Tarehe 26 Juni, 2019

Total Page:16

File Type:pdf, Size:1020Kb

Tarehe 26 Juni, 2019 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Hamsini na Tatu – Tarehe 26 Juni, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) Naibu Spika (Mhe. Dkt. Tulia Ackson) Alisoma Dua NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Tukae. Katibu! NDG. NEEMA MSANGI – KATIBU WA MEZANI: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA FEDHA NA MIPANGO:- Maelezo ya Waziri wa Fedha na Mipango kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2019 (The Finance Bill, 2019). MHE. MASHIMBA M. NDAKI – MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA BAJETI:- Maoni ya Kamati ya Bajeti kuhusu Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2019 (The Finance Bill, 2019). 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. DAVID E. SILINDE – NAIBU MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KWA WIZARA YA FEDHA NA MIPANGO:- Maoni ya Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni juu ya Muswada wa Sheria ya Fedha wa Mwaka 2019 (The Finance Bill, 2019). NAIBU SPIKA: Katibu! NDG. NEEMA MSANGI:- KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU NAIBU SPIKA: Maswali, Waheshimiwa Wabunge tutaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Frank George Mwakajoka, Mbunge wa Tunduma, sasa aulize swali lake. Na. 459 Mikataba ya Ajira kwa Madereva wa Malori na Mabasi MHE. FRANK G. MWAKAJOKA aliuliza:- Je, ni lini Serikali itasimamia na kuhakikisha Madereva wa Malori na Mabasi wanapata Mikataba ya Ajira ili kuboresha maslahi yao na kuongeza ufanisi katika Utumishi wao? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Frank George Mwakajoka, Mbunge wa Tunduma, kama ifuatavyo:- 2 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Mheshimiwa Naibu Spika, katika kushughulikia haki na maslahi ya Madereva nchini Tanzania, Serikali imechukua hatua mbalimbali katika kutatua changamoto zinazowakabili madereva ambapo mnamo tarehe 2 Mei, 2015 Mheshimiwa Mizengo Kayanza Peter Pinda, aliyekuwa Waziri Mkuu wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, aliagiza iundwe Kamati ya Kudumu ya Kutatua Matatizo katika Sekta ya Usafirishaji chini ya Uenyekiti wa Katibu Mkuu wa iliyokuwa Wizara ya Uchukuzi. Aidha, Kamati ndogo chini wa Uenyekiti wa iliyokuwa Wizara ya Kazi na Ajira iliundwa kwa ajili ya kushughulikia haki, maslahi na mkataba wa ajira wa Madereva. Mheshimiwa Naibu Spika, Serikali kwa kushirikiana na viongozi wa Vyama vya Wafanyakazi Madereva na Viongozi wa Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji nchini waliufanyia marekebisho na kuuboresha Mkataba wa ajira wa Madereva uliokuwepo. Mkataba ulioboreshwa uliidhinishwa na wadau katika kikao kilichofanyika tarehe 23 Juni, 2015 na ilikubalika kwamba Mkataba huo uanze kutumika rasmi tarehe Mosi, Julai, 2015. Mheshimiwa Naibu Spika, aidha, masharti yamewekwa kwamba kila Mmiliki wa basi au lori anayeomba leseni ya usafirishaji toka SUMATRA ni lazima awasilishe mikataba ya ajira ya Madereva wake ambayo imehakikiwa na Maafisa wa Kazi wa maeneo husika. Mheshimiwa Naibu Spika, Ofisi ya Waziri Mkuu inaendelea kusimamia majadiliano baina ya Vyama vya Wafanyakazi, Madereva na Umoja wa Wamiliki wa Vyombo vya Usafirishaji ili kuwawezesha kufikia muafaka wa viwango vya posho za safari na kujikimu wakati Madereva wanaposafiri ndani na nje ya nchi. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Frank George Mwakajoka, swali la nyongeza. MHE. FRANK G. MWAKAJOKA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante kwa kunipa nafasi ya kuuliza maswali mawili 3 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ya nyongeza. Pamoja na majibu ya Mheshimiwa Naibu Waziri, lakini bado kuna malalamiko makubwa sana kwa Madereva wa malori na mabasi na karibu asilimia 90 ya Madereva hao hawana mikataba ya kazi na kwa sababu Serikali inasema kwamba Mikataba yao ilitakiwa iboreshwe toka mwaka 2015 na mpaka sasa mikataba yao bado haijaboreshwa na bado hawajapewa mikataba. Je, Serikali ina mpango gani wa kuharakisha jambo hili ili wafanyakazi hao waweze kufanya kazi yao vizuri kwa sababu wakiwa na mawazo sana wanaweza wakasababisha ajali na Watanzania wengi wakapoteza maisha? Mheshimiwa Naibu Spika, swali la pili, kumekuwa na tatizo kubwa sana kwa sisi ambao tunaishi mipakani na mmeona kuna migomo mingi sana inatokea pale Tunduma watu Madereva wanapaki malori kwa sababu tu ya migongano kati ya wamiliki wa mabasi na malori kwa ajili ya mikataba hiyo? Sasa Serikali ina mpango gani wa kuhakikisha kwamba jambo hili linakwisha haraka kwa sababu ni muda mrefu sasa na Serikali ipo, inatoa majibu humu Bungeni lakini utekelezaji unakuwa hakuna? Ahsante. (Makofi) NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Waziri Mkuu, Mheshimiwa Anthony Peter Mavunde, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, KAZI, VIJANA NA AJIRA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kujibu maswali mawili ya nyongeza ya Mheshimiwa Frank Mwakajoka, Mbunge wa Tunduma, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, maswali yake nitayajibu yote kwa mkupuo. Katika kutekeleza Ilani ya Uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015 na katika ahadi ambayo Mheshimiwa Rais aliitoa akiwa Kahama mwaka 2015 juu ya Mikataba ya Wafanyakazi na hasa Madereva, Serikali inakuja na mpango mkakati ufuatao, hatua ya kwanza ilikuwa ni kuwataka Wamiliki wote wa Mabasi na Malori ambao watakwenda kuomba SUMATRA leseni ya usafirishaji wahakikishe kwamba 4 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) wanawasilisha na Mikataba ya Wafanyakazi kama eneo la kwanza la kuhakikisha kwamba Madereva hawa wanapata mikataba yao. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, katika kutekeleza hili, Serikali tumekuja na mkakati tofauti tumeona kwamba mkakati huu ulikuwa una mianya ya utekelezaji wake hivyo, siku mbili hizi zijazo Mheshimiwa Waziri wa Nchi, Ofisi ya Waziri Mkuu na Mheshimiwa Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, watatoa tamko na maelekezo ya kuanzia tarehe moja mwezi Julai ni hatua gani zitachukuliwa. Kuanzia hapo nina hakika kwa mkakati huo ambao wameuweka ni kwamba kila Dereva wa nchi hii atakuwa na mkataba wake na tutahakikisha kwamba pia kila Mmiliki wa Chombo cha Usafiri anafuata masharti ya sheria kama Kifungu cha 14 cha Sheria za Ajira na Uhusiano Kazini kinavyosema. Kwa hiyo, nimwondoe tu hofu Mbunge kwamba si maneno tu lakini mkakati umeshawekwa vizuri kabisa na tumekaa na wenzetu wa Jeshi la Polisi muda siyo mrefu kuanzia tarehe Mosi, Julai mtaona cheche za Wizara. NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge leo tuna maswali mengi sana, kwa hivyo tutaendelea na Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, Mheshimiwa Seif Khamis Gulamali, Mbunge wa Manonga, sasa aulize swali lake, kwa niaba yake Mheshimiwa Mwanne Mchemba. Na. 460 Ujenzi wa Vituo vya Afya vya Simbo, Ziba, Choma cha Nkola na Igurubi kwa Ufadhili wa Benki ya Dunia MHE. MWANNE I. MCHEMBA (K.n.y. MHE. SEIF K. GULAMALI) aliuliza:- Wilaya ya Igunga ilipata ufadhili wa Benki ya Dunia wa ujenzi wa Vituo vya Afya vya Simbo, Ziba, Chomachankola na Igurubi ambapo Vituo vya Afya vya Ziba, Chomachankola na Igurubi vimekamilika na vifaa tayari vipo japo majengo na vifaa katika Kituo cha Afya cha Chomachankola na 5 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) Igurubi bado havijaanza kufanya kazi; Kituo cha Afya cha Simbo bado hakijakamilika na vifaa havipo na Wafadhii walishakabidhi Halmashauri bila kukamilisha ujenzi huo:- Je, Serikali inachukua hatua gani kujua nini kilichojificha juu ya Mradi huo kukabidhiwa bila kukamilika? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE) alijibu:- Mheshimiwa Naibu Spika, kwa niaba ya Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Seif Khamis Gulamali, Mbunge wa Manonga, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Naibu Spika, ni kweli kuwa Wilaya ya Igunga ilipata ufadhili wa Benki ya Dunia kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya Simbo, Ziba, Chomachankola na Igurubi. Sababu kuu ya kushindwa kukamilika kwa miradi hiyo kwa wakati ilitokana na makadirio ya chini ikilinganishwa na gharama halisi za kukamilisha ujenzi. Ili kukamilisha ujenzi wa Vituo hivyo kwa kuzingatia ramani mpya, Serikali ilitoa jumla ya shilingi milioni 800 kwa ajili ya ujenzi wa Vituo vya Afya Simbo na Igurubi ambapo kila kituo kilipatiwa shilingi milioni 400. Mheshimiwa Naibu Spika, Kituo cha Afya cha Simbo kimekamilisha ujenzi wa majengo ya upasuaji na nyumba ya mtumishi na sasa vifaa tiba vinaendelea kuletwa. Aidha, Kituo cha Afya Igurubi kinaendelea na ujenzi wa majengo manne ambayo ni Maabara, Jengo la Wazazi, Jengo la Kufulia na Jengo la Kuhifadhia maiti. Majengo yote haya yapo katika hatua za ukamilishaji. NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Mwanne Mchemba, swali la nyongeza. 6 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. MWANNE I. MCHEMBA: Mheshimiwa Naibu Spika, ahsante. Nami naomba niulize swali dogo la nyongeza, kwanza nichukue nafasi hii kuipongeza sana Serikali yangu ya Awamu ya Tano kwa kazi nzuri ambayo inafanya kukamilisha Vituo vya Afya ambavyo mimi mwenyewe kama Mjumbe wa Kamati hiyo nimejionea kwa macho yangu mwenyewe. (Makofi) Mheshimiwa Naibu Spika, swali langu sasa, kwa kuwa Kituo cha Afya Simbo kimekamilika na bado hakijaanza kazi, je, ni lini sasa hivyo vifaa tiba vitapelekwa haraka sana ili kuwapunguzia adha wagonjwa ambao wanakimbilia kwenda Hospitali ya Private ya Nkinga? NAIBU SPIKA: Mheshimiwa Naibu Waziri, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa, majibu. NAIBU WAZIRI, OFISI YA RAIS, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (MHE. JOSEPHAT S. KANDEGE): Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nijibu swali la nyongeza la Mheshimiwa Mchemba,
Recommended publications
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 114 May - Aug 2016
    Tanzanian Affairs Issued by the Britain-Tanzania Society No 114 May - Aug 2016 Magufuli’s “Cleansing” Operation Zanzibar Election Re-run Nyerere Bridge Opens David Brewin: MAGUFULI’S “CLEANSING” OPERATION President Magufuli helps clean the street outside State House in Dec 2015 (photo State House) The seemingly tireless new President Magufuli of Tanzania has started his term of office with a number of spectacular measures most of which are not only proving extremely popular in Tanzania but also attracting interest in other East African countries and beyond. It could be described as a huge ‘cleansing’ operation in which the main features include: a drive to eliminate corruption (in response to widespread demands from the electorate during the November 2015 elections); a cutting out of elements of low priority in the expenditure of government funds; and a better work ethic amongst government employees. The President has changed so many policies and practices since tak- ing office in November 2015 that it is difficult for a small journal like ‘Tanzanian Affairs’ to cover them adequately. He is, of course, operat- ing through, and with the help of ministers, regional commissioners and cover photo: The new Nyerere Bridge in Dar es Salaam (see Transport) Magufuli’s “Cleansing” Operation 3 others, who have been either kept on or brought in as replacements for those removed in various purges of existing personnel. Changes under the new President The following is a list of some of the President’s changes. Some were not carried out by him directly but by subordinates. It is clear however where the inspiration for them came from.
    [Show full text]
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who Will Benefit from the Gas Economy, If It Happens?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013 Who will benefit from the gas economy, if it happens? Supported by: 2 TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2013: Who will benefit from the gas economy, if it happens? ACKNOWLEDGEMENTS Policy Forum would like to thank the Foundation for Civil Society for the generous grant that financed Tanzania Governance Review 2013. The review was drafted by Tanzania Development Research Group and edited by Policy Forum. The cartoons were drawn by Adam Lutta (Adamu). Tanzania Governance Reviews for 2006-7, 2008-9, 2010-11, 2012 and 2013 can be downloaded from the Policy Forum website. The views expressed and conclusions drawn on the basis of data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. TGRs review published and unpublished materials from official sources, civil society and academia, and from the media. Policy Forum has made every effort to verify the accuracy of the information contained in TGR2013, particularly with media sources. However, Policy Forum cannot guarantee the accuracy of all reported claims, statements, and statistics. Whereas any part of this review can be reproduced provided it is duly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. ISBN:978-9987-708-19-2 For more information and to order copies of the report please contact: Policy Forum P.O. Box 38486 Dar es Salaam Tel +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] Suggested citation: Policy Forum 2015.
    [Show full text]
  • Online Document)
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA NANE Kikao cha Sita – Tarehe 4 Februari, 2020 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Najma Murtaza Giga) Alisoma Dua MWENYEKITI: Waheshimiwa tukae. Katibu tunaendelea Waheshimiwa Wabunge na Mkutano wetu wa Kumi na Nane, kikao cha leo ni kikao cha tano, Katibu NDG. RAMADHANI ISSA ABDALLAH – KATIBU MEZANI: HATI ZA KUWASILISHA MEZANI Hati Zifuatazi Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, KAZI, AJIRA, VIJANA NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Matoleo ya Gazeti la Serikali pamoja na Nyongeza zake yaliyochapishwa tangu Mkutano wa Bunge uliopita kama ifuatavyo:- (i) Toleo Namba 46 la tarehe 8 Novemba, 2019 (ii) Toleo Namba 47 la tarehe 15 Novemba, 2019 (iii) Toleo Namba 48 la tarehe 22 Novemba, 2019 (iv) Toleo Namba 49 la tarehe 29 Novemba, 2019 (v) Toleo Namba 51 la tarehe 13 Desemba, 2019 (vi) Toleo Namba 52 la tarehe 20 Desemba, 2019 (vii) Toleo Namba 53 la tarehe 27 Desemba, 2019 (viii) Toleo Namba 1 la tarehe 3 Januari, 2020 (ix) Toleo Namba 2 la terehe 10 Januari, 2020 (x) Toleo Namba 3 la tarehe 17 Januari, 2020 (xi) Toleo Namba 4 la terehe 24 Januari, 2020 MHE. JASSON S. RWEIKIZA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA UTAWALA NA SERIKALI ZA MITAA: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Utawala na Serikali za MItaa kuhuus shughuli za Kamati hii kwa Mwaka 2019. MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA – MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE KATIBA NA SHERIA: Taarifa ya Kmaati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu shughuli zilizotekelezwa na Kamati hiyo kwa kipindi cha kuanzia Februari, 2019 hadi Januari, 2020.
    [Show full text]
  • MAJADILIANO YA BUNGE ___MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao Cha Thelathini Na Sita
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA _________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Thelathini na Sita – Tarehe 27 Mei, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, nawaomba tukae. Waheshimiwa Wabunge tunaendelea na Mkutano wetu wa 15, leo ni Kikao cha 36. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA NISHATI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Nishati kwa mwaka wa fedha 2019/2020. NAIBU WAZIRI WA MADINI: Hotuba ya Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2019/2020. 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) MHE. CATHERINE V. MAGIGE - K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA NISHATI NA MADINI) Taarifa ya Kamati ya Nishati na Madini Kuhusu utekelezaji na Majukumu ya Wizara ya Madini kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MHE. TUNZA I. MALAPO - K.n.y. MSEMAJI MKUU WA KAMBI RASMI YA UPINZANI BUNGENI KUHUSU WIZARA YA MADINI: Taarifa ya Msemaji Mkuu wa Kambi Rasmi ya Upinzani Bungeni juu ya Wizara ya Madini kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara hiyo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. SPIKA: Ahsante sana Mheshimiwa Tunza Malapo, tunakushukuru. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Tunaanza na TAMISEMI, swali la kwanza litaulizwa na Mheshimiwa Azza Hilal, Mbunge wa Viti Maalum - Shinyanga.
    [Show full text]
  • TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity?
    TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? With Partial Support from a TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? ACKNOWLEDGEMENTS This review was compiled and edited by Tanzania Development Research Group (TADREG) under the supervision of the Steering Group of Policy Forum members, and has been financially supported in part by Water Aid in Tanzania and Policy Forum core funders. The cartoons were drawn by Adam Lutta Published 2013 For more information and to order copies of the review please contact: Policy Forum P.O Box 38486 Dar es Salaam Tel: +255 22 2780200 Website: www.policyforum.or.tz Email: [email protected] ISBN: 978-9987 -708-09-3 © Policy Forum The conclusions drawn and views expressed on the basis of the data and analysis presented in this review do not necessarily reflect those of Policy Forum. Every effort has been made to verify the accuracy of the information contained in this review, including allegations. Nevertheless, Policy Forum cannot guarantee the accuracy and completeness of the contents. Whereas any part of this review may be reproduced providing it is properly sourced, Policy Forum cannot accept responsibility for the consequences of its use for other purposes or in other contexts. Designed by: Jamana Printers b TANZANIA GOVERNANCE REVIEW 2012: Transparency with Impunity? TABLE OF CONTENTS POLICY FORUM’s OBJECTIVES .............................................................................................................
    [Show full text]
  • Issued by the Britain-Tanzania Society No 124 Sept 2019
    Tanzanian Affairs Issued by the Britain-Tanzania Society No 124 Sept 2019 Feathers Ruffled in CCM Plastic Bag Ban TSh 33 trillion annual budget Ben Taylor: FEATHERS RUFFLED IN CCM Two former Secretary Generals of the ruling party, CCM, Abdulrahman Kinana and Yusuf Makamba, stirred up a very public argument at the highest levels of the party in July. They wrote a letter to the Elders’ Council, an advisory body within the party, warning of the dangers that “unfounded allegations” in a tabloid newspaper pose to the party’s “unity, solidarity and tranquillity.” Selection of newspaper covers from July featuring the devloping story cover photo: President Magufuli visits the fish market in Dar-es-Salaam following the plastic bag ban (see page 5) - photo State House Politics 3 This refers to the frequent allegations by publisher, Mr Cyprian Musiba, in his newspapers and on social media, that several senior figures within the party were involved in a plot to undermine the leadership of President John Magufuli. The supposed plotters named by Mr Musiba include Kinana and Makamba, as well as former Foreign Affairs Minister, Bernard Membe, various opposition leaders, government officials and civil society activists. Mr Musiba has styled himself as a “media activist” seeking to “defend the President against a plot to sabotage him.” His publications have consistently backed President Magufuli and ferociously attacked many within the party and outside, on the basis of little or no evidence. Mr Makamba and Mr Kinana, who served as CCM’s secretary generals between 2009 to 2011 and 2012-2018 respectively, called on the party’s elders to intervene.
    [Show full text]
  • Tarehe 4 Aprili, 2019
    NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ________ MAJADILIANO YA BUNGE _________ MKUTANO WA KUMI NA TANO Kikao cha Tatu – Tarehe 4 Aprili, 2019 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Job Y. Ndugai) Alisoma Dua SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba tukae. Leo ni kikao cha tatu cha Mkutano wetu wa Kumi na Tano. Katibu! NDG. STEPHEN KAGAIGAI – KATIBU WA BUNGE: HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI: Hati Zifuatazo Ziliwasilishwa Mezani na:- WAZIRI WA NCHI, OFISI YA WAZIRI MKUU, SERA, BUNGE, AJIRA, KAZI VIJANA NA WAZEE NA WENYE ULEMAVU: Taarifa ya Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. MOHAMED O. MCHENGERWA - MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA KATIBA NA SHERIA: Taarifa 1 NAKALA MTANDAO(ONLINE DOCUMENT) ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Katiba na Sheria kuhusu utekelezaji wa majukumu ya Ofisi ya Waziri Mkuu kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020. MHE. HASNA S.K. MWILIMA (K.n.y. MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA BAJETI): Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Bajeti kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Mfuko wa Bunge kwa Mwaka wa Fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Mfuko huo kwa Mwaka wa Fedha 2019/2020. MHE. DKT. JASMINE T. BUNGA - MAKAMU MWENYEKITI WA KAMATI YA KUDUMU YA BUNGE YA MASUALA YA UKIMWI: Taarifa ya Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Masuala ya UKIMWI kuhusu utekelezaji wa Bajeti ya Ofisi ya Waziri Mkuu (Tume ya Uratibu na Udhibiti wa UKIMWI) kwa mwaka wa fedha 2018/2019 pamoja na Maoni ya Kamati kuhusu Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Ofisi hiyo kwa mwaka wa fedha 2019/2020.
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NANE Kikao cha Thelathini na Tisa – Tarehe 2 AGOSTI, 2012 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) DUA Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua HATI ZILIZOWASILISHWA MEZANI Hati ifuatayo iliwasilishwa Mezani na:- NAIBU WAZIRI WA USHIRIKIANO WA AFRIKA MASHARIKI: Randama za Makadirio ya Mapato na Matumizi ya Wizara ya Ushirikiano wa Afrika Mashariki kwa Mwaka wa Fedha 2012/2013. SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, naomba mzime vipasa sauti vyenu maana naona vinaingiliana. Ahsante Mheshimiwa Naibu Waziri, tunaingia hatua inayofuata. MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Leo ni siku ya Alhamisi lakini tulishatoa taarifa kwamba Waziri Mkuu yuko safarini kwa hiyo kama kawaida hatutakuwa na kipindi cha maswali hayo. Maswali ya kawaida yapo machache na atakayeuliza swali la kwanza ni Mheshimiwa Vita R. M. Kawawa. Na. 310 Fedha za Uendeshaji Shule za Msingi MHE. VITA R. M. KAWAWA aliuliza:- Kumekuwa na makato ya fedha za uendeshaji wa Shule za Msingi - Capitation bila taarifa hali inayofanya Walimu kuwa na hali ngumu ya uendeshaji wa shule hizo. Je, Serikali ina mipango gani ya kuhakikisha kuwa, fedha za Capitation zinatoloewa kama ilivyotarajiwa ili kupunguza matatizo wanayopata wazazi wa wanafunzi kwa kuchangia gharama za uendeshaji shule? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, TAWALA ZA MIKOA NA SERIKALI ZA MITAA (ELIMU) alijibu:- Mheshimiwa Spika, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, naomba kujibu swali la Mheshimiwa Vita Rashid Kawawa, Mbunge wa Namtumbo, kama ifuatavyo:- Mheshimiwa Spika, Serikali kupitia Mpango wa Maendeleo ya Elimu ya Msingi (MMEM) imepanga kila mwanafunzi wa Shule ya Msingi kupata shilingi 10,000 kama fedha za uendeshaji wa shule (Capitation Grant) kwa mwaka.
    [Show full text]
  • The Politics of Gas Contract Negotiations in Tanzania: a Review
    DIIS WORKINGPAPER 2015: 03 0 GENDER EQUALITY AND LAND ADMINISTRATION: THE CASE OF ZAMBIA RACHEL SPICHIGER AND EDNA KABALA DIIS WORKING >PAPER 2014:04 Rasmus Hundsbæk Pedersen and Peter Bofin The politics of gas contract negotiations in Tanzania: a review 1 Rasmus Hundsbæk Pedersen Postdoc at DIIS [email protected] Peter Bofin Independent consultant [email protected] DIIS Working Papers make DIIS researchers’ and partners’ work in progress available towards proper publishing. They may include documentation which is not necessarily published elsewhere. DIIS Working Papers are published under the responsibility of the author alone. DIIS Working Papers should not be quoted without the express permission of the author. DIIS WORKING PAPER 2015: 03 DIIS· Danish Institute for International Studies Østbanegade 117, DK-2100 Copenhagen, Denmark Tel: +45 32 69 87 87 E-mail: [email protected] www.diis.dk ISBN 978-87-7605-760-2 (pdf) DIIS publications can be downloaded free of charge from www.diis.dk © Copenhagen 2015, the authors and DIIS 2 TABLE OF CONTENTS ABSTRACT........................................................................................................................ 4 INTRODUCTION ............................................................................................................ 5 THE EARLY PHASES IN TANZANIA’S EXPLORATION AND PRODUCTION HISTORY ........................................................................................................................... 9 THE GAS-TO-ELECTRICITY PROJECTS IN TANZANIA IN THE 1990S
    [Show full text]
  • Tarehe 2 Novemba, 2016
    NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) BUNGE LA TANZANIA ___________ MAJADILIANO YA BUNGE __________ MKUTANO WA TANO Kikao cha Pili – Tarehe 2 Novemba, 2016 (Bunge Lilianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Mwenyekiti (Mhe. Mussa A. Zungu) Alisoma Dua MWENYEKITI: Tukae. Katibu! NDG. CHARLES MLOKA - KATIBU MEZANI: MASWALI NA MAJIBU MWENYEKITI: Waheshimiwa kama kawaida tunaanza na Ofisi ya Waziri Mkuu. Mheshimiwa Ezekiel Maige, kwa niaba Mheshimiwa Mwambalaswa! Na. 16 Kuanzisha Mfuko wa Maafa Kitaifa MHE. VICTOR K. MWAMBALASWA (K.n.y. MHE. EZEKIEL M. MAIGE) aliuliza:- Kutokana na mabadiliko ya tabia nchi matukio ya majanga na maafa kama mvua za mawe pamoja na matetemeko ya ardhi yameanza kutokea mara kwa mara na mara zote Serikali imekuwa haina maandalizi ya kifedha na vifaa vya kusaidia wahanga kwa muda mfupi na muda mrefu na badala yake imekuwa ikitegemea zaidi wasamaria wema wa Mataifa mengine:- (a) Je, ni kwa nini Serikali imekuwa haisaidii kifedha na vifaa zaidi ya kuhamasisha wasamaria wema wasaidie na wenyewe kubaki na jukumu la kupeleka wataalam kama Madaktari na kuratibu misaada pekee? 1 NAKALA YA MTANDAO (ONLINE DOCUMENT) (b) Je, ni kwa nini Serikali isianzishe Mfuko wa Maafa Kitaifa ambao utakuwa unachangiwa wakati wote kwa njia endelevu? NAIBU WAZIRI, OFISI YA WAZIRI MKUU, WATU WENYE ULEMAVU alijibu:- Mheshimiwa Mwenyekiti, kwa niaba ya Mheshimiwa Waziri Mkuu, napenda kujibu swali la Mheshimiwa Ezekiel Magolyo Maige, Mbunge wa Msalala, lenye sehemu (a) na (b), kama ifuatavyo:- (a) Mheshimiwa Mwenyekiti, naomba kulifahamisha Bunge lako Tukufu kwamba, Serikali inatambua kuwa ni wajibu wake kusaidia wananchi pindi wanapokumbwa na maafa yanayoharibu mfumo wa maisha ya kila siku.
    [Show full text]
  • Hii Ni Nakala Ya Mtandao (Online Document)
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA ____________ MAJADILIANO YA BUNGE ___________ MKUTANO WA NNE Kikao cha Ishirini na Nne – Tarehe 18 Julai, 2006 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Spika (Mhe. Samuel J. Sitta) Alisoma Dua MASWALI NA MAJIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge, kabla sijamwita muuliza swali la kwanza nina matangazo kuhusu wageni, kwanza wale vijana wanafunzi kutoka shule ya sekondari, naona tangazo halisomeki vizuri, naomba tu wanafunzi na walimu msimame ili Waheshimiwa Wabunge waweze kuwatambua. Tunafurahi sana walimu na wanafunzi wa shule zetu za hapa nchini Tanzania mnapokuja hapa Bungeni kujionea wenyewe demokrasia ya nchi yetu inavyofanya kazi. Karibuni sana. Wapo Makatibu 26 wa UWT, ambao wamekuja kwenye Semina ya Utetezi na Ushawishi kwa Harakati za Wanawake inayofanyika Dodoma CCT wale pale mkono wangu wakulia karibuni sana kina mama tunawatakia mema katika semina yenu, ili ilete mafanikio na ipige hatua mbele katika kumkomboa mwanamke wa Tanzania, ahsanteni sana. Hawa ni wageni ambao tumetaarifiwa na Mheshimiwa Shamsa Selengia Mwangunga, Naibu Waziri wa Maji. Wageni wengine nitawatamka kadri nitakavyopata taarifa, kwa sababu wamechelewa kuleta taarifa. Na. 223 Barabara Toka KIA – Mererani MHE. DORA H. MUSHI aliuliza:- Kwa kuwa, Mererani ni Controlled Area na ipo kwenye mpango wa Special Economic Zone na kwa kuwa Tanzanite ni madini pekee duniani yanayochimbwa huko Mererani na inajulikana kote ulimwenguni kutokana na madini hayo, lakini barabara inayotoka KIA kwenda Mererani ni mbaya sana
    [Show full text]
  • Majadiliano Ya Bunge ______
    Hii ni Nakala ya Mtandao (Online Document) BUNGE LA TANZANIA _______________ MAJADILIANO YA BUNGE _______________ MKUTANO WA KUMI NA TATU Kikao cha Tatu – Tarehe 30 Oktoba, 2008 (Mkutano Ulianza Saa Tatu Asubuhi) D U A Naibu Spika (Mhe. Anne S. Makinda) Alisoma Dua MASWALI KWA WAZIRI MKUU NAIBU SPIKA: Waheshimiwa Wabunge kama kawaida yetu siku ya Alhamisi kazi zetu zinaanza kwa maswali kwa Waziri Mkuu kwa muda wa dakika 30. Kwa hiyo Mheshimiwa Waziri Mkuu mwulizaji wa swali la kwanza leo ni Mheshimiwa Mzee John Samwel Malecela. MHE. JOHN S. MALECELA: Mheshimiwa Naibu Spika, napenda kukushukuru kwa kunipa nafasi ya kuuliza swali la kwanza. Mheshimiwa Waziri Mkuu hivi sasa kuna tatizo la uandikishaji wa vijiji vipya, vijiji ambavyo zamani vilikuwa kama vitongoji lakini sasa vimekuwa vijiji vingi na vikubwa na pia kuna tatizo la ugawaji wa kata. Sasa mambo yote haya yanashughulikiwa na TAMISEMI. Je, Serikali haingeona uwezekano wa kukasimu madaraka ya uandikishaji wa vijiji yaende kwenye Halmashauri za Wilaya na suala la uandikishaji wa ugawaji wa kata liende kwa Ofisi ya Mkuu wa Mkoa, kwa hiyo kuondoa msongamano ambao sasa hivi uko TAMISEMI kiasi kwamba viko vijiji ambavyo vimependekezwa na Halmashauri zaidi ya miaka 10 iliyopita lakini mpaka sasa hakuna kilichofanyika? WAZIRI MKUU: Mheshimiwa Naibu Spika, naomba nimjibu Mheshimiwa Mzee Malecela swali lake zuri sana kama ifuatavyo. Mheshimiwa Naibu Spika, sababu ya kuendeleza utaratibu huu wa kutaka jambo hili liwe linaamuliwa katika ngazi hii ni kwamba kuna masuala ya kifedha ambayo yanaendana sambamba na uanzishwaji wa vijiji, kata na maeneo mengine mapya. Kwa hiyo, kwa msingi huo Serikali bado inaona ni vizuri uamuzi kama huo ukaendelea kubaki 1 mikononi mwetu ili hilo liweze kuwa ni jambo ambalo linatu-guide katika kuamua vijiji vingapi safari hii turuhusu itakuwa na component ya Watendaji na kata ngapi kwa sababu utaongeza mambo mengine ndani ya kata.
    [Show full text]