Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 BUNGE LA TANZANIA

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Nakala Ya Mtandao (Online Document) 1 BUNGE LA TANZANIA Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________________ MAJADILIANO YA BUNGE __________________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Tatu - Tarehe 19 Machi, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae. Katibu! MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, swali letu la kwanza ni ofisi ya Waziri Mkuu litaulizwa na Mheshimiwa Ritta Kabati. Na. 31 Hitaji la Gari la Wagonjwa Hospitali ya Wilaya ya Iringa MHE. RITTA E. KABATI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itapeleka gari la wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Iringa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ritta Enespher Kabati, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Hospitali Teule ya Wilaya ya Iringa (Tosamaganga) haina gari madhubuti la kuhudumia wagonjwa kutokana na uchakavu wa gari lililopo, hali inayosababisha gari hilo kuharibika mara kwa mara na kushindwa kutengenezeka. Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuimarisha huduma za Rufaa katika hospitali hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imepanga kutumia shilingi milioni 150 kutokana na Bajeti ya Mapato ya Ndani ya Halmashauri, kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016 kwa ajili ya ununuzi wa gari la kubebea wagonjwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana na kadhia hii ya utoaji wa huduma za rufaa kwa hospitali hii ya ngazi ya Wilaya, Halmashauri imekuwa ikitumia magari ya Vituo vya Afya vya Idodi, Isimani, Kimande, Kiponzelo, Nzii na Wapaaga ambavyo kwa sasa vituo hivi ndivyo vinavyohudumiwa na hospitali hii. Vituo hivyo vya Afya vina magari ya wagonjwa ambayo yanatumika kutoa huduma ya za rufaa katika ngazi za Wilaya, Mkoa na hadi ngazi ya Taifa pale inapohitajika. 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niulize maswali, ninayo maswali mawili tu madogo ya nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake na kwa kweli naomba tu nimfagilie kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiifanya hasa katika Mkoa wetu wa Iringa. Ninaomba kumwuliza kwamba ni vigezo gani hasa huwa vinatumika katika kutoa haya magari ya wagonjwa katika Wilaya zetu, kwa sababu Wilaya zetu zote za Mkoa mfano, Wilaya ya Kilolo, Wilaya ya Mufindi, Wilaya ya Iringa na hiyo ya Manispaa hakuna magari ya wagonjwa na hata hospitali yetu hiyo kubwa ya Mkoa magari yake ni chakavu sana. Vilevile kumekuwa na matukio mbalimbali ya ajali ambayo yamekuwa yakitokea. Hata juzi ajali imeua watu hamsini (50), majanga ya moto na kuna Mlima pale Kitonga. Swali la Pili nimwulize kwamba, kumekuwa na ongezeko kubwa sana kwenye Manispaa yetu ya Iringa katika Jimbo la Iringa Mjini. Lakini ile hospitali bila wewe isingefunguliwa. Ulikuja na ukaenda tukaifungua, lakini hakuna gari la wagonjwa na hospitali ile kuna wazazi ambao wamekuwa wakichukuliwa kwenye magari ambayo siyo special kwa ajili ya kuwapeleka kwenye hospitali ya Mkoa. Tayari walikuwa wameshaleta maombi maalum mara tano ya kupatiwa gari la wagonjwa. Je, ni utaratibu gani sasa unatumika kushughulikia haya Maombi Maalum? Aidha nikuombe kwa kweli kwa sababu kwenda Iringa hapo ni masaa mawili tu ikiwezekana tungeenda ukajionee wewe mwenyewe. Ahsante sana. MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, jibu sahihi ni muende wote kipindi hiki hiki. (Makofi/Kicheko) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kwa niaba ya Serikali na kwa niaba ya ofisi ya Waziri Mkuu naomba kumshukuru sana katika mazingira ya leo Mbunge kusimama hapa na kufurahi na kusema kwamba kazi inayofanyika ni nzuri. Ni jambo ambalo linatia moyo na ninashukuru sana. Equally, niseme pia kwa sababu amesema nilikwenda katika hii hospitali wanafahamu na Mheshimiwa Mchungaji Msigwa wanafahamu nilifika pale. Jitihada kubwa sana Mbunge huyu amesimama imara sana katika kuhakikisha kwamba hospitali ile inafunguliwa. Kwa hiyo, mimi napenda nimpongeze kwa kazi nzuri anazofanya katika hospitali hii. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vigezo ambavyo anavizungumzia Mheshimiwa Ritta najua kwamba ni kwanini anauliza swali hili. Swali linaulizwa kwa sababu kuna wakati fulani UNDP ilitusaidia kupata magari na kuna wakati fulani United Nations High Commissioner for Refugees naye aliwahi kusaidia. Baadaye sasa kwa vile hawa wote sasa hawatoi haya magari unaona swali kama hili linakuja hapa kwa sababu programu hizo hatunazo sasa hivi. Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachofanya hapa ni kwamba hawa wote unaosikia kwamba wana magari ni kwamba wanai-factor katika Bajeti yao. Yaani wanaangalia katika own source, wanaangalia katika mipango yao kuna hela zile wakati ule wa Local Government Capital Development Grant wanaingiza mle ndani. Kwa hiyo, wanapeleka kule. 2 Nakala ya Mtandao (Online Document) Lakini inapotokea kwamba kuna mahali ambapo tumepata magari haya tunaangalia sana maeneo yaliyopo pembezoni, wenzetu waliopo katika maeneo ya maziwa, waliopo katika maeneo ambayo kwa kweli unajua kabisa usipopeleka gari la wagonjwa kule au usipopeleka boti kule akina mama kule watakufa tu. Kwa hiyo, ndivyo vitu tunavyoviangalia. Tunaangalia hali halisi iliyopo katika hospitali ile kama ilivyoelezwa hapa, tukiona kabisa hapa pana tatizo tutapoteza maisha ya mama na mtoto au na watu wengine na wananchi waliopo kule tunafanya hivyo, ndicho tunachokiangalia. Kwa sasa hivi tunachofanya ni hicho. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, amezungumza habari ya kitu kinachoitwa Maombi Maalum. Hawa Wabunge wenzangu wote mmesikia maelekezo ya Serikali ni kwamba Maombi Maalum hatuna huo utaratibu tena, kitu ambacho mtu anaweza akafanya ni kuandika andiko, andiko likatafutiwa Development Partners wakatusaidia katika jambo hilo. Lakini kwamba kuna maombi maalum, mimi nimekuwa nasoma kidogo wakati tunapokutana katika Kamati tumeona kitu cha namna hiyo. Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ongezeko la Manispaa katika hii hospitali ya Iringa kama alivyosema, ambacho tunaweza tukafanya hapa kwa sababu sasa hivi ndiyo tunaandaa Bajeti, tutahakikisha kwamba tunazungumza na wenzetu wa Iringa ili tuhakikishe kwamba hii wanaiingiza kwa sababu kweli pale pana problem kubwa, pale pana magari mengine Hyundai zimechoka choka hazifanyi kazi tutasaidia kuona kwamba wanaingiza katika Bajeti zao kwa sababu sasa hivi ndiyo shughuli inayofanyika. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa kwa kifupi. MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri, mimi ndiye Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini na ninayajua mazingira ya Jimbo vizuri zaidi, niseme tu Mheshimiwa Waziri unapojibu maswali hunitendei haki, kwa sababu hospitali ile ya Iringa Mjini haikuanza kabla sijatoa vitanda na magodoro katika hospitali ile. Kwa hiyo, kumwagia sifa Mbunge wa Viti Maalum, kwamba yeye ndiyo amefanya juhudi kubwa si haki. Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu ni juhudi gani za makusudi baada ya Manispaa ya Iringa Mjini, kufanya juhudi kubwa kuijenga ile Hospitali na mimi kama Mbunge nilisaidia kuanzisha ile Hospitali ianze na juzi Waziri Mkuu alipokuja alinimwagia sifa na wewe ulizisikia, Serikali itatusaidiaje ili tupate hilo gari la wagonjwa tuendelee kufanya kazi vizuri? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali nililokuwa ninajibu hapa lilikuwa ni swali la Mheshimiwa Ritta Kabati, ndiye aliyeuliza swali. Mimi Mheshimiwa Msigwa hakuuliza au maswali haya hayakuulizwa jointly, kwa hiyo niwajibie wote. Mimi ninachosema nilikuwa najibu kuhusu Mheshimiwa Ritta Kabati, kwa sababu ndiye swali lililoletwa hapa. Mimi nataka niseme kitu kimoja hapa na wala mimi sitaki kuingia katika conflicts hizi kwamba Mheshimiwa Msigwa amefanyakazi amepeleka vitanda pale niliona kwa macho yangu. Lakini wananchi wanachohitaji hapa siyo kwamba ni nani ameleta hapa, tunahitaji concertedefforts, tunataka watu wote waliopo kule Mwenyekiti wa Halmashauri atusaidie, Mbunge wa Viti Maalum atusaidie, Mbunge mwenyewe wa Jimbo atusaidie, tunataka Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya watusaidie na tunataka sisi Wabunge wote tusaidiane hapa. Kwa 3 Nakala ya Mtandao (Online Document) hiyo ni kweli kwamba pale wananchi wenyewe wamefanyakazi kubwa kwa kushirikiana na viongozi wao na hiyo ndiyo credit ambayo ninaileta kwako. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa vile ameuliza mimi najua kwamba tulipokuja pale katika ile hospitali ilikuwepo na vitanda vililetwa pale, lakini equally ni kweli pia Mheshimiwa Ritta Kabati na yeye amechangia sana kama Mbunge wa Viti Maalum katika hilo eneo na wewe umechangia sana katika hilo eneo, wote mmechangia sasa ninafanya makosa gani? MWENYEKITI: Ahsante sana, tunaendelea Waheshimwia Wabunge leo tuna miswada miwili na yote hiyo inatakiwa iishe. Kwa hiyo, muda wetu ni mdogo sana. Mheshimiwa Mkosamali. Na. 32 Changamoto Zilizojitokeza Kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa MHE. FELIX F. MKOSAMALI aliuliza:- Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 umekuwa na changamoto nyingi sana:- (a) Je, ni kesi ngapi zimefunguliwa Mahakamani kutokana na uchaguzi huo kwa nchi nzima na zitaisha lini ikiwa zipo kesi za mwaka 2009 zimeisha mwaka 2014? (b) Je, ni kwa nini wananchi wa Kitongoji cha Nduta wamezuiwa kupiga kura? (c) Je, ni lini Serikali italeta Muswada wa Sheria ili Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usimamiwe na Tume huru ya Uchaguzi? MWENYEKITI: Mheshimiwa Jenista nani anajibu hilo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
Recommended publications
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who Will Benefit from the Gas Economy, If It Happens?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013 Who will benefit from the gas economy, if it happens? Supported by: 2 TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? ACKNOWLEDGEMENTS Policy Forum would like to thank the Foundation for Civil Society for the generous grant that financed Tanzania Governance Review 2013. The review was drafted by Tanzania Development Research Group and edited by Policy Forum. The cartoons were drawn by Adam Lutta (Adamu). Tanzania Governance Reviews for 2006-7, 2008-9, 2010-11, 2012 and 2013 can be downloaded from the Policy Forum website. The views expressed and conclusions drawn on the basis of data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. TGRs review published and unpublished materials from official sources, civil society and academia, and from the media. Policy Forum has made every effort to verify the accuracy of the information contained in TGR2013, particularly with media sources. However, Policy Forum cannot guarantee the accuracy of all reported claims, statements, and statistics. Whereas any part of this review can be reproduced provided it is duly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. ISBN:978-9987-708-19-2 For more information and to order copies of the report please contact: Policy Forum P.O. Box 38486 Dar es Salaam Tel +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] Suggested citation: Policy Forum 2015.
    [Show full text]
  • Tanzanian State
    THE PRICE WE PAY TARGETED FOR DISSENT BY THE TANZANIAN STATE Amnesty International is a global movement of more than 7 million people who campaign for a world where human rights are enjoyed by all. Our vision is for every person to enjoy all the rights enshrined in the Universal Declaration of Human Rights and other international human rights standards. We are independent of any government, political ideology, economic interest or religion and are funded mainly by our membership and public donations. © Amnesty International 2019 Except where otherwise noted, content in this document is licensed under a Creative Commons Cover photo: © Amnesty International (Illustration: Victor Ndula) (attribution, non-commercial, no derivatives, international 4.0) licence. https://creativecommons.org/licenses/by-nc-nd/4.0/legalcode For more information please visit the permissions page on our website: www.amnesty.org Where material is attributed to a copyright owner other than Amnesty International this material is not subject to the Creative Commons licence. First published in 2019 by Amnesty International Ltd Peter Benenson House, 1 Easton Street London WC1X 0DW, UK Index: AFR 56/0301/2019 Original language: English amnesty.org CONTENTS EXECUTIVE SUMMARY 6 METHODOLOGY 8 1. BACKGROUND 9 2. REPRESSION OF FREEDOM OF EXPRESSION AND INFORMATION 11 2.1 REPRESSIVE MEDIA LAW 11 2.2 FAILURE TO IMPLEMENT EAST AFRICAN COURT OF JUSTICE RULINGS 17 2.3 CURBING ONLINE EXPRESSION, CRIMINALIZATION AND ARBITRARY REGULATION 18 2.3.1 ENFORCEMENT OF THE CYBERCRIMES ACT 20 2.3.2 REGULATING BLOGGING 21 2.3.3 CYBERCAFÉ SURVEILLANCE 22 3. EXCESSIVE INTERFERENCE WITH FACT-CHECKING OFFICIAL STATISTICS 25 4.
    [Show full text]
  • Consequences for Women's Leadership
    The Politics Behind Gender Quotas: Consequences for Women’s Leadership Equity in African Legislatures by Christie Marie Arendt B.A. in Interdisciplinary Studies in Social Science, May 2004, Michigan State University M.A. in International Affairs, May 2006, The George Washington University A Dissertation submitted to The Faculty of The Columbian College of Arts and Sciences of The George Washington University in partial fulfillment of the requirements for the degree of Doctor of Philosophy January 31, 2017 Dissertation directed by Kimberly J. Morgan Professor of Political Science and International Affairs The Columbian College of Arts and Sciences of The George Washington University certifies that Christie Marie Arendt has passed the Final Examination for the degree of Doctor of Philosophy as of December 16, 2016. This is the final and approved form of the dissertation. The Politics Behind Gender Quotas: Consequences for Women’s Leadership Equity in African Legislatures Christie Marie Arendt Dissertation Research Committee: Kimberly J. Morgan, Professor of Political Science and International Affairs, Dissertation Director Jennifer Brinkerhoff, Professor of International Affairs, International Business, and Public Policy & Public Administration Eric Kramon, Assistant Professor of Political Science and International Affairs, Committee Member ii © Copyright 2017 by Christie Marie Arendt All rights reserved iii Dedication To my parents, Anne and Steve Arendt, none of this was possible without your enduring love and support. iv Acknowledgments This dissertation benefitted from the encouragement and guidance of a number of people. As an alumna of The George Washington University’s Elliott School of International Affairs, I knew that GW would provide a perfect environment to pursue my doctoral studies.
    [Show full text]
  • Tarehe 7 Februari, 2017
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA SITA Kikao cha Saba – Tarehe 7 Februari, 2017 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Tukae. Katibu. NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na: MHE. PROF. NORMAN A. S. KING – MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA MIUNDOMBINU: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Miundombinu kwa kipindi cha kuanzia Januari, 2016 hadi Januari, 2017. MHE. DOTO M. BITEKO -MWENYEKITI WA KAMATI YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Nishati na Madini kwa kipindi cha kuanzia Januari 2016 hadi Januari 2017. NAIBU SPIKA: Ahsante. Katibu! NDG. RAMADHAN ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tunaendelea na maswali, Ofisi ya Rais - TAMISEMI. Mheshimiwa Najma Murtaza Giga, Mbunge wa Viti Maalum, sasa aulize swali lake. Na. 69 Tatizo la Ulevi MHE. NAJMA MURTAZA GIGA aliuliza:- 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) Ulevi wa kupita kiasi hasa wa pombe za kienyeji umekuwa na athari kubwa za kiafya na kiakili kwa Watanzania wenye tabia ya ulevi wa kukithiri:- Je, Serikali imejipanga vipi kukabiliana na tatizo hilo hasa ikizingatiwa kuwa Sheria ya Vileo ya mwaka 1969 ni ya zamani sana kiasi kwamba inawezekana kabisa haikidhi mabadiliko ya hali halisi ya vileo kwa wakati huu. NAIBUWAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, TAMISEMI, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Najma Murtaza Giga, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, pombe za kienyeji zimeainishwa katika Kifungu cha pili (2) cha tafsiri katika Sheria ya Vileo, Sura ya 77.
    [Show full text]
  • Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ____________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Tatu – Tarehe 8 Mei, 2014 (Mkutano Ulianza Saa tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Job J. Ndugai) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA RAIS MENEJIMENTI YA UTUMISHI WA UMMA, UTAWALA BORA NA MAHUSIANO NA UTARATIBU: Randama za Makadirio ya Matumizi ya Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma, Utawala Bora na Mahusiano na Uratibu kwa Mwaka wa Fedha 2014/2015. MASWALI NA MAJIBU Na. 20 Kuhamisha Soko la Mwika MHE. DKT. AUGUTINE L. MREMA aliuliza:- Soko la Mwika liko barabarani na kuna hatari ya wananchi kugongwa na magari:- Je, Serikali ina mpango gani wa kutafuta eneo kubwa na kuhamisha soko hilo ili kukwepa athari hizi? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Dkt. Augustino Lyatonga Mrema Mbunge wa Vunjo kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, Soko la Mwika liko katika Halmashauri ya Wilaya ya Moshi karibu na barabara. Soko hili lina ukubwa wa ekari 2.5 na idadi ya wafanyabiashara wanaotumia soko hili ni kati ya 1,000 hadi 1,500. Kimsingi kuna ongezeko kubwa la wafanyabiashara kufuatia mahitaji ya walaji ambao wanajumuisha wananchi wa Kata ya Mwika Kaskazini na Mwika Kusini. Kwa kutambua changamoto ya soko hili kuwa karibu na barabara, Halmashauri inaandaa mpango wa kuboresha soko hilo ili liwe la kisasa na kuondoa athari za ajali katika eneo hilo.
    [Show full text]
  • Can President Samia Find a Way to Fulfilling Her Reform Ambitions?
    President Samia, Team JK and Magufuli Camp! By Gado Published by the good folks at The Elephant. The Elephant is a platform for engaging citizens to reflect, re-member and re-envision their society by interrogating the past, the present, to fashion a future. Follow us on Twitter. President Samia, Team JK and Magufuli Camp! By Gado When Samia Suluhu Hassan, the first female president of Tanzania, took office in March following the sudden death of the incumbent, John Pombe Magufuli, a sense of contagious optimism gripped the nation. Viewed by many as “calm, gentle and attentive”, she appeared to embody the possibility of a new beginning after five years of her predecessor’s autocratic and ruthless reign. However, the July arrest and detention of a leading opposition figure, Freeman Mbowe, on what many activists reject as spurious terrorism charges, has shown that the new president has not been able to devise a different way of dealing with the political constraints that besieged her predecessor, and that she is, ironically (given her supposed demeanour), incapable of tolerating political skirmish. The indefinite detention (terrorism charges aren’t bailable in Tanzania) of Mr Mbowe, a principled and unswerving chairperson of the Party of Democracy and Development (CHADEMA), coincided with growing agitation for a new constitution and an independent electoral commission. For the opposition, especially CHADEMA, and everyone else that believes the last five years (2015–2020) were a dark chapter in the country’s history of progressive governance, the death of President Magufuli needs to be seen as a historic window of opportunity, a once-in-a-lifetime trigger for enacting fundamental legal and governance reforms, with the intention of preventing a recurrence of the excesses witnessed under the previous regime.
    [Show full text]
  • Die Repression in Tansania Nimmt Zu
    LÄNDERBERICHT www.kas.de Konrad-Adenauer-Stiftung e.V TANSANIA STEFAN REITH Die Repression in Tansania nimmt September 2012 zu – Opposition, Medien und www.kas.de/tansania Menschenrechtsgruppen in gro- ßer Sorge Am 3. September publizierte die größte einer zunehmenden Repression und Eskala- tansanische Tageszeitung Mwananchi auf tion staatlicher Gewalt gegen die politische ihrer Titelseite ein schockierendes Foto. Opposition und regierungskritische Zivilge- Es zeigte die Erschießung des als regie- sellschaft. rungskritisch bekannten Journalisten Daudi Mwangosi durch die tansanische Insbesondere die größte tansanische Oppo- Polizei am Vortag. Auf internationaler sitionspartei CHADEMA (Chama cha De- Ebene sorgte der Vorfall für Sorge und Er- mokrasia na Maendeleo, Partei für Demo- staunen, gilt Tansania doch im Vergleich kratie und Fortschritt) ist seit ihrem starken zu seinen afrikanischen Nachbarn als ein Zuwachs bei den letzten Wahlen im Oktober weitgehend stabiles und friedliches Land. 20101 immer wieder Ziel von repressiven Maßnahmen und unverhältnismäßiger Ge- Daudi Mwangosi, Reporter des nationalen walt der tansanischen Polizei- und Sicher- Fernsehsenders Channel Ten, hatte in ei- heitsbehörden. Wiederholt waren dabei nem Dorf der zentraltansanischen Region zahlreiche Verletzte und vereinzelte Todes- Iringa das brutale Vorgehen der Polizei ge- opfer zu beklagen. gen die Anhänger der größten tansanischen Oppositionspartei CHADEMA dokumentiert Staatliche Gewalt gegen Opposition und war einem durch die Polizei bedrohten nimmt zu Kollegen zur Hilfe geeilt. Übereinstimmen- den Augenzeugenberichten zufolge wurde Bereits im Januar 2011 schlug die Polizei Mwangosi daraufhin von mehreren Polizis- eine Massendemonstration gegen die ge- ten brutal zusammengeschlagen, zu Boden fälschte Bürgermeisterwahl in Arusha, dem gedrückt und durch den Schuss einer Trä- Zentrum des Nordens in der Nähe des Kili- nengaskartusche in den Unterleib getötet.
    [Show full text]
  • 19 Desemba, 2013
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA __________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA KUMI NA NNE Kikao cha Kumi na Tatu - Tarehe 19 Desemba, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA ARDHI, NYUMBA NA MAENDELEO YA MAKAZI:- Taarifa ya Mwaka na Hesabu Zilizokaguliwa za Shirika la Nyumba la Taifa (NHC) kwa Mwaka ulioishia Tarehe 30 Juni, 2012 (The Annual Report and Audited Accounts of the National Housing Corporation (NHC) for The Year ended 30th June, 2012). 1 Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) WAZIRI WA KAZI NA AJIRA:- Taarifa ya Mwaka ya Mamlaka ya Usimamizi na Udhibiti wa Hifadhi ya Jamii (SSRA) kwa Mwaka 2011/2012 (The Annual Report of Social Security Regulatory Authority (SSRA) for the Year 2011/2012). MASWALI KWA WAZIRI MKUU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge leo ni siku ya Alhamisi, tunakuwa na Maswali kwa Waziri Mkuu. Kawaida yetu kama Kiongozi wa Upinzani yupo basi ndiye anayeanza. Naona sijamwona. Kwa hiyo, nitaanza na Mheshimiwa Murtaza Mangungu. Mheshimiwa Murtaza Mangungu. MHE. MURTAZA A. MANGUNGU: Nakushukuru sana Mheshimiwa Spika. Mheshimiwa Waziri Mkuu, kwa kipindi cha miaka ya 1970 kuja 1980 Serikali ilifanya jitihada kubwa sana kupanua elimu ya juu nchini. Lakini kutokana na matatizo ambayo hayajaelezeka kipindi kirefu hatujawekeza vya kutosha hivyo kuna upungufu mkubwa sana wa Wahadhiri katika Vyuo Vikuu hasa ukizingatia Sheria yetu ya ajira inatoa ukomo wa kustaafu siyo zaidi ya miaka 65 na maprofesa wote ambao ni full Professor wamezidi umri wa miaka 65.
    [Show full text]
  • Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA PILI Kikao cha Kwanza – Tarehe 26 Januari, 2016 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) WIMBO WA TAIFA (Hapa Wimbo wa Taifa Uliimbwa) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, tukae. Waheshimiwa Wabunge, Kikao cha Kwanza cha Mkutano wetu wa Pili ni leo, tunaendelea na utaratibu, sasa ninamwomba Katibu atuongoze. DKT. THOMAS D. KASHILILAH - KATIBU WA BUNGE: Kiapo cha Uaminifu. KIAPO CHA UAMINIFU Waheshimiwa Wabunge wafuatao waliapa kiapo cha uaminifu:- Mhe. Dkt. Abdallah Saleh Possi Mhe. Deogratias Francis Ngalawa Mhe. Godbless Jonathan Lema Mhe. Goodluck Asaph Mlinga Mhe. Prof. Makame Mnyaa Mbarawa Mhe. Omari Abdallah Kigoda Mhe. Dkt. Philip Isdor Mpango Mhe. Rashid Mohamed Chuachua Mhe. Shabani Omari Shekilindi SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba nichukue nafasi hii kwa niaba ya Wabunge wote kuwapongeza Wabunge wapya ambao tumewaapisha katika siku hii ya leo, hongereni sana na karibuni mjengoni. Katibu! DKT. THOMAS D. KASHILILAH - KATIBU WA BUNGE: Hati za Kuwasilisha Mezani. HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa mezani na:- Nakala ya Mtandao (Online Document) WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, VIJANA, AJIRA NA WALEMAVU: Taarifa ya Matoleo ya Gazeti la Serikali pamoja na Nyongeza zake zilizochapishwa tangu tarehe 4 Novemba, 2015 kama ifuatavyo:- (i) Toleo Na. 06 la Tarehe 06 Novemba, 2015; (ii) Toleo Na. 13 la Tarehe 13 Novemba, 2015; (iii) Toleo Na. 47 la Tarehe 20 Novemba, 2015; (iv) Toleo Na. 08 la Tarehe 27 Novemba, 2015; (v) Toleo Na. 46 la Tarehe 04 Desemba, 2015; (vi) Toleo Na.
    [Show full text]
  • Tanzania 2020 Human Rights Report
    TANZANIA 2020 HUMAN RIGHTS REPORT EXECUTIVE SUMMARY The United Republic of Tanzania is a multiparty republic consisting of the mainland region and the semiautonomous Zanzibar archipelago, whose main islands are Unguja (Zanzibar Island) and Pemba. The union is headed by a president, who is also the head of government. Its unicameral legislative body is the National Assembly (parliament). Zanzibar, although part of the union, exercises considerable autonomy and has its own government with a president, court system, and legislature. On October 28, the country held its sixth multiparty general election, resulting in the reelection of the union president, John Magufuli, with 85 percent of the vote, and the election of Dr. Hussein Mwinyi with 76 percent of the vote for his first term as president of Zanzibar. International and local election observers and civil society noted widespread election irregularities in the pre-election period, on election day, and in the postelection period which affected the credibility of the electoral process. Prior to the election, opposition candidates were routinely disqualified, harassed, and arrested. There were reports of significant and widespread voting irregularities, internet disruptions, intimidation of journalists, arrests, and violence by security forces both in mainland Tanzania and on Zanzibar resulting in an election that was neither free nor fair. Under the union’s Ministry of Home Affairs, the Tanzanian Police Force has primary responsibility for maintaining law and order. The Field Force Unit, a special police division, has primary responsibility for controlling unlawful demonstrations and riots. The Tanzania People’s Defense Forces include the army, navy, air force, and National Services.
    [Show full text]
  • Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Tisa – Tarehe 7 Februari, 2020 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SIKA: Waheshimiwa tukae. Katibu. NDG. JOSHUA CHAMWELA - KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati zifuatazo ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO: Maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Azimio la Kufuta Hasara itokanayo na Maduhuli ya Madeni ya Nyuma ya Ada na Leseni za Magari, Riba na Adhabu kwa Kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni, 2019. Muhtasari wa Tamko la Sera ya Fedha (Mapitio ya Nusu Mwaka 2019/2020) [Monetary Policy Statement (The Mid-Year Review 2019/2020)]. MHE. STANSLAUS S. MABULA - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA HESABU ZA SERIKALI: Maoni ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Hesabu za Serikali kuhusu Azimio la Kufuta Hasara itokanayo na maduhuli ya madeni ya nyuma ya ada na leseni za magari, riba na adhabu kwa kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni, 2019. MHE. IMMACULATE S. SEMESI - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI KWA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO: Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni kuhusu Azimio la Kufuta Hasara itokanayo na maduhuli ya madeni ya nyuma ya ada na leseni za magari, riba na adhabu kwa kipindi kinachoishia tarehe 30 Juni, 2019. WAZIRI WA KATIBA NA SHERIA: Maelezo ya Waziri wa Katiba na Sheria kuhusu Muswada wa Sheria ya Usuluhishi wa Mwaka 2020 (The Arbitration Bill, 2020).
    [Show full text]
  • 19 Aprili, 2013
    19 APRILI, 2013 BUNGE LA TANZANIA ________________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________________ MKUTANO WA KUMI NA MOJA Kikao cha Tisa - Tarehe 19 Aprili, 2013 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA KILIMO, CHAKULA NA USHIRIKA: Randama za Makadirio ya Matumizi ya Wizara ya Kilimo, Chakula na Ushirika kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. WAZIRI WA NCHI, OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MAZINGIRA NA MUUNGANO: Hotuba ya Bajeti ya Waziri wa Nchi,Ofisi ya Makamu, Mazingira na Muungano, kwa mwaka wa fedha 2013/2014. 1 19 APRILI, 2013 MHE. FAKHARIA KHAMIS SHOMARI (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KATIBA, SHERIA NA UTAWALA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Katiba, Sheria na Utawala Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano, kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MHE. ESTER A. BULAYA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA ARDHI, MALIASILI NA MAZINGIRA): Taarifa ya Mwenyekiti wa Kamati ya Ardhi, Maliasili na Mazingira Kuhusu Utekelezaji wa Majukumu ya Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira, kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MHE.PAULINE P. GEKUL (K.n.y.MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI KWA OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MUUNGANO: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Ofisi ya Makamu wa Rais, Muungano Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014. MHE. CECILIA D. PARESSO (K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI YA UPINZANI WA OFISI YA MAKAMU WA RAIS, MAZINGIRA: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi ya Upinzani kwa Ofisi ya Makamu wa Rais, Mazingira Kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2013/2014.
    [Show full text]