MKUTANO WA SABA Kikao Cha Ishirini Na Nne – Tarehe 13 Mei, 2
Total Page:16
File Type:pdf, Size:1020Kb
NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA SABA Kikao cha Ishirini na Nne – Tarehe 13 Mei, 2017 (Kikao Kilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae. Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. MHE. HUSSEIN M. BASHE (K.n.y. MHE. PETER J. SERUKAMBA - MWENYEKITI WA KAMATI YA HUDUMA NA MAENDELEO YA JAMII): Taarifa ya Kamati ya Huduma na Maendeleo ya Jamii kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa Fedha 2016/2017, pamoja na maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. 1 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. CECILIA D. PARESSO (K.n.y. MHE. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU WIZARA YA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA): Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kuhusu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia juu ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018. MWENYEKITI: Ahsante, Katibu. NDG. THEONEST RUHILABAKE – KATIBU MEZANI: HOJA ZA SERIKALI Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Serikali kwa Mwaka wa Fedha 2017/2018 - Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia MWENYEKITI: Mtoa Hoja. (Makofi) WAZIRI WA ELIMU, SAYANSI NA TEKNOLOJIA: Mheshimiwa Mwenyekiti, kufuatia taarifa iliyowasilishwa ndani ya Bunge lako Tukufu na Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii, naomba kutoa hoja kwamba sasa Bunge lako Tukufu lipokee na kujadili Taarifa ya Utekelezaji wa Bajeti ya Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka 2016/2017. Aidha, naliomba Bunge lako Tukufu lijadili na kupitisha Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa Mwaka 2017/2018. Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba nianze kwa kumshukuru Mwenyezi Mungu ambaye ametuwezesha sote hapa kuweza kufika siku ya leo na kuweza kushiriki katika Mkutano huu. Kwa namna ya pekee kabisa, naomba nitoe shukrani za dhati kwa Mheshimiwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Joseph Pombe Magufuli kwa kuendelea kuniamini na kunipa fursa ya kulitumikia Taifa letu na kuwatumikia Watanzania katika nafasi hii ya Waziri wa Elimu, Sayansi na Teknolojia. Naahidi kuwa nitaendelea 2 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) kutekeleza majukumu yangu kwa ufanisi wa hali ya juu na namwomba Mwenyezi Mungu aniongoze na kunisimamia katika kazi zangu. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, napenda pia kuchukua fursa hii kumpongeza Mheshimiwa Dkt. John Pombe Magufuli, Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwa uongozi wake thabiti na wenye mafanikio makubwa kwa Taifa letu. Namshukuru sana Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, mama yetu kipenzi Mheshimiwa Samia Suluhu Hassan na Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Mheshimiwa Kassim Majaliwa kwa maelekezo yao mazuri na miongozo wanayonipa katika kutekeleza kazi zangu. Aidha, nampongeza Rais na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Zanzibar, Mheshimiwa Dkt. Ali Mohamed Shein, kwa kuongoza vyema Serikali ya Mapinduzi Zanzibar. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa namna ya pekee nashukuru na kukupongeza wewe, Wenyeviti wa Bunge na Naibu Spika pamoja na Spika kwa kuliongoza Bunge letu vyema na kwa weledi wa hali ya juu. Natoa pia pongezi za dhati kwa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Huduma na Maendeleo ya Jamii chini ya Mwenyekiti wake Mheshimiwa Peter Joseph Serukamba, kwa kuichambua bajeti ya Wizara yangu na kwa ushauri ambao Kamati hii imeutoa ambao umewezesha na utaendelea kuiwezesha Wizara yangu kutekeleza majukumu yake kwa ufanisi. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa masikitiko makubwa sana, napenda kuungana na Watanzania wenzangu katika maombolezo tuliyonayo kutokana na msiba mkubwa uliolikumba Taifa letu kutokana na ajali iliyotokea Karatu tarehe 6 Mei, 2016 na kusababisha vifo vya wanafunzi 32, Walimu wawili na dereva wa Shule ya Msingi Lucky Vincent iliyopo Arusha. Msiba huu mkubwa umeacha simanzi na majonzi makubwa kwa Watanzania wote. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa mara nyingine, napenda kutoa pole kwa wazazi, walezi, ndugu, wanafunzi na uongozi wa Shule ya Lucky Vincent na wote waliopoteza 3 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wapendwa wao katika ajali hiyo mbaya iliyolikumba Taifa letu. Hakika Taifa letu limepoteza vijana ambao walikuwa wanajizatiti kielimu ili waweze kulitumikia Taifa lao kwa weledi. Tunamwomba Mwenyezi Mungu azilaze roho zao mahali pema peponi. Amina. MMheshimiwa Mwenyekiti, aidha, naomba tuendelee kuwakumbuka katika sala zetu majeruhi watatu kati ya watu 38 waliokuwa katika basi hilo ambao walisalimika katika ajali hiyo, ili Mwenyezi Mungu awape uponyaji wa haraka na hatimaye waweze kuendelea na masomo yao. Mheshimiwa Mwenyekiti, msiba huu uliwagusa pia majirani na marafiki zetu ndani na nje ya nchi. Kwa namna ya pekee kabisa, napenda kutoa shukrani za dhati kabisa kwa Rais wa Kenya, Mheshimiwa Uhuru Kenyatta ambaye alimtuma Waziri wake wa Elimu, Mheshimiwa Dkt. Fred Okengo Matiang’, kushiriki katika msiba huu. Serikali yetu ilifarijika sana kwa ushirikiano waliotuonesha katika kipindi hiki kigumu cha majonzi makubwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, nawashukuru sana pia Washirika wetu wa Maendeleo katika Sekta ya Elimu ambao wamekuwa wakitoa pole kwa barua na kwa simu kutokana na msiba uliotokea. Niseme tu kwamba msiba huu umewagusa watu wote na hivyo tunasema ahsante sana kwa watu wote ambao waliungana nasi. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, baada ya maelezo hayo ya utangulizi, naomba sasa nitoe taarifa ya utekelezaji wa kazi za Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia kwa Mwaka wa 2016/2017 na Mpango wa Bajeti ya Wizara kwa Mwaka wa 2017/2018. Nitaanza na mapitio ya utekelezaji wa Mpango wa Bajeti kwa Mwaka 2016/2017. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2016/2017, Bunge lako Tukufu liliidhinisha kiasi cha sh.1,396,929,798,625 ambapo Sh.499,272,251,000 zilikuwa ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida na sh.897,657,547,625 zilikuwa ni kwa ajili ya miradi ya maendeleo. 4 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Mwenyekiti, hadi kufikia tarehe 30 Aprili, 2017, jumla ya sh.979,785,341,945.18 zilikuwa zimetolewa ambapo sh.350,008,368,423.59 ni kwa ajili ya matumizi ya kawaida ambayo ni sawa na asilimia 70.1 ya bajeti iliyoidhinishwa na Bunge lako Tukufu. Fedha za maendeleo zilizotolewa zilikuwa ni sh.629,776,772,521.59 ambayo ni sawa na asilimia 70.2 ya bajeti ya maendeleo. Mheshimiwa Mwenyekiti, aidha, fedha zilizotumika; nazungumzia fedha ambazo zimepokelewa, fedha zilizotumika, hadi kufikia tarehe 30, Aprili, 2017 zilikuwa ni sh.924,821,633,369.42, ambayo ni sawa na asilimia 94.4 ya fedha zote zilizotolewa. Kati ya fedha hizo, sh.345,545,773,733.57 zilitumika kwa matumizi ya kawaida na sh.579,275,859,725.85 zilitumika kwa miradi ya maendeleo. Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba nijielekeze katika kazi ambazo zilitekelezwa na Wizara yangu kwa Mwaka 2016/2017. Kama tunavyofahamu, Wizara yangu ina jukumu la kusimamia na kutekeleza sera, sheria na taratibu katika Sekta ya Elimu, Sayansi na Teknolojia. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika mwaka 2016/2017, Wizara yangu imefanya uchambuzi wa mahitaji bora wa kisheria utakaowezesha kuwepo na usimamizi na uendeshaji fanisi zaidi wa elimu na mafunzo nchini. Kutokana na uchambuzi uliofanyika, imependekezwa kuwepo kwa Sheria moja Kuu ya Elimu kwa kuzingatia Sera ya Elimu na Mafunzo ya Mwaka 2014. Aidha, taasisi zilizo chini ya Wizara yangu zitaendelea na utekelezaji wa majukumu chini ya sheria zao mahususi kwa kuzingatia muktadha wa sheria kuu. Mheshimiwa Mwenyekiti, sasa naomba nizungumzie uboreshaji wa miundombinu katika taasisi za elimu. Kama tunavyofahamu, Serikali ya Awamu ya Tano imeweka kipaumbele katika kuboresha Sekta ya Elimu na imeweka kipaumbele katika kuhakikisha kwamba miundombinu katika Sekta ya Elimu inakuwa ni ambayo inavutia na inaweza ikawezesha wanafunzi kupata elimu iliyo bora. Katika mwaka 5 NAKALA YA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) 2016/2017, Wizara yangu ilifanya shughuli zifuatazo katika kuboresha miundombinu katika taasisi za elimu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, nitaanza kuelezea ukarabati wa shule kongwe. Wizara yangu imegharamia ukarabati wa shule kongwe ambazo ni pamoja na Jangwani, Azania, Kibaha, Kigoma Sekondari, Tosamaganga, Songea Wasichana, Malangali, Mirambo, Minaki, Nangwa, Mpwapwa, Musoma Ufundi, Mtwara Ufundi, Ifakara, Kantalamba, Tanga Ufundi, Ifunda Ufundi, Moshi Ufundi, Bwiru Wavulana, Iyunga, Zanaki, Kibiti, Ndanda na Tambaza. Mheshimiwa Mwenyekiti, vilevile tutakumbuka kwamba mwezi Septemba, 2016, ndugu zetu wa Mkoa wa Kagera walipatwa na tetemeko ambalo, pamoja na mambo mengine liliathiri pia miundombinu katika Sekta ya Elimu. Miundombinu ya Shule ya Sekondari ya Ihungo iliharibika kabisa kutokana na tetemeko la ardhi lililotokea Mkoani Kagera. Mheshimiwa Mwenyekiti, Serikali ya Uingereza kupitia Shirika lake la Maendeleo la Kimataifa, ilitupatia Pauni za Uingereza milioni 2.23 ambayo ni sawa na takribani shilingi bilioni sita, kwa ajili ya kujenga upya Shule ya Sekondari Ihungo ambapo ujenzi wa shule hiyo unaendelea chini ya usimamizi wa Wakala wa Majengo Tanzania na kwa sasa umefikia hatua ya upauaji. Mheshimiwa Mwenyekiti, Ukarabati wa Shule ya Msingi ya Mugeza Mseto. Sambamba na Shule ya Sekondari Ihungo, Shule ya Msingi ya Mugeza Mseto ambayo inachukua wanafunzi wenye mahitaji maalum nayo iliathirika na tetemeko katika baadhi ya majengo. Ukarabati wa shule hiyo pamoja