1 Bunge La Tanzania
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Thelathini na Tatu – Tarehe 20 Mei, 2020 (Bunge Lilianza Saa Nane Kamili Mchana) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Katibu. NDG. LAWRENCE MAKIGI – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MIFUGO NA UVUVI: Maelezo ya Waziri wa Mifugo na Uvuvi kuhusu Muswada wa Sheria ya Kusimamia na Kuendeleza Uvuvi wa Bahari Kuu wa Mwaka 2020 [The Deep Sea Fisheries Management and Development Bill, 2020] MHE. SIKUDHANI Y. CHIKAMBO - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KILIMO, MIFUGO NA MAJI: Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Kilimo, Mifugo na Maji kuhusu Muswada wa Sheria ya Kusimamia na Kuendeleza Uvuvi wa Bahari Kuu wa Mwaka 2020 [The Deep Sea Fisheries Management and Development Bill, 2020] 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. CECILIA D. PARESSO - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI WA WIZARA YA MIFUGO NA UVUVI: Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Muswada wa Sheria ya Kusimamia na Kuendeleza Uvuvi wa Bahari Kuu wa Mwaka 2020 [The Deep Sea Fisheries Management and Development Bill, 2020] SPIKA: Katibu. NDG. LAWRENCE MAKIGI – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU (Maswali yafuatayo yameulizwa na kujibiwa kwa njia ya mtandao) Na. 307 Huduma za Watu Wenye Ulemavu Nchini MHE. MWATUMU DAU HAJI aliuliza:- Kumekuwa na utekelezaji mdogo wa huduma za watu wenye ulemavu kwenye huduma za majengo, vyombo vya usafiri pamoja na vyombo vya habari:- Je, Serikali inasema nini katika kuhakikisha huduma za watu wenye ulemavu zinazingatiwa? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mwatumu Dau Haji, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali ilipitisha Sheria ya Watu Wenye Ulemavu Na. 9 ya Mwaka 2010 na Kanuni zake za mwaka 2012, ambapo vifungu vya 35 – 50 vya sheria hiyo 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) vinaelekeza kufikika kwa majengo, mazingira yanayotuzunguka na upatikanaji wa huduma na habari kwa watu wenye ulemavu. Mheshimiwa Spika, Serikali ilifanya mapitio ya Kanuni za Maudhui ya Vyombo vya Habari za Mwaka 2011 zinazovitaka vyombo vyote vya habari kuwa na wakalimani wa lugha ya alama. Baadhi ya vyombo vya habari vimekuwa vikitekeleza agizo hili mfano; Televisheni ya Taifa (TBC) na Uhai Tv (UTV). Serikali inaendelea kufuatilia suala hili ili kuhakikisha kuwa vyombo vyote vya habari vinatekeleza agizo hili. Aidha, kwa upande wa majengo, Serikali imeweka Mwongozo wa Utoaji wa Vibali vya Ujenzi, Usimamizi na Ukaguzi wa Majengo kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa wa mwaka 2017 ambao umezingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu. Serikali inaendelea kusimamia kuhakikisha sekta zote zinazingatia uwepo wa huduma bora za wenye ulemavu. Mheshimiwa Spika, Serikali kwa kushirikiana na wadau wa sekta binafsi na umma wanaandaa mpango wa Taifa wa kuimarisha huduma kwa watu wenye ulemavu (2020/21 - 2023/24). Moja ya Lengo mahsusi la kuanzishwa kwa mpango huo, ni kuimarisha mazingira ya upatikanaji na ufikiwaji wa huduma mbalimbali za jamii yenye kuzingatia mahitaji ya watu wenye ulemavu ikiwemo elimu, afya, hifadhi ya jamii, usafiri, barabara, michezo, burudani, vifaa saidizi, marekebisho, taarifa na mawasiliano. Na. 308 Kuruhusu Wananchi Kujenga Shule za Msingi MHE. JOEL M. MAKANYAGA aliuliza:- Shule nyingi za msingi hapa nchini zina wanafunzi wengi sana wanaozidi kiwango kinachotakiwa cha wanafunzi takribani 700. 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, ni kwa nini Serikali isiruhusu wananchi wajenge shule nyingine kwa mpango wa kujenga hata madarasa mawili kila mwaka na shule hizi zitambuliwe kisheria? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Joel Mwaka Makanyaga, Mbunge wa Chilonwa, kama ifuatavyo:- Mheshimwa Spika, Wananchi wanaruhusiwa kujenga shule katika maeneo yenye mahitaji kwa kushirikisha viongozi wa Halmashauri ili kusogeza huduma karibu na wananchi. Kupitia utaratibu huu, Serikali imefanikiwa kuwa na shule ya msingi kila kijiji na shule za sekondari kila kata. Aidha, Serikali kwa kushirikisha nguvu za wananchi imekuwa na utaratibu wa kujenga vituo shikizi katika maeneo ambayo shule mama iko mbali ili kuboresha mazingira ya kujifunzia na kufundishia. Baadhi ya vituo hivyo baadaye husajiliwa kuwa shule baada ya kukidhi vigezo. Na. 309 Tatizo la Umeme Mpaka wa Tunduma MHE. FRANK G. MWAKAJOKA aliuliza:- Serikali imeshindwa kutatua tatizo la upatikanaji wa umeme katika mpaka wa Tunduma kwa muda mrefu sasa jambo linalosababisha kupoteza wageni na wateja wa Bandari ya Dar es Salaam kwa kuhofia usalama wao kutokana na giza:- Je, Serikali iko tayari kuunganisha umeme wa Zambia ili huduma hii iwe inapatikana muda wote ili kulinda wateja wanaopitisha mizigo toka Bandari ya Dar es Salaam na mpaka wa Tunduma? WAZIRI WA NISHATI alijibu:- 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Frank George Mwakajoka, Mbunge wa Tunduma, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Mji wa Tunduma unatumia umeme wa Gridi ya Taifa kwa asilimia 100 kupitia njia ya msongo wa kilovoti 33 kutoka Kituo cha kupoza umeme cha Iyunga, mjini Mbeya na kusambaza umeme katika maeneo ya Wilaya za Mbozi, Momba na Songwe. Mheshimiwa Spika, kwa ujumla hali ya upatikanaji umeme kwa sasa ni ya kuridhisha. Hata hivyo, hitilafu katika baadhi ya miundombinu ya umeme imekuwa ikisababisha kuzima umeme ili kupisha matengenezo katika njia kuu ya umeme katika Mkoa wa Songwe na baadhi ya maeneo ya Wilaya ya Mbeya vijijini. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia TANESCO imekarabati miundombinu ya umeme ili kuimarisha upatikanaji wa umeme katika maeneo hayo. Aidha, katika mwaka wa fedha 2020/2021, TANESCO imepanga kujenga kituo cha umeme Mlowo (switching station) pamoja na njia ya umeme msongo wa kilovoti 33 yenye urefu wa kilomita 65 kutoka kituo cha kupoza umeme cha Iyunga Mbeya hadi Mlowo kwa gharama ya shilingi bilioni 1.2. Mradi huu unatarajia kuanza kutekelezwa mwezi Julai, 2020 na kukamilika mwezi Mei, 2021 kupitia Kampuni ya TANESCO M/S Electrical Transmission and Maintenance Company (ETDCO) Limited. Na. 310 Vifo Vitokanavyo na Ajali za Barabarani na Majini MHE. MASOUD ABDALLAH SALIM aliuliza:- Ajali za barabarani na majini zimekuwa zikisababisha vifo na majeruhi. 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Je, ni watu wangapi wamepoteza maisha kwa ajali za barabarani na majini kuanzia kutoka Juni, 2018 hadi sasa? WAZIRI WA MAMBO YA NDANI YA NCHI alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Masoud Abdallah Salim, Mbunge Wa Mtambile, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, katika Kipindi cha Juni 2018 hadi Aprili, 2020 ajali za barabarani zilitokea jumla ni 3,500, ambazo zimesababisha vifo 1,772 na majeruhi 4,906. Aidha, kwa upande wa ajali za majini kwa kipindi kama hiki kuanzia mwezi Juni, 2018 hadi mwezi Aprili, 2020 zimetokea ajali 17 zilizosababisha vifo vya watu 244 na majeruhi 41. Na. 311 Barabara ya Singida - Sepuka - Ndago – Kizaga MHE. MARTHA M. MLATA aliuliza:- Je, ni kitu gani kimesababisha kuchelewa kwa ujenzi wa barabara ya Singida – Sepuka – Ndago hadi Kizaga? WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Martha Moses Mlata, Mbunge Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, barabara ya Sabasaba – Sepuka – Ndago – Kizaga (kilometa 77.6) anayozungumzia Mheshimiwa Mbunge ni barabara ya Mkoa iliyojengwa kwa kiwango cha changarawe na inahudumiwa na Wakala wa Barabara Tanzania (TANROADS) Mkoa wa Singida. Barabara hii ni muhimu kiuchumi kwa kuwa inapita kwenye vijiji vingi vikiwemo vijiji vya Sepuka, Kaselya na Ndago ambavyo wakazi wake ni wakulima wa zao la alizeti. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, kwa kutambua umuhimu wa barabara hii, Serikali imeendelea kutenga fedha za matengenezo mbalimbali kila mwaka ili iendelee kupitika katika majira yote ya mwaka. Katika mwaka wa fedha 2018/ 2019, jumla ya Sh.1,403.81 zilitengwa kwa ajili ya kufanya kazi za matengenezo ya kawaida na sehemu korofi. Aidha, katika mwaka wa fedha 2019/2020, jumla ya shilingi 1,171.04 zilitengwa kwa ajili ya kufanya matengenezo ya kipindi maalum na sehemu korofi. Vilevile, Serikali imeanza kufanya upembuzi yakinifu na usanifu wa kina wa barabara hiyo kwa ajili ya kujenga kwa kiwango cha lami ambapo katika mwaka wa fedha 2020/2021, shilingi milioni 250 zimetengwa kwa ajili ya kazi ya usanifu wa kina. Mheshimiwa Spika, mara usanifu wa kina utakapokamilika, Serikali ifahamu gharama za ujenzi na kuanza kutafuta fedha kwa ajili ya ujenzi wa barabara hiyo kwa kiwango cha lami. Na. 312 Maeneo yenye Mawasiliano Hafifu – Wilaya ya Urambo MHE. MARGARET S. SITTA aliuliza:- Wilaya ya Urambo ina maeneo ambayo yana mawasiliano ya simu na mengine yenye mawasiliano hafifu na Wizara inayo orodha ya maeneo yenye mawasiliano hafifu Wilayani Urambo. Je, ni lini maeneo hayo yatafanyiwa kazi ili wananchi hao waweze kuwasiliana katika kujitafutia maendeleo? WAZIRI WA UJENZI, UCHUKUZI NA MAWASILIANO alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Margaret Simwanza Sitta, Mbunge wa Urambo, kama ifuatavyo:- 7 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Spika, nakiri kuwa, pamoja na juhudi za Serikali katika kuhakikisha mawasiliano ya simu yanasambazwa nchini kote hadi kufikia mwishoni mwa mwaka 2020, bado Wilaya ya Urambo ina maeneo ambayo mawasiliano ya