MAJADILIANO YA BUNGE MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao Cha
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA MBILI Kikao cha Ishirini na Mbili – Tarehe 11 Julai, 2008 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU Na.192 Serikali Kusimamia Sheria ya Udhibiti wa Mazingira MHE. LUDOVICK J. MWANANZILA K.n.y. MHE. PONSIANO D. NYAMI aliuliza:- Kwa kuwa, nchi yetu inaathirika na uharibifu mkubwa wa mazingira hasa uharibifu wa misitu kutokana na uchomaji wa mkaa na ukataji wa miti ovyo kwa ajili ya kilimo:- (a)Je, Serikali ina mpango gani kusimamia Sheria zilizotungwa kudhibiti uharibifu huo? (b)Je, ni lini Serikali itaweka mazingira rahisi ya utumiaji wa Nishati ya makaa ya mawe na kuhimiza matumizi ya umeme kwa kupikia ili kuokoa mazingira? WAZIRI WA NCHI OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MAZINGIRA alijibu:- Mheshimiwa Spika, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ponsiano Nyami, Mbunge wa Nkansi, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo: (a) Bunge lako tukufu lilipitisha sheria ya usimamizi wa Mazingira ya mwaka 2004 na sheria ya misitu ya mwaka 2002. sheria ya misitu inahimiza usimamizi shirikishi wa misitu na inawapa uwezo Halmashauri za Wilaya kutunga sheria ndogo katika usimamizi bora wa mazingira na misitu. ili kusimamia sheria hii pamoja na mambo mengine Serikali inafanya juhudi zifuatazo:- 1 (i) Imeandaa mwongozo wa uvunaji na usafirishaji wa mazao ya misitu ya mwaka 2006. mwongozo huo unasisitiza uvunaji bora unaozingatia mpango wa usimamizi; (ii)Inaendelea kuelimisha jamii kuhusu matumizi ya teknolojia rahisi ya nishati mbadala na jadidifu na kufanya utafiti kupitia Tume ya Sanyansi na Teknolojia zinazolenga kupunguza mahitaji ya kuni na mkaa; (iii)Imeanzisha vikosi vitano vya doria hadi sasa ili kukabiliana na biashara haramu ya mazao ya misitu ikiwemo kukata miti ovyo na kuchoma mkaa; (iv)Imeanzisha vituo vya ukaguzi wa mazao ya misitu katika maeneo yanayosafirisha mazao hayo kwa wingi nchini; (v)Imeandaa mwongozo wa mpango wa usimamizi wa misitu ambao utaanza kutumika katika usimamizi wa misitu asili, kwa mujibu wa mpango huo hairuhusiwi kuvuna misitu ambayo haina mpango wa usimamizi; (vi)Imeongeza idadi ya hifadhi asilia za misitu ambapo usimamizi wake umeboreka zaidi na hivyo kuzuia shughuli za ukataji miti ovyo na uchomaji wa mkaa; na (vii)Inatekeleza mkakati wa kuhifadhi mazingira ya ardhi na vyanzo vya maji, mkakati huu unawashirikisha wadau mbalimbali na unatekelezwa Mikoa yote nchini. Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Tume ya Sayansi na Teknolojia inafanya utafiti wa vitofali vya makaa ya mawe (coal-clay briquettes) katika mgodi wa Kiwira ili kupunguza muda wa kuwasha vitofali, makali ya moto na gesi chafu zenye oksidi za sulfur (Sox) zinazozalishwa na kutengeneza majiko ya bei nafuu. Hadi sasa utafiti umefanikiwa kupunguza ukali wa moto wa vitofali vya makaa ya mawe, utafiti unaendelea katika kupunguza muda wa kuwasha vitofali, wingi wa gesi chafu zinazozalishwa na makaa ya mawe na utengenezaji wa majiko ya bei nafuu. mapungufu hayo yakipata ufumbuzi Watanzania wengi zaidi watatumia makaa ya mawe kupikia na hivyo kuhifadhi mazingira nchini. Mheshimiwa Spika, aidha Serikali inahimiza uendelezaji wa matumizi ya nishati mbadala na jadidifu kama vile nishati ya jua, upepo, gesi asilia na bio-gas. Pia kuendeleza matumizi ya jiko sanifu mkaa unaotengenezwa kwa taka za nyumbani na jiko za moto poa. Ni matumaini yangu kuwa kupitia wakala wa nishati Vijijini maeneo mengi yatapata nishati ya kupikia ikiwemo ya umeme kwa gharama nafuu. MHE. LUDOVICK J. MWANANZILA: Mheshimiwa Spika, pamoja na majibu mazuri ya Mheshimiwa Waziri:- 2 (i)Je, Serikali haioni kwamba sheria ndogo ndogo hizi zinazotungwa na Halmashauri zinashindwa kutekelezwa vizuri kwa sababu Maafisa Misitu wanaopaswa kusimamia miradi hii ya kutokata misitu hawatoshi. Katika Wilaya ya Nkasi ambayo ina misitu mingi sana Maafisa Misitu hawatoshi, na katika Halmashauri ya Sumbawanga vijijini ndiyo maana msitu mkubwa wa Kalambo na Msitu mkubwa wa Dwafi unaendelea kufekwa kwa ajili ya kutengeneza mkaa na kwenda kuuza katika Miji ya Namanyere na Sumbawanga. Je, Serikali itachukua hatua gani kuhakikisha kwamba hawa maafisa wanaosimamia misitu wanaongezwa ili kuweza kusimamia hizo sheria ndogo ndogo za Halmashauri. (ii)Vipo vikundi vya akina mama ambao wamejitolea kufanya kazi ya kueneza matumizi ya Mkaa wa Mawe unaochanganywa kidogo na udongo wa mfinyanzi ili kujaribu kuzuia watu wasikate miti kutengeneza mkaa na badala yake watumie ule mkaa tulionao wa Kiwira na sehemu nyingine. Je, Serikali haioni kuwasaidia hawa akina Mama ambao wamejitokeza katika maonesho mbalimbali itakuwa ni jawabu la kusaidia kupunguza ukataji na uharibifu wa misitu katika nchi hii? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, naomba kumjibu Mheshimiwa Lodovick Mwananzila, maswali yake mawili kama ifuatavyo:- (i) Kuhusu jitihada za Serikali katika kuongeza Maafisa Misitu, napenda kumhakikishia kwamba kufuatana na hotuba inayoendelea sasa ya Wizara ya Maliasili na Utali kumeonyeshwa kabisa jitihada za kuongeza wataalamu hao. Lakini vilevile Serikali kupitia Ofisi yetu ya Makamu wa Rais Kitengo chetu cha Mazingira tupo katika hatua za mwisho za kuweza kuwaajiri Maafisa Mazingira katika maeneo yote ya Wilaya yetu, tayari Wilaya kadhaa zimesha ajiri Maafisa hao ambao kwa kweli kazi yao watashikrikiana pamoja na Maafisa Misitu katika kuhakikisha kwamba Mazingira yetu yanalindwa na kuhifadhiwa. (ii) Mheshimiwa Spika, swali lake la pili, napenda kwanza kumpongeza Mheshimiwa Mwananzila kwa jitihada zake za kuwa mwanaharakati na mpenzi wa kulinda Mazingira, mimi binafsi nilikutana na akina mama hao katika maonesho ya Saba Saba na tumekubaliana kwamba tutashirikiana nao katika maonesho ya Nane Nane hapa na kupitia Ofisi yetu ya Makamu wa Rais kitengo chetu cha Mazingira tutahakikisha kabisa kwamba tunashirikiana nao na kuhakikisha teknolojia hii rahisi ya kutumia vumbi za makaa ya mawe ambayo wanachanganya taka zingine inaweza kuendelezwa na kuweza kuokoa misitu yetu na kupunguza matumizi ya kuni na mkaa. MHE. ANNA R. LUPEMBE: Mheshimiwa Spika, Ahsante sana kwa kunipa nafasi ya kuweza kuuliza swali la nyongeza. Naomba nimpongeze Waziri kwa majibu 3 mazuri aliyotupatia, Mkoa wa Rukwa hususani Wilaya ya Mpanda pamoja na Nkansi kuna mapori mazuri sana pamoja na hifadhi za wanyama, sasa hivi hawa waharibifu wameshaanza kuingia katikati ya mapori hayo na kuzidi kuharibu mapori hayo. Je, Waziri yupo tayari kuja Mkoa wa Rukwa kuja kuona hali halisi ya mapori yetu jinsi yanavyoharibika? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, napenda kumjibu Mheshimiwa Anna Lupembe, Mbunge wa Viti Maalum, kutoka Rukwa swali lake kama ifuatavyo:- Kwanza nimpongeze na yeye kwa jitihada zake za kuweza kufuatilia masuala ya mazingira na nijibu tu kwamba mimi niko tayari kabisa kuandamana naye Mheshimiwa Anna Lupembe, Mheshimiwa Ponsiano Nyami na Mheshimiwa Mwananzila kwenda Mkoa wa Rukwa na kuweza kuangalia hali ilivyo. Lakini niwaeleze tu Waheshimiwa Wabunge kutoka Mkoa wa Rukwa na Mkoa wa Kigoma kwamba tarehe 25 tutakuwa na mkutano nao kuwaelezea masuala ya maendelezi ya ziwa letu Tanganyika kwa hivyo pamoja na hayo tutazungumzia mambo yote ya uhifadhi wa mazingira. MHE. ELIATA N. SWITI: Mheshimiwa Spika, ahsante sana kwa kunipa nafasikwa kuwa Mkoa wa Rukwa unayo Makaa yam awe ambayo sasa hivi yanachimbwa na mchimbaji mdogo lakini misitu yetu inaendelea kuteketea, Je Serikali inasemaje kama ingeweka nguvu ili makaa hayo ya mawe yaweze kutumika Mkoani Rukwa kupunguza uharibifu wa mazingira? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MAZINGIRA: Mheshimiwa Spika, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Eliata Switi, Mbunge wa Viti Maalum, kutoka Mkoa wa Rukwa kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, ni kweli kabisa kwamba kuna maeneo ambayo yanahifadhi hiyo ya makaa ya mawe na kama nilivyojibu katika jibu langu la msingi nilieleza kwamba tafiti zile ili kuhakikisha kwamba makaa ya mawe katika kutumika kwa matumizi ya kupikia hayatakuwa na madhara kwa binadamu. Lakini pia tuangalie ni jinsi gani tunaweza kupunguza ukali wa moto ule wa makaa ya mawe, kwa hivyo nakubaliana na wewe kabisa kwamba tafiti zitaendelea na pale tutafikia katika hatua nzuri ya kuweza kuhakikisha kwamba inaweza kutumika sasa tutahakikisha kwamba na watu wenye rasilimali hizo wanaweza kutumia na tunataka 4 lifanyike hivi kwa haraka kwa sababu tunataka kupunguza matumizi makubwa ya mkaa na kuni ambao unaharibu sana misitu yetu. Na. 193 Shamba la Mifugo Linalomilikiwa na SMZ huko Bagamoyo MHE. MOSSY SULEIMANI MUSSA aliuliza:- Kwa kuwa Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar iliwahi kuwa na shamba kubwa la mifugo (ng’ombe) ranchi huko Bagamoyo:- (a) Je, Serikali ya SMZ bado inamiliki shamba hilo? (b) Je, hadi kufikia kuboreshwa kwa shamba hilo SMZ ilitumia shilingi ngapi? NAIBU WAZIRI WA MAENDELEO YA MIFUGO NA UVUVI alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Waziri wa Maendeleo ya Mifugo na uvuvi naomba kujibu swali la Mheshimiwa Mossy Suleimani Mussa Mbunge wa Mfenesini lenye vipengele (a) na (b) kwa pamoja kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Spika kwa kuzingatia Ranchi ya Zanzibar Bagamoyo (RAZABA) iliyoko Makurunge katika Wilaya ya Bagamoyo inamilikiwa na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, Ranchi hiyo ilianzishwa mwaka 1976 baada ya kupata kibali kutoka kwa Kamishna wa Ardhi chenye kumbukumbu namba LD/70254/12/TBR cha tarehe 24/09/1971, hivyo kwa taarifa hizo Wizara yangu bado inaamini shamba la RAZABA bado ni mali ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar, hata hivyo kwa