako. Natumaini utalikubali. Hafidh: Ndio, tafadhali.

Muombezi: Usiku huu ningetaka niwe hakimu na wengine wawe mashahidi, ili kwamba uweze kuamua bila chuki yoyote iwapo dai langu ni haki. Baadhi ya waumini wasio na ujuzi wanasema kwamba hakuna maana kujadili suala ambalo limetokea miaka 1,300 iliyopita. Hawajui kwamba masula yanayohusiana na elimu yanajadiliwa katika kila zama.

Majadiliano ya haki hufichua ukweli na madai ya urithi yanaweza kufanywa kisheria na mwenye kurithi, kwa wakati wowote ule. Kwa vile mimi ni mmoja wa warithi, nataka kukuuliza swali. Tafadhali nakuomba unipe jibu la haki.

Hafidh: Ndio, nitapendezewa sana kusikia maelezo yako.

Muombezi: Kama kwa amri ya Mungu baba anampa mtoto wake mali, na, baada ya kifo cha baba, kama mali ile inachukuliwa kutoka kwa mtoto ambaye anamiliki mali ile, je, itakuwa ni aina gani ya madai?

Hafidh: Kitendo cha mnyang’anyi kitakuwa sio cha haki kabisa. Lakini unamkusudia nani wakati unaposema muonevu na muonewa?

Fadak Na Uporwaji Wake

Wakati ngome ya Khaibar iliposhindwa na kutekwa, malodi, makabaila na watu mashuhuri wa Fadak walikuja kwa Mtume. Fadak ilikuwa ni eneo katika bonde la milima ya Madina. Lilikuwa na vijiji saba ambavyo vimeenea mpaka kwenye mwambao wa bahari. Vingi vilikuwa na rutuba sana na kulikuwepo na chemchem nyingi zenye miti (oasisi).

Kulikuwepo na mkataba wa amani na watu unaosema kwamba nusu yote ya Fadak itakuwa chini ya miliki yao na nusu nyingine itakuwa mali ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ukweli huu umesimuliwa na Yaqut Hamawi, mwaandishi wa “Majimu’l-Buldan”, katika kitabu chake “Futuhu’l-Buldan, Jz. 6, uk. 343; Ahmad Bin Yahya Baladhuri Baghdadi (alikufa 279 A.H.) katika kitabu chake “Ta’rikh”; Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali katika Sharhe yake ya “Sharh-e-Nhju’l-Balagha”, (iliyochapishwa Misir), Jz. 4, uk. 78, akinukuu kutoka kwa Abu Bakr Ahmad Bin Abdu’l-Aziz Jauhari; Muhammad Bin Jarir Tabari katika kitabu chake “Ta’rikh-e-Kabir” na wengine wengi katika muhadithina na wanahistoria wenu.

Kuteremshwa Kwa Aya Ya “Mpe Haki Yake Jamaa Wa Karibu”

Wakati Mtume aliporudi Madina, Jibril aliteremsha aya ifuatayo: “Na mpe jamaa yako wa karibu haki yake, na masikini, na msafiri; wala usitumie ovyo kwa fujo.” (7: 26)

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitafakari juu ya umuhimu wa wahayi huu. Jibril alitokea tena na akamjulisha kwamba Allah ameamuru kwamba: “Fadak itolewe kwa Fatimah.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuita Fatima na akasema: “Allah emeniamuru kuitoa Fadak kama zawadi kwako.” Hivyo mara moja alimpa Fatima umiliki wa Fadak. Hafidh: Tafadhali fafanua unachosema kuhusu tukio ambalo aya hii tukufu imeteremshwa. Je, imeandikwa kwenye vitabu vya historia na tafsir vya Shi’a, au vile vile umeiona (habari hii) katika vitabu vyetu vya kutegemewa?

Muombezi: Mkuu wa wafasir, Ahmad Tha’labi katika kitabu chake “Kashfu’l-Bayan”; Jalalu’d-Din Suyuti katika “Tafsir” yake, Jz. 4, akisimulia kutoka kwa Hafidh Ibn Mardawiyya; yule mufasir mashuhuri Ahmad Bin Musa (aliyekufa 352 A.H.) Akisimulia kutoka kwa Abu Sa’id Khadiri na Hakim Abu ‘l-Qasim Haskani; Ibn Kathir; Imadu’d-Din Isma’il; Ibn Umar Damishqi; Faqih-e-Shafi’i katika kitabu chake cha “Ta’rikh”, na Sheikh Sulaimani Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, sura ya 39, akisimulia kutoka “Tafsir- e-Tha’labi”, “Jam’u’l-Fawaid” na “Uynu’l-Akhbar” wote wanasimulia kwamba wakati aya, “Na mpe jamaa yako wa karibu haki yake…”, ilipoteremshwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah alimuita Fatima na akampa Fatima Fadak kubwa kama zawadi kwake. Kwa hiyo, kadiri Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyoishi, Fadak ilibakia katika miliki ya Fatima. Bibi yule mtukufu aliikodisha ardhi ile; mapato yake yalikusanywa katika awamu tatu.

Kutoka katika hesabu hii alichukuwa pesa ya kutosha kwa ajili ya chakula chake na cha watoto wake na akagawanya alubaki kwa watu masikini wa Bani Hashim. Baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), maofisa wa Khalifa anayetawala walinyakua mali hii kutoka kwa Fatima. Nakuulizeni enyi waheshimiwa, mnieleze katika jina la uadilifu mtakiitaje kitendo hiki?

Hafidh: Hii ndio mara ya kwanza nimesikia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa Fatima Fadak kwa amri (ya Allah).

Muombezi: Inawezekana kwamba hukuweza kusikia kuhusu (suala) hili. Lakini kama ambavyo nimekuambia, wengi wa maulamaa wenu wakubwa wameandika kuhusu suala hili katika vitabu vyao vya kutegemewa. Ili kuthibitisha nukta hii kwa uwazi nakurejeshea kwa Hafidh Ibn Mardawiyya, Waqid na Hakim (Angalia Tafsir na Ta’rikh zao); Jalalu’d-Din Suyut “Durru’l-Mansur, Jz. 4, uk. 177; “Kanzu’l- Umma” ya Mullah Ali Muttaqi na maelezo mafupi ambayo ameandika juu ya ‘Kitabu’l-Akhlak’ ya “Musnad” ya Ahmad Bin Hanbal kuhusu tatizo la Sila-e-rahm; na “Sharh-e-Nahju’l-Balagha” ya Ibn Hadid,

Jz. 4. Maulamaa wote hawa wamesimulia katika njia tofauti, isipokuwa maelezo kutoka kwa Abu Said Khudr, kwamba aya hiyo hapo juu ilipoteremshwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliitoa Fadaka na kumpa Fatima Zahra.

Hoja Kutoka Hadith Ya ‘La Nurith’ – Hatuachi Urihti

Hafidh: Ni ukweli unaokubalika kwamba Mahalifa waliinyang’anya Fadak juu ya msingi wa hadithi inayojulikana sana iliyosimuliwa na Abu Bakr, ambaye alitamka kwamba yeye mwenyewe amemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Sisi Mitume hatuachi urithi wowote nyuma yetu; chochote tunachoacha kama urithi ni sadaka” (yaani, ni mali ya umma).

Fadaka Ilikuwa Zawadi – Sio Urithi

Muombezi: Kwanza, sio mali ya urithi bali ni zawadi. Pili, hiyo hadithi inayodaiwa kuwa ni ya Mtume haikubaliki.

Hafidh: Utatoa hoja gani ya kuikataa hadithi hii?

Muombezi: Kuna sababu nyingi za kuikataa hadithi hii.

Hadithi ‘La Nurith’ Ni Ya Kubuniwa

Kwanza kabisa, yeyote yule aliyeiandaa hadithi hii, aliitamka bila kufikiria kuhusu yale maneno aliyotumia. Kama angekuwa muangalifu kuhusu hadithi hii, kamwe asingelisema: “Sisi Mitume hatuachi urithi wowowte”, kwa sababu angelijua kwamba uwongo wake ungefichuliwa na maneno haya haya ya hadithi hii ya kubuni. Kama angetumia maneno “Sikuacha urithi wowote nyuma,” hadithi yake ya majaribio ingekuwa yenye kuelekea kuwa ya kweli zaidi.

Lakini wakati ametumia wingi “Sisi Mitume…” tunawajibika kuchunguza ukweli wa hadithi hii. Sasa kwa msingi wa maelezo yako mwenyewe tunarejea kwenye Qur’ani Tukufu kwa ajili ya mwongozo. Tunaona kwamba kuna idadi ya aya ambazo zinatueleza kwamba kwa kweli mitume waliacha urithi. Hii inathibisha kwamba hadithi hii ni ya kutupwa moja kwa moja.

Fatima Alitetea Madai Yake

Katika kitabu chake “Kitab-e-Saqifa” mwanachuoni mkubwa na muhadithina, Abu Bakr Ahmad Bin Abdu’l-Aziz Jauhari, ambaye kuhusu yeye Abi’l-Hadid anasema katika kitabu chake “Sharh-e-Nahju’l- Balaghah” kwamba alikuwa ni mmoja wa maulamaa wakubwa na muhadithina wa Masunni; Ibn Al-Athir katika kitabu chake “Nihaya”; Mas’ud katika “Akhbaru’z-Zaman” na katika “Ausat”; Ibn Abil-Hadid katika “Sharh-e-Nahju’l- Balaghah” Jz. 4, uk. 78, akinukuu kutoka kitabu cha Abu Bakr Ahmad Jauhari “Saqifa” na Fadak katika njia tofauti na kutoka kwenye idadi ya vyanzo, baadhi ambavyo hurejea kwa Imamu wa tano Muhammad Baqir kupitia kwa Siddiq Sughra Zainab-e-Kubra na baadhi ambavyo hurejea kwa Abdullah Ibn Hasan kutoka kwa Siddiq Kubra Fatima Zahra na kutoka kwa Ummu’l- Mu’minin Aisha na vile vile kutoka kwa Muhammad Bin Imran Marzabani, yeye kutoka kwa Zaid bin Ali bin Husein; yeye kutoka kwa baba yake, na yeye kutoka kwa baba yake, Imam Husein; na yeye kutoka kwa mama yake maarufu, Fatima Zahra; na maulamaa wengine wengi wa madhehebu yenu wamesimulia hotuba ya Fatima mbele ya mkusanyiko mkubwa wa Waislamu. Wapinzani walifadhaishwa wakati waliposikia hoja zake na hawakuweza kujibu. Kwa vile walikuwa hawana majibu ya kutoa walianzisha ghasia.

Hoja Ya Fatima Ya Kukataa Hadith ‘La Nurith’

Moja ya hoja za Fatima za kukataa hadithi hii ilikuwa kwamba, kama hadithi hii ingekuwa ni ya kweli, basi kwa nini kulikuwa na aya nyingi mno kuhusu urathi wa mitume.

Alisema: “Katika sehemu moja Qur’ani inasema: “Na Suleimani alikuwa mrithi wa Daudi.’” (27:16)

Kuhusu Mtume Zakariya Qur’ani Tukufu inasema:

{ﻓَﻬﺐ ﻟ ﻣﻦ ﻟَﺪُﻧْﻚَ وﻟﻴﺎ {5

{ﻳﺮِﺛُﻨ وﻳﺮِث ﻣﻦ آلِ ﻳﻌﻘُﻮب{6

“…Basi nipe mrithi kutoka kwako, ambaye atarithi kutoka kwangu na mrithi (vile vile) wa nyumba ya Yaaqub…” (19:5-6)

Kuhusu maombi ya Zakariya Qur’ani Tukufu inasema:

{وزَﻛﺮِﻳﺎ اذْ ﻧَﺎدﱝ رﺑﻪ رب ِ ﺗَﺬَرﻧ ﻓَﺮدا واﻧْﺖ ﺧَﻴﺮ اﻟْﻮارِﺛﻴﻦ {89

{ﻓَﺎﺳﺘَﺠﺒﻨَﺎ ﻟَﻪ ووﻫﺒﻨَﺎ ﻟَﻪ ﻳﺤﻴ{90

“Na Zakariya alipomuomba Mola Wake: ‘Mola Wangu, usiniache peke yangu (bila mtoto), na Wewe ndiye Mbora wa wanaorithi.’ Basi tukamkubalia na tukampa Yahya…” (21:89-90)

Baada ya haya akasema: “Ewe mtoto wa Abu Qahafa! Je, imo ndani ya Kitabu cha Allah kwamba wewe ni mrithi wa baba yako na mimi ninanyimwa urithi wa baba yangu? Umefanya kashfa kubwa mno. Enyi watu! Je, mmekiacha kwa mkusudi Kitabu cha Allah (Qur’ani Tukufu) na kukipuuza moja kwa moja? Je, mimi sio mtoto wa Mtukufu Mtume? Kwa nini unaninyima mimi haki yangu?

Kwa nini aya zote hizi za urithi, ambazo zimekusudiwa kwa watu wote kwa ujumla na hususan kwa Mitume zimejumuishwa katika Qur’ani Tukufu? Je, si kweli kwamba aya za Qur’ani zitabakia bila kubadilishwa mpaka Siku ya Hukumu?

Je, Qur’ani haisemi: “.....na ndugu wa nasaba wana haki zaidi wao kwa wao katika Kitabu cha Mwenyezi Mungu.....” (8:75) na: “Allah anakuusieni juu ya watoto wenu! Mtoto mwanaume atapata vigawanyo viwili vya mwanamke…” (4:11) na: Mmelazimishwa, mmoja wenu anapofikiwa na umauti, kama ameacha mali, kuwausia wazazi wake wawili na jamaa wa karibu kwa uadilifu. (Huu) ni wajibu kwa wamchao Mwenyezi Mungu” (2:180).

Basi kwa nini mimi hasa hasa niwe nimenyimwa urithi wa baba yangu? Je Allah ameteremsha aya maalumu kwako, ambazo zinamuondoa baba yangu (kutoka kwenye haki yake hii). Je, wewe unajua maana ya nje na ya ndani ya Qur’ani Tukufu kuliko baba yangu Muhammad na binamu yake Ali?”

Utetezi Wa Fatimah Hauna Mafanikio

Wakati waliponyamazishwa na hoja hizi na ukweli wa mambo, wakawa hawana majibu. Walikimbilia kwenye hila na lugha ya matusi.

Alilia huku akisema: “Leo mumeuvunja moyo wangu. Siku ya Hukumu nitafungua mashitaka dhidi yenu katika Mahakama Tukufu ya Haki na Allah Mwenye nguvu zote ataamua kesi hiyo kwa uadilifu.

Allah ndiye Hakimu bora zaidi. Muhammad ndiye mkuu na bwana; muda wa ahadi, wetu na wenu ni Siku ya Ufufuo.

Siku hiyo muonevu atakuwa mwenye hasara, na toba yenu haitawasaidia kitu. Kwani kwa kila kitu kuna muda maalumu uliopangwa na mtajua muda mfupi tu ujao nani atapatwa na adhabu ya dharau.”

Khalifa Alitumia Lugha Chafu

Hafidh: Nani atathubutu kukashifu kipande cha mwili wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Fatima Zahra? Hili siliamini. Hila na udanganyifu inawezekana, lakini kutumia lugha ya matusi haiwezikani. Tafadhali usiseme vitu kama hivyo.

Muombezi: Hakuna mtu aliyekuwa na ujasiri wa kusema vitu kama hivyo isipokuwa Khalifa wako, Abu Bakr. Akiwa ameshindwa kujibu hoja nzito za Bibi huyo muonewa, mara moja alipanda kwenye mimbari na kumtukana Fatimah na mume wake na binamu yake Mtume, kipenzi cha Allah na cha Mtume Wake, Amiru’l-Mu’minin Ali.

Hafidh: Nadhani riwaya hizi za kizushi zimeenezwa na mashabiki wa kidini.

Muombezi: umekosea. Riwaya hizi hazikuenezwa na mashabiki wa ki-Shi’a. Maulamaa wakubwa wa Sunni ndio waliozisambaza.

Kwa kiasi chochote cha kukosa uvumilivu wanachoweza kuwa nacho watu wetu wa kawaida, kamwe huwa hawabuni hadithi.

Kama utachunguza vitabu vyenu vya sahihi, utakiri kwamba maulamaa wenu wakubwa wameyakubali mambo haya. Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali katika “Sharh-e-Nahju’l-Balagha” Jz. 4, uk. 80, iliyochapishwa Misri, akisimulia kutoka kwa Abu Bakr Ahmad Bin Abdu’l- Aziz Jauhari, ameandika kwa urefu kuhusu Abu Bakr kupanda juu ya mimbari baada ya malalamiko ya upinzani wa Ali na Fatimah.

Kupingana Kwa Ali Na Abu Bakr

Wanachuoni wengi wamesimulia kwamba, wakati Fatimah alipomaliza kutetea hoja yake, Ali akaanza upingaji wake katika mkusanyiko wa hadhara wa Waislamu katika Msikiti wa Madina, akielekea upande alikokuwa Abu Bakr, alisema:

“Kwa nini unamnyima Fatimah urithi wa baba yake, ingawa alikuwa ndiye mmliki wake na alikuwa anaimiliki mali hiyo wakati wa kipindi cha uhai wa baba yake?”

Abu Bakr akajibu: “Fadak ni ngawira ya Waislamu. Kama Fatimah atatoa ushahidi kamili kwamba ni mali yake, kwa hakika nitampa; vinginevyo, nitamnyima mali hiyo.”

Mtukufu Imamu akasema: “Je, sio ukweli kwamba wakati unatamka hukumu kuhusu Waislamu, kwa ujumla, unapitisha hukumu inayokinzana mno kuhusiana na sisi.?”

“Je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakusema kwamba dhima ya kuthibitisha inakuwa juu ya mdai na ile ya utetezi juu ya mdaiwa? Umepuuza hukumu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kinyume na sheria ya dini, unataka mashahidi kutoka kwa Fatimah ambaye alikuwa katika umiliki wa mali hiyo tangu wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Aidha, je, maneno ya Fatimah, ambaye ni mmoja wa Ashab-e-Kisa (Watu wa Shuka) na ambaye amejumuishwa katika aya ya utakaso, sio ya kweli?”

Kama watu wawili wangetoa ushahidi kwamba Fatimah amefanya makosa fulani, hebu niambie ungemshughilikia vipi?” Abu Bakr akasema: “Ningetoa adhabu juu yake kama ambavyo ningefanya kwa mwanamke yeyote.”

Mtukufu Imamu akasema: “Kama ungefanya hivyo, ungekuwa kafiri mbele ya Allah, kwa sababu ungekuwa umekataa ushahidi wa Allah kuhusu usafi wa Fatimah. Allah anasema:

‘Hakika, hakika, Allah anataka kukuondoleeni kila aina ya uchafu, Enyi Watu wa Nyumba na kuwatakaseni kwa utakaso halisi.’ Je, aya hii haikuteremshwa katika kutukuza sisi?”

Abu Bakr akasema: “Kwanini isiwe hivyo?” Imamu akasema: “Je, inawezekana kwamba Fatimah, ambaye usafi wake umethibitishwa na Allah, angeweza kutoa madai ya uwongo kwenye mali ndogo kama hii? Unakataa ushahidi wa mtu aliyetakaswa na unakubali ushahidi wa Bedui ambaye anakojoa juu ya kisigino cha mguu wake mwenyewe!”

Baada ya kusema haya, Imam akarudi nyumbani kwake akiwa amekasirika. Malalamiko yake yaliamsha hisia za watu. Kila mtu alisema: “Ukweli uko pamoja na Ali na Fatimah.

Wallahi Ali anasema kweli. Kwa nini binti ya Mtume afanyiwe fedheha kiasi hicho?”

Ufidhuli Wa Abu Bakr

Ibn Abi’l-Hadid anasimulia kwamba watu walivutiwa sana upingaji wa Ali na Fatimah na wakaanza kuleta fujo. Abu Bakr ambaye aliona kwamba wale watu wawili watukufu tayari wameondoka pale Msikitini alipanda mimbari na akasema:

“Enyi watu! Kwa nini mnachanganyikiwa hivi. Kwa nini mumsikilize kila mtu? Kwa vile tu nimekataa ushahidi wao, wanazungumza upumbavu. Ukweli ni kwamba yeye ni mbweha ambaye amesalitiwa na mkia wake mwenyewe.

Anasababisha kila aina ya vurugu. Anapuuzia uzito wa vvurugu na kuchochea watu kufanya fujo na ghasia. Anatafuta msaada kutoka kwa wanyonge. Anatafuta msaada kutoka kwa wanawake. Yeye ni sawa na Ummu’t-Tihal ambaye watu wa nyumbani kwake mwenyewe walipendelea kuzini naye.”

Je, maneno haya si matusi ya kufedhehesha? Je, yanakubaliana na sifa, heshima, mapenzi na huruma ambavyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema vinawastahikia familia yake? Mpaka lini mtabakia na imani hii potofu na ushabiki? Mpaka lini mtawapinga Mashi’a na kuwaita Marafidhi na makafiri kwa sababu tu wanakosoa maneno na vitendo vya watu ambavyo vimeandikwa katika vitabu vyenu?

Historia Inahukumu Mtu

Lifikirieni suala hili kwa uadilifu. Je, ufedhuli ule wa sahaba mzee wa Mtume ulikuwa ni wa haki? Lugha mbovu na ya matusi ya Mu’awiya, Marwan na Khalid hazikuwa za kuhuzunisha hivyo kama ile ambayo inakuja kutoka kwenye mdomo wa mtu ambaye anaitwa “sahaba wa kwenye pango.”

Watukufu Waislamu! Hatukuwepo katika wakati ule. Tunasikia majina ya Ali, Abu Bakr, Umar, Uthman, Talha, Zubair, Mu’awiya, Marwan, Khalid, Abu Huraira, nk. Hatuna urafiki wala uadui na yeyote kati yao. Tunaona mambo mawili: kwanza, wale ambao walipendwa na Allah na Mtume Wake na ambao kwao heshima na utii vimeamriwa juu yao. Pili, tunapima matendo na kauli zao. Kisha tunaamua bila upendeleo. Tunajizuia kuruhusu upendeleo wetu kwa mtu fulani kupotosha uamuzi wetu.

Mshangao Wa Hadid Juu Ya Abu Bakr Kuwakashifu Ali Na Fatimah

Sio sisi peke yetu ambao tumeshitushwa na tabia kama hii. Hata maulama wenu waadilifu wanashangazwa kuyaona haya. Ibn Abi’l-Hadid anaandika katika “Sharh-e-Nahju’l- Balagha” yake, Jz. 4, uk. 80, kwamba maneno ya Khalifa yalimjaza na mshangao. Alimuuliza mwalimu wake Abu Yahya Naqib Ja’far Bin Yahya Bin Abi Zaidu’l-Basari, maneno haya ya Khalifa yalikuwa yanamhusu nani. Yeye alisema kwamba kauli hizo hazikuwa za kupitia. Uhusikaji wake ulikuwa wa wazi.

Ibn Hadid akasema: “Kama ungekuwa wa wazi, nisingeuliza.” Hapo alicheka na akasema: “Mambo haya yalisemwa dhidi ya Ali.”Ibn Hadid akayarudia maneno haya kwa mshangao: “Maneno yote haya yalisemwa dhidi ya Ali?” Mwalimu wake akasema: “Ndio, Ewe mwanangu! Hivi ndivyo utawala unavyomaanisha.”

Kumuudhi Ali Ni Kumuudhi Mtukufu Mtume

Kuhusu wote wawili Ali na Fatimah, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba shida zao ni shida zake yeye pia. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Yule ambaye anatawasumbua hawa wawili ananisumbua mimi, na mtu anayenisumbua mimi anamsumbua Allah.” Vile vile imeandikwa katika vitabu vyenu sahihi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Yeyote yule ambaye anamtukana Ali ananitukana mimi, ambaye ananitukana mimi anamtukana Allah.”

Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i, katika kitabu chake “Kifayatu’t-Talib” Sura ya 10, anasimulia hadithi ndefu kutoka kwa Ibn Abbas, ambaye alikiambia kikundi cha Wasiria ambao walikuwa wakimlaani Ali kwamba yeye alimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kumhusu Ali: “Yeyote yule anayekutuka wewe amenitukana mimi, na yeyote anaye nitukana mimi amemtukana Allah, na ambaye anamtukana Allah atatupwa moja kwa moja Motoni.”

Baada ya hadithi hii alinukuu hadithi nyingine nyingi kutoka kwenye vyanzo sahihi ambazo zote zinathibitisha kwamba wale ambao wanamtukana Ali ni makafiri. Sura ya 10 ya kitabu hiki inaitwa: “Kuhusu ukafiri wa mtu ambaye anamtukana Ali.”

Vile vile Hakim katika kitabu chake, “Mustadrak”, Jz. 3, uk. 121, ameinukuu hadithi hii hii. Hivyo kwa mujibu wa hadithi zote hizi, wale ambao wanamlaani Ali, wanamlaani Allah na Mtume Wake. Wote hao (kama Mu’awiya, Bani Umayyah, Manasibi, Khawariji) wenyewe wamelaaniwa.

Basi, sasa kiasi hiki kinatosha. Hakika Siku ya Hukumu kwa hakika itafika. Kwa vile wahenga wetu walioonewa walichukuwa njia ya ukimya na kuacha uamuzi juu ya Siku hiyo, sisi vile vile tutabakia kimya.

Kuna nukta ya pili ambayo inakataa ‘hadithi hii ya kudhaniwa’ “Sisi hatuachi urithi…” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Mimi ni jiji la elimu na Ali ni lango lake; na mimi ni nyumba ya hekima na Ali ni mlango wake.” Madhehebu zote zimelikubali hili.

Hakika mtu ambaye alikuwa ni lango la elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alielewa hadithi zote na maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hususan zile zinahusiana na matatizo ya mirathi.

Kwani ustawi wa taifa zima hutengemea juu ya hadithi hizi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vile vile alisema: “Mtu ambaye anataka kupata elimu lazima aje kwenye mlango wa Ali.”

Kama elimu yake ingelikuwa sio kamili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingesema kwamba Ali alikuwa hakimu bora katika Umma mzima. Alisema: “Ali ni mbora miongoni mwenu wote katika kuzitafsiri sheria.” Hadithi hii imeandikwa katika vitabu vyenu vyote vya sahihi.

Hivi Mtukufu Mtume angeweza kutangaza ubora wa ubingwa wa mtu wa sheria kama mtu huyo alikuwa hayaelewi matatizo ya mirathi na haki za watu? Sehemu ya lengo la Mtukufu Mtume lilikuwa ni kuleta mageuzi ya kijamii kwa ajili ya watu katika dunia hii na amani na starehe kwa ajili yao katika akhera.

Angeweza vipi basi kumfanya yeye Ali kuwa Amirul-Mu’minin na kisha bado asimfikishie desturi kama hii ambayo inaathiri utaratibu wote wa kijamii?

Sheikh: Hakuna kati ya vitu hivi viwili kilichothibitishwa kwa mujibu wetu. Hadithi ya Jiji la elimu haikubaliwi na maulamaa wetu mashuhuri na mas’ala ya umakamu na urithi (wa nafasi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)) pia vile vile yamekataliwa na wale maulamaa wakubwa.

Bukhari na Muslim katika kukusanya kwao hadithi na wengine miongoni mwa maulamaa wakubwa, wanasimulia kutoka kwa Ummu’l-Mu’minin Aisha kwamba, kichwa cha Mtume wakati wa kifo chake kilikuwa kimelala kifuani mwake mpaka alipokata roho. Alieleza kwamba hakutengeneza wosia. Lau angelitengeneza wosia Ummu’l-Mu’minin angesimulia na suala la wosia lingeliweza kutatuliwa.

Hadithi “Mimi Ni Jiji La Elimu Na Ali Ni Lango Lake”

Muombezi: Kuhusu hadithi hii umekuwa sio mkweli hata kidogo. Nilikwishakuambia tayari kwamba madhehebu zote kwa pamoja zinakubaliana kwamba hii imesimuliwa takiriban kwa mwendelezo kamili. Maulamaa wenu wafuatao wamethibitisha usahihi wa hadithi hii:

Imam Tha’labi, Firuzabadi, Hakim Nishapuri, Muhammad Jazari, Muhammad Bin Jarir Tabari, Suyuti, Sakhawi, Muttaqi Hindi, Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i, Muhammad Bin Talha Shafi’i, Kadhi Fadhl Bin Ruzbahan, Munawi, Ibn Hajar Makki, Khatib Khawarizmi, Sulaiman Qanduzi Hanafi, Ibn Maghazil Faqih Shafi’i, Dailami, Ibn Talha Shafi’i, Mir Sayyid Ali Hamadani, Hafidh Abu Nu’aim Ispahani, Sheikhu’l-Islam Hamwaini, Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali, Tibrani, Sibt Ibn Jauzi na Imam Abdu’r-Rahman Nisa’i.

Umakamu Ulitunukiwa Juu Ya Ali

Kuhusu mas’ala ya umakamu, kuna kauli nyingi za kuaminika zinayothibitisha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitengeneza wosia wake. Hakuna mtu mwenye ujuzi anayekataa jambo hili.

Nawab: Khalifa wa Mtume pia ni makamu wake, mtu ambaye aliendesha mambo yake ya ndani. Kwa mfano, walilipa posho kwa wake za Mtume. Kwa nini unasema kwamba Ali aliteuliwa kuwa makamu? Muombezi: Unasema kweli. Ni wazi kwamba Khalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa pia ni makamu wake. Wakati wa mikesha iliyopita nimewasilisha hoja zangu na kauli za kuaminika kuhusiana na ukhalifa. Kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteua Ali kuwa Khalifa wake na makamu wake ilikuwa ni sahihi kabisa.

Ambapo wengine walikuwa wanajishughisha na mambo yao na njama za kisiasa, huyo makamu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alishughulika na taratibu za mazishi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Baadaye alijishughulisha katika kurudisha fedha za amana na vitu vingine vya thamani na kuangalia masuala mengine ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ameyakabidhi kwake.

Hili liko wazi mno kiasi kwamba hakuhitajiki uthibitisho wowote. Maulamaa wetu wote wanakubalina kuhusiana na jambo hili.

Hadithi Kuhusu Ushika Umakamu

Ili kuthibitisha hoja yangu ngoja nirejee kwenye baadhi ya hadithi:

(1) Kuunda udugu:Imam Tha’labi katika kitabu chake “Manaqib” na “Tafsir”, Ibn Maghazili Faqih Shafi’i katika “Manaqib” yake na Mir Sayyid Ali Hamadani katika kitabu chake “Mawaddatu’l-Qurba” (Mawadda ya 6) anasimulia kutoka kwa khalifa wa pili, Umar bin Khattab, ambaye anasema kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anaanzisha undugu kati ya masahaba, alisema: “Huyu Ali ni ndugu yangu katika ulimwengu huu na kesho akhera. Miongoni mwa kizazi changu yeye ni khalifa wangu; ni mrithi wangu (makamu) katika Umma wangu. Yeye ndiye mrithi wa elimu yangu; ndiye mlipaji wa deni langu. Kilicho chake ni changu pia; kilicho changu ni chake pia; manufaa yake ni manufaa yangu na hasara yake ni hasara yangu. Yule ambaye ni rafiki yake kwa hakika ni rafiki kwangu na ambaye ni adui kwake kwa hakika ni adui kwangu.”

(2) Kuuliza kwa Salman: Sheikh Suleiman Balkhi Hanafi katika sura ya 15 ya “Yanabiu’l-Mawadda” amesimulia hadithi ishirini katika kuunga mkono umakamu wa Ali kutoka kwa Imam Tha’labi, Hamwaini, Hafidh Abu Nu’am, Ahmad Bin Hanbal, Ibn Maghazili, Khawarizmi na Dailami. Nawasilisha baadhi ya hizo kwa ajili ya mwongozo wenu. Anasimulia kutoka kwenye Musnad ya Ahmad Bin Hanbal (na Sibt Ibn Jauz katika Tadhkirat-e-Khawasu’l-Umma, uk. 26, na Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib yake vile vile wamesimulia hadithi hizi) kwamba Anas Ibn Malik amese- ma: “Nilimuomba Salman amuulize Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni nani mrithi wake (wasii). Salman akamuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), “Ewe Mtume wa Allah! Ni nani makamu wako?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema, “Ewe Salman! Ni nani mrithi wa Salman?” Akasema, “Yusha Bin Nun.” Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema, “Makamu wangu na mrithi wangu, ambaye atalipa madeni yangu na atakayekamilisha ahadi zangu, ni Ali Bin Abi Talib.

(3) Kila Mtume alikuwa na Mrithi wake, Ali ni Mrithi wangu: Imesimuliwa kutoka kwa Muwaffaq Bin Ahmad, ambaye ananukuu kutoka kwa Buraida kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kila Mtume alikuwa na makamu na mrithi, na kwa hakika, makamu na mrithi wangu ni Ali.” Muhammad Bin Yusuf Ganji Shai’i katika kitabu chake “Kifayatu’t-Talib”, sura ya 62, uk. 131 ananukuu hadithi hiyo hiyo ambayo vile vile imesimuliwa na Muhadith wa Syria katika kitabu chake “Ta’rikh”.

(4) Ali ni mwisho wa Mawasii: Sheikhu’l-Islam Hamwaini anasimulia kutoka kwa Abu Dharr Ghifari, ambaye amesema, “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema, ‘mimi ni mwisho wa Mitume na wewe, Ewe Ali, ni mwisho wa mawasii mpaka Siku ya Hukumu”.

(5) Ali ni makamu wangu kutoka kwenye kizazi changu: Imesimuliwa kutoka kwa Khatib Khawarizmi, ambaye anasimulia kutoka kwa Ummu’l-Mu’minin Ummi Salama, ambaye amesema; “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: ‘Allah amechagua mrithi kwa ajili ya kila Mtume na baada yangu mimi makamu wangu kutoka kwenye kizazi changu na Umma wangu ni Ali.’”

(6) Ali alitetea cheo chake katika hotuba: Imesimuliwa kutoka Maghazili Faqih Shafi’i, ambaye anasimulia kutoka kwa Asbagh Bin Nabuta, mmoja wa Masahaba wakubwa wa Amiru’l-Muminin, na Muslim na Bukhari vile vile wamenukuu kutoka kwake kwamba bwana wake Amiru’l-Mu’minin amesema katika moja ya hotuba zake: “Enyi watu! Mimi ni Imam (kiongozi) wa viumbe wote.

Ni mrithi wa (makamu) wa mbora mno wa viumbe; mimi ndio baba wa kizazi kilicho takasika kabisa na chenye kuongoza; mimi ni ndugu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); mrithi wake, rafiki yake muaminifu na mwenza wake wa karibu. Mimi ni bwana wa waumini; ni kiongozi wa wale ambao wana nyuso angavu, mikono angavu na miguu angavu; mimi ni mkuu wa Mawasii wote. Kupigana dhidi yangu ni kupigana dhidi ya Allah. Kufanya amani na mimi ni kufanya amani na Allah. Utii kwangu ni utii kwa Allah; urafiki na mimi ni urafiki na Allah; wafuasi wangu ni marafiki wa Allah; na wasaidizi wangu ni wasidizi wa Allah.”

(7) Allah alinifanya mimi Mtume na Ali makamu wangu: Vile vile Ibn Maghazili Shafi’i katika “Manaqib” yake anamnukuu Abdullah Bin Mas’ud kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ujumbe wa utume uliishilizwa kwangu mimi na Ali; katu hakuna kati yetu sisi aliyewahi kusujudu mbele ya sanamu; hivyo Allah alinifanya mimi Mtume na Ali kuwa makamu.”

(8) Umakamu wa Ali ni sehemu ya kanuni ya kiapo cha utii kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i anaandika katika kitabu chake “Mawaddatu’l-Qurba” Mawadda ya 4, kutoka kwa Atba Bin Amir Jahni, ambaye amesema: “Tunatoa kiapo cha utii kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), tukukiri ukweli kwamba hakuna mungu isipokuwa Allah. Ni Mmoja na mshirika na hakika Muhammad ni Mtume Wake na Ali ni makamu Wake. Hivyo kama tunaacha chochote kati ya mambo haya matatu tutakuwa makafiri.”

(9) Ninawaita watu kwenye haki na Ali anaitia nuru: Katika Mawaddatu’l-Qurba hiyo hiyo, vile vile imeandikwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Hakika Allah ameteua makamu kwa kwa ajili ya kila Mtume: Seth, makamu wa Adamu; Joshua, makamu wa Musa; Simon Petro makamu wa Yesu; na Ali ni makamu wangu; na makamu wangu ni mbora wa makamu wote. Nawaita watu kwenye haki na Ali anaitia nuru.”

Allah Alimteua Ali Kutoka Miongoni Mwa Watu Wote Kuwa Makamu Wangu

Mwandishi wa Yanabi ananukuu kutoka kwenye Manaqib ya Muwaffaq Bin Ahmad Khawarizmi, ambaye alisimulia kutoka kwa Abu Ayyub Ansari, ambaye amesema kwam- ba wakati Mtume wa Allah alipokuwa yu mgonjwa kitandani, Fatimah alikuja na kuanza kulia. Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Fatimah, wewe umebarikiwa makhususi na Allah ambaye amekupa mume ambaye Uislamu wake ni wa mbele zaidi, ambaye elimu yake ni bora kuliko ya mtu yeyote yule, na ambaye uvumilivu wake unapita uvumilivu watu mengine wote.

Kwa hakika Allah swt. Amewapa upendeleo maalumu watu wa ulimwengu huu. Kutoka miongoni mwao Alichagua na kuniteua mimi kama Mtume na Mjumbe Wake. Kisha akawapa baraka nyingine maalumu na kutoka miongoni mwa watu akamchagua mume wako. Na amenifunulia kwamba nikuoze wewe kwake na nimfanye makamu wangu.”

Ahlul-Bayt Wamejaaliwa Sifa Saba Zisizo Na Ushindani

Baada ya kuandika hadithi hii katika Manaqib yake, Ibn Maghazili Faqih Shfi’i anaandika maneno haya ya nyongeza, ya Mtukufu Mtume: “Ewe Fatimah! Sisi Ahlul-Bayt tumejaaliwa sifa saba, ambazo hakuna katika vizazi vya wanadamu kilichokuwa nazo, na hakuna miongoni mwa vizazi vyao kitakachokuwa nazo. Mtume mtukufu mno miongoni mwa Mitume anatokana na sisi, na ni baba yako. Makamu wangu ni mbora mno kwa makamu wengine wote, na ni mume wako. Shahidi (aliyejitolea mhanga) anayewapita mashahidi wengine wote, na ni ami yako, Hamza.

Kutoka miongoni mwetu sisi (Ahlu’l-Bayt) kuna mtu ambaye ana mbawa mbili ambazo kwazo anaruka kwenda popote anapopenda, huko Peponi, na ni binamu yako, Ja’far. Kutokana na sisi kuna wajukuu wawili ambao ni mab- wana wa vijana wa Peponi, na ni watoto wako. Na ninakuambia, kwa jina la Allah ambaye anamiliki uhai wangu, kwamba Mahdi wa Umma huu, ambaye kwamba Isa Bin Mariamu atasali Salat nyuma yake, atakuwa ni katika kizazi chako.”

Mahdi Ataijaza Ardhi Na Uadilifu

Ibrahim Bin Muhammad Hamwaini, baada ya kusimulia hadithi hii alinukuu maneno haya ya nyongeza: Baada ya kumtaja Mahdi Mtume alisema: “Ataujaza ulimwengu huu na uadilifu wakati utakapokuwa umejaa ukatili na dhulma. Ewe Fatima! Usihuzunike na usilie.

Kwa sababu ya mapenzi na heshima yangu kwako, Allah swt., ni mpole zaidi kwako kuliko mimi. Amekupa wewe mume mwenye mafanikio ya hali ya juu mno ya kiroho, na aliye tukuka mno katika hadhi ya kifamilia, mwenye huruma sana kwa watu, muadilifu mno katika kushughulikia mambo ya watu, na msahihi mno katika maamuzi yake.” Nafikiri kiasi hiki kinatosha kuridhisha udadisi wa Nawab Sahib na kuondoa kuelewa vibaya kwa Sheikh Sahib.

Wakati Wa Kifo Chake, Kichwa Cha Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Kilikuwa Juu Ya Kifua Cha Amir-Ul-Mu’minin (A.S.)

Amma kwa madai ya kwamba wakati wa kifo cha Mtume, kichwa chake kilikuwa juu ya kifua cha Ummu’l-Mu’minin Aisha, sio kweli. Maulamaa wenu wenyewe wameonesha kwamba wakati wa kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kichwa chake kilikuwa kimeegamia juu ya kifua cha Amirul-Muminin.

Sheikh: Ni katika kitabu kipi ambacho maulamaa wetu wameandika habari hii?

Muombezi: Soma “Kanzu’l-Ummal”, Jz. 4, uk. 55 na Jz. 6, uk. 392 na 400; na “Tabaqa” cha Muhammad Bin Sa’d Katib, sehemu ya 2, uk. 51; “Mustadrak” cha Hakim Nishapuri, Jz. 3, uk. 139; Talkhis-e-Dhahab; Sunan ya Ibn Shabih; “Kabir” cha Tabari; Musnad ya Imam Ahmad Hanbal, Jz.3; “Hilyatu’l-Auliya” cha Hafidh Abu Nu’aim. Pamoja na tofau- ti ndogo ya maneno, maandishi yote haya yanasimulia kutoka kwa Ummu’l-Mu’minin Umm Salma na Jabir Ibn Abdullah Ansari kwamba wakati wa kifo chake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuita Ali na kuweka kichwa chake juu ya kifua cha Ali mpaka alipofariki.

Kwa nyongeza ya maneno haya, kuna maelezo ya Amiru’l-Mu’minin mwenyewe ambayo yameandikwa katika kitabu chake cha Nahju’l-Balagha. Ibn Abi’l-Hadid katika “Sharhe Nahju’l-Balagha” yake, Jz. 2, uk. 561 anaeleza kwamba Mtukufu Imam kwa uwazi kabisa alisema: “Hakika roho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) iliondoka ulimwenguni hapa wakati ambapo kichwa chake kilikuwa juu ya kifua changu; alivuta pumzi yake ya mwisho akiwa mikononi mwangu.

Hivyo nilifuta mikono yangu kwenye uso wangu.” Ibn Abi’l-Hadid katika Jz. 2, uk. 562, ya kitabu chake anafafanua juu ya maelezo haya ya Imamu Ali, kwamba wakati kichwa cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kilipokuwa juu ya kifua cha Ali, matone kadhaa ya damu ya Mtume yalidondoka chini, ambayo Ali aliyafuta kwenye uso wake.

Na katika ukurasa wa 590 wa kitabu hicho hicho, katika kuandika kwake kuhusu mazishi ya Fatimah, anasema kwamba Ali alizungumza na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Hakika nilikulaza kwenye kaburi; roho yako ilikutoka kati ya shingo na kifua changu.”

Maelezo yote haya sahihi na hoja nzito zinazothibitisha wazi kwamba maelezo ya Aisha hayawezi kukubaliwa. Ni ukweli unaojulikana kwamba Aisha alimpinga Amiru’l-Mu’minin kuanzia mwanzo kabisa. Insha-Allah nitaelezea kuhusu hili vile vile kama hali itahitaji hivyo. Kudadisi Kuhusu Urithi Au Umakamu Unaofuatia Mara Moja

Hadithi hizi kwa uwazi zinaonesha kwamba Allah aliteuwa mitume na makamu. Vile vile alimteua Ali kama makamu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aidha, mrithi hapa ina maana ya ukhalifa, sio urithi wa hivi tu wa kifamilia. Kwa hiyo makamu alipewa mamlaka kamili juu ya watu binafsi na jamii katika mambo yao yote, mamlaka kama yale yale aliyokuwa nayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Maulamaa wenu wote mashuhuri wameukiri uongozi huu wa Umma, ambao ulitolewa kwa Ali. Hakuna aliyeukataa isipokuwa mashabiki wachache na maadui, ambao wamekataa kukubali sifa za hali ya juu za Mtukufu Imam. Ibn Abi’l-Hadid anasema katika Sharhe yake ya “Nahju’l-Balagha”, Jz. 1, (iliyochapishwa Misri): “Kwa mujibu wetu sisi hakuna shaka kwamba Ali alikuwa wasii (makamu) wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na kwa maoni yetu, mtu anayepinga ukweli huu ni yule tu ambaye ana chuki au uadui dhidi yake.”

Mashairi Ya Baadhi Ya Masahaba Kuhusu Umakamu

Ibn Abi’l-Hadid ananukuu idadi ya mashairi ambayo huthibitisha umakamu wa Amiru’l-Mu’minin. Miongoni mwa hayo ni mashairi mawili ya Abdullah Bin Abbas, ambaye yeye amesema:

“Mbali na kuwa kwako wewe ni Ahlu’l-Bayt, vile vile wewe ni wasii (makamu) wake, na pale mtu anakukabili wewe katika uwanja wa vita, wewe ndiye mpiganaji bora.”

Ananukuu mashairi ya Khazima Bin Thabit: “Mbali na ukweli kwamba umejumuishwa katika Ahlu’l-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), vile vile wewe ni mrithi (makamu) wake wa kufuatia mara moja, na ushahidi wa yote yale yaliyokuja kwake.” Vile vile ananukuu shairi la Sahaba, Abu’l-Hakim Tihan, ambaye alisema: “Hakika, ni yule mrithi (makamu) wa mara moja wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye ndiye Imam na bwana wetu. Pazia zimeondolewa na siri zimefichuliwa.”

Pengine hii inatosha. Kama unataka kuona mashairi zaidi juu ya nukta hii unaweza kusoma kitabu hicho hicho. Kama anavyosema Ibn Abi’l-Hadid kama asingekuwa anaogopa kukikuza mno kitabu hiki, angejaza kurasa zaidi kwa mashairi haya yanayothibitisha umakamu wa Ali. Hivyo ina maana kwamba, umakamu na utume hutegemeana. Hii ni hatua baada ya cheo cha utume na hii ndio maana ya Mamlaka ya Mungu.

Wosia Wa Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Kuhusu Umakamu Wa Ali Katika

Vitabu Vyote Sahihi

Sheikh: Kama riwaya hizi ni sahihi, kwa nini hatuoni rekodi kama hiyo ya wosia na uthibitisho wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kama tulivyo na zile ambazo zimeachwa na Abu Bakr na Umar wakati wa vifo vyao?

Muombezi: Unaweza kujionea kwa urahisi kuhusu masuala haya kutoka kwenye vitabu sahihi vya Shi’a, ambavyo vimeandika masuala haya kwa umoja wa maoni kutoka kwa Ahlu’l-Bayt, lakini kwa vile tumekubaliana katika usiku wa kwanza kwamba tusichukue njia ya hadithi za upande mmoja, inanipasa kurejea kwenye baadhi ya hadithi ambazo zinapatikana katika vitabu sahih vyenu wenyewe kama vile “Tabaqa” cha Ibn Sa’d, Jz. 2, uk. 61; “Kanzu’l-Ummal” cha Ali Muttaqi, Jz. 4, uk. 54, na Jz. 6, uk. 155, 393, 403; Musnad ya Imam Ahmad Hanbal, Jz. 4, uk. 164; na “Mustadrak” cha Hakim, Jz. 3 uk. 59, 111.

Mbali na hivi, wanachoni wenu mashuhuri kama Baihaqi katika Sunan na Dala’il yake, Ibn Abdu’l-Barr katika Isti’ab, Tabrani katika Kabir na Ibn Mardawiyya katika kitabu chake cha Ta’rikh kadhalika na wengine wamesimulia kwa maneno tofauti, yale maelekezo na maagizo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye alisema: “Ewe Ali! Wewe ni ndugu yangu na waziri wangu; utalipa madeni yangu. Utatimiza ahadi zangu na utatekeleza majukumu yangu.

Utaikosha maiti yangu, utalipa madeni yangu na kunihifadhi kaburini.” Mbali na riwaya hizi za wazi, kuna idadi nyingine kubwa za maagizo au amri, ambazo zilitamkwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusiana na suala hili.

Mtukufu Mtume Alizuiwa Kuandika Wosia Wake Wakati Wa Kifo Chake

Sheikh: Qur’ani Tukufu inasema: “Mmeandikiwa mmoja wenu anapofikiwa na mauti, kama akiacha mali afanye wosia kwa wazai wake jamaa zake kwa namna nzuri inayopendeza. Ni wajibu haya kwa wachamungu.” (2:180)

Kwa hiyo ilikuwa muhimu kwa Mtume kufanya wosia na kuteua mrithi wake wa mara moja. Wakati alipoona kifo chake kinakaribia kwa nini asifanye wosia wake kama walivyofanya Abu Bakr na Umar?

Muombezi: Kwanza, kwa maneno, “Wakati mmojawenu anapokaribiwa na kifo” je, una maana ya dakika za mwisho za uhai? Katika wakati huo ni aghalabu mtu yeyote kuwa na akili timamu na akawa na uwezo wa kutekeleza majukumu yake kwa makini. Hakika maelezo haya yanaashiria kwenye wakati wa dalili na ishara za uzee, udhaifu na ugonjwa vinapojitokeza.

Pili, kauli yako hii tena imenitonesha hisia zangu na kunikumbusha msiba ambao hauwezi kusahaulika, Mtukufu babu yangu, Mtume wa Allah, alisisitiza umuhimu wa Waislamu kufanya wosia. Alisema: “Yule ambaye atakufa bila kufanya wosia, anakufa kifo cha kijinga, iwapo kutatokea kutokuelewana miongoni mwa warithi.” Wakati wa kipindi chake cha miaka 23 ya maisha ya kijamii alirudia rudia kumtangaza ‘wasi’ wake, yule mtu ambaye Allah alikuwa amemteua kama mwandamizi. Wakati yeye mwenyewe alipokuwa katika kitanda chake alichofia alitaka kurudia kile ambacho amekitangaza mara nyingi sana ili kwamba Umma usije ukapotoshwa na kuangukia kwenye makundi yenye kugombana. Inasikitisha kwamba wanamizengwe wa kisiasa walimpinga na kumzuia kutekeleza wajibu wake wa kidini. Matekeo yake ni kwamba, hata wewe pia unapata fursa ya kuuliza kwa nini Mtume hakufanya wosia.

Kutotiiwa Kwa Amri Ya Mtume Hakuaminiki

Sheikh: Nafikiri maelezo yako haya hayana msingi wa kweli. Kwa hakika hakuna anayeweza kumzuia Mtume kutekeleza wajimu wake. Qur’ani Tukufu kwa uwazi kabisa inasema!: “Chochote anachokupeni Mtume kipokeeni, na chochote kile ambacho anakukatazeni, jiepusheni nacho.” (59:7) Vile vile katika aya nyingine nyingi utii kwa Mtume umefanywa kuwa ni suala la wajibu.

Kwa mfano, Allah anasema: “Mtiini Allah na mtiini Mtume.” Ni dhadhiri kabisa, kukataa kumtii Mtume wa Allah ni ukafiri. Hivyo, Mashaba na wafuasi wa Mtume wasingeweza kumzuia kutangaza wosia wake. Inawezekana hadithi hii ni ya kughushi, ambayo imesambazwa na makafiri kuthibitisha uzembe wa Umma.

Riwaya Sahihi Kuhusu Mtume Kuzuiwa Kuandika Wosia Wake

Muombezi: Tafadhali usijifanye kuwa mjinga. Hii sio riwaya ya kughushi. Ni hadithi inayojulikana, ambayo madhehebu zote za ki-Islamu wanaikubali.

Hata Bukhari na Muslim, ambao walikuwa waangalifu sana kuhusu hadithi yoyote kama hiyo, ambayo ingeweza kutishia maoni yao wenyewe, wamesimulia tukio hili katika vitabu vyao vya hadithi.

Wanaandika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wakati akiwa katika kitanda chake alichofia, aliomba karatasi na wino ili kwamba aweze kutoa maelekezo fulani yaandikwe kwa ajili yao ambayo yangewahifadhi wao wasipotee baada ya kifo chake. Baadhi ya wale waliokuwepo,wakishawishiwa na mwanasiasa, walisababisha vurugu kiasi kwamba Mtume akakasirika sana na akawaamuru waondeke.

Sheikh: Siwezi hata kwa dakika moja kuliamini hili. Nani atathubutu kiasi hicho kuweza kumpinga Mtume wa Allah? Hata kama mtu wa kawaida akitaka kuandika wosia wake, hakuna mtu anayeweza kumzuia.

Vipi mtu ataweza kumzuiya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kufanya wosia wake? Kutomtii yeye ni ukafiri. Kwa vile wosia wa watu wakubwa wa jumuiya ni chanzo cha mwongozo, hakuna mtu ambaye angeweza kuuzuia usitekelezwe. Khalifa Abu Bakr na Umar walifanya wosia wao, na hakuna mtu aliyewazuiya kufanya hivyo. Narudia tena, siiamini riwaya hii.

Muombezi: Unaweza ukaiamini au usiiamini. Kusema kweli kila Mwislamu anashangaa kuisikia. Kila mtu, wa taifa lolote au jumuiya awezayo kuwa, anapigwa na mshangao kusikia tukio kama hili. Ibn Abbas Analia Kwa Sababu Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Alizuiwa Kuandika Wosia Wake

Hili sio suala la huzuni kwako wewe na sisi tu peke yetu. Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) vile vile walisikitikia tukio hili la msiba. Bukhari, Muslim, na maulamaa wengine wakubwa wa madhehebu yenu wamesimulia kwamba Abdullah Bin Abbas mara kwa mara alitokwa na machozi na alisema:

“Oh! Alhamisi ile! Oh! Alhamisi ile! Jinsi gani ilivyokuwa katika Alhamisi ile!” Kisha alilia sana kiasi kwamba ardhi ilitota kwa machozi yake.

Watu walimuuliza ilitokea nini siku ya Alhamisi kinachomfanya alie. Yeye alijibu kwamba, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiwa amelala katika kitanda chake alichofia, aliomba karatasi na wino ili kwamba aweze kuandika wosia, ambao ungewazuia kupotea baada yake, baadhi ya wliokuwepo walimzuia kufanya hivyo na hata walithubutu kusema kwamba Mtume alikuwa anaweweseka (Allah anisamehe!). Alhamisi ile haiwezi kusahauliwa. Hawakumruhusu Mtume kuandika wosia wake na walimuudhi kwa kauli zao.

Umar Alimzuia Mtukfu Mtume Kuandika Wosia Wake

Sheikh: Ni nani aliyemzuia Mtume wa Allah kufanya wosia wake?

Muombezi: Alikuwa ni Khalifa wa pili, Umar Bin Khattab, ndiye ambaye alimzuia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kufanya wosia wake.

Sheikh: Nashukuru sana kwamba umenituliza. Maelezo haya yananisumbua sana. nilikuwa na mwelekeo wa kusema kwamba riwaya hizi zimeghushiwa na Mashi’a, lakini nilinyamaza kwa sababu ya kukuheshimu. Sasa nakuambia kile kilichoko moyoni mwangu. Nakushauri usieneze visa hivi vya kubuni.

Muombezi: Nakushauri usikubali au kukataa mambo bila kuangalia sawa sawa. umefanya haraka isiyo na sababu katika suala hili na umewashutumu Mashi’a wasio na hatia kwa ughushaji.

Vitabu vyenu wenyewe vimejaa riwaya tele ambazo zinaunga mkono haya maoni yetu.

Vyanzo Vya Hadithi Ya “Kuzuiwa Kwa Wosia”

Kama utaviangalia vitabu vyenu wenyewe, utaona kwa maulamaa wenu wenyewe wa kusifika, wamesimulia tukio hili. Kwa mfano, Bukhari, katika Sahih yake, Jz. 2, uk. 118; Muslim, katika Sahih yake (mwishoni mwa Kitab-e-Wasiyya); Hamidi katika Jam’i Bainu’s-Sahihain; Imam Ahmad Bin Hanbal, katika Musnad, Jz. 1, uk. 222; Ibn Abi’l- Hadid, katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 2, uk. 563; Kirmani, katika Sharh-e-Sahih Bukhari; Nuwi katika Sharh-e-Muslim; Ibn Hajar, katika Sawa’iq; Kadhi Abu Ali; Kadhi Ruzbahan; Kadhi Ayaz; Imam Ghazali, Qutbu’d-Din Shafi’i; Muhammad Ibn Abu’l-Karim Shahrastani; Ibn Athir; Hafidh Abu Nu’aim Ispahani; Sibt Ibn Jauzi; na wengine katika maulamaa wenu kwa ujumla wamethibitisha habari hii ya msiba. Wameandika kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anarudi kutoka kwenye hija yake ya mwisho, alishikwa na maradhi. Wakati kikundi cha Masahaba kilipokuja kumuona, alisema: “Nileteeni wino, na karatasi, ili nikuandikieni wosia ambao hautawafanya ninyi mpotee baada yangu.”

Umar Alisema: “Mtu Huyu Anaweweseka, Inatutosha Sisi Qur’ani”

Imamu Ghazali ameandika katika kitabu chake Sirru’l-Alamin, Maqala ya 4, ambapo kwayo Sibt Ibn Jauzi vile vile anainukuu katika kitabu chake Tadhkirat, uk. 36, na wengine wengi wa maulamaa wenu wakubwa wamesimulia kwamba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwataka watu kumletea wino na karatasi, na kwa mujibu wa baadhi ya hadithi alisema: “Nileteeni wino na karatasi ili nikuondoleeni kutoka katika mawazo yenu mashaka yote ya ukhalifa baada yangu; yaani nitakuambieni ambaye anayestahiki ukhalifa baada yangu.”

Kufikia hapa, wao wanaandika, Umar akasema, ‘Muacheni mtu huyu, kwani kwa hakika anaweweseka (Allah anisamehe!); Kitabu cha Allah kinatutosha sisi.’”

Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Anawaamuru Masahaba Wanaozozana Wamuondokee

Baadhi ya Masahaba walikubaliana na Umar, na baadhi wakakubaliana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kulikuwa na ghasia kubwa na rabsha kiasi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Niondokeeni; haifai kwenu kuonyesha hasira mbele yangu.”

Hii ilikuwa ndio vurugu ya kwanza miongoni mwa Waislamu mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika kipindi chake chote cha miaka 23 ya huduma yake ngumu sana. Chanzo cha tatizo hili kilikuwa ni Khalifa Umar, ambaye alipanda mbegu ya kutokuelewana miongoni mwa Waislamu.

Leo wewe na mimi, ndugu wawili katika Uislamu, matoleo yake tunakabiliana wenyewe kwa wenyewe katika upinzani.

Kumuita Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) “Mtu Huyu” Ilikuwa Ni Dharau Kubwa

Sheikh: Haikutegemewa kwa mtu kama wewe kuwa jasiri kiasi hicho cha kuweza kusema maneno ya uzushi kuhusu mtu mkubwa kama Khalifa Umar.

Muombezi: Tuambie iwapo nilionesha ufidhuli wowote katika kusimulia mambo ya kihistoria kutoka kwenye vitabu vyenu wenyewe. Je, unafikiri kwamba Khalifa Umar alikuwa fidhuli wakati alipomzuia Mtume kuandika wosia wake? Je, alikuwa fidhuli wakati alipomkashifu Mtume mbele yake?

Mshairi mmoja amesema kwa usahihi kabisa: “Unaona kibanzi katika macho yangu, lakini huoni boriti kwenye macho yako mwenyewe.” Je, Allah swt. Hasemi kwamba: “Muhammad si baba wa yeyote katika watu wenu, bali ni Mtume wa Allah na mwisho wa Mitume?” Jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lazima siku zote litajwe kwa heshima ipasayo na kwa staha. Lazima aitwe “Mtume wa Allah” au “Mwisho wa Mitume.”

Lakini Umar hakuonesha heshima juu ya amri hii ya Mungu, badala yake akamuita Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama “mtu huyu.” Sasa hebu sema kwa jina la Allah iwapo hiyo dharau ilitendwa na mimi au na Khalifa?

Neno ‘Hajar’ Lililotumiwa Na Umar Lina Maana Ya Kuweweseka

Sheikh: Kwa nini unasema kwamba Hajar maana yake ni kuweweseka?

Muombezi: Wafasiri wote na maulamaa wenu wakubwa wanatoa maana ya Hajar kama ni kuweweseka. Kwa mfano, Ibn Athir katika kitabu chake Jam’u’l-Usul, Ibn Hajar katika Sharh-i-Sahih Bukhari, na waandishi wengine wa ukusanyaji wa hadithi wanatoa maana hiyo hiyo. Mabwana waheshimiwa! kama mtu anasema “mtu huyu anaweweseka” kuhusu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah, je, hakuvunja adabu na amri ya Qur’ani?

Dharau Dhidi Ya Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Ni Ukafiri

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa hakupoteza utume wake wala uma’sum wake. Kama mtu atatafsir maneno yake kama “kuweweseka,” je hiyo haimaanishi kwamba mtu kama huyo hamuamini Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Sheikh: Je, ni sahihi kwa kutambua cheo chake kama Khalifa kumuona ni mwenye makosa kwa kusema kwamba hakumuamini Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Muombezi: Wakati unaposikia kwamba Mtume anashutumiwa kwa kuweweseka huna kipingamizi. Lakini mtu aliyekalia ofisi ya ukhalifa akitajwa na maulamaa wenu wengi kwamba alimkashifu Mtume, kwa mara moja unawatia Mashi’a kwenye makosa, badala ya kuyaweka makosa ambako kwa haki yanastahili.

Maulamaa wenu wenyewe kama Kadhi Ayaz Shafi’i katika Kitab-e-Shifa; Kirmani katika Sharh-e-Sahih Bukhari, na Nuwi katika Sharh-e-Sahih Muslim wameandika kwamba mtu ambaye ametumia maneno haya kwa uwazi hana imani kwa Mtume wa Allah.

Hivyo kama mtu yeyote akimpinga Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hususan kwa maneno ya matusi au akisema kwamba alikuwa akiweweseka, tunaona dhahiri kabisa kwamba alikuwa hana imani kwa Mjumbe wa Allah.

Fitina Ya Kwanza Katika Uislamu Mbele Ya Mtukufu Mtume (S.A.W.W.)

Unaniuliza ni kwa nini ninamlaumu kwa kusababisha kutokuelewana miongoni mwa watu. Maulamaa wenu wenyewe wamelikubali jambo hili. Mwanachuoni mkubwa Husein Meibudi anasema katika Sharh- e-Diwan kwamba ghasia za katika Uislamu kutokea kwa mara ya kwanza mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe, wakati alipokuwa katika kitanda chake alichofia. Matatizo yalianza wakati Umar alipomzuia Mtume kuandika wosia wake Shahrasan anasema katika kitabu chake Milal wa Nihal, Muqaddama ya 4 kwamba upinzani kati ya makundi mawili ya Waislamu ulianza wakati Umar alipokataa kuruhusu wino na karatasi kuletwa kwa Mtume kitandani kwake alipofia. Ibn Abi’l-Hadid alithibitisha ukweli huu katika kitabu chake Sharh-e-Nahju’l-Balagha Jz. 2, uk. 563.

Je, Mtume Angeweza Kuzungumza Upuuzi?

Sheikh: Kama Khalifa Umar amesema maneno haya, sioni kwamba ni kukosa heshima. Wakati mtu anaumwa sana anaweza kuweweseka. Kama akizungumza maneno yasioeleweka, tunaweza kuyaita mazungumzo yake kama ni ya kuweweseka. Katika hali hii hakuna tofauti kati ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na watu wengine.

Muombezi: Unatambua sana kwamba Mitume wote ni ma’sum na kwamba tabia hii hubakia mpaka kufa. Mtume Muhammad kwa hakika alikuwa ma’sum katika tukio hili wakati aliposema alitaka kuwakinga watu wake kutokana na kupotea baada ya kifo chake.

Kama utaziangalia aya tukufu za Qur’ani ambazo zinasema: “Na hasemi kwa matamanio (yake); hayo (maneno) bali ni wahyi ulioshushwa (kwake).” “Na lazima mfanye yale aliyoyaamrisha Mtume juu yenu…” “Na mtiini Allah na mtiini Mtume…”, wewe mwenyewe kwa uwazi utaelewa kwamba kuzuia wino na karatasi kuletewa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa hakika ilikuwa ni upinzani kwa Allah. Huo ni ukweli unaokubali- ka kwamba neno kuweweseka lilikuwa ni tusi la wazi, na Khalifa kumuita kama “mtu huyu” bado lenyewe ni tusi zaidi.

Maneno “Mtu Huyu Anaweweseka” Yalikuwa Ni Matusi Zaidi

Sasa ningependa uniambie ungejisikia vipi kama mtu katika mkutano huu, atakuashiria wewe aseme “mtu huyu anaweweseka.” Wewe na mimi hatuko huru kutokana na makosa na tunaweza kuweweseka. Je, utaiita hiyo ni tabia nzuri au ni kutukana? Kama mazungumzo ya namna hii ni ya matusi katika hali hii, itakubidi ukubali kwamba ufidhuli wowote kama huo dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ulikuwa ni matusi ya hali ya juu. Na hakuna mtu anayeweza kukataa ukweli kwamba ni wajibu wa kidini wa kila Mwislamu kuwa mbali na mtu ambaye tabia yake kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ya kuchukiza na kifidhuli kiasi hicho, wakati Allah amemuita katika Qur’ani Mtume Wake na Mwisho wa Mitume.

Kama utaachilia mbali chuki zako, je, akili zako za kawaida zitasema nini kuhusu mtu ambaye badala ya kumuangalia Mtume kama Mtume wa Mungu na Mwisho wa Mitume, anasema “mtu huyu anaweweseka?

Khalifa Hawezi Kutolewa Lawamani Kwa Kumkosea Adabu

Mtukufu Mtume (S.A.W.W.)

Sheikh: Tuchukulie tunakubali kwamba alikuwa katika makosa. Lakini kwa vile alikuwa Khalifa wa Mtume na alitekeleza busara zake kwa ajili ya usalama wa dini, alikuwa yuko huru kutokana na lawama zote.

Muombezi: Kwanza, kauli yako kwamba kwa vile alikuwa Khalifa na alitekeleza busara zake hayapasiki kabisa, kwa sababu katika siku ambayo alisema maneno hayo, yeye hakuwa Khalifa. Huenda pengine alikuwa hata hajauota.

Pili, kauli yako kwamba alitekeleza busara zake vile vile inashangaza. Je, hukufikiria kwamba mbele ya amri ya wazi, busara haina nafasi? Kwa kweli ni kosa ambalo kwamba mtu hawezi kusamehewa.

Tatu, umesema kwamba amefanya hivyo kwa ajili ya usalama wa dini. Kwa hakika inashangaza sana ulamaa kama wewe kuweza kupoteza hisia zote za uadilifu.

Ni Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Aliyekuwa Akihusika Na Usalama Wa

Dini Na Sio Umar.

Bwana mheshimiwa! Nani aliyekuwa na wajibu wa kuihifadhi dini – ni Mtme wa Allah au Umar Bin Khattab? Je, akili yako ya kawaida inakubali hoja ya kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) (baada ya kuelezea masharti ya “Hamtapotea baada ya kuandika wosia huu”) hakuweza kuelewa kwamba kuandika wosia kulikuwa ni kinyume cha dini, au kwamba Umar alikuwa akiilewa vizuri zaidi na akamzuia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuandika wosia huu? Kushangaza kulikoje! Unajua vizuri kabisa kwamba utokaji nje wowote kwenye misingi ya dini ni dhambi kubwa, na haiwezi kusahemeka.

Sheikh: Hapana shaka kwamba Khalifa Umar alizitathmini hali na mazingira ambayo yalikuwepo katika dini na akafikia uamuzi kwamba kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ataandika kitu chochote, ingesababisha hitilafu kubwa na machafuko. Hivyo ilikuwa kwa ajili ya msaada na faida ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe kwamba alizuia asipelekewe wino na karatasi.

Muombezi: Madhumuni ya hoja yako yanaelekea kuwa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye alikuwa ma’sum, wakati alipokuwa anaulekeza Umma huu, alikuwa hana habari ya kutosha ya uwezekano wa mgogoro baada ya kifo chake, na kwamba Umar alimuongoza katika sula hili. Lakini Qur’ani inatuambia: “Haiwi kwa muumini mwanamume wala muumini mwanamke kuwa na hiari katika jambo, Allah na Mtume Wake wanapokata shauri katika jambo lao. Na mwenye kumuasi Allah na Mtume Wake, basi hakika amepotea upotofu ulio wazi.” (33:36)

Khalifa Umar aliasi amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa kumzuia kuandika wosia wake. Aidha alikuwa fidhuli kwa kusema kwamba Mtume alikuwa anaweweseka. Ufidhuli huu uliumiza hisia za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kiasi kwamba aliwaambia watu waondeke mbele yake.

Qur’ani Tukufu Peke Yake Haitoshi Kwa Ajili Ya Mwongozo Wetu

Sheikh: Lakini nia nzuri ya Khalifa iko dhahiri katika maneno yake ya mwisho, “Kitabu cha Allah kinatutosha sisi (yaani, hatukuwa na haja ya maandishi ya Mtume wa Allah).”

Muombezi: Kwa hakika, maneno haya ndiyo uthibitisho mzuri wa ukosefu wake wa imani na kutokuijua kwake Qur’ani Tukufu. Lau angelijuwa ukweli wa Qur’ani Tukufu angelijua kwamba Qur’ani peke yake haitoshi kwa mambo yote.

Imeweka kanuni za msingi, lakini maelezo kwa urefu yameachwa kwa watarjuma na wafasiri wake. Qur’ani ina amri ambazo ni zenye kuendelea – (nasikh), na zilizofutwa - (mansukh), za jumla (‘am), haswa - mahususi (khass), zenye mipaka (muqayyad), zenye utata (mutashabih), halisi (mutlaq), mukhtasari (mujmal), au wazi (Mu’awwil).

Itawezekana vipi kwa mtu wa kawaida kupata maana kamili kutoka kwenye hii Qur’ani bila msaada wa baraka za kimungu na tafsiri iliyotolewa na wafasiri wake? Kama Qur’ani peke yake ilikuwa inatosha kwa ajili ya Umma, kwa nini aya hii iliteremshwa: “Lazima mfanye yale aliyowaamrisha Mtume kufanya; na lazima mjiepushe na yale ambayo amekukatazeni.” Allah vile vile anasema katika Qur’ani Tukufu: “…na kama wangelilipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, bila shaka wale wanaochunguza miongoni mwao wangeliweza kulijua…” (4:83)

Kwa hiyo ina maana kwamba Qur’ani peke yake isingeweza kukidhi madhumuni yake bila ufafanuzi wa wafasiri wake, yaani, Muhammad na kizazi chake kitoharifu. Hapa tena ninaweza kurejea tena kwenye hadithi inayokubaliwa na wote (ambayo niliinukuu pamoja na baadhi ya vyanzo vyake katika mikesha iliyopita) ambayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameirudia hata katika wakati wake wa kufariki akisema:

“Ninaacha nyuma yangu Vitu Viwili Vizito: Kitabu cha Allah na Ahlu’l-Bayt wangu. Kama mtashikamana katika viwili hivi kamwe, kamwe hamtapotea baada yangu; kwani hakika Viwili hivi, kamwe havitaachana vyenyewe kwa vyenyewe mpaka vinifikie katika chemchemu ya Kauthar.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alikuwa akipewa msukumo na Allah, hakuiona Qur’ani kwa kujitenga pekee kuwa ni yenye kutosha kwa ukombozi wetu. Alisema kwamba ni lazima tushikamane na Qur’ani na Ahlul’l-Bayt kwa vile (viwili hivyo) visingetengana mpaka Siku ya Hukumu, na kwamba hivi vilikuwa ni vyanzo vya mwongozo kwa ajili ya watu. Lakini Umar akasema kwamba Qur’ani peke yake inatutosha sisi. Hii inaonyesha kwam- ba hakukitupa tu kizazi kitoharifu bali pia aliikataa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Qur’ani Tukufu Vile Vile Hutuambia Tuwatake Ushauri Ahl Dhikr,

Yaani Ahlul-Bayt

Tunapaswa kumtii nani katika suala hili? Hakuna mtu mwenye akili ambaye atasema kwamba tuiache kando amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumfuata Umar. Basi kwa nini mmekubali maoni ya Umar, mkapuuza amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Kama Kitabu cha Allah kilikuwa kinatosha, kwanini tumeamriwa kuwauliza watu wa dhikir, kama Qur’ani Tukufu inavyosema: “…Basi waulizeni wenye kufahamu ikiwa ninyi hamjui.” (16:43)

Ni wazi kwamba ‘dhikr’ maana yake ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au Qur’ani Tukufu na ‘watu wa dhikr’ maana yake Ahlu’l-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Nilikwishafafanua katika mikesha iliyopita pamoja hoja halali na vyanzo sahihi kwamba maulamaa wenu wakubwa kama, Suyuti na wengine, wamesimulia kwamba “watu wa dhikr” maana yake Ahlul’l-Bayt.

Kukataliwa Maneno Ya Umar Na Qutbud-Din Shirazi

Qutbu’d-din Shirazi ambaye ni mmoja wa wanachuoni wenu wakubwa, anasema katika kitabu chake “Kashfu’l-Ghuyub”: “Ni ukweli unaokubalika kwamba hatuwezi kufanya maendeleo katika njia bila ya mwongozo. Tunashangaa madai ya Khalifa Umar kwamba, kwa vile tunayo Qur’ani kati yetu, hatuhitaji mwongozo wowote. Ni kama vile mtu akise- ma kwamba, kwa vile tunavyo vitabu vya madawa, basi hatuhitaji mganga.

Ni dhahiri kabisa utetezi huu ni wa uongo, kwa sababu mtu ambaye hawezi kutatutua tatizo lake kwa kusoma vitabu vya madawa, lazima amuone mganga kwa ushauri. Hali inakuwa hiyo hiyo katika suala la Qur’ani Tukufu. Kila mtu hawezi kupata faida kutoka kwenye Qur’ani Tukufu kwa uwezo wake mwenyewe. Lazima awaendee wale wenye elimu ya Qur’ani Tukufu.”

Qur’ani Tukufu inasema: “…Na lau kuwa wangelipeleka kwa Mtume na kwa wenye mamlaka kati yao, wale wanaochunguza wangelijua…” (4:83) Kusema kweli kitabu halisi ni moyo wa mtu ambaye ana elimu, kama Qur’ani Tukufu inavyosema: “Bali hii (Qur’ani) ni Aya zilizo wazi katika vifua vya wale waliopewa elimu…” (29:49)

Kwa sababu hiyo Ali alisema: “Mimi ni Kitabu cha Allah kinachozungumza, na hii Qur’ani ni Kitabu kilicho kimya.” Hivyo kwa mujibu wa watu wenye elimu Umar alikosea. Ilikuwa ni dhulma kubwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah kwamba alizuiwa kuandika wosia wake.

Abu Bakr Hakuzuiwa Kuandika Wosia Wake

Amma kuhusu madai yako ya kurudia rudia kwamba Abu Bakr na Umar hawakuzuiwa kuandika wosia wao, nakiri kwamba ni kweli. Inashangaza, kwa vile wanahistoria na wanahadith wote wameandika katika vitabu vyao sahihi, kwamba Khalifa Abu Bakr, wakati wa kufariki kwake, alimuambia Uthman bin Affan aandike kile anachosema.

Ilikuwa ni wosia wake. Aliandika kila alichoambiwa na Abu Bakr. Umar na wengine vile vile walikuwepo katika tukio hilo. Hakuna aliyepinga. Umar hakusema: “Kitabu cha Allah kinatutosha sisi; hatuhitaji wosia wa Abu Bakr.” Lakini hakumruhusu Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kuandika wosia wake.

Hii inaonesha kwamba tabia hii chafu na kumzuia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuandika wosia wake haikuwa chochote bali ni njama za kisiasa. Ibn Abbas alikuwa na haki kabisa ya kulia. Ulimwengu wote wa ki-Islamu unapaswa kutoa machozi ya damu. Kama Mtume angelipewa nafasi ya kuandika wosia wake, suala la ukhalifa lingetatuliwa kwa uwazi kabisa. Matangazo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyokuwa akiyatoa huko nyuma yangelithibitishwa. Lakini wanasiasa waliasi dhidi yake na kumzuia.

Sheikh: Kwanini unadai kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kusema kitu kuhusu ukhalifa?

Muombezi: Kabla ya kufariki kwa Mtume, sheria zote za dini zilikuwa zimewekwa wazi. Aya ya “Ukamilisho wa Dini” imelifanya hili kuwa wazi. Naam, kwa hakika suala la ukhalifa lilikuwa katika hali ambayo kwamba alitaka kuhakikisha kwamba kusingekuwa na utatanishi kuhusiana nalo.

Nilikwisha kuambieni kwamba Imamu Ghazali katika kitabu chake “Sirru’l-Alamin (Maqala ya 4) ameandika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Nileteeni wino na karatasi ili niweze kuwaondolea mashaka yoyote mawazoni mwenu kuhusu ukhalifa na kwamba niweze kurudia kuwaambieni ni nani anastahiki cheo hicho.”

Maneno yake “Ili kwamba msije mkapotea baada yangu” yanathibitisha kwamba lengo la wosia wake lilikuwa ni mwongozo wa Umma. Katika suala la mwongozo, hakuna msisitizo uliohitajika isipokuwa katika kuhusiana na ukhalifa na uimamu.

Mbali na hili hatusisitizi nukta ya kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitaka kusema kitu kuhusu huo ukhalifa au uimamu. Kwa hakika alitaka kuandika kitu kuhusiana na mwongozo wa watu ili kwamba wasije wakapotea baada yake. Basi kwa nini hakuruhusiwa kuandika wosia wake? Hata kama tukichukulia kwamba kumzuia kufanya hivyo ilikuwa sahihi, je ilikuwa ni lazima vile vile kumfedhehesha na kumtukana?

Hivyo Ni Wazi Kwamba Ali Alikuwa Mrithi Wa Mara Moja Wa

Mtukufu Mtume (S.A.W.W.)

Mambo haya yanafanya kuwa wazi kabisa kwamba Ali alikuwa mrithi wa mara moja wa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.). Ingawa Mtume alitangaza mara kwa mara jambo hili huko nyuma, alitaka katika hatua hii ya mwisho kuiandika katika wosia wake ili kwamba majukumu ya umma yaweze kuwa salama. Lakini wanasiasa walijua alichotaka kufanya kwa hiyo wakamzuia kufanya hivyo na wakamfedhehesha.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Mtume alisisitiza katika hadithi nyingi kwamba Allah (swt) aliteua waandamizi wa mitume: Adamu, Nuh, Musa, Isa na wengine, na kwamba alimteua Ali kama mwandamizi kwa jili yake. Vilevile alisema Ali ni mrithi na mwandamizi wangu wa mara moja baada yangu katika Ahlu’l-bayt na umma wangu.”

Sheikh: Kama riwaya hizi zitachukuliwa kuwa kweli, basi hazikusimuliwa kwa mwen- delezo kamili. Vipi utaweza kupata chanzo kutoka kwenye riwaya hizo?

Muombezi: Makubaliano ya maoni kuhusu wosia wa Mtume kwa mujibu wetu yanathibitishwa na maelezo ya kizazi kitukufu cha Mtume. Aidha, utakumbuka kwamba nilikuelezeni katika mikesha iliyopita kwamba maulamaa wenu huichukulia riwaya ya pekee kama sahihi. Mbali na hilo katika riwaya hizi, kama hakuna mapatano haswa ya maneno, basi kwa hakika kuna kupatana kwa maana ya jumla.

Hadithi Ya ‘La Nurith,’ Yakataliwa.

Mbali na hayo, unaambatanisha umuhimu usio na sababu kwenye mwendelezo wa riwaya (Mutawatir). Wakati unaponyamazishwa na hoja zetu, unakimbilia nyuma ya haja ya mutawatir. je unaweza kuthibitisha umutawatir wa hadithi ya “la nurith?” (hatuachi warithi)?

Wewe mwenyewe unakiri kwamba msimuliaji wa hadithi hii alikuwa ni Abu Bakr au Aus Bin Hadasan. Lakini mamilioni ya wana-tawhiid na Waislamu wanyofu katika kila zama wameikataa hii inayoitwa ati ni hadithi. Uthibitisho mzuri wa uwongo wa hadhithi hii, ni kwamba alikataliwa na lango la elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali na kizazi chote cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Watu hawa walidhibitisha kwamba hadithi hii ilikuwa ni ya kubuni. Kama nilivyokwisha sema awali, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kwa kila Mtume kuna mwandamizi na mrithi, hakika Ali ni mwandamizi na mrithi wangu” Ukhalifa Ni Mali Ya Mrithi Wa Elimu

Kama unasema kuwa urithi wao hakuwa na maana ya urithi wa mali bali ule wa elimu (ingawa imethibitishwa kwamba walimaanisha urithi wa mali) hoja yangu inakuwa dhahiri zaidi. Mrithi wa elimu wa Mtume alistahili cheo cha ukhalifa zaidi kuliko mtu yeyote kati ya wale ambao hawakuwa na elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Pili, Imethibitisha kuwa Mtume alimfanya Ali kuwa mwandamizi na mrithi wake wa mara moja, kwa mujibu wa hadithi ilivyosimuliwa na maulanaa wenu wenyewe. Allah alimteua kwenye cheo hiki. Je,ingewezekana kweli Mtume kupuuza kumtaja mwandamizi na mrithi wake? Aidha inashangaza kwamba katika kutatua masuala yanayohusiana na sheria za dini, Abu Bakr na Umar walikubali uamuzi wa Ali. Maulana wenu wenyewe na wana historia wameziandika hukumu zilizotolewa na Ali wakati wa uhalifa wa Abu Bakri, Umar na Uthman.

Hafidh: Inashangaza sana kwamba unadai kuwa makhalifa hakujua sheria za dini na kwamba Ali alikuwa akiwakumbusha mara kwa mara.

Mwombezi: Hakuna cha kushangaza kuhusu hilo. Kuzijua zote zote ni vigumu sana. Isingewezekana kwa mtu kuwa na elimu kamilifu kama hiyo isipokua kama angekuwa ni Mtume wa Allah au lango la elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Maulamaa wenu wenyewe wakubwa wamesimulia mambo haya kwenye vitabu vyao sahihi. Ninatoa mfano ili kwamba watu wasiojua wasije wakadhani tunasema mambo hayo ili kuwaudhi wao.

Hukumu Ya Ali Kuhusu Mwanamke Ambaye Alizaa Mtoto Baada Ya Ujauzito Wa Miezi Sita

Imamu Ahmad Hanbal katika Musnad yake; Imamul-Haram Ahmad bin Abdullah Shafi’i katika kitabu chake Dhakha’ir-e-Uqba; Ibn Abil-Hadid katika Sharh-e-Nahaju’l-Balagha; na Sheikh Suleiman Hanafi katika kitabu chake Yanabiu’l-Mawadda, sura 56, akinukuu kutoka kwa Ahmad Bin Abdullah; Ahmad bin Hanbal; Qala’i na Ibn Saman wanasimulia tukio lifuatalo:

Umar alitaka kumpiga mwanamke mawe kwa sababu alizaa mtoto baada ya ujauzito wa miezi sita. Ali akasema, “Allah anasema ndani ya Qur’ani tukufu kwamba ule muda, kuanzia kushika mimba, mpaka muda ulioagizwa wa kunyonyesha unachukua kipindi cha miezi thelathini. Kwa vile kipindi cha kunyonyesha ni miaka miwili, muda wa ujauzito ni miezi sita.” Hivyo Umar akamwachia huru yule mwanamke na akasema, ‘Kama Ali asingekuwepo hapa Umar angeangamia.’”

Katika sura hiyo hiyo ananukuu kutoka kwenye Manaqib ya Ahmad Bin Hanbali: “Wakati Umar anapokabiliwa na tatizo gumu na akawa hawezi kulielewa, alitegemea juu ya ujuzi wa Ali” Idadi ya matukio kama haya yalitokea wakati wa ukhalifa Abu Bakr na Uthman. Wakati watakapotatazika katika matatizo fulani, walimwita Ali kama mwamuzi wa halali. Wao wenyewe walitenda kwa mujibu wa uamuzi wake. Sasa unaweza kushangaa kwa nini hawakuukubali ushahidiwa Ali katika suala la Fadak. Sasa katika suala lile walichagua kufuata matamanio yao na wakaipora haki ya Fatima.

Hadithi Ya ‘La Nurath,’ Haikutumika Kwenye Mali Nyingine

Hoja ya tatu kudhibitisha uwongo wa hadithi hii ni maelezo na kitendo cha Abu Bakr mwenyewe. Kama hadithi hii ingelikuwa sahihi vitu vyote ambavyo Mtume ameviacha vingekuwa vimetwaliwa. Na warithi wasingekuwa na haki katika vitu vyote alivyoviacha, lakini Abu Bakr alitoa nyumba ya Fatima na kumpa yeye (Fatima) na vilevile akatoa nyumba za wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuwapa Aisha, Hafsa na wengine kama urithi wao.

Kurudisha Abu Bakr Fadak Kwa Fatima Na Kuingilia Kati Kwa Umar.

Mbali na haya, kama hadithi hii ilikuwa sahihi na kama Abu Bakr aliamini kuwa ni amri ya Mtukufu, basi kwa nini, baada ya kuitwaa Fadak (ambayo aliichukulia kwamba ni sada- ka inayo wahusu Waislamu) aliandika hati kwamba mali hiyo irudishwe kwa fatima? Baadae Khalifa Umar aliingilia kati na kuichanachana hati ile.

Hafidhi: Haya n maelezo ya pekee. Sijawahi kusikia kwamba Khalifa aliirudisha Fadak. Ni kipi chanzo cha taarifa hii?

Muombezi: Mpaka sasa utakuwa unaelewa kwamba kamwe sifanyi madai yoyote ambayo siwezi kulitetea kwa ukamilifu. Ibn Abi’l Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha na Ali Bin Burhanud-Din Shafi’i katika kitabu chake Ta’rikh Siratu-l-Halabiyya Jz. 3, uk. 391 anaandika kwamba Abu Bakr alitokwa na machozi kwa ajili ya hotuba ya Fatima yenye kutia hamasa.

Alilia kwa sababu ya masaibu ya Fatima na hatimaye aliandika hati akieleza kwamba mali hiyo inarudishwa kwake Fatima. Lakini Umar akaichana hati hati ile. Hata hivyo inashangaza zaidi kwamba Umar huyo huyo, ambaye wakati wa ukhalifa wa Abu Bakri alipinga kurudisha kwa Fadak, yeye aliirudisha kwa warithi wake wakati wa ukhalifa wake. Kadhalika makhalifa wa Amawi na Bani Abbas vilevile waliirudisha kwa warithi wa Fatimah.

Hafidhi: Unachosema kwa kweli kinashangaza. Inawezekana vipi kwamba Khalifa Umar, ambaye kwa mujibu wa maelezo yako, yeye alipinga vikali sana kurudishwa kwa Fadak kwa Fatima, leo aliirudisha kwa warithi wa Fatima?

Muombozi: Kwa hakika inashangaza mno. Nawasilisha kwa ruhusa yako, riwaya za ulamaa wenu wenye sifa kutoka kwa makhalifa ambao waliirudisha na kuichukua tena Fadak. Kurudisha Fadak Kwa Khalifa Kwa Kizazi Cha Fatimah

Mwanahadithi na mwanahistoria ajulikanaye sana wa Madina, Allama Samhudi (alikufa 911A.H.) katika kitabu chake “Ta’rikhu’l-Madina” na Jaqut Bin Abdullah Rumi katika kitabu chake Mu’ajamul-Buldan, wanaeleza kuwa wakati wa ukhalifa wake, Abu Bakri alichukua umiliki wa Fadak. Umari wakati wa utawala wake akairuidisha kwa Ali na Abbas.

Kama Abu Bakr aliihodhi kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akachukulia kama ni mali ya Waislam, ni kwa kanuni ipi ambayo Umari aliaminisha mali ya Waislamu wote kwa mtu mmoja binafsi?

Sheikh: Pengine nia yake katika kuitoa mali hiyo kwa mtu binafsi, ilikuwa kwamba itabakia katika hifadhi ya Waislamu.

Muombezi: Wakati mwingine shahidi anakuwa mwereru zaidi kuliko mdaiwa ambaye anamtolea ushahidi. Khalifa hukuwa na mawazo kama hayo. Kama mali hiyo ilirudishwa kwa ajili ya matumizi Waislamu, ingeandikwa hivyo katika historia. Lakini wanahistoria wenu wakubwa wanaandika kuwa ilitoewa kwa manufaa ya Ali na Abbas. Ali alipokea Fadak kama mrithi wake wa haki, sio kama Mwislamu binafsi. Mwislamu mmoja hawezi kumiliki mali ya Waislamu wote.

Kurudishwa Fadak Na Umar Ibn Abdul-Aziz

Sheikh: Pengine rejea hiyo ni kwa Umar Ibn Abdul-Aziz.

Muombezi: Ali na Abbas hawakuwa hai wakati wa Umar Ibn Abdu’l-Aziz. Hiyo ni hadithi nyingine tofauti. Allama Samhudi katika kitabu chake Ta’rikhul-Madina na Ibn Abil-Hadid katika kitabu chake Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 4, uk. 81, anasimulia kutoka kwa Abu Bakr Jauhari kwamba wakati Umar Bin Abdu’l-Aziz alipochukuwa nafasi ya ukhalifa alimwandikia Gavana wake wa Madina kurudisha Fadak kwa kizazi cha Fatima. Kwa hiyo alimwita Hasan bin Hasanu’l-Mujtaba (na kulinga na riwaya nyingine alimuita Imam Ali Ibnu’l- Husein) na akairudisha fadak kwake. Ibn Abi’l-Hadid anaandika kuhusu hili katika kitabu chake Sharh- e-Nahju’l-Balagha, Jz. 4, uk. 81 katika maneno yafuatayo:

“Hii ilikuwa mali ya kwanza ambayo iliporwa kinyume cha sheria na kisha ilitolewa na kupe- wa kizazi cha Fatima na Umar Bin Abdu’l-Aziz.” Ilibakia katika miliki yao kwa muda mrefu mpaka Khalifa Yazid Ibn Abdu’l-Malik alipoipora tena. Kisha Bani Umayya wakaikalia. Wakati ukhalifa ulipokwenda kwa Bani Abbas, Khalifa wa kwanza wa Bani Abbas, Abdullah Saffa, alitoa Fadak kwa watoto wa Imam Hasan ambao waligawanya mapato yake kwa mujibu wa haki za urithi, kwa kizazi cha Fatima. Kurudishwa Fadak Kwa Kizazi Cha Fatima Na Abdullah Mahdi Na

Mamun Bani Abbas

Wakati Mansur alipowatesa watoto wa Imam Hasan, aliipora Fadak kutoka kwao tena. Wakati mwanae Mahdi alipokuwa Khalifa, aliirudisha tena kwao. Wakati Musa bin Hadi alipokuwa Khalifa aliipora tena Fadak. Mamunu’r-Rashidi wa Bani Abbas alipokichukua kiti cha ukhalifa aliagiza Fadak kutoewa kwa kizazi cha Ali. Yaqut Hamawi ananukuu maagizo ya Mamun katika kitabu chake Mamun katika kitabu chake Mu’ajamu’l Buldan.” Mamun aliandika kwa Gavana wake wa Madina: “Hakika, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allah aliitoa Fadak kwa binti yake Fatima. Ukweli huu umethibitishwa na kujulikana wazi kwa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Mshairi ajulikanae sana, Di’bal Khuza’i, alikuwepo pia wakati huo. Alisoma baadhi ya mashairi, la kwanza ambalo likiwa na maana: “Leo wote tunayo furaha na shangwe. Mamum amerudisha fadak kwa Bani Hashim.”

Uthibitisho Kwamba Fadak Ilitolewa Kwa Fatima

Imimethibitishwa na hoja zisizokanushika kwamba Fadak ilitolewa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kumpa Fatima. Iliporwa bila haki yoyote. Lakini makhalifa wa baadae, katika misingi ya uadilifu au mitazamo ya kisiasa waliirudisha kwa kizazi cha Bibi yule aliyeonewa.

Hafidh: Kama Fadak ilitolewa kwake kama zawadi, kwa nini aliidai kama urithi na asiseme chohote kuhusu zawadi?

Muombezi: Kwanza aliidai kama zawadi. Lakini mashahidi walipohitajika kutoka kwa mmiliki wa mali, kinyume na mafundisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Uislamu, alitoa mashahidi. Ushahidi wao ulikataliwa. Hivyo alilazimika kutafuta kinga chini ya sheria ya mirathi.

Hafidhi: Nina wasiwasi umekosea. Hatujaona kumbukukmbu yoyote ya madai ya Fatimah kwamba Fadak ilikuwa zawadi.

Muombezi: La, sijakosea. Jambo hili halikusimuliwa kwenye vitabu vya Shi’a tu, bali pia katika vile vilivyoandikwa na maulama wenu wakubwa. Imeandikwa katika Siratu’l- Halabiyya, uk. 39, kilichokusanywa na Ali Bin Burhanud-Din Halabi Shafi’i (amekufa 1044 A.H) kwamba kwanza Fatima alipingana na Abu Bakr kwamba yeye (Fatima) alimiliki Fadak na kwamba yeye alipewa na Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.). Kwa vile ushahidi ulikataliwa alilazimika kudai haki yake kwa mujibu wa sheria za mirathi. vilevile Fakhru’d-din Razi katika “Tafsiri-e-Kabir” kuhusu madai ya Fatimah; Yaqut Hamwani katika kitabu chake Mu’ajamu’l-Buldan; Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali katika Sharh-e- Nahjul- Balagha, Jz. 4, uk. 80, kutoka kwa Abu Bakr Jauhari na yule shupavu Ibn Hajar katika Sawa’iq-e- Muhriqa, uk. 21, chini ya kichwa cha maneno Shuhubhati-e-Rafza, Shubha ya 7, anasimulia kwamba dai la kwanza la Fatimah lilikuwa kwamba Fadak ilikuwa zawadi. Wakati mashahidi wake walipokataliwa aliudhika sana na akasema kwa hasira kwamba hatazungumza tena na Abu Bakr na Umar.

Na hivyo ndivyo ilivyokuwa - hakuwaona tena na wala hakusema nao. Wakati wa kifo chake ulipokaribia alielezea bayana katika wosia wake kwamba asihudhurie hata mmoja wao katika sala yake ya jeneza. Ami yake Abbas, aliendesha ibada ya mazishi, na akazik- wa usiku. Kwa mujibu wa vyanzo vya Shi’a na kwa mujibu wa maelezo ya Maimam watukufu, Ali ndiye aliendesha ibada ya mazishi.

Hoja Kwamba Abu Bakr Alitenda Kwa Mujibu Wa “Aya Ya Ushahidi”

Na Majibu Yake.

Hafidhi: Naam kwa kweli hapana shaka kwamba Fatimah alikasirika sana, lakini Abu Bakr Siddiq si wakulaumiwa sana. Aliwajibika kutenda kwa mujibu wa sheria za kidini zilizowazi. Kwa vile “aya ya ushahidi” ni ya umuhimu wa jumla, na mdai lazima alete wanaume wawili au mwanaume mmoja na wanawake wawili au wanawake wanne kama mashahidi, na kwa vile katika suala hili idadi ya mashadi ilikuwa haitoshi, Khalifa asingeweza kutoa hukumu inayompendelea Fatima.

Muombezi: Hafidhi Sahib amesema kwamba Khalifa aliwajibika kutenda kwa mujibu wa sheria za dini, na kwa vile ushaidi kamili haukupatikana hakuweza kutoa hukumu. Nitajibu nukta hii, na naomba ninyi muwe waadilifu katika kupima kauli yangu.

Kudai Mashahidi Kutoka Kwa Wamiliki Ilikuwa Ni Kinyume Cha Sheria

Kwanza ulisema Abu Bakr ‘alilazimika chini ya sheria za kidini.’ Unaweza tafadhali ukaniambia ni amri ipi ya dini inayohitaji mashahidi kutoka kwa mtu ambaye amiliki mali? Imethibitishwa kwamba Fatimah alikuwa katika umiliki wa Fadak.

Kama ilivyoelezwa na maulamaa wenu wote, kuhitaji mashahidi kwa Abu Bakr kutoka kwa Fatima ilikuwa kinyume cha sheria za dini. Je, sheria zetu za dini hazisemi kwamba ushahidi lazima utolewe na mlalamikaji na sio yule mwenye kushikilia mali? Pili, hakuna anayekataa ile maana ya jumla ya aya ya ushahidi, lakini pia ina maana makhususi.

Hafidh: Una maanisha nini kwa maana yake makhususi?

Muombezi: Ushahidi wa hili ni riwaya iliyoandikwa katika vitabu vyenu sahihi vya hadithi, kuhusiana na Khazima Ibn Thabit. Alitoa ushahidi katika kumuunga mkono Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika kesi inayohusiana na uuzaji wa farasi. Mwarabu mmoja alitoa madai dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na ushahidi wake (Khazima) wa pekee ulichukuliwa kama wa kutosha. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akampa jina (lakabu) la Dhu’sh-Shahadatain kwa sababu alichukuliwa kama aliye sawa na mashahidi wawili waadilifu. Mfano huu unaonesha kwamba ‘Aya ya Ushahidi’ inaruhusu hali ya kipekee katika mazingira fulani.

Wakati Khazima, muumini mmoja binafsi na sahaba kutoka mion- goni mwa umma, alifanywa wa kipekee kwenye Aya hiyo, Ali na Fatima ambao walikuwa Ma’asum kwa mujibu wa ‘Aya ya utakaso’ walikuwa katika nafasi nzuri zaidi kufaidi upendeleo huu wa kipekee. Kwa hakika wao walikuwa mbali kutokana na uwongo wa aina yoyote. Kukataa ushahidi wao ilikuwa ni kukataa ushahidi wa Allah swt.

Kukataa Mashahidi Wa Fatima Ilikuwa Ni Kinyume Na Sheria Ya Kidini

Hadhrat Fatima alidai kwamba Fadak ilitolewa kwake kama zawadi na baba yake na kwamba ilikuwa katika miliki na usimamizi wake wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alitakiwa kutoa mashahidi. Alimtoa Amirul-Mu’uminin Ali Bin Abi Talib na Hasan na Husein kama mashahidi wake.

Lakini ushahidi wao ulikataliwa. Je, kitendo hiki hakikuwa cha kidhalimu? Haieleweki ni kwa vipi mtu yeyote aweze kukataa ushahidi wa Ali. Allah katika Qur’ani Tukufu anasema lazima tuwe na Ali, yaani, lazima tumfuate yeye. Zaid-e-Adl alikuwa mfano halisi wa ukweli kwa sababu ya ukweli wake uliozidi mno.

Halikadhalika, Ali aliitwa ‘mkweli’ kwani Allah anavyosema: “Enyi mlioamini! Mcheni Allah na kuwenu pamoja na wakweli.” (9:119) Neno ‘Wakweli’ hurejea kwa Mtume Muhammad, Ali na Ahlu’l-Bayt watukufu.

‘Wakweli’ Inaashiria Kwa Mtume Muhammad Na Ali

Hafidh: Ayah hii inathibitisha vipi maoni yako, ambayo yangemaanisha kwamba kumfu- ata Ali ni wajibu kwetu? Muombezi: (1) Wanachuoni wenu maarufu wameandika katika vitabu na tafsiri zao kwamba Aya hii iliteremshwa kwa kumsifia Muhammad na Ali. ‘Wakweli’ hurejea kwa watu hawa wawili watukufu, na kwa mujibu wa riwaya nyingine linamaanisha Ali; riwaya nyingine zinasema kwamba hurejea kwa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Imam Tha’labi katika tafsir yake Kashfu’l-Bayan, Jalalu’d-Din Suyuti akisimulia kutoka kwa Ibn Abbas katika kitabu chake Durru’l-Manthur, Hafidh Abu Sa’id Abdu’l-Malik Bin Muhammad Khargushi akisimulia kutoka kwa Asma’is katika Sharafu’l-Mustafa, na Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika kitabu chake Hilyatu’l-Auliya anasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Hawa wakweli ni Muhammad na Ali.” Sheikh Sulayman Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, sura ya 39, uk. 1191, akisimulia kutoka kwa Muwaffaq Bin Ahmad Khawarizmi, Hafidh Abu Nu’aim Ispahani, na Hamwaini wakisimulia kutoka kwa ibn Abbas, ambaye alisema: “Katika Aya hii ‘wakweli’ ni Muhammad na kizazi chake.”

Na Sheikhu’l-Islam Ibrahim Bin Muhammad Bin Hamwaini, mmoja wa wanachuoni wenu mashuhuri, katika kitabu chake Fara’idu’s-Simtain, Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib, sura ya 62, na Muhadith Sham katika Ta’rikh yake, akisimulia kutoka kwenye vyanzo vyake anaandika: “Pamoja na wa kweli, yaani, ni pamoja na Ali Bin Abi Talib.”

(2) Allah anasema:

{واﻟﱠﺬِي ﺟﺎء ﺑِﺎﻟﺼﺪْقِ وﺻﺪﱠق ﺑِﻪ ۙ اوﻟَٰﺌﻚَ ﻫﻢ اﻟْﻤﺘﱠﻘُﻮنَ {33

“Na yule ambaye aliyeleta ukweli, na yule aliyeusadikisha kama, hao ndio wamchao (Mwenyezi Mungu).” (39:33)

Jalalu’d-din Suyuti katika Durru’l-Manthur, Hafidh Ibn Mardawiyya katika Manaqib, Hafidh Abu Nu’aim katika Hilyatu’l-Auliya, Muhammad ibn Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib, sura ya 62, na Ibn Asakir katika Ta’rikh yake, akisimulia kutoka kwenye vitabu mbali mbali vya wafasiri, anasimulia yafuatayo kutoka kwa Ibn Abbas na Mujahid: “Yule anayeleta ukweli ni Muhammad, na yule ambaye anauthibitisha ni Ali Bin Abi Talib.”

(3) Allah anasema katika Sura ya al-Hadid (chuma) ya Qur’ani Tukufu: “Na (kwa) wale waliomuamini Allah na Mtume Wake, hao ndio Masidiki na Mashahidi mbele ya Mola wao; watapata malipo yao na nuru yao…” (57:19)

Imam Ahmad Hanbal katika “Musnad”na Hafidhi Abu Nu’aim Ispahan katika “Manazil Mina’l-Qur’ani fi Ali” anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Aya hii tukufu iliteremshwa katika kumsifia Ali ikimtaja kama aliye ni miongoni mwa wakweli.

(4) katika Suratun-Nisa (wanawake) Allah anasema: “Na wenye kumtii Allah na Mtume Wake, basi hao watakuwa pamoja na wale aliowaneemesha Allah miongoni mwa manabii na masidiki na mashahidi na watu wema, na hao ndio marafiki wema.” (4:69) Katika aya hii vilevile wakweli inaashiria kwa Ali.

Kuna hadithi nyingi zilizosimuliwa na maulamaa wetu na wenu, zikionesha kwamba Ali alikuwa ndiye mkweli wa umma na kwa kweli ndiye aliyetukuka mno miongoni mwa wakweli.

Ali Ametukuka Zaidi Miongoni Mwa Wakweli (Masidiq)

Wengi wa maulamaa wenu wakubwa wameandika katika vitabu vyao kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kuna masidiki wakubwa watatu - Hiziqil, yule Mu’mini wa watu wa Firauni, Habibu Najjar wa Suratal-Yasin, na Ali Bin Abi Talib ambaye ni mbora wa wote.”

Wameandika hadithi hii hawa wafuatao wote: Imamu Fakhru’d-Din Razi katika Tafsiri Kabir: Imam Tha’labi katika Kashfu’l-Bayani; Jalalud-Din Suyuti ndani ya Durru’l-Manthur; Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad; Ibn Shirwaih katika Firdaus; Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 2, uk. 451; Ibn Maghazil Shafi’i kati- ka Manaqib; na Ibn Hajar Makki katika Sawaiq-e-Muhriqa (hadithi 30 kati ya hadithi 40 ambazo amefafanua juu ya ubora wa Ali) akinukuu kutoka Bukhari ambaye anasimulia kutoka kwa Ibn Abbasi, isipokuwa kifungu cha mwisho.

Vilevile Sheikh Suleiman Balkhi katika “Yanabiu’l-Mawadda” sura ya 42, akinukuu kuto- ka Musnad ya Imam Hanbal; Abu Nu’aim Ibn Maghazili Shafii; yule msemaji mkubwa Khwarizmi, akinukuu kutoka kwa Abu Laila na Abu Ayyub Ansari, katika Manaqib yake, Ibn Hajar katika Sawai’q (na kundi la wengine) anasilia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema:

“Kuna Masidiki watatu - Habib Najjar, yule Mu’umin wa Sura ya Yasini ambaye alisema: ‘Enyi watu! Wafuateni Mitume;’ Hizqil, Muumini wa watu wa Firauni ambaye alisema “Je, mnamuua mtu ambaye anamuabudu Allah? na Ali Ibn Abi Talib ambaye ndiye mbora zaidi wa wote hao.”

Watu wanashangaa kuona jinsi uwelewa wako unavyokandamizwa na ukaidi wako. Ninyi wenyewe mnathibitisha kwa hadithi mbali mbali zenye kuafikiana na Qur’ani Tukufu kwamba, Ali alishikilia cheo cha juu miongoni mwa watu wakweli (Siddiq) na bado mnawaita watu wengine Siddiq ingawa hakuna hata aya moja ambayo imesimuliwa kuhusu kuwa kwao wakweli (masidiq).

Enyi waungwana! tafadhalini kuweni waadilifu. Hivi ilikuwa ni sahihi kuukataa ushahidi wa mtu ambaye Allah anamwita ‘Sidiq’ ndani ya Qur’ani, ambaye sisi tumeamriwa kumfuata?

Ali Yuko Pamoja Na Haki Na Quran.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ali yuko siku zote pamoja na haki na haki inamzunguka Ali.” Khatibu Baghdad katika kitabu chake “Ta’rikh,” Jz. 4, uk. 321, Hafidhi Ibn Mardawiyya katika ‘Manaqib,’ Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, Fakhru’d-Din Razi katika Tafsiri-e-Kabir, Jz. 1, uk. 111, Ibn Hajar Makki katika Jam’u’s-Saghir, Jz. uk. 74, 75, 140 na Sawa’iq-e-Muhriqa sura ya 9, Fasli ya 2, Hadith ya ishirini na moja akisimulia kutoka Ummi Salama na Ibn Abbas vilevile katika Yanabiu’l- Mawadda, Sura ya 65 uk. 185, akichukua kutoka “Jam’u’s-Saghir” ya Jalalu’d-Din Suyuti, kwa nyongeza katika “Tarikhu’l-Khulafa” uk. 116, Faidhu’l-Qadir, Jz. 4, uk. 358 akisimulia kutoka kwa Ibn Abbas, “Manaqibu’s-Sab’in,” uk. 237, hadithi ya 44 akinukuu kutoka kwa mwandishi wa Firdaus; Sawa’iq-e-Muhriqa, sura 59, sehemu ya 2, uk. 238, akisimulia kutoka kwa Ummi Salama na Muhammad Bin Yusufu Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib, baadhi yao wakisimulia kutoka kwa Umm Salama, wengine kutoka Aisha, na wengine kutoka kwa Muhammad Bin Abu Bakr wote wanasimulia kwamba wamemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Ali yuko pamoja na Qur’ani na Qur’ani ipo pmoja na Ali; kamwe hakutakuwa na tofauti kati ya viwili hivyo, na viwili hivyo havitatengana vyenyewe mpaka vinifikie kwenye hodhi ya Kauthar.”

Baadhi ya wapokezi wamesimulia maneno haya: “Haki wakati wote iko pamoja na Ali na yeye Ali wakati wote yupo pamoja na haki. Hakutakuwa na tofauti kati ya viwili hivyo, navyo viwili hivi havitatengana.”

Ibn Hajar anaandika katika Sawa’iq-e-Muhriqa, Sura ya 9 sehemu ya 2, uk. 77, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) juu ya kitanda chake alichofia, alisema: “Ninakuachieni baada yangu vitu viwili. Kitabu cha Alla pamoja na kizazi changu, Ahlu’l-Bayt wangu.”

Kisha wakati huku akiwa ameushika mkono Ali, aliunyanyua juu na akasema: “Huyu Ali yuko pamoja na Qur’ani an Qur’ani iko pamoja na Ali. Viwili hivi havitatengana mpaka vinifikie kwenye hodhi ya Kauthar. Kisha nitakiuliza kila kimoja chao kuhusu suala la uandamizi (Urithi),”

Vile vile imesimuliwa kiujumla kwamba Mtume alisema: “Ali yuko pamoja na haki na haki siku zote iko na Ali. Huzungukana wenyewe kwa wenyewe.” Sibt Ibn Jauzi, katika Tadhkrat-e-Khawasu’l-Umma, uk. 20, anasimulia kuhusiana na ‘Hadith-e-Ghadir’ kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Haki imfuate Ali, katika upande wowote atakaokwenda.”

Sibt ibn Jauz akitoa maoni kuhusiana na hili anasema: “Hadithi inathibit- sha kwamba kama kuna tofauti yeyote kati ya Ali na Sahaba yeyote mwingine, basi haki itakuwa pamoja na Ali.”

Utii Kwa Ali Ni Utii Kwa Allah Na Mtume Wake Mtukufu

Imeandikwa katika vitabu ambavyo vimetajwa na katika vitabu vyenu vingine sahihi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mara kwa mara alisema: “Yeyote ambaye anamtii Ali hakika ananitii mimi. Na yeyote anayenitii mimi, hakika anamtii Allah. Yule ambae hamtii Ali hakika hanitii mimi, na yule ambaye hanitii mimi hakika hamtii Allah.”

Abu’l-Fat’h Muhammad Bin Abdu’l-Karim Shahrastani anaandika katia kitabu chake “Milal-wa-Nihal” kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ukweli ni kwamba Ali siku zote yuko juu ya haki, na wale wanaomfuata yeye wako juu ya haki.”

Pamoja na riwaya zote hizi za wazi, ambazo zimeandikwa katika vitabu vyenu wenyewe sahihi, je, si kweli kwamba kukataa kukubaliana na Ali kulikuwa ni sawa na kukataa kukubaliana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?”

Khalifa Abu Bakr Hakufuata Sheria Ya Ushahidi Katika Kesi Nyingine.

Hoja ya pili ambayo umeileta ni kwamba Khalifa alilazimika kutenda kwa mujibu wa mtazamo wa nje wa kanuni ya dini kwa vile “aya ya ushahidi” katika maana yake ya kijumla ilitumika katika suala hili.

Kwa hiyo, kwa kutokuwepo kwa mashahidi, asingeweza kutoa “mali ya Waislamu” kumpa Fatima, kwa msingi wa madai yake peke yake. Bali alikuwa na tahadhari sana kwamba alidai, kinyume cha sheria ya kidini, mashahidi kutoka kwa mmiliki haswa wa mali hiyo.

Kwanza nilikwisha kuwelezeni kwamba Fadak haikuwa Mali ya Waislamu. Alipewa Fatima na baba yake kama zawadi na kushikiliwa kiumiliki na yeye.

Pili, kama kweli khalifa alitaka kufuata sheria ya dini, basi angeifuata hasa katika masula yote. Kwa nini alifuata sera ya undumilakuwili? Alizoea kutoa mali ya Waislamu kwa wengine kwa kukubali tu madai ya mdomo bila kuchukua ushahidi wa shahidi yeyote. Lakini katika suala la mali ya Fatima alichukua tahadhari isiyokuwa ya kawaida.

Ibn abi’l -Hadid ameandika katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 4, uk. 25, kwamba alimuuliza Ali ibnul- Fariqi, mwalimu katika Madrasa ya Gharbi huko Baghdad, iwapo Fatima alikuwa katika haki na alizungimza ukweli kuhusu madai yake. Alisema: ‘Ndio?’ Nikasema: ‘Kama alikuwa na haki na alisema kweli, kwa nini Khalifa hakurudisha Fadak kwake? Yeye (Fariqi) alitabasamu (ingawa kamwe hajafanya utani) na akasema kwamba kama angeirudisha Fadak kwa Fatima siku ile, kesho yake angelikuja kudai ukhalifa kwa ajili ya mumewe.

Halafu Khalifa angelazimika kurudisha haki ile vile vile, kwa vile angekuwa amekwishakubali ukweli wake katika suala liliopita.

Kwa mujibu wa wanachuoni wenu wakubwa, hali ilikuwa wazi kabisa. Walikuwa wamekubali ukweli kwamba kuanzia siku ya kwanza haki ilikuwa pamoja na muonewa Fatimah, lakini manufaa yao ya kisiasa yalihitaji kwamba lazima wamnyime bibi huyu asiye na hatia haki yake.

Abu Bakr Atoa Mali Kwa Jabir Bila Ya Kuita Mashahidi

Hafidhi: Ni lini ambapo Khalifa alitoa mali ya Waislamu bila shahidi yeyote?

Muombezi: Wakati Jabir alipodai kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amemuahi- di kwamba atalipwa kutokana na ngawira aliyochukuliwa kutoka Bahrain, alipewa dinar 1500 kutoka Baitul-Mal (Hazina ya Umma) bila ya kuleta kikwazo au kutaka shahidi yeyote kutoka kwake.

Hafidhi: Kwanza sijaona riwaya kama hiyo. Pengine ipo kwenye vitabu vyenu. Pia utawezaje kudai kwamba mashahidi hawakuhitajiwa? Muombezi: Ni ajabu kwamba hakuiona riwaya hii. Riwaya hii ya Jabir bin Abdullah Ansari ni moja ya hoja za maulamaa katika kuunga mkono maoni yao kwamba riwaya ya pekee ya sahaba muadilifu inakubalika. Kwa sababu hiyo, Sheikhu’l-Islam Hafiz Abdu’l-Fazl Ahmad Bin Ali bin Hajar Asqalani anasema katika kitabu chake Fathu’l-Bari Fi Sharh-e-Sahihu’l-Bukhari: Riwaya hii inathibitisha kwamba simulizi ya sahaba mwadilifu inakubaliwa hata ingawa inamnufaisha yeye mwenyewe binafsi, kwa sababu Abu Bakr hakutaka shahidi kutoka kwa Jabir katika kuunga mkono madai yake.

Bukhari anaandika taarifa hiyo katika maelezo marefu mno katika Sahih yake. Katika mlango wa ‘Man Yakfal un mayyit dainan’ na na Kitabu’l- Khuma fi Bab-e-ma Qata an-Nabi mina’l Bahrain,’ anaandika kwamba wakati ngawira ya Bahrain ilipoletwa Madina, Abu Bakr alitangaza kwamba yeyote yule ambaye aliahidiwa pesa na Mtume wa Allah au yeyote ambaye ana madai ambayo hayajatoshezwa aje apokee haki yake. Jabir alikuja na akasema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliniahidi kwamba wakati Bahrain itakaposhindwa na kuwa chini ya usimamizi wa Waislamu, nitapewa zawadi kuto- ka kwenye ngawira hiyo.

Hivyo mara moja Abu Bakri alimpa dinnar 1,500 bila ya kuitisha ushahidi wewote, juu ya msingi tu wa madai yake. Jalalud-Din Suyuti vile vile ameandika tukio hili katika kitabu chake “Ta’rikhu’l-Khulafa” katika sehemu juu ya ukahlifa wa Abu Bakr.

Enyi watu waadilifu: Tafadhali nakuombeni mnifahamishe kwa jina la Allah kama huu haukuwa utovu wa uadilifu. Isipokuwa kama kulikuwepo na chuki fulani ikifanya kazi, vipi ilikuwa halali kwa Abu Bakr kuihalifu “aya ya ushahidi” na kumpa Jabir pesa juu ya msingi wa madai yake peke yake? Mbali na hili, Bukhari katika Sahih yake na wengine wengi kati ya maulamaa na wanachuoni wenu wa sheria, wanakubali ushahidi mmoja wa sahaba muadilifu hata kama unatoa manufaa binafsi kwake mwenyewe.

Lakini wanayaona madai ya Ali kwamba hayakubaliki kwa misingi kwamba alitaka kitu kwa manufaa yake mwenyewe. Je, Ali hakuwa mtu mkamilifu miongoni mwa masahaba? Kama mtaliangalia suala hili kwa uadilifu mtakubali kwamba haikuwa tu unyimaji wa haki, bali yote yalikuwa ni mabavu na hila iliyowazi.

Hafidhi: Na fikiri Abu Bakr hakuhitaji mashahidi kutoka kwa Jabir kwa sababu alikuwa mmoja wa wale Masahaba waliofundishwa kwa karibu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa hakika amemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Kama mtu yeyote akitoa maelezo ya uwongo kuhusu mimi makazi yake yatakuwa motoni.” Akifahamu onyo hili kali, ni wazi kabisa kwamba Sahaba aliyefundishwa kwa karibu na muumini, asingeweza kuchukua hatua ya kimakosa kama hilo na asingeweza kuhusisha maelezo ya uwongo kwa Mtume wa Allah.

Muombezi: Je, Jabir alikuwa karibu na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au Ali na Fatima, ambao walifundishwa maalum na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Ali Na Fatima Walikuwa Wahusika Wa Aya Ya Utakaso

Hafidhi: Ni wazi kwamba Ali na Fatima walikuwa karibu zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wa Allhah, kwa sababu walikuwa chini ya mafundisho yake kuanzia kuzaliwa kwao hasa.

Muombezi: Hivyo itakubidi kukubali kwamba Ali na Fatima lazima walikuwa wafuasi makini wa onyo hili na wasingeweza kwa msingi wa hadith ya Mtume, kufanya madai yoyote ya uwongo.

Na ni wajibu juu ya Abu Bakr kukubali madai ya Fatima kwa vile cheo cha watu wote hawa wawili kilikuwa juu zaidi sana kuliko cha Jabir (kama ambavyo mwenyewe unakiri). Kwa kweli cheo chao kilikuwa cha juu zaidi kwa Masahaba wote wengine. Walikuwa wastahiki wa “Aya ya Utakaso” na walikuwa watu ma’sum.

Aya hii inadhihirisha utohara wa watu watano hawa watukufu: Muhammad, Ali, Fatimah, Hasani na Huseini. Kwa kweli maulamaa wenu wakubwa vile vile wameshuhudia ukweli wa watu hawa watukufu.

Ama kuhusu Amiru’l-Muminin, nimekwisha kukuambieni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuita ‘Mtu Mkweli wa Umma wote,’ na Allah vile vile amemuita ‘mkweli’ katika Qur’ani Tukufu. Kuhusu ukweli wa Fatimah Zahra, vile vile kuna hadithi nyingi za namna hiyo. Miongoni mwao ni iliyosimuliwa na Hafiz Abu Nu’aim Ispahani katika kitabu chake “Hilyatu’l-Auliya,” Jz. 2, uk. 42, kutoka kwa Aisha ambaye alisema: “Sijamuona mtu yeyote mkweli zaidi kuliko Fatimah isipokuwa baba yake.”

Hafidhi: Madai yako kwamba aya hii imeshuka kwa kuwasifia watu wale watano hayawezi kukubalika. Katika midahalo hii umeonesha ujuzi mkubwa kuhusu vitabu vyetu.

Unapaswa kukubali kwamba katika suala hili umekosea, kwa vile wafasiri kama Kadhi Baidhawi na Zamakhshari wanaamini kwamba aya hii tukufu iliteremshwa kwa kuwasifia wake za Mtume. Na kama kuna riwaya yoyote isemayo kwamba iliteremshwa kwa kuwasifia watu wale watano, basi itakuwa ni dhaifu. Sababu ni kwamba aya yenyewe kama ilivyo inajithibitisha kinyume na maana hiyo. Muktadha wa “Aya ya Utakaso” umeunganishwa na wake (wa Mtume) na sehemu ya kati haiwezi kuondolewa kwenye muktadha huo.

Kuthibitisha Kwamba Aya Ya Utakaso Haikuwa Kwa Kuwasifia Wake Za Mtume.

Muombezi: Dai lililoletwa na wewe linakanushika katika mitazamo mingi. Umesema kwamba sehemu ambazo zimetangulia na zinazofuatia zimehusishwa na wake za Mtume, na hivyo Ahlul’l-Bayt wameondolewa katika aya hii tukufu. Najibu hivi kwamba, kama inavyotokea mara kwa mara katika mazungumzo yetu, tunahamisha nadhari yetu kutoka kwa mtu mmoja kwenda kwa mtu mwingine na kisha kurudi kwa mtu yule wa kwanza.

Kuna mifano mingi kuhusu suala hili katika mashairi ya waandishi wakubwa na washairi wa Kiarabu. Katika Qur’ani Tukufu yenyewe kuna mifano mingi ya aina hii. Kwa kweli, kama utachunguza sura iliyoko kwenye mjadala, al-Ahzab baada ya kuhutubia wake za Mtume, nadhari inahamishwa kwa waumini.Kisha mwishowe, wake za Mtume wanahutubiwa. Muda hauniruhusu kuwasilisha ushahidi uliofafanuliwa zaidi kuelezea nukta hii zaidi.

Pili, kama aya hii ilikuwa inahusu wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), vijina vilivyotumi- wa ndani yake vyingelikuwa vya kike. Lakini kwa vile vijina vyilivyotumika ni vya kiume, tunajua kwamba kuashiria huko sio kwa ajili ya wake za Mtume, bali kwa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Nawab: Kama Fatimah vile vile amejumuishwa katika kundi hili kwa nini dhamiri ya kike haikutumika?

Muombezi: (Akiwageukia maulamaa) Mabwana: mnajua kwamba aya hii, ingawa Fatimah ni mmoja wa wanaotajwa, dhamiri ya kiume inatumika kwa sababu ya wingi wa wanaume. Yaani katika kundi la wanaume na wanawake, uzito zaidi unawekwa kwa wanaume.

Katika aya hii utumiaji wa dhamiri ya kiume wenyewe ni uthibitisho kwamba maelezo haya sio dhaifu, bali yana nguvu kamili. Mbali na hili, kwa kuangalia wingi wa jamaa wa kiume, kijina lazima kiwe katika dhamiri ya kiume kwa sababu katika Watukufu Watano kuna mwanamke mmoja na wanaume wanne.

Naam hakika lau kama aya hii ingekuwa kuhusu wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), utumiaji wa dhamiri ya kiume kwa ajili ya wanawake ungelikuwa ni kosa kabisa. Mbali na hili, uamuzi uliotolewa kutoka kwenye hadithi sahihi katika vitabu vyenu wenyewe ni kwamba aya hii tukufu iliteremshwa kwa sifa ya kizazi sio kuhusu wake zake.

Ingawa alikuwa mshabiki sana, Ibn Hajar Makki anasema katika kitabu chake, “Sawa’iq- e-Muhriqa” kwamba wafasiri wengi wanaamini kwamba aya hii iliteremshwa kwa sifa ya Ali, Fatimah, Hasan na Husein.

Wake Za Mtume Hawakujumuishwa Katika Ahlul-Bayt

Tukiziweka pembeni hoja hizi, wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hawakujumuishwa katika Ahlul-Bayt.

Imesimuliwa katika Sahih Muslim na Jam’u’l-Usul kwamba Hasan Ibn Samra alimuuliza Zaid Ibn Arqam iwapo wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walijumuishwa katika Ahlul- Bayt wake. Zaid akasema: “Kwa jina la Allah, hapana. Mke anabakia na mumewe kwa kipindi fulani, lakini wakati akimuacha, anakwenda kwenye nyumba ya baba yake, huungana na familia ya mama yake, na anakuwa ametoka kabisa kwa mumewe.

Ahlul-Bayt ni wale jamaa wa familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambao kwamba sadaka kwao ni haramu. Hawatatengana na Ahlul-Bayt popote watakapokwenda.”

Mbali na maafikiani ya maoni ya wote pamoja miongoni mwa Ithna’shari Shia kuhusu kizazi hicho kitukufu, kuna hadithi nyingi zilizoandikwa katika vitabu vyenu wenyewe, ambazo zinalikataa wazo la kwamba wake za Mtume wamejumuishwa katika Ahlul-Bayt. Hadithi Nyingi Zinazohusu “Aya Ya Utakaso” Ikiwa Katika Kuwasifia

Watukufu Watano

Imamu Tha’labi katika “Tafsir-e-Kashfu’l-Bayan”; Imamu Fakhru’d-Din Razi katika “Tafsir-e-Kabir”, Jz. 6, uk. 783; Jalalu’d-Din Suyuti katika “Durru’l-Mansur”, Jz. 5, uk. 199 na “Khasa’isu’l-Kubra”, Jz. 2, uk. 264; Nishapuri katika “Tafsiir”, Jz. 3; Imamu Abdu’r-Razzaq ar-Ra’sani katika “Tafsir Rumuzu’l-Kunuz; Ibn Hajar Asqalani katika “Isaba”, Jz. 4, uk. 208; Ibn Asakir katika “Ta’rikh” Jz. 4, uk. 204 na 206; Muhibu’d-Din Tabari katika “Riyazu’n-Nuzra,” Jz. 2, uk. 188; Muslim Bin Hajjaj katika “Sahih”, Jz. 2, uk. 133 na Jz. 7, uk. 140; Nabhani katika “Sharaful-Mu’ayyid”, chapa ya Beiruti, uk. 10; Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’t-Talib”, sura ya 100, pamoja na hadithi sahihi sita na Sheikh Suleimani Balkhi Hanafi katika “Yanabiu’l-Mawadda”, sura ya 33, kutoka kwenye Sahih Muslim akitegemea juu ya hadith ya Ummu’l-Muminin Aisha; hadithi kumi kutoka Tirmidhi, Hakim Ala’u’d- Dowlat Semnani, Baihaki, Tibrani, Muhammad Bin Jarir, Ahmad Bin Hanbal, Ibn Abi Shaiba, Ibn Munzir, Ibn Sa’d, Hafidh Zarandi, na Hafidh Ibn Mardawiyya kama hadithi za Ummu’l-Muminin Ummi Salma, Umar Bin Abi Salma (ambaye alilelewa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Anas Bin Malik, Sa’d Bin Abi Waqqas, Wathila Ibn Asqa, na Abu Sa’id Khudri wamesema kwamba “Aya ya Utakaso” imeteremka kwa sifa ya watukufu watano.

Hata Ibn Hajar Makki, pamoja na kuwa mpinzani wa Shia katika hali nyingi amekubali maana yake halisi katika njia saba. Anasema katika “Sawa’iq-e-Muhriqa” kwamba aya hii iliteremshwa kwa sifa ya Muhammad, Ali, Fatimah, Hasani na Huseini, na kwamba watu hawa tu, watukufu watano ndio waliokusudiwa katika aya hii.

Sayyid Abu Bakr Bin Shahbu’d-Din Alawi katika kitabu chake “Kitab-e-Rashqatu’s- Sa’adi min Bahr-e- Fadha’il Bani Nabiu’l-Hadi” (imechapisha na A’lamiyya Press, Misr, 1303 A.H.) sura ya 1, uk. 14-19, anasimulia kutoka kwa Tirmidhi, Ibn Jarir, Ibn Munzir, Hakim, Ibn Mardawiyya, Baihaqi, Ibn Hatim, Tibrani, Ahmad Bin Hanbal, Ibn Kathir, Muslim Bin Hajjaj, Ibn Abi Shaiba, na Samhudi katika misingi ya uchunguzi wa vitabu vya maulamaa wenu, kwamba aya hii iliteremshwa kwa sifa ya watu watano watukufu hawa.

Katika Jam’i-Bainu’s-Sihahu’s-Sitta, Muata cha Imamu Malik Bin Anas, Sahih Bukhari na Muslim, Sunan ya Abu Dawud na Sijistani, na Tirmidhi, Jam’ul-Usul na vitabu vingine, maulamaa na wanahistoria wenu kwa ujumla wanakiri kwamba aya hii iliteremshwa kwa sifa ya hawa watukufu watano. Na kwa mujibu wa madhehebu yenu, hadithi hii imesimuli- wa bila kukatishwa. Hadithi Ya Ummi Salama Kuhusu ‘Harrira’ (Chakula Kitamu Cha Kimiminika) Cha Fatimah Na Kushuka Kwa “Aya Ya Utakaso”

Wasimuliaji wengi wa hadithi wamesimulia tukio linalohusiana na harrira. Miongoni mwao ni Imam Tha’labi katika “Tafsir” yake, Imam Ahmad Bin Hanbal katika “Musnad”, na Ibn Athir katika “Jam’u’l- Usul,” akinukuu kutoka “Sahih Tirmidhi na Sahih Muslim”: wote wanasimulia kutoka kwa mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ummul-Mu’minin Ummi Salama, ambaye alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa nyumbani kwangu wakati Fatimah alipomletea kikombe cha harrira.

Wakati huo alikuwa amekaa kwenye baraza ambayo amezoea kulala. Alikuwa na joho la Khaibari chini ya miguu yake. Nilikuwa ninaswali chumbani mwangu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Fatimah amuite mumewe na watoto wake. Mara tu Ali, Hasan na Husein waliingia ndani na wote wakashirikiana ilie harrira. Jibril akajitokeza na kuteremsha aya hii tukufu kwa Mtume: “…Allah anapenda kuwaondoleeni uchafu enyi watu wa nyumba! Na kuwatakasa kwa utakaso kabisa…” (33:33)

“Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawafunika wote kwa joho lake, akanyanyua mikono juu mbinguni, na akasema: ‘Ewe Allah, hawa ndio wanaokifanya kizazi changu. Waondolee kila aina ya uchafu na uwatakase kwa utakaso ulio kamili.’”

Ummi Salama anasema kwamba alisogea mbele na akatamani kuingia katika lile joho akisema: “Ewe Mtume wa Allah, na mimi vile vile naweza kujiunga katika kundi hili?”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu akasema: “Hapana, bakia kwenye sheemu yako, wewe uko kwenye wema.” Hii ilikuwa na maana kwamba hakuweza kujumuishwa miongoni mwa Ahlul’l-Bayt na kupata cheo chao, lakini mwisho wake ulikuwa uwe mzuri. Imamu Fakhru’d-din Razi katika Tafsiir yake anaongeza kwamba Mtume alisema: “Dhambi zote zimezuiwa kwako” na “Umepewa majoho ya baraka.”

Kwa hakika inashangaza sana kwa maulamaa wenu wasio waadilifu, ambao wanaandika katika vitabu vyao sahihi kwamba Ali na Fatimah walijumuishwa katika “Aya ya Utakaso” (na uchafu mkubwa mno ni kusema uwongo). Bado wanakataa Uimamu wa Ali (uandamizi/urithi) na kukataa ushahidi wake katika kumuunga mkono Fatimah kuhusu madai yake ya Fadak. Haijulikani ni kwa kigezo gani wadai haki wanaunda hukumu.

Fadak Iliporwa Kwa Sababu Za Kisiasa

Sasa ngoja turudi kwenye nukta yetu ya mwanzo. Je, ilikuwa sahihi kukataa maelezo ya Ali na Fatimah na kuwanyima haki yao, lakini kukubali madai ya Jabir bila kusita kokote ingawa yeye alikuwa Mwislamu wa kawaida tu? Hafidh: Kamwe haiwezi kukubalika kwamba Khalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye alikuwa karibu mno na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), angeshawishika kuipora Fadak. Hakika Fadak haikuwa na maana kwa Khalifa, ambaye alikuwa na Baitu’l-Mal (Hazina ya Umma) ya Waislamu chini ya usimamizi wake.

Muombezi: Ni wazi kabisa kwamba hakuihitaji. Lakini kundi la kisiasa la wakati ule liliiona kwawmba ni muhimu kuiharibu familia tukufu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Waliwafanyia watu hawa watoharifu kila aina hofu, mateso na umasikini, ili kwamba wasiweze kuufikiria ukhalifa. Watu wapenda dunia hufanya chochote kilicho lazima kuwafanya wastawi katika ulimwengu huu.

Wanasiasa hawa walitambua kwamba kama familia hii kubwa ingekuwa inamiliki utajiri wa kidunia, watu kwa hakika wangeelekea upande wao. Mitazamo ya kisiasa iliwasukuma kuipora Fadak na kufunga njia zao zote za mapato ya kifedha.

Khums Yapigwa Marufuku

Miongoni mwa vitu vilivyopigwa marufuku kwa ajili yao ilikuwa ni khums, ambayo kwayo msisitizo mkubwa umewekwa ndani ya Qur’ani. Kwa vile Allah amekataza sadaka kwa ajili ya Mtume na kizazi chake, mlango wa khums ulifunguliwa kwa ajili yao. Anasema katika Qur’ani, Sura ya 8, Anfal (Ngawira za kivita).

واﻋﻠَﻤﻮا اﻧﱠﻤﺎ ﻏَﻨﻤﺘُﻢ ﻣﻦ ﺷَء ﻓَﺎنﱠ ﻟﻪ ﺧُﻤﺴﻪ وﻟﻠﺮﺳﻮلِ وﻟﺬِي اﻟْﻘُﺮﺑ واﻟْﻴﺘَﺎﻣ واﻟْﻤﺴﺎﻛﻴﻦ واﺑﻦ اﻟﺴﺒِﻴﻞ انْ ﻛﻨْﺘُﻢ آﻣﻨْﺘُﻢ {ﺑِﺎﻟﻪ وﻣﺎ اﻧْﺰﻟْﻨَﺎ ﻋﻠَ ﻋﺒﺪِﻧَﺎ ﻳﻮم اﻟْﻔُﺮﻗَﺎنِ ﻳﻮم اﻟْﺘَﻘَ اﻟْﺠﻤﻌﺎنِ ۗ{41

“Na jueni kwamba kitu chochote kile mnacho kipata, moja ya tano yake ni kwa ajili ya Allah na Mjumbe Wake na jamaa wa karibu na yatima na mwana njia.” (8:41)

Matumizi haya yaliwekwa ili kwamba kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kiweze kuishi kwa amani na kisije kikahitaji msaada wa jumuiya yao. Lakini mara tu baada ya kufariki kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), walinyimwa fursa hii pia. Khalifa Abu Bakr alizuia haki hii Ahlul’l-Bayt na kusema kwamba khums lazima itumike kwa ajili ya vifaa vya vita. Hivyo familia ya Mtume ilifanywa ikose msaada kutoka sehemu zote.

Imamu Shafi’i Muhammad Bin Idris anazungumzia kuhusu hili katika kitabu chake, “Kitabu’l-Umm” uk. 69: “Kizazi cha Mtume ambao kwamba Allah aliwapa fungu la khums badala ya sadaka, hawawezi kupewa mgao wowote, mkubwa au mdogo, kutoka kwenye sadaka za wajibu. Imekatazwa kwao kuzikubali. Wale ambao kwa makusudi huwapa sadaka hawatasamehewa kutokana na majukumu yao.

Kwa kuwanyima haki ya khums, sadaka ambayo imekatazwa kwao, haitakuwa halali. Hata katika wakati wa Khalifa Umar Bin Khattab, kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walinyimwa madai yao ya haki kwa msingi kwamba kiasi cha khums kilikuwa ni kikubwa sana na kwamba kisingeweza kutolewa kwa jamaa wa karibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Iliamuliwa kwamba pesa hizo lazima zitumike katika matumizi ya jeshi. Wananyimwa haki hii hadi leo.

Hafidh: Imamu Shafi’i anasema khums lazima igawanywe katika mafungu matano: fungu moja linakwenda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambalo hutumika kwa matumizi na mahitaji ya Waislamu, fungu la pili ni kwa ajili ya jamaa zake wa karibu na mafungu matatu yaliyobakia ni kwa ajili ya mayatima, mafukara, na wasafiri.

Muombezi: Wafasiri kwa ujumla wanakubali kwamba wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aya hii iliteremshwa kwa ajili ya msaada wa kizazi na jamaa wa karibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Khums ilitumika kwa matumizi yao. Kwa mujibu wa kanuni ya Shia, katika utiifu kwenye desturi iliyofutwa na familia ya Mtume na Maimamu watukufu, na vile vile kwa kuafikiana na maana ya aya tukufu iliyotajawa hapo juu, khums inagawanywa katika mafugu sita.

Mafugu matatu yaliyokusudiwa kwa ajili ya Allah, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na jamaa zake wa karibu yanaenda kwa Imam na, katika ghai- ba yake (huenda) kwa mwakilishi wake, mujtahid. Ni faqihi muadilifu na mzoefu, ambaye hutumia pesa kwa ajili ya faida ya Waislamu, kwa mujibu wa busara zake mwenyewe. Mafungu matatu yaliyobakia yanagawanywa kwa mayatima, mafukara na wafuasi safi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Lakini baada ya kufariki Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), haki hii walinyimwa kizazi chake. Maulama wenu wenyewe wakubwa kama, Jalalu’d-din Suyuti, katika “Durru’l-Mansur, Jz. 3; Tabari, Imam Tha’labi katika “Tafsir-e-Kashful’l-Bayan”, Jarullah Zamakhshari katika “Kashshaf”, Qushachi katika “Sharh-e- Tajrid”, Nisa’i katika “Kitab-e-Alfiy,” na wengine kwa pamoja wanakubali ukweli kwamba mabadiliko haya yaliingizwa kwa ujanja wa wanasiasa baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hafidh: Unaona kwamba mujtahid ana haki ya kutumia busara zake, je, Khalifa Abu Bakr na Umar hawakutumia maamuzi zao na kujaribu kuwasaidia Waislamu?

Khalifa Hawezi Kupitisha Amri Yenye Kuvunja Amri Ya Wazi Ya Allah Na Mwendo Wa Mtume

Muombezi: Naam hakika mujtahid anayo haki ya kutengeneza hukumu, lakini hawezi akageuza sheria ya wazi. Je, unapendelea maoni ya Khalifa Abu Bakr na Umar kuliko yale yaliyomo kwenye aya ya Qur’ani iliyoko kwenye mjadala na mwenendo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Tafadhali kuwa muadilifu na tuambie iwapo walikuwa na matilaba fulani makhususi nyuma ya yote haya.

Mtu mwenye akili za kawaida atashawishika kuamini kwamba haya hayakuwa mambo ya kawaida, bali yalilienga katika kuifanya familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kukaa bila msaada. Allah Amemfanya Ali Shahidi Wa Mtukufu Mtume (S.A.W.W.)

Mbali na yote haya, Allah amemtangaza Ali kuwa shahidi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Anasema katika Qur’ani: “Basi je, mtu ambaye ana dalili ya wazi itokayo kwa Mola wake, inayo fuatwa na shahidi anayetoka Kwake…ulinzi na rehma?” (11:17) Hafidh: Kadiri ambavyo elimu yangu inakwenda, “ambaye ana dalili wazi kutoka kwa Mola Wake” maana yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na “shahidi” maana yake Qur’ani Tukufu. Kwa nini unadai kwamba hapa “shahidi” maana yake Ali?

Muombezi: Sielezei maoni yangu binafsi kuhusu aya za Qur’ani. Tulichokijua kutoka kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni kwamba “shahidi” hapa maan yake Ali. Maulamaa na wafasiri wana maoni hayo hayo. Maulamaa wenu mashuhuri wameandika takriban hadithi thelathini katika kuliunga mkono hili. Kwa mfano, Imam Abu Ishaq Tha’labi anaandika hadithi tatu katika kitabu chake cha “Tafsir”; Jalalu’d- din Suyuti anaandika kati- ka kitabu chake “Durru’l-Mansur” kutoka kwa Mardawiyya, Ibn Abi Hatim, na Abu Nu’am; Ibrahim Bin Muhammad Hamwaini anaandika katika kitabu chake “Fara’idu’s- Simtain” kutoka kwenye vyanzo vitatu; Sulaimani Balkhi Hanafi anaandika katika kitabu chake “Yanabiu’l- Mawadda” kutoka kwa Tha’labi, Hamwaini, Khawarizmi, Abu Nu’aim, Waqidi na Ibn Abdullah Ansari na wengineo; Hafidh Abu Nu’aim Ispahani anasimulia kutoka vyanzo vitatu tofauti; Ibn Maghazili Faqih Shafi’i, Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali, Ibn Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i (tazama kitabu chake “Kifayatu’t-Talib” sura ya 62) na wengine katika maulamaa wenu wanasimulia pamoja na tofauti kidogo ya maneno kwamba “shahidi” katika aya hii maana yake Ali Bin Talib.

Khatib Khawarizmi anaandika katika kitabu chake “Manaqib” kwamba watu walimuuliza Ibn Abbas ni nini kilichomaanishwa na “shahidi”. Yeye alisema: “Hii inarejea kwa Ali, ambaye alitoa ushuhuda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Hivyo, kwa mujibu wa shuhuda za vitabu vyenu wenyewe vya kutegemewa, ilikuwa ni wajibu kwa jumuiya kukubali ushahidi wa Ali.

Allah Mwenyewe amemuita shahidi wa Mtume. Kama vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alivyokubali ubora uliowazi wa Khazima Bin Thabit na akaulinganisha ushahidi wake sawa na Waislamu wawili na akampa cheo cha Dhu’sh-Shahadatain, Allah swt. vile vile ameelezea katika aya hii cheo kitukufu cha Ali na akamtambulisha kama “shahidi” kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtu hushangaa ni katika misingi ipi ya dini watu hawa waliamua kukataa ushahidi wa Ali.

Je, unaweza kukubali hukumu yao kwamba Ali Bi Abi Talib, ambaye alikuwa akikirihish- wa mno na mali za dunia hii na ambaye adabu na tabia yake ilikubaliwa na marafiki na maadui halikadhalika, alikuwa mtu wa kidunia? Hata maneno yasiopendeza yalitumiwa dhidi yake, ambayo siwezi kuyasema. Yote yameandikwa katika vitabu vyenu.

Hivyo kutumia maneno “masilahi yake binafsi yalihusika katika kesi hiyo,” walikuwa wanajaribu kushawishi watu kwamba inawezekana kwa Ali kutoa ushahidi wa uwongo kwa ajili ya faida ya mkewe na watoto wake. (Allah ayasamehe maneno yangu!) Ajabu iliyoje kwamba ingawa Allah amemtambulisha kwama shahidi wa kuaminika, watu hawa wajanja walikataa ushahidi wake.

Maumivu Makali Ya Kiakili Ya Ali

Ingawaje Qur’ani inatambulisha uaminifu wa Ali, aliteseka kwa sababu ya shutuma za wanasiasa. Alisema katika khotuba yake ya Shiqshiqayya: “Nilivumilia maumivu makali. Ilikuwa kama ninachomwa katika jicho na kukabwa roho.” Maneno haya yanathibitisha vya kutosha na zaidi mateso makali ya Mtukufu Imam.

Alisema: “Naapa kwa jina la Allah kwamba mtoto wa Abu Talib ni mwenye kupenda mno kifo kuliko alivyo mtoto anyonyaye ziwa la mama yake.” Wakati maaluni Abdu’r-Rahman Ibn Muljim Muradi alipompiga dharuba la kichwa kwa upanga wenye sumu, yey Imam alisema: “Kwa Mola wa Kaaba, mimi ni mshindi.”

Mabwana, kile kilichotokea kilipaswa kisitokee. Lakini leo sio sahihi kwa ulamaa wenye busara kama ninyi kusababisha matatizo zaidi kwa mtu mpendwa mno wa Allah na Mtume Wake na kusababisha kutokuelewana miongoni mwa watu wasio na ujuzi. Mnajua kabisa kwamba kumbughudhi Ali Bin Abi Talib kwa hakika ni kumbughudhi Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.).

Hadithi Inayowalaumu Wenye Kumbughudhi Ali

Imamu Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, Imamu Tha’labi katika Tafsir yake na Sheikhu’l-Islam Hamwaini katika kitabu chake Fara’id wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Yule ambaye anamuonea Ali, ananionea mimi. Enyi watu, yeyote yule anayemuonea Ali atafufuliwa Siku ya Hukumu kama Myahudi au Mkiristo.”

Ibn Hajar Makki katika uk. 78 wa sehemu ya 2, sura ya 9, Hadithi ya 16 kutoka kwa Sa’d Ibn Abi Waqqas na Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib, sura ya 68, anasema kwa kutegemea juu ya maandishi sahihi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Yule ambaye anambughudhi Ali, kwa hakika ananibughudhi mimi.”

Nakumbuka hadithi nyingine. Niruhusuni niisimulie. Kusimulia hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuisikia ni ibada. Hadithi hii imeandikwa na Bukhari katika Sahih yake; Imamu Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake; Mir Seyyid Ali Hamadani Shafi’i katika Mawaddatu’l-Qurba; Hafidh Abu Nu’aim Ispahsni katika Maa Nazala Mina’l- Qur’ani fi Ali; Khatib Khawarizmi katika Manaqib na Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib yake wameisimulia hiyo.

Hakim Abu’l-Qasim Haskani vile vile anaisimulia kutoka kwa Hakam Abu Abdullah Hafidh, yeye kutoka kwa Ahmad Bin Muhammad Bin Abi Dawud Hafidh, yeye kutoka kwa Ali Bin Ahmad Ajali, yeye kutoka kwa ‘Ibad Bin Yaqub, yeye kutoka kwa Artat Bin Habib, yeye kutoka kwa Abu Khalid Wasti, yeye kutoka kwa Zaid Bin Ali, yeye kutoka kwa baba yake, Ali Bin Husein, yeye kutoka kwa baba yake, Husein Ibn Ali, yeye kutoka kwa baba yake, Ali Ibn Abi Talib; kila mmoja wa wasimuliaji hawa alisema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: huku akiwa ameshika unywele wa ndevu zake:

“Ewe Ali, yeyote ambaye ataumiza unywele wako mmoja, hakika ananiumiza mimi; yule ambaye ananiumiza mimi hakika anamuumiza Allah, na yule ambaye anamuumiza Allah analaaniwa Naye Allah swt.”

Sayyid Abu Bakr Bin Shahabu’d-din Alawi katika kitabu chake Rashfatu’s-Sa’adi min Bahr-e-Faza’il Bani Nabiu’l-Hadi, (kimepigwa chapa na A’lamiyya Press, Misri, 1303 A.H.) sura ya 4, uk. 60, anasimulia kutoka Kabir cha Tabrani, Sahih ya Bin Habban, na Hakim kutoka kwa Amiru’l-Mu’minin, kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alisema: “Laana ya Allah iwe juu yake yule ambaye ananihuzunisha mimi kuhusiana na kizazi changu.”

Ali Alibughudhiwa Na Kutukanwa

Mabwana, fikirieni yaliyo tokea. Ushahidi wa Ali ulikataliwa hadharani. Mali ya Fatimah ilipokonywa. Pigo hili la uonevu liliumiza sana hisia za Fatimah kiasi kwamba aliutoka ulimwengu huu katika umri wake mdogo wa ujana, akiwa amejawa na masononeko.

Hafidh: Ni wazi kwamba mwanzoni Fatimah alikuwa amesononeka mno, lakini mwishowe wakati alipoona kwamba hukumu ya Khalifa ilikuwa sahihi, hakuwa na hasira tena. Hatimaye aliutoka ulimwengu huu akiwa ameridhika kikamilifu na kutosheka.

Fatimah Alibakia Na Hasira Juu Ya Abu Bakr Na Umar Mpaka Kifo Chake

Muombezi: Kama unayosema ni sahihi, kwa nini maulamaa wenu wakubwa wameandika kinyume chake? Kwa mfano, wanachuoni wawili wa kutegemewa, Bukhari na Muslim, wanaandika katika Sahih zao kwamba Fatimah alimkataa Abu Bakr kwa sababu alikuwa amekasirika. Kwa sababu ya kutoridhika kwake hakuzungumza naye kwa muda wa uhai wake wote uliobakia. Wakati alipofariki, mume wake, Ali, alimzika usiku. Hakuruhusu Abu Bakr kujumuika kwenye mazishi yake na kumsalia.

Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i amesimulia kisa hicho hicho katika kitabu chake “Kifaya,” sura 99. Vile vile Abu Muhammad Abdullah Bin Muslim Bin Qutayba Dinawari katika kitabu chake “Imama wa’s- Siyasa”, uk. 14, anaandika kwamba, wakati Fatimah alipokuwa mgonjwa kitandani, alisema kumuambia Abu Bakr na Umar: “Allah na Malaika wawe mashahidi wangu kwamba ninyi wote (wawili) mmenisononesha. Wakati nitakapokutana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa hakika nitamlalamikia dhidi yenu.” Vile vile vitabu hivi vinaandika: “Fatimah alimkasirikia Abu Bakr na alikataa kuonana naye muda wote wa uhai wake uliobakia.”

Mbali na haya, kuna riwaya nyingi nyingine na hadithi zilizoandikwa katika vitabu vyenu sahihi.

Huzuni Ya Fatimah Ni Huzuni Ya Allah Na Mtume

Kuna hadith inayojulikana sana iliyosimuliwa na maulamaa wenu wengi, kama Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad; Sulaiman Qanduzi katika Yanabiu’l-Mawadda; Mir Sayyid Ali Hamadani katika Mawaddatu’l-Qurba; Ibn Hajar katika Sawa’iq, akisimulia kutoka kwa Tirmidhi, Hakim na wengine, pamoja na tofauti ndogo ya maneno, kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) Amesikika mara kwa mara akisema: “Fatimah ni sehemu ya mwili wangu, ni nuru ya macho yangu, yeye ni tunda la moyo wangu, ni moyo wangu katikati ya mbavu zangu mbili.

Yule ambaye anamhuzunisha Fatimah ananihuzunisha mimi; yule ambaye ananihuzunisha mimi, anamhuzunisha Allah; yule ambaye anamkasirisha yeye ananikasirisha mimi; kinachomuumiza Fatimah huniumiza mimi.”

Ibn Hajar Asqalani, katika kitabu chake “al-Isaba fi tamyiz as-Sahaba”, ananukuu kutoka kwenye Sahih za Bukhari na Muslim kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alisema: “Fatimah ni sehemu ya mwili wangu; kinachomuumiza yeye, huniumiza mimi; kile ambacho huendeleza ufanisi wake wa kiroho, huendeleza ufanisi wangu wa kiroho.”

Muhammad Bin Talha Shafi’i katika kitabu chake “Matalibu’s-Su’ul”; Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika Hilyatu’l-Auliya, Jz. 2, uk. 40, na Imamu Abdu’r-Rahman Nisa’i katika kitabu chake “Khasa’isu’l-Alawi,” wanasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alise- ma: “Hakika Fatimah, bint yangu ni sehemu ya mwili wangu; kinachomfurahisha yeye, hunifurahisha mimi; kinachomchukiza yeye hunichukiza mimi.”

Abu’l-Qasim Husain Bin Muhammad (Raghib Ispahani) anasimulia katika kitabu chake “Mahadhirratu’l- Ubada,” Jz. 2, uk. 204, kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alisema: Fatimah ni sehemu ya mwili wangu; kwa hiyo anayemkasirisha yeye ananikasirisha mimi.”

Hafidh Abu Musa Bin Muthanna Basri (alikufa 252 A.H.) katika kitabu chake “Mu’ajam”; Ibn Hajar Asqalani katika “Isaba”, Jz. 4, uk. 35; Abu Ya’ala Musili katika Sunan yake; Tibrani katika “Mu’ajam”; Hakim Nishapuri katika “Mustadrak”, Jz. 7, uk. 154; Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika “Fadha’ilu’s- Sahaba”; Hafidh Ibn Asakir katika “Ta’rikh-e- Shami”; Sibt Ibn Jauzi katika “Tadhkira”, uk. 175; Muhibu’d-din Tabari katika “Dhakha’ir”, uk. 39, Ibn Hajar Makki katika “Sawa’iq”, uk. 105 na Abu Irfanu’s-Subban katika “As’afu’r-Raghibin”, uk. 171, wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumwambia binti yake, “Ewe Fatimah, hakika, kama ukikasirika Allah Naye vile vile anakasirika; kama ukifurahi, Allah vile vile anafurahi.”

Muhammad Bin Ismail Bukhari katika Sahih yake, katika sura ya Manaqib Qarabat-e- Rasulullah, uk. 71, ananukuu kutoka kwa Miswar Bin Makhrama ambaye alisema kwam- ba, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Fatima ni sehemu ya mwili wangu, hivyo yeyote yule anayemkasirisha Fatima, hakika, ananikasirisha mimi.”

Kuna hadithi nyingi kama hizo zilizoandikwa kwenye vitabu vyenu sahihi, kama Sahih Bukhari; Sahih Muslim; Sunan ya Abu Dawud; Tirmidhi; Musnad ya Imamu Ahmad Hanbal; Sawa’iq-e-Ibn Hajar; na Yanabiu’l-Mawadda cha Sheikh Sulaiman Balkh. Utaoanisha vipi hadithi hizi na riwaya ambazo zinasema kwamba Fatima hakuutoka ulimwengu akiwa amewakasirikia watu hawa?

Tuhuma Kuhusu Ali Kukusudia Kumuoa Bint Ya Abu Jahl

Sheikh: Hadithi hizi ni sahihi, lakini vile vile imesimuliwa kuhusu Ali kwamba wakati alipokusudia kumuoa binti ya Abu Jahl, Mtume wa Allah akamkasirikia na akasema: “Yeyote yule anayemhuzunisha Fatimah ananihuzunisha mimi, na yeyote anayenihuzunisha mimi ni mtu aliyelaaniwa na Allah. Muombezi: Lazima tukubali au tukatae mambo kwa kutumia akili ya kuzaliwa na busara. Allah anasema katika Qur’ani: “Kwa hiyo wape habari njema waja wangu wale ambao wanaosikiliza maneno, kisha wakafuata yale yaliyo mazuri; hao ndio wale ambao Allah amewaongoza, na hao ndio watu ambao wanafahamu.”

Riwaya ilisimuliwa na wahenga wenu. Leo mnaunga mkono maneno yao bila kupima ubora wao. Ninawajibika kukupa jibu fupi. Kwanza, maulamaa wenu wenyewe wamekubali ukweli kwamba Ali alijumuishwa katika “aya ya utakaso” na alikuwa ameto- harika kikamilifu. Pili, katika “aya ya Mubahila”, Allah amemuita “nafsi” ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama tulivyokwisha kulijadili katika mikesha iliyopita.

Tumeonesha kwamba alikuwa vile vile “mlango wa elimu ya Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.)” na alikuwa anaelewa kwa ukamilifu amri na sheria za Qur’ani. Alijua kwamba Allah alisema katika Sura ya Ahzab ya Qur’ani Tukufu: “Na haiwapasi ninyi kwamba mumpe matatizo Mjumbe wa Allah.”

Kwa vile hii ni kweli, Ali angewezaje kufanya au kusema kitu chochote ambacho kingemuudhi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Na mtu atafikiriaje kwamba mfano halisi wa ubora, yaani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) atachukizwa na shaksiya ya mtu huyo aliyetukuka ambaye alipendwa na Allah? Na je, atachukizwa na kitendo ambacho kimeruhusiwa na Allah, kama Anavyosema katika Qur’ani Tukufu:“…basi oeni wanawake wale ambao wanaonekana wazuri kwenu, wawili, au watatu au wanne”?

Amri hii ya nikah (ndoa) ni ya umuhimu wa jumla na imekusudiwa kwa ajili ya umma wote halikadhalika na kwa ajili ya mitume na waandamizi. Na kama tukichukulia kwam- ba Amiru’l-Mu’minin alikuwa na kusudio lolote kama hilo, ilikuwa ni ruhusa kwake.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kuzuia tendo lolote linaloruhusiwa, wala hakutumia maneno kama hayo. Mtu yeyote mwenye akili, baada ya kuzingatia kwa makini, ataweza kujua kwamba riwaya hii ni moja ya riwaya za kughushi za Bani Umayya. Wanachuoni wenu wakubwa wanaukubali ukweli huu.

Uzuaji Wa Hadithi Wakati Wa Kipindi Cha Mu’awiyah

Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali ananukuu riwaya kutoka kwa kiongozi na mwalimu wake, Abu Ja’far Iskafi Baghdadi, katika kitabu chake “Sharh-e-Nahju’l-Balaghah”, Jz. 1, uk. 358, kwamba Mu’awiya Bin Abu Sufyani aliunda kikundi cha Masahaba na tabi’in (kizazi cha pili ambacho kilifuata mara tu baada ya Mtume) kwa madhumuni ya kughushi hadithi zenye kumlaani Ali.

Madhumuni yao yalikuwa ni kumfanya mlengwa wa shutuma ili kwamba watu wajitenge mbali naye. Miongoni mwao walikuwamo Abu Huraira, Amr Bin Aas, Mughira Bin Shaiba, Urwa Bin Zubair, mmoja wa tabi’in vile vile alikuwa pamoja nao. Abu Ja’far Iskaf vile vile amerejea kwenye baadhi ya hadithi zao za kughushi.

Akizungumzia kuhusu Abu Huraira, anasema kwamba alikuwa ni mtu ambaye alisimulia hadithi yenye maana ya kuonesha kwamba Ali alitaka kumuoa binti wa Abu Jahl wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hili likamasirisha Mtume, na akasema juu ya mimbar, “Rafiki wa Allah na adui wa Allah hawawezi kuwa pamoja. Fatimah ni sehemu ya mwili wangu. Yule ambaye anamhuzunisha yeye ananihuzunisha mimi. Yule ambaye anataka kumuoa bint ya Abu Jahl lazima atafute kutengana na binti yangu.”

Baada ya hili, Abu Ja’far anasema kwamba hadithi hii inajulikana kama hadithi ya Karabis, kwa vile kila hadithi isiyo na msingi inaitwa karabis (kilugha, muuzaji wa nguo).

Ibn Abi’l- Hadid anasema kwamba hadithi hii imesimuliwa katika Sahih mbili ya Bukhari na Muslim kutoka kwa Miswar Bin Makhrama za-Zahr.

Na Sayyid Murtaza Alamu’l-Huda, ambaye alikuwa mmoja wa maulamaa wakubwa wa Mashi’a, anasema katika kitabu chake “Tanzia’u’l-Anbia wa’l-A’imma” kwamba riwaya hii ilisimuliwa na Husein Karabisi, ambaye anajulikana kwa upinzani wake mkali kwa Ahlul’l-Bayt watukufu.

Alitokana na Nawasib na alikuwa mmoja wa maadui wakubwa wa familia hii tukufu. Riwaya yake haikubaliki. Kwa mujibu wa hadithi zilizosimuliwa katika vitabu vyenu sahihi, adui wa Ali ni mnafiki (munaafiq). Munafiq kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu, ni kiumbe muovu kabisa. Kwa hiyo hadithi yake haina ubora wowote.

Mbali na hili, hadithi zinazowalaani watu wanasababisha maudhi kwa Fatimah hazikomei kwenye maelezo ya Karabisi au ile riwaya ya kughushi ya Abu Huraira kuhusu binti ya Abu Jahl.

Kuna hadithi nyingi nyingine juu ya suala hili. Miongoni mwazo ni ile iliyosimuliwa na Parsa wa katika kitabu chake, “Faslu’l-Khitab”; moja iliyisimuliwa na Imamu Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake na Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i katika Mawadda 13 ya Mawddatu’l-Qurba, kutoka kwa Salman Muhammadi, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mapenzi ya Fatimah yana manufaa kwetu sisi katika sehemu mia moja, nyepesi mno ya hizo ikiwa ni Kifo, Kaburi, Mizani, Sirat (daraja) na Kusailiwa.

Hivyo, kama binti yangu Fatimah, yuko radhi na mtu fulani, mimi vile vile niko radhi naye huyo. Kama nikiwa radhi na mtu fulani, Allah vile vile atakuwa radhi naye. Kama binti yangu Fatimah hayuko radhi na mtu fulani, mimi vile vile sitakuwa radhi naye. Kama siko radhi naye, Allah vile vile hatakuwa radhi naye. Ole wake yule anayemuonea Fatimah na mume wake. Ole wake yule anayemuonea Ali na Fatimah na Mashi’a wao.”

Nawaulizeni ni uamuzi gani mtakaochukua katika mwanga wa hadithi hizi sahihi na hadithi zilizoandikwa na Bukhari na Muslim kwamba Fatimah alibakia amewakasirikia Abu Bakr na Umar mpaka kufa kwake.

Kuelewa Vibaya Kuhusu Hasira Za Fatima Kwamba Sio Za Kidini

Hafidh: Naam kwa hakika hadithi hizo ni sahihi na zimeandikwa kwa urefu katika vitabu vyetu sahihi. Kwa hakika hata mimi vile vile niliitilia shaka riwaya ya Karabisi kwamba Ali alitaka kumuoa binti ya Abu Jahl. Mimi sikuiamini, na sasa kwa hakika ninashukuru sana kwamba umenitatulia tatizo hili.

Pili, katika hadithi hizi “hasira” maana yake ni hasira za kidini na sio hasira za mambo ya kawaida ya kidunia. Hasira yake kuhusiana na Abu Bakr na Umar, ambayo imeandikwa katika vitabu vyetu vyote sahihi, haikuwa ya kidini. Yaani, Fatimah hakuwa na hasira na Abu Bakr na Umar kwa sababu walivunja amri yoyote ya kidini. Kwa hakika, kama mtu yeyote aliamsha hasira zake za kidini, angepasika na laana ya Mtume wake.

Lakini kwa kweli hasira ya Fatimah ilitokana na mabadiliko katika hali yake, ambayo kila mtu mwenye hisia huhisi wakati akishindwa kufikia lengo lake. Kwa vile Fatimah alitoa maombi kwa ajili ya Fadak na Khalifa hakukubali madai yake, kwa kawaida aliathirika kwalo na akajisikia hasira kwa wakati ule. Lakini baadae chuki hii ndogo ilitoweka katika mawazo yake, na aliridhika na uamuzi wa Khalifa.

Uthibitisho wa kuridhika kwake ni ukimya wake. Na wakati Ali alipochukua hatamu za ukhalifa, pamoja na mamlaka yote makubwa aliyokuwa nayo, hakuirudisha Fadaka chini ya miliki yake. Huu pia ni uthibitisho kwamba aliridhika na uamuzi wa makhalifa waliopita.

Fatimah Alikuwa Huru Kutokana Na Kujiambatanisha Na Mambo Ya Kidunia

Uombezi: Kwanza, umesema kwamba hasira ya Fatimah haikuwa ya kidini bali ilikuwa ya kidunia. Umeelezea mtazamo huu bila uchunguzi makini. Kwa mujibu wa kanuni za aya za Qur’ani na hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hakuna muumini mkamilifu angethubutu kuonesha chuki kama hiyo, achilia mbali kumtaja Fatima, ambaye utukufu wake uko wazi kutoka kwenye “Aya ya Utakaso” “Aya ya Mubahila” na Surat Hal Ata ya Qur’ani Tukufu (76: 1).

Kuna hadithi nyingi katika vitabu sahihi vya kwenu na vya kwetu, kwamba Fatimah alikuwa na cheo cha juu sana cha imani, na kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa uwazi alisema kuhusu yeye: “Hakika, Allah amemjaza kwa imani bint yangu, Fatimah, kuanzia kichwani mpaka miguuni.”

Hasira Ya Fatimah Imechochewa Na Dini

Muumini yeyote, mwamume au mwanamke, ambaye alama yake maalumu ni kuukubali ukweli, kamwe hataonesha hasira wakati hakimu akitoa amri ya haki. Wala muumini kama huyo hatashikilia kwenye hasira hizo na ghadhabu mpaka kifo chake akisisitiza katika wosia wake kwamba wale wote ambao kwa njia yotote walihusika na amri hizo wasiruhusiwe kujuinga katika sala yake ya mazishi.

Aidha, Fatimah ambaye kuhusu usafi wake Allah Mwenyewe anautolea ushahidi, asingeweza kamwe kufanya madai ya uwongo, hivyo kwamba hakimu aweze kulikataa dai lake.

Pili, kama hasira ya Bibi Fatimah ilikuwa tu ni “hasira ya kidunia” kama unavyoiita, au kuchukizwa kwake kwa kukataliwa dai lake, hasira yake ingelishuka mara moja, hususan baada ya kujuta kulikooneshwa na wale ambao walihusika na hasira yake hiyo. Kusingelikuwa na huzuni katika moyo wake.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Moja ya alama za muumini ni kwamba kwa kawaida huwa haweki mfundo wa moyo uliojengeka juu tamaa za kimwili, dhidi ya mtu yeyote.” Vile vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kama muumini akitokea kufanya kosa, muumini aliyechukizwa nalo hatakuwa na chuki kwake kwa zaidi ya siku tatu.”

Hivyo Fatimah Zahra aliye mkweli na safi, ambaye kwa mujibu wa ushuhuda wa Allah swt., amejazwa imani kutoka kichwani mpaka miguuni, kamwe asingeweza kuwa na kinyongo dhidi ya mtu yeyote. Na inakubaliwa na madhehebu zote kwamba Fatimah aliutoka ulimwengu huu akiwa amemkasirikia Abu Bakr na Umar. Hivyo inamaanisha kutokana na hili kwamba hasira ya Fatimah ilikuwa ya kidini kabisa.

Wakati alipoona kwamba hukumu inapitishwa dhidi yake kwa kuvunja amri ya Allah na ya Mtukufu baba yake, alijihisi kukasirika mno kwa maudhi ya kidini na hii ndio ile hasira inayoleta ghadhabu ya Allah na Mtume Wake.

Ukimya Wa Fatimah Haukuashiria Kuridhika Kwake

Tatu, umesema kwamba kwa vile ukimya wa Fatima ulimaanisha aliridhiana na uamuzi huo. Hapa tena umekosea. Ukimya sio lazima uwe na maana ya kukubaliana. Wakati mwingine ukatili wa mkandamizaji hulazimisha kukubali. Fatima si kwamba alihuzunishwa tu, bali aliutoka ulimwengu huu akiwa amekasirika. Wote wawili, Bukhari na Muslim wameandika: “Fatimah alimkasirikia Abu Bakr. Alijitenga naye na hakuzungumza naye kwa maisha yake yote yaliobakia.”

Ali Hakuwa Huru Kutenda Wakati Wa Kipindi Cha Ukhalifa Wake

Nne, umesema kwamba kwa sababu Ali, wakati wa ukhalifa wake, hakuchukuwa umiliki wa Fadak na kuirudisha kwa kizazi cha Fatimah, hii inaashiria kukubaliana kwake na uamuzi wa Makhalifa waliopita. Hata hapa pia umekosea. Mtukufu Imam alikuwa hayuko huru kutenda wakati wa kipindi chake cha ukhalifa ili aweze kuzuia bidaa yoyote au kurudisha haki yoyote. Wakati wowote alipotaka kuchukua hatua kama hiyo, kulikuwa na upinzani wa mara moja.

Kama angeirudisha Fadak kwa kizazi cha Fatimah, wapinzani wake, hususani Mu’awiya na wafuasi wake, wangelidai kwamba Ali anafanya kinyume na mwenendo waliofuata Abu Bakr na Umar. Mbali na hili, ili kupitisha hukumu kama hizo, mamlaka na uhuru vilikuwa ni muhimu sana.

Lakini watu hawakumruhusu kuwa na uwezo kama huo. Asingeweza kuanzisha kitu chochote ambacho kingevunja kanuni na mwenendo wa Makhalifa waliotangulia. kutokuwa kwake na uwezo Ali, kuko wazi katika mifano miwili ifuatayo.

Kwa vile Makhalifa waliotangulia waliiondoa mimbari kutoka mahali pake ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliiweka, Mtukufu Imam alikusudia kuirudisha kwenye sehe- mu yake ya asili.

Lakini watu walimpinga na hawakuweza kuvumilia kitu chochote kilicho kinyume na mwenendo wa Abu Bakr na Umar, hata kama kingekuwa hakiafikiani na mwenendo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Halikadhalika, wakati Mtukufu Imam alipowakataza watu kusali swala ya tarawehe kwa jamaa, walimpinga na wakadai kwamba Ali alitaka kubadilisha mwenendo wa Khalifa Umar.

Nawab: Mheshimiwa! Tarawehe ilikuwa ni kitu gani ambacho Ali alikataza isiswaliwe kwa jamaa?

Muombezi: Kilugha tarawehe ni wingi wa tarawia, ambayo maana yake “kikao”. Baadaye ikajakuwa na maana ya “kukaa kwa ajili ya kupumzika” baada ya rakaa nne za sala za usiku wakati wa mwezi wa Ramadhan. Kisha ikaja kumaanisha rakaa nne za sala ya sunna (iliyopendekezwa). Ni kanuni ya wazi katika sheria ya ki-Islamu kwamba ni sala za wajib tu ndizo ambazo huswaliwa kwa jamaa, ambapo zile za sunna kuzisali kwa jamaa imekatazwa.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alisema: “Hakika kusali nafila (sunna) katika jamaa wakati wa usiku katika mwezi wa Ramadhani ni uzushi (bid’a). Namaz-e-Chasht (wakati mwingine hujulikana kama Dhuha na husaliwa kabla ya adhuhuri, au jua linapochomoza na kupanda kidogo) ni dhambi. Enyi watu! Msisali sala za nafila (sunna) katika mwezi wa Ramadhan kwa jamaa na msisali Namaz-e-Chasht (Dhuha). Kwa kuwa na uhakika, kufanya kitendo kidogo cha ibada kwa mujibu wa sunnah ni bora kuliko kufanya kitendo kikubwa ambacho ni uzushi (bid’a). Naifahamike kwenu wote kwamba kila bid’a ni upotovu na kila upotovu unaongozea kwenye moto.”

Usiku mmoja wakati wa ukhalifa wake katika mwaka wa 14 A.H. Umar aliingia msikitini. Aliona kwamba watu walikuwa wamekusanyika pale. Akawauliza ni kwa nini wameku- sanyika. Wale watu wakasema wamekusanyika ili kuswali sunna. Umar akasema: “Kitendo hiki ni bid’a, lakini ni bid’a nzuri.”

Bukhari ananukuu katika Sahih yake kutoka kwa Abdu’r-Rahman Bin Abdu’l-Qari kwam- ba wakati Khalifa alipowaona watu wanasali kila mmoja peke yake, aliwaambia kusali kwa jamaa kunafaa zaidi. Alimuamuru Ubayy Bin Ka’b kuongoza sala hiyo kwa jamaa. Wakati alipokuja msikitini usiku uliofuatia, aliwaona watu wanasali jamaa kwa kutii amri yake. Akasema: “Uzuri ulioje wa bid’a hii.”

Ikawa ni jambo la kawaida mpaka wakati wa Amiru’l-Mu’minin. Yeye aliikataza, akisema kwamba kwa vile haikuwepo wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa hivyo ilikatazwa, kwa hakika isiruhusiwe kuendelea.

Wakati alipokuja Kufa, watu wa Kufa walimuomba Mtukufu Imam kuwateulia mtu kwa ajili ya kuongoza sala za nafila wakati wa usiku wa mwezi wa Ramadhani. Imamu aliwakataza kusali sala hiyo kwa jamaa. Pamoja na amri hiyo, kwa vile watu walikuwa wamezoea hivyo, hawakufuata amri ya Imamu.

Mara tu Imamu alipoondoka kwenye sehemu ile, walijikusanya pamoja na wakamteuwa mmoja wao kuongoza sala katika jamaa.

Punde tu habari zilimfikia Imamu, ambaye alimuita Hasan mtoto wake mkubwa na alimtaka achukue jambia na akawakataze watu wale kusali sunna kwa jamaa. Wakati watu walipoona hivyo, walipiga makelele wakisema: “Ewe Ali! Hasan amekuja, na haturuhusu sisi kuswali.”

Ingawa walijua kwamba jambo hili la kusali sala za sunna katika jamaa halikuwepo wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hawakufuata amri ya Ali ambayo iliafikiana na amri za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Sasa vipi Ali angeweza kuirejesha Fadak kwa kizazi cha Fatimah? Kama angelifanya hivyo, na aseme ilichukuliwa isivyo halali, watu wangepiga kelele kwamba Ali Bin Abi Talib amevutwa na mapenzi ya dunia na anapora haki ya Waislamu kwa ajili ya watoto wao.

Hivyo aliona ni bora kuwa na subira. Kwa vile mdai halisi alikuwa ametoweka ulimwenguni hapa, madai yake aliyaahirisha, ili kwamba wakati Imamu wa mwisho mwenye kuongozwa kimungu atakapokuja kurudisha haki kwa wahusika wake wa halali, na yeye atapata haki yake. Katika hali ya mambo kama hayo, ukimya wa Mtukufu Imamu haukuwa na maana kwamba aliridhika na uamuzi huo.

Kama angekichukulia kitendo cha Makhalifa waliotangulia kuwa ni cha haki, asinglihoji suala lake mbele yao. Vile vile, asingeelezea machungu yake na kuudhika kwake, na asigemuomba Allah kuwa muamuzi wake. Imeandikwa katika Nahju’l-Balagha kwamba katika barua aliyompelekea Gavana wa Basra Uthman Bin Hunaif Ansari, Ali aliandika: “Miongoni mwa vitu ambavyo kwamba mbingu hutupa kivuli chake juu yake ni Fadak, ambayo ilikuwa kwenye milki yetu. Lakini kundi moja likaonesha uchoyo, na upande mwingine, Fatimah na watoto wake waliacha kuendelea na madai yao. Na Allah Ndiye Hakimu aliye bora.”

Umesema kwamba Fatimah aliridhika na uamuzi huo katika siku zake za mwisho za uhai wake na akawasamehe wale ambao walihusika na suala hili. Nina wasiwasi hapa umekosea. Kwani kama ambavyo imethibitishwa mapema bila mashaka yoyote kwa hadithi zenye kutegemewa kwamba Bibi madhulum alibakia ni mwenye kukasirika mpaka alipofariki.

Abu Bakr Na Umar Walijaribu Kumtembelea Fatimana Kuelezea Maoni

Yao Lakini Hawakufanikiwa

Kuthibitisha maoni yangu ningependa kuwasilisha riwaya ifuatayo: Abu Muhammad Abdullah Bin Muslim Bin Qutayba Dinawari (alikufa mwaka 276 A.H.) katika kitabu chake “Ta’rikh-e-Khilafa’i’r-Rashidin” kijulikanacho kama ‘Al-Imama was-Siyasa’, Jz. 1, uk. 14 na wengine miongoni mwa maulamaa wenu, kama Ibn Abi’l-Hadid, wanaandika katika vitabu vyaovya sahih: “Umar alimuomba Abu Bakr waende pamoja naye kumtembelea Fatimah. Kwa hakika walikuwa wamemkasirisha sana. (baadhi ya riwaya zinasema alikuwa ni Abu Bakr aliyemuomba Umar kwenda naye kumtembelea Fatimah. Hii inaonekana ni yenye kukubalika zaidi).

Kwa ufupi wote kwa pamoja walikwenda kwenye mlango wa Fatumah lakini yeye hakuwaruhusu wamuone. Wakati walipomuomba Ali angilie kati yeye alinyamaza kimya, lakini aliwaruhusu kuingia ndani. Wakati walipoingia ndani na kumsalimu, aligeuzia uso wake ukutani. Abu Bakr akasema: “Ewe pande la ini la Mtume! kwa jina la Allah, nauthamini uhusiano wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wewe zaidi kuliko uhusiano wangu mimi na binti yangu Aisha.

Lau ingelikuwa nife mapema baada ya Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.). Najua cheo na daraja yako zaidi kuliko mtu mwingine yeyote. Kama nimekunyima haki yako ya kurithi, ni kwa sababu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye mimi mwenyewe nimemsikia akisema: ‘Sisi Mitume hatuachi urithi wowote. Tunachoacha ni sadaka (kwa ajili ya Waislamu).’

Fatima akamuambia Amiru’l-Muminin kwamba atawakumbusha hadithi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kuwataka waseme kwa jina la Allah kama hawakumsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiisema: “Furaha ya Fatuma ni furaha yangu, hasira ya Fatima ni hasira yangu. Hivyo mwenye kumpenda binti yangu Fatima ananipenda mimi; mwenye kumfurahisha Faima ananifurahisha mimi. Mwenye kumchukiza Fatima, ananichukiza mimi.” Wote wakasema: ‘Ndio tumesikia maneno hayo kutoka kwa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.).’ Kisha Fatimah akasema: ‘Namuomba Allah na malaika Wake kushuhudia kwamba ninyi wote mumenichukiza na hamkunitendea haki. Wakati nitakapokutana na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hakika nitamlalamikia juu yenu ninyi wote.’

Abu Bakr Alitambua Uzito Wa Hasira Ya Fatimah

Abu Bakr akiwa ameguswa na maneno haya, alianza kulia na akasema: ‘Najikinga kwa Allah kutokana na hasira ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).’ Fatimah alianza kulia na alisema: “Naapa kwa jina la Allah kwamba nitaomba laana ya Allah iwe juu yenu katika sala zangu zote.’

Baada ya kusikia haya, Abu Bakr alitoka nje huku akilia, watu wakamzunguuka na kumliwaza. Yeye akawaambia: ‘Ole wenu. Ninyi wote mna raha, mmekaa na wake zenu kwa raha, lakini mimi niko katika hali hii ya unyonge. Sihitaji kiapo chenu. Kiondoeni kutoka kwangu. Kwa jina la Allah, baada ya kile nilichokiona na kusikia kutoka kwa Fatimah, sitaki Mwislamu yeyote apate shida ya mzingo wa kiapo cha utii kwangu.’”

Riwaya hizi zilizosimuliwa na maulamaa wenu wenyewe wa kuheshimika, huonesha kwamba madhulumat Fatimah alikuwa amewakasirikia Abu Bakr na Umar mpaka saa ya mwisho ya uhai wake.

Fatima Alizikwa Usiku, Ikiwa Ni Ushahidi Wa Hasira Yake Ya Kudumu Kwa

Abu Bakr Na Umar

Ushahadi wa wazi kabisa wa hasira ya Fatimah kuhusiana na jambo hili, ni kwamba alimuusia mumewe Amiru’l-Mu’minin Ali kama ifuatavyo: “Asiruhusiwe hata mtu mmoja katika wale watu ambao walinidhulimu na kupora haki yangu, kushiriki katika mazishi yangu. Hakika ni maadui wangu na maadui wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Usimruhusu yeyote kati yao au washirika wao kusalia jeneza langu. Nizike usiku wakati watu wakiwa wamelala.”

Bukhari anaandika katika Sahih yake kwamba Ali alitekeleza wosia wa Bibi Fatimah na akamzika usiku kimya kimya. Watu walijaribu kwa bidii zao zote kutaka kujua alipozikwa Fatimah, lakini walishindwa kujua. Inakubaliwa na wote kwamba Fatimah alizikwa usiku kwa mujibu wa wosia wake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliacha binti mmoja ili awe kama kumbukumbu yake.

Maulamaa wenu wanakubali kwamba alisema: “Fatimah ni sehemu ya mwili wangu. Yeye ni urithi na amana yangu. Mheshimuni yeye kama mnavyoniheshimu mimi. Kamwe msifanye kitu chochote kitakachoamsha hasira zake dhidi yenu. Kama anawakasirikia ninyi, mimi vile vile nitawakasirikia.”

Mir Sayyid Ali Hamadani Faqih Shafi’i anaandika katika kitabu chake, “Mawaddatu’l- Qurba” kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Wale ambao wanamkasirisha Fatimah nitawashughulikia kwa ukali sana Siku ya Hukumu. Furaha ya Fatimah ni furaha yangu, na hasira ya Fatimah ni hasira yangu.

Ole wake yule ambaye anakasirikiwa na Fatimah.” Huzuni ilioje kwamba matamko yote haya, umma si kwamba umempuuza tu, bali vilevile wamempokonya haki yake na kumsabibishia mateso makubwa.

Hata wakati ambapo alikuwa msichana mdogo, alitamka: “Nilipatishwa na matatizo mengi mno kiasi kwamba kama siku zingepatwa na matatizo kama hayo, basi zingegeuka kuwa usiku.”

Mkutano Wa Tisa, Usiku Wa Ijumaa 2 Sha’ban 1345 A.H.

Sheikh: Siku zote unakosoa matendo ya Masunni, lakini hujali mwenendo wa Mashi’a. Unawatetea pasi na haki ingawa matendo yao yamepotoka.

Muombezi: Nimezoea kutetea haki. Imamu wetu Amiru’l-Mu’minin, aliwanasihi watoto wake, hususan Hasan na Husein kwa maneno haya: “Siku zote semeni kweli na fanyeni matendo yenu kwa kuzingatia kesho akhera. Kuweni wakali kwa madhalimu na wasaidieni wanaodhulumiwa.”

Kama nimewakosoa wapinzani au kuwatetea Mashi’a, nimefanya hivyo kwa kuunga mkono ukweli. Kile nilicholalamikia kilikuwa katika misingi ya hoja ya kimantiki. Nitasikiliza madai yako kuhusiana na matendo mabaya ya Mashi’a.

Mashi’a Kumshutumu Aisha Kwa Uzinifu Na Majibu Yake

Sheikh: Kitu kiovu kabisa ambacho Mashi’a wana hatia nacho ni kwamba wanamshutumu Ummu’l- Mu’minin Aisha na uzinifu. Ni ukweli unaokubalika kwamba alipata heshi- ma ya unyumba na Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.), na kwamba alikuwa mkewe kipenzi. Hawatambui shutuma hizi za masingizio zinaelekeza kwenye kitu gani. Hawakusoma Sura ya an-Nur ya Qur’ani Tukufu? Allah anasema: “Wanawake wabaya ni kwa wanaume wabaya, na wanaume wabaya ni kwa wanawake wabaya, na wanawake wema ni kwa wanaume wema, na wanaume wema ni kwa wanawake wema.” (24:26)

Muombezi: Kwanza madai ya kwamba Mashi’a wanamshutumu Ummu’l-Mu’minin Aisha kwa matendo ya kifisadi na uzinifu ni ya uwongo kabisa. Kamwe kitu kama hicho hakijasemwa na Mashi’a.

Madai haya ni uzushi wa dhahiri uliosambazwa na Nawasib na Khawarij karne nyingi zilizopita ili kuchochea ghasia. Waliyahusisha kwa Mashi’a yale ambayo wameyasema wao wenyewe. Matokeo yake wengine bila kufanya utafiti, wakawashambulia Mashi’a kama unavyofanya wewe sasa. Kama ungelisoma vitabu vya Mashi’a, usingeona mahali popote ambapo Ummu’l-Mu’minin Aisha ameshutumiwa kwa uzinzi.

Kumtoa Aisha Kwenye Shutuma Ya Uzinifu

Kama utosoma vitabu vya historia na vya tafsir vya Shi’a, utaona jinsi gani walivyomtetea Ummu’l- Mu’minin Aisha kutokana na shutuma za uzinzi. Ukweli ni kwamba riwaya kama hizi zilifanywa na kikundi cha wanafiki wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Baadhi ya waliohusika ni Mista Bin Uthatha, Hasan Bin Thabit na Abdullah Bin Ubayy. Kuhusu Aisha kutolewa katika shutuma za uwongo za wanafiki, aya saba ziliteremshwa katika Qur’ani Tukufu. Mashi’a wanaamini kwamba kutoa shutuma za uwongo za uzinzi au tendo la kifisadi dhidi ya Mwislamu ni haramu, sikuambii kumtaja mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), awe yeye ni Aisha au Hafsa.

Mume Na Mke Sio Lazima Washiriki Kiwango Kimoja Cha Mafanikio

Pili, Aya Tukufu ambayo umeisoma haina maana ya kile ulichokisema. Sio lazima hivyo kwamba kama mume ni muumini mwema na anayestahiki Pepo kwamba na mkewe naye atakuwa ni hivyo hivyo. Kuna mifano mingi ambayo inathibitisha kwamba wenza wanaweza kuwa viwango tofauti vya ubora.

Allah anasema katika Surat-Tahrim: “Allah anapiga mfano wa waliokufuru, kwa mke wa Nuhu na mke wa Luti, hawa wawili walikuwa chini ya waja wetu wema wawili, basi (wanawake hao) wakawafanyia khiyana, (lakini waume zao) hawakuwasidia chochote mbele ya Allah na ikasemwa: Ingieni motoni pamoja na waingiao. Na Allah anapiga mfano wa walioamini kwa mke wa Firauni aliposema: ‘Ee Mola Wangu! Nijengee nyumba peponi karibu Yako na uniokoe na Firauni na matendo yake, na uniokoe kutoka kwa watu madhalimu.” (66:10-11)

Sheikh: Inashangaza kwamba kwa kipindi kifupi hiki kunajitokeza mabadiliko katika maelezo yako. Muombezi: Tafadhali nieleze hicho unachoona kama mabadiliko.

Sheikh: Katika sehemu moja unasema kwamba kumshtumu mtu yeyote kwa uzinzi ni haramu, lakini katika sehemu nyingine unasema kwamba mke wa Nuhu na mke wa Luti hawakuwa waaminifu kwa waume zao. Je, kauli hizi mbili sio mbali mbali kwa kila moja? Je, si makosa kwako wewe kuwashutumu wake za mitume kwa uzinzi na kutokuwa waaminifu?

Muombezi: Nina hakika unajua kwamba unatumia njia ya hila. Unajua vizuri sana “kutoaminika” inamaanisha nini katika aya tukufu ya Qur’ani tuliyoirejea mwanzo. Maana Ya Kutoaminika Kwa Mke Wa Nuhu Na Mke Wa Luti

Ni ajabu juu yako kwamba unalikosea neno kutokuaminika kuwa lina maana ya uzinzi ingawa kuna tofauti kubwa kati ya maneno mawili haya. Wake wa Mitume walikuwa wameepukana kabisa na uzinzi. Hapa mjadala ni kuhusu kutokuaminika kwao. Kwanza, mke wa Mtume akitenda kinyume na maelekezo ya mumewe, basi hakika sio muaminifu. Pili, sio mimi ninayesema kwamba wameonesha kutoaminika. Qur’ani yenyewe inalielezea hilo: “Walikuwa sio waaminifu kwa waume zao,” na kutoaminika hakukuwa uzinzi. Kama nilivyosema mwanzo, wake za mitume wameepushwa kabisa na aina hii ya udanganyifu.

Hivyo maana ya kutoaminika kwao kulikuwa ni utovu wa utii (uasi). Mke wa nabii Nuhu alikuwa akipingana na mume wake na alikuwa akimfedhehi hadharani. Alisema: “Mume wangu ni mwenda wazimu. Kwa vile niko naye mchana kutwa na usiku, naijua hali yake halisi. Asikudanganyeni.” Mke wa Luti alikuwa akiwajulisha watu juu ya kila mgeni aliyekuja nyumbani kwake. Alikuwa akisababisha matatizo kwa kufichua siri za nyumbani kwa maadui zake.

Kutokuaminika Kwa Wake Hakumaanishi Kuwa Wachafu

Kwa mujibu wa mufasirina wa Qur’ani na vile vile kwa mujibu wa maelezo ya Ma’sumin, maana ya ya aya ya an-Nur, ambayo kwayo unatoa maoni yako, ni kwamba wanamke wachafu wanastahili wanaume wachafu na wanaume wachafu wanavutiwa nawo. Wanamke safi wanastahiki wanaume safi, na wanaume safi wanavutiwa nawo.

Katika sura hiyo hiyo katika aya iliyotangulia Allah anasema: “Mwanaume fasiki hataoa ila mwanamke fasiki au mwanamke mshirikina, na mwanamke fuska haolewi ila na mwanaume fuska au mshirikina .....” (24:3) Kwa ufupi, aya tukufu “wanawake wachafu kwa wanaume wachafu…” kwa njia yoyote haithibitishi hoja yako.

Kuhusiana Na Tabia Ya Aisha

Kukosolewa kwa Aisha sio kwa sababu ya chuki. Ni kwa sababu ya tabia yake mbaya. Aisha amefanya maovu ambayo hakuna mke mwingine wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), pamoja na Hafsa bint wa Umar aliyeyafanya. Aidha, ukosoaji wa Mashi’a uko hasa hasa ndani ya mipaka ya maelezo yaliyotolewa na maulamaa wenu wenyewe, ambao wanasimulia kwamba mwanamke huyu mwenye dukuduku alifanya maovu mabaya mno.

Sheikh: Je, ni sahihi kwa mtu mtukufu kama wewe kutoa shutuma kama hizo dhidi ya Ummu’l- Mu’minin?

Muombezi: Wake wote wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wako sawa kwa daraja isipokuwa Ummu’l- Mu’muminin Khadija (yeye daraja yake ni kubwa). Ummu Salama, Suda, Aisha, Hafsa, Maimuna, na wengine kwa mtazamo wetu sisi, wote ni Ummu’l-Mu’minin. Lakini tabia ya Aisha na maneno yake kwa hakika yalikuwa tofauti na yale ya wanawake wengine. Tena, haya sio maneno yangu tu, lakini maulamaa wenu wameandika kwamba maisha yake yalikuwa na dosari. Matendo mazuri na mabaya ya watu hayawezi kufichika daima. Hatimaye ukweli hujitokeza wenyewe.

Sheikh: Bila shaka, kwa sababu alimpinga Ali, unamkosoa kuhusiana na mambo yasiyo na maana.

Muombezi: Hatumkosoi kuhusiana na mambo yasiyo na maana. Upinzani wa Aisha kwa Amiru’l- Mu’minin, Imam Hasan, Imam Husein, na Ahlu’l-Bayt ni suala tofauti. Lakini msingi wa historia mbaya wa maisha yake uliwekwa wakati wa kipindi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Alikuwa akimuudhi na kumsumbua sana.

Sheikh: Inashangaza kwamba unamuona Ummu’l-Mu’minin Aisha, mke kipenzi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kuwa asiye na thamani kimaadili kiasi hicho na unathubutu kusema kwamba alimuudhi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tutaamini vipi madai yako wakati Ummu’l-Mu’minin kwa hakika alisoma Qur’ani Tukufu na aya ifuatayo: “Kwa hakika wale ambao wanamuudhi Allah na Mtume Wake, Allah amewalaani duniani na akhera, na amewaandalia adhabu ya kufedhehesha. (33:57).

Hivyo inawezekana kwa yeye kumuudhi Mtukufu Mtume ili aweze kulaaniwa na Allah? Hii kwa hakika ni moja ya kashfa za Mashi’a.

Muombezi: La hasha, huu sio uongo! Kuhusiana na aya hizi tukufu, ninakiri kwamba Ummul-Mu’minin Aisha atakuwa lazima amezisoma, bali baba yake na masahaba wengine mashuhuri watakuwa lazima wamezisoma. Kwa kuzingatia zile riwaya na hadith ambazo nimezitaja katika mikesha iliyopita, ukweli mwingi utafichuka kwetu alimuradi tu kwam- ba tunakuwa waadilifu.

Aisha Alimhuzunisha Mtukufu Mtume

Ukweli kwamba Aisha alimhuzunisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haukusimuliwa na Ulamaa wa ki-Shi’a tu, bali na ulamaa wenu mashuhuri pia. Imam Ghazali katika kitabu chake, Ihya’ul-Ulum, Jz. 2, mlango wa 3, Kitab-e-Adabun-Nika, uk. 135, amesimulia hadithi nyingi kuhusiana na tabia ya Aisha. Miongoni mwa hizo ni kugombana kwake na Mtukufu Mtume na Abu Bakr kuingilia kati. Tukio hili pia limesimuliwa na Mulla Ali Muttaqi ndani ya Kanzul-Ummal, Jz. 7, uk. 116; Abu Yala katika Musnad yake na Abu’sh-Sheikh katika Kitab-e-Amthal. Wanaandika kwamba Abu Bakr alikwenda kumuona binti yake, akakuta kwamba palikuwa na manung’unika kati ya Aisha na Mtukufu Mtume.

Uamuzi ya hilo uliachwa mikononi mwa Abu Bakr. Aisha akatumia lugha na kauli za matusi. Katika kuongea kwake, alimtaka Mtume kufanya haki katika tabia yake.

Kauli hii ya kifidhuli ilimfanya Abu Bakr akasirike kiasi kwamba akampiga kofi kwa nguvu sana usoni mwake mpaka damu ikachirizika hadi kwenye nguo zake.

Vile vile Imam Ghazali katika huohuo Mlango wa Ndoa na wengineo, pia wamesimulia kwamba safari moja, wakati Abu Bakr alipofika nyumbani kwa binti yake, alimkuta Mtume akiwa amemkasirikia Aisha. Yeye akawaomba wamueleze kuhusu kile kilichosababisha huzuni yao ili aweze kuleta suluhu baina yao.

Mtukufu Mtume alimuomba Aisha kama ataanza yeye kuelezea mkasa huo. Yeye akajibu, “Unaweza kuanza wewe lakini useme kweli.” Katika kauli yake iliyofuata akaongeza, “Wewe ni mtu anayejifikiria yeye mwenyewe kwamba ni Mtume!”

Maneno haya yanaonyesha kwamba isha hakuwa akiamini kwamba Mtukufu Mtume alikuwa ni Mtume aliyeteuliwa na Mungu. Kauli za dharau kama hizo zimesimuliwa katika vitabu vyenu kwa idadi kubwa. Zilikuwa ni chanzo cha maumivu makali sana kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)

Hakuna Riwaya Kama Hizo Kuhusu Wake Wengine Wa Mtukufu Mtume

Utaona kwamba ulamaa na wanahistoria wa madhehebu zote hawakusimulia mambo kama hayo kuhusu wake wengine wa Mtukufu Mtume. Hawakuhusisha mambo kama hayo hata kwa Hafsa binti ya Umar. Ilikuwa ni tabia tu ya Aisha iliyomsababishia aibu. Tumesimulia kiasi kile tu ulamaa wenu mashuhuri walichokisema kumhusu yeye.

Je, hukuvisoma vitabu vya Imam Ghazali, historia za Tabari, Mas’ud na ibn Atham Kufi na kadhalika, ambazo zinasimulia kwamba ulamaa wenu wakubwa wote wamemuelezea yeye kama asiyekuwa mtiifu kwa Mtukufu Mtume.

Bado unalalamika kwa sababu nimeishutumu tabia ya Ummul-Mu’minin. Kunaweza kuwa na doa la dhahiri katika tabia ya mtu kuliko kupituka dhidi ya amri ya Allah na Mtume Wake na kuasi dhidi ya khalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Katika Surat al-Ahzab, Allah swt. ameongea na wake za Mtukufu Mtume: “Na kaeni majumbani mwenu wala msijishauwe kwa majishauwo ya kijahilia ya zamani .....” (Al-Ahzab; 33: 33).

Kwa kweli wake wengine wa Mtukufu Mtume walikubaliana na amri hii na kamwe hawakuziacha nyumba zao bila ya sababu ya dharura muhimu. Hata A’mash amelisimulia jambo hili.

Ummul-Mu’minin Suda Hakutoka Japo Kwenda Hijja Au Umra

Imesimuliwa katika Sahih na vitabu vingine vya wanahistoria na wanahadithi wenu kwamba watu walimuuliza Suda, mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa nini hakwenda Hijja wala Umra.

Yeye alijibu akasema: “Ni wajibu juu yangu mimi kufanya Hijja moja na Umra na wala sio zaidi. Na Yeye anasema: “Na bakieni majumbani mwenu.” Hivyo kwa kuitii amri hii, mimi sitatoka nje ya nyumba yangu; bali nia yangu ni kwamba sitatoka, kwa kiasi inavyowezekana, nje ya chumba ambamo Mtukufu Mtume wa Allah ameniweka mpaka nitakapofariki.” Kwa kweli alifanya hivyo na ilikuwa ni mwili wake mfu ndio uliotolewa kutoka kwenye chumba hicho.

Suda, Aisha na Ummu Salma wote walikuwa ni wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na walikuwa ni Mama wa Waumini. Kwa hakika wanatofautiana kila mmoja wao kutokana na tabia zao. Kwa mujibu wa umma, Aisha na Hafsa walikuwa wanastahiki heshima, sio kwa sababu walikuwa mabinti wa Abu Bakr na Umar, ingawa mnawaheshimu kwa matokeo ya hoja hiyo, bali ni kwa sababu walikuwa ni wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Lakini wake za Mtume wanastahiki heshima kama wakiwa watiifu, kama ilivyoelezwa wazi ndani ya Qur’ani tukufu: “Enyi wake za Mtume! Ninyi sio sawasawa na wanawake wengine wowote.” (33: 32)

Aisha Atoka Kwenda Kupigana Dhidi Ya Ali

Hivyo Suda alikuwa mchamungu, mke mtiifu wa Mtume wa Allah. Aisha alikuwa mke mkaidi ambaye alikula njama na Talha na Zubair dhidi ya Ali na akaenda Basra. Kule Uthman Bin Hunaif, sahaba mkubwa wa Mtume na gavana wa Basra aliyeteuliwa na Ali, alikamatwa. Nywele zake na ndevu vilivutwa; aliteswa na akafukuzwa nje ya mji. Zaidi ya watu 100 wasio na hatia na wasiojiweza waliuawa. Ibn Athir, Mas’udi, Muhammad Bin Jarir Tabari, Ibn Abi’l-Hadid, na wengine wameandika kwa urefu kuhusu kadhia hii.

Baada ya kitendo hiki cha jeuri na ufisadi, alipanda ngamia aitwaye Askar, akiwa amevaa vazi lililotengenezwa kwa ngozi ya simba, akiwa amekingwa na jeshi aliingia kwenye uwanja wa mapambano kama mwana jeshi. Kwa sababu ya uasi wake, maelfu ya Waislamu walipoteza maisha yao. Je, uamuzi huu kwa upande wake haukuwa wa kuvuka mipaka dhidi ya amri ya Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Maadili Ya Ali Yamevuka Kiwango Kwa Idadi

Na kinachoshsngaza zaidi ni kwamba alichukuwa msimamo wa aibu dhidi ya Ali Bin Abi Talib, ambaye maadili yake na wema wake vimeandikwa kwa wingi sana na maulamaa wenu wenyewe mashuhuri kiasi kwamba sio rahisi kuyasimulia yote.

Imamu Ahmad Bin Hanbal katika “Musnad” yake, Ibn Abi’l-Hadid katika kitabu chake “Sharh-e-Nahju’l- Balagha”, Imam Fakhrud-Din Razi katika kitabu chake “Tafsir-e- Kabir”, Khatib Khawarizmi katika kitabu chake “Manaqib”, Sheikh Suleimani Balkhi Hanafi katika kitabu chake “Yanabiu’l-Mawadda”, Muhammad Yusuf Ganji Shafi’i katika “Kifayatu’t-Talib” Sura ya 62, na Mir Seyyid Ali Hamadani Shafi’i katika kitabu chake “Mawaddatu’l-Qurba”, Mawadda ya 5, anasimulia kutoka kwa Khalifa wa pili, Umar Bin Khattab na Abdullah Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali: “Kama bahari zote zingekuwa ni wino, miti yote ingelikuwa kalamu, na wanadamu wote wangelikuwa ni waandishi na majini wote wakatunza kumbukumbu, hata hivyo, Ewe Abu’l-Hasan! Maadili yako yasingeweza kuhesabiwa.”

Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema kwamba ‘binadamu na majini wote kwa pamoja hawawezi kuhesabu maadili yake, je, sisi tutaweza vipi, na akili zetu zenye ukomo kutoa hesabu kamili ya sifa zake? Mbali na ulamaa wa ki-Shia, maulamaa wenu wenyewe pamoja na ushupavu wao mkubwa wote, wamejaza vitabu vyao na sehemu tu ya maadili yake mengi.

Hadithi Katika Kusifia Maadili Ya Ali

Inakupaseni kuchunguza vitabu vyenu vya “Siha-e-Sitta” (vile vitabu sita maarufu vya hadithi). Mbali na hivi imeelezwa katika “Mawaddatu’l-Qurba” cha Mir Sayyid Ali Hamadani; “Mu’ajam Kabir” cha Tabrani “Matalibu’s-Su’ul” cha Muhammad Bin Talha Shafi’i; “Musnad” na “Fadha’il” vya Imam Ahmad Bin Hanbal; “Bainu’s-Sahihain” cha Hamid; “Manaqib” ya Khawarizmi; “Sharh-e-Nahju’l-Balagha” Jz. 2, uk. 449, cha Ibn Abi’l-Hadid; “Fusulu’l-Muhimma”, cha Ibn Sabbagh Maliki, hususan uk. 124, kutoka kwa Hafiz Abdu’l-Aziz Bin Al-Akhzaru’l-Janabiz, ambaye anaandika katika kitabu chake “Ma’alimu’l- Atratu’n-Nabawiyya” kwamba Fatima Zahra alisema kwamba katika usiku wa Arafa baba yake, Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.), alikuja kwake na akasema, “Allah (swt) huwa na fahari kwenu watu ninyi mbele za malaika na amekusameheni ninyi wote na hususan Ali.

Mimi, Mtume wa Allah ninasema bila kuzingatia upendo kwa ndugu kwamba hakika mtu mwenye bahati sana na mwenye kufuzu ni yule ambaye ni rafiki wa Ali wakati wa uhai wake na baada ya kifo chake. Mtu aliyelaaniwa zaidi miongoni mwa waliolaaniwa, ni yule ambaye ni adui wa Ali wakati wa uhai wake au baada ya kifo chake.”

Vile vile katika vitabu hivyo hapo juu kuna hadithi ndefu ambayo nafikiri niliitaja katika mikesha ya mwanzo, kutoka kwa Khalifa Umar Bin Khattab, ambaye alisema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali: “Mtu mwongo ni yule ambaye anafikiri kwamba ananipenda mimi ambapo ni adui wako. Ewe Ali! Yule ambaye ni rafiki yako ni rafiki yangu.

Kama mtu yeyote ni rafiki yangu, Allah ni rafiki yake pia. Kama Allah ni rafiki kwa mtu yeyote, basi humuingiza Peponi. Yule ambaye ni adui yako, ni adui yangu. Kama mtu yoyote ni adui yangu, Allah vile vile ni adui yake na humtupa Motoni.”

Urafiki Na Ali Ni Imani Na Upinzani Kwake Ni Ukafiri Na Unafiki

Vile vile imesimuliwa katika “Kitabu’l-Al” cha Ibn Khalawayh, akisimulia kutoka kwa Abu Sa’id Khadiri, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali: “Ewe Ali! Urafiki na wewe ni imani na upinzani kwako ni unafiki. Mtu wa kwanza kuingia Peponi atakuwa ni rafiki yako, na mtu wa kwanza kutupwa motoni atakuwa ni adui yako.” Mir Sayyid Hamadani Shafi’i katika kitabu chake “Mawaddatu’l-Qurba”, Mawadda ya 3, na Hamwaini katika kitabu chake “Fara’id” wanaandika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema wakati akiwa miongoni mwa Sahaba wake: “Hakuna anayempenda Ali isipokuwa mtu muumini, na hakuna aliye na uadui kwake isipokuwa yule ambaye ni kafiri.”

Na katika tukio lingine anasema: “Ewe Ali! Akupendaye wewe ni yule tu ambaye ni muumin, na mnafiki ni yule tu ambaye hukuchukia wewe.”

Ali Ni “Mbora Wa Viumbe” Amesema Mtukufu Mtume – Imesimuliwa Na Aisha

Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib, ukurasa wa 119, Sura ya 62, ananukuu kutoka kwenye Ta’rikh-e-Damishiq, Muhadith-e-Sham na Muhadth-e-Iraq, wakisimulia kutoka kwa Hudhaifa na Jabir kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ali ni mbora wa viumbe; mtu ambaye anakataa kulikubali hili, huyo ni kafiri.”

Vile vile imesimuliwa kutoka kwa Ata kwamba watu walimuuliza Aisha kuhusu Ali na akasema: “Ni mbora wa viumbe. Hakuna yeyote mwenye shaka ya aina yoyote ile isipokuwa kafir.”

Anasema kwamba Hafidh Ibn Asakir katika kitabu chake cha Ta’rikh, kitabu chenye juzuu 100, juzuu tatu kati hizo zimeandikwa kwa kumsifia Ali, ameisimulia hadith hii kutoka kwa Aisha.

Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibu’s-Su’ul, ukurasa wa 17, Ibn Sabbagh Makki katika kitabu chake Fusulu’l-Muhimma, wanasimulia kutoka kwa Tirmidhi na Nisa’i kwamba Abu Sa’id Khudri alisema: “Wakati wa uhai wa Mtume tulizoea kuwatambua wanafiki kwa uadui wao kwa Ali.”

Inasimuliwa katia Fusulu’l-Muhimma kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumuambia Amiru’l- Mu’minin Ali: “Ewe Ali! Kupigana dhidi yako wewe ni kupigana dhidi yangu; damu yako ni damu yangu.

Napigana dhidi ya yule ambaye anapigana dhidi yako wewe; ni yule tu aliyezaliwa ndani ya ndoa ndiye mwenye kukupenda wewe, na ni aliyezaliwa nje ya ndoa tu ndiye mwenye uadui na wewe. Ni mu’uminin tu ndiye ambaye anakupenda wewe, na ni mnafiki tu ndiye ambaye ana uadui na wewe.”

Sheikh: Hadith kama hizo sio za kipekee kwa Ali tu; zimesimuliwa vile vile kuhusu makhalifa wengine.

Muombezi: Tafadhali taja hadthi hizo kwa njia ya mfano.

Sheikh: Abdu’r-Rahman Ibn Malik Maghul anasimulia kutoka kwenye vyanzo vyake kwamba Jabir alisema kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alisema: “Mu’umin hana uadui kwa Abu Bakr na Umar, na mnafiki hana upendo kwao.”

Muombezi: Nimeshangazwa tena kusikia kitu kama hicho kutoka kwako. Umesahau makubaliano yetu ya pamoja tuliyoyafanya usiku wa kwanza kwamba hatutategemea juu ya hadithi zenye mashaka. Hupaswi kunukuu hadithi za kubuni, ambazo wasimuliaji wake ni waongo na waghushaji. Nukuu hadith sahihi.

Sheikh: Majibu yako yanaonesha kwamba kama ukisikia hadithi yoyote kutoka kwetu utaikataa.

Muombezi: Kamwe sifanyi hivyo, sio mimi peke yangu niliyeikataa hadithi hiyo. Hata maulamaa wako mwenyewe wameikataa. Rejea kwenye Mizanu’l-I’tidal cha Dhahabi na Ta’rikh ya Khatib-e-Baghdadi, juzuu ya 10, uk. 236. Utaona kwamba wengi wa wafasir wakubwa wameandika kuhusu tabia ya Abdu’r- Rahman Bin Malik wakisema:

“Hakika, huyu alikuwa ni muongo, mwenye kufuru na mghushaji wa hadithi kiasi kwamba hakuna yeyote mwenye shaka kuhusu hilo. Tafadhali tueleze kama hadithi hiyo ya upande mmoja iliyosimuliwa na muongo na mghushaji, inaweza kulinganishwa na hadithi zile ambazo maulamaa wako mashuhuri wamezisimulia, na ambazo baadhi yake nimezitaja.

Ningekushauri kuitazama Jami’u’l-Kabir, cha Suyuti, juzuu ya 6, uk. 390, Riyazu’n- Nazara, juzuu ya 9, uk. 215, cha Muhibu’d-Din; Jami’i Tirmidhi, juzuu 2, uk. 299; Isti’ab, juzuu ya 3, uk. 46, cha Ibn Abdu’l- Birr; Hilyatu’l-Auliya, juzuu 6, uk. 295, cha Hafidh Abu Nu’aim, Matalibu’s-Su’ul, uk. 17, cha Muhammad Bin Talha Shafi’i; Fusulu’l-Muhimma, uk. 126, cha Ibn Sabbagh Malik. Utaona kila mmoja wao amesimulia kwa hitilafu kidogo ya maneno kutoka Abu Dharr Ghifari ambaye alisema: “Wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tulizoea kuwatambua wanafiki kwa alama tatu: kumkataa Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kushindwa kuswali, na uadui kwa Ali Bin Abi Talib.” Imesimuliwa kutoka kwa Abi Sa’id Khudri kwamba Abu Dharr Ghifari alisema: “Tumezoea kuwatambua wanafiki kwa uadui wao dhidi ya Ali na wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tulikuwa hatuna alama nyingine ya kuwatambua wanafiki isipokuwa kwamba walikuwa maadui kwa Ali.”

Waandishi Wanaosimulia Hadithi Ya Mtukufu Mtume Kuhusu Chuki

Za Wanafiki Juu Ya Ali

Kwa nyongeza, waandishi wafuatao wanasimulia hadithi kuhusu chuki za wanafiki juu ya Ali: Imam Ahmad Hanbal katika Musnad, juz. 1, uk. uk. 95, 138; Ibn Abdul’l-Birr katika Isti’ab, juz. 3, uk. 37; Ahmad Khatib Baghdadi katika Ta’rikh-e-Baghdad, juz. 14, uk. 426; Ibn Abi’l-Hadid, katika Sharh-e- Nahju’l-Balagha, juz. 4, uk. 264; Imam Nisa’i katika Sunan yake, juz. 8, uk. 117 na Khasa’isu’l-Alawi, uk 27; Hamwaini katika Fara’id, Sura ya 22; Ibn Hajar katika Isaba, juz. 2, uk. 509; Hafidh Abu Nu’aim katika Hilyatu’l-Auliya, juz. 4, uk. 185; Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira, uk. 15; Suyuti katika Jami’u’l-Kabir, uk. 152 na 408; Muhammad Ibn Talha Shafi’i katika Matalibu’s-Su’ul, uk. 17; Tirmidhi katika Jami’i, juz. 2, uk. 13, wote hawa wameandika katika vitabu vyao kwa tofauti kidogo ya maneno kutoka kwa Ummu Salma au Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ewe Ali! Mnafiki sio rafiki yako na mu’umini sio adui yako. Ni mu’min tu yule ambaye anakupenda wewe, na ni mnafiki tu ndiye ambaye hukuchukia wewe. Mnafiki hampendi Ali na mu’umin hamchukii Ali.”

Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, juz. 1, uk. 367, anasimulia kutoka kwa Sheikh Abu’l- Qasim Balkhi, mkuu wa madhhebu ya Mu’tazili, kwamba amesema, “Hadithi zote kwa pamoja zinasimulia zile hadithi sahihi na hakuna shaka juu ya usahihi wa zile ambazo zinasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kumuambia Ali, “Hakuna mtu yeyote ambaye ni adui kwako isipokuwa yule ambaye ni mnafiki. Hakuna mtu yeyote ambaye ni rafiki yako isipokuwa ni mtu ambaye ni mu’umin.”

Vile vile, kati- ka juzuu ya 4 ya kitabu chake (Ibn Abi’l-Hadid), ukurasa wa 264, ananukuu hotuba ya Amirru’l-Mu’minin, ambayo kwayo Mtukufu Imam anasema:

“Kama ninampiga dharuba mu’umin na upanga huu katika uso wake ili kwamba awe na uadui juu yangu mimi, kamwe hawezi kuwa na uadui na mimi; lakini kama ninautoa ulimwengu mzima kumpa mnafiki ili anipende, kamwe hatanipenda.

Na hili ni kulingana na kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alisema: ‘Ni waumin tu wanaokupenda wewe, na ni wanafiki tu ndio wenye uadui na wewe. Kuna hadith nyingi za aina hii katika vitabu vyenu vya kuaminika. Nimevitaja tu baadhi ya hivyo. Je, uasi wa Aisha dhidi ya mamlaka ya Ali haukuwa ni uasi dhidi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe? Je, kupigana au kushawishi kwake watu kupigana dhidi ya Ali kulikuwa ni kwa sababu ya urafiki wake au ilikuwa ni kwa sababu ya uadui wake? Ni dhahiri, ilikuwa ni kwa sababu ya uadui.

Katika hadithi zote ambazo nimezisimulia hivi punde tu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba moja ya alama za unafiki ni kupi- gana dhidi ya Ali. Utaupatanisha vipi msimamo uliochukuliwa na Ummu’l-Mu’minin Aisha katika kupigana na Ali pamoja na hadithi hizi?

Imekuja kwenye akili yangu hivi punde kwamba Mir Sayyid Ali Hamadani Shafi’i katika Mawaddatu’l- Qurba, mawdda ya 3, amesimulia kutoka kwa Aisha mwenyewe kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Allah ameahidi neno Lake kwangu kwamba yeyote yule ambaye anaasi dhidi ya Ali ni kafiri na makazi yake ni Motoni.”

Inashangaza kwam- ba wakati watu walipomuuliza kwa nini aliasi dhidi ya Ali hali ya kuwa amesikia hadithi kama hiyo kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alijibu tu: “Niliisahau hadithi hii siku ya Vita vya Jamal (vita vya Ngamia). Sikuikumbuka mpaka nilipofika Basra.”

Sheikh: Lakini vipi unamuona Ummu’l-M’uminin kuwa na makosa wakati ni dhahiri kwamba kusahau ni ubinadamu.

Muombezi: Hata kama nitakiri kwamba alisahau hadithi ile siku ya Vita vya Jamal, je, hakuikumbuka wakati anarudi kutoka Makka na marafiki zake wote pamoja na wake wachamungu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walipomuonya kwamba asifanye kitendo kama hicho, kwa vile upinzani kwa Ali ulikuwa ni upinzani kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Wanahistoria wenu wenyewe ambao wameandika kuhusu Vita vya Jamal wamevuta nadhari kwenye ukweli kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ewe Aisha! Ogopa ile njia ambayo mbwa wa Haw’ab watakubwakia.” Hata hivyo wakati akiwa njiani kuelekea Basra, alifikia kijito kidogo cha Bani Kilab, mbwa wakamzunguka na kuanza kubweka. Aliwauliza watu hiyo ilikuwa ni sehemu gani. Aliambiwa kwamba hapo ni Haw’ab.

Kisha alikumbuka kile alichoambiwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwanini basi aliingia kwenye mtego wa Talha na Zubair? Kwa nini aliendelea mpaka akafika Basra ambako alis- ababisha fujo na ghasia kama ile? Je, utasema kwamba alikuwa amesahau na hili pia, au alipita njia ile kwa makusudi? Aliivunja amri ya Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa makusudi, na huku akiwa amekula njama na Talha na Zubair, alikwenda kupigana dhidi ya Khalifa na mwandamizi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ingawa yeye mwenyewe amesimu- lia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mtu anayepigana dhidi ya Ali ni kafiri.”

Je, hiyo haikuwa sababu ya kuhuzunisha kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba mara tu baada ya Amiru’l-Mu’uminin kuchuka hatamu za ukhalifa, vurugu zilianzshwa na wahai- ni walitayarisha vita dhidi yake. Niliwaambieni mapema kwa vyanzo sahihi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ambaye anamhuzunisha Ali, hakika ananihuzunisha mimi. Yule ambaye ananihuzunisha mimi, hakika anamhuzunisha Allah, Enyi watu! Yule ambaye atamhuzunisha Ali atafufuliwa kama Myahudi au Mkiristo hiyo Siku ya Hesabu.”

Mauaji Ya Masahaba Na Waumini Wasio Na Hatia Huko Basra Kwa Amri

Ya Aisha

Riwaya hizi zinaweza kupatikana katika vitabu vyenu sahihi. Kwa nini basi muwaone Mashi’a kuwa na makosa? Uwajibikaji kwa ajili ya damu ya waumini wasio na hatia, mateso na kufukuzwa kwa Uthman Bin Hunaif, na mauaji ya zaidi ya watu 100 pamoja na walinzi wa Hazina wasio na silaha ambao hawakuwa na habari na vita hivyo - 40 miongoni mwao ambao waliuawa msikitini - umeangukia sawasawa juu ya wachochezi wa vita hivyo.

Allama Mas’udi katika kitabu chake Muruju’z-Dhahib, juz. 2, uk. 7, ameandika kuhusu hili katika maneno haya: “Mbali na wale waliojeruhiwa, walinzi sabini wasio na silaha wa Hazina ya Umma waliuawa. Kati ya hawa sabini, hamsini walikatwa vichwa vyao ndani ya jela. Watu hawa walikuwa wa kwanza miongoni mwa Waislamu waliokuwa wameteswa mpaka kufa.” Miongoni mwa maulamaa wenu na wanahistoria, Ibn Jarir na Ibn Athir wametoa maelezo ya kinaganaga kuhusu matukio haya.

Mashi’a Wanasema Kuhusu Aisha Kile Haswa Kinachooneshwa Na Wanahistoria

Pengine itakulazimu kufuta riwaya hizi kutoka kwenye vitabu vyenu vya sahihi. Kwa kweli, katika machapisho ya marudio ya vitabu hivi, baadhi ya maulamaa wenu wamebadilisha baadhi ya maelezo haya wasiokubaliana nayo na katika hali nyingine wameyaondoa kabisa.

Itakupasa imma kukataa kile walichokiandika maulamaa na wanahistoria wenu mashuhuri, au itakupaseni kuacha kuwalaumu Mashi’a. Wanasema tu yale ambayo yame- andikwa kwenye vitabu vyenu wenyewe vya kuaminika.

Hakuna Ushahidi Kwamba Aisha Alitubia

Sheikh: Unachosema kwa hakika ni kweli, lakini Ummu’l-Mu’uminin Aisha alikuwa ni mwadamu tu; hakuwa ma’asum (asiyekosea). Akiwa katika hali ya kupotoshwa alifanya kosa. Ilikuwa kwa sababu ya wepesi wake wa kudanganyika kwamba alinasa kwenye mtego wa masahaba wawili mashuhuri, lakini baadae alitubia kwa ajili ya uasi wake. Allah alimsamehe kwa hilo.

Muombezi: Kwanza, umekiri kwamba baadhi ya masahaba mashuhuri walikuwa waovu, ingawa walikuwa miongoni mwa wale ambao walikuwa “chini ya mti” na katika Bai’atu’l- Ridhwan. Usiku mmoja uliopita ulitoa hoja kwamba masahaba walikuwa kama nyota, na tutakapomfuata yeyote miongoni mwao, tutaongozwa kwa haki. Sasa unakiri kwamba hii sio kweli.

Pili, umesema kwamba Ummu’l-Mu’minin Aisha alitubia kitendo chake hicho. Ni dai lililo tupu tu. Wakati ambapo uasi, vita na mauaji ya Waislamu yanakubaliwa na wote kwa pamoja, hakuna ushahidi wa kutubia kwake.

Aisha Anazuia Kuzikwa Kwa Imam Hasan Karibu Na Mtukufu Mtume

Kama mambo yalivyo, ni ukweli kwamba Ummu’l-Mu’minin Aisha hakutulizana. Alitenda makosa mengi ya kipumbavu. Lakini unadai kwamba alitubia kosa lake na kwa kusikia aibu, alijifungia nyumbani kwake. Lakini kama hii lingekuwa kweli kwa nini aufanyie vitendo vya aibu mwili wa mjukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Tumejadili jinsi alivyomhuzunisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hatimaye jinsi alivyok- enda kwenye vita akiwa amepanda ngamia kwenda kupigana dhidi ya mwandamizi wa Mtume. Lakini baadae, safari hii akiwa amepanda juu ya nyumbu, alizuia mwili wa mjukuu mkubwa wa Mtukufu Mtume usizikwe karibu na (kaburi la) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Maulamaa wenu mashuhuri na wanahistoria, pamoja na Yusuf Sibt ibn Jauzi katika kitabu chake Tadhkira Khawasu’l-Umma, uk. 122; Allama Mas’ud, mwandishi wa Muruju’z-Dhahab, katika Isbatu’l- Wasiyya, uk. 136; Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e- Nahju’l-Balagha, juz. 4, uk. 18, akisimulia kutoka kwa Abu’l-Faraj na Yahya Bin Hasan, mwandishi wa Kitabu’n-Nasab; Muhammad Khwawind Shah katika kitabu chake Raudhatu’s-Safa, na wengine wengi wameandika kwamba wakati mwili wa Imam Hasan ulipokuwa unapekwa Madina, Aisha, alipanda nyumbu na akifuatwa na kundi la Bani Umayyah na watumwa wao, walilisimamisha kundi lililokuwa na mwili wa Imam Hasan.

Walisema kwamba hawataruhusu mwili wa Imam Hasan kuzikwa kando ya (kaburi la) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). kwa mujibu wa riwaya ya Mas’udi, Ibn Abbas alisema: “Ni ajabu juu yako ewe Aisha! Je, haikukutosha ile siku ya Jamal, yaani siku ile ambayo uliingia kwenye uwanja wa mapambano ukiwa umepanda juu ya ngamia?

Je, sasa vile vile watu waweke kwenye kumbukumbu Siku ya Baghi (nyumbu)? Ukiwa umepanda nyumbu umelizuia jeneza la mtoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Siku moja umepanda ngamia, siku nyingine umepanda nyumbu, umeivunja staha ya Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.). Je, umedhamiria kuingamiza nuru ya Allah? Lakini kwa hakika Allah anaikamilisha Nuru Yake lau washirikina wachukie; hakika, sisi ni wa Allah na Kwake Yeye tutarejea.”

Baadhi ya watu wameandika kwamba Ibn Abbas alimuambia: “Wakati mmoja ulipanda ngamia na wakati mwingine nyumbu. Kama utaishi zaidi, utapanda tembo vile vile (yaani utapigana dhidi ya Mungu)! Ingawa katika moja ya nane una mgao wa moja ya tisa, bado umechukuwa miliki ya kitu kizima.”

Bani Hashim walichomoa panga zao na wakadhamiria kuwafukuzilia mbali. Lakini Imam Husein akaingilia kati na akasema kwamba kaka yake alimuambia kwamba hakutaka hata tone la damu limwagwe kwa sababu ya mazishi yake. Kwa hiyo, jeneza lilirudishwa kutoka pale na mwili wake ukazikwa Baqi (eneo la makuburi mjini Madina ambalo bado linatembelewa na mahujaji mpaka leo).

Kusujudu Kwa Aisha Wakati Wa Kuuliwa Kishahidi Kwa Amirul- Mu’minin

Kama Aisha alitubia kwa uasi wake dhidi ya Amirul-Mu’minin, kwa nini alifanya sijda ya shukurani wakati aliposikia habari za kuuliwa kishahidi kwa mtukufu Imam? Abu’l-Faraj Ispahani, mwaandishi wa Aghani, akiandika kuhusu mtukufu Imam katika kitabu chake Maqatilut-Talibin, anasema: “Wakati Aisha aliposikia habari za shahada ya Amirul- Mu’minin Ali, alifanya sijda (ya shukurani).” Baadae, hata hivyo, alimuuliza mtoa habari juu ya ni nani aliyemuua Ali. Aliambiwa kwamba alikuwa ni Abdur-Rahman Ibn Muljim wa ukoo wa Bani Murad. Mara moja alisoma ubeti wa shairi, ambao maana yake ni: “Kama Ali yuko mbali na mimi, habari za kifo chake zililetwa na mtumwa, ambaye anaweza kuwa hana vumbi katika mdomo wake.” Zainab, bint ya Ummu Salma alikuwepo wakati ule. Alimuuliza Aisha kama ilikuwa ni sahihi kwake yeye kuonyesha furaha yake na kutoa maneno kama hayo kuhusu Ali. Kilikuwa ni kitu kibaya sana. Aisha akajibu kwamba alirukwa na akili na kwamba alitoa maneno yale kwa kusahau. “Kama kitu kama hicho kikitokea tena kwangu na nikarudia maneno hayo, unaweza ukanikumbusha, ili nijizuie kufanya kitu kama hicho tena.” Mambo haya yanaonesha kwamba Aisha hakutubia baadae katika maisha yake kama unavyodai.

Kauli Za Aisha Zinazokinzana Kuhusu Uthman

Wakati huo huo nakumbuka akilini mwangu kitu kingine. Watu wenu wanawapinga Mashi’a kwa sababu wanamkosoa Khalifa Uthman kwa ajili ya makosa yake, makosa ambayo maulamaa wenu wenyewe wameyaandika katika vitabu vyao.

Kwa hiyo, pia hampaswi kumuangalia kwa upendeleo Ummu’l-Mu’minin Aisha vilevile, kwa sababu ulamaa na wanahistoria, kama vile Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha, juz. 2, uk. 77; Mas’ud katika Kitab-e-Akhiru’z-Zaman na Ausat; Sibt Ibn Jauzi katka Tadhkira Khawasu’l-Umma, uk. 36; Ibn Jarir, Ibn Asakir, na wengine wameandika kwamba Ummul-Mu’minin Aisha siku zote alikuwa akimsema vibaya Uthman, kiasi kwamba alikemea:

“Muuweni Na’thal (mzee mpumbavu) Allah naamuuwe huyo, kwani amekuwa kafir.” Lakini punde tu Uthman alipouawa, yeye kwa sababu ya upinzani wake kwa Ali, alianza kusema: “Uthman ameuawa kama mtu aliyeonewa. Kwa jina la Allah nitalipiza kifo chake. Hivyo simameni na munisaidie.”

Ibn Abi’l-Hadid anaandika: “Hakika Aisha alikuwa adui mkubwa wa Uthman. Kiasi kwamba alitundika nguo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika nyumba yake na alizoea kuwaambia watu ambao walikuja pale: ‘Hii ni nguo ya Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.). Bado haijachakaa, lakini Uthman ameizeesha na kuichakaza sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).’”

Ibn Abi’l-Hadid anaandika kwamba, wakati Aisha yuko Makka aliposikia habari za kuuli- wa kwa Uthman, alisema: “Allah amkatae kwenye rehema Yake. Alitenda matendo mabaya. Na Allah hawaonei viumbe wake, yaani, kama akimuadhibu yeyote, ni kwa sababu ya dhambi zake mwenyewe.

Mnazisikia kauli hizi kutoka kwa Aisha kuhusu Uthman bila ushahidi wowote na bado hamzitilii maanani. Lakini kama maneno kama hayohayo yanapotumiwa na Mashi’a, hara- ka sana mnawaita makafir.

Lazima tuchukue msimamo wa uadilifu wa mambo. Ni ukweli uliothibitika kwamba Ummul-Mu’minin Aisha alimpinga Imam Amirul-Mu’minin vikali sana.

Wakati aliposikia kwamba Waislamu wamekula kiapo cha utii kwa mtukufu Imam alisema: “Kuanguka kwa mbingu juu ya ardhi ni bora kuliko kusimamishwa kwa ukhalifa wa Ali. Uthman ameuawa kama mtu aliyeonewa.” Kwa hakika kauli hizi zisizopatana zinaashiria akili isiyotulia. Allah Ni Mwingi Wa Huruma Lakini Damu Ya Waislamu Wasio Na Hatia Haiwezi Kupita Bila Kuhojiwa

Sheikh: Kutokupatana huku kwa kauli hizi za Ummul-Mu’minin kwa hakika kwa ujumla kumesimuliwa sana, lakini mambo mawili yanakubalika na kuthibitika. Kwanza, kwamba alidanganywa na kwa muda mfupi alikuwa hakuzingatia uandamizi wa Ali.

Yeye mwenyewe alisema kwamba aliusahau na aliukumbuka tu wakati alipokuwa Basra. Pili, alitubia kwa ajili ya kitendo chake. Hakika Allah, akiwa amekwishamsamehe, atampa nafasi ya juu katika Pepo.

Muombezi: Sitarudia niliyokwisha sema kuhusu suala la kutubia. Damu ya Waislamu wale ambao waliuawa bila kosa lolote, fedheha na aibu waliyofanyiwa, na kuporwa kwa mali zao hakuwezi kupita bila kupingwa. Ni kweli kwamba katika mahali pa msamaha, Allah ni Mwenye huruma mno, lakini katika mahali pa adhabu, Allah ni mkali sana. Mbali na hili, yeye mwenyewe alikiri mpaka wakati wa kifo chake kwamba alihusika na matukio yote yale ya kuchukiza.

Kama maulamaa wenu wenyewe walivyosimulia, aliigiza katika wosia wake kwamba hawezi akazikwa kando ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alijua kwamba alisaidia katika vurugu nyingi baada yake.

Hakim katika kitabu chake, Mustadrak; Ibn Qutayba katika kitabu chake, Ma’arif; Muhammad Bin Yusuf Zarandi katika kitabu chake, Kitab-e-A’lam bi siratu’n-Nabi na Ibnu’l-Bayya Nishapuri na wengine wamesimulia kwamba Aisha alimsihi Abdullah bin Zubair katika maneno haya: “Nizike kando ya dada zangu katika makaburi ya Baqi. Nilizua mengi na mapya baada ya Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.).”

Aisha Hawezi Kudai Kupoteza Kumbukumbu Kwa Sababu Alikumbushwa

Na Ummu Salamah

Unasema kwamba alikumbuka nemsi za Ali wakati akiwa Basra na alisahau kile ambacho Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimkataza kufanya. Hii sio kweli. Inapaswa uangalie vitabu sahihi vya maulamaa wenu mashuhuri. Kwa mfano, rejea kwenye Sharhe-e-Nahju’l- Balagha, juz. 2, uk. 77 ya Ibn Abi’l- Hadid.

Ibn Abi’l-Hadid anaandika kutoka kwenye Ta’rikh ya Abi Makhnaf Lut Bin Yahya Azadi kwamba Ummu Salma naye vile vile alikuwa Makka, wakati aliposikia kwamba Aisha anakusudia kulipa kisasi kwa ajili ya mauaji ya Uthman na alikuwa anakwenda Basra.

Hili lilimshitua sana na akaanza kutangaza ubora wa Ali katika mikutano yote. Aisha alikwenda kwa Ummu Salamah ili kumshawishi juu ya msimamo wake huo kabla ya kuondoka kwenda Basra. Ummu Salamah akamuambia Aisha: “Mpaka jana ulikuwa unamtukana Uthman na kumuita mzee mjinga, na sasa umemgeukia Ali kutaka kulipa kisasi cha kuuawa kwa Uthman. Je, wewe hujui maadilifu ya Ali? Kama umesahau basi mimi nitakukumbusha.”

“Kumbuka siku ile, wakati nilipokuja chumbani kwako pamoja na Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.)? Kisha Ali akaingia ndani na akaanza kuongea faragha na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wakati mazungumzo ya faragha yalipoendelea kwa muda kiasi, uliamka na kumkaripia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Nilikusihi usifanye kitu kama hicho, lakini hukujali ushauri wangu. Ukamuambia Ali huku ukiwa umekasirika: ‘Katika siku tisa, moja ni kwa ajili yangu, na bado katika siku hiyo unakuja ndani kwangu na kumshughulisha na mazungumzo.’ Kwa sababu ya kitendo chako hicho Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikasirika sana kiasi kwamba uso wake uligeuka kuwa mwekundu na akasema: ‘Rudi! Naapa kwa jina na Allah kwamba yeyote yule ambaye ana uadui wa aina yoyote ule na Ali, awe anatokana na nyumba yangu au vinginevyo, anaondolewa katika imani.’ Kisha ukiwa umeabika, ulirudi nyuma.” Aisha akasema: “Ndio nakumbuka.”

Ummu Salamah akaendelea kusema: “Utakumbuka kwamba siku moja ulikuwa unaosha kichwa cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), nami nilikuwa natayarisha ‘hais’ (aina ya chakula). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alinyanyua kichwa chake na akasema:

‘Ni nani miongoni mwenu ambaye ni yule muovu ambaye atapanda Ngamia, na ambaye atabwakiwa na mbwa wa Haw’ab, na ambaye ataanguka kichwa chini kutoka kwenye Daraja ya Sirat.’ Kisha niliicha ile ‘hais’ na nikasema:

Ewe Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.)! Najikinga kwa Allah na Mtume Wake kutokana na kitendo kama hicho.’ Baada ya hili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akikupiga mgongoni kwako alisema: ‘Liepuke hili; ni wewe utakayefanya kitendo hiki.’” Aisha akasema: “Ndio nakumbuka.”

Ummu Salamah akaendelea: “Nakukumbusha kwamba katika moja ya safari wewe na mimi tulikuwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Siku moja Ali alikuwa anashona viatu vya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na sisi wawili tulikuwa tumekaa kwenye kivuli cha mti.

Ilitokea kwamba baba yako, Abu Bakr na Umar walikuja na kutaka ruhusa. Wewe na mimi tukaenda nyuma ya pazia. Walikaa chini na baada ya kuzungumza kwa muda, walisema:

‘Ewe Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.)! Hatujui ubora wa usuhuba wako. Hivyo tunakuomba utujulishe ni nani atayekuwa mwandamizii na Khalifa wako ili baada yako apate kuwa ndio kiongozi wetu.’”

Mtukufu Mtume akawaambia: “Ninaijua nafasi yake, cheo chake na hadhi yake, lakini kama nitamtambulisha moja kwa moja ninyi mtamkataa kama Bani Israil walivyomkataa Haruni.’

Wote walinyamaza kimya na mara wakaondoka. Baada ya kuwa wamekwisha kuondoka sisi tukatoka nje. Mimi nikamuuliza Mtukufu Mtume, ‘Ni nani atakayekuwa khalifa wako kwa ajili yao?’ Mtume akajibu, ‘Anatengeneza viatu vyangu.’ Tukaona kwamba hakuna mwingine isipokuwa Ali. Kisha nikasema, ‘Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! sikumuona yeyote isipokuwa Ali.’Yeye akasema, ‘Ali huyohuyo ndiye khalifa wangu.’”

Aisha akasema: “‘Nakumbuka.’ Kisha Ummu Salamah akasema: ‘Ikiwa unajua hadithi zote hizi, sasa unakwenda wapi?” Akajibu: “Nakwenda kufanya amani miongoni mwa watu.”

Kwa hiyo, ni wazi kwamba Ummul-Mu’minin Aisha alikuwa hakudanganywa na wengine tu. Yeye mwenyewe alisababisha matatizo makubwa, na akiwa anajua mambo yote haya, kwa makusudi alisimama katika uasi ingawa Ummu Salamah alimkumbusha hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Hata baada ya kukiri cheo na nafasi ya Amirul-Mu’minin, aliondoka na kuelekea Basra na kusababisha vurugu kubwa, ambayo yaliishia katika kuuawa kwa Waislamu wengi.

Hadithi Ya Kushona Viatu Ndio Ushahidi Mkubwa Wa Uimam Na

Ukhalifa Wa Ali

Hadithi ya kushona viatu ndio ushahidi mkubwa wa Uimam na ukhalifa wa Ali. Mashi’a wanafanya udadisi wa kitafiti kwenye mambo ya miaka 1400 iliyopita. Pamoja na ujuzi wa aya za Qur’ani Tukufu na vitabu sahihi vya maulamaa wa madhehebu zote, wanafikia mahitimisho ya haki.

Kwa hiyo, tunaamini kwamba, igawa kihistoria, Ali alipewa nafasi ya nne, nafasi hii ya chini kidhahiri kabisa, haiathiri ubora wake wala kudogesha umuhimu wa hadithi ambayo inathibitisha nafasi yake sahihi kama mrithi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Vile vile tunakubali kwamba ni ukweli uliohifadhiwa katika vitabu vya historia kwamba Abu Bakr (kwa hila za kisiasa) aliteuliwa kuwa Khalifa katika ukumbi wa Saqifa bila ya kuwepo Ali, Bani Hashim na masahaba wengine mashuhuri, pamoja na kuwepo upinzani wa ukoo wa Khazraj wa Ansari wa Madina. Baada ya hapo ikawa ni kwa udikiteta wa mtu mwenyewe binafsi, ambapo Umar na Uthmani walikalia kiti cha ukhalifa.

Lakini kuna tofauti. Watu hawa walikuwa makhalifa wa jumuiya; washirika wao ndio waliowafanya makhalifa. Kwa upande mwingine Amirul-Mu’minin Ali alikuwa ndiye Khalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na aliteuliwa na Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa mwandamizi wa Mtukufu Mtume.

Sheikh: Huku ni kutokuwa kwako na huruma. Kulikuwa hakuna tofauti kati yao. Watu wale wale ambao wote kwa pamoja waliamua kuukabidhi ukhalifa huo kwa makhalifa watatu, Abu Bakr, Umar na Uthman vile vile waliukabidhi kwa Ali. Tofauti Katika Mtindo Wa Uteuzi Wa Makhalifa Watatu Wa Mwanzo Ni Ushahidi Tosha Wa Kutosi- Hi Kwa Ukhalifa Wao

Muombezi: Kulikuwepo na tofauti nyingi za wazi katika namna ya uteuzi wa makhalifa. Kwanza, umetaja Ijma (uamuzi wa makubaliano ya pamoja). Hakuna ulazima wa kurudia hoja yangu. Nimethibitisha kutokuwepo kwa msingi wowote katika suala la Ijma katika mikesha iliyopita. Kwa hakika kulikuwa hakuna uamuzi wa pamoja kuhusu ukhalifa wa yeyote kati yao.

Ushahidi Mwingine Wa Ubatilifu Wa Ijmai

Pili, kama unategemea Ijmai (makubaliano ya wote pamoja) kama msingi wa ukhalifa na kuchukulia kwamba unakubalika kwa upande wa Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), basi wakati wowote anapokufa Khalifa, umma wote ungelikusanyika pamoja kuteua Khalifa. Yeyote ambaye angechaguliwa angekuwa Khalifa wa watu [kwa kweli sio wa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.)]. Na utaratibu huu ungelifuatwa katika zama zote.

Hata hivyo, lazima ukiri kwamba Ijmai kama hiyo au makubaliano ya wote kama hayo hayajawahi kufanyika kamwe. Hata Ijmai ile ambayo haikukamilika ambayo kwayo Bani Hashim na Answar (watu wa Madina) hawakuwepo pia haikufanyika kwa yeyote isipokuwa kwa Abu Bakr Bin Qahafa.

Ukhalifa wa Umar, kwa mujibu wa maoni ya wanahistoria wote na wanahadthi wa Uislamu, ulitegemea juu ya uamuzi wa pekee wa Abu Bakr Bin Qahafa. Kama Ijma ilikuwa ni kihitajio kwa ajili kuteuliwa kwa Khalifa, kwa nini isifanyike kwa ajili ya kuukabidhisha ukhalifa kwa Umar na kwa nini maoni ya wote pamoja yasitafutwe juu ya hilo?

Sheikh: Ni dhahiri kwamba wakati ambapo Abu Bakr alifanywa kuwa Khalifa kwa makubaliano ya wote pamoja (Ijmai), uamuzi wa Khalifa wa kumteuwa mrithi wake ulikwa halali kabisa. Kulikuwa hakuna haja ya kufanyika Ijma nyingine. Bali, uamuzi wa kila Khalifa wa uteuzi wa Khalifa baada yake kimsingi ulikuwa sahihi na wa kutosha.

Haki hii imewekwa kwa Khalifa ili kwamba aweze kumteua Khalifa baada yake ili kwamba watu wasije wakaachwa kwenye mchafuko na mkanganyiko. Kwa hiyo, wakati Khalifa aliyekubaliwa, Abu Bakr, aliyeteuliwa kwa makubaliano ya jumla, alimteuwa Umar kama Khalifa, na hivyo yeye (Umar) akawa ni Khalifa wa haki wa MtukufuMtume (s.a.w.w.).

Uteuzi Wa Mtukufu Mtume Juu Ya Ali Ulipuuzwa, Na Uteuzi Wa Abu Bakr Juu Ya Umar Ukahalalishwa

Muombezi: Unaamini kwamba Khalifa aliyekubaliwa ana haki ya kuteuwa mrithi. Ni jukumu lake kwamba asiuache umma kwenye mchafuko na bila kuongozwa, na uamuzi wake unatosha kwa ajili ya uteuzi wa Khalifa.

Lakini kama unaamini hivyo, kwa nini mnanyima Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haki hii? Na kwa nini mnazipuuza dalili zote zile za wazi ambazo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa dhahiri kwa kurudia rudia alizozitoa katika nyakati tofauti na sehemu tofauti, akimtaja

Ali kama mrithi wake, na dalili ambazo zimo zote katika vitabu vyenu sahihi. Unalikwepa kirahisi tu suala hili na kutetea tafsiri zisizo sahihi kama Ibn Abi’l-Hadid alivyoipuuza hadithi ya Umma Salma katika misingi ya ajabu isiyo na maana yoyote.

Aidha ni kwa msingi gani unaweza kudai kwamba Khalifa wa kwanza, ambaye aliteuliwa kwa njia ya Ijmai, alikuwa na haki ya kuteua mrithi wake. Je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitoa maelekezo kama hayo? Hapana. Vile vile unadai kwamba wakati Khalifa wa kwanza aliupata wadhifa wake kwa Ijma, kulikuwa hakuna haja ya uteuzi wa makhalifa wengine kwa njia ya Ijmai. Makhalifa hao hao walikuwa na mamlaka kutoka kwenye umma kuteua Khalifa kwa ajili yao.

Pingamizi Juu Ya Majlis-E-Shura(Kamati Ya Ushauri)

Kama hali ilikuwa hivyo, kwa nini kanuni hiyo ilitwaliwa kwa ajili ya ukhalifa wa Umar peke yake? Kwa ukhalifa wa Uthman kanuni hii haikufuatwa. Badala ya kuteuwa Khalifa baada yake, Umar aliliacha suala hili kuamuliwa na kamati ya ushauri ya watu sita. Sijui ni nini unachofikiria kama ndio kanuni ambamo kwamba uteuzi wa Khalifa umetegemea. Unajua kwamba kama kuna tofauti za msingi katika mabishano ya hoja, hilo suala halisi huwa batili.

Kama msimamo wako ni kwamba msingi wa ukhalifa ni Ijmai na umma wote kwa pamoja lazima ufanye uamuzi (bila kutaja ukweli kwamba Ijma kama hiyo haikufanyika kwa ajili ya ukhalifa wa Abu Bakr), basi kwa nini Ijmai kama hiyo isifanyike kwa ajili ya ukhalifa wa Umar?

Kama unachukulia kwamba Ijmai hiyo ilikuwa lazima tu kwa ukhalifa wa kwanza, na kwa ajili ya uteuzi wa makhalifa wa baadae uamuzi wa Khalifa aliyechaguliwa ulikuwa unatosha, basi kwa nini kanuni hii isifuatwe katika suala la ukhalifa wa Uthman? Kwa nini Khalifa Umar aliiacha kanuni iliyotangazwa wazi na Abu Bakr? Kwa nini aliacha uteuzi wa Khalifa kwenye Majlis-e-Shura (kamati ya ushauri)?

Khalifa Umar aliiteua kidikteta kamati hiyo ingawa ingepaswa kuwa kamati ya uwakilishi wa umma (kusudi kuweze kuwa na uwakilishi fulani kidogo wa maoni ya wengi). Pingamizi Kwa Abdu’r-Rahman Bin Auf Kuwa Ndio Msuluhishi

Kitu cha kushangaza zaidi ni kwamba haki za wajumbe wote wa kamati zilifanywa zinyenyekee kwa Abdu’r-Rahman bin Auf. Hatuelewi uteuzi wa Abdu’r-Rahman Auf umefanywa kwa misingi ipi. Je, ilikuwa dini, heshima, elimu au utendaji? Tunaweza tu kuona kwamba alikuwa jamaa wa karibu wa Uthman na hatamsaidia yeyote yule isikokuwa yeye. Iliamuliwa kwamba atakachosema Abdu’r-Rahman kitakuwa sahihi, na wakati akila kiapo cha utii kwa yeyote (katika wale watu watanoukimuondoa yeye mwenyewe), wengine wote lazima wamfuate.

Kwa Mujibu Wa Mtukufu Mtume, Ali Anapaswa Kufuatwa Kuliko Wengine Wote

Wakati tunapoliangalia suala hili kwa makini zaidi tunaona kwamba ilikuwa ni maagizo ya kidikiteta yaliyotolewa chini ya kisingizio cha Shura (kamati ya ushauri). Hata leo hii tunaona kwamba kanuni za demokrasia ziko kinyume kabisa na demokrasia yenyewe. Lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kurudia rudia alisema: “Ali anaiznguka haki na haki inamzunguka Ali.”

Vile vile alisema: “Ali ni ‘Faruq’ (Mbainishaji - wa haki na batili) wa umma huu na anavuta upambanuzi kati ya haki na batili.” Hakim katika kitabu chake Mustadrak, Hafidh Abu Nu’aim katika Hilya; Tabrani katika Ausat; Ibn Asakir katika Ta’rikh; Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib; Muhibu’d-Din Tabari katika Riyazu’n-Nuzra; Hamwaini katika Fara’id; Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e- Nahju’l-Balagha na Suyuti katika Durru’l-Mansur wanasimulia kutoka kwa Ibn Abbas, Salman, Abu Dharr na Hudhaifa kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mara tu baada yangu mimi vurugu zitaanza. Katika wakati huo itakuwa lazima kwenu ninyi kuji- ambatanisha wenyewe na Ali Bin Abi Talib kwa vile ni mtu wa kwanza ambaye atapeana mikono pamoja na mimi katika Siku ya Hukumu. Yeye ndiye mtu muaminifu mno zaidi na ndiye Faruq wa umma huu; yeye anaonesha kipambanuzii kati ya haki na batili, na ndiye kiongozi wa waumini.”

Kwa mujibu wa hadithi kutoka kwa Ammar Yasir (ambayo kwayo nimeitaja mapema pamoja na maelezo kamili ya vyanzo vyake), Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kama watu wote wanakwenda njia moja na Ali anakwenda njia nyingine, lazima umfuate Ali na kuwaacha wengine wote. Ewe Ammar! Ali hatakupotosha na hatakuelekeza kwenye maangamizi. Ewe Ammar! Utii kwa Ali ni utii kwangu mimi, na utii kwangu ni utii kwa Allah swt.”

Dhulma Mbaya Iliyofanywa Na Umar Kwenye Nafasi Ya Amirul- Mu’minin

Pamoja na hayo, Khalifa Umar, akiyadharau maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), anamfanya Ali kuwa ni mdogo kwa Abdu’r-Rahman katika Shura. Je, mamlaka hayo ni halali, ambayo yanawakana masahaba mashuhuri? Waheshimiwa mabwana! Kuweni wenye haki! Chunguzeni maelezo ya kihistoria ya wakati huo, kama vile Isti’ab, Isaba na Hilyatu’l-Auliya.

77Kisha mlinganisheni Ali na Abdu’r-Rahman, na muone iwapo kama yeye alistahiki kupata haki ya kura ya turufu (veto) au Amirul-Mu’minin. Mtaona kwamba ni kutokana tu na hila za kisiasa kwamba haki ya Ali iliporwa.

Aidha, kama njia ya uteuzi iliyofuatwa na Umar Bin Khattab ilikuwa inafaa kufuatwa, yaani kama Majlis - e- Shura ilikuwa lazima kwa ajili ya uteuzi wa Khalifa, kwa nini basi isifanywe wakati Amirul-Mu’minin alipofanywa Khalifa?

Inashangaza kwamba katika ukhalifa wa makhalifa wanne (Abu Bakr, Umar, Uthman na Ali) njia nne tofauti zilifuatwa. Sasa ni ipi katika njia hizo kimsingi ilikuwa haki na ipi ambayo ilikuwa batili? Kama unasema kwamba njia zote nne zilikuwa za halali, basi laz- ima ukubali kwamba ninyi hamna kanuni ya msingi kwa ajili usimikaji wa Khalifa.

Sheikh: Huenda maelezo yako ni sahihi. Umesema lazima tutafakari sana suala hili. Tunaona kwamba ukhalifa wa Ali vile vile ni wa hali ya kuleta wasiwasi, kwani aina ya Ijmai ambayo ilimteuwa Abu Bakr, Umar na Uthman vile vile imemteuwa Ali kama Khalifa.

Muombezi: Unachosema kingeweza kuwa chenye kuweza kutetewa lau isingekuwa kwa kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa hakika ukhalifa wa Ali haukutegemea juu ya Ijmai ya umma. Uliamriwa na Allah.

Ukhalifa Wa Ali Uliamriwa Na Allah

Mtukufu Imam alitwaa ukhalifa kwa njia ya kuirudisha haki yake kwake. Kama haki ya mtu imeporwa, anaweza kuichukua wakati wowote anapopata fursa ya kufanya hivyo. Kwa hiyo, wakati ilipokuwa hakuna vikwazo na hali ya hewa ilihitaji hivyo, mtukufu Imam alijipatia haki yake.

Kama umesahau hoja tulizosema huko nyuma, unaweza kuangalia magazeti, ambayo yameandika taarifa tulizowasilisha kuhusiana na suala hili. Tumethibitisha kwamba Ali kukalia kiti cha ukhalifa msingi wake ulikuwa juu ya aya za Qur’ani Tukufu na juu ya hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Huwezi kutaja hadithi hata moja inayokubaliwa na madhehebu zote ambayo kwayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema kwamba Abu Bakr, Umar, au Uthman walikuwa warithi wake.

Kwa hakika kama mambo yalivyo, mbali na hadithi katika vitabu vya Shi’a, kuna idadi kubwa ya hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zilizoandikwa kwenye vitabu sahihi vyenu wenyewe, ambazo zinaonesha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa dhahiri alimteuwa Ali kama mrithi wake. Sheikh: Vile vile kuna hadithi ambazo zinaonesha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba Abu Bakr alikwa ni Khalifa wake. Muombezi: Kwa dhahiri umesahau hoja yangu ya mikesha iliyopita ambayo inakanusha kukubalika kwa hadithi hizo. Hata hivyo, nitajibu tena usiku huu. Sheikh Mujaddidu’din Firuzabadi, mtunzi wa Qamusu’l- Lughat anasema katika Kitab-e-Safaru’s-Sa’adat: “Chochote ambacho kimesemwa katika kumtukuza Abu Bakr kimetegemea juu ya visa vya kubuni kiasi kwamba akili ya kawaida haivikubali kuwa ni vya kweli.”

Kama utachunguza vizuri zaidi tatizo la ukhalifa, utaona kwamba kwa hakika kulikuwa hakuna Ijma kwa yeyote kati ya makhalifa wakubwa wanne (Abu Bakr, Umar, Uthman na Ali) au kwa yeyote kati ya makhalifa wa Banu Umayya na Banu Abbas. Umma wote kamwe haukukusanywa wala wawakilishi wa umma kukusanya pamoja kupiga kura zao.

Lakini, tukizungumza kwa ulinganishi, tunaona kwamba ukhalifa wa Ali uliungwa mkono na kile ambacho kilikuwa karibu sana na Ijmai. Wanahistoria na maulamaa wenu wenyewe wanaandika kwamba kwa ukhalifa wa Abu Bakr kwanza kabisa walikuwa ni Umar na Abu Ubaida Jarra, yule mchimba makaburi, ndio waliokuwepo tu.

Baadae baadhi ya ukoo wa Aus ulikula kiapo cha utii kwake kwa sababu walikuwa wanapingana na ukoo wa Khazraj ambao walikuwa wamemteuwa Sa’d Bin Ubaida kama mgombea. Baadae zaidi wengine kwa kupitia vitisho, (kama nilivyoelezea mapema kwa urefu) na kundi jingine likichochewa na fikra za kisiasa walikula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Ma-Answari (watu wa Madina) ambao walimfuata Sa’d Bin Ubaida, hawakuukubali ukhalifa mpaka dakika ya mwisho.

Kisha ukhalifa wa Umar uliasisiwa tu kwa pendekezo la Abu Bakr, ambalo halikuhusika na chochote na Ijmai. Hatimaye Uthman alikuwa Khalifa kwa uamuzi wa Majlis-e-Shura (kamati ya ushauri) ambayo iliundwa kidikteta na Khalifa Umar.

Wakati wa ukhalifa wa Ali wawakilishi wengi wa nchi nyingi za Kiislamu, ambao kwa bahati walikuja Madina kutafuta marekibisho ya manun’guniko yao, walisisitiza juu ya Ali kuwa Khalifa.

Nawab: Je, wawakilishi hao wa nchi za Kiislamu walikusanyika Madina kwa ajili ya kumchagua Khalifa wao?

Muombezi: Hapana. Khalifa Uthman alikuwa bado ni Khalifa. Wawakilishi wa mengi ya makabila na koo kubwa za Kiislamu walikusanyika mjini Madina kulalamika juu ya ukatili wa magavana wa Banu Umayya, maofisa wao na watu wengine mashuhuri wa baraza lao, kama Marwan. Matokeo ya Ijma hii ilkuwa kwamba Uthman, ambaye aling’ang’ania katika sera zake za ukandamizaji, aliuawa.

Ilikuwa ni baada ya kadhia hii kwamba watu wa Madina walimfuata Ali na kwa msisitizo wa maombi na kumsihi kwingi walimleta msikitini, ambako watu wote walikula kiapo cha utii kwake. Makubaliano ya pamoja, ya hadharani kama hayo, hayajawahi kufanyika kwenye ukhalifa wowote katika makhalifa watatu wa kwanza. Watu wa Madina na viongozi wa nchi mbalimbali walikula kiapo cha utii kwa mtu makhususi na wakamkubali kama Khalifa wao.

Msingi Halisi Wa Ukhalifa Wa Ali Sio Ijmai Bali Ni Matangazo Ya

Mtukufu Mtume

Lakini licha ya Ijmai hii iliyofanywa kwa ajili Amirul-Mu’minin, hatuifikirii kama msingi wa Ukhalifa wake. Kuhalalisha ukhalifa wake tunategemea tu juu ya Qur’ani Tukufu na maamrisho ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ilikuwa ni kawaida ya mitume kwamba wao wenyewe, kulingana na amri ya Allah, waliwateua warithi na makhalifa.

Umesema kwamba hakuna tofauti kati ya Amirul-Mu’minin na makhalifa wengine. Na bado kuna dalili nyingi kwamba kulikuwa na tofauti kubwa kati ya Ali na makhalifa wengine.

Ali Alikuwa Mbora Kuliko Wale Makhalifa Wengine Wote

Sifa ya kwanza ya Amirul-Mu’minin ambayo imemfanya dhahiri kuwa yeye ni mbora zaidi kuliko makhalifa wengine wote ilikuwa kwamba yeye aliteuliwa na Allah na Mtume Wake kuwa mrithi wa Mtume. Mwengine wote wamechaguliwa na vikundi vidogo vya watu. Ni dhahiri kwamba Khalifa aliyeteuliwa na Allah na Mtume Wake lazima awe bora kuliko wale ambao wamechaguliwa na watu.

Kama mambo yalivyo, sifa mashuhuri zaidi ya Amirul-Mu’minin ilikuwa ni ubora wake wa elmu, maadili, na uchamumgu. Maulamaa wote wa umma (isipokuwa wafuasi wachache tu wa Abu Bakr wa ki- Khawarij na Nasibi) wanakubaliana wote kwa pamoja katika maoni yao kwamba, baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali anawapita wengine wote katika ilmu, uadilifu, haki, utukufu, na uchamungu. Katika kuunga mkono jambo hili huko nyuma nilinukuu idadi ya hadithi na aya kutoka kwenye Qur’ani Tukufu. Sasa nimekumbuka tena hadithi nyingine tena bado, kuhusiana na nukta hii.

Hadithi Ya Mtukufu Mtume (S.A.W.W.) Kuhusu Ubora Wa Ali

Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, Abu’l-Mu’ayyid Muwaffaq Ibn Ahmad Khawarizmi katika sura ya nne ya Manaqib, Mir Seyyid Ali Hamadani Shafi’i katika Mawaddatu’l-Qurba, Hafidh Abu Bakr Baihaqi Shafi’i katika Sunan, na wengine wengi wamesimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa tofauti kidogo ya maneno na tafsiri kwamba alisema: “Ali miongoni mwenu ndiye mwanachuoni msomi zaidi, muadilifu zaidi, na hakimu bora zaidi.

Yule ambaye anakataa kauli zake, kitendo chake au maoni yake, kwa kweli ananikataa mimi. Yule ambaye atanikataa mimi, anamkataa Allah, na yuko ndani ya mipaka ya ushirikina.” Aidha, Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali, ambaye ni mmoja wa maulamaa wenu mashuhuri, ameandika kwenye sehemu nyingi katika Sharh-e- Nahju’l-Balagha kwamba ubora wa Amirul-Mu’minin Ali ilikuwa ni imani ya masahaba wengi na wafuasi. Masheikh (Machifu) wa Baghdad vile vile walilikubali hilo.

Muombezi: Je, unaweza kunifahamisha tafadhali, unachochukulia kuwa ni nemsi katika mtu ambazo humfanya kuwa bora kuliko wote?

Sheikh: Kwa kweli kuna nemsi na tabia nzuri nyingi ambazo zaweza kustahili ubora kuloko nyingine, lakini katika maoni yangu sifa zenye kustahiki zaidi baada ya kuamini katika Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni hizi:

(1) Ukoo safi (2) Ilmu (3) Uchamungu.

Muombezi: Allah akubariki! Nitafungia mjadala wangu kwenye nukta hizi tatu.

Bila shaka kila sahaba, iwe alikuwa ni Khalifa au la, alikuwa na sifa fulani bainifu. Lakini wale ambao walikuwa na nemsi hizi walikuwa ndio haswa wabora kuliko wengine.

Kama nitathibitisha kwamba katika sifa hizi tatu ni Amirul-Mu’minin Ali ambaye anawazidi wengine wote, basi lazima ukubali kwamba mtu huyu mtakatifu alikuwa ni mdai mstahiki wa ukhalifa. Na kama alikoseshwa ukhalifa ni kwa sababu ya hila za kisiasa.

Kizazi Safi Halisi Cha Ali

Katika suala la kizazi ukimuondoa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hakuna mtu anayeweza kulinganishwa na Ali. Hata baadhi ya maulamaa washupavu wa madhehebu yenu, kama Ala’u’d-Din Mulla Ali Bin Muhammad Ushji, Abu Uthman Amr Bin Bahr Jahiz Nasibi, na Sa’idu’d-din Mas’ud Bin Umar Taftazani wamesema: “Tunayastahi sana maneno ya Ali ambaye amsema: ‘Sisi ni Ahlul’l-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). hakuna anayeweza kulingana na sisi.’”

Vile vile, katika khutba ya pili ya Nahju’l-Balagha, mtukufu Imam baada ya kukubali ukhalifa alisema: “Hakuna mtu katika umma huu anayeweza kulingana na familia ya Muhammad. Inawezekanaje wale ambao wamepokea rehema, ilmu, na upole kutoka kwao walingane nao? Wao ni msingi wa dini na nguzo za imani.

Wale ambao wanapotoka kutoka kwenye njia ya haki hugeukia kwao, na wale ambao wanakawia nyuma, hupiga hatua mbele kujiambatanisha kwao. Wao peke yao wana haki ya pekee ya uandamizi na Uimam.

Ilikuwa ni kwa ajili yao peke yao kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alifanya wosia wake. Walikuwa ni warithi wake wa haki. Sasa haki imerudi kwa mdai wake halali na tena ime- fikia sehemu ambayo kwamba ilikuwa imeondolewa.”

Maelezo haya ya Amirul-Mu’minin kuhusu madai yake la ukhalifa ni uthibitisho mzuri juu ya haki yake kwenye ukhalifa.

Lakini maneno haya hayakutamkwa na Amirul-Mu’minin peke yake. Hata wapinzani wake wamekiri kitu hicho hicho. Nilionesha katika usiku uliopita kwamba Mir Seyyid Ali Hamadani anasimulia katika Mawaddatu’l-Qurba, Mawadda ya 7, kutoka kwa Abi Wa’il, ambaye anasimulia kwamba Abdullah Bin Umar alisema: “Katika kuwaonesha masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), tulitaja majina ya Abu Bakr, Umar na Uthman.

Mtu mmoja akauliza liko wapi jina la Ali? Sisi tukasema, ‘Ali anatoka na Ahlu’l-Bayt ya Mtume, na hakuna mtu yeyote anayeweza kulinganishwa na yeye. Yuko pamoja na Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) katika daraja mmoja (isipokuwa utume).’”

Vile vile yeye anasimulia kutoka kwa Ahmad Bin Muhammad Kurgi Baghdadi, ambaye alisema kwamba Abdullah Bin Ahmad Hanbal (mtoto wa Imam wa madhehebu ya Hanbali) alimuuliza baba yake kuhusu ubora wa masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ailimtaja Abu Bakr, Umar na Uthman.

Kisha akamuuliza ni nini anachofikiria kuhusu Ali Bin Abi Talib. Ahmad Bin Hanbal akasema, “Anatokana na Ahlu’l-Bayt. Watu wengine hawawezi kulinganishwa naye.”

Amma kwa ukoo wa Ali, una vipengele viwili: kimoja cha nuru na kimoja cha mwili. Hivyo kulingana na hili Ali alikuwa na daraja ya pekee baada ya Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.).

Kuumbwa Kwa Ali Kutokana Na Nuru, Na Uhusiano Wake Na Mtukufu Mtume

Kutokana na mtazamo wa nuru, Amirul-Mu’minin alichukua nafasi ya juu kabisa, kama ambavyo maulamaa wenu wengi mashuhuri wanavyoonesha. Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, Mir Seyyid Ali Hamdani Faqih Shafi’i katika Mawaddatu’l-Qurba; Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib yake na Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibu’s-Su’ul fi Manaqib-e-alu’r-Rasul wanasimulia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba alisema: “Mimi na Ali Bin Abi Talib wote tulikuwa nuru moja mbele ya Allah miaka 14,000 kabla ya kuumbwa Adam. Wakati alipomuumba Adam, aliiweka nuru ile kwenye kiuno cha Adam.

Tulibakia pamoja kama nuru mmoja mpaka pale tulipotengana katika kiuno cha Abu’l-Muttalib. Kisha nilipewa Utume na Ali akapewa Ukhalifa.”

Mir Seyyid Ahmad Ali Hamdani Faqih Shafi’i katika Mawaddatu’l-Qurba, Mawadda ya 7, anaitaja nukta hii: “Ali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wanatokana na nuru moja. Ali alijaaliwa na sifa kama vile ambavyo hakupewa mtu yeyote mwingine katika ulimwengu wote.”

Miongoni mwa hadithi ambazo zimeandikwa katika Mawadda hii kuna riwaya kutoka kwa Khalifa wa tatu, Uthman Bin Affan, ambaye alisema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mimi na Ali tuliumbwa kutokana na nuru mmoja miaka 14,000 kabla ya kuumbwa kwa Adam. Wakati Allah alipomuumbwa Adam, aliiweka nuru ile katika kiuno cha Adam.

Tulibakia kama nuru mmoja mpaka tulipotenganishwa katika kiuno cha Abdu’l- Muttalib. Kisha nilipewa Utume na Ali akapewa uandamizi.”

Katika hadithi nyingine anaandika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wakati akimzunguzisha Ali, alisema: “Hivyo Utume na Unabii ukaja kwangu. Uandamizi (ushikamakamu) na Uimam ukaja kwako wewe Ali.” Hadithi hiyo hiyo ilisimuliwa na Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha, Jz. 2, uk. 450 (chapa ya Misir) kutoka kwa mwandshi wa Kita-e-Firdaus. Vile vile Sheikh Sulayma Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda, sehemu ya 1, anasimulia kutoka Jam’u’l-Fawa’id, Manaqib ya Ibn Maghazili Shafi’i, Firdaus ya Dailami, Fara’idu’s- Simtain ya Hamwaini na Manaqib ya Khawarizmi, pamoja na tofauti kidogo katika maneno lakini sio katika madhumuni, kwamba Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na Ali waliumbwa kutokana na nuru maelfu ya miaka kabla ya kuumbwa kwa ulimwengu na kwamba wote kwa pamoja walikuwa nuru moja mpaka walipotengenishwa katiki kiuno cha Abdu’l-Muttalib. Sehemu moja iliwekwa katika kiuno cha Abdullah na kutokana nayo alizaliwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Sehemu nyingine iliwekwa kwenye kiuno cha Abu Talib na kutokana nayo alizaliwa Ali. Muhammad aliteuliwa kuwa Mtume na Ali kuwa mwandamizi, kama ilivyoelezwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe.

Abu’l-Mu’ayyid Mu’affaq Bin Ahmad Khawarizmi na wengine wengi wamesimulia kutoka vyanzo vya kuaminika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mimi na Ali tumezaliwa kutokana na nuru moja. Tulibakia pamoja mpaka tukafikia kwenye kiuno cha Abdu’l-Muttalib ambamo tulitenganishwa.”

Kizazi Cha Kimaumbile Cha Ali

Kwa kadiri ambavyo uumbaji wa kimwili wa Ali unavyohusika, ni dhahiri ulikuwa ni wa daraja ya juu kwa pande zote, kikeni na kiumeni. Wahenga wake wote waliotangulia mpaka kufikia kwa Adam mwenyewe walikuwa ni wenye kumuabudu Allah.

Kamwe nuru hii haijatua katika kiuno au tumbo chafu la uzazi. Hakuna yeyote miongoni mwa masahaba anayeweza kutoa madai kama haya. Nasaba ya Ali ni kama ifuatavyo:

(1) Ali Bin (2) Abu Talib Bin (3) Abdu’l-Muttalib (4) Hashim (5) Abd-e-Manaf (6) Qusai (7) Kilab (8) Murra (9) Ka’b (10) Luwai (11) Ghalib (12) Fihr (13) Malik (14) Nazir (15)Kinana (16) Khazima (17) Mudrika (18) Ilyas (19) Muzar (20) Nizar (21) Ma’d (22) Adnan (23) Awwad (24) Al-Yasa (25) Al-Hamis (26) Bunt (27) Sulayman (28) Haml (29) Qidar (30) Isma’il (31) Ibrahim Khalil-Ullah (32) Ta’rikh (33) Tahur (34) Sharu (35) Abraghu (36) Taligh (37) Abir (38) Shale’ (39) Arfakhad (40) Sam (41) Nuh (42) Lumuk (43) Mutu Shalkh (44) Akhnukh (45) Yarad (46) Mahla’il (47) Qinan (48) Anush (49) Seth (50) Adam Abu’l-Bashir.

Isipokuwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tu, hakuna mwingine yeyote aliyekuwa na ukoo safi kama huu.

Baba Yake Ibrahim Alikuwa Ni Azar!!

Sheikh: Umesema kwamba wahenga wote wa Ali walikuwa wanaamini Mungu Mmoja. Nadhani umekosea. Baadhi ya wahenga wake walikuwa ni waabudu masanamu. Kwa mfano baba yake Ibrahim Khalilullah, Azar, aliabudu masanamu. Qur’ani Tukufu kwa uwazi inasema: “Na wakati Ibrahim alioposema kumuambia baba yake, Azar: je, mnayafanya masanamu kama miungu? Hakika nakuona wewe na watu wako katika upotofu ulio dhahiri.”

Muombezi: Unarudia yale waliyoyasema wakubwa zako, ingawa unajua kwamba wanachuoni wa nasaba kwa pamoja wote wanakubaliana kwamba baba yake Ibrahim alikuwa ni Ta’rukh, na sio Azar.

Sheikh: Lakini hii ni Ijtihad (hoja inayotegemea juu ya uamuzi wako mweyewe) mbele ya amri ya kimungu. Unaweka mbele mitazamo ya wanachuo wa nasaba katika kupingana na Qur’ani Tukufu, ambayo kwa uwazi inasema baba yake Ibrahim ni Azar, ambaye alikuwa muabudu sanamu.

Muombezi: Kamwe sibishani kwa kupingana na sheria ya ki-Mungu. Nia yangu ni kuta- ka kujua tafsiri halisi ya Qur’ani. Ili kufanikisha hili natafuta mwongozo kutoka kwa wale ambao wako sawa na Qur’ani Tukufu kama vyanzo vya mwongozo, nao ni Ahlu’l-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Neno hili katika aya hii tukufu limetumika katika maana ya jumla, kwa sababu katika maana ya jumla hata ami na mume wa mama vile vile huitwa ‘baba.’ Kuna mitazamo miwili katika suala la Azar. Moja ni kwamba alikuwa ni ami yake Ibrahim na wa pili ni kwamba zaidi ya kuwa ami yake, baada ya kufa baba yake Ibrahim (Tarukh), Azar alimuoa mama yake Ibrahim. Kwa hiyo Ibrahim alikuwa akimwita yeye ni baba yake kwa vile alikuwa ni ami yake na halikadhalika ni mume wa mama yake.

Sheikh: Hatuwezi kupuuza maana ya wazi ya Qur’ani Tukufu, mpaka tuone maana yake nyingine katika Qur’ani yenyewe, ikionesha kwa uwazi kwamba ami au mume wa mama vile vile huitwa ‘baba’. Kama ukishindwa kuonesha ushahadi kama huo (na kwa hakika utashindwa), hoja yako haitakubaliwa.

Muombezi: Kuna mifano katika Qur’ani ambako maneno yametumika katika maana yao ya jumla. Kwa mfano, Aya ya 133 Sura ya 2, Al-Baqarah, Qur’ani Tukufu inaunga mkono nukta yangu. Inaandika maswali na majibu ya Mtume Ya’akub na wanawe wakati wa kifo chake. Inasema: ام ﻛﻨْﺘُﻢ ﺷُﻬﺪَاء اذْ ﺣﻀﺮ ﻳﻌﻘُﻮب اﻟْﻤﻮت اذْ ﻗَﺎل ﻟﺒﻨﻴﻪ ﻣﺎ ﺗَﻌﺒﺪُونَ ﻣﻦ ﺑﻌﺪِي ﻗَﺎﻟُﻮا ﻧَﻌﺒﺪُ اﻟَٰﻬﻚَ واﻟَٰﻪ آﺑﺎﺋﻚَ اﺑﺮاﻫﻴﻢ {واﺳﻤﺎﻋﻴﻞ واﺳﺤﺎق اﻟَٰﻬﺎ واﺣﺪًا وﻧَﺤﻦ ﻟَﻪ ﻣﺴﻠﻤﻮنَ {133

“Aliposema kuwaambia watoto wake: mtaabudu nini baada yangu? Wakasema: tutamuabudu Mungu wako na Mungu wa baba zako, Ibrahim na Isma’il na Is’haq, Mungu Mmoja tu, na kwake tunajisalimisha.” (2:133)

Katika Aya hii uthibitisho wa dai langu ni neno Isma’il. Kwa mujibu wa Qur’ani, baba yake Ya’kub alikuwa ni Is’haq na Isma’il alikuwa ni ami yake, lakini, kwa mujibu wa matumizi ya kawaida, alizoea kumuita baba yake. Kwa vile watoto wa Ya’kub vile vile kwa mujibu wa matumizi ya kawaida, walimuita ami yao baba yao, walitumia neno hilo hilo katika kumjibu baba yao.

Mungu alijulisha swali na jibu lao kama ilivyokuwa. Halikadhalika, Ibrahim vile vile alizoea kumuita ami yake na mume wa mama yake ‘baba’, ingawa kwa mujibu wa ushahidi wenye nguvu wa kihistoria na maelezo ya kinasaba, ni jambo linalokubalika kwamba baba yake Ibrahim hakuwa ni Azar, bali ni Tar’ukh.

Baba Na Mama Zake Mtukufu Mtume Hawakuwa Washirikina Bali

Walikuwa Wote Ni Waumini

Ushahidi wa pili wa ukweli kwamba wahenga wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hawakuwa washirikina na makafiri ni Aya ya 219 Sura ya 26; Surat Shu’ara:“Na mageuko yako (ya kuinama na kuinuka na kusimama katika Sala) katika wale wanaosujudu.” (26:219)

Kuhusu maana ya Aya hii tukufu Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l- Mawadda, Jz. 2, na wengine wengi katika maulamaa wenu wamesimulia kutoka Ibn Abbas, ambaye alisema:

“Allah alihamisha chembe chembe za uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka kwenye kiuno cha Adam kwenda kwa mitume waliofuatia mmoja baada ya mwingine, ambao wote walikuwa wanaamini Mungu Mmoja, mpaka alipomfanya atokeze kutoka kwenye kiuno cha baba yake kupitia kwenye ndoa na sio kupitia njia ya haramu.”

Vile vile kuna hadithi mashuhuri sana ambayo maulamaa wenu wote wameisimulia. Hata Imam Tha’labi, ambaye anaitwa Imam wa hadithi, anaandika katika kitabu chake cha tafsiri na Sulaman Balkhi Hanafi katika kitabu chake Yanabiu’l-Mawadda, Jz. 2, anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Allah alinipele- ka duniani katika kiuno cha Adam na akanihamishia kwenye kiuno cha Ibrahim.

Aliendelea kunihamisha kutoka kwenye viuno mashuhuri na vitukufu kwenda matumbo (ya kina mama) safi mpaka aliponiumba kutoka kwa baba yangu na mama yangu, ambao kamwe hajakutana kiharamu.” Katika hadithi nyingine inasimuliwa kwamba alisema: “Kamwe Allah hakunichanganya mimi na elementi yoyote ya ujinga.”

Katika sura hiyo hiyo, Sulayman Balkhi anasimulia kutoka Ibkaru’l-Afkar kitabu cha Sheikh Salahu’d-din Bin Zainu’d-din Bin Ahmad ajulikanaye kama Ibnus-Sala Halbi na kutoka kwenye Sharh-e-Kibrit-e- Ahmar ya Sheikh Abdu’l-Qadir akisimulia kutoka kwa Ala’u’d-Dowlat Semnani hadithi yenye maelezo ya kinaganaga kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliulizwa kuhusu Allah alichoumba kwanza. Alijibu swali hilo kwa maelezo marefu ambayo siwezi kuyasimulia kwa wakati huu.

Kuelekea mwishoni mwa hadithi hiyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Halikadhalika, Allah aliendelea kuhamisha nuru yangu kutoka upande safi kwenda upande safi, mpaka aliponiweka kwa baba yangu, Abdullah Bin Abdu’l-Muttalib. Kutoka hapo Alinipeleka kwenye tumbo la mama yangu, Amina. Kisha alinifanya nitokeze katika ulimwengu huu, na akanipa cheo cha Sayidu’l-Mursalin (bwana wa Mitume) na Khatamu’n-Nabiyyin (Muhuri au Mwisho wa Mitume).”

Maelezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba aliendelea kuhamishwa kutoka mtu safi kwenda mtu safi yanathibitisha kwamba hakuna yeyote katika wahenga wake aliyekuwa kafiri. Kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu: “…Hakika washirikina ni najisi…” (9:28) kila kafiri na mshirikina ni najisi.

Alisema kwamba alihamishwa kutoka matumbo safi kwenda matumbo safi - ya uzazi. Kwa vile waabudu masanamu ni najisi, hivyo hii ina maana kwamba hakuna yeyote katika wahenga wake aliyekuwa muabudu sanamu. Katika sura hiyo hiyo ya Yanabiu’l-Mawadda moja hadithi kutoka Ibn Abbas inasimuliwa kupitia Kabir kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Sikuzaliwa kupitia ndoa ya haramu ya siku za ujahiliya. Nilizaliwa kupitia njia za Kiislamu za Nikah (ndoa).”

Je, hukusoma khutba ya 105 katika Nahju’l-Balagha? Amirul-Mu’minin anasema kuhusu wahenga wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). “Allah aliwapa (yaani mitume) sehemu bora (viuno vya wahenga wao) na matumbo safi ya uzazi ya mama zao. Aliwahamisha kutoka kwenye viuno maarufu na vyenye kuheshimiwa kwenda kwenye matumbo safi ya uzazi.

Wakati baba wa yeyote kati yao alipofariki, mtoto wake alimrithi yeye pamoja na dini ya Allah, mpaka Allah Mwenye nguvu zote alipomfanya Muhammad kuwa Mtume na Mjumbe Wake, hivyo alifanya chanzo cha uumbwaji wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa kilichotukuka mno zaidi. Nasaba ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilijumuisha Mitume Wake swt. ambao walikuwa wa daraja za juu kabisa.”

Kwa ufupi, wahenga wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kurudi nyuma mpaka kwa Nabii Adamu walikuwa waumini na wenye kuabudu Mungu Mmoja. Hivyo, ni dhahiri kabisa kwamba watu wa Ahlu’l-Bayt ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walijua zaidi kuhusu hadhi ya wahenga wao kuliko wengine. Wahenga Wa Ali Vivyo Hivyo Waliepukana Na Ushirikina

Wakati imethibitika kwamba wahenga wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa waumini na waabubu Mungu mmoja, bila shaka kabisa ina maana kwamba wahenga wa Ali vile vile walikuwa ni wenye kumuabudu Allah. Nimekwisha thibitisha kupitia kwenye vitabu vyenu wenyewe kwamba Muhammad na Ali wanatokana na nuru moja na wakati wote walibakia pamoja kwenye viuno na matumbo safi ya uzazi mpaka walipotenganishwa katika kiuno cha Abdu’l-Muttalib. Kila mtu mwenye busara atakiri kwamba mtu mashuhuri kama huyo alikuwa ni mdai wa haki wa ukhalifa.

Kutoeleweka Kuhusu Imani Ya Abu Talib Kwafafanuliwa

Sheikh: Naukubali ukweli kwamba Tarukh alikuwa baba yake Ibrahim, na umethibitisha utohara wa wahenga wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). lakini haiwezekani kupata ushahidi kama huo katika suala la Ali. Hata kama tukikubali kwamba wahenga wake wote kuanzia juu mpaka kwa Abdu’l-Muttalib walikuwa ni waabudu Mungu Mmoja, baba yake, Abu Talib, kwa hakika aliutoka ulimwengu huu akiwa ni kafiri.

Muombezi: Nakubali kwamba kuna tofauti ya maoni miongoni mwa umma kuhusu imani ya Abu Talib. Lakini tunapaswa kusema: Ewe Allah! Mlaani dhalimu wa kwanza ambaye alionesha udhalimu kwa Muhammad na ulaani na kizazi chake.

Laana ya Allah iwe juu ya yule ambaye alibuni hadithi ambazo matokeo yake ni kwamba Nasib na Khawariji walianza kudai kwamba Abu Talib alifariki dunia akiwa kafiri. Maulamaa wa Shi’a kwa ujumla na watu wote wa familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wanaamini katika imani ya Abu Talib. Ve vile, wengi wa wanachuo wenu na maulamaa wasiopendelea upande wowote, kama vile Abi’l-Hadid, Jalalu’d-Din Sututi, Abu’l-Qasim Balkhi, Abu Ja’far Askafi, walimu wao kutoka madhehebu ya Mu’tazali, na Mir Seyyid Ali Hamadani Faqih Shafi’i - wote wanakubaliana kwamba Abu Talib alikuwa ni Mwislamu.

Ijmai Ya Shia Kuhusiana Na Imani Ya Abu Talib

Shia wanaamini kwamba, kuanzia mwanzo kabisa Abu Talib alimwamini Mtukufu Mtume. Shia wanaowafuata Ahlu’l-Bayti wanakiri kwa kauli moja “Abu Talib kamwe hajaabudu masanamu; alikuwa ni mmoja kati ya warithi wa Ibrahim.” Mtazamo huo huo umeoneshwa pia katika vitabu sahihi vya maulamaa wenu wenyewe. Kwa mfano, Ibn Athir anasema katika kitabu chake Jam’u’l-usul: “Kwa mujibu wa Ahlu’l-Bayti tukufu, miongoni mwa ami zake wote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ni Hamza, Abbas, na Abu Talib tu walioukubali Uislamu.

Makubaliano ya pamoja ya watukufu Ahlu’l-Bayti kuhusiana na nukta yoyote, lazima ichukuliwe kama yenye maamuzi. Hadithi ya Thaqalain na hadithi nyingine ambazo nimezitaja kakita mikesha iliyopita zinathibitisha wazi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitoa maelezo ya wazi kuhusiana na uma’asum wa familia yake.

Walikuwa sambamba na Qur’ani Tukufu na moja ya Thaqalain (vizito viwili) ambavyo Mtume aliviacha kama vyanzo vya mwongozo usio na dosari kwa ajili ya watu wake. Ni muhimu kwamba Waislamu wote wavifuate ili kwamba wasipotoshwe.

Pili, kwa mujibu wa msemo “Watu wa nyumba wanajua vizuri kuhusu masuala ya familia”, familia hii iliyotukuka walijua zaidi kuhusu imani ya wahenga wao kuliko Mughira Bin Sha’ba, Banu Umayya, Khawarij na Nasib au watu wengine wasio na ujuzi.

Kwa hakika inashangaza kwamba maulamaa wenu hawakubali maelezo ya Ahlu’l-Bayti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), pamoja na Amir wa waumini, ambaye kwamba unyofu na uaminifu wake umethibitishwa na Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wote wanasema kwamba Abu Talib alikufa akiwa muumini. Hamuamini hilo, lakini mnakubali maneno ya Mughira, muongo na muovu aliyethibitishwa, na baadhi ya Amawi, Khawarij na Nasib.

Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali, ambaye ni mmoja wa maulamaa wenu mwenye sifa, anasema katika Sharh- e-Nahju’l-Balagha, Jz. 3, uk. 310: “Kuna tofauti ya maoni kuhusu Uislamu wa Abu Talib. Madhehebu ya Imamiyya (Shi’a) na wengi katika Zaidiyya wanasema kwamba aliutoka ulimwengu huu akiwa Mwislamu. Mbali na maulamaa wote wa Shia, baadhi ya maulamaa wetu wakubwa kama Abu’l-Qasim Balkhi na Abu Ja’far Askafi mtazamo wao ni kwamba Abu Talib aliukubali Uislamu, lakini hakuonesha imani yake ili kwamba aweze kumpa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) msaada kamili, na kwa sababu ya ushawishi wake (Abu Talib), wapinzani wasiweze kuzuia njia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Kuelewa Vibaya Kuhusu Hadithi Ya Kubuni Ya Zuhzah Kwafafanuliwa

Sheikh: Kwa dhahiri wewe huijui ile “hadithi ya Zuhzah” ambayo inasema: “Abu Talib yuko kwenye moto wa Jahannam.”

Muombezi: Hii ni hadithi ya kughushi iliyozushwa wakati wa kipindi cha Mu’awiyya Bin Abu Sufian na baadhi ya maadui wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Baadae Bani Umayya na wafuasi wao waliendeleza juhudi zao za kughushi hadithi dhidi ya Ali Bin Abi Talib na kuzisambaza miongoni mwa watu. Hawakuruhusu imani ya Abu Talib kujulikana kama ile ya Hamza na Abbas. Mghushaji wa hadithi ya Zuhzah alikuwa ni Mughira, ambaye alikuwa muovu na adui wa Amir wa waumini, Ali Bin Abi Talib. Ibn Abi’l-Hadid katika Sharhe-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 3, uk. 159-163; Mas’ud katika Muruju’z-Dhahab na maulamaa wengine wanaadika kwamba Mughira alifanya uzinifu huko Basra.

Wakati mashahidi wake walipoletwa mbele ya Khalifa Umar, watatu walitoa ushahidi dhidi yake, lakini wa nne alifundishwa kusema vitu ambavyo vilifanya ushahidi wake usikubalike. Kwa hiyo, mashahidi wale watatu walipewa adhabu, na Mughira aliachiwa huru. Mtunzi wa hadithi hii hata hivyo, alikuwa mzinifu na mlevi ambaye adhabu iliyowekwa na dini ilikuwa karibu itekelezwe juu yake. Alibuni hadithi kwa sababu ya upinzani wake kwa Amir wa waumini, Ali Bin Abi Talib na kumfurahisha Mu’awiya. Mu’awiya na wafuasi wake na Bani Umayya wengine waliimarisha hadithi hii ya uwongo na wakaanza kushuhudia kwamba “Abu Talib yuko katika moto wa Jahannam.” Aidha, wale ambao wameunganishwa na hadithi hii kama Adu’l-Malik Bin Umar, Abdu’l-Aziz Rawandi na Sufyan Thawri, ni wasimuliaji dhaifu na wasio kubalika.

Ukweli huu ulifafanuliwa na mfasir na mwanachuoni wenu mashuhuri Zahri, ambaye amelezea mtazamo huu katika kitabu chake Mizanu’l-Itidali, Jz. 2. Hivyo basi, ni vipi mtu atategemea juu ya hadithi kama hii, ambayo alisimuliwa na watu waongo na wasimuliaji wenye sifa mbaya kama hawa?

Ushahidi Juu Ya Imani Ya Abu Talib

Kuna ushahidi mwingi wa kuthibitisha imani ya Abu Talib:

(1) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema katika hadithi moja: (akiunganisha vidole vyake viwili) “Mimi na mwenye kumsaidia yatima wako pamoja katika Pepo kama vidole hivi viwili.” Ibn Abi’l-Hadid vile vile ameisimulia hadithi hii katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha yake, Jz. 4, uk. 312, anaandika kwamba, ni wazi kwamba katika kauli hii ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haimaanishi wenye kuwasidia mayatima wote, kwa vile wengi wa wanao wasaidia mayatima ni wenye dhambi.

Hivyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa hadithi hii alimaanisha Abu Talib na babu yake maarufu, Abdu’l- Muttalib, ambao walimlea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huko Makka alikuwa akijulikana kama yatima wa Abu Talib kwa sababu baada ya kufariki kwa Abdu’l-Muttalib, Mtume, kuanzia umri wa miaka nane alikuwa katika uangalizi wa Abu Talib.

(2) Kuna hadithi mashuhuri sana ambayo Shia na Sunni wameisimulia katika njia tofauti. Baadhi yao wanasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Jibrail alikuja kwangu na akanipa habari njema katika maneno haya: ‘Allah ameviepusha na moto viuno ambavyo kwavyo umetokea, tumbo lililokubeba, matiti yaliyokunyonyesha, na mapaja yaliyokusaidia wewe.’”

Mir Seyyid Ali Hamadani katika Mawaddatu’l-Qurba yake, Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, na Qadhi Shukani katika Hadith Quds yake wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Jibrail alikuja kwangu na akasema: ‘Allah anakutolea salamu na anasema, hakika Ameviepusha na moto viuno ambavyo vimekupa wewe hifadhi, tumbo ambalo lilihimili uzito wako, na mapaja ambayo yamkusaidia wewe.’”

Riwaya na hadithi hizi kwa uwazi zinathibitisha imani za watu ambao waliomsaidia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yaani, Abdu’l-Muttalib, Abu Talib na mkewe Fatima Bint Asad, na vile vile baba yake baba yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abdallah, na mama yake Amina Bint Wahhab, na mama yake aliyemnyonyesha, Halima. Beti Za Abil-Hadid Katika Kumtukuza Abu Talib

(3) Mwanachuoni wenu mkubwa, Izzu’d-din Abdu’l-Hamid Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali, alitunga beti zifuatazo katika kumsifia Abu Talib. Zimeandikwa katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha, Jz. 3, uk. 318: “Bila ya Abu Talib na mwanawe (Ali Bin Abu Talib) Uislamu usingelikuwa na heshima au nguvu. Abu Talib alimlinda Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huko Makka na akamsaidia na Ali huko Madina.

“Abd’al-Manaf (Abu Talib) kwa amri ya baba yake Abdu’l-Muttalib, aliendelea kumlea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ali, na akakamilisha juhudi hizo. Wakati Abu Talib alipok- ufa kwa utashi wa Allah, haikuleta hasara yoyote kwa sababu aliacha manukato yake (Ali) kama kumbukumbu yake. Abu Talib alianzisha huduma muhimu sana katika njia ya Allah na Ali akazikamilisha kwa ajili ya Allah. “Utukufu wa Abu Talib hauwezi kudhuriwa na kauli za kipumbavu za watu, au kwa ukandamizaji wa makusudi wa nemsi zake (unaofanywa na maadui zake), ni kama vile mtu anapouita mwanga wa mchana kuwa ni giza la usiku, mwanga huo hautadhurika chochote.”

Beti Za Abu Talib Huthibitisha Uislamu Wake

(4) Halikadhalika, beti za mashairi alizozilitunga Abu Talib mwenyewe katika kumsifia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ni uthibitisho wa wazi wa imani yake. Baadhi ya beti hizi zimeandikwa na Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha yake, Jz. 3, uk. 316. Aidha, maulamaa wenu mashuhuri kama Abu’l-Qasim Balkhi na Abu Ja’far Askafi, wamezitoa beti hizi kama ushahidi juu ya imani ya Abu Talib.

Abu Talib aliandika: “Naomba hifadhi kwa Allah kutokana na wale ambao hutushutumu sisi au kutuhusisha sisi na mwendo mbaya, kutokana na muovu anayetusema vibaya, na kutokana na mtu ambao hushirikisha vitu katika dini ambavyo tuko mbali navyo.

“Naapa kwa Nyumba ya Allah (Ka’aba), kwamba anadanganya yule anayesema kwamba tutamuacha Muhammad, ingawa bado hatujapigana dhidi ya maadui zake kwa panga na mikuki. “Kwa hakika sisi tutamsaidia yeye, mpaka tutakapo msaga adui yake. Tutajitoa mhanga kiasi kwamba, sisi tutasahau wake zetu na watoto wetu.

“Nuru yake ni ya namna ya kiasi kwamba, kupitia mwanga wa uso wake, sisi tunaomba rehema za Allah kutushukia.

“Yeye anakuja kwenye kuwasaidia mayatima; na yeye ni kimbilio la wajane.

Watu wa Bani Hashim wasiojiweza, hukimbilia kwake kwa ajili ya kutaka msaada, na wanabarikiwa kwa aina zote za neema.

“Naapa kwa uhai wangu kwamba, mimi nina mapenzi makali kwa Ahmad. Ninampenda yeye kwa mapenzi ya rafiki mkweli halisi.

“Niliiona nafsi yangu inafaa kujitoa mhanga kwa ajili yake, hivyo nilimsaidia kwa vile ni pambo kwa watu wa dunia hii, na ni laana kwa maadui na rehema kwa jamii.

“Namuomba Muumba wa ulimwengu amuimarishe kwa msaada Wake, na aidhihirishe dini Yake, ambayo ni njia ya kuelekea kwa Allah, na ambayo kwayo ndani yake hamna hata chembe ya kosa.”

Kuna baadhi ya beti maalumu za mashairi ya Abu Talib ambayo Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e- Nahju’l-Balagha, Jz. 3, uk. 312, na wengine wameyanukuu mashairi hayo kwa ushahidi wa imani yake. Katika maandishi ya wasifu wake, anasema:

“Watu hawa wanatutegemea sisi tupigane dhidi ya Uislamu kwa panga na mikuki; wanafikiri tutamuuwa Muhammad. Lakini nyuso zetu bado hazijapakwa damu katika kumsaidia yeye. Naapa kwa Nyumba ya Allah (Ka’aba) kwamba mumeniambia uwongo; mnaweza kuangukia kwenye janga.

Hatim na Zamzam vyaweza kujaa mpaka kwenye midomo yao kwa vichwa vilivyokatwa. Dhulma inafanywa kwa Mtume, ambaye ametumwa na Allah kuwaongoza watu. Amepewa Kitabu, ambacho kiliteremshwa na Mola wa Mbingu.”

Mbali na ushahidi huu wa wazi, ambao unathibitisha imani ya Abu Talib, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e- Nahju’l-Balagha yake, Jz. 3, uk. 315, ananukuu beti zifuatazo: “Mnashuhudia kuwepo kwa Allah!

Shuhudieni kwamba hakika nafuata dini ya Mtume wa Allah, yaani, Ahmad. Wengine wanaweza kupotoshwa katika dini yao, lakini mimi ni mmoja wa wale ambao wameongoka.” Mabwana! Kuwenu waadilifu na mtuambie kama muandishi wa mashairi kama haya anaweza kuitwa kafiri.

Sheikh: Mashairi haya hayakubaliki kwa sababu mbili. Kwanza, hakuna mwendelezo wa hadithi kuhusu mashairi haya. Pili, hakuna popote palipoonesha kwamba Abu Talib aliukubali Uislamu. Kusimulia baadhi ya mashairi yake hakuthibitishi kwa uhakika kwamba alikuwa Mwislamu.

Muombezi: Pingamizi lako kuhusu kukosekana kwa mwendelezo wa hadithi ni la ajabu. Wakati unapotaka, unakubali riwaya ya pekee na wakati ukiwa hutaki, unatumia silaha ya ukosefu wa mwendelezo. Kama utatafakari kwa muda kwamba kama mashairi haya hayakusimuliwa kwa mwendelezo na watu, hata hivyo, yakichukiliwa kwa ujumla, yanathibitisha kwamba Abu Talib aliamini utume wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kuna vitu vingi kama hivyo ambavyo mwendelezo wake wa hadithi huamuliwa kwa njia hii hii. Kwa mfano, vita alivyopigana Amir wa Waumini (Ali) na mifano ya ushujaa wake vile vile hutegemea juu ya riwaya za pekee. Lakini zikichukuliwa kwa ujumla taarifa hizi hujenga maana ya mwendelezo, ambao hutupa sisi elimu muhimu ya ushujaa wake. Ukarimu wa Hatim na uadilifu wa Nushirwan hujulikana kwa njia hiyo hiyo. Kwa vile wewe ni mpenzi sana wa mwendelezo, tafadhali tufahamishe ni vipi utathibitisha kwamba Hadithi ya Zuhza imewasilishwa kwa mfuatano.

Kukubali Kwa Abu Talib Imani Yake Juu Ya Allah Wakati Wa Kifo Chake

Ama kwa pingamizi lako la pili, jibu langu ni rahisi sana. Ni muhimu kuonyesha kukubali kwa mtu upweke wa Allah, utume, Siku ya Ufufuo, nk., katika nathari (lugha ya moja kwa moja isiyo ya kishairi). Lakini kama mtu akitunga mashairi ambayo kwayo anaelezea imani yake, huwa inatosha kabisa. Wakati Abu Talib aliposema: “Enyi ambao mnamumini Allah!

Shahudieni kwamba hakika mimi ninafuata dini ya Mtume wa Allah, Ahmad,” ilikuwa na athari ile ile kana kwamba ameisema katika nathari.

Mbali na hili, halikadhalika alikiri imani yake wakati wa kifo chake katika nathari vilevile. Seyyid Muhammad Rasuli Bazranji, Hafidh Abu Nu’aim, na Baihaqi wamesimulia kwam- ba kikundi cha wakuu wa Makureishi, pamoja na Abu Jahl na Abdullah Ibn Abi Umayya, walikuja kwa Abu Talib wakati alipokuwa anafariki.

Wakati huo Mtume alisema kumuambia ami yake Abu Talib: “Sema kwamba ‘hakuna mungu ila Allah,’ ili niwze kulishuhudia hilo mbele ya Allah.” Mara moja Abu Jahl na Abi Umayya walisema: “Abu Talib! Utaipa mgongo imani ya Abdu’l-Muttalib?”

Walirudia maneno haya tena na tena mpaka aliposema, “lazima muelewe kwamba Abu Talib anafuata imani ya Abdu’l-Muttalib.” Matokeo yake watu wale waliondoka pale wakiwa wamefurahi. Wakati alama za kifo zilipojitokeza juu ya Abu Talib, ndugu yake Abbas, ambaye alikuwa amekaa kwenye ukingo wa kitanda chake, aliona kwamba midomo yake ilikuwa inatikisika.

Wakati aliposikiliza alichokuwa anasema, alimsikia akisema: “Hakuna mungu ila Allah.” Abbas akamuambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.): “Ewe mpwa wangu! Naapa kwa jina la Allah kwamba ndugu yangu (Abu Talib) amesema kile ulichomuamuru kusema.” Kwa vile Abbas alikuwa bado hajaingia Uislamu wakati ule, hakuyatamka maneno hayo.

Tulithibitisha mapema kwamba wahenga wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wote walikuwa wanaamini katika upweke wa Allah (tawhid). Lazima uelewe kwamba ilikuwa ni kauli yenye kufaa kwa Abu Talib kusema kwamba anafuata imani ya Abdu’l-Muttalib. aliwaridhisha watu wale, na katika ukweli alikiri imani yake katika upweke wa Allah kwa sababu Abdu’l-Muttalib alifuata imani ya Mtume Ibrahim. Aidha, aliyatamka haya maneno “Hakuna mungu ila Allah.” Kama unachunguza taarifa za kihistoria kuhusu Abu Talib, kwa hakika utakiri kwamba alikuwa muumini.

Mazungumzo Ya Mtukufu Mtume Na Abu Talib Wakati Wa Tangazo La

Utume Wake

Katika siku ya bi’that (kutangazwa kwa utume) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), pamoja na ami yake Abbas, walikwenda kwa Abu Talib na akamuambia: “Hakika Allah ameniamuru mimi kutangaza amri Yake; hakika, amenifanya mimi Mtume Wake; basi wewe utanitendea vipi?”

Abu Talib alikuwa ni mkuu wa Makureishi, Kiongozi wa Bani Hashim na mtu mnyofu zaidi katika macho ya watu wa Makka. Alimlea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Lau angekuwa kafiri mara moja angelimpinga. Na ikiwa hilo halikuthibitisha vya kutosha, kwa vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuja kwake kutaka msaada wa kutangaza utume wake, Abu Talib kwa kuona kwamba hiyo ilikuwa ni kinyume na dini yake, angemzuia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au angalau angemfukuza kutoka kwenye eneo lake.

Kukataa kwa namna hiyo kungemkwaza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutokana na azima yake kubwa. Domo ya Abu Talib (tukichukulia kwamba ilikuwa ni ushirikina) ingeweza kuokolewa, na angeweza kupokea shukurani kutoka kwa washirika wake. Abu Talib angemkemea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama Azar alivyofanya kwa mpwa wake Mtume Ibrahim.

Tangazo La Ibrahim La Utume Na Mazungumzo Yake Na Azar

Katika Qur’ani Tukufu, Allah swt. anazungumzia kunyanyuliwa kwa Ibrahim Khalilu’r- Rahman kama Mtume wa Allah. Anasema kumuambia ami yake Azar: “Ewe baba yangu! Kwa yakini imenijia ilmu isiyokujia. Basi nifuate nikuongoze njia iliyo sawa. …Akasema: je! Unaichukia miungu yangu, ewe Ibrahim? Kama huachi lazima nitakupiga mawe. Na niondokee mbali, kwa muda mchache (huu)” (Qur’ani 19: 46)

Abu Talib Amhakikishia Mtukufu Mtume Msaada Kamili Na Pia Asoma Mashairi Katika Kuusifu Uislamu

Lakini kinyume chake, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipotaka msaada wake, Abu Talib alisema: “Ewe mpwa wangu endelea na kazi ujumbe. Hakika, wewe uko juu kwa cheo, mwenye nguvu katika ukoo wako na uliye tukuka zaidi katika nasaba ya familia. Naapa kwa jina la Allah kwamba ulimi utakaozungumza vibaya juu yako utajibiwa na mimi kwa upanga mkali. Kwa jina la Allah, dunia yote ya Arabia itapiga magoti mbele yako, kama mnyama anayenyenyekea mbele ya bwana wake.” Aidha, alitunga beti zifuatazo, akitaja ujumbe wa Mtume. beti hizi zimeandikwa na Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha yake, juz. 3, uk. 306, na Sibt Jauz katika Tadhkira yake, uk. 5:

“Wallahi naapa kwamba watu wale pamoja na wafuasi wao, kamwe hawatakufikia wewe, mpaka niwapeleke kwenye makaburi yao.

“Hivyo unaweza kuendelea kufanya kazi yako. Mimi nakupa habari njema za mafanikio yako. Yafanye macho yako yatulie kwayo.

“Umenilingania mimi kwenye dini yako. Naamini umeniongoza kwenye njia iliyonyooka; hakika wewe ndiye mkweli na wakati wote umekuwa mwaminifu.

“Umetuletea dini ambayo najua ni bora juu ya dini zote. Kama nisingekuwa na hofu ya dhihaka na lawama, ungeniona mimi nikikusaidia wewe kwa dhahiri kabisa.”

Mashairi haya yanaonesha kwamba Abu Talib alitambua Muhammad kwamba ni mjumbe wa Allah. Hata hivyo kuna mashairi mengine mengi kama haya ambayo Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha yake na maulamaa wengi wameyaandika kwenye vitabu vyao.

Je, mtu anayesoma mashairi kama haya ni kafiri au ni muumini wa kweli?

Abu Talib Alikuwa Msaidizi Na Mlezi Wa Mtukufu Mtume

Wengi wa maulamaa wenu maarufu wamealisimulia jambo hili. Unaweza kuangalia kitabu Yanabiu’l- Mawadda cha Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi Sura ya 52, ambamo ndani yake imesimuliwa kutoka kwa Abu Uthman Amr Bin Bahr Jahiz kwamba, akiandika kuhusu Abu Talib alisema: “Abu Talib alikuwa ni muunga mkono wa utume na unabii wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aliandika mashairi mengi katika kumtukuza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Alikuwa ndiye kiongozi wa Makureishi.”

Ushahidi huu wa wazi unathibitisha unyofu wa imani ya Abu Talib. Kwa jinsi ilivyo, Bani Umayya waliwashawishi watu kumlaani kiongozi wa waaminio Mungu mmoja, Amir wa waumini, na baba wa wajukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Hasan na Husein. Vile vile walibuni hadith kulaani mtukufu Imam na wakaghushi riwaya kwamba baba yake (Abu Talib), alikufa akiwa kafiri.

Msimuliaji wa riwaya hiyo alikuwa mlaaniwa Mughira Bin Sha’ba, adui wa Ali na rafiki wa Mu’awiya. Makhawarij na Manasib walieneza maoni ya kwamba Abi Talib alikuwa kafiri.

Watu wa kawaida walipotoshwa wakafanywa waamini kwamba huo ulikuwa ni mtazamo sahihi. Inashangaza kwamba walimuona Abu Sufyan, Mu’awiya na Yazid (Laana ya Allah iwe juu yao) kuwa ni waumini na Waislamu, ingawaje kuna dalili zisizo na idadi za kinyume chake. Na bado wanahusisha ukafiri kwa Abu Talib pamoja na uthibitisho wa wazi ambao unaonesha kwamba alikuwa muumini thabiti.

Sio Sahihi Kumwita Mu’awiya ‘Khalu’l-Mu’minin’

Sheikh: Je, ni sahihi kweli kwako wewe kumuita Khalu’l-Mu’minin (mjomba wa waumini), Mu’awiya Bin Abu Sufyan “kafiri” na kumlaani wakati wote? Je, utatufahamisha sisi tujue ni ushahidi gani ulionao kwamba Mu’awiya Bin Abu Sufyan na Yazid walikuwa makifiri na kustahili kulaaniwa? Watu hawa wawili maarufu walikuwa miongoni mwa makhalifa. Kusema kweli Mu’awiya alikuwa Khalu’l-Mu’minin na vile vile Khatib-e- Wahyi (mwandishi wa Wahyi).

Muombezi: Tafadhali, unaweza kunieleza ni vipi Mu’awiya amestahiki cheo cha Khalu’l-Mu’minin (mjomba wa waumini)? Sheikh: Kwa vile dada yake Mu’wiya Ummu Habiba, alikuwa mke wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ummul-Mu’minin (mama wa waumini), hivyo kaka yake Mu’awiya alikuwa Khalu’l-Mu’minin. Muombezi: Kwa maoni yako wewe, je! cheo cha Ummul-Mu’minin Aisha kilikuwa ndio kikubwa au kile cha Ummu Habiba, dada yake Mu’awiya? Sheikh: Ingawa wote ni Ummul-Mu’minin, Aisha kwa hakika alikuwa juu kuliko Ummu Habiba.

Muombezi: Kwa mujibu wa kigezo chako, makaka wote wa wake za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni Khalu’l-Mu’minin. Basi kwa nini humwiti Muhammad Bin Abi Bakr Khalu’l- Mu’minin? Kulingana na ninyi, baba yake alikuwa mbora zaidi kwa cheo kuliko Muawiya, na dada yake vile vile alikuwa ni mbora zaidi kwa dada yake Mu’awiya. Hapana, kuwa kwake Mu’awiya Khalu’l-Mu’minin hakuna ukweli.

Mu’awiya Alitamka Takbir Wakati Wa Kifo Cha Kishahidi Cha Imam Hasan

Abu’l-Faraj Ispahani katika Maqatilu’t-Talib, Ibn Abdu’l-Birr katika Isti’ab. Mas’ud kati- ka Isbatu’l- Wasiyya, na maulamaa wengine wengi wamesimulia kwamba Asma Ju’da, kwa amri na ahadi ya Mu’awiya, alimpa sumu Abu Muhammad Hasan Ibn Ali Bin Abi Talib. Ibn Abdu’l-Birr na Muhammad Bin Jarir Tabari vilevile wamesimulia kwamba wakati Mu’awiya alipojulishwa kifo cha mtukufu Imam, alipiga kelele ya takbira. Bila shaka, mtu mwenye laana kama huyo anaweza kuitwa Khalu’l-Mu’minin kwa maoni yako!

Muhammad Bin Abi Bakr Aliuawa Akiwa Na Kiu Na Kuchomwa Hadi Majivu Kwa Ajili Ya Mapenzi Ya Ahlu’l-Bayti

Lakini hebu mtazame Muhammad Ibn Abu Bakr, ambaye alilelewa na Amir wa waumini Ali Ibn Abi Talib, na alikuwa moja katika wale marafiki waaminifu wa watukufu Ahlu’l- Bayti! Akiizungumza na familia hii maarufu anasema: “Enyi kizazi cha Fatima! Ninyi ni sehemu yangu ya usalama na ni walezi wangu. Ni kwa kupitia kwenu ninyi kwamba katika Siku ya Hukumu, umuhimu wa matendo yangu mazuri utakuwa mkubwa. Kwa vile mapenzi yangu kwenu ni ya kweli, sitajali kama mtu atabweka karibu yangu.”

Ingawa alikuwa mtoto wa Khalifa wa kwanza, Abu Bakr na kaka wa Ummul-Mu’minin, Aisha, hajaitwa Khalu’l-Mu’minin. Alitendewa vibaya na kunyimwa urithi wa baba yake!

Wakati Amr Bin Aas na Mu’awiya Bin Khadij walipoishinda Misri, walimkatia mgao wa maji Muhammad Bin Abu Bakr. Wakati alipokuwa yuko karibu kufa kwa kiu, aliuawa. Kisha alifungashwa kwenye ngozi ya punda na kutupwa kwenye moto. Wakati Mu’awiya alipofahamishwa hili alifurahi sana.

Ukisikia habari hizi, huhoji ni kwa nini watu hawa waliolaaniwa walimtendea ukatili wa namna hii mtoto wa Abu Bakr, Khalu’l-Mu’minin Muhammad Bin Abu Bakr. Lakini wakati Mu’awiya anapolaaniwa haraka sana unakasirika.

Hivyo unaona upinzani kwa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na unaendelea mpaka leo!! Kwa vile Muhammad Bin Abu Bakr alikuwa mmoja wa marafiki wa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wewe hukumuita Khalu’l-Mu’minin wala kusikitia mauaji yake. Kwa vile Mu’awiya alikuwa adui mbaya kabisa wa Ahlu’l-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) unamuita Khalu’l-Mu’minin. Allah atuokoe na upotofu huu wa kishabiki!!!

Mu’awiya Hakuwa Mwandishi Wa Wahyi Bali Wa Barua Tu

Pili, Mu’awiya hakuwa mwandishi wa Wahyi. Aliingia Uislamu katika mwaka wa kumi Hijiriyya wakati wahyi ulikuwa umekamilika. Kwa kweli yeye alikuwa mwandishi ambaye aliandika barua. Alisababisha matatizo makubwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). katika mwaka wa nane Hijiriyya wakati Makka iliposhindwa na Abu Sufyan akaingia Uislamu, Mu’awiya aliandika barua nyingi kwa baba yake akimlaumu kwa sababu alikuwa ameukubali Uislamu.

Hata hivyo, wakati rasi yote ya Arabia na nje ya mipaka yake ilipokuja chini ya athari za Uislamu, Mu’awiya mwenyewe alilazimika kuingia Uislamu. Kwa kufanya hivyo alipoteza hadhi yake yote.

Kisha Abbas akamuomba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ampe Mu’awiya cheo chochote ili kwamba asiweze kujisikia amadhalilika. Kwa kuzingatia pendekezo la ami yake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimteuwa kama mwandishi kwa ajili ya kuandika barua.

Ushahidi Wa Ukafiri Wa Mu’awiya

Tatu, kuna sura nyingi za Qur’ani na hadithi ambazo zinathibitisha kwamba alikuwa kafiri anayestahili kulaaniwa. Sheikh: Ningependa sana kusikia Sura na hadithi hizo.

Muombezi: Chache tu ya hizo zitaoneshwa. Kama nitasimulia zote, zitafanya kitabu kamili. Muslim katika Sahih yake anasimulia: Mu’awiya alikuwa mwandishi wa Mtukufu Mtume.

Mada’ini anasema: “Sa’id Bin Thabit alikuwa ndiye mwandishi wa Wahyi na Mu’awiya alikuwa akiandika barua za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa makabila mengine ya Kiarabu.”

Ushahidi Kutoka Sura Za Qur’ani Tukufu Na Hadithi Kuwa Mu’awiya Na Yazid Wamelaaniwa

(1) Tafadhali rejea aya ya 60 ya Sura ya 17 (Bani Israil). Wafasiri kutoka kwa maulmaa wenu wenyewe, kama Tha’labi, Imam Fakhru’d-din Razi, na wengine wanasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliona katika ndoto kwamba Bani Umayya, kama manyani walipanda na kushuka mimbari yake. Baada ya hapo Jibrail alileta aya hii: “Na tulipokuambia: Hakika Mola wako amewazunguka watu. Na hatukuifanya ndoto ile tuliyo kuonesh ila kuwajaribu watu na katikaQur’ani mti uliolaaniwa. Na tunawahadharisha lakini haiwzidishii ila uasi mkubwa tu.” (7:60)

Allah swt., Amewaita Banu Umayya, ambao viongozi wao walikuwa ni Abu Sufyan na Mu’awiya, “Mti uliolaaniwa” ndani ya Qur’ani tukufu. Mu’awiya ambaye alikuwa tawi imara la mti huu, alikuwa kwa hakika amelaaniwa.

(2) Tena Allah swt., Anasema:

{ﻓَﻬﻞ ﻋﺴﻴﺘُﻢ انْ ﺗَﻮﻟﱠﻴﺘُﻢ انْ ﺗُﻔْﺴﺪُوا ﻓ ارضِ وﺗُﻘَﻄّﻌﻮا ارﺣﺎﻣﻢ {22

{اوﻟَٰﺌﻚَ اﻟﱠﺬِﻳﻦ ﻟَﻌﻨَﻬﻢ اﻟﻪ ﻓَﺎﺻﻤﻬﻢ واﻋﻤ اﺑﺼﺎرﻫﻢ {23

“Na kama ninyi mkipata utawala ni karibu mtaiharibu nchi na mtaukata ujamaa wenu. Na hao ndio ambao Allah amewalaani na amewatia uziwi na amewapofusha macho yao.” (47:22-23)

Katika aya hii wale ambao wanafanya uharibifu katika nchi na kuvunja mfungamano wa undugu wanalaaniwa na Allah.

Ni nani aliyekuwa mharibifu mkubwa kuliko Mu’awiya, ambaye ukhalifa wake ulikuwa wenye sifa mbaya kwa matendo yake ya kiovu. Mbali na hili alivunja mfungamano wa undugu.

(3) Vile vile Allah Ansema katika Qur’ani Tukufu: {انﱠ اﻟﱠﺬِﻳﻦ ﻳﻮذُونَ اﻟﻪ ورﺳﻮﻟَﻪ ﻟَﻌﻨَﻬﻢ اﻟﻪ ﻓ اﻟﺪﱡﻧْﻴﺎ واﺧﺮة واﻋﺪﱠ ﻟَﻬﻢ ﻋﺬَاﺑﺎ ﻣﻬِﻴﻨًﺎ {57

“Kwa hakika wale wanaomuudhi Allah na Mtume Wake, Allah amewalaani katika dunia na akhera, na amewaandalia adhabu yenye kufedhehesha.” (33:57)

Kwa hakika kumtesa Amir wa waumini na wajukuu wawili wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Hasan na Husein halikadhalika na Ammar Yasir na masahaba wengine maarufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ni sawa sawa na kumtesa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe.

Kwa vile Mu’awiya aliwatesa watu hawa wachamungu, kwa mujibu wa maneno ya wazi ya aya hii alikuwa kwa hakika aliye laaniwa katika dunia hii na katika akhera.

(4) Katika sura Mu’min, Anasema:

{ﻳﻮم  ﻳﻨْﻔَﻊ اﻟﻈﱠﺎﻟﻤﻴﻦ ﻣﻌﺬِرﺗُﻬﻢ ۖ وﻟَﻬﻢ اﻟﻠﱠﻌﻨَﺔُ وﻟَﻬﻢ ﺳﻮء اﻟﺪﱠارِ {52

“Siku ambayo hautawafaa madhalimu udhuru wao, na watapata laana na makazi yao yatakuwa mabaya.” (40:52)

(5) Katika sura Hud, Anasema:

{ا ﻟَﻌﻨَﺔُ اﻟﻪ ﻋﻠَ اﻟﻈﱠﺎﻟﻤﻴﻦ {18

“…Sasa kwa hakika laana ya Allah iko juu ya madhalimu.” (11:18)

(6) Katika sura Al-A’raf, Allah anasema:

{ﻓَﺎذﱠنَ ﻣﻮذِّنٌ ﺑﻴﻨَﻬﻢ انْ ﻟَﻌﻨَﺔُ اﻟﻪ ﻋﻠَ اﻟﻈﱠﺎﻟﻤﻴﻦ {44

“…Mara mtangazaji atatangaza baina yao kwamba laana ya Allah iko juu ya mad- halimu.” (7:44)

Halikadhalika, katika aya nyingine nyingi zilizoteremshwa kuhusu watu madhaalimu, ni wazi kwamba kila dhaalimu amelaaniwa. Sidhani yeyote katika ninyi atakataa dhuluma za wazi zilizofanywa na Mu’awiya.

Hivyo kwa ukweli wenyewe kwamba alikuwa dhaalimu, huthibitisha kwamba alistahili laana ya Allah kwa mtazamo wa dalili hizi za wazi, sisi pia tunaweza kumlaani mtu ambaye anastahili laana ya Allah.

(7) Katika sur ya Nisa Allah Anasema: {وﻣﻦ ﻳﻘْﺘُﻞ ﻣﻮﻣﻨًﺎ ﻣﺘَﻌﻤﺪًا ﻓَﺠﺰاوه ﺟﻬﻨﱠﻢ ﺧَﺎﻟﺪًا ﻓﻴﻬﺎ وﻏَﻀﺐ اﻟﻪ ﻋﻠَﻴﻪ وﻟَﻌﻨَﻪ واﻋﺪﱠ ﻟَﻪ ﻋﺬَاﺑﺎ ﻋﻈﻴﻤﺎ {93

“Na mwenye kumuuwa Muumini kwa kukusudia, basi malipo yake ni Jahannam, humo atakaa milele na Mwenyezi Mungu amemghadhibikia na amemlaani, na amemuandilia adhabu kubwa.” (4:93)

Mauaji Ya Waumini Mashuhuri Kama Imam Hasan, Ammar, Hajar Bin Adi, Malik Ashtar, Muhammad Bin Abi Bakr, Nk. Kwa Amri Ya Mu’awiya.

Aya hii tukufu kwa uwazi inasema kwamba kama mtu anamuua muumini mmoja kwa makusudi, anastashili laana ya Allah na makazi yake ni Jahannam. Je, Mu’awiya hakujihusisha na mauaji ya waumini? Je, hakuamuru mauaji ya Hajar Bin Adi na masahaba wake saba? Je hakuamuru kwamba Abdu’r-Rahman Bin Hasan Al-Ghanzi azikwe akiwa hai?

Ibn Asakir na Yaqub Bin Sufyan katika vitabu vyao vya Ta’rikh; Baihaqi katika kitabu chake Dala’il; Ibn Abdu’l-Birr katika Isti’ab; na Ibn Athir katika Kamil wamesimulia kwamba Hajar Bin Adi alikuwa mmoja wa masahaba maarufu ambaye, pamoja na masahaba wengine saba aliuawa kikatili na Mu’awiya. Kosa lao lilikuwa kukataa kumlaani Ali.

Imam Hasan alikuwa ni mjukuu mkubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Je, yeye hakujumuishwa katika As’hab-e-Kisa (Watu wa shuka/kishamia)? Je, yeye siye mmoja wa viongozi wawili wa vijana wa Peponi na Mu’mini wa daraja la juu? Kwa mujibu wa riwaya ya Mas’ud, Ibn Abdu’l-Birr, Abu’l-Faraj Ispahani, Tabaqa cha Muhammad Bin Sa’d, Tadhkira cha Sibt Ibn Jauzi, na maulamaa wengine maarufu wa Sunni, wanaandika kwamba, Mu’awiya alimpelekea sumu Asma Ju’da na kumuahidi kwamba kama akimuua Hasan Ibn Ali, atampa Dirham 100,000 na atamuozesha kwa mwanawe Yazid.

Baada ya kifo cha Imam Hasan, alimpa dirham 100,000 lakini akakataa kumuozesha kwa Yazid. Utasita kumita Mu’awiya mlaaniwa? Je, sio ukweli kwamba katika vita vya Siffin sahaba mkubwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ammar Yasir, aliuawa kwa amri ya Mu’awiya? Maulamaa wenu wote mashuhuri wanasema kwa muafaka mmoja kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ammar Yasir: Haitachukuwa muda kabla wewe hujauawa na kikundi cha kiuasi na kipotofu.”

Je, una mashaka yoyote kwamba maelfu ya waumini waaminifu waliuawa na wafuasi wa Mu’awiya? Je, askari safi na shujaa, Malik Ashtar hakulishwa sumu kwa amri ya Mu’awiya? Je, unaweza kukataa kwamba maofisa wakuu wa Mu’awiya, Amr Bin Aas na Mu’awiya Bin Khadij, walimuuwa kikatili gavana wa Amir wa waumini, mchamungu Muhammad Bin Abi Bakr? Bado hawakutosheka na hilo, wakauweka mwili wake kwenye mzoga wa punda na kuuchoma moto.

Kama nikisema niwape maelezo kuhusu waumini waliouawa na Mu’awiya na maofisa wake, itahitaji si usiku mmoja, bali zaidi.

Mauaji Ya Waumini 30,000 Waliouawa Na Busr Bin Artat Kwa Amri Ya Mu’awiya

Ukatili mkubwa kabisa ulikuwa ni ule wa Busr Bin Artat ambaye aliwauwa maelfu ya wau- mini kwa amri ya Mu’awiya. Abu’l-Faraj Ispahani na Allama Samhudi katika Ta’rikhu’l-Madina, Ibn Khallikan, Ibn Asakir na Tabari katika vitabu vyao vya Ta’rikh; Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha, Jz. 1, na wengine wengi wa katika maulamaa wenu maarufu wameandika kwamba Mu’awiya alimuamuru Busr kushambulia San’a na Yemen kutokea Madina na Makka. Alitoa amri kama hiyo hiyo kwa kwa Zuhak Bin Qais Al-Fahri na wengine.

Abu’l-Faraj anaisimulia katika maneno haya: “Yeyote katika masahaba na Shia wa Ali akionekana laz- ima auawe; hata wanawake na watoto wasiachwe.” Kwa amri hizi kali, walitoka na watu 3000 na akashambulia Madina, San’a, Yeman, Ta’if, na Najran.

Walipofika Yemen, gavana, Ubaidullah Ibn Abbas, alikuwa nje ya mji. Waliingia ndani ya nyumba yake na kuuwa watoto wake wawili Sulaiman na Daudi katika mapaja ya mama yao.

Ibn Abi’l-Hadid anaandika katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Jz. 1, uk. 121, kwamba katika shambulio hili watu 30,000 waliuawa, ukiondoa wale waliochomwa moto wakiwa hai. Je, mabwana nyie bado mna mashaka kwamba Mu’awiya anastahili kulaaniwa?

Mu’awiya Alitoa Amri Kwamba Ali Alaaniwe

Miongoni mwa ushahidi mwingi uliowazi kwamba Mu’awiya alikuwa kafiri na kustahili laana ilikuwa kumkataa kwake hadharani Amir wa Waumini na kuwaamuru watu wasome visomo vya malaanifu dhidi ya mtukufu Imam katika Qunuti zao. Jambo hili linakubaliwa na wote, ninyi na sisi.

Hata wanahistoria wa mataifa mengine wameandika kwamba matendo maovu yalikuwa yakifanywa wazi na kwamba watu wengi waliuawa kwa sababu hawakutoa maneno yale ya laana dhidi ya Imam Ali. Uovu huu ulisitishwa na Khalifa wa Banu Umayya, Umar Ibn Abdu’l-Aziz.

Ni dhahiri, mtu ambaye humlaani ndugu yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mume wa Fatima, Amir wa Waumini, Ali Bin Abi Talib na ambaye anawaamrisha wengine kufanya hivyo kwa hakika ni mlaaniwa. Jambo hili limeandikwa na ulamaa wenu wote maarufu katika vitabu vyao sahihi. Kwa mfano, Imam Ahamad Bin Hanbal katika Musnad yake, Abu Abdu’r-Rahman Nisa’i katika Khasa’isu’l-Alawi, Imam Tha’labi na Imam Fakhru’d- din Razi katika Tafsir zao, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira, Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, Mir Seyyid Ali Hamadani katika Mawaddatu’l-Qurba, Dailami katika kitabu chake Firdaus, Muslim Bin Hajjaj katika Sahih yake, Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalabu’s-Su’ul, Ibn Sabbagh Maliki katika katika Fusulu’l-Muhimma, Hakim katika Mustadrak, Khatib Khawarizzmi katika Manaqib yake, Abraham Hamwaini katika Fara’id, Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib yake, Imam’l- haram kati Dhakha’iru’l-Uqba, Ibn Hajar katika Saw’iq, na maulamaa wenu mashuhuri wamwesimulia katika tofauti kidogo ya maneno kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alise- ma: “Mtu ambaye anamtukana Ali, ananitukana mimi; na mwenye kunitukana mimi, haki- ka anamtukana Allah.”

Dailami katika katika Firdaus, Sulayman Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Mtu ambaye anamchukiza Ali, hakika ananichukiza mimi, na laana ya Allah iko juu ya yule ambaye ananichukiza mimi.”

Ibn Hajar Makki katika kitabu chake Saw’iq anasimulia hadithi inayohusu matokeo kwa mtu ambaye hulaani dhidi ya yeyote katika kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Anasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kama mtu yeyote atamlaani Ahlu’l-Bayti wangu, hakuna cho chote kwake bali kuondolewa katika Uislamu. Kama mtu yeyote atanichukiza mimi kuhusiana na Ahlul’l-Bayti wangu, laana ya Allah iwe juu yake.”

Kwa hiyo, kwa hakika Mu’awiya alikuwa amelaaniwa. Kama inavyosimuliwa na ibn Athir katika kitabu chake Kamil, Mu’awiya alizoea kumalaani Ali, wajukuu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Hasan na Husein na vile vile Abbas na Malik Ashtar katika Qunut ya sala zake za kila siku.

Imam Ahmad Hanbal anasimulia katika Musnad yake kutoka vyanzo mbali mbali kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kama mtu yeyote anamchukiza Ali atatendewa kama Yahudi au Mkirsto katika Siku ya Hukumu.” Kwa hakika lazima uelewe kwamba ni moja ya mafundisho ya Uislamu kwamba kumuita Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa majina mabaya humpeleka mtu kwenye ukafiri.

Muhammad Bin Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib sehemu ya 10, anasimulia kwamba siku moja Abdullah Ibn Abbas na Sa’id Ibn Jabir waliona katika ukingo wa Zamzam kikundi wa watu wa Syria wakimshutumu Ali. Walikwenda pale walipo na wakasema:

“Ni nani miongoni mwenu aliyekuwa anamtukana Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.)?” wakajibu: “Hakuna kati yetu aliyekuwa anamtukana Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).” Kisha wakasema: “Vema, nani miongoni mwenu aliyekuwa anamtukana Ali?” Wakasema: “Ndio tulikuwa tukimtukana Ali.”

Kisha Abdullah na Sa’id wakasema: “Yawapasa mshuhudie kwamba tulimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akimuambia Ali, ‘Mtu anayekutukana wewe kwa hakika hunitukana mimi; mtu ambaye hunitukana mimi, kwa hakika humtukana Allah. Kama mtu akimtukana Allah, Atamtumpa kichwa chini kwenye moto wa Jahannam.’” Masahaba Wa Mtume Walikuwa Katika Viwango Tofauti Vya Uwelewa

Sheikh: Je, ni sahihi kwa mtu wa hadhi yako kumlaani sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenye uwezo na hadhi kama huyu? Je, sio ukweli kwamba Allah swt., ameteremsha idadi ya aya katika kuwatukuza masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akawapa habari njema za kuokolewa kwao. Khalu’l-Mu’munin Mu’awiya, ambaye kwa hakika alikuwa sahaba mashuhuri, alistahiki sifa iliyomo katika aya hii tukufu. Je, kutukana sahaba sio sawa na kumtukana Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Muombezi: Huenda umesahau kile ambacho tayari nimekuambia katika mikesha iliyopita. Hakuna anayekataa kwamba aya zimeteremshwa katika kuwasifu masahaba. Lakini kama unaelewa maana ya sahaba, utakubali kwamba aya zilizoteremshwa katika kuwasifu masahaba kwa ujumla haziwahusishi masahaba wote. Hatuwezi kuwachukuliwa wote kuwa ni wasafi kabisa. Bwana mheshimiwa! Unajua vizuri sana kwamba sahaba kilugha ina maana ya kuunganika kwa watu pamoja.

Hivyo inaweza kuwa na maana ya kuishi pamoja au kama kwa kawaida inavyoeleweka, kusaidia au kutoa msaada kwa wengine.

Kwa mujibu wa leksikografia (usawidi kamusi) ya Kiarabu, Qur’ani, na hadithi, sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) maana yake ni mtu ambaye ametumia uhai wake katika kuwa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), imma awe alikuwa Mwislamu au kafiri.

Hivyo tafsiri yako kwamba masahaba wote wanastahiki Pepo sio sahihi. Hii inakinzana na akili ya kawaida na halikadhalika hukinzana na hadithi.

Katika Maneno Ya Qur’ani Tukufu Sahab Na Swahaba, Kwa Maana Ya “Wenzi” Hayana Maani Ya Kiheshima

Nitawasilisha aya za Qur’ani za nyogeza na hadithi sahihi kutoka wanachuoni wa Sunni ili kwamba usije ukakosea kuhusu neno sahaba.

Neno hili lilikuwa linatumika kwa sahaba wote, iwe walikuwa Waislamu au la:

(1) Katika Suratun Najm, Allah anawaambia washirikina:

{ﻣﺎ ﺿﻞ ﺻﺎﺣﺒﻢ وﻣﺎ ﻏَﻮﱝ {2

“Kwamba swahibu wenu hakupotea wala hakukosea.” (53:2)

(2) Katika Surat Saba, Allaha anasema: {ﻗُﻞ اﻧﱠﻤﺎ اﻋﻈُﻢ ﺑِﻮاﺣﺪَة ۖ انْ ﺗَﻘُﻮﻣﻮا ﻟﻪ ﻣﺜْﻨَ وﻓُﺮادﱝ ﺛُﻢ ﺗَﺘَﻔَﺮوا ۚ ﻣﺎ ﺑِﺼﺎﺣﺒِﻢ ﻣﻦ ﺟِﻨﱠﺔ ۚ{46

“Sema: mimi ninakunasihini tu kwa jambo moja kuwa; msimame kwa ajili ya Allah, wawili wawili na mmoja mmoja, kisha mtafakari: swahiba wenu hana wazimu…”(34:46)

(3) Katika Surat Kahf, Allah anasema:

{ﺛَﻤﺮ ﻓَﻘَﺎل ﻟﺼﺎﺣﺒِﻪ وﻫﻮ ﻳﺤﺎوِره اﻧَﺎ اﻛﺜَﺮ ﻣﻨْﻚَ ﻣﺎ واﻋﺰ ﻧَﻔَﺮا {34

“…Na akamwambia swahiba wake hali akibishana naye: mimi nina mali nyingi kuliko wewe na (nina) nguvu zaidi kwa wafuasi.” (18:34)

(4) Katika Sura hiyo hiyo, Allah anasema:

{ﻗَﺎل ﻟَﻪ ﺻﺎﺣﺒﻪ وﻫﻮ ﻳﺤﺎوِره اﻛﻔَﺮت ﺑِﺎﻟﱠﺬِي ﺧَﻠَﻘَﻚَ ﻣﻦ ﺗُﺮابٍ ﺛُﻢ ﻣﻦ ﻧُﻄْﻔَﺔ ﺛُﻢ ﺳﻮاكَ رﺟً {37

“Swahiba wake akamwambia hali ya kubishana naye: je, umemkufuru yule aliyekuumba kwa udongo, tena kwa tone la manii, kisha akakufanya mtu kamili.” (18:37)

(5) Katika Sura ya A’raf, Allah anasema:

{اوﻟَﻢ ﻳﺘَﻔَﺮوا ۗ ﻣﺎ ﺑِﺼﺎﺣﺒِﻬِﻢ ﻣﻦ ﺟِﻨﱠﺔ ۚ انْ ﻫﻮ ا ﻧَﺬِﻳﺮ ﻣﺒِﻴﻦ {184

“Je, hawatafakari? Swahiba wao hana wazimu, hakuwa yeye ila ni muonyaji dhahiri.” (7:184)

(6) Katika Sura ya An’am, Allah anasema:

ﻗُﻞ اﻧَﺪْﻋﻮ ﻣﻦ دونِ اﻟﻪ ﻣﺎ  ﻳﻨْﻔَﻌﻨَﺎ و ﻳﻀﺮﻧَﺎ وﻧُﺮد ﻋﻠَ اﻋﻘَﺎﺑِﻨَﺎ ﺑﻌﺪَ اذْ ﻫﺪَاﻧَﺎ اﻟﻪ ﻛﺎﻟﱠﺬِي اﺳﺘَﻬﻮﺗْﻪ اﻟﺸﱠﻴﺎﻃﻴﻦ ﻓ {ارضِ ﺣﻴﺮانَ ﻟَﻪ اﺻﺤﺎب ﻳﺪْﻋﻮﻧَﻪ اﻟَ اﻟْﻬﺪَى اﯨﺘﻨَﺎ ۗ ﻗُﻞ انﱠ ﻫﺪَى اﻟﻪ ﻫﻮ اﻟْﻬﺪَﱝ ۖ واﻣﺮﻧَﺎ ﻟﻨُﺴﻠﻢ ﻟﺮبِ اﻟْﻌﺎﻟَﻤﻴﻦ {71

“Sema: Je, tumuombe asiyekuwa Allah ambaye hatupi faida wala hawezi kutudhuru, na turudishwe nyuma baada ya Allah kutuongoza, sawa na yule ambaye mashetani yamempoteza akiwayawaya katika ardhi? Anao maswahiba wanaomwita kwenye mwongozo hasa ni mwongozo wa Allah, na tumeamrishwa tumnyenyekee Mola wa walimwengu wote.” (6:71)

(7) Katika sura ya Yusuf, Allah anasema: (Yusuf akiwaambia wafungwa wenzake wawili)

{ﻳﺎ ﺻﺎﺣﺒ اﻟﺴﺠﻦ اارﺑﺎب ﻣﺘَﻔَﺮِﻗُﻮنَ ﺧَﻴﺮ ام اﻟﻪ اﻟْﻮاﺣﺪُ اﻟْﻘَﻬﺎر {39 “Enyi maswahiba wangu wawili, je, waungu wawili wanaofarikiana ni bora au Allah Mmoja, Mwenye nguvu?” (12:39)

Hizi ni aya chache, ambazo nimezinukuu kwa njia ya mfano. Ni wazi kwamba maneno sahaba, sahib, musahib na ashab hayana uhusiano maalum kwa Waislamu. Hutumika katika kuwahusu Waislamu na washirikina halikadhalika.

Kama nilivyosema, mtu ambaye ana shughuli ya kijamaa na mtu mwingine anaitwa musahib au ashab. Masaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) huashiria wale ambao wana shughuli za kijamii pamoja na yeye.

Kwa hakika miongoni mwa sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na miongoni mwa wale ambao walikaa pamoja naye, walikuwa ni aina zote za watu, wazuri na wabaya, waumini na halikadhalika wanafiki.

Aya zilizoteremshwa katika kuwasifu masaba haziwezi kuhusishwa kwao wote. Zinaashiria tu kwa wale masahaba wazuri. Vile vile ni kweli kwamba hakuna katika mitume wakubwa wa zamani ambao walikuwa na masahaba maarufu mno kama wale wa Mtukufu Mtume wetu (s.a.w.w.).

Kwa mfano, masahaba wa Badr, Uhud, na Hunain walikuwa kiasi kwamba walitimiza kipimo cha wakati ule. Walimsaidia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na walikuwa imara katika uthabiti wao.

Lakini miongoni mwa masahaba wake vile vile ilikuwako idadi ya watu wenye tabia duni, maadui wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Ahlul’l-Bayti wake, watu kama Abdullah Bin Ubayy, Abu Sufyan, Hakam Bin Aas, Abu Huraira, Tha’labi, Yazid Bin Sufyan, Walid Bin Aqaba, Habib Bin Musailima, Samra Bin Jundab, Amr Bin Aas, Busr Bin Artat (mtawala dhalimu mwenye kiu ya damu), Mughira Bin Shu’ba, Mu’awiya Bin Abi Sufyan, na Dhu’s-Sadiyya.

Watu hawa, kwa nyakati zote, katika uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na hata baada ya kufa kwake, walisababisha ghasia kubwa miongni mwa watu. Mmoja wa watu kama hawa ni Mu’awiya, ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimlaani katika wakati wa uhai wake mwenyewe.

Baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wakati Mu’awiya alipopata fursa, alifanya uasi kwa jina la kulipa kisasi kwa ajili ya kifo cha Uthman na akasababisha umwagaji damu ya Waislamu wengi.

Katika mauaji haya masahaba wengi wenye kuheshimiwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kama Amar Bin Yasir, waliuawa kishahidi. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alitabiri kifo chke hicho cha shahada. Nimekwishataja baadhi ya hadithi zinazohusiana na tukio hili.

Qur’ani Tukufu Inawasifia Masahaba Wema Lakini Pia Inawalaani

Masahaba Waovu

Kuna aya nyingi katika Qur’ani Tukufu na hadithi zenye kuwasifia masahaba mashuhuri na waumini wachamungu. Na vile vile kuna aya nyingi na hadithi zenye kuwalaani wale masahaba waliokuwa ni watenda maovu.

Sheikh: Vipi utadai kwamba masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walisababisha vurugu za kijamii?

Muombezi: Hili sio tu dai langu. Allah swt., katika Sura ya Aali Imran anasema:

{وﻣﺎ ﻣﺤﻤﺪٌ ا رﺳﻮل ﻗَﺪْ ﺧَﻠَﺖ ﻣﻦ ﻗَﺒﻠﻪ اﻟﺮﺳﻞ ۚ اﻓَﺎنْ ﻣﺎت او ﻗُﺘﻞ اﻧْﻘَﻠَﺒﺘُﻢ ﻋﻠَ اﻋﻘَﺎﺑِﻢ ۚ{144

“Na hakuwa Muhammad ila ni Mtume aliyepitiwa na mitume kabla yake. Basi je, akifa au akiuliwa mtarudi nyuma kwa visigino vyenu?...” (3:144)

Mbali ya hii na aya nyingine za Qur’ani, maulamaa wenu wenyewe, pamoja na Bukhari, Muslim, Ibn Asakir, Yaqub Bin Sufyan, Ahmad Bin Hanbal, Abdu’l-Birr, na wengine wamesmulia idadi ya riwaya na hadithi kuhusiana na kulaaniwa kwa baadhi ya masahaba. Nitafanya rejea kwenye hadithi mbili tu. Bukhari anasimulia kutoka kwa Sahl Ibn Sa’d na Abdullah Ibn Mas’ud kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alisema: “Nitakuwa nawangojea kwenye chemchemu ya Kauthar.

Wakati kundi kati yenu litakapotoka kutoka kwenye njia yangu, nitasema, ‘Ewe Allah! Hawa walikuwa ni masahaba wangu!’

Kisha jibu kutoka Kwake litakuja kwangu: ‘Wewe hujui ni mangapi waliyoyazua baada yako.’”

Tena Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, Tabrani katika Kabir, na Abu Nasr Sakhri katika Ibana wanasimuliwa kutoka kwa ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Nataka kuwaokoeni ninyi kutoka kwenye adhabu ya Jahannam. Nawatakeni ninyi muogope moto wa Jahannam na kufanya mabadiliko kwenye dini ya Allah. Wakati nitakapofariki na kutenganishwa na ninyi, nitakuwepo kwenye chemchemu ya Kauthar.

Yeyote yule atakayenifikia mimi hapo atakuwa ameokolewa. Wakati wa mwisho nintakapoona idadi kubwa ya watu wameshikwa katika adhabu ya kimungu, nitasema: ‘Ewe Allah! Hawa ni watu wa umma wangu.’ Jibu litakuja: ‘Hakika, watu hawa walirudi kwenye imani yao ya zamani (waliritadi) baada yako.’

Kwa mujibu wa riwaya ya Tabrani katika Kabir, jibu litakuwa: “Hujui ni uzushi gani waliuanzisha baada yako. Walifuata dini yao ya zamani ya ujinga.”

Abu Talib Alikuwa Muumini Imara

Unasisitiza kwamba Mu’awiya na Yazid ni Waislamu ingawa ukatili wao mwingi umeandikwa katika kwenye vitabu vyenu wenywewe.

Baadhi ya maulamaa wa Sunni wameandika vitabu kamili katika kuwalaani, lakini kwa ukaidi unasisitiza kwamba walikuwa wanastahiki sifa na Abu Talib muumini mwaminifu alikuwa kafir! Ni dhahiri kabisa kwamba mazungumzo haya ya kipuuzi ni matokeo ya chuki dhidi ya Amir wa Waumini Ali.

Unajaribu kukataa hoja ambazo zinathibitisha ukafiri na unafiki wa Mu’awiya na Yazid. Na bado unakataa matamko ya wazi ya Abu Talib yanayohusiana na imani yake juu ya Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Ushahidi Wa Nyongeza Juu Ya Imani Ya Abu Talib

Je, sio kweli kwamba Ahlu’l-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wamesema kwamba Abu Talib alikuwa mu’mini na kwamba alikufa akiwa mu’mini? Je, Asbagh Bin Nabuta, mtu mwenye kuaminiwa sana, hakusimulia kutoka kwa Amir wa Wauimini kwamba alisema:

“Naapa kwa jina la Allah kwamba baba yangu, Abu Talib, babu yangu, Abdu’l-Muttalib Hashim, na Abdu’l-Manaf kamwe hawakuabudia masanamu.” Je, ni sahihi kwamba ukatae maelezo ya Ali na Ahlu’l-Bayti na kuamini maelezo ya mlaaniwa Mughira, ma-Awami, Makhawarij, Manasibi, na maadui wengine wa Amir wa Waumini?

Ja’far Tayyar Amekubali Uislamu Kwa Amri Ya Baba Yake

Aidha, wengi wa maulamaa wenu pamoja na Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, wameandika kwamba siku moja Abu Talib alikuja msikitini na akaona kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anaswali. Ali naye alikuwa anaswali upande wake wa kulia. Abu Talib akamuamrisha mtoto wake Ja’far ambaye alikuwa pamoja naye na alikuwa bado hajaingia katika Uislamu, akamuambia ‘Simama pembeni kwa binamu yako na uswali pamoja naye.’

Ja’far alisogea mbele na akasimama upande wa kushoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akaanza kuswali swala zake. Wakati huo Abu Talib akasoma beti hizi za shairi:

“Hakika Ali na Ja’far ni nguvu na faraja yangu katika huzuni na masikitiko. Ewe Ali na Ja’far! Kamwe msiachane na binamu yenu na mpwa wangu, bali msaidieni. Naapa kwamba kamwe sitamuacha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Je, yawezekana mtu akaacha kufuatana na Mtume wa familia tukufu kama hii?” Hivyo ni mtazamo wa wote pamoja wa maulamaa wenu kwamba kuingia Uislamu kwa Ja’far na kuswali pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ni kwa amri ya Abu Talib.

Mtukufu Mtume Alilia Sana Wakati Wa Kifo Cha Abu Talib Na Akaomba Baraka Za Allah Ziwe Juu Yake

Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha na Ibn Jauzi katika Tadhkirat-e-Khawasu’l-Umma wanasimulia kutoka Tabaqat-e-Muhammad, Ibn Sa’d, ambaye anasimulia kutoka kwa Waqidi na Allama Seyyid Muhammad Bin Seyyid Rasul Barzanji katika Kitabu’l-Islam Fi’l-‘am-u-Aba’-e-Sayyidul’l- An’am, riwaya kutoka kwa Ibn Sa’d na Ibn Asakir, ambao wanasimulia kutoka kwenye vyanzo sahihi kutoka kwa Muhammad Bin Ishaq kwamba Ali alisema: “Wakati Abu Talib alipokufa na nilipomjulisha Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) kuhusu kifo hicho, alilia sana. Kisha akaniambia, ‘Nenda ukaoshe mwili wake kwa ajili ya matayarisho ya mazishi, uuvishe mwili wake sanda, na umzike. Allah ambariki na awe na huruma juu yake!”

Je, inaruhusiwa na Uislam kufanya ibada za mazishi kwa mshirikina? Je, ni sawa kwetu kusema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliomba baraka za Allah juu ya kafiri na mshirikina? Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakutoka Nyumbani mwake kwa muda wa siku kadhaa na kuendelea kuomba kwa Allah kwa ajili amani ya milele ya Abu Talib.

Nauha Za Ali Kwa Ajili Ya Baba Yake, Abu Talib

Nauha za ali kwa ajili ya baba yake, Abu Talib- Nauha ni nyimbo za maombolezo.

Kama utaangalia kitabu Tadhkira cha Sibt Ibn Jauzi, uk. 6 utaona nini alichosema Amir wa Waumini katika nauha zake kwa ajili ya baba yake: “Ewe Abu Talib! Ulikuwa ni mbingu ya wenye kutafuta hifadhi, mvua ya neema kwa ardhi kavu, na mwanga ulio penyeza kati- ka giza. Kifo chako kimeporomosha nguzo za usalama. Sasa Mfadhili halisi ameweka rehema juu yako. Allah swt., amekuambatanisha na baraza Yake. Hakika ulikuwa ndiwe ami mbora wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Je, yaweza kuaminika kwamba mtu ambaye alikuwa mfano halisi wa tawhid angeweza kuandika nauha kama hii kwa ajili ya mtu aliyekufa kafiri?

Abu Talib Alificha Imani Yake Ambapo Abbas Na Hamza Walitangaza Zakwao

Sheikh: Kama Abu Talib alikuwa muumini, kwa nini asidhihirishe imani yake kama walivyofanya ndugu zake, Hamza na Abbas?

Muombezi: Kulikuwepo na tofauti kubwa sana kati ya Abbas na Hamza na Abu Talib. Hamza alikuwa haogopi kabisa na mtu mwenye kutisha sana kiasi kwamba watu wa Makka walimuogopa sana. Kuingia kwake Uislamu kulidhihirisha msaada mkubwa mno kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hata hivyo, Abbas hakutangaza Uislamu wake mara moja. Ibn Abdu’l-Birr anaandika katika kitabu chake, Isti’ab kwamba Abbas aliingia Uislamu wakati akiwa Makka, lakini aliificha imani yake kwa watu. Wakati Mtume alipohama kutoka Makka, Abbas vile vile alikusudia kuwa pamoja naye.

Lakini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuandikia kwamba kubakia kwake Makka kutakuwa na manufaa kwake (yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)). Kwa hiyo, alibakia Makka na akawa anampelekea habari Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutoka pale. Waabudu masanamu walikuja naye kwenye vita vya Badr. Wakati makafiri waliposhindwa, alichukuliwa mateka. Katika siku ya kuishinda Khaibar aliruhusiwa mwishowe kudhihirisha imani yake.

Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, sura ya 56, uk. 226, anasimulia kutoka kwenye Dhakha’iru’l-Uquba cha Imam’l-Haram Abu Ja’far Ahmad Bin Abdullah Tabari Shafi’i, ambaye anasimulia kutoka kwenye Fadha’il cha Abu’l-Qasim Ilahi kwamba wanachuoni wanajua kwamba Abbas aliingia Uislamu mwanzoni lakini ali- ificha imani yake.

Katika vita vya Badr wakati alipokuja na makafiri, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaeleza watu wake: “Yeyote atakayemuona Abbas asimuuwe kwa sababu ali- fuatana na makafiri bila hiyari yake. Alikuwa tayari kuhama, lakini nilimuandikia barua kwamba abakie kule awe ananipa habari kuhusu makafiri.” Siku ambayo Abu Rafi’i alimjulisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba Abbas ametangaza kukubali kwake Uislamu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuacha Abu Rafi’i huru.

Kwa Nini Abu Talib Afiche Imani Yake

Kama Abu Talib angeonesha imani yake Kureishi wote na taifa lote la Arabia lingeungana dhidi ya Bani Hashim. Abu Talib alifahamu faida ya kuficha Uislamu wake. Alijifanya kuwa mtiifu kwa Makureishi ili azuiye shughuli za adui.

Alimuradi Abu Talib anabakia hai, hali hiyo iliendelea, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa katika ulinzi. Lakini wakati wa kifo cha Abu Talib, Malaika Jibrail alitokeza mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akasema: “Sasa yakupasa kuondoka Makka. Baada ya Abu Talib huna msaidizi hapa.” Sheikh: Je, Uislamu wa Abu Talib ulijulikana wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.)? Na je, umma uliamini hivyo?

Muombezi: Ndiyo, ulijulikana sana kwa watu na walilitamka jina lake kwa heshima kamili kabisa.

Imani Ya Abu Talib Ilikuwa Ikijulikana Kwa Kawaida Wakati Wa Uhai

Wa Mtukufu Mtume

Sheikh: Inawezekanaje kwamba wakati wa uhai wa Mtume kitu kilikuwa kinazungumzwa sana na kwa kawaida kikajulikana kwa watu wote, lakini baada ya muda wa miaka thelathini, mtazamo wa kinyume ukapata nguvu kwa sababu ya hadithi za uwongo? Muombezi: Huu haukuwa mfano wa kipekee. Mara nyingi kile ambacho kilikubaliwa wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kilibadilika kabisa muundo wake baada ya miaka michache kwa sababu ya hadithi za kughushi.

Amri nyingine za kidini na matendo ya ibada yaliyokuwepo wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yaliachwa baada ya miaka kadhaa kwa sababu ya ushawishi wa watu.

Ndoa Ya Mut’a Na Hajj Nisa Zilikuwa Halali Mpaka Wakati Wa Abu Bakr

Lakini Zikaja Kuharamishwa Na Umar

Sheikh: Tafadhali hebu taja mfano mmoja wa mabadiliko kama hayo.

Muombezi: Kuna mifano mingi; miwili itatosha kuelezea nukta yangu. Nitajadili mut’a (ndoa ya muda) na Hajj Nisa. Madhehebu zote zinakubali kwamba matendo haya mawili ya kiibada yalikuwa ya kawaida wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Aidha, yalikuwa yakitekelezwa wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr na vile vile sehemu ya kipindi cha ukhalifa wa Umar. Lakini Khalifa Umar alisababisha ugeuzaji kabisa wa amri ya Qur’ani.

Alisema: “Mut’a mbili zilikuwa zinafanyika wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Sasa natamka kwamba zote ni haramu na nitawaadhibu wale ambao wanajishughulisha katika matendo haya.”

Kilichokuwa kumehalalishwa na Allah ghafla kilifutwa. Hukumu ya Umar ilitangazwa kwa mapana sana na ikafuatwa kibubusa sana kiasi kwamba ile sheria ya asili mara moja ikasahauliwa. Hata leo hii, wengi wa ndugu zetu Masunni wanaiona Mut’a kama uzushi wa Mashi’a.

Kama wazo la ajabu ajabu la Umar limeweza kugeuza amri ya wazi ya Allah na ukweli wa kihistoria kwamba mut’a ilikuwa ikifanyika, je, unaweza kuwa na shaka kwamba imani ijulikayo vizuri ya Abu Talib inaweza vile vile kukatiliwa?

Sheikh: Je, unataka kusema kwamba mamilion ya Waislamu wamevunja amri ya Qur’ani na sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Kumbuka, ulimwengu wote unatuita sisi Sunni, yaani, wafuasi wa Sunna. Mashi’a wanaitwa Rafidh, yaani, wale waliopotoka kutoka kwenye sunna ya Mtume.

Sunni Kwa Kweli Ndio Marafidhi Na Mashi’a Ndio Sunni Hasa

Muombezi: Kiukweli hasa Mashi’a ndio Masnni, yaani, wao wanafuata Qur’ani Tukufu na sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Ninyi watu nyie ni Marafidhi kwa sababu mnavun- ja amri za Qur’ani Tukufu na maamrisho ya Mtume. Sheikh: Hii ni ajabu kweli! Umewageuza mamiloni ya Waislamu safi kuwa marafidhi! Unaweza kuleta hoja yoyote ya kuunga mkono hili?

Muombezi: Nimekwisha kukuambia katika mikesha iliyopita kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilituagiza kwamba baada yake lazima tufuate Qur’ani Tukufu na kizazi chake.

Lakini ninyi watu kwa makusudi mkakitelekeza kizazi cha Mtume na kufuata wengine. Mmeutupa mwenendo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mliwaacha watu wale (Ahlu’l- Bayti) kwa amri ya masheikh wenu wawili na kisha mkawaita wafuasi halisi wa sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) Marafidhi.

Miongoni mwa maagizo hayo kuna amri nyingine ya wazi katika Qur’ani Tukufu ambayo inasema:

“Na jueni kwamba chochote mlichokiteka, basi sehemu yake ya tano ni ya Allah na Mtume na (jamaa zake Mtume) na yatima na masikini na msafiri (aliyeharibikiwa)…” (8:41)

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliitekeleza amri hii na akatoa khums (1/5) ya mali iliyopatikana kutoka kwa adui na kuwapa jamaa na ndugu zake. Lakini ninyi watu mnaupinga mwendo huu.

Kufanya mut’a ni mfano mwingine mzuri. Ilikuwa ni kwa mujibu wa amri ya Allah. Ilithibitishwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na masahaba zake.

Utekelezaji wake uliendelea wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr na vile vile kwa kipindi katika wakati wa ukhalifa wa Umar.

Lakini kwa amri yake Umar ninyi watu mmekifanya haramu kile Allah alichoki- fanya halali.

Aidha, mmeiuuza sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Na bado mnajiita wenyewe Sunni na kutuita sisi Rafidh.

Khalifa Umar mwenyewe hakutoa sababu yoyote ya kuifuta amri ya Mungu. Maulamaa wa Sunni wamejaribu bila mafanikio kuthibitisha kwamba uamuzi wa Khalifa Umar ulikuwa wa haki.

Hoja Za Uhalali Wa Mut’a

Sheikh: Unaweza ukathibitisha uhalali wa mut’a? unaweza ukathibitisha kwamba Khalifa Umar alivunja amri ya Qur’ani na sunna ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?

Muombezi: Uthibitisho wenye nguvu sana unatolewa na Qur’ani Tukufu. Katika Sura ya Nisa Allah anasema:

{ﻓَﻤﺎ اﺳﺘَﻤﺘَﻌﺘُﻢ ﺑِﻪ ﻣﻨْﻬﻦ ﻓَﺂﺗُﻮﻫﻦ اﺟﻮرﻫﻦ ﻓَﺮِﻳﻀﺔً ۚ{24

“…Na kwa wale ambao mmestarehe nao katika wao, basi wapeni mahari yao yaliyolazimu…” (4:24)

Kwa dhahiri amri ya Qur’ani Tukufu daima ni ya wajibu isipokuwa iwe imefutwa na Qur’ani yenyewe. Kwa vile haikufutwa, amri hii hubakia ya wajibu daima.

Sheikh: Vipi aya hii isihusike na ndoa ya kudumu? Ni aya hii hii ambayo hutoa maeleke zo kuhusu kulipa mahari.

Muombezi: Umeichanganya nukta yenyewe. Maulamaa wenu wenyewe, kama Tabari katika Tafsir-e- Kabir, Jz. 5 na Imam Fakhru’d-din Razi katika tafsiri yake Tafsir-e-Mafatihu’l-Ghaib, Jz. 3, wamethibitisha kwamba aya hii inazungumzia mut’a.

Mbali na tafsiri ya wazi ya maulamaa wenu na wafasir, vile vile una habari kwamba kati- ka Sura yote ya Nisa, aina mbali mbali za ndoa zimetajwa: ndoa ya kudumu, mut’a, (ndoa ya muda) na ndoa ya mulk-e-Yamin (watumwa).

Kwa ndoa ya kudumu Qur’ani Tukufu inasema:

{ﻓَﺎﻧْﺤﻮا ﻣﺎ ﻃَﺎب ﻟَﻢ ﻣﻦ اﻟﻨّﺴﺎء ﻣﺜْﻨَ وﺛَُث ورﺑﺎعَ ۖ ﻓَﺎنْ ﺧﻔْﺘُﻢ ا ﺗَﻌﺪِﻟُﻮا ﻓَﻮاﺣﺪَةً او ﻣﺎ ﻣﻠَﺖ اﻳﻤﺎﻧُﻢ ۚ{3

“…Basi oweni mnaowapenda katika wanawake, wawili au watatu au wanne; lakini kama mkiogopa kuwa hamuwezi kufanya uadilifu basi (oweni) mmoja au waliom likiwa na mikono yenu…” (4:3)

Kuhusu Mulk-e-Yamin (watumwa), Allah anasema:

وﻣﻦ ﻟَﻢ ﻳﺴﺘَﻄﻊ ﻣﻨْﻢ ﻃَﻮ انْ ﻳﻨْﺢ اﻟْﻤﺤﺼﻨَﺎتِ اﻟْﻤﻮﻣﻨَﺎتِ ﻓَﻤﻦ ﻣﺎ ﻣﻠَﺖ اﻳﻤﺎﻧُﻢ ﻣﻦ ﻓَﺘَﻴﺎﺗﻢ اﻟْﻤﻮﻣﻨَﺎتِ ۚ واﻟﻪ {اﻋﻠَﻢ ﺑِﺎﻳﻤﺎﻧﻢ ۚ ﺑﻌﻀﻢ ﻣﻦ ﺑﻌﺾٍ ۚ ﻓَﺎﻧْﺤﻮﻫﻦ ﺑِﺎذْنِ اﻫﻠﻬِﻦ وآﺗُﻮﻫﻦ اﺟﻮرﻫﻦ ﺑِﺎﻟْﻤﻌﺮوفِ ﻣﺤﺼﻨَﺎتٍ{25

“Na miongni mwenu asiyeweza kupata mali ya kuoa wanawake waungana wa Kiislamu, basi aowe katika wajakazi wenu wa Kiislamu mliowamiliki; na Allah anajua sana imani yenu. Baadhi yenu mnatokana na baadhi, basi waoeni kwa idhini ya watu wao na muwape mahari yao kwa haki…” (4:25)

Ile amri katika aya ya 24 ya sura Nisa inayosema: “…Na kwa wale ambao mmestarehe nao katika wao, basi wapeni mahari yao yaliyolazimu…” ilikuwa kwa ajili ya mut’a, au ndoa ya muda. Isingeweza kuwa kwa ajili ya ndoa ya kudumu, kwani vinginevyo, ingemaanisha kwamba katika sura hiyo hiyo amri inayohusu ndoa ya kudumu imerudiwa mara mbili, ambayo ni kinyume cha kanuni, na kama ni kwa ajili ya mut’a, basi kwa dhahiri ni amri ya kudumu na iliyo tofauti (na ndoa nyingine). Pili, sio Mashi’a tu bali Waislamu wote wanakubali kwamba mut’a ilikuwa ikifanyika wakati wa siku za mwanzo za Uislamu. Masahaba mashuhuri waliifanya wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Kama aya hii inaashiria ndoa ya kudumu, basi ni ipi aya kwa ajili ya mut’a? kwa dhahiri hii ndio aya inayohusu mut’a, ambayo wafasir wenu wenyewe wameikubali. Hakuna aya katika Qur’ani Tukufu ambayo inaifuta amri hii.

Ahli-Sunna Wazingatia Uhalali Wa Mut’a

Imesimuliwa katika Sahih Bukhari na Musnad ya Imam Ahmad Ibn Hanbal, kutoka kwa Abu Raja kutoka kwa Imran Ibn Hasin, kwamba aya ya mut’a iliteremshwa katika Kitabu cha Allah.

Hivyo tulifanya (mut’a) kwa mujibu wake wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). hakuna aya iliyoteremshwa kuifanya haramu, wala kamwe Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hajaikataza. Mtu mmoja aliamua kuibadilisha amri hii. Bukhari anasema kwam- ba mtu huyo alikuwa ni Umar.”

Muslim katika Sahih yake Jz. 1, katika sura ya Nikatu’l-Mut’a, anasema: “Hasan Halwa’i alitusimulia kwamba, aliambiwa na Abdu’r-Razzaq, ambaye alijulishwa na Ibn Jarih, ambaye alielezwa na ‘Ata kwamba Jabir Ibn Abdullah Ansari alikuja Makka kwa ajili ya Umra na walikwenda nyumbani kwake alikofikia. Watu walimuuliza maswali mengi.

Wakati walipokuja kwenye suala la mut’a, yeye alisema: ‘Ndio, tulizoea kufanya mut’a wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wakati wa ukhalifa wa Abu Abkr na Umar.’”

Vile vile katika kitabu hicho hicho Jz. 1, katika sura ya al-Mut’a Bi’l-Hajj wa’l-Umra, inasimuliwa kutoka kwa Abu Nazara kwamba alisema: “Nilikuwa pamoja na Jabir Ibn Abdullah Ansari wakati mtu mmoja alipokuja na kusema: ‘kuna tofauti ya maoni kati ya Ibn Abbas na ibn Zubair kuhusu hizi mut’a mbili, Mut’atu’n-Nisa na Mut’atu’l-Hajj.’ Kisha Jabir akesema: ‘Tumezifanya zote hizo wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Baada ya hapo, wakati Umar alipozikataza, hatukuweza kuzifanya.’”

Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, Jz. 1, uk. 25, anasimulia riwaya ya Abu Nazara katika njia nyingine. Vile vile wote wanasimulia riwaya nyingine kutoka kwa Jabir kwamba yeye alisema:

“Katika siku za uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Abu Bakr, tulizoea kufanya mut’a kwa makubaliano ya kiganja cha tende na unga mpaka Umar alipoikataza katika suala la Amr Bin Harith.”

Hamid, katika Jam’-e-Bainu’s-Sahihain, anasimulia kutoka kwa Abdullah Ibn Abbas kwamba alisema: “Tulizoea kufanya mut’a wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Wakati Umar alipokuwa Khalifa akasema: ‘Allah swt., alifanya chochote alichokitaka kwa ajili ya Mtume Wake. Sasa amekufa, na Qur’ani inachukuwa mahala pake. Hivyo wakati ukianza Hajj au Umra, lazima uzimalize kama Allah alivyokuamuruni. Lazima mtubie na mjiepushe kufanya mut’a, nileteeni yule aliyefanya mut’a ili niweze kumpiga mawe.’” Kuna riwaya nyingi kama hizo katika vitabu vyenu wenyewe vya kuaminika zikionesha kwamba mut’a iliruhusiwa wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Masahaba waliifanya mpaka Umar alipoiharamisha. Mbali na riwaya hizi, baadhi ya masahaba, kama Ubayy ibn Ka’b, ibn Abbas, Abdullah ibn Mas’ud, Sa’id ibn Jabir na Sa’d wamesoma aya ya mu’ta katika njia hii: “…na kwa wale ambao mmefanya nao mut’a mpaka muda uliowekwa…”

Jarullah Zamakhshari anasimulia katika Kash’shaf kutoka kwa kwa Ibn Abbas na vile vile Muhammad Bin Jarir Tabari katika Tafsir-e-Kabir na Imam Fakhru’d- din Razi katika Tafsir-e-Mafatihu’l-Ghaib, Jz. 3, wakiandika kuhusu aya hii tukufu na Imam Nuwi katika Sharh-e-Muslim, Sura ya 1, Nikatu’l-Mut’a anasimulia kutoka kwa Nazari kwamba Qadhi Ayaz alieleza kwamba “Abdullah Bin Mas’ud, yule mwandishi wa Wahyi, alizoea kusoma aya hii katika njia hiyo hiyo, yaani, ‘mpaka muda uliowekwa.’”

Imam Fakhru’d-din Razi, baada ya kunukuu maelezo ya Ubayy Ibn Ka’b na Ibn Abbas, alisema: “Umma haukukataa usomaji wao wa aya katika njia hii, hivyo tulichokisema kimekubaliwa kwa ijma (makubaliano ya wote pamoja).”

Tena katika ukurasa ufuatao anajadili kwa namna hii: “Usomaji huu kwa dhahiri huthibitisha kwamba mut’a inayo idhini ya kidini. Hatuna tofauti ya maoni kwamba mut’a iliruhusiwa katika wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume.”

Amri Inayoruhusu Mut’a Haikufutwa

Sheikh: Unaweza kuthibitisha kwamba ilikuwa halali wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kwamba haikufutwa baadae?

Muombezi: Kuna ushahidi mwingi kwamba amri hii haikufutwa. Hoja yenye kuvutia sana ni kwamba mut’a iliruhusiwa kuanzia wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka katikati ya ukhalifa wa Umar.

Maelezo ya Khalifa Umar mwenyewe yamesimuliwa kwa jumla na maulamaa wenu. Wameandika kwamba alipanda kwenye mimbari na akasema:

“Katika wakati wa Mtume mut’a mbili ziliruhusiwa. Mimi ninazifanya zote mbili hizi kuwa ni haramu, na kama mtu yeyote atazifanya, nitamuadhibu.”

Sheikh: Unachosema ni sahihi, lakini nukta yangu ni kwamba kuna amri nyingi ambazo zilikuwa zikitumika mwanzo katika wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini baadae zikafutwa. Mut’a vile vile iliruhusiwa wakati wa mwanzo, lakini baadae ikapigwa marufuku.

Muombezi: Kwa vile asili na msingi wa dini ni Qur’ani Tukufu, kama amri yoyote inakuwemo ndani ya Qur’ani ufutaji wake lazima vile vile uwe ndani yake. Sasa tafadhali nifahamishe ni wapi katika Qur’ani ambapo amri hii imefutwa. Sheikh: Katika Sura ya 23, Mu’minin, aya ya 6 inafuta amri hii. Inasema: “Isipokuwa kwa wake zao au kwa (wanawake) wale waliomilikiwa na mikono yao, basi hao si wenye kulaumiwa.” (23:6) Aya hii inaweka masharti mawili kwa ajili ya uhusiano wa kinyumba: ndoa au kuingiliana (kijamiiana) na mtumwa. Hivyo aya hii inathibitisha kwamba amri ya mut’a ilifutwa.

Muombezi: Aya hii kwa njia yoyote haithibitishi kwamba mut’a ilifutwa; bali inaithibitisha. Mwanamke aliyeunganishwa na mut’a ni mke halisi wa mwanaume huyo. Lau asingekuwa mke wake halisi, Allah asingeamrisha mahari yake ilipwe.

Aidha, sura ya al-Mu’minin iliteremshwa wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yuko Makka, Sura ya Nisa iliteremshwa wakati akiwa Madina. Ni dhahiri kwamba Sura za Makka zilitangulia zile za Madina. Je, inawezekana aya A kufuta aya B, ikiwa aya A ilikuja kabla ya B?

Masahaba Maarufu Na Imam Malik Wanasisitiza Kwamba Amri Ya

Mut’a Haijafutwa

Abdullah Ibn Abbas, Abdullah Ibn Mas’ud, Jabir Bin Abdullah Ansari, Salama Ibn Akwa, Abu Dharr Ghifari, Subra Bin Ma’bad, Akwa Bin Abdallah al-Aslami na Imran Bin Hasin wameeleza kwamba amri ya mut’a haijafutwa. Aidha, maulamaa wenu maarufu wamethibitisha kwamba haijafutwa.

Kwa mfano, Jarullah Zamakhshari, katika Tafsir-e-Kashshaf kuhusiana na maelezo ya Abdullah Ibn Abbas kwamba aya ya mut’a ilikuwa ni moja ya amri za wazi za Qur’ani Tukufu, anasema kwamba aya hii haijafutwa. Imam Malik Bin Anas vile vile alisema kwamba uruhusiwaji ya mut’a haukufutwa.

Mulla Sa’idu’d-din Taftazani katika Sharh-e-Maqasid, Burhanu’d-din Hanafi katika kitabu chake, Hidaya, Ibn Hajar Asqalani katika Fathu’l-Bari na wengine vile vile wamesimulia ile kauli na hukumu ya Malik ambaye anasema: “Mut’a ni halali. Imeruhusiwa na dini.

Uhalali wake, kwa ilivyothibitishwa na Ibn Abbas, hujulikana sana na wengi wa masahaba wake kutoka Yeman na Makka walikuwa wakiifanya.” Katika sehemu nyingine anase- ma: “Mut’a ni halali kwa vile imeruhusiwa, na uhalali wake na ruhusa yake imethibiti mpaka iwe imefutwa.” Utaona kwamba mpaka Malik alipokufa kulikuwa hakuna ushahidi kwamba amri ya mut’a imefutwa.

Aidha, wafasiri wenu maarufu, kama Zamakhshari, Baghawi, na Imam Tha’labi wamefuata msimamo wa Ibn Abbas na masahaba wengine maarufu na wameamini katika uhalali wa mut’a. Masharti Yote Ya Ndoa Yanatimizwa Katika Ndoa Ya Mut’a

Sheikh: Kwa vile hakuna masharti kwa mwanamke aliyeunganishwa katika mut’a, kama vile urithi, talaka baada ya muda kwisha na kumkimu, kama ilivyo muhimu kwa mke, hawezi kuwa mke halisi.

Muombezi: Mwanamke aliyeunganishwa na mwanaume kwa mut’a, analindwa na masharti yote ya mke yeyote isipokuwa yale ambayo kimantiki yameondolewa. Mut’a ni aina ya ndoa, ambayo kwayo mwanamke anastahiki kuwa mke halisi. Kama mambo yalivyo kwa ajili ya ustawi wa umma na kuwaokoa kutokana na uvunjaji wa sheria, baadhi ya masharti na taratibu zimeondolewa.

Ama kuhusu masharti yake, kwanza, haikuthibishwa kwamba urithi ni sharti la muhimu katika ndoa. Wanawake wengi, pamoja na kuwa wake, hawapati urithi kutoka kwa waume zao. Kwa mfano, wake wasio watiifu au wale wanaouwa wananyimwa urithi.

Pili, haikuthibitishwa kwa uhakika iwapo mwanamke aliyeunganishwa katika mut’a ananyimwa haki yake ya urithi. Wanachuo wa sheria wanahitalifiana katika maoni juu ya hili, na tofauti kama hizi zipo pia miongoni mwenu.

Tatu, maulamaa wa Imamiyya kwa kauli moja wanashikilia mtazamo wa kwamba mwanamke aliyeunganishwa katika mut’a vile vile lazima akae edda. Ufupi wake umewekwa kwamba ni siku 45.

Kama mume akifariki itambidi huyo mke akae edda ya kawaida ya miezi mine na siku kumi, awe amewahi kujamiana na mume wake au la, au iwapo amevuka umri wa kupata haidhi au la.

Nne, haki ya kumkimu sio sharti la muhimu liloambatanishwa kwenye ndoa. Kuna idadi ya wake ambao hawastahili matumizi ya kukimiwa, kama vile wale ambao sio watiifu au ambao wamewauwa waume zao.

Tano, kwisha kwa muda uliokubaliwa kwenyewe ni talaka. Halikadhalika, kwa ridhaa ya mume wake, anaweza kuachika kabla ya muda kwisha. Kwa hiyo, hakuna katika masharti uliyotaja aambalo lina nguvu yoyote ya kisheria. Mwanachuoni maarufu wa Shia, Allama Jamalu’d-Din Hilli (Hasan bin Yusuf Bin Ali Bin Mutahhari), alitoa katika maelezo marefu hoja hiyo hiyo kwa majibu ya mitazamo ya ulamaa wenu maarufu.

Nimeyataja kwa ufupi. Anayetaka kusoma kwa urefu, anaweza kuan- galia kitabu cha Allama Hilli, Mabahithat-e-Sunniyya wa Ma’rifat-e-Nussariyya.

Je, Amri Ya Qur’ani Juu Ya Mut’a Ilifutwa Na Mtukufu Mtume?

Sheikh: Mbali na aya hii tukufu vile vile kuna idadi kubwa ya hadithi ambazo zinazsema kwamba amri inayohusiana na mut’a imefutwa wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Muombezi: Tafadhali tufahamishe amri hiyo ya kufuta.

Sheikh: Imesimuliwa pamoja na tofauti fulani. Baadhi ya wasimuliaji wanasema kwamba ilifutwa siku ya kutekwa kwa Khaibar, baadhi wanasema ilitokea katika siku ya kutekwa Makka, baadhi wanasema kwamba ilikuwa wakati wa hija ya mwisho, na baadhi wanasema kwamba ilikuwa katika siku ya Tabuk. Wengine, hata hivyo, maoni yao ni kwamba amri hiyo ya kufuta ilitolewa siku ya Umratu’l-Qadhwa (Hija ya mwago).

Hoja Zinazohusu Kufutwa Kwake Wakati Wa Uhai Wa Mtume

Muombezi: Hizo riwaya zinakinzana zenyewe zinathibitisha wazi kwamba kulikuwa hakuna amri ya kufutwa. Na vipi riwaya hizo zitaaminika wakati kinyume chake kuna hadithi nyingi zilizosimuliwa katika Sahih-e-Sitta: Jam-e-Bainu’s-Sahihain, Jam-e- Bainu’s-Sahih-e-Sitta, Musnad, nk., kutoka kwa masahaba maarufu ambazo zinathibitisha kwamba aya hii haikufutwa mpaka wakati wa ukhalifa wa Umar.

Hoja ya kuvutia sana ambayo maulama wenu wenyewe wameinukuu ni ile kauli ya Khalifa Umar, ambaye alisema: “Naziharamisha zile mut’a mbili ambazo zilikuwa zikitumika wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Lau kungelikuwa na aya, au amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Khalifa angelisema: “Kwa mujibu wa maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambayo yanaungwa mkono na aya ya Qur’ani, kama mtu atafanya kitendo cha haramu kwa kuvunja amri iliyofutwa, mimi nitamuadhibu.”

Maelezo kama haya yangekuwa zaidi sana yenye kuvutia kwa watu. Lakini alisema tu: Mut’a mbili zilikuwa zimeruhusiwa wakati wa uhai wa Mtume, mimi naziharamisha.”

Hata hivyo, kama madai yako ni sahihi na aya ya mut’a ilifutwa, kwanini wanafunzi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kama Abdullah Ibn Abbas, Imran Bin Hashim na masahaba wengine waliifanya? Muhadithina na wanahistoria wenu wakubwa, ikiwa ni pamoja na Bukhari na Muslim, wameandika habari hii.

Taarifa zote hizi zinathibitisha kwa uwazi kwamba kutoka wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka wakati wa ukhalifa wa Umar masahaba walifuata sheria hii.

Je, Khalifa Umar Angeweza Kuifuta Mut’a?

Hivyo, ni wazi kwamba mut’a itaendelea kuwa halali daima. Abu Isa Muhammad Bin Sawratu’t-Tirmidhi katika Sunan yake, ambayo inachukuliwa na ninyi kama moja ya Sahih sita, Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, sehemu ya 2, uk. 95, na Ibn Athir katika Jam’u’l-Usul wamesimulia kwamba mtu mmoja wa Syria alimuuliza Abdullah Bin Umar Bin Khattab anachofikiria kuhusu Mut’a-e-Nisa. Yeye akasema: “Bila shaka, ilivyo hiyo ni halali.” Yule mtu akasema tena: “Lakini baba yako, Khalifa, alikataza watu kuifanya.” Akasema: “Iliamriwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.); hivyo, kama imekatazwa na baba yangu amri hiyo haiwezi kuizidi amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mimi ni mfuasi wa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Ama kwa riwaya ambazo zimesimuliwa, huenda watu walighushi hadithi baadae ili kuunga mkono kauli ya Umar. Suala hili liko wazi kiasi kwamba halihitaji ufafanuzi wa zaidi. Ukweli ni kwamba huna ushahidi wa kweli juu ya uharamu wa mut’a isipokuwa ile kauli ya Khalifa Umar.

Sheikh: Kauli ya Khalifa Umar yenyewe ni ushahidi wenye nguvu sana kwa ajili ya Waislamu, na lazima waifuate. Kama alikuwa hakuisikia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kuisema.

Muombezi: Je, kauli ya Khalifa Umar ni ya kushurutisha kiasi hicho kwamba Waislamu lazima waifuate? Sijaona hadithi hata moja kwenye vitabu vyenu, ambayo kwayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba kauli ya Umar Bin Khattab ilikuwa ni chanzo kilichothibitishwa au kwamba Waislamu lazima waifuate.

Kwa upande mwingine vitabu vyenu vimejazwa hadithi za kuaminika zinazosema kwamba lazima tufuate kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hususan Ali. Nimzitaja baadhi ya hadithi hizi katika mikesha iliyopita. Hao Ahlul’l-Bayti wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wamesema kwamba amri ya mut’a haikufutwa.

Umesema kwamba lau kama Khalifa Umar asingesikia amri hiyo ya kufuta mut’a kutoka Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), asingesema aliyoyasema. Lakini hili ni rahisi kulikanusha. Kwanza, kama Khalifa Umar alikuwa amesikia juu ya ufutwaji wa amri ya mut’a kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), angeisimulia wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka wakati wa ukhalifa wake mwenyewe.

Hii ingekuwa na umuhimu maalum kwa vile aliwaona masahaba mashuhuri walikuwa wakiifanya, na ilikuwa ni wajibu wake kuwaeleza watu kwamba matumizi ya mut’a yalikuwa yamefutwa. Kwanini hakutekeleza jukumu la kuzuiya uovu?

Pili, matumizi ambayo yalikuwepo miongoni mwa umma kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), yangeweza tu kufutwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kusingekuwa na ucheleweshaji katika suala hili. Je, inaingia akilini kwamba kama amri kwa ajili ya umma ilikuwa imekwisha kusambazwa na baadae ikafutwa, je, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingezungumza kwa mtu yeyote isipokuwa kwa Umar?

Na je, ingeleta maana yoyote kwamba Umar asingemuambia mtu yeyote mpaka baadae katika ukhalifa wake mwenyewe? Katika kipindi chote hiki wakati umma ukiendelea kufuata amri hii (inayodai- wa) iliyofutwa, je, hakukuwa na uwajibikaji kwa upande wa Umar?

Unasema kwamba ukatazaji wa matumizi “yaliyofutwa na yasiyo ya kidini” usingeweza kufanywa ujulikane kwa watu wengine na kwa hiyo umma uliendelea kuyafuata. Je, mtu mwingine yeyote yule mbali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anaweza kuwajibishwa kwa sababu ya kutokutangaza amri iliyofutwa, akiwa yeye kamuambia Umar peke yake tu? Je, sio ukafiri kusema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amepuuza kutekeleza kazi yake na kwamba umma kwa sababu ya kutokujua kwao, waliendelea kutenda amri iliyofutwa kwa muda mrefu?

Tatu, kama amri ya mut’a ilikuwa imefutwa wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Umar alikuwa amelisikia hili kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Umar angelisema wakati alipokuwa analikataza hili kwamba yeye mwenyewe amemsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema kwamba matumizi ya mut’a yamepigwa marufuku. Ni dhahari, kama angekuwa anarejea kauli ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), umma ungevutiwa mno na hilo.

Lakini alisema: “Wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mut’a mbili zilikuwa zimeruhusiwa, lakini mimi ninaziharamisha. Sasa nitawapiga mawe wale wanaoifanya.”

Je, sio jukumu la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kutangaza vitu kuwa ni halali au haramu? Au, inaweza kuwa haki ya Khalifa ambaye alichaguliwa na watu?

Sielewi ni kwa misingi ipi Umar alitangaza kuharamisha kile alichohalalisha Allah swt. Ajabu iliyoje Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe kamwe hajasema kwamba amekifanya kitu fulani kuwa halali au haramu. Wakati wowote alipotangaza amri yeyote, alisema kwamba Allah alimuamrisha kuifikisha kwa watu. Ujasiri ulioje alikuwa nao Umar aliposema: “Mut’a mbili zilikuwa zimeruhusiwa wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mimi nazifanya zote hizo kuwa haramu. Nitawaadhibu wale ambao wanatenda matendo hayo.”

Amri Ya Allah Au Ya Mtukufu Mtume Haiwezi Kufutwa Na Khalifa

Sheikh: Kwa hakika unafahamu kwamba baadhi ya wanachuoni wetu wenye ilmu ya juu wanaamini kwamba kwa vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa mujtahid katika masuala ya amri za kidini, mujtahid mwingine kwa mujibu wa utafiti wake mwenyewe, anaweza kuweka kando amri iliyotangulia. Ni kwa msingi huu kwamba Umar alisema: “Naviharamisha vitu viwili hivyo.”

Muombezi: Katika kujaribu kuweka sawa kosa moja unafanya makosa mengine mengi. Je, ijtihad ina maana yoyote katika kukanganya amri yoyote ya Qur’ani Tukufu. Je, kauli yako hiyo sio ya kichekesho kabisa na inayopingana na aya za Qur’ani? Allah swt., anasema katika Sura ya Yunus:

{ﻗُﻞ ﻣﺎ ﻳﻮنُ ﻟ انْ اﺑﺪِّﻟَﻪ ﻣﻦ ﺗﻠْﻘَﺎء ﻧَﻔْﺴ ۖ انْ اﺗﱠﺒِﻊ ا ﻣﺎ ﻳﻮﺣ اﻟَ ۖ{15

“…Sema: siwezi kuibadilisha kwa hiari ya nafsi yangu. Sifuati ila ninayofunuliwa kwa wahyi…” (10:15)

Ni kweli kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hawezi akafanya mabadiliko yoyte katika amri za dini isipokuwa mpaka aamrishwe na Allah kufanya hivyo. Vipi, amewezaje Umar, ambaye hana ujuzi wa Wahyi, kuwa na mamlaka ya kufanya haramu kile ambacho Allah amekifanya halali? Katika Suratun-Najm Allah anasema:

{وﻣﺎ ﻳﻨْﻄﻖ ﻋﻦ اﻟْﻬﻮﱝ {3

{انْ ﻫﻮ ا وﺣ ﻳﻮﺣ {4

“Wala hazungumzi kwa matamanio ya nafsi yake. Hayakuwa haya ila ni wahyi ulioteremshwa. (53:3-4)

Katika Surat Ahqaf, Allah anasema:

{ﻗُﻞ ﻣﺎ ﻛﻨْﺖ ﺑِﺪْﻋﺎ ﻣﻦ اﻟﺮﺳﻞ وﻣﺎ ادرِي ﻣﺎ ﻳﻔْﻌﻞ ﺑِ و ﺑِﻢ ۖ انْ اﺗﱠﺒِﻊ ا ﻣﺎ ﻳﻮﺣ اﻟَ وﻣﺎ اﻧَﺎ ا ﻧَﺬِﻳﺮ ﻣﺒِﻴﻦ {9

“Sema: mimi sio wa kwanza katika mitume, wala sijui nitakayofanywa mimi wala mtakayofanywa ninyi. Sifuati ila niliyoteremshiwa kwangu, na mimi siye ila ni muonyaji dhahiri. (46:9)

Utii kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni wajibu. Hakuna yeyote, awe Umar au mtu mwingine yeyote, aliye na haki ya kuingilia amri za Mungu na kufanya haramu alichokifanya Allah halali.

Manufaa Hayawi Msingi Kwa Ajili Ya Ufutaji

Sheikh: Kwa hakika Umar aliona inafaa na akaichukulia katika masilahi bora ya watu kuifuta amri ile. Tunaona siku hizi kwamba baadhi ya watu wanamchukua mwanamke katika mut’a kwa ajili ya kustarehe tu kwa muda wa saa moja, mwezi mmoja, au mwaka mmoja. Baadae bila kujali kama mwanamke ni mjamzito au la, wanamtelekeza.

Muombezi: Huu ni mzaha mkubwa! Uhalali huu wa amri ya Kiislamu unahusiana nini na watu wanaojiingiza katika uhusiano wa kujamiiana kuliko haramu? Kama tukifuata hiyo mantiki yako, huenda hata ndoa ya kudumu itafanywa kuwa haramu.

Kwani kuna watu wanawaoa wasichana wazuri wenye heshima zao kwa ajili ya pesa zao au urembo wao na baadae huwaacha bila kuwapa msaada wowote wa kifedha. Kwa vile baadhi ya watu wanafanya hivi, unafikiri ndoa ya kudumu lazima ifutwe?

Hapana. Lazima tuwahimize watu kuwa wanyofu na kuwapa mafunzo sahihi ya duni. Kama mtu mnyofu atajikuta hana uwezo wa kubeba jukumu la kuwa na mke wa kudumu, na kama anataka kuepuka kitendo cha haramu, atakuwa kwa kuafikiana na sheria ya dini, anataka kuchukua mwanamke katika mut’a au ndoa ya muda.

Kwa hiyo, atataka kujua masharti ya mut’a kwa sababu anajua kwamba kwa kila amri kuna masharti fulani. Wakati wa makubaliano ya wote wawili, atatoa kile kiasi cha mahari kwa ajili ya mwanamke ambacho kitatosha kwa matumizi ya kumkimu wakati wa edda, ambao ni siku 45, baada ya muda wa kipindi cha mut’a kwisha.

Pili, baada ya kutengana, atamuangalia mwanamke wakati wa kipindi chote cha edda. Kama atakuwa mjamzito, atamtunza mama huyo sawa sawa ili aweze kumchukua mtoto wake atakapo zaliwa. Kama baadhi ya watu wanashindwa kufuata masharti haya, haina maana kwamba amri ya halali ya kisheria imefutwa.

Ustawi wa umma ulikuwa unajulikana vizuri kwa Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuliko Umar. Na hawakukataza mut’a. Kama wao hawakuikataza, hakuna Khalifa au Imam, au mtu yoyote yule, hata aliyeteuliwa na Mungu, anayeweza kwa hiyari yake mwenyewe kukifanya haramu kile Allah alichokifanya halali. Hivyo madai yako kwamba ilikuwa ni kwa masilahi ya umma kwamba watu waache mut’a, hayathibitiki.

Mut’a haikuwa ndio sababu ya kuenea kwa uvunjaji wa sheria; bali ilikuwa ni kupigwa marufuku kwake ndiko ambako kumeeneza uzinifu.

Wale vijana wa kiume na wa kike ambao hawakumudu kuungana katika ndoa ya kudumu kama hawawezi kujidhibiti na kuzuia hamu zao za kujamiiana, watajiingiza katika ngono haramu. Na kama mambo yalivyo kuenea kwa zinaa na uasherati huharibu maadili mema ya mataifa yote kabisa.

Imam Tha’labi na Tabari katika Tafsir zao na Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, wakiandika kuhusiana na aya ya mut’a, wanasimulia kutoka kwa Amiru’l-Mu’minin Ali kwamba alisema: “Kama Umar asingezuia mut’a hakuna mtu yeyote, isipokuwa mwanaume mwenye bahati mbaya, angefanya uzinifu.”

Vile vile Ibn Jarih na Amr Bin Dinar wanasimulia kutoka kwa Abdullah Ibn Abbas ambaye alisema: “Kwa hakika mut’a ni rehema ya Allah, ambayo ameitoa kwa umma wa Muhammad. Kama Umar asingeipiga marufuku, hakuna mtu yeyote isipokuwa mtu mwenye bahati mbaya angefanya uzinifu.”

Hivyo, kwa mujibu wa maoni ya masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), sababu hasa ya kuenea kwa uzinifu ilikuwa ni kukatazwa kwa mut’a, na si kwa ajili ya kuifanya. Kwa hakika amri zote za Mungu zinazohusu halali na matendo ya halali ambazo zimewasilishwa kwa umma kupitia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) zilikusudiwa kwa ajili ya ustawi wa watu. Bado zinaendelea kuwanufaisha watu hadi hii leo.

Imani Ya Abu Talib Ilikuwa Inajulikana Sana Wakati Wa Mtukufu Mtume

Mada yetu ya kujadali haikuwa hii, lakini nilitaka kuondoa shaka yenu kwa vile umesema kwamba kile kilichokuwa kinajulikana wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kinawezakikafanywa kuwa bure kabisa kupitia hadithi za kughushi. Halikadhalika hakuna uhalali katika kukataa kwako kuhusiana na imani ya Abu Talib.

Imani yake wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa vile vile inajulikana sana na kuchukuliwa kwa heshi- ma. Lakini kwa kubuni hadithi ya Zahza, baadhi ya watu wakaeneza riwaya za kinyume kabisa. Watu wasio na ujuzi, wakiwafuata wakubwa zao kibubusa, wakazikubali riwaya hii ya uwongo.

Kwa ufupi, nilichosema kinathibitisha vya kutosha na zaidi kwamba Ali alitokana na familia bora kiasi kwamba hakuna yeyote katika masahaba maarufu anayeweza kulingana naye.

Mahali Alipozaliwa Ali Ilikuwa Ni Ndani Ya Ka’aba

Dalili nyingine ya hadhi maalum ya Ali ilikuwa ni mahali alipozaliwa. Hakuna mtu mwingine yeyote, kuanzia kwa Adam kuja chini kupitia mitume wote, aliyekuwa na sifa hii.

Kati ya wanadamu wote, ni yeye peke yake aliyezaliwa katika eneo takatifu la Ka’aba. Wakati wa kuzaliwa kwa Nabii Isa, mama yake mashuhuri alilazimika kutoka kwenye nyumba takatifu. Sauti ilimuambia: “Ewe Maiamu! Toka humo Baitu’l-Muqaddas, kwa vile ni sehemu ya kufanyia ibada na sio ya kuzalia watoto.”

Lakini wakati wa kuzaliwa Ali ulipokaribia, mama yake, Fatima Bint Asad, aliambiwa kuingia ndani ya Kaaba. Na hii haikuwa jambo la bahati kana kwamba mwanamke alikuwa ndani msikiti na ghafla akajifungua mtoto. Yeye aliitwa makhsusi kabisa kuingia ndani ya Kaaba, ambayo mlango wake ulikuwa umefungwa. Baadhi ya watu wasio na ujuzi wanafikiri kwamba Fatima Bint Asad alikuwa ndani ya Msikiti Mtukufu wakati aliposikia uchungu wa kuzaa, hakuweza kutoka nje, na akajifungua mtoto.

Ukweli ulikuwa ni kinyume cha hivyo. Ulikuwa ni mwezi wa Fatima Bint Asad wa kujifungua. Alikwenda Masjidu’l-Haram, ambako alisikia uchungu wa uzazi. Alimuomba Allah katika eneo takat- ifu la Kaaba akisema: “Ewe Allah! Nakuomba kwa jina la heshima Yako na kwa unyenyekevu, kunipunguzia uchungu huu wa uzazi.” Ghafla ukuta wa Kaaba, ambao ulikuwa mzima kabisa, ulitoa mwanya.

Riwaya nyingine inasema kwamba sauti ilisikika ikisema: “Ewe Fatima! Ingia ndani ya Nyumba (al- Ka’aba).” Fatima akaiingia ndani ya Nyumba ya Allah, mbele ya kundi la watu ambao walikuwa wamekaa pembeni mwa sehemu hiyo, ukuta wa Kaaba ulipasuka na Fatuma Bint Asad aliingia ndani kisha ukuta ule ukarudia hali yake ya kawaida. Watu wal- ishangazwa sana.

Abbas vile vile alikuwepo pale. Wakati alipoona kilichotokea, mara moja akamuambia Abu Talib kwa sababu alikuwa nazo funguo za mlango. Mara moja alikuja pale na akajaribu kwa bidii zake zote kufungua mlango, lakini mlango haukufunguka. Kwa muda wa siku tatu Fatima Bint Asad alibakia ndani ya Kaaba, inavyoonekana bila chakula cha aina yoyote.

Tukio hili lisilokuwa la kawaida likawa ni gumzo la mjini hapo. Hatimaye, katika siku tatu, sehemu aliyopitia ilifunguka tena, na Fatima akatoka nje. Watu wakaona kwamba alikuwa amepakata mtoto mzuri mikononi mwake. Madhehebu zote (Shia na Sunni) wanakubali kwamba hakuna mtu mwingine yeyote ambaye amewahi kupewa sifa kama hiyo kamwe.

Hakim katika Mustadrak yake na Nuru’d-din Bin Sabbagh Malik katika Fusulu’l-Muhimma, Fasl ya 1, uk. 14, anasema: “Hakuna yeyote kabla ya Ali aliyezaliwa ndani ya Kaaba. Hii ilikuwa ni sifa aliyopewa Ali ili kuzidisha ubora wa hes- hima, cheo, na hadhi yake.”

Asili Ya Jina La Ali Ilikuwa Ni Ulimwengu Usioonekana

Dalili nyingine ya hadhi maalumu ya Ali ni kwamba jina lake lilikuwa na asili katika ulimwengu usioonekana.

Sheikh: Umesema kitu kigeni. Hii ina maana Abu Talib alikuwa Mtume ambaye alimpa jina Ali kupitia msukumo wa ki-Mungu. Kauli yako ni moja kati ya ule uwongo ambao Mashi’a wameutunga katika mapenzi yao yaliyovuka mpaka (ghulu) kwa Ali.

Lakini ni kichekesho kusema kwamba Allah aliamuru kwamba mtoto huyo aitwe Ali. Ali lilikuwa ni jia la kawaida ambalo wazazi hao kwa utashi wao, walipanga kumpa mtoto wao. Halikuwa na cho chote cha kuhusiana na ulimwengu wa ghaibu.

Muombezi: Kitu nilichosema hakina ugeni ndani yake. Kustaajabu kwako kunatokana na kukosa ujuzi kwako kuhusu ustahili na sifa ya wilaya (uandamizi).

Kwanza, wewe unafikiri kwamba mtoto huyo alipewa jina baada ya kuzaliwa kwake, ingawaje haikuwa hivyo. Katika vitabu vyote vitakatifu, majina ya Muhammad na Ali yametajwa.

Allah swt., aliwapa majina miaka elfu kadhaa kabla ya uumbaji wa ulimwengu. Majina haya yaliandikwa mbinguni, kwenye milango ya mbingu na kwenye Arsh. Hayahusiani cho chote na wakati wa Abu Talib.

Sheikh: Hakika kauli hii ni mfano wa mapenzi yaliyovuka mpaka juu ya Ali. Umempandisha juu mno kiasi kwamba unadai kwamba jina lake liliandikwa zamani mno kabla ya kuumbwa ulimwengu. Matokeo ya kauli kama hizi ni kwamba wanachuo wenu wanachukulia kulitaja jina la Ali baada ya jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika adhana.

Muombezi: Hapana, bwana, kauli yangu haihusiani na mapenzi ya kuvuka mpaka. Na sio mimi niliyeandika jina lake mbinguni. Allah aliamrisha jina la Ali liandikwe pamoja na Jina Lake na jina la Mtume Wake.

Sheikh: Tafadhali taja yoyote katika hadithi hizo.

Baada Ya Majina Ya Allah Na Mtukufu Mtume Jina La Ali Limeandikwa Juu Ya Arsh

Muombezi: Muhammad Bin Jarir Tabari katika Tafsiir yake, Ibn Asakir katika Ta’rikh yake, Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i, katika Kifayatu’t-Talib, sura ya 62, Hafidh Abu Nu’aim, katika Hilyatu’l-Auliya, na Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l- Mawadda, uk. 238, sura ya 56, hadithi ya 52, wanasimulia kutoka kwenye Dhakha’iru’l- Uqba ya Imam’l-Haram Ahmad Bin Abdullah Tabari Shafi’i kutoka kwa Abu Huraira (pamoja na tofauti kidogo maneno) kwamba Mtukufu Mtukufu alisema: “Imeandika juu ya Arsh kwamba, ‘Hakuna mungu ila Allah, Mmoja Ambaye hana mshirika; na Muhammad ni Mjumbe na Mtume Wangu, ambaye nimemuimarisha kupitia kwa Ali Bin Abi Talib.’”

Vile vile katika Khasa’isu’l-Kubra ya Jalalu’d-Din Suyuti, Jz. 10, na Tafsir-e-Durr-e- Mansur, mwanzoni mwa sura ya Isra’il, inasimuliwa kutoka Ibn Adi na Ibn Asakir, ambao wanasimulia kutoka kwa Anas Ibn Malik, kwamba Mtukufu Mtume wa Allah alisema kwamba aliona maandishi kwenye Arsh: “Hakuna mungu ila Allah; Muhammad ni Mtume wa Allah; nimempa msaada kupitia kwa Ali.”

Katika Yanabiu’l-Mawadda inasimuliwa kutoka kwenye Dhakha’iru’l-Uqba ya Imam’l-Haram Tabari, kwa mujibu wa riwaya ya Sirat-e-Mullah, kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alisema: “Katika ule usiku wa Mi’raj, nilipochukuliwa mpaka kwenye mbingu ya juu kabisa, huko niliona maandishi upande wa kulia wa Arsh: ‘Muhammad ni Mtume wa Allah. Nimempa msaada kupitia kwa Ali.’”

Imesimuliwa katika Yanabiu’l-Mawadda, Hadith 19, kutoka kwenye Kitabu’s-Sabi’in cha Imamu’l-Haram Tabari, akinukuu kutoka Manaqib ya Faqih Wasti Ibn Maghazili Shafi’i, na vile vile Mir Seyyid Ali Hamadani Shafi’i anaandika katika Mawadda 6 kutoka Mawaddatu’l-Qurba hadithi mbili; Khatib Khawarizmi katika Manqib, Ibn Shirwaih katika Firdaus, na Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib, akisimulia kutoka kwa Jabir Bin Abdulla Ansari kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Imeandikwa katika mlango wa Pepo kwamba ‘hakuna mungu ila Allah, Muhammad ni mtume wa Allah, na Ali ni Wali (mwandamizi) wa Allah na ndugu wa Mtukufu wa Mtume wa Allah.’ Hiyo iliandikwa miaka 2,000 kabla ya kuumbwa kwa mbingu na ardhi.”

Nakumbuka hadithi nyingine. Mir Seyyid Ali Faqih Shafi’i anaandika katika Mawadda 8 ya Mawaddatu’l- Qurba kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali: “Nimeliona jina lako likiwa limeunganishwa na la kwangu katika sehemu nne:

(1) Katika usiku wa Miraji wakati nilipofika Baitu’l-Maqaddas (Kuba ya Jiwe), niliona maandishi juu ya jiwe: “Hakuna mungu ila Allah, na Muhammad ni Mtume wa Allah ambaye nimempa msaada kupitia kwa waziri wake Ali.” (2) Wakati nilipofika Sidratu’l-Muntaha, niliona maneno: “Hakika Mimi ni Allah; haku- na mungu ila Mimi, Mmoja, na Muhammad miongoni mwa viumbe wangu wote ndiye mpendwa Wangu. Nimempa msaada kupitia kwa waziri wake, Ali.”

(3) Wakati nilipofikia Arsh ya Allah swt, niliona kuna maandshi kwenye nguzo zake: “Hakika, Mimi ni Allah, na hakuna mungu isipokuwa Mimi. Katika viumbe Wangu wote Muhammad ni mpendwa Wangu. Nimemsaidia kupitia kwa waziri wake, Ali.”

(4) Wakati nilipofika Peponi, niliona maandishi kwenye lango lake: “Hakuna mungu, ila Mimi. Katika viumbe Wangu wote Muhammad ndiye mpendwa Wangu. Nimemsaidia kupitia kwa waziri wake, Ali.”

Imam Tha’labi katika Tafsir Kashfu’l-Bayan na Sheikh Sulaiman Balkhi katika Yanabiu’l- Mawadda, sura 24, akisimulia kutoka kwa Hafidh Abu Nu’aim Ispahani, Muhammad Bin Jariri Tabari katika Tafsir na Ibn Asakir katika Ta’rikh yake, anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas na Abu Huraira kwamba aya 62 ya Sura ya Anfal:

{ﻫﻮ اﻟﱠﺬِي اﻳﺪَكَ ﺑِﻨَﺼﺮِه وﺑِﺎﻟْﻤﻮﻣﻨﻴﻦ {62

“…Yeye ndiye aliyekusaidia kwa ushindi wake na kwa waumini.” (8:62) kisha wanasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Niliona maandishi juu ya Arsh kwamba: ‘Hakuna mungu ila Allah, Mmoja, ambaye hana mshirika, na Muhammad ni mtumishi na Mtume Wangu; nimemtia nguvu kwa Ali Bin Abi Talib.”

Kisha wanasimulia hadithi nyingine za aina hii kutoka kwenye Kitab-e-Sifa na Manaqib. Chanzo cha majina ya Muhammad na Ali ni Allah Mwenyewe.

Maneno Yaliyotumiwa Na Adam Kwa Ajili Ya Kukubaliwa Kwa Toba Yake Yalikuwa Ni Majina Ya Watoharifu Watano

Vile vile Imam Tha’labi katika Tafsiir Kashfu’l-Bayan na Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabi sura ya 24, wakisimulia kutoa kwa Faqih Wasti Ibn Maghazili Shafi’i ni maelezo juu ya aya 37 ya Sura ya 2 ya Qur’ani Tukufu:

“Kisha Adam akapokea maneno kutoka kwa Mola wake, akamkubalia toba yake; hakika Yeye ndiye apokeaye toba, Mwenye kurehemu.” (2:37)

Sa’id ibn Jabir alisimulia kutoka kwa Ibn Abbas, ambaye amesema: “Mtukufu Mtume aliulizwa kuhusu maneno ambayo Nabii Adam alikuwa amejifunza na ambayo yalisababisha kukubaliwa kwa toba yake. Mtukufu Mtume akasema: “Alimuomba Allah kwa majina ya Muhammad, Ali, Fatima, Hasan na Husein. Hivyo Allah swt. aliikubali toba yake na akamsamehe.” Wahyi Na Ilham Vilitolewa Kwa Watu Wengine Mbali Na Mitume,

Hata Kwa Wanyama

Kuhusu Abu Talib kupewa wahyi na utume, hapa tena umekosea. Wahyi na Ilham vina hatua ambazo sio za kipekee kwenye cheo cha utume tu. Istilahi hizi zinaashiria kwenye uwezo wa mtu wa kuelewa moja kwa moja ilmu iliyofichwa. Ilmu hii inatolewa kwa watu maalum na halikadhalika kwa wanyama.

Je, na nyuki alikuwa mtume ambaye kwaye Allah alitumia wahyi? Aya ya Qur’ani Tukufu katika Sura ya Nahl kwa uwazi inasema:

“Na Mola wako akamteremshia wahyi nyuki kwamba tengeneza majumba katika milima na katika miti na katika yale wanayojenga.” (16:68)

Je, unafikiri kwamba Nukhabuz (au, kwa mujibu wa wafasir wengine Yukhabuz), mama yake Nabii Musa alikuwa Mtume? Katika Surat al-Qasas imeelezwa wazi kwamba alipewa amri mbili, sheria mbili za kukataza, vipande viwili vya habari na bishara njema mbili kwa njia ya Wahyi, Allah alisema:

واوﺣﻴﻨَﺎ اﻟَ ام ﻣﻮﺳ انْ ارﺿﻌﻴﻪ ۖ ﻓَﺎذَا ﺧﻔْﺖِ ﻋﻠَﻴﻪ ﻓَﺎﻟْﻘﻴﻪ ﻓ اﻟْﻴﻢ و ﺗَﺨَﺎﻓ و ﺗَﺤﺰﻧ ۖ اﻧﱠﺎ رادوه اﻟَﻴﻚِ وﺟﺎﻋﻠُﻮه {ﻣﻦ اﻟْﻤﺮﺳﻠﻴﻦ {7

“Na tulimpelekea wahyi mama yake Musa kwamba mnyonyeshe, na utakapomhofia basi mtie mtoni na usiogope wala usihuzunike, kwa hakika sisi tutamrudiasha kwako, na tutamfanya miongoni mwa mitume.” (28:7)

Mbali na ukweli huu, sio muhimu kwa mwongozo wa watu kwamba maelekezo yote na amri za Allah ziwasilishwe kwa Wahyi.

Wakati mwingine huwaongoza watu kwa sauti. Imetokea mara kwa mara na Qur’ani Tukufu inatoa ushahidi wa habari hii katika Sura ya Mariamu, anasema jinsi alivyomuongoza Mariamu:

{ﻓَﻨَﺎداﻫﺎ ﻣﻦ ﺗَﺤﺘﻬﺎ ا ﺗَﺤﺰﻧ ﻗَﺪْ ﺟﻌﻞ رﺑﻚِ ﺗَﺤﺘَﻚِ ﺳﺮِﻳﺎ {24

“Kisha (sauti) (19:24-26) ikaita kutoka chini yake: Hakika Mola wako ameweka kijito chini yako.” (19:24)

Abu Talib Aliongozwa Na Allah Kumpa Mtoto Wake Jina La Ali

Katika njia hiyo hiyo ambayo nyuki, mama yake Musa na mama yake Isa walivyoelekezwa na Allah, ingawa hakuna hata mmoja kati yao aliyekuwa mtume, Abu Talib vile vile alielekezwa kumpa mtoto wake jina.

Aidha, hakuna mtu hata mmoja ambaye amewahi kusema kwamba Abu Talib ni mtume au kwamba Wahayi uliteremshwa kwake. Sauti ya ki-ungu na ubao ndio vilikuwa na maelekezo hayo ya kumpa mtoto jina. Maulamaa wenu wenyewe wameandika kuhusu habari hii katika vitabu vyao.

Sheikh: Ni wapi maulamaa walipoelezea hili? Muombezi: Kuna vitabu vingi kama hivyo.

Ufunuo Wa Lawh (Ubao) Kwa Abu Talib

Mir Seyyid Ali Hamadani Faqih Shafi’i, katika Mawaddatu’l-Qurba yake, Mawadda ya 8, kutoka kwenye riwaya ya Abbas Bin Abdu’l-Muttalib, ambayo Sulayman Balkhi Hanafi vile vile ameinukuu katika Yanabiu’l-Mawada yake sura ya 56, na Muhamaad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika kitabu chake Kifayatu’t-Talib wanasimulia pamoja na tofauti kidogo ya maneno kwamba wakati Ali alipozaliwa mama yake Fatima Bint Asad alimpa jina la baba yake Asad.

Abu Talib hakukubaliana naye na akasema: “Ewe Fatima! Twende kwenye vilima vya Qubais, na tumuombe Allah (baadhi ya wasimuliaji wanasema kwamba, alisema twende kwenye Masjidu’l-Haram).

Huenda akatueleza jina la mtoto huyu.” Ilikuwa usiku wakati walipowasili kwenye vilima vya Abu Qubais (au Masjidu’l-Haram) na wakaanza maombi yao. Abu Talib aliomba: “Ewe Muumba wa usiku huu wa giza na mwezi unaong’ara, tufahamishe tujue utashi Wako kuhusiana na jina la mtoto huyu?”

Katika wakati huo sauti ilisikika kutoka angani. Wakati Abu Talib aliponyanyua kichwa chake aliona ubao kama kito cha kijani, wenye misitari mine iliyoandikwa juu yake.

Aliuchukuwa ule ubao akaukumbatia kifuani kwake. Wakati alipousoma aliona maneno haya: “Nimewapa heshima maalum juu yenu nyote kwa kuwapeni mtoto twahir, maarufu. Amepewa jina la Ali kutoka upande wa Allah. Linatokana na ‘Aliy’ (Aliyetukuka).”

Ganji Shafi’i anaandika katika Kifayatu’t-Talib kwamba sauti ilikuja katika kujibu ushairi wa Abu Talib akisoma beti hizi mbili: “Enyi watu wa nyumba tukufu ya Mtume! nimewatukuza ninyi kwa kuwapa mtoto aliye twahara. Hakika, ameitwa Ali kutoka upande wa Allah swt. Jina hili linatokana na jina la Allah Mwenyewe la Al-Aliiyu.”

Abu Talib alifurahishwa mno na akaporomoka chini na akamsujudia Allah swt. Kama ishara ya shukurani kwa ajili ya tukio hili kubwa, alitoa dhabihu ngamia kumi. Alitundika ule ubao ndani ya Masjidu’l-Haram.

Bani Hashim walikuwa wakijifaharisha na ubao huo mbele za Makureishi. Ubao huo ulibakia umening’inia pale mpaka ulipotoweka wakati wa vita kati ya Abdullah Ibn Zubair na Hajjaj.

Riwaya hii vile vile inaunga mkono hadithi iliyotajwa huko nyuma ambayo inasema kwamba kuanzia mwanzoni hasa Abu Talib alikuwa ni muumin.

Alimuomba Allah kumtajia jina la mtoto. Alipoona neema ya ukarimu wa Allah, aliporomoka chini katika hali ya kusujudu mbele Yake. Je, hii ni tabia ya kafiri?

Jina La Ali Sio Sehemu Ya Adhana Au Iqama

Umedai kwamba wanachuoni wa Shia wanasisitiza kwamba jina la Ali huchukuliwa kama wajibu katika Adhana na Iqama. Kwa kweli hakuna mwanachuoni hata mmoja aliyeeleza kwamba jina la Ali ni sehemu muhimu ya Adhana au Iqama. Katika vitabu vyote vya fiqih mafaqih wote wa Shia bila kuhitilafiana wanasema kwamba kushuhudia wilayat ya Amirru’l-Muminin sio sehemu ya Adhana au Iqama.

Kuitamka katika adhana au iqama kwa nia hiyo ni haram. Kama wakati wa kuanza kwa Swala nia ni kwamba jina la mtukufu Imam ni sehemu ya lazima ya Swala, basi utekelezaji wa swala hiyo unakuwa Batili.

Lakini bila shaka, baada ya kutaja jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ukataja na jina la Ali bila kulichukulia ulazima kwa madhumuni hayo, bali kwa ajili ya heshima na kubarakiwa inafaa. Allah amelitaja jina lake kila mahali baada ya kutaja jina la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama nilivyokwisha kutaja huko nyuma. Sasa tunakuja kwenye hoja yetu kubwa: hakuna yeyote miongoni mwa sahaba mashuhuri aliyekuwa na nasaba tukufu kama alivyokuwa Ali.

Uchamungu Wa Ali

Ama kwa uchamungu wa Ali, hakuna mwingine yeyote anayelingana naye. Wote marafiki na maadui zake wanakubali kwamba baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hakuna mwingine aliyekuwa mchamungu kama alivyokuwa Ali. Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e- Nahnu’l-Balagha na Muhammad Ibn Talha Shafi’i katika Matalibu’s-Su’ul, wanasimulia kutoka kwa Umar Ibn Abdul’l-Aziz kwamba mtukufu Imam alikuwa mbora zaidi katika uchamungu kuliko wanadamu wote.

Yeye anasema: “Hatumjui mtu yeyote katika umma baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambaye alikuwa mtiifu zaidi na mchamungu kuliko Ali Bin Abi Talib.” Mullah Ali Qushachi, pamoja na chuki yake kubwa, anaandika kwamba wanadamu hawawezi kutambua fadhila za Ali. Katika kitabu chake Sharh-e-Tajrid anasema: “Watu wanashangazwa wanaposikia matendo ya maisha ya Ali.”

Riwaya Ya Abdullah Bin Rafi’i

Abdullah Ibn Rafi’i anasema kwamba katika mwisho wa siku ya funga, alikwenda kwa Amiru’l-Mu’minin. Aliona kwamba mfuko uliofungwa kwa lakiri uliletwa kwake. Wakati Ali alipoufungua, ulionekana kuwa unga ambao haukuchekechwa. Imam alichota mafumba matatu ya unga, akayala, akanywa maji kidogo, na akatoa shukurani kwa Allah. Abdullah Bin Rafi’i akasema: “Ewe Abu’l-Hasan! Kwanini umeufunga kwa lakiri mdomo huo wa mfuko?” Imam akajibu: “Ni kwa sababu watoto wangu ambao wananipenda sana wasije wakachanganya mafuta ya zeituni au sukari pamoja na unga huu, ambao utafanya nafsi ya Ali kuonja utamu wake.”

Hivyo alikuwa na tabia ya kujiweka mbali na vyakula vitamu ili asije akalainishwa navyo. Sulaiman Balkhi Hanafi vile vile ameitaja hadithi hii katika Yanibiu’l-Mawadda, sura ya 51, kutoka kwa Ahnaf Bin Qais.

Riwaya Ya Suwaid Bin Ghafla

Aidha,Sheikh katika Yanabiu’l-Mawadda, Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalabu’s-Su’ul, Khatib Khawarizmi katika Manqib, na Tabari katika Ta’rikh yake wamesimulia kutoka kwa Suwaid Bin Ghafla kwamba alisema: “Siku moja nilipa bahati ya kumtembelea Amiru’l-Mu’minin.

Niliona mbele yake kikombe cha maziwa ambayo yalikuwa chachu mno kiasi kwamba niliweza kusikia harufu yake. Imam alikuwa na mkate mkavu katika mkono wake. Ulikuwa mkavu sana kiasi kwamba haikuwezakana kuuvunja. Imam aliuvunja kwa kuuweka chini ya goti lake na baada ya kuulainisha katika maziwa yale chachu, aliula.

Alinikaribisha na mimi nile pamoja naye. Nilimuambia kwamba nimefunga. Imam akasema: “Nimesikia kutoka kwa swahiba yangu, Mtume wa Allah, kwamba kama mtu amefunga na anapenda chakula fulani, lakini hakili kwa ajili ya Allah, basi Allah atampa vyakula vya kimbinguni.” Suwaid aliendelea: “Nilipoona hali ya Ali, nilishangazwa sana. Nilimuuliza mtumishi wa Imam, Fizza, ambaye alikuwa amesimama karibu yangu, kwa nini hamuogopi Allah, yaani, kwa nini alipika ule mkate wa shayiri bila kuondoa mapumba.

Fizza alisema kwa kuapa kwamba Ali mwenyewe alimuagiza kwamba asiondoe mapumba. Imam akaniuliza nilichokuwa nazungumza na Fizza. Nilimuambia kwamba nilikuwa nikimuuliza ni kwa nini hakuuchekecha huounga. Ali akasema: ‘Baba yangu na mama yangu watolewe kafara kwa ajili ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)! Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kamwe hakuwahi kuondoa mapumba; kamwe hajazima njaa yake kwa mkate wa ngano kwa muda wa siku tatu mfulilizo. Mimi ninafuata mwenendo wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.),’”

Ali Alijizuia Kula Halwa

Muwaffaq Bin Ahmad Khawarizmi na Ibn Maghazili Faqih Shafi’i wanaandika katika Manaqib zao kwamba siku moja wakati wa ukhalifa wa Ali, kiasi fulani cha halwa (aina ya chakula kitamu) kililetwa mbele yake. Alichukua kidogo akakinusa, na akasema: “Kuvutia kulikoje na harufu nzuri iliyoje!

Lakini Ali hajui ladha yake. Kamwe sijawahi kula halwa.” Msimuliaji akasema kumuambia: “Ewe Ali! Je, kwani halwa ni haramu kwako?” Imam akajibu: “Kile ambacho Allah amekifanya kuwa halali hakiwezi kamwe kuwa haramu. Lakini je! naweza kuridhika kulijaza tumbo langu ambapo kuna watu wenye njaa katika nchi? Je, naweza kulala, na tumbo langu likiwa limejaa wakati watu katika Hijazi yote wanakufa kwa njaa? Vipi nitaridhika mimi mwenyewe na jina langu likiwa ni Amiru’l-Mu’minin? Kwanini nisijishirikishe na watu katika ufukara na shida zao.” Vile vile Khawarizmi anasimulia kutoka kwa Abi Bin Thabit kwamba siku moja ‘faluda’ (kinwaji kitamu) kililetwa mbele ya Ali, lakini alizuia hamu yake na hakuinywa.

Hii ni baadhi ya mifano ya mwenendo wake kuhusiana na kula na kunywa. Alikula mkate mkavu wa shayiri wakati mwingine pamoja na siki au chumvi na wakati mwingine pamoja na mboga kidogo na maziwa. Kamwe kulikuwa hakuna aina mbili ya chakula katika kitambaa cha meza ya chakula.

Katika mwaka wa 40 A.H. katika usiku wa mwezi 19 Ramadhani, wakati Abdu’r-Rahman Muljim Muradi (L.A) alipomtia lile jeraha baya, yeye alikuwa mgeni nyumbani kwa bint yake,Ummu’l-Kulthum, kwa ajili ya kufuturu.

Wakati mkate, maziwa na chumvi vilipowekwa kwenye kitambaa cha chakula, Ali ambaye alikuwa na mapenzi makubwa na bint yake Ummu’l-Kulthum, kwa hasira akasema: “Sijaona msichana kuwa katili hivi kwa baba yake.” Ummu’l-Kulthum akasema: “Baba! Nimefanya kosa gani?” Ali akasema: “Ulisha wahi kumuona baba yako akiwa na vyakula vya aina mbili katika kitambaa chake cha chakula?”

Kisha aliamuru kwamba maziwa yaondolewe. Hata hivyo, alikula vipande vichache vya mkate na chumvi na kisha akasema: “Itatubidi kuja kutoa hesabu kwa ajili ya vitu vyote vya halali; kuna adhabu kwa ajili ya matendo haramu.”

Mavazi Ya Ali

Mavazi ya Ali yalikuwa duni sana. Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib, Imam Ahmad Ibn Hanbal katika Musnad yake, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira, na wengine katika maulamaa wenu wameandika kwamba: “Mavazi yake yalikuwa ni nguo yenye mikwaruzo, gwanda (lisilo laini), iliyonunuliwa kwa dirham tano.”

Aliweka viraka kwenye nguo zake. Viraka vilikuwa vya ngozi au majani ya mtende, viatu vyake vile vile vilikuwa vimetengenezwa kwa majani ya mtende.

Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibu’s-Su’ul, Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l- Mawadda, na Ibn Abi’l-Hadid Mut’azali katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha wameandika kwamba Ali alikuwa na viraka vingi sana katika nguo zake kiasi kwamba wakati wa ukhalifa wake, binamu yake Abdullah Ibn Abbas aliviona na akahuzunika. Ali akasema: “Nina viraka vingi katika nguo zangu kiasi kwamba sasa namuonea haya huyo mshona viraka. Kwani Ali anahusika nini na mapambo ya kidunia? Vipi nitatosheka na starehe ambazo ni za kutoweka na neema ambayo sio ya kudumu?” Mtu mwingine alipinga jinsi Ali anavyoonekana akisema: “Kwa nini unaweka viraka kwenye nguo zako hata wakati wa ukhalifa wako na ukubwa?” Hali hii hufanya maadui wakudharau.” Ali akasema: “Hili ni aina ya vazi ambalo huzuia majivuno yetu, huondoa hisia za kiburi ndani ya mtu, na hukubaliwa na muumini.”

Muhammad Bin Talha katika Matalibu’s-Su’ul, Khawarizmi katika Manaqib yake, Ibn Athir katika kitabu chake Kamil, na Sulaiman Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda wamesimulia kwamba Ali na mtumishi wake walikuwa na nguo zinazofanana. Alinunua nguo mbili za aina moja na bei moja, moja alivaa mwenyewe na moja alimpa mtumishi wake, Qanbar.

Hizi zilikuwa ndio desturi za Ali kuhusiana na chakula na mavazi. Yeye mwenyewe alikula mkate mkavu wa shayiri na kuwapa masikini na yatima mikate iliyotengenezwa kwa ngano, sukari, asali na tende. Alivaa nguo zenye viraka yeye mwenyewe, lakini aliwapa mayatima na wajane nguo nzuri.

Mazungumzo Ya Zurar Na Mu’awiya Kuhusu Ali

Kuna mifano mingi ya Ali kuipa nyogo dunia, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha, Hafidh Abu Nu’aim Isfahani katika Hilyatu’l-Auliya, Jz. 1, uk. 84, Sheikh Abdullah Bin Amir Shabrawi Shafi’i katika Kitabu’l-I’ttihad Bil Hubbi’l-Ashraf, uk. 8; Muhammad Bin Talha katika Matalibu’s-Su’ul, uk 33; Nuru’d-din Bin Sabbagh Malik kati- ka Fusulu’l-Muhimma, uk. 128; Sheikh Sulaiman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l- Mawadda, sura 51; Sibt Bin Jauzi katika Tadhkira Khawasu’l-Umma mwishoni mwa sura ya 5, na wengine wengi katika maulamaa na wanahistoria wenu maarufu wameandika kwa urefu mazungumzo kati ya Mu’awiya na Zurar Bin Zumra.

Mwishoni mwa mazungumzo yake na Mu’awiya, Zurar alimtukuza Ali katika maneno haya: “Katika nyakati fulani nimemuona Ali wakati wa usiku, nyota zikiwa zimezagaa mbinguni, akiwa ameshika ndevu zake na kutapatapa kama mtu aliyeumwa na nyoka, akilia kama vile yuko kwenye maumivu makali, akisema: ‘Ewe dunia! Mdanganye mwingine badala yangu mimi.

Je, unanikumbatia mikononi mwako na una mapenzi makubwa na mimi? Hili haliwezekani. Nimekupa talaka tatu, ambazo kwazo baada yake kuungana tena ni muhali. Muda wako ni mfupi, hofu unayoleta ni kubwa, na starehe yako ni yenye kufedhehesha sana.

Allah atuokoe na uhaba wa njia za kusafiria, umbali wa mashukio, na hatari za njiani!’ Kisha Mu’awiya akaanza kulia na kusema: ‘Allah amhurumie Abu’l-Hasan. Wallahi alikuwa kama hivyo.’ Vile vile alisema: ‘Wanawake hawana uwezo wa kuzaa mtu kama Ali Bin Abi Talib.’”

Utambuzi Wa Mtume Juu Ya Uchamungu Wa Ali

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alitambua uchamungu wa dhahiri wa Ali, Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayayu’t-Talib, sura ya 46, anasimulia kutoka kwa Ammar Yasir, ambaye alisema kwamba alisikia kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba alimwambia: “Hakika Allah amekupa wewe pambo ambalo mfano wake hakumpa yeyote yule ambaye Alimpenda. Na (pambo) hilo ni uchamungu wako katika ulimwengu huu.

Amekufanya hivyo kiasi kwamba hunufaiki kutokana na ulimwengu huu, wala hauwezi kukufanya wewe kuuelekea. Amejaalia juu yako wewe upendo kwa masikini na mafukara. Hivyo walifurahishwa na Uimam wako na mimi vile vile nimefurahishwa nao kwa sababu ya kukufuata wewe. Aliyebarikiwa ni yule anayefanya urafki na wewe na kukukubali; na laana iwe kwa yule ambaye ni adui kwako. Wale wanaokupenda na kukubali wewe watakuwa majirani zako katika Pepo na maswahiba wako katika kasir yako. Wale ambao walikuwa wakikupinga wewe watahesabiwa kama waongo na Allah Siku ya Hukumu wapewa adhabu yao inastahili.”

Allah Na Mtukufu Mtume Walimuita Ali ‘Imamu’l-Muttaqin’

(Kiongozi Wa Wachamungu)

Alifikia hatua ya hali ya juu ya uchamungu kiasi kwamba marafiki na maudui wanamuita Imam’l-Muttaqin (kiongozi wa wachamungu). Kwa hakika mtu wa kwanza kumuita kwa sifa hii ni Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe. Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha, Jz. 2, uk. 450; Hafidh Abu Nua’aim Ispahani katika Hilyatu’l-Auliya; Mir Seyyid Ali Hamadani katika Mawaddatu’l-Qurba na Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib, sura ya 54, wanasimulia kutoka kwa Anas Bin Malik kwamba siku moja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia amletee maji kwa ajili ya kuchukulia wudhu.

Wakati alipoleta maji Mtumkufu Mtume alichukuwa wudhu na kisha akasali Sala ya rakaa mbili. kisha akasema: “Ewe Anas! Mtu atakayefuatia kuingia mlango huu ni mkuu wa wachamungu, kiongozi wa Waislamu, mtawala wa waumini, na mwisho wa mawasii (warithi) ambaye atawaongoza watu wenye nyuso na mikono angavu mpaka Peponi.”

Anas anasema: “Nilimuomba Allah moyoni mwangu mwenyewe kwamba aweze kumleta Ansar (mtu wa Madina) mmoja kwenye mlango huo, lakini nililifanya ombi langu kuwa siri. Ghafla, nilimuona Ali akiingia mlangoni. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akauliza huyo alikuwa ni nani. Nikajibu kwamba alikuwa ni Ali Bin Abi Talib. Kisha Mtufufu Mtume kwa furaha akaamka kumuamkia Ali.

Alimkumbatia kwenye mikono yake na kumfuta jasho katika uso wake. Ali akasema, ‘Ewe Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)! Unanifanyia mimi leo kiasi ambacho hujanifanyia kabla!’ Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: ‘Kwa nini nisifanye hivyo wakati ambapo wewe utawasilisha utume wangu kwa umma, utafanya wasikie sauti yangu, na utawaelezea yale mambo ambayo kwayo wamehitalifiana kimaoni.’”

Vile vile Ibn Abi’l-Hadid katika Shahr-e-Nanju’l-Balagha, Jz. 2, na Hafidh Abu Nu’aim katika Hilyatu’l- Auliya wanaandika kwamba siku moja Ali alikuja kwa Mtume. Mtume akamuambia: “Karibu, kiongozi wa Waislamu na Mkuu wa wachamungu.” Ali akasema: “Namtukuza Allah kwa neema ambayo ameiweka juu yangu, na naomba ukarimu Wake kwangu.” Muhammad Bin Talha Shafi’i vile vile anasimulia hadithi hii mwishoni mwa juzu ya 4, sehemu ya 1, ya Matalibu’s-Su’ul na kwayo inathibitisha kwamba Ali alikuwa Imam wa wachamungu wote.

Hakim, katika Mustadrak, sehemu ya 3, uk. 38 na Bukhari na Muslim, kila mmoja katika Sahih yake, wanasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Allah amenitumia wahyi kuhusu Ali unaohusiana na mambo matatu: (1) ni maula na mkuu wa Waislamu; (2) ni mkuu wa wachamungu; na (3) ni kiongozi ambaye atawaongoza watu wenye nyuso na mikono angavu (kwenda Peponi).”

Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i anasimulia katika Kifayatu’l-Talib sura ya 45, kutoka kwa Abdullah Bin Asad bi Zurara kwamba Mtume alisema: “Katika usiku wa Miraji, wakati nilipochukuliwa kwenda mbinguni, niliruhusiwa kuingia kasir ya lulu, ambayo sakafu yake ni ya dhahabu inayomeremereta.

Kisha wahyi ulitumwa kwangu, na nilielezwa vitu vitatu kuhusu Ali: (1) kwamba kwa hakika yeye ni maula na mkuu wa Waislamu; (2) kwamba yeye ni Imam na mkuu wa wachamungu; na (3) kwamba yeye ni kiongozi ambaye atawaongoza watu wenye nyuso na mikono angavu (kwenda Peponi).”

Imam Ahmad Bin Hanbal anaandika katika Musnad yake kwamba siku moja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali hivi: “Ewe Ali! Kuutazama uso wako ni ibada; hakika wewe ni mkuu wa wachamungu na kiongozi wa waumini. Yule aliye rafiki yako ni rafiki yangu, na aliye rafiki yangu kwa hakika ni rafiki wa Allah. Yeye ambaye ana nia mbaya dhidi yako ana nia mbaya dhidi yangu, na yule ambaye ana nia mbaya dhidi yangu hakika ana nia mbaya dhidi ya Allah.”

Hivyo inatosha kwa cheo kitukufu cha Ali kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisisitiza kwamba Ali anawapita masahaba katika uchamungu. Yeye peke yake ndiye aliyekuwa amepewa cheo cha ‘Imam’l- Muttaqin,’ na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mara kwa mara alimtaja kama hivyo.

Kamwe Imam’l-Muttaqin Ali Hakuwa Na Mapenzi Ya Kujiingiza Kwenye

Anasa Au Mamlaka

Sheikh: Mtu hawezi kusema sana katika kumtukuza Ali, bila shaka Mu’awiya alisema kitu sahihi: wanawake wa ulimwenguni hawana uwezo wa kuzaa mtu kama Ali.

Muombezi: Sasa ni wazi kwamba miongoni mwa masahaba wenye kuheshimika Ali alikuwa mkuu wa wachamungu. Kuna wazo limenijia sasa hivi. Kama mtaniruhusu nitawaomba kitu kimoja.

Sheikh: Ndio tafadhali fanya hivyo.

Muombezi: Baada ya kukiri kwamba miongoni mwa masahaba maarufu Ali alikuwa na hadhi ya kipekee ya kuwa mkuu wa wachamungu, je, utaweza kufikiria kwamba alikuwa na mwelekeo wowote wa kujiingiza kwenye anasa au mamlaka?

Sheikh: Haiwezekani kufikiria kitu kama hicho kuhusu yeye. Umeonesha jambo linalojulikana sana kwamba Ali aliipa dunia talaka tatu. Tukiwa tumethibitisha kujitenga kwake na dunia vipi ataiinamia. Mbali na hili, cheo chake ni kitukufu mno kiasi kwamba haiwezekani kuhusisha ndani yake dhana ya uwongo kama hiyo kwake.

Muombezi: Hivyo ina maana kwamba matendo yote ya mtu mfano wa uchamungu kama huyo yalikuwa ni kwa ajili ya Allah. Kamwe hakugeuka hata inchi moja kutoka kwenye ile njia ya haki.

Sheikh: Ni dhahiri kwamba sisi hatukatai mambo haya kuhusu Ali.

Kukataa Kwa Ali Kutoa Kiapo Cha Utii Kwa Abu Bakr Kunathibitisha Mbinu Ya Kuchaguliwa Kwake Kama Khalifa Haikuwa Sahihi

Muombezi: Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipofariki, kwa mujibu wa wosia wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali alifanya taratibu zote za mazishi. Baadhi ya watu, wakiwa wamekutana huko Saqifa-e- bani Sa’ida, walikula kiapo cha utii kwa Abu Bakr.

Baadae, wakati Ali alipoitwa, kwanini alikataa kula kiapo cha utii?

Kama namna ambayo kwamba Abu Bakr alichaguliwa kuwa Khalifa ilikuwa sahihi na suala la Ijma lilithibitika kuwa la haki, basi Ali, akiwa mchamungu kiasi kikubwa mno asingepotoka kutoka kwenye haki.

Utakumbuka hadithi ambayo niliitaja katika mikesha iliyopita, ambayo kwayo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali.”

Kama mkutano kule Saqifa ulikuwa umetegemezwa juu ya uadilifu na uchaguzi wa Abu Bakr kama Khalifa ulikuwa halali, Imam (Ali) angewakaribisha na kumkubali Abu Bakr kama Khalifa wa haki. Lakini kwa kweli alipinga uchaguzi ule kwa nguvu zote.

Upinzani wa Ali lazima utakuwa uliegemea juu ya moja ya mambo mawili. Amma Ali alikuwa anakwenda kinyume na njia ya haki, na alivunja amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), au alichukulia hiyo Ijma kuwa ni kichekesho.

Amma kwa uwezekano huu wa kwanza, hiyo haiwezekani kufikiria kwamba Ali angeweza kuikataa haki. Kwa mujibu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) “Ali yuko pamoja na haki na haki iko pamoja na Ali.” Aidha, hakuna hata mtu mmoja ambaye amewahi kudai kwamba yeye (Ali) alikuwa anapenda mamlaka ya kidunia. Aliupa ulimwengu talaka tatu. Hakuwa na haja ya kupata umaarufu wa kisiasa. Ilikuwa ni ile hali ya pili ambayo ilimchochea yeye kukataa kuukubali ukhalifa wa Abu Bakr. Alijua unapingana na utashi wa Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Sheikh: Ni ajabu kwako wewe kusema kwamba Ali hakula kiapo cha utii kwa Abu Bakr. Rejea katika vitabu vyenu na vyetu vya historia vithibitisha kwamba Ali alikula kiapo cha utii kwa Khalifa Abu Bakr na hakupinga Ijma.

Muombezi: Je, umesahau mijadala yetu yote iliyopita ambayo kwayo nilitoa maelezo kamili ya kauli za maulamaa wenu mashuhuri? Hata Bukhari na Muslim wameandika kila mmoja kwenye Sahih yake kwamba Ali hakutoa kiapo cha utii katika wakati ule.

Maulamaa wenu kwa ujumla wamekiri kwamba katika siku ya kwanza, wakati mtukufu Imam alipoburuzwa kwa nguvu na kwa matusi kutoka nyumbani kwake kwenda msikitini (kama ilivyoelezwa mapema) yeye hakutoa kiapo bali alirudi nyumbani. Ibrahim Bin Sa’d Saqafi (kafa 283 A.H.), Ibn Abi’l- Hadid, Tabari na wengine wameandika kwamba Ali alitoa kiapo cha utii baada ya miezi sita (yaani, baada ya kifo cha Fatima). Hata kama tukubali, kwa njia ya kukisia, kwamba Imam alitoa kiapo cha utii, kwa nini alingojea mpaka baada ya miezi sita kabla ya kufanya hivyo?

Sheikh: Kwa hakika lazima kulikuwa na sababu fulani kwa hilo. Yeye peke yake ndiye alilijua hilo. Lakini kwa nini tuwe na wasi wasi kuhusu kutoafikiana kwa wakubwa zetu? Kwa nini tudasisasi tofauti zao baada ya miaka 1300? (kicheko kikubwa kutoka kwa wasikilizaji).

Muombezi: Wakati unapokuwa huwezi kupata jibu kuthibitisha hoja yako, unategemea juu ya jibu kama hilo. Lakini mbele za watu wapenda haki suala hilo liko wazi mno kuhitaji ufafanuzi wowote au uthibitisho.

Amma kwa maelezo yako kwamba hatuhitaji kuingilia katika tofauti za watangulizi wetu, bila shaka uko sawa, kwa kadiri kwamba mambo yao sio mzigo juu yetu. Lakini katika suala lililopo sasa umekosea kwa sababu ni wajibu wa kila Mwislamu mwadilifu kuwa na imani iliyoegemea juu ya mantiki, sio kwa kufuata kibubusa bila kuelewa. Kwa kufanya utafiti kuhusiana na dini, tunasoma historia inayofahamika ya Waislamu.

Tunaona kwamba baada ya kufariki Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) madhehebu mbili zilijitokeza. Kwa hiyo, tunapaswa kufanya utafiti wa kina ili tujue ni madhehbu ipi ambayo imeongozwa kwa sawa sawa. Ni dhahiri hatupaswi kuwafuata kibubusa watangulizi wetu bila kuelewa.

Sheikh: Hakika hoja yako ni kwamba ukhalifa wa Abu Bakr haukuwa wa haki.

Lakini kama Abu Bakr hakuwa ndiye Khalifa wa haki, na kama ilikuwa ni haki ya Ali kuijaza nafasi hiyo, kwa nini asitumie nguvu zake na ujasiri maalumu kusimamisha haki? Alikuwa akihudhuria katika Sala vile vile, na mara kwa mara alikuwa akitoa ushauri wa kufaa kwa makhalifa mashuhuri katika masuala muhimu. Ukimya Wa Mitume Watukufu

Muombezi: Kwanza, Mitume na warithi wao walitenda kwa mujibu wa utashi wa Allah. Kwa hiyo, hatuwezi kuleta pingamizi lolote la kwa nini hawakupigana vita, au kwa nini walitwaa kunyamaza kimya mbele ya adui, au kwa nini walishindwa.

Kama utachunguza taarifa za kihistoria kuhusiana na maisha ya mitume watukufu na warithi wao, utaona mifano mingi kama hii ya kunyamaza kimya. Qur’ani Tukufu imesimulia baadhi ya matukio hayo.

Katika Surat al-Qamar, Qur’ani Tukufu inasimulia kile alichosema Nabii Nuh pale watu wake walipompuuza:

{ﻓَﺪَﻋﺎ رﺑﻪ اﻧّ ﻣﻐْﻠُﻮب ﻓَﺎﻧْﺘَﺼﺮ {10

“…Kwa hakika nimeshindwa, kwa hiyo nisaidie.” (54:10)

Katika Surat Mariam, Qur’ani inatusimulia ukimya wa Nabii Ibrahim wakati alipotaka msaada kutoka kwa ami yake Azar na akapokea jibu la kuvunja moyo:

{واﻋﺘَﺰِﻟُﻢ وﻣﺎ ﺗَﺪْﻋﻮنَ ﻣﻦ دونِ اﻟﻪ{48

“Na mimi najitenga nanyi na mnayoyaabudu kinyume cha Allah…”(19:48)

Hivyo kama vile ambavyo Nabii Ibrahim alivyojitenga kutoka kwa watu wakati alipokosa msaada kutoka kwa ami yake Azar, Ali vile vile lazima atakuwa alijitoa kwa watu na akajitenga nao.

Sheikh: Nafikiri kujitenga huku kunaonesha kujitoa kwa moyo. Yaani, alijitoa na akakaa mbali nao lakini hakuchukua kujitenga kwa kimwili.

Muombezi: Kama utachunguza maelezo ya wafasiri wa madhehebu zote, utaona kwamba kujitoa kwake huku kutoka kwa watu kulikuwa ni kwa kimwili, sio tu kwa kisaikolojia. Nakumbuka kwamba Imam Fakhru’d-din Razi anasema katika tafsiri yake Tafsir-e-Kabir, jalada la 5, uk. 809: “Kujitenga kutokana na kitu maana yake ni kukaa mbali nacho.

Alichomaanisha Ibrahim ilikuwa kwamba alitaka kukaa mbali nao, kimwili na kwa msimamo wa kidini.” Taarikh zinasimulia kwamba baada ya kukataa huku Ibrahim alihama kutoka Babylon kwenda Kuhistan iliyoko Fars (Iran ya sasa) na akaishi maisha ya kujitenga katika mazingira yale ya milima kwa muda wa miaka saba. Kisha baadae akarudi Babylon na tena akatangaza hadharani ujunbe wa Allah na akavunja masanamu ya watu.

Katika hili watu wakamtupa kwenye moto. Allah akaufanya moto kuwa baridi na salama kwa ajili yake, na hivyo utume wake ukasimama imara. Katika Surat al-Qasas, kisa kinachohusu Mtume Musa kukimbia kwa kuhofia maisha yake kimesimuliwa katika njia hii:

{ﻓَﺨَﺮج ﻣﻨْﻬﺎ ﺧَﺎﺋﻔًﺎ ﻳﺘَﺮﻗﱠﺐ ۖ ﻗَﺎل ربِ ﻧَﺠِﻨ ﻣﻦ اﻟْﻘَﻮم اﻟﻈﱠﺎﻟﻤﻴﻦ {21

“Basi (Musa) akatoka akiogopa, akiangilia huku na huku, akasema: Mola wangu! niokoe katika watu madhalimu.” (28:21)

Katika Surat al-A’raf, Qur’ani Tukufu inatuelezea masaibu ya Harun wakati Musa alipomucha katika uongozi wa Bani Israil. Punde watu wakaanza kuabudu ndama wa dhahabu, kwa sababu Harun hakuwa na mtu wa kumsaida, aliamua kunyamaza kimya. Qur’ani inasema:

{ﻗَﺎل اﺑﻦ ام انﱠ اﻟْﻘَﻮم اﺳﺘَﻀﻌﻔُﻮﻧ وﻛﺎدوا ﻳﻘْﺘُﻠُﻮﻧَﻨ{150

“…Na akakamata kichwa cha nduguye akamvuta kwake akasema: Ewe mwana wa mama yangu! Hakika (watu) hawa wamenidharau, na hata walikaribia kuniuwa…” (7:150)

Hali Ya Ali Inafanana Na Ya Harun

Hivyo, kwa mujibu wa Qur’ani Tukufu Harun hakuchomoa upanga dhidi ya watu. Alijichukulia njia ya ukimya wakati wao walipofuata ndama wa dhahabu wa Samiri kama kitu cha kuabudu kwa sababu yeye (Harun) alitambua kwamba alikuwa amezidiwa kwa wingi wao.

Halikadhalika, Ali, ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimtangaza kuwa ana cheo sawa na Harun (kama tulivyoeleza kwa urefu huko nyuma), vile vile alikuwa sawa sawa kabisa katika kuchukua njia ya kunyamaza kimya na uvumilivu wakati alipoachwa peke yake.

Mtukufu Imam aliletwa msikitini kwa nguvu na upanga wa wazi uliwekwa kichwani mwake ili kumlazimisha kula kiapo cha utii. Baadae alikwenda kwenye kaburi la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akayarudia maneno yale yale ambayo Allah ameyasimulia kwa ulimi wa Harun.

Harun alisema kumuambia Musa: “…Hakika (watu) hawa wamenidharau, na hata walikaribia kuniuwa…”

Kunyamaza Kwa Mitume

Mfano wa Mtume Muhammad kuhusiana na nukta hii kwa hakika zaidi ni mwongozo. Lazima tufikirie ni kwa nini alikaa kimya kwa muda wa miaka kumi na tatu mbele ya harakati mbaya za maadui huko Makka mpaka mwishowe akalazimika kuuacha mji wake wa nyumbani wakati wa giza la usiku. Sababu ilikuwa ni kwamba alikuwa hana wasaidizi.Kwa kweli, hata wakati wa mamlaka yake, hakuweza kuachana na baadhi ya mambo yaliyozushwa.

Sheikh: Inakuwaje wewe unasema Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alishindwa kuangamiza mambo ya uzushi?

Mtukufu Mtume Hakuweza Kufanya Mabadiliko Makali Kwa Kuhofia Watu

Muombezi: Imesimuliwa na Hamidi katika Jam’i bainu’s-Sahihain na Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad kutoka kwa Ummu’l-Mu’minin Aisha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwambia: “Lau kama watu hawa wasingekuwa karibu na zama za ukafiri na ujinga, na kama nisingeogopa kwamba ingeharibu imani zao, ningeamuru Nyumba ya Ka’ba ibomolewe na chochote kilichokuwa kimechukuliwa kutoka humo kirudishwe.

Baada nikiwa nimeisawazisha, ningelisimamisha milango miwili kuelekea upande wake mashariki na magharibi kama ilivyokuwa wakati wa Nabii Ibrahim, na ningeijenga tena juu ya misingi iliyowekwa na Ibrahim.”

Bila shaka kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alikuwa hakuweza kupinga mageuzi makubwa yaliyokwisha kuanzishwa, Ali alikuwa na haki ya kutekeleza kanuni hiyo hiyo wakati alipokabiliana na changamoto kama hiyo. Faqihi mkubwa, Wasti Ibn Maghazili Shafi’i, na Khatib Khawarizmi wanasimulia katika Manaqib zao kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali: “Umma una kinyongo kikubwa dhidi yako.

Punde tu baada ya kifo changu watakulaghai na kufichua kile walichokuwa nacho katika nyoyo zao. Nakuagiza kuwa mvumilivu na ujizuiye mwenyewe kwa wakati huo ili kwam- ba Allah aweze kukupa malipo yake na fidia nzuri.

Baada Ya Kifo Cha Mtukufu Mtume Uvumilivu Wa Ali Ulikuwa Ni Kwa

Ajili Ya Allah

Pili, Amiru’l-Mu’minin kamwe hakujiangalia yeye mwenyewe bali alikuwa siku zote mwenye kumkumbuka Allah. Alikuwa amezama kabisa kwa Allah. Alijitolea yeye mwenyewe na watu wake kwenye utashi wa Allah. Kwa hiyo, subira na uvumilivu wake katika kupata haki yake ilikuwa kwa ajili ya Allah ili kwamba kusije kukawepo na kutokuelewana miongoni mwa Waislamu, na kwamba watu wasije wakarudia kwenye ukafiri wao wa zamani.

Wakati Fatima aliponyang’anywa mali yake, alirudi nyumbani akiwa amehuzunika na kuvunjika moyo. Alimuambia Ali: “Umerudi nyuma kama kilengwa. Umejitenga na ulimwengu kama mtu aliye shutumiwa na umevunja mbawa zako zifananazo na mwewe. Sasa mbawa hizo dhaifu za ndege hazikusaidii wewe.

Huyu Ibn Qahafa (Abu Bakr) ananinyang’anya kwa nguvu zawadi ya baba yangu na uwezo wa kujikimu wa watoto wangu. Kwa hakika watu hawa wamenitukana kwa nia mbaya ya wazi na kunikaripia.” Alizungumza kwa muda mrefu.

Mtukufu Imam alimsikiliza Fatima mpaka aliponyamaza. Kisha akampa jibu fupi ambalo lilimridhisha. Alisema: “Ewe Fatima! Katika suala la dini na kulingania haki, kamwe mimi sijawa mnyonge. Je, unataka kwamba hii dini takatifu ibakie imara na kwamba jina la baba yako mtukufu liwa linatajwa msikitini (katika adhana) hadi milele na miliele?” Akasema: “Ndio. Hiyo ndio hamu yangu kubwa.”

Ali akasema: “Basi lazima uwe na subira. Baba yako amenipa maelekezo kuhusu hali hii, na najua kwamba lazima niwe mvumilivu. Vinginevyo, ninazo nguvu kiasi kwamba naweza kumshinda adui na kuirudisha haki yako kutoka kwao. Lakini lazima uelewe kwamba katika hali hiyo dini itaharibika. Hivyo, kwa ajili ya Allah na kwa ajili ya usalama wa dini ya Allah, kuwa mvumilivu. Malipo ya akhera kwa ajili yako ni bora kuliko haki ambayo imeporwa.”

Ni kwa aliji hii kwamba Amiru’l-Mu’minin aliifanya subira kuwa ni tabia yake. Alitwaa uvumilivu na kukaa kimya kwa ajili ya usalama wa Uislmu. Katika khutba zake nyingi amelirejea suala hili.

Maelezo Ya Ali Juu Ya Kufaa Kwa Kimya Chake Baada Ya Kifo Cha

Mtukufu Mtume

Ibrahim Bin Muhammad Saqafi, ambaye ni mmoja wa maulamaa wa kuaminika wa Sunni, Ibn Abi’l- Hadid, na Ali Ibn Muhammad Hamadani wanasimulia kwamba Talha na Zubair walivunja kiapo chao na wakaenda Basra, Ali aliamuru watu kukusanyika msikitini. Kisha baada ya kumshukuru Allah swt., alisema: “Baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tulisema kwamba sisi ni Ahlu’l-Bayti, warithi wake, na watu wenye haki kupokea mirathi yake. Hakuna mtu yeyote isipokuwa sisi tu anayeweza kudai utawala baada yake.

Lakini kikundi cha wanafiki kimepora utawala wa Mtukufu Mtume wetu (s.a.w.w.) kutoka kwetu na kuuweka kwa wale ambao walikuwa ni wapinzani wetu. Wallahi, nyoyo zetu na macho yetu yalilia kwa ajili hilo. Wallahi, tulijawa na huzuni kubwa na simanzi.

Naapa kwa jina la Allah kwamba kama kusingekuwa na hofu kwamba umma wa Kiislamu utaangamia, tungeweza kuupindua ukhalifa. Walikalia kiti cha utawala mpaka wakafikia mwisho wao. Sasa Allah amerudisha ukhalifa kwangu. Na watu hawa wawili (Talha na Zubair) vile vile walikula kiapo cha utii kwangu. Sasa wameelekea Basra wakidhamiria kusababisha gha- sia miongoni mwa watu.”

Miongoni mwa wanachuoni wenu wakubwa, Ibn Abi”l-Hadid na Kalbi, wamesimulia kwamba wakati wa kutoka kwake kwenda Basra, Ali aliwahutubia watu.

Yeye alisema: “Wakati Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alipofariki, Makureishi walitushtukiza na wakatunyang’anya haki ambayo tuliistahiki zaidi kuliko yeyote yule. Hivyo niliona kwamba ni bora kuchukua subira wakati ule, kuliko kuwaacha Waislamu watetengane na damu yao kumwagwa, kwani walikuwa ndio wameingia kwenye Uislamu hivi karibuni tu.”

Ukimya wa Ali na kuacha kuupa changamoto ukhalifa wa Abu Bakr na Umar hakukuwa kwa ajili kupatana nao. Ilikuwa ni kwa sababu alitaka kuepusha kusababisha mgogoro mkali miongoni mwa watu na kwa sababu alitaka kuikoa dini kutokana na kuangamia.

Hivyo, baada ya miezi sita ya ukimya na kutokubali, basi, kama ilivyoelezwa na maulamaa wenu, alitoa kiapo cha utii na akashirikiana nao. Katika barua aliyoipeleka kwa watu wa Misri kupitia kwa Malik Ashtar, yeye anaandika wazi kwamba kimya chake kilikuwa ni kwa ajili ya kuhifadhi Uislamu.

Maandishi ya asili ya barua ya Ali ambayo Ibn Abi’l-Hadid ameyaandika katika Sharh-e- Nahju’l- Balagha, jalida ya 4, uk. 164, ni kama ifuatavyo:

Barua Ya Amiru’l-Mu’minin Kwa Watu Wa Misr Kuelezea Ukimya Wake Wakati Aliponyimwa Ukhalifa

“Allah swt., alimtuma Muhammad kama shahidi wa mitume ili kuwaonya watu. Hivyo wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokufa Waislamu wakabishana wenyewe kwa wenyewe kuhusu ni nani atakayemrithi.

Naapa kwa Allah kwamba kamwe sikufikiria au kuamini, wala hakukuwa na dalili japo kidogo juu ya hilo, kwamba watu wa Arabuni wataichukua haki ya urithi kutoka kwa Ahlu’l-Bayt na kuwapa wengine baada yao.

Ilikuwa haiwaziki kwamba baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), pamoja na amri yake ya wazi, wao wangeninyima mimi haki hiyo. “Nilihuzunishwa sana kwamba watu walikimbia kuelekea kwa mtu fulani (Abu Bakr) na kula kiapo cha utii kwake. Hivyo, nilijitenga mpaka nilipoona kwamba kundi la watu walikengeuka kutoka kwenye Uislamu na kukusudia kuuangamiza.

Kisha nikahofia kwamba kama sikuusaidia Uislamu na Waislamu, Uislamu ungepatwa na uharibifu kiasi kwamba ungezidisha maumivu kwangu kuliko ilivyokuwa kwa kuporwa ukhalifa. Bila shaka nguvu za kisiasa haziwezi kudumu kwa muda mrefu. Lazima zitatoweka kama mawingu. Ilikuwa ni kwa hali kama hizi kwamba ilinilazimu kusimama, ili kwamba upagani uweze kuwa mnyonge na Uislamu kuwa imara.” Khutba Ya Amirul-Mu’minin Baada Ya Kuuawa Shahidi Kwa Muhammad

Bin Abu Bakr

Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, jalada la 2, uk. 35, anasimulia kutoka Kitabu’l-Gharat cha Ibrahim Ibn Sa’d Bin Hilal Saqafi, ambaye anasimulia kutoka kwa Abdru’r-Rahman Bin Jundab, ambaye anasimulia kutoka kwa baba yake kwamba wakati maadui walipoikalia Misr na Muhammad Bin Abu Bakr alipokuwa ameuawa, Amiru’l-Mu’minin alitoa khutba ambayo ndani yake alionesha hisia zake za uchungu dhidi ya msimamo waliouchukua Waislamu baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aliandika maelezo yake kwa watu wa Misri. Mtukufu Imam alisema: “Mtu mmoja aliniambia; ‘Ewe mwana wa Abu Talib! Uchu ulioje ulionao kwa ajili ya ukhalifa.’

Nikamuambia: ‘Wewe ni mwenye uchu zaidi kuliko mimi na uko mbali mno na kwenye nafasi hiyo. Nani mwenye uchu zaidi kati yetu? Je, ni mimi ambaye nadai haki yangu, ambayo kwamba Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wamenifanya mimi mdai mwenye haki zaidi, au ninyi, ambao Mmenizuia haki hiyo na umeweka vikwazo kati yangu na haki yangu.?’“Wote walifungwa midomo na hawakuweza kusema hata neno moja. Hakika, Allah hawasaidii watu waovu.”

Maelezo haya na khutba nyingine za Imam Ali huonesha kwamba sababu ya Imam kutokumkabili adui, bali akachukua njia ya ukimya na (kama inavyosemwa na maulamaa wenu) akatoa kiapo cha utii baada ya miezi sita, haikuwa kwamba alikubaliana nao katika uamuzi wao kuhusiana na ukhalifa. Ilikuwa ni kwa sababu alihofia kwamba

Uislamu ungetoweka na kwamba Waislamu wangegawanyika. Kama Ali angesimama kuichukuwa haki yake, bila shaka baadhi ya watu wangemuunga mkono (wengi walimuomba kufanya hivyo) na vita ya wenyewe kwa wenyewe ingeanza.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amekufa tu hivi punde. Waislamu walikuwa karibu sana na zama za ukafiri, na mizizi ya imani ilikuwa bado haijaimarika. Mayahudi, Wakirsto, waabudu masanamu, na wanafiki, ambao walikuwa maadui wakubwa, wangepata fursa ya kuharibu heshima ya Waislamu. Hatimaye Uislamu ungeanguka.

Amirul-Mu’minin aliyaelewa mambo haya. Aidha, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia kwamba msingi wa Uislamu hautaharibiwa na kwamba dini ilikuwa kama jua, ambayo inaweza kufichwa wakati mwingine kwenye mawingu ya ujinga na uadui lakini mwishowe itajitokeza ikiangaza mwanga wake kila sehemu.

Kwa ufupi, alidai haki yake kwa muda wa miezi sita na akathibitisha usahihi wa haki yake katika idadi ya mikutano na mikusanyiko, lakini hakula kiapo cha utii. Ingawa hakukim- bilia kwenye kupigana, aliendelea kudai haki yake kwa hoja na malalamiko. Khutba Ya Shaqshiqayya Vile Vile Inaelezea Ukimya Wa Ali

Mtukufu Imam alianza khutba yake ya Shaqishaqiyya kwa nukta ile ile.

“Wallahi! mwana wa Abu Qahafa (Abu Bakr) amejivisha nao (ukhalifa) ingawa kwa hakika alijua kwamba uhusiano wangu nao ulikuwa kama nafasi ya mhimili katika mashine ya kusaga, maji ya mafuriko yanatiririka kutoka kwangu, na hakuna anayeweza kufikia kiwango cha ujuzi wangu.

Nilijitenga na ukhalifa. Kisha nikaanza kutafakari iwapo niichukuwe haki yangu kwa nguvu au nivumilie giza hili kwa ukimya, ambalo kwalo aliye komaa anyongeshwa, mdogo anakua na kuwa mzee, na muumini wa kweli kwa anashughulika kwa mashaka mpaka akutanane na Allah (wakati wakufariki). Niliona kwamba subira ndio njia nzuri ya kufuata.

Hivyo, nilikuwa mvumilivu ingawa kulikuwa na muwasho kwenye macho na kusongwa kwenye koo. Nilitazama uporaji wa urithi wangu mpaka wa kwanza akaondoka. Lakini akaukabidhi ukhalifa kwa Ibn Khattab (Umar) baada yake.”

Khutba hii imejaa mihemuko mizito ya Ali. Lakini kiasi hiki kinatosha kuthibitisha nukta yetu.

Mashaka Kuhusu Khutba Ya Shaqshaqiyya

Sheikh: Kwanza kabisa khutba hii haithibitishi kutokuridhika kwa Imam. Pili, khutba hii haihusiani na Ali. Kwa kweli, ni kazi ya Seyyid Sharif Razi, ambaye aliijumuisha katika khutba za Ali. Kwa kweli Ali hana malalamiko dhidi ya makhalifa. Bali yeye alikuwa ameridhika kabisa nao.

Muombezi: Kauli yako hii imeegemea juu ya chuki ya hali ya juu kabisa. Kile ambacho Ali ameelezea na kulalamikia kimekwisha simuliwa mapema. Huzuni za Imam hazikuishia kwenye khutba hii. Tuhuma yako kwamba mtunzi wa khutba hii alikuwa ni yule mwanachuoni mashuhuri mchamungu, Seyyid Raziu’d-din, sio sahihi.

Wanachuoni wenu mashuhuri, kama Izzu’d-din Abdu’l-Hamid Ibn Abi’l-Hadid, Sheikh Muhammad Abduh, Mufti wa Misri, na Sheikh Muhammad Khizari katika Muhadhirat-e-Ta’rikhu’l- Uma’imu’l- Islamiyya, uk. 127, wametamka kwamba khutba hii ni ya Ali.

Wanachuoni wenu wenyewe wameandika sharhe juu ya khutba hii. Baadhi ya maulamaa wenu washupavu wa zama za baadae kidogo walifanya juhudi kubwa kusababisha mashaka kuhusu usahihi wake, lakini hakuna yeyote katika zaidi ya wale maulamaa mashuhuri arobaini wa Sunni na Shia, ambao wameandika sharhe juu ya Nahju’l-Balagha, aliyesema kitu cha ajabu kama hicho. Seyyid Razi

Bila shaka, mwanachuoni mchamungu mkubwa, Seyyid Raziu’d-din, angezuia kuhusisha moja ya khutba zake kwa Ali. Aidha, wataalamu katika lugha ya Kiarabu na fasihi yake ambao wamechunguza khutba za Nahju’l-Balagha wameamua kwamba, kwa mtazamo wa mtindo bora na fikra za kina, kazi hii (khutba) haiwezekani kuigwa na mtu yeyote.

Maulamaa wenu mashuhuri, kama Izza’d-di Abdu’l-Hamid Bin Abi’l-Hadid Mut’azali na Sheikh Muhammad Abduh, wamekiri kwamba uzuri na ujuzi wa kina wa khutba za Ali huthibitisha kwamba kazi hii iko chini katika ubora tu kwa maneno ya Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Ibn Abi’l-Hadid anamsimulia Musaddiq Bin Shabbib akisema kwamba mwanachuo mashuhuri Ibn Khashshab alisema: “Haiwezekani kwa Razi au kwa yeyote yule kutoa mtungo kama huu. Tumezipitia kazi za Razi; haziwezi kulinganishwa na maandiko haya na khutba hizi tukufu.”

Khutba Ya Shaqshaqiyya Iliandikwa Zamani Kabla Ya Kuzaliwa Kwa Seyyid Razi

Wakipuuza vipengele vingine vyote vya suala hili, wanachuo wengi, muhadithina, na wanahistoria (wote Shia na Sunni) wamesimulia juu ya kuwepo kwa khutba hii kabla ya kuzaliwa kwa mwanachuoni huyu mkubwa Seyyid Razi na baba yake Abu Ahmad Naqibu’t-Talibin.

Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha anaandika kwamba aliiona khutba hii katika vitabu vya Sheikh wake, Abu’l-Qasim Balkhi Imam-e-Mut’azila, ambaye aliishi katika wakati wa Muqtadir B’illah Abbasi. Ni dhahiri, Seyyid Razi alizaliwa muda mrefu baada yake.

Vile vile anaandika kwamba aliiona khutba hii katika Kitabu’l-Insaf, cha mubalighin mashuhuri, Abu Ja’far Bin Qubba, ambaye alikuwa mmoja wa wanafunzi wa Sheikh Abu’l-Qasim Balkhi na ambaye amekufa kabla ya kuzaliwa Seyyid Razi.

Vile vile Sheikh Abu Abdullah Bin Ahmad, anayejulikana sana kwa jina la Ibn Khashshab, anasimuliwa kwamba alisema: “Niliiona kutba hii katika vitabu vilivyoandikwa miaka 200 kabla Seyyid Razi hajazaliwa. Vile vile nimeiona khutba hii katika vitabu vya wanachuo wa fasihi ambao wameviandika kabla ya kuzaliwa baba yake Seyyid Razi, Ahmad Naqibu’t-Talibin.”

Amma kwa madai yako kwamba Ali alikuwa ameridhika na wapinzani wake. Haya bila shaka yanapuuza kauli zisizoidadi za kinyume chake zilizotolewa na maulamaa wenu, ambazo nimezionesha huko nyuma. Nitaonesha mfano mwingine tena bado. Ibn Abi’l- Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, jalada la 2, uk. 561, anamsimulia Ali akisema: “Nilibakia na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuanzia mwanzo mpaka kifo chake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipumua pumzi yake ya mwisho juu ya kifua changu. Alikuwa ni mimi niliyeuosha mwili wake pamoja na msaada wa malaika, niliendesha sala ya mazishi yake, na nikamzika. Hivyo, hakuna mtu yeyote aliye karibu zaidi naye, au mrithi wa haki zaidi kwake kuliko mimi.”

Kuelekea mwisho wa khutba yake anawataja wapinzani wake katika maneno haya: “Naapa kwa jina la Allah, aliye Mmoja, kwamba niko kwenye njia iliyo sahihi na kwamba hao wapinzani wangu wako kwenye njia ya upotofu.”

Lakini wewe unadai kwamba Ali aliwachukulia wapinzani wake kuwa katika njia sahihi. Natamani ungeiangalia kwa makini ile aya ya Qur’ani Tukufu inayosema:

{ﻳﺮِﻳﺪُونَ انْ ﻳﻄْﻔﯩﻮا ﻧُﻮر اﻟﻪ ﺑِﺎﻓْﻮاﻫﻬِﻢ وﻳﺎﺑ اﻟﻪ ا انْ ﻳﺘﻢ ﻧُﻮره وﻟَﻮ ﻛﺮِه اﻟْﺎﻓﺮونَ {32

“Wanataka kuzima nuru ya Allah kwa vinywa vyao, lakini Allah amekataa isipokuwa kutimiza nuru Yake, ijapokuwa makafiri wanachukia.” (9:32)

Mkutano Wa Kumi, Jumamosi Usiku 3 Sha’ban 1345 A.H

Uchambuzi Wa Elimu Ya Umar Juu Ya Sheria Za Kiislam.

Nawab: Asubuhi hii kijana wangu, Abdu’l-Aziz, ambaye ni mwanafunzi katika chuo cha Islamiyya, ametueleza kuwa mwalimu wao ameliambia darasa kuwa Khalifa Umar ibn Khattab alikuwa ndio mwanasheria mkuu wa wakati wake mjini Madina.

Alikuwa na ujuzi kamili wa aya za Qur’ani na maana zake. Alikuwa mbora zaidi ya wanasheria wote mashahuri kama Ali bin Abi Talib. Abdullah bin Mas’ud , Abdullah bin Abbas, Akrama na Zaid bin Thabit.

Hata Ali Bin Abi Talib ambaye ujuzi wake wa Fiqh, alipokabiliana na suala gumu ulikuwa mkubwa, alimtaka ushauri Umar kuhusiana na haki za Waislam. Khalifa kila mara aliyatatua matatizo magumu ya Ali. Sisi sote tunalikubali hili kwa sababu wanachuoni wetu wanasema kwamba Umar alishika nafasi kubwa isiyo kifani katika elimu na ujuzi. Ninakuomba uielezee nukta hii ili sisi sote, pamoja na mwanangu huyo, tuweze kuuelewa ukweli.

Muombezi: Ni ajabu kwamba huyo Mwalimu amesema hivyo. Hata wanachuoni wenu hawajathubutu kudai hivyo kamwe. Kama baadhi ya watu mashabiki kama Ibn Nazm Zahiri alisema hivyo, walipingwa vikali na wanachuoni wenu. Aidha sifa hii haikudaiwa na Khalifa Umar mwenyewe. Hakuna mwanachuoni hata moja wa kwenu aliyeandika jambo hili katika vitabu vyao.

Wapokezi au wanahistoria ambao wameandika chochote juu ya maisha ya Khalifa Umar Bin Khattab wamedokeza juu ya tabia yake ya ujanja, ugumu wa moyo wake na hila zake za kisiasa lakini hawakujishughulisha sana juu ya elimu yake.

Elimu Ya Umar Juu Ya Sheria Za Kiislamu Ilikuwa Dhaifu

Kwa hakika, vitabu vya madhehebu zote vimejaa mifano ambayo inaonyesha wazi kwam- ba Umar hakuwa mjuzi sana katika masuala ya elimu na fiqh. Kila alipokabiliwa na mambo kama hayo alikuwa akitaka ushauri kwa Amiru’l-Mu’minin Ali, Abdullah bin Mas’ud na Mafaqihi wengine wa Madina.

Ibn Abi’l-Hadid anataja jina la Abdullah Bin Mas’ud hasa, miongoni mwa mafaqihi wa Madina, na anasema kwamba Umar alisisitiza kwamba Abdullah wakati wote abaki naye ili kwamba wakati wowote hali ikijitokeza, ataweza kutakiwa ushauri juu ya mambo ya fiqh.

Sheikh: (Kwa hasira). Ni wapi imeandikwa kwamba Umar hakuwa mjuzi wa masuala ya dini na elimu ya fiqh?

Muombezi: Sikusema kwamba Khalifa Umar alikuwa hana ujuzi kabisa. Nilisema kwam- ba hakuwa mjuzi sana katika masuala ya fiqh na elimu. Ninaweza kuthibitisha haya ninayosema.

Sheikh: Utathibitisha vipi kwamba Khalifa Umar alikuwa na elimu dhaifu katika mambo yanayohusiana na fiqh na sheria za kidini?

Muombezi: Kuna hadithi nyingi sana katika vitabu vyenu vya Sahih. Mbali na hili, kuna kukiri kwa Umar mwenyewe ambako amekufanya mara nyingi.

Mwanamke Amnyamazisha Umar Katika Jambo La Sheria.

Jalalud-Din Suyuti kaitka Tafsir Durru’l-Mansur” Juzuu ya 11 uk. 133; Ibn Kathir katika Sherehe yake Juz. 1 uk. 468; Jarullah Zamakhshari katika Tafsir Kashshaf Juz. 1, uk. 357, Fadhil Nishapuri katika Tafsir-Gharibu’l-Qur’an Juz. 1, kuhusiana na Sura ya Nisa (Mwanamke) ya Qur’ani Tukufu, Qartabi katika Tafsir yake Juz. 5, uk. 99. Ibn Maja Qazwini katika Sunan yake Juz. 1, Asadi katika Hashiyya–e- Sunnan Juz. 1, uk. 583; Baihaqi katika Sunan Juz, 7, uk. 233, Qastalani katika Irshadu’s-Sari-Sharh-e- Sahih Bukhari Juz. 8, uk 57; Muttaqi Hindi katika Kanzu‘l-Ummal Juz. 8 uk. 298; Hakim Nishapuri katika Mustadrak Juz. 11, uk. 177; Abu Bakr Baglani katika Tamhid yake uk. 199; Ajluni katika Kashful-Khufa’ Juz. 1, uk. 270; Qadhi Shukani katika Futuhu‘l-Qadir Juz. 1, uk 407; Dhahabi katika Takhlis-e- Mustadrak, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e- Nahjul-Balagha Juz. 1 uk. 61, na Juz. 7, uk. 96; Hamid katika Jam’-e-Bainu’s-Sahihain, Faqih Wasiti Ibn Maghazili Shafi’i katika Manqib yake; Ibn Athir katika Nihaya yake, na wengineo. Kwa usahihi wamesimulia, pamoja na tofauti kidogo ya maneno kwamba siku moja Khalifa Umar, akiwa katika kuwahutubia watu alisema: “Ikiwa yeyote ataoa na akaweka kiwango cha Mahari cha zaidi ya dirham 400 kwa mkewe, nitamtwisha ile adhabu iliyoamriwa juu yake na nitakihifadhi kile kiasi kilichozidi kwenye Baitul-Mal (Hazina ya Umma)”

Mwanamke mmoja katika ile hadhara akasema kwa Sauti kubwa: “Umar! Hicho una- chokisema ndio chenye kukubalika zaidi au sheria ya Allah? Je, Allah Mwenye Nguvu hasemi: “Na ikiwa unataka kuwa na mke (mmoja) badala ya mwingine na umempa mmoja wao rundo la dhahabu, basi usichukue chochote kutokana nayo.” (4:20)

Alikwisha kuisikia aya hii na yale majibu makali ya mwanamke huyo, Umar akasema:‘Wewe unayo elimu nzuri ya fiqh na matatizo kuliko Umar, nyote nyie pamoja na hata wale wanamke wanaotawa waliokaa majumbani mwao.’”

Halafu Umar akapanda tena juu ya mimbari na akasema: “Ingawa nimewakatazeni kutoa zaidi ya dirham 400 kama mahari kwa wake zenu, sasa ninawaruhusuni kutoa kiasi chochote mnachotaka zaidi ya kiwango kilichowekwa. Hakuna ubaya ndani yake.”

Hadithi hii inaonyesha kwamba khalifa Umar hakuwa na ujuzi sana juu ya Qur’ani na fiqh. Vinginevyo asingeweza kusema jambo lisilo sahihi waziwazi namna hiyo kiasi kwamba akaweza kunyamazishwa na mwanamke asiyekuwa na elimu.

Sheikh: Hapana sivyo hivyo, ukweli ni kwamba Khalifa alitaka kuwalazimisha watu kupunguza kiwango cha mahari kulingana na Sunna. Ingawa Uislam unaruhusu tutoe kiasi kikubwa, ni vyema tukajieupusha na hilo ili masikini wasiumie. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba alisema kiasi cha mahali kisiwe kinazidi kile kiasi kilichowekwa kwa wakeze Mtukufu Mtume.

Kunyang’anya Kiasi Chochote Cha Mahari Ni Kinyume Cha Sheria

Muombezi: Hii ni namna ya kisingizio kisicho na maana ambacho hata Umar hakuwa na habari nacho. Vinginevyo angeweza kukubali kosa lake mwenyewe na asingelisema. “Ninyi ni mafakihi wazuri kuliko Umar, nyote nyie, ukijumuisha na wake wa nyumbani.” Vinginevyo pia angeliweza kusema haya unayoyasema sasa.

Mbali na hili, kila mtu anajua kwamba kitendo kilicho kinyume cha sheria hakiwezi kufumbiwa macho kama njia ya kupata matokeo mazuri na ya kisheria. Ni dhahiri ile mali ya mwanamke, ambayo ameimiliki kulingana na kanuni za Qur’ani haingeweza kwa sheria kuporwa kutoka kwake na kuwekwa kwenye Baitu’l-Mal.

Mbali na mazingatio yote hayo, si sheria kutoa adhabu igusayo kimwili kwa mtu ambaye hajatenda kosa. Angalau sijawahi kuona uamuzi wowote kama huo ukifanywa kulingana na kifungu chochote cha Sheria. Naomba unifahamishe kama unaweza kueleza mfano kama huo. Ikiwa hakuna kanuni yoyote katika hukumu za sheria, basi itakubidi ukubali kwamba hilo dai la Mwalimu huyo lilikuwa la uongo.

Umar Kukataa Kifo Cha Mtume Kunathibitisha Kwamba Alikuwa Hazijui Baadhi Ya Aya Za Qur’ani

Kwa bahati mbaya, Umar alikuwa amejenga tabia ya kuwa na hasira, na ili kuwatishia wengine alisema: “Nitakuadhibuni!”

Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake; Hamidi katika “Jam’-e-Bainu’s- Sahihain; Tabari katika Ta’rikh yake, na wanachuoni wengine wamesimulia kwamba alipokufa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Umar alimwendea Abu Bakr na kumuambia kwamba alikuwa na wasiwasi kwamba kuna uwezekano kwamba Muhammad hakufa.

Huenda amejifanya tu kuwa kafa ili aweze kuwatambua marafiki na maadui zake, au pengine ametoweka kama Musa na atarudi tena kuwaadhibu wale waliokuwa sio waaminifu na watiifu kwake.

Umar aliendelea kusema: “Hivyo kama mtu yeyote atasema kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amekufa, nitamuadhibu.” Abu Bakr alipoyasikia haya akawa naye pia hana uhakika nayo, na watu pia wakachanganyikiwa na tofauti zikazuka miongoni mwao. Wakati Ali alipolifahamu hili, alitokeza mbele ya lile kundi la watu na kusema.

“Enyi watu! kwa nini mnafanya tafarani za kijinga hivyo? Mmeisahau ile Aya tukufu, ndani yake ambamo Allah amemuambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) “Hakika wewe utakufa, na pia watu wa Umma wako.” (39:30)

Kwa hiyo, kulingana na aya hii Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ameiaga dunia hii.” Hoja hii ya Ali iliwaridhisha watu na wakaamini kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amekwishafariki kweli. Ndipo Umar akasema: “Ilikuwa ni kana kwamba nilikuwa sijawahi kuisikia aya hii.”

Ibn Athir katika Kamil na Nihaya yake, Zamakashari katika Asasu’l-Balagha, Shahrastani katika Milal wa’n-Nihal (Mugaddama IV) na wengineo wengi wa wanachuoni wenu wameandika kwamba Umar alikuwa akikemea: “Mtukfu Mtume hajafa,” wakati Abu Bakr alipomfikia na kusema: “Je Allah Mwenye Nguvu hasemi: ‘Hakika utakufa na vile vile na watu wa Umma wako.”

Pia anasema ikiwa basi atakufa au kuuawa, mtageuka nyuma juu ya visigino vyenu. (3:144) Umar kisha akawa kimya na akasema: “ Ilikuwa ni kama kwamba sijawahi kuisikia aya hii. Sasa ninaamini kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amekufa. Amri Ya Umar Ya Kuwapiga Mawe Watu Watano Na Kukatizwa Na Ali

Hamidi anasimulia katika “Jam’-e-Bainu’s-Sahihain” yake kwamba katika wakati wa Ukhalifa wa Umar, watu watano walikamatwa kwa kosa la uzinzi na kufikishwa kwa Umar. Ilithibitika kwamba watu watano hao wamefanya zinaa na mwanamke fulani.

Umar mara moja akaamuru wapigwe mawe mpaka wafe. Wakati huo Ali akaingia mle Msikitini na baada ya kuwa amesikia kile Umar alichoamuru akamuambia: “Hapa amri yako ni kinyume na sheria ya Allah.”

Umar akasema: “Ali! Zinaa imethibitika. Kifo kwa kupigwa mawe ndio adhabu iliyoag- izwa kwa dhambi hii.”

Ali akasema: “Katika suala la uzinzi, kuna hukumu tofauti katika hali tofauti, kwa hiyo katika kesi hizi zilizopo, hukumu tofauti ni lazima zitolewe.

Umar akamuomba afafanue ni hukumu gani za Allah na Mtume wake juu ya kesi hizo, kwani Umar alimsikia Mtume akisema katika nyakati tofauti: “Ali ndiye mtu mwenye elimu zaidi na hakimu bora.

Ali akaagiza wale watu watano waletwe mbele yake. Aliamuru yule mtu wa kwanza akatwe shingo. Akamuru yule wa pili apigwe mawe mpaka afe. Akaamuru yule wa tatu apigwe viboko 100.

Mtu wa nne alipigwa viboko 50. Na mtu wa tano alipata viboko 25. Umar akiwa ameshangaa na kuduwaa, akasema: “Abu’l-Hasan, vipi umeamua kesi hizi katika njia tano tofauti.”

Mtukufu Imam akasema: “Yule mtu wa kwanza alikuwa ni kafir chini ya ulinzi wa Kiislam. Amefanya zinaa na mwanamke Muislam. Kwa vile amepoteza ulinzi wa Uislam alipaswa kuuliwa.

Yule wa pili alikuwa na mke, kwa hiyo amepigwa mawe mpaka kufa. Yule mtu wa tatu alikuwa hajaoa, hivyo, amehukumiwa kupewa viboko 100. Yule mtu wa nne alikuwa mtumwa ambae anastahili adhabu nusu ya yule mtu huru, ambayo ni viboko

50. Na yule mtu wa tano alikuwa ni mwenda wazimu, hivyo alifanyiwa Ta’ziir - alipewa adhabu hafifu, ambayo ni viboko 25 (kama kumuadabisha)

Kisha Umar akasema: “Kama Ali asingekuwapo, Umar angeangamia: Ewe Abu’l-Hasan! Natumai sitakuwepo hai wakati wewe ukiwa huko miongoni mwetu.”

Umar Kuamrisha Mwanamke Mwenye Mimba Kupigwa Mawe Mpaka Afe Na

Ali Kuingilia Kati

Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib Fi Manaqib-e-Amiru’l-Mu’minin Ali Bin Abi Talib; Imam Ahmad Ibn Hanbal katika Musnad; Bukhari katika Sahih yake; Hamid katika Jam’e-Bainu’s- Sahihain; Sheikh Sulaiman Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda, sura ya 4, uk. 75, kutoka Manaqib ya Khawarizmi; Imam Fakhru’d- din Razi katika Arba’in, uk. 466; Muhibu’d-din Tabari katika Riyazu’n- Nazara, Jz. 2, uk. 196; Khatib Khawarizmi katika Manaqib, uk. 48; Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibu’s-Su’ul, uk. 113; na Imam’l-Haram katika Dhakha’iru’l-Uqba, uk. 80, anankuu riwaya ifuatayo:

Mwanamke mjamzito aliletwa mbele ya Umar Bin Khattab. Katika kuhojiwa alikiri kwamba alikuwa na hatia ya kufanya zinaa, na hivyo Khalifa akaamuru apigwe mawe. Kisha Ali akasema: “Amri yako inatekelezeka kwa mwanamke huyu, lakini huna mamlaka juu ya mtoto wake.”

Umar akamuachia yule mwanamke na akasema: “Wanawake hawana uwezo wa kuzaa mtu kama Ali. Kama Ali asingekuwa hapa, Umar angeangamia.”

Aliendelea kusema: “Allah asiniache niishi kiasi cha kukabiliana na tatizo ambapo Ali hayupo ili alitatue.”

Umar Atoa Amri Mwanamke Punguani Apigwe Mawe - Na Ali Kuingilia Kati

Imam Ahmad bin Hanbal katika Musnad yake, Imam’l-Haram Ahmad Bin Abdullah Shafi’i katika Dhakha ‘iru’l-Mawadda sura ya 2, uk. 75, kutoka kwa Hasan Basri, Ibn Hajar katika Fat’hul-Bari Juz. 12, uk 101; Abu Dawud katika Sunan yake Juz. 2, uk. 227; Munadi katika Faizu‘l-Qadir Juz. 4 uk 257; Hakim Nishapuri katika Mustadrak Juz. 2, uk. 59, Qastalani katika Irshadu’s-Sari Juz. 10, uk. 9; Baihaqi katika Sunan Juz. 8, uk. 164 Mahibu‘d-Din Tabari katika Riyazu’n-Nazar juz. 2, uk. 196; Khatib Khawarizmi katika Munaqab uk. 48; Muhammad Ibn Talha Shafi’i katika Matalibu’s-Su’ul; Imam’I-Haram katika Dhakha’irul-Uqba uk. 80; Ibn Maja katika Sunan Juz. 2, uk. 227; Bakhari katika Sahih yake mlango wa la yarjumu’l-Majnun wal-Majnuna, na wengi wa Ulamaa wenu wamesimulia tukio lifuatalo:-

Siku moja mwanamke punguani aliletwa mbele ya Khalifa Umar Bin Khattab. Alikuwa amefanya zinaa na akakubali kosa lake. Umar akaamuru apigwe mawe. Amirul-Muminin alikuwapo pale. Akamuambia Umar: “Unafanya nini wewe? Nimesikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema watu wa aina tatu wako huru kutokana na mkono wa sheria: Mtu aliye- lala mpaka atakapoamka, mwendawazimu mpaka atakapopona na akapata fahamu tena, na mtoto mpaka atakapopata umri.” Kusikia hili, Umar akamuachia huru yule mwanamke.

Ibnu’s-Saman katika Kitabu’l-Muwafiqa ameandika habari nyingi kama hizi. Kuna baadhi ya maelezo ambayo yanasimulia hukumu za Umar takriban 100 za kimakosa na uongo.

Elimu Na Sifa Za Ali

Nuru’d-Din Bin Sabbagh Malaki katika Fusulu‘l-Mahimma Sura ya 3, uk. 17 akiandika kuhusu Ali amesema: “Sura hii ina mambo yanayohusiana na elimu ya Ali. Mojawapo ya vipengele hivyo ni ile elimu ya fiqh (Sha’ria) ambayo juu yake yamesimama matendo ya halali na ya haramu ya mwanadamu.

Ali alielewa undani wa Sheria. Mas’ala yake magumu, yalikuwa ni mepesi kwake na alizielewa tafsiri zake kwa ukamilifu.

Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kuwa Ali ndiye mtu anayefaa zaidi wa Umma huu kwa kufafanua maswali ya sheria. Imam Abu Muhammad Husein ibn Mas’ud Baghawi katika Masabih yake anasimulia kutoka kwa Anas kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipowateua kila mmoja wa sahaba zake kwenye nafasi maalum, alimteua Ali kwenye cheo cha Hakimu na kusema: “Ali ni Hakimu bora miongoni mwenu wote nyie (masahaba na Umma).

Kwa kweli unapolinganisha maneno ya huyu Mwalimu wa chuo asiyefahamu na Hadithi za wanachuoni wenu wakubwa, utathibitisha kwamba dai lake halina msingi. Mwalimu huyu anadai zaidi ya alivyodai kiongozi wake.

Umar mwenyewe alikuwa daima akionye- sha udhaifu wake dhidi ya Ali. Imam Ahmad Bin Hanbali katika Musnad yake, Imam‘l-Haram Ahmad Makki Shafi’i katika Dhakha’irul-Uqba, Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda Sura ya 56, na Muhibu’d-Din, Tabari katika Riyadhu’n- Nazara, Juz. ya 2, uk. 195, wanamnukuu Mu’awiya akisema: “Kila mara Umar Bin Khattab alipokabiliwa na tatizo gumu, alitafuta msaada wa Ali.”

Abu’l-Hajaj Balawi kati- ka Alif-Ba yake Juz. 1, uk. 222 anaandika kwamba wakati Mu’awiya aliposikia habari za kuuawa Shahidi kwa Ali, alisema “Kwa kifo cha Ali, Fiqh na Elimu vimeanguka.” Vile vile ananukuu Sa’id Bin Masayyab akisema kwamba Mu’awiya alisema: “Umar daima alitafuta kimbilio kwa matatizo ambayo Ali hakuwepo kumsaidia.”

Abu Abdullah Muhammad Bin Ali al-Hakim al-Tirmidhi katika sherhe yake ya Risalat-e- Fathu’l-Mubin anaandika: “Masahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walimtaka ushauri Ali katika mambo yanayohusiana na hukumu za Qur’ani Tukufu na kukubali fatwa zake.

Umar Bin Khattab amesema katika nyakati tofauti kwamba: “ Kama Ali asingelikuwako, Umar angeangamia.” Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) pia amesema: “Mtu mwenye elimu ya juu zaidi miongoni wa Umma wangu ni Ali Bin Abi Talib.”

Yaliyosimuliwa kwenye vitabu vya Hadithi na Historia yanathibitisha kwamba Umar alikuwa amekosa sana elimu ya kawaida na ya fiqh kiasi kwamba alikosea hata kulingana na matatizo ya kawaida. Masahaba ambao walikuwa wa rika lake walimuonya kutokana na udhaifu wake.

Sheikh: Wewe huna huruma kwa kumsingizia Umar mambo kama hayo. Inawezekana kwa Khalifa kukosea katika masuala ya dini?

Muombezi: Ukali huu hautoki upande wangu. Maulamaa wenu wameonyesha ukweli kuhusu jambo hili.

Sheikh: Kama ukiweza tafadhali tujulishe mambo haya kwa vyanzo sahihi ili ukweli uweze kudhihirika wazi.

Muombezi: Kuna mifano mingi ya namna hiyo. Takriban 100 kati ya hiyo imo kwenye vitabu vyenu, lakini nitatoa mmoja kati ya hiyo kama mfano:-

Muslim Bin Hajjaj katika Sahih yake, sura aya Tayamamu; Hamidi katika Jam-e-Bainu’s –Sahihain, Imam Ahmad Hanbali katika Musnad yake Juz. 4, uk 265, 319, Baihaqi katika Sunan Juz. 1, uk. 209, Abu Dawud katika Sunan Juz. 1, uk 53, Ibn Maja katika Sunan Juz. 1 uk. 200, Imam Nisa’i katika Sunan yake Juz. 1, uk 59-61, na wengine wa Ulamaa wenu wakubwa kwa njia tofauti na maneno tofauti, wameandika kwamba wakati wa Ukhalifa wa Umar, mtu mmoja alimjia na kusema: Imekuwa ni lazima kwangu nifanye ghusl (josho la tohara) lakini hakuna maji yanayoweza kupatikana. Nitafanya nini katika hali kama hii. Umar akasema: “Mpaka upate maji ya kufanyia josho, vinginevyo usisali.”

Kwa wakati huo Ammar-e-Yasir, Sahaba wa Mtume, alikuwepo. Yeye akasema: “Ewe Umar! Umesahau kwamba katika moja ya safari ambazo wewe na mimi tulitokea kuwa tunahitaji kufanya josho.

Kwa vile maji hayakupatikana wewe hukusali, lakini nilifikiria njia ya tayammum badala ya josho ni kwamba ni budi vumbi lipakwe juu ya mwili wangu wote. Hivyo nilipaka vumbi katika mwili wangu na nikatekeleza Sala.

Tulipokwenda kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alisema, huku akitabasamu: “Kwa tayammum kiasi hiki kinatosha kwamba viganja vya mikono yote vinaguswa kwenye udongo kwa pamoja na viganja hivyo vifutwe kwenye paji la uso, kisha nyuma ya mkono wa kulia kufutwe na kiganja cha kushoto na kisha nyuma ya mkono wa kushoto ufutwe na kiganja cha kulia.” Sasa kwa nini unamwambia huyu mtu asitekeleze Sala?

Umar aliposhindwa kutoa jibu alisema: “Ammar muogope Allah.” Kisha Ammar akasema, “Unaniruhusu nisimulie hadithi hii? Umar akasema: “Nakuachia ufanye unavyopenda.

Kwa kuzingatia hadithi hii sahihi ambayo Ulamaa wenu wenyewe wameisimulia, utakiri kwa kweli kwamba dai la Mwalimu huyo lilikuwa la uongo mtupu.

Anaweza mtu mwenye elimu nzuri ya fiqh na ambaye amekuwa mara kwa mara pamoja na Mtume na amesikia kutoka kwa Mtume jinsi tayammum inavyopaswa kufanyika wakati maji hayakupatikana, kuja kumuambia Muislam kwamba kama hatapata maji ajiepushe na kuswali Sala zake? Hii ni ajabu hasa kwa vile Qur’ani Tukufu inatuambia sisi kwamba katika hali kama hiyo tunapashwa kufanya tayammum.

Kitendo cha tayammum miongoni mwa Waislam ni maarufu sana kwamba hata Muislam asiye na elimu anajua kwamba, chini ya masharti maalum inachukua nafasi ya kanuni za udhuu na taratibu za josho. Sasa tutasemaje kuhusu Sahaba wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Khalifa? Je, hapashwi kulijua jambo hili? Katika suala hili mimi sio ninadai kwamba Khalifa Umar aliibadili sheria ya Allah kwa makusudi.

Lakini hili kwa hakika linawezekana: alikuwa dhaifu katika uwezo wake wa kuhifadhi habari na ilikuwa ni vigu- mu kwake kukumbuka Sheria. Na hii ndio ilikuwa sababu, kama Ulamaa wenu walivyoandika, alizoea kumwambia Faqih hodari, Abdullah Ibn Ma’sud: “Unapashwa daima kuwa nami ili kwamba wakati wowote mtu akiniuliza swali, utaweza kumjibu.” Sasa, enyi waungwana! Mnapashwa kuamua ni tofauti gani iliyopo kati ya mtu ambaye elimu yake ni haba hivyo kwamba hawezi kuelewa maswala mepesi na yule ambaye mara moja tu anayaelewa masuala magumu.

Sheikh: Nani mwingine anaweza kuwa mtu huyo mbali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)? Muombezi: Ni dhahiri kabisa kwamba, baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuna mtu miongoni mwa Masahaba aliyekuwa na elimu kama hiyo ila lile “lango la elimu” ya Mtume, Ali ambaye kuhusu yeye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe amesema: “Ali ndiye mwenye elimu zaidi kati yenu.

Elimu Yote Ilikuwa Iko Dhahiri Kabisa Kwa Ali.

Abu’l’Mu’ayyid Mu’affaq Bin Ahmad Khawarizmi anasema katika Manaqib yake kwam- ba siku moja Umar alimuambia Ali Bin Abi Talib kwa namna ya mshangao kwamba: “Ni vipi kwamba ikiwa swali lolote unaulizwa wewe, unatoa jibu lake bila chembe ya kusita hata kidogo?”

Imam Mtukufu akaufungua mkono wake mbele yake na kusema: “Unaona vidole vingapi? Umar mara moja akasema: “Vitano.” Ali akasema: “Kwa nini hukutafakari juu ya hili?

Umar akasema: “Hakukuwa na haja ya kutafakari kwa vile vidole vyote vitano vilikuwa mbele ya macho yangu.” Kisha Ali akasema: “Basi vivyo hivyo, masuala yote na mambo ya elimu kwangu yanaonekana wazi kabisa. Ninatoa majibu yake bila ya kuwaza.”

Sasa, enyi waungwana! Hivi sio kwa sababu ya hisia za upendeleo tu kwamba, mwalimu huyu anaongoea upuuzi kama huu na kuwapotosha vijana wasio na elimu! Je, inaingia akilini na kukubalika kwamba yule mtu aliyekuwa na ujuzi mkubwa wa elimu na sayansi zote na aliyekuwa ndio “lango la elimu” ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), aweze kumtaka ushauri Umar ili amtatulie matatizo yake? Mu’awiya Anaitetea Nafasi Ya Ali

Hadithi moja imefanya kunijia, naiweka mbele yenu kama ushahidi wa ziada wa hoja yangu. Ibn Hajjar Makki, mwanachuo anayejulikana kwa kutostahimili kwake anaandika katika kitabu chake Sawa’iq-e- Muhriqa, sura ya 2, Maqsad ya 5, uk. 110 chini ya aya 14, kwamba Imam Ahmad Hanbal amesimulia na pia Mir Seyyed Ali Hamadani katika Mawaddatu’l-Qurba na Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahjul’l- Balagha wamesimulia kwamba, mtu mmoja alimuuliza Mu’awiya swali. Mu’awiya akasema: “Muulize Ali juu ya hilo kwani ndiye mtu mwenye elimu zaidi.. “Yule Mwarabu akasema: “Nalipendelea jibu lako wewe kuliko jibu la Ali.”

Mu’awiyya akasema: “Umetamka jambo baya sana: umemkataa mtu ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe amemfunza na ambaye kwake alimuambia: “Unao uhusiano kwangu sawasawa na Harun aliokuwa nao kwa Musa, isipokuwa tu kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu. Na zaidi ya hayo, kila wakati Umar alipotatizwa na masuala magumu, alimuuliza Ali juu yake na kuomba maoni yake.” Hii inakumbusha ule usemi: “Uadilifu hasa ni ule ambao hata adui anautolea ushahidi.”

Umar Akiri Juu Ya Kutojua Kwake Kuhusu Mas’ala Magumu, Na Kutamka Kwake Kwamba Kama Ali Asingemsaidia Matatizo Yake Yasingeli- Fumbuliwa

Ili kuendeleza kuunga mkono zaidi ubora wa Ali juu ya Umar tunanukuu kile Ulamaa wenu mashuhuri walichosema. Nuru’d-Din Bin Sabbagh Maliki katika Fusulu’l- Muhimma, Muhamamd Bin Talha Shafi’i katika Matalibu’s-Su’ul; Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad; Khatb Khawarizmi katika Manaqib Sulayman Balkhi Hanafi kati- ka Yanabiu’l-Mawadda na wengine wengi wameandika kwamba katika nyakati sabini Umar amesema: “Kama Ali asingelikuwepo, Umar angeangamia.”

Nuru’d-Din Maliki katika Fasulu’l-Muhimma anaandika kwamba wakati mmoja mtu mmoja aliletwa kwa Umar. Aliulizwa mbele ya halaiki ya watu: “Umeianzaje asubuhi yako” Yeye akasema: “Niliamka asubuhi hii katika hali hii: Nikiyapenda matamanio na kuichukia haki, nilishuhudia ukweli wa Mayahudi na Wakristo, nikaamini ambacho sijakiona na katika ambacho hakijaumbwa bado.” Umar akaamuru Ali aletwe mbele yake. Suala hili lilipowekwa mbele ya Amiru’l-Mu’minin, yeye akasema, alichokisema mtu huyu ni sahihi. Anasema anapenda vishawishi. Anamaanisha kwa hili, mali na watoto. Allah anasema ndani ya Qur’ani Tukufu:

{واﻋﻠَﻤﻮا اﻧﱠﻤﺎ اﻣﻮاﻟُﻢ واودﻛﻢ ﻓﺘْﻨَﺔٌ وانﱠ اﻟﻪ ﻋﻨْﺪَه اﺟﺮ ﻋﻈﻴﻢ {28

“Na jueni kwamba mali zenu na watoto wenu ni mtihani.” (8:28).

Kwa kuchukia haki unamaanisha kifo. Qur’ani inasema: {وﺟﺎءت ﺳﺮةُ اﻟْﻤﻮتِ ﺑِﺎﻟْﺤﻖ ۖ ذَٰﻟﻚَ ﻣﺎ ﻛﻨْﺖ ﻣﻨْﻪ ﺗَﺤﻴﺪُ {19

“Na hofu ya mauti itakuja kwa ukweli.” (50:19)

Kwa kushuhudia ukweli wa Mayahudi na Wakristo anamaanisha kile Allah Anachosema:

{وﻗَﺎﻟَﺖِ اﻟْﻴﻬﻮد ﻟَﻴﺴﺖِ اﻟﻨﱠﺼﺎرﱝ ﻋﻠَ ﺷَء وﻗَﺎﻟَﺖِ اﻟﻨﱠﺼﺎرﱝ ﻟَﻴﺴﺖِ اﻟْﻴﻬﻮد ﻋﻠَ ﺷَء وﻫﻢ ﻳﺘْﻠُﻮنَ اﻟْﺘَﺎب ۗ{113

“Mayahudi walisema kwamba Wakristo hawakuwa kwenye njia iliyonyooka na Wakristo walisema kuwa Mayahudi hawakuwa katika njia iliyooka.” (2:113).

Hii ni kwamba Madhehebu zote hizi zina zinasingiziana. Hivyo Mwarabu huyu anasema anakubaliana nazo zote, au kwamba anazikataa zote. Anasema kwamba anaamini kile ambacho hajakiona, akimaanisha kwamba anamwamini Allah swt. Mwenye Nguvu zote.

Anaposema kwamba, anaamini katika ambacho hakijaumbwa bado, yaani ambacho hakipo sasa, anaashiria Siku ya Hukumu, ambayo bado haijafikia wakati wake wa kuwepo.

Kisha Umar akasema: “Naomba hifadhi ya Allah kutokana na hali ngumu ambayo Ali atakuwa hayupo kunisaidia.”

Hadithi hii fupi ya kweli imesimuliwa kwa namna inayojieleza nzuri zaidi na ya tofauti, na wengineo kama Muhammad Bin Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib Sura ya 57, kutoka kwa Hudhaifa Bin Al-Yaman, aliyeinukuu kutoka kwa Khalifa Umar.

Kuna idadi ya matukio kama hayo wakati wa ukhalifa wa Abu Bakr na Umar, ambao wote walikuwa hawana uwezo wa kutoa jawabu sahihi. Alikuwa ni Ali aliyetoa jawabu. Hasa wakati Mayahudi, Wakristo na Wanachuoni wa Sayansi ya asili walipokuja na kujadili masuala magumu, alikuwa ni Ali peke yake aliyeyatatua.

Kulingana na Ulamaa wenu, kama Bukhari na Muslim, kila mmoja katika Sahih yake; Nishapuri katika Tafsiir yake; Ibn Maghazili Faqih Shafi’i katika Manaqib; Muhammad Bin Talha katika Matalibu’s-Su’ul, Sura ya 4 uk. 13 na 18; Hafiz Ibn Hajar Asqalan (aliyek- ufa mwaka 852 A.H) katika Tahdhibu’t-Tahdhib (Kilichochapishwa Hyderabad Daccan) uk. 338; Qadhi Fadhlullah Ruzbahar Shirazi katika Ibta’lu’l-Batil, Muhibu’d-Din Tabari katika Riyadhu’n-Nazala Juz. 2, uk. 39, Ibn Kathir katika Ta’rih yake Juz. 7 uk. 369; Ibn Qutayba Dinawazi (aliyekufa 276 A.H.) katika Ta’wil-e-Mukhtalafu’l-Hadith (kili- chochapwa Misri), uk. 201-202; Muhamamd Bin Yusuf Ganji Shafi’i (aliyekufa 658 .A.H). katika Kifayatu’t-Talib sura ya 57, Jalala’d’Din Suyuti katika Ta’rikhu’l Khulafa uk. 6, Seyyed Mu’min Shabalnji katika Nuru’l-Absar uk 73, Nuru’d-Din Ali Bin Abdullah Samhudi (aliyekua (911 A.H) katika Jawahiru’l-Iqdain, Al-Hajj Ahmad Afindi katika Hidayatu’l-Murtab uk. 146 na 153, Muhammad Bin Ali As-Sabban katika Ishafu’r- Raghbin uk. 52, Yusuf bin Sibti Ibn Jauzi katika Tadhkira Khawasu’l-Ummal, sura ya 6 uk. 37, Ibn Abi’l-Hadid (aliyekufa 655 A.H) katika Sharhe-Nahju’l-Balagha Juz. 1; Mula Ali Qushachi katika Sharh-e-Tajrid, uk. 407; Akht Abu’l-Khutaba Khawarizmi katika Manaqib uk. 48 na 60, hata yule asiyemvumilivu, Ibn Hajar Makki (Kafa 973 A.H) katika Sawa’iq Muhriqa uk. 78; Ibn Hajar Asqalani katika Isaba Juz. 2, uk. 509 na Allama Ibn Qayyim Jauzia katika Turuqu’I-Hikmiyya uk. 47 na 53 wameandika mambo mengi yanay- oonyesha kwamba Umar alipeleka masuala magumu na mazito, hususan masuala magumu ya Mfalme wa Roma, kwa Amiru’l-Mu’minin. Umar mara kwa mara alipeleka masuala kwa Ali kwa ajili ya ufumbuzi, na alipokuwa akisikia uamuzi wake alikariri kusema: “Ninaomba ulinzi wa Allah kutokana na hali ngumu ambamo Ali huyupo kunisaidia.” Wakati mwingine alisema: “Kama Ali asingekuwapo, Umar angeangamia.”

Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib yake, na Hamidi katika Jam’-e-Bainu’s-Sahihain wanaandika kwamba Makhalifa walichukua ushauri kwa Ali katika masuala yote na kwamba alikuwa ndio tegemeo kubwa ambaye alifutu mas’ala magumu ya kidini na kidunia, makhalifa hao walisikiliza kwa makini maelezo na maagizo yake na wakayatekeleza.

Ali Ndiye Aliyefaa Zaidi Kwenye Nafasi Ya Ukhalifa.

Elimu ndiyo kipimo bora zaidi cha kipaumbele. Qur’ani Tukufu kwa uwazi inaeleza. “Ni yeye basi aongozaye kwenye haki anayestahiki zaidi kufuatwa, au ni yule ambaye yeye mwenyewe haendi sawa ila zaidi kufuatwa, au ni yule ambaye mwenyewe hakuongoka ila mpaka aongozwe? Basi sasa mna nini nyie, ni vipi mnavyoamua? (10:35).

Hii ni kwamba, yule aliye na sifa nzuri za uongozi lazima awe ndio kiongozi mkuu wa watu, sio yule ambaye hana ujuzi wa namna ya kuongoza na ambaye yeye mwenyewe anatafuta muongozo toka kwa wengine.

Aya hii ndiyo (hoja) ushahidi mzito kwamba mtu mbora hawezi kufanywa kuwa chini ya mtu dhaifu. Suala la Ukhalifa, Uimam, na Uandamizi wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) unakuja chini ya kanuni kama hii. Hii inashuhudiliwa na aya nyingine ambayo inasema:

{ﻗُﻞ ﻫﻞ ﻳﺴﺘَﻮِي اﻟﱠﺬِﻳﻦ ﻳﻌﻠَﻤﻮنَ واﻟﱠﺬِﻳﻦ  ﻳﻌﻠَﻤﻮنَ ۗ{9

“Je, wale wanaojua na wale wasiojua wako sawa?” ( 39:9)

Kwa Viwango Vyote Ali Alikuwa Ndiye Aliyekuwa Na Haki Zaidi Ya Ukhalifa:

Sheikh: Tunakubali kwa dhati kwamba Ali alikuwa na sifa zote bora kama ulivyozitaja. Hakuna yeyote ila Makhawarij wakaidi, aliyewahi kuukana ukweli huu. Lakini hili nalo linakubalika: Seyyed Ali mwenyewe kwa hiari na furaha alikubali ukhalifa wa makhalifa (watatu wa kwanza) na akaridhia ubora wao na haki yao ya kumtangulia yeye.

Hivyo kuna faida gani ya sisi kuwa na wasiwasi, baada ya miaka 1300, juu ya uamuzi wao na kupigana baina yetu juu ya kwa nini umma uliwachagua Abu Bakr, Umar na Uthman.

Hivyo kuna madhara gani kama tunakuwa kwenye amani na urafiki na kila mmoja kati yetu na kukubali historia ilichokiandika na kile ambacho ulamaa wenu vile vile kwa ujumla wamekikubali: baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abu Bakr, Umar na Uthman kwa kufuatana, walishika nafasi ya ukhalifa.

Tungeishi pamoja kama ndugu na kwa pamoja tukaukubali ubora wa Ali katika elimu na matendo na uhusiano wake makhsusi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Katika njia ile ile ambayo Madhehebu zetu nne zimeungana, Mashi’a pia wangeshirikiana nasi.

Hatukatai daima ubora wa elimu ya Ali na tabia, lakini unapaswa ukubali kwamba kulingana na suala la umri, mbinu za kisiasa, uvumilivu na utulivu usoni wa adui, Abu Bakr alikuwa bila shaka ni bora kuliko Ali.

Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba kupitia uamuzi wa pamoja wa Umma, yeye alikalia kiti cha ukhalifa.

Ali alikuwa kijana bado kwa wakati ule na hakuwa na uwezo wa kubeba majukumu ya ukhalifa.

Hata miaka 25 baadae, pale alipochukua ukhalifa, machafuko mengi yalitokea kwa sababu tu hakuwa mwanasiasa mwenye uwezo.

Kiapo Cha Utii Cha Ali Kwa Makhalifa Ni Cha Kulazimishwa.

Muombezi: Kwanza, umesema kwamba Amiru’l-Mu’minin kwa hiari yake alitoa kiapo cha utii kwa wale makhalifa watatu. Kuna simulizi inanijia akilini ambayo ni yenye kufaa kwa mjadala huu.

Katika siku za zamani barabara kuu za Iran zilikuwa zenye hatari, na wale waliokuwa wakienda kuzuru kwenye makaburi matakatifu walikabiliana na matatizo wakati wa safari zao. Msafara fulani uliangukia kwenye makucha ya waporaji, ambao waliiba mali za watu hao.

Walipokuwa wakigawana ngawira miongoni mwao, sanda ya hujaji mmoja ikaangukia mikononi mwa mporaji mzee. Akasema: “Enyi waungwana mahujaji! Sanda hii ni ya nani?

Hujaji mmoja akasema: “Ni yangu” Yule mporaji akasema: “Mimi sina sanda, kwa hiyo tafadhali unipe mimi sanda hii ili iwe ni yangu kihalali. Yule hujaji akasema: “Mali yangu yote ni yako, lakini nirudishie sanda hiyo, kwa vile niko katika hatua za mwisho za maisha yangu na imenichukuwa taabu kubwa kwa matayarisho ya vazi hili kwa ajili yangu kwa ajili ya Akhera. Huu ni utajiri wangu nilioutunza.”

“Yule mporaji akasisitiza kwa mkazo sana juu ya dai lake, lakini yule hujaji alirudia jambo lile lile kwamba hataiachia haki yake ile kwa mtu yeyote yule.” Yule mporaji, akichomoa upanga wake, alianza kumparura yule hujaji kati ya kichwa chake na uso na kusema kwamba angeendelea kumpiga mpaka atakapomuachia yeye sanda hiyo na kusema: “Ni halali.”

Maskini hujaji yule mzee alipigwa hivyo kiasi kwamba alianza kupiga kelele. “Bwana! Halali! Halali! Halali! Ni halali zaidi kuliko maziwa ya mama yake mtu.”

Natumaini mtanisamehe. Lakini nilitaka kuvuta usikivu wenu kwa haya ninayotaka kuelezea. Pengine mmesahau yale ambayo nimeyathibitisha kwenye mikesha iliyopita.

Nilitaja kumbukumbu sahihi za kihistoria, ambazo Ibn Abi‘l-Hadid, Jauhari, Tabari, Baladhuri, Ibn Qutayba, Mas’udi na wengine katika ulamaa wenu wamezihakikisha, kwamba walitishia kuchoma moto nyumba ya Ali, yeye akaburuzwa hadi msikitini na aliamriwa kwa upanga kooni mwake; “Toa kiapo cha utii, vinginevyo utakatwa shingo.” Je, huu ni mfano wa kiapo cha hiari?

Kusiwepo Na “Imani Povu” Katika Dini:

Pili, nimekwishasema mapema kwamba tusiwe na “Imani povu” katika misingi ya dini. Unasema kwamba kwa vile historia inatuambia sisi kwamba makhalifa hawa wanne walikuwa watawala, tungewafuata wazee wetu na tuwe na imani juu yao.

Lakini akili ya kawaida na Hadithi vinatuambia kwamba imani kimsingi isimame juu ya mantiki.

Ninarudia tena kwamba wanahistoria wenu na wetu wameandika kwamba baada ya kifo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Umma uligawanyika katika madhehebu mbili. Madhehebu moja ikasema kwamba Abu Bakr angepaswa kufuatwa na ile madhehebu nyingine iliamini kuwa Ali angefuatwa.

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kumtii Ali ni kunitii mimi, na kutomtii Ali ni kutonitii mimi.” Kwa hiyo utii kwa Ali kulikuwa, kulingana na amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kulikuwa ni lazima.

Hivyo ilikuwa ni wajibu wa kila mmoja wa madhehebu zetu mbili kusikiliza hoja za pande hizi mbili na kuchagua njia ya sawa.

Imani Inapaswa Kusisimama Juu Ya Mantiki Na Uchunguzi Wa Dhati.

Imani yangu juu ya Allah imesimama juu ya maarifa. Nimesoma vitabu vya madhehebu na dini mbali mbali. Ninaukubli ukweli kwamba Muhammad alikuwa Mtume wa mwisho kwa msingi wa mantiki na sio kuwafuata wazee wangu kwa mkumbo tu. Vivyo hivyo, nimejifunza kwa undani mamia ya vitabu vya madhehebu zote, hususan vile vya madhehebu ya Sunni ambavyo ndani yake mna hoja za wazi za kuthibitisha Uimam na Ukhalifa wa Amiru’l-Mu’minina. Ninyi watu mnatupa tu macho juu juu kwenye Aya na Hadithi zenye kumtukuza Ali na kisha mnafanya tafsiri za ajabu ajabu juu yao.

Tatu, unasema kwamba tungekubali mpangilio na historia wa makhalifa: Abu Bakr, Umar, Uthman, na Hodhrat Ali. Lakini huu ni upumbavu. Ubora wa mwanadamu juu ya wanyama ni kutokana na elimu yake na hekima. Kwa hiyo hatuwezi kuwafuata wazee wetu vivi hivi kwa upovu tu.

Kwa mujibu wa ulamaa wenu mashuhuri, ubora wa Ali katika elimu umethbitishwa wazi kabisa. Kwa hiyo, haki ya kutangulia kwake kama Khalifa ni lazima pia ikubaliwe. Madhali alikuwa ndie “Lango la Elimu” ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kumkiuka yeye ni kukiuka toka kwenye uongofu.

Tunakiri kwamba baada ya kifo cha Mtukufu Mtume, Abu Bakr alikuwa Khalifa kwa miaka miwili na miezi mitatu, akifuatiwa na Umar kwa miaka kumi, na Uthman kwa miaka kumi na mbili. Lakini ukweli huu hauondoi nafasi sahihi ya mantiki na hadith. Historia haiwezi kumnyima “Lango la Elimu” ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) haki yake.

Firdaus, Dailami, Abu Nu’aim Ispahani, Muhammad bin Ishaq Muttalabi, mwandishi wa kitabu Maghazi, Hakim, Hamwaini, Khatib Khawarizmi na Ibn Maghazili wanasimulia ama toka kwa ibn Abbas, au Sa’id Khadiri, au Ibn Mas’ud ambao wote wanamnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Watakuja kuulizwa juu ya Uandamizi (Ukhalifa) na Ali Bin Abi Talib.”

Amri Ya Mtume Ya Kumtii Ali.

“Na chochote anachokupeni Mtume, kipokeeni, na kutokana na chochote ana- chokukatazeni kiacheni. (59:7)

Kwa hiyo ni lazima tutii maamrisho ya Mtume Mtukufu. Tunapoangalia kwenye maagizo ya Mtukufu Mtume tunaona (kama ilivyoandikwa kwenye vitabu vyenu vya kuaminika) kwamba miongoni mwa Umma wake wote, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amemwita Ali peke yake lango la elimu yake na ametuamuru sisi tumtii yeye. Kwa kweli amesema kwamba utii kwa Ali ulikuwa sawa na utii kwake.

Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, Imam‘l-Haram katika Dhakha’iru’l Uqba, Khawarizmi katika Manaqib, Sulayman Hanafi katika Yanabui‘l-Mawadda, Muhammad bin Yusuf Ganji shafi’i katika Kifayatu’t-Talib na Ulamaa wengine wameeleza kwamba Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) amesema:

“Enyi Ansar! Niwaonyesheni mtu ambaye mtamuambata na ambaye kamwe hata waongoza kombo?” Watu hao wakasema: “Ndio, hebu tumfahamu mtu huyo.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ni Ali, kuweni rafiki yake, mheshimuni yeye, na mfuateni yeye. Hakika yuko na Qur’ani na Quran iko pamoja naye. Kwa kweli atawaongozeni kwenye njia ya haki na hatakuacheni mpotee. Chochote nilichowaambieni, mimi nimekiambiwa na Jibril.

Vile vile, kama ilivyosimuliwa na ulamaa wenu, Mtukufu Mtume alimwambia Ammar al-Yasir: “Kama wanadamu wote watakuwa upande mmoja, na Ali akawa upande mwingine, unapaswa kutwaa njia ya Ali na uache ya wengine.” Pia, kwa nyakati tofauti na mahali tofauti, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kurudiarudia amesema: “Yule ambaye anamtii Ali, kwa kweli amenitii mimi. Yule anayenitii mimi anamtii Allah.”

Hakuna Hadithi Inayopatikana Yenye Kuwataja Makhalifa Wengine Kama “Viongozi Wa Umma” Au “Milango Ya Elimu.”

Hakuna hata hadithi moja katika vitabu vyenu ambayo ndani yake Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anasema: “Baada yangu, kiongozi wa kwenye njia ya sawa, au ‘lango langu la elimu’ au Mshika Makamu au Khalifa wangu’ ni Abu Bakr, Umar, au Uthman. Unaweza kutaja Hadith kama hiyo ambayo sio ya kuzushwa na vikundi vya Bakari na Amawi? Lakini mnatutaka sisi tutoe nafasi ya nne kwa “Lango la Elimu” la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), “Mrithi na Khalifa” wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa kunukuu maneno ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe, na tuwafuate wale ambao juu yao hakuna maagizo yoyote yale. Kama tutafuata ushauri wako, hatutakuwa tumevunja utii kwa Allah na Mtume wake Mtukufu?

Ulamaa Wa Kisunni Hawataki Ushirikiano Na Sisi.

Nne, Umesema kwamba, kama hizi madhehebu nne (Hanafi, Maliki, Hanbali na Shafi’i) tungekuwa nasi tujiunge nanyi. Lakini ninyi watu mnawaita Shia ni Rafidhi, washirikina na makafiri.

Kwa hakika washirikina na waumini hawawezi kuungana. Sisi, hata hivyo, tuko tayari kabisa kushirikiana na ndugu zetu Sunni. Kwa kweli sharti ni kwamba ninyi na sisi tuwe na uhuru sawa wa kutetea imani zetu za kidini.

Kama vile ambavyo wafuasi wa madhehebu hizi nne walivyo huru katika matendo yao, wafuasi wa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) nao pia wawe huru katika matendo yao. Tunaona kwamba, kati ya madhehebu zenu hizi nne kuna tofauti mbaya sana kiasi kwam- ba baadhi yao wanawaita wengine makafiri na watenda dhambi.

Bado mnawachukulia wao kama ni Waislamu na kuwaruhusu uhuru wa vitendo. Lakini kuwaita maskini Mashi’a washirikina na makafiri, mnawatoa nje ya Kundi la Waislamu na kuwanyima uhuru wao wa kuitekeleza dini yao. Tutategemeaje kuwa na umoja na ushirikiano?

Kusujudu Juu Ya Udongo Kwa Shi’a Kunapingwa Na Wengine Bila Ya Sababu.

Chukua mfano wa kusujudu kwetu kwenye udongo. Ni makelele gani hayo mnayofanya kwa ajili ya udongo huo na turba, kipande kidogo cha udongo wa ardhi tukufu ya Karbala, ambacho juu yake tunaweka vipaji vyetu vya uso wakati wa kusujudu.

Ninyi mnashikilia kwamba ni sanamu na mnatuita sisi waabudu sanamu, ingawa tunasujudu juu ya udongo kwa idhini ya Allah na Mtukufu Mtume wake (s.a.w.w.). Aya za Qur’ani zinatuagiza sisi kufanya sijida, na kusujudu maana yake ni kuweka paji la uso juu ya ardhi. Bila shaka kuna tofauti ya maoni kati yetu na ninyi juu ya vitu ambavyo tunasujudia juu yake.

Sheikh: Basi kwa nini hamfanyi sijida kama wafanyavyo Waislam wengine wote ili kwamba pasiwe na tofauti na kutoelewana huku kukaweza kutoweka.

Muombezi: Kwanza, tafadhali hebu natufahamu kwa nini ninyi Shafi’i mnatofautiana sana na Maliki na Hanbali katika vyote, shuruti za matendo na misingi ya Imani zenu. Wakati mwingine wanafikia mpaka kuitana “Mtenda dhambi” na “Kafir.” Ingekuwa bora kama wote wangekaa pamoja na kupata imani moja, ili kwamba kusiwepo na tofauti.

Sheikh: Ipo tofauti ya maoni miongoni mwa mafakihi, lakini yeyote kati yetu atakayem- fuata yeyote kati ya Mafakihi hawa - Imam Shafi’i, Imam A’zam, Imam Maliki au Imam Ahmad Bin Hanbal - atalipwa na Allah.

Tofauti Kati Ya Madhehebu Manne Zinapuuzwa Bali Shi'a Hawavumiliwi

Muombezi: Tafadhali sana kuwa mwadilifu, huna sababu ya kuwafuata mafakihi hawa wanne ila tu kwamba, baadhi yao walikuwa ni watu wenye elimu. Mnawafuata bila ya kufikiria. Mnaongozwa na pua na bado mnadai kwamba matendo yenu yatalipwa ingawa kuna tofauti katika imani na matendo miongoni mwao.

Tunafuata amri za familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambao, kulingana na Mtume mwenyewe na wanachuoni wenu wenyewe, walikuwa wenye elimu zaidi nanyi bado mnasema sisi ni makafiri.

Ni lazima mkiri kuwa uadui huu hautokani na tofauti katika maoni. Chanzo chake ni kwamba sisi tunaipenda familia ya Mtume, na maadui zetu wanalea chuki ya siri dhidi yao.

Kiasi ambacho tofauti katika misingi ya Imani na Vitendo vya Ibada vinahusika, ziko nyin- gi mno miongoni mwa madhehebu zenu hizi nne, Nyingi ya fatwa na maimam na mafak- ihi wenu zinapingana na maelekezo ya wazi yaliyomo ndani ya Qur'ani Tukufu. Lakini hamkutamki neno lolote dhidi ya wale ambao wanatoa fatwa kama hizo na wale wanaozitekeleza. Bado wakati Shi'a wanaposujudu kwenye udongo halisi kulingana na Sheria ya Qur'ani Tukufu, mnawaita makafiri!

Fatwa Za Wanachuoni Wa Sunni Zinakwenda Kinyume Na Maelekezo Ya Qur'ani

Sheikh: Ni wapi wanachuoni wa Fiqh wa Sunni na Maimam wanne wametoa fatwa zina- zokwenda kinyume na Qur'anii Tukufu?

Muombezi: Mara nyingi wametoa amri kinyume na amri za Qur'ani Tukufu na kinyume na maoni (ijma) yaliyokubaliwa na umma. Ulamaa wenu wenyewe wameandika idadi kadhaa ya vitabu juu ya tofauti miongoni mwa madhehebu haya manne. Nakushauri usome kile kitabu maarufu Masa'ilu'l-Khalif fi'l-fiqh cha Sheikhu’t-Ta’ifa Abu Ja’far Muhammad Ibn Hasan Ibn Ali Tusi, ambaye ameandika tofauti zote za mafakihi wa Kiislam kutoka kwenye sura ya Tohara mpaka kwenye sura ya Diyat (Kisasi). Nitatoa mmoja kati ya mifano mingi ya kanuni za kisheria, zilizoamuliwa kinyume na Qur’ani Tukufu.

Seikhh: ndiyo, hebu tupe mfano wa hili.

Katika Kukosekana Maji Kwa Ajili Ya Josho Na Udhu Mtu Afanye Tayammam

Ninyi waungwana mnafahamu kwamba josho la wajibu ni kanuni muhimu ya Kiislam. Kutegemea mazingira, mtu huosha mwili mzima (josho) au sehemu yake (udhu). “Mnaposimama kusali. Osheni nyuso zenu na mikono yenu mpaka kwenye kongo mbili.” (5:6)

Kama vilivyo, tunapaswa tutawadhe kupata udhu kwa maji safi. Wakati hatuna maji, tufanye tayammam, kulingana na Aya:“Na kama msipopata maji basi chukueni udongo (safi) na mpake nyuso zenu na mikono yenu.” (4:43)

Tunapaswa kufanya tayammam kwa udongo safi. Katika suala la awali, maji kwa ajili ya udhuu ni muhimu. Katika suala la pili, maji hayapatikani, au kama kuna sababu nyingine ya udhuru basi, iwe tumo katika safari au tupo nyumbani, tutapaswa kufanya tayammam, kupaka mikono na nyuso kwa vumbi safi, badala ya udhu. Katika nukta hii, mafakihi wote wa Kiislam wanakubaliana, ama wewe Shi’a Ithna Ashari, Maliki, Shafi’i, au Hanbali,

Fatwa Ya Abu Hanifa Kwamba Kama Maji Yasipopatikana Tunaweza Kufanya Josho La Udhu Kwa Kutumia (Nabiz) Kosha La Mtende.

Lakini Imam wenu mkubwa sana, Abu Hanifa (ambaye fatwa zake nyingi sana zimetegemea kwenye dhana) anasisitiza kwamba wakati tukiwa safarini na kama hatuwezi kupata maji, tunapaswa kuoga josho kutumia Nabiz ( maji ya kosha la mtende). Lakini kila mtu anajua kwamba Nabiz ni kosha la mtende na sio halali kuchukua udhu kwa maji yaliyochanganyika.

Qur’ani Tukufu inaagiza kamba ni lazima juu yetu sisi kuchukua udhu kwa ajili ya ibada ya Sala kwa kutumia maji safi. Kama maji hayapatikani, tunapaswa kufanya tayammam.

Imam A’zam Abu Hanifa anasema kwamba tunaweza kuoga josho au udhu kutumia Nabiz. Huu ni uvunjaji wa wazi wa Sheria ya Qur’ani. Kwa upande mwingine , Bukhari katika Sahihi yake ameandika hivi “Sio halali kuchuku udhu kwa Nabiz au kilevi.”

Hafidh: Ninafuata madhehebu Shafi’i na ninakubaliana na wewe kabisa katika suala hili. Kama hakuna maji tufanye tayammam, na hairuhusiwi kuchukua udhu kwa Nabiz. Fatwa hii imezushiwa Imam Abu Hanifa kwa msingi ya umaarufu wa jumla wa hiyo nabiz.

Muombezi: Kwa kujua ukweli halisi unafanya kisingizio hiki. Fatwa hii ya Abu Hanifa imesimuliwa kwa mfululizo sana.

Ninamnukuu Fakhru’d-Din Radhi anayesema katika sherehe yake ya Mafatihul-Ghaib, Juzuu ya 3 uk. 553 kuhusiana na aya hii ya tayammam, mas’ala ya 5; Shafi’i anasema kwamba “Udhu kwa kutumia Nabiz (kosha la mtende) sio halali, na Abu Hanifa anasema kwamba ni halali wakati mtu anapokuwa yuko kwenye safari. Pia Ibn Rushd ameandika fatwa hii ya Abu Hanifa katika kitabu chake Hidayatu’l- Mujtahid.

Sheikh: Utasemaje kwamba fatwa hii ni kinyume na amri ya Qur’ani? Baadhi ya Hadith, zinaithibitisha kwa uwazi kabisa kutoka kwenye kitendo cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Muombezi: Unaweza kutaja Hadithi yeyote yenye kuunga mkono hoja yako?

Sheikh: Katika Hadithi ambayo Abu Zaid, mtumwa wa Amr Bin Harith anasimulia kuto- ka kwa Abdullah Bin Mas’ud kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia, kwenye usiku wa majini (Lailatu’j-Jinn usiku ambapo Mtume alipokea kiapo cha utii kutoka kwa majini) kwamba: “Je, unayo maji kidogo” Yeye ( Abu Zaid) akasema: “Hapana, ipo nabiz kidogo tu” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Mtende ni msafi, na maji pia ni masafi. Kusema hivyo akachukua wudhu.

Kuna Hadithi nyingine ambayo Abbas Bin Walid Bin Sabihu’l-Halal Damishqi anasimu- lia kutoka kwa Marwan Bin Muhammad Tahir Damishqi ambaye alisimulia kutoka kwa Abdullah bin Lahi’a ambaye ameisimulia kutoka kwa Abdullah Bin Mas’ud ambaye alisema: Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliniambia katika usiku wa majini “Je unayo maji”

Nikasema: “Hapana, lakini kuna Nabiz katika hiyo ndoo.” Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Mtende ni msafi, na maji yake ni masafi. Nimiminie.” Hivyo nilimmiminia (juu ya viungo vyake), na akachukua udhu nayo.”

Ni dhahiri, kitendo hiki cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni mfano kwa ajili yetu sisi wa kuufuata. Hakuna kanuni au hoja iliyo bora kuliko vitendo vyake. Ni kwa sababu hiyo kwamba Imam wetu A’zam amekubali uhalali wake.

Muombezi: Pengine ingelikuwa vyema kama ungelinyamaza kimya. Sasa ndugu zetu Sunni watajua kwamba Viongozi wao walikosea. Walitoa fatwa kwa misngi ya dhana tu. Kwanza kabisa, natuchunguze hawa wasimuliaji wa Hadithi hii walikuwa ni nani.

Kwanza, Abu Zaid, mtumwa wa Amir Bin Harith, ni mtu asiyejulikana, na kulingana na wanachuoni au Hadithi, ni mtu asiyekubalika kama alivyoelezwa na Tirmidh na wengineo.

Dhahabi katika Mizanu‘l-itidal yake anasema: “Mtu huyu hajulikani kwetu na hadithi hii ambayo imesimuliwa kutoka kwa Abdullah Bin Mas’ud siyo sahihi.” Hakim anasema; “Hakuna hadithi nyingine iliyosimuliwa na mtu huyu asiyejuliakana.”

Bukhari pia amemtaja kama msimuliaji wa Hadithi asiyetegemewa. Kwa sababu hii, Ulamaa mashuhuri, kama Qastalani na Sheikh Zakariyya Ansari, wameandika katika Sherehe zao za Sahih Bukhari kwamba “udhu sio halali kwa kutumia nabiz au vileo.” Wanaeleza kwamba hadithi iliyorejewa hapo juu ni dhaifu.

Hii hadithi ya pili pia nayo haikubaliki. Kwanza, hakuna mwanachuo, ispokuwa Ibn Maja, aliyeisimula kwa namna hii.

Pili, Ulamaa maarufu hawakuiingiza katika Sunna zao kwa sababu sanadi ya wasimulizi wake ina utata.

Dhahabi katika Mizanu’l-Itiqad yake amenukuu idadi ya kauli zinazoonyesha kwamba Abbas Bin Walid sio wakutegemewa. Hivyo wasanifu na wafasiri wamemkataa yeye moja kwa moja. Na kuhusu Marwan Bin Muhammad Tahiri, alikuwa ni wa lile kundi lililo potoka la Marhaba. Ibn Hazm na Dhahabi wamethibitisha kwamba alikuwa msimuliaji hadithi asiyetegemewa.

Vivyo hivyo, Abdullah Bin Lahi’a pia ametiliwa mashaka na Ulamaa mashuhuri na wafasiri. Kwa hiyo pale sanadi ya wasimulizi wa hadithi inapokuwa ni ya asili ya mashaka hivyo kwamba ulamaa wenu wenyewe wanaikataa, hadithi hiyo inapoteza thamani.

Tatu, kwa msingi wa hadithi, ambayo wanachuoni wenu wameisimulia kutoka kwa Abdullah Bin Mas’ud, hakukuwa na mtu yeyote pamoja Mtukufu Mtume kwenye Lailatu’j’Jinn. Abu Dawud katika Sunnan yake, sura ya Udhu, na Tirmidhi katika Sahih yake wanasimulia kutoka kwa Al-Qama kwamba Abdullah Bin Mas’ud aliulizwa: “Ni nani miongoni mwenu aliyekuwa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika ule usiku wa Lailatu’j-jinn? Yeye akasema: “Hakuna mtu aliyekuwa naye kutoka miongoni mwetu.”

Nne, Lailatu’j-Jinn ulitokea Makkah kabla ya Hijra (kuhama kwa Mtume), ambapo wafasiri wote wanasema kwamba aya ya Tayammam ilishuka Madina.

Hivyo amri hii kwa hakika inaifuta ile amri iliyotangulia huko nyuma. Ilikuwa ni kwa sababu hii kwamba mafakihi wenu wakubwa, kama vile Imam Shafi’i, Imam Malik na wengineo wameitamka kwamba ni haram.

Inashangaza kwamba huyu Sheikh anawasilisha Hadithi dhaifu kama yenye kuaminika usoni mwa Qur’an Tukufu na anajaribu kuthibitisha maelezo ya Abu Hanifa kuwa ya sawa- sawa na sahihi.

Kuosha Miguu Katika Udhu Ni Kinyume Na Sheria Ya Qur’ani

Mbali na kanuni zilizokubalika za udhu zilizotajwa katika Aya ya hapo juu, baada ya kuosha uso na mikono, sehemu ya kichwa na za miguu mpaka kwenye vifundo ni za kupakwa. Aya hii tukufu inasema wazi: “Na pakeni sehemu ya vichwa vyenu na sehemu ya miguu yenu mpaka kwenye vifundo.”

Lakini wanachuoni wenu wote wa fiqh wanashikilia kwamba miguu ioshwe, wakipinga hukumu ya wazi ya Qur’ani. Kuna tofau- ti kati ya kuosha na kupaka.

Sheikh: Kuna Idadi kadhaa ya Hadith zinazoonyesha kwamba miguu ni ya kuoshwa.

Muombezi: Kwanza, hadithi zinazorandana na hukmu za Qur’ani tu ndio zinazokubali- ka. Kwa hakika, kutangua aya wazi ya Qur’ani kwa hadith moja tu haiwezi kamwe kuwa halali. Aya hii tukufu kwa uwazi kabisa inaagiza kupaka, sio uoshaji wa miguu.

Kama utafikiri kwa uangalifu kidogo utaona kwamba aya yote mzima inaelekea wenye maana hiyo hiyo. Inaanza na hukmu ya “osha uso wako na mikono yako.” Hiki kiungo “na” kinaashiria kwamba baada ya kuosha uso, tunapaswa pia kuosha kichwa mikono. Kadhalika, katika hukmu ya pili: “na pakeni sehemu vichwa vyenu na sehemu ya miguu yenu.”

Kupakwa kwa kichwa na kwa miguu kumeunganishwa na kile kiungo “na.” Hii inaonyesha wazi kwamba baada ya kupaka kichwa, na miguu nayo ni lazima ipakwe.

Inapita bila kupingwa kwamba kuosha hakuwezi kubadilishwa na kupaka. Hivyo kama kuosha uso na mikono kulivyo lazima, kule kupaka kichwa na miguu pia ni lazima. Hairuhusiwi kwamba kimoja kipakwa na kingine kioshwe. Vinginevyo, hiki kiungo “Na” kitakuwa hakina maana yoyote.

Hali kadhalika, mbali na maana hizi za wazi, sheria ya Kiislam haibebi hukumu ngumu na zenye uzito. Kuosha miguu ni kugumu zaidi ya kupaka hiyo miguu.

Hukumu ya kidini imedhamiriwa kufanya kuchukua udhu kuwe kwepesi, kama usemi wa aya unavyopendekeza pia. Imam Fakhru’d-Din Razi, mfasiri mkubwa wa Kisunni, anatoa hoja yenye maelezo zaidi kuhusu hali halisi ya ulazima wa kupaka miguu katika udhu. Utafaidika kwa kuisoma hiyo.

Kupaka Juu Ya Soksi Ni Kinyume Na Sheria Ya Wazi Ya Qur’an Tukufu

La ajabu zaidi kuliko kuosha miguu ni kupaka juu ya soksi. Kuna hitilafu miongoni mwa mafaqihi wa Kisunni juu ya kwamba inaweza kufanywa wakati wa safari au ukiwa nyumbani.

Hukmu hii ni kinyume na maelekezo ya Qur’ani ambayo inashurutisha kwamba tunapaswa kupaka miguu na sio soksi. Hukmu hii pia inapingana na hukmu ya awali ya kuosha miguu. Ikiwa kupaka miguu sio halali, kwa nini wamefanya kupaka juu ya soksi kuwa ni halali?

Sheikh: Kuna Hadithi nyingi zinaoonyesha kwamba bwana Mtume alipaka soksi zake. Kwa maana hiyo, mafaqihi wakaichukulia hiyo kama uthibitisho wa uhalali wa kitendo hicho.

Muombezi: nimerudiarudia kushauri kwamba, kulingana na amri ya Bwana Mtume, hadithi inayodaiwa imesimuliwa kutoka kwake ambayo hairandani na Qur’ani Tukufu ni ya kukataliwa. Wazushi hawa na wanasiasa wajanja wametunga Hadithi nyingi. Kwa sababu hiyo, Ulamaa wenu mashuhuri wamekataa Hadithi za namna hii.

Mbali na ukweli kwamba hadithi hizi haziendani na sheria za wazi Qur’ani Tukufu, zenyewe ziko zinapingana. Ulamaa wenu wakubwa wenyewe wameukubali ukweli huu.

Kwa mfano, yule mwenye hekima nyingi, Ibn Rushd Andalusi, katika Badaytu’l-Mujtahid wa Nihayyatu‘l- Muqtasid yake Juz. 1, uk. 15-16, anasema juu ya tofauti hii. “Sababu ambayo wanahitilafiana nayo ni kwamba riwaya juu yao zinapingana zenyewe.” Mahali pengine anasema: “Sababu ambayo wanahitalafiana kwayo ni kwamba, riwaya juu yao haziendani daima.”

Kwa hiyo, kusimamisha hoja juu ya riwaya na hadithi ambazo zinapingana zenyewe na ambazo pia ni kinyume kabisa na maagizo ya Qur’ani ni kichekesho kabisa. Unajua kwamba kati ya hadith ambazo zinapingana zenyewe, ni zile tu ambazo zinakubaliana na Qur’ani Tukufu ndizo zinazokubaliwa. Ikiwa hadithi yoyote inapingana na Qur’ani, hiyo ni ya kutupwa moja kwa moja.

Kupaka Juu Ya Kilemba Ni Kinyume Na Sheria Ya Qur’ani

Aya hii inaeleza wazi kwamba, “Na pakeni sehemu ya vichwa vyenu” (baada ya kuosha uso na mikono). Kwa misingi ya amri hii ya Qur’ani, mafaqihi wa Kishia, kwa kuwafuata Maimam wao, wanashikilia kwamba, kichwa chenyewe ni cha kupakaza katika kuchukua udhu.

Mafaqih wa Shafi’i, Maliki, Hanfi wanapatana. Lakini Imam Ahmad Bin Hanbali, Ishaq, Thawri na Quza’i wamesema kwamba kupaka juu ya kilemba inasihi. Hii imeandikwa na Imam Fakhru’d-Din Razi katika Tafsir-e- Kabir. Mtu yeyote mwenye fahamu anajua kwamba kupakaza juu ya kilemba na kupakaza juu ya kichwa ni mambo mawili tofauti kabisa.

Shi’a Pekee Ndio Wanaolaumiwa Kwa Tofauti Kama Hizo:

Kuna tofauti nyingine za hali ya juu sana miongoni mwa mafaqihi wenu na miongoni mwa madhehebu nne hizi. Ingawa nyingi ya hizo zinapishana waziwazi na maagizo ya Qur’ani, hamtoani makosa kati yenu. Kila mmoja wao yuko huru kudumisha maoni yake.

Hamumuiti Abu Hanifa na mahanafiya kuwa ni washirikina, wanaporuhusu udhu kuchukuliwa kwa Nabiz (Maji ya mtende yaliyochachuliwa) wala hamshutumu tafsir zinazojipinga zenyewe za sheria, ambazo zinavunja hukumu za Qur’ani. Lakini mnawapinga Shi’a ambao, wanawafuata kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa kweli mnawaita wafuasi ile familia tukufu Rafidhi na Makafiri!

Umesema kwa kukariri katika mikesha iliyopita kwamba ibada za Kishi’a zinathibitisha kuwa wao ni washirikina. Umeuliza kwa nini hatufanyi Sala kama Waislam? Sisi tunaswali Swala zile zile ambazo wewe na Waislam wengine wote wanazosali; rakaa mbili za Al-fajir, (sala ya asubuhi), rakaa nne za Adhuhuri (Sala ya mchana), rakaa nne za Asr (Sala ya alasiri), rakaa tatu za magharibi (Sala ya wakati wa kuzama jua), na rakaa nne za Isha (Sala ya jioni).

Na kwa tofauti katika kanuni za ibada, zipo tele katika madhehebu zote za Kiislamu. Kwa mfano, kuna tofauti ya wazi kati ya Abu’l-Hasan Ash’ari na Wasil Bin Ata katika misingi na kanuni za ibada.

Pia Maimam wenu wanne (Abu Hanifa, Maliki, Shafi’i na Ahmad Hanbal) na mafaqihi wengine wakubwa kama Hasan, Dawud, Kathir, Abu Sur, Quza’i, Sufyan Thawri, Hasan Basr na Qasim Bin Salam n.k, wana tofauti miongomi mwao.

Katika namna hiyo hiyo, hukumu za Maimam watukufu wa Ahlul Bayt zinatofautiana na kauli za mafaqihi wenu. Ikiwa tafsiri za kisheria za mafaqihi hawa na tofauti zao za maoni zinaweza kushutumiwa, kwa nini shutuma kama hizo zisitolewe dhidi ya madhehebu tofauti za Kisunni?

Kwa Mujibu Wa Ulamaa Wa Kisunni Kusujudu Juu Ya Kinyesi Kikavu

Na Kinyesi Cha Mnyama Ni Halali.

Ulamaa wengi wa Sunni wanazikubali tafsiri za kisheria ambazo zinakiuka amri ya wazi ya Qur’ani na bado wanatoa tafsiri potovu kwa amri zenye kueleweka wazi. Mafaqih wengine wanatoa maoni tofauti. Bado hamzichukulii tafsiri zao au ibada zao kama ni ukafiri. Lakini kuhusiana na ufanyaji wetu wa sijda mnatoa upinzani kwa sauti kubwa, mkisema kwamba, Shi’a ni waabudu sanamu, wakati mnapuuza tamko la ulamaa wenu wenyewe kwamba kusujudu juu ya kinyesi kikavu kunaruhusiwa.

Kusujudu Juu Ya Mazulia Badala Ya Ardhi Ni Kinyume Na Agizo La Qur’ani

Maamuzi ya kisheria ya mafaqih wa Shi’ah, wakiwafuata Maimam wao watukufu, yanakubaliana kwa uwazi na maagizo ya Qur’ani Tukufu. Kwa mfano, mafaqihi wenu wanachukulia mazulia ya sufi, pamba, hariri na mazulia mengine sawa sawa na udogo. Lakini ni wazi kwamba mazulia haya sio udongo wenyewe.

Lakini Shi’ah, kwa utii kwa Maimam wao wa Ahlul-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wanasema: “Sijda haisihi juu ya chochote isipokuwa juu ya udongo au vile vitu, vinavyokua kutoka kwenye udongo na havitumiki kwa kula au kuvaliwa.”

Kwa hili mnawakemea na kuwaita washirikina. Kwa upande mwengine hamuiti kusujudu kwenye kinyesi kikavu ni ushirikina. Ni dhahiri kabisa kwamba, kusujudu juu ya udongo kama ilivyoamriwa na Allah na kusujudu juu ya mazulia ni vitu tofauti kabisa.

Sheikh: Ninyi watu mnafanya Sijda kwenye vipande vya udongo wa Karbala. Mnakuwa na vibonge hivyo vidogo vya udongo kutoka nchi ile. Viko kama sanamu, na mnachukulia kusujudu juu yao ni lazima. Kwa kweli, kitendo hiki ni kinyume na taratibu na ibada za Waislam.

Muombezi: Imekuwa ni desturi yako kuwafuata wakubwa wako kiupofu ingawa haipen- dezi mtu muungwana kama wewe kusema kwamba ule udongo halisi wa Karbala ni kama sanamu.

Rafiki yangu mheshimika! Shutuma juu ya imani yoyote ni lazima itegemee juu ya ushahi- di. Kama ungevisoma vitabu vya Ilmu vya Shi’ah, ungelipata jawabu la shutma zako, na usingewapotosha ndugu zetu Sunni kwa upinzani wa uongo.

Shia Hawachukulii Kusujudu Juu Ya Udongo Wa Karbala Kuwa Ni Wajibu

Kama unaweza kutuonyesha kutoka kwenye tafsiri yetu yoyote hadithi moja au tamko linaloashiria kwa kusujudu juu ya udongo wa Karabala ni wajibu, tutayakubali maelezo yako yote kwamba ni sahihi. Kwa kweli, katika vitabu vyetu vyote vya kanuni za kidini, kuna maelekezo ya wazi kwamba, kwa mujibu wa amri ya Qur’ani Sijda ni lazima ifany- we juu ya udongo halisi. Hii inajumuisha vumbi, mawe, mchanga na majani, ili mradi tu isiwe ni madini. Zaidi ya hayo, Sijda inaweza kufanywa juu ya vile vitu vinavyoota kutoka kwenye ardhi, mradi tu havitumiwi kwa chakula au kuvaliwa.

Sheikh: Basi kwa nini mnayo kawaida ya kuwa navyo vibonge vidogo vya udongo toka Karbala na mnafanya Sijda juu yake wakati wa Sala? Shia Wanakuwa Na Vidonge Vya Udongo Kwa Ajili Ya Kusujudia Wakati Wa Sala.

Muombezi: Kusujudu juu ya udongo safi ni faradhi. Ibada ya Sala kwa kawaida inafanyika kwenye nyumba ambazo zimepambwa na mazulia (makapeti).

Hata kama mazulia hayo yataondolewa, ile ardhi iliyo chini yao kwa kawaida inakuwa na chokaa na vitu vingine ambavyo juu yao sijda hairuhusiwi. Kwa hiyo, tunakuwa na kipande cha udongo ili kwamba tuweze kusujudia. kwa hiyo, tunakuwa na kipande cha udongo ili kwamba tuweze kusujudia juu yake. (Mujtahid wengi wa Shia’h wanachukulia chaki, plasta, chokaa na mawe ya kuchimbuliwa kama vile ageti vyenye kuruhusika tu pale vinapokosekana vile vitu vilivyopendekezwa, lakini hata hivyo vinaondoa mawe yenye madini halisi na madini yaliyosafishwa - Mfasiri).

Sheikh: Tunachokiona ni kwamba, Shi’ah wote wana vidonge vya udongo wa Karbala na wanachukulia kufanya sijda juu yake ni faradhi.

Kwa Nini Tunasujudu Juu Ya Ule Udongo Wa Karbala

Muombezi: Ni kweli kwamba sisi tunasujudu juu ya udongo wa Karbala, lakini sisi hatulichukulii hilo kwamba ni wajibu. Kulingana na maelekezo yaliyomo ndani ya vitabu vyetu vya Fiqh tunachukulia sijda ni wajibu juu ya udongo safi. Hata hivyo, kulingana na Ahlul’Bayt, sajda juu ya udongo safi wa sehemu aliyozikiwa Husain (a.s) kule Karbala, ni bora zaidi

Inasikitisha kwamba baadhi ya watu kwa uovu tu wanashikilia kwamba Shi’ah wana- muabudu Husein. Wanatilia nguvu maoni yao kwa kusema kwamba Shi’ah wanafanya Sajda zao juu ya udongo uliochulikuliwa toka Karbala.

Kwa kweli kamwe hatumuabudu Husain, Ali au Muhammad. Tunamuabudu Allah swt. peke yake, na ni kulingana na amri ya Allah kwamba tunafanya Sajda juu ya udongo halisi tu.

Kusujudu kwetu sio kwa ajili ya Husain. Lakini kutokana na maagizo ya Maimam wasiokosea wa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kusujudu juu ya udongo safi wa Karbala kunapelekea kwenye malipo makubwa juu yetu, lakini sio wajibu.

Sheikh: Utadai vipi kwamba udongo wa Karbala una sifa maalum na kwamba unastahili kupendelewa zaidi ya udongo mwingine?

Sifa Za Hali Ya Udongo Wa Karbala.

Muombezi: Kwanza, ni ukweli kwamba sehemu tofauti zina sifa tofauti. Kila kipande cha ardhi kina sifa maalum ambayo ni mtaalam wa utafiti wa ardhi na mawe (geologist) tu anayezijua. Wasio wataalam hawayajui mambo haya.

Pili, sifa, hali maalum ya udongo wa Karbala zilijulikana kabla ya wakati wa Maimam watukufu. Kilikuwa ni kitu chenye mazingatio maalum katika wakati wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pia, kama ilivyokuwa imeandikwa kwenye vitabu sahihi vya Ulamaa wenu wenyewe.

Katika Khasa’isu’I-Kubra cha Jalalu’d-Din Suyuti, idadi ya hadithi za Ummu’I-Mu’minin Umm Salma, Ummu’I-Mu’minin Aiyesha, Ummu’I-Mu’Minin Fadhl, Ibn Abbas na Anas Bin Maliki na kadhalika, juu ya udongo wa Karbala zimesimuliwa na Ulamaa wenu mashuhuri na wasimulizi wanaotegemewa kama Abu Nu’aim Ispahani, Baihaqi na Hakim.

Hadithi moja inasema: “Nilimuona Husain amekaa katika paja la babu yake, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliyekuwa na donge jekundu la udongo mkonini mwake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa akibusu ule udongo na kulia. Nilimuuliza udongo ule ulikuwa nini? Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akasema:

“Jibril amenijulisha kwamba mwanangu, huyu Husain, atauawa huko Iraq. Ameniletea udongo huu mimi kutoka kwenye ardhi ile. Ninalia kwa sababu ya mateso yatakayomfika Husein.”

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaukabidhi ule udongo kwa Ummu Salma na akamuam- bia: “Pale utakapoona kwamba udongo huu unageuka kuwa damu, utajua kwamba Husain wangu amechinjwa.”

Ummu Salma aliuweka udongo ule kwenye chupa na akaweka uangalizi juu yake mpaka akaona mnamo siku ya Ashura, mwama 61 A.H. kwamba umegeuka kuwa damu. Ndipo akajua kwamba Husain Bin Ali ameuawa shahidi.

Imeandikwa na Ulamaa wenu mashuhuri na mafaqihi wa Kishia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Maimam waliweka mazingatio maalum juu ya udongo halsi wa Karbala.

Baada ya kuuawa shahidi Imam Husain, Imam Seyyedu’s-Sajidin Zainur’I- Abidin, Ali Bin Husain aliuokota kidogo, akautangaza kuwa ni udongo Mtakatifu na akauweka kwenye begi lake. Imam huyu Mtukufu alitumia kufanya Sajda juu yake na alitengeneza tasbihi kutokana nao na akadhukuru sifa za Allah kwayo.

Baada yake, Maimam wote walaiomfuatia waliuchukulia udongo ule kuwa ni mtakatifu na walitengeneza tasbih kutokana nao na kidongo kidogo cha kusujudia juu yake. Waliwashawishi Shi’ah kufanya sajda juu yake, kwa kuelewa kuwa haikuwa ni wajibu, lakini kwa maoni ya kutarajia kupata malipo makubwa.

Maimam watukufu walisisitiza kwamba kusujudia mbele ya Allah lazima kuwe juu ya udongo safi tu, na kwamba ingekuwa ni bora zaidi kama ingefanywa juu ya udongo ule wa Karbala.

Yule mwanachuoni mkubwa, Abu Ja’far Muhammad Bin Hasan Tusi anaandika katika kitabu chake Misbahu’l-Mutahajjid kwamba Imam Ja’far as-Sadiq aliweka udongo kidogo kutoka kwenye kaburi la Imam Husain katika kitambaa cha rangi ya manjano ambacho alikifunua wakati wa sala na kufanya Sajda yake juu yake. Shi’ah kwa muda mrefu wame- jiwekea udongo huu.

Kisha, kwa kuhofia kwamba ungeweza kunajisika, waliukanda vidonge vidoga au vipande, ambavyo sasa vinaitwa Muhr. Tunavichukulia kwamba ni vitakatifu na wakati wa sala tunasujudu juu yavyo, sio kama tendo la wajibu lakini kwa mtazamo wa sifa yake maalum, vinginevyo tunapokuwa hatuna udongo halisi, tunasujudu juu ya ardhi safi, au jiwe safi. Kwa namna hii, tendo letu la faradhi (sajda) linatimia.

Tunashangazwa na tabia ya Ulamaa wenu ambao hawaoni makosa kwenye fatwa za haya madhehebu manne ya Sunni. Ni kwamba, kama Imam A’ zam anasema kwamba katika kukosekana maji udhu unaweza kuchukuliwa kwa nabiz, Shafi’i, Maliki na Hanbali hawana pingamizi juu yake.

Ikiwa Imam Ahmad Bin Hanbali anaamini kuonekana kwa Allah au anachukulia ni halali kupaka maji juu ya kilemba katika utaratibu wa udhu, ulamaa wa hizo madhehebu zingine hawamshutumu.

Halikadhalika, hawalaumu fatwa za kipekee kama ile ya kuungana katika ndoa na wafulana wadogo wakati wa safari, kusujudu juu ya kinyesi au kitu chochote kilichonajisika, au kuingiliana na mama zao kwa kutumia nguo ya kujifunika.

Lakini tunaposema kwamba kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wamesema kwamba, kusujudu juu ya udongo wa Karbala ni jambo lenye thamani mnasema kwamba hawa Shi’ah ni washirikina.

Umri Mkubwa Sio Kigezo Cha Ukhalifa.

Sasa nitaijibu hoja yako. Kuzungumzia juu ya umri uliosogea na makubaliano (ijma), ume- sema kwamba kwa sababu ya umri wake, Abu Bakr alistahili kipaumbele. Hata baada ya mikesha kumi, wakati ambamo nimetengua hoja yako kuhusiana na ijima (makubaliano ya pamoja) na upendeleo kutegemea juu ya umri, unaizusha tena hoja hiyo kana kwamba hakuna lililosemwa. Hata hivyo, sitakuacha bila ya kujibiwa.

Ali Ateuliwa Kuwasilisha Aya Za Surat Bara’a (Tawba) Ya Qur’ani Tukufu

Umetoa hoja kwamba Abu Bakr alistahili kipaumbele kwa sababu ya umri wake na mbinu zake za kisiasa, lakini ni vipi kwamba baadhi ya watu waliamua kwamba kwa kusudi kubwa ilikuwa ni sharti kwa mtu kuwa mzee na mwenye mbinu za kisiasa, lakini Allah na Mtume wake hawakulielewa hili. Kwa kukuziwasilisha aya arobaini za mwanzo za Bara’a kwa watu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuuzulu Abu Bakri na kumtuma huyo kijana Ali badala yake.

Nawab: Bwana Mheshimika! Tafadhali usiiache nukta hii katika hali ya kutoeleweka vizuri. Tufahamishe ni kwa lengo gani Abu Bakr aliuzuliwa na akachaguliwa Ali mahali pake. Nilipowauliza watu hawa (akiwanyooshea kidole Ulamaa wake) juu ya hili, walitoa jibu la wasi wasi, wakisema kwamba lilikuwa ni jambo lililokuwa halina umuhimu. Tafadhali hebu lielezee jambo ili.

Muombezi: Umma wa Kiislam, pamoja na ulamaa na wanahistori wa madhehebu zote (Shi’ah na Sunni) wanaukubali ukweli kwamba wakati ziliposhuka zile aya za mwanzo za Sura ya Bara’a katika kuwashutumu wanaoabudu sanamu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuita Abu Bakr akampa aya hizo, akimuagiza yeye kuzipeleka Makka na kuzisoma kwa watu wa Makka wakati wa Hijja.

Abu Bakr alikuwa amekwenda mwendo mfupi tu wakati Jibril alipotokea na kusema: “Ewe Mtume wa Allah! Allah swt. anatuma salam Zake kwako na anasema kwamba hili suala la Qur’ani Tukufu liwe limepelekwa ama na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe au na mtu ambaye anatokana naye.”

Kwa hali hiyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamuita Ali na kumwambia: Mkimbilie Abu Bakr na uchukue zile aya za Bara’a toka kwake na ukaziwasomea waabudu masanamu wa Makka. Ali akaondoka mara moja. Alimkuta Abu Bakr hapo Dhu’l-Halifa na akamfikishia ule ujumbe wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Akazichukua ziel aya toka kwa Abu Bakr na alipofika Makka, akazisoma kwenye mkusanyiko wa watu.

Nawab: Habari hizi zimeandikwa kwenye vitabu vyetu vya Sahih?

Muombezi: Nilikwisha kueleza punde kwamba Umma wote unakubaliana juu ya suala hili. Nitakupa baadhi ya rejea sasa hivi, ili kwamba utakapofikiria juu ya suala hii utaweza kujua kwamba ni suala la maana sana. Waandishi mashuhuri wafutao wameiandika habari hii katika vitabu vyao na kwa ujumla wakathibisha ukweli wake.

Bukhari katika Sahih yake, Jz. ya 4 na 5; Abdi katika Jam-e-Bainu’s–Sihahi’s-Sitta, Jz. Ya 2, Baihaqi katika Sunan uk. 9 na 224; Tirmidhi katika Jam’i; Juz 2, uk. 135, Abu Dawud katika Sunan, Khawarizmi katika Manaqib; Shukani katika Tafsir Juz. 11, uk. 319, Ibn Maghazili katika Manaqib, Faqih Shafi’i’ katika Fadha’il yake, Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibu’s-Su’ul uk. 17; Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l- Mawadda Sura ya 18, Muhibu’d-Din Tabari katika Riyazu’n-Nazara uk. 147 na Dhakha’iru’I-Uquba uk. 69, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira Khawasu’I-Umma uk. 22, Imam Abdu’r-Rahman Nisa’i (mmoja wa Maimam wa Sihah) katika Khasa’isul-Alawi uk. 14 (ameandika hadithi sita zinazohusiana na suala hili); Ibn Kathir katika Ta’rikh-e-Kabir Juz. 5, uk. 38 na Juz. 7, uk. 357 Ibn Hajar Asqalani katika Isaba Juz. 11 uk. 509, Jalalu’d- Din Suyuti katika Durru’I-Mansur Juz. 3, uk. 208, ( katika Sherehe juu ya Aya ya kwan- za ya Bara’a) Tabari katika Jam’uI-Bayan, Juz . 10, uk. 41, (katika Sherehe ya Bara’a); Imam Tha’labi katika Tafsiri-e-Kashfu’I-Bayan, Ibn Kathir katika Tafsir Juz. 11 uk. 333; Alusi katika Ruha’l-Ma’ani Juz 3, uk. 268, yule mkaidi, Ibn Hajar Makki katika Sawa ‘iq uk. 19 Haithami katika Majma’u’z-Zawa’id Juz. 7, uk. 29, Muhammad Bin Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib uk. 125 Sura ya 62 (akisimulia kutoka kwa Abi Bakr na Hafiz Abi Nu’aim na kutoka kwenye Musnad ya Hafiz Damishqi kama ilivyosimuliwa na Abi Nu’aim katika njia tofauti); Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, Juz. 1 uk 3 na 151, Juz. 3, uk. 283 na Juz IV uk. 164-5; Hakim katika Mustadrak, Juz. 2, Kitab Maghazi uk. 51 na katika Juz. 2 ya kitabu hicho hicho uk. 331; Mulla Ali Muttaqi in Kanzu’l-Ummal, Juz. 1 uk 246 mpaka 249 na Fadha’il-i-Ali Juz. 6, uk. 154.

Sababu Ya Kuteuliwa Ali.

Seyyed Abdu’l-Hayy: Kwa nini Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye vitendo vyake vina- tokana na Allah, asimpangie Ali kazi hii tangu mwanzo? Muombezi: Kwa vile hakuna sababu juu ya ukweli huu zilizoandikwa, sisi hatujui. Lakini maoni yangu ni kwamba mabadiliko haya yamekusudiwa kuonyesha ubora wa Ali. Kwa kiwango chochote, kwa hakika inatengua lile dai la umri au uzoefu wa kisiasa kuwa ndio zilizokuwa sababu za kumuondoa Ali katika Ukhalifa. Kama Ali angeteuliwa katika kazi hii mwanzoni, lingeonekana ni jambo la kawaida, na isingewezekana kwetu sisi kuwathi- tishia ninyi ubora wa Ali.

Kama umri wa Abu Bakr na uwezo wa kisiasa vingethibitisha ubora wake asingeweza kurudishwa kwenye kazi kama hiyo. Lakini ukweli ni kwamba, kuwasilisha ujumbe wa utume ni kazi ya Mtume au Khalifa wake.

Hadithi Ya Kufuatana Ya Abu Bakr

Seyyed Abdu’l-Hayy: Kwa mujibu wa baadhi ya hadithi, Abu Huraira anasema kwamba Ali alikuwa ameagizwa kwenda Makkah pamoja na Abu Bakr kuwafundisha watu kanuni za Hijja. Ali alikuwa asome zila aya za Bara’a kwa watu. Kuwasilisha ujumbe wa utume kwa namna hii kunaashiria kwamba wote walikuwa cha cheo kinacholingana.

Muombezi: Kwanza, hii ni hadithi ya kughushi ya wafuasi wa Abu Bakr. Wengine hawakuisimulia hii. Pili, umma wote ulikubaliana kwamba Abu Bakr alirudishwa na nafasi yake ikachukuliwa na Ali. Jambo hili limesimuliwa kwa wingi sana katika vitabu vya hadithi vya madhehebu zote. Ni dhahiri, makubaliano ya umma wote ni kwamba ni lazima tutegemee kwenye zile hadithi ziliyosimuliwa kwa wingi na sahihi. Kama kuna hadithi ya peke inayotofautiana na hadithi sahihi, hiyo tuikatae.

Maoni haya yanashikiliwa na watu wote wenye msimamo na wasimuliaji. Kuteuliwa kwa Ali, kurudi kwa Abu Bakr katika hali ile ya huzuni na kukata tamaa, Mtukufu Mtume kumliwaza na kumridhisha yeye kwamba hayo yalikuwa ni matakwa ya Allah - yote haya ni mambo ya kweli ambayo yanakubalika kwa jumla.

Ushuhuda Mwingine Kwamba Umri Sio Kigezo Cha Ukhalifa:

Kuna ushahidi mwingine kwamba haki ya kipaumbele haina uhusiano wa umri. Haki ya upendeleo inapatikana katika elimu na Ucha-Mungu. Yeyote anayezidi katika elimu na Ucha-Mungu atastahiki upendeleo. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Watu wote ni wafu, lakini watu wenye elimu wako hai.” Kwa sababu hiyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimpa Ali nafasi ya kwanza miongoni mwa masahaba na akasema. “Ali ndio lango la elimu.” Ni wazi kwamba lango la elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lazima awazidi wengine.

Bila shaka, wale waswahaba wengine wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) waliobakia kuwa watiifu kwake, walikuwa wote ni watu waadilifu (wema). Daima hatukatai ile nafasi ya uadilifu wa Masahaba, lakini sifa zao haziwezi kuchukua ulinganisho na sifa za lango la elimu la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Mtukufu Mtume Alimtuma Ali Kwenda Yemen.

Wanazuoni wenu maarufu wameandika kwa kirefu juu ya Ali kutumwa kwenda Yemen kuwaongoza watu wa huko. Imam Abdu‘r-Rahman, Nisa‘i amesimulia hadithi sita kuhusu suala hili katika Khasa’isu’l-Alawi yake.

Vile vile Abu’I-Qasim Husain Bin Muhammad Raghib Ispahani katika Mahadhiratu‘l- Udaba yake Juz. 2, uk. 212 na wengine, wameandika kwamba wakati Mtukufu Mtume alipomuamuru Ali kwenda Yemen, Ali alijitetea kwamba alikuwa mdogo na alihisi namna ya uzito juu ya kuwekwa juu ya watu wazima wa kabila lake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu: “Hakika Allah atauongoza moyo wako na kuupa nguvu ulimi wako.”

Kama umri ulikuwa hitajio la kupendekezea, kwa nini basi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mbele ya Masahaba mashuhuri na watu wazima kama Abu Bakr, alimtuma Hadhrat Ali kwenda Yemen kuwaongoza watu kule?

Baada Ya Mtukufu Mtume Ali Alikuwa Ndiye Kiongozi Wa Umma

Akizungumza na Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.), Allah akasema katika Qur’ani Tukufu :

{اﻧﱠﻤﺎ اﻧْﺖ ﻣﻨْﺬِر ۖ وﻟﻞ ﻗَﻮم ﻫﺎدٍ {7

“Wewe ni muongozaji tu na (kuna) kiongozi kwa kila watu” (13:7)

Imam Tha’labi katika Tafsir-e-Kashfu‘I-Bayan yake; Muhammad Bin Jarir Tabari katika Tafsir yake; Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu‘t-Talib Sura ya 62, kutoka kwenye Ta’rikh-e-Ibn Asakir; Sheikh Suleyman Balkhi Hanafi katika Yanabiu‘I- Mawadda mwisho wa Sura ya 26 kutoka kwa Tha’labi, Hamwaini, Hakim, Abu’I-Qasim Haskani, Ibn Sabbagh Maliki, Mir Seyyed Ali Hamadani na Manaqib ya Khawarizmi, wakisimulia kwa idhini ya Ibn Abbas, Amiru’l-Mu’minin na Abu Buraid Aslami katika maneno tofauti, wamesimulia hadithi kumi na moja ambazo lengo lake kuu ni kwamba, wakati iliposhuka aya hiyo hapo juu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), akiweka mkono wake juu ya kifua chake mwenyewe, alisema; “Mimi ndiye yule muonyaji.” Kisha akiweka mkono wake kwenye kifua cha Ali, akasema: “Baada yangu mimi, wewe ndiye kiongozi wa Umma. Wale watakaopokea muongozo toka kwako watakuwa ndio walioongoka.”

Njama Za Maadui

Vile vile umesema baada ya miaka 25, wakati alipokuwa Khalifa, ilikuwa kutokana na ukosefu wake wa uzoefu katika Siasa kwamba ndipo machafuko na umwagaji damu ukatokea. Sina uhakika kwamba una maana gani unaposema siasa. Kama siasa ina maana ya udanganyifu, njama na kuchanganya haki na batili (kama vile watu katika zama zote walivyofanya ili kujipatia Mamlaka), ningeweza kukiri kwamba Ali alikuwa ametolewa mbali kabisa kwenye siasa ya namna hiyo. Kwangu mimi siasa ina maana ya uadilifu na utendaji wa mamlaka halali.

Ali Alichukia Siasa Ya Dhulma - Chafu:

Ali ambaye alikuwa ni mfano wa haki, alijitenga mbali na siasa za kidhalimu. Kama nilivyosema mapema, wakati Amiru‘l-Mu’minina aliposhika ukhalifa dhahiri, mara moja aliwaengua viongozi wote wa awali na watumishi. Abdullah Ibn Abbas (binadamu yake) na wengineo wakasema: “Ingekuwa vema kama ungeiahirisha amri hii kwa siku chache, ili kwamba viongozi na magavana na majimbo waukubali ukhalifa wako. Kisha unaweza kuwauzulu.”

Imam Mtukufu akasema: “Mmenipa ushauri kuhusu siasa ya jambo hili. Lakini hamuelewi kwamba endapo nitayumbishwa na kile kinachoitwa ‘Siasa’ na nikaruhusu watawala waonevu wabaki katika nafasi zao, ingawa iwe ni kwa muda mfupi tu, ningewajibika kuulizwa mbele za Allah kwa ajili ya kipindi hicho. Wakati wa kuulizwa, ningewajibishwa kwa hilo.

Hili haliwezi kutarajiwa kwa Ali.” Ili kurejesha haki, Ali aliamuru mara moja kuuzuliwa kwa watawala waonevu. Hatua hii ilisababisha kuwepo upinzani toka kwa Mu’awiya Talha, Zubair na wengine ambao walipanga maasi na kusababisha ghasia kubwa na umwagaji wa damu katika nchi. Enyi waungwana! Hamlielewi vizuri hili jambo. Kwa vile hamkufanya uchunguzi wa suala hili, mnapotoshwa na wanapropaganda wanaodai kuwa yale maasi wakati wa ukhalifa wa Ali yalitokana na kukosa kwake kuwa na ujuzi wa siasa. La hasha. Kulikuwa na agenda zingine zikifanya kazi.

Vurugu Wakati Wa Ukhalifa Wa Amirul-Mu’minin Zilitokana Na

Uadui Dhidi Yake.

Kwanza, kwa muda wa miaka 25 watu walikuwa wameshawishiwa kumpinga Ali. Ilikuwa ni vigumu kwa hiyo kukubali uandamizi na Ukhalifa wake au kuitambua hadhi yake kubwa. Mfano wa upinzani huu ulitokea katika siku ya kwanza ya ukhalifa wake.

Mtu maarufu mmoja aliingia kwenye lango la Msikiti, na alipomuona Imam juu ya mimbari, akakemea: “Nalipofuke jicho lile ambalo linamuona Ali juu ya mimbari badala ya Khalifa Umar!”

Pili. haikuwa rahisi kwa watu wenye tamaa ya dunia kukubali uadilifu wa Ali, hasa kwa vile matamanio yao yalikwishapewa mwanya huru wakati wa Ukhalifa wa Uthman. Kwa hiyo walisimamisha upinzani dhidi yake, ili kwamba mtu ambaye angetimiza haja zao angewaza kutwaa madaraka.

Matakwa yao yalitimilizwa wakati wa Ukhalifa wa Mu’awiya. Kwa hiyo, Talha na Zubair mwanzoni walitoa kiapo cha utii kwa Ali, lakini walipoona haja zao za kutaka mamlaka hazikutimizwa, wakavunja kiapo chao na wakampinga waziwazi katika vita vya Ngamia (Jamal).

Aisha Kwa Kiasi Kikubwa Alihusika Sana Na Maasi Dhidi Ya Ali

Tatu, historia inatuambia kuhusu ni nani hasa aliyekuwa mchochezi mkuu wa machafuko kuanzia mwanzoni mwa Ukhalifa huo. Je, alikuwa ni mwingine yeyote mbali na Ummu’l- Mu’min Aisha? Hakuwa ni Aisha ambaye kulingana na kauli za wapokezi wa Sunni na Shi’ah kwa pamoja, aliyepanda Ngamia (kinyume na amri ya wazi ya Allah na Mtume wake Mtukufu kwamba akae ndani ya nyumba yake) akafika Basra na akachochea vita kubwa sana?

Unadai kwamba vita vilivyoleta madhara kwa pande zote vilitokana na Ali kukosa upeo wa kisiasa. Hii ni kauli yenye kupotosha sana. Kama Aisha asingefanya maasi dhidi yake, hakuna hata mtu mmoja ambaye angeweza kuwa na ujasiri wa kumpinga Ali, baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuwa amekwishatangaza wazi kuwa “Kupigana dhidi ya Ali ni kupigana dhidi yangu.” Aisha aliwachochea watu kupigana dhidi ya Ali.

Vita Vya Ali Vya Jamal, Siffin Na Nahrwan Vilikuwa Kama Vita Vya Mtukufu Mtume Dhidi Ya Makafiri.

Vita vya Ali dhidi ya maadui na wanafiki huko Basra, Siffin na Nahrwan vilikuwa kama vile vita vya Mtukufu Mtume dhidi ya makafiri.

Sheikh: Ilikuwaje vita dhidi ya Waislamu viwe kama vita dhidi ya makafiri?

Muombezi: Ulamaa wenu mashuhuri kama Ahmad Bin Hanbal katika Musnad yake, Sibt Ibn Jauzi katika Tadhkira, Sulayman Bakhri katika Yanabiu’I-Mawadda, Imam Abdur-Rahman Nisai katika Khasa’isu’l-Alawi; Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibu’s- Su’ul; uhammad bin Talha Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib Sura ya 37, na Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahjul-Balagha wameandika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitabiri vita vya Ali dhidi ya “Nakisin, “Qasitin” na “Mariqin” miognoni mwao “nakisin” ilimaanisha Talha, Zubair na wafuasi wao; “Qasitin” ilimaanisha Mu’awiya na wafuasi wake, na “Mariqin” ilimaanisha Khawarij (waliojitoa) wa Nahrwan.

Wote kwa pamoja walikuwa ni waasi ambao kuuwawa kwao kulikuwa ni halali na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliamuru adhabu hiyo hiyo juu yao wakati alipobashiri mapigano ya vita hivyo.

Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib sura ya 37, amesimulia hadithi toka kwa Sa’id Bin Jabir, ambaye ameisimulia hadith hii kutoka kwa Ibn Abbas, kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ummu Salma: “Huyu ni Ali Bin Abi Talib. Nyama yake ni nyama yangu, damu yake ni damu yangu, na yeye kwangu, ni kama Harun alivyokuwa kwa Mussa isipokuwa tu kwamba hakutakuwa na Mtume baada yangu.

Umm Salma, huyu Ali ni kiongozi wa walioamini, ni kiongozi wa Waislam, ndiye hafidhi wa elimu yangu, mshikamakamu (mwandamizi) wangu na lango la elimu. Ni Ndugu yangu katika dunia hii na Akhera, yuko nami katika sehemu iliyotukuka mno, atapigana dhidi “Nakisin” “Qasitin” na “Mariqin.”

Baada ya kusimulia hadithi hii Muhammad Bin Yusuf anasema kwamba haidthi hii inathibitisha kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amemjulisha Ali kuhusu vita hivyo dhidi ya makundi yale matatu na kwamba alikuwa amemuamuru Ali kupigana dhidi ya makundi haya matatu. Makhnaf Bin Salim anasemekana kwamba alisema kuwa wakati Abu Ayyub Ansari (aliyekuwa sahaba maarufu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa akienda na jeshi kupigana katika vita hivyo, alisema “Abu Ayyub! Ajabu iliyoje juu yako! Wewe ni yule yule mtu aliyepigana dhidi ya washirikina katika upande wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), lakini sasa hivi umejipinda kupigana dhidi ya Waislam!” Kisha Abu Ayyub akasema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliniamuru mimi nipigane dhidi ya makundi haya matatu: nayo ni akina Nakisin, Qastin na Mariqin,”

Imam Abdu’r –Rahman Nisa’i katika Khasa‘isul’l-Alawi, hadithi ya 155, akisimulia kuto- ka kwa Abu Sa’id Khadiri na Sulayman Balhi Hanafi katika Yanabi uk. 59 (sura ya 2) kutoka kwenye Jam’u’l-Fawaid anasema kwamba Abu Sa’id amesema: “Tulikuwa tumekaa na Masahaba, tukimsubiri Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa anakuja kuelekea kwetu, tuliona kuwa bakozi ya kiatu chake imevunjika. Alibwaga kiatu chake kwa Ali, ambaye alianza kukirekebisha. Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: Hakika, kuna mmoja kati yenu ambaye atapigana kutetea tafsir halisi ya Qur’ani Tukufu kama nilivyopigana (dhidi ya Makafiri).”

Kisha Abu Bakr akasema: “Mtu huyo ni mimi?” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “La” Kisha Umar akasema: “Je, ni mimi?”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema; “La! Ni yule mtu anayerekebisha viatu vyangu. Hadithi hii inaonyesha kwamba vita vya Ali vilipiganwa kwa ajili ya tafsiri halisi ya Qur’ani Tukufu. Kwa hiyo ina maana kwamba, ghasia za watu wakati wa ukhalifa wa Ali hazikuwa kutokana na udhaifu wa kisasa wa Amiru’l-Mu’minin bali zilitokana na uadui wa wapinzani wake. Baada Ya Mtukufu Mtume Ali Alikuwa Ndiye Bingwa Zaidi Wa Mambo

Ya Utawala

Ninyi waungwana mnaweza kuona kwamba inaelimisha zaidi kuyachunguza maagizo Ali aliyoyatuma kwa magavana wake na maofisa wa kijeshi na kiraia. Kwa mfano, zile amri na maagizo aliyotuma kwa Malik Ashtar na Muhammad Bin Abu Bakr kwa ajili ya kuitawala Misri, kwa Uthman Bin Hunaif na Abdullah bin Abbas wa Basra, na kwa Qutham bin Abbas kwa ajili ya kuiongoza Makkah ni mifano ya uongozi bora wa Umma na vile vile haki ya jamii. Nyaraka hizi ni sehemu ya Nahjul’Balagha.

Ali Alikuwa Na Elimu Ya Ulimwengu Wa Ghaib

Ukweli huu umekubaliwa wote, wafuasi wa Ali na maadui zake. Huyu Imam Mtukufu alikuwa ni Imamu’l- Muttaqin (Kiongozi wa wacha Mungu). Alikuwa na elimu kamili ya maana ya Qur’ani Tukufu. Zaidi ya hayo, alikuwa na elimu ya Ghaib.

Sheikh: Haijaniingia akilini vizuri hii kauli yako isiyoeleweka kwamba Ali alikuwa na elimu ya Ghaib. Tafadhali hebu ielezee.

Muombezi: Hakuna utata wowote ndani yake. Kupambanukiwa na Ghaib, maana yake ni kujua siri za ulimwengu (mbingu na Ardhi), ambazo zilijulikana kupitia Neema Tukufu kwa Mitume wote na waandamizi wao. Kila mmoja alipewa kiasi cha elimu ya Ghaib kama Allah alivyoona inatosheleza kwao kwa ajili ya kufikisha ujumbe Wake. Baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Amiru’l-Mu’minin alijaaliwa na elimu kama hiyo.

Sheikh: Kamwe sikutegemea kama utashikilia maoni ya wale Shi’ah wakorofi. Sifa hii imezidi mno kiasi kwamba hata huyo anayesifiwa asingeikubali. Kuwa na elimu ya Ghaib ni sifa inayomhusu Allah peke yake, hakuna katika viumbe vyake anayeweza kuwa na uhusiano nayo.

Muombezi: Kuamini kwamba Mitume wakubwa, na washikamakamu wao, na watumishi wengine watukufu wa Allah walikuwa na elimu ya Ghaib hakuna chochote kinachohusiana na ukorofi. Bali hasa, ilikuwa ni moja ya sifa zao, iliyoonyesha kujitoa kwao kwa Allah. Tunao ushahidi wa wazi wa ukweli huu kutoka kwenye hadithi na Qur’ani Tukufu.

Je Elimu Ya Ghaibu Imetengwa Kwa Allah Tu?

Sheikh: Qur’ani Tukufu inapingana na kauli yako. Muombezi: unaweza kuzzsoma Aya hizo ambazo zinapingana na kauli yangu? Sheikh: Kuna Aya nyingi ndani ya Qur’ani Tukufu, ambazo zinaunga mkono maoni yangu. Kwa mfano, Qur’ani Tukufu inasema:“Na ziko kwake funguo za (mambo) yaliyofichikana hakuna anayezijua ila Yeye tu, na anajua yaliyomo barani na baharini, na halianguki jani ila analijua, wala punje ndani ya giza la ardhi, wala chochote cha kijani au kikavu bali yote yamo ndani ya kitabu kidhihirashacho.” (6:59)

Huu ndio ushahidi unaotosheleza sana kwamba hakuna hata mmoja ila ni Allah tu mwenye elimu ya Ghaib.

Ikiwa mtu ataamini mtu mwingine yeyote kuwa na elimu ya Ghaib, amemfanya mmoja wa viumbe Wake kuwa mshirika katika sifa za Allah. Unadai kwamba Ali alikuwa na utambuzi wa yaliyo ghaib.

Hii ina maana kwamba mbali na kumfanya kwako yeye ni mshirika katika sifa za Allah, umekifanya cheo chake kuwa ni cha juu zaidi kuliko kile cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alirudiarudia kusema: “Mimi ni mtu kama ninyi.

Allah pekee ndie aijuaye Ghaib.” Mtukufu Mtume kwa uwazi kabisa alielezea kutokuwa kwake na elimu ya Ghaib. Umeisoma Aya ya Qur’ani inayosema:

{ﻓَﻤﻦ ﻛﺎنَ ﻳﺮﺟﻮ ﻟﻘَﺎء رﺑِﻪ ﻓَﻠْﻴﻌﻤﻞ ﻋﻤً ﺻﺎﻟﺤﺎ و ﻳﺸْﺮِكْ ﺑِﻌﺒﺎدة رﺑِﻪ اﺣﺪًا {110

“Waambie: Bila shaka mimi ni binaadamu tu kama nyie, ninaletewa Wahyi kwamba Mungu wenu ni Mungu Mmoja tu.....” ( 18:110).

Hii ni kwamba, yaani tofauti pekee kati yenu na mimi ni kwamba, ufunuo (Wahy) kutoka kwa Allah unakuja kwangu mimi.

Mahali pengine Allah anasema:

ﻗُﻞ  اﻣﻠﻚُ ﻟﻨَﻔْﺴ ﻧَﻔْﻌﺎ و ﺿﺮا ا ﻣﺎ ﺷَﺎء اﻟﻪ ۚ وﻟَﻮ ﻛﻨْﺖ اﻋﻠَﻢ اﻟْﻐَﻴﺐ ﺳﺘَﺜَﺮت ﻣﻦ اﻟْﺨَﻴﺮِ وﻣﺎ ﻣﺴﻨ اﻟﺴﻮء ۚ انْ {اﻧَﺎ ا ﻧَﺬِﻳﺮ وﺑﺸﻴﺮ ﻟﻘَﻮم ﻳﻮﻣﻨُﻮنَ {188

“Sema: Mimi sina mamlaka ya kujipa nafuu wala ya kujiondolea madhara ila kama apendavyo Allah; na kama ningejua ya Ghaib, bila shaka ningejizidishia mema mengi, wala lisingelinigusa dhara. Mimi sio lolote bali ni muonyaji na mtoaji wa habari njema kwa watu wanaoamini. “ (7:188)

Na tena anasema:

{و اﻗُﻮل ﻟَﻢ ﻋﻨْﺪِي ﺧَﺰاﺋﻦ اﻟﻪ و اﻋﻠَﻢ اﻟْﻐَﻴﺐ{31 “Wala sikuambieni kwamba nina hazina za Allah, wala kwamba nayajua mambo ya ghaib” (11:31).

Allah anasema tena:

{ﻗُﻞ  ﻳﻌﻠَﻢ ﻣﻦ ﻓ اﻟﺴﻤﺎواتِ وارضِ اﻟْﻐَﻴﺐ{65

“Hakuna hata mmoja katika mbingu na ardhi anayejua yaliyoko ghaibuni ila Allah: Na hawajui ni lini watafufuliwa (27:65)

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe alikiri kwamba alikuwa hajui ya ghaib na kwamba elimu yake ilikuwa kwa Allah pekee tu. Unawezaje kudai kamba Ali alikuwa na elimu kama hiyo?

Imani yako ni jaribio la kuukweza ubora wa Ali kuliko ule wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Je, Qur’ani Tukufu haisemi:

{وﻣﺎ ﻛﺎنَ اﻟﻪ ﻟﻴﻄْﻠﻌﻢ ﻋﻠَ اﻟْﻐَﻴﺐِ{179

“Wala hakuwa Allah ni mwenye kuwajulisha yaliyo ghaib…” (3:179).

Ni kwa msingi gani wewe unaamini kwamba kuna yeyote, isipokuwa Allah, analiye na elimu ya ghaib?

Muombezi: Utangulizi wa maelezo yako ni sahihi. Lakini umaliziaji uliochukua una makosa. Umesema kwamba mjuzi wa Ghaib ni Allah; kwamba funguo za Ghaib anazo Allah Mwenye nguvu, na kwamba kwa mujibu wa ile aya ya mwisho ya Sura ya Al-Kahf (pango), mwisho wa Mitume, Mitume wengine wote, wandamizi (warithi) wao, na Maimam watukufu walikuwa ni sawa na binaadamu wengine. Katika maumbile yao ya kimwili waliumbwa kama wengine wote.

Mambo yote haya ni kweli, na madhehebu ya Shia inayakubali yote. Pia, aya zote ulizozisoma ni za kweli hasa katika fuo lake halisi. Lakini haya maneno “Mtukufu Mtume ” kutoka kwenye Sura ya Hud yanaashiria kwa Mtume Nuhu. Aya ya 50 ya Sura ya Al-An’am (Ng’ombe) inaashiria kwa Mtume wetu aliyetukuka. Wakati makafiri walipomuuliza ni kwa nini hakukuwa na dalili zozote za yeye kuwa na hazina za Mwenyezi Mungu au elimu ya yaliyoghaib, hii ikateremshwa.

{ﻗُﻞ  اﻗُﻮل ﻟَﻢ ﻋﻨْﺪِي ﺧَﺰاﺋﻦ اﻟﻪ و اﻋﻠَﻢ اﻟْﻐَﻴﺐ و اﻗُﻮل ﻟَﻢ اﻧّ ﻣﻠَﻚٌ ۖ انْ اﺗﱠﺒِﻊ ا ﻣﺎ ﻳﻮﺣ اﻟَ ۚ{50

“Sema! Mimi siwaambii kwamba ninazo hazina za Allah, wala ninayajua ya Ghaib, wala siwaambii kwamba mimi ni malaika, sifuati lolote ila kile kilichofunuliwa kwangu .....”(6:50)

Aya hii ilikuwa ni majibu kwa ile dhana potofu kwamba matendo ya Mtume yanaweza kuathiriwa na mtazamo wa tamaa za kidunia. Na kuhusu elimu ya ghaib, tunaamini kwamba Mitume na washikamakamu wao walikuwa nayo. Siwahusishi na sifa za Allah. Lakini zawadi hii ni sehemu ya wahyi na Ilham (Wahai na msukumo kutoka kwa Allah ) ambavyo viliondoa mapazia ya ujinga toka kwenye uono wao na kufichua ukweli kwao. Nitaelezea hii kwa kirefu.

Elimu Ni Ya Namna Mbili, Ya Dhati (Ya Asili) Na Arzi (Ya Kutafuta)

Sisi Shi’ah wa madhehebu ya Imamiyya tunaamini kwamba elimu ina namna mbili: Dhati na Arzi. Elimu ya Dhati au ya asili ni makhususi kwa Allah. Tunaweza kuitambua lakini hatuwezi kuufahamu ukweli wake. Kwa njia yoyote tutakayoweza kujaribu kuieleza, elimu ya asili iko nje ya ufahamu wa wanaadamu. Arzi, au elimu ya kutafuata ni ile ambayo kwa asili yake mwanadamu hanayo, Ima awe ni Mtume au la. Anakuja kunufaika nayo baadae. Elimu hii pia ni ya aina mbili: Tahsili na ladunni. Tahsili ni ile elimu inayopatikana kwa kusoma na uzoefu.

Ikiwa mwanafunzi ataandamana na utaratibu wa kawaida wa elimu, kwa mfano, anakwenda shule na anajifunza toka kwa mwalimu wake. Kama Allah akipenda, atapata elimu kulingana na juhudi zake za ule muda atakaoutumia kwa kujifunza.

Ladunni inarejea kwenye ile elimu ambayo mtu anaipokea moja kwa moja kutoka kwa Allah. Haijifunzi kupitia kwenye herufi na maneno bali anaipokea moja kwa moja toka kwa Mwenye ukarimu wote. Allah anasema katika Qur’ani:

{وﻋﻠﱠﻤﻨَﺎه ﻣﻦ ﻟَﺪُﻧﱠﺎ ﻋﻠْﻤﺎ {65

“Na ambaye tulimfundisha elimu itokayo kwetu.” (18:65)

Shi’ah hawadai kwamba elimu ya ghaib ilikuwa ni ya asili ndani ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) au maimam au kwamba wao waliielewa kama anavyoielewa Mwenyezi Mungu. Tunachokisema ni kwamba Allah hayuko hakufungika au kuwa na mipaka.

Anaweza kutoa elimu na mamlaka kwa yeyote amtakae. Wakati mwingine hutoa elimu mwa mtu kwa njia ya mwalimu na wakai mwingine moja kwa moja kutoka kwake. Hii elimu ya kupewa moja kwa moja inaitwa elimu ya ghaib. Sheikh: Maelezo yako ya awali ni sahihi. Lakini utashi wa ki-Ungu hauwezi kuruhusu mambo yasiyo ya kawaida kama kumpa mtu elimu ya ghaib moja kwa moja, yaani, bila ya uwakala wa mwalimu.

Muombezi: Hapana, wewe na marafiki zako mmekosea. Kwa hakika mara kwa mara, bila kujua, mnapingana na wengi wa wanazuoni wenu mashuhuri. Allah aliweka juu ya Mitume wake wote na waandamizi wao elimu ya ghaib. Chochote kilichohitajika kwao ili kutekeleza kazi zao. Sheikh: Kwa kukabiliana na aya hizi za Qur’ani Tukufu, ambazo kwa uwazi kabisa zinakataa wazo la elimu ya ghaib ya mtu, una ushahdi gani kwa kutia nguvu hoja yako hiyo?

Muombezi: Hatuko kinyume na aya hizo za Qur’ani Tukufu. Kila aya ya Qur’ani tukufu ilishushwa kwa sababu maalum ambayo, kulingana na mazingira, ilikuwa wakati mwingine kinyume na wakati mwingine kwa hakika yake (positive).

Hii ndio maana inasemekana kwamba miongoni mwa aya za Qur’ani Tukufu, aya moja inaipa nguvu nyingine. Kwa vile makafiri mara kwa mara walidai miujiza kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), zile aya za kinyume zilizotajwa hapo juu zikashushwa. Ili kuthibitisha lengo halisi aya zenye kujihakiki pia zilshushwa ili kwamba hali iweze kueleweka.

Ushahidi Wa Qur’ani Kwamba Mitume Walikuwa Na Elimu Ya Ghaib

Sheikh: Hii ni ajabu sana. Unasema kwamba kuna ushahidi wa uhakika ndani ya Qur’an kwamba Mitume walikuwa na elimu ya ghaib. Tafadhali zisome aya hizo.

Muombezi: Usishikwe na mshangao. Wewe unazijua.

Allah Mwenye nguvu zote anasema:

{ﻋﺎﻟﻢ اﻟْﻐَﻴﺐِ ﻓََ ﻳﻈْﻬِﺮ ﻋﻠَ ﻏَﻴﺒِﻪ اﺣﺪًا {26

{ا ﻣﻦ ارﺗَﻀ ﻣﻦ رﺳﻮلٍ ﻓَﺎﻧﱠﻪ ﻳﺴﻠُﻚُ ﻣﻦ ﺑﻴﻦ ﻳﺪَﻳﻪ وﻣﻦ ﺧَﻠْﻔﻪ رﺻﺪًا {27

{ﻟﻴﻌﻠَﻢ انْ ﻗَﺪْ اﺑﻠَﻐُﻮا رِﺳﺎتِ رﺑِﻬِﻢ واﺣﺎطَ ﺑِﻤﺎ ﻟَﺪَﻳﻬِﻢ واﺣﺼ ﻛﻞ ﺷَء ﻋﺪَدا {28

“Ni mjuzi wa yaliyo ghaib! Hivyo hamfichulii yeyote siri zake, ila kwa Mtume ambaye amemridhia; basi kwa hakika humwekea walinzi (watembee) mbele yake na nyuma yake, ili aweze kujua (mtume) kwamba wamekwisha fikisha ujumbe wa Mola wao, na Yeye anayajua yale waliyonayo, na amedhibita idadi ya vitu vyote.” (72:26-28)

Aya hii inaonyesha kwamba Mitume watukuka wa Allah ambao wamejaaliwa na elimu ya ghaib ni wa namna yao pekee.

Pili, ile aya ya Sura ya familia ya Imran, sehemu yake ambayo umeisoma, inathibitisha hoja yangu. Aya nzima inasomeka kama ifuatavyo: “Wala hakuwa Allah kuwajulisheni ya ghaib, lakini Allah humchagua katika Mitume wake yule anayempenda, kwa hiyo muamini Allah na Mtume wake, kama mtaamini na mkamcha mungu, basi mtakuja kupata malipo makubwa.” (3: 179)

Aya hizi zote zinaonyesha wazi kwamba Mitume wa Allah walipewa elimu ya ghaib. Ikiwa hakuna yeyote isipokuwa Allah, aliyekuwa na elimu ya ghaib, hiki kifungu “anachagua katika Mitume wake yule ampendaye.” Kingeuwa hakina maana yoyote. Allah anasema katika Sura ya Hud:

{ﺗﻠْﻚَ ﻣﻦ اﻧْﺒﺎء اﻟْﻐَﻴﺐِ ﻧُﻮﺣﻴﻬﺎ اﻟَﻴﻚَ ۖ ﻣﺎ ﻛﻨْﺖ ﺗَﻌﻠَﻤﻬﺎ اﻧْﺖ و ﻗَﻮﻣﻚَ ﻣﻦ ﻗَﺒﻞ ﻫٰﺬَا ۖ ﻓَﺎﺻﺒِﺮ ۖ انﱠ اﻟْﻌﺎﻗﺒﺔَ ﻟﻠْﻤﺘﱠﻘﻴﻦ {49

“Hizi ni katika habari za ghaib tunazokufunulia wewe, ulikuwa huzijui; wewe wala watu wako kabla ya hii (Qur’ani kuteremshwa). Kwa hiyo kuwa na subira, hakika mwisho (mwema) ni wa wale wamchao (Mwenyezi Mungu).” (11:49)

Katika Sura ya Shura Yeye anasema:

وﻛﺬَٰﻟﻚَ اوﺣﻴﻨَﺎ اﻟَﻴﻚَ روﺣﺎ ﻣﻦ اﻣﺮِﻧَﺎ ۚ ﻣﺎ ﻛﻨْﺖ ﺗَﺪْرِي ﻣﺎ اﻟْﺘَﺎب و اﻳﻤﺎنُ وﻟَٰﻦ ﺟﻌﻠْﻨَﺎه ﻧُﻮرا ﻧَﻬﺪِي ﺑِﻪ ﻣﻦ ﻧَﺸَﺎء ﻣﻦ {ﻋﺒﺎدِﻧَﺎ ۚ واﻧﱠﻚَ ﻟَﺘَﻬﺪِي اﻟَ ﺻﺮاط ﻣﺴﺘَﻘﻴﻢ {52

“Na hivyo ndivyo tulikushushia Wahiy kwa amri yetu. Ulikuwa hujui kitabu ni nini, wala imani (ni nini), lakini tumekifanya (Kitabu hiki) ni nuru, kwayo tunamuongoza tumtakaye katika waja wetu .....” (42:52)

Kama elimu ya ghaib isingekuwepo duniani, ni vipi Mitume walifichua mambo yanasio- julikana na kuwaambia watu juu ya maisha yao ya siri? Je, hakimo ndani ya Qur’ani kile Isa (a.s) alichosema kwa wana wa Israeli?

{واﻧَﺒِﯩﻢ ﺑِﻤﺎ ﺗَﺎﻛﻠُﻮنَ وﻣﺎ ﺗَﺪﱠﺧﺮونَ ﻓ ﺑﻴﻮﺗﻢ ۚ{49

“Na niwape habari na mnachokula na kile mnachokiweka akiba katika nyumba zenu ..... (3:49)

Kama nitasoma aya zote za Qur’ani Tukufu, zinazounga mkono ukweli huu, itaweza kuchukua muda mrefu. Kiasi hiki kinaelekea kutosheleza.

Sheikh: Maelezo kama haya yanawapa moyo wapiga ramli, wabashiri, watazama viganja na watazamia vyota na waongo wengine wanaowadanganya watu na kujaza mifuko yao na pesa.

Madai Ya Kuwa Na Elimu Ya Ghaib Kupitia Njia Nyinginezo Ni Ya Uongo.

Muombezi: Imani katika kweli haielekezi kwenye matokeo mabaya: Ni ujinga wa watu unaowateka nyara. Kama Waislam wangemfuata yule mwenye elimu, kwa mujibu wa maelekezo ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hasusan kama wasingelitelekeza lile lango la elimu kuanzia mwanzo kabisa, wasingeliweza kuangukia mateka kwa watu waovu. Qur’ani Tukufu inasema wazi: “Yoyote yule amchaguaye kati ya

Mitume.” Neno mtume linaonyesha dhahiri kwamba kuna waja wataule wa Allah ambao wanapokea elimu ya ghaib moja kwa moja kutoka Kwake bila ya kupata kujifunza kupitia njia za kawaida.

Endapo mtu yoyote, ambaye sio mtume au Imam atadai kwamba anaweza kutabiri mambo ya ghaibu kwa njia ya falaki, utazamia viganja au kutupa simbi kuelezea bahati, huyo ni muongo. Waislam wa kweli, ambao wanafuata Qur’ani Tukufu kamwe hawawaamini watu kama hao, wala hawawi mawindo ya ulaghai wao kwani wanajua kwamba hawapaswi kufuata chochote ila Qur’ani Tukufu na wabebaji na wafasiri wa Qur’ani Tukufu, yaani, Mtukufu Mtume Muhammad (s.a.w.w.) na kizazi chake, ambao wanalingana na Qur’ani.

Kwa kifupi, ikiwa yeyote isipokuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na waandamizi wake watoharifu atadai kwamba anayo elimu ya ghaibu na akasema kwamba anaweza kutabiri matukio ya baadae, yeye ni mbabaishaji, kwa njia yoyote ile atakayochukua.

Waandamizi Wa Mitume Pia Walikuwa Na Elimu Ya Ghaib.

Sheikh: Kwa vile Mitume walipokea wahyi takatifu walikuwa kulingana na kauli yako wana elimu ya Ghaib. Lakini kwani Ali naye alikuwa Mtume? Au alihusishwa na shughuli za utume ambazo kwazo alijua mambo ya ghaibu?

Muombezi: Kwanza, kwa nini unatupotosha sisi kwa kutumia maneno “kulingana na kauli yako?” Badala ya hayo kwa nini usitumie maneno “kulingana na kauli ya Allah.” Sisemi lolote kwa hiari yangu. Ninazungumzia hukumu za Qur’an Tukufu na kwa misingi ya maeleo ya mfasiri wa Qur’ani Tukufu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ninatoa ile maana yake halisi.

Nimewasilisha kwenu, kwa misingi ya ushahidi wa Aya za Qur’an, Mitume na manabii wa Allah walikuwa watu watukufu mno na walikuwa na elimu ya ghaib. Wanazuoni wenu wenyewe mashuhuri wameukubali ukweli huu na wamelazimika kusimulia mifano ya Mtukufu Mtume kuwa na elimu ya ghaib. Ibn Abi’l-Hadid Mut’azali katika Sharh-e-Nahjul- Balagha Juz. 1, uk. 67 (kilichochapish- wa Misri), anaandika hadithi kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba alimuambia Ali: “Baada yangu, utapigana dhidi ya Nakisin, Qasistin na Mariqin.” Anasema kwamba hii ni moja ya uthibitisho wa Utume wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa sababu inatabiri wazi wakati ujao usiojulikana. Matukio yaliyotabiriwa yalitokea karibuni miaka 30 baadae, vilevile haswa kama yalivyotangulia kuelezwa. Pili, Shi’ah hawadai kamba Amiru‘l-Mu’minin au Maimam Watukufu walikwa Mitume. Tunaamini kwamba Muhammad alikuwa ndiye Mtume wa mwisho wa Allah. Hakuna hata mmoja aliyeshirikishwa naye katika utume. Tunaamini kwamba, ikiwa yeyote angekuwa na imani kinyume na hii, basi huyo sio muumini. Bila shaka, sisi tunaamini katika ule Uimam ki-Mungu aliopewa Ali na kuwatambua (kuwachukulia) watu kumi na moja katika kizazi chake kama Maimam wetu watukufu na Waandamizi wa haki na Makhalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Tunaamini kwamba Allah Mwenye nguvu zote amewajaalia wao na elimu ya ghaib kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Tunaamini kwamba uoni wa watu wa kawaida umewekewa pazia hivyo kwamba wanaweza kuona tu vitu vyenye kuonekana. Kadhalika hivyo ndio ilivyokuwa kwa mitume na mawasii ila kwamba, kulingana na wakati na mazingira, Allah, Mjuzi wa yote, aliliondoa pazia na akafichua habari muhimu kwao kutoka kwenye ulimwengu wa ghaib.

Na wakati elimu ya Ghaib ilipokuwa sio ya lazima, lile pazia liliwatenga wao pia na huo ulimwengu mwingine.

Hivyo, wakati mmoja Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Kama ningejua ya ghaib, kweli kabisa ningeweza kuwa na wingi wa mazuri.” Yaani, kwa asili hasa, alikuwa hana elimu ya ghaib. Aliijua tu wakati ambapo, kwa rehema za Allah, pazia hilo lilipofunuliwa.

Sheikh: Ni vipi na ni wapi ambapo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anawapa watu habari kuhusu ghaib?

Muombezi: Kwa kuzingatia aya ya Qur’ani ambayo kwayo tayari nimekwishairejea, wewe unamfikiria kwamba Muhammad ni mwisho wa Mitume, ni Murtaza (aliyechaguli- wa) na ni Mtume wa kweli wa Allah?

Sheikh: Hilo ni swali la ajabu. Ni dhahiri kabisa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ndiye mchaguliwa na wa mwisho wa Mitume.

Muombezi: Basi kwa mujibu wa aya hii tukufu: “Mjuzi wa yaliyo ghaib! Hivyo habain- ishi siri zake kwa yeyote ila kwake yule ambaye anamchagua kuwa Nabii” basi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa anayo elimu ya ghaib. Aya hii inasema wazi kwamba Allah hutoa elimu Yake ya ghaib kwa mtume wake aliyemchagua.

Sheikh: Ukichukulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa na elimu ya ghaib, hii inahusiana vipi na madai yako kwamba Ali alikuwa na elimu hii ya ghaib pia?

Muombezi: Tena, kama ninyi watu mtachunguza kwa busara zile hadithi sahihi na Sunna za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mtaweza kuelewa haraka sana ukweli kuhusu hili na mambo mengine mengi.

Sheikh: Kama ujuzi wetu una mpaka, kwa neema za Allah, wewe unayo akili pana na ulimi fasaha. Tafadhali tusimulie hizo hadithi zinazothibitisha kwamba Ali alikuwa na elimu ya ghaib. Kama elimu ya ghaib ni muhimu kwa mawasii wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kusingekuwa na ubaguzi katika hali hii. Washikamakamu wote, hususan wale makhalfia wakubwa wangekuwa wanayo elimu ya ghaib, ingawa tunaona hakuna hata mmoja katika makhalifa hao aliyewahi kudai kuwa nayo. Bali, kama Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), walielezea kutokuwa na uwezo kwao wa kuijua. Kwa nini basi unamfanya Ali ni tofauti?

Muombezi: Kwanza, nilikisha kuwaambieni kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakuna na uwezo wa kiasili wa kujua ya Ghaib. Wakati aliposema “Kama ningeyajua ya ghaib, kwa hakika ningeweza kuwa na wingi wa mema,” alimaanisha kwamba elimu ya ghaib siyo ya asili kwake, kama ilivyokuwa kwa Allah. Wakati Allah alipokuja kuliondoa pazia kutoka kwa Mtukufu Mtume, alikuja kujua mambo yaliyofichika.

Maimam Watukufu Walikuwa Ndio Makhalifa Wa Kweli Na Walikuwa

Na Elimu Ya Ghaib.

Pili, unasema kwamba, kama Ali alikuwa na elimu ya ghaib, hawa makhalifa wengine wangekuwa nayo vile vile. Tunakubaliana na wewe. Tunasema pia kwamba makhalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wangekuwa na elimu zote, ya dhahiri na ya vitu visivy- oonekana.

Kwa kweli uwezo na sifa za makhalifa zingefanana hasa sawa na zile za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) katika mambo yote, isipokuwa lile jukumu la Utume lenyewe na unabii, ambalo linajumuisha uwezo wa kupokea wahyi moja kwa moja. Bila shaka unawaita makhalifa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) watu wale ambao walichaguliwa tu kuwa hivyo na watu wachache ingawa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa amewalaani, kwa mfano, Mu’awiya.

Lakini tunasema kwamba makhalifa na mawasii wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni wale ambao wameteuliwa kuwa makhalifa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mwenyewe, kama vile mitume waliotangulia walivyoteua mawasii wao wenyewe.

Hivyo wale makhalifa na mawasii walioteuliwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa amri ya Allah, waliziwakilisha vizuri sana sifa zake, na kwa sababu hiyo walikuwa nayo elimu ya ghaib. Wale makhalifa wa kweli walikuwa watu kumi na mbili ambao majina yao yameandikwa katika vitabu vyenu wenyewe vya hadithi. Nao ni wale wa familia ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wanamjumuisha Ali na wale kumi na moja wa kizazi chake.

Na ukweli kwamba wale watu wengine hawakuwakuteuliwa Makhalifa unadhihirishwa na kauli yako mwenyewe, ambayo inathibitishwa na Ulamaa wenu wakubwa kwamba walikuwa mara kwa mara wakielezea kutokujua kwao kwa hata mambo ya kawaida, ukiachilia mbali kuitaja elimu ya ghaib. Lango La Elimu.

Tatu, unaulizia ni hadithi gani inayothibitisha kwamba Amiru’l-Mu’minin Ali alikuwa nayo elimu ya ghaib, kwa kweli zipo hadithi nyingi zinazounga mkono jambo hili. Moja inaitwa “Hadithi ya Madina.” Imehadithiwa na madhehebu zote (Shia na Sunni) takriban kwa wingi sana kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema katika nyakati na matukio mengi kuhusu Ali, kwamba alikuwa ni “Lango la elimu yake.” Haya yalikuwa ndiyo maneno yake; “Mimi ni jiji la elimu na Ali ndie lango lake. Hivyo yoyote anayetaka kutafuta elimu lazima aje kwenye lango.”

Sheikh: Hadidhi hii sio sahihi kwa mujibu wa ulamaa wetu. Hata kama kuna hadithi kama hiyo, lazima itakuwa ni ya pekee, moja ya hadithi dhaifu.

Muombezi: Inasikitisha kwamba unaiita hadithi hii yenye nguvu kwamba ni simulizi iliy- opeke yake, au mojawapo ya hadithi dhaifu. Ulamaa wenu mashuhuri wamelithibitisha hii. Ungelikitazama Jam’u-l- Jawami’y cha Suyuti, Tahdhibu‘I-Ansar cha Muhammad bin Jarir Tabari, Tadhkiratu‘l-Abrar cha Seyyed Muhammad Bukhari, Mustadrak ya Hakim Nishapuri, Naqdu’s-Sahili cha Firuzabadi, Kanzu’l-Ummal cha Ali Muttaqi Hindi, Kifayatu’t-Talib cha Ganji Shafi’i, na Tadhkiratu‘l-Muzu’a cha Jamalu’d-Din Hindi. Wanaandika “Ikiwa mtu ataikataa hadithi hii atakuwa kwa hakika amekosa.” Pia katika Rauzatu’l-Nadiya cha Amir Muhammad Yamani, Bahru’l-Asanid cha Hafiz Abu Muhammad Samarqandi na Matalibu’s- Su’ul cha Muhammad Bin Talha Shafi’i, kwa ujumla wamethibitisha ukweli wa hadithi hii.

Hadithi hii imesimuliwa katika njia nyingi tofauti na kutoka kwenye vyanzo mbali mbali. Wengi wa Masahaba na wafuasi wameisimulia hadithi hii, pamoja na Ali, Abu Muhammad Hasan Bin Ali, mjukuu mkubwa wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Abdullah Bin Abbas, Jabir Ibn Abdullah Ansari, Abdullah Ibn Mas’ud, Hudhaifu Bin Al-Yaman, Abdullah Ibn Umar, Anas Bin Maliki, na Amr Bin Aas.

Miognoni mwa Tabi’ in (Kizazi cha pili baada ya Masahaba) wafuatao wameisimulia hadithi hii: Imam Zainu’I-Abidin, Imam Muhammad Baqir, Asbagh Bin Nabuta, Jarir Azzabi, Harith bin Abdullah Hamdani Kufi, Sa’d Bin Ta’rifu’l-Hanzali Kufi, Sa’id Bin Jabir Asadi Kufi, Salam Bin Kuhail Hazarmi Kufi, Sulayman Bin Mihran A’mash Kufi, Asim Bin Hamza Saluli Kufi, Abdullah Bin Uthman bin Khisam al-Qari al-Makki, Abdur- Rahman Bin Uthman, Abdullah bin Asila al-Muradi, Abu Abdullah Sanabahi, na Mujahid Bin Jabir Abu’I Hajjaj al-Makhzumi al-Makki.

Mbali na Ulamaa wa Shi’ah, ambao kwa kauli moja wameikamata hadithi hii, wengi wa wasimulizi na wanahistoria wenu mashuhuri wameiandika hadithi hii. Nimeziona rejea kama mia mbili kutoka wa ulamaa wenu ambao wamesimulia hadithi hii tukufu. Nitataja baadhi ya wale Ulamaa mashuhuri na vitabu vyao. Ulamaa Wa Sunni Ambao Wamesimulia Ile Hadithi Ya “Jiji La Elimu”

(1) Mfasiri na mwanahistoria wa karne ya tatu Muhammad Bin Jarir Tabari (kafa. 310 A.H.): Tahdhibu’I- Athar, (2) Hakim Nishapuri (kafa 405 A.H): Mustadrak, Juz. 3, uk. 126, 128, 226 (3) Abu ‘Isa Muhammad Bin Tirmidhi (kafa 289 A.H): Sahih (4) Jalul’d-Din Suyuti (kafa 911 A.H); Jam’u’l-Jawami’y na Jam’u’s-Saghir Juz. 1, uk. 374 (5) Abu’l-Qasim Sulayman Bin Ahmad Tabrani (kafa 491 A.H): Kabir na Ausat. (6) Hafiz Abu Muhammad Hasan Samarqandi (kafa 491. A.H): Bahru’l-Asanid (7) Hafiz Abu Nu’aim Ahmad bin Abdullah Ispahani (kafa 410 A.H): Ma’rifatu’l-Sahaba. (8) Hafiz Abu Amr Yusuf Bin Abdullah Bin Abdu’l-Bar Qartabi (kafa 463 A.H): Isti’ab Jz. (9) Abu’l Hasan Faqih shafi’i Ali bin Muhammad Bin Tayyib al-Jalabi Ibn Maghazili (kafa483 A.H): Manaqib (10) Abu Shuja’ Shirwaih Hamadani Dailami (kafa 509 A.H): Firdausu’l-Akhbar. (11) Abu’l-Muayyid Khatib Khawarizmi (kafa 568 A.H): Manaqib uk. 49 na Maqtalu’l- Husain Juz, 1. uk. 43 (12) Abu’l-Qasim bin Asakir Ali Bin Hasan Damishqi (kafa 572 A.H): Ta’rikh-e-Kabir. (13) Abu’l-Hujjaj Yusuf Bin Muhammad Andalusi (kafa 605 A.H): Alif-Bas Juz. 1, uk, 222 (14) Abu’l-Hasan Ali Bin Muhammad bin Athir Jazari (kafa 630 A.H): Asadu’l-Ghaiba Jz.4, uk. 22 (15) Muhibu’d-Din Ahmad Bin Abdullah Tabari Shafi’i (kafa 694 A.H) Riyazu’l-Nuzra, Juz. 1, uk. 129, na Dhakha’iru’l-Uqba uk. 77 (16) Shamsu’d-Din Muhammad Bin Ahmad Dhahabi Shafi’i (kafa 748 A.H) Tadhkiratu’l- Huffaz, Juz, 4, uk 28. (17) Badru’d-Din Muhammad Zarkashi Misri (kafa 749 A.H.): Faizu’l-Qadir Juz. 3, uk.4 (18) Hafiz Ali Bin Abi Bakr Haithami (kafa 807 A.H): Majma’u’z-Zawaid, Juz. 9, uk. 114 (19) Kamalu’d- Din Muhammad Bin Musa Damiri (kafa 808 A.H): Hayatu’l-Haiwan Juz.1, uk. 55 (20) Shamsu’d-Din Muhammad Bin Muhammad Jazari (kafa 833 A.H): Asnu’l-Matalib uk. 14 (21) Shahabu’d-Din Bin Hajar Ahmad Bin Ali Asqalani (kafa 852 A.H): Tahdhibu’l- Tahdhib Juz. 7, uk. 337 (22) Badru’d-Din Mahmud Bin Ahmad Aini Hanafi (kafa 855 A.H): Umdatu’l-Qari Juz. 7, uk. 631 (23) Ali Bin Hisamu’d-Din Muttaqi Hindi (kafa 975 A.H): Kanzu’l-Ummal, Juz. 6, uk. 156 (24) Abu’r-Ra’uf Al-Munawi Shafi’i (kafa 1031 A.H): Faizu’l-Qadir, Sharh-e-Jami’u’l- Saghir, Juz. 4, uk. 46 (25) Hafiz Ali Bin Ahmad Azizi Shafi’i (kafa 1070 A.H): Siraju’l-Mumir, Jam’u’s-Saghr Juz. 3. 63 (26) Muhammad Bin Yusuf Shami (Kafa 942 A.H): Subulu’l-Huda wa’l-Rishad fi Asma’I Khairu’l-Ibad. (27) Muhammad Bin Yaqub Firuzabadi (kafa 817 A.H): Naqdu’s-Sahih. (28) Imam Ahmad Hanbal (kafa 241 A.H): Mujaladab-e-Munaqab, na Musnad. (29) Abu Salim Muhammad Bin Talha Shafi’i (kafa 652 A.H): Matalibu-s-Su’ul. (30) Sheikhu’l-Islam Ibrahim Bin Muhammad Hamwaini (kafa 722 A.H): Fara’idu’s- Simtain. (31) Shahabu’d-Din Dowlat Abadi (kafa 849 A.H ): Hidayatu’s-Su’ada. (32) Alama Samhudi Seyyd Nur’d-Din Shafi’i (kafa 911 A.H): Jawahiru’l-Iqdain. (33) Qazi Fadhl Bin Ruzbahan Shirazi: Ibta’lu’l-Batil. (34) Nur’d-Din Bin Sabagh Maliki (kafa 855 A.H): Fusulul-Muhimma (35) Shahabu’d-Din Bin Hajar Makki (Adui mbaya na shabiki, alikufa 974 A.H): Sawa’iq- e-Muhriqa, (36) Jamalu’d-Din Ata’ullah muhadith-e-Shirazi (kafa 1000 A.H): Arbain (37)Ali Qari Harawi (kafa 1014 A.H): Mirqat Sharh-e-Mishkat (38) Muhammad Bin Ali As-Subban (kafa 1205 A.H): Is’afu’l-Raghbin. (39) Qadhi Muhammad Bin Sukani (kafa 1250 A.H): Fawa’idu’l-Majmu’a fi’l-Ahadithi’l- Muzua. (40) Shahabu’d-Din Seyyed Mahmud Alusi Baghdadi (kafa 1270 A.H): Tafsir-e-Ruhu’l- Ma’ani. (41) Imam al-Ghazali:- Ihya’u’l-Ulum (42) Mir Seyyed Ali Hamadani Faqih-e-Shafi’i: Mawaddatu’l-‘Qurba. (43) Abu Muhammad Ahmad Bin Muhammad Asimi: Zainu’l-Fata (Sherehe juu ya Sura ‘Hal Ata’) (44) Shamsu’d-Din Muhammad Bin Abdu’r-Rahman Sakhawi (kafa 902 A.H): Maqasidu’l-Hasana. (45) Sulayman Balkhi Hanafi (kafa 1293 A.H): Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 14. (46) Yusuf Sibt Ibn Jauzi: Tadhkirat-e-Khawasu’l-Umma. (47) Sadru’d-Din Seyyed Husain Fuzi Harawi: Nuzahatu’l-Arwah. (48) Kamalu’d-Din Husain Meibudi: Sharh-e-Diwan. (49) Hafiz Abu Bakr Ahmad Bin Ali Khatib Baghdadi (kafa 463 A.H): Ta’rikh Juz. 2, uk. 377, Juz. 4, uk 348 na Juz. 7, uk. 173. (50) Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i (kafa 658 A.H): Kifayatu’t-Talib, mwishoni mwa Sura ya 58.

Baada ya kunukuu hadithi sahihi tatu kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), anasema: “Kwa kifupi, wale masahaba waliokuwa na elimu ya juu, kizazi kilichofuatia baada yao, na kile kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), wote walikiri ubora, elimu pana, na hukmu za Ali.

Ili kuwa na uhakika Abu Bakr, Umar, na Uthman na masahaba wengine waliokuwa na elimu walikuwa wakimuoma yeye kuhusu mas’ala ya kidiini na walifuata ushauri wake katika mambo ya utawala. Walikiri kwamba alikuwa hapitiki katika elimu na maarifa.

Na hadithi hi haimkadirii cha zaidi (ya alivyo) kwani cheo chake mbele ya Allah, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), na waumini ni kikubwa sana zaidi kuliko hivyo, Imam Ahmad Bin Muhamamd Bin Al-Sidiqqi Magharibi katika kuthibitisha hadithi hii tukufu ameandika kitabu, Fathu’l-Mulku’l-Ali bi Sihat-e-Hadith- e-Bab-e-Madinatu’l-Ilm. (Kilichochapishwa na Ilamiyyah Press, Misri, 1354 A.H). Kama hamjatosheka hata sasa hivi, ninaweza kuku- peni rejea zaidi.

Kusimulia Sifa Za Ali Ni Ibada

Seyyed Adil-Akhtar (Mwanachuoni, mwandishi wa vitabu, na kiongozi wa Sunni): Mara kwa mara nimeona katika hadithi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema kwamba kusimulia sifa za Ali ni ibada. Yule mwanazuoni mkubwa, Mir Seyyed Ali Hamadani Shafi’i, anaandika katika Mawaddatu’l- Qurba yake kwamba, “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema kwamba Malaika wanauangalia kwa makini makhususi mkusanyiko ambamo ubora na sifa za Ali zinasimuliwa.

Wanaomba rehma za Allah juu ya watu hao. Zaidi ya hayo, kusimulia hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hilo peke yake ni ibada. Hivyo, ninaomba kwamba utusimulie hadithi zenye maelezo zaidi ili kwamba mkusanyiko huu uwe ni kitovu cha ibada kamilifu zaidi.

Hadithi Ya “Mimi Ni Nyumba Ya Maarifa.”

Muombezi: Ipo hadithi ambayo kwa kweli imesimuliwa kwa mfululizo mkubwa sana. Wasimulizi wa Madhehebu zote wameisimulia. Miongoni mwa ulamaa wenu ambao wameismulia ni Imam Ahmadi Bin Hanbal (katika Manaqib, Musnad), Hakim (Mustadrak), Mulla Ali Muttaqi (Kanzu’l-Ummal Jz. 6, uk. 401, Hafiz Abu Nu’aim Isfahani (Hilyatu’l-Auliya, Juz. 1, uk. 64). Muhammad Bin Sabban Misri (Is’afu’r- Raghibin) Ibn Maghazili Faqih Shafi’i (Manaqib) Jalalu’d-Din Suyuti (Jam’us-Saghir, Jam’ul-Jawami’y na La’aliu’l-Masnua), Abu Isa Tirmidh (Sahih, Jz. 2, uk. 2140), Muhammad Bin Talha Shafi’i (Matalibu’s- Su’ul), Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi (Kifayatut-Talib) Sibt Ibn Jauzi (Tadhkirat-e- Khawasu’l-Umma), Ibn Hajar Makki (Sawa ‘iq Muhriqa) Sura ya 9, Faslu ya 2, uk. 75) Muhibu’d-Din Tabari (Riyazun- Nuzra), Sheikhu’l Islam Hamwaini (Fara’idus-Simtain), Ibn Sabbagh Maliki (Fasulu’l-Muhimma) Ibn Abi’l-Hadid Mu’tazali (Sharh-e-Nahjul-Balagha) na kundi la wengine. Wanathibitisha usahihi wa hadithi hii na wamemnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema : “Mimi ni Nyumba ya maarifa na Ali ni lango lake, hivyo ikiwa mtu ana tamaa ya kupata elimu basi anapashwa kuja kwenye lango.

Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i ametenga sura ya 21 kwa ajili ya hadithi hii. Baada kutoa vyanzo vyake na rejea zake, anatoa maoni yake binafsi juu yake. Anasema hadithi ina hadhi ya juu sana. Yaani, Allah Mtukufu ambaye ndie chanzo cha maarifa na elimu ya mambo yote na ambaye amefundisha kuhimiza mema na kukataza maovu kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ndiye ambaye pia amezitunuku zawadi hizi juu ya Ali.

Kwa hiyo, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ali ndiye mlango wa maarifa yangu. Yaani, kama mnataka kufaidika na maarifa yangu budi mgeukie kwa Ali, ili kwamba hali halisi iweze kufichuliwa kwenu.” Ibn Maghazili Shafi’i katika Manaqib, Ibn Asakir katika Ta’rkih yake (akiandika kutoka wka Masheikh wake mwenyewe), Khatib Khawarizmi katika Manaqib yake, Sheikhu’l- Islam Hamwaini katika Fara’id, Dailami katika Firdaus, Muhammad Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib Sura ya 58 Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l- Mawadda Sura ya 14, na wengineo katika Ulamaa wenu mashuhuri wamesimulia kutoka kwa ibn Abbas na Jabir Ibn Abdullah Ansari kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akiwa amemshika Ali mkono, alisema: “Huyu ni Ali - Bwana na kiongozi wa wacha-Mungu muuaji wa makafiri. Yeyote atakayemsaidia yeye ni mwenye kuungwa mkono, na yeyote atakayemtupa atakuwa yeye mwenyewe ametupwa.” Kisha Mtukufu Mtume akinyanyua sauti yake, akasema: “Mimi ni Jiji la elimu na Ali ni lango lake.”

Pia Shafi’i anaandika kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Mimi ni jiji la elimu, na Ali ni lango lake, hakuna aingiaye kwenye nyumba ila kupitia kwenye lango.”

Yule mtunzi wa Manaqib-e-Fakhira anasimulia kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alisema: “Mimi ni jiji la Elimu, na Ali ni lango lake. Hivyo yeyote anayetaka kupata elimu ya dini ni budi aje kwenye lango.” Kisha akasema: “Mimi ni jiji la elimu na wewe Ali ndio lango lake. Anadanganya anayefikiri kwamba atanifikia mimi kupitia njia nyingine kuliko kupitia kwako.”

Ibn ‘Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahjul-Balagha yake, Abu Ishaq Ibrahim Bin Sa’da’d–Din Muhammad Hamwaini katika Fara’idu’s-Simtain kutoka kwa Ibn Abbas yule mashuhuri Khatib Khawarizmi katika Manaqib kutoka kwa Amr Bin Aas, Imam’I-Haram Ahmad bin Abdullah Shafi’i katika Dhakha’iru’l- Uquba, Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, Mir Seyyed Ali Hamdani katika Mawaddatu’l-Qurba, na vilevile yule mkaidi mkubwa, Ibn Hajar katika Sawa’iq-e-Muhriqa, Sura ya 9, Fasilu ya 11 uk. 75, hadithi ya 9 kutoka kwa Bazaz miongoni mwa zile hadithi arobaini ambazo ameziandika kuhusu sifa za Ali, Tabrani katika Ausat yake kutoka kwa Jabir Ibn Abdullah Ansari, Ibn Adi kutoka kwa Abdullah Ibn Umar, Hakim na Tirmidhi kutoka kwa Ali wamesimulia kwamba Mtume wa Allah alisema: “Mimi ni Jiji la Elimu, na Ali ni lango lake. Hivyo yeyote anayetafuta elimu hanabudi kuja kupitia langoni.”

Kisha wanasema kuhusu hadithi hiyo hiyo: Watu wasioelewa wamesita kuikubali hadithi hii na wengine wao wamesema kwamba hii ni hadithi ya kughushi.

Lakini pale Hakim (Mtunzi wa Mustadrak) ambaye kauli yake mnaichukulia kuwa ni yenye nguvu, alipoyasikia mambo haya akasema: “Hakika, hadithi hii ni ya kweli.”

Ufafanuzi Wa Hadithi Ya “Lango La Elimu”

Mtunzi wa Abaqatu’l-Anwar, Allama Seyyed Hamid Husain Dihlawi Sahib, amekusanya juzuu mbili zenye kuonyesha vyanzo na usahihi wa hadithi hii. Kila moja ya juzuu hizi ina ukubwa kama juzuu yeyote ya Sahih ya Bukhari.

Sikumbuki ni vyanzo vingapi amevitaja kutoka kwa Ulamaa maarufu wa Sunni kuthibitisha kwamba wasimulizi wa haidthi hii wanafanya mfululizo wa usimuliaji usiokatika,bali ninakumbuka kiasi hiki:

Nilipokuwa ninakisoma kitabu hicho, niliomba dua kwa ajili ya mtu yule maarufu, ambaye alikuwa msomi sana na ambaye alikuwa amechukua uangalifu wake mwingi sana katika ukusanyaji wa kitabu hicho. Kitabu hicho kinathibitisha kwamba Ali alikuwa na hadhi ya kipekee miongoni mwa masahaba wa Mtukufu Mtume.

Sasa, juu ya tafadhali, hebu kuweni wakweli. Hivi ilikuwa ni sawa kuufunga mlango wa elimu ambao Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikuwa ameufungua kwa ajili ya Umma wote? Je! Watu walihalalishwa katika kufungua mlango wa mtu wa chaguo lao, ambaye hakuwa na mahusiano yoyote na kiwango cha elimu ya Ali?

Sheikh: Tumekwishajadili vya kutosha lile jambo la kwamba hadithi hii kwa ujumla inakubaliwa na Ulamaa wetu. Hakuna shaka baadhi ya wasimuliaji wamesema kwamba ni dhaifu, ni hadithi ya peke yake, wakati wengine wametamka kwamba imesimuliwa kwa mfululizo sana. Lakini hii inahusiana nini na “elimu ya Ghaib,” ambayo Ali anafikiriwa kuwa alikuwa anayo?

Ali Alikuwa Na Elimu Ya Ghaib

Muombezi: Hivi hamkukubali mapema kwamba yule mwisho wa Mitume alikuwa ni mbora wa viumbe vyote vilivyoumbwa? Na je! Qur’ani haisemi kwamba Allah hafichui siri zake kwa yeyote “ukiacha kwa yule kati ya Mitume wake ambaye amemchagua? Allah alimuondolea pazia yeye, na akajaalia juu yake yeye elimu ya Ghaib. Hivyo, mbali na aina zingine za elimu, alikuwa nayo elimu ya Ghaib. Wakati Mtukufu Mtume aliposema, “Mimi ni jiji la elimu na Ali ni lango lake,” elimu yote ya jiji ingeweza kupatikana kupitia kwenye “lango la elimu.” Elimu kama hiyo ilichanganya pamoja na ile elimu ya ghaib.

Ali Alijua Maana Ya Dhahiri Na Ya Ndani Ya Qur’ani Tukufu

Miongoni mwa wengine, Hafiz Abu Nu-aim Ispahani katika Hilyatu’l-Auliya, Juz.1 uk. 65 Muhammad Bin Yusufu Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib Sura aya 74 na Sulaiman Balkh Hanafi katika Yanabiu’l- Mawadda, Sura ya 14 uk. 74 kutoka kwenye Faslu’l-Khitab, anamnukuu Abdullah Ibn Ma’sud yule mwandishi wa wahyi akisema kama: “Hakika, Qur’ani Tukufu imeshushwa juu ya hefufi saba, herufi ambazo kila moja ina maana ya dhahiri na iliyofichika. Kwa hakika Ali anazielewa maana zote za Qur’ani, za dhahiri na ya ndani.

Mtukufu Mtume Alifungua Milango 1000 Ya Elimu Katika Moyo Wa Ali.

Ulamaa wenu wakubwa wemekiri katika vitabu vyao vya sahihi kwamba Ali alikuwa na elimu ya ghaib. Baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) yeye alikuwa ni Murtadha (aliyechaguliwa) miongoni mwa Umma wote. Abu Hamid Ghazali katika Kitabu chake Bayan-e-Ilm’l-Ldunni ameandika kwamba Ali alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliweka ulimi wake kinywani mwangu. Kutoka kwenye mate ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), milango 1000 za elimu ilifunguliwa kwangu, na kutoka katika kila mlango, milango mingine 1000 ilifunguliwa kwangu.” Yule kiongozi wenu mashuhuri, Suleyman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda Sura ya 14. uk ,7 anasimulia kutoka kwa Asbagh Ibn Nabuta ambaye amemnukuu AmruI-Mu’minin kwamba alisema: “Hakika, Mtukufu Mtume alinifundisha mimi milango 1000 ya elimu kila mlango ambao ilifungua, milango mingine 1000 kufanya milango milioni moja. Hivyo, ninajua nini kimekwisha tokea tayari na nini kitakachotokea mpaka Siku ya Hukumu.

Katika sura hiyo hiyo anasimulia, kutoka kwa Ibn Maghazili kwa idhini ya huyu wa mwisho mwenyewe, kutoka kwa Abu’s-Sabba, ambaye alisimulia kutoka Ibn Abbas, ambaye amemnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Katika usiku wa Miraj, wakati nilipokuwa mbele za Allah, Alizungumza nami kwa siri. Kila chochote nilichojifunza, nilimfundisha Ali. Yeye ni lango la elimu yangu.”

Yule mwandishi maarufu, Mu’affaq bin Ahmad Khawarizmi, amesimulia vivyo hivyo kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwa njia hii: “Jibrail aliniletea busati kutoka peponi. Nilikaa juu yake mpaka nikafikishwa karibu na Mola wangu. Kisha alizungumza nami na akaniambia mambo ya Siri. Kila nilichojifunza nilikifikisha kwa Ali. Yeye ndiye lango la elimu yangu.”

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwita Ali na akasema: “Ali! Kukubaliana na wewe ni kukubaliana na mimi; kukupinga wewe ni kunipinga mimi. Wewe ndio elimu ambayo inaniuganisha mimi na Umma wangu.”

Hafiz Abu Nu’aim Ispahani katika Hilyatu’l-Auliya, Mulla Ali Muttaqi katika Kanzu’l- Ummal, Juz. 6, uk. 392, na Abu Ya’la wanasimulia kutoka kwa Ibn Lahi’a, ambaye alisimulia kutoka kwa Hayy Bin Abd Maghafiri, ambae alisimulia kutoka kwa Abdu’r- Rahman, ambaye alisimulia kutoka kwa Abdullah Bin Umar, ambae alisimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipokuwa kwenye kitanda chake cha mauti alisema “Nileteeni ndugu yangu hapa kwangu.” Wakati Abu Bakr alipomjia, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aligeuzia uso wake kando. Tena akasema, “Niitieni ndugu yangu hapa.” Kisha Uthman akaja, na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamgeuzia uso pia. Baadhi ya wengine wanasimulia kwamba baada ya Abu Bakr, Umar alikuja na kisha Uthman.

Baada ya hayo, hata hivyo Ali aliitwa ndani. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamfunika na blanket lake na akapumzisha kichwa chake juu yake.

Wakati Ali alipotoka nje, watu wakamuuliza: “Ali! Ni nini alichokuambia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)?”

Imam akasema, “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amenifundisha milango 1000 ya elimu na kila moja ya milango hiyo una milango 1000 mingine.

Hafiz Abu Nu’aim Ahmad bin Abdullah Ipahani (kafa 430 A.H) katika Hiliyatul-Auliya yake Jz. 1, uk. 65, akiandika kuhusu sifa za Ali, Muhammad Jazari katika Asnu’l-Matalib uk. 14, na Muhammad bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib, sura ya 48, wamesimulia kwa vyanzo vya kuaminika kutoka kwa Ahmad Bin Imran Bin Salma Bin Abdullah kwamba alisema: “Tulikuwa pamoja na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati alipoulizia kuhusu Ali Bin Abi Talib. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisiema: “Maarifa yamegawanywa katika sehemu kumi, ambazo tisa zilipewa Ali na moja ilitolewa kwa wanadamu wote.

Pia Mua’ffaq Bin Ahmad Khawarizmi katika Manaqib, Mullah Ali Muttaqi katika Kanzu’l-Umal Juz. 6, uk. 156 na 401 kutoka kwa wanazuoni wengi maarufu, Ibn Maghazili Faqih Shafi’i katika Faza’il na Sulayman Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda kwa vyanzo hivyo hivyo kutoka kwa mwandishi wa Wahyi, Abdullah bin Mas’ud, Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibu’s-Su’ul uk. 14 na wengineo wengi wanasimulia kutoka kwa Hulays Bin ‘Alqama kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoulizwa kuhusu Ali alisema:

“Maarifa yamegawanywa katika sehemu kumi ambazo kati ya hizo, tisa amepewa Ali na wanadamu wote wamepata sehemu moja. Katika hiyo sehemu moja, fungu la Ali pia lilikuwa ndio kubwa.”

Pia katika Yanabiu’l-Mawadda, sura ya 14, imesimuliwa kutoka kwenye Sharh-e-Risala Fathu’l-Mubin cha Abu Abdullah Muhammad Bin Ali al-Hakim Tirmidhi kwamba Abdallha Bin Abbas alisimulia hadithi ifuatayo: “Elimu ina sehemu kumi. Sehemu tisa ni za Ali peke yake, na ile ya kumi iliyobakia ni ya wanadamu wote. Katika hiyo sehemu moja pia, Ali aligaiwa fungu kubwa zaidi.”

Pia Muttaqi Hindu katika Kanzu‘l–Ummal Juz. 6, uk. 153, Khatib Khawarimi katika Manaqib, uk 49, na Maqtalu’l- Husain, Juz. 1, uk. 43, Dailami katika Firdausu’l-Akhbar, na Sulayman Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda, sura ya 3, anamuelezea Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba alisema; “Baada yangu mimi, miongoni mwa Umma wote, mtu mwenye elimu na hekima zaidi ni Ali Bin Abi Talib.”

Kuikabidhi Elimu Ya Mtume Kwa Ali.

Hatusemi kwamba Ali Bin Abi Talib na hawa watu kumi na moja wa Kizazi chake, hawa Maimam, walipokea elimu moja kwa moja toka kwa Allah kupitia wahyi (ufunuo) kama ilivyokuwa kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Lakini tunaamini kwamba huyu wa mwisho katika Mitume wa Allah alikuwa ndio kitovu cha rehma za Allah. Faida yoyote wanayoipata viumbe inatoka kwa Allah Mwenye uwezo, kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.)

Kwa hiyo elimu yote, pamoja na matukio muhimu ya wakati uliopita na ujao, yalifanywa yafahamike kwao wakati wa uhai wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Elimu nyingine ilikabid- hiwa kwao na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) wakati alipokuwa karibu na kuiaga dunia hii.

Maulamaa wenu wamesimulia hadithi kutoka kwa Ummu’l-Mu’minin Aisha kuhusu nukta hii. Mwisho wa hadithi hii yeye alisema: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimwita Ali na akamkumbatia na akamfunika kichwa chake na shuka. Nilichomoza kichwa changu mbele na nikajajribu sana kuwasikiliza, lakini sikuweza kuelewa chochote. Wakati Ali aliponyanyua kichwa chake, paji la uso wake lilifunikwa na kijasho chembamba. Watu wakamwamba, Ali Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amekwambia nini kwa muda mrefu wote huo?

Kisha Ali akasema: ‘Hakika Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amenifundisha milango 1000 ya elimu, kila mmoja ambao ulifungua milango mingine 1000.’ Katika siku za mwanzoni za Utume wake (kama nilivyotaja katika mikesha iliyopita)

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliandaa chakula kwa watu arobaini katika ndugu zake wa karibu kwenye Nyumba ya Abu Talib. Baada ya kutangaza Utume wake, Ali alikuwa wa kwanza kutangaza imani yake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimshika katika mikono yake na akamtemea mate yake mdomoni mwake. Ali baadae alisema kuhusu tukio hili “Mara tu baada ya hili, chemchemi za maji ziliibuka ndani ya kifua changu.” Ulamaa wenu mashuhuri, wenyewe wamesimulia kwamba wakati akitoa hotuba, Imam aliashiria kwenye maana hiyo hiyo akasema; “Niulizeni mimi juu ya lile msilolielewa kabla sijafa. Kifua changu ni hifadhi ya elimu isiyo na mpaka.” Kisha akiashiria kidole kwenye tumbo lake akasema, “Hii ni ghala ya elimu, haya ni mate ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hiki ndicho Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alichonilisha mimi kama nafaka.”

Muda wote wa maisha yake ya ukubwani Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alitoa elimu na neema kwa Ali katika njia tofauti. Kila elimu Allah aliyompa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Mtume aliweka ndani ya kifua cha Ali.

Jafr-E-Jami’a Na Asil Yake

Moja ya vyanzo vya neema tukufu ambazo Ali alizipokea kutoka kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuja kupatia Jafr-e-Jami’a, kitabu kilichojaa siri za ulimwengu. Ulamaa wenu maarufu,wenyewe wanakubali kwamba kitabu hiki na elimu maalum ni miongoni mwa neema adimu kwa Ali na Maimam watukufu.

Hujjatu’l-Islam Abu Hamid Ghazali ameandikwa kwamba, “Kuna kitabu kutoka kwa bwana na kiongozi wa wachamungu Ali Bin Abi Talib. Jina lake ni Jafar-e-Jam’ud-Dunia wa’l-Akhira. Kitabu hicho kinazo sayansi zote, ukweli na mambo yaliyofumbika, mambo ya ghaib, asili ya vitu na athari zake, asili ya majina na herufi, ambavyo hakuna anayevi- fahamu isipokuwa Ali na watu kumi na moja wa kizazi chake. Ukweli ni kwamba wamerithi kitabu hiki kutoka kwa baba zao.”

Kadhalika, Sulayman Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda, uk. 403, anatoa maelezo marefu kuhusu kitabu hicho, kutoka kwa Muhammad Bin Talha Shafi’i kwenye kitabu chake Durru’l-Munazzam. Anasema kwamba Jafr-e-Jami’a, kina funguo za elimu, kina kurasa 1,700 na ni mali ya Ali Bin Abi Talib pekee.

Pia imeandikwa katika Ta’rikh-e-Ningaristan kutoka kwenye Shar-e-Mawaqif kwamba Jafr na Jami’a ni vitabu viwili ambayo ni mali ya Ali pekee. Vinaelezea, kupitia elimu ya hefufi, matukio yote mpaka mwisho wa dunia. Kizazi chake vile vile, kinatabiri kwa msin- gi wa vitabu hivyo.

Nawab: Tafadhali tupatie habari zaidi kuhusu kitabu hiki cha Jafr.

Muombezi: Katika mwaka wa kumi Hijiria, wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliporudi kutoka Hijja yake ya mwisho, Jibril alimjia na kufahamisha juu ya kifo chake. Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alinyanyua mikono yake juu na akasema, “Ewe Mungu Wangu! Umeniahidi mimi; nawe kamwe si mwenye kurudi nyuma juu ya neno Lako.”

Jibu kutoka kwa Allah likaja: “Mchukue Ali pamoja na wewe, na mkiwa mmekaa juu ya milima ya Uhud, na migongo yenu ikielekea kibla, waite wanyama wa porini. Wataitikia wito wako. Miongoni mwao atakuwepo mbuzi mwekundu, mwenye pembe kubwa. Muamuru Ali amchinje na kumchuna ngozi yake na uigeuze nje ndani. Itaonekana ikiwa imekaushwa.

Kisha Jibril atakuja na kalamu na wino, ambao utakuwa tofauti na wino wa duniani. Mwambie Ali aandike kile Jibril atakachosema. Maandishi hayo pamoja na hiyo ngozi vitadumu hasa katika hali hiyo hiyo na kamwe haitaoza. Daima itabakia salama. Kila itakapofunuliwa itakutwa ni safi” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikwenda kwenye vilima vya Uhud na akatekeleza maagizo yale matukufu. Jibril alikuja na akaiweka ile kalamu na wino mbele ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), ambaye alimuamuru Ali ajiandae kuandika.

Jibril alimsimulia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) matukio yote muhimu ya dunia naye alimuagiza Ali kuyaandika kwenye ile ngozi. Aliandika hata kwenye ngozi ya mikono na miguu. Aliandika kila kitu ambacho kilikwisha tokea au kile ambacho kingetokea hadi Siku ya Hukumu. Aliandika majina ya wanae ambao walikuwa hawajazaliwa, na vizazi vyao na majina ya marafiki na maadui zao. Aliandika vile vile kila kile ambacho kingewatokea kila mmoja wao hadi Siku ya Hukumu.

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akakitoa kile kitabu na elimu ya Jafr kwa Ali na akakifanya ni sehemu ya urithi wa Uimam. Kila Imam kwa zama, alikikabidhi kwa wasii wake.

Hiki ni kitabu kile kile ambacho Abu Hamid Ghazali kuhusu hicho anasema: Jafr-e-Jami’a ni kitabu ambazo kwa jumla ni mali ya Ali na watu kumi na mmoja kwa kizazi chake. Kina kila kitu.”

Nawab: Inawezekana vipi kwamba mambo yote ya dunia yawe ni ya kuandikwa kwenye ngozi ya mbuzi?

Muombezi: Kwanza, hadithi yenyewe inaonyesha kwamba haikuwa ni mbuzi wa kawaida. Alikuwa ni mbuzi mkubwa ambaye aliumbwa kwa madhumuni haya.

Pili, kilichokuwa kimeandikwa hakikuwa ni maandishi ya kwenye vitabu vya kawaida. Kiliandikwa kwa herufi na alama za siri.

Nimekwisha kuwaambieni kwamba mwandishi wa Ta’rikh-e- Nigaristan ameeleza kutoka Sharh-e- Mawaqif kwamba Jafr na Jami’a vina herufi za kialfabeti ambazo kupitia kwazo habari hufichuliwa.

Kisha Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.) alikabidhi ufunguo wa siri hii kwa Ali, ambaye, kwa amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), aliikabidhi kwa warithi wake, hao Maimam watukufu.

Ni yule tu ambaye anamiliki funguo hiyo ndiye anaweza kusoma siri za kitabuni humo. Vinginevyo mtu hana uwezo wa kujua chochote cha ghaib. Kwa mfano, Mfalme anampa alama za kutambua siri waziri wake, au viongozi ambao anawatuma majimboni.

Ikiwa ufunguo wa kuzielewa alama hizo unabakia na mfalme au mawaziri, basi hakuna mtu angeweza kutambua maandishi yale yalikuwa na maana gani. Kwa namna hiyo hiyo, haku- na yoyote isipokuwa Ali na wale kumi na mmoja wa kizazi chake, anayeweza kukielewa kitabu cha Jafr-e-Jami’a.

Siku moja Amirul-Mu’minin alimpa kitabu hicho mwanae Muhammad Hanafiyya mbele ya wanae wote wengine wa kiume lakini hakuweza kuelewa chochote ndani yake ingawa alikuwa mtu mwenye elimu ya juu sana na mwerefu.

Nyingi ya amri walizotoa Maimam Maasumini hawa, au habari wakizozieleza, zilitoka kwenye kitabu hicho hicho. Watu hawa watukufu walielewa siri za vitu vyote na waliweza kueleza ni mateso yaliyokuwa yawapate wao, vizazi vyao na Shi’ah wao, kutoka kwenye kitabu hicho hicho. Jambo hili limeandikwa kwa kirefu katika vitabu vy Hadithi.

Imam Ridhaa Alitabiri Kifo Chake.

Maelezo kina ya makubaliano kati ya khalifa Mamun ar-Rashid Abbasi na Imam Ridha yameandikwa katika Sharhe-e-Mawaqif. Baada ya mawawasiliano ya maandishi kwa miezi sita, pamoja na vitisho vya Mamun, Imam Ridha alilazimika kukubali kuwa mrithi wa Khalifa. Mkataba uliandikwa na Mamun akauweka sahihi, ukitamka kwamba, baada ya kifo cha Mamun, Ukhalifa utahamishiwa kwa Imam Ridha.

Wakati karatasi ya mkataba ilipowekwa mbele ya Imam Ridha, yeye aliandika maoni haya yafuatayo juu yake ( Mkataba): “Mimi, Ali Bin Musa Bin Ja’far, natamka hapa kwamba mtumishi wa waumini (Mamun ur-Rashid), (Ajaaliwe kusimama imara kwenye haki na Allah amuongoze kwenye njia iliyonyooka), yeye ameitambua haki yetu, ambayo wengine hawakuitambua, hivyo ameunganisha yale mahusiano ambayo yalikuwa yametengwa, ametoa amani na kuridhika kwa wale watu ambao walikuwa wamefikwa na hofu, badala yake amewahuisha baada ya kuwa walikuwa wameshushwa hadi kwenye maangamizi; amewafanya kuwa wenye ustawi na wenye kuridhika wakati walikuwa wakiendesha maisha ya wasiwasi, ili kwamba aweze kuzipata rehma za Allah na hakika karibuni Allah atatoa malipo mazuri kwa wale, ambao wanatoa shukrani kwake na Yeye habatilishi malipo ya wakweli. Hakika, amenifanya mimi kuwa mrithi wake na amenitwisha mimi mamlaka makubwa madhali tu niishi baada yake?”

Mwishoni mwake, Mtukufu Imam aliandika: “Lakini Jaf-e-Jami’a inasema kinyume chake, (yaani kwamba, mimi sitaishi kumzidi yeye) na mimi mwenyewe sijui ni vipi wewe na mimi tutakavyotendewa. Ni Allah pekee, anayeamuru, ambaye amri yake ni ya kweli kabisa, na ambaye ndio hakimu bora.

Sa’d Bin Mas’ud Bin Umar Taftazani katika Sharh-e-Maqasidut-Talibin fi-ilm-e-Usulud-Din, akirejea kwenye maneno “Jafr wa Jami’a” yaliyoandikwa kwa mkono wa Imam kwenye mkataba, anatoa maoni kwa undani kwamba Imam alimaanisha kwamba kwa majibu wa Jafr na Jami’a, Mamun hangeweza kuidumisha ahadi yake na dunia iliona ni nini kilichotokea. Yule kipenzi mzawa wa kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliuawa shahidi kwa njia ya kupewa sumu. Hivyo ukweli na usahili wa elimu ya Imam Mtukufu ulithibitika na ilifahamika kwa kila mmoja kwamba familia hii iliyotukuka ilikuwa na habari juu mambo yote yanayojulikana na yasiyojulikana.

Jibril Alileta Kitabu Kilichofungwa Sili (Sealed) Kwa Ajili Ya Wasii Wa

Mtukufu Mtume:

Moja ya zawadi tukufu zilizopokelewa na Ali kupitia kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ilikuwa ni kitabu kilichofungwa kilicholetwa na Jibril. Mwanachuoni mkubwa na mwana historia, Allama Abu’l-Hasan Ali Bin al-Husain Mas’ud, anayeheshimiwa na madhehebu zote anaandika katika kitabu chake Isbatu’l- Wasiyya hivi: “Jibril na Malaika waaminiwa walileta kutoka kwa Allah Muweza, kitabu kilichofungwa, kwa Mtukufu Mtume na akamwambia: ‘wale wote walioko hapa pamoja nawe, isipokuwa wasii wako, waondoke ili niweze kukupa kile Kitab-e-Wasiyya (Kitabu cha agano la mwisho)’”

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawaamuru wale waliokuwa pale kuondoka isipokuwa Amiru’l- Mu’minin, Fatima, Hasan na Husein.

Jibril akasema: “Ewe Mtume! Allah anatuma salam Zake kwako na anasema kwamba hii ndio hati ambayo ndani yake amekufanyia ahadi na amewafanya Malaika Zake kuwa mashuhuda kwayo na kwamba Yeye Mwenye ni shahidi kwayo.”

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaanza kutetemeka na akasema: “Salaam ni Yeye na Salaam zinatoka Kwake na Salam zinarudi Kwake.”

Akikichukua kile kitabu kutoka kwa Jibril, akakisoma na akakitoa Ali - Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Hii ni ahadi na dhamana kutoka kwa Mungu Wangu kuja kwangu. Hakika nimetekeleza kazi yangu na nimefikisha ujumbe wa Allah.”

Amirul-Mu’minin akasema: “Mama yangu na baba wawe wenye kutoa kafara maisha yao kwa ajili yako! Nami pia nashuhudia kwenye ukweli wa ujumbe huu. Masikio yangu, macho, nyama na damu vinatoa ushahidi juu ya ukweli huu.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akamwambia Ali: “Hapa huu ni Usia wangu kutoka upande wa Allah. Upokee na uwe wewe ni mdhamini wake mbele ya Allah. Ni juu yangu mimi kutimiza wajibu wangu.” Ali akasema: “Nitakuwa mdhamini wake, na ni juu ya Allah kunisaidia mimi.”

Katika kitabu hiki, Amiru’l-Mu’minin ametakiwa kutimiza ahadi zifuatazo; “Kuwa na uraffiki kwa marafiki wa Allah, kuwa mkali kwa maadui wa Allah. Kuwa na subira kwa maonevu, kwa subira sana kuvumilia na kuzuia hasira wakati haki zake zinapoporwa, wakati anapotukanwa na wakati anaposhambuliwa bila haki?

Amiru’l-Mu’minin akasema: “Nakipokea, na nimeridhika nacho. Ikiwa nitaonyeshwa kuvunjiwa heshima, ikiwa hadithi zitakataliwa, ikiwa hukmu za Quran Tukufu zitapuuzwa, ikiwa Ka’ba itabomolewa kusawazishwa na aradhi, na ikiwa ndevu zangu zitapakwa damu ya kichwa changu hata hivyo nitavumilia na kuwa na subira.”

Baada ya hayo, Jibril, Michael na Malaika wengine wa karibu walitangazwa kama mashahidi wa Amiru’l- Mu’minin. Kadhalika Hasan, Husein na Fatima pia walikabidhiwa wajibu huo huo.

Matatizo na hali ambazo zilikuwa ziwakabili, hayo waliyaambiwa kila mmoja wao kwa kirefu. Baada ya hapo lile agano lilifungwa kwa sili ya dhahabu ghafi na kupewa Ali.

Agano hili lina hadithi za Allah Muweza, Hadithi za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) upinzani wa wale wenye kupinga na kubadili hukmu tukufu na matukio na majanga yote yaliy- otokea baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Na hivi ndivyo anavyosema Allah: “Na kila kitu tumekiweka ndani ya Imam (Kiongozi) mwenye kudhihirisha yaani Ali”

Kwa kifupi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alirithisha elimu yake kwa Ali na kwa kizazi chake Ali, Maimam Ma’sumin. Ingekuwa vinginevyo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingelimuita Ali “lango la elimu” na asingelisema: “Kama unataka kunufaika na elimu yangu, nenda kwenye mlango wa Ali.”

Kama Imam huyo Mtukufu asingekuwa anamiliki elimu yote Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) asingeweza kutangaza mbele ya wote, marafiki na maadui kwamba: “Niulizeni lolote mnalotaka kabla sijafa na kuwaacheni.”

Hakuna mwingine tena isipokuwa Ali tu aliyeweza kudai kamwe kuwa nayo sifa hii mwenyewe. Wakati wengine ambao waliodai kuwa na elimu walipoulizwa juu ya mambo yanayojulikana na yasiyojulikana walibaki kuaibika.

Hafidh Ibn Abdu’l-Barr Maghribi Andalusi katika kitabu Isti’ab fi Ma’rifati’l-As’hab ame- sema: “Yeyote aliyesema ‘Niulizeni mimi kabla sijafa na kuwaacheni’ alikuwa muongo isipokuwa Ali Bin Abi Talib.”

Abdul’l-Abbas Ahmad Ibn Khallikan Shafi’i katika Wafaya yake na Kitab-e-Baghdad katika Ta’rikh yake Juz. 13, uk. 163 anasimulia kwamba siku moja Maqatil Bin Sulayman, aliyekuwa mmoja wa wanazuoni mashuhuri aliyejulikana kwa uwezo wake wa kujibu maswali haraka, alitangaza mbele ya mkusanyiko wa hadhara kwamba: “Niulizeni mimi kuhusu lolote chini ya mbingu.”

Mtu mmoja alitoa swali hili kumuuliza yeye: “Ni lini Nabii Adam alipofanya Hijja? Ni nani aliyemkata nywele alipomaliza? Maqatil alitatizwa na akabakia kimya.

Mtu mwingine akamuuliza: “Je, mdudu chungu ananyonya chakula kupita tumboni au kupitia njia nyingineyo? Kama ni kupitia tumboni, liko wapi tumbo na utumbo wake?”

Maqatil aliduwaa tena. Akasema: “Allah ameliweka swali hili moyoni mwake, ili kwamba majivuno juu ya elimu yangu yaweze kuwekwa kwenye aibu.”

Ni yule tu ambaye anao uwezo wa uhakika kikamilifu wa kujibu maswali yote anayeweza kudai hivyo. Katika Umma mzima hakuna yeyote isipokuwa Ali Bin Abi Talib aliyekuwa na hadhi hiyo.

Kwa vile alikuwa “lango la elimu” ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), alikuwa na ujuzi kamili wa mambo yote, yanayojulikana na yasiyojulikana kama vile alivyokuwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa hiyo, alikuwa anaweza kusema, “Niulizaeni mimi” naye akatoa majibu ya papo kwa papo na yenye kukinakisha kwa maswali yote. Miongini mwa Masahaba, vile vile, hapakuwa na mtu hata mmoja isipokuwa Ali, ambaye alitoa madai kama haya.

Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, Muwaffaq Bin Ahmad Khawarizmi katika Manaqib, yule Khwaja maarufu Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, Baghawi katika Mu’jim, Muhibu’d-Din Tabari katika Riyazu’n-Nuzra Juz. 2, uk. 198 na Ibn Hajar katika Sawa’iq uk. 76 wamemnukuu Sa’id Bin Musayya akisema kwamba hakuna yeyote katika Masahaba, isipokuwa Ali Bin Abi Talib aliyewahi kusema: “Niulizeni mimi lolote mnalotaka.”

Tangazo La Ali La Niulizeni Mimi Na Riwaya Za Masunni.

Idadi kubwa ya ulamaa wenu mashuhuri, kama Ibn Kathir katika Tafsir yake, Juz. 4, Ibn Abdul’l-Birr katika Isti’ab, Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, Muhiy’d-din Khawarizmi katika Manaqib, Imam Ahmad katika Musnad, Hamwaini katika Fara’id, Ibn Talha katika Durru’l-Manzum, Mir Seyyed Ali Shafi’i katika Mawaddatu’l-Qurba, Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika Hilyatul-Auliya, Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibus-Su’ul, Ibn Abi’l-Hadid katika Nuhju’l-Balaghah na baadhi ya wanazuoni wengineo mashuhuri wa Sunni wamesimulia pamoja na tofauti kidogo ya maneno, kutoka kwa Amir Bin Wathila, Ibn Abbas, Abi Sa’id al-Buhturi, Anas Bin Malik na Abdullah Bin Mas’ud kwamba Amiru’l-Mu’minin alitangaza kutoka kwenye Mimbar kwamba: “Enyi watu! Niulizeni mimi chochote mnachotaka kabla sijafa, hakika moyo wangu ndio ghala ya elimu yote. Niulizeni mimi kwa sababu ninayo elimu ya yale yote yaliyopita na ya yale yote yatakayokuja?

Abi Dawud katika Sunan yake uk. 356, Imam Ahmad Bin Hanbali katika Musnad Juz. 1, uk. 278, Bukhari katika Sahih Juz. 1, uk. 46 na Juz. 10, uk. 241 wamesimulia kwa mam- laka kabisa kwamba Ali alisema: “Mnaweza kuniuliza juu ya chochote mnachotaka, ninaielewa asili ya kila jambo ambalo mngeliuliza juu yake. Madai Ya Ali Kwamba Angeweza Kuhukumu Kesi Kwa Mujibu Wa Taurati Na Vile Vile Kwa Injili.

Sheikh Sulayman Bakhi Hanafi katika Yanabuu’l-Mawadda sura ya 14, uk. 74 anasimulia kutoka kwa Mu’affaq Bin Ahmad Khawarizmi na Sheikhil-Islam Hamwaini anasimu- lia kutoka kwa Abu Sa’id Buhturi kwamba yeye (Abu Sa’id) amesema: “Nilimuona Ali juu ya Mimbar akiwa amevaa joho la Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), upanga na kilemba chake. Alikifunua kifua chake na akasema; “Niulizeni mimi chochote mnachotaka, kabla sijafa, kwa sababu kifua changu kimebeba maarifa mengi sana.

Hili ni tumbo langu ambalo ni ghala ya elimu. Haya ni mate ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hiki ndicho Mtukufu Mtume alichonilisha kama nafaka. Ninaapa kwa Allah kwamba ikiwa zulia litatandikwa na nikakaa juu yake, hakika nitamuelekeza mfuasi wa Taurati, kwa mujibu wa Taurati. Nitamuelekeza mfuasi wa Injili kwa mujibu wa Injili mpaka Taurati na Injili, zote ziweze kuongea na kutoa ushahidi kwa yafuatayo: Ali amesema ukweli na fatwa ambayo ameitoa ni ya kulingana na kile kilichodhihirishwa ndani yetu. Wakati unapokisoma hicho kitabu huelewi kiasi hiki.

Elimu Ya Ali Kuhusu Aya Za Qur’ani Tukufu.

Sheikhul-Islam Hamwaini katika Faraid na Muayyidud-Din Khawarizmi katika Manaqib yake anasimulia kwamba huyu Imam Mtukufu alisema maneno haya kutoka mimbarini “Niulizeni mimi kuhusu nini msichokielewa kabla sijafa.

Naapa kwa Allah aliyetawanyisha nafaka na akamuumba mwanadamu, kwamba kama mtaniuliza mimi kuhusu aya yoyote, ya Kitabu kitukufu cha Allah, nitakuelezeni juu yake - lini iliposhuka, ni wakati wa mchana au usiku, kituo gani cha njiani, nyikani au mlimani, kumhusu nani iliteremshwa, muumini au dhidi ya mnafiki, nini Allah amemaanisha kwayo, na kama aya hiyo ni ya jumla au ni aya maalum.

Hapa ndipo Ibn Kawwa, Khawarij huyu, akasimama na kusema: Hebu nifahamisha ni nini anachomaanisha Allah kwa kusema, “Wale walioikubali Imani na wakatenda matendo mema ndio wabora wa watu.”

Imam Mtukufu akasema: “Aya hii inaashiria kwetu na wafuasi wetu, ambao nyuso zao, mikono na miguu vitakuwa vyenye kung’ara Siku ya Kiyama. Watatambuliwa kwa vipaji vya nyuso zao.”

Imam Ahmad Ibn Hanbal katika Musnad yake na Sheikh Sulayman Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda sura ya 14 uk.74, wanasimulia kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Ali alisema maneno haya akiwa mimbarini: “Niulizeni mimi kuhusu nini msichokielewa kabla sijafa. Hakuna aya ambayo kwamba siielewi zaidi kuliko mtu mwingine yeyote anavyoielewa. Ninajua ni vipi na wapi ilikoshukia. Niulizeni kuhusu ghasia yoyote, kwani hakuna ghasia ambayo kwamba simjui aliyeisababisha na ni nani aliyeuawa ndani yake.” Ibn Sa’d katika Tabaqat Abu Abdullah Muhammad Bin Yusuf Ganji Shafi’i katika Kifayatu’t-Talib sura ya 52, na Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika Hilyatu’l-Auliya Juz. 1, uk. 68 wanasimulia kwa rejea sahihi kwamba Amirul-Mu’minin alisema: “Wallahi, hakuna aya iliyoteremshwa ila ninajua kwa uhakika ni kuhusu nani imeshushwa, na wapi ilishushwa. Hakika Allah amejaalia juu yangu moyo wenye hekima na ulimi fasaha.”

Katika vitabu hivyo hivyo imesimuliwa kwamba Amiru’l-Mu’minin alisema: “Niulizeni mimi kuhusu Kitabu cha Allah, Hakuna aya hata moja ambayo kwamba sijui iwapo kama imeshushiwa vilimani ama nyikani.”

Elimu Ya Ali Kuhusu Watu Wanaoongoza Au Wanaopotosha

Khawarizmi anasimulia katika Manaqib yake kutoka kwa A’mash, ambaye amesimulia kwamba Ubaya Bin Rab’i alisema: “Ali mara nyingi alizoea kusema ‘niulizeni kuhusu nini msichokielewa kabla sijafa, naapa kwa Mungu Wangu kwamba hakuna mbuga ya kijani au ardhi ya jangwa, au kikundi cha watu kinachopotosha watu mia moja au kuongoza watu mia moja, ila ninawajua.

Ninawajua vizuri zaidi ya yeyote wale wanaoongoza watu au wanaowachochea kwenye maovu hadi Siku ya Hukumu.”

Jalalu’d-din Suyuti katika Ta’rikhu’l-Khulafa uk. 124, Badru’d-din Hanafi katika Umdatu’l-Qari, Muhibu’d-din Tabari katika Riyazu’n-Nuzra Juz. 2, uk. 198, Suyuti katika Tafsir-e-Itqan Juz. 2, uk. 319, na Ibn Hajar Asqalani katika Fathu’l-Bari Juz. 8, uk. 485 na pia katika Tahdhibu’t-Tahdhib Juz. 7, uk 338 wanasimulia kwamba Ali alisema: “Niulizeni chochote mnachotaka, na ninaapa kwa Allah kwamba nitawaambia mambo yote yatakayotokea hadi Siku ya Kiyama.

Kama mtaniuliza kuhusu Kitabu cha Allah, naapa kwa Mungu Wangu kwamba hakuna aya hata moja ambayo siielewi vizuri. Ninajua iwapo kama aya ilishushwa wakati wa usiku au mchana, nyikani au katika vilima”

Anaweza mtu yeyote, isipokuwa yule mwenye elimu ya ghaib, kutoa madai kama hayo mbele ya wote, marafiki na maadui?

Kutabiri Kwamba Sinan Bin Anas Alikuwa Ndiye Muuaji Wa Imam Husain.

Ibn Abil-Hadid Mut’azali ameandika hadithi hizo hizo katika Sharh-e-Nahjul’l-Balagha Juz. 1, uk. 208 kutoka Gharat cha Ibn Hilal Saqafi. Yeye anasema kwamba mtu mmoja alisimama na akasema: “Hebu nijulishe kuhusu nywele za kichwa changu na ndevu zangu:”

Imam Mtukufu akasema: “Rafiki yangu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alinifahamisha kwam- ba kuna malaika katika mzizi wa kila unywele wa kichwa chako nayekulaani wewe. Kuna shetani katika mzizi wa kila unywele wa ndevu zako anayekupotosha. Kuna ndama katika nyumba yako atakayemuua mtoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).”

Mtu huyu alikuwa ni Anas Nakh’iy, ambaye mwanae, Sinan, alikwua kitoto kidogo wakati wa utabiri wa Ali. Mnamo mwako 61 Hijiria, Sinan alifika Karbala na alikuwa mmoja wa wauaji wa Imam Husain.

Baadhi ya muhadithina wanasema kwamba yule mtu ambaye aliuliza lile swali alikwua Sa’d Bin Abi Waqas na kwamba mwanae (ndama) alikuwa ni yule mlaaniwa Umar Bin Sa’d ambaye alikuwa ndio kiongozi wa majeshi ya Yazid, mtu muhimu katika masaib ya Karbala.

Vile vile inawezekana kwamba wote wawili waliuliza swali hilo katika mikutano miwili tofauti. Simulizi hizi hata hivyo, zinaonyesha kwamba Imam Mtukufu alivuta mazingatio kwenye ukweli kwamba alikuwa anatambua mambo ya Ghaib.

Kuutabiri Ule Ushika Bendera Wa Habib Bin Ammar

Ulamaa wenu mashuhururi, kama Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad na Ibn Abi’l- Hadid katika Sharh-e-Najur-Balagha, Jz. 1, uk. 208 wamesimulia kwamba wakati wa Ukhalifa wake wa dhahiri, Amirul-Mu’minina alikuwa amekaa katika msikiti wa Kufa pamoja na sahaba zake wakati mtu mmoja aliposema kwamba Khalid Ibn Uwaita alikuwa amefariki huko Wadiyu’l-Qurba.

Mtukufu Imam akasema: “Huyo hajakufa, na hatakufa mpaka aje kuwa kiongozi wa jeshi lililopotoka. Mshika bendera wake atakuwa Habib Bin Ammar.”

Kijana mmoja akasimama kutoka kwenye ule mkusanyiko na akasema: “Mimi ndiye Habib Ibn Ammar, na ni mmojawapo wa marafiki zako wakweli na waaminifu.”

Ali akasema: “Mimi sijasema uongo na kamwe sitakujasema uongo. Nipo, kama imekuwa namuona Khalid, kiongozi wa jeshi lililopotoka, na wewe ndio mshika bendera wake. Watu nyie mtaingia msikitini humu kupitia pale akiashiria kidole kwenye mlango Babu’l-fil) na kitambaa cha bendera hiyo kitachanwa na lile lango la msikiti.”

Miaka ikapita. Wakati wa Ukhalifa wa yule muovu Yazid, Ubaidullah Bin Ziyad akawa ndiye gavana wa Kufa na akatuma majeshi yenye kutisha kwenda kupigana na Imam Husain. Siku moja wengi wa wale waliousikia utabiri wa Amirul-Muuminin kuhusu juu yao Khalid na Habib Ibn Ammar, walikuwa wamekaa Msikitini humo wakati kelele za askari hao na miito yao zikisikika.

Watu hao waliona kwamba Khalid Ibn Uwaita, kiongozi wa lile jeshi lililopotoka wakienda Karbala kupigana dhidi ya mtoto wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), waliingia Msikitini humo kupitia mlango ule ule wa Babu’l-Fil kufanya onyesho. Habib Ibn Ammar alikuwa amebeba bendera. Wakati Habib alipoingia msikitini humo, kitambaa cha bendera yake kilichanwa.Wanafiki walionyeshwa ni jinsi gani elimu ya Ali ilivyokuwa nzito na jinsi ukweli wa utabiri wake ulivyokuwa. Hivi, dalili hizi na utabiri huu havithibitishi kwamba Ali alikuwa na elimu ya ghaib? Kama utasoma kwa makini Nahju’l-Balagha ambacho ni mkusanyiko wa khutba na semi tukufu za Ali, utagundua kwamba mna utabiri mwingi wa wazi kuhusu majanga na machafuko, mambo kuhusu wafalme wakubwa, maasi ya watu wa Zanj, utawala wa wa-Mongoli, utawala wa Genghis Khan, Maelezo ya uonevu wa makhalifa na matendo yao kwa Shi’ah.”

Ibn Abil- Hadid ameyazungumzia mambo haya katika Nahjul-Balagha Juz.1, uk. 208-211. Yule Mwanazuoni mkubwa Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, vile vile ameyazungumzia jinsi Ali mara kwa mara alivyoonyesha elimu yake nzito ndani ya khutuba zake na utabiri.

Kutabiri Ukandamizaji Wa Mu’awiya

Imam huyu, Mtukufu vile vile alitabiri kwamba Mu’awiya atawashinda watu wa Kufa na atawaamuru kumkataa yeye (Ali). Kwa mfano, Mtukufu Imam alisema; Mara tu, baada yangu, mtu mwenye koo kubwa na tumbo nene atawatawaleni ninyi. Atakula kila atakachokipata, na kama hatakipata, basi atakidai. Hivyo mnapaswa mje mumuuwe yeye huyo.

Lakini kamwe hamtamuua. Hakika, mara moja atawaamrisheni kuniita mimi kwa majina maovu na kuwawekeni mbali na mimi. Hivyo ninawaruhusuni kunitukana mimi kwa sababu ni maneno ya mdomoni tu, ambayo kwangu mimi ni chanzo cha utakaso na kwenu ninyi ni ulinzi dhidi ya madhara ya mtu huyu.

Lakini, kwa vile kujitenga na chuki vinatoka moyoni, msijechukua tabia ya chuki juu yangu. Nilizaliwa katika asili ya Uislam na Umoja wa Allah na nimekuwa wa mwanzo katika mambo ya Imani na Hijra (kuhama).”

Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha, na wanazuoni wenu wengine wa vyeo vya juu wanathibitisha kwamba yule mtu aliyeashiriwa hapo juu alikuwa ni Mu’awiya Bin Abu Sufyan. Utawala wake ulipokuwa imara uliwaamuru watu kumtukana na kumkashifu Ali. Mwenendo huu mbaya uliendelea kwa miaka themanini, na Imam Mtukufu alitukan- wa kwenye misikiti, na kwenye khotuba za sala za Ijumaa.

Wakati Umar Bin Abdu-Aziz Amawi alipokuwa Khalifa, hata hivyo, aliikataza tabia hii ya kuchukiza. Kutabiri kwa Ali juu ya mwenendo huu muovu ni ushahidi mwingine wa kuwa kwake na elimu ya ghaib. Ali alibashiri matukio mengi ambayo yalithibitishwa baada ya miaka mingi.

Kutabiri Mauaji Ya Dhu’th-Thadiyya.

Kabla ya vita vya Nahrwan, Imam Mtukufu alitabiri kuuawa kwa Makhawarij hususan ya Tazmala anayejulikana kama “Dhu’th-Thadiyya.”

Alibashiri pia kwamba kati ya Khawarij hao sio hata watu kumi watakaosalimika na kwamba kati ya wailsam sio watu zaidi ya kumi watakaouawa. Ibn Abil-Hadid na yule mwanazuoni mkubwa, Balkhi, na wengineo wamesimulia kwamba kile alichokisema Imam kilitokea kuwa kweli. Ibn Abil-Hadid katika Shar-e-Nahjul-Balagha Juz. 1, 425 anaandika hivi: “Hii ni moja ya zile hadithi, ambazo zimesimuliwa takriban kwa mfululizo mwingi. Inajulikana sana na imesimuliwa kwa mapana sana. Inachukuliwa kama moja ya miujiza ya Mtukufu Imam.”

Unaona kwa hiyo ile tofauti kubwa sana kati ya Ali na “Makhalifa’ wengine. Kama angekuwa hana elimu ya ghaib, angeweza vipi kutabiri matukio ambayo yalitokea miaka mingi baadae?

Kwa mfano, alitabiri kuuawa kwa Mitham Tammar katika mikono ya Ubaidullah Bin Ziyad, kuuawa kwa Juwairiyya na Rashid Hajari kulikofanywa na Ziyad, na kuuawa kwa Amr Bin Humuq katika mikono ya marafiki wa Mu’awiya. Alitabiri kufa shahidi kwa mwanae, Imama Husain kwa kuwaambia watu wengi vile vile

Utabiri Juu Kufa Shahidi Kwake Mwenyewe, Na Kuhusu Ibn Muljim

Alitabiri vilevile kifo chake menyewe cha kishujaa. Yeye alisema kwamba muuaji wake alikuwa Abdu’r- Rahman Bin Muljim Muradi ingawa mtu yule aliyelaaninwa alidai kuwa mwaminifu na mwenye kumuunga mkono. Ibn Kathir anaandika katika Usudu’l-Ghaiba sura ya 4, uk. 25 na wengine pia wamesimulia kwamba Ibn Muljim alikuja kwa Imam Mtukufu, mashairi yenye kumtukuza Amiru’l- Mu’minin mbele ya Masahaba. Alisema: “Wewe ndio kiongozi wa kweli, uliye huru kutokana na makosa yote na mashaka.

Wewe ni mkarimu na mpole nawe u mtoto wa wale wahenga wenye roho za simba na majasiri ambao walitambulika sana kwa ushujaa tangu mwanzo kabisa; ewe mrithi wa Mtume! Allah amekupa wewe hadhi hii na akajaalia juu yako zile sifa na umaarufu mkubwa ulioko ndani ya Qur’ani Tukufu.

Masahaba walishangazwa sana na ufasaha wake na mapenzi makali. Kisha mtukufu Imam akamjibu kwa ubeti: “Nakushauri unipende kwa moyo mweupe, ingawa ninajua wewe ni mmojawapo wa maadui zangu.” Ibn Hajar anasema katika Sawaiq-e-Muhriqa uk. 82 kwamba Mtukufu Imam, akimjibu Ibn Muljim kwa ushairi, alisema: “Namuombea yeye kuishi, lakini yeye anataka kuniua.

Huyu rafiki wa wazi anatokana na ukoo wa Murad.” Abdu’l-Rahman akasema: Pengine ulilisakia jina langu na kwamba unalichukia jina langu hilo.”

Imam Mtukufu akasema: Laa sio hivyo, ninajua bila shaka hata kidogo kwamba wewe ni muuaji, na haitachkua muda mrefu kabla hujazipakaza ndevu zangu nyeupe na damu ya kichwa changu. Ibn Muljim akasema: “Kama hivyo ndivyo, unaweza kufanya niuawe.” Masahaba nao pia walisisitiza kwamba angeuawa. Lakini Mtukufu Imam akasema: “Kamwe haitawezekana. Dini yangu hairuhusu hukumu ya kisasi kabla ya kutendeka hio dhambi. Ninajua kwa yakini kuwa wewe ndio muuaji wangu, lakini hukmu za dini zinahusu matendo ya dhahihri. Kwa vile bado hujatenda tendo la kidhalimo, siwezi kutoa adhabu yoyote juu yako.”

Thomas Carlyle wa Uingereza anaandika katika mfululizo wa hotuba zake za, ‘Juu ya Mashujaa,’ kwamba Ali Bin Abi Talib aliuawa kwa sababu ya uadilifu wake. Yaani ni kwamba, kama angehukumu kisasi kabla ya kutendeka hiyo dhambi, angeweza kwa haki- ka, kubakia salama. Hii ndio iliyokuwa kawaida kwa wafalme wa dunia ambao, mara moja, walimuua yeyote - hata ndugu wa karibu ambaye waemmhisi kuwa ni adui yao.

Tukio hili ni ushahidi mwingine wa ukweli kwamba hakuna yeyote mwenye elimu ya ghaib isipokuwa aliye Mtume au Imam ambaye ni Ma’sum (safika kwa maana ya kuhifadhiwa kutokana na kutokosea). Kama angekuwa mwenye kutokosea tu, kwa kule kuwa kwake mwenye kutambua hali halisi ya mambo, angeweza kusababisha ghasia.

Lakini Mtume au Imam, ambaye pia ni mwenye kutokosea, baada ya kumtambua muuaji wake, huwa hatoi adhabu kabla ya kutendeka hasa kwa hiyo dhambi. Mifano hii yote haitoshelezi kuthibitisha kwamba huyu Imam Mtukufu alikuwa ni utambuzi kamili wa matukio yajayo siku za baadaye?

Ubora Wa Ali

Sheikh Sulayman Balkhi anasimulia mwanzoni mwa Yanabiu’l-Mawadda zile beti za Amiru’l-Muminin ambazo zimechukuliwa toka kwenye Durru’l-Munazzam cha Ibn Talha Shafi’i. Mtukufu Imam alisema; “Kwa hakika, mimi ninayo elimu kamili ya vianzio vyote, na ninashutumiwa kuficha elimu ya viishilizio vyake.

Mimi ndio mfachuaji wa mambo yaliyojificha na yasiyofahamika ninayo mbele yangu kumbukumbu ya yote yaliyopita na ya wakati huu. Kwa kweli ninayo mamlaka juu ya vitu vyote, vikubwa na vidogo, na elimu yangu inazingira ulimwengu wote.

Imam Mtukufu huyu pia alisema: Ninaweza kuwabebesha ngamia sabini kwa mzigo wa sherehe ya Suratul-Fatiha (ya Qur’ani Tukufu).” Mtukufu Mtume amesema: “Mimi ni jiji la elimu na Ali ndio lango lake. Pia Allah Muweza anasema tuingie kwenye nyumba kupitia milangoni. Hivyo yeyote anayetaka kupata elimu hanabudi ya kupitia mlangoni.”

Mbali na mambo mengine, hii mifano miwili inatosha kuthibitisha ubora wa Ali dhidi ya wengine. Angepaswa, moja kwa moja, kumrithi Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kama kiongozi wa Waislam. Wakati ni ukweli unaokubalika kwamba Ali alikuwa ndio aalim mkubwa sana kuliko wote, ni kichekesho kabisa kuchukulia kwamba mtu asiyekuwa na elimu alikuwa na haki ya kushika nafasi yake. Allah Asingeweza Kukubali Kwamba Mtu Mbora Ashikiwe

Nafasi Yake Na Mtu Duni.

Hata Ibn Abi’l-Hadid katika kitabu chake, kuhusu hotuba ya kwanza anasema: “Mtu mwenye hadhi ndogo alipewa upendeleo juu ya mtu wa hadhi iliyotukuka sana.” Kauli hii ni yeye utambuzi wa ubora wa Imam Mtukufu lakini, ukaidi wake unamlazimisha kuongeza, “Allah amekubali kwamba yule dhaifu awe badala ya yule mbora.”

Kauli hii inahuzunisha, kuja kama ilivyo, kutoka kwa mtu kama Ibn Abi’l-Hadid. Watu wote wenye burasa wataikataa. Madai yake yanapingana na uadilifu wa Allah, lakini kwa hakika Allah ni Muadilifu sana Mwenye hekima.

Hatoi kipaumbele kwa mtu dhaifu na kumruhusu kushika nafasi ya mwenye haki zaidi. Allah anasema katika Qur’ani Tukufu,

{ﻗُﻞ ﻫﻞ ﻳﺴﺘَﻮِي اﻟﱠﺬِﻳﻦ ﻳﻌﻠَﻤﻮنَ واﻟﱠﺬِﻳﻦ  ﻳﻌﻠَﻤﻮنَ ۗ{9

“Sema: wale wanaojua na wale wasiojua wanafanana? (39:9)

Tena anasema: “Hivi basi ni yule anayeongoza kwenye ukweli aliyebora zaidi kufuatwa, au yule ambaye binafsi haendi sawa labda aongozwe?” Ibn Abi’-Hadid anakubali kwa uwazi kabisa kwamba Ali alikuwa ndio mtu hasa aliyestahi- ki Ukhalifa. Anasema katika Sharh-e-Nahjul-Balagha Juz. 1, uk. 4, “Hakika Ali alikuwa mbora kuliko binadamu wote baada ya Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.). Kuhusu hili swala la Ukhalifa, alikuwa ndie mtu mwenye haki zaidi ya Waislam wote.”

“Jiji La Elimu” Inathibitisha Haki Ya Ali Kuwa Khalifa Wa Kwanza

Zaidi ya hayo, ile kauli yenye kueleweka vyema ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), mwishoni mwa hadithi hii, inathibitisha ubora wa Ali, ikisema: “Yule ambaye anapenda kutafuta elimu ni lazima aje kwenye mlango.” Hili neno “Mlango” hapa bila shaka ni Ali.

Hivyo ni huyu lango kuu la uongozi ambaye Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ametuamuru kum- fuata, ndiye mwenye haki zaidi au yule ambaye watu wa memchagua? Jibu liko wazi. Amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) lazima itiiwe. Pili, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) pia aliweka kigezo cha kipaumbele na upendeleo, ambacho ni kule kuwa na elimu ya juu zaidi.

Sheikh: Kama Ali alikuwa na haki ya kipaumbele kwa sababu ya elimu yake ya juu, Mtukufu Mtume Allah (s.a.w.w.), angetamka kwa kupambanua ili kwamba Umma ungejua kwamba utii kwake yeye ulikuwa ni wajibu. Lakini hakuna kauli ya namna hiyo inayoweza kuonekana.

Muombezi: Ninapata uchungu sana kusikia matamshi kama hayo kutoka kwako. Una bahati mbaya ya kuwa na tabia ya kukataa kila kitu - hata ukweli wa wazi - pale unapopin- gana na maoni yako. Ndugu yangu mheshimiwa. Nimekuwa nikizisimulia kauli hizo kwa mikesha kumi iliyopita.

Hadhara hii na baadhi ya magazeti ya hapa yatashuhudia ukweli wa jambo hili. Lakini bado unasema hujaona kauli ya wazi ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hata vitabu vyenu wenyewe vya Sahih vimejaa tele matamshi ya wazi kuhusu jambo hili. Hebu ngoja nikuulize hivi: Je Umma unahitaji elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na Sirat (hadithi na Suna)?

Sheikh: Hilo ni jambo la dhahiri. Masahaba wote na Umma wanahitaji uongozi, elimu na Sunna na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) mpaka Siku ya Kiyama.

Muombezi: Allah akubariki! Kama ingekuwa hakuna hadithi zingine makhsusi ila Hadithi ya Madina, hata hii ingekuwa inatosha kuthibitisha nukta yangu. Mtume kwa uwazi kabisa anasema: “ Mimi ni jiji la elimu na Ali ndie lango lake, yule ambaye anataka kupata elimu hanabudi kuja kwenye mlango huu.”

Kwa Mujibu Wa Mtukufu Mtume Ali Aliwazidi Wengine Wote Katika Elimu.

Ni tamko gani linaweza kueleweka wazi zaidi ya hadithi hii ambamo Mtukufu Mtume anasema kwamba “yeyote anayetaka kupata manufaa ya elimu yangu hana budi kuja kwenye mlango wa Ali kwa sababu yeye ndie lango la elimu!” Sasa kunakaribia kucha.

Kwa usiku mzima nimekuwa wote nimekuwa nikijadili hoja hii kwa shauku kubwa na nimechukua muda wenu wote. Lakini sasa hivi umeipoza jazba yangu. Kama wahenga wako, unakataa kusikiliza, na matokeo yake, ukipuuza maelezo yangu yote yenye kukubalika, unaukataa ukweli uliodhahiri.

Ni tamko gani litakalokuwa bora kuliko hili tamko la kuhusu elimu? Hivi mtu yeyote mwenye akili timamu atatetea kumkataa mtu mwenye hekima kwa kumpendelea mtu asiye na elimu? Bila shaka jibu ni hapana, kwa hiyo, lazima ukubali hoja yangu, ambayo sio hoja yangu tu bali ni kanuni inayokubalika kwa watu wote wenye elimu: kwa vile Ali alikuwa mbora katika elimu na hekima miongoni mwa Umma wote, utii kwake ni wajibu.

Hali kadhalika, kama nilivyokwishataja, ulamaa wenu mashuhuri, kama Imam Ahmad Bin Hanbali (Musnad), Khawarizmi (Munaqab) na pia yule mkaidi, Ibn Hajar Makki katika Sawa’iq wamemnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Katika Umma wangu, Ali Bin Abu Talib amewazidi wengine wote katika elimu.”

Hapakuwa na hata mtu mmoja miongoni mwa Masahaba aliyelingana na Ali katika elimu. Ibn Maghazili Shafi’i katika Munaqab, Muhammad Bin Talha katika Matalibus-Su’ul, Hamwaini katika Fara’id na Sheikh Sulayman Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, Sura ya 14, wanasimulia kutoka kwa Kalbi kwamba yule mwanazuoni mkuu wa Umma, Abdullah Ibn Abas, alisema: “Elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) inatoka kwenye elimu ya Allah, elimu ya Ali inatoka kwenye elimu ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Elimu yangu na elimu ya masahaba wote, ikilinganishwa na ya Ali, ni kama tone la maji mbele ya zile bahari saba.”

Katika Nahju’l-Balagha, khotuba ya 108, Ali anasema: “Sisi (Maimam ma’sumin) ni Mti wa Utume, ndio makazi ya salama ya ujumbe mtakatifu, mahali pa mashukio ya Malaika, migodi ya elimu na ndio vyanzo vya hekima.”

Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha yake Juz. 2, uk. 236 akitoa maoni yake kuhusu khotuba hii, anasema: “Sifa hii alikuwa nayo dhahiri Mtukufu Imam kwa vile Mtume wa Allah alisema: “Mimi ni jiji la elimu na Ali ndio lango lake, yeyote anayetaka kupata elimu hana budi kuja kwenye lango hilo.”

Pia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Ali ndio hakimu bora miongoni mwenu.”

Ibn Abi’l-Hadid anaendela kusema: “Welekevu wa hukumu unahitaji aina nyingi za elimu: kiwango chake cha elimu kilikuwa ni cha juu sana kiasi kwamba hakuna yeyote aliyeweza kulingana naye. Kwa kweli hakuna yeyote aliyemkaribia. Hivyo alikuwa na haki ya kudai kwamba: “sisi ni migodi ya elimu ya vyanzo vya hekima.” Kwa hiyo baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) hakukuwa na yeyote aliyekuwa na haki zaidi ya kudai mambo haya kwa ajili yake binafsi.”

Ibn Abdu’l-Birrr katika Isti’ab Juz. 3, uk. 38, Muhammad bin Talha katika Matalibu’s- Su’ul uk. 23 na Kadhi Aiji katika Mawaqif, uk. 276 wamemnukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Ali ndio hakimu bora miongoni mwenu nyote.”

Suyuti katika Ta’rikhu’l-Khulafa uk. 115, Hafidh Abu Nu’aim katika Hilyatu’l-Auliya Juz.1, uk. 65, Muhammad Jazari katika Asniu’l-Matalib uk. 14, Muhammad Bin Sa’d katika Tabaqa uk. 459, Ibn Kathir katika Ta’rikh-e-Kabir, Juz. ya 7, uk. 359, na Ibn Abdu’l’Barr katika Isti’ab Juz. 4 uk. 38, wanamnukuu Umar Ibn Khattab akisema: “Ali ndie hakimu bora miongoni mwetu.”

Imesimuliwa katika Yanabiu’l-Mawadda kwamba Ibn Talha, mwandishi wa Durru’l-Munazzam anasema: “Huna budi kujua kwamba siri zote na miujiza ya vitabu vitakatifu inakuwamo ndani ya Qur’ani Tukufu. Chochote kilichoko ndani ya Qur’ani Tukufu kimo ndani ya Suratul-Fat’ha. Chochote kilichomo ndani ya Suratul-Fat’ha kimo ndani ya aya ya Bismillah ar-Rahman ar-Rahim (kwa jina la Mwenyezi Mungu mwingi wa neema, mwenye kurehemu.).

Chochote kilichoko ndani ya aya Bismillah ar-Rahman ar-Rahim kimo ndani ya Ba (B) ya Bismillah. Kila kilicho ndani ya Ba ya Bismillah kimo ndani ya doti iliyoko chini ya Ba ya Bismillah. Ali alisema “Mimi ndio lile doti ambayo iko chini ya herufi Ba ya Bismillah.

Pia Sulayman Balkhi katika Yanbiu‘l-Mawadda anamsimulia ibn Abbas akisema “Safari moja kwenye usiku na mbaramwezi baada ya sala ya Isha, Ali, akinishika mkono alinion- gozea kwenye makaburi ya Baqi na akasema: “Abdullah! Soma” Nikaisoma aya ya Bismillah ar-Rahman ar-Rahim. Yule Imam Mtukufu aliendelea kunielezea siri na miujiza ya ile herufi ya Ba ya kwenye Basimillah mpaka mapambazuko.”

Madhehebu zote kwa pamoja kwamba kuhusiana na elimu yake ghaib na kuwa kwake ndio mrithi wa elimu ya Mitume, Ali anashikilia nafasi ya pekee miongini mwa Masahaba wote. Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matalibu’s-Su’ul, Khatib-e-Khawarizmi katika Manaqib na Sulayman Balkh Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda wamesimulia kutoka kwenye Durru’l-Munazzam cha Ibn Talha Halbi kwamba Ali alisema: “Niulizeni mimi kuhusu mambo ya ghaib na miujiza isiyojulikana, kwa sababu kwa kweli mimi ndio Mrithi wa elimu ya Manabii Watukufu na Mitume wa Allah.”

Pia Imam Ahmad Bin Hanbal katika Musnad, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l- Balagha na Sulayman Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda wanasimulia kwamba Ali alitamka kutoka kwenye mimbari kwamba: “Niulizeni mimi kuhusu lile msilolielewa kabla sijafa. Ulizeni toka kwangu kuhusu njia za angani kwa sababu, kwa hakika ninajua zaidi kuhusu njia zile kuliko hizi njia za ardhini.” Ali alifanya hivi zamani sana kabla ya kugunduliwa darubini (Telescope). Watu mara kwa mara walimuuliza yeye kuhusu maumbile ya kwenye anga naye aliyajibu maswali yao.

Maelezo Ya Kanda (Zones ) Za Angani Yanavyokubaliana Na Elimu

Ya Kisasa Ya Unajimu.

Yule mwanazuoni Mkuu wa hadithi, Sheikh Ali Ibn Ibrahim Qummi wa karne ya 3 H.A katika sherehe yake ya Sura ya Saffa (37), yule mwanazuoni mashuhuri, Sheikh Fakhru’d- Din Ibn Tarih Najafi, anayejulikana kwa ucha–Mungu wake, katika Kitabu’l-Lighat Ma’rafat-e-Majma’ul-Bahrain, kilichokusanywa takriban mika 300 iliyopita, na Allama Mullah Muhammad Baqir Majlis, katika Biharu’l- Anwar Juz. 14 wanasimulia kwamba Ali alisema: “Zile nyota zilizoko mbinguni zimejazwa miji kama dunia hii ilivyo.” Sasa tafadhali sana hebu kuwa mkweli. Wakati ule hakukuwa na fikra ya unajimu wa kisasa.

Ulimwengu uliikubali ile dhana ya Ptolem kwamba dunia ndio kitovu cha ulimwengu. Ikiwa mtu alielezea kitu kipya kuhusu maeneo ya nyota na kikaja kuthibitishwa kuwa ni kweli miaka elfu moja baadae, hutaweza kusema kwamba alikuwa na elimu ya ghaib?

Ali Alizimudu Sayansi Zote

Ukweli ni kwamba, baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), Ali alikuwa ndio mtu mjuzi zaidi katika falsafa, fasaha ya lugha, fiqih (sharia), unajimu, elimu ya nyota za angani Jafr (ubashiri) hisabati, ushairi, ufasaha wa uongeaji ( rhetonic) na fani ya kuandika kamusi. Katika Sayansi zote, alitoa mchango muhimu sana ambao wataalam katika nyanja hiyo wameuchukua kama msingi wa maendeleo ya zaidi.

Kwa mfano, alimuabia Abu’l-Awadu’d-Du’ali (Mwandishi ambaye kwa jumla anasadikiwa kuhusika na ugunduzi wa irabu (alama) za kiarabu cha maandishi) kwamba kulikuwa na sehemu tatu za uzungumzaji (speech) jina, kitendo, kihusishi.

Pia, aliweka kanuni za sarufi na sintaksi (upangaji na uhusishaji vipasho na maneno) ya lugha ya kiarabu na vile vile maelezo ya utamkaji na msamiati. Na kwa kupanga utamkaji sahihi kwa maandishi, aliilinda Qur’ani kutokana na tafsiri potovu baadae.

Kukiri Kwa Ibn Abi’l-Hadid Ule Ubora Wa Elimu Ya Ali.

Katika utangulizi na Sharh-e-Nahju’l-Balagha cha Ibn Abi’l-Hadid Mut’azali, utakuta jinsi mwanazuoni huyu alivyozikubali na kuzisifu sifa za Ali katika nyanja zote za elimu.

Anasema: “Nitasema nini juu ya mtu huyu ambaye kwake sifa zote zimehusishwa, ambaye ni mfano bora kwa kila taifa kufuata, na ambaye kwake, wote wanataka kujifananisha naye? Yeye kwa hakika ndiye chimbuko la sifa zote. Baada yake, yeyote aliyepata umaarufu, alinufaika kutoka kwake, kwani alifuata nyayo zake.”

Ibn Abi’l-Hadid anasema kwamba ile elimu ya wale mafaqih wakuu wanne, Abu Hanifa, Imam Malik, Imam Shafi’i, na Imam Hanbal imetokana na elimu ya Ali. Anasema “Wale masahaba walioelimika vyema katika fiqhi, waliijifunza hiyo kutoka kwa Ali.”

Nisingependa niwachukulie muda wenu mwingi kwa kunukuu zaidi kutoka kwa mwanachuoni huyu maarufu. Lakini ninawasihi mkasome ule utangulizi wake kwenye Sharh-e-Nahjul-Balagha yake. Mtaweza kugundua jinsi mwanahistoria na mwanachuoni huyu mashuhuri alivyozikubali sifa za Ali. Yeye anasema, “Suala la Ali ni la ajabu. Maishani mwake mwote hajawahi kutamka maneno haya: ‘Mimi sijui.’ Alikuwa na elimu juu ya kila jambo.’”

Mwishoni, mtunzi huyu anasema: “Ukweli huu unaweza kuhesabiwa kama moja ya miu- jiza ya Mtukufu Imam huyu. Elimu kama hii iko nje na uwezo na kuelewa kwa mwanadamu.”

Kuzaliwa Kwa Imam Husain Na Pongezi Za Malaika.

Watu walikuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumpongeza kwa kuzaliwa kwa Imam Husain. Mmoja wa watu hao akasema: “Ewe Mtukufu Mtume! Tumeona kitu cha ajabu kwa Ali.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akauliza, “Mmeona nini?” Yule mtu akasema: “Tulipokuja kutoa pongezi, tulizuiwa na kuambiwa kwamba Malaika 120,000 wamekuja toka mbinguni na walikuwa pamoja nawe. Tulishangazwa kuona ni vipi Ali angeweza kujua hili na vipi ameweza kuwahesabu hao.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akatabasamu na akamuuliza Ali ni vipi amejua kwamba Malaika wengi kiasi hicho wamekuja kwake. Imam Mtukufu akasema: “Baba yangu na mama yangu watoe muhanga maisha yao kwa ajili yako!

Kila mmoja wa Malaika aliyekuja kwako na akakusalimu wewe aliongea katika lugha tofauti. Katika kuhesabu, niliona kwamba wamezungumza katika lugha 120,000 hivyo nikajua kwamba Malaika 120,000 walikuja kwako.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Ewe Abu’l-Hasan! Allah akuzidishie elimu yako na staha zako.” Kisha, akiwageukia wale watu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema:

“Mimi ni jiji la elimu, na Ali ndio lango lake. Hakuna tukio kubwa mno na dalili kubwa mno kuliko alivyo yeye. Yeye ni kiongozi wa watu, mbora wa watu, dhamana ya Allah na ghala ya elimu yake. Yeye ni ‘Ahlu-Dhikr’ (wale wanaojua) miongoni mwa wale walioashiriwa kwa maneno ya Allah: ‘Kwa hiyo waulizeni wale wanaojua kama humjui.’ Mimi ni hazina ya elimu na Ali ndio funguo yake. Kwa hiyo yeyote anayetaka kuipata hazina hii aje kwenye ufunguo.”

Kama mtaweza kuonyesha sahaba mmoja au ndugu wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) anayeweza kushindana na hadhi ya Ali, kwa hakika nitasalimu amri mbele yake. Lakini kama hamtaweza basi itakuwa ni wajibu wenu wa kidini kujiambatanisha wenyewe kwenye haki bila kujali dunia itafikiri nini. Kisha alinyanyua mikono yake kuelekea mbin- guni na akaomba kwa Allah:

“Ewe Allah! Kuwa shahidi yangu kwamba kwa uwazi kabisa nimeielekeza njia ya kwenye haki na nimetekeleza wajibu wanug wa kidinin.

Kukubali Ushi’ah Kwa Nawab Sahib.

Nawab: Bwana Mtukufu, kwa mikesha kadhaa iliyopita tumesikia majadiliano mengi katika majlis hizi. Baadhi yetu tulikuwa tukichambua zile hoja za majadiliano miongoni mwetu kila siku. Ninamshukuru Allah Mwenyezi, kwamba ametuonyesha njia. Zile taarifa potofu kabisa za wapinzani zilitupoteza sisi. Sasa ni wazi kwamba Shi’ah Ithna Ashari wameongoka sawa sawa.

Wote wale ambao tulikuwa tukihudhuria majilis hizi na watu wengi wa mji huu ambao wamezisoma makala za mijadala hii kwenye magazeti tumeonyeshwa ukweli kuhusu Uislam. Bila shaka wote hawawezi kutamka hadharani imani zao kwa sababu ya mahusiano yao binafsi ya shughuli zao na wapinzani, lakini wametueleza sisi kwa siri kwamba wameukubali Ushi’ah.

Lakini baadhi yetu hatuna woga na yeyote na tuko tayari kutangaza kwamba katika mikesha hii tulitaka kudhihirisha mabadiliko yetu ya utii. Hakukuwa na fursa ya kufanya hivyo. Tumezisikia hoja zako zenye mvuto na sasa imani zetu ni imara kabisa.

Tunaomba uturuhusu sasa kulivuta pazia pembeni. Acha majina yetu yaandikwe kama wafuasi wa Bwana wetu, Amiru’l-Mu’minin na hao Maimam kumi na mbili. Tafadhali tangaza kwa watu wa madhehebu ya Shi’ah kwamba sisi tu wamoja pamoja nao.

Uwe shahidi Siku ya Kiyama mbele ya mahakama tukufu ya Haki na mbele ya babu yako aliyetukuka kwamba tunayo imani kamili juu ya Maimam kumi na wawili hawa kama warithi na washika makamu (waandamizi) wa Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.).

Muombezi: Nianayo furaha kwamba baadhi yenu mmeitambua haki. Kwa mujibu wa hadithi iliyoandikwa na Imam Ahmad Bin Hanbal kaitka Musnad yake, Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha na Muhammad Bin Talha Shafi’i katika Matulibu’s-Su’ul, na Ibn Maghazili katika Faza’il, na Khawarzmi katika Manaqib, na Sulayman Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, na wengine wengi, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ametuongoza kwenye njia hii. Alisema: “Njia ya Ali ndio njia ya kwenye ukweli.” Ninatumaini kwam- ba ndugu zangu wengine katika Uislam pia wataacha ushabiki wao.

Nawab: Tunao wingi wa shukrani kwa ufasiri wako wa mambo kwa upole na kisomi. Kuna nukta moja bado ambayo inatusumbua. Inahusu Uimam wa Maimam hawa kumi na mbili na majina yao. Katika mikesha kumi iliyopita, Amiru’l-Mu’min Ali alikuwa ndio kitovu cha mjadala wetu. Kwanza tuambie ile aya ya Qur’ani Tukufu inayothibitisha Uimam wa Maimam hawa kumi na mbili. Pili, je majina ya Maimam hawa kumi na mbili yameandikwa kwenye vitabu vyetu?

Muombezi: Ni swali muafaka na nitafurahi kulijibu lakini sasa ni karibu ya alfajir, na jibu langu haliwezi kuwa fupi sana. Kesho ni siku ya kuzaliwa (wilada) kwa mjukuu wa Mtukufu Mtume, Imam Husain na familia ya Qizilbash imeandaa tafrija katika ukumbi wa Risaldar Imambara pengine huenda nitalijibu swali lako wakati huo.

Nawab: Ninakubaliana kabisa na wewe.

Jumapili, Sha’ban 4, 1345 A.H Wilada Ya Imam Husein.

Tafrija kubwa kabisa ilifanyika kuadhimisha wilada ya Imam Husain. Mwandishi huyu, Seyyed Muhammad Sultanu’l-Wa’idhin Shirazi, aliihutubia hadhara hiyo. Ilikuwa ndio khotuba yake ya mwisho, na kama alivyoahidi usiku uliopita, alijibu lile swali kuhusu Uimam, idadi na majina ya Maimam katika Qur’ran tukufu na hadithi. Aliianza hotuba yake kwa aya ifuatayo:

“Enyi mliamini! Mtiini Allah, na mtiini Mtume na wale wenye mamlaka miongoni mwenu. Kisha mtakapohitilafiana katika jambo lolote, lirud- isheni kwa Allah na Mtume, kama mnamuamini Allah na Siku ya Mwisho. Hii ni bora sana na ni kheri nzuri mwishoni. (4:59)

Uhuru Halisi

Fikra ya uhuru, kwamba watu wawe huru, limekuwa kwa muda mrefu ni wazo la kawaida. Fikra ya juu juu kuhusu uhuru ni kwamba ina maana ya mtu kufanya kama anavyotaka, fikra ambayo imeishia kwenye kupuuza sheira tukufu. Lakini kwa kweli uhuru halisi ni unyenyekevu, utii kwa Allah, Muumba wa vitu vyote.

Qur’ani Tukufu mara nyingi inawamrisha waumini kumtii Allah na wale wanaofaa kufuatwa kutoka miongoni mwetu wenyewe. Ile aya tukufu ambayo nimeisoma kama dhamira ya mazungumzo yangu ni moja ya aya kama hizo ambayo inaashiria ni nani tunapaswa kumtii.

Inatuamrisha kumtii Allah, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na wale waliopewa mamla- ka. Hakuna tofauti ya maoni miongini mwa Waislam kuhusu utii unaomstahili Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Hata hivyo kuna tofauti ya maoni juu ya maana ya maneno. “Wale waliopewa Mamlaka miongoni mwenu.”

Imani Ya Sunni Kuhusu Maana Ya “Wale Waliopewa Mamlaka”

Ndugu zetu Sunni, wanaamini kwamba katika aya hiyo hapo juu, yale maneno “wale waliopewa mamlaka (ulu’l-amr) yanawahusu viongozi wa nchi. Kwa hiyo, wao wanachukulia utii kwa wafalme na magavana ni wajibu hata kama viongizi hawa wangekuwa waovu.

Kwa hakika imani hii ni ya makosa. Uhaba wa muda hauniruhusu kutoa mazungumzo marefu kuunga mkono maoni yangu, hivyo nitawasumbueni tu na maelezo mafupi.

Njia Tatu Za Uteuzi Wa ‘Ul’l-Amr’ (Wale Waliopewa Mamlaka)

Kwa hakika watawala wanapata mamlaka yao katika mojawapo ya njia hizi:

1. Wanachaguliwa kwa Ijma (makubaliano ya wengi) 2. Wanapata Mamlaka kwa nguvu. 3. Wanawekwa ki-Mungu - (kuteuliwa na Allah)

Ikiwa kiongozi anapata mamlaka kwa makubaliano ya Umma, sio wajibu kumtii yeye kama mtu anavyomtii Allah au Mtume. Haiwezekani kwa Waislam wote kumteua kiongozi mwadilifu kwa sababu hata wawe waerevu kiasi gani au waangalifu kiasi watakavyokuwa, wataweza tu kumuamulia mtu kutokana na muonekana wake wa nje. Hawawezi kuusoma moyo wake au kujua kiwango cha imani yake. Viongozi Wa Bani-Israel Walioteuliwa Na Musa Walionekana Hawafai

Ni dhahiri kwamba Waislam hawawezi kudai kuwa na uelewa bora zaidi ya Nabii Musa. Yeye alichagua watu sabini kutoka kwenye maelfu kadha kwa uaminifu wao wakuonekana dhahiri na akawachukua kwenda pamoja naye mpaka mlima Sinai. Lakini wote katika kuchunguzwa, wakathibitika kwamba ni bure tu kwa sababu imani zao hazikuwa thabiti.

Ukweli huu umetajwa katika Qur’ani Tukufu, aya 154 ya sura ya 7. Ikiwa wale walioch- aguliwa na Musa walithibitika kuwa sio waumini mioyoni, ni dhahiri kwamba mtu wa kawaida atakuwa na uwezo wa chini zaidi wa kuchagua watawala wao wenye uwezo. Inawezekana kabisa kwamba wale waliochaguliwa kwa ucha-mungu wao wa dhahiri, haltimaye wanaweza kutokea kuwa sio waumini. Hakika utii kwa watawala kama hao utad- hoofisha dini.

Maneno ‘Uli’l-Amr’ Hayaashirii Kwa Watawala

Kwa hakika Allah asingewataka waja wake kumtii mtenda dhambi kama ambavyo wangemtii Yeye au Mtume Wake. Zaidi ya hayo, kama uteuzi wa ‘Ul’l-Amr’ ungefanywa kupitia makubaliano ya kweli, upiga kura ungebidi ufanyike kwa kila uteuzi mpya.

Raia wote wa mataifa yote ya Kiislam wangepaswa kukubaliana juu ya mteuliwa katika kila uchaguzi. Katika miaka 1300 ya Uislam tunaona kwamba, baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), hakuna makubaliano kama hayo yaliyowahi kutokea, sasa hivi ni vigumu kupata makubaliano kama hayo kwa sababu ulimwengu wa kiislam umegawanyika katika idadi ya nchi, kila nchi ikiwa na mtawala wake.

Zaidi ya hayo, kama kila nchi itachagua ‘Uli’l- Amri wake, pangekuwa na idadi kubwa ya ‘Uli’-l- amr’ wake, pangekuwa na idadi kubwa ya ‘Ul-l amr’ kila mmoja akitiiwa ndani ya nchi yake, na watu wa nchi moja wasingeweza kumtii ‘Uli’l-amr’ wa nchi nyingine.

Bila shaka basi kuna suala la kiapo cha utii wakati kunapotokea tofauti - kama zilivyotokea mara kwa mara katika miaka 1300 iliyopita - baina ya ‘Mamlaka’ mbili. Halafu tunao Waislam wanaowaua Waislam wengine kwa jina la Uislam.

Lakini Uislam wa kweli hauhitaji tabia ya kichekesho kama hiyo ambayo itapelekea kwenye ugomvi wa wenyewe kwa wenyewe miongoni mwa Waislam. Kwa hiyo, ina maana kwamba huyo ‘Uli’l-amr’ ambaye tunayomriwa kumtii amepata mamlaka yake kwa makubaliano( Ijma). Mjadala huu uliotokea kwenye magezeti. Mtawala Anayetwaa Madaraka Kwa Nguvu Hawezi Kuitwa ‘Uli’l- Amr.’

Ni sawa na kichekesho kushauri kwamba utii kwa dhalimu ni wajibu. Kama ingekuwa hivyo, kwa nini wanazuoni wa Sunni wanawashutumu watawala waonevu na makhalifa, kama Mu’awiya, Yazid, muovu Ziyad Ibn Abib, Ubaidullah, Hajjaj, Abu Salma na Muslim. Ikiwa yeyote atadai kwamba utii kwa watawala wakarofi ni wajib (na baadhi ya Ulamaa kwa kweli wamesema hivyo) itakuwa ni kinyume kabisa na amri za Qur’ani. Allah mara kwa mara amewalaani watenda madhambi katika Qur’ani Tukufu na amewakataza Waislam kuwatii.

Hivyo inawezekanaje katika aya hii Yeye atuamuru kuwatii madhalim? Ni dhahiri kabisa, sisi hatuwezi kuhusisha amri mbili zinazopingana kwa Allah Muweza. Hivyo, Imam Fakhru’d-din Razi kwa uwazi, anasema kuhusu aya hii tukufu kwamba hawa ‘Uli’l-amr’ lazima wawe na uadilifu kamili. Vinginevyo Allah asingeweza kuunganisha wajibu wetu wa kuwatii wao pamoja na wajibu wa kumtii Allah Mwenyewe na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

‘Uli’l-Amr’ Lazima Aagizwe Na Kuteuliwa Na Allah

Kwa mujibu wa Shi’ah, hawa ‘Uli’l-amr’ lazima wawe huru kutokana na dhambi na wasiokosea. Na kwa vile hakuna yeyote isipokuwa Allah, anayeweza kujua ukweli wa kina wa moyo, hawa ‘Uli’l-amr’ lazima wateuliwe na Allah. Hivyo Allah ambaye anawaagiza Mitume pia ndie anawaagiza ‘Uli’l-amr’ aliye ‘Uli’l- amr’ ni dhahiri kwamba lazima awe na sifa zile zile alizokuwa nazo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Katika aya hii tukufu, neno atwi’u (Mtii) limetumika mara mbili.

Anasema “Mtii Allah na mtii Mtume.” Anapozungumzia juu ya ‘Uli’l-amr’ Yeye hatumii hili neno atiw’u tena lakini anatumia kiunganisha ‘na’ yaani, pamoja na ‘Uli’l-amr.’ Kuunganisha haya maneno katika njia hii ina maana kwamba ‘Uli’l-amr’ wana sifa sawa na alizonazo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) isipokuwa zile ambazo ni Makhsusi, za kipekee tu kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kwa mfano ‘Wahyi’ (ufunuo), Utume, na kadhalika. Kwa ufupi sifa za Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni budi awe nazo ‘Uli’l-amr’ isipokuwa bila shaka, kwa kile cheo cha Utume.

Kwa hali hiyo Shi’ah wanaamini kwamba haya maneno ‘Uli’l-amr’ yanawalenga hawa Maimam kumi na mbili, yaani Amirul-Mu’munin na wengine kumi na mmoja wa kizazi chake, Ahlul-Bayt wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Aya hii ni moja uthibitisho wa Uimam wa Maimam hawa kumi na mbili. Mbali na hii, kuna aya nyingine nyingi zenye kuunga mkono maoni yetu juu ya nukta hii.

(1) Kwa mfano, Qur’ani Tukufu inasema:

واذِ اﺑﺘَﻠَ اﺑﺮاﻫﻴﻢ رﺑﻪ ﺑِﻠﻤﺎتٍ ﻓَﺎﺗَﻤﻬﻦ ۖ ﻗَﺎل اﻧّ ﺟﺎﻋﻠُﻚَ ﻟﻠﻨﱠﺎسِ اﻣﺎﻣﺎ ۖ ﻗَﺎل وﻣﻦ ذُرِﻳﺘ ۖ ﻗَﺎل  ﻳﻨَﺎل ﻋﻬﺪِي {اﻟﻈﱠﺎﻟﻤﻴﻦ {124 “Akasema: Hakika nitakufanya wewe kuwa Imam wa watu.” (Ibrahim) akasema: Na katika kizazi changu?” Akasema (ndiyo, lakini) Ahadi yangu haiwafikii madhalim.” (2:124)

اﻟﻨﱠﺒِ اوﻟَ ﺑِﺎﻟْﻤﻮﻣﻨﻴﻦ ﻣﻦ اﻧْﻔُﺴﻬِﻢ ۖ وازْواﺟﻪ اﻣﻬﺎﺗُﻬﻢ ۗ واوﻟُﻮ ارﺣﺎم ﺑﻌﻀﻬﻢ اوﻟَ ﺑِﺒﻌﺾٍ ﻓ ﻛﺘَﺎبِ اﻟﻪ ﻣﻦ {اﻟْﻤﻮﻣﻨﻴﻦ واﻟْﻤﻬﺎﺟِﺮِﻳﻦ{6

“Nabii anayo haki zaidi juu ya waumini kuliko nafsi zao, na wake zake ni mama zao; na wenye nasaba wana haki zaidi wao kwa wao katika Kitabu cha Allah kuliko wengine wauminio au Muhajirina “ (33:6)

{ﻳﺎ اﻳﻬﺎ اﻟﱠﺬِﻳﻦ آﻣﻨُﻮا اﺗﱠﻘُﻮا اﻟﻪ وﻛﻮﻧُﻮا ﻣﻊ اﻟﺼﺎدِﻗﻴﻦ {119

“Enyi mlioamini! Mcheni Mwenyezi Mungu na kuweni pamoja na wakweli.” (9:119)

{اﻧﱠﻤﺎ اﻧْﺖ ﻣﻨْﺬِر ۖ وﻟﻞ ﻗَﻮم ﻫﺎدٍ {7 ۗ

“.....Hakika wewe ni muonyaji tu, na kila Umma una Kiongozi wake.”(13:7)

{وانﱠ ﻫٰﺬَا ﺻﺮاﻃ ﻣﺴﺘَﻘﻴﻤﺎ ﻓَﺎﺗﱠﺒِﻌﻮه ۖ و ﺗَﺘﱠﺒِﻌﻮا اﻟﺴﺒﻞ ﻓَﺘَﻔَﺮق ﺑِﻢ ﻋﻦ ﺳﺒِﻴﻠﻪ ۚ{153

“Na kwa hakika hii ndio njia yangu iliyonyooka, basi ifuateni, wala msifuate njia mbali mbali zikakutengeni mbali na njia yake.” (6:153)

{وﻣﻤﻦ ﺧَﻠَﻘْﻨَﺎ اﻣﺔٌ ﻳﻬﺪُونَ ﺑِﺎﻟْﺤﻖ وﺑِﻪ ﻳﻌﺪِﻟُﻮنَ {181

“Na katika wale tuliowaumba, kuna watu wanaongoza kwa haki na wanafanya uadilifu kwa haki hiyo.” (7:181)

{واﻋﺘَﺼﻤﻮا ﺑِﺤﺒﻞ اﻟﻪ ﺟﻤﻴﻌﺎ و ﺗَﻔَﺮﻗُﻮا ۚ{103

“Na shikamaneni katika kamba ya Mwenyezi Mungu wote kwa pamoja na wala msifarikiane” (3:103)

{ﻓَﺎﺳﺎﻟُﻮا اﻫﻞ اﻟﺬِّﻛﺮِ انْ ﻛﻨْﺘُﻢ  ﺗَﻌﻠَﻤﻮنَ {43 “Hivyo basi waulizeni wenye kujua (Ahlu’l-Dhikr) ikiwa ninyi hamjui .” (16:43)

{اﻧﱠﻤﺎ ﻳﺮِﻳﺪُ اﻟﻪ ﻟﻴﺬْﻫﺐ ﻋﻨْﻢ اﻟﺮِﺟﺲ اﻫﻞ اﻟْﺒﻴﺖِ وﻳﻄَﻬِﺮﻛﻢ ﺗَﻄْﻬِﻴﺮا {33

“Hakika Mwenyezi Mungu anataka kuwaondoleeni uchafu, enyi watu wa nyumba (ya mtume) na kukutakaseni kwa utakaso ulio kamili.” (33:33)

{انﱠ اﻟﻪ اﺻﻄَﻔَ آدم وﻧُﻮﺣﺎ وآل اﺑﺮاﻫﻴﻢ وآل ﻋﻤﺮانَ ﻋﻠَ اﻟْﻌﺎﻟَﻤﻴﻦ {33

{ذُرِﻳﺔً ﺑﻌﻀﻬﺎ ﻣﻦ ﺑﻌﺾٍ ۗ واﻟﻪ ﺳﻤﻴﻊ ﻋﻠﻴﻢ {34

“Hakika Mwenyezi Mungu amemchagua Adam na Nuh na kizazi cha Ibrahim na kizazi cha Imran juu ya walimwengu. Kizazi cha wao kwa wao, mmoja kutokana na mwingine.(3:33-34)

{ﺛُﻢ اورﺛْﻨَﺎ اﻟْﺘَﺎب اﻟﱠﺬِﻳﻦ اﺻﻄَﻔَﻴﻨَﺎ ﻣﻦ ﻋﺒﺎدِﻧَﺎ ۖ{32

“Kisha tukawapa Kitabu (kama urithi) wale ambao tumewachagua kutoka miongo- ni mwa waja wetu.....” (35:32)

“Mwenyezi Mungu ndie nuru ya mbingu na aridhi, mfano wa nuru yake ni kama shubaka (tundu) ndani yake mna taa, taa hiyo imo ndani ya tungi, na tungi hiyo ni kama nyota inayong’ara sana, inayowashwa katika mti uliobarikiwa wa mzaituni usio na mashariki wale magharibi, mafuta yake yanakaribia kung’aa, ingawa moto hauyagusa.....” (24:35)

Kuna aya nyingine nyingi ambazo zingeweza kunukuliwa. Wengi wa ulamaa wenu mashuhuri wamesimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Moja ya nne ya Qur’ani Tukufu ni yenye kuitukuza Ahlul-Bayt.”

Ibn Abbas anasemekana kwamba alisema. “Zaidi ya aya 300 zimeshushwa katika kumtukuza Ali.”

Sasa, ninakuja kwenye hoja yangu ya asili kwamba hawa ‘Uli’l-amr’ ni lazima wawe wenye wa kutotenda makosa kwa sababu utii kwao umeugnanishwa na utii kwa Allah na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Imam Fakhru’d-din Razi katika Tafsiir yake anakiri kwamba kama hatuwachukulii ‘Uli’l-amr kama wasiotenda makosa (ma’sum) itakuwa, katika utekelezaji, kusimamisha vitu viwili vinavyopingana kuwa ni vya kweli. Wanazuoni wenu wenyewe wamethibitisha kwamba sifa hizI walikuwa nazo Maimam hawa kumi na mbili pekee. Hii aya tukufu ya Utakaso (33:33) pia inathibisha ukweli huu. Kutotenda Dhambi Na Makosa (Uma’sum) Kwa Maimam Watukufu Kumesimuliwa Kwa Jumla Sana.

Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda sura ya 77, uk. 445, na Hamwaini katika Fara’idu’s-Simtain wanasimulai kwamba Ibn Abbas amesema: “Nilimsikia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: ‘Mimi na Ali, Hasan, Husain na watu tisa katika kizazi cha Husain tuko safi kabisa na tusiofanya makosa ( ma’sum).’”

Salman Farsi anasema kwama Mtukufu Mtume, akiweka mkono wake kwenye bega la Husein, alisema: “Huyu ni Imam na mtoto wa Imam, na katika kizazi chake watakuwapo Maimam tisa ambao watakuwa wote ni hujjat waadilifu wa Allah na wema sana.”

Zaidi Ibn Thabit anasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema; “Hakika kutokana na kizazi cha Husain watazaliwa Maimam watakaokuwa Hujjat wema sana, Mahakimu wasiokosea kabisa.”

Imran Ibn Hasin anasimulia kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alimuambia Ali: “Wewe ni mrithi wa elimu yangu. Wewe ni Imam na khalifa baada yangu. Wewe utawaeleza watu kile wasichokijua. Wewe ni baba wa wajakuu zangu na mume wa binti yangu, katika kizazi chako watakuwepo Maimam wasiokosea (ma’sum).

Elimu Ya Ahlul-Bayt.

Abu Ishaq Hamwaini katika Fara’idu’s-Simtain, Hafidh Abu Nu’aim Ispahani katika Hiliyatu’l-Auliya, na Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahjul-Balagha wanasimulia kutoka kwa Ibn Abbas kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Kizazi changu kiliumbwa kutokana na mbegu ile ile ambyo kutokana nayo niliumbwa mimi. Allah Mwenye uwezo amejaalia juu yao elimu na hekima. Laana naiwe juu yake yule atakayewakataa.”

Ibn Abi’l-Hadid katika Sharh-e-Nahju’l-Balagha na mtunzi wa Siratu’s-Sahaba, wanasimulia kutoka kwa Hudhaifa Bin Asaid kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ninawachieni nyuma yangu vizito viwili: Kitabu cha Allah na ‘Ahlul-Bait’ wangu. Kama mtashikamana navyo viwili hivi mtaongoka”

Tabrani anasimulia nyongeza. “Msikatae mamlaka yao, vinginevyo mtaangamia. Msionyesha utovu wa nidhamu mbele yao ama kuwapuuza, la sivyo mtaangamizwa. Msijaribu kuwafundisha wao kwa sababu hakika wanajua vizuri zaidi kuliko ninyi.”

Katika simulizi zingine Hudhaifa Bin Asaid anamukuu Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akisema: “Baada yangu kutakuwa na Maimam watokanao na kizazi changu. Idadi yao itakuwa sawa na idadi ya Wajumbe wa Bani Israil, yaani, kumi na mbili, ambao kati yao tisa watakuwa ni kizazi cha Husain.

Allah ameijaalia juu yao wote elimu yangu na hekima. Hivyo msiwafundishe kwa sababu kwa kweli wao wanajua vizuri zaidi kuliko ninyi. Wafuateni wao kwani kwa uhakika wako pamoja na haki, na haki iko pamoja nao.”

Kwa Nini Majina Ya Hawa Maimam Hayatokezi Ndani Ya Qur’ani Tukufu

Kwanza, Kitabu hiki kitukufu ni cha kifupi sana. Ndani yake kinazo kanuni nyingi za jumla lakini maelezo ni machache, ambayo yameachiwa mfasiri mkuu, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kuyaelezea. Allah anasema: “Na chochote Mtume anachokupeni kipokeeni, na chochote anachokukatazeni, kiacheni. (59:7)

Kwa sababu haya majina na idadi ya Maimam hawa kumi na mbili hayakutajwa ndani ya Qur’ani Tukufu, baadhi ya watu hawayakubali. Lakini kwa msingi huohuo wangewakataa makhalifa wao wenyewe kwani hakuna aya ya Qur’ani Tukufu inayotoa utajo wowote wa makhalifa wao isipokuwa Ali Bin Abi Talib, wala Makhalifa wa Bani Umayya au wa Bani Abbas, au wa mamlaka waliyopewa umma kumchagua khalifa kwa makubaliano (ijma). Pili, ikiwa ni muhimu kukataa kitu chochote ambacho hakikuelezwa wazi ndani ya Qur’ani Tukufu, basi mngelikataa nyingi ya taratibu na namna za ibada zetu kwa vile hakuna utajo wa maelekezo yake ndani ya Qur’ani Tukufu.

Hakuna Utajo Wa Raka’a Za Swala Ndani Ya Qur’ani Tukufu.

Ibada ya sala pengine ndio tendo kuu la kiibada katika maisha ya Muislam. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisisitiza kuitenda kwake. Alisema; “Sala ndio nguzo na mlinzi wa Dini. Kama sala itakubaliwa, basi matendo mengine yote ya kidini yatakubaliwa. Kama itakataliwa, matendo mengine yote ya kidini pia yatakataliwa.”

Bila shaka, hakuna utajo ndani ya Qur’ani Tukufu wa idadi ya rak’aa za kutekelezwa kwa kila sala au maelezo maalum yoyote kuhusu namna gani sala zitakavyoendeshwa. Je, hii ina maana kwamba tuzitelekeze Sala? Qur’ani Tukufu inasema kifupi tu: “Simamisheni sala” Hakuna maelezo yoyote yanayotofautisha matendo ya wajib na ya sunna. Hayo yalielezwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

Kwa njia hiyo hiyo amri zingine zimeandikwa katika Qur’ani Tukufu kwa kanuni tu. Maelezo yake, shuruti na maelekezo yanayostahili yalielezwa na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Vivyo hivyo, kuhusu Uimam na Ukhalifa, Qur’ani Tukufu inasema tu: “Mtiini Allah na mtiini Mtume na wale wenye Mamlaka miongoni mwenu.” Na tunalazimishwa kufuata amri ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kuhusu hili kwa namna ileile tunavyofuata maelekezo yake kuhusu uchambuzi wa ibada ya sala.

Wafasiri wa Kiislam, imma Sunni au Shi’ah, hawawezi kutoa maelezo (sharh) yao wenyewe juu ya Qur’ani Tukufu. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Ikiwa mtu yoyote atatoa maelezo yake mwenyewe juu ya Qur’ani Tukufu, mahali pake ni Motoni.” Kwa sababu hiyo, kila Muislam mwenye busara humgeukia mtafsiri halisi wa Qur’ani Tukufu, yaani, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.). Kwa miaka mingi nimezisoma tafsiri za Qur’ani za wote Sunni na Shi’ah na Hadithi lakini sijakuta hata hadithi moja ambayo ndani yake Mtukufu Mtume amesema kwamba ‘Ul’l- amr’ inawalenga viongozi wa kisiasa.

Kwa upande mwingine, vitabu vyao wote Sunni na Shi’ah vimejaa idadi kubwa ya simulizi kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliulizwa kuelekeza maana ya ‘ul’l’-amr’ na alijibu kwamba ‘ul’l-amr’ ilimhusu Ali na wengine kumi na mmoja wa kizazi chake. Nitatoa chache tu ya hizi hadithi nyingi ambazo zimesimuliwa kupitia vyanzo vinavyokubaliwa na Sunni.

‘Uli’l-Amr Inaashiria Kwa Ali Na Maimam Wa Ahlul- Bait.

1. Abu Ishaq, Sheikhu’l-Islam Hamwaini Ibrahim Bin Muhammad anaandika katika Fara’idu’s-Simtain yake: “Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ametuambia kwamba ‘Uli’l-amr’ inamhusu Ali Bin Abi Talib na Ahlul Bait wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.).

2. ‘Isa Bin Yusuf Hamadani anasimulia kutoka kwa Abu’l-Hasan na Salim Bin Qais, ambao wanasimulia kutoka kwa Amiru’l-Mu’minin Ali kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Wenza wangu ni wale ambao utii kwao umeunganishwa na Muweza Allah pamoja na utii Kwake Yeye mwenyewe. Ni wale ambao kwao anawaashiria wakati anaposema: ‘Wale wenye Mamlaka kutoka mingoni mwenu.’ Ni lazima kwamba hampingi wanachokisema. Muwatii na kufuata amri zao” Amirul-Mu’minin anaendela kusema kwamba: “Nilipoyasikia haya, nilisema: “Ewe Mtume, nifahamishe niwajue hao ‘Uli’l-amr’ ni akina nani.” Mtume akasema: “Oh, Ali! Wewe ndie wa kwanza wao.”

3. Muhammad Bin Mu’min Shirazi, mmoja wa wanachuoni wa kidini maarufu sana wa Sunni, anaandika katika Risala-e-l’tiqadat yake kwamba wakati Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipomteua Amiru’l-Mu’minin kuwa mwakilishi wake hapo Madina aya ya “Uli’l-amr minkum” (Na wale wenye mamlaka kutoka miongoni mwenu) ilishushwa kumhusu Ali Bin Abi Talib.

4. Sheikh Sulayman Balkhi Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda, sura ya 38 anasimulia kutoka kwenye Manaqib kwamba imeandikwa katika Tafsir-e-Mujahid kwamba aya hii ilishushwa kumhusu Amiru- Mu’minin wakati Mtukufu Mtume alipomteua kama mwak- ilishi wake huko Madina. Imam Mtukufu alisema: “Oh! Mtukufu Mtume wa Allah (s.a.w.w.)! Umeniteua mimi kuwa Khalifa juu ya wanawake na watoto? Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema “Wewe huridhiki kwamba una uhusiano nami sawa na Harun alivyokuwa kwa Musa?”

5. Sheikhu’l-Islam Hamwaini anamsimulia Salim Bin Qais Hilal kwamba amesema yafu- atayo: “Wakati wa Ukhalifa wa Uthman, niliona baadhi ya Muhajir na Ansar wamekaa pamoja wakijisifu wenyewe. Ali alikuwa kimya miongoni mwao. Wale watu wakamuomba Ali azungumze. Yeye akasema: “Hamjui kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: ‘Mimi na Ahlul Bait wangu tulikuwa nuru moja. Iliyokuwepo kwenye umbaji wake miaka 14000 kabla ya kuumbwa Adam? Wakati alipomuumba Adam, Aliiweka nuru ile katika uti wa mgongo wakepale aliposhuka kuja dunaini. Kisha akaiweka kwa Nuhu ndani ya safina yake, kisha katika mgongo wa Abraham alipokuwa kwenye moto, vivyo hivyo katika migongo safi ya mababa na katika matumbo safi ya akina mama, ambao hakuna mmoja wao aliyezaliwa kinyume cha sheria” Wale waliokuwemo kwenye lile kundi ambao walikuwa wa mbele katika vita vya Badr na Hunain wakasema: “Ndio, tumeyasikia maneno haya.” Kisha Ali akasema: “Niambieni kwa kiapo kama mnajua kwamba katika Qur’ani Tukufu Allah ametoa kipaumbele kwa wale wa mwanzo kabisa, na kwamba katika Uislam hakuna anaelingana na mimi kwa sifa.” Wao wakasema: “Ndio, tunalithibitisha hili.”

Kisha Ali akasoma kutoka kwenye Qur’ani Tukufu: “Na waliotangulia ni wa mbele kabisa, hawa ndio wale waliovutwa karibu na Allah.” (56:10-11)

Akasema: “Wakati aya hii iliposhushwa, watu walimuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni nani walio wa mbele kabisa, na ni kuhusu nani aya hii imeshushwa. Sasa niambieni kwa kiapo kama mnajua kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliwaambia kwamba Allah Muweza Aliishusha aya hii kuhusu mitume na washika makamu (waandamizi) wao.

Mimi ni wa mbele kabisa miongoni mwa Mitume na Ali, wasii (mwandamizi) wangu ni wa mbele kabisa miongoni mwa washika makamu wote?”

Kisha Ali akasema: “Qur’ani Tukufu inatumbia, ‘Mtiini Allah na mtiini Mtume na wale waliopewa mamlaka kutoka miongoni mwenu’ (4:59) na hii aya: ‘Hakika, hakika kiongozi wenu (si mwingine) ila Allah na Mtume wake (Muhammad) na wale walioamini, wale wanaosimamisha swala na kutoa zaka, huku wakiwa wamerukuu (5:55) na hii aya: “Hawakuchukua yeyote kama mtegemewa mbali na Allah na Mtume wake na wale walioamini.” (9:16)

Allah baadaye alimuamuru Mtume wake Mtukufu kumtambulisha yule aliyodhamiriwa kwa haya maneno ‘Uli’l-amr’ wale waliopewa mamlaka kwa namna ile ile kama ibada ya Sala, Saumu na Hijja zilivyopambanuliwa. Kwa hiyo, pale Ghadir-e-Khum Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) aliniteua mimi kuwa juu ya watu na akatamka: “Enyi watu wakati Mwenyezi Mungu aliponipa utume nilihisi wasiwasi kwamba watu watanipinga mimi”

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaendelea “Enyi watu mnajua kwamba Allah Mtukuka zaidi ndie Mola wangu? Ninayo mamlaka zaidi juu ya nafsi za waumini zaidi ya wao waliyonayo juu yao wenyewe? Wote walipothibitisha kwamba hivyo ndivyo ilivyokuwa, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akatangaza: ‘Ambaye yeyote mimi ni bwana kwake, Ali ni bwana wake; Ewe Allah kuwa rafiki wa yale ambae ni rafiki wa Ali na kuwa adui wa yeye ambaye ni adui wa Ali’

Kisha Salman akasimama na kuuliza: “Ewe Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni upi mfano dhahiri wa ubwana wa Ali? Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akajibu: ‘Ubwana wa Ali ni kama ubwana wangu mimi mwenyewe. Ambaye yeyote mini ni bwana kwake Ali pia ni bwana wake.’” Kisha aya hii ikashushwa: “Leo hii nimewakamilishia dini yenu na nimeitimiza neema Yangu kwenu na nimeweachangulia Uislam kama dini.” (5:3)

Hapo ndipo Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Allahu-Akbar, Mungu ni Mkubwa, aliyeikamilisha hii dini, akatimiza neema Yake juu yangu, na ameridhishwa na Utume wangu na ameridhika na Ali kuwa mshika makamu (mwandamizi) baada yangu.

Hadithi hii inathibitisha zile hadithi ambazo nimezisimulia katika mikesha iliyopita kuonyesha kwamba bwana (Maula) pia ina maana umiliki zaidi ya ule wa mtu mwenyewe.

“Kisha watu wakasema “Ewe Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) tuambie majina ya washika makamu (waandamizi) wako.” Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Wao ni Ali, ambaye ni ndugu yangu, mrithi wangu na wasii wangu na bwana wa kila muumini baada yangu, kisha mwanawe, Hasan, kisha Husein, kisha watoto tisa wa Husain wanaofuatana, mmoja baada ya mwingine. Qur’ani Tukufu iko pamoja nao na wao wako pamoja na Qur’ani Tukufu, Hawatatengana nayo, nayo haitatengana nao mpaka wanikute mimi kwenye Haudhi ya Kauthar.’”

Baada ya kuandika habari hii nzima amesimulia hadithi nyingine tatu kutoka kwenye Manaqib zilizosimuliwa na Salim Bin Qais, Isa Bin Sirri na Ibn Mu’awiya zinazoonyesha kwamba haya maneno ‘Uli’l-amr’ yanawahusu Maimam kumi na wawili wa ‘Ahle Bait.’ Ninaamini kwamba hadithi hizo hapo juu zinatosha kufafanua maana halisi ya ‘ul’l-amr.’

Na kuhusu idadi na majina ya Maimam watukufu, nitasimulia hadithi zilizosimuliwa na wanazuoni maarufu wa Sunni, bila kurejea, kama ilivyokuwa desturi yangu, kwenye hadithi nyingi za wanazuoni wa Shi’ah.

Majina Ya Maimam Na Idadi Yao - (Kumi Na Mbili).

(1) Sheikh Sulayman Balkh Hanafi katika Yanabiu’l-Mawadda yake, sura ya 76 anasimulia kutoka Fara’idu’s-Simtain cha Hamwaini, anayesimulia kutoka kwa Mujahid, anayesimulia toka kwa ibn Abbas, kwamba Myahudi anayeitwa Na’thal alikuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na akamuuliza maswali kuhusu Tawhid (Upweke wa Allah) Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akayajibu maswali yake na Myahudi yule akaingia Uislam. Kisha akasema: “Ewe Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), kila Mtume alikuwa na Wasii (mshika makamu) wake. Mtume wetu Musa Bin Imra, aliusia kwa Yusha Bin Nun. Tafadhal hebu niambie ni nani wasii wako?”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Mwandamizi (wasii) wangu ni Ali Bin Abi Talib, baada yake ni Hasan, na Husain na baada yao kuna Maimam tisa, ambao ni mfululizo wa kizazi cha Husain.”

Na’thal akamuuliza Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) majina ya Maimam hao. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Baada ya Hussein, mwanawe Ali atakuwa Imam, baada yake mwanawe Muhammad, baada yake mwanae Ja’far, baada yake mwanae Musa, baada yake mwanae Ali, baada yake mwanae Muhammad, baada yake mwane Ali, baada yake mwanae Hasan, baada yake mwanae, Muhammad Mahdi atakuwa ndio Imam wa mwisho. Watakuwepo Maimam kumi na mbili.

Zaidi ya majina haya ya Maimam tisa, hadithi hii inaeleza zaidi kwamba kila mmoja wao atafuata kama Imam baada ya baba yake. Na’thal aliulizia maswali zaidi na Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akaelezea namna ya kifo cha kila Imam.

Kisha Na’thal akasema: “Nashuhudia kwamba hakuna mungu ila Allah na kwamba wewe ni Mtume wake Mtukufu. Nashuhudia kwamba Maimam, hawa kumi na mbili ndo washika makamu wako baada yako. Uliyoyasema ni sawa sawa hasa yale yaliyoandikwa kwenye vitabu vyetu na katika usia wa Musa.”

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akasema: “Pepo ni yake yule anayewapenda na kuwatii hawa, na Moto wa Jahanamu ni kwa ajili yake yule atakayewachukia na kupinga hawa.”

Kisha Na’thal akasoma tenzi zenye maana kwamba ‘Allah aliyetukuka ashushe rehma juu yako, Mtume uliyechaguliwa na fahari ya Bani Hashim. Allah ametuongoza sisi kupitia kwako na watu watukufu kumi na mbili uliowataja. Hakika Allah amewatakasa na kuwahifadhi kutokana na uchafu.

Yule anayewapenda wao amefuzu. Yule anayewachukia hawa yu mwenye hasara. Wa mwisho wa Maimam hawa atakata kiu ya wenye kiu. Yeye ndiye yule watu watakayemngoja. Ewe Mtume wa Allah, kizazi chako ni rehma kwangu na waumini wote. Wale wanaogeuka na kuwapa kisogo punde watatupwa kwenye Moto wa Jahannam.

(2) Yule mwanazuoni mkuu, Sheikh Sulayman Balkhi katika Yanabiu’l-Mawadda yake, sura ya 76, anasimulia toka kwenye Manaqib ya Khawarizmi, ambaye anasimulia kutoka Wathila Bin Asqa’ Bin Qarkhab, ambaye anasimulia toka kwa Jabri Bin Abdullah Ansar, na pia Abu’l-Fazl Shaibani na yeye kutoka kwa Muhammad Bin Abdullah Bin Ibrahim Shafi’i, anayemnukuu Jabir Ansari (mmojawapo wa masahaba wakuu wa Mtume) kwam- ba amesema; “ Jundal Bin Junadab Bin Jubair, ambaye ni Myahudi, alikuja kwa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) na kumuuliza kuhusu Tawhid.

Baada ya kusikia jibu lake, yule mtu akawa Muislam. Akasema kwamba katika usiku uliopita alimuona Musa katika ndoto akimuambia; ‘Ingia Uislam kwenye mikono ya wa mwisho katika Mitume, Muhammad, na ujiambatanishe wewe kwa washika makamu wake baada yake.’ Alimshukuru Allah kwa neema ya Uislam. Kisha ndipo akamuomba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amtajie majina ya Washika Makamu wake. Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alianza kwa kusema: “Washika Makamu wangu ni kumi na mbili kwa idadi.”

Yule mtu akasema alikwishaliona jambo hili ndani ya Taurat. Alimuomba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amtajie majina yao, na Mtume akasema: “Wa kwanza wao ndiye mkuu wa washika makamu na baba wa Maimam hao, naye ni Ali. Kisha wanafuata wanawe wawili Hasan na Husain. utawaona hawa watatu. Pale utakapofikia hatua ya mwisho ya uhai wako, Imam Zainu’l-Abidini atazaliwa, na kitu cha mwisho utakachokula cha dunia hii kitakuwa ni maziwa. Kwa hiyo sikamana nao hawa ili ujinga usije ukakupotosha.”

Kisha yale mtu akasema ameona katika Taurati na katika Maandiko mengineyo majina ya Ali, Hasan na Hussein kama Elias, Shabbar, na Shabbir. Akamuomba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amtajie majina ya hao Maimam wengine.

Kisha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) akawataja wale Maimam tisa waliobakia pamoja na Lakab zao na akaongeza: “Wa mwisho wao, Muhammad Mahdi, ataishi, lakini atatowe- ka. Atatokeza baadae na ataujaza ulimwengu na haki na usawa, kwani utakuwa umekumbwa na dhulma na ukandamizaji.

Hakika pepo ni kwa wale watakaoonyesha uvumilivu wakati wa ghaib (kutoweka) kwake. Pepo ni kwa wale ambao ni imara katika mapenzi juu yake.

Hawa ndio wale ambao Allah Muweza amewasifu ndani ya Qur’ani Tukufu na kwa ajili ya wale ambao Qur’ani Tukufu ni ‘muongozo kwa wale wanaojilinda ( kutokana na maovu). Wale ambao wanaamini katika yaliyo ghaib” Pia anasema “Hawa ni kundi la Allah: sasa hakika kundi la Allah ni la wenye kufuzu.”(58:22)

Idadi Ya Makhalifa Baada Ya Mtukufu Mtume Ni Kumi Na Mbili

Mir Seyyed Ali Shafi’i Hamadani katika Mawaddatu’l-Qurba yake, (Mawadda ya 13), anasimulia kwamba Umar Bin Qais alisema: “Tulikuwa tumekaa katika kundi ambamo Abdullah Bin Mas’ud pia alikuwemo. Mara akaja Mwarabu mmoja na kusema: “Yupi miongoni mwenu ndio Abdullah?” Abdullah akasema: “Ni mimi.” Akasema (yule Mwarabu): Abdullah! Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alikueleza kuhusu Makhalifa baada yake.?”

Abdullah Bin Ma’sud akasema: “Ndio, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: ‘Baada yangu watakuwepo Makhalifa kumi na mbili, wanalingana na idadi ya Maimam wa Bani Isra’ili.”

Hadithi hii pia imesimuliwa kutoka kwa Sha’bi ambaye ameisimulia kutoka kwa Masruq, aliyeisimulia kutoka kwa Abdullah Shiba.

Pia Jurair, Ash’ath, Abdullah Bin Mas’ud, Abdullah Bin Umar na Jubair Bin Samra wote wanamsimulia Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) kwamba alisema: “Watakuwepo Makhalifa kumi na mbili baada yangu. Idadi yao italingana na Makhalifa wa Bani Isra’ili.” Kwa mujibu wa simulizi ya Abdul’l-Malik, Mtukufu Mtume aliongeza: “Na wote watakuwa kutoka Bani Hashim.”

Wanazoni wengi wa Sunni, akiwemo Tirmidhi, Abu Dawud, Muslim, Sha’bi wamesimulia vivyo hivyo. Yahya Bin Hasan, mwanazuoni mkubwa wa fiqh, amesimulia katika kitabu chake Kitab-e-Umda kutoka kwenye vyanzo kumi na mbili tofauti, kwamba “Hakika, kuna Makhalifa kumi na mbili baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.), nao wote wanatokana na Maquraish.”

Bukhari amesimulia kutoka kwenye vyanzo vitatu, Muslim kutoka vyanzo tisa, Abu Dawud kutoka vyanzo vitatu, Tirmidhi toka chanzo kimoja, na Hamid toka kwenye vyanzo vitatu kwamba Mtukufu Mtume amesema: “Makhalifa na Maimam baada yangu ni kumi na mbili, na wote wanatokana na Maqurish.” Kwa mujibu wa baadhi ya simulizi zingine, Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema. “Wote hao watatokana na Bani Hashim.”

Katika uk. 446 Yahya Bin Hasan anasema: “Baadhi ya wanazuoni wamesema kwamba hadithi zenye kuunga mkono hoja ya kwamba idadi ya Makhalifa na Maimam baada ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ni kumi na mbili ni zenye kujulikana sana.

Kila mmoja anafahamu kwamba Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alipoainisha kwamba idadi ya Makhalifa wake itakuwa kumi na mbili, alimaanisha kuwa watatokana na ‘Ahlul-Bait’ wake.

Kusema kwamba alimaanisha Makhalifa waliokuwa sahaba zake itakuwa ni kinyume na ukweli (kwa vile wao walikuwa wanne tu).

Wala haiwezi kusemwa kwamba alimaanisha wale wafalme wa Bani Umayya, ambao wao walikuwepo kumi na watatu. Zaidi ya hayo, wao walikuwa wakandamizaji isipokuwa Umar Bain Abdu’l-Aziz (ingawa hata yeye aliupora ukhalifa na kumlazimisha Imam wa zama hizo kubalikia kizuizini ndani ya nyumba yake).

Kwa vile Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) alisema: “Wote wanatokana na Bani Hashim.” Bani Umayya sio wa kuhesabika.

Kwa hiyo ni dhahiri kwamba Makhalifa wa haki wa Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) walikuwa ni wale Maimam kumi na wawili waliokuwa ni kizazi cha Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) ambao waliwazidi wengine wote katika elimu na ucha-Mungu. Ukweli huu unathibitishwa na hadithi hii ya Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) iliyosimuliwa sana (mutawatir). “Ninaacha nyuma yangu vizito viwili, Kitabu Kitukufu cha Allah (Qur’ani Tukufu) na ‘Ahlul-Bayt’ wangu. Kama mtashikamana na viwili hivi, kamwe, kamwe, hamtapotea baada yangu.

Hakika viwili hivi havitatengana mpaka vinikute mimi kwenye Haudhi ya Kauthar. Kama mtashikamana na viwili hivi, hamtapotoshwa kamwe.”

Mtukufu Mtume (s.a.w.w.) amesema: “Tafuteni elimu hata ikiwa .” Tumetumia mikesha kumi mirefu kujadili mambo yahusuyo elimu adhimunjia ya Uislamu.

Tumeona tofauti nyingi baina ya madhehebu ya Sunni na ile ya Shi’ah, na tunatumaini kwamba ukweli wa kihistoria na hoja zenye mantiki vimefafanua asili ya tofauti hizo. Inshallah mijadala hii itawavuta watafutaji elimu wakweli kwamba: “Anaeongozwa na Mwenyezi Mungu hakuna yeyote wa kumpoteza.” Orodha Ya Vitabu Vilivyo Chapishwa Na Al-Itrah Foundation:

1. Qur’ani Al-Kariim - Tafsir Al-Kashif Juzuu ya kwanza mpaka kumi na Tisa 2. Uharamisho wa Riba 3. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya kwanza 4. Uharamisho wa uwongo Juzuu ya pili 5. Hekaya za Bahlul 6. Muhanga wa Imamu Husein (A.S.) 7. Mikingamo iliyomzunguka Imamu Ali (A.S.) 8. Hijab vazi Bora 9. Ukweli wa Shia Ithnaashari 10. Madhambi Makuu 11. Mbingu imenikirimu 12. Abdallah Ibn Saba 13. Khadijatul Kubra 14. Utumwa 15. Umakini katika Swala 16. Misingi ya Maarifa 17. Kanuni za Ndoa na maadili ya Familia 18. Bilal wa Afrika 19. Abudharr 20. Usahihi wa Historia ya Uislamu na Waislamu 21. Salman Farsi 22. Ammar Yasir 23. Qur’ani na Hadithi 24. Elimu ya Nafsi 25. Yajue Madhehebu ya Shia 26. Ukusanyaji na Uhifadhi wa Qur’ani Tukufu 27. Al-Wahda 28. Ponyo kutoka katika Qur’ani 29. Uislamu mfumo kamili wa maisha ya kijamii 30. Mashukio ya Akhera 31. Al Amali 32. Dua Indal Ahlul Bayt 33. Udhuu kwa mujibu wa Kitabu na Sunna 34. Haki za wanawake katika Uislamu 35. Mwenyeezi Mungu na sifa zake 36. Amateka 37. Nafasi za Ahlul Bayt (a.s) 38. Adhana. 39 Upendo katika Ukristo na Uislamu 40. Nyuma yaho naje kuyoboka 41. Amavu n’amavuko by’ubushiya 42. Kupaka juu ya khofu 43. Kukusanya swala mbili 44. Bismillah ni sehemu ya Qur’ani na husomwa kwa Jahara 45. Kuwaongoza vijana wa kizazi kipya 46. Kusujudu juu ya udongo 47. Maulidi 48. Tarawehe 49. Malumbano baina ya Sunni na Shia 50. Kupunguza swala safarini 51. Kufungua safarini 52. Kuzuru makaburi 53. Umaasumu wa Manabii 54. Qur’ani inatoa changamoto 55. Tujifunze misingi ya dini 56. Nahjul Balagha Sehemu ya Kwanza 57. Nahjul Balagha Sehemu ya Pili 58. Dua Kumayl 59. Uadilifu wa masahaba 60. Asalaatu Khayrunminaumi 61. Sauti ya uadilifu wa binadamu 62. Umaasumu wa Mitume Sehemu ya kwanza 63 Maswali na Mishkili Elfu Sehemu ya kwanza 64. Umaasumu wa Mitume Sehemu ya pili 65. Umaasumu wa Mitume Sehemu ya tatu 66. Maswali na Mishkili Elfu Sehemu ya pili 67. Maswali na Mishkili Elfu Sehemu ya Tatu 68. Sala ni nguzo ya dini 69. Malezi ya mtoto katika Uislamu 70. Shia asema haya, Sunni asema haya, wewe, wewe wasemaje? 71. Ubora wa Imam Ali Juu ya Masahaba 72 Hukumu ya Kujenga Juu ya Makaburi Ndani ya Sheria Back Cover

Mikesha ya Peshawar ni nakala ya mjadala kati ya wanavyuoni mbalimbali wa Kisunni na mwanachuoni mmoja wa Kishia mzaliwa wa Shiraz (Iran) aitwaye Sayyid Abdu ‘l-Fani Muhammad al-Musawi Sultanu ‘l-Wa’idhiin, ambaye wakati huo alikuwa na umri wa miaka 31 tu.

Mjadala huu ulifanyika katika mji wa Peshawar ambao wakati huo ilikuwa ni sehemu ya Bara Hindi na hivi sasa ni sehemu ya Pakistan. Ulifanyika kuanzia tarehe 27

Januari 1927 na kuundelea kwa mikesha kumi ndani ya msikiti ambako watu zaidi 200 walihudhuria kila usiku. Mjadala huu ulifanywa kwa muundo mzuri wa kuheshimiana pande zote bila ya kuvunjiana heshima. Mwandishi mwenyewe amejiita katika kitabu hiki kama “Da’i” yaani mtu anayewaombea mema watu wengine, sisi tumelitafsiri neno hilo kama “Muombezi”.

Huu ulikuwa ni mjadala uliopangwa vizuri, wa kielimu na utumiaji wa vipawa vya akili ambapo kila hoja iliyotolewa ilitumika elimu na akili kuiwasilisha mpaka pande zote zikaridhika.

Kimetolewa na kuchapishwa na: Al-Itrah Foundation S.L.P. 19701 Dar es Salaam, Tanzania Simu: +255 22 2110640 / 2127555 Barua Pepe: [email protected] [12] Tovuti: www.ibn-tv.com [13]

Source URL: https://www.al-islam.org/sw/mikesha-ya-peshwaar-sayyid-muhammad-al-musawi-al-shirazi#commen t-0

Links [1] https://www.al-islam.org/sw/person/sayyid-muhammad-al-musawi-al-shirazi [2] https://www.al-islam.org/sw/organization/al-itrah-foundation-0 [3] https://www.al-islam.org/printpdf/book/export/html/24736 [4] https://www.al-islam.org/printepub/book/export/html/24736 [5] https://www.al-islam.org/printmobi/book/export/html/24736 [6] https://www.al-islam.org/sw/person/dr-m-s-kanju [7] https://www.al-islam.org/sw/tags/ahl-al-bayt [8] https://www.al-islam.org/sw/tags/history [9] https://www.al-islam.org/sw/tags/shia [10] https://www.al-islam.org/sw/person/prophet-muhammad [11] https://www.al-islam.org/sw/person/fatimah-al-zahra [12] mailto:[email protected] [13] http://www.ibn-tv.com