Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________________ MAJADILIANO YA BUNGE __________________ MKUTANO WA KUMI NA TISA Kikao cha Tatu - Tarehe 19 Machi, 2015 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge tukae. Katibu! MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa Wabunge, swali letu la kwanza ni ofisi ya Waziri Mkuu litaulizwa na Mheshimiwa Ritta Kabati. Na. 31 Hitaji la Gari la Wagonjwa Hospitali ya Wilaya ya Iringa MHE. RITTA E. KABATI aliuliza:- Je, ni lini Serikali itapeleka gari la wagonjwa katika hospitali ya Wilaya ya Iringa? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI) alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Ritta Enespher Kabati, Mbunge wa Viti Maalum, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Mwenyekiti, ni kweli Hospitali Teule ya Wilaya ya Iringa (Tosamaganga) haina gari madhubuti la kuhudumia wagonjwa kutokana na uchakavu wa gari lililopo, hali inayosababisha gari hilo kuharibika mara kwa mara na kushindwa kutengenezeka. Mheshimiwa Mwenyekiti, ili kuimarisha huduma za Rufaa katika hospitali hiyo Halmashauri ya Wilaya ya Iringa imepanga kutumia shilingi milioni 150 kutokana na Bajeti ya Mapato ya Ndani ya Halmashauri, kwa mwaka wa fedha wa 2015/2016 kwa ajili ya ununuzi wa gari la kubebea wagonjwa. Mheshimiwa Mwenyekiti, katika kukabiliana na kadhia hii ya utoaji wa huduma za rufaa kwa hospitali hii ya ngazi ya Wilaya, Halmashauri imekuwa ikitumia magari ya Vituo vya Afya vya Idodi, Isimani, Kimande, Kiponzelo, Nzii na Wapaaga ambavyo kwa sasa vituo hivi ndivyo vinavyohudumiwa na hospitali hii. Vituo hivyo vya Afya vina magari ya wagonjwa ambayo yanatumika kutoa huduma ya za rufaa katika ngazi za Wilaya, Mkoa na hadi ngazi ya Taifa pale inapohitajika. 1 Nakala ya Mtandao (Online Document) MHE. RITTA E. KABATI: Mheshimiwa Mwenyekiti, ahsante kwa kunipa nafasi niulize maswali, ninayo maswali mawili tu madogo ya nyongeza. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kabisa nimshukuru Mheshimiwa Waziri kwa majibu yake na kwa kweli naomba tu nimfagilie kwa kazi nzuri ambayo amekuwa akiifanya hasa katika Mkoa wetu wa Iringa. Ninaomba kumwuliza kwamba ni vigezo gani hasa huwa vinatumika katika kutoa haya magari ya wagonjwa katika Wilaya zetu, kwa sababu Wilaya zetu zote za Mkoa mfano, Wilaya ya Kilolo, Wilaya ya Mufindi, Wilaya ya Iringa na hiyo ya Manispaa hakuna magari ya wagonjwa na hata hospitali yetu hiyo kubwa ya Mkoa magari yake ni chakavu sana. Vilevile kumekuwa na matukio mbalimbali ya ajali ambayo yamekuwa yakitokea. Hata juzi ajali imeua watu hamsini (50), majanga ya moto na kuna Mlima pale Kitonga. Swali la Pili nimwulize kwamba, kumekuwa na ongezeko kubwa sana kwenye Manispaa yetu ya Iringa katika Jimbo la Iringa Mjini. Lakini ile hospitali bila wewe isingefunguliwa. Ulikuja na ukaenda tukaifungua, lakini hakuna gari la wagonjwa na hospitali ile kuna wazazi ambao wamekuwa wakichukuliwa kwenye magari ambayo siyo special kwa ajili ya kuwapeleka kwenye hospitali ya Mkoa. Tayari walikuwa wameshaleta maombi maalum mara tano ya kupatiwa gari la wagonjwa. Je, ni utaratibu gani sasa unatumika kushughulikia haya Maombi Maalum? Aidha nikuombe kwa kweli kwa sababu kwenda Iringa hapo ni masaa mawili tu ikiwezekana tungeenda ukajionee wewe mwenyewe. Ahsante sana. MWENYEKITI: Mheshimiwa Waziri, jibu sahihi ni muende wote kipindi hiki hiki. (Makofi/Kicheko) NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, kwanza kwa niaba ya Serikali na kwa niaba ya ofisi ya Waziri Mkuu naomba kumshukuru sana katika mazingira ya leo Mbunge kusimama hapa na kufurahi na kusema kwamba kazi inayofanyika ni nzuri. Ni jambo ambalo linatia moyo na ninashukuru sana. Equally, niseme pia kwa sababu amesema nilikwenda katika hii hospitali wanafahamu na Mheshimiwa Mchungaji Msigwa wanafahamu nilifika pale. Jitihada kubwa sana Mbunge huyu amesimama imara sana katika kuhakikisha kwamba hospitali ile inafunguliwa. Kwa hiyo, mimi napenda nimpongeze kwa kazi nzuri anazofanya katika hospitali hii. Mheshimiwa Mwenyekiti, kuhusu vigezo ambavyo anavizungumzia Mheshimiwa Ritta najua kwamba ni kwanini anauliza swali hili. Swali linaulizwa kwa sababu kuna wakati fulani UNDP ilitusaidia kupata magari na kuna wakati fulani United Nations High Commissioner for Refugees naye aliwahi kusaidia. Baadaye sasa kwa vile hawa wote sasa hawatoi haya magari unaona swali kama hili linakuja hapa kwa sababu programu hizo hatunazo sasa hivi. Mheshimiwa Mwenyekiti, tunachofanya hapa ni kwamba hawa wote unaosikia kwamba wana magari ni kwamba wanai-factor katika Bajeti yao. Yaani wanaangalia katika own source, wanaangalia katika mipango yao kuna hela zile wakati ule wa Local Government Capital Development Grant wanaingiza mle ndani. Kwa hiyo, wanapeleka kule. 2 Nakala ya Mtandao (Online Document) Lakini inapotokea kwamba kuna mahali ambapo tumepata magari haya tunaangalia sana maeneo yaliyopo pembezoni, wenzetu waliopo katika maeneo ya maziwa, waliopo katika maeneo ambayo kwa kweli unajua kabisa usipopeleka gari la wagonjwa kule au usipopeleka boti kule akina mama kule watakufa tu. Kwa hiyo, ndivyo vitu tunavyoviangalia. Tunaangalia hali halisi iliyopo katika hospitali ile kama ilivyoelezwa hapa, tukiona kabisa hapa pana tatizo tutapoteza maisha ya mama na mtoto au na watu wengine na wananchi waliopo kule tunafanya hivyo, ndicho tunachokiangalia. Kwa sasa hivi tunachofanya ni hicho. (Makofi) Mheshimiwa Mwenyekiti, amezungumza habari ya kitu kinachoitwa Maombi Maalum. Hawa Wabunge wenzangu wote mmesikia maelekezo ya Serikali ni kwamba Maombi Maalum hatuna huo utaratibu tena, kitu ambacho mtu anaweza akafanya ni kuandika andiko, andiko likatafutiwa Development Partners wakatusaidia katika jambo hilo. Lakini kwamba kuna maombi maalum, mimi nimekuwa nasoma kidogo wakati tunapokutana katika Kamati tumeona kitu cha namna hiyo. Mheshimiwa Mwenyekiti, hili ongezeko la Manispaa katika hii hospitali ya Iringa kama alivyosema, ambacho tunaweza tukafanya hapa kwa sababu sasa hivi ndiyo tunaandaa Bajeti, tutahakikisha kwamba tunazungumza na wenzetu wa Iringa ili tuhakikishe kwamba hii wanaiingiza kwa sababu kweli pale pana problem kubwa, pale pana magari mengine Hyundai zimechoka choka hazifanyi kazi tutasaidia kuona kwamba wanaingiza katika Bajeti zao kwa sababu sasa hivi ndiyo shughuli inayofanyika. (Makofi) MWENYEKITI: Mheshimiwa Msigwa kwa kifupi. MHE. MCH. PETER S. MSIGWA: Mheshimiwa Mwenyekiti, ninakushukuru. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Waziri, mimi ndiye Mbunge wa Jimbo la Iringa Mjini na ninayajua mazingira ya Jimbo vizuri zaidi, niseme tu Mheshimiwa Waziri unapojibu maswali hunitendei haki, kwa sababu hospitali ile ya Iringa Mjini haikuanza kabla sijatoa vitanda na magodoro katika hospitali ile. Kwa hiyo, kumwagia sifa Mbunge wa Viti Maalum, kwamba yeye ndiyo amefanya juhudi kubwa si haki. Mheshimiwa Mwenyekiti, swali langu ni juhudi gani za makusudi baada ya Manispaa ya Iringa Mjini, kufanya juhudi kubwa kuijenga ile Hospitali na mimi kama Mbunge nilisaidia kuanzisha ile Hospitali ianze na juzi Waziri Mkuu alipokuja alinimwagia sifa na wewe ulizisikia, Serikali itatusaidiaje ili tupate hilo gari la wagonjwa tuendelee kufanya kazi vizuri? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (TAMISEMI): Mheshimiwa Mwenyekiti, swali nililokuwa ninajibu hapa lilikuwa ni swali la Mheshimiwa Ritta Kabati, ndiye aliyeuliza swali. Mimi Mheshimiwa Msigwa hakuuliza au maswali haya hayakuulizwa jointly, kwa hiyo niwajibie wote. Mimi ninachosema nilikuwa najibu kuhusu Mheshimiwa Ritta Kabati, kwa sababu ndiye swali lililoletwa hapa. Mimi nataka niseme kitu kimoja hapa na wala mimi sitaki kuingia katika conflicts hizi kwamba Mheshimiwa Msigwa amefanyakazi amepeleka vitanda pale niliona kwa macho yangu. Lakini wananchi wanachohitaji hapa siyo kwamba ni nani ameleta hapa, tunahitaji concertedefforts, tunataka watu wote waliopo kule Mwenyekiti wa Halmashauri atusaidie, Mbunge wa Viti Maalum atusaidie, Mbunge mwenyewe wa Jimbo atusaidie, tunataka Mkuu wa Mkoa na Mkuu wa Wilaya watusaidie na tunataka sisi Wabunge wote tusaidiane hapa. Kwa 3 Nakala ya Mtandao (Online Document) hiyo ni kweli kwamba pale wananchi wenyewe wamefanyakazi kubwa kwa kushirikiana na viongozi wao na hiyo ndiyo credit ambayo ninaileta kwako. Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa vile ameuliza mimi najua kwamba tulipokuja pale katika ile hospitali ilikuwepo na vitanda vililetwa pale, lakini equally ni kweli pia Mheshimiwa Ritta Kabati na yeye amechangia sana kama Mbunge wa Viti Maalum katika hilo eneo na wewe umechangia sana katika hilo eneo, wote mmechangia sasa ninafanya makosa gani? MWENYEKITI: Ahsante sana, tunaendelea Waheshimwia Wabunge leo tuna miswada miwili na yote hiyo inatakiwa iishe. Kwa hiyo, muda wetu ni mdogo sana. Mheshimiwa Mkosamali. Na. 32 Changamoto Zilizojitokeza Kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa MHE. FELIX F. MKOSAMALI aliuliza:- Uchaguzi wa Serikali za Mitaa mwaka 2014 umekuwa na changamoto nyingi sana:- (a) Je, ni kesi ngapi zimefunguliwa Mahakamani kutokana na uchaguzi huo kwa nchi nzima na zitaisha lini ikiwa zipo kesi za mwaka 2009 zimeisha mwaka 2014? (b) Je, ni kwa nini wananchi wa Kitongoji cha Nduta wamezuiwa kupiga kura? (c) Je, ni lini Serikali italeta Muswada wa Sheria ili Uchaguzi wa Serikali za Mitaa usimamiwe na Tume huru ya Uchaguzi? MWENYEKITI: Mheshimiwa Jenista nani anajibu hilo? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA
Details
-
File Typepdf
-
Upload Time-
-
Content LanguagesEnglish
-
Upload UserAnonymous/Not logged-in
-
File Pages110 Page
-
File Size-