Tarehe 11 Aprili, 2017
NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Tano – Tarehe 11 Aprili, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae, Katibu! NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, swali letu la kwanza leo Ofisi ya Rais, TAMISEMI litaulizwa na Mheshimiwa Lameck Okambo Airo. Na. 35 Hitaji la Jengo la Upasuaji Kata ya Koryo - Rorya MHE. KISWAGA B. DESTERY (K.n.y. MHE. LAMECK O. AIRO) aliuliza:- Wananchi wa Kata ya Koryo kwa kushirikiana na Mbunge wao na wananchi wa Rorya wanaoishi Mwanza, Arusha na Dar es Salaam wamejenga wodi ya akina mama na watoto pamoja na kununua jokofu lakini mapungufu yaliyopo sasa ni Jengo la upasuaji. 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, Serikali sasa haioni ipo haja ya kusaidia jengo hilo pamoja na vifaa vyake? NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Lameck Okambo Airo, Mbunge wa Rorya, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, katika Bajeti ya mwaka wa fedha 2016/2017 mradi uliidhinishiwa shilingi milioni 30 kwa ajili ya kuendeleza ujenzi wa jengo la upasuaji. Fedha zote zimepokelewa na tayari Halmashauri imeanza taratibu za kumpata mkandarasi. Aidha, katika mwaka wa fedha 2017/2018 Serikali imepanga kutumia shilingi milioni 25 kwa ajili ya ukamilishaji wa ujenzi wa jengo hilo. MHE. KISWAGA B. DESTERY: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninayo maswali mawili ya nyongeza. Pamoja na majibu mazuri ya Serikali, je, Serikali ina mpango gani wa kuzielekeza Halmashauri kutumia force account ili miradi midogo midogo kama hii iweze kutengenezwa kwa fedha ndogo na iweze kuleta impact? Swali la pili, kwa kuwa jambo hili linafanana kabisa na vituo vya afya vilivyoko Jimbo la Magu katika kituo cha afya Lugeye pamoja na Nyanguge.
[Show full text]