MKUTANO WA NANE Kikao Cha Thelathini Na Tatu

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

MKUTANO WA NANE Kikao Cha Thelathini Na Tatu Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _________________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Thelathini na Tatu – Tarehe 26 Julai, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI NA MADINI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati na Madini kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. NAIBU WAZIRI WA VIWANDA NA BIASHARA: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MHE. ABUU HAMOUD JUMAA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA VIWANDA NA BIASHARA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Viwanda na Biashara Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka 2011/2012 Pamoja na Maoni ya Kamati Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. MHE. HIGHNESS SAMSON KIWIA - MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA VIWANDA NA BIASHARA: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani juu ya Wizara ya Viwanda na Biashara Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Viwanda na Biashara kwa mwaka wa Fedha, 2012/2013. MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, maswali leo kwa Waziri Mkuu naona Kiongozi wa Kambi ya Upinzani hatumwoni. Kwa mujibu wa Kanuni zetu kama hayupo hawezi kuweko mbadala wake na kwa hiyo, nitaendelea na wale ambao walishaomba. MHE. ANNE K. MALECELA: Mheshimiwa Spika, kabla sijamwuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu swali, naomba tuwatakie heri Mama Anna Abdallah na Mama Makinda leo ni siku yao ya kuzaliwa, kwa hiyo happy birthday. (Makofi) Mheshimiwa Spika, baada ya hapo napenda kumwuliza Mheshimiwa Waziri Mkuu swali. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kuwa sisi wana Siasa hasa sisi tulioko humu ndani tuna uwezo mkubwa sana wa kuijenga nchi hii. Lakini pia tuna uwezo wa pili wa kuibomoa nchi hii na hata kuiingiza katika vita. Mheshimiwa Waziri Mkuu, siku za karibuni mmeanza tabia ambayo nilikuwa sijaiona muda wote tangu nimekuwa Mbunge katika kipindi changu cha tatu hiki Wabunge kuingia kwenye Majimbo ya wenzao na kuchukua hatua ya kuwakosoa kiutendaji na kutoa maneno yasiyoridhisha mbele ya wananchi kitu ambacho kimepelekea vurugu zikatokea mwishoni mwa wiki hata kuleta madhara. Je, Serikali inatoa tamko gani kwa sababu tabia hii ikiachiwa kuna siku tutaingia kwenye vita ya wenyewe kwa wenyewe? (Makofi) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, kwanza naomba nipongeze maana kama ni birthday yako nafikiri unastahili. (Makofi) SPIKA: Ahsante sana. WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, naomba nijaribu kutoa maelezo kuhusu suala ambalo Mheshimiwa Anna Kilango Malecela, amejaribu kulieleza. Mimi nataka nikubali kwamba ni kweli ziko dalili za namna hiyo. Kwa bahati mbaya hata Jimboni kwangu yalinipata. (Makofi/Kicheko) Lakini mimi tafsiri yangu ilikuwa ni rahisi tu kwa sababu mambo haya yanategemea ukomavu wa mwanasiasa mwenyewe ambaye anakwenda kwenye eneo hilo. Maana wale waliokomaa wenye kuelewa dhamira ya Serikali ambao wanajua nia yetu hasa ni nini anajua wajibu wake anapokuwa katika maeneo haya ni kuzungumzia Sera za Chama chake, ama kusaidia kuweka sawa baadhi ya maeneo ambayo wanafikiri yanastahili kuboreshwa zaidi. Lakini sasa ukiwa na mwanasiasa ambaye kidogo hajafikia mahali pa kupevuka ni kweli ataanza kushughulikia individuals badala ya ku-deal na issues. (Makofi) Lakini mapema kabla hatujaja hapa Bungeni nilipata nafasi ya kuzungumza na msajili wa Vyama na nikamsihi sana kwamba asaidie vyama hivi vyote kwa kujaribu kukutana nao kimoja kimoja kujaribu kuwaelimisha juu ya ujenzi wa Demokrasia ya Vyama Vingi na maana yake hasa ni nini kwa sababu inaonekana bado wengi hatuelewi katika vuguvugu hili wajibu wetu hasa ni kitu gani. (Makofi) Mheshimiwa Spika, lakini wakati huo huo, Sheria ya Msajili wa Vyama ya Mwaka 1992 ambayo tulifanya Marekebisho hapa mwaka 2009 ukichukua na Kanuni zake za mwaka 2007 zinajieleza bayana kabisa, zimetoa maelezo mazuri sana namna Vyama vinavyopaswa kuendesha shughuli zake hasa nyakati hizi ambazo si za kampeni. Zimeeleza bayana kabisa. (Makofi) Lakini kizuri zaidi kwenye Sheria hizo na mimi naomba mzipitie msome kwa makini kama ni Chama ambacho kiko kwenye usajili wa muda Msajili wa Vyama anaweza akakifuta kwa matendo ambayo yanaashiria uvunjifu wa amani kwa maana ya matusi, kujaribu kudharauliana na kadhalika. Lakini hata Chama kilichoandikishwa kinaweza vile vile chini ya Sheria hiyo kufutwa endapo Msajili ataridhika na jambo hilo. (Makofi) Kwa hiyo, mimi nadhani nataka niwasihi viongozi wote kwa ujumla tuko hapa sisi wote ni watu wazima, tuko hapa kwa nia njema, tunataka kujenga nchi yetu vizuri, chonde chonde twende kwenye Majimbo tuzungumze masuala ya msingi ya Sera ya namna ya kutekeleza na kupeleka nchi hii mahali pazuri. Narudia tena unajua Mwanasiasa anayekaa anahangaika na individuals, watu hivi Pinda hiki, ujue na yeye vile vile ana tatizo kubwa sana katika upeo wake. (Makofi) Kwa hiyo, mimi nadhani kwa ufupi naweza nikalisema hivyo na kuwasihi wote tujaribu kufanya kazi hiyo kwa umakini mzuri kwa lengo la kujenga taifa letu na kwa heshima ya nchi yetu. (Makofi) MHE. MWIGULU LAMECK MCHEMBA MADELU: Mheshimiwa Waziri Mkuu, Serikali imeweka utaratibu mzuri sana kwa Waheshimiwa Wabunge, kwa kuanzisha Mfuko wa Jimbo, Mfuko wa Kuchochea Maendeleo. Lakini maendeleo hayo yanachochewa kwa kushirikiana na Madiwani. Lakini tofauti ni kwamba Madiwani wamekuwa wakichochea hayo maendeleo kwa kutumia posho zao wanazozipata. Je, Serikali haioni kuwa ni vyema kuwaangalizia utaratibu Madiwani wa kuwatengea fungu hata dogo tu linalolingana na Kata ili na wenyewe wanapoitwa kuchochea shughuli za maendeleo ambazo sote tunashuhudia wamekuwa wakisumbuliwa sana waweze kutumia mfuko huo tofauti na sasa wanavyotumia posho zao? (Makofi) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, kwanza namshukuru sana Mheshimiwa Mwigulu Mchemba. Ni swali zuri lakini si rahisi sana kulijibu. Mimi ni Diwani vile vile wakinisikia na mimi nasema ovyo ovyo huko ni taabu vilevile. Lakini Sheria ile inachosema hapa ni nini kwa sababu ule mfuko ni wa Kuchochea Maendeleo katika Majimbo. Kuchochea maana yake nini hapa? Sheria inasema unapokuwa katika Jimbo lako miradi inayoendelea katika maeneo hayo. Unapofika mahali fulani na ukaombwa pengine msaada kumalizia mabati 40 au 50 Mfuko huu utakusaidia kuwezesha shule au zahanati hiyo kukamilisha ule mradi. Kwa maneno mengine ni fedha ambayo inakwenda kutoa mkusumo kwa wananchi katika maeneo yanayohusika. Si fedha ambayo unakuwa nayo unatembea unagawa kwa kila mtu unayemwona hapana. (Makofi) Kwa hiyo, basi kikubwa ninachokiona ni vizuri Waheshimiwa Wabunge ambao ndio Wenyeviti wa Mifuko ile na katika Sheria ile tumesema Madiwani, angalau wawili wawemo, tuhakikishe wale Madiwani, wawili wanakuwemo kwa sababu wanasaidia kuainisha baadhi ya miradi ambayo iko chini ya Kata fulani fulani kwa lengo la Mbunge kuweza kujua akipita pale asaidie namna gani. Sasa rai yake ni nzuri lakini kwa uwezo wa kibajeti tulionao leo pengine si rahisi sana. Lakini tunachoweza kuahidi tu mbele ya Bunge hili bado tutaendelea sisi kuboresha mafao/posho za Madiwani, ili kile kidogo kinapobanwa basi waweze kuchangia kwa kadri watakavyoona inafaa. (Makofi) MHE. MCH. PETER SIMON MSIGWA: Mheshimiwa Spika, nakushukuru kwa kunipa nafasi hii. Nichukue fursa hii kabla sijauliza swali kuwatakia heri Waislam wote katika huu Mfungo wa Ramadhani katika Nguzo yao Muhimu. (Makofi) Mheshimiwa Waziri Mkuu swali langu, kwa mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, ambalo suala la Muungano ni suala la Katiba. Kila mtu anao uhuru wa kuabudu dini anayoitaka pasipokuingilia uhuru wa dini nyingine. Tarehe 20 Julai, 2012 Waziri wa Katiba wa Serikali ya Zanzibar alilihutubia Taifa la Zanzibar kupitia Televisheni na Radio akiwaambia watu wote wanaoishi Zanzibar na wanaoingia Zanzibar kuendana na Mfungo wa Ramadhani, akiamrisha kwamba Hotels zote na Restaurant zote zisiuze vyakula wakati wa asubuhi na mchana. Kama vile haitoshi alisema “watu wote wanaovaa nguo fupi hasa wanawake zinazoweza kuwatamanisha wanaume vyombo vya dola vichukue hatua” alisema vile vile “kwamba yeyote anayepatikana anakula chakula wakati wa mchana mamlaka ichukue hatua. (Makofi) Mheshimiwa Waziri Mkuu jambo hili ni hatari sana kwa Mujibu wa Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, jambo hili linadhalilisha Dini zingine. Naomba tuvumiliane nyie mkisema tunawavumilia. Jambo hili linatikisa uhuru wetu na Muungano wetu, ninaomba msimamo wa Serikali yako. (Makofi) WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Spika, kwa bahati mbaya mimi sikusikiliza hiyo taarifa naomba kwanza niseme hilo. Lakini la pili sielewi hasa alisema nini naona ume-quote hivi. Kwa hiyo, sina hakika kama ndivyo ilivyokuwa au hapana. Lakini vyovyote vile itakavyokuwa kama unazungumza Serikali mbili iko Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania na iko Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. Kauli imetoka kwa Kiongozi wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. (Makofi) Ninachokifikiria hapa kwamba inawezekana kabisa kwa mazingira ya Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar wakati wa mwezi Mtukufu wa Ramadhani wameona hilo linaweza likasaidia kuwafanya wawe na mfungo mzuri. Kwa hiyo, mimi nadhani rai nzuri hapa ni kusema tuache waliendeleze kwa namna wanavyoona kwa mazingira yao inafaa. (Makofi) Lakini moja hili la uvaaji wa nguo fupi, nguo fupi nadhani tunakubaliana tu kwamba ni jambo ambalo si zuri halina staha. Linahitaji kwa kweli kusemwa na kila mtu, wala si jambo ambalo nasema linahatarisha Muungano hata kidogo, ni jambo tu ambalo linaeleweka tu.
Recommended publications
  • 9Aprili,2013
    9 APRILI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Kwanza - Tarehe 9 Aprili, 2013 WIMBO WA TAIFA (Hapa Waheshimiwa Wabunge Waliimba Wimbo wa Taifa) (Mkutano Ulianza Saa 3.00 Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa msimame tena. Mtakumbuka kwamba wakati wa Vikao vyetu vya Kamati, kwa bahati mbaya sana tulimpoteza mpenzi wetu Mheshimiwa Salim Hemed Khamis. Kwa hiyo, tumkumbuke kwa dakika moja. (Hapa Waheshimiwa Wabunge walisimama kwa Dakika moja kumkumbuka Mheshimiwa Salim Hemed Khamis aliyekuwa Mbunge wa Chambani Mwenyezi Mungu aiweke roho yake mahali pema peponi, Amin. Ahsanteni sana na karibuni tukae. 1 9 APRILI, 2013 Waheshimiwa Wanbunge, katika Mkutano wa Tisa, Bunge lilipitisha Muswada wa Sheria ya Serikali uitwao The Plant Breeders` Rights Bill, 2012, kwa taarifa hii napenda kulialifu Bunge hili Tukufu kwamba, Mswada huo umekwisha pata kibali cha Mheshimiwa Rais na kuwa Sheria ya nchi iitwayo: The Plant Breeders` Rights Act, 2012 Na. 9 ya mwaka 2012. Kwa hiyo, ule sasa ni sheria ya Nchi. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE: Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kuwasilisha mezani Taarifa ya Matoleo yote ya Gazeti la Serikali pamoja na nyongeza zake zilizochapishwa tangu Kikao cha mwisho cha Mkutano wa Bunge uliopita. Mheshimiwa Spika, naomba kuwasilisha. MASWALI NA MAJIBU Na. 1 Kujenga Barabara ya Old Moshi kwa Lami MHE. GODFREY W. ZAMBI (K.n.y. MHE. DKT. CYRIL A. CHAMI) aliuliza:- Je, Serikali itatekeleza lini ahadi ya kujenga kwa kiwango cha lami Barabara ya Old Moshi inayoanzia Kiboriloni kupitia Kikarara, Tsuduni hadi Kidia? 2 9 APRILI, 2013 NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA, (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt.
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 112 Sept - Dec 2015
    Tanzanian Affairs Issued by the Britain-Tanzania Society No 112 Sept - Dec 2015 ELECTION EDITION: MAGUFULI vs LOWASSA Profiles of Key Candidates Petroleum Bills Ruaha’s “Missing” Elephants ta112 - final.indd 1 8/25/2015 12:04:37 PM David Brewin: SURPRISING CHANGES ON THE POLITICAL SCENE As the elections approached, during the last two weeks of July and the first two weeks of August 2015, Tanzanians witnessed some very dra- matic changes on the political scene. Some sections of the media were even calling the events “Tanzania’s Tsunami!” President Kikwete addessing the CCM congress in Dodoma What happened? A summary 1. In July as all the political parties were having difficulty in choosing their candidates for the presidency, the ruling Chama cha Mapinduzi (CCM) party decided to steal a march on the others by bringing forward their own selection process and forcing the other parties to do the same. 2. It seemed as though almost everyone who is anyone wanted to become president. A total of no less than 42 CCM leaders, an unprec- edented number, registered their desire to be the party’s presidential candidate. They included former prime ministers and ministers and many other prominent CCM officials. 3. Meanwhile, members of the CCM hierarchy were gathering in cover photos: CCM presidential candidate, John Magufuli (left), and CHADEMA / UKAWA candidate, Edward Lowassa (right). ta112 - final.indd 2 8/25/2015 12:04:37 PM Surprising Changes on the Political Scene 3 Dodoma to begin the lengthy and highly competitive selection process. 4. The person who appeared to have the best chance of winning for the CCM was former Prime Minister Edward Lowassa MP, who was popular in the party and had been campaigning hard.
    [Show full text]
  • 25 JUNI, 2013 MREMA FULL.Pmd
    25 JUNI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Hamsini na Sita - Tarehe 25 Juni, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Ifuatazo Iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA:- Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za TCRA Consumer Consultative Council (TCRA (CCC) kwa Mwaka ulioshia tarehe 30 Juni, 2012 (The Annual Report and Audited Accounts of TCRA Consumer Consultative Council (TCRA – CCC) for the Year Ended 30th June, 2012). MASWALI NA MAJIBU Na. 457 Wakuu wa Mikoa/Wilaya Kuwa Wabunge MHE. CHRISTOWAJA G. MTINDA aliuliza:- Moja ya majukumu ya Bunge ni kuisimamia na kuishauri Serikali na pia Ibara ya 67(2)(g) ya Katiba ya Jamhuri 1 25 JUNI, 2013 ya Muungano wa Tanzania inaeleza kukoma kwa mtu kuwa Mbunge endapo mtu huyo amepewa madaraka ya Afisa Mwandamizi katika Utumishi wa Umma. (a) Je, ni kwa maana gani Wabunge ambao ni Wakuu wa Mikoa au Wakuu wa Wilaya wanatimiza majukumu yao ya Kibunge? (b) Je, ni kwa namna gani viongozi hao wanakiuka Ibara ya 67(2)(g)ya Katiba pamoja na kuwa wanateuliwa na Rais? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Christowaja Gerson Mtinda, Mbunge wa Viti Maalum, lenye sehemu (a) na (b) kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Naibu Spika, Wabunge ambao ni Wakuu wa Mikoa au Wilaya wanatimiza majukumu yao ya Kibunge kwa kuzingatia Ibara 63(3)(a) – (e) ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
    [Show full text]
  • 1458125471-Hs-6-8-20
    [Show full text]
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who Will Benefit from the Gas Economy, If It Happens?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013 Who will benefit from the gas economy, if it happens? Supported by: 2 TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? ACKNOWLEDGEMENTS Policy Forum would like to thank the Foundation for Civil Society for the generous grant that financed Tanzania Governance Review 2013. The review was drafted by Tanzania Development Research Group and edited by Policy Forum. The cartoons were drawn by Adam Lutta (Adamu). Tanzania Governance Reviews for 2006-7, 2008-9, 2010-11, 2012 and 2013 can be downloaded from the Policy Forum website. The views expressed and conclusions drawn on the basis of data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. TGRs review published and unpublished materials from official sources, civil society and academia, and from the media. Policy Forum has made every effort to verify the accuracy of the information contained in TGR2013, particularly with media sources. However, Policy Forum cannot guarantee the accuracy of all reported claims, statements, and statistics. Whereas any part of this review can be reproduced provided it is duly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. ISBN:978-9987-708-19-2 For more information and to order copies of the report please contact: Policy Forum P.O. Box 38486 Dar es Salaam Tel +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] Suggested citation: Policy Forum 2015.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA SITA _________________ Kikao cha Thelathini na Mbili – Tarehe 18 Julai, 2009 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA: Hotuba ya Bajeti ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. Taarifa ya Mwaka na Hesabu za Kituo cha Kimataifa cha Mikutano cha Arusha kwa Mwaka wa Fedha 2007/2008 (The Annual Report and Accounts of Arusha International Conference Center for the Year 2007/2008) MWENYEKITI WA KAMATI YA MAMBO YA NJE, ULINZI NA USALAMA: Taarifa ya Kamati ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka 2008/2009, pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. MHE. HEMED MOHAMMED HEMED (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA WIZARA YA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA): Taarifa kwa Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. NAIBU WAZIRI WA MAWASILIANO, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: 1 Randama za Makadirio ya Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010. HOJA ZA SERIKALI Makadirio ya Matumizi ya Serikali kwa Mwaka 2009/2010 – Wizara ya Mambo ya Nchi za Nje na Ushirikiano wa Kimataifa WAZIRI WA MAMBO YA NJE NA USHIRIKIANO WA KIMATAIFA: Mheshimiwa Naibu Spika, kufuatia Taarifa iliyowasilishwa leo hapa Bungeni na Mwenyekiti wa Kamati ya Bunge ya Mambo ya Nje, Ulinzi na Usalama (NUU), naomba kutoa hoja kwamba, Bunge lako Tukufu, likubali kujadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa kwa Mwaka wa Fedha 2009/2010.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Ishirini na Tatu – Tarehe 12 Julai, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Jenista J. Mhagama) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA ULINZI NA JESHI LA KUJENGA TAIFA: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ulinzi na Jeshi la Kujenga Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2011/2012. MASWALI NA MAJIBU Na. 213 Ugumu wa Kutekeleza Kazi za Kiutawala Jimbo la Kwela MHE. IGNAS A. MALOCHA aliuliza:- Jimbo la Kwela, limegawanyika katika Makao Makuu Mawili yaliyojitenga Kijiografia, yaani eneo la ukanda wa juu (Mlimani) na eneo la ukanda wa chini (Bonde la Mto Rukwa) ambapo husababisha ugumu katika kuzitekeleza kazi za kiutawala za uwakilishi hasa ikizingatiwa pia kuwa miundombinu ya barabara ni duni sana:- (a) Je, Serikali haioni kuwa inafaa kuligawa eneo hilo kulingana na Jiografia ili kupata Jimbo jingine au Wilaya? (b) Je, ni kasoro gani zilizosababisha jimbo hilo kukosa sifa za kugawanywa kupata Majimbo mawili kulingana na Jiografia jinsi ilivyo? WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, URATIBU NA BUNGE alijibu:- 1 Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ignas Aloyce Malocha, Mbunge wa Kwela, kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, Jimbo la Uchaguzi hugawanywa kwa kuzingatia Vigezo 13, kama ifuatavyo:- 1. Idadi ya watu; 2. Upatikanaji wa mawasiliano; 3. Hali ya kijiografia; 4. Mgawanyo wa wastani wa idadi ya watu; 5. Hali ya kiuchumi ya Jimbo; 6. Ukubwa wa eneo la Jimbo husika; 7.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 2 AGOSTI, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba mzime vipasa sauti vyenu maana naona vinaingiliana. Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri, tunaingia hatua inayofuata. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Leo ni siku ya Alhamisi lakini tulishatoa taarifa kwamba Waziri Mkuu yuko safarini kwa hiyo kama kawaida hatutakuwa na kipindi cha maswali hayo. Maswali ya kawaida yapo machache na atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Vita R. M. Kawawa. Na. 310 Fedha za Uendeshaji Shule za Msingi MHE. VITA R. M. KAWAWA aliuliza:- Kumekuwa na makato ya fedha za uendeshaji wa Shule za Msingi - Capitation bila taarifa hali inayofanya Walimu kuwa na hali ngumu ya uendeshaji wa shule hizo. Je, Serikali ina mipango gani ya kuhakikisha kuwa, fedha za Capitation zinatoloewa kama ilivyotarajiwa ili kupunguza matatizo wanayopata wazazi wa wanafunzi kwa kuchangia gharama za uendeshaji shule? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) imepanga kila mwanafunzi wa Shule ya Msingi kupata shilingi 10,000 kama fedha za uendeshaji wa shule (Capitation Grant) kwa mwaka.
    [Show full text]
  • Coversheet for Thesis in Sussex Research Online
    A University of Sussex DPhil thesis Available online via Sussex Research Online: http://sro.sussex.ac.uk/ This thesis is protected by copyright which belongs to the author. This thesis cannot be reproduced or quoted extensively from without first obtaining permission in writing from the Author The content must not be changed in any way or sold commercially in any format or medium without the formal permission of the Author When referring to this work, full bibliographic details including the author, title, awarding institution and date of the thesis must be given Please visit Sussex Research Online for more information and further details Accountability and Clientelism in Dominant Party Politics: The Case of a Constituency Development Fund in Tanzania Machiko Tsubura Submitted for the Degree of Doctor of Philosophy in Development Studies University of Sussex January 2014 - ii - I hereby declare that this thesis has not been and will not be submitted in whole or in part to another University for the award of any other degree. Signature: ……………………………………… - iii - UNIVERSITY OF SUSSEX MACHIKO TSUBURA DOCTOR OF PHILOSOPHY IN DEVELOPMENT STUDIES ACCOUNTABILITY AND CLIENTELISM IN DOMINANT PARTY POLITICS: THE CASE OF A CONSTITUENCY DEVELOPMENT FUND IN TANZANIA SUMMARY This thesis examines the shifting nature of accountability and clientelism in dominant party politics in Tanzania through the analysis of the introduction of a Constituency Development Fund (CDF) in 2009. A CDF is a distinctive mechanism that channels a specific portion of the government budget to the constituencies of Members of Parliament (MPs) to finance local small-scale development projects which are primarily selected by MPs.
    [Show full text]
  • Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 BUNGE LA TANZANIA
    Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE _____________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini na Tatu - Tarehe 16 Juni, 2014 (Mkutano Ulianza Saa 3.00 Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge tukae. Katibu! HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na :- MWENYEKITI WA KAMATI YA BAJETI: Taarifa ya Kamati ya Bajeti Juu ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2013 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka 2014/2015 Pamoja na Tathmini ya Utekelezaji wa Bajeti ya Serikali kwa Mwaka 2013/2014 na Mapendekezo ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. RAJAB MBAROUK MOHAMMED (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA OFISI YA RAIS, MAHUSIANO NA URATIBU): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Ofisi ya Rais (Mahusiano na Uratibu) Juu ya Hali ya Uchumi wa Taifa kwa Mwaka 2013 na Mpango wa Maendeleo wa Taifa kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MHE. CHRISTINA LISSU MUGHWAI (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA WIZARA YA FEDHA): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani wa Wizara ya Fedha juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. Na. 240 Ukosefu wa Hati Miliki MHE. NYAMBARI C. M. NYANGWINE aliuliza:- Ukosefu wa Hatimiliki za Kimila Vijijini unasababisha migogoro mingi ya ardhi baina ya Kaya, Kijiji na Koo na kupelekea kutoweka kwa amani kwa wananchi kama inavyotokea huko Tarime. 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) (a) Je, ni kwa nini Serikali haitoi
    [Show full text]
  • Tarehe 12 Aprili, 2011
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA TATU Kikao cha Tano – Tarehe 12 Aprili, 2011 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU): Taarifa ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali za Mitaa kwa Mwaka wa Fedha ulioisha tarehe 30 Juni, 2010 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Financial Statements of Local Government Authorities for the Financial Year ended 30th June, 2010). NAIBU WAZIRI WA FEDHA (MHE.GREGORY G. TEU): Taarifa ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Hesabu zilizokaguliwa za Serikali Kuu kwa Mwaka ulioishia tarehe 30 Juni, 2010 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Audit of the Financial Statement of the Central Government for the Year ended 30th June, 2010). Taarifa ya Mwaka ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Hesabu zilizokaguliwa za Mashirika ya Umma kwa Mwaka 2009/2010 (The Annual General Report of the Controller and Auditor General on the Financial Statement of Public Authorities and other Bodies for the Financial Year 2009/2010). Taarifa ya Mdhibiti na Mkaguzi Mkuu wa Hesabu za Serikali juu ya Ukaguzi wa Ufanisi na Upembuzi kwa kipindi kilichoishia tarehe 31 Machi, 2011 (The General Report of the Controller and Auditor General on the Performance and Forensic Audit Report for the Period ended 31st March, 2011).
    [Show full text]
  • Consequences for Women's Leadership
    The Politics Behind Gender Quotas: Consequences for Women’s Leadership Equity in African Legislatures by Christie Marie Arendt B.A. in Interdisciplinary Studies in Social Science, May 2004, Michigan State University M.A. in International Affairs, May 2006, The George Washington University A Dissertation submitted to The Faculty of The Columbian College of Arts and Sciences of The George Washington University in partial fulfillment of the requirements for the degree of Doctor of Philosophy January 31, 2017 Dissertation directed by Kimberly J. Morgan Professor of Political Science and International Affairs The Columbian College of Arts and Sciences of The George Washington University certifies that Christie Marie Arendt has passed the Final Examination for the degree of Doctor of Philosophy as of December 16, 2016. This is the final and approved form of the dissertation. The Politics Behind Gender Quotas: Consequences for Women’s Leadership Equity in African Legislatures Christie Marie Arendt Dissertation Research Committee: Kimberly J. Morgan, Professor of Political Science and International Affairs, Dissertation Director Jennifer Brinkerhoff, Professor of International Affairs, International Business, and Public Policy & Public Administration Eric Kramon, Assistant Professor of Political Science and International Affairs, Committee Member ii © Copyright 2017 by Christie Marie Arendt All rights reserved iii Dedication To my parents, Anne and Steve Arendt, none of this was possible without your enduring love and support. iv Acknowledgments This dissertation benefitted from the encouragement and guidance of a number of people. As an alumna of The George Washington University’s Elliott School of International Affairs, I knew that GW would provide a perfect environment to pursue my doctoral studies.
    [Show full text]